www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all. |
KWA
JINA
Sifa zote njema ni zake Yeye ambaye ameumba bila ya
Yeye mwenyewe kuumbwa.
Nilfikiriya mwenyewe kuwa ni mwenye bahati
Ningependa kuhakikisha pande zote kwamba hakuna
kishawishi chochote cha pesa kwenye uchapishaji huu, na kwamba imefanywa tu kwa
kutaka radhi za Allah (s.w.t.).
Namshukuru pia Akhiy Mohammed Kanju aliyegeusha
kitabu hiki kwenye Kiswahili.
Mtumishi wa Allah
Bashir Alidina
Muhammad Bin Sanah anasimulia kwamba Mufazzal Bin
Umar alimsimulia hivi :
"Siku moja baada ya Sala ya Alasiri nilikaa
baina ya Mimbari na Kuba
Nikiwa nimezama katika kuwaza huko, mara alitokea Bin
Abi Al Auja, kafiri mshirikina na akakaa umbali wa kuweza kumsikia. Sahiba wake
alimfuata na akakaa kwa utulivu ili kusikiliza.
Bin Ali Auja alianza mazungumzo kwa kusema,
"Mwenye Kuba hili amepata fadhila kubwa za pekee kwa ukamilifu wa heshima
kuu katika yote aliyoyafanya." Sahaba wake aliongeza kwa kuthibitisha
akasema: "Alikuwa filossofa na alifanya dai kubwa likiungwa mkono na
miujiza ambayo kwamba ilishangaza akili za kawaida. Waliojifanya ni wenye
hekima walizama kwa undani wa vina vya akili zao kupenya kwenye maajabu hayo
(ili kuyajua) lakini bila mafanikio.
Ujumbe wake ulipokubaliwa na watu wastaarabu, wenye
maarifa na wasomi watu kwa ujumla waliingia katika imani yake makundi kwa
makundi. Sehemu za ibada na Misikiti ya sehemu zote ambako popote ulipofika wito
wa utume wake ulianza kusikika kwa nguvu na kueleweka pamoja; na jina lake
(kutajwa) sambamba na lile
Bin Ali Auja akasema: "Weka kando habari za
kumtaja Muhammad (s.a.w.) ambaye kuhusu yeye, akili yangu ina shangazwa vikubwa
na mawazo yangu yamefadhaishwa.
Hebu tuongelee ukweli katika msingi wa watu kukubali
imani ya Muhammad (s.a.w.) - Mwenye Rehema kwa ulimwengu. Je, kuna kiumbe wa
namna hiyo au hapana?"
Kisha alirejea katika asili na uumbaji wa mpangilio
mkubwa wa ulimwengu. Alifanya dai lisilosadikika kwamba hakuna aliyeviumba na
hakuna Muumba, wala Msamii wala Mtengenezaji - Ulimwengu umejitokeza wenyewe.
Katika kuwepo na ataendelea kuwepo na kwa hiyo hauna mwisho."
Nilijisikia vibaya umno kusikia hivi na nikamwambia :
"Ewe usiye amini! Huwamini katika imani ya Allah (s.w.t.) kwa kukanusha
moja kwa moja kuwepo kwake ambaye amekuumba wewe katika umbo zuri, akakugeuza
kutoka hali moja kwenda hali nyingine, mpaka ukafikia katika umbo ulionalo
sasa? Lau ungejifikiria wewe mwenyewe na lau akili zako nzuri zingekusaidia
kiukweli, ungeweza kutambua katika nafsi yako mwenyewe hoja hizi za wazi za
kuwepo kwa Allah Mtukufu Ishara ya vitu vyake vyote anavyoviruzuku na ushahidi
wa Usanii wake usio na mipaka.
Alisema, "Tutajadili suala hili
Kwa hili, nilitoka nje nikiwa na huzuni mno na mawazo
tele kwasababu ya kutokuamini kwao katika Allah (s.w.t.) na matokeo ya huzuni
na majonzi ya Uislamu na Wachaji wake, kwasababu ya kutokuamini kwao na usahifi
usio na maana wa ulimwengu huu.
Nilikwenda mwenyewe kwa Bwana wangu, Imam Ja'afar Al
Sadiq (a.s.). Aliponiona nimehuzunika, aliniuliza sababu ya kuwa hivyo.
Nilimsimulia mazungumzo ya wale mushirikina na jinsi nilivyo jaribu kuoenyesha
uongo wa hoja zao.
Aliniambia nije siku inayofuatiya (yaani kesho yake)
wakati atakapo weka wazi kwangu ustadi mkubwa mno wa mwenye nguvu zote msanifu
aliyedhihirika katika ulimwengu wote ulio na wanyama, na ndege, wadudu, vitu
vyote vilivyo hai ama viwe ni wanyama au jamii ya mimea, miti izaayo matunda au
dufu na ile isiyo na matunda, mboga zinazolika na zisizolika - maelezo ya
kiustadi yatakayokuwa kama kifungua macho kwa wale ambao watakubali maelekezo;
faraja kwa waumini na fadhaa kwa wazushi.
Niliposikia haya, nilirudi kutoka sehemu yake tukufu
nikiwa katika hali ya furaha. Ujio wa usiku ule ulionekana kuwa mrefu kwasababu
ya shauku yangu kubwa ya kujifunza kutoka kwa Mwanachuo mstahiki huyo, mambo
aliyoahidi kuyaeleza kesho yake.
Asubuhi na mapema niliwasili mwenyewe na baada ya
kukaribishwa vizuri, nikisimama kiheshima mbele ya sehemu yake tukufu, na
kushukua nafasi yangu ya kukaa ambayo nimepewa. Kisha yeye (a.s.) alikwenda
kwenye chumba cha faragha ambacho mara kwa mara huenda kujipekesha. Na mimi
vile vile nilinyanyuka baada ya kuamrishwa, nilimfuata. Aliingia chumba kile
cha faragha na miminilikaa chini mbele yake.
Akasema, "Mufazzal! Nahisi kwamba umekuwa na
usiku mrefu kwa sababu ya shauku yako kwa ajili ya kesho. Nilithibitisha maneno
yake kiheshima.
Alianza, "Allah (s.w.t.) alikuwepo kabla
hakujakuwa na kitu chochote na utakuwepo kiroho kupindukia milele. Atukuzwe
Yeye kwa vile Ameufanya ufunuo wake kwetu. Kwake Yeye Anastahiki shukurani zetu
za dhati kwa sababu ya tunu yake kwetu. Ametupa sisi daraja kubwa pamoja na
elimu bora na akatuanisha sisi pamoja na utukufu wa cheo (kwani kwa vile tu)
kizazi cha Hadhrat Ali Ibne Abu Talib (a.s.) kupita viumbe vyote kwa elimu
yake, ikiwa ni dhamana tukufu, pamoja nasi ya upambamizi wa (mambo) ya
ulimwengu huu.
Niliomba ruhusa aweke picha kamili yale yote
yaliyotoka mdomoni (kinywani) mwake, kwa vile nilikuwa na kila kitu muhimu kwa
kuandikia, kitu ambacho alikubali kwa furaha.
Akasema, "Ewe Mufazzal! Wababaishaji wameshindwa
kufahamu siri na sababu zilizo msingi wa asili ya viumbe, na akili zao zimebaki
kutokuwa na habari ya ustadi usio na kosa uendeleao kuwepo chini ya uumbaji wa
jamii mbali mbali (za viumbe) wa bahari na bara, tambarare na miinuko miinuko.
Wakawa makafiri, na kwa sababu ya kasoro ya elimu yao
na ufinyu wa akili, wakaanza ulaghai ushindanao pamoja na ukweli, kiasi kwamba
waliukataa uumbaji na kudai kwamba ulimwengu wote huu hauna maana yoyote ni
bure tu, bila kuwa na ustadi wowote wa usanii juu ya uhusikaji na usanii au
Muumba - bila kusudio usio na mwisho bila uwiyano au utulivu.
Allah (s.w.t) yu mbali mno na yale yote
wanayomhusisha nayo. Na wapotelee mbali! Kulioje Kupotoka kwao! katika upofu
wao wa kupotoka na bumbuazi, wako kama watu vipofu wapapasao kulia na kushoto
katika nyumba iliyopambwa vizuri, iliyojengwa vizuri pamoja na mabusati mazuri,
vitu vitamu vya chakula na vinywaji, aina mbalimbali za nguo na vitu vingine
muhimu vya matumizi ya lazima, vyote vimewekwa kwa kutosheleza kwa kiasi kizuri
na kuwekwa kwa ukamilifu makini na ustadi wa kusanii. Katika upofu wao
wameshindwa kuliona jengo
Kutokulingana huku kwa tabia hushikilia vizuri katika
kadhia ya tapo, ambalo hukataa nguvu iumbayo na hoja hiyo ipendeleayo usanii wa
Kiungu. Hushindwa kutambua ubora wa riziki zao, ukamilifu wa uumbaji na uzuri
wa Usanii, wanaanza kutangatanga katika mapana ya dunia, wakifadhaishwa kwa
kutokuweza kwao kufahamu kwa akili zao sababu na misingi iliyo chini yake.
Hutokea hivyo wakati mwingine kwamba mmoja miongoni mwao anayo habari ya kitu,
lakini katika ujinga wake juu ya ukweli wake, kusudio na mtaji, huanza mara
moja kulitafutia kosa akisema, "Ni kosa lisilothibitika."
Wafuasi wa Mani (Mtu aliyeanzisha Dhehebu
Inampasa mtu ambaye Allah (s.w.t.) amemjaliya na
elimu ya maajabu ya Kiroho ya ukweli na ambaye amemuongoza kwenye imani yake,
na ambaye amepewa kuona na kutafakari juu ya ujuzi wa usanii ulio chine ya
uumbaji, na ambaye ametunukiwa uelezaji wa sifa wa vitu hivyo, juu ya msingi wa
akili isadikishayo na sifa nzuri. Inampasa mtu kama huyo kumtukuza Allah
(s.w.t.) kwa ukamilifu kama Mola wake na fadhila za Kimbinguni, na kumuomba
Yeye kwa kumzidishia elimu ya mambo ya Kiroho na msimamo imara ndani yake, na
uwezo wa juu wa maelezo juu ya hayo.
Yeye (s.w.t.) asema, "Nitaongeza fadhila zangu,
kama mtakuwa ni wenye kushukuru, na adhabu yangu ni kali
Muundo wa Ulimwengu huu ni mwongozo wa juu zaidi na
hoja ya kuwepo Allah (s.w.t.) - jinsi sehemu zake (huo ulimwengu)
zilivyounganishwa pamoja na kuwa na ufundi mzuri wa Usanii.
Hali ya kufaa kutafakari na akili kuangalia kuhusu
sehemu moja moja hudhihirisha kwamba ulimwengu huu unalinganishwa na nyumba
iliyopambwa na vitu vyote muhimu kwa ajili ya mwanadamu.
Mbingu hii ni kama chandalua; ardhi imetandazwa kama
busati ambapo nyota zimewekwa katika safu juu ya safu zikijitokeza
Mtu, katika Ulimwengu huu, ni
Na siyo jamii tofauti za mimea zipatikanazo kukidhi
mahitaji ya mtu binafsi - baadhi ni chakula cha wanyama, nyingine ni dawa kwa
Wanadamu; baadhi ni kwa mapambo tu, baadhi ni kumpatia mtu manukato kwa burdani
yake, baadhi ni dawa kwa wanyama, baadhi ni lishe kwa Mwanadamu, baadhi kwa
ndege tu na nyingine kwa wanyama wa miguu miine peke yao na kuendelea. Jamii
tofauti za wanyama zimepangiwa kazi kwa mahitaji na faida maalum.
Tunaanza sasa na maelezo ya kuumbwa Mwanadamu kabla
hujajifundisha somo litokanalo humo. Hatua ya kwanza katika kuumbwa kwa
Mwanadamu hurejea kwenye hali wakati Kijusu (Mimba) kinapowekwa kimpango katika
tumbo la uzazi, ingawa imefungwa ndani ya aina tatu za sitiri zilizo wazi na
aina tatu za viza. Ya kwanza ikiwa ni ile ya ukuta wa nje, ya pili ni ya tumbo
la uzazi na ya tatu ni ya Kondo la nyuma. Huu ni wakati ambapo kijusu hakiwezi
kujilisha wala kuondoa madhara yoyote yatokanayo nayo.
Mtiririko wa Heidh umeadilishwa ili kutoa lishe kwa
ajili yake, kama vile maji yanavyochukua lishe kupeleka kwenye mimea. Hivyo
mpango huu huendelea mpaka kufikia wakati ambao viungo vyake vimekamilishwa,
ngozi juu ya mwili wake huwa imara kiasi chakustahimili hali ya hewa - hivyo
kwamba haiwezi kupata madhara yoyote kutoka kwenye hewa na macho yake yanapata
uwezo wa kustahimili mwanga. Wakati vyote hivi vinapokuwa vimekwisha fanyika,
mama yake hupatauchungu wa uzazi, ambao kwa ukali humtikisa kumfikisha kwenye
kuhangaika, kufikia upeo wa kuzaliwa mtoto.
Na kwa kuzaliwa mtoto, mtiririko wa heidhi uliokuwa
ukipeleka lishe kwenye tumbo la uzazi unabadilishwa kwenda kwenye matiti ya
mama.
Ladha yake inabadilishwa hivo hivo na rangi yake, na
kuwa lishe aina ya pekee tofauti ambayo hufaa hasa kwa hali ya mtoto, kama na
wakati ahitajiayo (hayo) hayo, kulinganishwa na mtiririko wa damu.
Wakati ule ule wa kuzaliwa kwake anaanza kutikisa na
kulamba midomo yake kwa ulimi wake kuonyesha hamu yake ya (kunyonya) maziwa
hukuta jozi ya matiti ya mama yake matamu mno yaliyohifadhiwa yakining'inia
tayari kwa kumpatia lishe kwa ajili yake. Hupata lishe yake kutoka maziwa
katika njia hii mpaka wakati huo, kwa vile mwili wake bado ni mororo, viungo
vyake na matumbo yake ni laini na dhaifu.
Kama aanzavyo kutembea na kuhitaji chakula kigumu
kujenga mwili weneye nguvu, magego yake hutokeza kutafuna vyakula kurahisisha
uyeyushaji wachakula tumboni. Huendelea na lishe hiyo mpaka anapofikia balehe.
Mwnaume anaota nywele katika uso kama alama ya uume
kupata heshima kama mwanaume, hivyo kupita hatua ya utoto na kufanana na
wanawake. Mwanamke huuweka uso wake safi, upendezao na bila nywele, kuuweka
umaridadi wake na umbo zuri. Kama mvutio kwa wanaume katika huduma ya kulifanya
Taifa liishi.
Je, unaweza ukafikiria hali ambayo mtu katika kupitia
kwenye hatua zote hizi tofauti ameongozwa na kukamilishwa, zinaweza zikatoka
bila ya kuwa na Msanii na Muumba? Je, unafikiri kama mtiririko wa heidhi
usingegeuzwa kwake wakati ni kijusu katika tumbo la uzazi,je, asingeweza
kukauka kama vile mimea ikaukavyo, ikinyimwa maji? Na je, kama isingekuwa ni
kusukumwa kwa uchungu wa uzazi baada ya kukomaa kwa uzazi, je, asingezikwa
katika tumbo la uzazi kama vile mtoto anaeishi anavyozikwa katika ardhi?
Na je, kama asingepatiwa aina nzuri ya maziwa, je,
asingekufa kwa njaa? kama asingelishwa na lishe nzuri zenye kulingana na hali
ya uwezo wake ya kuukamilisha mwili wake na kama meno yake yasingetoka katika
wakati mahususi, je, isingekuwa matatizo kwake kula, kutafuna na kuyeyusha
chakula chake? Na kama asingepitia kipindi cha utoto cha kunyonya, mwili wake
usinge umia katika sulubu na kudhoofika kwa kazi yoyote kwa matokeo ya
mabadiliko ya kudumu juu ya mama yake kwa kumfanya ashughulike na silika yake
tu na kumlea, bila muda wa kutafuta mtoto wa pili?
Uso wake usingeota nywele katika wakati mahususi, je
asingekuwa yu ngali katika hali yautoto na maumbile ya wanawake, bila ya murua
wowote au sifa kama vile matoashi ambao wana sura mbaya kwa kukosekana ndevu?
Ni nani basi huyo, ambaye amemuumba mtu bure bure tu,
ambaye amekuwa mjenzi wa thamani yake, ambaye daima ni mwenye hadhari kumpatia
mahitaji yake wakati wote?
Kama kujitokeza kwa uumbaji bila Msanii maalum kuna
weza kukubalika chini ya masharti ya kawaida hii, basi matilaba ya Kizazi na
uwiano thabiti wa uumbaji unaweza kuwa chanzo cha kosa na fadhaa, kwa vile
viwili hivi vinapingana na kujitokeza kwa uumbaji bila usanii maalum.
Maelezo kama hayo ni ya upuuzi wa hali ya juu kwamba
mpango na kurekebisha kwa pasa kutokea hivi bila Muumba, na mpango mbaya na
usio faa wa usanii na maumbile vingepaswa kuhusishwa na Muumba. Asemaye hivi ni
juha kwa sababu kitu chochote kilicho tengenezwa bila usanii kamwe hakiwezi
kuwa sawa na kulingana ambapo visivyo mpango na ukaidi haviwezi kuepo pamoja na
usanii wa mpango. Allah (s.w.t.) yuko mbali na wanayo sema wapotofu.
Na kama mtoto angezaliwa na akili pevu,
angepumbazishwa na ulimwengu huu jinsi ulivyo mgeni kwake, katika mazingira
yasiyoeleweka yaliyo zunguukwa na wanyama na ndege wa kila aina pande zote,
ambavyo vingeonekana katika macho yake kila muda wa siku.
Ifikirie katika hali ya mtu anayehamia nchi nyingine
kutoka jela ya nchi nyingine, kama ana akili timamu, utamwona akiwa ametatazika
na kufadhaika. Hawezi kujifundisha lugha ngeni kiasi cha kutosha kwa mara moja,
wala kuupata mwenendo na tabia za mahali hapo. Kwa upande mwingine, yule ambaye
anachukuliwa kama mfungwa kupelekwa nchi ngeni katika siku zake za mwanzo
wakati akili yake ni changa, mara moja atajifundisha lugha hiyo, mwenendo na
tabia za sehemu hiyo.
Hivyo hivyo, kama mtoto angezaliwa na akili pevu
angeshangazwa katika kufumbua macho yake na kuona vitu mbali mbali
vilivyopangwa kwa mpango namna hiyo, aina mbali mbali ya maumbile na mawazo
yaliyo wazi ya umoja na faraka. Kwa muda mrefu, asingeelewa ni lini amekuja na
ni wapi alipofikia na iwapo yale yote aliyokuwa akiyaona ni ndoto.
Kisha, kama angezaliwa na akili pevu angejisikia
kinyaa na kushushwa hadhi, kujiona yeye mwenyewe ni mwenye kupakatwa huku na
huku miknoni, akilishwa kwa maziwa, kufungwa ndani ya vitata (desturi ya
Waarabu) na kulazwa katika susu - hatua zote hizi zikiwa za muhimu kwa mtoto
wachanga kwasababu ya umororo na ulaini wa miili yao.
Yasingekuwepo haya, kama wangezaliwa na akili pevu,
kudekezwa huku, wala kudekezwa kule, wala upole huu kwa watoto wachanga katika
akili za watu wazima ambako kikawaida huonekana kutokana na huba kwa watoto
ambao hawakufundishwa kwa sababu ya unyofu wao hujenga hadhari maalum kw ajili
yao. kwa hivyo anazaliwa katika ulimwengu huu bila kuelewa kitu chochote, bila kuelewa
kabisa ulimwengu na kila kilichomo humo. Anayaangalia mambo yote haya na akili
yake changa na upungufu wa kuelewa, na hivyo hajiskii kutatazika.
Akili yake na kuelewa kidogo kidogo, polepole muda
hadi muda, kukua kidogo kidogo, hivyo ili kumuingiza kwa taratibu kwenye vitu
vilivyo mzunguuka na kuizoeza akili yake ipasavyo ili kumzoesha kwa hayo bila
kuhitaji udadisi zaidi na maajabu, hivyo kumwezesha kutafuta riziki yake kwa
utulivu pamoja na kuelewa na kupanga, kuweka juhudi zake humo, na kujifunza
masomo ya utii, makosa na utovu na adabu.
Na tazama! Kuna sehemu nyingine za mambo. Kama mtoto
mchanga angezaliwa na akili pevu pamoja na kuelewa kazi zake, kungelikuwa na
nyakati chache za deko lihisiwalo katika kawaida ya mtoto mdogo, na mahitaji,
ambayo kwamba wazazi wanajikuta nyakati zote tangu mwanzo wanajishughulisha kwa
mambo ya vijana wao, yasingejitokeza. Pendo na huba, vihisiwavyo kwa watoto wa
kawaida, kufuatia taabu walizopitia kwa ajili yao, isingekuwepo baina ya wazazi
na vizazi vyao. Kwa sababu ya akili zao pevu, watoto wasingehitaji matunzo ya
wazazi. Mtengano ungeanza punde tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto mchanga kutoka
kwa wazazi wake. Hata mama au dada wangekuwa wageni kwake na kwa hivyo (pia)
katika mipaka ya ndoa.
Huoni kwamba kila kitu kikubwa au kidogo kimeumbwa
katika mpango usio kombo bila dosari au kosa?
Hebu tizama faida ya matokeo kwa watoto itokanayo na
kulia. Kuna maji katika ubongo wa mtoto ambayo kama hayakutolewa, huweza
kusababisha matatizo au maradhi, hata pengine jicho kupotea. Kutoka kwa maji
kutoka katika ubongo wake huliacha kuwa na afya na macho kuwa na mng'aro zaidi,
mtoto anafaidika kwa kulia, ambapo wazazi wake katika kutokojua kwao, hujaribu
kuzuia kulia kwake kwa kumpatia matakwa yake, bila kujua faida ya huko kulia.
Ziko faida nyingine kama hizo ambazo walahidi
wameshindwa kuzifahamu, na kama wangeweza kuzifahamu, wasingeweza kukanusha
kuwepo kwa faida hizo katika hili. Watu wenye elimu ya kiroho wanaelewa ni nini
kisichotambulikana kwa wakanushaji hawa. Hutokea hivyo wakati mwingine kwamba
viumbe hawajui hekima iliyoko humo, ingawa iko katika elimu ya Muumba.
Udende utokao midomoni mwa watoto huweza kusababisha
uharibifu mkubwa kama hautaruhusiwa kutiririka. Hii inaweza kuonekana kwa wale
wenye mate mengi ambao huzama chini katika hali ya mabaradhuli, mapunguani na
wapumbavu, na kuwa chambo cha magonjwa mengine kama kiharusi - (kupooza) mwili
nzima na (kiharusi cha) uso. Allah Azza
Wa Jalla, ameamrisha kwamba maji haya yanapasa kutolewa kwa njia ya mdomo ili
kumweka katika siha nzuri kwa uzuri wake wa baadae.
Majaaliwa yametoa fadhila hii, ya uzito ambao wao
hawajui. Wanaruhusiwa nafasi hii kupata elimu ya hekima iliyomo ndani yake, ili
kwamba wawe wenye elimu ya Kiroho na kama watu hawa wangeshukuru fadhila zote
hizi, wasingebakia katika dhambi kwa muda mrefu hivi. Hivyo sifa zote na
utukufu ni wake Yeye. Ukubwa ulioje wa rehema zake. Baraka zake ni kwa wote
wawe wamestahiki au hawastahiki, Yuko mbali, ametukuka juu ya yale wanayosema
watu hawa waliopotoka.
Hebu fikiria viungo vya mwanaume na mwanamke vya
ngono. Kiungo cha mwanaume kina uwezo wa kuamka (kwa ashiki) na kuongezeka ili
kuweza kuutolea manii mfuko wa uzazi - hiyo ikiwa ndiyo kazi yake, ikiwa
chenyewe hakina uwezo wa kukuza kilenga na kwa hivyo kuhitaji uhamisho wa manii
kwenda mfuko wa uzazi wa mwanamke - mfuko ulio ndani ulinganao na kuhifadhi
kiufanisi matone mawili ya mbegu za uzazi, kukuza kilenga kwa kutanuka kikadiri
kwa kuongezeka ukubwa wake, kuzuia shinikizo lolote juu yake, kukihifadhi mpaka
kinaimarishwa na kufanywa imara. Je, haikusanifiwa hivyo na msanii aonae kwa
undani zaidi? Je, kazi zote hizi za ustadi, au kadiri hizi jamala (uzuri)
zimejitokeza hivi hivi zenyewe? Allah Azza Wa Jalla Yu mbali, ametukuka juu ya
upotofu wa Washirikina.
Hebu fikiria viungo mbali mbali vya mwili, kazi
zitakiwazo kwa kila kimoja kufanya na ukamilifu wa usanii uliomo ndani ya kila
kiungo.
Mikono yote imekusudiwa kutumika kwa shughuli, miguu
yote imekusudiwa kwa mwendo, macho kwa kuona kwayo, mdomo ni kuchukua chakula
ndani, tumbo ni kukiyeyusha, ini ni kusindika lishe yake kwa kusambaza kwenye
sehemu mbali mbali za mwili baada ya chakula hicho kufanyizwa kuwa damu,
nyongo, maji ya tezi, belghamu, tundu za mwili zimekusudiwa kuondoa uchafu
mwilini na utaona kwamba kila kiungo, kimelinganishwa barabara kufanya kazi
zake maalum, kimefanyizwa kwa usanii kamili."
Nilisema, "Maulana! Baadhi ya watu huwamini
kwamba yote haya ni matokeo ya kazi ya maumbile - kila kiungo hujitokeza na
kuwepo kama na wakati kihitajiwapo na maumbile."
Yeye (a.s.) akasema, "Hebu waulize kama maumbile
yanayofanya kazi katika mpango mzuri namna hiyo na uzuri wa taratibu za umbo
vile vile huhitaji kuwa na elimu na uwezo au ni pasipo akili na sababu, bila
uwezo na bila elimu?"
Kama wakikubali kwamba inahitaji kuwa na elimu na
uwezo, kipi basi kinawazuia katika imani ya kuwepo muumba? Tunachosema ni
kwamba vitu vyote vimeumbwa na mmoja ambaye ni Bwana wa Elimu na Uwezo.
Wanasema kwamba hakuna Muumba na bado wanakubali kwamba Maumbile yamefanya hivi
kwa ustadi na mpango. Kana kwamba maumbile hayo ndiyo sababu ya kuumbwa kwao,
ambapo wanamkana Muumba. Kama watasema kwamba maumbile hufanya vitu kama hivi
bila ya elimu na uwezo - bila kujua inachokifanya wala bila kuwa na uwezo
wakukifanya katika uhusiano pamoja na aina na usanii na ustadi ule unaendelea
kuwamo katika mambo yote, inashangaza kwamba kitu kinaweza kufanywa bila
ulinganifu wa uwezo wa kukifanya na bila ya elimu ya kufanya hicho kitu. Kwa
hivyo ni wazi kwamba kitendo huanzia kutoka kwa Muumba mwenye kujua yote,
Ambaye amepanga kama njia ya pekee katika Uumbaji wake kutokana na Ujuzi wake,
ambao watu hawa huita Maumbile. Kwa maneno mengine Allah (s.w.t.) Ameamuru njia
ya kutengeneza kila kitu kutokana na sababu halisi na kanuni.
Kama kwa mfano, mbegu huhitaji maji kuchipua hakuna
mvua hakuna nafaka; mtoto anazaliwa kwa muungano na Mume na Mke, na bila mpago
huu wa muungano na kukutana kwa mbegu za uzazi; hakuna mtoto awezaye kuzaliwa;
maji hugeuka hewa kusababisha wingu, wingu hilo husukumwa na upepo huku na huko
na kuleta mvua; hakuwezi kuwepo na mvua bila taratibu hii.
Walahidi hawa huchukulia sababu hizi na maumbile kama
ndiyo Muumba haswa, wakikanusha kuwepo kwa Muumba juu ya yote haya. Hili ni
kosa la dhahiri, kwa kuwa maji hayana uhai, na mpaka yapatishwe uhai na mtoaji
wa uhai, vipi yatatoa nafaka?
Na inawezekana vipi manii isyokuwa na akili, igeuke
kuwa mtoto mchanga, ila itiwe nguvu na Mwenye Enzi zote Kuumba kichwa kutoka
sehemu moja, mikono na miguu kutoka sehemu zingine, mifupa kutoka sehemu
nyingine? Maumbo mengine ya uumbaji yanaweza kufikiriwa ipasavyo.
Hebu fikiria lishe isambazwavyo katika mwili, na
mpango wa kistadi uliomo ndani yake.
Hebu ona kwamba kifikapo tumboni, chakula
kinaratibiwa kuwa mseto wa matibabu na mseto huo unahamishiwa kwenye ini na
kapilari mororo zifanyazo kimia katika kiungo hicho.
Tumbo linageuzwa kuwa kama mrekebishaji kwa kuhamisha
vitu kwenda kwenye ini katika hali iliyo safishwa sana, kuzuia madhara katika
umbo hili laini.
Kisha ini huchukuwa mseto huo wa lishe ulioingizwa
ndani yake, na kwa ustadi usiofahamika huubadili kuwa damu ili kusukumwa na
moyo kwenda sehemu zote za mwili kwa kutumia mishipa ya damu, katika hali kama
ya mifereji ya kunyweshea ionekanavyo katika mabustani na mashamba kusambaza
maji kwenda sehemu yoyote ihitajikayo kunyweshwa.
Uchafu wote na sumu hutolewa na kupelekwa kwenye
viungo vilviyokusudiwa kutoa nje uchafu na sumu hizo, kama kibofu cha nyongo,
utumbo, tezi za jasho za makwapa na nyonga, na kadhalika. Jauhari ya nyongo
huenda kwenye kibofu cha nyongo, baadhi ya jauhari huenda kwenye bandama na
unyevunyevu huenda kwenye kibofu cha mkojo.
Hebu fikiria ustadi ambao umefanywa katika kuujenga
mwili! Uzuri ulioje uliounganishwa kwa viungo hivi! Jinsi mishipa (ya damu na
maji), utumbo na kibofu n.k. vimepangwa kukusanya uchafu wa mwili ili kwamba
kuuzuia kutokana na kutawanyika mwili wote na kusababisha magonjwa na uchafu.
Basi utukufu ni wake yeye ambaye ameumba viungo hivi
kutokana na mpango wneye sifa na ustadi. Sifa zote ni zake Yeye, Ambaye
anastahiki kwayo."
Nilisema. "Kunradhi Maulana! Nieleze kukua kwa
mwili kidogo kidogo, hatua kwa hatua mpaka kufikia ukamilifu wake."
Yeye (a.s.) akasema, "Hatua ya kwanza ya kukua
huku ni kijusu ndani wa mfuko wa uzazi - isiyooenekana kwa jicho na isiyofikiwa
kwa mkono. Kukua kwake hutokea kwa kasi, mpaka anakamilishwa katika mwili
pamoja na viungo vyote na sehemu kukamilika kwa kila jambo, moyo, ini, utumbo
na sehemu zote zifanyazo kazi, mifupa, misuli, nono, mishipa ya ubungo, mishipa
ya damu, mifupa laini n.k. vyote vimekuzwa kikamilifu.
Anaingia ulimwengu huu, na unaona jinsi anvyoendelea
kukua pamoja na viungo vyake katika uwiyano, wakati huo huo akihifadhi maumbo
yake yote bila ongezeko lolote au upungufu wowote. Hakuna mtengano wowote wa
sehemu, kuongezeka chochote katika nyama au kuondolewa chochote kilichozidi.
Mwili huendelea kukua, huku ukihifadhi umbo lake lililoumbwa vema, mpaka
kukomaa kwake, iwe muda wake wa uhai umerefushwa au kufupishwa mapema.
Je, si mpango wake wa maana sana na ustadi mzuri
uliosanifiwa na Msanii mweny kujua yote?"
Hebu fikiria ubora wa uumbwaji wa mtu juu ya wanyama.
Anasimama wima na kukaa sawa sawa kumuwezesha kushika vitu mikononi mwake,
kuvipata kwa viungo vyake, kufanya kazi kwa mpango. Kama mtu angekunjwa kama wanyama, asingeweza
kufanya kazi azifanyazo sasa.
Hisia tano za fahamu ni bora zaidi, tofauti na zile
za wanyama kwa maana ya hulka na ufanisi ili kwamba kumjaalia sifa maalum kwa
sababu hii.
Macho yamewekwa katika kichwa kana kwamba ni taa
iliyowekwa juu ya nguzo kumuwezesha kuona kila kitu. Hayakuwekwa katika sehemu
za chini za miguu kuilinda salama dhidi ya majeraha na ajali wakati wa kazi au
mwendo, ambao ungeweza kuyadhuru na kudhoofisha ufanisi wake.
Yangewekwa katikati ya sehemu ya mwili kama vile
tumboni, mgongoni au kifuani, ingekuwa vigumu kuyazunguusha au kuona vitu kwa
mgeuko wa haraka. Kichwa ni kivutio - sehemu bora kabisa kwa hisia hizi za
fahamu, pakufaa kulinganisha na kiungo kingine chochote.
Hisia hizi za fahamu ziko tano kwa idadi kujibu aina
zote za vichokoo na bila kukiacha kichokoo chochote kutogundulika.
Macho yamehulkiwa ili kutofautisha kati ya rangi.
Rangi zingelikuwa hazina maana bila kuwa na welekevu huu wa macho, kwa vile
rangi hizi zipo kwa njia ambayo kwamba vitu vyaweza kutofautishwa kutoka kimoja
na kingine, au macho hayo yangepata burudani kwayo.
Masikio yamewekwa katika kichwa kutambua sauti,
ambazo kwamba zisingekuwa na maana bila uwelekevu huu wa masikio. Kadhalika ni
sawa na hali ya hisia nyingine za fahamu - bila welekevu wa hisia ya fahamu ya
kuonja, vyakula vyote vitamu vingekuwa visivyokolea, bila hisia ya fahamu ya
kugusa, hisia ya joto, baridi, ulaini, ugumu, ingekuwa sawasawa tu kana kwamba
hazipo; na bila hisia ya kunusa, manukato yote yangekuwa kama kifu.
Na hivyo hivyo, kama kungekuwa hakuna rangi, macho
yangekuwa hayana nguvu. Bila sauti, masikio pia yasingekuepo. Hivyo hebu
fikiria jinsi ilivyoamrishwa kwamba kuna uafikiano wa dhahiri baina ya kiungo
cha hisia ya fahamu na hisia - kichokoo kuingiliana - kiutendaji kazi zao
kiuafikiano. Hatuwezi kusikia kwa macho yetu, wala kutofautisha rangi kwa
masikio yetu, wala kunusa ila kwa pua zetu, na kadhalika.
Kisha kuna vijumbe (media) viunganishavyo
vilivyowekwa kati ya kiungo cha hisia na kichokoo cha hisia, ambapo bila hivyo
kiunganisho (baina ya viungo) kisingewekwa. Kama kwa mfano kutokuepo nuru
kuinga'risha rangi, macho hushindwa kutambua rangi na bila hewa kufanya mawimbi
ya sauti, masikio yasingekuwa na uwezo wa kutambua sauti yoyote.
Basi yaweza kufichika, kutoka kwa ambaye amejaliwa na
akili nzuri na mtu ambaye hutumia akili yake sawa sawa, baada ya maelezo yote
haya niliyotoa kuhusu mwingiliano wa viungo vya hisia, hisia-kichokoo na
vijumbe (media) viunganishavyo kukamilisha hatima hii, kwamba kazi yote hii
imepangwa na kutekelezwa na mjuzi wa yote mwenye nguvu zoto Allah (s.w.t.).
Yawezekana utratibu huu, ustadi huu utokee to
wenyewe? Vipi maumbile yenyewe yataweza kufahamu namna gani jicho au sikio
liumbwe, na kazi zipi kila kimoja izifanye na kijumbe (medium) gani kitakifaa
kila kimoja kama njia kwa mfungano sahihi ili kukiumba kila kimoja?
Je, ni yenye kuwazika katika maumbile yasiyo na
akili, isipokuwa Msanii Mwenye nguvu zote avipangilie juu ya Msingi wa ujuzi wa
Mwenye kujua yote?
Hebu fikiria hali ya mtu ambaye amepofuka macho yake
na hasara anayopata katika kazi zake za kila siku. Hawezi kufahamu pa kuweka
mguu wake, iwapo miguu yake itaangukia katika bonde katika muinuko, wala hawezi
kuona mbele, wala kutambua rangi, wala hawezi kufahamu uso wa furaha au
wakuchukizwa. Hatakuwa na uwezo wa kujua penye shimo, wala kujua adui na upanga
(mkononi) uliofutwa, wala hawezi kufanya kazi yoyote ya mikono kama kuandika,
biashara au utengenezaji wa kipambo kidogo. Ubongo wake hudokeza njia fulani
kumuwezesha kutembea huku na huku au kula chakula chake, ambapo bila hivyo
angelikuwa sawa na jiwe lililotulia.
Kadhalika ni sawa nahali ya mtu mwenye kasoro katika
kusikia. Hupata hasara juu ya mambo mgeni. Hana furaha ya kusema katika
maongezi, wala fahamu ya kuhisi sauti ya kupendeza au mbaya. Watu wanapata tabu
ya kuongeya naye, hujichukia mwenyewe. Ingawa yu hai, yuko kama aliyekufa kwa
upande wa kuongea. Ingawa yupo, bado ni kama mtu aliye mbali sana asiye na
habari za aina yoyote.
Mtu asiye na akili ni mwenye hali mbaya sana kuliko
ng'ombe, kwani hata ng'ombe hutambua mambo mengi yasio na maana kwake. Je,
huoni kwamba viungo hivi, mambo haya akili hizi na kila kitu kingine
kihitajiwacho kwa marekebisho yake na ambapo bila hivyo yuko katika hasara
kubwa katika hali ya ukamilifu wa kuumbwa kwake, amevipatiwa ipasavyo?
Je, vyote hivi vimetengenezwa bila uwiyano, owezo na
elimu? Hakika sivyo! Kiumuhimu hivi ni matokeo ya Usanii halisi na mpango wa
Msanii Mwenye nguvu zote."
Niliuliza, "Maulana! Vipi inakuwa kwamba baadhi
ya watu wanapungukiwa katika viungo hivyo na mambo hayo na wanapatwa na hasara
hizo ambazo umezieleza?"
Yeye (a.s.) akasema: "Ni kwa ajili ya ukumbusho
kwa mtu aliyepungukiwa viungo na watu wengine hali kadhalika.
Mfalme anaamrisha raia zake katika njia za namna hii,
amri kama hiyo haichukiwi, bali inafurahiwa kwa hila na kusifiwa.
Watu hao ambao wameumizwa hivyo watafidiwa baada ya
kufariki, maadamu ni wenye shukurani kwa Allah (s.w.t.) na kugeukia kwake
kiukarimu hivyo kwamba shida zote walizopata kutokana na upungufu wa viungo
hivyo kuonekana duni katika ulinganifu (kwa fidia walizopata). Kiasi kwamba
kama baada ya kufariki watapewa nafasi ya kurudi tena kwenye shida hizo,
wangeikaribisha fursa hiyo ili kupata fidia kubwa zaidi.
Hebu fikiria ustadi na usanii uliooanishwa katika
msingi wa Uumbaji wa viungo na maumbo katika jozi au kitu kimoja. Hebu fikiria
kichwa ambacho kimeumbwa ni kitu kimoja na hii si kwasababu nyingine, bali
kuweka kwa kusudi fulani tu, kisiwe kimeumbwa kwa zaidi ya kitu kimoja. Kichwa
cha pili ingekuwa ni ongezeko la uzito tu, usio na umuhimu kabisa, kwa kuwa
kichwa kimoja hukusanya hisia zote za fahamu zihitajiwazo kwa mtu. Vichwa
viwili ingekuwa na maana ye sehemu mbili za watu. Hivyo kama angetumia kimoja
kuzungumzia, kingine kingekuwa hakina kazi. Kutumia vyote kwa pamoja kwa
mazungumzo hayo hayo kusingekuwa na maana yoyote kwani hakuna kusudi la zaidi
lipatikanalo kwayo.
Mtu angekuwa amekwazishwa mno katika shughuli zake
anazopaswa kufanya, kama angaliumbwa na mkono mmoja badala ya miwili.
Je, huoni kwamba fundi seremala au fundi mwashi
angeshindwa kuendelea na kazi yake kama mmoja wa mikono yake umepooza?
Na hata kama angejaribu kufanya kazi yake kwa mkono
mmoja hawezi kuifanya kiustadi na kiufanisi kama ambavyo angefanya kwa mikono
miwili.
Hebu fikiria sauti ya mtu na mazungumzo, na kuumbwa
kwa viungo vinavyohusika na hii sauti. Kongomeo, ambalo hutoa sauti ni kama
mrija ambapo ulimi, midomo na meno hutengeneza sauti kuwa herufi na maneno.
Je, huoni kwamba kibogoyo hawezi kutoa sauti ya erufi
ya 'S', ambaye midomo yake imekatwa hawezi kutamka 'F', ambapo ulimi mzito
hauwezi kutoa sauti ya 'V'? Zumari hufanana mno nalo (hilo kongomeo). Kongomeo
hufanana na Mfuko ambamo hewa hupulizwa humo, kulingana na mapafu yenye hewa.
Misuli inayowezesha mapafu kutoa sauti hufanana na
vidole vinavyo bonyeza hewa ya mfuko kwenda kwenye bomba. Midomo na meno ambayo
hutengeneza sauti kuwa herufi na maneno hulingana na vidole katika tundu
zabomba na kutoa muziki na wimbo.
Kongomeo hapa linachukuliwa kuwa sambamba na zumari
kwa njia ya maelezo, ambapo kwamba kiuhakika zumari ni ala (ya muziki)
iliyotengenezwa katika mfano wa kiungo cha asili, kongomeo.
Viungo vya kunena vilivyo fafanuliwa hapa, yatosha
kuwa mfano sahihi wa herufi. Iwayo yote, viungo hivi, matumizi mengine
yamefanyizwa anwani na hivi. Kongomeo kwa mfano, limebuniwa hivyo kuingiza hewa
safi kwenye mapafu kwa kusambaza kwenye damu na moyo, ambapo kama likishindwa
hata kwa muda mdogo tu, ingeleta kifo.
Ulimi umefanyizwa kutofautisha kati ya mionjo
mbalimbali ya vyakula kimoja kutoka kingine, kitamu kutoka kichungu, kichungu
halisi kutoka kitamu, kichungu cha chumvikutoka kitamu. Ulimi vile vile
husaidia kuhisi uzuri wa maji na chakula. Meno hutafuna chakula kuwa laini
vyakutosha kuyeyushwa. Vilevile huzuia midomo kubonyea ndani ya kinywa.
Kibogoyo anaonekana kuwa na ndomo iliyolegea. Midomo husaidia kunyonya maji
ndani, hivyo kuruhusu kiasi cha kufaa kuingia tumboni kama yahitajiwavyo, sio
kuvimbiza kwa kulingana kwake na kuleta kusongwa roho katika koo, au kuacha
uvimbe kwa baadhi ya vitu vya ndani kwa uwezo wa kutiririka kwake kwa nguvu.
Zaidi ya hapa, midomo miwili inafanya kazi, kama mlango kuweka mdomo kufunga
upendapo. Tumekueleza namna mbali mbali za matumizi yaliyofanywa na hiyo midomo
na ulimi na matokeo ya faida (za kimaumbile) kutoka kwayo, kama vile chombo cha
aina moja kiwezavyo kufanya miradi tofauti. Kwa mfano shoka ambayo fundi
seremala anaweza kuitumia na ambayo yaweza kutumika kuchimba ardhi na kwa
matumizi mengine.
Kama ukiangalia kwenye ubongo, utaona umefunikwa
katika ngozi nyembamba moja juu ya nyingine kuuhifadhi kutokana na madhara na
mtikisiko. Fuvu la kichwa huuhifadhi kama kofia ya chuma dhidhi ya kuvunjwa
vipande pande kwa kugonga au mshindo kwenye kichwa. Fuvu limefunikwa na nywele
kama mfuniko wa manyoya ya kondoo kuulinda salama dhidhi ya joto na baridi.
Nani, basi, isipokuwa Allah Mwenye Nguvu zote
ameujalia ubongo na usalama huo na kifuniko, na ambaye amekifanya ni asili ya
hisia za fahamu, na ambaye amefanya mipango kwa hifadhi yake ya ajabu katika
kulinganisha na sehemu nyingine zote za mwili kwa sababu ya kiwango cha umuhimu
wake katika uwelekevu wa mwili?
Hebu fikiria ukope, jinsi ulivyoundwa kama pazia la
jicho pamoja na kope zake kama kitani, kwa kunyanyulia na kuteremshia pazia.
Hebu angalia mboni ilivyowekwa kwenye tundu ikifunikwa na kivuli cha pazia na
nywele.
Nani ameustiri moyo ndani ya kifua na kuufunika na
pazia ambalo mnaliita utando? Nani aliyepanga hifadhi yake kwa njia ya mbavu,
misuli na nyama zilizosokotwa katika njia ambayo ni ya kuzuia kitu chochote
kisiingie ndani yake na kusababisha mchubuko? Nani aliyezifanyiza tundu mbili
katika koo, moja kwa utoaji wake wa sauti imewekwa kwa ukaribu na mapafu na
niyingine inaitwa umio inaelekea kwenye tumbo kwa upitishaji wa chakula. Na ni
nani aliyeyweka kilango, kimio, (kidaka tonge) juu ya tundu inayoelekea kwenye
kongomeo, kuzuia chakula kuingia kwenye mapafu, ambacho kingesababisha kifo
kama kama isinge dhibitiwa hivyo? Nani aliyefanya mapafu kupuliza hewa kwenye
moyo pasipokuchoka bila kupumzika kuondoa sumu ambazo vinginevyo zingeuaribu?
Nani aliyetengeneza misokoto ya misuli, izuiyao mkojo
na kinyesi kutoka nje, kama vigwe vya mfuko, kufunguliwa au kufungwa kwa
kupenda sio kuchurizika wakati wote wenyewe, na kuwa matokeo ya udhia wa kudumu
katika maisha? Kadhalika kuna mambo
ambayo kadiri ingekadiria, lakini mengine ambayo mtu hana elimu nayo, yako
mbali na ukadiriaji. nani amejaalia kunepa huku kwa misuli ya tumbo ambalo
limeamrishwa kuyeyusha chakula cha ukakasi? Na ni nani aliyeifanya ini laini na
mororo kupokea lishe iliyochujwa na katika hali ya kusfishwa sana na kufanya
kazi kwa uborazaidi kuliko tumbo? Yawezekana kazi zote hizi kufanywa na yoyote
isipokuwa na Mwenye Enzi yote Mwenye Nguvu zote? Unaweza ukufikiria kwamba yote
haya yaweza kufanywa na maumbile mfu? Hakika sivyo! Vyote hivi ni mpango wa
Mwenye nguvu zote msanii Mwenye Enzi zote, ambaye ana elimu iliyojaa na ana
ukamilifu wa Enzi zote kabla ya uumbaji. Yeye ni Allah, Mjuzi wa yote Mwenye
nguvu zote.
Hebu fikiria kwa nini ute mororo wa mfupa ulivyowekwa
kwa hifadhi ndani ya Mirija ya mfupa - kwa ajili tu ya kuuhifadhi dhidhi ya
kuharibika kwa kuathiriwa na joto la jua ambalo linge uyeyusha, au kule
(kuathirika) kwa baridi ambako kungeufanya ugande, ambapo maisha yangeangamia -
ute wa mfupa ni kichanganyiko muhimu cha asili kitoleacho nishati kwa mahitaji
ya mwili.
Na kwa nini huu mzunguko wa damu umewekwa katika
mishipa ya damu, isipokuwa ni kwamba ifanye kazi ndani ya mwili na sio
kutiririka nje? Kwa nini hizi kucha zimewekwa kwenye vidole isipokuwa ni kwamba
ziweze kuvihifadhi dhidhi ya madhara, na kusaidia katika ufanisi mzuri, kwani
bila kuwa nazo, kuwepo kwa nyama peke yake kusingemuwezesha mtu kuokota kitu
kwa kufinya kutumia kalamu kwa kuandika au kuweka uzi kwenye sindano?
kwa nini sikio limewekwa sehemu nyingi kama nyumba ya
jela, isipokuwa ni kwamba sauti zingechukuliwa kwenda kwenye utando (ngoma ya
sikio) kwa utambuzi bila madhara kwalo kwa mshindo na mgongano wa hewa?
kwa nini nyama hizizisokotwe juu ya nyonga na matako
ya mtu, isipokuwa ni kwamba, asipate kutaabika kwa ugumu wa sakafu katika kukaa
kama ilivyo kwa mtu mwembamba na mwenye umbo lililodhoofika, mpaka kitu kiwekwe
kati yake na sakafu kupunguza ugumu, kama mto au tandiko?
Nani aliyeumba taifa la kibinadamu kama mwanaume na
mwanamke? Ni Yeye Ambaye ameamrisha taifa kustawi kwa njia ya muungano wa
jinsia mbili au iwayo yote kudumisha wingi wa nguvu zake kwa njia wa
utofautishaji wa jinsia hizo mbili.
Na ni nani aliyemfanya kuwa yeye ni Mzazi wa kizazi?
Kwa hakika ni Yule Ambaye alitia tumaini ndani yake. Isingekuwa shauku hii
kusuka suka kifua chake, kwa nini kuwe na chagiza (hamu ya ndani) ya wao kwa
wao kuungana. Tizama uzazi wa vitu vinavyoishi kati yao ambavyo havikuwekwa
ulazima (wa kuzaa) kwa muungano na kijinsia, lakini huletwa kwa hatua fulani ya
kukua ya uke. Havina utofautishaji wa ume na uke kabisa. Je, yawezekana mtu
yoyote, kwa mfano, kueleza kati ya ume na uke wa nyigu?
Nani aliyempa yeye (mtu) viungo kwa kufanya kazi?
Hakika ni yule ambaye amemfanya (kuwa) mfanya kazi. Na ni nani aliyemfanya
mfanyakazi? Hakika ni yule ambaye ameuumba kuwa mhitaji kwani mtu asingelifanya
kazi kama hanahaja ya kukidhi. Kama asinge kuwa na haja kukidhi njaa yake, kwa
nini ajitaabishe, kwa nini ajitie katika shighuli na utendaji. Angelikuwa hana
haja ya kulinda nwili wake salama dhidhi ya joto na baridi, kwa nini impase
kujifundisha kushona, kutengeneza sindano,kusokota nyuzi, kufuma, ukulima wa
pamba na kadhalika. Na kutowepo kwa yote haya, ni matumizi gani yangelikuwa kwa
viungo vya kufanya kazi na vidole? Na ni nani aliyemuumba yeye fukara? Hakika
ni Yule Ambaye ameumba kwa ajili yake hali ya ufukara. Na ni nani aliyemuumba
kwa ajili yake hali ya ufkara? Hakika ni Yule Ambaye amejichukulia juu yake
mwenyewe jukumu la kumpatia mahitaji.
Nani amemjaalia yeye (mtu) kuwa na akili? hakika ni
Yule Ambaye amefanya malipo na adhabu kama kanuni kwa ajili yake.
Asingelihitaji akili kama asingelipasika kwa malipo na adhabu. Mwenye Nguvu
zote Muumba amemjalia yeye kuwa na akili ili kutofautisha kati ya jema na ovu,
Akiwa ameamua juu ya malipo na adhabu kama kanuni kwa ajili yake kupata malipo
kwa wema na adhabu kwa uovu. Viumbe hai ambavyo havipasiki malipo na adhabu
havina hisia ya jema na ovu, wala havijui kutofautisha baina ya haramu na
halali, na aina ya matendo yaliyokatazwa na yaliyo ruusiwa. Walakini hutambua
mambo yahitajiwayo nao kwa ajili ya kuishi kwa jamii yao au kiupweke. Kama kwa
mfano, ndege anayo lazima ya kutambua kwamba (yeye) ndege ni mawindo ya tai, na
hivyo kumuona kwake tu, humfanya aruke kwa kasi, au kulungu hujua vizuri kwamba
simba angemchanilia mbali, hivyo kule kumuona kwake tu, hukimbia kuokoa maisha
yake.
Nani aliye mjalia kuwa na maarifa na fahamu? Hakika
ni Yule Ambae amembariki yeye kwa nishati. Na ni nani aliye mbariki yeye kwa
nishati? Hakika ni Yule Ambaye ameamuru uthibitisho wa kuongoza juu yake. nani
anamsaidia yeye katika shughuli zote hizi ambazo kwayo mipango yake hushindwa?
hakika ni yule, ambaye anastahili shukurani zetu za juu mno.
hebu fikiria mambo niliyo kwisha kukuelezea. Je,
yawezekana kuwepo na mpangilio na taratibu kama hizi bila ya kuwepo upangaji?
Hakika sivyo! Allah Mwenye Nguvu zote yu mbali na ametukuka juu ya mambo
wanayoyasema watu hawa.
Iwapo ungeona ubao mmoja wa mlango ukiwa na komeo
lililokazwa juu yake. Je, unaweza kufikiria kwamba limefungwa hapo bila ya
kusudio lolote? Hakika utatanabahi kwamba liko pale kuunganishwa kwenye ubao
mwingine kwa faida ya dhahiri. Kadhalika utaona kiumbe wa kiume kama mmoja
katika jozi kimeumbwa kwa ajili ya kiumbe mwanamke kwa muungano kuendeleza
taifa.
Allah (s.w.t.) awaangamize wale ambao wanadai kuwa ni
mafilosofa, lakini ni wadhaifu wa kuona katika kuyaendea maajabu haya ya
uumbaji na hulka ambazo wamezikana katika uumbaji wa ulimwengu, usanii wa
Msanii mwenye Nguvu zote na Kupenda kwa Bwana Mpangaji.
Hebu tizama kwa macho ya uheshima katika fadhila
kubwa ya Allah Mwenye nguvu zote katika kutulia kwa taabu baada ya kula chakula
na kinywaji. Je, huu siyo uzuri wa mpango katika ujenzi wa nyumba kwamba choo
chapaswa kuwa sehemu iliyotengwa kwa hii nyumba?
Katika njia kama hiyo, Allah Mwenye Nguvu zote
ametengeneza tundu kwa ajili ya uchafu utokao katika mwili wa mtu katika sehemu
ya faragha. Siyo katika uwazi wala
haikujitokeza, bali imewekwa hivyo kwa kufichika kikamilifu kwa
muunganiko wa nyonga na matako na nyama zao. Wakati mtu anataka kukidhi haja na
akawa katika hali ya kuchutama, tundu huruhusu uchafu kutoka.
Hebu fikiria seti ya meno katika kinywa cha mtu,
baadhi ni makali, ambayo huchanja na kupasua chakula. Mengine ni butu ambayo
utafuna na kufunda. Kwa vile aina zote zinahitajika, amepatiwa ipasavyo.
Hebu fikiria na tambua ustadi uliomo ndani kwa nini
ni sahihi kunyolewa nywele na kucha kupunguzwa. Zinakua na kuongezeka na hivyo
huhitaji kukatwa. Kwa ajili hiyo hazina hisia kuepusha maumivu kwa mtu. kama
kukata hivyo kungesababisha maumivu, ima zingeachwa zikue bila mpangilio na
kuwa mzigo wa kuudhi, au ingelitia maumivu katika kukatwa."
Niliuliza, "Maulana! Kwa nini zisirekebishwe
bila ya kutononeka kufikia kwamba kukatwa kwao kuwe lazima?"
Yeye (a.s.) alisema, "naam, ziko baraka zisizo
na idadi za Allah Mwenye Nguvu zote kwa Viumbe vyake zifahamikazo kwao, na
ambazo kama wangelizijua, wangeshukuru kwayo.
Elewa kwamba matatizo na maradhi ya mwili yanatulizwa
kwa njia ya nywele hizi zitokazo nje ya vinyweleo. Vidole hupata nafuu ya
maradhi yao kupitia kwenye kucha. hiindiyo sababu ukataji wa kucha kwa juma,
kunyoa kichwa na kuondoa nywele zilizozidi lazima kufanywe, ili kwamba kucha na
nywele ziweze kukua haraka na kutuliza maradhi na matatizo, kama sivyo, maradhi
hubaki yamezuiwa mwilini kufuatiwa na maumivu na magonjwa.
Hakuna ukuaji wa nywele uanoruhusiwa kwenye sehemu za
mwili ambako zingeleta madhara kwamtu. Kama nywele zingeota ndani ya macho
angepofuka. kama zingeota ndani ya kinywa, je, maji na chakula visingezuiwa?
kama zingeota kwenye matumbo ya viganja vya mikono, je, zisingepunguza uwezo wa
hisia ya kugusa na hali hiyo isingeingilia ufanyaji sahihi wa kazi nyingi na
utambuzi wa ugusaji halisi?
Kuna ustadi mkubwa uliomo ndani kuweka sehemu
makhsusi za mwili bila nywele. Je, maumbile yangeweza kuwa na utambuzi wa
busara nzuri au mipango ya usanii huu mzuri ingeweza kuhusishwa na haya
maumbile?
Msiba uwapate walahidi hawa na upumbavu wao. hii
habari ya uumbaji, na tizama ilivyo kosa na madhara kwa hayawani na manyama
wengine, ambao uzazi wao hutegemea ngono, wanafananishwa hivyo hivyo.
Unaona kwamba miili yao yote imefunikwa na nywele,
isipokuwa sehemu maalum kwa sababu hizo hizo. hivyo fikiria habari hii ya
uumbaji na tizama jinsi gani njia za makosa na madhara zilivyoepukwa ambapo
maadili na faida vimewekwa salama.
Wakati wafuasi hawa wa mani na wale wa namna yao walipojaribu
kukana imani hii katika uumbaji wa kimadhumuni, waliona kosa la uotaji wa
nywele katika kinena na makwapa. Walishindwa kufahamu kwamba kuota huko
kumetokea kwa sababu ya unyevunyevu unaochuruzika kwenye sehemu hizo. nywele
hizo huota pale kama vile majani yaotavyo katika sehemu ambayo maji
hujikusanya. Je, huoni namna gani sehemu zinavyotayarishwa kwa kukusanya uchafu
na kuuzuia?
bado busara nyingine iliyomo ndani yake, ni kwamba,
inaondoa udhia mmoja zaidi mtu engediriki, kuhusiana na mwili wake, na yeye ni,
mbali na hayo, kwa vile ameshughulishwa na usafi wa mwili wake na uondaji wa
nywele zake, kazuilika kufanya matendo ya uchoyo, ukatili, kiburi na ufedhuli,
ambayo kwamba hangepata fursa ya kuyafanya.
Hebu fikiria mate katika kinywa na ona hekima iliyomo
ndani yake. Yamefanyizwa hivyo ili kuhakikisha mchirizi wa kudumu kuweka unyevu
katika koo na kaa la kinywa siyo kuruhusu ukavu kwayo ambao ungesababisha kifo.
Bila hayo chakula kisingeweza kutafunika wala kisingemezeka. Yote haya ni wazi
na kuthibitishwa kwa uchunguzi. Na elewa kwamba maji haya chimbuko lake
nikutokana na chakula na yakifika ndani husaidia kazi ya nyongo.
Baadhi ya wabishanaji wajinga na wadai wenye akili
pungufu katika filosofia, kwa sababu ya uelewaji wao wenye kasoro na elimu
potofu, wamesema, "Ingelikuwa vizuri zaidi kama tumbo la mtu lingekuwa
kama joho kumuwezesha daktari kulifngua apendapo, kuangalia vitu vyake vya
ndani na kuingiza mkono wake ndani kwa ajili ya matibabu, na sio kama jinsi lilivyo
(kuwa na ukuta wa nyama na ngozi), limefichwa ki-ajabu kwa kuonekana na macho
na kufikiwa na mkono. Magonjwa ya ndani yanaweza tu sasa kupimwa kwa dalili za
ugonjwa kwa uchunguzi wa mkojo, mapigo ya mishipa na kadhalika, ambapo haziko
katika kosa na shaka kufikia kwamba kosa kama hilo katika uchunguzi wa mapigo
ya mishipa na mkojo laweza kusababisha kifo.
Lau kama wangejua wadai hawa wajinga katika Filosofia
na washindani, kwamba ingeondoa hofu yote ya ugonjwa na kifo. Basi mtu angepumbazika na maisha yake ya
umilele na ya siha nzuri, ambayo yangemfanya kuwa mkaidi na mwenye
majivuno. Tumbo lililo wazi lingeruhusu
mchuruziko wa daima wa unyevunyevu, hivyo kuharibu kikao chake, kitanda na
mavazi yake mazuri; kwa ufupi, maisha yake yote yangekuwa katika hali hizo.
Tumbo, ini na moyo hufanya kazi sawasawa kutokana na
joto muhimu, ambalo lingeathiriwa na hewa ya nje ipitayo kwenye tumbo
lifanyiwalo matibabu, lililowazi lionekanalo na jicho na kufikiwa na
mkono. Hii ingesababisha kifo.
Huoni kwamba udhanifu wote juu ya asili ya kweli ya
uumbaji na muundo usio na maana ni wa upuuzu?
Hebu fikiria jambo la kulisha, kupumzika na ngono,
ambavyo vimeumbwa kwa ajili yake na manufaa yaliyomo ndani yao. Kila kimoja katika hivyo kinasukumiwa
tamanio, ambalo husababisha hamu na msisimko kwayo. Njaa huhitaji chakula ambacho huleta uhai na
nishati katika mwili na uimara wake.
Usingizi huhitaji kupumzika kwa ajili ya afya ya mwili kuondoa uchovu.
Kama mtu angekula chakula kwa ajili tu ya mahitaji ya
mwili wake bila tamanio kutoka ndani limlazimishalo kula, inawezekana kwamba
angeupa mwanya ulegevu kwa sababu ya uchovu au shinikizo, mwili wake
ungedhoofika na kusababisha kifo, kama vile mtu aachavyo kunywa dawa ambayo
ndiyo pekee ahitajiayo kustawisha hali yake.
Na hii ingesababisha kifo chake.
Kadhalika angeacha usingizi kwa ulegevu na kwa hiyo
kudhoofisha mwili wake, kama angekusudia tu kwa sababu hii ya kupumzika kwa
ajili ya mwili wake na uondoshaji wa uchovu wa viungo vyake. Kama kuzaa kungekuwa ndiyo lengo pekee la
muungano kwa jinsia isingekuwa yamkini kwa upande wake kuzembea, na kutokea
kupungua kwa idadi ya watu na mwisho wa kukoma kwao, kwani kuna watu hawana
hamu ya kuwa na Kizazi (Watoto) wala haja yoyote kwayo.
Angalia, basi
kwamba tendo lile lile linalohusu siha ya mtu na ustawi limetiliwa nguvu
kwa tamanio lishurutishalo lililowekwa ndani yake katika asili yake
likimwongoza kwayo.
Na elewa kwamba umbo la mwili lina Stadi nne :-
(1) Stadi ivutayo - Hii hupokea chakula na kukisukuma
ndani ya tumbo.
(2) Stadi ya kuhifadhi - Hii hukihifadhi chakula kwa ajili ya kufanyiwa
taratibu za kawaida juu ya chakula hicho.
(3) Stadi ya kugeuza - Hii hufanya chakula kutoa
mseto wake ili kuusambaza katika mwili.
(4) Stadi ya kuondosha - Hii huondoa uchafu baada ya
Stadi ya kugeuza kukamilisha kazi yake.
Hebu fikiria mrekebisho huu uliofanywa mwilini baina
ya Stadi hizi nne. Hizi zimefanywa
kutosheleza mahitaji ya mwili kama sehemu ya Usanii wa Mwenye Kujua Yote.
Bila Stadi ya kuvuta, angewezaje kukitumia chakula
hicho ambacho ni muhimu kwa ujenzi na ustawi wa mwili wake?
Bila Stadi ya kuhifadhi, vipi chakula hicho
kingehifadhiwa tumboni kwa kuyeyushwa?
Bila Stadi ya kugeuza, vipi chakula kingetengenezwa
kupata mseto kwa kusambazwa mwilini bila usumbufu?
Na bila Stadi ya kuondosha, vipi uchafu, uliotolewa
na tumbo ungeweza kuondoshwa kila wakati?
Je, huoni jinsi Mtukufu Mwenye Nguvu zote Allah
Ameamuru na kuzipanga Stadi hizi kwa ajili ya kazi na
sharti la kuleta Afya ya mwili kwa kutimiza Ufundi wake na Enzi Kuu ya Mamlaka?
Hebu ngoja tuonyeshe kwa mfano. Hebu chukulia mwili kama Ikulu ya Kifalme, pamoja na watumishi wake na jamaa
wakaao humo. Wako wafanya kazi
wakihusika na uendeshaji wake. Mmoja wao
amepewa jukumu la kuleta vyakula kwa jamaa.
Wa pili amepewa jukumu la kukihifadhi ili kiweze kuwekwa kwa
kubadilishwa kuwa lishe. Wa Tatu ni
mwenye kukitengeneza na kukisambaza. Wa
nne kufagia uchafu ulioachwa.
Mfalme wa Ikulu hiyo ni Mwenye Kujua Yote, Mwenye
Nguvu zote, Mola wa Ulimwengu Wote.
Ikulu ni Mwili wa Mtu, jamaa ni viungo vya mwili, ambapo Stadi Nne zile
ni Wafanyakazi.
Huenda, pengine, ukafikiria maelezo niliyoyatoa
kuhusu Stadi hizi nne na kazi zao kama nyingi mno zisizo na umuhimu. Bado maelezo yangu hayafuati mpango wa Vitabu
uliotolewa na Madaktari, wala 0mahadhi ya mazungumzo yangu hayafuati ya kwao,
Watu hao wamezitaja Stadi hizi nne katika msingi wa kwamba unahitajika katika
fani ya uganga kwa ajili ya kuponyesha.
Tunautaja kutoka mtizamo wa hitaji lake la kuimarisha imani na
matengenezo ya watu vichwa ngumu, kama yalivyo maelezo yangu machache yenye
ufafanuzi mpana na mfano, kuonyesha Usanii wa Mwenye Kujua Yote.
Fikiria juu ya Stadi zilizowekwa ndani ya nafsi ya
mwanadamu na jinsi zilivyopangwa katika kuelewa, kuamua, kudhania, kuhoji,
kukumbuka n.k. Ingekuwa vipi hali ya mtu
kama angenyimwa Stadi ya kumbukumbu, na kwa kiasi gani mambo yake ya maisha
yangevurugika - mambo yake ya kiuchumi, na biashara yake. Asingekumbuka anachowiwa na watu wengine na
anachowia wengine. Maafikiano ya bei
aliyofanya, alichosikia na alichosema:-
Asingekumbuka aliyemfanyia tendo jema na aliyemtendea
tendo ovu, na kipi kilichomnufaisha na kipi kilichomdhuru. Asingekumbuka njia aliyopita mara
nyingi.
Asingekumbuka kitu chochote hata kama angeendelea
kujifunza Sayansi maisha yake yote, wala asingeliweza kuamua juu ya itikadi au
imani, wala kuweza kulinganisha kitu kimoja na kingine kwa muafaka. Kwa kweli, angeliambuliwa nje ya utu moja kwa
moja. Hebu ona faida iliyoje ya Stadi
hizi kwa mtu. Ukiziacha nyingine, hebu
fikiri juu ya moja na nafasi ichukuayo katika maisha yetu.
Hata fadhila kubwa zaidi ambayo kumbukumbu ni yenye
usahaulifu, bila huo mtu hangepata faraja katika huzuni yoyote, wala daima hangeondokana na maudhi, wala
ansigeondokana na uovu. Angeshindwa
kupendezwa na chochote katika vitu vya ulimwengu huu, kwa sababu ya kumbukumbu
za huzuni zenye nguvu, wala kamwe hangekubali tumaini lolote la kudhoofisha nadhari
ya Mamlaka yake ya husuda ya wenye kuhusudu.
Je, huoni
jinsi Stadi zikinzanazo za kumbukumbu na usahaulifu zilivyoumbwa ndani ya mtu,
kila moja imeamrishwa kwa lengo maalum?
Na watu wale, kwa mfano wafuasi wa Mani, ambao
huamini katika Waumbaji wawili tofauti wa ulimwengu wote hawawezi kwa njia
yoyote kutegemewa kufikiria vitu viwili tofauti kama waumbaji wa Stadi hizi
mbili tofauti, kwani stadi hizi mbili zinazo faida ambazo unaziona kutokana
nazo.
Hebu fikiria ubora ambao kwamba mtu peke yake
amejaaliwa na hakuna kiumbe kingine ashirikianae nao (huo ubora) - Stara. Bila hiyo (Stara), hakuna mtu ambaye
angeonyesha ukarimu kwa mgeni, wala yoyote kuweza kutekeleza ahadi yake, wala
haja ya mtu yoyote kuweza kutekelezwa, wala wema wowote kupatikana. Kuna Wajibati nyingi zinafanywa tu kwa Stara. Yule ambaye anaacha Stara, hakiri haki za
wazazi wake, wala wajibati za ndugu wa
damu, wala kuheshimu dhamana yake, wala kuepuka ufedhuli.
Je, huoni jinsi yote haya yalivyo jaalia katika mtu
kiukamilifu hivyo ili kumnufaisha yeye na kukamilisha mambo yake?
Fikiria baraka ya uzungumzaji ambao kwamba amejaaliwa
na Allah Azza wa Jallah, ambao ni chombo cha kuelezea wazo lake la ndani
(moyoni) na hisia zake kunjufu zichipukazo kutokana na fikira yake na ambao kwa
huo pia huelewa maana za ndani za wengine.
Bila Stadi hii angelikuwa kama wanyama wa miguu minne si wa kuweza
kupeleka wazo lake mwenyewe la moyoni kwa wengine wala kuelewa maneno ya
mzungumzaji.
Na hivyo ndivyo ilivyo katika fani ya uandishi ambayo
ni njia ya kujua habari za watu waliopita na kwa kuwafikishia wale wote waliopo
kwa vizazi vijavyo. Kutokana na fani
hiyo hiyo, mafanikio ya Sayansi na maandiko yanahifadhiwa katika vitabu kwa
muda mrefu. Kutokana na fani hiyo hiyo,
huhifadhiwa mijadala na taarifa kati ya mtu mmoja na mwingine. Bila fani hii, muda mmoja
usingelijulikana kabisa kutoka mwingine;
wala zisingepatikana habari zozote kutoka kwa wale walio mbali na nchi zao.
Sayansi pia zingetoweka. Taarifa juu ya uadilifu na uungwana
zingelipotea na madhara makubwa katika mambo ya mwanadamu yangelitokea kama
vile pia katika mafundisho ya dini na simulizi, ambayo watu huhitaji kujua na
elimu hiyo ingekuwa isiyowezekana.
Pengine ungefikiria kwamba, hoja hii imetimizwa na
mtu kwa msaada wa kubuni kwake mwenyewe na akili zake. Hairithiwi katika maumbile ya mtu. Na hali ni hiyo hiyo katika kuzungumza na
lugha, kwani hili pia ni jambo la istilahi na azimio, huamuliwa na watu
kufuatana na maafikiano yao ya kuelewana katika kuzungumza. Hivyo ndiyo sababu makundi tofauti yana lugha
tofauti na maandishi yao, kwa mfano, Kiarabu, Kishamo, Kiebrania, Kirumi n.k.;
ambayo kila moja ni tofauti na nyingine, kila moja ikiwa imeamua juu ya
istilahi zake yenyewe ya lugha na maneno.
Kwa ambaye anafanya dai kama hilo, jibu litakuwa
kwamba ingawa katika mambo yote haya kupanga kwa mtu na kutenda kume changia
katika lengo, bado njia ambazo kwayo kupanga kwake na kutenda kumefikiliza
lengo, ni kipaji katika ukarimu wa Allah Azza Wajalla uliyomo kwayo. Iwapo asingetunukiwa mahadhi ya kuzungumza,
au akili isingeliwekwa juu yake kumwongoza katika harakati hizo, asingelikuwa
na uwezo wa kuzungumza, na kama asingebarikiwa
kuwa na Kiganja na vidole, kamwe isingeliwezekana kwake kuandika. Na huo ni msingi uliowekwa na Mwenye Nguvu
zote Muumbaji na Asili ya Maumbile ya mtu kama fadhila maalum, kwa fadhila hiyo
yoyote mwenye kushukuru kwayo atapata
malipo ya Mbinguni, ambayo yoyote atakaye ikanusha atapuuzwa, kwani
Allah Azza Wa Jallah ni Mwenye Kujitegemea kwa ulimwengu wote.
Fikiria mambo ambayo kwamba elimu amejaaliwa nayo mtu
na yale ambayo hakupewa elimu nayo.
Amejaaliwa na Elimu kwa mambo yote haya ambayo humpelekea kwenye mema
yake kwa upande wa imani hali kadhalika na maisha yake hapa duniani.
Elimu ya Kiroho ya Allah Azza Wa Jallah Muumba
inapatikana kwa njia za hoja na ushahidi upatikanao katika kuwepo kwa
uumbaji. Na pia elimu ya mambo ya wajibu
juu yake, kwa mfano, haki kwa Wanadamu wote, upendo kwa wazazi, kutekeleza dhamana,
huruma kwa wanao onewa na kudhulumiwa
n.k. elimu na ruhusa ambayo Mataifa yote wanayo kimaumbile ni ukweli na mambo, ima kwa kupatana nasi au
dhidi yetu.
Kadhalika amepewa elimu ya vitu vile ambavyo ni vya
manufaa kwa maisha yake kidunia, kwa mfano ukulima, uendelezaji wa kilimo cha
bustani, ufugaji, kutoa maji kutoka kwenye visima na chemchemi, utafiti wa miti
shamba kwa ajili ya matumizi ya uganga, uchimbaji wa aina mbalimbali za mawe ya
thamani, uzamiaji katika bahari, mipango aina mbalimbali ya kuwinda wanyama na
ndege, uvivu, viwanda, kazi na mbinu za biashara na mambo mengine ambayo
yanahitaji maelezo marefu, ambamo mna utekelezaji wa mambo ya maisha ya kidunia
ya mtu, uboreshaji wa mambo ya dini yake na ya ulimwengu wake. Elimu kama hiyo imefanywa ipatikane kwake kama ilivyo bora kwa faida
zake.
Mambo, ambayo elimu iko nje ya uwezo wake, wala hali
yake haiihitaji, hayafanuliwi kwake, kwa mfano, elimu ya ghaibu, mambo ambayo
yatatokea baadae au baadhi ya mambo yaliyotokea wakati uliopita, yale yanayo
fungamana kwa yaliyo ndani ya bahari na katika eneo kubwa la ulimwengu, au
yaliyo katika akili za watu yaliomo katika tumbo la uzazi n.k. Watu waliodai kuwa na elimu ya hayo madai yao
yalibatilishwa kufuatia matukio yao kuwa kinyume chake.
Hivyo hebu angalia, kwamba elimu ya vitu aliyopewa
mtu ni ya muhimu kwa mambo yake ya Kilimwengu na ya Kidini. Amezuiliwa kujua vitu visivyo vya lazima
kumvuta katika ubora wake na kasoro yake katika yote haya mna uzuri wake. Hebu fikiria kwa nini mtu hakupewa elimu ya
muda wa maisha yake.
Kama angejua muda wa maisha yake duniani kuwa mfupi
maisha yake yote yangechukiza, kwa kujua hivi angelingojea muda wake wa
kufa. Hali yake ingekuwa ya mtu ambaye
mali yake yote imepotea au karibuni sana itapotea. Na angehisi umasikini wake na uhitaji. Jinsi gani angehofia katika kutazamia
kuharibika kwa mali yake na ufukara wa mwisho, huzuni na uchungu ambao angeuona
kwa tazamio la kifo ungekuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa tazamio la kuharibika
kwa mali yake, kwani mwenye kupoteza mali yake wakati wote hubakia na tumaini
kwamba huenda atapata zaidi ya hiyo na hilo lingempatia faraja katika akili
yake
Kinyume chake yule ambaye amesadikishiwa mwisho wa
maisha yake atakuwa amevunjika moyo zaidi.
Kama angelikuwa na muda mrefu wa kuishi, tumaini hili katika kuishi kwake
kungempa tumaini lisilofaa. Angeweza
kuelemezwa na anasa na ufisadi juu ya dhana kwamba angeomba toba katika siku za
mwisho za maisha zilizobakia kwa anasa hizi za sasa zinazo mshughulisha. Hili ni jambo ambalo Allah (s.w.t.) halitaki
kutoka kwake wala halitaki kwa viumbe vyake.
Iwapo unaye mtumishi ambaye anaendelea kukukosea kwa
mwaka mzima, na anatumaini husamehewa dhidi ya utumishi mzuri wa siku moja au
mwezi mmoja. Hakika usingeipenda na
mtumishi huyu asingekuwa na sifa sawa na mtumishi mzuri ambaye daima yuko tayari kutii amri yako.
Unaweza kuleta kinzano kwa hili kwa kusema kwamba
haitokei kwamba mtu hupita njia ya upotofu, kisha akatubia na toba yake
ikakubaliwa. Jibu letu kwa hili ni
kwamba hii hutokea tu wakati mtu ameshindwa na ashiki yake kufikia hali
isiyoweza kuzuilika, lakini wakati wote hana uamuzi katika utii wake juu ya
dhana kuonyesha toba baadae wakati anajiingiza katika hawaa kwa sasa Allah
(s.w.t.) hamsamehi nje ya Rehema Zake zisizo na mwisho (yaani anasamehewa ndani
ya Rehema za Allah (s.w.t.).
Lakini katika Suala la yule ambaye ameamua juu ya
upotofu kiasi atakachopenda, akitegemea msamaha katia hatua ya baadae,
anajaribu kwa sababu hii kumdanganya Yeye, ambaye hawezi kudanganywa,
akifikiria kupata anasa zaidi za muda huu huku akitegemea kusamehewa kwa sababu
ya toba yake ya baadae. Pia, kwa hali
hii ya jambo hili, kwamba kwa sababu ya aina fulani ya mfumo wa maisha wa
kujiingiza katika anasa huenda usingemruhusu hata nafasi kwa ajili ya toba
hususan katika uzee, wakati mwili umepita kiasi kikubwa cha udhaifu umzuiao
kuyatekeleza mategemeo yake.
Na mwenye kutafuta visingizio katika kutoa toba yake,
isingewezekana kwake katika kifo cha shambulio la ghafla na angeutoka ulimwengu
bila kutubia. Angekuwa kama mdaiwa
ambaye ana bidii ya kulipa madeni yake lakini huahirisha mara kwa mara mpaka
kifo kumfikia mali yake huharibika na madeni yake husimama dhidi yake, kwa hiyo
ni katika usawa wa mambo kwamba elimu ya muda wa kuishi mtu ifanywe ni siri
kwake ili kwamba ategemee kifo kumtokea wakati wowote na katika hofu hiyo,
aepuke uasi na kuchagua kufanya tendo jema.
Unaweza kuleta Kinzano nyingine kwamba ikiwa muda
wake wa kuishi ni siri kwake, na daima yuko kwenye wasiwasi kuhusu kifo chake,
hufanya maovu na matendo ya haramu.
Majibu yetu kwa hili ni kwamba mpango uko katika kulingana na hali
ijitokezayo. Kama mbali na haya yote mtu
hajizuii na uovu, ni dalili ya tabia yake kupoteka na ugumu wa moyo wake. Hakuna kosa katika kupanga kama mgonjwa baada
ya kujulishwa kikamilifu faida za dawa makhsusi na makosa ya mambo maalum mabaya, haitamfaa kutumia taarifa kwa
kuto heshimu maelekezo ya Daktari.
Daktari si wa kulaumiwa bali mgonjwa aliyekengeuka kufuata agizo la
mganga.
Mbali na wasiwasi kuhusu kifo ambao anao kwa sababu
ya kutokujua kwake kuhusu muda wa maisha
yake, haachi kufanya maasi. Angekakamia
katika fisadi na uovu sana wa dhambi zisizoelezeka, iwapo angeipata elimu
kamilifu ya muda wa maisha yake na kuishi.
Kwa ajili hiyo wasiwasi kuhusu kifo kwa namna yoyote ni bora kwake kuliko
tumaini lake la kuishi maisha marefu.
Kama kuna jamii ya watu ambao, mbali na wasiwasi wao kuhusu kifo, ni
wazembefu na hawafaidiki kwa ushauri, kuna jamii nyingine hufaidika kwa
ushauri, hujiepusha kutenda dhambi na badala yake kutenda mema. Huwapa wenye kuhitaji na masikini kwa kutoa
Sadaka ya vitu vyao vizuri. Isingekuwa
haki kuinyima jamii hii kutokana na kupata faida kwayo.
Hebu fikiria kdoto na ustadi wake uliomo ndani
yake. Kuna ndoto zinazotokea kuwa kweli
na ndoto ambazo hazitokei kuwa kweli, zote zimechanganyika.
Kama ndoto zote ni za kweli watu wote wangelikuwa
Mitume. Kama ndoto zote zingekuwa za
urongo zingalikuwa hazina faida bali huzidi na kutokuwa na maana.
Ndoto wakati mwingine ni za kweli ambazo humnufaisha
katika shughuli zake za maisha chini ya mwongozo wao, au kuepusha, hasara
ambayo amejulishwa kwayo. Zaidi siyo za
kweli isiwe watu wakazitegemea.
Hebu fikiria vile vitu ambavyo unaviona viko duniani
vimewekwa kukidhi mahitaji ya mwanadamu.
Udongo kwa kujenga nyumba, Chuma kwa ajili ya
Kiwanda, mbao kwa kujengea, mashine n.k. Jiwe kwa matumizi kama kijaa, shaba
kwa ajili ya vyombo vya nyumbani, dhahabu na fedha kwa ajili ya shughuli za
biashara, johori kwa ajili ya hazina, nafaka kwa ajili ya chakula, vitu vya
manukato kwa ajili ya burdani, madawa kuponya ugonjwa, wanyama wa miguu minne
kama wanyama wa kubeba mizigo, miti mikavu kama nishati, majivu kwa ajili ya
dawa (kemikali) mchanga kwa manufaa ya ardhi na inawezekana mtu kuhesabu vitu
vyote hivi ambavyo havina idadi?
Unafikiri kwamba kama mtu ataingia nyumba na kuiona
imewekewa mahitaji yote ya mwanadamu; nyumba nzima imejaa hazina na kila kitu
kimewekwa kwa madhumuni halisi, anaweza akafikiria vitu vyote hivyo vimejipanga
vyenyewe bila ya yeyote kuupanga (mpango huo)?
Sasa vipi itawezekana mtu yeyote mwenye akili akadokeza kwamba ulimwengu
huu na vitu vyote hviti vimejitokeza vyenyewe?
Jifunze somo kutokana na vitu ambavyo vimeumbwa
kukidhi mahitaji ya mwanadamu na ustadi mkubwa uliomo ndani yao. Nafaka zimezalishwa kwa ajili yake lakini
amepewa jukumu la kazi ya kuzisaga, kuukanda unga na kupika. Sufi imezalishwa kwa ajili yake ambayo lazima
aichambue, kusokota nyuzi na kuzitengeneza nguo. Mti umetengenezwa kwa ajili yake lakini
lazima apande mbegu, ainyweshe na kuichunga.
Miti shamba imeumbwa kama madawa kwa ajili yake lakini lazima aitafute
aichanganye na kuifanyiza dawa.
Kadhalika utaona vitu vyote vilivyotengenezwa na
Muumba kukidhi mahitaji ya mwanadamu katika njia ambayo kwamba hakuna mpango wa
mtu ungeweza kufanya kazi kwa kutoshelezea kazi yao na kutumia kwayo. Haja na
hali kwa kazi hiyo imeachwa juu yake kwa faida yake. Kama Allah (s.w.t.) angefanyiza vifaa vyote
hivi na mtu hana la kufanya kwa njia ya mshughuliko wake, angeanza kuzunguuka
juu ya ardhi katika pande zote nne na ardhi isingeweza kuvumilia udhia
wake. Mtu asingekuwa na maisha ya raha
kama mahitaji yake yote yangetimizwa bila juhudi na, wala asinge furahia kitu
kama hicho.
Huoni kwamba mgeni akaae kwa muda na mahitaji yake
yote yakitekelezwa kama kawaida na mwenyeji, bila juhudi yoyote kwa upande wake
kuhakikisha ulaji wake, kinywaji, malazi au kikao, anachoka kwa kukaa kwake
bure na kutokushughulika. Anahitaji
baadhi ya shughuli, ingekuwa vipi hali yake kama kutokushughulika kwake
kungekuwa ni kwa maisha yake yote?
Hii basi imeamriwa kwa mtu kuhodhi mipaka yake
kufanya shughuli zake kwa faida zake, isiwe ulegevu na kutokushughulika
kukamsababishia unyong'onyevu.
Zaidi ya hayo angezuiwa kutokana na kufanya kazi hizo
kwa vile ziko nje ya uwezo wake, na ambazo hazina faida kwake hata kama
zimekamilishwa.
Elewa kwamba haja ya msingi ya mtu ni chakula na
maji. Ona mpango ambao umo humo.
Mtu anahitaji zaidi maji kuliko mkate, kwa sababu
anaweza kuvumilia njaa kwa muda mrefu kuliko kiu. Anahitaji maji kwa kunywa, kutawadha, kufua
nguo, kunywesha wanyama wa miguu minne, kunywesha mimea. Kwa hiyo maji, yametolewa kwa wingi bila
kuhitaji kuya-nunua kumwokoa mtu kwa
haja ya kuyatafuta. Mkate lazima
upatikane kwa juhudi na kupanga kumfanya mtu ashughulike na kazi yake na
kumzuia kutokana na majivuno na kiburi na kazi zisizo na maana.
Huoni kwamba mtoto katika umri wake wa mwanzo
anapelekwa kwa mwalimu kwa ajili ya maelekezo kumzuilia na michezo wakati wake
wote, ambayo ingempelekea yeye au Mzazi wake kwenye matatizo. Kadhalika kama mtu angewekwa bila shughuli
angejitwalia majivuno na kiburi na angejiingiza katika matendo ambayo
yangemdhuru vibaya sana.
Mtu aliyezaliwa na kulelewa katika malezi ya anasa
chini ya masharti ya ukwasi na jamaa wake wengi, ni wazi atatumbukia kwenye
tabia hizo, kufafanisha hali hiyo.
Elewa kwa nini mtu mmoja hafanani na mwingine kama
walivyo ndege na wanyama n.k., wakiwa wamefanana mmoja na mwingine. Unaona kundi la kulungu na kundi zima la
kwale kila moja akifanana na mwingine bila tofauti kubwa kati yao, ambapo
kwamba watu, kama unavyoona, wana maumbo yenye kupambanulika na hulka, kiasi
kwamba hakuna watu wawili wanaofanana kwa mfumo ule ule.
Sababu ni haja ya kila mmoja inatakikana atambuliwe
mwenyewe kwa umbo mahsusi na sura, kwa vile wataendesha biashara miongoni mwao
ambayo haiwahusu wanyama. Huoni kwamba
mshahaba wa wao kwa wao miongoni mwa wanyama na ndege hakuwaletei madhara? Sivyo ilivyo kwa mtu, kwani ikiwa kwa bahati
jozi ya mapacha watafanana katika umbo, watu wanahisi kuchanganyikiwa kwa kiasi
kikubwa katika kushughulika nao ambacho angepasa apewe huyu kinatolewa kwa
mwingine kwa makosa. Mmoja anashikiliwa
pahala pa mwingine katika adhabu (au kisasi).
Hutokea hivyo katika mambo mengine hivyo hivyo kwa
sababu ya mshabaha. Mshabaha wa wanadamu
unaweza kuwa na madhara zaidi. Nani basi, aliyetoa ufasaha huu na ukamilifu,
ambao una pumbaza mawazo? Hakika ni Yeye
yule aliye umba yote haya, ambaye Rehema zake zimeenea kwa vitu vyote.
Je, utamwamini mtu asemae kwamba picha iliyoko
ukutani, ambayo unaiona, imejitokeza yenyewe bila msaada wa msanii? Hakika sivyo, utamcheka. Vipi basi unaweza kuamini kwama mtu anayeishi
akiwa na stadi za uzungumzaji na mwendo
anaweza kujitokeza na kuwepo mwenyewe, ambapo huko tayari kukubali imani
hiyo kuhusu picha isiyo na uhai?
Kwa nini inatokea kwamba miili ya watu haikui kuupita
mpaka mahsusi mbali na ukweli kwamba wanaendelea kuishi na kula? Hii ni kwa sababu gani kama si kwa utambuzi
wa ndani?
Mwenye Nguvu zote Allah Ameamuru hivyo kwamba kila
jamii zote za viumbe vyenye uhai vyapaswa kuwa na ukomo maalum wa kukua si
ukubwa zaidi wala udogo zaidi.
Vimeendelea kukua mpaka kufikia ukomo huo na kisha husimama kukua,
ingawa, ulishaji unaendelea bila kusimama.
Kama isingeamuriwa hivyo vingeendelea kukua mpaka miili yao ingekuwa nje
ya mipaka itambuliwayo.
Kwa nini katika suala hususan la wanadamu kwamba
mwendo na shughuli huleta uchovu kwao na wanaepuka kazi laini kwa sababu tu
mahitaji yake kama mavazi n.k., huhitaji juhudi zaidi? Kama mtu hakupata shida na maumivu, vipi
angeweza kuepuka matendo ya uovu, kusujudi mbele za Allah (s.w.t.) au kuwahurumia
watu?
Huoni kwamba mara tu mtu anapopatwa na maumivu, basi
hugeuka kumuelekea Allah (s.w.t.) kwa unyenyekevu kamili, akioma mbele ya Mola
wake ili arejeshewe Afya yake na kufungua mikono yake katika ukarimu? Kama mtu asingepata maumivu kwa kupigwa, vipi
Serikali zingewarudi wakaidi? Vipi atoto
wangefundisha Sayansi na Sanaa? Vipi
watumwa wangejisalimisha kwa Mabwana zao kwa hiari?
Je, hakuna onyo katika yote haya kwa Ibn Abi Al Auja
na Sahaba zake ambao wanakana madhumuni, na wafuasi wa Mani ambao wanakana
Ustadi ulio ndani ya Kazi na maumivu?
Iwapo Viumbe vya Kiume tu au vya Kike tu vingeumbwa
katika viumbe hai, je, Jamii yao isingetoweka? Hivi ndiyo sababu ya kuhifadhi
jamii zao, kwamba mchanganyiko wa viumbe vya Kiume na vya Kike umeletwa kwa
viumbe katika uwiano ulio sawa.
Kwa nini inakuwa kwamba wanaume na wanawake
wanapofikia baleghe, ni Wanaume peke yao tu huota ndevu? Je, haiko katika kawaida na amri ya
Usanii? Hii ni kwa sababu mwanaume
ameumbwa kama Bwana ma Mwanamke kama Mtunzaji wa Nyumba. Mwanambe huyo ndiye msimamizi wa maslahi ya
Mume na msiri wake. Mwanaume, kwa hivyo,
amepewa ndevu kumpa sifa na kuonekana Bwana wa Heshima. Mwanamke anaruhusiwa urembo na uzuri badala
yake kama mvuto kwa muungano.
Je, huoni sifa hizi kamili kwamba uumbaji huu
unapatikana kwa Usanii wa Mwenye Kguvu zote Allah? Kila kitu kinapasika kwa kipimo halisi. Hakuna kinachotolewa ambacho hakihitajiki.
Sasa ilikuwa ni adhuhuri, Bwana wangu alinyanyuka kwa
ajili ya Sala akaniambia nije kwake siku ifuatayo (kesho). Insha Allah. Nikiwa nimejawa na furaha kwa
maelezo niloyo yapata, nilirudi na moyo wa shukurani kwa Allah (s.w.t.) kwa
ajili ya Baraka niliyopatiwa juu yangu.
Nilikuwa na usiku mzuri kwa ajili ya maelekezo yenye
thamani yaliyowekwa juu yangu na Bwana wangu.
Baraza La
Asubuhi na mapema niliwasili kwa Bwana wangu, na
baada ya kupata ruhusa ya kuingia katika vyumba vyake niliketi kwa ruhusa yake.
Yeye (a.s.) alianza:
Sifa zote njema zamstahiki Yeye Ambaye ni Muumba wa mabadiliko ya
nyakati Ambaye huleta hatua moja baada ya nyingine na hali moja baada ya
nyingine ya miongo ya muda, kuwalipa wema na kuwaadhibu waovu, kwa sababu ni
Mwenye Haki. Majina yake yote
yametukuzwa. Baraka zake ni adhimu. Hafanyi dhuluma hata ndogo kwa viumbe wake,
walakini, mtu anajifanyia udhalimu mwenyewe!
Maneno ya Allah (s.w.t.) mwenyewe yanathibitisha
ushuhuda kwa haya: "Basi atakayefanya kheri (jema) uzani wa mdudu chungu
atauona. Na atakayefanya uovu uzani wa
mdudu chungu (pia) atauona" (Qur'an 99:7 - 8).
Kuna Aya nyingine katika Kitabu Kitukufu katika maana
hii hii zikitoa kinaganaga maelezo ya mambo yote. Uwongo hauwezi kuja mbele yake wala nyuma
yake. Ni kitabu kilichofunuliwa na Mwenye Nguvu zote Mwenye Kustahiki
Shukurani Allah. Ni kwa maelezo haya
kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwa jambo hili kwamba " Matendo
yenu yatarudishwa kwenu."
Imam (a.s.) aliinamisha chini kichwa chake kwa muda
na akasema: "Ewe Mufazzal! Mwanadamu amefadhaika na kupotea, ni kupofu,
amepumbazika katika ukaidi wake, kufuatia mashetani yao na vioja. Wana macho lakini hawaoni, wana ndimi lakini
ni mabubu na hawaelewi. Wana masikio lakini
hawasikii. Ni wenye furaha katika ufisadi wao duni. Wanadhania wameongozwa vema. Wamepotoshwa kutoka sifa za viumbe vyenye
akili. Wanakula juu ya mboga
zilizonajisiwa na uchafu wa watu wachafu. Wanadhani wenyewe wako salama
kutokana na msiba wa kifo cha ghafla na adhabu ya matendo. Ole! Ajali mbaya iliyoje iwapatao watu hawa!"
Hii ilinifanya mimi nitoe machozi, na Imam (a.s.)
alinifariji kwa kusema kwamba nimeokolewa, kwa sababu ya kuikubali iman na
elimu ya kiroho, na nimepatiwa wokovu.
Yeye (a.s.) aliendelia: Sasa napenda kukuelezea kuhusu ulimwengu wa
Wanyama, ili kwamba upate maelezo zaidi kuhusu (Ulimwengu) huo kama ulivyopata
kuhusu mengine.
Hebu fikiria umbile la mwili na mfumo wa muundo
uliomo katika uumbaji wao. Siyo wagumu
kama mawe, kwani wangekuwa hivyo, wasingeweza kufanya shughuli, wala siyo laini
kwani kwa hali hiyo wasingeweza kuzunguusha vichwa vyao au wenyewe kusimama
wima bila mhimili.
Wamefanyizwa
na misuli hiyo ya kupinda kama kuinama na kujikunja. Wametengenezwa kwa mifupa migumu ambayo
imeshikwa kwa misuli na ambayo imefungwa pamoja kwa makano juu ya kila
mfupa. Ifunikayo mifupa hii na misuli
hii ni ngozi yao ambayo huenea juu ya mwili vote.
Wanasesere wa miti na matambara yaliyo zunguushwa juu
yao na kufungwa na vigwe na Sandarusi ya gundi ju ya umbo lote, itafafanisha
jambo hili, ifanye mbao iwe kama mifupa, matambara kama misuli, vigwe kama
makano no sandarusi kama ngozi.
Kama inawezekana katika hali ya viumbe vyenye uhai na
mwendo kujitokeza kuwepo kwa vyenyewe, ingekuwa busara kutegemea kutokea maumbo
haya yasio na uhai. Na kama haiwezekani
kwa wanasesere hawa, itakuwa ni upuuzi zaidi kwa wanyama.
Kisha angalia kwa uangalifu sana kwenye miili yao,
imefanyizwa kwa misuli na mifupa kama ya wanadamu. Wamejaaliwa macho na masikio, ili kwamba
kumuwezesha mtu kupata huduma kutoka kwao, wasingaliweza kutekeleza lengo lake
(huyo mtu) kama wangekuwa vipofu au viziwi.
Wamenyimwa Stadi za akili na hoja, ili kwamba wabakie
ni wenye kutii kwa watu na wasije wakawa wasiotii hata kama akihusishwa na kazi
nzito isiyovumilika na kuelemea.
Kinzano laweza kuletwa katika hali ya watumwa
wanadamu, wenye akili na hoja, hutii mabwana zao kiunyonge japokuwa ni dhiki na
kazi ngumu.
Jibu kwa hili ni kwamba watu wa aina hii ni wachache
kiidadi. Wengi wa watumwa ni wafanyaji
kazi ngumu bila kupenda, ambapo wanyama ni watii hata katika kulemewa kuzito na
wakati wa kuzunguusha kijaa n.k. hawawezi kuathirika kwa mfadhaiko kama kazi
zao mahsusi zihusikavyo kwa mtu.
Kama mtu angefanya kazi ya ngamia mmoja au nyumbu,
watu wengi wangehitajika, na kusababisha kizuizi katika shughuli nyingine. Majukumu haya rahisi yangechukua wafanyakazi
wote, bila kuacha watu wowote kando kwa ajili ya Sanaa na Taaluma. Zaidi ya hayo watu wangepatwa na uchovu wa
akili.
Hebu fikiria miundo ya aina tatu ya viumbe hai
ifuatayo, na Sifa ambazo kwamba wamejaaliwa nazo.
(1) Mtu, akiwa ameamriwa kuwa na akili na hoja
kufanya kazi hizo za ufundi kama useremala, uashi, uhunzi, kushona n.k.
amejaaliwa kuwa na viganja vipana na vidole vinene kumwezesha kushika aina zote
za ala zilizo muhimu kwa ajili ya taaluma hizi.
(2) Wanyama walao nyama, wakiwa wameamriwa kuishi kwa
kula wanyama (nyama) wametunukiwa viganja laini na makucha yawezekanayo
kufichika ndani. Ni wazuri kwa kuwinda
lakini hawafai kwa kazi za sanaa za kitaaluma.
(3) Wanyama walao majani, wakiwa wameamriwa si kwa
sanaa za kitaaluma wala kwa uwindaji, wametunukiwa, baadhi na kwato
zilizopasuliwa kuwasaidia kutokana na ugumu wa ardhi wakati wa kulisha ambapo
wengine wana kwato imara kuwawezesha kusimama sawa sawa juu ya ardhi kwa
ulinganifu mzuri kama wanyama wa mizigo.
Wanyama walao nyama katika mfumo wao wa kuumbwa wana
meno makali, kucha ngumu, na vinywa vipana kuwasaidia katika lishe yao kwa
chakula cha mnyama kama ilivyoamriwa kwao, na wameumbwa ilivyo. Wamepewa silaha hizo na vyombo vya kazi kwa
kuwafaa katika uwindaji.
Kwa ulinganifu wa sawa, utaona mdomo na kucha
vikiwafaa kwa kazi zao mahsusi. Kama
kucha hizo wangepewa wanyama walao majani, zingekuwa mbaya zaidi kuliko manufaa
kwani kamwe hawawindi wala kukamata kiwiliwili.
Na wanyama walao nyama wangepewa kwato badala ya kucha wangeshindwa
kupata mahitaji yao katika kukosekana vifaa vya kufaa kwa mahitaji hayo.
Huoni kwamba aina zote hizi za wanyama wametunukiwa
sawasawa na vitu vyenye kufaa (kwa kusudi la kila mmoja) kwa ulinganifu na haja
zao, humo kwayo mna kuishi kwao.
Sasa watazame wanyama wa miguu minne na angalia jinsi
wanavyowafuata Mama zao. Kamwe
hawahitaji kubebwa wala kulishwa kama ilivyo kwa watoto wa kibinadamu. Hii ni kwasababu kwamba mama wa watoto hao hawana nyenzo
ambazo mama wa watoto wa Kibinadamu wanazo.
Wana Upendo, Huba na Elimu ya Sanaa ya Maumbile na Mikono maalum na
Vidole vya kuwanyanyulia. Wamefanyizwa
hivyo ili kuwasaidia katika aina zote za kazi.
Utaona namna hiyo hiyo katika ndege, kwa mfano,
Vifaranga vya Kuku, Kwale na jamii ya Kuku (k.v. Kanga) huanza kuokota nafaka
na kwenda huku na huko mara tu
vinapoanguliwa kutoka kwenye mayai.
Ndege ambao vifaranga vyao ni dhaifu, bila nguvu ya kusimama, kwa mfano
wale wa porini na njiwa wa nyumbani, wana mama wenye silika zaidi za kimama,
ili kwamba wawaletee lishe kwenye vinywa vya vifaranga vyao waliyoiweka kwenye
maumio yao.
Malisho aina hiyo huendelea mpaka vifaranga viweze
kujikimu vyenyewe. Njiwa hana makinda wengi kama kuku, kuwezesha
majike kuyalea kiutoshelezaji bila kuwaua kwa njaa. Hivyo kila kimoja hupata mgao wa kutosha
kutoka baraka za Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote Allah (s.w.t.)
Hebu tizama jinsi miguu ya wanyama ilivyoumbwa katika
jozi kuwawezesha kutembea kwa urahisi, ambapo ingekuwa vigumu, kama ingeliumbwa
katika idadi ya witir. Mnyawa atembeaye
hunyanyua mguu mmoja ambapo mwingine
anautuliza juu ya ardhi. Wenye miguu
miwili ananyanyua mmoja na kupata msaada juu ya mwingine. Wa miguu minne hunyanyua jozi moja na kutulia
juu ya pande tofauti.
Kama mnyama wa miguu minne angenyanyua jozi ya miguu
katika upande mmoja, tutusa kwa jozi ya upande mwingine kungekuwa kugumu kama
ambavyo ubao hauwezi kusimama juu ya miguu miwili. Mguu wa mbele wa upande wa kulia na mguu wa
nyuma wa upande wa kushoto inanyanyuliwa pamoja, na kinyume chake. Kwa ajili ya mwendo thabiti.
Je, huoni kwamba punda anaendesha Kijaa kama kazi
nyongeza ya ubebaji mizigo, kwa kuwa farasi anaruhusiwa pumziko na faraja kwa
kulinganishwa na punda? Na ngamia
anafanya kazi zaidi, ambayo haiwezi kumalizwa na idadi ya watu.
Ingekuwa hali gani kama angekataa kutii amri? Husalimu Amri hata kwa mtoto aliyepo
hapo! Vipi Maksai anasalimu amri kwa
Bwana wake akilima Shamba na mhimili shingoni mwake?
Farasi wenye asili bora hukimbia kuelekea makali ya
panga na mikuki kama wafanyavyo mabwana zao wakati wa mapigano. Mtu mmoja anaweza akachunga kundi la
kondoo. Kama kondoo wangetawanyika kila
mmoja akaenda njia yake, vipi mtu angeweza kuwatafuta?
Kadhalika, Jamii nyingine za wanyama ni zenye kufaa
kwa mtu, kwa nini? Hii ni kwa sababu
hawana akili yoyote, wala uwezo wowote wa kuhoji mambo. Kama wangelikua na akili, wangejitoa katika
kutekeleza kazi nzuri ya mahitaji ya mtu.
Ngamia angekataa kusalimu amri, na fahali angeasi
dhidi ya bwana wake, kondoo wangetawanyika na kadhalika. Kama wanyama wa kuwindwa wangekuwa na akili
na hoja wangeshindana kwa ajili ya vitu vya kula na watu. Nani basi angeweza kushindana na ushauri wao
wa pamoja dhidi ya watu?
Je, huoni jinsi walivyozuiwa kutokana na kufanya
hivyo? Wanaogopa makazi ya watu na
kumkimbia mwanadamu, badala ya mwanadamu kuwaogopa wao (na kuwakimbia). Hawatoki nje wakati wa mchana kutafuta
chakula, bali wakati wa usiku. Wanaogopa
watu na utukufu wao wote utishao bila kupata dhara lolote au onyo kutoka
kwao. Kama hii isingeamriwa hivyo,
wangekuja wakirukaruka kwenye makazi ya wanadamu na kufanya maisha yao kuwa ya
mashaka.
Mbwa, (akiwa) miongoni mwa hayawani, amejaaliwa tabia
maalum, utii kwa bwana wake, utumishi wake kwake na ulinzi wake kwake. Huweka
ulinzi wakati wa usiku wa giza, hubweka huko na huko katika nyumba akilinda
usalama dhidi ya wezi. Yuko tayari
kujitoa mhanga maisha yake ili kumwokoa mtu na watu wake. Huo ndio utii wake kwa bwana wake. Anaweza kujiweka na njaa na maumivu kwa ajili
ya bwana wake.
Kwa nini, mbwa ameumbwa katika mfumo huu, isipokuwa
tu amtumikie na kumlinda mtu, na meno yake imara, kucha madhubuti, ubwekaji wa
kutisha, kwa nini? Ni kwa kuwatisha wezi
na kuwazuia kukaribia mali iliyo dhaminiwa kwa ulinzi wake.
Tizama katika nyuso za wanyama wa miguu minne na
angalia vipi zilivyoumbwa. Utaona kwamba
macho yao yamewekwa mbele, wasije wakagonga ukuta au kutumbukia shimoni. Utaona vinywa vyao vimepasuliwa chini ya
pua. Kama vingekuwa kama vile vya watu
wasingeweza kuokota chochote kutoka ardhini.
Huoni kwamba mtu haokoti chakula chake kwa kinywa chake? Hufanya hivyo kwa mikono yake.
Huu ni ubora wa pekee kwa mtu katika mlingano na
walishi wengine. Kwa kuwa wanyama wa
miguu minne hawakupata mikono kama hiyo kuwawezesha kuokota majani, sehemu ya
chini ya pua imepasuliwa humwezesha kuokota majani na kuyatafuna. Anasaidiwa zaidi na midomo iliyo refushwa
kufikia vitu vilivyoko mbali zaidi kama vile afikiavyo vilivyo karibu zaidi.
Fikiria mikia ya wanyama na faida zilizoamriwa
kwayo. Ni aina fulani ya mfuniko kwa
viungo vyake vya siri vya kutolea uchafu.
Vilevile husaidia kufukuza inzi na mbu ambao hutua juu ya uchafu katika
miili yao. Mkia yao imefanyiwa mfano wa
mapanga boi ambayo kwa hiyo hufukuzia inzi na mbu. Vile vile hupata afueni kwa kupungia mikia
yao daima.
Wanyama hawa husimama juu ya migu yote minne, hawana
muda wa kuitembeza huku na huku, kwa hivyo, huhisi kufarijika kwa kupungia
mikia yao.
Kuna faida nyingine hata hivyo ambazo mawazo ya
mwanadamu si yenye kuweza kuzishika na ambazo zinajulikana tu inapotokea haja,
miongoni mwa faida hizi, mkia ni silaha ya zaidi sana mkononi kwa kuunyongotoa
kumtoa mnyama anasapo kwenye matope. Mwengo
wa mkia unaweza vile vile kutumiwa na watu kwa manufao kadhaa.
Kiwiliwili cha wanyama hawa kimefanywa bapa kwa
kulala juu ya miguu yote minne kurahisisha ngono kwa sababu ya hali ya sehemu
zao zinazohusiana.
Fikiria mkonga wa tembo na ustadi mkubwa uliopo
katika muundo wake. Unasaidia dhumuni la
kuchukua chakula na maji kupeleka ndani tumboni, kama mkono wa mtu. Bila huo tembo hawezi kunyanyua chochote
kutoka ardhini, kwa kuwa shingo yake siyo ndefu vya kutosha, ambayo angeweza
kuinyoosha mbele kama wanyama wa miguu minne.
Kwa kutokuwepo kwa shingo ndefu amepewa mahala pake
mkonga mrefu ili kwamba aweze kuunyoosha na kukidhi haja yake. Nani aliyempa kiungo hiki kufidia kwa
kutokuwepo kwa kile kilicho kosekana?
Hakika, Yeye Ambaye ni Mwenye Huruma Sana juu ya Viumbe Vyake. Na hii itawezekana vipi bila kupanga Usanii
kama ilivyojitokeza kwa Wataalam wapotofu na walahidi?
Kwa kinzano kwamba kwa nini hakujaaliwa kuwa na
shingo sawa kama ile ya wanyama wengine, jibu ni kwamba kichwa na masikio vya
tembo vikiwa ni vizito sana vingeweza kusababisha mvuto mkubwa wa nguvu, hata
pia kuvunjika, hivyo kichwa chake kimeungwa moja kwa moja na mwili kukikinga
dhidi ya matokeo hayo na badala yake kwa ajili hiyo mkonga umefanyizwa
kushughulikia madhumuni yote hayo inayohitaji, pamoja na yale ya kulisha.
Hebu fikiria umbo la twiga na asili mbalimbali ya
viungo vyake vifananavyo na wanyama wengine mahsusi. Kichwa chake hufanana na ile cha farasi,
shingo kama ile ya ngamia, kupasuka kwato kama zile za ng'ombe, na ngozi yake
kama ile ya chui.
Baadhi ya watu wajinga wamedhania kwamba haya ni
matokeo kutokana na muungano wa aina mbalimbali za wanyama wajao sehemu za
kunyweshea, jamii moja binafsi huingia katika muungano wa ngono na jamii
nyingine binafsi, na kutokea uzao wa namna hii. Na kwa hiyo unakuwa mfano wa umbo
mbalimbali.
Kusema hivi ni kuudhihirisha ujinga, na ukosefu wa
elimu ya kiroho ya Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) utukufu uwe kwake. Hakuna mnyama aingiaye kwenye muungano
ufanyikao kati ya farasi na ngamia jike au ngamia na ng'ombe. Muungano wa ngono unaweza kuwepo (au kutokea)
tu kati ya wanyama wenye umbo linalofanana katika kuumbwa, kwa mfano farasi na
punda jike hutokea (kuzaliwa) kwa nyumbu, au mbwa mwitu na mbweha hutokea
(kuzaliwa) chotara.
Hata hivyo, kamwe haitokei kwamba uzao wa muungano wa
namna hiyo unaweza kuchukua kiungo kimoja kutoka mmoja wa mwenzi mwingine. Twiga ana kiungo kimoja kifananacho na kile
cha farasi, mwingine na kile cha ngamia ukwato wa mwingine na ule wa ng'ombe. Lakini unaona kwamba nyumbu kichwa chake,
masikio yake, mgongo wake, mkia na kwato zake vi katikati baina ya vile vya
punda na vya farasi, na ndivyo ulivyo mlio wake u katikati baina ya mlio wa
farasi na mlio wa punda. Hoja hii
yaonyesha kiutoshelezaji kwamba twiga si uzao wa muungano wa jamii
inayojifanyia tu, bali ni ajabu moja ya uumbaji wa ajabu wa Mwenye Nguvu zote
Allah (s.w.t.) kuthibitisha Enzi yake Kuu.
Yapasa pia ifahamike kwamba Muumba wa jamii za
Wanyama zisizo idadi Huumba viungo vyovyote vile Apendavyo ya hivyo vilivyo
sawa kimoja na kingine na vile vingine ambavyo havifanani. Anaongeza katika uumbaji chochote apendacho
na hukataza humo namna Apendavyo. Hii ni
kwamba Enzi Yake Kuu iweze kuthibitishwa na hakuna kitu kinachoweza kumzuia
katika lolote Apendalo.
Kwa nini shingo yake ni ndefu na faida gani
zipatikanazo kwake kutokana nayo? Faida
ipo katika kumwezesha kufikia majani na matunda ya miti mirefu kwa lishe yake
ambapo anaishi, anakaa, na amezaliwa na sehemu zake za kujilishia, ni misitu
minene.
Hebu fikiria uumbaji wa Kima na ufanano ambao upo
kati ya viungo vyake na vile vya mtu, kichwa, mabega yote, kifua na viungo vya
ndani.
Zaidi ya hayo, amepewa akili na utambuzi/uwelekevu
kwa sababu ya hizo huelewa ishara na maelekezo ya bwana wake. Kwa ujumla huiga matendo ya mtu kama
anavyomwona. Yuko karibu sana na mtu
katika ubora wake, tabia na asili ya kuumbwa.
Inapasa iwe kama ni onyo kwa mtu kwamba azingatie
akilini kwamba katika asili na umbo ni sawa na wanyama akifanana nao kwa
ukaribu sana na kama asingepewa akili, ujuzi/utambuzi na uzungumzaji angekuwa
sawa tu kama wanyama.
Kuna maongezeko kidogo katika muundo wa (kuumbwa)
kima umtofautishao na mtu k.m. kinywa, mkia mrefu, nywele zifunikazo mwili
mzima. Tofauti hizi, hata hivyo,
zisingemzuia kuwa mwanadamu, kama angelipewa stadi za hoja, akili na
uzungumzaji kama mtu. Tofauti yenyewe
hasa ya mpaka baida yake na mtu, kwa hiyo, ni kwa ajili (ya kukosa) tu njia za
hoja, akili na uzungumzaji.
Hebu fikiria Rehema za Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.)kwa
wanyama hawa katika kuipa miili yao mfuniko wenye aina mbali mbali za nywele
kuwalinda dhidi ya misukosuko/matatizo ya kipupwe. Na wamepewa kwato, zilizopasuliwa na
zisizopasuliwa, au miguu fumba kwa kuwahifadhi.
Si wenye mikono, wala viganja wala vidole kusokotea nyuzi na kufuma, na
kwa hiyo mavazi yao yamefanywa ni pamoja na sehemu ya umbo la miili yao,
kuwahifadhi maisha yote bila kutengeneza na kubadilisha.
Mtu, iwayo yote, ana mikono na ufundi wa kufuma nguo
na kusokota nyuzi. Hutengeneza nguo na
mara kwa mara huibadilisha kwa faida nyingi upande wake. Miongoni mwa hizo hujishughulisha na
utengenezaji nguo zake na kwa hiyo akaepukana kutokana na shughuli (mbaya)
zenye kudhuru na uvivu. Huiacha kazi
yake ya kushona wakati apendapo kuwa nyumbani.
Anaweza kutengeneza aina mbalimbali za mavazi kwa burdani apatayo katika
kubadili kwa njia ya fahari na kadhalika.
Hutayarisha soksi na viatu kwa njia ya utendaji mzuri kuhifadhi miguu
yake. Vibarua, na wafanya biashara kwayo
hupata riziki zao na riziki za jamaa zao.
Hizi aina tofauti za nywele huwasaidia wanyama kama mavazi ambapo kwato
zao na miguu - fumba kama viatu.
Hebu fikiria tabia hii ya asili ya wanyama, nayo ni,
ufichaji wa miili ya wafu wakati inaokufa kama vile watu wanavozika maiti
wao. Hakuna hata mwili mfu mmoja wa
hayawani na wanyama unaoonekana. Hawako
mbali sana kiasi cha kutokuonekana. Kwa
ukweli idadi yao ni kubwa zaidi kuliko ile ya watu.
Yatazame makundi ya kulungu, nyati, punda wa porini,
mbuzi mawe na paa na pia jamii mbali mbali za wanyama na hayawani kama vile
simba, nyumbu, mbwa mwitu, chui n.k., na aina aina za wadudu waishio ndani ya
matumbo ya ardhi na kutembea juu take, katika majangwa na milima, na kadhalika
ndege warukao kama kunguru, kwale, bata, korongo, njiwa, na ndege wa
mawindo. Hakuna mizoga yao tunayoiona
isipokuwa michache ambayo mwindaji huipata, kama mawindo au ile inayonyafuliwa
na hayawani. Likiwa ni jambo la ukweli,
wakati wanyama hawa wanapopata hisia za kukaribia kifo (kufa), ujificha katika
baadhi ya sehemu za siri na kufia humo.
Zitazame sanaa ambazo mtu (mwanadamu) amejifunza
kutoka wanyama hawa - mfano wake wa kwanza.
Aliona kunguru wawili wakipigana.
Mmoja akamuua mwingine na kisha akauzika mwili wake mfu, hivyo Kabil
akajifundisha kuchimba shimo na kuzika maiti ya ndugu yake Habil. Hayo yalifanyika chini ya mwongozo wa Mwenye
Nguvu zote Allah (s.w.t.). Wanyama hawa
walipewa hisia hizi kumwokoa mwanadamu (mtu) kutokana na msiba wa matatizo hayo
na milipuko ya magonjwa ambayo yangeweza kuja (kutokea).
Fikiria silika ambazo kwazo (wanyama) kwa desturi
wamepewa na Mwenye Kguvu zote Allah kwa Rehema zake zisizo na mwisho ili kwamba
asiache kiumbe chochote kunyimwa Rehema zake ingawa hii haiko chini ya Stadi za
kufikiria hali ya usawa.
Paa humeza nyoka lakini hanywi maji hata kama kiu
yake itakavyokuwa kali namna gani, kwa kuchelea sumu inayosambaa ndani ya mwili
wake ambayo kwa sababu ya maji ingemuua.
Huzunguukia mapipa ya maji.
Hupiga kelele kwa sababu ya ukali wa kiu lakini hagusi maji kwa kuchelea
(kuogopa) kifo. Unaona kujizuia kukubwa
huku ambako wanyama hawa wanako bila kujali kiu kali kwa sababu ya hofu au
dhara katika hali ambayo mtu mwenye akili na busara hawesi kustahimili.
Mbweha nae, asipopata chakula kwa njia yoyote ile
hujifanyia "kifo cha hadaa na kulitanua tumbo lake kuwadanganya ndege
waamini kuwa kafa. Maru tuu ndege wakija
kumzunguuka kwa kutaka kuunyofoa mwili
uonekanao kama mzoga, huwashambulia na kufanya mlo mzito wa nyama zao.
Sasa, sema, nani aliyetoa wlekevu huu kwa mbweha
asiyezungumza na asiye na akili? Hakika
ni Yeye Yule Ambaye amechukua juu Yake Mwenyewe Jukumu la kumlisha. Kwa vile mbweha hawezi kufanya shughuli zile
ambazo hayawani wengine wanaweza, k.m.
shambulio la moja kwa moja juu ya mtesi, amepewa werevu na hadaa kama
njia za kujipatia riziki (maisha).
Dolfin (Samaki kama nyangumi mdogo) huhitaji ndege
kama watesi. Humkamata samaki na kumuua
na kumuweka ili kwamba aelee juu ya maji ambapo yeye mwenyewe akijificha chini
yake akiyavuruga maji wakati wote kuufanya mwili wake ufichike. Mara tuu ndege anapomrukia ghafla yule
samaki, huruka kwa ghafla juu yake na kumshikilia yule ndege. Kwa werevu huu humpata mtesi wake (riziki).
Kisha niliomba maelezo kuhusu chatu na wingu.
Imam (a.s.) akajibu kwamba: Wingu ni mfano wa
Malaika kumkamatia (kumshikilia) chatu wake popote atakapomwona, kama vile jiwe
la sumaku linavyoshikilia chuma.
Hanyanyui kichwa chake kutoka ardhini kwa sababu ya kuchelea (kuogopa)
wingu hilo, isipokuwa katika (majira ya) kiangazi wakati anga ni nyeupe bila
dalili ya wingu na kisha litokeapo tu (hilo wingu) mara moja hutoweka.
Niliuliza, Kwa nini wingu limefanywa mtawala wa
chatu kumshililia popote litakapomwona?
Imam (a.s.) akajibu,"Kumwokoa mtu (mwanadamu)
kutokana na madhara yake."
Nilisema, "Maulana! umetoa maelezo ya ulimwengu
wa wanyama kwa ukamilifu kufanya kama kifungua macho kwa kila mtu. Tafadhali hebu toa baadhi ya maelezo kuhusu
Siafu na ndege".
Imam (a.s.) akasema,"Timaza katika taya za siafu
huyu mdogo. Je, unaona kasoro yoyote
ndani yao inayoathiri faida yake? Je,
umetoka wapi ulinganifu huu na hadhari?
Hakika ni kutokana na ustadi uleule na usanii ambao umetomika katika
ujenzi wa uumbaji wote, mkubwa au mdogo.
Hebu tizama siafu jinsi wanavyokusanyika pamoja
kukusanya chakula kwa ajili yao. Utaona
kuwa wakati siafu wengi wakiazimia kuchukua nafaka kupeleka kwenye nymba zao
wanafanana na watu wengi wanaojishughulisha na kupeleka nyumbani nafaka
zao. Siafu kwa kweli huonyesha juhudi na
shughuli ambazo watu hawawezi kuzifanya.
Huoni jinsi wanavyosaidiana kila mmoja katika kuchukua nafaka kama
watu? Wanazivunja nafaka vipande vipande
zisije zikachipua na kuwa zisizo na maana kwa dhumuni lao. Kama zikipata unyevu nyevu, huzisambaza
zipate kukauka. Siafu hotoboa mashimo
yao sehemu zilizonyanyuka, mbali kutokana na hatari ya mafuriko.
Shughuli zote hizi, iwayo yote, hazipo bila uamuzi wa
hoja, wenye silika halisi, ambazo kwazo miundo yao imejaaliwa nazo, kwa ukarimu
wa Mwenye Nguvu zote Allah.
Hebu mtizame mdudu aitwae "Lais" (aina ya
buibui) kwa kawaida huitwa simba wa inzi.
Ukubwa ulioje wa werevu na ustadi na upole aliojaaliwa mao kwa utafutaji
wa riziki zake. Uatona kwamba wakati ana
hisia ya kufikiwa na inzi humpuuza kwa muda kujifanya kama kamba vile mwili
wenyewe ni usio na uhai (umekufa).
Wakati akihisi kwamba inzi hayupo katika hofu yoyote ya kukamatwa na
hana habari kabisa ya kuwepo kwake (buibui) huanza kunyemelea kuielekea katika
mwendo wa kunyata pole pole hatua kwa hatua mpaka amfikie karibu kiasi cha
kuweza kuikamata, akiwa yu ngali ameishikilia, huikumbatia na kuizingira kwa
mwili wake wote kuzuia kuponyoka kwake.
Hushikilia hivyo mpaka ahisi kuwa inzi huyo ameishiwa nguvu na viungo
vyake vimetulia, na hapo sasa huigeukia za kuila. Hii ndiyo njia aitumiayo kwa kuishi.
Buibui wa kawaida hutanda utando wake na kuutimia
kama mtego kwa kukamatia inzi. Hukaa
amejificha ndani yake. Mara tu inzi
anaponaswa humrukia kumkamata na kumkata
kata katika vipande. Huendelea
kuishi katika njia hii. Na hali hii
indivyo ilivyo kwa mbwa, simba muwinda na mtengo wa kunasia wakati wa
kuwinda. Hebu angalia mdudu huyu mnyonge
jinsi alivyotunukiwa na silika (akili) ya kukamatia windo lake ambalo mtu
hawezi kufanya bila kutumia matengo na ala (vyombo vya kazi).
Usitoe kasoro katika kitu chochote, kwani kila kitu
kina funzo (Somo) la kufundisha kama vile siafu n.k. Maana nzuri mara nyingi huelezewa kwa kitu
kidogo bila kupunguza thamani yake kama vile dhahabu haipunguki thamani kama
itapimwa dhidi ya (vipimo) vitu vitokanavyo
na chuma.
Hebu fikiria umbo la mwili wa ndege kama alivyoamriwa
kwamba angeruka juu angani. Ametunukiwa
mwili mwepesi na kiulinganifu muundo imara.
Ana miguu miwili badala ya minne, vidole vinne badala ya vitano, tundu
moja kwa kutolea uchafu badala ya mbili.
Ametunukiwa kifua kilichochongoka (kumuwezesha)
kuruka angani kama vile mashua ilivyojengwa kupasua majini. Ana manyoya marefu magumu katika mbavu zake
na mkia kumsaidia kuruka juu. Mwili wote
umefunikwa na manyoya kwa kujazwa hewa ya kurukia juu angani.
Kwa kuwa imeamriwa kwake kwamba lishe yake itakuwa ya
nafaka na nyama ambazo atameza bila ya kutafuna, meno yamekosekana katika umbo
lake na amepewa mdomo imara kwa kutafutia chakula ambao kwa huo anaweza
kuokotea chakula. Hauumizwi wakati
aokotapo wala kuvunjika amegapo nyama.
Kwa vile hana meno lakini hula nafaka na nyama
mbichi, joto jingi hufanyizwa ndani ya tumbo lake ambalo hufanya kazi ya kupika
chakula chake bila kuhitaji kutafuna. Ni
kama vile mfano wa mbegu za zabihu hutoka nje ya tumbo la mtu kama zilivyo
ambapo zinapikika kabisa/kikamilifu katika tumbo la ndege.
Wameumbwa hivyo kwamba watage mayai badala ya kuzaa
watoto ili kwamba wasije wakapata uzito wa aina yoyote wa kuvumilia wakati wa
kuruka kwa sabubu ya kilengwa katika mfuko wa uzazi kikaacho humo ili kikuzwe
kikamilifu.
Kila kitu katika muundo wake kimeumbwa hivyo ili kiwe
cha kutosheleza kufaa kwa hali yake katika maisha. Iliamriwa pia kwamba ndege ambao ni wenye
kuruka juu angani wakae kwa juma moja au juma mbili au juma tatu wakilalia
mayai, kwa kutotoa vifaranga vyao. Kisha
huvigeukia kwa hadhari yao yote.
Analo gole kubwa la kutosha kuwaletea vifaranga vyake
na chakula ambacho kwama kwa hicho pia anaweza kujilisha.
Nani aliyemuwekea majukumu kwanza ajaze gole lake kwa
nafaka zilizochumwa shambani, na kisha aweke mavuno hayo katika umio la
vifaranga?
Kwa nini anachukua taabu yote hiyo ingawa hana stadi
ya kuhoji wala hana mategemeo yoyote ambayo mtu hawazia kuhusu watoto wao -
heshima, kuishi kwa jina, na urithi n.k.
Hii ni shughuli ambayo huonyesha kwamba ni fadhila maalum kwa vifaranga
vyake chini ya mgawo maalum wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) ambao udege
mwenyewe hawezi kujua, wala kuhoji juu yake.
Na ni nini hicho? Ni mpango kwa
ajili ya kuishi kwa taifa.
Hebu mtizame kuku na uone jinsi alivyo na wasiwasi wa
kutaga mayai na kutotoa vifaranga ingawa hana kiota chochote mahsusi wala si
mayai kutoka jamii hiyo hiyo. Hupiga kidoko
(mlio wa kuku mwenye vifaranga au anayetaka kutaga), hutimua manyoya yake,
huacha lishe yake, isipoluwa ipewe mayai ya kulalia na kutotoa vifarange, kwa
nini?
Ni hivyo ili kuhifadhi taifa. Isingeamriwa hivyo kiasili, nani ambaye
angeifadhili kwa hifadhi ya taifa, ingawa haina stadi ya akili au ya kuhoji?
Hebu tizama kwenye umbo la yai na jauhari nyeupe na
njano ndani yake. Sehemu moja ni kwa
ajili ya kufanyizwa kifaranga ambapo inyingine ni ya kukipatia lishe mpaka
wakati huo kitakapolitoka yai.
Hebu fikiria ustadi ulio ndani yake kwa vile umbo la
kifaranga lilikuwa libebwe humo kiusalama ndani ya ganda (kaka) bila kuruhusu
zahama yoyote ya nje, lishe yake imewekwa ndani yake ambayo ni ya kutosha mpaka
kitoke nje.
Mtu ambaye amefungwa (jela) kiusalama bila ya fikio
lolote kwake huwa anapatiwa chakula cha kadiri kumtosha mpaka kuachiliwa kwake.
Hebu fikiria gole/umio la ndege na ustadi ulio ndani
yake. Tumbo limekaribiwa na mrija
mwembamba kuruhusu lishe kufika ndani yake kwa kiasi kidogo kidogo. Bila gole/umio nafaka ingalichukua muda
kufika tumboni.
Ndege katika ujuzi wake wa kuhisia hali ngumu ya
baadae, hujaza gole/umio lake kwa haraka. Gole/umio lake limeumbwa katika
muundo wa shanti (aina ya mkoba)
iliyoangikwa mbele yake, ili kwamba ijae kwa haraka kwa chochote kile
ikipatacho, kisha pole pole hukihamishia tumboni.
Kuna faida nyingine katika gole/umio. Baadhi ya ndege hushughulika na kuhamisha
chakula kuwapelekea watoto wao.
Gole/umio huwasaidia kukihamisha kwa urahisi.
Baadhi ya watu wa mafundisho haya ya maumbo ya asili
hudai kwamba rangi kuwa mbalimbali na maumbo tofauti ya ndege vimetokana tu na
mchanganyiko wa vitu vya asili na tabia katika linganifu mbalimbali. Havikutokea kuwa hivyo kutokana na Usanii
wowote mahsusi.
Urembo huu unaouona kwenye tausi au kwale na uzuri
halisi, kama kwamba msanii fulani mwenye brashi nzuri ameitimiza sanaa ya uzuri
wa picha.
Utaweza vipi mchanganyiko huu usio wa akili uulete
uzuri huo wenye kuonekana bila kombo yoyote?
Ikiwa vitu hivi vya sanaa vimejitokeza kuwa viumbe
bila ya Msanii Mwenye Nguvu zote, ni vipi uzuri huu na mfanano ungehifadhika?
Hebu tizama kwa makini katika manyoya ya ndege,
utayaona kama nguo iliyofumwa na nyuzi nzuri.
Unywele mmoja umesokotwa na mwingine kama vile kipande kimoja cha uzi
kinavyosokotwa na kingine.
Tizama katika umbo lake. Kama unalifungua, hufunguka bila kuchanika
kuruhusu kewa kujazwa ndani na kuruhusu ndege kuruka wakati apendao.
Ndani ya unyoya utaona ufito madhubuti uliofunikwa na kitu kama unywele
ili kwamba, kwa sababu ya umadhubuti wake huyashikilia (manyoya haya). Ufito u wazi ndani (kama mrija) ili kwamba
usiwe mzigo kwa ndege huyo na kuzuia urukaji wake.
Je, umewahi kuona ndege wa miguu mirefu na ukadiriki
kufikiria faida aliyonayo kwa miguu mirefu hiyo?
Mara nyingi (ndege huyo) huonekana kiulinganifu
katika maji ya kina kifupi. Utamwona
kana kwamba yuko katika lindo mahali alipo akiwa amesimama juu ya miguu yake
mirefu.
Hufanya lindo kwa vipitavyo katika maji. Akiona kitu chochote chenye kulika pole pole
hukisogelea na hudaka na kumshikilia mtesi wake. Kama miguu yake ingekuwa
mifupi zaidi, tumbo lake lingegusa maji katika nyendo zake za kumnyemelea mtesi
wake na pengine lingevimba na kushindwa kumkamata mtesi wake. Kwa hiyo ametunukiwa na mihimili (miguu)
miwili mirefu kukidhi/kutimiza haja yake bila kikwazo.
Hebu fikiria kazi nyingine za umahiri (ufundi) ambazo
zimetumika katika kuumbwa kwa ndege.
Unaona kila ndege mwenye kinga ya miguu mirefu amepewa shingo ndefu
vilevile kumuwezesha kuokota chakula chake kutoka ardhini. Wakati mwingine hutokea kwamba mdomo mrefu
unatengenezwa kufanya kazi ya shingo ndefu ikipelekea kwenye urahisi utakiwao.
Je, huoni kwamba uumbaji wowote unaofikiria utauona
barabara na umejaa ustadi?
Tizama kwenye mimea ambayo ndege hawa wanaitafuta
nyakati za mchana. Haitokei kamwe kwamba
haipatikani lakini hawaipati ikiwa
imekusanyika mahali pamoja.
Wanaipata kwa kuitafuta na kwenda
huku na huko. Hali kama hii hujitokeza
katika viumbe wengine
Utukufu ni wake Mwenye Nguvu zote Allah
(s.w.t.). Ambaye amegawanya riziki na
akapanga njia mbalimbali za namna ya kuisambaza.
Haikupangwa katika hali ya kwamba isifikiwe
(isipatikane hiyo riziki) kwa viumbe ambavyo huihitaji wala haikupangwa, kwamba
njia ya kuifikia iwe nyepesi na kwamba ipatikane bila juhudi zozote kufanyika
kwani kuwa hivyo kungekuwa hakuna maana kama chakula kingelipatikana kwa wingi
katika sehemu moja yoyote ile wanyama wangekuwa walafi, kamwe wasingeitoka
sehemu hiyo, ingepelekea kutokuyeyushwa chakula tumboni na (kutokea)
maangamizi.
Watu pia, kwa sababu ya uwingi (wa riziki) wangepatwa
na hali ya kuwa na kiburi na majivuno na matokeo ya misiba na matendo
maovu."
Imam (a.s.) aliniuliza, "Unajua kuhusi ndege
kama vile bundi na popo ambao hutoka nje wakati wa usiku tu, na kuhusu vitu
walavyo kama chakula chao?
Nilijibu,"Sijui."
Yeye (a.s.) akasema, "Chakula cha hawa ni
mchanganyiko wa aina mbalimbali za wadudu waliotawanyika katika anga, k.m. mbu,
nondo, wadudu walio kama nzige na buibui n.k.
Siku zote wako kwenye anga, hakuna sehemu ilivyo huru bila wao
kuwepo. Kama ukiwasha taa usiku juu ya
paa au sehemu yoyote ya eneo la nyumba, wengi wa aina mbalimbali za wadudu hao
hujikusanya kuizunguuka taa (hiyo).
Wametokea wapi?
Hakika wametokea sehemu za karibu tu.
Kama mtu yoyote atasema kwamba wanatokea misituni na mashambani,
atajibiwa kwa kuulizwa kwamba ni vipi wanafika upesi sana na vipi wanaweza
kuiona taa iliyowashwa ndani ya nyumba iliyozunguukwa na nyumba nyingine
nyingi, ambapo kusema kweli hawachukui muda mrefu kuja kuizunguuka hiyo
taa. Ni wazi kutokana na hili kwamba
wote hawa wametawanyika kila mahali katika anga na ndege wale wanaotoka usiku
kuwakamata na kujilisha kwa hao.
Tizama vipi lishe ilivyoandaliwa kwa ajili ya ndege
ambao wanatoka usiku kwa njia ya wadudu hawa, waliotawanyika katika anga.
Jaribu kuelewa madhumuni ya uumbaji wa viumbe hivi
vyenye uhai, isije ikawa mtu fulani akafikiria kwamba vimeumbwa bure bila faida
yoyote.
Popo ni kiumbe wa ajabu, yu katikati baina ya ndege
na mnyama wa miguu minne, kwa kweli amejamiika zaidi kwa mnyama wa miguu minne,
na masikio mawili yatokezayo, meno na nywele nzuri. Huzaa watoto wake, ambao huwalisha kwa maziwa
yake. Hukojoa na kunya. Hutembea katika misimu yote minne. Tabia hizi zote ni kinyume (tofauti) na zile
za ndege. Hujitokeza nje usiku tu na
kujilisha kwa wadudu waliosambaa katika anga.
Baadhi (ya watu) husema hali chochote, bali huishi tu
kwa hewa fufutende (vuguvugu) kama lishe.
Hii siyo sahihi kwa sababu mbili, kwani kukojoa na
kunya, ni vithibitisho vya matumizi ya chakula kigumu. Kisha ana meno, kama asingekuwa anakula, meno
yangekuwa hayana maana, ambapo kwamba hakuna kitu katika uumbaji kisicho na
maana.
Kiumbe huyu ana sifa zijulikanazo vizuri. Kinyesi chake kimechanganyika na vitu
vingine. Umbile lake la kushangaza
lenyewe ni la ajabu. Huruka huku na huko
kama apendavyo kwa faida yake mwenyewe - ishara ya Ujuzi Mkuu wa Mwenye Nguvu
zote Allah (s.w.t.).
Ndege afumae (kiota) hujenga kiota chake wakati
mwingine katika miti. Kama akiona nyoka
mkubwa anaelekea kwenye Kiota chake, hupatwa na wasiwasi. Hutafuta huku na huko njia za usalama Mara
tuu anapopata mbegu yenye miba huichuma na kuitupa kutokea kwa juu kwenye mdomo
uliowazi wa nyoka. Nyoka huanza
kugaragara kwa uchungu na humsukasuka mpaka kufikia kifo.
Kama nisingekuelezea hivi, je, ungeweza kudhania
kwamba mbegu yenye miba ingeweza kuwa na faida kama hizi, au mtu yoyote angeweza kufikiri kwamba ndege mkubwa au
mdogo, angeweza kufanikisha mpango kama huo?
Jifunze somo kutokana na hili. Yako mambo mengine mengi yenye faida
zisizojulikana ambazo huhitaji maelezo ya matukio mapya au habari zitakiwazo
kufahamika.
Hebu fikiria kuhusu nyuki na juhudi za pamoja za
kuzalisha asali na kundi la nyuki la pande sita, na werevu mwingi wa silika
uliowekwa ndani (yake). Utaona ni wa
kustaajabisha mno na wa kutatanisha, wakati ukifikiria kazi zake. Utaona
uzalishaji wao (wa asali) ni mkubwa kabisa na ni tumizi zuri kwa wanadamu.
Na kama utamtizama fundi huyo (nyuki) utamuona hana
akili, asingeweza kujitambua mwenyewe, nini la kusema kuhusi mengine.
Hivyo kuna hoja iliyo wazi katika hili kwamba usahihi
katika ufundi na ustadi si vyenye kutokana na nyuki (mwenyewe) bali ni (Ufundi
na Ustadi) Wake Yeye Mwenye Kuweza yote,
Ambaye amemuumba katika umbo hilo na akamtiisha kwa kuwahudumia
wanadamu.
Hebu mtizame nzige alivyo mnyonge, lakini aliye
imara. Hakuna yoyote awezaye kujikinga
dhidi ya kundi la nzige, kama litauvamia mji.
Je, hujui kwamba kama yeyote yule katika Wafalme wa
ulimwengu mzima atoke na majeshi na jamaa zake kuwapiga nzige, asingeshinda?
Je, hii siyo hoja yenye kudhihirisha Uwezo Mkuu wa
Mwenye Ngugu zote Allah (s.w.t.) kwamba (viumbe) vyenye nguvu nyingi kabisa
katika uumbaji wake visingeweza kuhimili shambulio la viumbe vilivyo dhaifu
kabisa katika Viumbe Vyake? Watazame
jinsi wanavyoifunika ardhi yote kama mafuriko, wakizagaa juu mlimani, jangwani,
uwandani na mjini, wote kwa umoja, hivyo kwamba kundi lao huzuia hata mwanga wa
jua.
Sasa kadiria ni miaka mingapi ingehitajika
kutengeneza kundi hilo kwa mkono (wa mtu).
Mwenye Nguvu zote Allah ametoa hapa hoja nyingine ya
uwezo Wake Mkuu ambao hakuna kiwezacho kuupunguza na kwa huo hakuna kiwezacho
kuuongeza.
Hebu fikiria samaki na hili ambazo zipo chini ya mazingira iliyo amriwa
kuendelea kupelekea maisha yake. Haina
miguu, kwa kuwa makazi yake ni katika maji na haihitaji kutimbea (na
miguu). Haina mapafu, kwa vile haiwezi
kuvuta hewa. Imewekwa (iishi) chini ya
uso wa maji.
Badala ya miguu, imejaaliwa na mapezi madhubuti
ambayo kwayo hupazua maji katika pande zote; kama vile baharia wa mashua
akatavyo maji katika pande zote kwa
makasia yake. Ina mfuniko wa magamba
mazito yaliyounganishwa na kile lingine kama pete za koti la deraya kujilinda
dhidi ya ajali. Ina stadi kali ya
kunusa, kama fidia kwa uoni dhaifu usababishwao hivyo na maji. Hunusa kitu chake kutoka kwa mbali na (hapo)
hukifuatia. Ni kwa njia ipi nyingine
ingeweza kutumia kufahamu asili na mahali kilipo chakula (chake)? Na, elewa vilevile, kwamba inazo tundu sehemu
zote kuanzia kinywani mpaka masikioni, ambazo kwazo maji hupita na kuipa
stawisho la kuburudika sawasawa kama lile linalopatikana kwa wanyama wengine
kwa kuvuta kewa halisi iliyopoa ya upepo
wa asubuhi.
Sasa, fikiria tabia zake za kiuzazi. Idadi ya mayai ndani ya samaki ni zaidi ya
kadiri. Sababu ni kuongeza chakula
kiwezekanacho kuwa kwa viumbe vingine hai kwa vile wengi zaidi katika wao
wanaishi kwa kula samaki pembezoni mwa madimbwi ya maji, katikati ya mapori.
Mara tu samaki apitapo, humrukia juu yake.
Kwa vile samaki ni mawindo ya hayawani, ndege, watu na hata samaki
wengine, mambo yamepangwa kwa namna kuiweka idadi ya samaki kuwa juu.
Hebu fikiria aina za wanyama wenye rangi mbalimbali,
ma-kaka (maganda), maisha ya majini na jamii mbalimbali za samaki, kupata
fununu ya ustadi mkubwa mno wa Mwenye nguvu zote Allah kwa upande mmoja na
silika (maumbile) dhaifu ya elimu hii imilikiwayo na viumbe. Hawana mpaka katika idadi wala sifa zao
hauziwezi hujulikana, isipokuwa kwamba asijue moja baada ya nyingine kwa fursa
ziwezazo kutokea.
Kama kwa mfano "Cochineal" (vitu vyenye
rangi angavu nyekundu iliyofanywa kutokana na miili iliyokauka ya aina fulani
ya wadudu), rangi yake ilisomwa yote na watu, imeelezwa mbweha azururaye
ufukweni mwa bahari, alimpata na kumla Halzuuni (mdudu mwenye rangi). Mdomo wake ulipatwa na rangi. Rangi hiyo iliwavutia watu ambao walianza
kumtumia mdudu "Cochineal" kama rangi ya kuchovyea vitu. Viko vitu vingine vingi ambavyo tabia zao
huja kujulikana kwa watu mara kwa mara.
Ilikuwa adhuhuri.
Bwana wangu aliamka kwa ajili ya Sala, akiniambia nije kwake (tena)
mapema asubuhi ijayo.
Nilirejea nyumbani nikiwa nimefurahishwa maradufu kwa
tunu ya maelekezo katika elimu niliyopata kutoka kwake.
Kwa shukurani nyingi kwa Mwenye Nguvu zote Allah
niliupitisha usiku huo kwa kufurahia sana.
Niliwasili mapema asubuhi ya siku ya tatu, na kwa
kuruhusiwa, niliingia, na nilipoombwa kukaa nilikaa.
Yeye (a.s.) alianza, Ewe Mufazzal! nimekuelezea kwa
kina na ukamilifu zaidi kuhusu uumbaji wa mwanadamu na usanii ustaajabishao wa
Mwenye Nguvu zote Allah ambao umepelekea kwenye ukamilifu wake na masomo ya
kujifunza kutokana na mabadiliko kidogo ya manzili zake. Vilevile nimeshughulika na maelezo ya
ulimwengu wa Wanyama.
Sasa natoa maelezo yenye kuhusu anga, jua, mwezi,
nyota, mbingu, mchana na usiku, kiangazi na kipupwe, pepo, kanuni za misimu
minne, mvua, miamba, milima, ulimwengu wa mimea, mitende na miti ya kawaida
kuonyesha kwayo ishara na masomo ya kujifundisha humo.
Hebu itizame rangi ya mbingu na ona jinsi Usanii
ufaavyo kwa makusudio (ya mambo). Rangi
hii mahsusi ni dawa ifaayo kuliko zote kwa kutia afya na nguvu ikilinganishwa
na rangi nyingine zote. Hata madaktari humuelekeza mtu kuangalia kwenye rangi
ya kijani au katika rangi nyingine iliyozidi katika kijani kibichi kwa ajili ya
maradhi fulani ya jicho.
Madaktari walio wafanisi (hodari) humuelekeza mtu
mwenye udhaifu wa kuona kuangalia kwenye beseni la rangi ya kijani lililojazwa
maji.
Hebu tizama
jinsi Mwenye Nguvu zote Allah alivyoiumba mbingu kwa rangi ya kijani ikageuzwa
kuonekana nyeusi ili isije ikasababisha upungufu fulani, kwa kule kurudia rudia
kuangalia.
Hali hii hii ambayo watu wameigundua kitokana na
kufikiri na kufanya majaribio ni hali halisi ili kwamba wale ambao wangejifunza
somo kutoka humo, na wapotofu - Allah (s.w.t.) awaangamize, wanapotoka.
MAWIO NA
MACHWEO (YA JUA)
Hebu fikiria kuchomoza na kuchwa kwa jua katika
kuingia kwa mchana na usiku. Bila
kuchomoza jua, shughuli zote za ulimwengu zingesimama. Ulimwengu ungezama katika giza bila kuwepo
uwezekano wa kazi au maisha (riziki).
Kungekuwa hakuna raha (furaha) katika maisha bila ya athari nzuri ya
mwanga wa jua.
Faida za mawio ya jua ziko wazi kabisa na hazihitaji
simulizi nyingi. Hebu fikiria kuchwa kwa
jua. Kama lisinge tua, watu wasingepata
wasaa wala pumziko lolote. Watu bila
kukosa, huhitaji kupumzika na kupata faraja ili kuziponya stadi ya kuyeyusha na
utumiaji mzuri wa chakula (mwilini) na kutuliza na kupumzisha mishipa ya fahamu
ya mwili.
Tamaa yao, kwa kutaka kuendelea kufanya kazi (bila ya
kupumzika), kungesababisha matatizo makubwa kimwili, kwani wengi wameazimia na
kukakamia kwamba mpaka usiku uwafunike, hawatakuwa na faraja na pumziko, katika
utafutaji wa maisha (riziki) na ulimbikizaji wa mali.
Kuendelea kuwaka kwa jua daima, nako kungeipasha
ardhi kwa joto kali sana na (hivyo) kurudishwa nyuma kwa maisha ya wanyama na
mimea. Mwenye Nguvu zote Allah kwa ajili
hiyo, ameamuru kwamba kutakuwa na vipindi vya kuwaka jua na vya giza, kama taa
ambayo huwashwa na watu wa nyumbani pindi tu wanapoihitaji, na huzimishwa
isipohitajika, ili kuwapa faraja na pumziko.
Nuru na giza vinakinzana vyenyewe kwa vyenyewe na
bado vyote vimefanywa kufaa kwa faida za uboreshaji wa ulimwengu na mtengenezo
mzuri.
Kisha hebu fikiria misimu minne ya majira ya mwaka,
kwa matokeo ya upandaji juu wa jua na utelemkaji wake (kutua) na faida na
mpango uliomo humo.
Miti na mimea hupata mchipuko (muinuko)wa uhai ndani
ya vipindi viwili muhimu vya mwenendo wa jua.
Ugandaji wa mvuke katika anga husababisha kufanyika
mawingu hatimae kuleta mvua. Wanyama
huimarika miili yao na kupata nguvu katika msimu huu.
Kuna upatikanaji wa joto muhimu la uhai katika
kiangazi na vile vile pia kukua kwa vitu ambavyo hukomaa katika kipupwe, mimea
hupata maua na matunda katika msimu huu.
Wanyama hupata msisimko wa kufanya ngono.
Anga hupatishwa joto katika kiangazi ambalo hupelekea
katika kuiva kwa matunda. Taka za mwili
hukazwa. Ardhi hukauka na kufaa kwa
ujenzi na shughuli nyingine.
Hewa husafika wakati wa kipupwe, maradhi hupitishwa (huepushwa). Miili hupata afya. Usiku huwa mrefu zaidi na hivyo kusaidia
katika kufanya majukumu fulani kwa sababu ya vipindi virefu.
Hewa katika msimu huu hufaa shughuli nyingi na vile
vile, ambazo zitachukua muda mrefu kusimulia.
Sasa fikiria mwendo wa jua kupitia mafungu kumi na
mbili ya Zodiac (Burji) kuukamilisha mwaka na ustadi uliomo ndani yake. Hiki ni kipindi ambacho kina misimu hii minne
ya majira - Kipupwe Kiangazi, Masika na Demani ("Spring") katika
ukamilifu wao. Nafaka na matunda huiva
katika mwendo huu wa jua katika mwaka kukidhi haja za wanadamu. Mafuatano ya nyakati hizi za mwaka ni muendelezo
unaojirudia rudia
Je, hujui kwamba kupita kwa jua hili katika kanda za
mbinguni, kutoka ukanda wa Samaki (pisces) na mpaka kuurudia tena, hufanya
mwaka mmoja? Miaka hii n.k. imeendelea
kuwa kama vipimo vya kukadiria muda tangu mwanzo wa dunia katika nyakati zote
zilizopita. Watu wanakadiria kwayo
vipindi vya muda wa maisha, mikopo, mikataba, na mambo mengine ya
biashara. Ni katika mwenendo wa jua hili
kwamba mwaka hukamilika na ukadiriaji sahihi wa wakati ukaanzishwa.
Hebu tizama jinsi jua litoavyo mwanga wake katika
ulimwengu na ustadi gani jua hili limeamriwa kwayo. Kama lingeangaza daima kwenye sehemu moja ya
"Zodiac", bila kubadilisha sehemu yake, faida za mionzi yake
isingepenya katika pande zote kwa sababu ya kuwepo milima na kuta.
Kwa hiyo, limeumbwa hivyo kwamba linachomoza kutoka
Mashariki katika wakati wa kabla ya adhuhuri, likitoa mwanga wake juu ya vitu
vilivyoko upande wa Magharibi, huenda hivyo daima, likieneza mwanga wake kutoka
upande huu kwenda upande huu mpaka kuelekea upande wa Magharibi kutoa na
kutawanya mwanga wake juu ya vitu ambavyo vilishindwa kuupata wakati wa kabla
ya adhuhuri, hivyo ili kutoruhusu pembe yoyote kubakia bila faida na dhumuni
lililokusudia kufanya.
Kama kwa mwaka mzima au sehemu yake tu hali
ingebadilika kuwa kinyume, unaweza ukafikiria msiba wa wanadamu. Kwakweli
ni njia ipi wangeweza kuitumia kwa kuishi?
Je, mtu hachunguzi
mpango huu adhimu ambamo humo taratibu zake zingeshindwa kabisa? Zinafanya kazi kwa kujiendesha zenyewe bila
kuzembea, wala hazichelewi nyuma ya muda uliowekwa kwa uendeshaji wa utaratibu
wa ulimwengu huu na ustawi (wake).
Kuna ishara iliyofunuliwa na Mwenye Nguvu zote Allah
katika uumbaji wa mwezi -kielekezo kizuri.
Watu kwa ujumla wanakadiria miezi katika msingi wake, lakini mwaka
haukuanzishwa kisawasawa nao. Mwendo
wake haukufanyizwa mabadiliko ya msimu wala nyakati za kuchanua maua na kuiva
kwa nafaka. Hii ndiyo maana hesabu ya
miezi na miaka ya miezi iwakaya
hutofautiana kutoka hesabu ya miezi na miaka ya jua. Mieze ya miezi iwakayo hubadilika, hivyo
kwamba wakati mwingine mwizi ule ule una angukia katika majira ya Kiangazi na
wakati mwingine katika kipupwe. Na hivyo
ndivyo ilivyo kwa miezi mingine. Kwa
mfano mwezi wa Muharram unaweza ukachukua kipindi ndani ya majira ya Kiangazi
wakati mwingine, (na) ndani ya majira ya msimu wa mvua kwa nyakati nyingine na
ndani ya majira ya Kipupwe katika wakati mwingine. Hii huonyesha kwamba hesabu ya miezi kwa
miezi iwakayo na hesabu ya miezi ya jua huendelea kubadilika na hailingani kwa
kila mwingine.
Fikiria kwa nini mwezi huwaka usiku na ustadi uliomo
ndani yake. Viumbe hai huhitaji ubaridi
kidogo upatikanao kutokana na giza ili kupata pumziko na faraja. Kukosekana kabisa kwa mwanga na giza leusi
kusingekuwa na ubora wowote, hata hivyo, bila ya uwezekano kwa kazi ya aina
yoyote. Watu huhitaji kufanya kazi
kidogo kwa kutaka kupata burdani la kupumzika wakati wa mchana. Inaweza ikawa kwamba kwa ajili ya ukomo
(ukali) wa joto (la jua) anaweza akafanya kazi katika mwanga wa mwezi kwa
mfano, kilimo, ukamuaji wa maziwa,
ukataji kuni n.k. Mwanga wa Mwezi
huwasaidia watu kufanya kazi kwa kutafuta maisha yao (riziki) wakati wowote wanapopenda kufanya
hivyo. Wasafiri huuona ni mvutio katika
safari zao. Kuchomoza mwezi kumeamriwa
kwa vipindi mbali mbali vya usiku ambao unafanywa kuwa na mwanga mdogo zaidi
kuliko wa jua kwa wakati wa kipindi sawa, wasije watu wakaanza kufanya kazi
katika taratibu ile ile kama wanavyofanya wakati wa mchana bila kupumzika hata
kulazimisha kifo.
Katika awamu tofauti za mwezi, kutokea kwake kama
mwezi mwandamo, kutoweka kwake wakati wa mausiku ya mwishoni mwishoni, kufifia
kwake na kupungua na kupatwa kwake, kuna vielekezo mahsusi kwamba mabadiliko
yote haya yameamriwa kwa faida ya ulimwengu na Mwenye Nguvu zote Muumba Allah
(s.w.t.) ambavyo vinaweza vikasaidia kama mwongozo kwa mtu yoyote apendae
kuufuata mwongozo huo.
Hebu fikiria kuhusu nyota na nyendo zao zenye
kupambanulika. Kuna baadhi miongoni mwao
ambazo hazisogei kutoka maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili yao. Ziko nyingine ambazo husogea kutoka eneo
mpaka eneo na zina nyendo zao zenye kupambanulika. Kila moja katika hizo ina nyendo mbili moja
kwa sababu ya taratibu ya mwendo wa ulimwengu mzima kwa muelekeo wa upande wa
magharibi, na mwingine ni mwenndo wake yenyewe kwa muelekeo wa upande wa
mashariki.
Hii hufananishwa kwa nyendo mbili za mdudu chungu
akiwa upande wa juu wa Kipande cha Kijaa.
Kijaa huzunguuka kwa upande wa kulia na mdudu chungu huenda upande
kinyume (kushoto). Katika hali hii mdudu
chungu atakuwa na nyendo mbili - moja ni ya mwendo wake mwenyewe, mwelekeo wa mbele
na mwingine usiokusudiwa, pamoja na Kijaa.
Sasa hebu ulizia kutoka watu hawa ambao hudai kwamba
nyota hizi zimejitokeza kuwepo zenyewe bila ya Usanii wa Msanii Mwenye Nguvu zote, ya kwamba ni kitu gani
kilichokuwa pingamizi kwa maumbo yao haya yote yawe ni yenye kusimama tu mahali
pamoja au yote kuwa yenye kuzunguuka (kutembea)?
Uumbaji bila Muumba huthubutu mfumo mmoja, kwa nini
kutokee nyendo aina mbili tofauti juu ya mfumo mahsusi na uliopendelewa? Yote haya huonyesha wazi kabisa kwamba mwendo
wa namna mbili za nyota kama unavyoendelea sasa, ni matokeo ya dhumuni halisi,
Usanii na Ustadi, siyo kitu cha bure kisicho na maana kama wanavyodai Walahidi hawa wapendao vitu vya kidunia tu.
Kama Kinzano litaletwe kwamba kwa nini baadhi ya
nyota zimetulia ambapo nyingine zina sogea,
jibu letu litakua kwamba kama zote zingekuwa zimetulia, ishara pambanuzi
ambazo zinaonyeshwa sasa na nyendo zao
kutoka eneo mpaka eneo (lingine) zisingekuwepo.
Siri nyingi hufahamika kwa matukio yaliyohusishwa na juu na nyota
nyingine kwa sababu ya nyendo zao katika njia zao mahsusi. Faida
ipatikanayo sasa katika suala la msimu wa nafaka na hata bashirio n.k.
katika nyendo za nyota chache kwa sasa, isingeweza kufikiwa.
Kama zote zingekuwa na msogeo, kituo chao cha kufika
kisingekuwa na doria za kuweza kutambuliwa.
Mwenendo wa Sayari zisogeazo katika maeneo yao yalizopangiwa, huwezesha
kupatikana taarifa muhimu, kama kadiri ya mwendo wa msafiri inavyopimwa kwa
kipimo cha umbali. Kwa kutokuwepo vipimo
vya maili, au hatua, kadirio la kiasi cha mwendo lingekuwa vigumu (kufanyika).
Kadhalika, kama nyota zote hizi zingekuwa na msogeo
na misogeo ya matakwa tofauti wakati huo, kadirio la kiasi cha msogeo wao
lisingewezekana, kwa sababu katika mahali pa kwanza zilikuwa hazina idadi kuwezekana
kufanya hesabu kwa chombo chochote kile cha kufanyia hesabu au mnajimu, na pili
kwa sababu ya mahali pao ziliopo - baadhi ziko upande wa mashariki, nyingine
upande wa magharibi, bado nyingine ziko pande wa kasikazini na tena nyingine
katikati au katika ncha (mbili za dunia) au hapa, pale na kila mahali. Maeneo yao yangekuwa vigumu kwa kweli
kupangika, na tatu kwa sababu ya ugumu utakanao na nyota zote kupitia katika
safu kumi na mbili. Kisha ingekuwa
haiwezekani kufanya upambanuzi wa aina yoyote, na kwa sababu hii dhumuni lote
la msogeo wao na kuwepo kungebatilishwa.
Kama zote zingesogea kwa kiasi cha mlingano mmoja wa
usogeo, lengo lililomo lingefanywa kuonekana bila faida yoyote kwa mchanganyiko
wa makundi yao (nyota).
Kinzano katika hali hiyo kutoka kwa fundi mtoa makosa
lingepata nafasi kwa kusema kwamba ulinganifu wa mwendo (msogeo) juu ya mfumo
mmoja huonyesha kutokuwepo kwa Msanii - Muumba, kama tulivyokwisha kubalisha
kwa ushahidi wa maelezo kuwepo kwa uhai wa Mwenye Nguvu zote Alah (s.w.t.). Ndiyo maana ni wazi kabisa kwamba nyendo zao
tambuzi, mabadiliko na mizunguuko yao
ikiwa ni yenye malengo, ni kazi ya usanii na upambanuzi.
Hebu fikiria nyota ambazo hutokea vipindi fulani
fulani katika mwaka na hupotea wakati wa vipindi vingine vya mwaka, kwa mfano,
kilimia (Pleides), Mpini kata (Orion), jozi ya nyota za "Sirius" na
"Canopus". Kama zote
zingetokea kwa pamoja, hakuna hata moja ingejitokeza kuwa kama alama maalum kwa
watu kuipambanua, kuijua na kupata
mwongozo, kama watu wapatavyo maarifa kutokana na kupotea kwa
"Orion" na "Taurus" (thaura). Kutokea huku na kupotea kwa lika kimoja
katika nyakati mahsusi kuliamriwa kwa faida ya wanadamu.
Kama vile nyota za kilimia ziliamriwa kutokea na
kupotea katika nyakati tofauti kwa faida mahsusi za watu, kadhalika kundi la
nyota la "Bear" limeamriwa kwa
mandhari isiokoma kamwe isipotee, kwa vile ina jukumu lingine la kufanya, ikiwa
kama boya kwa ajili ya watu kutafuta njia zao katika vijia katikati ya msitu na
bahari.
Kwa vile nyota za kundi hili (la falaki) daima ziko
kwenye mandhari (zinaonekana), watu huzitizama mara tu wanapohitaji kujua kijia
kwa upande wowote. Mambo yote haya mbalimbali hutekeleza faida za wanadamu.
Mbali na hayo, ndani yake mna mwelekezo wa wakati,
kwa ajili ya kilimo, (jumla), kilimo cha bustani, usafiri katika nchi kavu na
baharini. Vilevile kuna udhahiri wa
mambo mengine ambayo yana rejea kwenye nyakati tofauti, kwa mfano kunyesha
mvua, kuvuma kwa pepo majira ya misimu ya Kiangazi na Kipupwe.
Zaidi ya hayo, watu hupata njia yao kwa msaada wao
(nyota) ndani ya Safari (zao) katika nyanda zinazotisha na bahari zinazoogofya
wakati wa masaa ya masiku ya giza. Juu
ya hayo, kuna masomo mengi makubwa ya kujifundisha kutoka nyota hizi ambazo
sama huenda mbele, baadhi hurudi nyuma katika muelekeo wa upande wa Mashariki
au wa Magharibi.
Mambo ya Kimbinguni, mwezi na jua husogea kwa haraka
sana, na kama yangekuwa karibu zaidi nasi na mwendo wao ungekuwa ni wa kusikiwa
kiusawasawa kama ilivyo je, hufikiri kwamba macho yangekuwa kiwi kwa mng'aro
wao na miali kama vile yanavyokuwa kiwi kwa miali ya radi wakati inapoanza
kutoa miali moja kwa moja, ikiiwasha anga iliyoko kati ya nchi na mbingu kama
moto?
Mfano mwingine wa hili ni nyumba yenye dari lake
lililofungwa na mishumaa mingi iwakayo ikikizunguuka kichwa kwa nyendo za kasi
sana. Maho yatalazimika kupofuka na
mhusika kuanguka chini kifudifudi. Hebu
angalia jinsi ilivyoamriwa kwamba (jua na mwezi) vingetembea kwa kasi yao
iliyopo sasa katika umbali mkubwa mno kutoka sisi ili kuuzuia uwezo wetu wa
kuona dhidi ya uharibifu na ugonjwa, wakati bado zinakuwa na masafa yao ya
ajabu kwa dhumuni yatakayo yahudumia.
Nyota ni zenye kung'ara tu kutoshako kutoa mwanga
wakati wa ukosekanaji wa mwezi na kutuwezesha sisi kutembea huku na huko katika
vimulimuli vyao. Mtu nyakati nyingine
huhitaji kusafiri wakati wa usiku, na katika kukosekana kumetameta kwao,
angeona ni vigumu kujisogeza katika njia yake.
Hebu fikiria upole na ustadi ulioamriwa katika
uumbaji huu. Giza nalo pia lilihitajika
na kwa hiyo kipindi kimewekwa, na kuongezeka kwa vimuli muli, ili kutekeleza
malengo tuliyokwisha yashughulikia.
Hebu fikiria ulimwengu pamoja na jua lake, mwezi
wake, nyota zake na "Zodiac"' ambazo daima zinazunguuka kwa kupasika
na amri halisi na hukumu ili kuleta humo faida nyingi kwa wakazi wa ardhini,
kwa mnyama wa rangirangi na falme za mimea katika mabadiliko ndani ya misimu
minne ya majira, siku na mausiku, ambavyo (vyote hivi) vimeelezewa kwako. Je, mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufikiri
kwamba mpango huu ulioratibishwa na usanii ambao hutegemea kanuni na utaratibu
wa ulimwengu unaweza kujitokeza na kuwepo hivi hivi bila ya Msanii Mwenye Kujua
Yote?
Kama mtu mmoja atasema kwamba ni bahati tu ndiyo
iliyosababisha hivi (ulimwengu huu kujitokeza na kuwepo), ni kwa nini hasi
hasemi jambo lile lililo sawa katika uhusiano kwa gurudumu
Na kama akitoa maelezo kama hayo kuhusu gurudumu
Je, atalikataa hili katika suala la gurudumu la mbao
Je, mtu anazo njia au mbinu za kuonea usawa kama kitu
chochote kile kinaiendea mrama mbingu, kama vile vipuli vya mbao vinapotoka nje
ya taratibu (kuharibika).
Hebu fikiria uhusiano wa saa za mchana na usiku. Zimerekebishwa kwa faida ya uumbaji. Saa za mchana au za usiku hazizidi saa kumi
na tano.
Je, unajua kwamba kama masaa ya mchana yangerefushwa
kufikia masaa mia moja au mia mbili, uhai wa wanyama na mimea ungetoweka?
Kipindi hicho kirefu bila pumziko na wasaa (faraja)
kingewaua hayawani, ambapo wanyama wa miguu minne wangeendelea tu
kujilisha.
Watu, vilevile, wangeendelea kufanya kazi tu bila
kusimama na kutokezea kuhatarika kwa maisha.
Uhai wa mimea ungeteketea kabisa
kwa kuathiriwa na kipindi kirefu cha joto la mchana.
Kadhalika, kama usiku ungerefushwa ukalingana
kiusawa, jamii zote za viumbe hai vingezuilika kutembea huku na huko kutafuta
lishe na matokeo ni kufa njaa. Mimea ingepoteza joto lao muhimu, kukawia na
kutoweka, kama vile unavyoona ile mimea ambayo imewekwa hivyo kwa kupata mwanga
mdogo tu wa jua.
Fikiria mzunguuko wa joto na baridi kuhusu ongezeko,
punguko na usawa, na kutokea misimu minne ya majira ya mwaka ifuatanayo mmoja
baada ya mwingine katika ulimwengu na ikishughulika kwa faida yetu.
Zaidi ya hayo, miili husitawi na kutiwa afya
kwayo. Hii hupelekea kwa afya zao na
maisha marefu, kwani kukosekana kwa athari ya joto na baridi moja baada ya
ingine kwa mawumbo yenye mwili wangeumia kwa uharibifu, mvunjiko na udhoofu.
Hizi mbili (joto na baridi), kimoja kuchukua nafasi
ya kingine kidogo kidogo na pole pole.
Utaona kwamba mipunguko inatoa nafasi kidogo kidogo kwa mfuatio wa
muongezeko wa mwingine. Ikiwa mmoja
ghafla umeingilia kati utaratibu wa mwingine.
Ungepelekea kwenye madhara makubwa, kwenye ugonjwa kwa viumbe vyenye
mwili kama vile mtu awezavyo kupata dhara na ugonjwa, kama kwa ghafla atajitoa
kutoka ndani ya bafu yenye maji moto na kujiingiza katika sehemu ya
baridi. Mwenye Nguvu Zote Allah (s.w.t.)
ameamuru badiliko la joto na baridi kidogo kidogo kumzuia mtu kutokana na dhara
la ghafla wa badiliko.
Kama yeyote yule atadai kwamba ukidogo kidogo huu na
kawio, katika mjio wa matokeo ya joto na baridi hufanya mzunguuko wa jua na
mwinamo wake ukivutia sana muda wa mchana, anaweza kuulizwa kama sababu ipi
kuhusu msunguuko wa jua na mwinamo wake wa kidogo kidogo ukivutia sana kawio na
ukidogo kidogo. Kama atajibu kwamba ni
kwa sababu ya anga za pande za Mashariki na Magharibi, anaweza kuulizwa kama
kwa nini iwepo hivyo. Maswali katika
kusudio hili yataendelea kurudiwa rudiwa kuulizwa mpaka alazimike kukubali
umuhimu wa kuwepo Mwenye Kujua yote, Mwenye Dhumuni na Msanii.
Bila joto, matunda mabichi, machachu yaliyo magumu
yasingeweza kupevuka yakawa na utamu na maji mengi yatumikayo kwa kiungo au
viungo, vibichi au vikavu. Bila baridi,
vikonyo visingechipua masikio ya punje kwa usaaji mwingi mno kwa utoshelezaji
wa lishe na mbegu.
Je huzitambui faida za joto na baridi, pamoja na sifa
zao zote ni chanzo cha matatizo kwa miili vile vile? Mna fundisho kwa wale ambao wangetafakari juu
ya hili na uthibitisho kwamba taratibu zote hizi ni kwa faida ya ulimwengu na,
kila kimoja katika viumbe kuna faida kwayo kutokana na Usanii wa Mwenye Nguvu
zote Mwenye kujua yote.
Ngoja nikufahamishe kuhusu baraka za hewa. Je, huoni wakati inapoacha kuvuma kuna udhia
ukaribiao msongo wa roho? Watu wenye
afya kamili huanza kuugua wanaoumwa hudhoofika, matunda huharibika, mboga mboga
huoza, maumbo ya mwili huambukizwa na nafaka huozeshwa? Hii huonyesha kwamba kuvuma kwa hewa ni kwa
faida ya uumbaji wa mpango wa Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote.
Tabia (sifa) nyingine ya hewa imeelezwa hapa. Sauti hufanyizwa kwa mgongano wa vitu, kimoja
juu ya kingine. Inapeperushwa na hewa
mpaka kuyafikia masikio. Watu wote
huendelea kuongea sehemu ya kipindi cha usiku au cha mchana kuhusiana na
mahitaji ya shughuli za kila siku. Kama
hutuba hii ingeacha alama yake katika hewa kama ambavyo maandishi yaachavyo
chapa kwenye karatasi, anga yote iizunguukayo dunia ingejazwa kwayo, na
kufuatia mashaka na fadhaa. Wangehitaji
badiliko katika anga - hewa. Hoja kwa ajili hii ingekuwa kubwa zaidi
kuliko ile ya badiliko la karatasi, kwa kiasi kwamba hutuba ya kuongea
imependekezwa zaidi kuliko maelezo ya kuandikwa.
Mwenye Nguvu zote Muumba, Utukufu ni wake, ameumba njia
hii ya ajabu, ambayo huhifadhi fikira (chapa) kwa muda utoshao tu kuhudumia
mahitaji ya watu wa dunia na hufanya hali nzuri itengenezwe kwa fikira mpya
kupatikana nayo, ambayo ungesababisha mgongano kwayo.
Kupata fundisho kutokana na baraka za upepo uliopoa
uitwao hewa ni lenye kukutosha. Hii hewa
ni msingi wa uhai kwa maumbo yenye miili.
Husaidia kupata uhai wakati tunaivuta ndani kutoka mahali pasipoeleweka na kuiruhusu na
kuhusikana na roho ndani ya mwili. Hewa
hii hii ni njia au chombo kwa kupeleka mawasiliano katika mfumo wa mawimbi ya
sauti kwenda sehemu za mbali. Hewa hii
hii huchukua harufu nzuri kutoka sehemu hadi sehemu. Hebu angalia vipi hewa hupeperusha aina mbalimbali
za manukato kwenye pua yako. Na vilevile
sauti. Hewa hii hii ni chombo cha
kuchukulia joto na baridi, ambavyo hupishana kimipango kwa faida ya ulimwengu.
Hewa inayovuma ni upepo ambao huondoa maradhi mengi
ya mwili. Huhamisha mawingu kutoka
mahali fulani mpaka mahali pengine kwa faida ya jumla kwa njia ya kuganda mvuke
na kuleta mvua. Kisha huyakaza na
yanatawanyika mbali. Husababisha mimea
kutoa maua na matunda. Hufanya milo
laini matunda kuwa na maji mengi. Hupoza
maji kuwa baridi. (Hewa) Inawasha mioto
na kukausha unyevunyevu. Kwa ufupi,
husaidia na kuhuisha vitu vyote vya ardhini.
Bila kuvuma huku kwa hewa (upepo) mboga mboga zingekauka, uhai wa
wanyama ungetoweka na kila kitu kingepotea.
Fikiria vitu vinne vilivyopo vya asili vilivyoumbwa
na Mwenye Nguvu zote Allah kukamilisha dhumuni la kuumbwa kwao
kiutoshelezaji. Miongoni mwao ni ardhi
na eneo lake. Je, ingetosheleza vipi kwa
mahitaji ya mwanadamu kuhusu ujenzi wa nyumba, kilimo, mashamba ya majani,
misitu, vichaka, miti shamba (kwa kutengenezewa dawa) na madini ya thamani,
kama isingekua kubwa mno?
Mtu asingependezwa na angelaumu kuhusu nyanda zisizo
na miti na sehemu zenye kutisha zisizokalika na kuhoji utumikaji wake. Hizi ni sehemu za kuishi wanyama pori, (ni)
makazi yao na mbuga za kujilishia.
Watu wana eneo kubwa mno la kuhamia kama wakihitajia
kufanya hivyo. Sehemu nyingi za uwanda
zisizokalika zimegeuzwa kuwa bustani za matunda na majumba makubwa kwa
kuyafanya makazi ya kudumu ya wanadamu.
Kama ardhi isingekuwa kubwa kno, watu wenweye wangejiona (wangejikuta),
kama waliojengewa ukuta ndani kwa ngome nyembamba, kwani wasingeweza kutoka
kwenye nyumba zao hata kama wangeshinikizwa na hali ngumu.
Tena, fikiria silika iliyopewa ardhi nayo ni kwamba
imewekwa sawa vizuri mno ili kutolekeza kuwa makazi yenye kufaa kwa viumbe
vyote. Mtu amewezeshwa humo kutembea
huku na huko, apate pumziko na wasaa (faraja) ajihusishe katika kilimo na
biashara kwa uthabiti halisi. Kama
ingeelekezwa katika muinamo ingekuwa vigumu kusimamisha majengo na kufanya
biashara na kazi n.k. chini ya hali hizi za matetemeko ya mara kwa mara, maisha
yao yangekuwa mbali mno na yale ya kupendeza.
Hebu yaelewe haya kutokana na matetemeko ya ardhi
ambayo hudumu kwa muda tu na bado watu wanaopatwa nayo huyakimbia makazi
yao. Wangepataje basi pumziko na wasaa
kama hali ya ardhi ingekuwa ya tetemeko wakati wote?
Kama mkinzani akiuliza kwamba ni kwa nini tetemeko la
ardhi hutokea, atajibiwa kwamba tetemeko la ardhi na misiba mingine kama hiyo
iko katika asili ya ilani na maonyo kwa watu kuchukua hadhari dhidi ya matendo
maovu. Kadhalika matatizo ya misiba
ambayo huipata miili yao na mali zao yana dhumuni lilelile kimaoni, wawe tayari
kufanya matengenezo yao na uboreshaji.
Kama wakiwa wema, malipo watakayopata akhera yatazidi thamani ya vitu vyote
vya kidunia. Hutokea wakati mwingine
kwamba kuna malipo yapatikanayo hapa hapa katika ulimwengu huu, kama malipo
hayo ni yenye faida katika ujumla wa watu.
Ardhi katika asili yake ni baridi na kavu, hayo
ndivyo yalivyo mawe. Je, unaweza kuona
kwamba kama ardhi ingepewa asili ya ukavu zaidi kidogo kuwa ngumu kama jiwe
ingeweza kuzalisha mimea yoyote ambayo kwama ni tegemeo la uhai wa
wanyama?
Je, kilimo cha aina yoyote kingewezekana au aina
yoyote ya ujenzi kuwezekana?
Je, huoni kwamba inakushikana shikana kidogo zaidi
kuliko jiwe? Mgeuko wa ulaini kutokana
na asili yake ni kwa ajili ya kutegemewa.
Sura nyingine ya asili ya ardhi kama ilivyoamriwa na
Mwenye Nguvu zote Allah; Utukufu ni Enzi Yake Kuu, ni mwinamo wake wa kidogo
kidogo kutoka kaskazini kuelekea kusini.
Kwa nini Mwenye Nguvu zote Allah, Utukufu uwe kwake, ameiamuru
hivyo? Hakika ni kwa kuruhusu ziada ya
maji baada ya kuinywesha nchi yatiririkie baharini, kama vile paa (la nyumba)
limefanywa kuinama kutoka upande mmoja kuelekea mwingine kuzuia maji
kujikusanya na kuruhusu upitaji wake kuwa rahisi. Nchi imefanywa kuinama kwa sababu hiyo.
Kama isingekuwa hivyo, ardhi yote ingejazwa na maji
yaliyosimama na kutokea kuzuiwa katika biashara na mawasiliano ya barabarani.
Kadhalika, kama hewa isingepatikana kwa wingi mno,
watu wangesongwa roho kwa sababu ya moshi na mvuke kuisongasonga. Kama anga isingekuwa kubwa mno, isingefanya
kazi kama kijumbe kwa ajili ya mwanga na mawingu mazito, ambayo sasa
yanajikusanya kidogo kidogo kwa kufyonza maji.
Maelezo ya hii hewa yamekwisha tolewa ambayo yanapasa kutosha.
Na hiyo ndiyo hali ya moto. Ungekuwa mwingi kama maji na hewa,
ungeteketeza kila kitu katika ulimwengu, bila kuacha njia yoyote ya kuanzisha
kudhibitiwa kwa moto huo, kwani, ni wenye faida kwa mtu kama ilivyo kazi.
Kwa namna hiyo umetunzwa kwenye kuni. Unaweza kutumika wakati inapotokea haja. Umehifadhiwa kwa njia ya kuni. Hauruhusiwi kuzimishwa wote kabisa bali
baadhi yake unahifadhiwa. Kwa namna hiyo
huuhitajiki kuweka bila kikomo kwani kufanya hivyo kungeleta usumbufu
sana. Wala si wa kutawanyika sana
kufanya uteketeze kila kitu katika ujirani wake. Imeumbwa tu katika kipimo sawa huepusha
upungufu.
Una sifa nyingine, kuridhia, umekusudiwa kwa faida ya
wanadamu tu. Wanyama hawana haja
nao. Uchumi wa wanadamu ungeridhika
vikubwa katika kukosekana kwa moto. Ama
kwa wanyama wa miguu minne wao hawana matumizi nao.
Kama Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) alivyoamuru
matumizi yake (huo moto) yawe kwa ajili ya wanadamu peke yao mtu amejaaliwa
kuwa na viganja na vidole ili kwamba aweze kuuwasha na atumie, wakati ambapo
wanyama hawakutunukiwa na viungo hivyo.
Hana hivyo, wamewezeshwa kuvumilia kwa utulivu kutokana na usumbufu wa
ushari wa tumbo na kuwaokoa kutokana na matatizo ambayo mtu atayapata kwa
kukosekana moto.
Ngoja nikuambie sifa ndogo ya moto, ambayo ni bora
sana na ya kufaa, kukuelewesha, ni taa hii ambayo watu huiwasha kupata mahitaji
maalum ya usiku kama watakavyo. Bila
huo maisha ya wanadamu, yangefananishwa
na kuzikwa kaburini. Angewezaje mtu kusoma,
kuandika, kufuma, kushona kwa mashine au kushona kwa mkono katika giza la
usiku? Nini ingekua taabu ya mtu
anayeumwa kutokana na maumivu ya ugonywa akihitajia kutaka kuweka dawa ya
kusugua au kunyunyizia daw ya uvumbi kama uganga uponyao?
Kama maji haya yasingekuwa mengi mno yakitiririka
kutoka kwenye chemchem, mabonde na mifereji, yangesababisha udhia mkubwa mno
kwa watu, ambao huyahitajia wenyewe, kunywesha wanyama wao wa miguu minne na
hayawani, kwa kilimo chao, mimea yao na mashamba yao ya nafaka. Na wakati huo huo wanyama wakali, ndege na
hayawani au samaki na viumbe hai vyenye asili ya nchi kavu na majini
vinavyoishi majini vingeumia kiasi kikubwa mno.
Mbali na hayo, yana faida nyingine ambazo una habari
nazo, lakini thamani kubwa sana na sifa kwayo wewe huzijui. Kisha hebu ona, mbali na faida za jumla na
zenye thamani zilizomo kwayo, kukubali ukweli, uhai wote wa hayawani na mimea
katika uso wote wa ardhi una asili katika maji, yanatumika katika taratibu
nyingine za vinywaji kuvifanya mororo kwa ladha ya kupendeza. Hutumika kuondoa uchafu mwilini hali
kadhalika na kufulia nguo. Udongo
huloweshwa kwayo kuufanya ufae kwa kutengezea vyombo vya nyumbani n.k. yanatumika
kuzimishia moto kama utawaka kusababisha madhara. Mtu hupata kuburudika baada ya uchovu na
utumishi. Vili vile kuna vitu vingine
vihudumiwavyo na maji, ubora mkubwa na thamani iliyomo humo huweza kujulikana
tu wakati wa kuhitajika.
Pamoja na kuhusu haya yote, unatia shaka juu ya
thamani ya wingi huu wa maji
yatiririkayo katika mito na bahari, basi elewa kwamba maji haya haya ni
makazi ya uhai kwa jamii nyingi ya wanyama waishio majini na samaki. Hii ni nyumba ya hazina ya lulu, rubi, mawe
njano na vitu aina mbalimbali ya vito vya thamani ambavyo hutolewa kutoka
katika mito na bahari. Sehemu zinazozunguuka hifadhi za maji hukutwa kukiwa na
harufu nzuri za "aloes". Miti
pamoja na harufu nzuri ya vitu vya rangi rangi na miti shamba (itengenezwayo
dawa).
Zaidi ya hayo, ni njia ya usafirishaji. Ni njia itumikayo kwa kubadilishana biashara
kati ya nchi za mbali kutoka kila nchi nyingine k.m. kutoka nchi ya Irak kwenda
nchi ya Uchina na kinyume chake (toka Uchina kwenda Irak) na Irak yenyewe. Biashara ingeharibika kwa kutokuwepo kwa njia
hizi, mbali na hayo uchukuzi juu ya migongo ya wanyama na ya wanadamu na bidhaa
za biashara vingebakia kwenye nchi zalishaji na pia kubakia katika mikono ya
walaji wenyeji. Usafirishaji wao
ungegharimu zaidi kuliko gharama zao za uzalishaji. Hakuna mtu ambaye angethubutu kudiriki
kuyasafirisha.
Hii ingepelekea kwenye upungufu wa aina mbili. Vitu vingi vya (matumizi ya) lazima
visingepatikana. Wazia kwamba
yichanganyiko vya matumizi ya dawa kuhitaji "henna" au
"aloes" au matunda kama zambarau au baadhi ya dawa ya tiba au dawa ya
lishe kutoka miji ya Asia au Ulaya, kama vingekuwa visafirishwe juu ya migongo
tu bila njia ya mashua kupitia kwa kujitia kati ya bahari, vipi zingefika Uhindini (India) na vipi Wahindi wangefaidika
nazo. Na kwa upande wa pili watu ambao
sasa wanaendesha maisha yao kwa faida zipatikanazo kutokana na safari zao (za
kibiiashara), wangepoteza tegemeo lao la kiuchumi.
Faida nyinginezo ni katika kupikia, kupashia mwili
joto, juzikia vitu vya umajimaji na kuyeyushia vitu vigumu n.k. ni nyingi mno kiasi kwamba
haziwezi kuhesabika. Ziko wazi kiasi
kwamba haziwezi kuelezeka.
Fikiria anga wakati ni nyeupe na wakati mvua
inyeshapo. Hupishana kwa faida ya
ulimwengu. Endeleo la hali moja yoyote
kungesababisha machafuko (na matatizo).
Huoni kwamba inapoanza kunyesha mfululizo, mboga mboga na mimea huanza
kuoza. Miili ya hayawani hupata
misukosuko. Anga - hewa huzidiwa na baridi na kufuatia maradhi, barabara na
njia huharibika. Wakati anga inapokuwa
nyeupe kwa muda mrefu, ardhi hukaushwa,
mimea hunyauka. Hapo mtu hupatwa na
madhara kwayo. Hewa hupata UKAVU na
kufuatia magonjwa.
Wakati (hali)
zikipishana hivi kiutaratibu, hali ya hewa huwa sawasawa. Kila moja kwa zamu yake hufidia upungufu wa
(hali) nyingine. Kila kitu huenda sawa.
Mkimzani angeuliza kwa nini haikuamriwa kwamba kusiwe
na athari za madhara. Jibu likakuwa
kwamba hii ni hivyo ili kwamba mtu mara kwa mara asumbuliwe ili kumuepusha na
kutenda maovu. Mtu mgonjwa, kwa mfano,
anapewa dawa chungu na isiyopendeza ili kumponya. Kadhalika wakati mtu mwenyewe hujichukulia
katika makuu na kiburi huhitaji kupewa kitu ambacho kitamsumbua ili kumkinga
kutokana na hasara na madhara yaletwayo makusudi na muhuweka juu ya ukarimu na
utengeneko mzuri. Kama mfalme
atawafanyia ukarimu watu wake, je, ukarimu wake huu hautavuta akili zao kwa
heshima yake na mshangao? Wakati ambapo
ukifikiria ni mfananisho gani walio nao yale mamilioni na mvua ambayo ni chanzo
cha upatikanaji wa chakula na hali ya kustawi kwa sehemu zote za ulimwengu kwa
unyweshaji wake wa mashamba ya nafaka.
Huoni, baraka kubwa iliyoje ya mvua hii ndogo kwa
wanadamu? Bado watu ni wenye kuzembea
kwayo. Mara nyingi wakati kiasi cha
haja ndogo ya mtu kikizuiliwa, huanza
kunung'unika na kufanya ufadhuli.
Hupendelea zaidi haja yake ndogo kuliko zile faida kubwa zenye matokeo
mazuri. Hii ni kwasababu ameshindwa
kuthamini kuikamilifu sifa za fadhila hii bora.
Fikiria ustadi uliomo ndani ya myua ilinyesha na kumwagikia chini kutoka
juu (na) kunywesha kila mahali na uwanda wa juu pia. Kama ingekuwa ije kutoka kwa pembeni,
ingeziwacha nyanda za juu zimenywesheka, (lakini) bila kuwepo eneo la
kilimo. Nchi zenye unywesheaji wa
mifereji (ambao siyo kwa njia za asili) ni pungufu kwa eneo.
Maji ya mvua huienea ardhi yote. Mara nyingi kilimo kinaweza kikaendeshwa katika
sehemu kubwa ya majangwa na maeneo ya milimani na kutokea kupatikana wingi wa
nafaka.
Watu wanaepushiwa taabu ya kuchukua maji kutoka
sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Mashambulizi mengi ya kikabila huibuka kutokana na umilikaji wa sehemu
zenye maji ukifanywa na Mfalme mmoja na kulinyima kundi dhaifu. Matukio kama hayo vile vile huzuiliwa.
Basi kwa kuwa iliamriwa, imepangwa hivyo ili kufanya
hazi kama marasha rasha juu ya ardhi kuifanya ilowane na kuinywesha. Kama ingekuja na wepesi wa haraka kama
mafuriko, isingenywea ndani. Katika hali
ya mfuriko (mafuriko) ingeng'oa nafaka zote zilizosimama. Kwa hiyo, basi imeamriwa kunyesha katika
manyunyu mepesi, ili kuziwezesha mbegu kuchipua, nchi iweze kunywesheka na
mimea iliyosimama ipate kustawishwa.
Kuna baraka nyingine katika unyweshaji huu. Hutuliza miili, huisafisha anga, kuiondolea
uvundo uliosababishwa na usimamaji wa
maji. Mimea ya bustani huponywa ugonjwa
na njano na kadhalika.
Kama mkinzani atasema, iwapo mvua nyakati nyingine
husababisha hasara kubwa kwa uwingi wake au katika hali ya mvua za mawe,
husababisha nafaka kuteketea na anga kupata unyevunyevu mwingi usiofaa kwa afya
na hatimae kutokea magonjwa na matatizo.
Jibu litakuwa kwamba hasara hii pia wakati mwingine
inakusudiwa kwa kumboresha mtu (na) kumkinga (au kumzuilia) kutokana na
kujitumbukiza katika kuvuka mipaka ya Allah (s.w.t.).
Faida ambayo atakuja ipata katika uboreshaji wa imani
yake itapita hasara aliyoipata katika mali zake za kilimwengu (alizomiliki).
Tizama kwenye milima hii iliyofanyizwa kwa udongo na
mawe, ambayo mtu asiyojua hufikiri kama isiyo na maana na isiyo na umuhimu
wowote. Hufanya umbo lenye manufaa yenye
kuonekana. Miongoni mwao ni theluji
ambayo huanguka na kubakia juu ya vilele vyao.
Yeyote yule anaweza kunufaika nayo, wakati ikiyeyuka hufanya chanzo cha
chemchem za kububujika maji na vijito vya ajabu. Hutoa mitishamba (ya dawa) na mimea ambayo
haiwezi kukua sehemu tambarare na katika nyanda za chini. Ina matundu na mapango kwa ajili ya hayawani
wanyama wakali wawindao. Hutumika kwa
jinsi zilivyo ngome za muundo wa hali ya juu kiujenzi kama vituo vya
ulinzi. Huweza kuchangwa na kufanywa
makazi. Inakatwa na kufanywa vijaa. Ina madini ya mawe ya thamani ya rangi rangi
namna mbalimbali.
Mbali na haya, ina sifa nyingine, ambazo Yeye Pekee
Ambaye ameiumba katika vipimo halisi, hujua kwa Elimu Yake ya asili ya umilele
wote.
Fikiria aina mbambali za madini ambazo huchimbwa
kwenye migodi kwa mfano, chkaa, chokaa malighafi (lime) itengenezwayo Saruji na
chokaa (mortar), jipsa (gypsum), sumu mrututu (sulphurate of carsenicum),
risasi (lead oxide), zebaki (mercury), shaba (copper), bati (tin), fedha
(silver), dhahabu (gold), kito cha kijani (beryl), kito cha kundu (ruby), kito
nyekundu (garmet) na aina mbambali za mawe
na kadhalika vikitokezea kupatikana lami (tar), mafuta mgando (vaseline),
mrututu (Sulphur), mafuta ya taa (kerosene) hutumiwa na watu.
Je, basi hili ni fumbo kwa kiumbe mwenye akili kwamba
hazina zote hizi zimewekwa kwa matumizi ya mtu ambazo anaweza kuzichimbua kama
na wakati akizihitaji?
Watu hata hivyo, ni wenye tamaa na wanataka vitu
vyenye thamani ndogo kuwa dhahabu na fedha.
Wanafanya juhudi kubwa katika upande huo lakini zaidi sana bila
mafanikio. Mipango yao haitoi
faida. Kama watu hawa wangefanikiwa
katika kutafuta kwao elimu, ingekuwa elimu ya kawaida. Dhahabu na fedha zingechimbuliwa kwa wingi
mno kwamba zingepoteza thamani yao mbele ya macho ya watu. Manufao yaliyopatikana kutokana na shughuli
za madini na biashara yangepotea na si wafalme wala mtu yeyote yule angeweka
bohari za mali hizo.
Walakini, watu walipewa elimu ya (kuwawezesha)
kuibadilisha shaba kuwa shaba bandia na kuwa kioo, bati kuwa fedha na fedha
kuwa dhahabu, ambayo haifanyi madhara sana.
Hebu tizama uone kwamba elimu ilitolewa mahali ambapo ikitumika haileti
madhara sana, ambapo kwamba ile ambayo ni ya kudhuru imezuiwa.
Na wakati mtu akiingia kwenye mgodi anaweza akakuta
ndani yake vijito visivyotambulika vya maji yatiririkayo na mawe yenye rangi ya
kifedha.
Fikiria Usanii uliomo katika hili
Kuielezea kwa mfano, fikiria mtu amegundua kitu
kipya, kwa mfano, vyombo au vitu vingine vya matumizi. Ni vyenye ubora, vikubwa na vyenye thamani
maadamu tu vipatikane kwa uchache na adimu.
Na wakati vitu hivyo vitazidi hitajio na kufidia kila mfuko (kila mtu)
hupunguka katika thamani na huwa visivyo na maana. Kila kitu hufikiriwa kuwa kizuri pale tu
kinapokuwa adimu.
Fikiria mimea na mahitaji mbalimbali
inayotimiza. Tunda hutumika katika
lishe, majani makavu kama chakula kwa wanyama, kuti kama nishati, mbao hutumika
kwa (kazi ya) useremala wa kila aina.
Kuna faida mbalimbali zipatikanazo kutokana na maganda yao, majani,
mizizi mikubwa na midogo na gundi.
Fikiria matunda tunayotumia kwa lishe yetu. Kama yangekuwa yanapatikana sehemu moja
badala ya kuwa yamening'inizwa kwenye matawi ambayo huyazaa, mchafuko ulioje wa
mpango ungesababishwa katika maisha yetu!
Lishe ingepatikana bila shaka yoyote, lakini vipi
kuhusu manufaa yenye thamani tuyapatayo kutoka mbao za miti, majani makavu na
sehemu nyingine tulizozitaja.
Zaidi ya hayo, furaha ambayo huletwa na uzuri wa
kimandhari na hewa safi ya mimea kiulinganifu ni bora zaidi kwa anasa na furaha za ulimwengu wote.
Hebu fikiria jinsi kilimo kilivyoamriwa kustawi. Mia au zaidi ya nafaka zinatoka kwenye mbegu
moja. Nafaka moja kutoka kwenye mbegu
moja kungekuwa na mantiki. Kwa nini basi
kuongezeka huku? Hakika ni kuizidisha
nafaka ili kwamba hiyo hiyo isaidie kwa chakula kufikia vuno lingine mbali na
uwekaji wa nyingine kama mbegu kwa wakulima.
Fikiria Mfalme akusudiaye kuujaza mji na watu. Hupanga kutoa kiasi kikubwa cha nafaka
ambacho kitatoshelezea wakazi kuwasaidia kwa chakula mpaka mavuno yajayo mbali
na kuweka nyingine kwa ajili ya mbegu.
Angalia jinsi mpango huu unavyosimamiwa katika taratibu za Mwenye Nguvu
zote Allah Utukufu uwe kwake, kwamba kilimo kingepelekea kwenye ongezeko kubwa
sana kama hili ili kuhudumia vyote viwili, hitajio la lishe na vile vile kwa
lile la mbegu.
Ni sawasawa hali hiyo katika miti, mimea na
mtende. Huzaa matunda mengi mno. Unaona kwamba kuna mzizi mmoja, lakini kuna
machipukizi mengi. Kwa nini?
Hakika kwa ajili ya dhumuni la kuzalisha zaidi kizazi
kutokana na mbegu, baada ya watu kuziweka kwa matumizi yao. Kama kungekuwa na mzizi mmoja bila ya matawi
kuchipua kwa wingi hivyo, isingeyamkinika kuchukua chochote kutoka kwenye mimea
kwa kupanda au kwa shughuli yoyote nyingine.
Katika hali ya kutokea maafa ya ghafla mimea ya asili ingetoweka bila ya
kuwepo uwezekano wa mmea mwingine
kuchukua nafasi yake.
Fikiria nafaka za kunde, choroko, dengu na
maharage. Zote hukua kwenye maganda kama
hifadhi ya madhara, mpaka zinapokomaa kwenye ugumu, kama vile kondo la
nyuma. Nafaka za ngano na nafaka
nyingine kama hizo zimepangwa tabaka kwa tabaka katika maganda magumu, zikiwa
na ncha kali kwenye miishilizo yao kama mikuki kuwazuia ndege na kuongeza mazao
kwa wakulima.
Kama mkinzani akiuliza iwapo ndege hawapati kitu
katika nafaka za ngano n.k. jibu kwake litakuwa kwamba hapana shaka wanazipata
nafaka na imeamriwa hivyo kwao, kwa kuwa ndege nao vilevile ni katika viumbe
vya Mwenye Nguvu zote Allah. Yeye
(s.w.t.) Amewaamria sehemu ya mazao ya ardhi.
Nafaka hizi zimehifadhiwa katika mifuniko wasije wakapata kumiliki
nafaka yote kupelekea kwenye hasara ya dhahiri kwa upotezaji ulio tukutu.
Katika kukosekana kwa hifadhi kama hii ndege
wangeruka juu ya nafaka na kufanya kazi nyepesi (na ndogo) ya wao wote. Wangeumia kutokana na uyeyushaji dhaifu wa
chakula katika tokea jingine, kwa dhahiri ya madhara yao, Wakulima vile vile,
wangekuwa wenye hasara. Mifuniko hii ya
hifadhi kwa hiyo, imetokea kupewa ili kwamba ndege wapate kiasi chao cha
kuwatosha tuu kwa chakula, wakiacha sehemu kubwa kwa matumizi ya wanadamu. Wanayo haki kubwa zaidi kwayo kwa sababu ya
kazi iliyofanywa na wao, na hitaji lao la nafaka ni kubwa kuliko lile la ndege.
FIkiria uzao wa mimea na jamii mbalimbali za
miti. Huhitaji lishe sawa kama
wanyama. Hata hivyo haina vinywa vya
kujilishia, wala haiwezi kwenda huku na huko kutafuta chakula chao. Kwa hiyo,
imetnikiwa mizizi chini ya ardhi, kupokea lishe yao kwa upelekaji kwenye matawi
yao, majani na matunda.
Ardhi huihudumia kama mama ambamo kutoka humo
inanyonya lishe yao kupitia mizizi yao ambayo huitumikia (kikazi) kama vinywa
kuipatia chakula chao. Kama vile watoto wadogo
wa wanyama hujilisha kwa maziwa kutoka matiti ya mama zao. Je, huoni hizi mambo
zilivyohimilishwa wima bila hofu au kuanguka au kuinamisha mahema na kutiwa
ngvu kwa njia ya kamba zilizfungwa imara?
Kadhalika, utauona kila mmea umesimikwa katika ardhi
kwa mizizi iliyosambaa kila upande kuupa nguvu. Vipi miti mikubwa ya mitende
yote ingesimama imara dhidi ya dhoruba?
Angalia! Ustadi wa uumbaji ulivyo tangulia mbele
umahiri wa utendaji kazi. Umahiri
uliotumika katika kusimamisha mahema na kutiwa nguvu na mafundi, ulitumika
nyuma kabla katika usanifishaji wa mpango wa usimikaji miti ambao hutangulia
uhitaji wa mahema kwa mambo na nguzo vyote vikiwa vimepatikana kutokana na
miti.
Ni wazi kwamba umahiri huu umeigizwa kutoka ustadi
uliotumika katika kusimika miti.
Fikiria utokaji wa majani ya mimea kwa uangalifu na
utaona yametanda katika misokoto yake kitu kifananacho na mfumo wa mizizi
itambaayo sehemu zake zote za marefu na mapana.
Baadhi yao ina kapilari nyororo iliyounganishwa na iliyo minene, yote
ina nguvu sana na mizuri. Kama
ingetayarishwa kwa mkono mtu asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya kazi juu ya
mti mmoja katika muda wa mwaka.
Angelihitaji ala (zana), nia, kielelezo na mafunzo katika kuifanya.
Katika siku chache za majira ya msimu wa demani
majani mengi mno hujitokeza kiasi kwamba milima na maeneo ya mabonde ya ardhi
hujazwa nayo bila ya neno kusemwa au kufanywa shughuli yoyote kama vile tu
katika matokeo ya wangwa kuenea vitu vyote - ruhusa ya mgawo mmoja usiodhuru.
Elewa, tena, jambo la asili linalohusikana na
kapilari nyororo. Zimefumwa katika
misokoto ya majani ili kuinyweshea kama vile kimia cha kapilari katika mwili
kichukuavyo lishe kupeleka sehemu zote.
Kuna ustadi mwingine katika vena (chelewa) nene za majani. Kwa sababu ya uwezo wao wa kujirudi haraka na
nguvu, hushikilia kwa nguvu msokoto wa jani kuyakinga kutokana na
kuchanika. Majani haya ni sawa na majani
bandia yanayo tengenezwa kutokana na nguo na ambayo yametengenezwa kwa marefu
na mapana na kushikishwa kwa nguvu dhidi ya uchakavu. Kwa hiyo majani bandia yafanywayo kwa mkono
hufuata yale ya asili, ingawa kamwe hayawezi kuweka uhai wa kweli.
Fikiria kokwa ya mbegu iliyochimbiwa ndani ya tunda,
ambayo itawezesha kuzalisha nyingine iwapo mti utapotea kwa ajili ya baadhi ya
majangwa. Ni zao zuri tu la matumizi ya
kudumu, linahifadhiwa katika sehemu witri liweze kupatikana katika sehemu
nyingine kama hii ikipata ajali katika sehemu moja. Kisha kwa sababu ya kurudi upesi kwenye hali
zao za kawaida (baada ya kunyofolewa) na ugumu huzuia tunda kuwa laini sana na
utovu mwingi. Bali bila kokwa hizi
matunda yangepasuka na kuwezesha udhaifu.
Baadhi ya kokwa zinalika na mafuta hukamuliwa kutoka
nyinginezo kwa matumizi katika kazi tofauti.
Na kwa kuwa umejifunza dhumuni lifanywalo na kokowa, yakupasa ufikirie
nyama ya tunda iliyofungika ndani ya mbegu ya tende na ile inayozunguuka kokwa
ya zabibu, ubora kwayo na sababu gani ya umbo lake, ambapo kwamba ilikuwa
inawezekana kutoa/kuzalisha badala ambayo isingekuwa ya kulika kama vile miti
ya "cypress" na miti (mingine) maarufu. Hakika ni hivyo kwamba mtu akute lishe tamu,
afurahi.
Fikiria sifa, nyingine za mimea. Utaona kwamba inaathiriwa na majira ya msimu
wa masika, hivyo kwamba joto lao muhimu huhifadhiwa katika vitawi vyao, na
malighafi kwa uzalishaji wa tunda hutengenezwa.
Majira ya msimu wa demani huivalisha majani na kupata aina zote za
matunda, kama vile unavyopanga aina mbalimbali za vyakula vitamu mbele yako
ambavyo vimepikwa kwa zamu.
Hebu ona vitawi vitoavyo matunda yao kwako kwa mikono
yao.
Na unayatazama kwa furaha maua ambayo yanakuja mbele
yako juu ya vikonyo vyao kama kwamba vinajiwakilisha vyeme kwako?
Nani amepanga hivi?
Hakika ni Yeye Ambaye ni Mwenye kujua yote Mwenye Kuamuru. Na ni dhumuni
gani linakusudiwa kwayo?
Hakika, ni kwamba mtu afurahie matunda na maua. Ajabu ilioje, kwamba badala ya shukurani kwa
baraka hizi, watu humkana Mtoaji moja kwa moja.
Hebu fikiria Komamanga na umahiri na ustadi ambao
umetumika katika uzalishaji wake.
Utaona, ndani yake lote ni duara na madoido ya nafaka zilizowekwa tabaka
juu ya tabaka, kama vile zimepangwa kwa mkono.
Nafaka hizi zimegawanywa kwenye
sehemu tofauti na kila sehemu imefunikwa katika kitani, zimefanyizwa katika
hali iliiyo bora sana ya kipekee. Zote
hizi zimezunguukwa na ganda la nje.
Ustadi wa Kisanii uliomo humo ni kwamba kwa kuwa
nafaka haziwezi kusaidiana kila moja katika ukuaji wa nyama ya tunda, utando
umewekwa ndani ya Komamanga ya kulisha katika huo, unaona zote nafaka na nyama
ya tunda zimetiwa ndani sana na kukazwa imara. Tando hizi husaidia kuziweka
mahali pamoja zisizosogezeka. Juu ya
yote haya, mfunika wenye nguvu umewekwa kuziweka salama kutokana na madhara ya
nje.
Hizi ni nukta chache kuhusu Komamanga, ambalo yoyote
ambaye hupenda maelezo zaidi (kwa urefu) anaweza kuongeza mengi zaidi. Maelezo yaliyotolewa hapa ni, hata hivyo,
yenye kutosha kwa dhumuni la hoja na funzo.
Hebu ona mtambaazi huu mnyonge (dhaifu). Mitambaazi hii hutoa nje (huzaa) mamung'unya
makubwa mno, matango na mitikiti -maji.
Ustadi ulioje umeendelea katika Usanii wake! Kwa kuwa imeamriwa kwamba
itazaa matunda makubwa mno, mmea huu umesanifiwa utambae juu ya ardhi. Ingekuwa kama mimea mingine isimamayo wima,
usingeweza kuhimili mavumo yakushangaza ungevunjika na kuanguka chini kabla (ya
mazao yake) hayajawa. Angalia jinsi
unavyojitandaza (na kuenea) juu ya udongo kuweka uzito wa mazao yake juu ya
ardhi. Pengine ungeweza kuona kwamba
mizizi ya mitambazi mmung'unya na tikiti-maji husambaa katika ardhi na mazao
yake (matunda) yakilala juu ya ardhi pande zote, kama vile paka alalae chini
akinyonyesha watoto wake (maziwa) - matunda.
Fikiria ukweli kwamba mitambaazi hii hukua tu katika
majira maalum ya misimu iliyowekwa kuifaa (mimea hii) katika joto kali
Hutokea wakati mwingine kwamba matango yanazaliwa
katika kipupwe. Watu kwa ujumla
huyaepuka, isipokuwa walafi pamoja na
hisia ya madhara na magonjwa.
Fikiria mitende.
Kuna miti ya Kike miongoni mwao.
Kwa uzazi wao miti ya kiume huzaliwa pia, ambayo huzalisha bila ya
kupangwa kilimo cha bustani. (Miti)
dume, kama yale (madume) ya wanyama, huzalisha, lakini yenyewe ni gumba.
Fikiria kiuangalifu shina la mtende. Utaona kwamba limefumwa kama utando, ingawa
hakuna nyuzi ndefu. Liko kama vile
kipande cha nguo kimefumwa na mkono kulifanya kuwa na nguvu na kunyooka kuweza
kustahamili pepo zenye nguvu na ubebaji wa vichala vikubwa vya matunda, katika
kukomaa, na kisha mwishowe kutumika kwa kupauliwa na madaraja. Utaona ndani yake nyuzi zimesokotwa kwa
marefu na mapana. Liko imara vya kutosha kutumika katika utengenezaji wa ala
(zana).
Kama lingekuwa gumu kama jiwe, lisingetumika katika
majengo kama mbao, kwa mfano, milango kazi ya kimia, mbao za miti na makasha
n.k.
MBAO
Kuna sifa moja kubwa katika mbao. Inaelea juu ya maji. Kila mtu anaijua hii lakini hatambui thamani
yake kwa ukamilifu.
Kutokuwepo kwa tabia hii, vipi mashua
zingetengenezwa, ambazo hubeba milima ya bidhaa za biashara kutoka mji kwenda
mji kwa juhudi kubwa? Shida zilioje
ambazo zingekuwa zistahimiliwe katika kusafirisha bidhaa za biashara?
Vitu vingi vya matumizi vingetoweka sokoni au
vingepatikana kwa bei ya aghali sana.
Fikiria hii miti shamba na tabia ambazo kila mmoja
amejaaliwa nazo kama madawa. Hupenyeza
chini kwenye viungio, huteketeza takataka na jauhari za sumu kutoka humo, kwa
mfano, ugonjwa uitwao, Shahtra, baadhi ya mitie mingine hutuliza ulegevu wa
moyo, kwa mfano mti wenye dawa iitwayo "ateemoon", baadhi ya mingine
huondoa riahi, kwa mfano siki, baadhi ya mingine hutuliza uvimbe, kwa mfano
zabibu pori na kadhalika kwa ufanisi wao.
Nani basi ameijaalia kuwa na sifa kama hizi? Hakika Yeye Ambaye ameiumba na dhumuni. Nani
amewapa watu elimu kwayo? Hakika Yeye
ambaye ameyajaalia madawa haya na hali kama hizi. Vipi mambo haya yangefika kwenye fahamu za
mwanadamu kwa bahati na yenyewe tu kama wale waaminio mambo ya bahati nasibu
wanavyodai?
Haya, hebu natukubali kwama mtu amejifunza yote haya
kutokana na akili yake na hoja, taamuli na majaribio ya kimaabara. Lakini ni nani amewafundisha wanyama?
Baadhi ya hayawani, wanapojeruhiwa (na kuumia),
hutumia miti shamba kujiponyeshea, na baadhi ya ndege wakiumwa kutokana na
kufunga choo hupata afueni kwa kuharisha kwa kutumia maji ya bahari na
kadhalika?
Unaweza, pengine, kutia shaka manufao/faida ya uhai
wa mimea au faida za nchi zilizoachwa (vihameni) na za tambarare ambako hakuna uhai wa binadamu upatikanao na
kuufikiria kuwa wote ni bure na hauna maana.
Sivyo hivyo vilivyo. Wanyama pori
hujilisha kwayo na nafaka yao inatumiwa na ndege kwa chakula. Vitawi vyao na kuni hutumiwa na watu kama
nishati.
Kuna nukta nyingine vile vile zenye faida
kuzijua. Ina tumika kwa madawa ya kutibu
(kuponya). Ngozi hudubaiwa kwayo. Nguo hutiwa rangi na kadhalika. Inazo sifa nyinginezo pia.
Je, hujui kwamba mti wa chini kabisa kwa daraja na
uliodharauliwa ni (ule uitwao) "Khairya Baradi?" Pia hiyo ina sifa mbalimbali. Karatasi hutengenezwa kwayo kwa matumizi ya
Wafalme na watu wa kawaida. Hutengenezwa
kuwa mikeka/busati kwa matumizi ya wote na vyote. Hutumika katika kutengeneza vifniko vya
kufunikia vyombo vya nyumbani vilivyotengenezwa kwa kioo n.k. ambavyo hujazwa
nayo kuzuia kuvunjika. Ina sifa nyingi nyinginezo
kwa nyongeza ya hizi.
Kisha jifunze somo kutoka namna nyingi na faida
ambazo hupatikana kutokana na viumbe vidogo na vikubwa kama vile pia kutoka
vitu vile ambavyo havina thamani na vile ambavyo vina thamani. Isiyo na thamani zaidi ya yote haya ni
kinyesi cha ng'ombe na uchafu utokao mwilini ambao ni taka zisizo na thamani,
na fikiria faida ambazo hupatikana kutokana nazo kwa kilimo na mboga. Zina faida hivi kiasi kwamba hazina
kifani. Hakuna mboga mboga inayeweza
kuwa na thamani isipokuwa iwe imewekewa mboji ambayo ni ya kuchukiza kiasi
kwamba mtu haikaribii kwa kuona kinyaa.
Elewa hili nalo, kwamba thamani ya bidhaa haitegemei
juu ya thamani ya pesa peke yake. Ina
thamani mbili tofauti katika masoko mawili tofauti. Hutokea wakati mwingine kwamba bidhaa haina
thamani katika soko la uchumi na bado bidhaa hiyo hiyo ina thamani katika soko
la elimu.
Inaweza kuwa kwamba unaweza kufikiria kitu kwamba
hakina faida kwa sababu ya thamani yake yu chini kifedha. Hebu angalia ni thamani kubwa kiasi gani
ingekuwa kwa uchafu wa wanadamu (kinyesi na mkojo) kama hali/sifa zake zingefahamika
kwa mkemia. Ni ukweli kwamba majaribio
mahsusi ya kemia hayawezi kufanywa bila uchafu wa wanadamu."
Ilikuwa sasa ni wakati wa Sala za adhuhuri, na Imam
(a.s.) aliniambia kuja siku ifuatayo (yaani kesho), Insha - Allah!
Nilirudi mwenye furaha kwa sababu ya maelezo
niliyopata kutoka kwa Imam (a.s.).
Nilimshukuru Allah (s.w.t.) kwa maelezo yenye thamani
niliyopokea.
Nilipitisha usiku kwa amani halisi.
Baraza La
Baada ya Sala za kawaida na kumshukuru Mwenye Nguvu
zote Allah, Imam (a.s.) alisema, "Ewe Mufazzal! Nimekupa maelezo kwa
kinaga hoja kwa kufafanua zaidi na uchunguzi kuhusu mpango halisi na Usanii
kuhusiana na wanadamu, wanyama na ufalme wa mimea. Inapasa itoshe kwa njia ya mafunzo kwa wote
ambao wanatamani mwongozo.
Sasa nakupa maelezo kamili ya majanga na machafuko
ambayo hutokea kwa nyakati na ambayo hawa watu wajinga husimamia kama hoja kwa
ukano wao wa uumbaji na Usanii wenye dhumuni wa Muumba.
Nitaelezea vilevile kwa undani zaidi hekima iliyomo
kwa kuletwa matatizo na machungu ambao walahidi na wafuasi wa dhehebu
Watu hao
wamesema ulimwengu huu umejitokeza na kuwepo kwa bahati tupu, hivyo basi
maelezo haya yatakuwa ni yenye kutupilia mbali hoja zao. Allah (s.w.t.) awaangamize - kulioje
kupotezwa kwao. Baadhi ya watu wajinga
wanatafsiri matukio haya ambayo hutokea wakati kwa wakati, kwa mfano milipuko
ya maradhi ya kuambukiza, kutokuwepo kwa "Chlorophyll" (Klorofil) ya
miti, mvua za mawe, nzige, kama hoja ya ukano wa dhumuni la uumbaji wa Muumba.
Jibu kwa hili ni kwamba kama hakuna Msanii wa
ulimwengu huu, kwa nini hakuna machafuko makali zaidi, kama kwa mfano mvurugiko
kamili wa ulimwengu wote, kupasuka kwa ardhi, ukomo wa kuchomoza jua, ukaukaji
wa maji katika makalio ya mito ivyo kutoacha hata tone la maji kuweza kulowesha
midomo, hewa kusimama tuli na kupelekea kwenye mvurungiko wa mpangilio wa
mambo, kusambaa kwa maji ya bahari kwenye ardhi na kuizamisha. Nani analinda matukio yote haya? Ni nani
mpangaji wa mandhari hizi?
Wakati usemapo kwamba kama kungekuwa na Msanii na
Muumba, Kundi kama hili la nzige lisingetufikia kusababisha madhara makubwa
hivi, milipuko ya magonjwa haya ya kuambukiza yasingechukua kiwango kikubwa cha
mamilioni ya maisha ya watu, mvua za mawe zisingekuwa kubwa na uzito hivyo hata
mpaka kuharibu mashamba yetu ya nafaka.
Ikiwa yote haya ni katika hakika ya mambo, kwa nini ulimwengu huu
usipate kuvurugika katika taratibu za uumbaji na kupelekea kwenye uangamizi wa
ulimwengu wote? Kwa nini bahari
isizamishe ardhi kwa maji yabubujikayo?
Kwa nini hewa isisimame na kutulia tulii na hivyo kusongeka kwa viumbe
hai vyote? Kwa nini yote haya yasitokee?
Hii huonyesha kwamba Msanii yupo, ambaye huzuia tukio
kama hilo ili kwamba ulimwengu usije chafuka na kuharibika wala jamii kuja
kutoweka wala uharibifu kabisa wa jumla usitokee. Kinachotokea ni kwa njia ya kawaida ya
matokeo kutokana na matendo ya mtu mwenyewe, ni onyo la kujizuia na maovu
yafanyikayo mara kwa mara katika hali ya milipuko ya magonjwa ya kuambukiza,
nzige, kuangamia kwa nafaka na mashamba, mvua za mawe n.k. Huu ni ukano wa hoja dhidi ya uumbaji wa
kidhumuni. Nawauliza kwa nini hii
milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na makundi ya nzige hayaendelei moja kwa
moja hivyo ili kuungamiza ulimwengu?
Hufika mara chache, na baada ya muda, huondoka.
Je, huoni kwamba huu ulimwengu umehifadhiwa dhidi ya
misiba hii ya kutisha na machafuko? Kama
mojawapo lolote katika matukio haya lingetokea katika ulimwengu huu,
ungeharibika kabisa moja kwa moja.
Majanga haya hutukia mara chache, katika hali ya ukali uliopunguzwa ili
tu kuwaonya watu na kuzirekebisha tabia zao kuwa nzuri.
Hayadumishwi bali huondolewa kama na wakati mtu
apatapo fadhaa kuhusiana na usalama wao.
Majanga haya hutukia kama onyo na kuondolewa kwa Rehema za Ki-Ungu.
Kama vile waumini wa dhehebu
Ingekuwa hivyo, kiburi cha mtu na uchoyo
vingempelekea kwenye tabia ambayo isingekuwa katika ulinganifu na dini au
maisha yake ya dini. Kama vile unavyoona
watu wamelelewa katika anasa na wasaa (faraja) na ambao wengi wao kabisa
wanasahau utu wao na hali yao ya kuwa wamelelewa na kukuzwa na mtu fulani. Wanasahau kwamba wanaweza kupata maumivu
fulani au huzuni au kwamba misiba fulani inaweza kuwapata. Hata husahau iwapo kuna kuwahurumia watu
wanyonge au kuwasikitikia watu wenye kuhitaji.
Hawako tayari kuongozwa kuhisi kusikitika kwa matatizo ya watu wengine
au kuhisi kuhurumia juu ya wanyonge au kuonyesha upendo kwa nafsi zenye
matatizo.
Wakati, hata hivyo, matatizo yanapowapata, huhisi
uchungu wake na hapo akili hufunguka wanazindukana kwa kiwango kikubwa zaidi
kuliko katika ukadiri ya ujinga wao na upumbavu. Wanaanza kutenda katika njia ambayo iliwapasa
juu yao wakati wote. Kama matatizo haya
yasingewapata, wangeendelea kujiona kama waungu (na) kuendesha maisha yao katika
hali ya kiburi, kutokuwa na masikitiko au huruma na mtu yoyote yule. Je, tabia kama hii ingekuwa ni yenye faida
kwa dini yao na ulimwengu huu? Hakika
sivyo! Pamoja na dini potofu wangepata
madhara ya kilimwengu. Watu
wangewachukia na kuwalaani. Watu wachoyo
kama hawa wangesababisha mchafuko katika ulimwengu huu katika mambo yote, kazi
biashara, elimu na tabia ya wao kwa wao n.k.
Watu wanaokana mambo haya, wakiyaona kama yasiyo na
maana, ni kama wale watoto wadogo ambao wanalaumu dawa vhungu na isiyo pendeza
na kuchukizwa na tahadhari dhidi ya vyakula vyenye madhara. Hawataki kazi, na hupenda kucheza tu huria
(bila kuzuiwa) hupenda kujiingiza katika mambo ya kipumbavu, kula na kunywa
bila pingamizi au kizuizi. Hawajui
kwamba ruhusa kama hii na uvivu kutadumaza ukuaji wa akili zao, uadilifu wao na
miili yao, kwamba vyakula hivi vya kumezeka lakini vyenye madhara vinaweza
kupelekea kwenye mateso tofauti tofauti na magonjwa. Uboreshaji wao umo katika upatikanaji wa
elimu, na dawa zina faida nyingi kwao mbali na huko kutokumezeka kidogo.
Wanasema ni kwa nini watu hawakupewa tabia ya
kutokufanya dhambi ili kwamba Mwenye Nguvu zote Allah hangehitajika na kuwatia
adabu kwa uchungu wa matatizo. Jibu kwao
litakuwa kwamba katika hali hii mtu hangekuwa na thamani ya itibari (sifa)
yoyote kwa uzuri wala kupasika na malipo kwayo.
Kama wataendelea kusema zaidi kwamba kuruhusiwa kila
aina ya anasa na wasaa (faraja) lingekuwepo wapi dhara lolote humo kama
hangepata itibara au malipo kwa wema wa uzuri wake? Jibu litakuwa ni kulifikisha swali hili kwa
mtu mwenye akili timamu na mwenye siha nzuri na kumwambia akae tu bila kufanya
kazi, na kumhakikishia ukamilifu wa mahitaji yake yote bila juhudi zozote. Kisha tazama kama akili yake itakubaliana na
hilo. Utamwona kuridhika zaidi na
kutosheka kwa kidogo apatacho kwa juhudi yake kuliko kupata kikubwa na kingi
ambacho huja kwake bila stahiki, pasipo kukifanyia juhudi. Kadhalika baraka za Akhera (ulimwengu ujao)
zitakuwa zenye tabia ya namna ile ile kwao ikiwa tu kama zimepatikana kwa
juhudi.
Kwa hiyo mtu anaruhusiwa boma mbili za baraka. Kwanza kabisa kupata ujira mkubwa kwa juhudi
zake katika ulimwengu huu wa sasa (dunia).
Pili, ameonyeshwa njia za kuitafuta kwa juhudi zake ili kwamba apate
ridhio la kiwango cha juu sana kwa fanikio hilo. Ni kawaida kabisa kwa mtu kutokuruhusu kukipa
thamani kitu chochote kilichopatikana bila juhudi au haki. Kinyume chake, chochote apatacho kwa matokeo
ya juhudi na haki, hukiwekea bohari kubwa.
Na kwa hali hiyo, baraka za Mwenye Nguvu zote Allah ambazo zitawekwa juu
yake kwa wema wa kujizuia kwake ndani ya mipaka iliyoamriwa zitakuwa bora zaidi
kithamani kwake kwa mlinganisho, na hali ya akili ambapo hakuwa ni mwenye
kuzuia tamaa zake mbaya na kila kitu kilicho haramu kimekoma kuwa na mvuto kwa
ajili yake. Katika haki hii, baraka za
Akhera zilizowekwa na Mwenye Nguvu zote Allah zisingekuwa na thamani hivyo
kwake. Malipo ambayo kwamba atapata kwa
matokeo ya juhudi ya nguvu zake na chumo yatakuwa ya thamani kubwa sana kwake.
Kama sasa wanasema iwapo haitokei hivyo kwamba baadhi
ya watu wamependezwa sana kupata baraka bila haki yoyote, kwa hiyo, hoja gani
italetwa juu ya kadhiaa hizi kwa watu ambao watahisi kupendezwa kwa kupata
baraka za akhera?
Jibu litakuwa kwamba hili ni somo kwamba watu
watashawishika kwalo, kwamba watapata baraka za Akhera bila juhudi itapelekea
kwenye namna zote za madhara yaliyoletwa
makusudi, hali ya kutenda dhambi, ushukaji wa uadilifu na uovu. Nani basi angejizuia kutokana na uovu wa
uadilifu au kufanya juhudi kuwa na tabia njema wakati kwamba ameshajijua
mwenyewe kama mpokeaji mstahiki wa baraka za Akhera? Nani angekuwa na hakika ya hatua ya maisha,
heshima na mali yake mwenyewe na ya ahali wake kuhsu madhara ambayo watu
wangefanya kama kungekuwa na hofu ya adhabu na kisasi? Uharibifu kwayo ungesababishwa katika maisha
haya ya sasa kwa watu kabla ya siku ya mwisho (ya ulimwengu huu).
Haki na ustadi vyote vingetupwa. Ingetiliwa shaka
kama ukosekana taratibu huku na mchafuko kungeingia kwenye usanii.
Vile vile huzungumzia matatizo na usumbufu ambao
wakati mwingine yana matumizi ya jumla yakiwaumiza na watu wema na kupelekea
watu waovu bila kudhurika. Wanasema, itawezekana vipi kuwa Usanii wenye kufaa
wa Mwenye kujua yote, hoja gani unaleta?
Jibu kwa hili itakuwa kwamba matatizo kama haya
huwapata wote wema na waovu/wabaya na kuna faida kwa makundi yote zilizoamriwa
na Mwenye Nguvu zote Allah. Wema
huteseka kwa matatizo na usumbufu mwingi na malipo ya baraka kwao husababisha
shukurani na Wokovu ndani yao.
Na kwa watu waovu matatizo yao huanza kutokea
kutokana na tabia ovu. Iko faida ya
uboreshaji kwa wale wote ambao wangeepushwa kutokana na kishindo cha matatizo
haya.
Mbali na makundi mawili haya, kwa watu wema hali ya
uzuri ni chanzo cha furaha na kishawishi zaidi na utambuzi wa uendeleaji wa
tabia njema zaidi. Kwa wafanya maovu pia
hifadhi dhidi ya madhara ni fadhila maalumu kutoka kwa Mwenye Nguvu zote Rehema
za Allah zinaonyeshwa kwao bila ya wao kujistahiki. Hii huwavuta wawe wapole na kuwasamehe wale
ambao hufanya ubaya kwao.
Mkinzani anaweza kusema kwamba matatizo kama haya
huangukia mali zao, bado wakati mwingine miili yao huteseka hata kuangamia,
kama vile kuunguzwa, kufa maji, kuchukuliwa na mafuriko au kuzikwa ungali hai.
Jawabu kwao litakuwa kwamba Mwenye Nguvu zote Allah
ameamuru ndani yake uzuri wa makundi yote.
Kwa watu wema kwa sababu ya kuutoka ulimwengu huu na matatizo yake na
mauchungu yake, na kwa watu waovu ni kwamba uwezo wao wa kufanya dhambi kwayo
huondolewa.
Kwa muhtasari, Mwenye Nguvu zote Allah hugeuza
matokeo ya matendo yote haya kwa kujua kwake yote na Mwenye Enzi Kuu na
kuelekeza wenye uboreshaji, kama vile mti unapoangushwa chini na upepo,
seremala mzuri huugeuza kwa matumizi yenye faida.
Kadhalika, Mwenye Nguvu zote Msanii hugeuza matokeo
ya maafa haya ambayo huzipata mali zao na miili yao kwa faida zao na
uboreshwaji wao. Kama mtu atauliza kama
ni kwa nini misiba hii iwapate watu, jibu litakuwa, wasije wakageukia kwenye
hali ya kutenda kwa sababu ya kipindi kirefu cha Usalama, wasije watenda maovu
wakajiingiza moja kwa moja katika hali ya kufanya madhambi ambapo watu wema
wakawa ni wenye kuzembea katika kufanya mema.
Aina zote hizi za tabia huwazidi nguvu watu wakati
wanapopewa muda mrefu wa starehe na faraja.
Matukio kama haya huwafanya kuonyeka na kuwaepusha kutokana na tabia
hizi - na ndani yao muna uzuri kwao.
Kama wangeondolewa matatizo moja kwa moja, wangevuka
mipaka ya kufanya dhambi kama vile walivyofanya watu wa nyakati zilizopita
hivyo kwamba ilibidi wateketezwa kwa dharika kuisafisha ardhi kutokana nao.
Kuna nukta moja imefungwa kwenye akili za wakanushaji
hawa wa Usanii na dhumuni, kuitaja ni, kifo na uharibifu. Wanafikiri kwamba ingekuwa sawasawa kama mtu
angepewa hai wa milele bila tatizo lolote au dhara.
Ni muhimu
kuchukua hoja hii na kuipeleka kwenye mwishilizio wa kihoja ili kuona kwamba
inapelekea kwenye maokeo gani. Hebu
tazama kwamba kama watu wote, wangeishi maisha ya umilele, ardhi hii ingekuwa
finyu sana kwao; wasingepata nafasi ya kutosha kwa makazi yao, kilimo chao na
mahitaji ya riziki kwa kuendeshea maisha yao.
Ijapokuwa shoka la kudumu la kifo linafanya kazi wakati wote, wakati
ambapo kuna migongano kuhusiana na makazi na mashamba ya nafaka, hata vita
hupiganwa na damu kumwagwa juu ya suala hili.
Ingekuwa vipi hali yao kama asingekufa hata mtu mmoja wakati uzazi wa
watu wapya unaendelea? Sasa hivi hata
ingawa vifo vinaendelea, tunayo matatizo haya.
Je, kungekuwa na hatari za namna gani kama daima
asingekufa hata mtu mmoja? Watu
wangezidiwa nguvu kwa choyo, tamaa mbaya na ugumu wa nyoyo. Kama wangehakikishiwa uhai wa umilele, hakuna
ambaye angetosheka na anavyomiliki.
Hakuna ambaye angekubali kutoa chochote kwa wenye kuhitajia (mafukara na
masikini), wala kusingekuwa na faraja baada ya msiba. Wangechoshwa na maisha na mambo yote ya
ulimwengu. Mtu mwenye maisha marefu
huchoshwa nayo, hutamani mno kutokewa na kifo na kupata afueni.
Wanasema kwamba ingepaswa iamriwe kwamba matatizo
yote na maradhi yangeondolewa kutoka miongoni mwao, hivyo kwamba
wasingependelea kukiomba kifo wala kuwa ni wenye kukitamani. Jibu kwa hili ni kwamba wangetumbukia kwenye
njia za uovu na utovu wa utii.
Kama wakisema kwamba kuondoa fadhaa na upungufu wa
nyumba na hali (mbaya) za maisha, uzazi wao ungesimamishwa, jibu litakuwa
kwamba katika hali hiyo idadi isiyoelezeka ya viumbe ingekoseshwa fursa ya
kuingia katika ulimwengu huu na hivyo kukoseshwa baraka za Mwenye Nguvu zote
Allah katika uhai wa ulimwengu huu na wa Akhera, ikiwa kizazi kimoja
kingeruhusiwa kuingia bila uwezo wa uzazi zaidi.
Na kisha wangesema kwamba Yeye (s.w.t.) angeliumba
watu wote,wale waliozaliwa na wale watakaozaliwa katika siku zijazo, katika
mkupuo mmoja.
Jibu kwao litakuwa, kama lilivyokwisha elezwa tayari,
kwamba matukio yatajitokeza kama vile upungufu wa nyumba na njia za
Kilimo. Wapi nafasi ya kutosha
ingepatikana kwa kjengea nyumba, kuendeshea kilimo, kuanzishwa kwa
mawasiliano. Katika hali hiyo kutokuwepo
kwa mahusiano ya kijinsia (kwa ngono), kusingekuwa na faida za kujamii (umma)
niongoni mwa jamaa na ndugu, hakuna msaada wa wao kwa wao katika nyakati za
shida na huzuni. Wapi ingepatikana
furaha ya mzazi katika kuwalea watoto?
Hii huonyesha kwamba upande woote mawazo yasogeavyo
mbali kutoka Usanii wa kidhumuni, huhakikisha kuwa siyo wa kuthibitika ni
upumbavu na upuuzi.
Mkinzani anaweza, pengine, kuleta pingamizi kutoka
nukta nyingine ya mtazamo na kusema kuwa vipi itaweza kujulikana kwamba kuna Muumba na Msanii, wakati tunaona katika
maisha mtu mwenye nguvu akijitwalia kila kitu, mwenye nguvu kumkandamiza
mnyonge, wakati ambapo mnyonge anaonewa na anatukanwa. Wema ni windo la taabu na matatizo wakati
mwovu mno ni mwenye afya na tajiri. Yule
ambaye haheshimu kanuni na kawaida haadhibiwi kwa haraka.
Kwa hayo inamaliziwa kwa kusema kwamba kama kungekuwa
na Usanii ueneao na kuujaza ulimwengu wote, shughuli zote zingeendeshwa
sawasawa. Watu wema wangelishwa vizuri
na wabaya na waovu wangepata hasara.
Wenye nguvu wangezuiwa kuwakandamiza wanyonge. Mwenye kutenda uovu angepata adhabu haraka.
Jibu kwa hili litakuwa kwamba katika hali hii wema,
ubora maalum wa mtu ungepoteza thamani yake.
Vilivyobaki katika Uumbaji havina ubora wa ushawishi katika ahadi za
malipo ya Mwenye Nguvu zote Allah na hivyo kutoa tamaa zao kwenye nidhamu ya
tabia ya uzuri. Wao, katika hali hiyo
wangekuwa kama wanyama wa miguu minne, ambao wako chini ya udhibiti kwa fito
(fimbo) na uhitajio wa tumbo. Kwa wao
daima ama huonyeshwa jambia, au hupewa ukoka kuwaweka katika mpango. Hakuna hata mmoja ambaye angetenda katika
upasiko pamoja na ushawishi wa kupata jaha ya Kiroho au Jahannamu. Wangedhalilishwa na kushushwa daraja kutoka
daraja ya ubinadamu kupewa ile ya unyama.
Hakuna ambaye angejali baraka za Kiroho.
Mtu angefanyia bidii shughuli za malipo ya mara moja ya wakati huo huo
(papo hapo). Mtu mwema angetenda kwa
kujipatia chakula tu na kwa mali za kilimwengu, wakati mtu mwovu angejizuia
kutokana na ukandamizaji na uonevu kwa sababu tu ya hofu ya adhabu ya ghafla ya
wakati kuo huo hivyo kwamba matendo yote ya watu yangevutwa katika hali ya papo
hapo ya wakati huo. Kusingekuwepo na
wazo hata la mbali sana kwa ajili ya malipo mema na adhabu zilizoamriwa na
Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) wala wasingepasika kwenye baraka za Kiroho za
Akhera. Yote haya, yangepelekea kwenye
hali mbaya.
Ijapokuwa, na yote haya, umasikini na ukwasi
uliotajwa na mkizani haviko moja kwa moja mbali na ilivyokusudiwa. Ni ukweli kwamba kama watu wanavyofahamu watu
wema pia hupata rasilimali za mali za ulimwengu huu, hivyo kwamba watu wasije
wakadhania kwamba ni wasioamini tu (Makafiri) ndiyo waliopendelewa nayo, hali
ya kwamba watu wema wamenyimwa starehe za maisha haya (ya dunia) wasije watu
kwa ujumla wakajichukulia tabia ya ujeuri.
Unaona vile vile kwamba wajeuri wanaadhibiwa katika ulimwengu huu,
wakati ujeuri wao unapovuka mipaka yote na watu wakadhurika mno kutokana na
jeuri zao hizo, kama vile Firauni alikufa maji, Nebukadreza aliumbuliwa na
Bilbis aliuwawa.
Kama katika maelezo ya baadhi ya Dhumuni
Hii hata hivyo, haipunguzi nguvu ya sera. Kwa ukweli Kadhia hizi, wakati
zinachelewesha, zinaonekana kuwa zenye ulinganifu zaidi na sera za utawala na
ni zenye kuona mbali. Na kama ushahidi
mzito wa kutosha wenye nguvu na mwishilizio kwayo yote haya yakalazimisha
kwenye imani ya kwamba lazima kuwepo Muumba na Msanii wa vitu vyote vya
ulimwengu huu, kitu gani kinaweza kumzuia Yeye (s.w.t.) kupanga uzuri kwa
viumbe vyake? Hakuna akili ya mwanadamu
iwezayo kudhania kwamba Muumba atauwacha Uumbaji wake hivi hivi tu (huria),
isipokuwa iwe kwamba kwa ukosefu wa nguvu na uwezo, kwa ujinga au umakusudi,
yote haya ambayo ni mageni kwa Usanii wa Allah Mwenye Nguvu zote. Allah (s.w.t.) Si Asiye na uwezo kwa
uboreshaji wa Uumbaji Wake, wala Si Asiye na habari na hali zao, wala Allah
(s.w.t.) aepushilie mbali, Yeye kimakusudi anapotoka.
Kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ya kukosa nguvu
na uwezo, ujinga na upunguani, kunaeleweka zaidi kama ilivyo kwamba asiye na
nguvu na uwezo hana uwezo wa kuumba viumbe watakatifu hawa wa ajabu, mjinga hana
utambuzi wa njia za maadili na ustadi wakati mkaidi hawezi kugeuka akawa kwenye
Uumbaji Mtukufu huu wa kazi hii muhimu na ya ufundi mkuu.
Na mambo kuwa kama yalivyo, hueleweka kwamba Muumba
wa ulimwengu atakuwa, kama jambo la kweli na sawa, aangalia kwenye uboreshaji
wa Uumbaji wake ingawaje maana ya Usanii yaweza isitambulikane kwa watu kwa
ujumla. Hata mamlaka za kiulimwengu
hazifahamiki, ambazo kwa kuchunguza zaweza kuonekana sahihi wakati zikiwekwa
kwenye kipimo.
Ikiwa una mashaka na asili ya dawa au lishe, na baada
ya majaribio mara mbili au tatu asili yake ikawa dhahiri kabisa, je,
hutaiondolea mashaka yote kuhusu asili yake kwenye akili yako?
Kwa nini basi usilipasikie jambo hili na kipimo? Kwa nini usitambue kwamba lolote linaloamriwa
na Mwenye Nguvu zote Allah ni katika faida zilizo bora mno kuliko zote kwa
viumbe vyake? Vipi basi kuhusu hawa watu wajinga, ambao mbele za ushahidi mzito
huu, ambao hauwezi kukadiriwa hawawezi kuvutika na Muumba na Msanii wa
ulimwengu?
Hata kama nusu
ya ulimwengu na vilivyomo vingeonekana kuwa vimeharibika na visivyo na mpango,
itakuwa hoja mbovu na elimu potofu.
Kuufikiria kama usio na Dhumuni na Usanii, kwa kuwa nusu nyingine iko
katika hali ya ukamilifu na uzuri, ambao huondoa mara moja neno
lisilothibitika. Huwezekana vipi neno
kama hili lisilothibitika likubaliwe kwa kuwa kila kitu katika ulimwengu
kinaonekana kwa kuchunguzwa na uangalizi, kuwa vilivyopangwa na hali ya uzuri
zaidi, kiasi hivyo kwamba hakuna kinachoweza kudhaniwa ambacho hakina mfano
bora zaidi miongoni mwa Uumbaji wa Ki-Mungu.
Elewa kwamba ulimwengu unaitwa kwa jina la 'Cosmos',
ambalo lina maana ya mapambo katika lugha ya Kiyunani, na Mafilosofa na
wajifanyao wahenga. Imeitwa hivyo kwa
sababu ya ukamilifu wa mpangilio. Kwa
nini wasiuite Amri ya Ki-Mungu? Jina la
'Cosmos' huonyesha kwamba mpango mzuri wa maongozi ya Mungu yako kwenye msingi
wa utashi na umaridadi.
Nashangazwa na watu hawa ambao wanaachilia makosa
katika elimu ya uganga, ambayo ni yenye hitilafu sana, lakini huleta hoja za
kutaka kujua mpango wa ulimwengu, ambao ni kamili bila waa (kosa).
Nashangazwa na mwenendo wa wadai wa filosofia, ambao
hawana elimu ya utukufu wa Uumbaj na bado wanahoji utukufu wa Mwenye Nguvu zote
Allah. Namshangaa hususan mtu huyu
mwenye bahati mbaya na duni, Mani, ambaye anadai kuelewa maajabu ya elimu
wakati ni mjinga halisi wa hoja za ubora
mno wa Uumbaji, na hivyo kujitia kwenye kuhoji Hekima Kuu ya Mwenye Nguvu zote
Allah (s.w.t.) katika Kadhia ya Uumbaji.
Juu ya wote hao, Walahidi ni wa kuhurumiwa, ambao
wanataka kumwona kwa macho yao Yule Ambaye ni fumbo hara kwa akili, wameamua
kukana kabisa kuwepo kwake. Walidai kwa
nini Hawezi kuzunguukwa ndani ya
akili? Hushinda akili kama vile vitu
vilivyo nje ya fani ya kuona, haviwezi kutambulika kwa macho.
Kama kwa mfano, unaona kipande cha jiwe kinapita juu
angani (kimerushwa), mantiki ya maana utakayo chukuwa ni kwamba mtu fulani
kalitupa juu. Jicho linaweza likawa
halikuliona (likitupwa) na bado akili hutambua hivyo kwa sababu ya uwezo wake
wa utambuzi, ya kwamba kipande cha jiwe hakiwezi kujirusha chenyewe juu
angani. Unaona kwamba jicho limesimama
katika hatua fulani na haliwezi kuendelea mbele. Kadhalika akili husimama ghafla katika mpaka
wake ilioruhusiwa katika kadhia ya kuwapo pote kiroho. Haiwezi kuendelea mbele zaidi.
Tunasema, hata hivyo, kwamba akili ambayo hutambua
kwamba mtu humiliki dhati na nafsi (roho), ijapokuwa ni ukweli kwamba hakuna
aliyeiona dhati kwa macho ya umbo, akili hiyo hiyo yapasa kuwa na uwezo wa
kufahamu na kukubali kuwepo kwa Muumba, bila kuwa na uwezo wa kutambua Nafzi
Yake.
Na kama sasa wakiuliza kwa nini Ameweka wajibat
(ulazima) juu ya mtu mdogo kupata utambuzi Wake kwa akili zake kwa kuwa hawezi
kutambua Yeye kikamilifu, jibu litakuwa kwamba dai la kumtambua Yeye ni kwenye
masharti kwa kiwango ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanya, kwa uwezo
ilionao. Ni kuamini kuwepo Kwake na
Kutii amri na makatazo Yake. Hawatakiwi
kuzunguuka kuwepo Kwake Pote (kila mahali) na Sifa Zake. Hakuna mtawala atakaye raia zake wajue hali
ya miliki na ukamilifu wake, Yote yale atakiwayo ni uaminifu na utii kwa sheria
za nchi.
Wazia kwamba mtu atausogelea moango wa Ikulu ya
Kifalme na kumtaka Mtawala ajitokeze kwake ili amjue kikamilifu, tena zaidi
angeweza akaacha kumtii, hujiweka Mwenyewe wazi katika hatia. Kadhalika yeye ambaye hushurutia imani yake
kwa Mwenye Nguvu zote Muumba kwa elimu kamili ya kuwepo Kwake Pote humchukiza
Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.).
Na kama watauliza kuwa ni kwa nini ni mpungufu, jibu
litakuwa kwamba dhana haiwezi kuruka kina cha utukufu wake na bado ijaribu
kupata kimo kile ambacho ni nje ye uwezo wake, kwa kweli hata utambuzi wa vitu
vya hali ya chini viko nje ya mpaka wake.
Jua hutoa kielelezo Kwayo. Unaliona hutoa mwanga kwenye ulimwengu wote
na bado hakuna anayejua ukweli uliopo unaolihusu. Mna idadi ya mambo yasiyothibitika
(yanayokubaliwa kwa ajili ya hoja tu) kulihusu (hilo jua) kwa maelezo hayo na
kwa kuwa maoni tofauti miongoni mwa wanachuoni yapo kuhusu hilo.
Baadhi wanazema ni umbo Kimbinguni lenye uwazi ndani
uliojaa moto unaotoa miali kutoka tundu mahsusi. Baadhi husema kwamba ni namna ya
"nebula" (jamii ya nyota nyingi kama wingu). Baadhi wanasema liko kama kioo katika
kimaumbile, lenye uwezo wa kuhifadhi joto na kisha kutapanya nuru yake
ulimwenguni. Baadhi wanasema kwamba ni
umbo nyororo kabisa lililotangamana na maji.
Wengine wanasema kwamba asili nyingi mbalimbali za moto zimeungana
pamoja.
Bado wengine wanathibitisha kwa maneno ya hoja tu
kwamba ni ziada ya kitu cha asili kwa
vile vingine vinne vya asili (ardhi, maji, hewa na moto).
Watu hawa wamehitilafiana (wametofautiana) miongoni
mwao wenyewe kwa wenyewe kuhusu umbo lake (jua). Wengine wanasema liko bapa kama ukurasa (wa
kitabu), wengine hulifikiria kama mpira usunguukao. Vile vile kuna tofauti kwenye ukubwa
wake. Baadhi hufikiria kuwa sawa kwa
ukubwa kama ardhi. Wengine wanafikiri ni
dogo kwa ukubwa kuliko ardhi. Baadhi
wanasema ni kubwa kuliko kisiwa hiki kikubwa mno (dunia). Watu wa elimu ya jometri (geometry) wanasema
kwamba liko mara mia moja na sabini kwa ukubwa wa ardhi.
Inaonyeshwa na maelezo yanayokinzana ya watu hawa
kwamba hawajui asili yake. Akili imekuwa
haina uwezo wa kuelewa asili ya jua ambalo macho yanaweza kuona na akili
kutambua, yawezekana vipi basi Nafsi Yake iwe ifahamike Ambaye ni nje ya weupe
wa akili na kufichika kutokana na mawazo?
Kama wao, basi wanasema kwa nini Amefichika kutokana
na mawazo, jibu litakuwa kwamba hakujificha kwa kitu kilichotengenezwa kama mtu
anavyoweza kuwa nyume ya milango na mapazia kutokana na kuonwa (kuonekana)
na watu wengine. Wakati tunaposema kwamba Mwenye Nguvu zote
Allah haonekani kwa macho tunamaanisha kwamba kuwapo Kwake Pote ku-laini mno
kwa mawazo na akili za kiumbo kuweza kufahamu kuwapo Kwake Pote, kama vile
nafsi (roho) ni laini mno, ingawa ipo pia ni moja miongoni mwa Uumbaji na bado
ni nje ya duru ya mawazo.
Kama sasa watasema ni kwa nini Yulaini mno kuwepo juu
ya kila kitu, swali hili litakuwa lisilothibitika, kwani zaidi sana sana Muumba
wa kila kitu lazima awe juu ya kila kitu na dhahiri kwayo.
Kama wanauliza kwamba kwa nini imejulikana kwamba
Yeye ni juu ya kila kitu na dhahiri kwayo?
Jibu litakuwa kwamba kuna ilani nne za elimu katika niaba hii:-
(1) Kuona kama
kuwapo kwa kitu ni thabiti.
(2) Asili
halisi na nafsi kwayo.
(3) Ni sifa
gani ilizonazo?
(4) Kwa nini
ni kwa vipi kuwapo Kwake.
Hakuna kiumbe anayeweza kutumia ilani hizi katika
kuhusiana na Muumba, ila kujua tu kwamba Yupo.
Hakuna anayeweza kujua kuhusu nafsi yake. Kuuliza kwa nini na kuwepo Kwake wapi kumhusu
Yeye moja kwa moja (ni swali) lisilothibitika, kwa kuona kuwa Yeye ni Muumba wa
kila kitu, na hakuna chochote kiwezacho kusimama kama chanzo au sababu ya
kuwapo Kwake.
Kwa vile watu wamekwisha elewa kwamba Yeye yupo, siyo
lazima kwamba wajue na Nafsi Yake pia, kame vile uelewaji wa roho hakufanyi
kuwa na elimu ya asili. Hali ni sawa
hivyo hivyo kwa asili ya vitu vingine vya Kiroho. Kama wanasema kwamba
unamzungumzia Yeye kama aliye mbali na kutambuliwa kwa vile Yeye ni Hai
asiyejulikana, jibu litakuwa kwamba kwa upande mmoja kimaoni kwa kweli ni
hivyo, kama akili inataka kupata elimu ya Nafsi/Asili yake. Kwa upande mwingine wa maoni, hata hivyo,
Yeye yuko karibu kuliko kila kitu, kwa kuwa ufanisi wa hoja umefanya
kuthibitisha kuwapo Kwake.
Kwa hiyo, kutoka mtazamo wa upande mmoja, Yeye yuko
dhahiri, na hakufichika kwa ye yote, kutoka mtazamo wa upande mwingine Yeye
amefichika kwa kufikiwa na akili za hisia za mwili wa mwanadamu. Ni hivyo hivyo
na akili. Hujulikana kwa hoja na
ushahidi lakini asili yake ni fumbo.
Wataalamu wa viumbe hai na mimea wanasema maumbile
hayafanyi chochote bure wala kuacha chochote feleti (bila kufanyika) ambayo
hupelekea kwenye ukamilifu wa kitu, hutoa ushuhude kwa hili. Jibu Kwao litakuwa, nani aliyefundisha
maumbile ustadi huu na elimu ya mipaka ya kila kitu, isiruke mipaka ya maana
halisi na kwenda nje ya uwezo wote, wakati ambapo hili ni jambo ambalo akili
haijifundishi hata baada ya majaribio ya uchunguzi wa mara kwa mara?
Kama wanasema kwamba maumbile yana hali ya kujua yote
na kuweza yote, kwa hiyo wanakubali kile walichokikana, kwani hizi ni sifa za
Muumba, kwamba Yeye ni Mwenye Kujua yote (Hekima Kuu) na ni Mwenye Kuweza yote
(Enzi zote). Wamempa Yeye jina la
"maumbile", sisi tunamwita Yeye Allah, Mwenye Nguvu zote, Mwenye
Kujua yote, Mwenye Kuweza yote n.k. Kama
wanakana hilo, basi Uumbaji wote huu wenye Ustadi unaita kwa nguvu kwamba
ulimwengu huu sharti uwe ni kazi ya Muumba ambaye ana sifa hii kubwa mno -
Mwenye kujua yote.
Miongoni mwa watu wa kale walikuwepo baadhi ambao
walikana Dhumuni na Usanii. Waliamini
kwamba ulimwengu ulijitokeza na kuwepo wenyewe kwa bahati tu.
Hoja yao ilikuwa kwamba wakati mwingine watoto
wachanga wanazaliwa tofauti na umbo la kawaida kama vile waweza kuwa
wameharibika viungo kwa ongezeko la kidole au kwa ubaya wa sura usio wa
kawaida. Wamehoji kwamba ulimwengu
umejitokeza kuwapo bila dhumuni na mpango.
Kwamba (watoto hao) wamejitokeza kuwa hai wenyewe na kwa bahati tu.
Mtaalam mmoja aitwae Aristotle alikania hoja
yao. Jibu lake lilikuwa kwamba kama kitu
chochote, hutokea kwa kadiri ionekanavyo kwa bahati, hicho pia kina sababu
mahsusi ambazo hukipotea kutoka shughuli zake za kawaida. Bahati ile kamwe haiko kwenye daraja la
shughuli za Kawaida ambazo huenda zikaendelea daima.
Unaona jamii tofauti za wanyama wafuatao mtindo wa
kawaida na kupata maumbo dhahiri, kwa mfano mtoto mchanga wa kibinadamu wakati
anazaliwa ana mikono miwili, miguu miwili na vidole vitano (vya mikono na
miguu) kila mmoja kama inavyoonekana kikawaida miongoni mwa watu. Hata hivyo, wakati mwingine, mambo huwa
tofauti - kinyume kutokana na baadhi ya sababu zinazoathiri jauhari za uzazi
ambazo hufanya kukua kwa kilengwa katika mfuko wa uzazi; kama vile inavyotokea
hivyo kwa sababu ya baadhi ya khitilafu katika ala (zana za kazi), ambazo
anafanyizia kitu maalum ambacho kinatengenezwa, hakiji sawa na usanii wa
fundi.
Kadhalika, sababu fulanihutambaa kwa mtoto wa wanyama
ambazo hupelekea kuharibika viungo, kupungua au kuongezeka katika mipaka,
lakini kijumla wako kikawaida mfumo sawa bila kombo.
Kama vile khitilafu itambaavyo, kwenye mambo fulani
katika hali ya njia halisi bila kuwa kinyume na mpango na bila kutoa ushahidi
kwamba siyo vyombo vya ufundi vya mafundi; kadhalika mambo fulani yanaathiwa na
vikwazo fulani katika shughuli za kawaida za maumbile, hauwezi kufanya kuwa ni
sababu katika pendeleo la kutokea hivi hivi na bahati. Kwa hiyo yeyote, ambaye juu ya msingi wa
kweli kinume na maumbile, husema kwamba kila kitu kimejitokeza kuwepo kwa
bahati tu, anafanya kitu kisichothibitika na maelezo yasiyo na akili.
Kama wanasema ni kwa nini vitu fulani vina maumbo
kamili ambapo vingine vina kasoro moja, jibu litakuwa kwamba ni kuonyesha
kwamba vitu vya ulimwengu haviko kwa sababu ya ulazimisho wa maumbile wala si
lazima kwamba kama ilikuwa kwa sababu ya maumbile, vyote vingepaswa kuwa na
mfumo mmoja kama wakinzani hawa wanavyosema. Yote haya hutokea chini ya kupenda
na Dhumuni
UTUKUFU UWE KWA MWENYE NGUVU ZOTE ALLAH, MHIFADHI WA
MALIMWENGU !
Elimu ambayo nimeiweka juu yako yapasa isomwe kwa
moyo. Yapasa uwe na shukurani kwa Mwenye
Nguvu zote Allah na Mhimidi Yeye kwa baraka Zake. Yapasa uwatii Wapenzi Wake.
Nimetoa kidogo jumla yote ya elimu na ushahidi wa
Mpango mkamilifu na Dhumuni kama hoja kwa uumbaji wa ulimwengu huu. Fikiri na tafakari juu ya hii na jifunze somo
kwayo.
Nilimuahidi Imam (a.s.) kupambanua siri ya maana ya
yote haya.
Imam (a.s.) aliweka mkono juu ya kifua changu na
akasema: "Kumbuka yote haya na hutayasahau".
Nilizirai.
Wakati nilipopata fahamu zangu, Imam (a.s.) akasema: "Ewe
Mufazzal! Unajisikiaje sasa?"
Nilijibu: "Kwa msaada wa Mola wangu, ninajitegemea
kwa kurejea kwenye kitabu hiki ambacho nimekiandika. Kila kitu kiko kwenye kumbukumbu yangu kama
vile naweza kuonyesha yote kutoka viganja vya midono yangu. Utukufu uwe kwa Mola wangu Mwenye Nguvu zote
Allah, ambaye kwake zinastahiki Shukurani na Sifa njema kama
zinavyopasika."
Imam (a.s.) akasema: Ewe Mufazzal! Uwe mkamilifu
kwenye utulivu katika akili yako, ubongo na hoja. Insha-Allah, nitakupa maelezo
ya mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoumbwa na Mwenye Nguvu zote Allah kama
maajabu yake ya Uumbaji na jamii mbalimbali na makundi ya malaika mpaka uu
kabisa kwenye "zenith" na sifa zao pamoja na viumbe vyote kuchangnya
majini na binadamu, mpaka kwenye nukta ya mwisho ya "nadir", ili
uelewe kwamba uliyojifundisha kwa sasa ni sehemu ndogo tu ya yote.
Unaweza kwenda sasa.
Unayo nafasi tukufu karibu yetu na heshima hii katika nyoyo za maumini
kama inavyohisika hamu ya maji wakati mtu ana kiu. Usiniulize kuhusu niliyokuahidi mpaka mimi
mwenyewe nisikie kupenda kuzungumza na wewe kwayo.
Nilirudi kutoka kwa Imam (a.s.) na tunu ambayo hakuna
mtu yeyote amediriki kuipokea.
Mufazzal Ibn Umar