MASIMULIZI ( HADITHI ) KATIKA QUR’AN

  

Kimekusanywa na kutarjumiwa na:AMIRALY M. H. DATOO

Bukoba - Tanzania


YALIYOMO

 

1.      MANENO MAWILI...... 3

2.      MAISHA YA MTUME LUT a.s...... 4

3.      MAISHA YA MTUME SALEH A.S.  a.s.. 11

4.      WATU WA UKHDUD  (Mahandaki).. 18

5.      WATU WA RAS..... 24

6.      WATU WA  SABT  ( Sabbath )...... 27

7.      MALAIKA : HARUT   NA   MARUT....... 30

8.      YAJUJ  NA  MAJUJ.... 34

9.      PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD..... 37

10.  WATU WA TEMBO ( As-Hab-i-Fiil ). 43

11.  WATU WA PANGONI (Kahf)...... 47

12.  BWANA DHUL-QARNAIN.. 55

13.  SHAYTANI  WASWAS-KHANNAS..... 75

14.  MI’RAJ – UN – NABII...... 77

15.  D A J J A L...... 87

16.  VITABU VILIVYOTARJUMIWA .... 91

 


 

MANENO MAWILI

Bismillahir Rahmanir Rahiim.

Namshukuru Allah swt  pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahlul Bayt a.s. kwa kunijaalia tawfiqi ya kuweza kukitayarisha kitabu hiki.

 

Mimi binafsi nimekuwa na shauku kubwa ya kusoma hadithi na visa mbalimbali kuanzia utoto wangu na kwa hakika ndiyo maana nimeweza kuwa na faida kubwa kiilimu kwani mafundisho yanayopatikana katika maandiko haya matakatifu na ya wahenga wetu, yanakuwa yamejaa nasiha na mafundisho ambayo si rahisi kuyapata kwengineko. Lakini vitabu vingi vipo ambavyo vinavyo hadithi za uchimvi na vinavyosababisha watu kumomonyoka maadili yao na hivyo kupotoka. Na ndivyo maana inatubidi kujiepusha navyo.

 

Hadithi hizi nimezitoa kutoka mchanganyiko wa vitabu mbalimbali ili kuwanufaisheni nyinyi wasomaji muvisome na kuwaelezea wananyumba wenu ili nao wafaidike na kuweza kuelewa kuwa Dini na Qur’an Tukufu si kitabu cha kuchosha, bali kama tutasoma ipasavyo, basi sisi tutafaidika mno kwani ndani mwake kuna hazina kubwa ya ilimu na hekima.

 

Vile kuna vitabu vinginevyo vinavyozungumzia visa, masimulizi kama haya, yaani Visa vya Bahlul, Fadhail na Hukumu zilizotolewa na Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki na vinginevyo nilivyovikusanya na kuvitarjumu vitawasaidieni nyote. Iwapo utakuwa na maoni yoyote yale nitashukuru iwapo utanitumia ili kuweza kusaidia katika siku za mbeleni.

 

Wakati huo ninaendelea kutayarisha masimulizi na hadithi nyinginezo za kuongezea hapo mbeleni.

Wabillahi Tawfiq,

Amiraly M.H.Datoo,    4 April 2002

P.O.Box  838

BUKOBA – Tanzania  ( datooam@hotmail.com )


MAISHA YA MTUME LUT a.s.

 

Mtume Lut a.s. alikuwa ni ndugu wa kijamaa wa Mtume Ibrahim a.s. yaani mtoto wa mamake mdogo na dada yake Mtume Lut a.s. aliolewa na Mtume Ibrahim a.s.

 

Tendo ovu kabisa lililokuwa katika ukoo wa Mtume Lut a.s. ni tendo la Ulawiti [1]

 

Tabia mbaya

Ulizidi ufisadi katika mji mmoja miongoni mwa miji ya zamani kiasi kwamba atakapoona mtu ufisadi unatendwa na mmoja kati yao basi hakatazwi na mtu mwingine atakapo shuhudia heri inafanywa na ndugu yake basi humkemea mpaka aache heri anayoifanya. Kila mtu katika kijiji hicho alikuwa katika upotevu na uovu na ujinga, hawasikii wala hawasikilizi ilikuwa ni mamoja kwao apatikane mtu wa kuwapa mawaidha wao au mtu wa kuwanasihi wao kulikuwa hakuna tofauti yoyote. Walikuwa ni watu waovu na wabaya zaidi na wenye tabia mbaya miongoni mwa watu, uhai wao (ulikuwa ni khiana na tabia mbaya) na wote hao wakati huo walikuwa ni wenye tabia mbaya sana na nia mbaya. Lakini unaonaje ewe msomaji je walijizuia na maovu yao haya au walizidi katika upotevu na ufijari na madhambi ?

 

Kuenea mambo ya haramu.

Ilikuwa kama kwamba nafsi zao hazikutosheka na kule kusema uongo na kuwa na tabia mbaya na ghadr na mengineyo mengi, wakasababisha na kuleta mambo ya unyama ambayo hakutangulia kufanya yeyote kabla yao. Je ni mambo gani hayo?

 

Hakika waliacha mambo aliyoyahalalisha Allah swt kwao kwa wanawake na wakawa hawaoi wanawake ! Wakawaacha wake zao na kuanza maovu ya kuingiliana na wanaume wenzao. Jambo ambalo Allah swt aliliharamisha kabisa.

 

Na laiti wao wangesitiri haya maovu au wakajaribu kujiepusha kutoka katika maovu haya au kujiweka mbali nayo ingelikuwa afadhali lakini wao walijitumbukiza katika mambo hayo na wakawa wanayatangaza wazi wazi mpaka ukaenea ufisadi na kukaenea mambo ya haramu na zikawa tabia zao mbaya ni rahisi kiasi kwamba zikawa zimefikia daraja kubwa sana na yote hayo yalikuwa ni madhambi na ufisadi wala hawezi mtu yeyote kuyafanya wala kufikiria binaadamu au kupiga picha ya  binaadamu katika akili yake.

 

Mlinganio wa Mtume Lut a.s.

Na walipofikia hali yao ya ufisadi kiwango hiki ndipo Allah swt alipompa Wahyi mtu mmoja miongoni mwao jina lake Mtume Lut a.s. na kukaanza kwake yeye matangazo ya wema na heri. Allah swt  alimpa Wahyi akamwamrisha kwamba afanye kazi ya kuubadilisha umma wake au kaumu yake na Mtume Lut a.s. alijibu maombi haya ya Allah swt  wake na moja kwa moja akaanza kufanya kazi hii ya kuwalingania watu kwenye heri na wema na akawa anasema:

“Enyi watu wangu! Zitoharisheni nafsi zenu na acheni mambo maovu.

 

Enyi watu wangu! Hakika kitendo chenu hiki ni haramu na Allah swt  haridhii kuwaacheni nyinyi katika hali hii bila ya kukupeni uongofu basi anayenituma mimi kwenu na mimi ni miongoni mwenu na siwezi kunyamaza juu ya jambo hili la haramu.

 

Enyi watu wangu! Fanyeni Tawbah ya Allah swt  na mjiepushe na nia zenu kwa ajili Yake.”

 

Kiburi.

Lakini kaumu ya Nabii Mtume Lut a.s. ambao uliwazidi wao uovu na ukawafunika wao mambo ya haramu hawakusikiliza maneno ya Mtume Lut a.s. isipokuwa walizidisha kiburi na wakapinga ‘ibada ya Allah swt  na kuacha mambo haramu na wala hawakunyamaza kuyafanya maovu yao bali waliendelea kufanya kiburi na wakafanya njama kwamba wamwondoe Mtume Lut a.s. na watu walioamini maneno ya Mtume Lut a.s. katika kijiji chao kwa sababu Mtume Lut a.s. na watu walio mwamini Mtume Lut a.s. hawafanyi mambo ya uovu kama wanavyofanya wao bila wanajitoharisha. Hivyo wakamwendea Mtume Lut a.s. huku wakimwonya na wakimtaka kwamba atoke kwenye kijiji chao. Na vile vile walimwahidi kuwa atatoka tu kwani watamfanyia njama na majungu mpaka atoke kijijini humo.

 

Maonyo.

Wakati walipoona Mtume Lut a.s. njama na kiburi kutoka kwa kaumu yake, akarudia maneno yake kwa kuwaambia wao na kuwaonya na kuwafahamisha matokeo ya njama zao watakavyo fanya na akuwaambia wao

“Enyi kaumu yangu ! Kama hamtafanya Tawbah na kuacha haya maasi basi kwa hakika Allah swt  atawashushieni adhabu kutoka mbinguni. Hakika Allah swt anakuoneni nyinyi na wala hakuathirika na nyinyi na yeye hapendi ukafiri na wala ufisadi na wala hawapendi watu wanaofanya ufisadi.

 

Rejeeni na mfanye tawbah kwa Allah swt na acheni madhambi na mambo mauovu.

 

Hakika mimi naogopa adhabu ya Allah swt  na mateso yake yatakayo shuka kwenu”.

 

Na pamoja na haya hawakusikiliza maneno yake isipokuwa walimfanyia mzaha na kumtania na wakamkemea kwamba atatoka tu pamoja na watu walio mwamiani yeye kwa sababu wao wanajitoharisha wenyewe kwa wenyewe na hawakujali wao kwamba yeye Mtume Lut a.s. ni mfanya dhambi au makosa yoyote.

 

Kujibu kwa Allah swt .

Na hakika Allah swt hakumwacha Mtume Lut a.s. na watu walio mwamini yeye bila ya kuwanusuru na kuwapa ushindi wala hakuwaacha makafiri waliokuwa madhalimu bila ya kuwaadhibu wao.

 

Ni hawa makafiri ambao wamedhihirisha ufisadi na huyu Mtume Lut a.s. ambaye anawatahadharisha na kuwazuia wao  bila ya kupata majibu yoyote mwisho.

 

Hatimaye Mtume Lut a.s. akalazimika kumwomba Allah swt awateremshie juu ya watu hawa adhabu na tutanaona kwamba madhalimu hawataweza kumtoa Mtume Lut a.s. au kuizuia au kuifukuza adhabu itakayowamiminikia juu yao.

 

Allah swt akajibu dua ya Mtume Lut a.s. na akaishusha  !

 

Malaika wako kwa Mtume Ibrahim a.s.

Allah swt  amewatuma Malaika kwenda kwa watu wa mji huu wakapitia kwanza katika nyumba ya Mtume Ibrahim a.s. na Malaika hawa walikuwa katika umbile la binaadamu (Mtume Ibrahim a.s. aliwakaribisha na kuwawekea chakula ili wale, lakini wao hawakula, kwani Malaika huwa hawali chakula) Mtume Ibrahim a.s. akawaogopa wao.

 

Malaika wakamwambia Mtume Ibrahim a.s.

“Usiogope hakika sisi ni Malaika kutoka kwa Allah swt  na tumetumwa kwa kaumu ya Mtume Lut a.s. watu waovu ili tuwaadhibu wao lakini tumepita kwako ili tukubashirie wewe kwamba utazaa mtoto.”

 

Mtume Ibrahim a.s. kwa kuyasikia hayo alifurahi mno yeye pamoja na mke wake (na yeye akiwa ni mwenye umri mkubwa hakuzaa mpaka hivi sasa).

 

Mtume Ibrahim a.s. aliwaonea huruma watu wa kaumu ya Mtume Lut a.s. na akaogopa kwamba yasije yakamfika madhara Mtume Lut a.s. kwa hiyo Malaika nao wakamjibu kwamba (hakuna hofu yoyote juu ya Mtume Lut a.s. isipokuwa mke wake alikuwa ni miongoni mwa makafiri………..!

 

Kwenda kwenye kijiji cha Mtume Lut a.s.

Wakamwacha Mtume Ibrahim a.s. na wakaenda zao kwa Mtume Lut a.s. wakiwa katika maumbo ya vijana wa kiume wenye sura nzuri sana wakaenda moja kwa moja mpaka kwenye kijiji cha watu wadhalimu na wakaingia katika nyumba ya Mtume Lut a.s., Mtume Lut a.s. akaogopa kwamba wasije wakamfedhehesha watu wake kwa mambo yao maovu yanayo julikana.

 

Mtume Lut a.s. alijaribu kuwaficha hao na habari za wageni wake bila kujua kwamba wao ni malaika lakini wale Kaumu waligundua jambo lile na wakapeana habari wao kwa wao kwamba waanze kufanya uovu wao kwa wale wageni wa Mtume Lut a.s. Basi ni nani ambaye ametangaza siri ile iliyofichwa kwamba nyumbani kwa Mtume Lut a.s. kulikuwa na wageni wazuri ?

 

Hakuna shaka kwamba yuko aliyejua jambo lile na akaenda kwa makafiri kuwapa habari na hakuna shaka kwamba huyu aliyeitoa habari ni kafiri kama wao na kwa sababu hii ndipo akawajulisha wao juu ya jambo hili la uovu.

 

Mke wa Mtume Lut a.s.

Hakika mke wa Mtume Lut a.s. ndiye aliyetoa habari kuwapa wale watu na kuwafahamisha jambo la wageni na kwamba yeye huyo mwanamke alikuwa kafiri na alitangaza ukafiri na akaitoa nje siri na haraka wakaja makafiri katika nyuma ya Mtume Lut a.s. wakawa wanamtaka Mtume Lut a.s. awakabidhi wao wageni wake ili wawafanyie mabaya.

 

Akaogopa Mtume Lut a.s. na akawaomba wao wajitenge na kujiepusha kabisa na jambo hilo lakini wao walikuwa ni makafiri na watu waovu kabisa ambao wamefikia daraja kwamba hawasikii nasaha ya mtu yeyote na wala hawawezi kujiepusha na maovu.

 

Mtume Lut a.s. alifunga milango mbele yao na aliwaghadhabikia sana na katika dakika chache tu wao kwa ujeuri wakaingia kwenye nyumba na wakataka kufanya ulawiti juu ya wageni wa Mtume Lut a.s.

 

Ukweli

Alikaa Mtume Lut a.s. akiwa mwenye kuhuzunika kwa kuingia waovu ndani ya nyumba yake lakini wale wageni ambao walikuwa mle ndani walicheka tu kwa kuingia watu hawa ndani ya nyumba ya Mtume Lut a.s. na waligeuza nyuso zao kumwelekea Mtume Lut a.s.na wakamtuliza yeye kwa kumwambia kuwa wao ni Malaika kutoka kwa Allah swt na wakamwambia Mtume Lut a.s. :

“Hakika sisi tumekuja kukuokoa wewe pamoja na waliokuamini wewe. Usituogopa na tunakuomba uiache nyumba yako wakati wa mwisho wa usiku.

 

Wewe pamoja na wafuasi wako  mutajitenga mbali na kutoka katika kijiji hiki ambacho kitashushiwa adhabu kutoka kwa Allah swt.

 

Na tunakuomba umwache mkeo kwani yeye ni Kafiri aliye pamoja na watakao adhibiwa naye ni mfano wao anafanya na kuwapa msaada watu waovu.”

 

Na baada ya hapo alifurahi mjumbe wa Allah swt na ikamwondokea hofu moyoni mwake.

 

Mwisho wa woga.

Akatoka Mtume Lut a.s. na watu wake (isipokuwa mkewe) Mtume Lut a.s. akakiacha kile kijiji bila ya kukisikitikia mpaka akawa mbali kabisa na kile kijiji na ikaja amri kutoka kwa Allah swt ya kushushiwa adhabu. Yakashuka mawe na ikatikisika ardhi na yakapinduliwa majumba na kubomoka na zikaanguka sakafuni na ikawa ardhi yao juu chini na chini juu.

 

Je nini kimepita ? Hiyo ni adhabu ya Allah swt na hayo ndiyo mateso hakika wamekuwa makafiri chini ya kupondwa pondwa na kuharibiwa majumba yao na kubomolewa na mizoga yao kutawanyika yote haya ndio malipo ya kazi yao mbaya ya ukafiri na ubishi wao kwani wao walifanya kiburi na wakapinga uongofu.

 

Mwisho wa Haki.

 

Na baada ya kufa makafiri je kwa maoni yako nani alibakia ? Ni nani alipata ushindi na akaishi ?

 

Jibu ni kwamba wale walioamini ( Mtume Lut a.s. na watu wake ambao walimwamini yeye) ama mke wake ambaye alishiriki na makafiri na hivyo alikufa pamoja na makafiri na hivyo ndivyo ilivyo uongofu siku zote huwa juu na uovu hurudi chini na hali hii ni ya kudumu.

 

Enyi ndugu zangu kwa hivyo tutakapopigana Jihadi, tukasubiri na kuvumilia magumu, hakika ushindi utakuja kuwa pamoja nasi mwisho wake na Allah swt atawagharikisha wale wenye kiburi.  Hakika Allah swt yu pamoja na wacha Mungu ambao wao ndio wenye kufanya wema.

 

Na ninataka kukuulizeni enyi vijana mashujaa kabla sijawaageni mwisho wa kisa hiki :

Je mnajua kwa nini tunasoma visa hivi?

 

Kwa hakika sisi tunasoma visa hivi ili tufahamu haki kutokana na visa hivi na hakika ya sisi tutazichukua nafsi zetu moja kwa moja kufuata haki hii na tutafuata maneno yaliyo mazuri na maana iliyo nzuri na sisi tuko pamoja na Allah swt na wanao mcha Allah swt na waumini na tunamshukuru Allah swt kwa kutoa neema ya imani ya ucha Mungu.

 

MWISHO

 


MAISHA YA MTUME SALEH A.S.  a.s.

 

Mtume Saleh a.s. aliitwa:

Mtume Saleh a.s. bin Abud bin Asif bin Nasikh bin Abud bin Hadir bin Thamud bin Amir bin Sam bin Nuh.

 

Kabila lake lilikuwa likiishi mipaka ya Kusini ya Syria katika milki iliyokuwa ikijulikana  kama Al-hijr au  Al-Hajar na ilijulikana kama Wadi-ul-Qura.

 

Mtume Saleh a.s. alikuja baada ya Mtume Hud a.s. na alitokana na kizazi cha tisa cha Mtume Nuh a.s.

 

Urithi.

Baada ya kuangamiza Allah swt  Qaum-u-‘Aad ambao hawakuyasikiliza maneno ya Mtume wao Hud a.s. na baada ya kufa hao wote ikabaki ardhi yao bila majumba wala wakazi wala mimea hata wanyama na baada ya haya yote Allah swt  aliirithisha ardhi yao kwa Qaum nyingine nao ni Qaum Thamud. Wakaja Qaumu Thamud mahali pakawa Qaum-u-‘Aad Allah swt  aliwaneemesha neema nyingi kuliko Qaum ‘Aad.

Walijenga Qaum Thamud majumba kati ya majabali na wakalima mabustani na makonde na wakatoboa mito lakini pamoja na masikitiko makubwa hazikuwa akili zoa zina maendeleo kuliko Qaum iliyotangulia.

Ni hao hao ambao waliabudu masanamu na mawe na wakadhani kwamba neema yao haitoondoka na wala haitatoweka.

 

Ujumbe

Na mbele ya utakafiri huu na ujinga Allah swt  alimtuma kwao mwanamme miongoni mwao anayeitwa Mtume Saleh a.s. na yeye miongoni mwa watukufu wao na mwenye akili katika wao ambaye alimuamini Allah swt  wake na Allah swt  alimchagua yeye ili awaongoe hawa Majahili waliopotea akawalingania wao kwenye ibada ya Allah swt na akatilia mkazo na akawaimiza wao juu ya Tawhid yaani kumpwekesha Allah swt  na kuacha kumshirikisha Yeye ni Yeye ambaye aliwaumba wao na akawaumbia wao ardhi na akawapa wao miongoni mwa fadhila Zake na neema Zake kisha akawakataza wao kuabudia masanamu ambayo wameyatengeneza wao wenyewe.

Kwani hayo masanamu hayadhuru wala hayanufaishi chochote na wala hayamtoshelezi mtu kutoka kwa Allah swt  chochote kisha akawakumbusha wao kwamba yeye ni miongoni mwa wao na yeye anapenda kuwanufaisha wao na wanapojipatia maslaha yao na akawaamrisha wao wamtake msamaha Allah swt  na watubu kwake Yeye kwani yeye ni mwenye kusikia na mwenye kujibu na anakubali toba kwa yule mwenye kutaka msamaha kwake.

 

Upingaji

Lakini masikio hayakusikiliza  wala nyoyo hazikufunguka na macho hayakuona wakapinga na kumpinga Mtume Saleh a.s. pamoja na ujumbe wake na wakawa wanamfanyia mzaha kwa ujumbe wake na wala hawakusimama kwao ukafiri mpaka kufikia kiwango hiki bali walisema kumwambia Mtume Saleh a.s.:

“Ewe Mtume Saleh a.s. sisi tumekujua wewe kwamba ni mwenye akili na mwongozi na tulikuwa tunakuuliza wewe na tulikuwa tunakutaka ushauri wewe katika mambo yetu una nini leo unatamka mambo ya upuuzi na upi huu msamaha ambao wewe unatuitia sisi kwao aidha sisi tunaabudu walichokua wanaabudu mababa zetu miongoni mwa masanamu na miungu aidha sisi hivi sasa tupo katika shaka kwa kile unachotuitia sisi kwacho na wala hatutaamini maneno yako na wala hatutosadiki na kuacha itikadi zetu na itikadi za mababu zetu kwa ajili yako.”

 

Kutahadharisha

Aliposikia Mtume Saleh a.s. kutoka kwao maneno haya aliwajibu wao kwa hali ya subira na kihekima akisema:

“Enyi watu hakika ambayo nayasema ni haki na hakika ya mnacho kiabudu miongoni mwa mawe ni batili na hakika mimi naogopa kwenu kutokana na nguvu za Allah swt  ambaye mnamkufurisha baada ya kukupeni nyinyi mali na majumba na mabustani.

 

“Enyi watu mtakeni msamaha Allah swt  hakika mimi ni mjumbe wa Allah swt  kwenu wala sitaki kwa nyinyi mali wala urais hakika si jambo lingine nachotaka mimi ni kukuongoeni nyinyi na kujalieni nyinyi mfikiri na malipo yangu mimi yapo kwa Allah swt  Bwana wa viumbe wote ambaye amenituma mimi kwenu na yeye ambaye atanilipa mimi Akhera na ataneemesha kwenu neema nyingi ikiwa nyinyi mtajibu na kukubali Da’awa yangu kwa imani na kwa kusilimu.

 

Wanyonge.

Na katika kila kaumu enyi ndugu zangu hupatikana watu wenye akili na ambao wanapenda nasiha na katika Qaumu ya Thamud kulikuwa na kikundi cha watu wachache miongoni mwa watu wanyonge ambao waliona kwamba utajiri haunufaishi chochote mbele ya ujahili wakafikiria kwa akili zao wakaona kwamba hakika anachowaitia Mtume Saleh a.s. ni cha haki na kuingia akilini.

 

Hakika Allah swt  ameumba ulimwengu na masanamu hayanufaishi chochote japokuwa waliabudia hayo masanamu mababa na mababu vikafunguka vifua vya kikundi hiki cha watu wachache na wakaingia katika dini mpya na wakatangaza kusilimu kwao na wakaingia katika imani na kwa hali hii wakawa pamoja na Mtume Saleh a.s. baadhi ya watu walio amini miongoni mwa kaumu yake walioshudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah swt na kwamba yeye Mtume Saleh a.s. ni mjumbe wa kutoka kwa Allah swt .

 

Subira na Jihadi.

Na ama ambao waliofanya kiburi na wakazuia Da’awa ya Mtume Saleh a.s. kwa vitimbi vyao na wakashikamana kwa ibada zao za kuabudu masanamu na wakamwambia Mtume Saleh a.s. kwamba hakika Shetani amekutania wewe na ukawa unatamka mambo ya wazimu kisha wakawa wanamzuia yeye kunako dini yake lakini yeye alisubiri na akavumilia kutokana na maudhi yao na vitimbi vyao na akaendeleza tablighi yake na akasema :

“Enyi watu hakika mimi sikuacha dini ya haki na nikakufuru kama mlivyo kufuru nyinyi na wala hamtoweza kurudisha kwangu mimi adhabu inayotoka kwa Allah swt .”

 

Lakini ikiwa mmeingia katika Uislam na mkapata uongofu na imani hakika Allah swt  atakuingizeni nyinyi baada ya kuamini kwenu Jannat (peponi) siku ya Qiyama.

 

Enyi watu hamkuwa nyinyi isipokuwa ni waongo mnaacha kutumia akili zenu na mkafata matamanio yenu na mkawa miongoni mwa makafiri.

 

Hofu

Na walipo kutakwamba imani imepata nguvu na subira na mshikamano wenye nguvu waliogopa Mustakbirun kwamba kikundi cha waumini wachache kitazidi na kuwa chenye nguvu hakika waliogopa enyi ndugu zangu juu ya mali zao na maslaha yao na wakaogopa juu ya dola yao na ufalme wao basi vipi wataishi kesho ikiwa idadi ya Muumina itaongezeka.

 

Hakika hakuna budi ila kuondoa mushkili huu walifikiri makafiri juu ya jambo hili ambalo lilikuwa linawahuzunisha wao na serikali yao wakaona kwamba wamuombe Mtume Saleh a.s. baadhi ya mambo ayafanye wakidhani kwamba hatoweza kuyafanya hayo mambo na baada ya hapo watajitenga watu ambao walioamini baada ya kudhihiri kushinda kwake na udhaifu wake.

 

Kuomba muujiza

Na kawaida ya makafiri ambao hawaamini wao hupenda kuwatenganisha watu kutoka kwenye imani ili wawe kama wao na walidhani hawa makafiri kwamba makafiri kutoka kaumu ya Mtume Saleh a.s. kwamba watakapo mtaka Mtume wao jambo gumu na atakapo shindwa kulifanya hakika wanachomtakia wao kitakuja kuthibitika. Na watakuja hao makafiri kwa Mtume Saleh a.s. wakizungumza naye kuhusu muujiza wake na wakimtaka awaletee wao huo muujiza ili hiyo dalili juu ya ukweli kwa jambo lake na kwamba yeye ni mtume wa Allah swt  kama wanavyodai kwake.  Na hakika walisema kwamba watakapo taka tukuamini wewe na kuamini ujumbe wako tuletee muujiza ili tukuamini la sivyo sisi tutabaki katika ibada yetu ya masanamu.

 

Ngamia

Hakika ya Mtume Saleh a.s. hawezi kufanya jambo lolote isipokuwa kwa idhini ya Allah swt  na vipi ataweza kufanya jambo na yeye ni mtu kama wao. Hakika Allah swt  enyi ndugu zangu anajua kwamba makafiri wengi hawaamini hata kama wataona muujiza lakini ili uwe ukafiri wao ni hoja iliyo batilika hakika Allah swt  alituma kwao Ngamia wa ajabu na muujiza wa Ngamia huyu kwamba yeye anakunywa maji siku moja na kujizuia kunywa maji siku ya pili na akasema Mtume Saleh a.s. kuwaambia kaumu yake kwamba huyu Ngamia amemtuma Allah swt  na atakuwa kinywaji chake katika kijiji ni cha kupokezana siku moja ni yenu nyinyi na siku moja ni yake yeye. Jiepusheni na kumuuzi Ngamia huyu na msibadilishe amri na nidhamu hii.

 

Hofu kutoka kwa makafiri

Na hakika Mtume Saleh a.s. alijua kwamba makafiri imewaogopesha amri hii ya Allah swt  kwa hivyo watafanya njama ya kumuua Ngamia.

 

Kwa sababu hiyo alikwenda Mtume Saleh a.s. kwa kaumu yake na yeye akiwaambia kwamba (msimfanyie mabaya Ngamia huyu na mtakapo muudhi Ngamia huyu basi Allah swt atashusha adhabu juu yenu kwa haraka). Hakika amewafikishia Mtume Saleh a.s. ujumbe na akawatahadharisha wao na akawaonya lakini makafiri waliona kwamba huo muujiza uko wazi na unajulisha wazi Utume wake, wakaogopa isije ikazidi idadi ya walioamini na wakaongezeka waliokuwa pamoja na Mtume Saleh a.s., basi wao yaani makafiri hawapendi watu waamini au waamini mwingine zaidi ya walioamini kwa sababu hiyo kwamba wao walifikiri katika njia nyingine kinyume cha Mtume Saleh a.s. na sasa hawataki tena muujiza mwingine na kwamba wao walikengeuka kwenye kitu kingine.

 

Njama.

Hakika waliangalia makafiri kumwangalia Ngamia mnene wa ajabu wakaogopa juu ya serikali yao kutokana na muujiza huu ulio wazi na wadhahiri na kwamba muujiza huu unavuta nyoyo za watu na unazivutia nafsi za watu. Yote haya yaliwafanya wao wafikirie juu ya muujiza huu nao ni Ngamia kwamba ni muujiza wa hatari na wao hawawezi kuepuka hatari hii ila kwa kumuua Ngamia, wakafikiria mbinu ya kutimiza njama zao na mwisho wakaafikiana kwamba waende baadhi yao mahali anaponywea maji Ngamia na huko huko watamwulia wakati Ngamia anaporejea kutoka mahali anaponywe maji na wao watakuwa wamejiepusha na muujiza huo wa Mtume Saleh a.s. wenye kutisha na kuogopesha.

 

Mapambano ya Ngamia.

Moja kwa moja kikatoka kikundi cha makafiri kikaenda zake hadi kwa Ngamia wakisubiri marejeo yake kutoka mahali anaponywea maji na wakati alipokuwa akirejea Ngamia, akatupa mmoja wao kumtupia Ngamia mshale ambao ulimchoma na akaanguka Ngamia juu ya ardhi na wala hakutosheka na hayo bali wakamchinja ngamia na kumuua kisha wakarudi kumwendea Mtume Saleh a.s. huku wakisema kwamba hakika ulitutahadharisha sisi na adhabu ikiwa tutamuua Ngamia, tuletee adhabu ! Haya hatutarudia kukuogopa wewe wala Ngamia wako. Mtume Saleh a.s. akawajibu fanyeni starehe zenu kabla ya adhabu ya Allah swt na mateso, hakika nilikutahadharisheni kwa kutokumuua Ngamia na mkamuua basi subirini adhabu iliyo ahidiwa na Allah swt .

 

Maiti zilizoganda

Hakika ahadi ya Allah swt ni kweli na adhabu ni karibu, kisha makafiri wakamuomba Mtume Saleh a.s. afanye haraka au aharakishe adhabu kwao na wao waliyasema haya katika hali ya kumfanyia mzaha Mtume Saleh a.s. wakaafikiana makafiri upya kwamba wamuue Mtume Saleh a.s. na watu wake wakiwa wao usingizini usiku, lakini Allah swt hakusahau na wala hakumsahau Mtume wake aliye muumin na walioamini pamoja waliomwamini Mtume Saleh a.s. na ulipoingia usiku ikaja ahadi ya Allah swt na adhabu yake ukavuma upepo mkali ulio mkubwa na wenye kutisha ukawafanya makafiri kuwa ni miili iliyoganda haitikisiki abadan, akaamka Mtume Saleh a.s. na akaona yaliyo pita juu ya makafiri na akajua kwamba Allah swt amesha wateketeza na kuwaangamiza wao, na Allah swt akamwamsha Mtume Saleh a.s.

 

Na yeye akawaamsha wale waliokuwa wamemwanini  yeye na akasema:

“Enyi watu wangu! Hakika nimekufikishieni nyinyi ujumbe wa Allah swt  na nikakuonyeni lakini hamuwapendi wenye kutoa nasiha.”

 

Mwisho.

Na sasa je mmeona enyi ndugu zangu vipi kafiri asiyamini vile muujiza usivyomfaa yeye chochote na anavyouogopa ?

 

Nao waliomba muujiza kutoka kwa Allah swt naye akatuma Ngamia na Mtume Saleh a.s. akawatahadharisha wao wasimwudhi Ngamia na wao wakamwudhi na vile vile wakamwua na Mtume Saleh a.s. aliwatahadharishia adhabu, wao wakaiomba adhabu na kisha Mtume Saleh a.s. akawaahidi wao adhabu na wakasema iletwe haraka kwao.

 

Je walipata faida yoyote kutoka kwa muujiza ?

 

Jibu ni kwamba wao hawakufaidika chochote.

 

MWISHO


WATU WA UKHDUD  (Mahandaki)

Qurani Tukufu inatuambia: Sura Al-Buruj, 85, Ayah ya 4 - 9.

Kuwa walioangamizwa walikuwa watu wa mahandaki. Ya Moto wenye kuni. Walipokuwa wamekaa hapo. Wakitazama yale waliyokuwa wakiwatendea waumini. Wao waliwatesa (hao) si kwa kingine ila hao walimwamini Allah, Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa. Ambaye ni Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi; na Allah ni Mwenye kuona kila kitu.

 

Kuulizia

Imam wa tano, Muhammad ibn-‘Ali Al-Baquir a.s. anasema kuwa siku moja Imam wa kwanza, Imam ‘Ali ibni Abi Talib a.s. alimtuma mtu kwenda kwa wakuu wa dini ya Wakristo wa Najran kwa kuwauliza kuhusu watu wa Mahandaki  ---  na baada ya kupata majibu yao, aliwatumia ujumbe kuwa:

“Kile mukihadithiacho kuhusu watu hao, si hadithi ya kweli na kwa hakika hadithi ya kweli ni kama ifuatavyo.”

 

Kisa cha kweli

Zu-Nuwas alikuwa ni mfalme wa mwisho wa kabila la Hamir, mwishoni mwa  karne ya  sita A.D. Yeye alikuwa ni mfuasii wa dini ya Juda ( dini ya Kiyahudi) na hivyo ilikuwa ndiyo dini ya Serikali. Dini hiyo ya Juda ilikuwa imeachwa na watu baada ya kuja Mtume ‘Isa a.s. Lakini Zu-Nuwas aliendelea kuwaadhibu vikali mno wale wote walioifuata dini ya Mtume ‘Isa a.s. na alitumia mbinu mbalimbali na hila za kuimaliza dini hiyo katika kila sehemu za ardhi. Yeye alikuwa akiwapendelea mno Mayahudi na kuwatesa vikali mno Wakristo. Yeye aliwateketeza Wakristo popote pale walipoonekana katika ufalme wake. Yeye alikuwa ameamua kuusambaza Uyahudi katika kila sehemu za dunia huku akizimaliza na kuzifyeka dini zingine zote. Yeye hakubakiza juhudi zake zozote katika kufikia lengo lake hilo. Yeye vile vile alikuwa akizishambulia nchi zozote zile ambazo zilikuwa zikifuata dini mbali na dini ya Juda.  Na vile vile alikuwa mwepesi wa kuzishambulia sehemu zozote zile zilizokuwa zikifuata dini mbali na dini ya Juda na hatimaye kuwalazimisha kuifuata dini yake.

 

Allah swt  alimtuma Mtume mmoja wa Kihabeshi kwenda kuhubiri watu wa Habeshi. Mtume huyo alipambana sana na mfalme huyo ambaye alikuwa akiipigania dini yake ya Kiyahudi kwa hali na mali.

 

Katika kuupiga vita Ukristo

Siku moja alipata habari kuwa wakazi wa Najran wamekubalia dini ya Mtume ‘Isa a.s. isipokuwa Wayahudi wachache tu ndio waliokuwa wamebakia katika dini yao. Habari hizi zilimghasi na kumbughudhi mno huyo Zu-Nuwas kiasi kwamba aliupoteza usingizi wake na kukosa raha kabisa na kufikia uamuzi wa kuishambulia sehemu hiyo kwa haraka iwezekanavyo. Na hivyo alilitayarisha jeshi kubwa mno na kuwapatia silaha nyingi zilizo nzuri na alijitolea mwenyewe kuongoza vita hivyo vya kuishambulia Najran. Kwa hakika alikuwa amewaghadhabikia mno wakazi wa Najran kiasi kwamba alikuwa anataka awarudishe wote kwa pamoja katika dini ya Kiyahudi kwa haraka iwezekanavyo. Alipoukaribia mji wa Najran, aliwataka baadhi ya watu waliokuwa wameheshimika huko kuja kuwawakilisha wakazi wa Najran katika mazungumzo yao pamoja na Zu-Nuwas. 

 

Wakati watu hao walipoletwa mbele yake, yeye aliwaambia:

“Mimi nimekuja hapa baada ya kupata habari kuwa wakazi wote wa mji wenu wameiacha dini ya Kijuda na wamekubali dini ya (Mtume) ‘Isa a.s. kwa sababu ya kudanganywa na kushawishiwa na Mkristo wa Kikatoliki aitwaye Dus. Hivyo mutambue kuwa mimi nimefika hapa pamoja na jeshi langu hili lililo kubwa sana ili kuirudisha dini ya Kijuda hapa Najran na kuutokomeza kabisa Ukristo. Swala hili la kuwaiteni nyinyi hapa ni kuwatakeni nyinyi murejee kwenu mukaongee na wazee wenu ili wakazi wote wa Najran warudie katika dini ya Kijuda na kuiachilia mbali dini ya Kikristo. Kuna mambo mawili tu yaliyo bayana mbele yenu. Ama mukubali kuingia katika dini ya Kijuda ama sivyo mujiweke tayari kwa adhabu kali kabisa ambayo hayatakuwa chini ya adhabu ya kifo na maangamizo.”

 

Watu wamkabili Zu-Nuwas

Wawakilishi hawa wa wakazi wa Najran walikuwa ni watu ambao walikuwa na imani thabiti ya dini yao na hivyo wote kwa pamoja walimwelezea wazi wazi mfalme Zu-Nuwas kuwa:

·         “Sisi kamwe hatutaki ushauri na uwakilishi wa mtu yoyote yule.

·         Sisi tumeshatambua na kuipata njia ya haki na uongofu na hivyo tunafuata mafunzo na maamrisho yake.

·          Sisi kamwe hatuogopi mauti.

·         Sisi tupo tayari kukabiliana na hali yoyote ile itakayotokezea na tutakabiana nayo ipasavyo na hata kama itabidi kujitolea mhanga, basi tutafanya hivyo ili kuilinda dini na imani yetu.”

 

Zu-Nuwas alikuwa hakutegemea kupewa majibu makali na yaliyo wazi kabisa kuhusu msimamo wa wakazi wa Najran, na hivyo alizidi kukasirika.

 

Alifikia uamuzi wa kuwamaliza na kuwateketeza Wakisto wa Najran. Hivyo yeye aliwaamuru majeshi yake kuchimba mahandaki na kuyajaza kwa moto mkali kabisa. Yeye pamoja na majeshi yake walikaa kandoni kwa kuzunguka mahandaki hayo kwa kushuhudia hali mbaya kabisa. 

 

Baadaya ya hapo, alitoa amri ya kuwa waumini wote wa dini ya Kikristo waletwe mbele yake.  Kwa kutolewa amri hiyo, majeshi yake yalitoka kuwatafuta Wakristo wote na kuwaleta mbele ya Zu-Nuwas.

 

Ikatolewa amri ya kuwatupa hao katika mahandaki hayo yaliyokuwa yakiwaka moto mkali sana. Wengi walisukumwa na kuchomwa hivyo na wengine walichinjwa. Vile vile walikuwapo wengine ambao walikatwa viungo vya mwili kama masikio, pua, mikono na miguu. Hivyo ndivyo Najran ilivyotokana na watu ambao waliikuablia dini ya Mtume ‘Isa a.s.

 

Inasadikiwa kuwa Zu-Nuwas amewaua watu zaidi ya elfu ishirini (20,000) katika kulazimisha dini ya Kijuda.

 

Kutorokea Roma

Mmoja wa Wakristo alipoyaona mateso na maagamizo waliyokuwa wakitendewa wafuasi wenzake wa Kikristo, alifanikiwa kutoroka na kwenda mjini Roma akipitia majangwa na milima hadi kwa Czar, aliyekuwa mfalme, na kumpa habari zote zilizowafikia Wakristo wa Najran chini ya amri za Zu-Nuwas na alitoa ombi la kupatiwa majeshi ili kuweza kulipiza kisasi na kumshinda.

 

Majibu ya Czar

Czar alikuwa Mkristo kwa dini na alihuzunika mno kwa kusikia unyama wa Zu-Nuwas. Yeye alimwambia yule mtu kutoka Najran kuwa:

“Kwa hakika nchi yenu ipo mbali mno na kwetu na hivyo mimi siwezi kuchukua hatua yoyote ile dhidi ya Zu-Nuwas. Hata hivyo mimi ninamtumia risala maalum mfalme wa Habeshi, Najjashi (Negus) ambaye pia alikuwa Mkristo. Ufalme wake upo karibu na Yemen, ufalme wa Zu-Nuwas.  Kwa hakika itakuwa rahisi kwa Najjashi kumshinda Zu-Nuwas.”

 

Mfalme wa Kiroma alimtumia risala maalum Najjashi akimtaka amng’oe Zu-Nuwas na kuwakomboa Wakristo wa Najran. Mtu huyo aliichukua barua hiyo ya Czar na alikwenda Habeshi na akatoa habari zote za ukatili na mauaji wa Zu-Nuwas aliyowafanyia Wakristo wa Najran.

 

Najjashi alikubali kuishambulia Yemen na kuikomboa kutoka kwa Zu-Nuwas. Zu-Nuwas naye pia alijitayarisha na kujitolea kukabiliana na Najjashi. Hatimaye kulizuka vita vikali mno baina yao ambamo Najjashi alipata ushindi na Zu-Nuwas aliuawa katika vita hivyo. Najjashi aliiunganisha Najran pamoja na ufalme wake na kuirudisha dini ya Kikristo huko ambayo ndiyo ikawa dini ya Watawala.

 

Habari zaidi ya hayo

Vile vile kuna habari ifuatayo nimeipata katika utafiti mwingine:

Kulikuwapo na mwanamke mmoja muumini pamoja na mtoto wake aliyekuwa mchanga mikononi mwake. Nao pia walikuwa watupwe ndani mwa mahandaki yenye moto mkali na pale alipoukaribia moto huo, mapenzi ya mtoto wake aliye mchanga, yalimfanya arudi nyuma.

 

Mtoto huyo aliyekuwa bado yu mchanga, kwa amri za Allah swt akamwambia mamake kwa sauti kubwa

“Ewe Mama yangu ! Ruka ndani mwa mahandaki yawakayo moto mkali pamoja nami kwani moto huu ni mdogo kabisa katika mtihani wa Allah swt .”

 

Kwa hayo mwanamke huyo alijitupa motoni humo pamoja na mtoto wake huyo.  Lakini kwa amri za Allah swt, Mtume, waumini wote, mwanamke huyo pamoja na mtoto wake walikuwa salama u salimini katika mahandaki hayo bila ya kudhurika hata kidogo.

 

Kwa kusoma kisa hicho kutoka Qur’an tukufu, kwa hakika nyoyo zetu zimejawa na majonzi na masikitiko kwa kuona udhalimu ulivyokuwa katika zama za ujahiliyya. Lakini hata katika zama hizi tunazoziita sisi za maendeleo, bado udhalimu huu unaendelea humu duniani kidhahiri na batini kwa kupitia njama tofauti tofauti. Mfano mmoja wa hivi karibuni ni wa Raisi Saddam wa Iraq, alivyowaua Mashia ambao ndio raia wake.

 

Kila mtu mwenye akili na busara  atakubaliana kuwa ni dhuluma tupu kuwatesa na kuwaua na kuwateketeza watu ambao wamekuwa wakifuata madhehebu kwa mappenzi ya Ahlul-Bait ya Mtume Muhammad s.a.w.w. Someni vitabu vya historia na mtaona kuwa Mashia wameuawa kwa mamilioni  wakiwemo wanaume, wanawake na hata watoto walio wachanga ati kwa sababu ni Ma-Shia wa Imam ‘Ali a.s.

 

Katika Qur’an tukufu kuna mahala pengi panapoelezewa habari za waumini kuhukumiwa adhabu za kuuawa na kuchomwa moto. Wadhalimu watendaji hao wanapofanya hayo hushuhudiwa na watazamaji huku wakiona furaha. Kwa hakika Qur’an kwa uwazi kabisa unawalaani si wadhalimu tu bali hata wale wanaokaa kuyatazama dhuluma wafanyiwao waumini na wale ambao wanaangalia tu bila ya kujitahidi kufanya lolote ili waweze kuzuia hayo yasitokee. Ujumbe huu ni kwa watu wa Makkah ambao walikuwa wakiwahukumu kwa kuwaonea wale wote waliokuwa wameukubali Uislamu, na vivyo hivyo inatumika kwa ajili ya mateso na mauaji ya kikatili dhidi ya waumini ambao wanawafuata kikamilifu Ahlul-Bait a.s.

 

Na kwa sababu hii ndiyo maana imesemwa katika Ziyarat:

“La’anallahu Ummatan Zahamatka wa La’anallahu Ummatan Sami’at bidhalika wa radhiat bihi.”

 

 

Yaani

“Laana ya Allah swt  iwe juu ya wale wote wasiotenda uadilifu kwako na walaaniwe wale wote waliosikia haya na wakayaridhia.”

 

MWISHO

 


WATU WA RAS

 

Allah swt  anatuambia katika Qur’an Tukufu Sura al-Qaaf, 50, Ayah: 12 - 14

Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuhu na wakazi wa Rass na Thamudi.

Na Adi na Fir’auni na watu wa Mtume Luti.

Na wakazi wa kichakani, ( watu wa Nabii Shuaibu ) na watu wa Tubba ( Yemen ).Wote walikadhibisha Mitume; kwa hivyo onyo langu likathubutika ( juu yao ).

 

Watu wa Ras walikuwa ni wale watu ambao walikuwa wakiishi ukingoni mwa mto uliokuwa ukiitwa Ras. Wao waliishi katika zama baada ya Mtume Suleyman a.s. mwana wa Mtume Da’ud a.s.

 

Mto Ras ulikuwa ni mto mkubwa na watu  waliitumia ardhi iliyoizunguka katika kilimo. Wao walikuwa wakiishi maisha ya raha na mustarehe na walitosheka na mahitajio ya maisha, vyakula kwa wingi, maji matamu kwa ajili ya kunywa, miti ilijaa kwa matunda, hali ya hewa ilikuwa nzuri, ardhi nzuri na yenye mandhari nzuri ya kuvutia.  

 

Ukingoni mwa mto huo kulikuwa na mti mmoja mkubwa na mrefu kabisa kiasi kwamba unaweza kudhani kuwa ulikuwa ukigusa mawingu, uliota kwa sababu ya hali nzuri ya hewa, ukiitwa msonobari.

 

Hatimaye Shaytani alifanikiwa kuwapotosha watu hao kuuabudu mti huo kwani ulikuwa wa aina yake pekee wakati huo. Masikini watu waliingia katika mtego huo wa Shaytani na wakaanza kuuabudu mti huo kama ndio mungu wao. Watu walianza kuchukua matawi yake na kwenda kupanda sehemu zao kila mahala na kuanza kuabudu baada ya kukua katika miti kamili. Imani za watu ziliendelea kuwa madhubuti katika mti huu kiasi kwamba ukafika wakati ambapo hawakuwa na imani hata kidogo juu ya Allah swt . Wao walikuwa wakiusujudia mti huo na walikuwa wakitoa dhabihu hapo. Ujahili na upagani wao huo kiasi kwamba wakafika wakati ambapo wao walijifanyia maji ya mto huo kuwa haramu kwa ajili yao na wengine wote na badala yake wakawa wanatumia maji kutokea sehemu zinginezo kama mito na chemichemi. Wao walikuwa wakidhani kuwa maisha ya mungu wao huyo, yalikuwa yameunganika na mto Ras na hivyo hakuna mtu yeyote aruhusiwaye kuyatumia maji hayo. Na kama ilitokea kuwa kuna mtu au mnyama yeyote aliyekunywa maji ya mto huo, basi wao walimwua kwa kitali kabisa.

 

Watu hawa walikuwa wakisherehekea siku moja katika mwaka kama ndiyo siku yao tukufu. Wao walikuwa wakikusanyika karibu na chini ya mti huo huku wakitoa sadaqa zao za wanyama na baadaye kuichoma moto nyama yao.  Wakati moshi ulipokuwa ukipaa juu hadi kufikia mawinguni, wao walikuwa wakijiangusha chini kusujudu hapo mtini na walikuwa wakisoma ibada zao kwa sauti. Kwa kuyaona hayo, Shaytani alifurahishwa mno kwani alishuhudia ufanisi wake katika kuwapotosha hawa majaheli kwa kuwazuzua kuuabudu msonobari. Yeye alikuwa daima akiwazuzua kwa kila njia ili mradi watu hao wasirejee katika kumwabudu Allah swt  .

 

Ikapita miaka huku watu wa Ras wakiendelea na kuuabudu msonobari huo.  Hatimaye Allah swt  alimtuma Mtume wake kuja kuwaongoza katika njia ya Allah swt  na hivyo kuwaokoa. Mtume huyu alitokana na kizazi cha Mtume Ya’qub a.s. na kama Mitume a.s. yote iliyokuwa imetumwa sehemu zote, naye pia alianza kazi zake za tabligh na kuwaita watu katika njia ya Allah swt. Ili wafanye ‘ibada ya Allah swt tu na wala si mwingine (hata si mti huo wa msonobari). Lakini watu hao walitupilia mbali maneno ya Mtume huyo na waliendelea kuuabudu msonobari huo. Ikatokea kuwa siku yao ya maadhimisho ikawadia na Mtume huyo akashuhudia vile watu wao walivyokuwa wamejiandaa kwa matayarisho kamambe kwa ajili ya sikukuu yao hiyo ambayo ilisherehekewa na watu wote.

 

Wakati Mtume huyo alipoyaona mambo hayo ya ujahili, alimwomba Allah swt aukaushe kamili mti huo ili watu hao waweze kuzinduka kutoka ndoto yao hiyo kuwa mti huo haukustahili kuabudiwa.

 

Kwa hakika dua ya Mtume huyo ikakubaliwa na msonobari huo ukakauka kabisa kwa ghafla, na majani yake yote yakanyauka na kuanza kudondoka ardhini. Lakini watu badala ya kujipatia funzo kutokana na tukio hilo, wao waliukaribia zaidi mti huo na kudhani kuwa Mtume huyo kwa uchawi wake ameudhuru mti wao.  Wengi wao walisema kuwa Mtume huyo alikuwa ameudharau na kuukashifu mti huo hivyo kuingiwa na hasira, mti huo umebadilisha hali yake. Hivyo Mtume huyo lazima auawe kikatili kabisa ili mti huo ukifurahi uweze kurudia hali yake ya kawaida. Na hivyo mungu wao huyo (msonobari) utawawia radhi tena.

 

Kulibuniwa njama za kutaka kumwua Mtume huyo. Wao walichimba shimo kubwa mno na kumtupa Mtume huyo humo huku wakiufunika mdomo wa shimo hilo kwa jiwe kubwa. Kwa muda fulani kulikuwa kukisikika sauti za mlio wa Mtume huyo kutokea shimoni, na hatimaye sauti hiyo haikusika kamwe kwani Mtume huyo alikuwa amejitolea mhanga kwa ajili ya kutaka kuwanusuru watu wasipotee na wala wasiangamie katika adhabu za Allah swt.  Kwa matokeo ni kwamba Allah swt  alikasirishwa mno na kulianza kutokezea dalili za adhabu za Allah swt. Kulitokea kimbunga chekundu cha upepo ambacho kiliwateketeza watu wote. Kulitokezea na wingu jeusi kabisa ambalo lilifunika eneo zima kuwa kiza tupu. Hivyo watu wa Ras wamekuwa ni funzo la kujifunza kwa vizazi vilivyofuatia.

 

 

MWISHO


WATU WA  SABT  ( Sabbath )

 

Qurani Tukufu inatuambia: Sura Al-Aaraf, 7, Ayah ya 163 & 164.

Na  waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari, (watu wa mji huo) walipokuuwa wakivunja (sheria ya) Jumamosi (ambayo waliambiwa wasifanye kazi katika sikuu hiyo, wafanye ibada tu. Na kazi yao ilikuwa uvuvi). Samaki wao walipowajia juu juu siku za Jumamosi zao; na siku isiyokuwa Jumamosi hawakuwa wakiwajia (hivyo). Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu ya kuasi kwao.

 

Na (wakumbushe wakati) baadhi ya watu katika wao waliposema (kuwaonya waliovunja hishima ya Jumamosi kwa kuvua, na hali yakuwa wamekatazwa; waliposema): ‘Pana faida gani kuwaonya watu ambao Allah swt  atawaua au atawaadhibu kwa adhabu kali

 ( papa hapa)?”

Wakasema:“Tupate kuwa na udhuru mbele ya Allah swt  wenu (kuwa tumewaonya lakini hatukusikilizwa) na huenda wakaogopa.’

 

Mtume Musa a.s. mwana wa Imran aliwahubiri wana wa Isra’il kuwa wawe na siku moja maalum katika juma kwa ajili ya kumwabudu Allah swt  ili wao wasijishughulishe na kazi zinginezo mbali na ibada ikiwemo kuuza na kununua bidhaa za aina zote.

 

Siku hiyo ilikuwa makhsusi  ya Ijumaa lakini wana wa Isra’il waliiomba siku ya Jumamosi kama ndiyo siku maalumu ya kufanya ibada ya Allah swt  na hivyo siku ya Jumamosi ikawa ndiyo siku Kuu ambamo biashara za aina zote zilikatazwa. Hivyo kila Jumamosi Mtume Musa a.s. alikuwa akiwahutubia mkusanyiko maalum wa wana wa Isra’il.  Ilipita miaka na watu waliichukulia Jumamosi kama siku njema na maalum kwa ajili ya ibada za Allah swt .

 

Baada ya kuaga dunia kwa Mtume Musa a.s. kulianza kutokea mabadiliko mengi katika jamii ya wana wa Isra’il, hata hivyo wao waliendelea kuiheshimu siku ya Jumamosi kama ndiyo siku maalum kwa ajili ya ibada za Allah swt. Lakini ulipofika zama za Mtume Daud a.s., kikundi kimoja cha wana wa Isra’il waliokuwa wakiishi ukingoni mwa bahari, mji wa Ela, walipuuza utukufu wa siku hiyo ya Jumamosi na hivyo wakajishughulisha kuvua samaki.

 

Habari kamili ya matukio hayo ni kama ifuatavyo:

Wakati uvuaji wa samaki ulipokuwa umepigiwa marufuku katika siku za Jumamosi, samaki walibuni njia yao, walikuwa wakijitokeza kwa wingi ufuoni mwa bahari katika siku hizo na kwa siku zilizobakia walikuwa wakiondoka kwenda mbali kabisa katika maji mengi ili wasiweze kuvuliwa na wavuvi. Watu wa Bani Isra’il ambao walikuwa wakitilia maanani maslahi yao ya kidunia, walikusanyika na kulizungumzia swala hili na kutoa kauli yao:

“Sisi hatuna budi kubuni mikakati ya kuweza kudhibiti swala hili la uvuaji wa samaki. Katika siku za Jumamosi, samaki wengi mno huonekana ufuoni kuliko siku zinginezo. Hivyo itatuwia rahisi mno kuvua samaki siku hiyo kwani siku zingine tunambulia kapa kwani wao wanakwenda katika maji yenye kina kikubwa mno hivyo kutuwia vigumu uvuvi.”

 

Katika kikao hicho kuliafikiwa kuwa wabuni taratibu za kuvulia samaki. Hivyo wakaafikiana kuchimba mito na mifereji midogo midogo ili samaki wanapokuja ufuoni katika siku za Jumamosi waweze kupitiliza katika mifereji hiyo, hivyo kuwawia rahisi katika kuwanasa.

 

Hivyo wao walitekeleza mpango wao huo na wakachimba mito kutokea baharini. Katika siku za Jumamosi samaki wengi mno walikuwa wakiogelea kwa furaha hadi ukingoni mwa bahari na kupenya katika mito hiyo. Katika nyakati za usiku wakati samaki hao walipokuwa wakitaka kurudi baharini, hao walikuwa wakiziba midomo ya mito hiyo ili samaki hao wasiweze kurudi baharini na badala yake wabakie katika mito hiyo. Siku iliyofuatia wao walikuwa wakiwanasa samaki wote waliokuwa katika mito hiyo.

 

Hata hivyo watu wenye busara na fahamu waliwakanya watu hao wasijifanye wajanja mbele ya amri za Allah swt . Wao waliwaonya na kuwabashiria adhabu na maangamizo makubwa yaliyokuwa yakija kwao, lakini haya pia hayakufua dafu.

 

Hata hivyo watu hao wema waliendelea na juhudi zao za kuwakanya kwa njia mbalimbali kuhusu adhabu na maangamizo ya Allah swt, lakini walafi hao hawakuwasikiliza na badala yake waliwapuuza na kuwadharau. Hao waovu waliwaondoa wale wenye hekima na busara na badala yake wakaanza kuwafuata wale waliokuwa wakisema:

“Jee kwa nini nyinyi mnawahubiri watu ambao watateremshiwa adhabu kali kabisa za Allah swt na hatimaye watateketezwa kabisa ?  Hivyo muwaache katika hali yao walivyo.”

 

Kikundi cha waja wema wakawaambia hao kuwa:

“Sisi tunawahubiria ubashiri mwema hawa watu ambao hawapo katika fahamu zao kamili ili kwamba na Allah swt  aone kuwa kwa kweli hawa watu ni masikini mbele ya macho ya Allah swt .”

 

Hao wapotofu walikuwa wameshughulika mno na unasaji wa samaki kwa wingi mno bila kujali nasiha za kundi la kwanza la watu wema katika Bani Isra’il na walikuwa wakijionea ufakhari na majivuno juu ya  ufanisi wao katika mipango yao hiyo.

 

Baada ya maonyo ya siku chache, hao wapotofu walipokithiri katika kutotii amri ya Allah swt , waliteremshiwa adhabu kutoka kwa Allah swt  kwamba nyuso zao ziligeuka kuwa za wanyama na baada ya kupita siku tatu, Allah swt  aliwateremshia adhabuu kali kiasi kwamba wote kwa pamoja wakateketea.

 

MWISHO


 

MALAIKA : HARUT   NA   MARUT

 

Imepokelewa riwaya kutoka kwa Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa:

Baada ya kifo cha Mtume Sulayman bin Daud a.s., Ibilisi alitengeneza uchawi na kuuviringa na nyuma yake aliandika kuwa mzigo huu umetengenezwa na Asif bin Barkhiyyah kwa ajili ya ufalme wa Mtume Suleyman, na kwamba imetolewa kutoka hazina ya ilimu. Na kwa nguvu zake kila jambo linawezekana. Na baada ya hapo aliifukia chini ya kiti cha Mtume Sulayman a.s.  Na baadaye aliifukua chini ya kiti hicho na kuidhihirisha mbele ya watu wa zama hizo. Kwa kuyaona hayo, wale waliokuwa Makafiri walianza kusema kuwa Mtume Suleyman a.s. aliweza kuwatawala kwa uchawi lakini wale waliokuwa Mumin walikuwa wakisema kuwa Mtume Sulayman a.s. alikuwa ni Mtume wa Allah swt  na mwenye taqwa.  Allah swt  anatuambia kuwa ni Sheitani ndiye asemaye kuwa Mtume Suleyman a.s. alikuwa ni mchawi. Na jambo hilo ndilo walilolifuata na kuliamini Mayahudi.  Lakini Mtume Suleyman a.s. kamwe hakufanya tendo lolote la kukufuru au la ushirikina hivyo kamwe hawezi kuwa mchawi. Wale wanaohalalisha uchawi ni makafiri kwa sababu Masheitani walikuwa wakifanya uchawi na kuwafundisha watu uchawi na ushirikina.

 

Baada ya kupita zama za Mtune Nuh a.s., kulikuja zama moja ambamo wakazi wake walikuwa wakijishughulisha mno na mambo ya uchawi na ushirikina, kwa sababu ya kufuata imani hizo zilizopotofu, kulikuwa kukitendeka matendo maovu kabisa. Hivyo wakazi walikuwa wameupuuzia Uislamu, na kwa hayo Allah swt aliwatuma malaika wawili waliokuwa wakiitwa Harut na Marut, ambao walitumwa katika mji uitwao Babul, katika maumbile ya mwanadamu ili waweze kuwazuia wanadamu wasiendelee na uchawi na ushirikina uliokuwa umepindukia kiasi. 

 

Malaika hao walitii amri ya Allah swt  na walimwelezea Mtume wa zama hizo kuwa uwafundishe mambo fulani fulani wakazi wako ili waweze kujiepusha na uchawi na ushirikina huo uliokuwa umewapotosha kabisa.  Basi Mtume huyo aliwaambia watu wake kuwa wajifunze mafunzo hayo makhsusi ili waweze kujiepushe na uchawi na kamwe wasiwatendee chochote wenzao.  Allah swt  anatuambia kuwa katika mji huo wa Babul kulikuwapo na Mayahudi ambao wao kwa hakika walikuwa wakitenda kinyume na kile walichokuwa wakiambiwa na Mtume huyo,  yaani wao badala ya kuutokomeza uchawi, wao ndio wakawa waabudu wa uchawi na wakawa wakifanya uchawi.  Malaika wakawaambia sisi tunawafundisheni haya kwa ajili ya kutaka kuwajaribu na kuwajua wale waliona imani ya kurudi kwa Allah swt  na hivyo kujiepusha na uchawi. Na kutaka kuwatambua wale walioasi na kutumia ilimu hii kwa ajili ya kuwadhuru wengine. 

 

Hapo ndipo watu walikuwa wakijifunza uchawi za aina zote mbili yaani watu hao walikuwa wakijifunza uchawi uliokuwa umezuliwa na Shaytani kwa jina la Asif bin Barkhiyyah na ilimu waliofundishwa na Mtume Suleyman a.s. kwa ajili ya kujikinga na uchawi wa aina yoyote.  Wao walikuwa wakijifunza uchawi hata wa kuwatenganisha mume na mke wake na walikuwa wakiwapatia hasara kubwa sana watu. Kwa hakika sote tunaelewa kuwa Allah swt  kamwe hapendezewi na matendo kama haya na hivyo huwaadhibu wale wote wanaojishughulisha na matendo maovu kama haya ya Sihri. Katika Ayah hapa panazungumziwa neno idhn ingawaje kunamaanisha bila ya ruhusa ya Allah swt, lakini wanazuoni wanasema kuwa kuna maana nyingi na kwa neno idhn hapa kunamaanishwa ilimu yaani kujua, hivyo Allah swt  anayajua yote yanayotendeka. Iwapo sisi tutachukulia maana ya idhn kuwa ni idhini basi kumwua Mtume na kumdhulumu haki zake ni kwa idhini yake Allah swt. Na kwa hakika Allah swt si dhalimu na hivyo hawezi kamwe kuwafanyisha watu mambo yoyote yaliyo batili.

 

Na hapo anasema kuwa wao wanajifunza mambo ambayo yatawaletea hasara siku ya Qiyama na wala hawapati faida ndani mwake katika Dini na duniya. Kwa uhakika hao Mayahudi wana fahamu kuwa mtu yeyote aiachayo Dini ya Allah swt kwa badili ya kuchukulia uchawi, kwake hana faida ya aina yoyote huko Akhera na kamwe hawatapata uokovu kutokea adhabu za Jahannamu. Hivyo wao kwa makusudi wamejichukulia adhabu za Jahannam na kwa hayo wao kwa hakika wameziuza nafsi zao. Ni mambo maovu kabisa. Iwapo wao walitambua ubaya wa mambo hayo basi wao kamwe hawakufuata kiasi chochote walichokuwa wameelewa na hivyo watambue kuwa ni sawa na kutojua chochote.

 

Habari nyingine isemayo…

Wengi wanasema kuwa Harut na Marut ni Malaika waliokuwa wametumwa na Allah swt. Wao walikusanyika katika nyumba ya mwanamke mmoja na humo walikunywa pombe, wakaua na kuabudu miungu na kwa hayo wameadhibiwa adhabu ya kuning’inizwa katika kisima kimoja kilichokuwa kikijulikana kwa jina la Babul.

 

Kwa hakika masimulizi kama haya hayana uhakika wowote kwa masimulizi kama haya yanapotosha na ni yenye kuzuliwa kwani ni kinyume na akili zetu.  Kwa sababu Malaika ni viumbe wasio na wala hawatendi madhambi ya aina yoyote ile.

 

Katika ‘Uyunul Akhbar al-Ridha ni mashuhuri kuwa mtu mmoja alimwuliza Imam al-Ridha a.s. kuwa nimesikia kwamba dunia ilipojaa madhambi na maovu, basi Allah swt  aliwatuma Malaika Harut na Marut kama makhalifa na kuwatuma duniani. Vile vile inasemekana kuwa wao walifanya mapenzi pamoja na mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Zehra, na pia walikunywa pombe, wakaabudu miungu, wakaua na kuzini, walizini. Ewe Mjukuu wa Mtume s.a.w.w., unasemaje kuhusu habari hizi ?

 

Malaika hawakufuru…

Kwa kuyasikia hayo, Imam a.s. alijibu Madhallah!  Si hivyo kwani Malaika ni viumbe visivyo na makosa na wapo mbali na kufuru na maovu. Imam a.s. aliwathibitishia hao kuwa Malaika ni viumbe visivyo na kasoro zozote kwa Ayah za Qur’an na kuwaambia kuwa nyinyi ni lazima muamini kuwa Allah swt aliwatuma hao Malaika katika maumbile ya mwanadamu ili waweze kuwaonya na kuwaonyesha wanaadamu kuhusu uchawi uliokuwa ukiendelea katika zama zao.  Kwa kifupi Malaika hawatendi makosa ya aina yoyote.

 

Kwa hayo watu waliuliza,

“Ewe Imam wetu ! Iwapo Malaika hawatendi makosa, sasa je Ibilisi Sheitani hakuwa Malaika?” 

 

Basi Imam a.s. aliwajibu kuwa

“Yeye alikuwa ni Jinn na hayo yamesemwa katika Qur’an Tukufu”.

 

Nasiha: 

Inatubidi sisi tuisome Qur’an tukufu na kuielewa maana ya Ayah zilizomo na kujaribu kujifunza kutokana na kusoma kwetu ili tuweze kuishi vile Allah swt atutakavyo na tujiepushe pamoja na maovu ambayo ndiyo sababu kuu za maangamizo na mateketezo yetu. Vile vile tuwe na tahadhari ya masimulizi na maelezo ya mufassirina wengine ambao wanaweza kutupotosha kwani maelezo yao yanapingana pamoja na Ayah za Qur’an Tukufu pamoja na masimulizi tuliyoyapata kutoka kwa Mtume s.a.w.w. pamoja na Aimma Toharifu a.s.

 

MWISHO


YAJUJ  NA  MAJUJ

 

Allah swt  anasema katika Quran, Sura Al-Kahf, 18, Ayah 92 - 99.

Kisha akaifuata njia.

Hata alipofika katikati ya milima miwili,alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).

Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je,tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”

Akasema:“Yale ambayo Allah swt  wangu amenimakinishia ni bora  (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”

Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.”

Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.

Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Allah swt  wangu.Na itakapofika ahadi ya Allah swt  wangu ya kufika Qayama), atauvunjavunja. Na ahadi ya Allah swt  wangu ni kweli tu.”

 

Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vyenye miguu minne na wakifanana na wanaadamu kisura na wao walikuwa ni wafupi mno mbele ya watu wa zama hizo. Na watoto wao walikuwa wakizaliwa kama watoto wa wanaadamu na walikuwa hawakui zaidi ya shubiri tano na sura zao zilikuwa aina moja na walikuwa wazururaji.Kwa kuwa ngozi zao zilikuwa ngumu kama zile za ngamia, hivyo hawakuathirika kwa baridi wala joto. Walikuwa na makucha makubwa na meno makali na masikio yao yalikuwa marefu kiasi kwamba walikuwa wakitandika moja na kujifunika kwa la pili. Walikuwa wakiingiliana kama wanyama na chakula chao kikubwa kilikuwa ni samaki kwa sababu kulikuwa kukinyesha mvua za samaki, na kama kulikuwa na kasoro ya samaki basi walikuwa wakishambulia miji na kuchafua na kuvuruga kila kitu kiasi kwamba watu walipokuwa wakizisikia sauti zao,walikuwa wakikimbia na kuacha makazi yao kwa sababu ilikuwa ni vigumu mno kuwakabili kwani walipokuwa wakiingia mijini basi miji yote ilikuwa ikijaa wao tu. Idadi yao ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ajuaye isipokuwa Allah swt . Wao walikuwa hawafi hadi wamezaa watoto zaidi ya elfu moja.

 

Katika vitabu tunapata habari zaidi kuwa Yajuj na Majuj ni makabila mawili yaliyokuwa makubwa kutokana na kizazi cha Yafus, mwana wa Mtume Nuh a.s.. Na katika Agano la Kale, Majuj anaelezwa kuwa ni Chifu wa Mashech na Tunal. Kwa sasa Moscow ndio mto unaosimama mji huo,uitwao Moscow, mji mkuu wa Urusi; Tabul ni mto huko Urusi ambapo kuna mji Tobolsk.

 

Katika eneo la Ulaya ya Kusini na Urusi ya Kiasia,baina ya Wacarpathiani na Don, kulikaliwa katika enzi za zamani na kabila katili kabisa ambao waliiteka Asia ya Magharibi kuanzia karne ya 7 Kabla ya Kristo hadi mwanzoni mwa kipindi cha Kikristo, wakati mashambulizi yao yalipokwisha kwa sababu ya Bwana Dhulqarnain alipoujenga  huo  ukuta.

 

Vile vile inasemekana kuwa neno  Mongol  ni mvurugano wa neno la Kichina Mongog  au  Manchog Iwapo utafiti huu utakuwa wa kweli,hivyo. Hivyo itamaanisha kuwa eneo la Yajuj na Majuj inaanzia Mto wa Moscow hadi Turkistan ya Kichina na Mangolia.

 

Maelezo ya ‘kuta’ katika Quran Tukufu yanaonyesha kuwa lazima iwe imejengwa pale penye njia ili kuzuia makabila hayo ya wachochezi na wakatili kuwashambulia majirani wao waliokuwa mafundi stadi katika kazi za kufua vyuma na walikuwa matajiri.

Sheikh Abul-Kalam Azad,katika moja ya makala yake (katika Jannatul-Ma’arif) anaelezea kuwa kuta hizo zimeendelea hadi Uturuki.

 

Ayatullah Agha Haji Mirza Mahdi  Puya Yazdi (katika hashia ya Tafsiri ya Quran iliyofanywa na S.V. Mir Ahmad Ali) anawanakili wengine wakisema kuwa kuta hizo zipo baina ya milima ya Armenia na Azerbaijan.

 

Hata hivyo kuna tofauti ya maoni kuhusu utambulisho wa Dhulqarnain. Bwana ‘Abdullah Yusuf Ali anadhani kuwa jina hilo linaelezea kuwa ni Alexandar Mkuu wa Misri.

 

Wengineo,kama Agha Puya, wanafikiri kuwa huyo anatambulishwa kama ni Mfalme wa Kiajemi aliyekuwa akiitwa Darius.

 

Kwetu sisi hatumaanishi kuingia katika mazungumzo mengi kuhusu mjadala huu lakini inatubidi liwe jambo lililowazi mbele yetu kuwa kwa mujibu wa Quran Tukufu, Dhulqarnain alikuwa ni mcha Mungu hivyo kamwe haiwezekani kumtambulisha Dhulqarnain kama kafiri  au  mpagani.

 

Kwa mujibu wa Quran Tukufu,Itakapokaribia Siku ya Qayama, kabila hizi zitafanikiwa kuvunja kuta, yaani zitaenea zaidi kuliko mipaka yao ya awali.Upanuzi huo unaweza kuwa kimantiki;ambapo inaweza kumaanisha kuwa itikadi zao (ukomunisti na ukafiri) zinaweza kuenezwa nje ya mipaka ya nchi zao. Au itakuwa aina ya kikoloni yaani kukalia maeneo ya mashariki ya Ulaya,Asia ya Kusini na maeneo mengineyo. Au inaweza kumaanisha yote.

 

Imeandikwa katika Tafsir Majma’-ul-Bayan kuwa baada ya kuteka maeneo ya ardhi watajararibu kuiteka mbingu.“Hivyo watatupa mishale yao kuelekea angani,na itawarejea zikiwa na alama kama za damu. Hivyo watasema:‘Sisi tumekwishawateka wakazi wa dunia na tumewateka wakazi wa angani.”

 

Ni dhahiri kuwa  mishale  inamaanisha maroketi na vyombo vya angani. Maneno itawarejea zikiwa na alama kama za damu inamaanisha kuwa vyombo vya angani vitafikia malengo yao na kurejea duniani.

 

Kwa mujibu wa Tafsiri hiyo,“wakati watakapokuwa na takabari kubwa kwa sababu ya kushinda anga za juu, Allah swt  atawaumba funza au minyoo ambayo itawaingia masikio yao, na kuwaua wote.Inamaanisha kuwa hatima yao itakuwa kwa kuangamizwa kwa maafa makhsusi, au kwa magonjwa ya kuambukizwa yatakayotokana na vijidudu.

 

 

 

MWISHO


PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD

 

Je Shaddad ni nani …

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokwenda katika Mi’raj alikutana na Malakul Mauti. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza :

“Je ni wakatigani ambapo wewe kwa hakika ulisikitika katika kutoa roho ya wanaadamu ?”

 

Kwa hayo Malakul Maut akajibu :

“Ewe Mtume wa Allah swt !

Zipo nyakati mbili tu ambapo mimi kwa hakika nilisikitika mno wakati wa kutoa Roho nazo ni, kwanza kulikuwa na jahazi moja iliyokuwa baharini ikiwa na wasafiri walikuwamo humo, na Allah swt aliniamrisha kuipindua jahazi hiyo na kuzitoa roho zote za wasafiri waliokuwamo isipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa ana mimba. Nami nikafanya hivyo hivyo nilivyoamrishwa.

 

Mwanamke huyo aliweza kuelea kwa msaada wa ubao alioupata wakati wa kuzama. Wakati mwanamke huyo anaelea, alimzaa mtoto, ndiye aliyeitwa Shaddad.  Alipomzaa mtoto huyo, mama huyo akafa( hapa niliposikitika wakati wa kuitoa roho ya mama huyu) na mtoto akabakia peke yake majini juu ya ubao, ambapo kwa amri za Allah swt aliweza kufika salama u salimini hadi nchi kavu (kisiwa kilichokuwapo karibu).Hapo Allah swt alimwamrisha Swala mmoja kumnyonyehsa maziwa mtoto huyo kwa muda usipungua miaka miwili.

 

Ulifika wakati ambapo kulitokezea wasafiri kisiwani hapo na walipomwona mtoto huyo na alivyokuwa mzuri, walishauriana kumpelekea mfalme kwani alikuwa hana mtoto. Na walifanya hivyo, na Mfalme alimpenda mtoto huyo na kumchukua kama mtoto wake …..

 

Mtume Adam a.s. tangu aje duniani humu ilipofika miaka 2647 ndipo Mtume Hud a.s. alipozaliwa na kulipofika miaka 2700 ndipo Shaddad bin ‘Aad alipokuwa Mfalme na ni Mfalme huyu ambaye ametengeneza mfano wa Jannat (Peponi) yenye bustani za kupendeza humu duniani.  Humu yeye alijenga majumba ya kuvutia na kupendeza, na aliweka wajakazi warembo:wasichana kwa wavulana kutoka sehemu mbalimbali humu duniani ambao kwa hakika waliifanya pepo yake ipendeze na kuvutia.

 

Je kuna mtu aliyebahatika kuiona Pepo hiyo?

Katika zama za Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. kuna mtu mmoja aitwaye ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ndiye aliyebahatika kuiona. Na hapa tunaelezea vile inavyopatikana katika vitabu vya historia.

 

Wasemavyo wanahistoria

“Katika Bara la Uarabuni kulikuwa na Shakhsiyyah moja aliyekuwa akiitwa ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ambaye alikuwa na Ngamia wake aliyekuwa ametoroka na kupotelea katika majangwa ya ‘Aden na katika kumtafuta huyo ngamia wake alifika katika majangwa ambapo aliuona mji mmoja ukivutia. Mji huo ulikuwa umezungukwa na ngome. Ndani ya mji huo kulikuwa na majumba ya kupendeza na yenye kuvutia sana. Na juu ya kila jengo kulikuwa  na bendera zilizokuwa zikipepea. Yeye anasema kuwa alifanikiwa kuingia ndani ya mji huo.

 

‘Bwana ‘Abdullah anaelezea alivyiona pepo ya Sahaddad

“Mimi niliteremka chini kutokea ngamia wangu na nikamfunga katika nguzo mojawapo. Nikauchukua upanga wangu nikawa ndani ya ngome hiyo. Milango yake ilikuwa ni madhubuti na ya kupendeza sana kiasi kwamba kamwe nilikuwa sijawahi kuona kabla ya hapo. Milango ilikuwa imetengenezwa kwa ubao mzuri sana na manukato mazuri sana na ufundi uliotumika ulikuwa ni wa utalaamu wa hali ya juu sana na juu ya mbao zake kulikuwa kumepachikwa Yaqut za rangi mbalimbali. Ukiangalia chumba kimoja utakisahau chumba cha pili katika ngome hiyo. Madirisha yake yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu na shaba, ukiona milango , kuta  na sakafu yake ilivyokuwa iking’ara na kwa hakika kila kitu humo utakachokiona utastaajabika mno.”

 

‘Bwana ‘Abdullah alipoyaangalia majengo hayo yaliyokuwa mazuri na yenye kuvutia alishangazwa kuona kuwa hapakuwapo na mtu yeyote, na alijaribu kusonga mbele akaona miti ambayo imejaa maua ikiwa inapeperushwa na upepo mzuri sana. Na chini mwake kulikuwa na mito iliyokuwa ikitiririsha maji.

 

Kwa hakika hii ndiyo ile Jannat ambayo Allah swt ametupa habari zake. Basi mimi kwa hayo nilimshukuru Allah swt  kwa kunijaalia bahati hiyo. Mimi niliokota vipande vidogo vidogo vyenye harufu nzuri mno ya Mishk na Ambar. Na hapo nikawaza kuwa sasa itabidi nitoke zangu nje kwa haraka. Nilipofika katika mji wa Yemen huko niliwasimulia watu kuhusu Jannat hii. Kwa hakika nilishangazwa kuona kuwa habari zangu hizi zilienea kila mahali kama upepo.

 

Mu’awiya alimtuma mjumbe kwenda kwa Hakim San’aan ili kumwita ‘Bwana ‘Abdullah na kutaka kujua kwa undani zaidi kuhusu swala hili. Huyo ‘Bwana ‘Abdullah alielezea yote yale kwa uhakika vile alivyokua ameyaona. Na hapo Mu’awiya alimwita Ka’bul Ahbar na kumuuliza

“Je yanayozungumzwa na ‘Bwana ‘Abdullah yanapatikana katika vitabu vya historia vyovyote vile unavyovijua wewe ?  Je kuna mji wowote humu duniani ambao umetengenezwa na kurembeshwa kwa fedha  Ambamo kuna aina mbalimbali za miti na mimea zinazoota ? Na ardhi ambayo inanukia kwa manukato mazuri sana, na badala ya mchanga kumetandazwa vito mbalimbali vya thamani ?”

 

Ka’bul akamjibu kuwa mji huu kama ulivyo wa Jannat umetengenezwa na mtoto wa ‘Aad aliyekuwa akiitwa Shaddad kama vile ambavyo Allah swt  anaizungumzia ka tika Qur'an Tukufu.: Sura Al-Fajr, 89, ayah 6-8.

Kwani hakuona jinsi Allah swt  Mlezi alivyo wafanya kina A’adi ?

Wa Iram, wenye majumba marefu ?

 

Kwa kuyasikia hayo yote Mu’awiya alimwambia Ka’bul kuwa

“Mimi ninataka habari kamili za kihistoria kuhusu watu wa Makabila hayo ya ‘Aad.

 

Ka’bul alimwambia

“Kabla ya ‘Aad kulikuwapo na ‘Aad mmoja katika Kabila la Mtume Hud a.s.  Naye alikuwa ana watoto wawili. Mmoja alikuwa akiitwa Shadiid na mwingine akiitwa Shaddad na baada ya ‘Aad kufa basi watoto wote wawili wakawa Wafalme ambao walikuwa wanatawala dunia nzima na hivyo watu wa mashariki hadi magharibi kwa kila upande walikuwa wakiwafuata kama ndio watawala wao. Na Shadiid pia baada ya muda si mwingi alikufa, na hivyo akabakia Shaddad ambaye akawa ndiye mfalme pekee wa dunia nzima.

 

Shaddad alikuwa na tabia ya kusoma sana na alikuwa amesoma mambo mengi sana na katika kusoma kwake huku mara nyingi alikuwa akisoma kuhusu habari na sifa na mandhari za Jannat ambayo Allah swt  ameitengeneza kwa ajili ya muumin na waja wake wema.

 

Shaddad naye pia akasema kuwa yeye angeweza kutengeneza Jannat kama vile alivyoitengeneza Allah swt . Na azma yake hiyo alitaka kuitekeleza haraka iwezekanavyo.

 

Mtume aliyekuwapo wakati wa zama zake alipokuwa akifanya kazi ya Tabligh, Shaddad alikuwa akimwuliza ‘je kwa kuwa mja mwema Allah swt  atakulipa nini ?’ Basi Mtume wa zama zake hizo alimjibu kuwa, ‘Allah swt  atakulipa Jannat.’

 

Na kwa hayo Shaddad aliuliza ‘Je Jannat ni nini na humo kuna nini.’ Huyo Mtume aliyekuwepo katika zama za Shaddad alimjibu na kumwelezea ‘mazuri yote yalivyokuwa katika Jannat ya Allah swt .’

 

Shaddad kwa kuyasikia hayo alimwambia Mtume huyo kuwa yeye pia alikuwa na uwezo kamili wa kuweza kutengeneza Jannat kama hiyo na hapo ndipo alipojitangaza kuwa yeye ni mungu.  Hivyo watu wote wamwabudu yeye. Ili kutaka kutimiza azma yake hiyo yeye aliwakusanya wataalamu mia moja wa fani mbalimbali na kila mmoja wao aliwapa watu elfu moja wafanye kazi nao haraka iwezekanavyo kwa kutafuta kwanza kabisa mahali yeye anapotaka kujenga mji mmoja wa kiajabu kabisa ambao haujawahi kutokea. Mji ambao utakuwa na majumba ya kushangaza na kuvutia mno ambayo yatakuwa yamejengwa kwa dhahabu na fedha na watandaze Yaqut na lulu na almasi chini na kuwe na manukato ya kila aina yaliyo bora kabisa kiasi kwamba hata hewa inapovuma inavuma iwe ya manukato. Mtengeneze mito inayotiririka maji humo vizuri.

 

 Kwa kuyasikia hayo hao walistushwa kwa maagizo hayo na wakamwuliza Shaddad : ‘Ewe Mfalme wetu! Je kiasi chote hiki cha dhahabu, fedha, almasi na lulu tutatoa wapi ?’

 

Kwa kuyasikia hayo Mfalme mwenye kiburi alianza kupiga makelele kama inavyo unguruma radi na akasema :

‘Je dunia nzima haipo mikononi mwangu ? Machimbo yote ya ulimwenguni ya fedha na dhahabu na vito vingine vya thamani vyote vichukuliwe mikononi mwetu na si hayo tu bali raia wote wanyang’anywe fedha na dhahabu na vito vya thamani walivyonavyo na ujenzi wa mji huu wa ajabu kabisa uanze mara moja bila ya uchelewesho wa aina yoyote ile. Muwaandikieni barua magavana mia nne kuwa wao nao washiriki nami katika kutekeleza swala hili.”

 

Kwa kutokana na amri hii au mwito huu uliotolewa na Shaddad Magavana wote walimwitikia na kushirikiana naye katika kulitimiza azma aliyokuwa anayo yeye.

 

Kwa hivyo wafanya kazi wote walikuwa wakifanya kazi ngumu sana kwa usiku na mchana na hatimaye baada ya miaka mia tatu kupita (wengine wanasema miaka mia moja) mji huu wa ajabu na wa aina yake ulikuwa tayari. Shaddad aliwatafuta wasichana na wavulana warembo kabisa kutoka sehemu mbalimbali za duniani kuja kubakia katika Jannat hiyo ambayo yeye aliipa jina la babu yake Iram na humo aliwaleta matajiri kabisa waje kuishi humo.

 

Shaddad alitoa amri kuwa raia wote wajiandae kwa ajili ya sherehe kubwa ambayo ataitangaza kuhusiana na kuwa tayari kwa Jannat yake hiyo. Inasemekana kuwa kulichukua muda wa miaka kumi kufanya matayarisho ya kwenda katika Jannat yake hiyo. Shaddad pamoja na jeshi lake na watu wengi mno kupita kiasi waliandamana kwenda katika Jannat hiyo.

 

Wakati anaendelea na safari yake ya kwenda katika Jannat yake hiyo, kulipobakia safari ya kama masaa ishirini na manne alisikia sauti moja ambayo ilimtia hofu mno na alipoinua macho yake akaona uso wenye kuchukiza na kutisha mno. Na hakusita kuuliza,

 “Je ni nani wewe ?”

 

Akajibiwa kuwa

“Mimi ni Malakul Mauti yaani mimi ni yule malaika ambaye natoa roho za watu humu duniani. Na mimi nimetumwa na Allah swt  kuja kuitoa roho yako.”

 

 Shaddad alimwambia :

“Ninaomba unipe muhula kiasi cha kwamba mimi niweze kwenda kuangalia Jannat na mabustani niliyoyatengeneza !!!”

 

Malaika huyo mtoa roho akamwambia kuwa

“Wewe hauna ruhusa hiyo.”

 

Na imepatikana katika riwaya kwamba mguu wake mmoja ulikuwa ndani ya Jannat na mguu wa pili ulikuwa nje ndipo hapo roho yake ilipotolewa na pepo hiyo na mabustani yake ikapotea katika macho ya watu. Na watu waliokuwamo humo wote wakateketea kwa pamoja.

 

Kwa kusema hayo Ka’bul Ahbar akasema kuwa katika zama hizi kutatokezea mtu mmoja ambaye atakuwa ametoka kwenda kumtafuta ngamia wake huko porini na atabahatika kuangalia mabustani haya. Mtu huyo uso wake na nywele zake zitakuwa za rangi nyekundu, atakuwa ni mtu mfupi, na upande wa shingo utakuwa na madoa mawili meusi.

 

Wakati mazungumzo haya yalipokuwa yakifanyika

 

Bwana ‘Abdullah Kalaba alikuwa ameketi hapo. Na wakati Ka’bul anazungumza alimwona huyo mtu na mara kwa ghafla akasema kwa sauti ya juu:

 “Bwana ‘Abdullah mwenyewe aliyeiona Jannat ya Shaddad ndiye huyo aliyeketi hapo.”

MWISHO.


 

WATU WA TEMBO ( As-Hab-i-Fiil )

 

Allah swt  anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Al Fiil, 105, Ayah ya 1-5 :

Kwani hukuona jinsi Allah swt, Mlezi wako alivyo watendEa wale wenye tembo ?

Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika ?

Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,

Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,

Akawafanya kama majani yaliyoliwa !

 

Najjashi (Negus), alikuwa ni Mfalme wa Abisynnia ambaye alijichukulia jukumu la kueneza Ukristo na alifanya kila jitihada alizoziweza ili aweze kuirudisha vile ilivyo kuwa miongoni mwa watu wake na ikafuatwa na wingi wa raia zake.

 

Alipopata habari kuwa watu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwenguni walikuwa wakienda Makka kuhiji huko Al Ka’abah Tukufu, basi naye aliamua kuvumbua jambo ambalo litawavutia watu kutokwenda Makkah kuizuru Al Ka’abah Tukufu na badala yake waende nchini mwake.

 

Hivyo, basi yeye alijenga Kanisa moja kubwa katika Sana’, mji uliopo Yemen na kuipamba vizuri kwa kila kitu cha kuvutia zikiwemo mazulia, mapazia n.k. Kwa hakika lilikuwa ni jambo la kuvutia sana kwa mtu yeyote aliye angalia kwa kuona ufundi wa kistadi uliotumika katika ujenzi wake. Najjashi alifikiria kuwa baada ya kuona maajabu ya ujenzi huo wa Kanisa watu hawatakwenda tena Makkah kuzuru Al-Ka’abah Tukufu na badala yake watakwenda Sana’ kuzuru hilo Kanisa, na vile vile watu wa Makkah pia watakuja kuhiji hapo Sana’, Yemen. Pamoja na hayo yote watu wa Makkah hawakujali chochote. Vile vile sio kwamba ni watu wa Yemen na Abisynnia tu walioisahau Makkah, laa, wao kama kawaida yao waliendelea na safari zao za kwenda mji mtukufu wa Makkah na kuzuru Al Ka’abah Tukufu.

 

Kwa kuona haya kulimwia jambo la kusikitisha na likawa ndilo tatizo kubwa kwake. Na kwa hakika likawa ni jambo gumu kabisa kuwalazimsha watu wenye imani zao kwenda kinyume na imani na itikadi zao.

 

Ikatokezea kwamba kukawa na msafara wa wafanya biashara kutoka Makkah waliofika Sana’. Wao wote wakawa ni Waarabu na wakawa wamekuja huko katika safari ya kibiashara. Baadhi yao walipumzika hapo Kanisani usiku katika safari yao na usiku huo ulikuwa ni wa baridi na ili kutaka kupata ujoto kidogo wao walikoka moto ili kupunguza ubaridi uliokuwa humo chumbani na kwa bahati mbaya wakati wa kuondoka wao walisahau kuuzima huo moto, na ikatokezea kwamba Kanisa hilo likashika moto na likachomwa na kuwaka moto. Najjashi alipopata habari kuwa Kanisa hilo limechomwa moto, hakusita kufikiria kuwa Waarabu wale waliokuwapo usiku huo ndio walioichoma moto kwa makusudi. Na katika ghadhabu hii yeye aliamua kwenda kuiteketeza na kuibomoa Al Ka’abah Tukufu huko Makka.

 

Ili kutimiza azma yake hii, yeye alimtuma Kamanda Amir Jeshi wake Abraha kutangulia Makka pamoja na jeshi moja kubwa wenye farasi, waliopanda tembo na vikosi mbalimbali.

 

Abraha alielekea Makka akiwa pamoja na jeshi lenye nguvu sana na wakiwa njiani, miji yote walipopita waliiteketeza na kuiharibu na walikuwa wakishika wanyama waliokumbana nao humo njiani. Katika jangwa la Arabia yeye alikutana na mtu mmoja mwenye ngamia wasio pungua mia mbili. Ngamia hao walikuwa ni mali ya Bwana ‘Abdul Muttalib. Abraha aliwachukuwa hao ngamia wa Bwana ‘Abdul Muttalib. Yeye aliendelea kuelekea Makkah. Alipoukaribia mji wa Makka alipiga kambi katika vitongoji vya kukaribia Makka. Abraha alikuwa amekaa katika kiti chake na maaskari walikuwa wakimlinda. Punde akaja askari na kusema,

“Ewe Mheshimiwa ! Mheshimiwa wa Makka na Chifu wa kabila la Quraishi, ambaye jina lake ni Bwana ‘Abdul Muttalib, yuko nje ya kambi yetu na anataka kuonana nawe.”

 

Abraha alimwambia askari wake amruhusu Bwana ‘Abdul Muttalib aje mbele yake. Na punde si punde Bwana ‘Abdul Muttalib aliingia ndani ya hema lake. Heshima pamoja utukufu na nuru yalikuwa yakionyesha usoni mwa Bwana Bwana ‘Abdul Muttalib.

 

Abraha alipo mwona tu Bwana Bwana ‘Abdul Muttalib, aliinuka na kutoa heshima na kumwambia akae karibu naye. Na kwa kupitia Mkalimani Abraha alimwuliza sababu ya Bwana ‘Abdul Muttalib kutaka kumwona yeye.

 

Bwana ‘Abdul Muttalib alijibu,

“Mimi nimepata habari kuwa majeshi yako wamewachukua ngamia zangu. Na nimekuja hapa kukuomba unirudishie ngamia zangu hizo.”

 

Abraha akasema :

“Jambo gani hili la kushangaza ? Mimi nimekuja hapa kuiteketeza na kuiharibu kabisa Al Ka’abah na kuuondoa kabisa utukufu wake. Lakini mtu huyu naona hayajali hayo na badala yake naona anawajali ngamia zake. Lau kama Bwana ‘Abdul Muttalib angekuja kuniomba mimi nisiivunje na kubomoa Al Ka'abah Tukufu, basi kwa hakika kwa heshima zote nisingebomoa na badala yake ningerudi bila kutenda vurugu yoyote.”

 

Kwa kumjibu Abraha, Bwana ‘Abdul Muttalib alijibu,

“Mimi ni mmiliki wa ngamia zangu na hiyo Nyumba Tukufu (Al Ka'abah Tukufu) inayo mmiliki wake, vile vile. Mimi inanibidi nijali mali yangu na mwenye Nyumba hiyo Tukufu atajua mwenyewe namna ya kuiokoa na kuinusuru.”

 

Abraha kwa kusikia hayo alishangazwa mno na alitoa amri kuwa ngamia wa Bwana ‘Abdul Muttalib zirejeshwe kwake. Na baadae aliendelea na safari yake ya azma yake ya kuibomoa na kuiteketeza Al Ka'abah Tukufu.

 

Jeshi zima kuteketezwa

Alikuwa bado hajafika mbali katika kuukaribia Makka mara akakuta kundi kubwa la ndege wadogo wadogo waliokuwa wameitwa Ababil walionekana katika anga za Makkah na wakakuta wote wapo wanaruka juu ya vichwa vya majeshi ya Abraha. Kwa hakika ndege hawa walikuwa ni kama ndege za kivita kwani wao walikuwa wanavyo vijiwe vidogo vidogo mdomoni mwao na walikuwa wakiyadondosha juu ya vichwa vya wanajeshi hao wa Abraha. Na kila jiwe lililodondoshwa juu ya kichwa cha mwanajeshi kiligonga kichwa na kukipasua na wakawa wanajeshi hao wanaanguka juu ya ardhi na kufa papo hapo.

 

Mmoja aponea chupuchupu

Katika muda mchache kabisa wanajeshi wote wa Abraha waliuawa na ndege hao isipokuwa mmoja tu ambaye alinusurika na akakimbia hadi Abisynnia kwenda kuripoti hali hii ya maajabu yaliyotokea, kwa mfalme Najjashi. Baada ya kufika hapo alielezea habari zote za jeshi kubwa la Abraha lilivyoangamizwa na kuteketezwa na viumbe vidogo kabisa visivyo na nguvu ya aina yoyote. Najjashi alimwomba huyo mtu ampe habari zaidi kuhusu aina ya ndege aliokuwa amewaona yeye. Na ikatokezea kwamba ndege mmoja kama hao waliokuwa huko Makka alitokezea mbele yao na mtu huyo alimwelezea Najjashi kwa kumnyooshea ndege huyo kidole akisema :

“Ewe Mtukufu ! Huyu ndege ni hatari kabisa kwani hawa ndio wameweza kuliteketeza jeshi lote zima la maaskari.”

 

Punde alipomaliza tu kuyazungumza hayo na kutoa taarifa kamili ndege huyo alimpiga na kijiwe kidogo kutoka mdomo wake, jiwe ambalo likaenda kumpiga kichwani na hatima yake akafa papo hapo mbele ya Najjashi.

 

Tukio hili limetokea katika mwaka huo huo ambao Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. aliokuwa amezaliwa Makka.

 

 

MWISHO.


 

WATU WA PANGONI (Kahf).

 

Allah swt  anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Al Kahf, 18, ayah 9-14:

Bali unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu ?

Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Allah swt  wetu Mlezi ! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengenezee uwongofu katika jambo letu.

Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa.

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa.

Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio mwamini Allah swt  wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu.

Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Allah swt  wetu Mlezi ni Allah swt  Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

 

Daquis kujitangaza kuwa u mungu…

Katika ardhi ya Roma kulitawala Mfalme aliyekuwa mwadilifu kwa watu wake na ambaye alikuwa mkarimu pia. Yeye alitawala kwa kipindi kirefu cha kutosha na raia wake waliishi katika amani na hali nzuri.

 

Wakati Mfalme huyu alipokufa kulizuka tofauti miongoni mwa raia wake na ndicho kilichokuwa sababu ya kuleta maangamizo yao wenyewe. Mfalme wa nchi ya jirani, aliyekuwa akiitwa Daquis aliivamia nchi yao na kuimega katika ufalme wake.

 

Daquis alijenga ngome imara kwa ajili yake mwenyewe na aliipamba kwa kila kitu alichoweza kuipamba. Yeye aliwachagua watu sita wenye busara na waliokuwa na uwezo kutokana na watu wa ardhi zile alizoziteka na kuwafanya Mawaziri. Na baadae yeye aliwalazimisha watu kumwabudu yeye kama ndiye mungu. Majahili na wapumbavu miongoni mwa watu hao walimkubalia yeye kama ndiye mungu wao na walianza kumwabudu kwa kujitupa chini na kumwangukia sujuda.

 

Sherehe na habari za kuvamiwa

Kulipita muda na kuliwadia siku ya kusherehekea sherehe yao ya maadhimisho. Katika sherehe hizi Mfalme pamoja na baraza lake na raia wote walishirikiana kwa mbwembwe na shangwe kubwa. Wakati hawa wote wanasherehekea sherehe hizi, kulikuja na mleta habari na alimpa ujumbe Mfalme. Pale aliposoma habari hizo, rangi ya uso wake ulibadilika kwa sababu ya maafa yaliyokuwa yakitaka kumpata yeye pamoja na ufalme wake. Katika ujumbe huo kulikuwa kumeandikwa kuwa majeshi ya Mfalme wa Uajemi alikuwa tayari ameishaingia katika mipaka ya Roma na walikuwa wakisonga mbele kuukaribia mji mkuu wake. Kwa kuona taabu na shida hiyo katika uso wa Mfalme, iliyotokana na kusoma habari za kuvamiwa na uvamizi kutoka nje, mmoja wa Mawaziri wake sita wa Mfalme huyo aliweza kuvumbua na kujua kutokana na sura ya Mfalme huyo na alipoangalia nyuso za wenzake watano kwa kutaka kufanya utafiti, nao pia walionyesha dalili hizo. Kwa hayo tu wao waliweza kubashiri kuwa jambo fulani kubwa la kihistoria liko litatokezea.

 

Baada ya sherehe kumalizika kila mmoja aliondoka kwenda nyumbani kwake na Mawaziri pia waliondoka kurudi majumbani kwao ambapo wao walizoea kuitisha vikao vyao. Wakati wote walipokuwa wamesha keti pamoja, wao walizungumzia kile walichopeana habari kwa kutazamana nyuso. 

 

Vuguvugu la uasi na kutoroka kwa mawaziri sita

Mmoja wao akasema,

“Je mliona uso wa kiajabu wa Mfalme ! Yeye anadai kuwa yeye mwenyewe ndiye mungu wa watu ambapo yeye anawachukulia kama ni watumwa wake. Lau kama angekuwa kweli ni mungu wa watu, basi kamwe asingekuwa ni mtu ambaye ameshtushwa kwa kupata habari zisizo mfurahisha. Hali hii ya yeye kutoweza kujisaidia imetupa sisi kiasi cha kutosha cha kufikiria, na kwa hakika imetufungua macho vya kutosha kushuku kuwa kwake mungu wa malimwengu zote.

 

Je ni nani muumbaji?

Enyi wenzangu ! Mimi kwa hakika ninatilia maanani sana na kuliwazia jambo muhimu sana. Je nani aliyejenga ulimwengu huu ni nani aliyezipachika hizi nyota ndani yake na kwa hukumu ya nani nyota na mwezi vinazunguka katika mizunguko yake ?  Kwa nini niende mbali hadi kuzungumzia jua na mwezi ? Kwa nini nisijifikirie mimi mwenyewe ? Kwa nini nisifikirie ni nani ambaye amenileta mimi hapa nilipo akanitia katika tumbo la mama yangu, ambaye amenilea na amenipa mimi kila kitu cha kuweza kuishi na hizi nguvu nilizonazo za kimwili ?

 

Mimi kwa hakika sasa nimekuwa na imani kuwa mambo yote haya yanafanywa na Allah swt  ambaye ni Allah swt  wa Malimwengu yote na kamwe huyu hawezi kuwa mwenye Taqwa. Yeye ni mwerevu sana na wala hawezi kuzuzuliwa na kiumbe kidogo kama yeye.

 

Enyi marafiki zangu ! Maisha yetu yamekuwa ya kufedhehesha kwa kubakia kama watumwa wa Daquis na jambo hili haliwezi kuwa la kudumu milele. Lazima sisi tujitoe nje ya mambo ya dunia na starehe na raha ambazo zinatupeleka mbali zinatutoa mbali na ibada halisi ya Allah swt  na lazima tumuombe Allah swt  atusamehe kwa madhambi yetu yote.”

 

Athari za hotuba …

Mtu huyo mwenye hekima alizungumza mambo haya kwa hali ya kusisitiza kiasi kwamba wenzake waliathirika sana na wote sita kwa pamoja waliamua kutoroka njia ya wenye kuabudu masanamu na wakaamua kwenda kuishi porini na jangwani huko katika maisha ya kujitenga kwa ajili ya ibada tupu na kumwabudu Allah swt .

 

Kutoroka kwao . . .

Siku iliyofuatia hawa sita kwa pamoja walitoa majumbani mwao kisirisiri na wakaelekea jangwani. Walipofika maili fulani kutoka majumbani kwao, wao walimwaona mchungaji mmoja akichunga kondoo zake. Wao walimwomba maji kwa ajili ya kunywa. Na mchungaji aliwaambia,

“Mimi ninahisi kwenu nyie hewa ya utukufu na ucha Mungu. Je ni nani nyie na mnakwenda wapi ?”

 

Wao walijibu,

“Sisi tuko sita ni Mawaziri wa Mfalme, lakini tumekana nyadhifa zetu tulizopewa na mamlaka yake. Sisi tunajitenga na tunajitolea maisha kwa ajili ya ‘ibada ya Allah swt , Allah swt  wa malimwengu yote kwa sababu kumwabudu Daquis ndiko kuliko tumaliza sisi kiroho na hakika nafsi zetu tunahisi vibaya mno.”

 

Mchungaji awa mtu wa saba…

Kwa hayo mchungaji akasema,

“Nami pia nina msimamo kama nyie, na nitapenda kuungana nanyi na kuungana nanyi pamoja katika safari yenu na kuwa nanyi katika ‘ibada ya Allah swt .”

 

Wao walikubaliana na ushauri na ombi alilolitoa mchungaji huyo. Mchungaji huyo aliwarudisha kondoo wote kwa mwenye mali na akarejea kuungana pamoja na hawa watu sita katika safari yao hiyo.

 

Mbwa kujiunga nao katika safari yao…

Mchungaji huyo alikuwa na mbwa ambaye naye pia alijiunga nao katika safari hiyo. Kwa kuwafuata fuata.  Hao sita walipinga mbwa kuja nao, kwa sababu walikuwa wana hofu kuwa iwapo mbwa angebweka basi pale walipojificha patajulikana.

 

Nao wakasema, “Itakuwa vyema iwapo sisi tutamwondoa huyu mbwa na kumwacha hapa na tukaendelea na safari yetu.” Kwa hivyo walifanya jitihada zao zote za kumwacha mbwa nyuma, lakini mbwa hakuacha kumfuata mmiliki wake. Basi wakawa hawana chaguo lingine isipokuwa kumkubalia mbwa awafuata na kuungana nao.

 

Mchungaji huyo aliwachukua hawa wenzake sita katika majabali mlimani, ambapo upande wa pili wake kulikuwa na mabonde yaliyokuwa na mashamba yamestawi vizuri na kumejaa miti ya matunda. Kulikuwa na mto pia ukipita hapo.  Kulikuwa na hewa nzuri iliyokuwa ikipita katika bonde hilo. Wao walikula matunda, wakanywa maji, na wakaingia katika mapango yaliyokuwa yakiitwa Kahf. Miale ya jua ilikuwa ikipita katika sehemu ambayo palikuwa wazi katika pango hilo. Wao walipumzika kwa kipindi kidogo na wakajishughulisha katika ‘ibada ya Allah swt .

 

Usingizi mrefu: Je ni nusu siku au siku moja au miaka 300?

 

Allah swt  anatwambia katika Qur'an Tukufu Sura Al Kahf, 18, ayah

19-20:

Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapete kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Allah swt  wenu Mlezi anajua zaidi muda mliokaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote.

Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao;  na hapo hamtafanikiwa kabisa !

 

Baada ya hawa kufanya ‘ibada walipolala pamoja na mbwa wao katika kiingilio cha pango hilo. Upepo mzuri na wa kupendeza ulikuwa ukipita juu yao pole pole na vile vile miale ya jua pia iking’ara juu yao kwa kupitia upande uliokuwa wazi wa pango lakini wao walikuwa hawana habari yoyote na hayo kwa sababu waliingia katika usingizi mrefu. Hawa As-Hab Kahf (Watu wa Pangoni) walilala zaidi ya miaka mia tatu na katika kipindi hiki cha usingizi wao mrefu wao hawakuamka kutoka usingizini mwao. Lakini baada ya kupita kipindi hicho wao waliamshwa kwa amri ya Allah swt  na wakawa wakiangalia mahala palipo wazunguka. Wao walianza kuongelea kuhusu wao wenyewe. Baadhi yao walisema, “Sisi tumelala kwa siku moja”, wengine wakasema, “Tumelala nusu siku.” Lakini jambo ambalo liliwashtua na kuwastaajabisha ni kule kupotea kabisa kwa mimea na wao walikuwa wakihisi njaa pia. Wao walikuwa wakijaribu kujiuliza itawezekanaje kwa siku moja kupotea kwa mto na uoto kwa pamoja. Hatimaye wao waliamua kwenda kufuata chakula mjini kwani hawakuweza kustahimili njaa tena na zoezi hili lilikuwa lifanyike kwa mpango kabisa ili kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kushuku au kujua mahala wao walipojificha, ama sivyo watu watawaua au kuwalazimisha kurudia katika kuabudu miungu.

 

Hivyo mmoja miongoni mwao aliyekuwa na uzoefu alivaa mavazi ya mchungaji na akaelekea mjini kwenda kutafuta chakula kwenda kutafuta mikate kwa fedha kidogo walizokuwa nazo.

 

Mtu huyo alipo karibia katika vitongoji vya mji, akaona imebadilika kabisa na ndani ya mji akaona mambo yote ya kustaajabisha kabisa. Mitaa, vichochoro na barabara na mistari ya milango na mistari ya majumba yalivyokuwa yamejengwa yote yalikuwa yameshabadilika kabisa. Hata mavazi ya wakazi wa mjini pia yalikuwa yamebadilika kabisa. Na hivyo alishikwa na bumbuwazi kwa kuona mabadiliko hayo kwa kiasi hicho katika mpangilio wa kila jambo katika mji huo. Na hivyo aliwaza kama yeye alikuwa katika fahamu zake sahihi au hapana au alikuwa akiota ndoto. Je ameingia katika mji mwingine kwa kupotea njia ya kwenda mji wake ? Je kwa nini ameshindwa kuwatambua watu ambao aliokuwa anawajua katika mji wake huo ?

 

Hatimaye alifika katika tanuru la mwoka mikate. Yeye aliagiza mikate michache kwa mategemeo ya kumlipa kwa pesa alizokuwa nazo. Mwoka mkate huyo alipoziona fedha hizo, alimwuliza,

“Ewe kijana ! Je kuna mahali umevumbua hazina?”

 

Mtu huyu wa Mapango alijibu,

“Laa, hizi fedha mimi nimelipwa na nimezipata baada ya kuuza tende zangu juzi. Na baada ya hapo nilikuwa nimekwenda safari nje ya mji na hivi ndipo nimerudi.”

 

Mwoka mikate hakuridhishwa na aliyoyasema huyo mtu, na hatimaye akamfikisha mbele ya Mfalme na kusema,

“Mtu huyu amevumbua hazina. Na uthibitisho wake ni kwamba ni kutokana na fedha alizonazo mikononi mwake.”

 

 Mfalme akamwambia mtu huyo,

“Ewe kijana ! Usiniogope mimi. Niambie ukweli. Sisi kamwe hatutakudhuru. Mtume wetu Issa a.s. mwana wa Bi. Mariam ametuamrisha kutoza Khums (Kodi ya kidini) kutoka mtu yeyote yule anayevumbua hazina.”

 

Mtume huyo alimlilia Mfalme ili aweze kusikiliza kilio chake hicho.  Yeye akasema,

“Mimi ni mkazi wa mji huu. Ni siku mbili tu zilizopita mimi na wenzangu tuliondoka tukaenda mapangoni kwa ajili ya kufanya ibada ya Allah swt . Wakati wetu wa kuondoka kulikuwa na Mfalme aliyekuwa akiitwa Daquis (Daqyanus), ambaye ndiye alikuwa mtawala wa mji huu na ambaye alikuwa akiwalazimisha watu wamwabudu yeye kama mungu na kujitupa mbele yake katika Sujuda. Na kwa kutokana na sisi kutokumwamini  yeye kama ni mungu, ndicho sisi kilicho tusababisha kuhama mji huu na kujificha katika mapango huko jangwani. Na wenzangu wapo wanasubiri kurudi kwangu mimi kwao.”

 

Mfalme akasema,

“Sisi tutakwenda pamoja nawe ili tukashuhudie mambo wenyewe lau kama unasema ukweli katika habari zako hizi, kwa sababu mambo unayoyazungumza wewe ni ya kustaajabisha sana, ni mambo mapya kabisa. Ni kiasi cha miaka mia tatu iliyopita tangu Daquis alipotawala huku.”

 

Mfalme kwenda pangoni

 

Kwa hivyo Mfalme pamoja na watu wa baraza lake waliandamana naye huyo mtu hadi katika mapango na yeyote yule aliyepata habari hizi pia alishirikiana nao wakaenda mpaka kwenye mapango hayo.

 

Wao walipofika katika mpitio wa mlima, mtu huyo wa pangoni akamwambia Mfalme,

“Itakuwa vyema iwapo nyie mtabaki hapa. Iwapo mtatokezea ghafla mbele ya wenzangu wataogopa na kushtushwa. Na inawezekana mshtuko huu ukawagharimu ukawa hatari kwao. Naomba mimi niende peke yangu mbele yao na niwaeleze habari zote ndipo nyie mje.”

 

Mtu huyo alipoingia ndani ya mapango na kuwaambia wenzake,

 “Enyi wenzangu ! usingizi wenu ambao mnaufikiria kuwa ni wa siku moja haukuwa hivyo, ua haukuwa usingizi wa nusu siku, bali usingizi umechukuwa baadhi ya karne. Mimi nimekwenda mjini na nimeona kule kila kitu kimebadilika kabisa. Mfalme mdhalimu Daquis amekufa zaidi ya miaka mia tatu iliyopita, na hakuna chochote kinachoonyesha yeye au ufalme wake. Na kwa amri ya Allah swt  ametumwa Mtume kwa jina la Issa a.s. mwana wa Bi. Mariam katika ardhi hiyo, na watu wa huko ndio wafuasi wake.  Kwa hakika mimi nimekumbana na matatizo makubwa sana nikiwa hapo mjini. Na sarafu niliyokuwa nayo nilipowaonyesha watu, waliona maajabu kwao. Na hivyo wakadhani kuwa mimi nimevumbua hazina fulani. Wao wakanichukua kwa Mfalme wao na hapo ndipo nikaja kutambua kuwa sisi tumelala usingizi kwa amri ya Allah swt  kwa zaidi ya miaka mia tatu. Mfalme na watu wa baraza lake wametusubiri hapo nje. Wao wamekuja kuthibitisha hayo niliyoyasema. Kama nyinyi mtanikubalia, mimi ninaweza kuwaleta hapa mbele yenu.”

 

Wale wenzake katika pango hawakumwamini huyo mwenzao. Wao walidhani kuwa mwenzao anataka kuwaponza na wakamatwe na Mfalme. Basi hapo wao walimlilia Allah swt  na kumwomba kuwa yeye Allah swt  awarudishe katika hali waliyokuwa nayo. Wao waliinua mikono yao juu na kuomba,

“Ewe Allah swt  ! tuokoe sisi kutokana na janga hili na uturudishe katika hali yetu tuliyokuwa nayo.”

 

Dua yao ilikubaliwa na Allah swt  aliwafanya wao tena wakarudia usingizi wao mrefu. Mfalme na watu wake waliwasubiri hao kwa muda mrefu bila kuona mtu akirejea. Nao waliingia katika pango hilo na kwa amri ya Allah swt  wale waliokuwa wamelala hawakuweza kuonekana machoni mwa Mfalme na watu wake.

 

Kwa amri ya Mfalme, hapo kulijengwa Msikiti kwa ajili ya ‘ibada ya Allah swt .

 

Tukio hili ni mojawapo la ‘ishara za Allah swt  yaliyoonyeshwa kwa watu ili waweze kujifunza masomo kuhusu ukuu wa Allah swt , Allah swt  wa malimwengu zote.

MWISHO.


BWANA DHUL-QARNAIN

 

Bwana Dhulqarnain alikuwa akiitwa Ayash. Na yeye alikuwa ndiye Mfalme wa kwanza baada ya Mtume Nuh a.s., wengi wa watu wanadhani kuwa yeye ndiye Alexandria wa Kirumi lakini haya si kweli kama vile tunavyopata maelezo kutoka riwaya mbalimbali, vile vile wengi wanauliza iwapo Bwana Dhulqarnain alikuwa ni Mtume? Kwa hivyo jibu sahihi ni kwamba Bwana Dhulqarnain yeye hakuwa mtume bali alikuwa mja mwema wa Allah swt  .

 

Allah swt  anasema katika Quran, Sura Al-Kahf, 18, Ayah 83 - 98.

Wanakuuliza khabari za Dhul-Qarnain, Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadith yake.

Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu

Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope mausi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini ! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.

Akasema: Ama aliye dhulumu basi tutamuadhibu, na kisha atarudishwa kwa Allah swt  wake Mlezi amuadhibu adhabu isiyo julikana.

Na ama aliye amini na akatenda mema basi atapata malipo mazuri. Nasi tutamwambia lilio jepesi katika amri yetu.

Kisha akaifuata njia.

Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).

Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”

Akasema:“Yale ambayo Allah swt  amenimakinishia ni bora  (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”

Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.”

Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.

Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Allah swt . Na itakapofika ahadi ya Allah swt  ya kufika Qayama, atauvunjavunja. Na ahadi ya Allah swt  ni kweli tu.”

 

Je ni kwa nini akaitwa Dhulqarnain ?

Zipo sababu nyingi zinazopatikana za kuitwa kwake Dhulqarnain kwa sababu mojawapo ni kwamba yeye ncha zote za dunia Mashariki mpaka Magharibi alikuwa anaendesha hukumu yake, alikuwa ameishinda, na Allah swt  alimpa uwezo juu ya Nuru na Kiza (Dhulmat) na ndio hii sababu moja kubwa ya kupata jina hili la Dhulqarnain.

 

Katika safari mojawapo watu walimwuliza iwapo mtu atakufuru je wewe utamwadhibu ? Naye aliwajibu kuwa yeye angewaadhibu vikali sana wale Mushiriki na Dhalimu na vile vile Allah swt  atawaadhibu vikali mno, lakini yule atakayekuwa ameleta imani na anatenda matendo mema basi yeye atapata malipo yaliyo mema bora kabisa.

 

Bwana Dhulqarnain alikuwa na Malaika mmoja aliyekuwa anaitwa Rukail ambaye alikuwa ni rafiki yake sana na mara nyingi walisikika wakiwa wanaongea na siku moja yeye alimwuliza Malaika,

“Je ibada zinazofanywa na watu wa ulimwenguni ni sawa na zile zinazofanywa na Malaika mbinguni ?”

 

Malaika alimwambia,

“Kwa hakika Malaika wanazofanya ibada mbinguni ni bora kabisa kuliko zile zinazofanywa na wanaadamu humu duniani.”

 

Mbingu imejaa Malaika na wote kwa pamoja wapo wanafanya ibada ya Allah swt  kwani humu kuna wengine maisha yao yote wako katika Rukuu, wengine wako katika hali ya Kusujudu. Kwa kuyasikia hayo Bwana Dhulqarnain alilia sana na akamwambia Malaika kuwa yeye iwapo atajaariwa umri mrefu basi atafaya ‘Ibadah za Allah swt  vile itakiwavyo. Malaika Rukail kwa kusikia hayo akamwambia,

“Ewe rafiki yangu juu ya ardhi hii ya ulimwengu kuna chemchemi moja inaitwa 'Aynul Hayat (Chemchemi ya maisha ya milele) na kwamba yeyote yule atakaye kunywa maji yake basi hatakufa mpaka pale yeye mwenyewe atapoomba kufa. Hivyo Allah swt  amekula kiapo kuwa yeyote yule atakaye kunywa maji ya chemchemi hiyo hatakufa na nakushauri nawe pia unywe maji ya chemchemi hiyo ili usife kama vile unavyotaka wewe.”

 

Kwa kuyasikia hayo Bwana Dhulqarnain alimwuliza,

“Je chemchemi hiyo ipo wapi ?”

 

Malaika Rukail alimjibu,

“Kwa kweli mimi siijui ilipo lakini nimesikia kuwa Allah swt  ameiumba chemchemi hiyo katika Dhulmat (Kiza kali) na humo ndipo kulipoumbwa chemchemi ya maisha hiyo ambayo hadi sasa hakuna binaadamu wala majini yeyote aliyeweza kuifikia chemchemi hiyo.”

 

Bwana Dhulqarnain alimwuliza,

“Je hiyo (Dhulmat) iko wapi ?”

 

Basi Malaika Rukail akamjibu kuwa,

“Mimi sina habari nayo.”

 

Na kwa hayo Malaika huyo akarudi mbinguni akimwacha Bwana Dhulqarnain katika hali ya masikitiko makubwa mno kwani hakupata habari kamili alizokuwa akizitaka ili kuweza kuifikia hiyo chemchemi ya maisha marefu.

 

Bwana Dhulqarnain alianza kuwaita Ma’ulamaa wakubwa, Mafuqaha ambao walikuwa na ilimu ya vitabu vitukufu vya Allah swt  na habari za Mitume a.s. waliotangulia,[2]

 

Basi Bwana Dhulqarnain alijaribu sana kama wao wanajua habari yoyote kuhusu chemchemi hiyo ya maisha nao wote walikuwa wakimwambia kuwa wao walikuwa hawajui chochote kuhusu swala hilo na vile vile Bwana Dhulqarnain aliwauliza iwapo wao walishawahi kusoma kuhusu Dhulmat katika vitabu vyao, nao wakajibu kuwa hawajawahi kusoma habari zake.

 

Kwa jitihada zake zote hizo Bwana Dhulqarnain hakufanikiwa kupata ufumbuzi wa maswala ambalo alikuwa akitaka kujua habari zake ndipo kulimfanya yeye akawa mtu mmoja mwenye hali ya uzuni kabisa na ambaye hakuwa na raha ya aina yoyote katika baraza lake na hali hii ilikuwa inadhihirika miongoni mwa raia wake. Kwa kuona hali hii ya Bwana Dhulqarnain katika baraza lake kulikuwapo na mtoto mmoja mdogo ambaye yeye alikuwa anatokana na warithi wa Mtume katika zama hizo, aliinuka na kwa heshima na taadhima akamwambia Mfalme huyo Bwana Dhulqarnain kuwa,

“Mheshimiwa yale uliyowauliza hawa watu waliokuwa na ilimu mbalimbali ambayo wao hawayajui chochote lakini mimi ninayo ilimu na habari za maswala unayotaka kuyajua ! !”

 

Kwa kuyasikia hayo Mfalme huyo alistaajabishwa na kushtushwa sana kwa kumwona kijana mdogo akimwambia kuwa yeye anajua habari za maswala ambayo yamemtatanisha yeye kutafuta ufumbuzi wake. Na Bwana Dhulqarnain akamwuliza kijana huyo,

“Je kweli unasema wewe kuwa unaelewa kuhusu mambo hayo ?”

 

Na mtoto huyo bila kusita akajibu,

“Ndio mheshimiwa !”

 

“Mimi nimesoma katika kitabu cha Mtume Adam a.s. (sio lazima kitabu kiwe kama vitabu vyetu siku hizi bali juu ya kitu chochote ambacho kiliandikwa juu yake wakati wa zama hizo) nimeona kuwa juu ya ardhi hii ya ulimwengu huu ipo chemchemi hiyo ya maisha katika Dhulmat. Na yeyote yule atakaye fanikiwa kunywa maji ya chemchemi hiyo hatakufa kamwe hadi pale atakapoomba yeye mwenyewe afe, na chemchemi ya maisha hiyo iliopo katika Dhulmat na pale ilipo hiyo chemchemi ya maisha katika Dhulmat hakuna binaadamu wala majini wowote waliopita”

 

Kwa kuyasikia haya Bwana Dhulqarnain kwa hakika roho yake ilianza kutulia sana na alijawa na furaha sana na katika siku chache zilizofuatia alianza matayarisho ya safari kuelekea Dhulmat palipo na chemchemi hiyo ya maisha, na alifunga safari akiwa amewachukua watu wenye ilimu wapatao elfu moja, Mafuqaha  na Wanazuoni na aliondoka kuelekea upande wa mashariki wa dunia.

 

Msafara huu wa Bwana Dhulqarnain pamoja na wale waliokuwa wameambatana naye waliendea na safari kwa muda wa miaka kumi na miwili na ndipo walipokaribia Dhulmat ambapo kuna kiza kali kabisa kiasi kwamba kiza cha usiku haufai chochote mbele yake na hapo aliweka kambi akawaita wale wote aliokuwa amesafiri nao katika msafara huo na kuwaambia kuwa,

“Mimi kuanzia hapa sasa ninataka niende safari hii peke yangu na Allah swt  akinijaalia nitafanikiwa katika azma yangu hiyo !”

 

Kwa kusikia hayo hao watu wenye ilimu na maarifa aliokuwa nao walimwambia,

“Ewe Mtukufu Mfalme wetu ! Unavyoona wewe kuwa hii Dhulmat ni kiza kali kabisa na tuna hofu kama utakwenda peke yako Mungu apishe mbali kama utapata matatizo yoyote utakuwa peke yako bila msaada wowote hivyo tunakushauri usiende peke yako.”

 

Kwa hayo Bwana Dhulqarnain akawajibu,

“Naam mimi ni matumaini yangu kuwa nifike huko penye chemchemi hiyo ya maisha na niweze kunywa maji hayo”

 

Basi kwa masikitiko makubwa sana wote wakasema

“Iwe vile atakavyo Mfalme wetu !”

 

Inasemekana kuwa Mtume Khidhr a.s. alikuwa pamoja naye. Mfalme aliwauliza Ma’ulamaa swali kuwa,

“Hebu niambieni katika wanyama wote ni mnyama gani huona vizuri zaidi kuliko wengine ?”

 

Wao walimjibu kuwa,

“Farasi jike akiwa bikira”

 

Hivyo Mfalme huyo alitayarisha jeshi la watu wenye akili na busara kuliko wengine elfu sita pamoja na Mafarasi jike bikira elfu sita na alimteua Mtume Khidhr a.s. awe ndio kiongozi wa msafara huo. Wakati anaondoka kwenda zake kuanza safari yake hiyo alitayarisha jeshi jingine la elfu sita aliowaacha hapo nyuma na kuwaambia wamsubiri kwa muda wa miaka kumi na mbili na lau kama hakurudi katika muda huo basi wao wanaweza kurudi nchini kwao. Wakati wanaingia katika kiza hicho Mtume Khidhr a.s. alimwuliza lau kama mtu atapotea katika kiza hicho watamtafutaje ? Basi kwa hayo Bwana Dhulqarnain alitoa Almasi moja iliyokuwa ya rangi nyekundu akampa Mtume Khidhr a.s. na kumwambia lau itatokea hivyo basi hii almasi nyekundu kama utaitupa ardhini basi itatoa sauti na itatoa mwanga mkubwa na hivyo wale wote watakaoisikia sauti hiyo waelekee kwenye sauti hiyo, na wao wakaendelea na safari zao huku Mtume Khidhr a.s. akiwa mbele na Bwana Dhulqarnain akimfuata.

 

Wakaendelea na safari yao na ikafika siku moja katika kiza kali kabisa Bwana Dhulqarnain akaona maji na akawaambia maaskari wake wasubiri pale pale ila yeye tu ndiye atakayeendelea mbele na akateremka kutoka farasi wake (Mtume Khidhr a.s.) na akaenda kwa miguu hadi pale penye maji akatupa ile almasi yake nyekundu na alishangazwa sana kuona ni kwa nini haikutokea sauti wala mwanga.  Wakati hiyo almasi ilipofika kwenye kina cha chini ya maji ikagonga ardhi hapo ndio ikatokezea sauti na mwanga na Mtume Khidhr a.s. alipoangalia maji aliona ni meupe kuliko hata maziwa na yalikuwa matamu kuliko hata asali basi yeye akayanywa hayo maji akaoga na akaichukua tena hiyo almasi yake na kuwatupia wenzake waliokuwa amekuja naye na ilipogonga chini kwa kutokana na sauti na mwanga wenzake aliokuwa ameambatana nao wakaja na Bwana Dhulqarnain alikuwa yupo nyuma yao na kuja kuangalia wakaona chemchemi ya maisha haipo wala haionekani dalili yoyote kama ilikuwepo hapo. Kwa muda wa usiku na mchana arobaini wao wakaendelea na safari yao katika kiza kali hicho na mwishoni wakakuta kuna mwanga unaonekana mbele. Mwanga huo ambao inasemekana ulikuwa ni mwanga kwa kudura za Allah swt  na wakakuta kuna jumba moja zuri kabisa, Mfalme aliwaamuru majeshi wake wote wakae hapo wasubiri hapo na yeye peke yake alielekea na kuingia ndani ya jumba hilo na humo kulikuwa na susu moja na ambalo lilikuwa na ndege mmoja mdogo wa rangi nyeusi na kwa kumwona yeye,  ndege huyo akauliza,

“Je wewe ni nani ?”

 

Kwa kusikia swali hilo kutoka kwa ndege huyo Bwana Dhulqarnain akajibu,

“Mimi ni Dhulqarnain.”

 

 

Kwa kusikia hayo ndege huyo mdogo akasema,

“Wewe ni Mfalme mkubwa sana, kwa nini umeacha nchi yako adhimu na umekuja kufanya nini hapa ? Je nchi hiyo kubwa kabisa haikutoshi wewe ?”

 

Kwa kusikia hayo yeye akashtuka ! Na hapo ndege akaendelea kusema kuwa,

“Usishtuke isipokuwa naomba kila nikuulizacho unijibu”,

 

Hapo Bwana Dhulqarnain akamwambia,

“Naam endelea kuuliza utakacho kuuliza !!!

 

Hapo ndege akauliza,

“Je katika nchi yako watu wako wanapenda sana kuimba na kusikiliza nyimbo na muziki?” 

 

Kwa hayo Bwana Dhulqarnain akajibu,

“Naam !”

 

Kwa kusikiliza hayo ndege huyo aliaza kutetemeka sana na susu lile likajaa kama sehemu mbili hivi ! Kwa kuona haya Bwana Dhulqarnain aliona maajabu makubwa sana, baada ya hapo ndege huyo aliendelea kuuliza,

“Je watu wa nchi yako wanapendelea kutoa ushahidi uongo ?”

 

Bwana Dhulqarnain akajibu,

“Naam !!”

 

Kwa kusikia hayo tena ndege huyo akaanza kutetemeka na susu hilo likajaa !

 

Kwa kuona hayo Bwana Dhulqarnain alishangazwa mno !

 

Ndege huyo akamwambia Bwana Dhulqarnain usishtushwe wala kuona maajabu !

 

Ndege aliendelea kuuliliza kumwambia Bwana Dhulqarnain naomba uniambie,

“Je watu wako wameacha kusema Lailaha Illallah, kalimah tukufu ?”

Bwana Dhulqarnain akajibu:

“Hapana”

 

Kwa kusikia hayo ndege huyu akapungua kwa sehemu mbili na tena akauliza swali,

“Je watu wako wameacha kusali ?”

 

Kwa hayo Bwana Dhulqarnain akamjibu,

“Laa watu hawajacha kufanya ibada wala kusali.”

 

Na kwa majibu hayo ndege huyo akapungua tena akawa mdogo akapungua na akaendelea kuuliza,

“Je watu wa nchi wameacha Ghusl-i-Jannaba ?

 

Na Bwana Dhulqarnain akajibu,

“Hapana wanafanya ghusl-i-Janaba!”

 

Kwa swali hilo ndege huyo akarudi katika hali aliyokuwa nayo hapo mwanzoni basi Bwana Dhulqarnain aliona ngazi moja iko mbele yake pale akaenda akapanda ngazi na akaona kuna kibanda kimoja ambamo kulikuwa na kijana mmoja mzuri sana huku akiwa ameinua kichwa chake anaangalia angani.  Kijana huyo akamwuliza Bwana Dhulqarnain,

“Je wewe ni nani ?”

 

 

Bwana Dhulqarnain akajibu,

“Mimi ni Mfalme !”

 

Kijana huyo akamwambia,

“Je imekuwaje wewe umeacha nchi kubwa sana na ukaja mpaka huku, je ulicho nacho hakikutoshi ?”

 

Bwana Dhulqarnain akamwambia,

“Ni kwa nini wewe unaangalia mbinguni na huku umeweka mikono juu ya midomo yako ?”

 

Kijana huyo akamwambia,

“Mimi nasubiri amri ya Allah swt  ya kupiga mbiu siku ya Qiyama.”

 

Hapo Malaika huyo akachukua kijiwe kimoja akampa Bwana Dhulqarnain na kumwambia alichukue jiwe hilo pamoja naye kwani jiwe hilo lina njaa, likibakia na njaa nawe utabakia na njaa na litakapo shiba basi na tumbo lako litashiba, baada ya hapo Bwana Dhulqarnain alirudia kwa watu wake akawauliza watu ninaomba munielezee kitendawili hiki cha jiwe, nani anajua ?

 

Hapo wale watu waliokuwa na akili na maarifa na busara wa hali juu waliokuwa wameambatana nao waliagiza mizani moja na wakachukua jiwe lile ambalo Bwana Dhulqarnain alilopewa na yule Malaika wakaliweka katika sahani moja na sahani ya pili wakaweka jiwe lingine kuangalia kama litakuwa sawa katika uzani lakini wakaona kuwa jiwe lile alilopewa Bwana Dhulqarnain na Malaika likawa ni zito, wenyewe wakaendelea kuongezea mawe mengine katika sahani ile ya pili na mpaka sahani ya pili ikajaa bado lile jiwe likawa ni zito kuliko mawe rundo yaliyowekwa katika sahani ya pili. Kwa kuona uhakika huo hao wote walimwambia Bwana Dhulqarnain kuwa sisi tumeshindwa kitendawili hiki cha jiwe hili ulilopewa na Malaika !

 

Hapo Mtume Khidhr a.s. akamwambia Dhulqarnain,

“Ewe Mfalme kitendawili hiki cha jiwe hili hawa watu hawataweza kukuambia lakini mimi ninajua jibu lake.”

 

Kwa kusikia hayo Bwana Dhulqarnain moyo wake ulitulia na akamwomba Mtume Khidhr a.s. amtatulie kitendawili hicho. Mtume Khidhr a.s. aliliweka jiwe katika sahani moja ya mzani na katika sahani ya upande wa pili aliweka kijiwe kimoja cha udongo na mara wakaona wote kuwa jiwe hilo likawa ni zito na hawakuweza kujizuia kusema,

“Tunajua kuwa Mtume Khidhr a.s. si mchawi na hivyo tuna yakini kuwa yeye si  mchawi lakini hatuelewi siri ya jambo hili.”

 

 Kwa kuyasikia hayo Bwana Dhulqarnain akamwambia Mtume Khidhr a.s. awaelezee siri hiyo watu hao ambao wana shauku ya kujua ! Hapo Mtume Khidhr a.s. akasema,

“Ewe Mfalme!  Utukufu wa Allah swt  sisi hatuwezi kujifanya wajuaji mbele Yake kwani yeye anawajaribu waja wake kwa njia mbalimbali mfano anamjaribu ‘Alim kwa ‘Alim (mwenye ilimu anajaribiwa kwa mwenye ilimu), ilimu inajibiwa kwa ilimu, aliyesoma anajaribiwa kwa aliye mjahili, na aliye jahili anajaribiwa kwa aliye soma na hawa wote ndivyo wanavyo jaribiwa, na mimi na wewe pia tunajaribiwa kwa pamoja”

 

Na kusikia hayo Dhulqarnain akasema,

“Ewe Mtume Khidhr a.s.! Rehema za Allah swt  zikushukie wewe lakini naomba utuambie basi kuhusu kitendawili hiki cha jiwe hili.”

 

Kwa hayo Mtume Khidhr a.s. alianza kumjibu akasema,

“Ewe Mfalme Malaika huyo amekupa jiwe hili ambalo lina matamanio yasiyo toshelezwa kwani umejionea mwenyewe kuwa kila ulivyokuwa ukiendeleza kuongeza jiwe upande wa pili wa sahani ilikuwa haitoshi mkaendelea kuongezea na maelfu ya majiwe mkaweka lakini bado jiwe hilo halikutosheka lilikuwa linataka mawe zaidi na zaidi. Lakini pale nilipoweka mie kirundo kidogo cha udongo basi kikavunja uroho wake wa kutamani mawe mengine” [3]

 

Mtume Khidhr a.s. akamwambia,

“Ewe Mfalme na hali yako wewe ni sawa na jiwe hili kwani Allah swt  amekujaalia nchi kubwa sana lakini bado hauna subira na bado uko katika harakati za kujiongezea zaidi ! Kwa hakika hapa ulipo wewe leo ni mahala ambapo hakuna binaadamu wala majini yeyote walio kwisha kufika hapa je nchi uliyo nayo wewe haikukutosha ?”

 

Binaadamu hali yake ni hivi hivi hadi pale atakapofikishwa kaburini ndipo atakapokuwa ameyaacha hayo.

 

Kwa kusikia hayo Bwana Dhulqarnain aliangua kilio na akakiri kuwa kile ukisemacho wewe Mtume Khidhr a.s. ni mambo ya kweli na yaliyo ya haki tupu nami kamwe sitataka kujiongezea zaidi ya yale niliyonayo na aligeuka na kuelekea Dhulmat na katika vikanyagio vya mafarasi kulikuwa kukija sauti kama kuna changarawe, kwa hayo wale aliokuwa ameambatana nao katika msafara huo wakamwuliza,

“Je ni nini hayo ?”

 

Akajibu kuwa,

“Yeyote yule atakaye chukua atajuta na yeyote yule hatakaye chukua pia atajuta !!!”

 

Wengi wao walichukua na pale walipotokezea nje ya kiza hicho wakaona kuwa hayo waliyoyazoa wakisikia sauti za changarawe kumbe si changarawe bali ni almasi, hivyo wale ambao hawakuchukua walianza kuonyesha majuto yao na wale waliokuwa wamechukua walianza kujiambia je ni kwa nini hawakuchukua zaidi ili wangenufaika zaidi ! Baadaye wakafika Darul Hukumah Humatul Jandal ambapo aliaga dunia.

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. wakati anaelezea alisema kuwa Allah swt  amteremshie rehema ndugu yangu Bwana Dhulqarnain kwani yeye hakuwa na kosa la binafsi bali alikuwa anategemea kufika pale alipokuwa akitarajia na kama wakati wa kwenda angeona almasi hizo ambazo zilikuwa zikisikika kama changarawe basi bila shaka angezoa kwa sababu wakati wa kwenda alikuwa na mapenzi ya dunia lakini wakati wa kurudi alikuwa hana matamanio na dunia hivyo hakuokota almasi yoyote na vile vile aliwaonya wale waliotaka kuokota. Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliulizwa,

“Je Bwana Dhulqarnain alikuwa ni Mtume au ni Malaika ?”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alijibu kuwa,

“Bwana Dhulqarnain hakuwa Mtume wala Malaika bali alikuwa ni mja mwema wa Allah swt .”

 

Imepatikana riwaya kutoka Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. kuwa Bwana Dhulqarnain alikuwa ni mja mwema wa Allah swt  ambaye alikuwa akiwalingania watu kuja katika haki na ikatokea kwamba yeye alijeruhiwa kichwani na kwa kipindi fulani akawa Ghaib na baada ya  kipindi fulani tena akatokezea mbele yao na tena akajeruhiwa kichwani mwake na baada ya hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema miongoni mwenu pia kuna Shakhsiyyah mmoja anayeitwa 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye juu ya ardhi hii ni mtu ambaye ana uwezo wa hali ya juu kabisa na ambaye amejaaliwa utukufu na ambao utukufu huu utaendelea hadi kwa Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. na kwa ajili yake ardhi zote zitatapika yale yote yaliyo kuwa ndani mwake na yeye ndio atakae kuwa akihukumu nyoyo za watu”.

 

Bwana Dhulqarnain akawa anawalingania watu katika haki na njia ya Allah swt  na akawajengea Msikiti mmoja mzuri kabisa na tena alianza safari yake ya kutembelea dunia na njiani akamwona mzee mmoja ambaye alikuwa akifanya ‘ibada ya Allah swt , naye akamkaribia huyo mtu akamwambia,

“Je kwa nini ulipouona uso wangu huu wa kutisha wewe haukushtuka ?”

 

Mzee huyo akamwambia,

“Kwa hakika jeshi la Allah swt  ni jeshi kubwa kabisa kuliko lako sasa itawezekanaje mimi ninamuomba Allah swt  na lau kama nitaacha kulenga moyo wangu mawazo yangu na fikara zangu kwake yeye nikakugeukia wewe sasa nani atakaye nitimizia mimi maswala yangu ?”

 

Bwana Dhulqarnain akamwambia mzee huyo,

“Kama utakubali ninaomba nikushirikishe wewe katika ufalme wangu na uishi pamoja nasi !”

 

Mzee huyo akamwambia Bwana Dhulqarnain,

“Kama wewe utanipa dhamana ya mambo manne basi mimi niko tayari kukubali jambo hilo uliloniambia:

1. Neema, na Raha kamwe isiondoke,

2. Unipatie siha (afya) ambamo mimi kamwe nisiwe mgonjwa,

3. Unijalie ujana ambao uzee hautanikaribia kamwe,

4. Maisha yale ambayo mimi sitapata kifo !!! ”

 

Bwana Dhulqarnain akamwambia mzee huyo,

“Ewe mzee ! Vitu hivi vinne binaadamu hanavyo katika uwezo wake.”

 

Na hapo huyo mzee akamwambia Bwana Dhulqarnain,

“Wewe Dhulqarnain huna vitu hivi vinne, havipo katika uwezo wako lakini Allah swt  ninaye muabudu mimi yeye anao uwezo na viko chini katika kudura yake, na wewe pia uko chini yake.”

 

Kwa kuyasikia haya Bwana Dhulqarnain akamwambia huyo mzee,

“Ewe mzee kwa kweli wewe uliyoyasema ni mambo ya ukweli na haki kabisa.”

 

Na akaendelea na safari yake, njiani wakati anaendelea na safari yake akakutana na ‘Alim na kufanya mazungumzo naye basi huyo Alim akamwuliza Bwana Dhulqarnain,

·         “Naomba uniambie ni vitu gani hivyo viwili ambavyo daima vinakaa vikizunguka?

·         Je ni vitu gani viwili ambavyo vipo katika ulimwenguni tangu ulipoanza ?

·         Je ni vitu gani viwili ambavyo moja inaifuatia ya pili yake ?

·         Je ni vitu gani viwili ambavyo ni maadui miongoni mwao ?

 

Yeye Bwana Dhulqarnain akajibu kuwa,

·         Ni mwezi na jua.

·         Kile kilichopo kwa milele ni ardhi na mbingu,

·         kile ambacho moja kinafuatia kingine ni usiku na mchana na

·         vile vilivyo na uadui baina yao ni kifo na maisha.”

 

Huyo Alim kwa kusikia majibu hayo alisema kwa hakika wewe ni mwenye ilimu na busara ya hali ya juu !

 

Bwana Dhulqarnain aliendelea na safari yake pamoja na jeshi lake na mara akamwona mzee mmoja mkongwe alikuwa akigeuza geuza mafuvu ya vichwa vya watu walio kufa miaka mingi iliyopita kama kwamba anatafuta kitu fulani katika nyuso za mafuvu hayo. Kwa kuona maajabu haya, Dhulqarnain alishangazwa ni kwa nini huyo mzee anageuza geuza mafuvu haya na akamwuliza,

“Je ni kwa nini wewe unageuza geuza mafuvu haya ?”

 

Basi mzee huyo mkongwe akamjibu Dhulqarnain,

“Mimi ninatafuta katika mafuvu haya ni nani alikuwa tajiri na nani alikuwa masikini, je ni nani alikuwa mfalme na ni nani alikuwa fakiri ?

 

Kwa kusikia haya Bwana Dhulqarnain akasema,

“Kwa hakika mambo haya ni mambo yenye nasiha kubwa kwangu mimi kwani baada ya kufa hakuna tofauti kati ya tajiri wala masikini kwa sababu wote wanakuwa hali moja !”

 

Bwana Dhulqarnain kutoka hapo aliendelea mbele na safari yake akakuta kuna kabila moja ambalo watu wake wote walikuwa wakiishi kwa pamoja kwa kushirikiana na kama ndugu moja na wakifanya ‘ibada ya Allah swt  na walikuwa hawamtendei mtu yeyote ubaya wa aina yoyote ile na akaona jambo la kustaajabisha kuwa wao walikuwa wametengeneza makaburi mbele ya majumba yao. Kwa hayo Bwana Dhulqarnain hakujizuia na akawauliza watu hao,

“Je ni kwa nini mnatengeneza makaburi mbele ya majumba yenu ?”

 

Wao walimjibu,

“Sisi tunafanya hivi kwa sababu daima tuwe tukikumbuka mauti !”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je ni kwa  nini majumba yenu hayana milango?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Miongoni mwetu hakuna waovu wala wezi !”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je kwa nini nyie hamna kiongozi ?”

 

Wao walimjibu

“Sisi hatutendeani dhuluma miongoni mwetu!”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je kwa nini hamna mahakama ?”

 

Wao wakajibu,

“Sisi hatugombani wala hatuna mtafaruku wa aina yoyote’

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je kwa nini hamna Mfalme yoyote ?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Hakuna yeyote miongoni mwetu aliye na matamanio zaidi na hivyo wote tuna matakwa yetu yaliyo sawa,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je ni kwa nini mna mali wote sawa sawa ?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Sisi tunafanya mgawano kwa uadilifu miongoni mwetu”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Kwa nini nyie hamgombani ?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Sisi tunaishi kwa mapenzi na udugu,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Kwa nini nyie muna kauli na shauri moja ?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Kwa sababu sisi tumeisha changua njia moja wote kwa pamoja ! Sisi hatutakiani ubaya wowote miongoni mwetu wala hakuna mtu anaye msuta mwenzake,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Kwa nini miongoni mwenu hakuna mauaji yoyote ?

 

Wakajibu,

“Kwa sababu sisi tunazidhibiti vyema nafsi zetu,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je ni kwa nini nyie hamghadhabikiani na  hamuhamaki ?”

 

Wao wakajibu,

“Kwa sababu sisi tuna muelekeo wa kunyenyekeana na kupendana,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je ni kwa nini wakazi wa kabila lenu wana umri mrefu kuliko makabila mengine ?”

 

Wo wakajibu kuwa,

“Kwa sababu sisi tunatimiza haki miongoni mwetu na tumejiepusha mbali na dhuluma za kila aina.”

 

Bwana Dhulqarnain aliendelea kuuliza,

“Kwa nini hampatwi na balaa la njaa ?”

 

Wakajibu,

“Sisi daima huwa tunafanya toba kwa Allah swt ,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je kwa nini nyie hamna misiba au huzuni na majanga ?”

 

 

Wakajibu,

“Sisi huwa tunafanya subira kwa balaa tunapopatwa na huwa tunajipa moyo katika sura kama hizo ili tuweze kukabiliana nayo,”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je kwa nini mali zenu haziharibiki au kuteketea ?”

 

Wakajibu,

“Sisi tuna imani kamili juu ya Allah swt  peke yake kwa sababu tunajua kile kinacho fanyika kitakacho tusibu itakuwa ni maslahi anayo tutakia Allah swt  mwenyewe na bila shaka ni mema tu kwa ajili yetu.”

 

Bwana Dhulqarnain akaendelea kuwauliza,

“Je mababu zenu pia walikuwa na utamaduni na desturi na tabia “kama za kwenu hizi ?

 

Wakajibu,

“Naam mababa na mababu zetu walikuwa daima wakiwahurumia sana masikini na walikuwa wakiwasaidia na kuwatimizia haja zao na yeyote yule aliye kuwa akiwakosea wao walikuwa wakiwasamehe na daima wakiwawia wema, wakiwa takia msamaha kwa uhalifu wote, walikuwa na uhusiano mwema pamoja na majamaa zao, na kamwe walikuwa hawafanyi hayana katika amana, na walikuwa wakitekeleza mema yote na ndiyo maana Allah swt  amewawia kwa ukarimu.”

 

Vile vile inapatikana katika historia ya kuwa Bwana Dhulqarnain yeye alikuwa ni mtu kutokea Alexandria, na alikuwa ni mtoto mmoja tu wa wazazi wake, alikuwa na tabia njema na alikuwa akiongea na watu kwa tabia nzuri na alikuwa mnyenyekevu na alikuwa daima akiwalingania watu katika haki kiasi kwamba watu walijishughulisha mno katika ibada za Allah swt , na kwa hakika yeye aliwajengea kaumu hiyo Msikiti mmoja mkubwa uliokuwa wa kisasa katika zama hizo, na baada ya hapo ndipo yeye alipotoka kwenda kuzunguka dunia ambapo watu walimsisitiza kuwa asiende popote na Kaumu yake walikuwa wamejitolea tayari kumtumikia kwani kwa sababu yake ukoo mzima ulikuwa una raha na amani na kwamba mama yake pia alikuwa ni mzee hivyo alimhitaji Dhulqarnain akiwa kama ni mtoto mmoja tu, yeye aliwaambia

“Maneno yenu ni kweli lakini hali yangu ni sawa na mtu ambaye ameng’olewa macho yake na moyo wake na masikio yake hayapo katika uwezo wake na kwamba kuna anaye mkimbiza mbele yake sasa mtu kama huyu masikini atafanyaje?”

 

“Basi hali yangu ni sawa hali ya mtu kama huyo kwani uwezo fulani uwezo fulani unao nivuta mimi basi mimi ndivyo ninavyo vutika kwenda huko na ninawausieni mje msikitini humu kufanya ‘ibada, mfanye utiifu na daima muwe mkimpa moyo mama yangu na mumfikishieni habari njema daima ili apate kuishi kwa raha.” 

 

Na baada ya hayo yeye akaondoka katika safari yake hiyo.

 

Kuwazuia Yajuj na Majuj

Ili kuwaokoa kaumu hiyo wasishambuliwe na kuingiliwa Yajuj na  Majuj, Bwana Dhulqarnain aliwajengea ukuta kaumu hiyo kama vile ilivyoelezwa katika habari iliyopita. Hawa Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vilivyokuwa vinaonekana kama binaadamu vifupi

 

Allah swt  anasema katika Quran, Sura Al-Kahf, 18, Ayah 83 - 98.

Wanakuuliza khabari za Dhul-Qarnain, Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadith yake.

Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu

Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope mausi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini ! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.

Akasema: Ama aliye dhulumu basi tutamuadhibu, na kisha atarudishwa kwa Allah swt  wake Mlezi amuadhibu adhabu isiyo juulikana.

Na ama aliye amini na akatenda mema basi atapata malipo mazuri. Nasi tutamwambia lilio jepesi katika amri yetu.

Kisha akaifuata njia.

Hata alipofika katikati ya milima miwili,alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).

Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je,tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”

Akasema:“Yale ambayo Allah swt  wangu amenimakinishia ni bora  (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”

Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.”

Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.

Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Allah swt  wangu.Na itakapofika ahadi ya Allah swt  wangu ya kufika Qayama),atauvunjavunja.Na ahadi ya Allah swt  wangu ni kweli tu.”

 

Maumbile ya Yajuj na Majuj

Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vyenye miguu minne na wakifanana na wanaadamu kisura na wao walikuwa ni wafupi mno mbele ya watu wa zama hizo. Na watoto wao walikuwa wakizaliwa kama watoto wa wanaadamu na walikuwa hawakui zaidi ya shubiri tano na sura zao zilikuwa aina moja na walikuwa wazururaji. Kwa kuwa ngozi zao zilikuwa ngumu kama zile za ngamia, hivyo hawakuathirika kwa baridi wala joto. Walikuwa na makucha makubwa na meno makali na masikio yao yalikuwa marefu kiasi kwamba walikuwa wakitandika moja na kujifunika kwa la pili. Walikuwa wakiingiliana kama wanyama na chakula chao kikubwa kilikuwa ni samaki kwa sababu kulikuwa kukinyesha mvua za samaki, na kama kulikuwa na kasoro ya samaki basi walikuwa wakishambulia miji na kuchafua na kuvuruga kila kitu kiasi kwamba watu walipokuwa wakizisikia sauti zao, walikuwa wakikimbia na kuacha makazi yao kwa sababu ilikuwa ni vigumu mno kuwakabili kwani walipokuwa wakiingia mijini basi miji yote ilikuwa ikijaa wao tu. Idadi yao ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ajuaye isipokuwa Allah swt . Wao walikuwa hawafi hadi wamezaa watoto zaidi ya elfu moja.

 

Katika vitabu tunapata habari zaidi kuwa Yajuj na Majuj ni makabila mawili yaliyokuwa makubwa kutokana na kizazi cha Yafus, mwana wa Mtume Nuh a.s. Na katika Agano la Kale, Majuj anaelezwa kuwa ni Chifu wa Mashech na Tunal. Kwa sasa Moscow ndio mto unaosimama mji huo,uitwao Moscow, mji mkuu wa Urusi; Tabul ni mto huko Urusi ambapo kuna mji Tobolsk.

 

Katika historia tunapata kujua kuwa Bwana Dhulqarnain alikuwa ni mtoto wa mama mdogo wa Mtume Khidhr a.s. na utawala wake ulienea 3457 baada ya Mtume Adam a.s. kuja humu duniani, na katika mwaka 3460 aliujenga ukuta huo kwa ajili ya kuwazuia Yajuj na Majuj, na katika 3470 alikutana na Mtume Ibahim a.s., na kwa muda wa miaka 40 alikuwa akizunguka duniani na hatimaye katika umri wa miaka 500 yaani 3497 tangu Mtume Adam a.s. aje humu duniani yeye alifariki akaaga dunia na amezikwa katika Makka Al Mukarramah.

 

MWISHO

 


SHAYTANI  WASWAS-KHANNAS

 

Katika tafsiri 'Majmaul Bayaan' na 'Al-Miizan fi Tafsiril Quran' Juzuu ya nne na Juzuu ya ishirini uk. 398 ya ‘Allamah  Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai. Chapa ya pili 1974 Beirut. Ipo riwaya ifuatayo juu ya Istighfaar:

Baada ya kuteremka kwa Aya 3:135, Sheitani alikuja Makkah na kupiga sauti kubwa mno juu ya mlima Thur, ambayo iliwafanya mashabiki wake wote wakusanyike, nao walipokuja walimwona huyo amezongwa na mushkeli mkubwa sana na hapo hawakusita kumwuliza: "Je umekuwaje na hoja gani ya kutukusanya hapa?"

 

Akajibu:

“Imeteremka Aya isemayo kuwa Ummah wa Muhammad utasamehewa kabisa madhambi yake na masharti ya Tawbah yaliyokuwa yamewekewa Ummah yaliyotangulia, yameondolewa kwao.  Na iwapo sisi hatukubuni mbinu dhidi yake, basi juhudi zetu zote za kuwapotosha hazitakuwa na athari yoyote kwani wao watakapofanya Tawbah, madhambi yao yatasamehewa yote kwa pamoja na hata kubadilishwa kuwa matendo mema."

 

Kwa hivyo nimekuiteni hapa ili tutafute mbinu za kukabiliana na swala hili ama sivyo sisi hatutakuwa na kazi yoyote ile."

 

Kila mmoja wao alitoa mpango wake aliinuka mmoja wa Masheitani, akasema:  "Nitafanya hivi na vile."  Lakini hawakukubaliana naye, nao wengine pia walisema walivyokuwa wakiona, nao wote walikwenda wakipingwa mmoja baada ya mwingine.

 

Na hapo akainuka Waswas - Khannas, naye akasema: "Nitawatia watu katika hatia (madhambi) na papo hapo nitawasahaulisha Istighfaar (Tawbah) na nitawaambia kuwa :

"Ewe binadamu! Bado unao muda mwingi wa kufanya Tawbah, haraka ya nini?  Huu ndio muda wako wa kustarehe na kufaidi umri wako! Siha yako na vile nguvu zako zinakuruhusu ufanye hivyo, hivyo starehe hadi utakapokuwa mzee, utafanya Tawbah kiasi utakacho!”

 

Kwa hayo, Masheitani wote walifurahi mno na yeye Khannas alikabidhiwa kazi hiyo hadi kufika siku ya Qiyama.

 

 (Tafakari Sura an-Naas, 114, Ayah 1-4 :

Sema: Ninajikinga kwa Allah swt  Mlezi wa wanaadamu,

Mfalme wa wanaadamu,

Mungu wa wanaadamu,

Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas.

 

Hizi ndizo wasiwasi za Sheitani ambazo huwapotosha watu wengi hasa vijana ambao hudhani kuwa wao bado wanao umri mrefu wa kufanya Tawbah hapo mbeleni. Sisi twachukulia uzee ndio wakati wa kufanya Tawbah, lakini nani anayejua kuwa uzee huo ataufikia au atakufa kabla yake.  Je siku hizi hatuoni kuwa wazee ndio waliobakia hai ambapo vijana wamekufa kwa magonjwa kama ukimwi? Na magonjwa mengine ambayo hayana hata muda wa kuyashughukikia vyema kama homa ya uti wa mgongo, n.k. Kwa hivyo fanya lile uliwezalo leo badala ya kungojea kesho, kwani unaweza kuugua vibaya sana na hata kufa! Jambo linalotubidi kujiambia ni :

"Sielewi ni lini mauti yangu itanifikia na kunichukua, labda hata sasa hivi ipo mgongoni mwangu ikinichukua, hivyo ni aibu kufika mbele ya Allah swt  huku nimejitwisha mzigo mzito wa madhambi bila ya kufaidi fursa ya Tawbah!"

 

Je, ndugu zangu, Imani yetu haipo hatarini?  Labda tukafa mauti isiyo ya Islam na ambapo Allah swt  anatuambia tusife ile tukiwa Waislamu! 

 

Quran Tukufu inatuambia katika Sura ar-Ruum, 30, Ayah 10:

Kisha ubaya ndio ulikuwa mwisho wa wale waliotenda uovu, kwa kukadhibisha Aya za Allah swt , na kwa haya walizoea kudhihaki. 

 

Vile vile twaambiwa katika Sura Aali Imraan, 3, 132:

Na harakisheni kwa (njia ya kujipatia) Maghfirah kutoka Allah swt  wenu! 

 


 

MI’RAJ – UN – NABII

 

Qur’an Tukufu, Surah Bani – Israil, 17, Ayah:1

Kwa jina la Allah swt Mwingi wa Rehema na Ne’ema.

“Utukufu ni wake Yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku (mmoja tu ) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Mugaddas-Falastini) ambao  (tumeubariki na ) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake. (Tulimpeleka hivyo) ili tumwonyeshe baadhi ya Alama zetu.

Hakika yeye Allah swt ni mwenye kusikia (na ) Mwenye kuona.

 

 

Umri wa Mtume Muhammad Mustafa bin ‘Abdullah s.a.w.w. ulikuwa ni  miaka 52 ambao ni mwaka wa pili kabla ya Hijrah au ni mwaka 621 A.D.

 

Huko Makka, tarehe 27 ya mwezi Rajab katika mwaka kumi na mbili wa Utume wake, wakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. baada ya sala zake za usiku katika nyumba ya binamu wake, binti wa Abu Talib a.s. aitwae ‘Umma Hani na ambapo wote waliokuwa nyumbani walikuwa wamelala, mara Malaika Jibraili a.s. alitokezea na kuja kwake na kumchukua hadi Al-Ka’aba Tukufu huku akiwa amemwendesha Farasi mzuri, mwenye uso kama wa Kibinadamu mwenye mabawa meupe, aliyeitwa Buraq na limwelekeza hadi huko Jerusalemu ambako wao waliutembelea Msikiti. Baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuongoza sala ya Mitume iliyokuwa imemtangulia, yeye tena alipanda Farasi wake na alichukuliwa hadi Jannat ( Peponi ) na vile vile kuyaona yale matisho ya Jahannam ( Motoni ).

 

Miongoni mwa zile Nuru za Hidaya za kudumu alizopata kutoka kwa Allah swt, alipewa mafundisho na maamrisho mapya na ile amri ya kusali sala tano za kila siku kwa ajili ya ‘Ummah wake, yeye aliliona jina lake pamoja na jina la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. likiwa limeandikwa katika Kalimah:

‘Hakuna mungu mwingine illa Allah swt na Muhammad ni Mtume Wake na ‘Ali ibn Abi Talib ni Khalifa baada yake.’

 

Baada ya kuonyeshwa hayo yote yaliyo kuwemo Jannat ( Peponi ), na Jahannam (Motoni) basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alirudishwa hapo nyumbani mwake, alitambua kuwa kuweko kwake nje kulikuwa ni kitambo tu. Huu usiku wa safari unatambuliwa kama Lailat-al-Mi’raj au Usiku wa Mi’raj ambavyo vile vile imelezwavyo katika Qur’an Tukufu, Surah Bani – Israil, 17, Ayah:1

Kwa jina la Allah swt Mwingi wa Rehema na Ne’ema.

“Utukufu ni wake Yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku (mmoja tu ) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Mugaddas-Falastini) ambao  (tumeubariki na ) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake. (Tulimpeleka hivyo) ili tumwonyeshe baadhi ya Alama zetu.

Hakika yeye Allah swt ni mwenye kusikia (na ) Mwenye kuona.

 

Haistahiliki kwa Mwislamu yeyote yule kuwa na shaka kuhusu tukio hili. Kuna alama ya miguu ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. yuu ya jiwe la Msikiti wa Jeruslem, ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipopandia yule Buraq kuelekea mbinguni. Msikiti ulijengwa na jiwe ambalo bado lipo papo hapo.

 

Je ‘Ayesha na Mu’awiyah walikuwapo wakati wa Mi’raj ?

Hata hivyo kuna shakhsiya zingine ambao wao walikuwa hawakukubali yale yaliyokuwa yamesimuliwa na Allah swt kuhusu hii safari yake ya kwenda mbinguni mbali na kuthibitishwa na Qur’ani Tukufu. Nao ni Ayesha binti Abu Bakr, mkewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mwingine ni Mo’awiya, mwana mashuhuri wa Abu Sufiyan.

 

Natumaini kuwa kwa kueleza mambo hapa hakutanifanya mimi kujisahau yale niyazungumzayo. Wakati wa Mi’raj ulipokuwa, Ayesha alikuwa na umri wa miaka saba (7) tu na ambavyo alikuwa bado chini ya malezi ya wazazi wake na wala siyo kuwa alikuwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.; lakini yeye alikabidhiwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. baada ya miaka miwili aliyofuatia baada ya hayo kutokea huko Medina. Mzazi wake Ayesha, Abu Bakar, ingawaje nafsi yake mwenyewe alikuwa anaamini na kuwa na uadilifu juu ya Mi’raj .

 

Mu’awiya alikuwa bado hakuzaliwa wakati wa Mi’raj. Alizaliwa mwaka mmoja baadaye (katika mwaka ule ambao Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijisitiri katika mapango) walipokuwa wameamua wazazi wake ambao walikuwa maadaui halisi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika nyakati hizo. Yeye alikuwa Mwisalmu kiasi cha miaka kumi baadaye.

 

Yafuatayo ni meelezo zaidi yaliyo kuwa mengineyo yamekusanywa kuhusu safari hii ya usiku ya Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., aliyoandikwa na W. Irving katika kitabu chake cha ‘Life of (Mtume) Muhammad Mustafa s.a.w.w.’ hasa kufuatana na maelezo ya Al-Bukhari, Abul Fida ambavyo ni kwa ajili ya manufaa kwa wasomaji ili kupata kujua zaidi.

 

Kisa cha Mi’raj …

Wakati wa masaa za katikati za saa za usiku, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  aliamshwa na sauti iliyokuwa ikisema, “Amka, wewe uliyelala!” Mkuu wa Malaika wote, Farasi mweupe mwenye umbo la ajabu kabisa na sifa za ajabu zake ambavyo yeye Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa hajawahi kumwona hata (kabla) wakati mmoja katika maisha yake yote hayo hapo awali; na kusema ukweli, huyu farasi anatofautiana kabisa na farasi wengineo kwani hakuwanazo dosari zozote zile kulinganishwa na farasi wengineo wa kawaida. Farasi alikuwa na uso wa kibinadamu lakini mashavu yake yalikuwa ya ki-farasi; macho yake yalikuwa kama mekundu-manjano (kama jiwe lenye thamani sana) na macho yakiwa yakimetameta kama nyota. Alikuwa na mabawa ya furukombe zote zilikuwa zikitoa miale ya nuru; mwili wake ulikuwa umejaa johari na majiwe mazuri na vyenye thamani. Kutokana na ule mwendo wake wa kasi kabisa basi aliitwa Buraq au Radi (mwale wa nuru).

 

Mtume kusali Mlima Sinai …

Mnyama alimjongelea na kujituliza ili akaliwe, na alirudi kupaa akiwa amekaliwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mgongoni mwake, basi alipaa hadi kufikia juu kabisa, juu ya milima ya Makkah. Hawa walivyopita ni kama radi baina ya mbingu na ardhi, basi Malaika alitoa sauti kwa nguvu; ‘Simama; Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.: rudi ardhini na usalishe sala.” Wao waliteremka juu ya ardhi na baadaye kumaliza sala ….” Oh rafiki na mpendwa sana wa roho yangu; alinena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., “Kwanini umenitaka nisali hapa?”. “Kwa sababu ni Mlima Sinai, ambako Allah swt  alikuwa akiongea na Mtume Musa a.s.”

 

Mtume asalisha Baitul Muqaddas …

Wakiendelea na safari yao hiyo walifika katika lango la msikiti wa Jerusalem, ambako kutokana na Nuru ya Buraq, yeye alipitiliza hadi kule kuingia msikitini yeye aliwaona Mitume Ibrahimu, Musa na Isa a.s. na wengineo wengi. Baaada ya yeye kusalisha sala pamoja nao, mara Nuru iliteremka toka mbinguni ikiwa katika hali ya ngazi ambayo ncha yake ya mwisho uligusa na kuegemea juu ya Shakra au jiwe la Msingi la nyumba tukufu, ilikuwa ni jiwe la Yakub. Akisaidiwa na Malaika Jibraili a.s. basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliipanda ile ngazi ya nuru kuendelea na safari yake.

 

Kuwasili mbingu ya kwanza

Baada ya kufikia mbinguni ya kwanza, Malaika Jibraili a.s. aligonga kilango.

Je yuko nani? Sauti iliuliza kutoka ndani. ‘Malaika Jibraili a.s. “Je uko na nani pamoja?”. “Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w..” “ Je yeye ameshaupokea Utume wake?” “Ndiyo ameshaupokea.” “Basi anakaribishwa!” Na ule mlango ulifunguliwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipojongea ndani tu, mtu wa Kale sana alimkaribisha, na Jibraili a.s. alisema, “Huyu ni baba yako Adamu a.s., mtolee heshima.” Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alifanya hivyo na Mtume Adam a.s. alimkumbatia, huku akiwa akinena kuwa mkuu wa wana wake wote na mkwanza wa Mitume yote. Katika mbingu hii ya kwanza, kulikuwa na wanyama waliokuwa na kila aina ambao walikuwa ni Malaika ambao waliomba kuwa kama wale wanyama waliomo ardhini. Miongoni mwao alikuwa ndege mwenye urefu wa mshangao ambaye kishungi chake kilikuwa kikigusa mbingu ya pili, ingawaje ni safari ya miaka mia tano kutokea ile ya kwanza. Huyu ndege wa ajabu alikuwa anaimba kila siku kwa sauti yake tamu kila asubuhi. Wanyama wote juu ya ardhi, humsaidia binadamu; na wanaamshwa na sauti yake na wale ndege wote wa namna au kundi lake pia wanafuatisha sauti zake.

 

Ndege wa namna huyo huyo ameelezwa, anavyosema Dr. Prideaux, katika Bava-Bartha cha kitabu cha mafundisho cha Babyloi cha aliyeitwa ‘Zig’, ambaye alisimama juu na miguu yake juu ya ardhi na kulifunika jua lote na hivyo kulisababisha kupatwa kwa jua kikamilifu. Huyu ndege Chaldee kulingana na ufafanuzi juu ya kazi inatuelezea kuwa huwa anawika kila asubuhi, na Mola huwa anampa busara kutokana na kazi hiyo.

 

Kuwasili mbingu ya pili

Sasa wao walifika katika mbingu ya pili. Jibraili a.s. kama hapo awali alibisha hodi, maswali na majibu yalimiminika kama hapo awali, mlango ulifunguliwa nao waliingia humo. Huko wao walikutana na Mtume Nuh a.s., ambaye, alimkumbatia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na alimchukua na kumsifu kuwa alikuwa Mkuu kuliko Mitume yote iliyomtangulia.

 

Kuwasili mbingu ya tatu

Walipofikia mbingu ya tatu, waliingia kwa shangwe hizo hizo. Hapa alikuwa malaika ambaye hapimiki kwa ukubwa, ambaye macho yake yalikuwa mbali na nyingine kiasi cha safari ya siku elfu sabini. Yeye alikuwa na vikosi mamia ya maelfu ya watu ambao waliokuwa wakisubiri amri yake. Mbele yake kulikuwa na kijitabu kikubwa kweli kweli ambamo yeye kila mara alikuwa ameshughulika na kuandika na kupekua pekua na kufutia mbali mengineyo. Malaika Jibrail a.s. alimweleza kuwa: “Huyu, Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.” aliendelea Jibraili a.s.“Ndiye Izraeli, Malaika wa vifo, ambaye yuko katika amri ya Allah swt. Katika kitabu chake hicho yeye alikuwa anaandika tu kila wakati majina ya wale waliokuwa wameshamaliza maisha yao, yaani wale waliokwisha kuhitimu maisha yao au kufikia wakati wao na ambao wanafariki papo hapo.

 

Kuwasili mbingu ya nne

Na hapo baadaye, wao walifikia sasa mbingu ya nne. Miongoni mwa wale Malaika waliokuwamo huko. Kulifikia sasa mbingu ya nne. Miongoni mwa wale Malaika waliokuwamo huko, kulikuwako na malaika mmoja ambaye akianziwa kuanzia Mbinguni hadi kichwani kunachukua muda wa miaka mia tano. Uso wake ulikunjika na ya kusumbulika na mito ya machozi yaliyokuwa yakitiririka tokea machoni mwake. “huyu,” alisema Malaika Jibraili a.s., “ni malaika wa machozi, ameteuliwa kuwachunguza wana wa Adamu wanavyotenda madhambi na kuwabashiria maovu yanayowasubiri.”

           

Kuwasili mbingu ya tano

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokelewa na Mtume Harun a.s. na huku akipongezwa na wale Malaika wa kuadhibu ambao wanaishi huko na ambao huwa wanautawala moto. Kulingana na Malaika wote ambao walionwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Malaika mmoja tu ambaye alikuwa anatisha sana kuliko wote wenzake. Uso wake ulikuwa wa shaba, alikuwa amevikwa au kufunikwa na mauvimbe na visugu. Macho yake yalikuwa yaking’ara kama radi na alikuwa ameudaka moto. Yeye alikuwa amekalia kiti kilichokuwa kimezungukwa na moto, na mbele yake kulikuwako na minyororo miekundu kwa sababu ya moto. Kama yeye akifika ardhini basi milima yote itayeyuka, maziwa na bahari yatakauka na viumbe vyote vitakufa kwa vishindo vyake. Kwake yeye na  Malaika, mawaziri wake, ndiko walikopewa amri ili kuteremsha ile adhabu ya Mola kwa ajili ya wale makafiri na watenda madhambi.

           

Wakiacha yale ya kutisha hapo, waliwasili mbingu ya sita.

Walipofika mbingu ya sita, hapo palikuwa na Malaika mkubwa kabisa na ambaye nusu upande alikuwa ni theluji ya nusu upande mwingie alikuwa ni moto; na katika hivyo hiyo theluji na nusu upande mwingine alikuwa ni moto; na hata hivyo hiyo theluji haikuyeyuka hata moto pia haukuzimika Wakimzunguka huyo malaika wengi sana walikuwa wakisema: “Ewe Allah swt ! Ambaye ameviunganisha moto na theluji; waunganishe wale watawa wako wote katika utekelezaji wa amri zao.” ‘ Huyu’ alisema Malaika Jibraili, “ni mlinzi na mlezi wa Malaika wa mbinguni na ardhini.” Hapa palikuwa na Mtume Musa a.s., ambaye badala ya kumkaribisha kwa furaha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kama walivyokuwa wamefanya Mitume mingine iliyomtangulia, yeye, alilia sana

 

Na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwona aliuliza

“Je nini kinachokuliza?”

 

 

Mtume Musa a.s. alijibu:

“Kwa sababu tu kuwa mimi niko na mrithi wenu, ambaye ametumwa ilikuwarekebisha watu wa taifa lake kuingizwa huko Jannat (Peponi ) kuliko hata mimi nilishindwa kutimiza na kufikia kwa ajili ya hao wapotofu wana wa Israili.”

 

Kuwasili mbingu ya saba.

Alilakiwa na furaha nyingi na Mzee Mkuu mwenye heshima, Mtume Ibrahim a.s. Hapa pamejaa mwanga wa Nuru na kudura ya Allah swt, usifa wake ambao kwa kweli ulimi wala mdomo wa mtu hauwezi kuuelezea. Mmoja wao tu atosha kutupa mwangaza juu ya wengineo tutakavyowafikiria. Yeye amegawa dunia katika mistari mirefu sambamba, na alikuwa na vichwa elfu sabini, na kila kichwa kilikuwa na midomo elfu sabini, na kila mdomo ulikuwa na ndimi elfu sabaini; na kila ulimi ulisema lugha elfu sabini mbalimbali; na yote haya yaliyokuwa yakisemwa yalishughulika na kumsifu Allah swt!”

 

Wakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikaa huku akishika tama kuhusu huyu kiumbe, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mara kwa ghafla alivutiwa na mmea uliokuwa Myungiyungi ambao uliitwa Sedrat, ambao unanawiri vyema kwa upande wa kulia wa kiti cha Enzi cha Allah swt. Matawi yake yalisambaa zaidi ya umbali wa kati ya jua na ardhi. Malaika zaidi ya hata mchanga wa pwani au kingo za mito, wanafurahi chini ya kivuli cha mti huo. Majani yake ni sawa na masikio ya tembo kwa ukubwa ambako hujazana ndege mbalimbali na wote wakiwa wanasoma zile aya za Qur’an Tukufu. Matunda yake yalikuwa ni meupe kuliko maziwa na matamu, moja tu lingelitosha wote kwa chakula chao. Kila mbegu ilikuwamo na Mwanamwali mzuri au Hur al-‘ain mwenye kuwaongoza wenye Imani huko Jannat ( Peponi ).

 

Al-Ma’mour

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mwongozi wake waliongozana hadi kufikia Al-Ma’mour au Nyumba ya kusujudia, lililokuwa na sifa sita kupendeza sana; ambalo lilijengwa kwa majiwe manjano-mekundu au mawe ya vitu vyekundu vya thamani; ikiwa imezungukwa na taa chungu mzima zilizokuwa zikiwaka. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia ndani, alikaribishwa kwa vyungu vitatu, kimoja kikiwa kimejaa pombe, ya pili maziwa na ya tatu asali. Yeye alilichukua chungu la maziwa na kuyanywa. “Vyema kabisa ulivyofanya ndilo chaguo jema sana,” alinena Malaika Jibraili a.s.. “Kama ungalikunywa pombe basi watu wa ‘ummah yako wangali potea. “Nyumba hiyo tukufu inalingana kabisa na ile Ka’aba ambayo iko Makkah, na ipo juu ya mbingu ya saba moja kwa moja juu yake.

 

Walikuwapo wakati huo wakifanya Tawaf yaani kulizunguka jumba hilo mara saba ambapo ndipo naye Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  alijiunga nao.

 

Sasa umefika wakati ambako Malaika Jibraili a.s. hawezi tena kusonga mbele kwani hapo ndipo palipokuwa  kikomo chake. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. sasa aliendelea peke yake, mwepesi hata kuliko mawazo, uwanja mkubwa, akipitia eneo mbili zenye kuwaka taa na moja giza tupu. Kutokezea hapa gizani yeye alijiwa na wimbi la ukimya na uoga wakati alipojiona yuko amesimama mbele ya Allah swt . Lakini alishukuriwa mara mbili kutoka kiti cha Enzi. Alihisi kuwa alijawa na wimbi la furaha ambayo ndiyo kulivyofuata, wakati mzuri na manukato yalinusika pote mzungukoni ambavyo hakuna mwingine ambaye anaweza kuelewa ila yule tu ambaye yuko mbele yake – Allah swt .

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa sasa alipata kutoka Allah swt zile Imani ambazo zimeelezwa na kuambatanishwa katika Qur’ani Tukufu; na sala tano za siku zilielezwa kuwa ni fardhi ya waumini kuzisali.

 

Kwa kuishikilia ile ile ngazi ya Nuru ambayo iliyokuwa imemleta hadi mbinguni ndiyo aliyoshukia nayo hadi katika Msikiti wa Jeruslem, ambako alimkuta Buraq akiwa amefungwa kama vile alivyokuwa amemwacha; na mara alimpanda na kurudishwa nyumbani mwake wakati ule ule na pale pale ambako alikuwa amechukuliwa na Malaika Jibraili a.s..

 

Maelezo yote haya yanayoelezwa hapo juu kuhusu hii safari ya usiku ni kufuatana na maneno yaliyonenwa au kuelezwa na wana historia mashuhuri kama vile Abul Fida, Al-Bokhari na vile vile yameelezwa kwa mapana zaidi sana na Irwing katika chacke cha ‘Life of Muhammad’ kilichoandikwa katika lugha ya Kiingereza.

 

Safari hii yenyewe imefungua mlango wa mabishano na maoni mbalimbali na chuki miongoni mwa wasomi. Baadhi yao wamethibitisha kuwa hakuna chochote zaidi ya ndoto za usiku au ni mawazo tupu; na hujikinga na kujiunga mkono kwa kunakili zile habari za mapokeo ya Ayesha kuwa kiwiliwili chake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kilikuwa vile vile bila ya kutingishika na kwamba ni ki-roho tu ambavyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alifanya hiyo safari ya usiku – Mi’raj.

 

Kwa kuelezea haya maelezo ya mapokeo, nasikitika sana kwani wao (hao wanaosema) hawakufikiria wala kuwaza na vile vile hawakuchunguza, ni kwamba wakati hiyo safari ilipotokea, ‘Ayesha alikuwa bado yu mtoto na ingawaje alikuwa ameposwa, lakini bado hakuwa mkewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na hivyo alikuwa bado nyumbani kwa babake mzazi – Abu Bakar.

 

Wengine husema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alifanya safari kimwili. Kulingana na Ahmad bin Joseph, safari ya usiku huko Msikitini (Jeruslem) imehakikishwa na mtu Mzee mwenye heshima, mkazi wa Jeruslem. “Wakati huo,” amesema yeye, “ ambapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipotuma ujumbe kwa Mfalme Heraclius, huko Costantinopole, akimwalika kuukubali Uislamu, basi huyu mzee alikuwako hapo pamoja na Mfalme. Huo ujumbe ulipoelezea kuhusu ile safari ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ya usiku, basi yule mzee alishikwa na maajabu makuu, na yeye huyo mzee alimwelezea Mfalme vivyo hivyo yule mfalme kama vile walivyoelezea wale wajumbe. “Hiyo ni tabia yangu ,” alinena Mzee “ilikuwa ni mwiko kwangu mimi kulala kabla ya kufunga milango yote ya Msikitini. Katika usiku ambao unaelezwa, mimi nilifunga milango yote isipokuwa mlango mmoja tu ambao uligoma kufungika. Kutokana na hayo, mimi niliwaita mafundi seremala ambao baada ya kuufugua vyema ule mlango, walinihakikishia kuwa kizingiti chake juu ya mlango na jumba lenyewe yamepishana katika nyuzi upimo mkubwa ambavyo ilikuwa ni zaidi ya nguvu za kuweka kuufunga mlango huo. Na hivyo mimi nililazimika kuuacha wazi. Alfajri na mapema, palipokucha, mimi nilipatembelea hapo na kuwepo hapo, na pale pale palipo kuwa pamewekwa jiwe lilikuwa limetobolewa na kulikuwa na dalili za alama ya kufungwa kwa Buraq zilithibitika. Hapo ndipo mimi nilisema, kuwa huu mlango usingelikuwa umebandikwa kama kusingelikuweko na kuzuru kwa Mitume kwa ajili ya Sala.”

 

Habari zingine zanakili kuwa wakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokuwa akielezea ‘Ummah juu ya safari yake hiyo ya usiku huko Makka, basi wengi walikuwa wakionekana wakiamini na wengineo walikuwa na kigeugeu ambapo wana wa Qureisha walivunjika mbavu kwa vicheko na huku wakimdharau. “Amesema kuwa ati yeye alikuwa katika Msikiti wa Jerusalem!?” Alibweka Abu Jahal; “Athibitishe maneno yake kwa kutoa ushahidi hai na maelezo yake. “Kwa muda huo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alighafilika kwa sababu yeye alikuwako huko Msikitini usiku ule ambamo vilikuwa havionekani, na mara kwa ghafla alitokea Jibraili a.s. ubavuni mwake na kuyaweka yale yote yaliyotokea ule usiku mbele yake na hivyo ndivyo alivyokuwa ameweza kuyajibu maswali hata madogo kabisa.


                                                 D A J J A L

 

Ni neno la Kiarabu likimaanisha mhaini mkubwa na mleta balaa kubwa mno.Hivyo wale wote walio wahaini na waleta balaa basi wajijue kuwa wao pia na ma-Dajjal wa zama zetu hizi.Lakini Dajjal anayezungumziwa hapa ni yule ambaye anaitwa Sayyid na utambulisho wake ni Dajjal.Yeye atakuwa ni mchawi mkubwa.Hapo mwanzoni atakapojitokeza atadai kuwa yeye ni mtume na baadaye atajiita kuwa yeye ni mungu.Yeye atatokezea pale ambapo Mashariki ya kati itakuwa imekwisha dhoofika kwa sababu ya ukame utakaodumu kwa miaka mitatu kwa mfululizo. Katika mwaka wa tatu kutakuwa hakuna dalili ya majani na hakutakuwapo na mvua kabisa.

Hili jitu lenye jicho moja litakuwa na urefu wa mita ishirini. Jicho lake la kulia litakuwa halifanyi kazi na litakuwa kama donge la nyama nyekundu.Jicho lake la kushoto litawaka kutokea paji la uso.Yeye atakuwa akimwendesha punda mwekundu, mwenye manywele ambaye miguu yake itakuwa mieusi kutokea mifupa ya juu hadi magoti na nyeupe kutokea magoti hadi makwata. Kutasikika sauti ya muziki kutokea nywele zake na za punda wake.

 

Watu wanyonge,wanawake,Mabedui wa Kiarabu na Kiyahudi watamtii na kumfuata. Dajjal mwenyewe atakuwa Myahudi wa asili ya ukoo wa Qutama na kwa kutokana na udugu wa Abu Yusuf. Kwa hakika watu watamkubalia kama mtume (ingawaje atakuwa ni mzushi) .

 

Kwa kupatiwa msaada wa wanajeshi sabini elfu wa Kiyahudi na wenye silaha na matayarisho yote,yeye ataeneza kila mahala hali ya dhuluma na  uoga.Mioyo ya watu itajawa kwa khofu na hatari. Wakati huo,Jerusalemu ndio itakapokuwa mahala pa usalama kwa sababu Mtume  Issa  a.s. atateremkia. Imam Mahdi  a.s. atafika hapo pia. Hapo kutatokea vita vikali na Mtume Issa a.s. atamwua Dajjal.Wayahudi wataangamizwa.Ulaji wa nyama ya nguruwe utaachwa.Hakutakuwapo na alama za Msalaba.Na hapo kutakuwapo na Dini moja tu duniani -- ISLAM.

 

Mapokezi yafuatayo yametolewa kutoka Kitabu cha Kamal-ud-Din ambamo Muhammad Ibn Ibrahim anarikodi kama Hadith sahihi iliyopokelewa na Ibn Sabra,anayesema:

 

"Wakati mmoja Imam Amir-al-Mominiin Ali ibn Abi Talib  a.s. alituambia hivi:

 

Sifa zote ni za Allah swt na Salaam ziwe juu yake Mtume Mtukufu s.a.w.w.,na baadaye aliendelea kusema: "Niulizeni kile mukitakacho..."

 

Saasaan ibn Suhan aliinuka na kuuliza "Ewe Mawla wetu! Naomba utuambie ni lini atakapotokezea Dajjal.

 

Imam Ali a.s alimwambia aketi na kumjibu. Saasan aliketi na Imam Ali a.s. alianza kuelezea:

 

"Allah swt amekusikiliza na anajua kile ukitakacho.Zitapita dalili moja baada ya nyingine.Je niwaambieni ?"

 

Watu waliokuwapo walisema: "Naam tunaomba hivyo, Ewe Abul Hasan ! "

 

Imam Ali ibn Abi Talib  a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake, (1) watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa. (2)Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi (3)Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi (4)  Waislamu wataanza kuchukua riba (5) Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida (6) Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa (7 Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia  (8)Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao [4](9)Wanaume watawataka wanawake ushauri na uongozi (10)Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu (11) Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida [5](12) Mauaji na umwagaji wa damu utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe (13) Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na  wadhalimu watakuwa wenye nguvu.(14).Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu (15) Wasufi na wasomaji wa Quran watakuwa wapumbavu (16) Kutakuwa kukitolewa ushahidi  wa kughushiwa (17) Quran Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu (18) Misikiti itakuwa ikijengewa minara mirefu (19) Watu waovu watakuwa wakiheshimwa (20)Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao (21) Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale (22) Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume wao  kwa uroho wa mali (23) Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana. (24).Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu (25).Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa (26) Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji (27).Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi. (28).wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.(29).Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke)na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme[6].(30).Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea (31).Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.(32) Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .(33) Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko  kitu chochote kile (34) Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.

Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema "Ewe Bwana,naomba utwambie Dajjal atakuwa ni mtu wa aina gani?"

Imam Ali a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.(35).Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.(36).Jua litakuwa pamoja naye.(37).Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.(38).Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,(39) Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.

(40)Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal yatakauka hadi siku ya Qayama,(41).baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."

(42).Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.(43)Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa,(44) wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,(45) huyo Dajjal atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria, atauawa siku ya Ijumaa mchana,(46) Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam Mahdi a.s.(47)  na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

 

 

 

 

 


 

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA

                            AMIRALY  M. H.  DATOO  - P.O. Box  838 

                                         BUKOBA TANZANIA

                                     e-mail : datooam@hotmail.com

Na unaweza kuvipata katika Internet katika :

                                 http://www.al-islam.org/kiswahili

 

1.    UHARAMISHO WA KAMARI

2.    UHARAMISHO WA RIBA

3.    UHARAMISHO WA ULEVI

4.    UHARAMISHO WA ULAWITI

5.    UHARAMISHO WA  ZINAA

6.    UHARAMISHO WA UWONGO  (juzuu ya kwanza )

7.    UHARAMISHO WA UWONGO  (juzuu ya pili )

8.    USAMEHEVU KATIKA ISLAM

9.    TAJWID ILIYORAHISISHWA

10. KITABU CHA TAJWID

11. KESI YA FADAK

12. TAWBA

13. BWANA ABU TALIB a.s. MADHULUMU WA HISTORIA

14. FADHAIL ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

15. TADHWIN AL-HADITH

16. TAFSIRI YA JUZUU’ ‘AMMA

17. HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

18. MSAFARA WA AL-IMAM HUSSEIN IBN ‘ALI IBN ABI TALIB A.S MADINA – KARBALA

19. DALILI ZA QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.

20. NDOA KATIKA ISLAM

21. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 1

22. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 2

23. UWAHHABI – ASILI NA KUENEA KWAKE

24. HEKAYA ZA BAHLUL

25. SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

26. HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM

27. WAANDISHI MASHIA KATIKA SAHIH NA SUNAN ZA AHL SUNNA

28.  USINGIZI NA NDOTO

29. MAJINA KWA AJILI YA WATOTO WAISLAMU

30. QURBAA - MAPENZI YA WANANYUMBA YA MTUME S.A.W.W.

31.  TUSIUPOTEZE WAKATI

32.  DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA, KHUMS NA SADAQAH

33.  JANNAT NA JAHANNAM

34. MASIMULIZI YA HADITH KUTOKA QUR’AN

35. SADAQAH

36. JUMLA YA FAHRISTI YA AYAH YA QUR’ANI KIMAUDHUI



[1] Mimi nimekitarjumu kitabu kimoja katika kiswahili juu ya Maudhui haya Katika Islam Uharamisho wa ulawiti. Hivyo unaweza kusoma ukapata kujua ni kwa nini Uislamu umeharamisha ulawiti.

[2]  Vitabu vikuu vitukufu vya Allah swt  ni vinne.

    1. Tawrat  - Kilicho teremshwa kwa Mtume Musa a.s

    2. Zaburi – Kilicho teremshwa kwa Mtume Daud a.s.

    3. Ijili       - Iliyoteremshwa kwa Mtume Issa a.s.

   4. Qur'an Tukufu – Iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w.

 

Mitume mingi hawakupata vitabu hivi vitukufu lakini walikuwa wanapata vitabu vinavyoitwa Sahifa.

 

[3] Hapa jambo la busara tunalo ambiwa ni kwamba mfano wa jiwe hilo ni sisi binaadamu ambao kamwe hatutosheki kwa kidogo  wala haturidhiki kwa kingi wala hatukinai kwa kingi hadi hapo mauti itakapo fika ndipo matumaini yetu matamanio yetu yatakapokwisha. Tunaona kuwa leo mtu anataka kujilimbikizia mali na utajiri kwa kiasi alicho nacho hatosheki bali anataka kutafuta zaidi na zaidi kwa njia yoyote ile iwe halali iwe haramu yeye mradi  ajilimbikizie utajiri. Na Qur'an Tukufu anakumbusha kuwa tutakapofika kabirini ndipo hapo tutakaposhtuka kuona kuwa sasa ndio tumezinduka kutoka usingizini mwetu.

[4] Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!

[5]  Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya  mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya  misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.

[6]  Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6.30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza  k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.

Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.