DALILI ZA QAYAMA NA UBASHIRI   WA KUDHIHIRI IMAM  MAHDI  (a.s.)

  


 

KUJITOLEA.....

UTANGULIZI...

MANENO MACHACHE...

 

QAYAMAT  AU  SIKU YA HUKUMU.....

UBASHIRI WA KUJA KWA IMAM MAHDI  A.S....

KUANGAMIZWA KWA NCHI NA MIJI MBALIMBALI.

MITUME SITINI BANDIA...

VITA PAMOJA NA WEUPE NA MAANGAMIZO..

 

IMAM ALI A.S. AELEZEA UBASHIRI KUMI:.

UBASHIRI WA LAZIMA..

KUDHIHIRI KWA MTUME ISSA A.S. KUTOKA MBINGUNI....

UBASHIRI  WA  SIKU ZA MBELENI....

UDONDOZI KUTOKA VITABU VYA KIARABU...

JE WATURUKI NI AKINA NANI?....

MAWAIDHA YA MTUME S.A.W.W. KUHUSU KUJIHAMI..

KUONEKANA MKONO NA USO  MWEZINI...

Sufiani: kuinuka na kuanguka kwake....

 

MOTO..

MAAFA YATAKAYOWAFIKIA  WAISLAMU..

MUDA WA BINADAMU JUU YA ARDHI.

KUSHIRIKISHWA  KWA WANAWAKE.

MZOZO WA KUANDAMA KWA MWEZI....

ALA ZA MUZIKI....

WATU MATAJIRI.

GHUBA YA AQABA.

KUHUSU OMAN.....

KUHUSU TEHERAN......

 

UBASHIRI WA BAADA YA VITA VYA NAHARWAN....

HADITH  MUFADHDHAL...

WAKATI MAALUM.

MADONDOO YA KUDHIHIRI IMAM : KITAB AL- IRSHAD......

MAFAFANUZI WA DALILI NA BASHARA KWA MUKHTASARI.....

NDUGU WA MIRZA NA  MAAJABU YAO....

WAKATI WA KUDHIHIRI..

WATU WATAKAOMFIKIA IMAM a.s. BAADA YA KUDHIHIRI......

IMAM ALI A.S.  AFAFANUA  KUHUSU  WATU  313.....

MAJINA YA WAFUASI WA IMAM MAHDI A.S.....

KUONANA NA IMAM KATIKA KIPINDI CHA GHAIBAT...

 

MUKHTASARI WA DALILI.....

HALI YA WAIRAQI  NA VIKWAZO VYA HIJA....

  

UTHIBITISHO WA KUWAPO KWA  IMAM MAHDI  A.S  kwa mujibu wa wanazuoni wa ahli sunna   

  

KADIANI : MADHEHEBU YA MAAHMADIYA......

BABI, AZALI, BAHAI....

UBAHAI....

 INDEX...  

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

    

Kimekusanywa na Kutarjumiwa

       AMIRALY  M.H. DATOO

                BUKOBA - TANZANIA

 

 



KUJITOLEA

Safina ya msafara wa mwisho wa mwanadamu ipo inakaribia mwisho wake katika dimbwi la hatari ya imani yake potofu ya kuamini dunia hii tu bila ya kujali Aakhera. Uroho huu umeongezeka katika udanganyifu wetu wa kIssayansi kiasi kwamba mwanadamu anataka kuiendesha sayari ya Venus,Mwezi na Jua. Uroho huu umemfanya kiasi cha kuweza kusahau matatizo ya dunia yetu hii.

 

Mashabiki wa utamaduni wameudhalilisha ubinadamu kufikia tabaka la chini kabisa la shimo la aibu kiasi kwamba hata kilio cha Baba Adam a.s. pia kitakuwa kimelowana kwa jasho la udhalilisho.

 

Kidhahiri,dunia hii imejaa mwangaza lakini kiza cha ujahiliya kinaenea mbali na kwa mapana. Kizazi cha Shetani kimekwisha tayarisha mipango kamambe ya kulipiza kIssasi chake cha kudharauliwa na kizazi cha Mtume Adam a.s..Hali mbaya na machafuko ya matendo ya aina yote ya madhambi ndivyo vilivyosababisha kufungwa milango ya mwanadamu ya kuwa huru.Kivuli cha kiza kikubwa cha misiba ndiyo mambo yanayotia uchungu wa moyo juu ya ubinadamu.

 

“Lakini,mwale wa nuru moja tu wa matumaini katika janga hili la kutokuwa na matumaini ni ile nuru ya nafsi  yako (Imam Mahdi a.s.) ambayo ipo inang'ara  mbali na pazia isiyoonekana. Tunakuomba Ewe Imam Mahdi a.s.! Udhihiri haraka iwezekanavyo na kwamba ufupishe hayo masaa ya subira yetu kwa ajili yako wewe ingawaje kamwe hatuwezi kupoteza subira zetu kwa ajili yako.

 

Tuombee,udhihirishe yale yaliyo batini na uifanye nuru yako ing'arishe ulimwengu mzima.Dhihirisha maneno ya Allah swt kuwa "Allah swt ataikamilisha nuru yake hata kama makafiri watachukia".Udhahiri wako ndio dalili ya kuja kwa Siku ya Qayama lakini kutokuwapo kwako pia ni yenye maumivu kama Siku ya Mwisho. Wanaadamu tunaoathirika tunakuhitaji mno na mimi ninayo imani kamili ya kuja kwako na mwelekeo mwema katika kudhihiri na njia moja ya kukukaribisha, kwa kunyenyekea ninakitoa kitabu hiki"Qayamat-i-Sughra" mbele yako na natumaini kuwa utanikubalia mimi kama mtumwa wako na hakika hii itakuwa ndiyo uokovu wangu”.

 

Amiraly M.H.Datoo

Bukoba,  4 Januari 1996

UTANGULIZI

Qayamat -i- Sughra ni kitabu ambacho kinazungumzia mambo mengi hasa kuhusiana na ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s., jambo ambalo linakubaliwa na Waislamu wa Madhehebu yote kwa pamoja kuanzia mwanzoni hadi siku hii ya leo. Waandishi wa Kishiah wamefanya kazi kubwa mno katika swala hili na vile vile juhudi za waandishi wa Kisunni pia zinastahili pongezi kwani wao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuthibitisha waziwazi kuja kwa Imam Mahdi a.s..

 

Hivyo hapa chini munaletewa marejeo ya maandiko kutoka vitabu vya Kisunni:

1.

Jame'  Sahih

Muhammad ibn Ismail Bukhari

Ahadith

13

2.

Jame'  Sahih

Muslim ibn Hajjaj.

Ahadith

11

3.

Jame' Sahihain

Hamidi

Ahadith

2

4.

Jama bain Sihah Sitta

Zaid ibn Muawiya Abdari

Ahadith

11

5

Fadhail-us-Sahaba

Abdul Aziz Abkari

Ahadith

7

6.

Tafsir

Tha'labi   

Ahadith

5

7.

Gharib-ul-Hadith

Ibn Qataiba

Ahadith

6

8

Al-Firdous

Ibn Shirwiyah Dailami

Ahadith

4

9.

Musnad-i-Fatimah

Hafidh Abul Hasan Darqutni

Ahadith

6

10

Musnad-i-Ali

Hafidh Abul Hasan Darqutni

Ahadith

3

11

Al-Mubtada

KIssai

Ahadith

3

12

Al-Masabih

Husain ibn Masud Atra

Ahadith

5

13

Al-Malahim

Abul Hasan Manadiri

Ahadith

34

14

Kitabu cha Hafidh Ibn Mutayyan

 

Ahadith

3

15

Ar-Riaya-li-Ahlir Riwaya

Muhammad Ismail Farghani

Ahadith

3

16

Khabar-i-Soteh

Hamidi   

Ahadith

2

17

Istiab

Yusuf ibn Abdul Aziz Numairi

Ahadith

2

 

Katika karne hizi kumi na tatu kumeweza kutokea watu wachache ambao wanakanusha kabisa swala hili la kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. na idadi yao ni ndogo mno. Hapana shaka kuwa kuna watu ambao wanadai kuwa Yazid bin Muawiya bin Abi Sufiyan kuwa khalifa halali.Kunaweza kuwapo sababu mbili tu za kukanusha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.Moja,iwapo wao watakubali na kuthibitisha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s., basi kutakuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua shakhsiyah yake na nasaba yake,maisha na mienendo yake,n.k.hivyo mambo yote kama hayo yangalijitokeza mbele yao ambavyo wao wasingaliweza kufanya hila za kuzikubalia taarifa hizo.

 

Sababu ya pili ni kwamba kumewahi kutokezea watu waongo na ambao waliojiita Mahdi,hivyo watu walikwisha choshwa na wazushi hao kiasi kwamba hawataki kumkubalia Mahdi a.s. wa kweli. Na hii ni mbinu ya kukwepa tu ambavyo hoja kama hizi hazikubaliki katika Islam.

Kwa hakika sisi hatuwajali wale wote wanaomkanusha Mahdi a.s. kwa hoja zao zisizo na misingi wala faida. Lau hoja zao zingalikuwa halisi na za kimsingi basi kusingalikuwapo na Mahdi wazushi na wafuasi wao. Hapa sisi tunazingatia wale ambao wamejivika Umahdi katika miili yao isiyo toharifu. Kumekuwapo na Mahdi katika Banu Abbas,Banu Fatima,n.k. vile vile mabara yote ya Indo-Pak na Afrika imeshirikiana katika kupatikana kwao. Lakini historia imewakanyaga  Mahdi wengi waongo na wazushi.

 

Tabia na desturi ya mwanadamu imekuwa daima ikivutiwa na mitindo na mambo mapya,vivyo hivyo ndivyo hao Mahdi waongo ndivyo walivyoweza kufaidi na kuwavutia watu. Imesemekana kuwa wale wotakaomkimbilia Mahdi kwa pupa bila ya kuwa na maarifa kamili,basi wamepotoka - Halakal Mustaji'un!

 

Kwa hakika zipo Ahadith nyingi mno ambazo zilizo sahihi na kutegemewa kuhusu Imam Mahdi a.s. na hivyo hakuna mwanya wowote ule wa kutokezea Mahdi waongo. Lakini hao wazushi huwa watu wenye hila  ambazo wao hujihusisha na ubashiri fulani na huweza kujitangaza kuwa wao ni Mahdi. Kwa bahati mbaya,wale wote wenye ilimu ndogo wamekuwa daima wakiwakubali Mahdi kama hao na wakiwazunguka hadi kufa kwa Mahdi mzushi. Hivyo itakuwa ni vyema kwa kuchapisha habari kamili kuhusu Mahdi wa kweli ili mwanya wowote wa upotofu ufungwe kabisa. Faida ya pili ya uchapishaji kama huo utasaidia kuwapambanua Mahdi wazushi bila hata ya kutokezea magomvi na mafarakano.

 

Kwa mfano,kumekuwapo na kikundi kimoja ambacho kimedai kuwa Mtume Issa a.s. na Imam Mahdi a.s. ni mtu mmoja tu. Katika swala hili,iwapo mtu atakuwa akijua kuhusu ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. na kwamba Mtume Issa a.s. atamsaidia na atasali nyuma yake,basi swala hili litajitatua lenyewe bila ya kuzusha ubishi wowote. Vile vile itakuwa vyema iwapo tutajihusisha zaidi katika swala hili.Kuna hoja mbili katika wazo hili:(1) Masiha aliyeahidiwa hatakuwa Mahdi bali atakuwa akilingana navyo. (2) Ipo Hadith moja isemayo kuwa  'La Mahdi illa Masih'  yaani 'hakutakuwapo na Mahdi  illa ni Masihi.

 

Inawezekana kuthibitisha habari yoyote kama ni kweli kwa kutoa maelezo ya kimantiki. Popote pale panapozungumziwa ubashiri wa Mtume Issa  a.s.katika Hadith,basi tujue waziwazi kuwa yeye atakuwa Issa bin Maryam na wala si mtu mwingine kama yeye. Na wala haipatikani Hadith kama hiyo katika maandishi ya Mashia.

 

Hadith kama hizo zinapatikana katika maandishi ya Masunni ambapo Wanazuoni wao wamezipuuzia na kusema kuwa walioziripoti ni watu dhaifu.Kinyume na hivyo,zipo Hadith nyingi mno ambazo zinaelezea na kuthibitisha kuwa Mtume Issa a.s. atakuwa Mwisraili na Mahdi a.s. atatokana na kizazi cha Mtume Muhammad s.a.w.w. Hivyo imetuwia dhahiri kuwa Mahdi na Masihi ni watu wawili walio tofauti kabisa.

 

Hao Mahdi waongo wameleta hasara kubwa miongoni mwa jamii zetu na hivyo halitakuwa jambo la ajabu iwapo Mahdia.s.wa kweli atapata upinzani.Hivyo inatulazimu kuwa na ilimu kamili ya Mahdi a.s. wa kweli. Kwa hakika ulimwengu kwa hivi sasa umejaa matatizo na misiba,na hivyo kumjua mtetezi wetu moyoni mwetu ni jambo la kutufariji mno.Kitabu hiki ni kiungo kimoja cha ilimu juu ya Imam Mahdi a.s.

 

Maandiko ya Mashia yamejaa kwa Ahadith kuhusu Imam Mahdi a.s. na kijitabu hiki sio cha kwanza kwa aina yake bali kina habari ambazo zitatuongoza kwa njia haki. Vile vile jambo la kututia moyo ni kwamba habari nyingi mno zimetolewa na Ahli Bayti a.s. ya Mtume s.a.w.w. ambapo haziwezi kuwa ni habari za uzushi. Wanazuoni wa Kisunni wamethibitisha usahihi wa Ahadith hizo na wamekana wale wote ambao wanajaribu kupotosha ukweli na usahihi wa Ahadith na riwaya hizo.

 

Si kazi ngumu kukusanya Ahadith bali kazi iliyo ngumu kabisa ni ile ya kuthibitisha usahihi na ukweli wake hivyo ni vyema kuwadokezea mambo machache kuhusu hayo:

 

(1).Maandiko mengi ya watu wa mji wa Kufa yamepitia mabadiliko kabla ya kutufikia sisi.Wao wamekuwa na utaratibu tofauti wa maandiko yao na katika kuleta mabadiliko ya maandishi,kumeweza kutofautiana katika maana na maelezo.Mfano'maberamu yatachomwa moto katika mitaa ya Kufa' au inapatikana hivi 'maberamu yatachanwa katika mitaa ya Kufa' Mfano wa pili,ipo Hadith inayomzungumziaAuf-Salmi, ambaye makazi yake yanajulikana kama ni Tikrit na kwa mujibu wa maandiko ya Kufa inawezekana pia kupatikana kuwa ni Kuit. Miji yote hiyo miwili ipo Saudi Arabia na ni vigumu kuamua uhakiki wake.Kwa kuchukulia mojawapo ni lazima lakini uasili wa Maandiko ya Kufa yatapotea.

 

(2).Katika riwaya na mapokezi,majina ya miji na mahala pengine yanatumika majina ya kale ambayo kwa sasa hayatumiki tena.Hivyo ni vyema kupata majina  yanayotumika  kwa sasa sambamba na majina ya kale ili Hadih hizo zieleweke vyema.

 

(3).Taarifa kamili ya kimsingi ya Hadith itolewe,nani aliyeiripoti,mbele ya nani iliripotiwa,mahala pa kuripotiwa,n.k.,ili taarifa hizo ziweze kutambulisha vyema kuhusu Hadith hiyo.

 

(4).Ahli Bayt a.s. ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. wamerekebisha kipindi katika nyanja mbalimbali za jamii,maadili,kiuchumi,n.k.Hivyo Ahadith zinazozungumzia  mambo ya ubashiri hayatakuwa na mushkeli kueleweka na kukubalika.Vile vile kuna mambo mengine manne pia,nayo ni:(1)Uhakiki, (2)Isiyo na uhakiki (3) Makhsusi, (4)Kawaida. Ubashiri wowote ule ambao ni wenye uhakiki,basi hayo yatatokea tu katika hali yoyote ile.Na Mabashiri yale yasiyo na uhakiki yanaweza kutokea,inategemea. Mabashiri ya kawaida yanaweza kupatikana kila mahala.Namabashiri makhsusi yamefungamanishwa na muda na mahala maalum.Ni matumaini kuwa mafungu haya ya uchambuzi yatasaidia kutambua matatizo na mabishano yoyote yatakayotokea.

 

(5).Ahadith za ubashiri hazihitaji tafsiri au maelezo.Ama hayo yamekwishatokea au yatatokea kama vile yalivyoelezwa.Kwa watu kujaribu kuchambua kwa kuongezea chumvi na pilipili kutaongezea kuleta hali ngumu ya kueleweka na kufahamika.

 

Ninayo furaha kuwaelezea kuwa kitabu hiki cha Qayamat-i-Sughra kimejaribu kutimiza mahitaji na masharti kama hayo. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa Qayamt-i-Sughra  kinazungumzia mabashiri ambayo hayajatokea bado mfano uasi utakaoongozwa na Hasan Sayyed, mchokozi wa Sufiani,kuteketezwa kwa baadhi ya sehemu za Mashariki ya Kati,n.k. mabashiri ambayo bado mahdi wazushi hawajaweza kuzibashiri.

 

Kwa kumalizia mazungumzo haya,ninawaomba wasomaji wote wakisome kitabu hiki kwa makini sana na wala si kwa kuupoteza muda tu bali waweze kuzingatia makusudio  ya kuandika kitabu hiki.Imethibitika kwa mamlaka ya Quran Tukufu na vile vile Ahadith kuwa ni lazima kuwepo na kiongozi wa Kidini katika ulimwengu na kwamba mtu yeyote yule atakayekufa bila ya kumjua Imam wa zama zake basi atakufa kifo cha ujahili. Hivyo ilimu na maarifa ya Imam ni swala la Aakhera pia na ambapo ni faradhi kwa wanawake na wanaume wote kwa pamoja.

 

Mwishoni mwa kitabu hiki nimejaribu kuongezea makala juu ya uthibitisho wa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. kwa mujibu wa Wanazuoni wa Ahli Sunna  ili msomaji aweze kutambua umuhimu wa Imam Mahdi a.s. katika madhehebu mengine ya Islam.

 

Amiraly M.H.Datoo

Bukoba, 5 Januari 1996

MANENO MACHACHE

 

Kwa jina la Allah swt.

 

Watu walio hodari humu duniani wanakubali kuwa busara ni mwongozo na mtoa ushauri wa mwanadamu.Huwa inamwongoza kuelekea mema na kumzuia na mabaya. Ni busara hiyo ambayo ndiyo inayomtofautisha mtu na mnyama na kumfanya awe kiumbe bora kuliko wote.

 

Allah swt anawaamrisha watu watumie busara katika kutatua matatizo yao.Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu kuwa 'aya zake kwa ajili ya wale wanaofikiri.' Maneno machache kiasi gani hayakosi hekima ndani yake. Iwapo tutafuata mambo kama vipofu basi hatutakuwa na tofauti na wanyama na labda tutakuwa dhalili kuliko hao kwa sababu mtu kama huyo inavyoonekana hajijali. Busara bila ya elimu pia ni bure kwa sababu ilimu ni nuru ya busara.Lakini  ilimu ni kiasi kidogo sana kwa kulinganisha na ukubwa wa ulimwengu. Allah swt anatuambia kuwa hatukupewa isipokuwa ilimu kidogo tu,rejea  17:85. Hivyo ni ujahili mtupu iwapo sisi tujigamba kwa ilimu yetu kwa kutaka kukanusha sharia za Allah swt ambapo jambo la msingi ni kutokuelewa kwetu vyema masuala hayo.

 

Hivyo ni dhahiri kuwa yale yote ambayo yameelezwa na kubashiriwa katia Kitabu cha asili na kudura na yale ambayo yamesemwa  na Mtume Mtukufu s.a.w.w. hayawezi kamwe kuwa uongo ati kwa sababu sisi hatuelewi. Kila mmoja atakubaliana nasi iwapo tutasema kuwa kazi za kubuni na kufikiri hayana uhakika wowote mbele ya uchunguzi na matendo.

 

Kujitumbukiza katika mambo ya kubuni na uzushi ni tabia ya Shaitani kwani yeye alijitakabarisha kiasi cha kumuasi Allah swt. Kufuata ilimu kwa njia sahihi ni kule kufanya uchunguzi na utafiti juu yake kabla ya kutekeleza. Mtume Muhammad s.a.w.w. alisema kuwa "Mimi ni mji wa ilimu na Ali ni mlango wake" na vile vile alisema kuwa  "Mimi ni hazina ya ilimu na Ali ni ufunguo wake". Kwa hivyo tumepata ushahidi wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. kuwa kuna shakhsiya waliobarikiwa ilimu kwa kudura za Allah swt. Hivyo ilimu yake Imam Ali a.s. haiwezi kupimika au kuelezeka.

 

Kwa hivyo ni faradhi kwetu sote kuamini na kusadiki yale yaliyoelzwa katika Qurani Tukufu na marejeo ya Qurani katika Ahadith za Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Mrithi wake i.e. Imam Ali a.s. na Ahali yake a.s..Haitupasi sisi kamwe kukataa misemo yao  ambayo sisi hatuzielewi kikamilifu. Kutoamini na kutosadiki huku katika Islam kunamfanya mtu akufuru.

 

Na mojawapo ya maudhui hayo ni kuhusu Qayama -- ambayo ni mojawapo ya misingi ya Din ya Islam.Hivyo kuna mabashiri mengi kabla ya kufikia Qayamah.Mambo yaliyobashiriwa yanapatikana katika Quran Tukufu na katika Aha- dith.Katika mabashiri yote hayo kuna ubashiri  mmoja muhimu kabisa wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. Na ubashiri huu upo unapatikana katika Aya za Qurani Tukufu,Ahadith,misemo ya Wanazuoni wakuu na Mafuqahaa.Hivyo litakuwa ni jambo la kuaibisha iwapo atatokezea mtu kupinga ubashiri huo ati kwa sababu ya ujahili wake. Jee huyo mtu ataweza kukabiliana na Qurani,Ahadith na wanazuoni?

 

Waislamu wote kwa ujumla wanaamini kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. ingawaje kuna tofauti kidogo. Mashiah wanaamini kuwa Imam Mahdi a.s. yu hai na yupo ghaibu  (mafichoni) kama vile walivyo Mtume Issa a.s.,Ilyas,Khizr n.k. Kwa upande wa Masunni wao wanaamini kuwa yeye bado hajazaliwa na atajidhihirisha atakapofikia umri wa miaka arobaini.Kwa mukhtasari,Masunni wanaamini kuwa atakuwa ghaibu kwa kipindi cha miaka arobaini ambapo wanazuoni wakubwa wanaungana na Mashiah katika masuala hayo.

 

Kukanusha kuwapo kwa Mahdi ni uthibitisho wa kufr,kwa sababu Mtume s.a.w.w. amesema kuwa yeyote atakaye kataa kuwapo kwa Mahdi basi ni Kafiri. Jambo dogo kabisa linalotuhakikishia kuwapo kwa Mahdi a.s. ni kule kutokezea kwa Mahdi-bandia ambao wapo wanapatikana katika historia. Kwa hivyo iwapo utataka nakala basi itatokana na nakala asilia,kama hakuna nakala asilia basi huwezi kupata nakala yake.Vile vile kuna habari kamili katika vitabu vya kale kuhusu Imam Mahdi a.s.,nasaba yake n.k. hivyo inatuwia rahisi kwetu sisi kuweza kutofautisha baina ya Mahid wa kweli na wale bandia..

 

Hao mahdi bandia wameweza daima kuwazuzua wale wote waliokuwa majahili na wasiozijua sifa za Imam a.s. na ambao hawajui kuhusu ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. Hivyo ni faradhi kwetu sote kufahamu na kujua ilimu na maarifa ya Imam a.s. hasa katika kipindi hiki kilichojaa kwa uovu na dhuluma za kila aina za Shaitani. Watu wengi hawana mapenzi na Dini,na hapa ndipo Shaitani anapopata nguvu na wafuasi wake katika mambo ya maasi. Dunia yetu inakaribia kuangamia kwani dalili za Qayama zipo mbele yetu hivyo kunakaribia kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. Hivyo nimejaribu kuzikusanya mabashiri yote ya kuja kwa Imam Mahdi a.s. ambayo bado hayajatokea katika kitabu hiki na kukipa jina la Qayamat-i-Sughra ambavyo ni matumaini yangu kuwa wasomaji wote watafaidika na kuifanya imani yetu kuwa madhubuti katika Dini na kujitayarisha kumpokea na kukutana na Imam Mahdi a.s. Mwokozi na mkombozi wetu sote !

 

Sababu ya kukipa jina hili la Qayamat-i-Sughra  ni kwamba Imam Mahdi a.s. hatadhihiri hadi hapo dunia nzima ichafuke kwa maonevu na dhuluma kwa kiasi cha kupindukia. Hivyo jina hili linamaanisha 'kipindi kitakachotangulia Qayama'

 

Kitabu hiki kimezungumzia na kugusia mambo mengi mno zikiwemo itikadi za watu,dini zao,mila na desturi,utamaduni,ilimu,mawazo na fikara zao. Hivyo ninawaombeni nyote kunitumia maoni yenu kwa kukubalia maandiko au kuyapinga au kuyafafanua zaidi ili yanisaidie katika kuendeleza kazi hii iwe vyema zaidi hapo siku za mbeleni. Yote mutakayonitumia lazima ziwe na hoja na ufafanuzi mzuri kwani zitaweza kuingizwa katika chapa zitakazokuja.

 

Hatimaye ninatoa shukrani zangu za dhati kwa wote.

 

Amiraly M.H.Datoo                                                    5 Januay 1996

P.O.Box  838,

Bukoba, Tanzania  (E.Africa)

QAYAMAT  AU  SIKU YA HUKUMU

 

Nguzo ya tano katika Dini ya Islam ni kuamini katika Qayama. Na imani katika nguzo hii ni fardhi kwani ni siku moja maalum iliyokwisha pangwa,na swala la lini ni siri ya Allah swt na Waja wake makhsusi.Zipo mabashiri mengi yatakayotokezea kabla ya kuja kwa Qayama..

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. ameripotiwa kusema: "Zipo dalili kumi kutokezea kabla ya kuja kwa Qayama. (1).Uasi wa Sufiani. (2)Kuja kwa Dajjal (3)Moto na moshi  (4) Dabbatul Ardh  (5) Kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. (6)Kuchomoza kwa jua kutoka Magharibi  (7)Kuja kwa Mtume Issa a.s. kutokea mbinguni (8) Kuachinika kwa ardhi katika Mashariki (9)Kuachanika kwa ardhi katika Bara la Arabia (10)Moto undani mwa Aden  ambayo itawakusanyisha watu katika ardhi tambarare.[1]

UBASHIRI WA KUJA KWA IMAM MAHDI  A.S.

Wale waliokuwa wakitoa ubashiri walikuwa wakiishi huko Bara la Arabia na walikuwa wakijua vyema kiwango fahamu za watu wenzao na hivyo tutaona kuwa ubashiri mwingi utazungumzia Mashariki ya kati.Popote pale walipokuwa wakiulizwa maswali,wao walikuwa wakizingatia ilimu na fahamu ya mwulizaji. Zipo jumla zingine zilizotumika kijumla kama 'ardhi' n.k. katika mabashiri.

 

Jambo lingine la kukumbuka ni kwamba kumetokea mabadiliko na hata kamili katika mazingira na kisiasa kuanzia wakati huo. Majina ya miji imebadilika na miji mingi kuangamizwa kabisa  na ikatoweka. Na miji mipya kutokezea. Hivyo ni ombi kwa msomaji kujaribu kupitia vitabu vya jiografia vya mambo ya kale ili aweze kupata ufafanuzi zaidi.

 

IIikuwa ni desturi ya Waarabu kujulikana kwa majina ya baba,familia au ukoo,hivyo ndivyo ilivyo tumika muundo huo huo katika majina humu kitabuni.

 

Ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. umegawanywa na kuchambuliwa kama ifuatavyo:(1) Ubashiri wa kawaida, (2) Ubashiri maalum na (3) Ubashiri wa lazima.

 

Abdullah ibn Abbas (r.a.) amesema kuwa baada ya kumaliza Hajj  ya mwisho (mwaka wa 10 Hijriyyah),Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisimama mbele ya mlango wa Ka'aba Tukufu,akiwa ameshikilia komeo ya mlango, huku akiwauliza ma-Sahaba wake: "Je,nikuambieni dalili za siku ya Qayama?"  Salman Farsi (r.a.) ambaye alikuwa karibu naye,alisema:"Ndiyo,Ewe Mtume wa Allah swt."

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema,"Hakika,miongoni mwa dalili za saa, ni kuwa (1) watu watapuuza sala,(2) watafuata matamanio yao wenyewe (3)wataelekeza kujipendelea wao wenyewe,watawaheshimu matajiri,(4) na watauza Dini yao kwa manufaa ya kidunia (5) wakati huo roho na moyo wa Muumin itayayuka (kwa huzuni) kama chumvi inavyoyayuka katika maji,kwa sababu ataona mambo yaliyoharamishwa na hataweza kuyabadili."

 

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?"

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

 

"Ewe Salman, (6) wakati huo watawala watakuwa wadhalimu (7) Mawaziri watakuwa waasi,(8) na wadhamini (wale waliopewa amana kwa kuaminiwa) watafanya hiana,(9) hakika wakati huo maovu yatakuwa mema na mema yatakuwa maovu,(10)wale wafanyao hiana wataaminiwa na waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;na mwongo atasadikiwa,na msema kweli atahesabiwa mwongo.(11)Wakati huo kutakuwapo na utawala wa wanawake,(12)Masuria watashauriwa,(13) na watoto watakaa juu ya mimbar,(14) udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu(15)na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini;na mateka ya vita (yaani mali ya ummah) yatakuwa kama ni mali ya mtu binafsi;na mtu atakuwa mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema kwa marafiki zake,(16) na wakati huo kutatokea na nyota zenye mikia (comets)."

 

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?"

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

 

"Ewe Salman!(17) wakati huo mwanamke atakuwa mshiriki wa mumewe katika biashara, (18) na mvua itakuwa moto sana (19)na watu wema watabaki katika huzuni;na masikini hawata heshimiwa;na wakati huo masoko yatakaribiana, (20)Tena huyu atasema,"Mimi sikuuza chochote,na yule atasema, "Mimi sikupata faida yoyote." Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote asiyemlalamikia Allah swt.

"Ewe Salman! (21) tena itatokea iwapo watu watawazungumzia watawala wao, watawaua, na ikiwa watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali yao, watanyimwa heshima zao,watamwaga damu yao na mioyo ya watu itajaa woga;kisha hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga,mwenye khofu,ametishika na ameshstushwa”

 

"Ewe Salman! (22) Bila shaka wakati huo mambo fulani yataletwa kutoka Mashariki (23) na mambo fulani yataletwa kutoka Magharibi, (24) Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) katika Ummah wangu kutokana na hayo;Ole ya Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na huruma juu ya wadogo wao,wala hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa.Miili yao  itakuwa  ya wanadamu,lakini mioyo yao itakuwa ya mashetani."

 

"Ewe Salman! (25) Wakati huo wanaume watawaashiki wanaume, (26) na wanawake watawaashiki wanawake; (27) na watoto wa kiume watapambwa kama wanawake;(28) na wanaume watajifanya kama wanawake(29)na wanawake wataonekana kama wanaume; (30)na wanawake watapanda mipando (31) Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt juu ya wanawake wa Ummah wangu."

 

"Ewe Salman! (32) Bila shaka wakati huo Misikiti itapambwa (kwa dhahabu n.k.) kama inavyofanywa katika masinagogi na makanIssa,(33) na Quran zitapambwa (kwa nakshi na rangi za kupendeza n.k.) (34) na minara ( ya misikiti) itakuwa mirefu;na safu za watu wanaosimama katika sala zitazidi,lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao yatatofautiana."

 

"Ewe Salman! (35) Wakati huo wanaume watatumia mapambo ya dhahabu;kisha watavaa hariri,na watatumia ngozi za chui."

 

"Ewe Salman! (36)Wakati huo riba itakuwako,(37)na watu wata- fanyia biashara kwa kusemana na rushwa (38)na dini itawekwa chini,na dunia itanyanyuliwa juu."

 

"Ewe Salman!(39)Wakati huo talaqa zitazidi(40)na mipaka ya Allah swt hayatasimamishwa (41)Lakini hayo hayatamdhuru Allah swt."

 

"Ewe Salman!  (42) Wakati huo watatokea wanawake waimbaji, (43) na ala za muziki (44) na wabaya kabisa watawatawala Ummah wangu."

 

"Ewe Salman! (45) Wakati huo matajiri katika Ummah wangu watakwenda Kuhiji kwa matembezi,na walio wastani kwa biashara,na masikini kwa kujionyesha.(46) Hivyo basi wakati huo watakuwapo watu ambao watajifundisha Quran si kwa ajili ya Allah swt na wataifanya Quran kama ala ya muziki. (47)Na watakuwapo watu ambao watasoma dini si kwa ajili ya Allah swt  (48) na idadi ya wanaharamu itazidi  (49) watu wataiimba Quran, (50) na  watu watavamiana kwa uroho wa kidunia."      

 

"Ewe Salman!(51)Haya yatatokea wakati heshima zitakapo- ondoka,na madhambi yatatendwa (52)na watu waovu watakuwa na uwezo juu ya watu wema, (53) na uongo utaenea na mabishano (matusi) yatatokea (54) na umasikini utaenea,(55) na watu watajiona kwa mavazi yao (56) na itakuwepo mvua wakati si wake(57) na watu watacheza dama, kamari na Ala za muziki, (58) na hawatapenda kuhimizana mema wala kukatazana maovu (59) na kwa ajili hali itakavyokuwa hata itafikia wakati huo kuwa Muumin atakuwa na heshima ndogo kuliko hata mjakazi (60) na wanaosoma na wanaotumia wakati wao katika kumwabudu Allah swt watalaumiana.(61) Hao ndio watu watakaoitwa wachafu na wanajisi katika Ufalme wa mbinguni."

 

"Ewe Salman! (62) Wakati huo matajiri hawataogopa chochote isipokuwa mtu masikini; hadi kwamba masikini wataendelea kuomba kati ya ijumaa mbili,na hawatamwona mtu yeyote wa kutia chochote mikononi mwao."

 

"Ewe Salman! (63) Wakati huo itazungumzwa Ruwaibidhah."

 

Salman akauliza:"Ni nini Ruwaibidhah ? Ewe Mtume wa Allah swt, baba na mama yangu wawe fidia kwako."

 

Mtukufu Mtume s.a.w.w. akajibu:(64)"Watu fulani watazungumza kuhusu mambo ya watu ambayo hayakuwahi kuzungumzwa namna hii zamani.(65) Tena baada ya muda mchache machafuko yatatokea duniani,na kila nchi itafikiri kuwa machafuko yapo katika nchi yao tu."

 

(66)"Watabaki katika hali hiyo kwa muda ambao Allah swt atapenda wabaki; (67) kisha ardhi itatapika vipande vya moyo wake dhahabu, fedha na madini mengineyo;(Hapo Mtume s.a.w.w.) alinyosha kidole chake penye nguzo, na akasema:"Kama hizi(kwa ukubwa),lakini siku hiyo dhahabu wala fedha hazitamsaidia mtu yeyote. Na hii ndiyo maana ya maneno ya Allah swt 'Hakika dalili Zake zimekuja.'[2]

 

Zipo habari zingine zilizoelezwa katika vitabu vinginevyo kwa kupitia Jabir Ibn Abdullah Ansari, ambavyo ninazitaja:

"Ewe Salman! Wakati huo (1)Wazee watajitumbukiza katika mambo ya ushirikina na uchawi,(2)ghiba ndiyo itakuwa mazungumzo yenye kupendeza,(3) mali iliyopatikana kwa njia za haramu, itachukuliwa kama ndiyo neema,(4) wazee hawatakuwa na mapenzi ya wadogo na vile vile wadogo hawatawajali wazee na kuwaheshimu (5)Islam itabakia kwa jina tu kwani wafuasi wake hawatakuwa wakifuata maadili na maamrisho yake, (6) Kimbunga kikubwa cha rangi nyekundu kitatokezea mbinguni na kutaanguka mawe kutoka mbinguni(7)nyuso zitakuwa za kuchukiza(8)kutakuwa na mitetemeko na kuporomoka kwa ardhi  kila mara.

 

Hapo Sahaba walimwuliza Mtume s.a.w.w.,"Ewe Mtume wa Allah swt,je lini yatakapotokea hayo yote?"(pamoja na nishani na dalili za hapo juu,baadhi zimeongezeka hapa chini)

 

Mtume s.a.w.w. aliwajibu:(1)"Watu watakuwa watumwa wa shahwa au matamanio yao,(2) watu watakuwa walevi wa kupindukia kwani matumizi ya ulevi utakithiri na utakuwa ukipatikana kwa udhahiri bila ya watu kuona aibu ya aina yoyote,(3) Wanaume watakuwa wakiwatii wake zao,(4)jirani atakuwa wakiwaudhi na kuwatesa majirani wenzake,(5)Wakubwa hawatakuwa watu wenye huruma, mioyo yao itakuwa imejaa kwa maonevu, (6) vijana hawatakuwa na heshima (7) watu watajenga majumba imara na marefu mno,(8)wafanyakazi watadhulumiwa haki zao,(9)ushahidi wa kiuongo utachukuliwa kuwa wa kawaida, (10) ndugu atakuwa akimwonea wivu ndugu yake halisi  (11)watu watakaokuwa wakifanya biashara kwa ushirika, basi watakuwa daima wakifikiriana mbinu za kumdhulumu mwenzake,(12) mambo ya zinaa yatakuwa kama kawaida kwani  yatatendeka na kusikika pia.(13) ile mioyo ya kutaka kusaidia watu wengine itakuwa imetoweka, (14)Maasi na dhuluma itaongezeka kupita kiasi,(15) matumbo ya watu itachukuliwa kuwa ndiyo miungu yao,kwani hawatajali kiwevyo,ilimradi wapate chochote kile, (16) wanawake watakuwa wakitawala akili za wanaume na watakuwa wakiwaendesha wanaume vile watakavyo wao, (17) kutatokea Maulamaa au wanazuoni waovu kabisa kwani watajionyesha kuwa ni wacha Mungu na wenye ilimu,ambapo kwa hakika watakuwa waroho wa mali ya dunia tu."

 

Hapo Mtume Mtukufu s.a.w.w.liwaonya:"Kumbukeni,wakati kama huo utakapokuja,basi Allah swt atatumbukiza watu katika balaa za aina nne,(1) kutawaliwa na watawala dhalimu (2)ukame na vitu vya matumizi ya kila siku kuwa bei ghali yaani kupanda kwa maisha,(3) dhuluma za watawala (4)kuabudu miungu."

 

Sahaba waliposikia  hayo walishtushwa na kuuliza: "Ewe Mtume wa Allah swt ! Je kweli kuwa Mwislamu atakuwa akiabudu miungu na masanamu?"

 

Mtume s.a.w.w. aliwajibu:"Naam! Kwao mapesa yatakuwa kama miungu kwani watakuwa wakiziabudu kupindukia kiasi."

 

Kwa hakika sisi tunayashuhudia haya yote yakitokea  ambayo Mtume s.a.w.w. amekwisha bashiri karibu karne kumi na nne zilizokwishapita. Imam Ali a.s. katika khutba yake ijulikanayo kama Al-Bayan  anaelezea ubashiri kwa undani zaidi. Wasomaji wenye kutaka kupata habari zaidi wanaweza kutazama (1) Yanabi-ul-Muwaddah  (2) Basharat-ul-Islam, Sayyid Mustafa Ali-Sayyid Haider al-Kazami,chapa ya Baghdad.

 

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq a.s. ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam,Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran.

Imam a.s. alisema:(1)"Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki hawatapatikana.(2) Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.(3)Kufuata Quran kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.(4)Zitatolewa maana ya Aya za Quran kwa mujibu wa matakwa ya watu,hivyo mafhum ya Quran itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.(5).Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.(6)Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.(7)Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.(8) Ulawiti utakuwa ni jambo la kawaida.(9)Muumin  atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa (10)Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.(11)Huruma itakuwa imepotea kabisa.(12)Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.(13)Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume wenzao.(14)Wanawake watawaoa wanawake wenzao.(15) Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.(16) Starehe,anasa na zinaa zitashamiri.(17)Zinaa itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.(18) Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.(19) Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.(20)Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza  fitina na yale wanayozusha.(21) Ushauri mzuri utakanwa. (22) Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.(23)Al-Kaaba haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.(24)Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah kuhiji.(25)Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.(26)Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.(27)Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao(28)na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara kuma zao.(29)Wanawake wataunda vilabu vyao,mashirika na umoja wao.(30)Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.(31)Wanaume watajirembesha kama wanawake.(32)Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli.

 

Na Banu Abbas watalipia ulawiti.(33) Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume watakuwa hivyo hivyo. (34) Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu. (35)riba ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.(36)Ushahidi wa uongo utakuwa ukIssadikiwa mno.(37)Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.(38) Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.(39)Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.(40) Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.(41) Rushwa ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.(42)Wanaume wata walawiti wake zao.(43)Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.(44)Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka,nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawake.(45)Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa.(46) Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.(47)Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.(48)Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa  ulimini.(49)Pombe na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa. (50) wanawake wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri,ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.(51)Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.(52)Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.(53)Usomaji na usikilizaji wa Quran utakuwa ni bughudha kwa watu. (54) Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.(55)Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.(56) Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo. (57)Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.(58) Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.(59)Misikiti itarembeshwa kwa dhahabu.(60) Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.(61) Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara. (62)Kumwaga damu ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.(63)Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi mabaya ili kuwatishia watu wengine.

 

Imam a.s. aliendelea kusema: (64)"Watu watakuwa wakipuuzia sala na kutojali.(65) Watu hawatakuwa wakilipa zaka ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.(66)Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.(67) Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe. (68)Watu watakuwa wakIssali katika mavazi ya kiajabu. (69) Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.(70)Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu. (71)Watu watasali kwa kuonyesha tu.(72) Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.(73) Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.(74)Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali,watasifiwa kwa midomo tu.(75)Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah na Madina.(76)Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.(77)Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.(78)Matajiri wataigwa.(79)Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.(80) Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko,maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi. (81)Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.(82)Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.(83)Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume wao.(84) Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi,basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.(85) Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.(86) Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.(87)Pombe itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.(88)Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.(89)Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala.(90)Misikiti itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.(91)Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala za jamaa'  na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Kabla ya kuja kwa Qayama, vitu vitatu vitakuwa vya kawaida(1) ugonjwa wa bawasiri, (2) vifo vya ghafla, (3) Saratani ya damu.

 

Vile vile Mtukufu Mtume s.a.w.w. amesema: "Mojawapo ya sharti kwa kuja Siku ya Qayama ni moto utakaotanda Mashariki hadi Magharibi."

 

Ameendelea kusema, "Idadi ya wanawake itazidi idadi ya wanaume kwa uwiano wa wanawake hamsini kwa mwanamme mmoja."

KUANGAMIZWA KWA NCHI NA MIJI MBALIMBALI

Mwanachuoni mkuu wa Kisunni Mohiuddin, Bara la Arabia ameandika katika Muhadherat-ul-Abrar na Muthammerat-ul-Akhyar, riwaya kutoka Ilyas, mtiririko hadi kumalizikia kwa Hudhaifah,kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema:(1)"Misri haitaangamizwa hadi hapo Basra imeteketezwa, Basra itateketezwa kwa sababu ya Iraq na Misri itaangamizwa kwa sababu ya mto Nile.(2)Makkah itatekwa na Ethiopia.(3)Madina itakumbwa na mafuriko.(4)Yemen itateketezwa na ndui.(5)Eila itaangamizwa kabisa katika kutekwa.(6)Uajemi utatekwa na Saalik kutoka Dailam na Dailam atatimuliwa na Waarmenia na wao watatekwa na Waturuki.(7)Waturuki watakumbwa na kuangamizwa kwa radi.(8)Sind itatolewa na India (9)na India itapinduliwa na  Wachina. (10)China itaharibiwa na mchanga au nzige.(11) Rafdha itaipoteza Ethiopia.(12) Sufiani atawatilia vikwazo wale wanaokwenda kuzuru makaburi ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. na MaImamu a.s.(13) Ramla itateketezwa nusu  na (14) Iraq itakumbwa na ukame.

MITUME SITINI BANDIA

Abdullah ibn Umar anaripoti kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema:"Qayama haitakuja hadi Mahdi atakapodhihiri kutokana na kizazi changu;na yeye pia hatajitambulisha hadi hapo patakapotokea watu sitini watakaodai kuwa wao ni mitume (bandia)."

VITA PAMOJA NA WEUPE NA MAANGAMIZO

Imeripotiwa katika kitabu cha  Aqdud Dur cha Auf Ibn Malik kuwa mimi nilimwijia Mtume s.a.w.w. ambapo alipokuwa ameketi katia hema lenye rangi ya udongo. Kwa utaratibu alitawadha na kuniambia,"Qayama inasubiri ubashiri sita(1)mvua ya changarawe kutoka mbinguni (labda inaweza kumaanisha kuporomoka kwa mabomu na matokeo yake). Hili ndilo la kwanza."

 

Mimi nilimjibu: "Naam,Bwana wangu!"

 

Aliendelea Mtume Mtukufu s.a.w.w.(2)"Ushindi wa kuishinda Jerusalem. (3) Mauaji kupindukia kiasi. Watu watakuwa wakiuawa kama ng'ombe na mbuzi. (4) Kuzidi kwa mali ambayo haitoshelezi kukamilisha matakwa ya mtu.(5)Yatatokea magomvi na hakuna hata nyumba moja itakayobakia salama bila ya kukumbwa na magomvi hayo.(6).Watu weupe watawageuka.Wao watakushambulieni katika mabatalioni themanini na kila batalioni litakuwa na askari kumi na mbili elfu.

 

 

Katika Manaqib ya Ibn Shahar Ashub imerekodiwa kutoka kwa Qatada ambaye ameripoti kutoka Saeed Ibn Musayyab: "Imam Ali a.s. aliulizwa juu ya Aya ya Quran Tukufu:Na hakuna taifa lolote ila alipita humo Muonyaji.'  Hapo Imam Ali a.s. alitoa tafsiri ndefu mno na humo alitoa ubashiri wa kuangamizwa kwa baadhi ya miji. (1).Samarqand,Jaj,Khwazim, Isfehan na Kufa vitaharibiwa na Waturuki.(Hapa Waturuki wanamaanishwa Warusi).(2)Hamadan na Ray yataangamizwa na watu wa Kazvin.(3) Tabrusa,Madina na sehemu ya Ghuba ya Uajemi yatakumbwa na ukame na njaa.(4)Makkah itatekwa na Ethopia. (5) Basra na Balkh yatazama majini.(6)Sind itatolewa na India.(7)India na Tibet(8)Tibet na China. (9)Majeshi yatatetemesha Badakshan,Saani Kirman na baadhi ya sehemu za Syria.(10).Yemen itaangamizwa na watawala (11).Sijistan na baadhi ya sehemu za Syria zitaangamizwa kwa gesi (12)Saman Itaangamizwa na magonjwa na nzige wataiharibu Marv (13).Nyoka watua viumbe katika Hirat (16).Naishapur itateketezwa.(17) Azarbaijan itavamiwa na majeshi na radi kali zitapiga ( labda kwa sababu ya mabomu)(18).Mto Nile utafurika (19).Bokhara itazama majini(20).Kutakuwapo na ukame na miji ya Salam  na Baghdad  itaangamizwa. 

 

 

Abu Abdullah Jafar ibn Muhammad anaripoti kutoka kwa Imam Husain a.s. ambaye alimwuliza baba yake:"Tafadhali sana baba naomba utuambie ni lini Allah s.w.t. ataitakasa ardhi kutokana na watu waovu?"

 

Imam Ali a.s. alimjibu:"Ardhi haitaweza kamwe kutakasika hadi hapo damu ya wazushi itakapokuwa imekwisha mwagika kikamilifu."

Hapo Imam Ali a.s. akizungumzia tawala za Banu Umaya na Bani Abbas, alisema: "Kabla ya kuja kwa Qaim kutatokezea mtu mmoja Sayyid Hasani atakayejiweka huko Khorasan.Yeye ataiteka Kirman na Multan. Na hapo baadaye ataendelea mbele kuelekea Basra (Yaani mbali na pwani).Hapo Qaim kutokana na sisi, atajitokezea katika Jilan. Watu wa Astrabad na Kazvin watamtii.Hapo baadaye kutatokezea kupandishwa kwa bendera za Uturuki.Hapo kutakuja kutokezea vita vikali mno.Hapo ndipo Basra  itakapokuja kuangamizwa na makao makuu ya Waarabu itakuja kuwa Misri.

Hapo ndipo Imam Ali a.s. aliendelea kusema hadithi moja iliyo- kuwa ndefu ya tukio, na alisema:"Mikuki itaimarishwa na kusimamishwa na watu walio dhaifu na wastani watawaua watu walio wema.(Ikitoa ishara vile warusi wanavyowaua na watakavyowaua Waislamu)"

Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Imam Ali a.s. alisema: "Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim a.s. kutatokezea kwa aina mbili za vifo - nyekundu na nyeupe. Kwa nyekundu kunamaanisha damu yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali. Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafa ya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala."

Tanbihi: Kwa vifo vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damu itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia.Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande.  Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n.k. yanavyoua watu kwa mamilioni.

Imam Ali a.s. alisema:"Kutazuka vita katika Syria na itashambuliwa kwa mabomu. Katika matokeo yake takriban watu laki moja watakuwa wameuawa. Allah swt atabariki Waumin na kuwaadhibu Makafiri. Ole wenu wakati huo!"

Farasi wakiwa na mabendera ya rangi ya njano watatokezea Magharibi (Iraq ipo upande wa Mashariki ya Syria). Wao watafika Syria na huko kuna kijiji kimoja kiitwacho Harsa au Kharsa  ambacho kitadidimia ardhini.Muwe tahadhari kwa hayo!Ni ubashiri kuwa kutakuwapo na uasi wa Sufiani ambaye atatokezea kutoka mabonde makavu ya Palestina (vitabu vya zamani vya jiografia vinaelezea kuwa Kharsa au Harsa ipo karibu na Damascus huko Syria).

Asbagh ibn Nabata anaripotiwa kusema: "Sisi tulisikia tafsiri ya Aya ifuatayo ya Quran Tukufu kutoka kwa Imam Ali a.s.Kisha tukakurudishieni nguvu zenu juu yao na tukakuongezeeni mali na watoto na tukakufanyeni wenye kundi  kubwa kuliko wao' (Sura Bani Israil, 17:6)  hapo Imam Ali a.s. alisema:  Humo kuna baadhi ya mabashiri na dalili. Kwanza ni kule kuzingirwa na kutekwa kwa mji wa Kufa. Kutachimbwa mahandaki kuuzunguka mji kwa sababu ya khofu ya maadui. Kutachomwa au kuchanwa mabendera katika mitaa ya mji wa Kufa. Msikiti Mkuu wa kufa utabakia tupu kwa  siku arobaini kwa sababu hakutakuwapo na mtu wa kuja kusali humo.Wakristo watakuwa na nguvu katika maeneo hayo.Kutapeperushwa kwa mabendera tatu kwa pamoja. Kutamwagika damu kwa wingi mno ambamo muuaji na aliyeuawa wote wataingia motoni Jahannam. Mcha-Mungu pamoja na watu sabini watauawa katika kitongoji cha Msikiti wa Kufa.Huko Makkah, baina ya Rukn na Maqam atakuja kuuawa mcha -Mungu mwingine.[3]

IMAM ALI A.S. AELEZEA UBASHIRI KUMI:

(1).Katika mitaa ya mji wa Kufa, kutapeperushwa bendera nyingi mbalimbali (2).Misikiti haitatumika vile ipasavyo (3).Zitafungwa kila njia zielekeazo kwenda Hijja (kwa kila mbinu) (4).Kuzama kwa ardhi huko Khorasan (5).Watu watakuwa wakibadili makazi na maishio yao (watahamahama ovyo ) kwa sababu ya vita na machafuko kila mahala(6).Nyota zenye mikia zitakuwa zikionekana(7).Baadhi ya nyota zitakutanika mahala pamoja(8).Kutatokea na umwagaji wa damu kwa wingi na kila upande(9).Mauaji na maangamizi yatatokea kwa kupindukia kiasi(10).Tawala za kikatili na kutisha zitawaghalibu watu kila mahala.Kuna mshangao kwa kila ubashiri na baada ya kutokea kwao Al-Qaim wetu atadhihiri."

Imerekodiwa katika Oqdatud-Durr kuwa Imam Ali a.s. amesema:"Al- Mahdi a.s. hatadhihiri hadi hapo theluthi moja ya watu wa dunia hii hawatauawa na theluthi ya pili hawatakufa kwa mauti.Kwa hivyo kutakuwa kumebakia theluthi moja tu walio hai!"

 

IRAN:

Imam Husain a.s. ameripotiwa akisema kuwa kutatokezea vita vya makundi mbalimbali katika Iran na maelfu ya watu watauawa.

"Kinyume na desturi ya kupatwa kwa mwezi na jua katika mwezi mmoja, kutatokezea kupatwa kwa mwezi tarehe 5 ya mwezi na kutapatwa kwa jua mnamo tarehe 15 ya mwezi huo huo. Jambo kama hilo halijawahi kutokezea kamwe tangia Mtume Adam a.s "  Hayo yameripotiwa yakisemwa na Imam Muhammad al-Baquir a.s.

Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:"al-Qaim a.s. hatadhihiri hadi (1).dunia nzima kukumbwa na woga na khofu.(2).Kutakuwa na mitetemeko mingi na watu watakuwa wamejawa kwa woga (3).Kutatokea na kuzagaa kwa magonjwa yenye kuuwa kwa wngi (4).Kutazuka vita vikali mno miongoni mwa Waarabu (5).Kutazuka tabia ya watu kuzozana mno (6).Dini itakuwa dhaifu (7).Hali za jamii zitakuwa mbaya mno kiasi kwamba watu watakuwa wakiomba mauti kila usiku na mchana.

Imam Jaafer as-Sadiq a.s. amesema: "Kutatokea wazushi kumi na wawili watakaojiita Mahdi, kabla ya kudhihiri al-Mahdi  wa kweli."

Imam Jaafer Sadiq a.s. siku moja alipokuwa akimwambia kijana mmoja huko Kufa: "Katika mji wenu wa Kufa, karibu na Msikiti, watu wapatao elfu nne wa  kabila la Saabun watauawa na Lango la Tembo katika Siku ya Waarabu.

 

 

(3).UBASHIRI WA LAZIMA

Mabashiri haya yatatokea kwa lazima kabla ya kudhihiri kwa Al Qaim a.s. Katika kitabu hiki ninawakusanyieni baadhi tu, hivyo msomaji mwenye shauku zaidi anaweza kutafuta katika vitabu vingine vya Kiarabu, Kiajemi n.k.

Mtu mwovu mwenye sura isiyopendeza na yenye kuchukiza, mwenye macho - paka na makengeza kutoka kabila la Bani Umayya aitwaye Uthmaan bin Utba au Ushba ataongoza uasi karibu na Palestina. Uasi wake utatokezea baada ya vita vikuu vya dunia. Jeshi lake litakuwa katili mno na wenye kiu cha damu.Kiasi cha Wayahudi elfu sabini watajiunga naye.Wanajeshi wake wote watakuwa wanaharamu.Udhihiri wa al-Mahdi a.s. utakuwa katika miaka hiyo hiyo.Sufiani atatawala takriban Bara la Arabia zima kwa vitisho na maangamizo.Madina, Syria na Iraq vitateketezwa.Baada ya hapo yeye atajitayarisha kwa ajili yaMakkah.Mahala pamoja panapoitwa Beda, katika jangwa la Madina, ardhi itapasuka na Sufiani pamoja na jeshi lake zima litatumbukia humo na kuangamia.

Tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, usiku wa Alhamisi, kabla ya Alfajiri, kutasikika sauti moja kubwa mno.Itamfikia kila mtu popote pale alipo na ataielewa. Sauti hiyo nzuri kabisa itakuwa ni ya Bwana Jibrail a.s. ikitangaza ubashiri mwema wa kudhihiri kwa Al-Mahdi a.s. Hapo baadaye katika saa za mchana kutasikika sauti nyingine kama hiyo, nayo itakuwa ni sauti ya Ibilisi. Sauti ya kufanana itatosheleza kuwapotosha watu.[4]

Kwa mara ya kwanza yatatokea katika nchi za Mashariki, baadaye katika nchi za Magharibi na baadaye katika bara la Bara la Arabia.[5]

Katika baadhi ya riwaya kumeripotiwa kwa mitetemeko ya ardhi yatatokea katika taratibu hizo katika mwaka mmoja. Allah swt ndiye mwenye kujua zaidi!

Baadhi ya wana-Hadith wanasema kuwa hiyo ndiyo dalili mojawapo ya Siku ya Qayama. Kwa kufanyia utafiti zaidi tumeweza kujua kuwa jua litabakia kati kati saa za asubuhi mbele ya macho ya wakazi wa dunia na itabakia hivyo hadi wakati wa mchana na itaanza kupanda kama kwamba inaanza kuchomoza kutokea Magharibi. Kwa hakika ubashiri huu ni mgumu kuusadiki.Katika mabadiliko hayo ya utaratibu wa jua kunaweza kuleta maafa na mabadiliko makubwa mno. Ingawaje mimi si bingwa katika mambo ya mahesabu, lakini ni kama wataalamu walivyosema.Lakini hii itatokea kama ni ubashiri wa mwisho.

Ni neno la Kiarabu likimaanisha mhaini mkubwa na mleta balaa kubwa mno.Hivyo wale wote walio wahaini na waleta balaa basi wajijue kuwa wao pia na ma-Dajjal wa zama zetu hizi.Lakini Dajjal anayezungumziwa hapa ni yule ambaye anaitwa Sayyid na utambulisho wake ni Dajjal.Yeye atakuwa ni mchawi mkubwa.Hapo mwanzoni atakapojitokeza atadai kuwa yeye ni mtume na baadaye atajiita kuwa yeye ni mungu.Yeye atatokezea pale ambapo Mashariki ya kati itakuwa imekwisha dhoofika kwa sababu ya ukame utakaodumu kwa miaka mitatu kwa mfululizo. Katika mwaka wa tatu kutakuwa hakuna dalili ya majani na hakutakuwapo na mvua kabisa.

Hili jitu lenye jicho moja litakuwa na urefu wa mita ishirini. Jicho lake la kulia litakuwa halifanyi kazi na litakuwa kama donge la nyama nyekundu.Jicho lake la kushoto litawaka kutokea paji la uso.Yeye atakuwa akimwendesha punda mwekundu, mwenye manywele ambaye miguu yake itakuwa mieusi kutokea mifupa ya juu hadi magoti na nyeupe kutokea magoti hadi makwata. Kutasikika sauti ya muziki kutokea nywele zake na za punda wake.

 

Watu wanyonge,wanawake,Mabedui wa Kiarabu na Kiyahudi watamtii na kumfuata. Dajjal mwenyewe atakuwa Myahudi wa asili ya ukoo wa Qutama na kwa kutokana na udugu wa Abu Yusuf. Kwa hakika watu watamkubalia kama mtume (ingawaje atakuwa ni mzushi) .

 

Kwa kupatiwa msaada wa wanajeshi sabini elfu wa Kiyahudi na wenye silaha na matayarisho yote,yeye ataeneza kila mahala hali ya dhuluma na  uoga.Mioyo ya watu itajawa kwa khofu na hatari. Wakati huo,Jerusalemu ndio itakapokuwa mahala pa usalama kwa sababu Mtume  Issa  a.s. atateremkia. Imam Mahdi  a.s. atafika hapo pia. Hapo kutatokea vita vikali na Mtume Issa a.s. atamwua Dajjal.Wayahudi wataangamizwa.Ulaji wa nyama ya nguruwe utaachwa.Hakutakuwapo na alama za Msalaba.Na hapo kutakuwapo na Dini moja tu duniani -- ISLAM.

 

Mapokezi yafuatayo yametolewa kutoka Kitabu cha Kamal-ud-Din ambamo Muhammad Ibn Ibrahim anarikodi kama Hadith sahihi iliyopokelewa na Ibn Sabra,anayesema:

 

"Wakati mmoja Imam Amir-al-Mominiin Ali ibn Abi Talib  a.s. alituambia hivi:

 

Sifa zote ni za Allah swt na Salaam ziwe juu yake Mtume Mtukufu s.a.w.w.,na baadaye aliendelea kusema: "Niulizeni kile mukitakacho..."

 

Saasaan ibn Suhan aliinuka na kuuliza "Ewe Mawla wetu! Naomba utuambie ni lini atakapotokezea Dajjal.

 

Imam Ali a.s alimwambia aketi na kumjibu. Saasan aliketi na Imam Ali a.s. alianza kuelezea:

 

"Allah swt amekusikiliza na anajua kile ukitakacho.Zitapita dalili moja baada ya nyingine.Je niwaambieni ?"

 

Watu waliokuwapo walisema: "Naam tunaomba hivyo, Ewe Abul Hasan ! "

 

Imam Ali ibn Abi Talib  a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake, (1) watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa. (2)Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi (3)Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi (4)  Waislamu wataanza kuchukua riba (5) Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida (6) Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa (7 Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia  (8)Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao [6](9)Wanaume watawataka wanawake ushauri na uongozi (10)Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu (11) Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida [7](12) Mauaji na umwagaji wa damu utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe (13) Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na  wadhalimu watakuwa wenye nguvu.(14).Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu (15) Wasufi na wasomaji wa Quran watakuwa wapumbavu (16) Kutakuwa kukitolewa ushahidi  wa kughushiwa (17) Quran Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu (18) Misikiti itakuwa ikijengewa minara mirefu (19) Watu waovu watakuwa wakiheshimwa (20)Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao (21) Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale (22) Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume wao  kwa uroho wa mali (23) Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana. (24).Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu (25).Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa (26) Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji (27).Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi. (28).wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.(29).Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke)na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme[8].(30).Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea (31).Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.(32) Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .(33) Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko  kitu chochote kile (34) Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.

Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema "Ewe Bwana,naomba utwambie Dajjal atakuwa ni mtu wa aina gani?"

Imam Ali a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.(35).Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.(36).Jua litakuwa pamoja naye.(37).Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.(38).Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,(39) Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.

(40)Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal yatakauka hadi siku ya Qayama,(41).baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."

(42).Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.(43)Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa,(44) wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,(45) huyo Dajjal atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria, atauawa siku ya Ijumaa mchana,(46) Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam Mahdi a.s.(47)  na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

 

Allah swt anasema katika Quran,Sura 18 : 92 - 99.

 

Kisha akaifuata njia.

Hata alipofika katikati ya milima miwili,alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).

Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je,tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”

Akasema:“Yale ambayo Mola wangu amenimakinishia ni bora  (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nIssaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”

Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.”

Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.

Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Mola wangu.Na itakapofika ahadi ya Mola wangu ya kufika Qayama),atauvunjavunja.Na ahadi ya Mola wangu ni kweli tu.”

 

Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vyenye miguu minne na wakifanana na wanaadamu kisura na wao walikuwa ni wafupi mno mbele ya watu wa zama hizo. Na watoto wao walikuwa wakizaliwa kama watoto wa wanaadamu na walikuwa hawakui zaidi ya shubiri tano na sura zao zilikuwa aina moja na walikuwa wazururaji.Kwa kuwa ngozi zao zilikuwa ngumu kama zile za ngamia, hivyo hawakuathirika kwa baridi wala joto. Walikuwa na makucha makubwa na meno makali na masikio yao yalikuwa marefu kiasi kwamba walikuwa wakitandika moja na kujifunika kwa la pili. Walikuwa wakiingiliana kama wanyama na chakula chao kikubwa kilikuwa ni samaki kwa sababu kulikuwa kukinyesha mvua za samaki, na kama kulikuwa na kasoro ya samaki basi walikuwa wakishambulia miji na kuchafua na kuvuruga kila kitu kiasi kwamba watu walipokuwa wakizisikia sauti zao,walikuwa wakikimbia na kuacha makazi yao kwa sababu ilikuwa ni vigumu mno kuwakabili kwani walipokuwa wakiingia mijini basi miji yote ilikuwa ikijaa wao tu. Idadi yao ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ajuaye isipokuwa Allah swt. Wao walikuwa hawafi hadi wamezaa watoto zaidi ya elfu moja.

 

Katika vitabu tunapata habari zaidi kuwa Yajuj na Majuj ni makabila mawili yaliyokuwa makubwa kutokana na kizazi cha Yafus, mwana wa Mtume Nuh a.s.. Na katika Agano la Kale, Majuj anaelezwa kuwa ni Chifu wa Mashech na Tunal. Kwa sasa Moscow ndio mto unaosimama mji huo,uitwao Moscow, mji mkuu wa Urusi; Tabul ni mto huko Urusi ambapo kuna mji Tobolsk.

 

Katika eneo la Ulaya ya Kusini na Urusi ya Kiasia,baina ya Wacarpathiani na Don,kulikaliwa katika enzi za zamani na kabila katili kabisa ambao waliiteka Asia ya Magharibi kuanzia karne ya 7 Kabla ya Kristo hadi mwanzoni mwa kipindi cha Kikristo,wakati mashambulizi yao yalipokwisha kwa sababu ya Bwana Dhulqarnain alipoujenga  huo  ukuta.

 

Vile vile inasemekana kuwa neno  Mongol  ni mvurugano wa neno la Kichina Mongog  au  Manchog Iwapo utafiti huu utakuwa wa kweli,hivyo. Hivyo itamaanisha kuwa eneo la Yajuj na Majuj inaanzia Mto wa Moscow hadi Turkistan ya Kichina na Mangolia.

 

Maelezo ya ‘kuta’ katika Quran Tukufu yanaonyesha kuwa lazima iwe imejengwa pale penye njia ili kuzuia makabila hayo ya wachochezi na wakatili kuwashambulia majirani wao waliokuwa mafundi stadi katika kazi za kufua vyuma na walikuwa matajiri.

Sheikh Abul-Kalam Azad,katika moja ya makala yake (katika Jannatul-Ma’arif) anaelezea kuwa kuta hizo zimeendelea hadi Uturuki.

 

Ayatullah Agha Haji Mirza Mahdi  Puya Yazdi (katika hashia ya Tafsiri ya Quran iliyofanywa na S.V. Mir Ahmad Ali) anawanakili wengine wakisema kuwa kuta hizo zipo baina ya milima ya Armenia na Azerbaijan.

Hata hivyo kuna tofauti ya maoni kuhusu utambulisho wa Dhulqarnain. Abdullah Yusuf Ali anadhani kuwa jina hilo linaelezea kuwa ni Alexandar Mkuu wa Misri.

 

Wengineo,kama Agha Puya,wanafikiri kuwa huyo anatambulishwa kama ni Mfalme wa Kiajemi aliyekuwa akiitwa Darius.

 

Kwetu sisi hatumaanishi kuingia katika mazungumzo mengi kuhusu mjadala huu lakini inatubidi liwe jambo lililowazi mbele yetu kuwa kwa mujibu wa Quran Tukufu, Dhulqarnain alikuwa ni mcha Mungu hivyo kamwe haiwezekani kumtambulisha Dhulqarnain kama kafiri  au  mpagani.

 

Kwa mujibu wa Quran Tukufu,Itakapokaribia Siku ya Qayama, kabila hizi zitafanikiwa kuvunja kuta, yaani zitaenea zaidi kuliko mipaka yao ya awali.Upanuzi huo unaweza kuwa kimantiki;ambapo inaweza kumaanisha kuwa itikadi zao (ukomunisti na ukafiri) zinaweza kuenezwa nje ya mipaka ya nchi zao. Au itakuwa aina ya kikoloni yaani kukalia maeneo ya mashariki ya Ulaya,Asia ya Kusini na maeneo mengineyo. Au inaweza kumaanisha yote.

 

Imeandikwa katika Tafsir Majma-ul-Bayan kuwa baada ya kuteka maeneo ya ardhi watajararibu kuiteka mbingu.“Hivyo watatupa mishale yao kuelekea angani,na itawarejea zikiwa na alama kama za damu. Hivyo watasema:‘Sisi tumekwishawateka wakazi wa dunia na tumewateka wakazi wa angani.”

 

Ni dhahiri kuwa  mishale  inamaanisha maroketi na vyombo vya angani. Maneno itawarejea zikiwa na alama kama za damu inamaanisha kuwa vyombo vya angani vitafikia malengo yao na kurejea duniani.

 

Kwa mujibu wa Tafsiri hiyo,“wakati watakapokuwa na takabari kubwa kwa sababu ya ‘kushinda anga za juu’, Allah swt atawaumba funza au minyoo ambayo itawaingia masikio yao, na kuwaua wote.Inamaanisha kuwa hatima yao itakuwa kwa kuangamizwa kwa maafa makhsusi, au kwa magonjwa ya kuambukizwa yatakayotokana na vijidudu.

 

Saasaan  anaelezea zaidi.: "Sisi tulimwuliza Imam Ali a.s.  je ni nini kitakachotokea baadaye?"

Ali a.s. alijibu:"Karibu na mlima Saffa  na Marwa, Dabbatul Ardh atakuja.Yeye atakuwa na pete ya Mtume Suleiman na atakuwa na mkongojo wa Mtume Musa a.s. na yeye atakuwa akiiweka hiyo pete juu ya vipaji vya makafiri na  loh ! kutatokezea dalili za kuonyesha kuwa huyu mtu ni kafiri,na ukafiri wake utaonekana usoni mwa mtu huyo aliyegusishwa pete ya Mtume Suleiman a.s.Dabbatul ardh pia atakuwa akiwaangalia waumini na ataweza kuwatambulisha kuwa wao ni waumini, yeye kwa amri ya Allah swt atakuwa akiangalia juu ya mbingu na ataweza kuona Mashariki na Magharibi papo hapo. Na tukio hili litatokezea baada ya jua kuchomoza kutoka Magharibi hapo ndipo milango ya tawba  itakuwa imefungwa, muda wa kufanya tawba utakuwa umekwisha. Matendo na amali havitasaidia chochote. Ninawaombeni msiniulize baadaye kitakachotokea kwa sababu nimempa ahadi Mtume s.a.w.w. kuwa sitaitoboa hii siri isipokuwa kwa yule atakayekuwa mrithi wangu."

Mpashaji habari wa tukio hili Taran ibn Sabra alimwuliza Saasan ibn Suhan "Je nini maana hili jambo aliloliezea Imam Ali a.s. "

Saasan alijibu: "Ewe ibn Sabra, Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya  Imam wa 12 (kumi na mbili ) katika kizazi cha Imam Ali a.s. na ni mtu wa kizazi cha tIssa (9) katika kizazi cha Husein ibn Ali a.s. Huyo atakuwa ni jua litakalo chomoza kutoka Magharibi,yeye ataitakasisha ardhi baina ya Rukn na Msikiti na ataeneza uadilifu duniani kote. Baada ya hapo hakutakuwapo na dhuluma ya aina yoyote."

KUDHIHIRI KWA MTUME ISSA A.S. KUTOKA MBINGUNI

Ni imani ya Waisilamu wote kuwa Mtume Issa a.s.alikuwa hakusulubiwa wala hakuuliwa bali alichukuliwa na Allah swt katika mbingu za juu na  yupo hai.Kwa wakati maalum uliowekwa na Allah swt, Mtume Issa a.s. atadhihiri duniani kutoka mbinguni hadi Syria.Wakati huo Imam Mahdi a.s.atakuwa humu humu duniani na Mtume Issa ataungana naye.Pamoja na Imam Mahdi a.s.wakati wa sala Imam Mahdi a.s.atakuwa akiongoza sala na Mtume Issa a.s. atakuwa akIssali sala nyuma yake. Wao wote kwa pamoja watatangaza vita dhidi ya Dajjal ambaye atauawa. Baada ya hapo Wayahudi wote na Wakristo wote watakuwa Waislamu .

Quran Tukufu inatupa habari kwa urefu na mapana kuhusu Mtume Issa a.s. vile vile tunapata habari nyingi sana katika Hadithi tukufu.Vile vile kulitokezea na mtu ambaye alidai kuwa Mtume Issa a.s. amekufa na yeye alikuwa ni masiha mtu huyo anajulikana kwa jina la Mirza Gulam Ahmad Kadiani,mimi sitapenda kuingilia maswala haya na kuyachambua kwani mambo haya yametobolewa khususani katika nchi ya Pakistani na serikali ya Pakistani imefichua siri za hawa watu na imetangaza kuwa wafuasi wa Kadiani si Waislamu na haya ndiyo yalikuwa maamuzi ya Mahakama  yaliyosikiliza kesi zao.Iliyochukua nafasi muhimu katika mahakama ya Pakistani .

Allah swt anasema katika Quran ,Sura Ad -Dukhan 44 : 10 - 16

Basi ingoje siku ambapo mbingu zitakapoleta moshi uliodhahiri.

Utakaowafunika watu;Hii ni adhabu iumizayo.

(Wao watasema) ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu hii hakika (sasa) mumin.’

Nini faida ya kukumbuka kwao ? Na alikwisha wajia Mtume abainishaye.

Wakampa kisogo na wakasema:’Amefunzwa  ni mwendawazimu.

Kwa yakini Sisi tutaiondoa adhabu kidogo,nyinyi mtarudia (makosa yenu).

(Na itakuja) siku ambapo tutawateka (wote) kwa mteko mkubwa;Kwa hakika sisi ni wenye kulipiza.

 

Kwa mujibu wa riwaya nyingi mno,Aya hizi zinabashiria moshi utakaokuwapo karibu na Qayama. Moshi huo utaingia katika masikio (na macho), na vichwa vya watu vitaonekana kama yamechomwa.Lakini haitawadhuru waumini;wao watahisi mwasho wa kawaida wa kama baridi. Na dunia nzima itakuwa mfano wa nyumba iliyoshika moto na ambayo haina madirisha wala sehemu za kutokezea moshi. Na sura hii itadumu kwa muda wa siku arobaini.

 

Dalili hii itakuwa ni ishara ya kuonywa;na kama inavyoonekana katika Aya  wanaadamu watapewa muda wa kurejea katika imani na njia iliyo ya haki na wajirekebishe.Maneno‘Kwa hakika Sisi tutaiondoa adhabu kidogo’inatudhihirishia kuwa moshi utaondolewa, lakini maneno yanayofuata nyinyi mutarudia (makosa yenu)  inatuonyesha kuwa kuondolewa kwa adhabu hiyo tu,basi si watu wengi watakaotafakari juu ya suala hilo.Labda wengi watatafuta visingizio vya kijiografia au zinginezo kwa ajili ya kutokezea kwa adhabu hiyo,na watasahau ahadi zao walizompa Allah swt kuwa Mola wetu !... hakika (sasa)  muumin.

 

Kwa hakika si vigumu kukubaliana na mambo yaliyoeelezwa hapo juu:

1.Umande na moshi unakuwapo hata leo hivyo Allah swt anao uwezo wa

   kuumba moshi utakaotanda duniani kote.

2. Allah swt anaweza kuwaepusha mumin kutokana na athari mbaya kabisa za

    moshi huo.Kwani hata leo tunaona kuwa si watu wote wanaoathirika na

    maafa yanapozuka katika maeneo fulani.

3. Na kuna idadi kubwa kabisa isiyohIssabika ya makafiri wanaotubu pale

    wanapopatwa  na adhabu au matatizo,na husahau kwa urahisi ahadi zao

    kwaAllah swt (za kuwa mumin) za kuomba, mara baada ya kuondokea na

    matatizo yao.

Ubashiri huu umeelezwa katika vitabu vingi vya Hadith, kutakuwa na moshi mwingi sana katika anga zetu kwa sababu hiyo kutakuwapo kwa moto kila mahali.

Inawezekana ubashiri huu unadalilisha utumiaji wa aina nyingi za magesi ambayo yanalipuka yenye hatari na moto ndio utakuwa sababu ya gesi hizi ,majaribio ya nyukilia vile vile yanatoa gesi nyingi na miale ya radio active vile vile katika ubashiri mwingine imeelezwa kutakuwapo na moto unaotokea ndani mwa ardhi ya Aden, nimeelezea maswala haya katika kurasa zilizopita.

Kuna mabashiri mengi katika kuelezea kuteketezwa kwa baadhi ya miji khususan kuteketezwa kwa mji wa Baghdad ndiyo imeelezwa kwa zaidi na wanazuoni wengi wanasema kuwa ubashiri huo ni wa kweli.

Imam Jaafer Sadiq a.s. alitoa hotuba ndefu sana kuhusiana na swala hilo.  Imam Ali a.s. pia ameelezea kwa undani zaidi katika hotuba zake na hapa ninawachambulia machache kutoka hotuba hiyo:"Enyi watu kutabuniwa mji mpya utakaoitwa Baghdad (Labda alimaanisha Baghdad mpya) Mji huo utakithiri kwa madhambi na maasi kiasi kwamba adhabu za Allah swt zitakuwa zikilengwa sana huko.Balaa za kila aina zisizojulikana, magonjwa yakuangamiza,ukame, mafuriko ya mto Tigris na mvua zisizo na mpangilio vile vile tufani za kila aina zitakuwa zikitokea kuuangamiza mji huo.Na kuangamizwa kwa mji huu kutatokea baada ya aina tatu za bendera kuchomoza katika mji huo. Bendera ya kwanza itakuwa rangi Njano, ya pili aina ya bendera itakuwa kutoka pande za magharibi, na ya tatu itatokezea sehemu za kuizunguka,na labda hii ndiyo dalili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kijana huyu  atakuwa mzuri na atakuwa ametokana na kizazi cha Imam Hasan a.s. na katika baadhi ya Hadith anapewa jina la Hasan, atatokezea kutoka kijiji cha Dailam (karibu na Kazvin) yeye hatajitangazia uongozi wowote wa kidini bali atakuwa akiwaita watu baada ya kuona hali ya jamii na jumuia imeharibika na kuvurugika, atawaita watu waache maovu na wajirekebishe.Watu wa Taliqan watakuwa ndio watu wa kwanza kuutikia wito wake.Watu watamzunguka na watajiunga kwa wingi katika harakati zake,ujumbe wake utaenea katika sehemu  zinazozunguka za karibuni na kufikia hadi Multan kupitia Kirman na vile vile atafika Basra.Sehemu zote hizi zitakubaliana na mazungumzo na mambo yake.Baaada ya hapo ataelekea Kufa na huko atapata habari kuwa Imam Mahdi a.s.amedhihiri na Imam a.s.ameondoka kuelekea Iraq kupitia Makkah  na Madina. 

Wakazi wa Kufa watakuwa wakiishi maisha yasiyo wafurahisha wao wenyewe. Huyu Hasan Sayyed ataonana na Imam Mahdi a.s. kutaka kujua miujiza na uthibitisho wa uhalali wake wa kuwa Imam Mahdi a.s. baada ya kuthibitishiwa atakula kiapo kwa Imam Mahdi a.s. pamoja na jeshi lake la utiifu.

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:"Kwa jina la Allah swt,Hasan Sayyed atakuwa akimtambua vyema kabisa Imam Mahdi a.s. lakini ili kuwahakikishia watu na kuwathibitishia na kuwatolea shaka watu kuwa huyu ndiye Imam Mahdi a.s. atamuomba Imam amthibitishie kwa miujiza uhalali wake. Wanajeshi elfu nne wa Zaid kutoka Yemen watakaokuwa katika jeshi la Hasan Sayyed wataaasi. Hapo Imam Mahdi  a.s. atamshauri Hasan Sayyed awatulize hao vijana wa kabila la Zaid wajIssalimishe. Mazungumzo hayo yataendelea kwa muda wa siku tatu,lakini wanajeshi wa Zaid hawatakubali, hatimaye wote watauawa.

(4). UBASHIRI  WA  SIKU ZA MBELENI

Kwa hakika mabashiri yafuatayo yanahitaji kuzingatiwa mno, hapa chini ninawaleteeni machache na nitawapa maelezo kidogo juu yake:

 

Yeye atakuwa ni mtu mwema na ataanzisha uasi wake katika mji wa Samarqand. Mambo mengi ya muhimu yatatokea wakati wake. Hadithi nyingi zinaelezea kuwa ama yeye atakuwa ni  kamanda katika jeshi la Hasan Sayyed au Imam Mahdi a.s.

 

Huyu atakuwa ni mtu mwema atakayewaita watu katika mawazo yake baada ya vita vikuu, huyu  mtu atakuwa amesimamia mapinduzi kutoka Kuwait hadi Syria  ambapo ndipo atakapouawa.

 

(3). Uasi wa Yamani :

Kutatokezea kwa mtu asiyejulikana kutokea huko Yemen ambapo ataleta maangamizi na ataleta fitina na ugomvi wa hali ya juu sana.

 

Katika lugha ya Kiarabu Algeria,Tunisia,Morocco na Libya,zinaitwa Maghreb kutatokezea mtu katika nchi hizi yaani Maghreb ambaye atakuja Misri na atahukumu nchi hizo zote ikiwemo Syria.

 

Imam Ja'afer as- Sadiq a.s. amesema: "Siku kumi na tano tokea kudhihiri kwa Mahdi a.s. mtu mtakatifu sana kwa jina la Muhammad ibn Hasan Zakiyya ambaye atakuwa ni mmoja wa wafuasi wakubwa wa Imam Mahdi a.s. atauawa karibu na Al-Ka'aba baina ya  Rukn na Maqam..

 (6).  Kutokezea kwa ikhtilafu 

Kutatokezea ikhtilafu kubwa sana miongoni mwa Bani Abbas.

 

(7). Mtu maarufu sana

Mtu maarufu sana mcha Mungu ajulikanaye kwa jina la  nafsi Zakiyyah atauawa pamoja na Sayyid sabini nyuma  ya Msikiti wa Kufa. Ukatili na mauaji haya ya kikatili yatatendwa na jeshi la Sufiani.

 

(8). Mji wa Makkah

Mtu mmoja kutoka Bani Hashim, mcha Mungu kabisa atauawa katika mji wa Makkah.

 

(9). Mahakama ya Kufa

Chumba cha Mahakama ya Kufa kitaharibiwa pamoja na ukuta wa Msikiti wa Kufa.

 

(10). Theluji ya kushangaza

Kutakuwepo na kuanguka kwa theluji ya kushangaza katika Roma kila kipande cha theluji kitakuwa kama yai.

 

Kutachomoza kwa nyota kutoka Mashariki, mwanga wake utakuwa sawa na wa mwezi. Mkia wake utakuwa ukipotea pole pole na hatimaye kupotea. Nyota hizi za kuanguka zimekuwa zikitokea daima lakini hakuna hata moja ambayo imeweza kuwa na nuru kama mwezi.

 

(12). Moto katika anga za juu:

Katika anga za juu baina ya anga na ardhi kutatokezea moto utakaowaka siku tatu mfululizo au siku saba kwa hakika litakuwa jambo kubwa la kustaajabisha.

 

(13). Rangi nzito mbinguni. Rangi nzito nyekundu iliyoiva itazagaa mbinguni.

 

(14).Moto Mashariki ya kati.

Kutakuwa na mioto ikiwaka kila mahala khususan Mashariki ya kati.Moto utakuwa wa kutisha sana kiasi kwamba watu wataanza kutubu madhambi yao.

 

Hakuna hata mmoja atakayeweza kumsaidia mwenzake  kwa moyo kwani kila mmoja atakuwa akitenda vile atakavyo kwa masilahi yake mwenyewe.

 

(16). Mfalme wa Iran ataanguka:

Yaani ufalme wa Iran utakwisha na utawala wake utatokomea na utawala mpya utatokezea yaani katika mwaka 1978|79 ubashiri huu umetokezea kuwa kweli wakati Shah Muhammad Riza Pahlawi alipopinduliwa na umma wa Waislam chini ya uongozi shupavu wa marehemu Ayatullah Ruhullah Al-Musawi al- Khomeini (a.r.) utawala wa Shah ulidumu zaidi ya karne mbili na nusu.

 

(17). Amir wa Misri atauawa: 

Atakuwa ni mtu mmoja mwenye mamlaka ya utawala na atakuwa ni mtu mashuhuri katika Misri.Katika Kiarabu hapa neno lililotumiwa ni Amir  yaani hakukutumiwa jina la Sultani au Malkia hivyo inatudhihirishia aina ya utawala utakaokuwepo wakati huo. 

 

Kutakuwa na bendera zilizoinuliwa kutokea Misri zikielekea Syria na kutatokezea bendera moja kutokezea Khorasan na bendera zote hizi tatu zitadai kumilki Syria na wote hawa watapigania katika ardhi ya Syria. Vita ambavyo vitaangamiza na kuteketeza Syria.

 

(19). Majeshi kupitia  mipaka ya Magharibi wataingia Syria :

Yaani inawezekana majeshi ya Wazungu na nchi za Magharibi zitaingia Syria kupitia Uturuki ili kuikalia Syria.

 

(20). Bendera rangi nyeusi

Bendera rangi nyeusi zitachomoza kutoka Khorasan (Labda linamaanisha jeshi la Hasan Sayyid).

 

(21). Kutajengwa njia za kupita chini ya ardhi kutokea mto wa Furati.

Kipitio hicho kitapitia Kufa na itauletea utajiri mji huo. Wakazi wake watakuwa idadi kubwa na utashamiri (Ubashiri huu umeshatokea na kukamilika pia).

 

(22). Watu  sitini

Kutatokezea watu sitini watu wenyewe watakuwa waovu na majangiri ambao watadai kuwa wao ni mitume kwa hakika kutokana na wanavyovutia na wanavyojionyesha wataweza kuwavuta watu wengi upande wao  (kiasi cha watu hamsini na nane wameishatokezea kudai utume hadi leo).

Kutokana na kizazi cha Abu Talib watu kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imam , kizazi cha Imam au warithi wa Imam au wao ni Mahdi   (baadhi ya watu wameshatokezea na wameshapita na wengine bado watatokezea  nao pia  watapita ).

(24). Mtu atachomwa moto

Mtu mwenye heshima sana kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai baina ya Jehula na Khanqin (tunaweza kusema kuwa huyo mtu ni Abdus Salaam Arif ambaye aliungua moto katika ajali ya ndege )

Kujengwa daraja mpya katika mto wa Tigris katika upande wa Karkh,kutajengwa daraja huko Baghdad (daraja kama hili lilijengwa miaka michache iliyopita labda kunaweza kujengwa daraja lingine jipya).

 

Watu wengi wa mji wa Baghdad watauawa kutokana na mitetemeko mingi ya ardhi na kutatokezea maafa na tufani nyeusi wakati wa mchana ambapo kutaleta matishio mbalimbali kwa wakazi wa Baghdad.

 

(27). Basra itazama..

Basra itazama katika maji kufuatia tufani kubwa ya mawimbi ya maji makubwa (Wasomaji wanashauriwa kusoma Nahjul  Balaqgha  kwa utabiri huu ).

 

(28).  Magonjwa sugu yataenea duniani

Kutakuja kuangamizwa na magonjwa sugu yataenea duniani kote na itaua watu kwa idadi kubwa sana.

 

(29).Makundi makubwa mno ya nzige 

Kutakuwa na makundi makubwa mno ya nzige duniani kote, vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Iraq,kutakuwa na umwagaji wa damu kupindukia duniani kote na kutokezea vita vikali sana huko Iran baina ya makundi mawili kiasi cha watu elfu themanini watauawa  (Au imekamilika  mwaka 1978 |79) .

 

(30).Nyuso za wanadamu zitabadilika

Hali ya nyuso za wanadamu zitabadilika na zitageuka kuwa za nyani na nguruwe.

(31).Kutatokezea mkono karibu na jua

Kutatokezea mkono karibu na jua ambapo wakazi wa duniani wataona pamoja na kustaajabika       (jambo hili litatokezea muda mchache kabla ya kudhihiri kwa Mahdi  a.s.).

 

(32).Kunyesha mvua yenye fujo

Duniani kote kutaanza kunyesha mvua yenye fujo sana kuanzia tarehe 16 Jamadi us-Thani hadi tarehe 10 Rajab.

 

Kila Mwislamu mwenye kuwa na imani kamili juu ya Allah swt anaamini kuwa mvua hainyeshi  kwa sababu ya misimu tu bali ni kwa sababu za amri na idhini za Allah swt.

Allah swt anatuambia katika Quran Tukufu kuhusu mvua:

Sura 25, Furqan Aya 48

   Naye ndiye azitumaye pepo kuwa bashara  njema kabla ya rehema

    yake ya mvua; na tunayateremsha kutoka mawinguni maji safi.

 

Sura 35,Fatir Aya 9:

Allah ndiye aliyetuma hewa inayopeleka mawingu.

 

Sura 6,An-Am Aya 6:

Sisi tumeifanya mbingu kuwa yenye kunyesha mvua iendeleayo.

 

Sura 15 Al-Hijr Aya 22:

Sisi tumefanya mawingu na kunyesha mvua kutoka mbinguni.

 

Sura 29 Ankabut,Aya 63:

Na ukiwauliza,’Ni nani ateremshaye maji na kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake?’ Bila shaka watasema ‘Allah’ .

 

Sura 50 Qaf Aya 9:

Na tumeyateremsha kutoka mawinguni maji yaliyobarikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka zivunwazo.

 

Sura 8 Anfal, Aya 11:

Na anakuteremshieni mani kutoka mawinguni ili kukutakasisheni.

 

Sura 40 Muminun, Aya 18:

Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi.

 

Katika Aya hizo Tukufu za Quran kuwa  upepo ndio unaosafirisha mawingu kuelekea mashariki,magharibi au kaskazini na kusini.Yaani inachukua kwa amri za Allah swt. Vile vile tumeona waziwazi kuwa kunyesha kwa mvua na kiasi chake kinahusishwa na Allah swt.

 

Baada ya kusoma hizo Aya tukufu tumeona kuwa mvua imekuwa daima ni rehema na idhini ya Allah swt ndipo inaponyesha juu ya ardhi.

 

Imeonekana kuwa katika baadhi ya nyakati neema na baraka hii inakuwa imezuiliwa. Na katika sura hii kuna riwaya nyingi kutoka kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Maimamu a.s. zinazotuambia tusali sala za  Istisqaa.

Tunapata mapokezi kutoka vitabuni kuwa katika zama za Imam Ali a.s. na Maimamu  a.s. wamekuwa wakIssali sala za Istisqaa kwa ajili ya kuomba mvua,na mvua zilikuwa zikinyesha.

 

Mvua hii isiyo na mpangilio itanyesha kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. na haijulikani kama itanyesha  Mashariki ya Kati tu au mahala penginepo.

 (33). Watu waliokufa watakuwa hai

Watu waliokufa watakuwa hai  (matukio haya  yatatokea muda mchache kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. Baadhi ya vitabu vinataja majina ya watu wataofufuka kupata maisha mara ya pili).

 

(34).Misikiti itarembeshwa

Misikiti itarembeshwa kwa mabati ya dhahabu vile vile Quran tukufu itarembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.

Sehemu tatu duniani zitadidimia ardhini au zitamezwa na ardhi pamoja na wakazi wake,ya kwanza itakuwa katika upande wa Magharibi baadaye katika Mashariki na hatimaye katika Bara la Arabia.

 

Islamu itabakia kwa jina tu. Maamrisho ya dini yatapotea. Watu wataingiliana sana kiasi kwamba itakuwa vigumu sana kumwelewa Mwislamu na yule asiye Mwislamu yaani Waislamu watakuwa wamepoteza hata ile sura yao ya Kiislamu.

Nchi za Kiislamu zitaiga mitindo na maisha ya nchi zile zisizo za Kiislam. Waislamu wataomba misaada kutoka wale wasio Waislamu.Nchi za Kiislamu watauana miongoni mwao, watagombana kwa kutaka urafiki wa nchi zile ambazo zinamkanushaAllah swt (nchi za Kiislamu zitagombana miongoni mwao kwa kushawishiwa na nchi zile zisizo za Kiislamu )[9]

Imam Ali a.s.amebashiri kuwa utawala wa Bani Hashim utakwisha duniani. Mtawala wa mwisho atakuwa kijana mmoja mdhaifu, asiye na ujuzi wala utaalamu wowote na vile vile atakuwa akifuata ushauri wa watu wengi  (katika dunia hii leo kuna utawala wa Bani Hashim nchi moja tu duniani kote nayo ni Jordan ).

Miaka thelathini ya mwisho katika karne atakayodhihiri Imam Mahdi a.s. kutakuwa na vitu vya ajabu ajabu na vya kustaajabisha mno.

 Tanbihi   Kuanzia mwaka 1370 A.H., inahitaji uchambuzi hadi siku ya leo, dunia imeona maajabu ya mageuzi ya mapinduzi na mauaji ya kushtusha na mambo mengi ya ajabu ajabu yasiyoweza kusadikiwa na watu kuwa binadamu anaweza kufanya mambo haya maovu kwa binadamu mwenzake.

Kufika kwa Waturuki katika pembe la Bara la Arabia katika Hadith maneno ya Turki na Jazira yametumika. Wataalam wa uchambuzi wa maswala haya wanasema:"Neno Turuki lina- maanisha Warusi na Jazira ni Bara la Arabia, hivyo ni ubashiri mmoja muhimu sana wa kuzingatia kuwa Warusi wataingia Bara la Arabia yaani inawezekana wakaingia kwa mabavu (kwa nguvu) au wanaweza kuingia kwa upole kwa kutumia njia nyinginezo (tunaona Warusi wameingia katika Bara la Arabia ).

 

(42). Wazungu kuingia katika Palestina:

Watu wa Roma ni wazungu na Ramla ni Palestina hivyo kutakuwa na mvutano wa hali ya juu katika Bara la Arabia kwa sababu ya kugombania nguvu baina ya Waamerika , Wazungu  na  Warusi.

 Mtu mwenye kuheshimiwa mno kutoka Bani Abbas atatoswa majini katika mto Tigiris karibu na daraja jipya huko Baghdad.

 Kijiji cha Jabiya karibu na Damascus itadidimia ardhini.

 

 Ziwa Sawa litajaa kwa maji kwa mara nyingine tena. Ziwa hili liko karibu na mji mtukufu wa Qum lilikauka pale Mtume s.a.w.w alipozaliwa. Wale wote wanaokwenda ziara ya Masuma -i-Qum wanashuhudia ubashiri huu.

Taratibu za tawala za nchi zitakuwa zikipata sura mpya mpya za kutawala vile vile utawala wa kifalme utatokomea.

 Kutaonekana kitu kama kizingiti baina ya ardhi na mbingu, kweli litakuwa ni jambo la kustaajabisha kabisa hasa Mashariki ya kati.

 Jumuiya ya wale wasio waumini wataenea Bara la Arabia na nchi nyingine za Kiarabu (ama wao ni Warusi au Wachina kwani Warusi wameishajidhatiti katika nchi nyingi za Kiarabu).

 Kuwasili kwa Wachina katika Bara la Arabia ni ubashiri mkubwa wa vita vikubwa hali mbaya kabisa isiyoelezeka itatokea baada ya wao kuwasili huko.

 Kutakuwa na michafuko ya aina mbalimbali kuanzia Azarbaijan na Armenia. Machafuko haya yataenea hadi mlima mwekundu.Matokeo haya na hatima yake yatakuwa mabaya kiasi kwamba watoto watakuwa kama wamezeeka na wazee watatamani mauti.Machafuko haya yatafika mpaka mji wa Kufa kupitia Wast na vita hatari kabisa vitatokea karibu na mji wa Najaf.Kwa hakika maovu na matisho haya hayaelezeki Vile vile vita vitatokezea karibu na Teheran.

Kutakuwa na mipango mbalimbali ya kuzuia kizazi na  mbinu hizo zitashurutishwa kwa njia mbalimbali. 

UDONDOZI KUTOKA VITABU VYA KIARABU

Ingawaje mabashiri yote yaliyoelezwa katika kurasa zilizopita yametoka katika vitabu vingi vya Kiarabu mabashiri yafuatayo yanatoka khususan kutoka kitabu kimoja kiitwacho al-malahim wal fitan. Bashiri hizi zilikusanywa na bwana mmoja anayejulikana kwa jina la Ali ibn Musa ibn Jaafer ibn Muhammad ibn Taus Ali Hasan wal-Husaini. Kitabu hiki kilIssambazwa kwa mara ya kwanza katika  mwaka wa 604 A.H.

Taasisi inayojulikana kwa jina la Manshuratul  Atba'atul Haidariyyah huko mjini Najaf. Mabashiri haya yalikusanywa zaidi ya karne saba zilizopita:

(1).Mtume Mtukufu s.a.w.w.amesema:"Jihadharini na bendera nyeusi mwanzoni mwake ni mbaya katikati mwake kuna upotofu na mwishoni wake ni ukafiri   ( utawala huo unagawanywa katika sehemu tatu kipindi cha kwanza, kipindi cha pili na kipindi cha mwisho ).

(2).Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Mjikusanye mnapoona bendera nyeusi msiendeshe mikono yenu na mikuki yenu muisimamishe kutatokezea watu warefu na jumuia isiyoaminika isiyotegemewa itatokezea, mioyo yao itakuwa migumu kama chuma wao watakuwa matajiri lakini watasita kutimiza wajibu wao, wao watawaita watu katika mambo mema lakini wao wenyewe watakuwa wamepotoka majina yao yataanza katika majina ya urithi  (ukoo)  hoja zao na busara zao zitafanana na zile za wanawake, kutaongezeka kutokezea kwa ikhtilafu baina yao na hatimaye  Allah  swt  atawabainishia ukweli.

(3).Mtume Mtukufu s.a.w.w. ameshauri:"Kimbieni kwa usalama wenu pale mtakapoona bendera za rangi  nyekundu zikipepea huko Misri.Watakapofika Syria, lazima muanze kutenda matendo.Kimbieni hata kama mtaweza kufika mbinguni kimbieni juu ya mawingu kama mtaweza ama sivyo mjaribu kujihifadhi mahali popote duniani. Hadithi ya juu hiyo ilinakiliwa na Hasan.

(4).Rawi anasema:"Nilimsikia Abdullah ibn Omar akisema akiwa katika Ka’aba kutatokezea bendera nyeusi kutoka Mashariki na bendera za rangi ya njano kutokea upande wa Magharibi,watawala wa bendera zote hizo mbili watapambana vikali huko Syria kwa hakika ni maafa na maangamizo makubwa kabisa (kwa kuwa msemaji alikuwa akiongelea katika Kaaba hivyo upande wake wa Mashariki ni Iran na upande wake wa Magharibi ni Misri.).

(5).Hasan Basir ameripotiwa akisema "kutokea ndani mwa Teheran kutatokezea mtu mmoja atainuka, ataitwa jina la Shuayb ibn Saleh Tamimi, mtu huyo atakuwa  rangi nyeupe, kifua kipana na ndevu zilizochakaa. Mtu huyo atakuwa akiwaongoza watu elfu nne wenye bendera rangi nyeusi atakuwa na bendera ya Imam Mahdi a.s. ambavyo atakuwa hawezekani katika vita.

(6).Muhammad Hanafi anaripotiwa kwa kusema mwanzoni bendera nyeusi itakuwa ya Bani Abass na baadaye zitatokezea Khorasan.Kofia zao zitakuwa nyeusi na nguo zitakuwa nyeupe au inaweza kumaanisha upande wa juu wa bendera unawezekana ukawa mweusi na upande wa chini ukawa mweupe (kiongozi wa kikundi hicho atakuwa Shuayb ibn Saleh Tamim.Wao watawashinda wenyeji wa Sufiani na watafika hadi mji wa Jerusalem na baada ya kufika Jerusalem watamkabidhi Imam Mahdi a.s. mamlaka yote na vile vile watamsaidia. Kiasi cha watu mia tatu wa Syria watamsaidia Shuayb ibn Saleh Tamim ibn  Saleh.  Kitakuwa ni kipindi cha miezi sabini na miwili baina ya kuinuka  kwa Shuayb na kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.

 

(7).Makhul anaripoti kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Mimi nimeona vyema kutumia jina Turk  kuliko kutumia neno la Warusi. Waturuki watakuja mara mbili mara ya kwanza watatokezea upande wa Azarbaijan na mara ya pili majeshi yao yatapitia mto wa Furati (Euphrate) baada ya hapo wataacha mashambulizi yao (Hapa waturuki wanaomaanishwa kutokea upande wa Azarbaijan sio watu wengine bali ni Warusi) .

(8).Hodhaifa Yamani ameripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema: "Piganeni kabisa na Waturuki mtakapowaona wameingia Bara la Arabia. Mpigane nao mpaka washindwe ama sivyo wataharibu heshima yenu.Msaada wa Allah swt uwe pamoja nanyi  (Ubashiri huu unaelezea  uingiliaji  wa dola za Magharibi huko Bara la Arabia utakuja kutokomezwa )."

(9).Abu Hureira ameripoti kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Kufufuliwa kwa ajili ya siku ya Qayama haitatokea hadi hapo kupite vita dhidi ya Waturuki. Waturuki hao watakuwa na nyuso nyekundu, macho madogo na pua zilizo pana.Nyuso zao zitakuwa ngumu kama chuma kilichonyooshwa."

(10).Mtume s.a.w.w.amesema:"Waturuki watasonga mbele haraka haraka wakielekea Tigris.Watakuwa na vyombo vya kusafiria vya rangi ya njano wakijipanga katika mistari kuelekea mto wa Tigris."

(11).Mtume s.a.w.w. amesema:"Ninaona kuwa Waturuki wanasafiri juu ya mafarasi wenye masikio mafupi, mguu mmoja huku mguu mmoja upande wa pili na wanawafunga mafarasi wao kandoni mwa mto."

(12).Utambulisho zaidi wa Waturuki, Mtume s.a.w.w. amesema:"Wafuasi wangu itawabidi wapigane vita dhidi ya wale watu wanye nyuso pana,macho madogo na wenye miili migumu.Kutatokezea mashambulizi mara tatu.Safari ya kwanza watu wangu watakimbia ili kujinusurisha kwa mashambulizi,ya pili, baadhi ya watu wangu watauawa na wengine wataponea chupuchupu na katika mashambulizi ya tatu maadui watashinda. Na wao ni Waturuki. Kwa hakika mIssafara yao itakuwa inawekwa nje na kuzunguka Misikiti ya Waislamu. Umma wangu utakuwa katika hali ya hatari. Wao watakuwa wakikimbia, wakichukua kile chochote wapatacho ili waweze kukimbia navyo."

(13).Imam Hasan a.s ameripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema:"Siku ya Qayama haitafika kabla ya nyinyi kupambana na watu wafupi na wenye nyuso pana na mashambulio ya pili pamoja na wale watu ambao viatu vyao vitakuwa vimetengenezwa na nywele. Wale watu wa kwanza watakuwa ni Waturuki na wale wa pili watakuwa ni wa-Qurdi. "

(14).Kaab ameripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema: "Waturuki watakuja katika Bara la Arabia. Mafarasi wao watakunywa maji ya mto Furati.Hapo Allah swt atawaambukiza ugonjwa mbaya nao watauawa.Hakuna hata mmoja miongoni mwao atakayebaki hai."

Katika hadithi nyingine imeelezwa kuwa Waturuki watakuja katika upande wa kushoto wa Mto Tigris.Watakapofika Iraq wao watakumbana na kuanguka kwa theluji na magonjwa ya kuambu- kizwa hapo, wao watakufa kwa idadi kubwa sana.

(15).Kuingia Wa-China katika Bara la Arabiia - Abdullah ibn Omar anaripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema:"Bani Qantura(Wachina)watawadhalilisha watu wa Khurasan na Sijistan.Wao wataendelea na msafara wao hadi watakapofika katika mabustani huko Palestina, hapo baadaye watawaonya watu wa Basra waache ardhi zao waondoke.Hapo baadaye wao watajigawanya katika makundi matatu,kundi moja litaelekea Magharibi, kundi la pili litaendelea Syria na kundi la tatu litajihami dhidi ya  maadui.

(16).Habari za Bani Qantura:: Abu Hureira anaripoti kuwa washambuliaji watakuwa na macho kama ya mijusi.Nyuso zao zitakuwa na ngozi zilizo ngumu, wao watabainisha vita sehemu tatu: "Kwanza baina ya eneo la mto Furati na mto Tigris. Pili Kijiji cha Mazhar-e-Hamar,kijiji kaskazini mwa Syria, tatu ufukoni mwa mto Tigris wao watadhibiti njia zote zipitiapo hapo na kila atakayekuwa akipita atalazimishwa alipe Dinar mia moja.Na kiwango hicho cha kutoza watu hela za kuvuka zitakuwa zinaongezwa kila mara.

(17).Mtume s.a.w.w. amesema:"Katika kipindi hicho wenye mabendera makubwa watayachana mabendera madogo,hali hii ya kushambuliana itaendelea hadi hapo kutakapokuja kundi la watu wenye nyuso pana na macho madogo. Watu hao watakuwa ni Bani Qantura (Wachina).Wao watapitia Kurdistan huko Iraq na watawashinda baada ya kuwashambulia Wakurdi, baadaye watawakabili Waarabu na kutatokea vita vikali kabisa ambavyo vitasababisha miji kubakia mitupu, watu wote watakuwa wamekimbia. Hapo baadaye kutatokea mitetemeko na ardhi itapasuka na ardhi nyingi itadidimia watu watakimbia huku na kule bila kujua wanapokwenda. Eneo la kwanza la kuteketezwa litakuwa ni mji Baghdad.Kutafuatia na kuvurugika na kuchafuliwa kwa Misri. Mutakapoanza kuona hizi bashiri zikitokea huko Syria basi muelewe kuwa kuna kifo kila mahala.Hapo ndipo mtaona Wazungu wanaanza mbinu na hila zao, watakapofika Bara la Arabia kutazuka mapambano makubwa ya kuteketeza.

 

(18).Mtume s.a.w.w. amesema: "Utawala wa Waarabu utakwisha”. Kauli hii aliitoa mara tatu kiasi kwamba wanaoiripoti walimuuliza, Je ni nani atakayeumaliza utawala wa Waarabu?" Hapo  Mtume  s.a.w.w. alijibu: "(Bani Qantura) jumuia ile ambayo nyuso zao ni pana wana pua tambarare na wana macho madogo.Wao wataingia Bara la Arabia kwa sababu vita vikali vitakuwa  vimeanza kutokezea."

Hapo Waturuki wataleta masharti ya usuluhishi kwamba Waarabu wawarudishie wale wote wasio Waarabu. Waarabu watawaambia wale wasio Waarabu marafiki zao wajiunge na Waturuki. Hapo marafiki wa Waarabu watawaambia Waarabu, Ole wenu! Kwenu nyinyi kuupa mgongo Uislamu (kwa kuvunja umoja na jumuia yao).

Hapo baadaye marafiki wa Waarabu watapigana peke yao na watawashinda na kuwateketeza maadui zao.Waarabu watakapoona marafiki zao wamenufaika kwa vita wataanza kuomba hIssa humo.Hapo marafiki wa Waarabu watasema:"Kwa haki ya Allah swt! Hatutawapeni chochote kwa sababu nyinyi mmevunja uhusiano wetu."

JE WATURUKI NI AKINA NANI?

Ni udanganyifu kuelewa kuwa wale watu wanaoishi katika nchi ya Uturuki ya leo ndio wanaitwa Waturuki.Kwa mujibu wa mwanahistoria Farishta,asili ya Waturuki wanaanzia kwa Mtume Nuh a.s. ambaye alikuwa na mtoto Yafis na huyo alikuwa na mtoto akiitwa Turki.Popote pale kizazi hicho kilipofika waliitwa Waturuki.Mtoto mwingine wa Yafis alikuwa akiitwa Chin.Ardhi kubwa sana iliitwa kwa jina lake ambayo leo ndiyo China.Hivyo katika utafiti huu inatudhihirishia wazi wazi kabisa kuwa Waturuki na Wachina ni watu wawili waliotofauti.

Katika jangwa la Gobi kuliishi makabila mawili tofauti, kabila moja lilikuwa likiitwa Mongoli na lingine lilikuwa likiitwa Turuki mababu zao walikuwa sawa.Hao Wamongoli walikuwa wakijulikana kama Yun. Na mababu zao walifika hadi katika ya Urusi.Wao walikuwa wakijulikana kwa majina tofauti tofauti kama Yuji,Quishen n.k.Wachina waliendelea kuwaita Yuji.Kabila zilianza kujulikana kama Waturuki katika karne ya sita kizazi kimojawapo kiliishi Azarbaijan katika karne ya tano.Kwa mujibu wa baadhi ya wana historia wao walichukua sehemu muhimu iliyokuwa karibu na Marv hapo baadaye kabila hilo lilitawanyika mbele na kuchukua ardhi ambayo leo inajulikana kama Uturuki.Popote pale walipokwenda wao wanajulikana kama Waturuki na kwa sababu hiyo katika ramani utaona kuna sehemu nyingi zinazoitwa Turkistan ya China,Turkastan ya Urusi,n.k.Watu waliokuwa wakiishi katika Turkistani ya China walikuwa na macho rangi ya buluu, nywele nyekundu na warefu.Maumbile haya hayalingani na maumbile na wa-China wa siku hizi.

Waturuki ambao waliiteketeza Iran, Iraq n.k. walikuwa ni wa-Mongolia. Wachina wa siku hizi hawafanani na Waturuki na hivyo wao ndio wanajulikana kama Bani Qantura kwa mujibu wa Hadithi.Hivyo Waturuki ambao wanazungumziwa katika Hadithi tukufu za Mtume s.a.w.w. ni Warusi na Bani Qantura ni Wa-China na Bani Asfar  ni  Wazungu.

Tofauti hizi lazima tuzizingatie vizuri na tuzitilie maanani kabisa vivyo hivyo itabidi kuzingatia mipaka ya kijiografia ya China ya siku hizi haioani na ile ya zama za Mtume s.a.w.w.

Kauli ya Imam Muhammad Baqir a.s. ambayo imetolewa kutoka Majlis-i-Thannia ya Sayyid Muhsin  Al Amin  Al Husein, Al Amir wa Beiruti.

 

Imam  Ali a.s. amesema:"Kutatokea  mfarakano mkubwa sana baada ya kufika kwa Warusi katika Bara la Arabia na Wazungu kufika katika Palestina na mifarakano hiyo itasababisha kuangamia na kuteketea kwa Syria ambayo itatokea baada ya mapigano baina ya wapinzani wa bendera tatu (Bendera tatu inamaanisha kutakuwa na makundi matatu yanayopingana) bendera hizo zitakuwa ni za: (1).Sayyid Hasan, (2).Bani Omaiyya, na (3).Bani  Qais.

 

Mabango ya Sayyid Hasan yatatokezea Iran, bendera ya Bani Omaiyya itatokezea Syria na bendera ya Bani Qais itatokezea Misri. 

 

Imam a.s. aliendelea kutoa usia: "Lazima mtulie, msijitie kwenye harakati, mikono yenu na miguu yenu pale mtakapoona dalili hizi, lakini nyinyi hamtawaona (watu wa zama hizo). Dalili hizi ni: (1).Kuwasili kwa Waturuki katika Bara la Arabia, (2).Kuwasili kwa Wazungu katika Palestina,(3).Waturuki,Warusi,watakaribishwa vizuri kabisa pale watakapofika Bara la Arabia. Hivyo hivyo Wazungu  watakaribishwa vyema kabisa na Wayahudi pale watakapoingia Palestina. 

MAWAIDHA YA MTUME S.A.W.W. KUHUSU KUJIHAMI

Ibn Masud anaripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema: "Mjikumbatie pale mtakaposikia sauti toka mbinguni katika mwezi wa Ramadhani, kwa sababu kutakuwa na misukosuko mingi katika mwezi wa Shaban.Vita vya wenyewe kwa wenyewe na umwagaji wa damu kupindukia kiasi vitaanza katika mwezi wa Dhilqaad,mauaji na uporaji na kila aina ya wizi vitaanza katika mwezi wa dhil-hijjah.Mwezi wa Muharram ni mwezi wa pekee kwa aina yake  (kwa huzuni ya Muharramu ndiyo imepita mipaka yake isiyoweza kuelezwa).

 

Hapo baadaye Mtume s.a.w.w. alisema mara tatu: "Loh, loh, loh,! Idadi kubwa kabisa ya watu watauawa wakati huo."

 

Mwenye kuripoti alimwuliza  Mtume s.a.w.w. wakati huo:"Ewe bwana wetu !  Je hiyo sauti ya kutisha toka mbinguni itakuwaje na  itatokea lini?"

 

Mtume s.a.w.w. alimjibu:"Sauti hiyo ya kutisha na kushtusha itatokea katika mwezi wa Ramadhani katikati ya siku.Muwe tahadhari kwani sauti hii itamwamsha yeyote atakayekuwa amelala na yeyote yule atakayekuwa amesimama ataketi.Baada ya kumaliza sala ya Ijumaa muingie majumbani mwenu mfunge milango yenu yote na kuziba matundu  yote yatakayokuwemo ndani mwa nyumba zenu.Zibeni masikio yenu kwa uangalifu na mzizuie pumzi zenu.Mwangukieni Mola wenu mtakapohisi sauti hiyo na muombe Subhanal Quddus, Rabunal Quddus. "Mtu yeyote atakayefanya hivyo ataokoka na mshirikina ataangamizwa."

 

Muda huo tarehe, mwezi na siku tunavijua katika Hadith kwa mujibu wa Hijaz lakini sisi huku kwetu tuangalie tofauti ya muda ili tujue kwetu hapa itatokea muda gani,vile vile katika baadhi ya Hadith Maimamu a.s.  wameripotiwa kusema tarehe 23 mwezi wa Ramadhan. Jambo hili linafanya swala hili liwe wazi zaidi.

 

Jambo lingine la kuzingatia hapa ni kwamba:"Usia huu tumepewa kama tahadhari."Labda inawezekana tunatanabahishwa na mashambulizi ya ndege na kutupwa kwa mabomu kunaweza katika zama hizo kukazuka vita vikali, ndege zitaanza kutupa rIssasi ovyo na mabomu ambavyo vitaangamiza watu hivyo watu wanashauriwa kuingia majumbani kujifungia ndani na wamwombe Allah swt awaepushe na  balaa ipite.

KUONEKANA MKONO NA USO  MWEZINI

 

Imerekodiwa katika Majlis -i- Thannia kuwa Moman anaripoti kutoka  kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. ambaye anasema:"Kabla ya kutokezea sauti kubwa ya mlipuko wa anga kutaonekana dalili tatu katika mbingu. Mwenye kuripoti alimwuliza: "Je ni dalili gani hizo "Imam alimjibu:"Uso wa mwanadamu utaonekana ukinga’a na mkono utaonekana katika mbingu(labda inamaanisha mwanadamu atafika mwezini na katika stesheni zinginezo huko juu).

Kutokezea kwa Sufiani: kuinuka na kuanguka kwake.

 

(1).Hudhaifa Yamani ameripotiwa akisema:"Wa-Sufiani wataingia Misri na kuiteka nchi hiyo kwa miezi minne. Atakuwa na utawala wa mauaji na wenye vitisho sana wanawake watalia kwa kupoteza heshima zao, jamaa zao na hadhi zao. Watu watakuwa wakiomba wafe ili wapone na dhuluma watakazokuwa wakifanyiwa".

 

Katika Hadith nyingine zinaripotiwa kuwa baada ya Sufiani kuiteka Misri,Sufiani atatuma jeshi lake kwenda Madina hawa wanajeshi watakuwa waovu kabisa na kupambana na Muslim ibn Akbar baadaye wataelekea Makkah.Watakapofika Beda wote watakufa kwa kupasuka ardhi na wote watatumbukia katika ardhi na kumezwa.

 

(2) Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:"Uasi wa Sufiani na kudhihiri kwa Mahdi a.s. vitatokea katika mwaka mmoja.

 

Katika habari nyingineyo imeripotiwa kuwa Sufiani, Yamani na Khurasani wote watatu watatokezea katika mwaka huo mmoja.

 

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:"Sufiani atatokezea katika mwezi wa Rajab na atamiliki Damascus,Yemen,Jordan ,Palestina na  Qansain.

 

Imam Zainul Abedin a.s.amebashiri kabla ya kudhihiri kwa Mahdi a.s.,atatokezea mtu kutoka Kuwait aitwaye Auf Aslami. Huyo atauawa katika Msikiti huko Syria, baada ya hapo Shuayb ibn Saleh atatokezea katika Samarkand na Sufiani atatokezea huko Palestina. 

MOTO

(1).Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: "Utakapoona moto mwekundu njano ukiwaka siku tatu au siku saba mfululizo huko Mashariki basi ujue ndio wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.[10]

 

(2). Moto mkubwa sana utatokezea huko Bara la Arabia. 

 

Imam Jaafer Sadiq a.s. vile vile amebashiri kutokezea kwa moto katika Mashariki.

 

 

(1).Imerekodiwa na Imam a.s.kuwa Mtume Issa a.s.atateremka Baitul Muqaddas wakati wa sala ya alfajiri ambapo watu watakuwa wanajitayarisha kusali.Imam Mahdi a.s.atamkaribisha na kumwambia,  karibu , njoo utuongoze katika sala, Mtume Issa a.s. atamchukua Imam mbele na yeye mwenyewe atasali nyuma ya Imam a.s.

 

(2).Dajjal atakuwa na wanajeshi elfu sabini, Mtume Issa a.s. atakapowaona tu miili yao itakufa ganzi, hali yao ya kupigana vita na Mtume Issa a.s. na Imam Mahdi a.s. itayeyuka kama vile chumvi inavyoyeyuka katika maji. Mtume Issa a.s. atawateketeza Mayahudi wote na ataivunja  mIssalaba na kuwaua nguruwe.Hivyo kurudi kwa Mtume Issa a.s. humu duniani kunamaanisha ndiyo  mwisho wa dini ya  Judea na dini ya Kikristo kwa sababu atakanusha kusulubiwa na kuwapo sharia katika Tawrati inayoharamisha ulaji wa nguruwe. Hivyo tunaweza kuelewa vyema zaidi sababu ya Allah swt kumweka hai Mtume Issa a.s. hadi kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. kwa sababu mtu yeyote anapotaka kukabiliana (kuhusu mazushi) vyema na watu hivyo inambidi yeye mwenye akabiliane nao ndipo litakapokuwa jambo la msingi.

 

Jabir Jaufi anaripoti kutoka Imam Jaafer Sadiq a.s. kuwa:"Wakati khalifa wa Bani Abbas alipozuru Khorasan, nyota yenye mkia ilitokezea ambayo ilikuwa ikiitwa Al- Qarb-Zushshifa. Nyota hii ya mkia ilionekana kabla ya kuangamia kwa ukoo wa Mtume Nuh a.s. na wote walizama katika tufani  ya maji vile vile nyota hii ilito- kezea mbele ya Mtume Ibrahim a.s. na hatimaye yeye akatupwa katika moto.Nyota hii ilionekana tena kabla ya kuangamizwa kwa Firaun katika zama za Mtume Musa a.s.Nyota hii ilionekana tena wakati Yahya ibn Zakaria (John Babtisti alipouawa).Hivyo mwombeni Allah swt awaokoeni wakati mnapoona hii nyota yenye mkia mbinguni.Kuonekana kwake kutafuatia kwa kupatwa kwa mwezi na kupatwa kwa jua.Baada ya kuonekana kwa nyota yenye mkia kutachomoza bendera nyeusi na nyeupe ama bendera ya rangi ya buluu na nyeupe huko Misri,na huu ndio mwanzo wa machafuko na majanga na machafuko ya kila aina kutokezea. Nyota hii itaonekana katika mwezi wa Safar (mwezi wa pili katika Kalenda ya Kiislamu).

 

Vile vile imerekodiwa kuonekana kwa nyota yenye mikia miwili huko mbinguni na hii ni ishara katika kipindi kifupi kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. nyota hiyo itaonekana iking'ara kama mwezi.

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Kutaonekana mstari wima wa mwanga baina ya ardhi na mbingu katika mwezi wa Ramadhani.Shawwal utakuwa ni mwezi wa machafuko.Kutakuwa na macha- fuko na magomvi kila mahali katika mwezi wa Dhil-Qaad.  MIssafara ya wale waendao kuhiji itashambuliwa na kuporwa,na barabara ziendazo kuhiji zitawekewa vipingamizi.Haya yote yatatokea katika mwezi wa Dhil-hijja wakati mambo ya kutisha mno ya mwezi wa Muharram hayawezi kuelezeka. 

 

 

(1).Abdullah ibn Umar ameripoti kuwa Mtume s.a.w.w. amesema: "Mwisho wa dunia utaanza pale kutakapoanza kushtushwa kwa vichwa. Na wakati haya yataanza kutokea, basi ndio mwanzo wa maangamizo ya mwanadamu".

Alipoulizwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. juu ya umuhimu wake,alijibu ndiyo maangamizo ya Syria.Maangamizo na mateketezo hayo yataanzia Syria.

 

(2).Katika kitabu cha Al-Malahim wal Fitan imeandikwa kuwa upotofu utazuka na kutawanyika katika Syria kama vile mchezo wa watoto. Na wala hakuna nyumba yoyote itakayosalimika.Hayo yataendelea mpaka kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.

 

Utafika wakati wanaume wataanza kuwauza wake zao ili mradi wapate chakula kidogo.Vile vile utafika wakati ambapo baba atamwuza binti wake mzuri kwa hoja hiyo hiyo. 

 

Imeripotiwa kuwa Imam Mahdi a.s.atatokana, atakuwa ndiye Khalifa wa mwisho wa Bani Hashim.Yeye atatawala kwa muda wa miaka arobaini.Yeye ataikomboa Roma na Kostantinopoli.

 

Hadith kama hiyo imeripotiwa na Muhammad Hanafi akiongezea kuwa Jerusalem itajengwa upya wakati wa utawala wake.Mtume Issa a.s.atatokezea baada ya kukombolewa kwa Roma na Kostantinopoli. 

 

KUISHINDA INDIA

Imam Mahdi a.s. atapeleka batalioni ya jeshi lake moja kutoka Jerusalem kwenda India.  Jeshi hilo litaishinda India na kuchukua mali ya thamani iliyokuwa imezikwa hadi Jerusalem.Mji huo mtukufu wa Jerusalem utarembeshwa.  Jeshi hilo litakuwa na kituo chake hapo India hadi  kushindwa kwa Dajjal.

MAAFA YATAKAYOWAFIKIA  WAISLAMU

(1).Imerekodiwa kuwa Abdulla ibn Umar amesema:"Umma wa Mtume Muhammad s.a.w.w. watakabiliana na maafa matano mawili kati ya hayo yamekwisha kupita na matatu yatatokezea:- (a).matatizo katika Urusi (b).Matatizo yatakayoletwa na Wazungu (c) matatizo yatakayoletwa na Dajjal. Baada ya hapo hakutakuwa na matatizo yoyote lakini matatizo haya matatu yatakuwa makali na mabaya kabisa kiasi kwamba watu watahama kutoka nafasi moja kwenda nafasi ya pili kama wanyama na watu watauawa kama ng'ombe na mbuzi wanavyouawa kwa idadi kubwa kabisa.

 

(2).Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Umma wangu utafanya maovu yote kama vile mauaji hayo yalivyokuwa yakifanywa na umma wa Mitume iliyotangulia.

 

(3).Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.kabla ya kudhihiri kwa Mahdi a.s. makafiri watadhibiti mito mitano mashuhuri duniani.(1).Saihun,(2).Jaihun (3).Tigiris, (4).Furati, (5). Mto Nile

 

(4).Imam Ali a.s. amebashiri kudidimia na kuanguka kwa utawala wa Bani Hashim kabla ya kuja kwa Imam Mahdi a.s.

(5).Imam Ali a.s amesema:"Zipo dalili kumi za kuja kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.(1).Kuchomwa moto kwa bendera katika mitaa ya Kufa(2).Misikiti itakuwa haitumiki(3).Njia ziendazo Hijja zitafungwa(4).baadhi ya sehemu zitadidimia ardhini(5).Kutatokezea mitetemeko mikali sana katika ardhi katika baadhi ya sehemu.(6).Watu watatoka majumbani mwao katika hali ya mivurugano(7).kutaonekana nyota yenye mkia wa ajabu kabisa.(8).kutaonekana vitu vya ajabu mbinguni(9).kutakuwa na mauaji ya umwagaji damu (10).Unyang'anyi na wizi vitakuwa ni vitu vya kawaida."

MUDA WA BINADAMU JUU YA ARDHI

Abdullah ibn Umar ameripotiwa akisema:"Mwanadamu ataishi juu ya ardhi hii miaka mia moja sabini baada ya kuchomoza jua kutoka Magharibi.

KUSHIRIKISHWA  KWA WANAWAKE

Imerekodiwa katika Raudhatul - Kafi kuwa mwanamke atapanda mimbar na kuwahutubia watu. Kutakuwa na wanawake watawala na magavanana wabumge. Wanawake watashirikiana bega kwa bega pamoja na waume zao katika kazi zao.Wao watawapanda farasi na kuendesha magari n.k.Wanawake wataanzisha taasisi zao na vilabu vyao.Wanawake wataanza kutengeneza nywele zao ambazo zitakuwa sawa sawa na nundu za ngamia. Mambo yote haya yatatokea katika zama za mwisho wa dunia. 

MZOZO WA KUANDAMA KWA MWEZI

Watu watakuwa wameikhtilafiana mno juu ya swala la kuandama kwa mwezi . Wao hawatakuwa wakifunga siku ya kwanza ya Ramadhani wakati ambapo siku ya Iddi watakuwa katika hali ya saum.  Hadithi hii imetolewa katika Biharul Anwaar. [11]

ALA ZA MUZIKI

Ala za muziki zitapatikana huko Makkah na Madina.

WATU MATAJIRI

Watu matajiri watakwenda Hijja kwa matembezi na watu wa daraja la kati watakwenda kwa ajili ya biashara na masikini watakwenda kujionyesha kuwa wao pia wanakwenda Hijja kuwa nao wanao uwezo.  (Biharul Anwaar ).

GHUBA YA AQABA

Katika kitabu cha Ilzaam-un-Nasib  imeandikwa kuwa ardhi ya Aqaba itageuka kuwa nyekundu kwa sababu ya damu ambayo itamwagika kwa sababu ya vita vikali vitakavyokuwa vikiendelea hapo. 

KUHUSU OMAN

Msemo huu ufuatao wa Imam Ali a.s umetolewa kutoka hutuba iitwayo Bayyinah  amesema: "ninawasikitikia watu wa Oman kwani wao watazingirwa pande zote, waume wao watauawa na wake zao watachukuliwa mateka. "

KUHUSU TEHERAN

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:"Watu wa Ray (Teheran) watauawa katika mamilioni wakati huo kitovu cha Ilimu ya dini kitakuwa ni Qum na haya yatatokea kipindi kifupi kabla ya kudhihiri Imam Mahdi a.s. 

 

MAFURIKO, NYOKA NA NZIGE

Imeandikwa katika kitabu cha Nur-ul-Anwaar kwamba makundi makubwa makubwa ya nzige ni dalili mojawapo ya kudhihiri kwa Imam. (imetokezea hivyo katika mwaka wa 1254 A.H. katika Bara la Arabia ;1268 A.H.katika Iran na nchi za Sudan na Somalia tumesikia kuwa mambo haya yakitokea ).Vile vile miongoni mwa dalili za kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. ni mafuriko,nyoka katika maji.Mambo haya ni ya kawaida siku hizi kusikia kuhusu mafuriko.

 

DALILI ZA AJABU NA KUSHANGAZA MNO

Mtume Mtukufu s.a.w.w.alimwambia Jabir "Maisha yako yatakuwa mema na wewe utainuliwa siku ya Qayama ukiwa umeongoka. Lakini ole wa wakati ule, wakati ambapo Ukristo utakuwa na nguvu duniani na wakati ambapo ng'ombe dume watakapoanza kuongea.Zama hizo vitu vya ajabu vitaanza kutokezea.Kutakuwa na moto kila mahala (vita).Bendera ya utawala wa Othman utakuwa katika Bonde Jeusi.Basra itakumbwa na misukosuko.Baadhi ya watu watawakalia watu wengine na kuwanyanyasa. Majeshi yatatembea kati ya Taliqan, Shuyb ibn Saleh Tamim atakubaliwa.Katika Khuzistan, watu watakula viapo vya kumtii Sayyid Musawi.Bendera ya Wa-Qurdi shupavu itabuniwa. (Hadith hii ni ndefu mno isipokuwa tumechagua yale yaliyokuwa yakihusiana na somo letu.)

UBASHIRI WA BAADA YA VITA VYA NAHARWAN

Baada ya Imam Ali a.s. kutokea vita vya Naharwan, alisema:"Ni jambo la kustaajabisha mno, kwa matukio yatakayotokea baina ya Jamadiul Aakhir na mwezi wa Rajab.Hakutakuwa na maelewano yoyote popote pale.  Mapanga yatavuma na sauti baada ya sauti itasikika. "

HADITH  MUFADHDHAL

Mufadhadhl  ibn  Omar alimuuliza Imam Jaafer Sadiq a.s.:"Ewe mola wangu, Zuura  ni sehemu ipi?"

 

Imam a.s. alimjibu:"Hiyo ni Baghdad ambayo itakuwa ni kitovu cha adhabu na maangamizo ya Allah swt. Ole! sehemu hiyo kutachomoza kwa bendera za rangi ya njano na hapo bendera za kutoka nchi mbalimbali zitakusanyika.Adhabu za Allah swt zitateremshwa nchini humo.Matukio yasiyojulikana au yasiyopangwa au yasiyosikika au yasiyoonwa kabla ya hapo yatatokea huko Baghdad.Kutakuwa na hujuma za mapanga na hujuma hizo zitaongezeka mno. Mji huo utaongezeka kwa idadi ya watu na vile vile utakuwa ukiteketezwa, hali hiyo itakuwa ikitokezea kila mara lakini kufikia kipindi cha mwisho, kutakuwa na matendo maovu mengi sana kiasi cha kuwa mustahiki wa adhabu za Allah swt.Michafuko itakuwa imekithiri hadi hapo Hasan mtu kutoka Kazwin na Dailam atapokuja pamoja na jeshi lake juu ya mafarasi weupe.Mkuu wa kikosi chake atakuwa mtu wa Tamin ajulikanae kwa jina la Shuayb ibn Saleh.Wao watamkabili mkandamizaji na kutuliza moto wa michafuko. Baada ya hapo wataondoka kuelekea mji wa Kufa.

WAKATI MAALUM

Imeandikwa katika kitabu cha Kamalud-din kuwa Husein ibn Khalid alimwuliza Imam Ridha a.s. "Ewe Mola wangu ! Je wakati maalum ni lini."

 

Imam alimjibu: "Wakati maalum ni wakati ule wa kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. "Khalid  aliuliza: "Je huyo Mahdi katika ahadi zenu ni nani?"

 

Imam alimjibu:"Yeye atakuwa ni wa nne katika kizazi changu, Allah swt ataondoa dhuluma na ukandamizaji duniani kote kwa kupitia huyu Mahdi a.s.Kwa kuwa kipindi chake cha kuwa mafichoni (ghaibat) utakuwa ni muda mrefu hivyo watu wataingiwa shaka na wasi wasi na watu watakuwa na shaka iwapo amezaliwa au bado hajazaliwa.

 

Kabla ya kuja kwa Imam Mahdi a.s. kutasikika sauti kubwa duniani kote kutoka mbinguni.Habari hiyo itawajulisha watu kuwa mwokozi wetu ameishafika karibu na Al- Kaaba. Kudhihiri kwake kutaleta nuru duniani kote. Jina la baba yake ni Hasan.Yeye atakuwa ni  Qaim -bil- Haq  na  Al-Muntadhar. 

Mwenye kuripoti anauliza: "Je kwa nini majina yake yawe hayo?"

 

Imam alimjibu:"Watu wengi wenye kuamini katika Uimam labda watakuwa wameishageuka makafiri."Yeye ni yule anayengojewa, kwa sababu ya muda mrefu wa yeye kubakia mafichoni,katika kipindi hicho watu wengi wataanza kubishana na wataleta mzaha kwa swala zima hili ni wachache tu waliowaumini watakaosubiri tukio hili la Imam Mahdi a.s.kwa wale watakaofanya haraka (kwa sababu watatokezea wengi ni waongo ).Basi hao watakuwa wamepotea na wale Waislamu halisi wataokoka.

 

MADONDOO YA KUDHIHIRI IMAM : KITAB AL- IRSHAD

 

Kutoka dalili na mabashiri ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. hapa kuna madondoo machache ambayo yamechambuliwa:(1).Uasi wa Sufiani,(2).kuuawa kwa Hasan,(3).Ikhitilafu baina ya Bani Abbas kwa matakwa ya dunia.(4).Kupatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani, ikifuatiwa na kupatwa kwa mwezi mwishoni mwa mwezi huo wa Ramadhani.(5).Beda (mahala baina ya Makkah na Madina) itadidimia ardhini, (6) Ardhi katika upande wa Mashariki na upande wa Magharibi zitadidimia,(7)Jua wakati wa asubuhi litaonekana liko papo hapo bila kutembea hadi wakati wa mchana na baadaye litachomoza kutoka Magharibi.(8)Mcha Mungu atauawa nyuma ya msikiti wa Kufa pamoja na watu sabini wengine.(9) Mtu mwema kutoka ukoo wa Bani Hashim atachinjwa baina ya Rukn na Makam huko Makkah. (10)Kuta za Msikiti wa Kufa zitaporomoka.(11)Bendera nyeusi zitatokezea huko Khorasan.(12)Mtu kutoka Yemen ataongoza uasi. (13)Mtu atakayetokea nchi za Maghreb ataonekana huko Misri na ambapo atapata mamlaka makubwa.(14)Warusi watafika Bara la Arabia,(15)Wazungu watafika Palestina.(16)Upande wa Mashariki kutaonekana kwa nyota yenye mkia. Mwanga wake utaonekana kama ule wa mwezi na ncha zake zote zitakuwa moja (zitaungana).(17)Kutaonekana uwekundu mkubwa sana mbinguni.(18)Kutazuka moto mkubwa sana katika Mashariki ya kati ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu hadi saba. (19)Wale wasio Waarabu watawafukuza Waarabu kutoka ardhi zao.(20)Utawala wa kifalme utakwisha nchini Iran.(21)Wamisri watamuua kiongozi wao.(22) Bendera tatu zitakusanyika Syria.(23)Kutazuka mizozo mikubwa na Syria itateketezwa(24) Bendera za Waarabu na Bani Qais zitatoka Misri.(25)Bendera ya Banu Kinda itapepea Khorasan.(26) Jeshi kubwa sana litapita Hira(27) mabango meusi yatafika kutokezea Mashariki.(28).Maji ya mito ya Furat yatafurika katika mitaa ya Kufa.(29)Kutatokezea watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume. (30) Sayyid kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imamu Mahdi (31)Mtu mwenye heshima kubwa kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai karibu na Khankin.(32) Kutajengwa na daraja katika Baghdad katika sehemu za Kharah.(33) Kutakuwa na tufani ya upepo mkali katika Baghdad wakati wa asubuhi na kutafuatiwa na kupasuka kwa ardhi ambamo baadhi ya sehemu itadidimia ardhini.(34)Mauti,vifo na maangamizo yatakithiri huko Iraq kiasi kwamba watu watakuwa kama wamewehuka (35)vikundi vitapigana mno huko Iran.(36) Sura za jumuia zitachafuliwa.(37)Watumwa wataanza kutawala nchi za Mabwana wao.(38) Sura kama ya binadamu itaonekana karibu na jua.(39) Makaburi yatafumuliwa na (40) waliokufa watapewa uhai.(41)Kutakuwa na mvua itakayonyesha kwa mfululizo wa siku ishirini na nne ambayo itahuisha ardhi iliyokuwa imekufa.  Kwa hakika wakati huo ndio utakuwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.

 

Miongoni mwa dalili na bashara za hapo juu kuna mengineyo yenye masharti.  Allah swt tu anaelewa kitakachotokea na lini.

MAFAFANUZI WA DALILI NA BASHARA KWA MUKHTASARI

Vitabu vingi vimeandikwa juu ya bashara na dalili za kipindi kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. kwa hakika swala hili lipo kwa mapana sana kiasi kwamba ni vigumu mno kukusanya kwenye kitabu kama hiki. Hata hivyo kumefanywa juhudi kubwa sana ya kuweza kukusanya mabashiri haya kwa kiasi ilivyowezekana.Tumejaribu kuona kuwa mengi yametokezea na mengi bado yatatokezea.Wakati unakwenda ukiiva kwa ajili ya matukio mengine kutokezea, na mengine yapo yanatokezea lakini habari bado hatujazipata. Hapa chini tumejaribu kutoa baadhi ya maelezo yetu ambayo hatuwezi kujidai kuwa sisi ni mabingwa  wa mambo haya, anayejua zaidi ni Allah swt peke yake. 

 

Inaonekana kuwa sura ya Islam itabadilika sana siku za mbeleni.Mashauriano yataonekana ni mambo ya upweke.Kutatokea mabadiliko katika maisha ya jamii na ya kijumuia na ya kiutamaduni,tamaduni za binadamu zitachafuliwa mno.Hukumu za Allah swt zitapuuzwa na hazitatekelezwa.Watu watawakimbilia wale wasio mtii Allah swt, hivyo dunia nzima itajawa kwa vitisho na ukandamizwaji.Haki na usawa utakuwa umetokomezwa kabisa.Maasi na madhambi yatakuwa yamekithiri kila mahala.

Kwa yote yaliyoandikwa hapo juu inamaanisha waziwazi kuwa ulimwengu umejiandaa kwa ajili ya adhabu na ghadhabu za Allah swt na wa hakika kama tutatenda kinyume na maamrisho ya  Allah swt basi hivyo tukae tayari kwa ajili ya adhabu zake. 

 

Mwanzoni mwake kutatokezea kwa michafuko huko Mashariki ya kati ambayo yataenea dunia nzima hapo baadaye.Kutatokezea maajabu mbinguni na kuonekana kwa nyota yenye mkia inayong'aa huko mbinguni. 

 

Warusi wataanza kuingilia kati mambo ya Mashariki ya kati.Wazungu watajiingiza huko Palestina na kuleta uchafuzi.Na hivyo kutaanza kwa vita ambavyo vitaenea duniani kote.Labda itawezekana silaha za kinyukilia zikatumika huko na zikasababisha mitetemeko ya ardhi, kudidimia kwa ardhi na kuteketezwa kwa watu. Baadhi ya sehemu zitateketezwa kabisa. Nchi za Kiisilamu zitaathirika sana kwa hayo.Vita hivyo vya huku na huko mwisho vitakuja kuwa vya dunia nzima. Misri itachafuliwa kabisa kabisa. Baghdad na Basra vitateketezwa kabisa, miale ya mioto itatokezea Bara la Arabia.  Kutalipuka moto mkali sana katika sehemu za machimbo ya mafuta  huko Aden.

 

Katika vita hivi vya dunia, kutatumiwa silaha mbaya kabisa zenye kuleta maangamizo na maafa makubwa kabisa. Anga zetu zitakuwa zimejaa kwa gesi ya sumu kali.Kujiingiza kwa Wachina katika vita hivi kunamaanisha  hali kuchafuka kabisa.Takriban theluthi moja ya dunia nzima watauawa katika vita hivi.

 

Baada ya kumalizika kwa vita hivi itafuatia hali ya kuangamiza kabisa.  Kutatokezea magonjwa ya kuambukizwa, kutatokezea balaa za kila aina ambazo zitaharibu maisha ya watu na watu watakufa wengi mno. Ukame utawamaliza watu wengi sana kiasi cha theluthi moja ya wakazi wa dunia nzima wataweza kuponea chupuchupu maafa haya.

 

Mwanadamu ameishafika mwezini, Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa uso wa mwanadamu utaonekana mwezini na mkono wake utaonekana mbinguni yaani mwanadamu ataweza kuzishinda anga za juu. Binadamu pamoja na kuwa na maendeleo haya ya kIssayansi lakini kwa kutokuwa na umoja, upendo na undugu wataimaliza dunia. Utumiaji wa silaha za kIssasa na za hatari kabisa zitabadilisha hali ya hewa ya ulimwenguni na taratibu za jua zitaathirika sana, hasa dunia yetu hii.Kwa hali hii ama jua litaonekana limebaki pale pale ama dunia yetu hii itaacha kuzunguka kuanzia asubuhi hadi mchana.Kwa hivyo kutatokezea kupatwa kwa jua na mwezi kwa mwezi mmoja jambo ambalo kihesabati haiyumkiniki kwa sasa. 

 

Usiku wa Alhamisi tarehe 23 mwezi wa Ramadhani kutasikika mshtuko mkubwa sana angani na hii ndiyo dalili halisi ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. Kwa wakati huo Mashariki ya kati itakuwa imekumbwa na majanga mengi hasa ya njaa na vile vile Sufiani atakuwa ametokezea.Wakazi wa Algeria na Morocco watasonga mbele kuelekea Misri huku wakiwa wamebeba mabendera ya rangi njano. Mtu mmoja kutokea kizazi cha Imam Hasan a.s. atatokezea kutoka Taliqan.Kamanda mkuu wa jeshi lake atakuwa Shuayb ibn Saleh Tamim. Jeshi lao watakuwa wamepanda farasi weupe na huku wamebeba bendera zenye rangi nyeusi na nyeupe.Hao makamanda wawili watajaribu kurekebisha na kunyoosha taratibu za dunia ambazo zitakuwa zimevurugika na kupotoshwa kabisa.Katika vita vyao vitukufu hivi wao watapitia Kirman na Multan, kupitia njia za mwambao watafika Basra na hapo baadaye watasonga mbele hadi Kufa.

 

Kutasikika sauti toka mbinguni kuwa Imam Mahdi a.s. amedhihiri.Siku hiyo hiyo mchana kutasikika na sauti potofu ya uongo kama vile ilivyosikika hapo awali.  Watu wengi watapotoshwa kwa sauti hii ya pili, lakini watu wapatao 313 wataweza kumfikia Imam a.s. Kwa vyovyote vile na watakutana naye huko Al-Kaaba, haya yatatokea alfajiri. 

 

Jeshi la Sufiani likielekea Kaaba litateketea katika kudidimia kwa ardhi huko Beda. Watu wawili ndio wataponea chupuchupu katika gharika hii.Hapo Imam Mahdi a.s. pamoja na watu wake wataelekea huko Syria na wataweza kumwangamiza Sufiani .Hadi wakati huo Mtume Issa a.s.atakuwa ameteremka duniani. na ataungana na Imam Mahdi a.s. na wote kwa pamoja katika vita vya Sufiani wataweza kumuua huyo Sufiani.

 

Imam Mahdi a.s hapo baadaye ataelekea Kufa.Huko Sayyid Hasan atampokea na kumpa heshima zote.  Kiasi cha wanajeshi elfu nne wa Zaid wa jeshi la Hasan wataasi na watakataa kutii amri hiyo na hatimaye watauawa nao. Hapo kutakuwa na kikao cha hali ya juu katika Msikiti wa Kufa. 

 

Baada ya hapo Imam Mahdi a.s.ataelekea Jerusalem na ataufanya mji huo uwe makao yake makuu.Kutokea hapo atawatuma wajumbe na mabalozi duniani kote.Ulimwengu mzima utamkubalia na kumtii na kutakuwa na dini moja duniani kote -ISLAM. Dajjal atatokezea na ataleta maharibifu na ataleta kila aina ya balaa duniani lakini naye atafyekwa katika kipindi hicho.

 

Utawala wa Imam Mahdi a.s.utakuwapo kwa muda wa miaka sabini na dunia yetu itakuwa ni mahala pa salama, amani na wema.Dunia hii itaendelea kuwapo kwa kipindi kirefu lakini kutatokea mabadiliko katika mwenendo wake. Maimamu Watukufu a.s. wote watakuja tena humu duniani.Baada ya muda mrefu kabisa ndio kutafika kipindi cha Qayamat Kubra. Ahadi ya Allah swt itatekelezwa wakati  huo.Hali halisi na vitisho vya Qayama siku  ya mwisho ya dunia imeelezwa vyema katika Quran Tukufu.

 

Katika vitabu vinginevyo vimeandika kuwa Imam Mahdi a.s. atatawala dunia kwa muda wa miaka saba vile vile imeongezwa kuwa miaka kumi yetu ya hivi sasa itatokea kuwa mwaka mmoja wakati huo wa Imam Mahdi a.s. (hivyo ni sawa na miaka sabini).

NDUGU WA MIRZA NA  MAAJABU YAO

 

Mtume s.a.w.w.na Ahl-i-Bait a.s.,wamesema kuwa tukio la Imam Mahdi a.s.halitatokea hadi hapo watokee watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume.Msemo wa watu watukufu hawa haiwezi kuwa uongo,maneno waliyozungumza hawa viongozi wetu Watukufu haiwezi kamwe kuwa uongo na hivyo inamaanisha kuwa kutaendelea kutokezea kwa mitume wazushi.Hivyo tujue idadi ya mitume wazushi wameshatokezea na bado wanaendelea kutokezea na hatima yao ipo karibuni.

 

Madai ya hawa wazushi haitadumu kwa muda mrefu na itapasuka kama mabaluni kwa sababu watu wa zamani walikuwa na mapenzi sana na dini zao.Lakini siku hizi, watu wameiga mitindo na tabia za nchi za Magharibi hivyo wamekuwa na imani hafifu kabisa za dini zao.Hivyo watu imani zao zimekuwa hafifu sana na zisizokuwa na msimamo kwa sababu kila mpiga firimbi yake anapata wafuasi wake wasiojua mbele wala nyuma.Hivyo katika hali kama hii watu imani zao kuwa dhaifu na hawana ilimu ya dini zao sawa sawa itasababisha kutokezea mitume kama hawa na miongoni mwa watu walioweza kufaidi hali hii ni Miza wawili.Mzushi mmoja alikuwa ni mtu kutoka Iran.Dini aliyoianzisha yeye inaitwa dini ya Bahai. Na mzushi mwingine alikuwa ni Mhindi.Wafuasi wake wanajulikana kwa jina la Kadiani au Ahmadia.

 

Watu hao wawili walikuwa hodari sana katika mbinu zao.Madai yao ya ajabu imewapatia sifa nzuri miongoni mwa watu.Mirza Ali Muhammad Bab alijitangaza kwanza kuwa yeye ni Imam na baadaye alidai kuwa yeye ni Mtume.Na baada ya kuona mbinu zake za upotofu zimeshika mizizi vizuri na ameweza kuwahadaa watu kwa wingi alijitangaza kuwa yeye ni Mungu na alikitiyarisha kitabu kinachoitwa Al-bayan.

 

Huyu mzushi wa India alijitangaza kuwa yeye ni Mahdi na baada ya kuendelea mbele alijiita yeye ni Mariamu (mama yake Mtume Issa a.s.), akabadilika akawa Yesu -Masiha aliyeahidiwa.Watu hawa walikuwa ni waandishi wazushi na madai yao yanaonekana wazi katika vitabu vyao.Wazushi hawa katika kuwapoteza watu na kuwa zuzua watu wameweza kupata wafuasi wengi mno na hata leo wapo wanaowafuata.Haishangazi kila mwenye kuonyesha maon- yesho kuvutia watu.Hata kama watu watajua katika maonyesho hayo hakuna ukweli wowote lakini wanakusanyika kuona.Watu hawajali kuwa wao wanapoteza muda wao, fedha zao, na hata mali zao hivyo watazamaji wanachoona kuwa wao wamestarehe inawatosha. Kikundi kama hicho kinapata misukumo na misaada ya serikali pia, na vile vile wanasiasa pia  huwasaidia. 

Kinachotushangaza sisi hapa ni mawazo yao na utafiti wao.Iwapo mtu atafanya utafiti wa undani zaidi kuhusu watu hawa utaona watu hawa wametafsiri Quran  na  Hadith kwa mujibu wa matakwa yao. Na ajabu ni kwamba wafuasi wao ndio watu wanaotafsiri mapotofu hayo,mara nyingine madai na maelezo yao yame-shangaza mno kiasi kwamba yanastahili kicheko cha farasi.

 

Hapa chini ninawadondoshea kidogo juu ya maelezo yao:Ubashiri wa Dajjal ni mashuhuri na uliosahihi kabisa kiasi kwamba huyu mzushi wa Kihindi hakuweza kujikwepa nayo.Amejaribu kutifua bongo lake na ameleta maelezo yafuatayo kuhusu Hadith tukufu ya  Mtume s.a.w.w.Yeye amebainisha kuwa ubashiri wa Dajjal umetimizwa kwa kutokezea kwake  yaani huyu Mirza wa Kadiani alipokuja, ubashiri wa Dajjal umetimizwa tayari.

 

Watu hawakusita kumwuliza:"Je vipi"Naye alijibu:"Ni reli  ya gari moshi.Kwa sababu gari moshi lina jicho moja lenye mwanga mkubwa sana katikati  ya uso wake mbele na ni taa kubwa sana.  Kwa hakika vitabu vyao vimejaa vitu hivi na  matabiri ya ajabu ajabu.

 

Kwa hakika hao wazushi wamesaidia sana kuonekana uhakika wa Hadith za Mtume s.a.w.w.Sifa walizojaribu kujibandika yamekwisha kubashiriwa na Maimamu Watukufu a.s.na wameelezea waziwazi dalili na sifa kuhusu Imam Mahdi a.s. hivyo kubadilisha uzushi wowote ule unaotokezea.Watu walishikwa na bung'aa  kwa sababu ya wao kukosa ilimu kwa mujibu wa madai waliyokuwa wameyafanya, hivyo sababu kubwa ya kukitayarisha kitabu hiki na kufanya uchunguzi wa hali ya juu katika swala hili ni kazi moja kubwa ya kuwatanabahisha watu na kuwaelewesha watu na kuwaelimisha watu kuhusu kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. na mambo mengine yote yaliyoandikwa humu dhidi ya hawa wazushi watakaotokea.

 

Kuna Waislamu wengine wanaocharuka kiasi kwamba wanapinga imani ya Imam Mahdi a.s.Wao wanatoka nje ya Uislamu kwa kukataa imani ya Imam Mahdi a.s. kwa sababu vitabu na maandiko ya Masunni na Mashia yanaandika wazi wazi kuhusu kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. (kuhusu imani ya wanazuoni wa Ahli Sunna tafadhali soma sehemu ya pili ya kitabu hiki). Kumwamini Mtume s.a.w.w. kuwa anasema yote yaliyokweli na haki ni amri ya Mwislamu kukubali hivyo,na chochote atakachosema Mtume s.a.w.w.kuhusu Imam Mahdi a.s. ni kweli na inambidi kila Mwislamu  aamini. 

 

Allah swt anatuambia katika Quran tukufu

"wanataka kuzima nuru ya Allah swt  (ya Uislamu ).Kwa vinywa vyao,na Allah swt atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri  watachukiwa. (61: 9 ).

WAKATI WA KUDHIHIRI

Misemo ya Mtume s.a.w.w. na Imam a.s. inatudhihirishia wazi kuwa mtu yeyote atakayejaribu kutuambia kuwa Imam Mahdi a.s. atadhihiri wakati fulani basi huyo mtu ni mwongo na mzushi.

WATU WATAKAOMFIKIA IMAM a.s.BAADA YA KUDHIHIRI

Imerikodiwa katika Ghayatul-Maram kwamba Abu Jaafer Muhammad ibn Jarar Tairi amechukua udondozi huu kutoka Safina Fatima  na hapo imetolewa kutoka misemo ya Abdullah Hasan Muhammad ibn Harun ambaye ni katika mfululizo wa wapokezi mpaka kufikia Abu Basir, mfuasi mashuhuri wa Imam Jaafer Sadiq a.s .

 

Abu Basir siku moja alimwuliza Imam Jaafer Sadiq a.s."Niwe fidia yako ewe bwana wangu ! Je Imam Ali a.s. alikuwa akijua majina ya wafuasi wa Imam Mahdi a.s. ?"

 

Imam Jaafer Sadiq a.s. alimjibu: "Kwa kiapo cha Allah swt, yeye alijua vyema majina yao pamoja na majina ya wazazi  wao, na majina ya familia zao, ukoo wao na pale wanapoishi.Vile vile alijua hali na desturi ya kila mtu .Chochote alichojua Imam Ali a.s. ndicho alichojua Imam Hasan a.s. baada ya Imam Hasan, Imam Husein, alipata ilimu yote.Baada yake Imam Ali ibn Husein na baada yake Muhammad ibn Ali, na mimi ninajua kila kitu kuhusu hao. " 

 

Abu Basir aliuliza:"Ewe bwana wangu !Je ipo katika maandishi?"Imam alimjibu:"Naam imeandikwa katika kitabu cha moyo wetu na kamwe haichafuliki."

 

Abuu Basir alimwomba sana Imam a.s. amwambie majina hayo kwa hivyo Ijumaa iliyofuatia, Imam a.s.alimtajia majina kwa kumwambia:"Hawa watu watamfikia Imam a.s. mara baada ya kutokea sauti huko mbinguni, nao watakusanyika huko Makkah.  Watu hawa ni wacha Mungu,shupavu na hodari kabisa." 

Abu Basir alikuwa ni mfuasi mkubwa wa Imam Jaafer Sadiq a.s. katika kitabu hiki nitajaribu kuwatafutia majina ya makazi tu na katika baadhi ya hutuba majina yanapatikana lakini majina ya miji, kote ni sawa kabisa. Wasomaji watakaokuwa na shauku ya kusoma zaidi wanaweza kusoma vitabu vingi mojawapo ni (1). Bashar tul Islam na (2) Ghayatul Maram.  Hapa chini najaribu kuwaletea orodha ya miji na idadi ya watu watakaoonana na Imam Mahdi a.s. huko Makkah mara tu baada ya kutokezea sauti mbinguni:

Na.    Jina la mji        Idadi               Na.    Jina la Mji                  Idadi

1

Isfahan

1

 

53

Sanaa

2

2

Ahwaz

2

 

54

Saniani

2

3

Astakhal

2

 

55

Tazimat

1

4

Antapia

2

 

56

Tus

5

5

Aswan

1

 

57

Taliqan

24

6

Ela

2

 

58

Tabaristan

7

7

Armenia

2

 

59

Tabaliya

1

8

Alexandria

2

 

60

Tripoli

1

9

Bagh

1

 

61

Akbir

1

10

Basra

3

 

62

Aden

1

11

Bahrain

5

 

63

Palestina

1

12

Beirut

2

 

64

Farghand

1

13

Babsanj

4

 

65

Qandhar

1

14

Baalik

1

 

66

Qaryat

1

15

Bada

1

 

67.

Qum

18

16

Balorak /Balora

1

 

68.

Qasat

4

17

Balkh

1

 

69.

Qairwan

2

18

Tirmiz

1

 

70.

Qazwin

2

19

Tarafa

2

 

71.

QalIssa

1

20

Tarmaza

1

 

72.

Qalis

1

21

Allepo

4

 

73.

Qubba

1

22

Haran

2

 

74.

Qadsiya

1

23

Hairuzan

3

 

75.

Kiraman

3

24

Haiwan

1

 

76.

Kosha

1

25

Harr

1

 

77.

Kufa

14

26

Halwan

2

 

78.

Karbala

3

27

Hilla

2

 

79.

Korea

22

28

Emessa

1

 

80.

Makkah

4

29

Qalat

1

 

81.

Madina

2

30

Khatt

1

 

82.

Mervared

2

31

Khaibar

1

 

83.

Merw

12

32

Damascus

3

 

84.

Mosul

1

33

Dailum

4

 

85.

Mulyan (Multan)

1

34

Dajeel  (Danil)

1

 

86.

Madain

8

35

Ray (Teheran)

7

 

87.

Maidaniya

1

36

Ruqqa

3

 

88.

Muqan

1

37

Raba

1

 

89.

Mau’ud

8

38

Randa

1

 

90.

Nishapur

8

39

Rabat

1

 

91.

Nasibain

1

40

Sijistan

3

 

92.

Nawi

3

41

Salima

5

 

93.

Niil

1

42

Sanjar

4

 

94.

Wadi-ul-Qura

1

43

Sindh (Pakistan)

3

 

95.

Wasita

1

44

Sama Sata

1

 

96.

Harib ila Sardania

1

45

Sarandip

4

 

97.

Harib min Balkha

1

46

Samar Qand

3

 

98.

Hirat

12

47

Samarra

2

 

99.

Hamdan

4

48

Samawa

1

 

100

Yaram

1

49

Sarbih

1

 

101

Yemen

14

50

Salaat

1

 

102

As-habi Kahaf

7

51

Syria

2

 

103

Wakimbizi Waislam

11

52

Shiraz

1

 

 

wa Roma

 

 

Tanbihi:

ANTAKIY:

Hawa watu wawili watakuwa wakitokea sehemu mbali na hapo.  Mmoja atakuwa ni bwana na mwingine atakuwa ni mfanyakazi wake. Wao watakuwa wakIssafiri kupitia Antakiy wakati hiyo sauti itakaposikika.

 

SARANDIP (SRI  LANKA):

Hawa watu watakuwa ni wafanyabiashara wa asili ya Iran ambao watakuwa wanazuru Ceylon kwa ajili ya biashara.  

 

QIRYAT:

Hii ni ama jina la mahala ambalo linaelezea kijiji baina ya Mash-had na Qand-har.

 

 QALIIQA

Hii ni Kurdistan,mahala baina ya Iran na Iraq.Vile vile inawezekana kuwa ni sehemu nyingineyo. 

 

MULIYAN:

Jina hili linapatikana katika riwaya moja.Mahala kwingine linapatikana kama ni Multan.Allamah Husein Amir ameandika Multan katika kitabu chake Darul Majalis-us-Sina.Multan inavyo- onekana ndio jina sahihi la kutumika.

 

HARB ILA SARDANIA

Hawa ni Waislamu ambao wamekimbia kutoka nchi yao ya asili. Wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. wao watakuwa katika Sardania. 

 

HARB MINAL BALKH:

Watu hawa watakuwa wamekimbia kutoka Balkh kwa sababu ya hofu ya wanaume wa ukoo wao. Wao wataitwa na Imam Mahdi a.s. mara pale watakapofika sehemu fulani jina ambalo linapatikana katika Khutba. 

 

WAKIMBIZI WAISLAMU WA KIROMA:

Hawa watu watakuwa ni watu wa sehemu nyingine lakini watakuwa wakiishi huko Roma (Ulaya) kama wakimbizi wa kisiasa. 

 

WATU WENGINE WATAKAO ONANA NA IMAM   a.s.

Katika baadhi ya Hadith,inapatikana kuwa Abdal sita wataungana na Imam a.s. Baadhi ya majina ya Mawali  (watu wa kikundi cha Maulai pia yamepatikana ) penginepo imeelezwa kuwa kiasi cha wanawake hamsini kutoka Makkah wataungana na Imam a.s. kwa hakika idadi hii ndiyo sahihi ya watu watakaokutana na Imam huko Makkah.Baadaye jeshi la Imam a.s. litaongezeka hadi watu elfu kumi.Kiasi cha majina mawili ya Wahindi pia yanapatikana mmoja ni kutoka India ya kusini na mwingine ni kutoka India ya Kaskazini. Majina kwa ujumla yanayopatikana katika vitabu mbali mbali yanazidi kiasi cha elfu moja. Katika kitabu hiki kidogo haitawezekana kuendelea kwa zaidi kwa sababu ya udogo wa kitabu hiki.Maimam wetu Watukufu a.s. wametupatia kila habari hata udogo wa kiasi gani wa kila somo au kila hoja.Ni kwa sababu ya ujahili wetu na kutosoma kwetu ndiyo sisi tunabakia kuwa majahil na watu wanaopotoshwa na matukio madogo madogo.Inshallah ijapo Allah swt atatujaalia tahfiqi mbeleni nitajaribu kuendeleza maudhui haya katika kitabu kinginecho,Inshallah.

IMAM ALI A.S.  AFAFANUA  KUHUSU  WATU  313

Habari ifuatayo imepatikana katika kitabu cha Ghayatul Maram. Imam Ali ibn Abi Talib a.s.amesema: "Kutokezea kwa Sufianiataanza kuwamaliza watu wote wenye majinayaMuhammad,Ali,Fatima,Hasan,Husein,Jaafer,Musa,Zainab,Mariam,Sakina,Khadija,Rukia, n.k.Baada ya hapo atawatuma maaskari na majasusi wake kwenda katika miji mbali mbali na sehemu tofauti tofauti kutekeleza kama hayo mauaji ya kikatili.Na hii hakuna sababu nyingine isipokuwa uadui wake dhidi ya Ahlul Bait  ya Mtume Mtukufu s.a.w.w.Baada ya hapo yeye atakuja Kufa na ataanza kuua binadamu kama wanyama.Nakutoka hapo atakwenda madina, na ataanza kuua maulamaa na wazee kwa muda wa siku saba.Kutatayarishwa miti kwa ajili ya kunyongea watu, na watu wengi wa Madina watanyongwa na kuangamia hapo. 

 

Mambo mengi yatatokea na Sufiani ataghalibiwa na hofu ya maisha,kwa hivyo atakimbilia Syria ambapo kule hatapata upinzani wowote.Na huko hatatulia ataanza tena ukatili wake na vitisho vya kila aina.Yeye atathibiti hata kupasua matumbo ya wanawake wenye mimba na kuyatoa matumbo nje.Na hakuna hata m- moja atakayethubutu kusema neno la kumpinga.

 

Uovu na ukandamizaji wake utazidi kiasi kwamba hata Malaika huko mbinguni watakuwa hawana raha.Na Allah swt atakuwa amekasirishwa mno na matendo yake maovu kama haya na atamwadhibu,na hapo ndipo atakapokuja kudhihiri Imam Mahdi a.s.

 

Malaika Jibrail atateremka Baitul Muqaddas na atasema:"Ukweli umefika na Uongo umetoweka."Uongo huwa ndiyo wenye kutoweka. (Sura Bani Israil, 17: 81)."Sikilizeni enyi watu wa ardhi !  Mahdi ameteremka Makkah.  Mtiini yeye na mumsaidie.”

 

Wakati Imam a.s.alipofika hapa baadhi ya Maulamaa walisimama na kumwuliza:"Ewe Maula wetu, tunaomba utuelezee Mahdi, tunahamu kubwa sana ya kumjua yeye. "Imam Ali a.s. alijibu: "Atakuwa na uso wenye nuru na utakaokuwa unang’aa kama mwezi. Yeye atadai haki kutoka kwa makafiri.Jina lake litakuwa jina la Mtume s.a.w.w. Jina la baba yake litakuwa ni Hasan ibn Ali.Yeye ni kutokana na watoto wa Fatima a.s. na kizazi cha Husein a.s.Kwa hakika sisi ndio ilimu halisi. Sisi ndio watu wa Allah swt,Sisi ndio kianzio cha matendo na sisi ndio pazia baada ya pazia ya Allah swt, na sisi ni watu tulioongozwa na Allah swt  na bora wa viumbe vyote.

 

Kutokezea kwa Imam Mahdi a.s. watu idadi sawa na idadi ya watu wa Badr watakuwa karibu na Imam a.s. Wafuasi wake watakuwa na idadi sawa na idadi ya Mtume Taalut.Wao watakuwa ni idadi ya 313.Wao watakuwa na mioyo migumu kama chuma na hawatajali hata kama milima itawazuia njia yao.Allah swt ameshakwisha kujaribu mioyo yao katika umoja,sauti zao zinasikika usiku wa giza wakimkumbuka Allah swt.Wao wanafunga mchana na wanasali usiku kucha. Nyoyo zao zimejaa mapenzi yetu na wako imara juu ya amri zetu.Mimi ninajua majina yao pamoja na majina ya wazazi wao. 

 

Kikundi cha watu kilisimama na kuuliza:"Ewe nduguye Mtume s.a.w.w.!Tafadhali sana tunaomba kujua majina yao na sehemu watakazotoka, nyoyo zetu zinakuwa na shauku ya kusikiliza maneno yako." 

Imam Ali a.s. aliwajibu:"Sikilizeni, mtu wa kwanza atakuwa akitokea Basra, na mtu wa mwisho atatokea  Abdal . 

Ifuatayo ni orodha kufuatana na mpangilio wa herufi za kiarabu

No

Jina la mji au kabila

Majina ya watu

1

Assir

Miqdad  na  Harun

2

Armenia

Ahmed na Husein

3

Isfahan

Yunus

4

Iskandariya

Hasan na Sayyid

5

Afranj (Ulaya)

Ali na Muhammad

6

Basra

Feali  na  Maharib

7

Bur’a

Yusuf,DawudAbdullah

8

Balkh    

Asdaqa

9

Bilsat    

Warith

10

Bahrain

Amir,Jaafer,Nasir,Bukair

11

Ballis

Muhammad

12

Baitul  Muqaddas

Bashir,Dawud, Imran

13

Baduu  (Misri)

Ujlan, Darraj

14

Baduu - Aqil       

Subna, Thabit, Irban

15

Baduu - No’man

Omar

16

Baduu - Shaban

Nahrash

17

Baduu - Quba

Jabir

18

Baduu -  Kilab     

Qatar

19

Algeria

Maruz na Nuh

20

Jiddah

Ibrahim

21

Jabal Kaam

Abdullah , Obaidullah

22

Dasra

Ahmed na Hilal

23

Dujail

Muhammad

24

Dina

Shuayb

25

Duuq

Abdul Ghafur

26

Hajar

Musa na Abbas

27

Hamdan               

Khaliq,Marik,Naufil,Harqil,Ibrahim

28

Hirash  

Nahrush

29

Hijr       

Abdul Quddus

30

Wasat

Aqil

31

Zubaida       

Hasan,Mahamud, Fahad.

32

Zura (Baghdad)       

Abdull Muttalib,Ahmed , Abdullah

33

Zahid

Husein

34

Hijjar

Homair,Nasir,Malik,AbdulQayyum,Ali,Jahan,

Yaglam, Taher, Thualab, na Kasir

35

Abysinia

Ibrahim,Issa,Muhammad,Imran,Ahmed,Salam

-Halla, Muhammad, na Ali.

36

Taef   (Yaman)

Hilal.

37

Tuuka

Wasail na Fadhil

38

Teheran (Ray)

Majma

39

Tabriya

Filaj

40

Taif - Ali       

Sabir, na Zakariyya

41

Taliqan

Saleh,Jaafer,Muhammad,Yahya,Hud,Dawud,Jamil,Fadhil,Issa,Jabir,Khalid,Alwan,Abdullah,,Ayub,Salaib,Hamza,AbdulAziz,Luqman,Saad,Fizzah,Mohjir,Abdun,Abdul -Rahman,Saleh na Ali

42

Yamama

Tahir,Aqil (Yemen), Khabir,Hush,Malik,Kaab

43

Kushan

Abdullah,Obaidullah,ahmed,Shaban,Amir,Hammad,Fahad,Josh,Kulthum,Jabir,Muhammad.

44

Kinda    

Ibrahim

45

Kirman 

Abdullah, Muhammad

46

Kufa

Muhammad,Hud,GhiyasObaba (Karbala) Hasan na Husein

47

Karkh (Baghdad)       

Qasim

48

Lawiha

Kausar

49

Maajama

Muhammad,Umar,Malik(Maada),Suwaid,Ahmad,Muhammad,Hasan, Yaqub, Abdullah.

50

Mansuriya

Abdul-Rahman na  Abdullah

51

Makkah

Ibrahim,Muhammad, Abdullah

52

Madina

Ali,Jaafer,Hamza,Abbas,Tahir,Hasan,Husein,Qasim,Ibrahim, Muhammad.

53

Maragha

Asdaqa

54

Mosul

Harun, Fahd

55

Nishapur

Ali na Muhajir

56

Nasibain

Ahmad,Ali(Najaf)Jaafer, na Mohamad

57

Najd

Marwan, Saad

58

Sind

Abdul Rahman

59

Sudawa

Ahmed, Yahya na Falah

60

Samarqand

Ali,Majid,Omar,Yunus, Muammar

61

Samarrah

Moradi  na Amir

62

Sailan   

Nuh, Hasan na Jaafer

63

Sanjar

Zibyan na Ali

64

Sarkhas

Hasaf na Nafia

65

Salmas  

Harun

66

Samadha

Zohaib, Shuayb na Saadan

67

Afar

Ghaffar na Ahmad

68

Abuuqin

Abdus-Salaam,Faras,Kulaib

69

Oman

Muhammad

70

Saleh     

Dawud,Hawail,Kausar,Yunus.

71

Aden

Aun  na Musa

72

Makkah       

Mukarram

73

Asqalan

Muhammad,Yusuf,Umar,Fahd, na Harun.

74

Anbarah

Omair.

75

Arfa

Faikh.

76

Abedan 

Hamza,Shaiban,Amir,Hammad,Fahd,Hanjrash,Kulthu, Jabir, Muhamad

77

Sanaa   

Husein, Jobair, Hamza, na Yahya

78

Sar 

Nusair

79

Saula    

Muhassar.

80

Saad

Ali na Saleh

81

Saraf

Khalifa

82

Qandhar       

Ibrahim na Ahmed

83

Qarina

Malik.

84

Qarquf

Shuayb,Bashir

85

Qazwin

Harun,Abdullah,Jaafar,Saleh,Omar,Lais,Ali,Muhammd,Shalakh,Hasan

86

Qum

Yaaqub.

87

Qadsiyyah       

Hafidh .

88

Raqantat

Fir’aun,Ahmed,Abdus-Samad,Yunus na Tahir

89

Qadim   

Bahrut na Talut .

90

Rabat

Jaafer.

91

Shiraz   

Abdul Wahab.

92

Sherwan       

Abdullah, Saleh, Jaafar na Ibrahim

93

Shaqa   

Harun na Miqdad.

94

Shush    

Shaiban na Abdul-Wahab.

95

As Shahim       

Jaafer.

96

Khurasan

Nakba na shuut.

97

Khat      

Ambriz na Mark.

98

Saghaira       

Malik na Yahya.

99

Al-Faidh

Alam na Suhail.  

 

Hapa ninajaribu kuwapatieni maelezo juu ya habari za miji au makabila yaliyotajwa hapo juu kwani majina mengi yamebadilika na kuingia katika mipaka mingine.

No

Jina la Mji

Maelezo

1.

Armenia

Ni sehemu kubwa sana

2.

Iskandariyya

Kwa sasa imegawanyika katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Uturuki.

3

Afranj

Haijulikani kama ipo huko Ulaya au Ufaransa

4

Abna’

Ipo mipakani mwa Iraq na Syria,sikuhizi hujulikana kama Rutbah.

5

Al Natakiyyah

Ni mji mojawapo huko Syria

6

Adal      

Ni jina la zamani la Bahrain

7

Aus

Ni jina maarufu la kabila la Kiarabu

8

Balis      

Ni jina la mji mmojawapo huko Syria,kwa sasa linajulikana kama Maskinah.

9

Bur’a

Kitongoji huko Taif.

10

Balkh

Mji maarufu huko Afghanistan.

11

Balsat   

Kijitongoji kimojawapo huko Askandariyyah.

12

Balqa’   

Mji huko Jordan.

13

Muhjam

Mji huko Yemen.

14

Nasibain

Ni jina la mji katika nchi za Iraq na Syria.

15

Nuba

Ni jina la sehemu huko Sudan na Misri.

16

Najar    

Ni jina la kitongoji huko Bahrain,Yemen na Najd.

17

Hamdan

Ni mji katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Yemen.Pia ni jina la kabila moja.

18

Sunain  

Ni jina la mji wa Jabal Amil.

19

Dast

Jina la mji huko Iraq,Yemen,Syria na Afghanistan.

20

Yamamah

Jina la mji huko Arabia,siku hizi linajulikana kama Aridh.

21

Abdal

Ma-Awliya’ wa Allah swt.

22

Baidha’

Mji katika Iran,Algeria,Libya Yemen ya Kusini.

23

 Tamim

Kabila la Kiarabu.

24

Tistar

Jina la mji wa Khuzistan.Jina la asili ni Shustar

25

Tughayyin

Dola ya Georgia.

26

Thaqib

Kitongoji huko Yamamah

27

Kohi Alkam  

Katika Antakiyyah,inasemwa kuwa ni mlima.

28

Ju’arah 

Ni mji huko Iraq karibu na mji wa Najaf-i-Ashraf.

29

Habsha’

Katika Pembe ya Afrika,nchi hiyo kwa sasa inajulikana kama Ethiopia.

30

Jamiir   

Jina la kabila huko Yemen.

31

Khullat 

Sehemu moja kubwa sana huko Arabia.

32

Khunj

Mji  huko Iran Kaskazini.

33

Dhihab 

Mji karibu na Khorasan (Mash-had ya siku hizi).

34

Ramlah 

Mji mashuhuri huko Palestina.

35

Wahat   

Mji wa nyongeza huko Arabia.

36

Zura’

Jina la mahala ilipo Baghdad ya siku hizi.Zamani ilikuwa ikijulikana hivyo.

37

Zaid

Mji huko Syria.

38

Yasjar

Mji ulipo huko Urusi.

39

Sarkhas

Mji karibu na Mash-had.

40

Suhan   

Mji karibu na Takrit huko Iraq.

41

Sanjad  

Mji huko Iraq na Syria.

42

Sindh    

Huko Pakistan.

43

Susan    

Mji katika Maghreb na Iran.

44

Siraf

Mji katika Iran.

45

Ceylon

Kisiwa katika Bahari Hindi ( Indian Ocean).

46

Shizar   

Mji huko Syria.

47

Dhaif     

Mji katika Najd.

48

Taliqan 

Mji katika Iran huko Qazwin na Afghanistan

49

Tabriyah      

Ipo huko Palestina.

50

Arafa’   

Makazi huko Makkah.

51

Asqalan

Mji katika Afghanistan na Palestina.

52

Askar Mukarram 

Mji huko Jamhuri ya Kiislam ya Iran.

53

Aqar

Mji katika Palestina na jina la vitongoji vinne huko Iraq.

54

Aska

Mji huko Palestina.

55

Umarah

Mji katika Iraq.

56

Anizah

Jina la kabila na mji huko Najd.

57

Fistat

mji huko Misri.

58

Qashan 

Mji huko Iran.

59

Qadsiyyah    

Mji huko Iraq.

60

Qazrun  

Mji huko Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

61

Kabash

Mji huko Iraq.

62

Karkh

Kitongoji cha Baghdad.

63

Kard

katika Iran na  jina la  kabila huko Iran na Iraq Mji

64

Kurah   

Mji huko Lebanon.

65

Muragha      

Mji huko Iran.

66

Marw    

Mji katika Iran na Urusi

67

Mu’azah

Mji katika Yemen.

 

Watu watatu ni katika wafanyakazi wa Imam Mahdi a.s. nao ni Abdullah, Hanif na Akbar. Na katika watumwa wa Mtume s.a.w.w. ni Sabbah, Sobaih, Maimun na Hud. 

 

Wafuatao ni wafalme: Nasih  na Abdullah.

 

Watakuwepo watu sita majina yao ambayo yatakuwa ni Abdullah.  Hawa watu wote watakusanyika pamoja na Imam Mahdi a.s.  kuanzia alfajiri mpaka magharibi.[12]

MAJINA YA WAFUASI WA IMAM MAHDI A.S. KWA MUJIBU WA IMAM JAAFER SADIQ A.S .

 

Imam Jaafer Sadiq a.s. alimwambia Abu Basir hawa watu ndio watakaokuwa wafuasi wa Imam Mahdi a.s. wao watamfikia Makkah.  Wao watakuwa watu wenye nyoyo safi, wacha Mungu, waaminifu  na moyo wa kujitolea.

 

Hapa ifuatayo ni orodha ya majina yao pamoja na majina ya baba zao na nchi zao za asili.  Habari zao zinaweza kupatikana katika kitabu cha Ghayatul Maram na Basharatu Islam.

Na.  Jina la mji                Jina la mtu

1.     Ahwaz

Hamad ibn Jamhur,Issa ibn Tamam,Jaafer ibn  Saed

2.     Istakhar

Al-Muwakkil ibn Ubaidullah, na Hisham ibn Fadhail.

3.  Antakiyyah

Musa ibn Auf, Suleyman   ibn Hara pamoja na mtumwa wake wa Kiroma.

4.     Eila       

Yahya ibn Budaail,Hawasha ibn Al-Fadhl.

5.     Bagha

Saleh ibn Harun,Sarhil al   Saadi

6.     Balis

Ibn Safar,Ahmed ibn Muslim,Ali ibn Maad.

7.     Basra

Abdul Rahman ibn Atef, Ahmed Malih,Hammad ibn Jaber.

8.  Bab Sakh

Zabir ibn Umar (atakuwa mashuhuri kama Aslah), Talha ibn Talha,Hasan ibn Hasan,Imran ibn Umar ibn Hashim.

9.  Ba’al bak

Anzal ibn Imran

10.  Buda \Bala

Ibn Aueda.

11. Ba’almurak

Ausaf ibn Saed,Ahmed ibn Hamid

12  Bab-ulAbwab

Jaafar ibn Abdul Rahman.

13. Balkh

Naradas ibn Muhammad.

14.  Barura

Zaid ibn Abdul Rahman, Abbas ibn Fadhl,Suhaiq ibn Salaman al-Khayyat,Ali ibn Khalid, Salam ibn Salim,Mahbub ibn Abdul Rahman,Hadir ibn Rustam, Harb ibn Saleh,Ammar ibn Muammir.

15.  Tawi

Laqit ibn Farat

16.  Jurjan

Ahmed ibn Harqil,Zarara ibn Jaafer,Al Husain ibn Ali,Hamid ibn Nafe’,Muhammad ibn Khalid,Alan ibn Hamid,Ibrahim ibn Ishaq,Ali ibn Alqama, Salman ibn Kurduya.

17.  Alleppo

Yunus ibn Yusuf, Hamidullah Qais,Wasim ibn Mudrik,Saleh ibn Maimun,Mahdi ibn Hind.

18.  Haran

Zakariyyah al-Saadi.

19.  Hawazan

Kurd ibn Hanif,Asim ibn   Khalil al Khayyat,Zaid ibn Durain.

20.  Hulwan

Ma’un ibn Kathir, Ibrahim ibn Muhammad.

21.  China

Shahid ibn Chin Hua, Bokair ibn Abdullah ibn Abdul Wahid.

22.  Qalat

Wahab ibn Harnid.

23.  Khaybar

Suleyman ibn Dawud.

24.  Damascus

Nuh ibn Jurair,Shuayb ibn Musa,Rahjar ibn Abdullah Al-Farawi.

25.  Dumyat

Ali ibn Zaida

26.Teheran

Israil ibn Qahtan,Ali ibn Jaafar,Uthman ibn Ali, Muskan ibn Jabal,Kurd     ibn Shaiban, Hamadan ibn Kurd, Suleyman ibn Dailami.

27.  Rabi’a

Aziz ibn Asim, Malih ibn Sa’ad

28.  Ruqqa

Ahmed ibn Salman, Naufil ibn Umar, Ash-ash ibn Malik

29.  Ruba

Kamil ibn Ozair.

30.  Rabza

Hammad ibn Muhammad

31.  Sijistan

Al Khalil ibn Nasr, Turki ibn Shaiba, Ibrahim ibn Ali.

32.  Salima

Alqama ibn Ibrahim.

33.  Sanjar

Abdullah ibn Zuraik, Shaham  ibn Qatar, Hibatullah Arbaq, Hinbal ibn Kamil

34.  Sindh

Shabal ibn Abbas ibn Muhammad,Nasar ibn Mansur.

35.  Samsat

Musa ibn Zarqan

36.  Sarandip

Jaafer ibn Zakariyya, Daniyal ibn Dawud

37.  Sunder

Hud ibn Tarkhan, Saed ibn Ali, Sha ibn Barzakh, (mpanda farasi hatakaye onekana  juu ya farasi wake) Mundhir ibn Zaid, Hur ibn Sabah, Yusuf ibn Hurma  na Ibrahim (mchinjaji huko Subkan).

38.  Sana

Fayyaz ibn Zurad, MaIssara ibn Mundhir.

39.  Saliqan

Ahmed ibn Umar al-Khayyat Ali ibn Abdus Samad (mfanya biashara),Khalid ibn Said.

40.  Zinad

Bandar ibn Ahmed Subka (msafiri).

41.  Taif

Abdullah ibn Said.

42.  Tus

Shahur ibn Himran, Musa ibn Mahdi, Suleyman ibn Taliqibnul Wad (ambaye amezikwa karibu na Kaburi la Imam Ridha a.s.), Ali ibn us Sindi Sairafi.

43.  Taliqan

Ibn Radhial Jubelli,Abdullah ibn Umar,Ibrahim ibn Umar,Suhail ibn Muhammad, Muhammad ibn Jamhur,Jamil ibn Amir,Khalid  na Kasir ( wafanyakazi wa Juraid),Abdullah ibn Farat, Fazarah ibn Bahram,Maadh ibn Salam,Khulaid al-Tammar, Hamid ibn Ibrahim Jamiut-ul-Quraa,Aziz ibn Afsar,Hamza ibn Abbas,Kain ibn Jalbad al Zaia,Alqama ibn Mudrak, Maharwan ibn Khalil, Zahur (mwana wa mfanyakazi wa Ibn Ibrahim),Jamhur ibnul Husain, Ryash ibn Sa’ad.

44.  Tabariyya

Hushad ibn Kardum, Bahram ibn Ali, Al-Abbas ibn Hadsam,Abdullah ibn Yahya.

45.  At Tai

Al-Hubab ibn Sa’ad,Saleh ibn Taufur

46.  Akbira

Zaid ibn Huba.

47.  Ghariyat

Sahuya ibn Hamza, Ali ibn Kulthum

48.  Palestina

Suwaid ibn Yahya

49.  Filzim

Ar Rihya ibn Umar, Saib ibn Abdullah

50.  Qum

Ghassan ibn Muhammad, Ali ibn Ahmed, Naim ibn Ya’qub,Imran ibn Khalid,Subail ibn Ali,Abdul Adhim ibn Abdullah,Maska ibn Muslim,Hus ibn Ahmed,Yalil ibn Malik, Musa ibn Imran,Abbas ibn Zafar,Al Harith ibn Bashir,Marwan ibn Ulaba ibn Juzhuz (atakuwa mtu anayejulikana sana), Safar ibn Ishaq, Kamil ibn Hisham.

51.Qissat

Nasar ibn Hawash, Ali ibn Musa, Ibrahim ibn Siffin, Yahya ibn Naim.

52.  Qarya

Al Haditha.

53.  Qairwan

Ali ibn Musa, Atira ibn Qartaba

54.  Qas

Muhammad ibn Muhammad, Ali ibn Hamuya.

55.  Qumas

Rabab ibn Jalda,Jalil ibn Sayyid

56.  Qandail

Umar ibn Rarda

57.  Korea

Hanuz ibn Hazwan

58.  Kufa

Rabia ibn Ali,Tamim ibn Ilyas, Asar ibn Issa,Matraf ibn Umar,Harun ibn Saleh,Waqa ibn Sa’ad, Muhammad ibn Dawwaha,Hur ibn Abdullah, Aurtul Aam, Khalid ibn Abdul Quddus,Ibrahim ibn Masud Ibn Saad, Ahmed ibn Rayhan, Gharas al Aawani.

59.  Karbala

 

60.  Madina

Hamza ibn Tahir,Sharjil ibn Jamil

61.  Marwaid

Jaafar, Insha, Ad-Daqaia, Joz (mfanyakazi wa Husaid).

62.  Marw

Nabdar ibn Khalil Attar, Muhammad ibn Umar Saidani, Gharib ibn Ubaidullah (mfanyakazi wa Qahtaba), Saad (Mroma), Saleh ibn       Dajal.Maad ibn Hani, Kros al Azadi, Udhem ibn Jabir, Tashif ibn Ali, Faran ibn Zaid, Javir ibn Ali, Husbah ibn Jurair.

63.  Musal

Suleyman ibn Sabih

64.  Qalik

Kurdwin ibn Jabir.

65.  Madain

Muhammad na Ahmed ibn Mandhar (watu wawili wema ni ndugu), Maimun ibn Harath, Maad ibn Ali, Al Hasan ibn Said, Zuhair ibn Taba,Nasar ibn Mansur.

66.  Mulbar

Haidar ibn Ibrahim.

67.  Maw-ud

Majma ibn Jamhur, Shahid na Shaabbar ibn Bandar, Dawud ibn Jurair, Khalid ibn Issa, Zaid ibn Saleh, Musa ibn Adrud ibn Kurd.

68.  Nishapur

Saman ibn Khazir,Abu Lubaba ibn Mudrik,Ibrahim ibn Yusuf,Malik ibn Harb, Zardu ibn Sokan,Yahya ibn Khalid, Maadh ibn Jibrail,Ahmed ibn Umar,Issa ibn Musa as-Sawaq,Yazid ibn Daulat, Muhammad ibn Hammad, Jaafar ibn Tufan, Alan Mahuba, Abu  Maryam, Umar ibn Umair, Yalil ibn Wahab.

69.  Nasibain

Dawud ibn Mahbur, Hamid Sahib al Bawari

70.  Naqalbas

Muhammad ibn Zaid, Hani al Ataridi, Jawad ibn Badr,Salim ibn Wahsad, Fadhl ibn Umair.    

71.  Lukanuba

Abdullah ibn Muhammad

72.  Nil

Shakir ibn Ubda

73.Wadi-ulQura

Al Hur ibn Razzaq

74.  Hirat

Said ibn Uthman, Akbar ibn Abdullah (Atakuwa akijulikana kama Ghulam.Kindi) Saban al Qassab, Harun ibn Imran, Saleh ibn Jurair,Almark ibnMuammar,Ubaidul Ali ibn Ibrahim,Nazal ibn Hazam,Saleh ibn Haithami,Adam ibn Ali, Khalid al-Qawas.

75.  Hamdan

Harun ibn Imran,Taifur ibn Muhammad,Aban ibn Muhammad, Itab ibn Malik.

76.  As-habi Kahaf

(Watu saba)Kamsalina na wenzake,mfanyabiashara kutoka Antaqiyya, Musa ibn Auf,Suleyman ibn Hamd na mfanyakazi wake wa Kiroma,watu kumi na moja,Mohib ibn Abbas, Faafar ibn Jalal, Zarar ibn Sai, Hamid al Quddus, Malik ibn Khulaid, Bukair ibn Hur, Habib ibn Hannan, Jabir ibn Sufiani.

77.

Badhi ya watu kutoka Shiraz na waasi Sardania, Sanjar,Abdus Samad Qabaili na baadhi ya Nasibi. Wote kwa pamoja watakuwa ni watu mia tatu na kumi na tatu.       

 

Tanbihi:  Majina ya miji hiyo yote ni katika Kiarabu cha asilia na kwa mujibu wa Jiografia ya wakati huo.  Na kwa hivi sasa miji mipya imechomoza na mipaka ya miji na nchi imebadilika yaani ni tofauti na mipaka ya miji na nchi ilivyokuwa kati ya zama za Mtume s.a.w.w.na Maimam a.s. Ili kutosheka na kiu hiki cha utafiti, itambidi msomaji ajaribu kuchunguza majina ya kale katika vitabu na habari za kale, hiyo ni kazi ya msomaji. (hata hivyo nimejaribu kutafuta majina hayo na kuyaelezea katika footnotes za hapo awali).

 

KUONANA NA IMAM KATIKA KIPINDI CHA GHAIBAT

 

Sisi tumewahi kuona katika nyakati za mvua kuwa jua huwa linakuwa limejificha nyuma ya mawingu ambavyo macho yetu hayawezi kuona na jambo hili halituthibitishii kuwa jua halipo, jua lipo lakini limejificha nyuma ya wingu lakini inatuthibitishia faida yake kama kawaida.Kama jua baada ya kujificha nyuma ya wingu hilo halitatimiza wajibu wake basi utaratibu wake wote wa kiulimwengu utaharibika na kutatokea maafa makubwa sana. Kwa hivyo akili yetu inatuambia kuwa jua lipo na linafanyakazi yake inavyolipasa. Vivyo hivyo kwa amri ya Allah swt mwokozi wetu Imam Mahdi a.s. naye pia yupo haonekani machoni mwetu kwa kudura za Allah swt, na hivyo kutokuwapo kwa Imam mbele ya macho yetu ambayo yana pazia hakumaanishi kuwa Imam hayupo ulimwenguni yeye yupo na anawafaidisha wanadamu wote kwa pamoja.  Kunaweza kutolewa hoja nyingi sana kuthibitisha kuwapo kwa Imam a.s.,lakini kitabu hiki kidogo sana hakiniruhusu kuzungumzia kwa undani zaidi hoja hizi,hata hivyo kwa mujibu wa riwaya, vitabu na hadithi tumeweza kuona Imam a.s. yupo, kwani katika sehemu ya pili ya kitabu hiki kuna sura inazungumzia uthibitisho wa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. kwa mujibu wa Wanazuoni wa Ahli Sunnah kwa hiyo msomaji akisoma sura hiyo ataelewa zaidi kuwa Imam Mahdi a.s. yupo. 

 

Nina imani kamili kuwa Imam a.s. yupo hapa isipokuwa sisi hatuna uwezo hatujakamilika kumwona yeye.Hivyo inatubidi sisi tujirekebishe na tuwe wacha Mungu zaidi na tuwe watu safi nyoyo zetu ziwe safi ili kutaka kumwona Imam Mahdi a.s. Na hapo baadaye tujidhatiti vyema katika kufuata muongozo uliotolewa na Imam a.s. katika njia ya Allah swt.Inshallah, tutafanikiwa lazima kuonana na Imam wetu huyu wa zama hizi.  Inawezekana kuwa sisi tusielewe kuwa sisi tumeonana na nani, na hapo baadaye tukajakuhisi kuwa si mtu mwingine tuliyeonana naye ila Imam Mahdi a.s. Na wanazuoni wameandika habari nyingi sana kuhusu kuonana na Imam Mahdi a.s. vitabu katika lugha nyingi vinapatikana kuzungumzia kuonana na Imam Mahdi a.s.

 

Hapa chini kuna miongozo ifuatayo michache iliyotolewa na Maimam a.s ili kujitakasisha hatimaye tuweze kuonana na Imam Mahdi a.s. 

(1). Inambidi mtu apitishe usiku 40 za alhamisi katika Msikiti wa Kufa bila ya kutokea pengo katikati au apitishe usiku 40 za Jumatano katika Masjidi Sahar bila ya kukosa.  Anatakiwa awe mashuhuri katika Ibada na kusoma dua na awe na nia halisi na safi ya kuonana na Imam Mahdi a.s.

 

(2). Mtu asome Dua a-i ahad  kila alfajiri.Kwa uhakika mtu ataonana na Imam Mahdi a.s. katika uhai wake iwapo nafasi itaturuhusu tutaweza kuichapa dua hii hapo mwishoni hata hivyo dua hii inapatika katika Mafatihul Jinan.

 

(3). Mtu yeyote atakayekuwa anafanya Aamal za Ashura  kila siku basi lazima ataonana na Imam Mahdi a.s. kabla ya kifo chake.

 

Vile vile kuna Aamal  na dua nyingi katika vitabu vingi sana. Vile vile vitabu vingi sana vinatoa miongozo namna ya kufanya ili mtu aweze kukutana na Imam Mahdi a.s.

MUKHTASARI WA DALILI

(1).Baghdad itateketezwa kabisa.(2).Basra itazama.(3)Waarabu watatawaliwa na mfalme wa ukoo mmoja tu kwa nguvu.(4)Msikiti wa Borasa (baina ya Baghdad na Kazmain) utadhoofika. (5).Kutakuwa na nchi nyingi za Kiislamu na kutakuwa na soko la kawaida (6)Qum itakuwa ni kitovu cha mafunzo ya Kiislamu, kitakuwa ni kituo kipya kuliko kile cha Najaf (Iraq). Na hapo ndipo kutakuwa kukitolewa ahkamu za dini.(7) Kutakuwapo na reli kupitia katika nchi za Kiislamu. (8)Azarbaijan itakumbwa na vita (9) Wanawake watakosa heshima kabisa.(10)Duniani kote kutaenea sheria za kidemokrasia.(11)Kutakithiri kizazi cha wanaharamu.(12) Kutakithiri riba na rushwa (13) Kuzaliwa kwa wanawake waovu katika familia nzuri.(14) Watu wenye hali ya chini wataweza kujenga majumba makubwa. (15) Watu wema na waaminifu watakuwa wakiomba mauti ili waepukane na maudhi wanayoyapata.(16) Watoto na majahili watapanda juu ya Mimbar, na watajulikana kama khatib.(17) Wanazuoni watajiingiza katika mambo ya dunia.(18) Madhumuni ya kutafuta Elimu itakuwa ni kutaka kutafuta pesa.(19)Badala ya kusalimiana matusi ndiyo yatakayo kuwa yakitumika watu watakapokuwa wakikutana.(20) Watu watatoka katika dini zao kwa sababu ya ulafi wa vitu.(21)Dini ya Kiislamu itakuwa dhaifu(22)Mambo ya kuingiliana yatakuwa yakifanyika kidhahiri kama vile wafanyavyo wanyama.(23) Wanawake watasuka nywele zao kama nundu za ngamia. (24)Kupatwa kwa mwezi na jua na mitetemeko vitatokea Mashariki na Magharibi na baadaye katika Bara la Arabia.(25) Kutakuwa na ongezeko katika kuzaliwa watoto wa kike.(26) Ulawiti na pombe vitakuwa ni vitu vya kawaida. (27) Mitetemeko ya kila mara itaongezeka (28) Wanawake watakuwa na taasisi zao.(29) Wanawake watafanya kazi pamoja na wanaumme katika kutafuta maisha yao.(30) Usafiri utakuwa wa haraka sana. (31) Kutakuwa na muongezeko wa ajali za njiani. (32) Mavazi yatakuwa mafupi (33)Mwanamme na Mwanamke watajaribu kuonana sawa kijinsia (34)Kutakuwa na ndoa za kuoa jinsia yake yaani mwanamme atamuoa mwanamme mwenzake na mwanamke atamuoa mwanamke mwenzake (na mambo haya hasa yanatokea katika nchi za Ulaya).(35)Wakazi wa Kufa na Najaf watakuwa wamekaribiana sana.(36)Wakazi wa Makkah na Madina wataongezeka.(37)Hijab itakuwa imepotea (hijab, bubui)(38)Maji yataanza kujaa katika ziwa Sawa.(39) Kutakuwapo na nyota yenye mkia karibu na Capricorn (40) Watu wengi sana  watakufa kwa sababu ya kuenea kwa vita (41)Misikiti na Quran itarembeshwa kwa dhahabu (42) Kutatokea  na moto mkubwa sana katika mashariki na utaendelea kuwaka kwa siku saba.Na moto huo utatia khofu kubwa sana kwa mioyo ya watu(43) Kutakusanyika bendera tofauti tofauti huko Kufa na kusababisha mifarakano mikubwa.(44) Utawala wa Kifalme utakwisha huko Iran (45)Kutatokea na mivurugo katika nchi za Kiaarabu.  Kila nyumba ya mwarabu na nchi zote za Kiislamu zitahusishwa humo.(46)Kukosa Imani kutaenea kote.(47)Waislamu wataiga tamaduni na mila za maadui zao. (48) Vifo vya ajali vitaongezeka. (49) Ala za muziki zitaenea kiasi kwamba hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayesalimika kwa sauti zao. (50) Watu wataanza kukataa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.(51)Kutaonekana sura katika jua, na sauti zao zitasikika duniani kote.(52)Mwanadamu atafika mwezini.(53)Sufiani atatokezea na kueneza utawala wake wa vitisho. (54) Sayyed Hassan atatokezea huko Iran.Na yeye atafika Multan kwa kupitia Kirman huku akiteka sehemu zote. Yeye atamfikia Imam a.s. Yeye atamfikia Imam Mahdi a.s. na kujIssalimisha mbele yake. (55)Kutatokezea wazushi wa mtume sitini.(56) Mtume Issa a.s.atateremka kutoka mbinguni. (57)maafa, magonjwa ya kuambukiza na ukame utaenea kote.(58)Nafsi ibn Zakia atauawa katika al- Khaaba (mtu mcha Mungu atauawa katika al-Kaaba) (59) Jua litachomoza kutoka Magharibi kwa siku moja.(60) Warusi wataingia Bara la Arabia na watu weupe wataingia Bara la Parestina.Nao baadaye watapambana.(61)Wachina wataingia Bara la Arabia na kusababisha maangamio na maafa ambayo yatakuwa ni mambo ya kawaida.(62) Baadhi ya miji itateketezwa kwa sababu ya maafa na misukosuko. (63) Sauti ya kutisha itasikika kutoka mbinguni(64)Kutokezea kwa Dajjal(65)Moto na moshi itakuwa kawaida duniani.(66)Mvua zitatokezea pasipo na misimu yake(67) Kuongezeka kwa joto katika anga za juu.(68) Kulipuka kwa moto mkubwa katika Aden(69)Baadhi ya makundi ya wanaume yatakuwa yamegeuka maumbo.(70) Kutatokea na mabadiliko ya ajabu katika sayari ya Capricorn (71)Mkuu wa Dola ya Misri atauawa. (72) Kutakuwapo na mvua ya mfululizo kwa muda wa siku ishirini na nne(24).Dunia nzima itakuwa imejaa michafuko, maafa na maangamizo n.k. 

HALI YA WAIRAQI  NA VIKWAZO VYA HIJA.

 Amesema Imam Jaafer Sadiq a.s. :-

“Ripoti ifuatayo yenye kuaminika imetolewa kutoka Majalis Tusi.  Humo Sudir Sairafi anaripotiwa kwa kusema:“Mimi nilikuwapo mbele ya Imam Jaafer Sadiq a.s.,kulikuwapo na kikundi cha Wakufi.Na Imam a.s. aliwaambia watu kutoka Kufa.”  “Timizeni amri za Hijja kabla hamjakosa fulsa hiyo, timizeni wajibu wenu wa Hijja kabla Barjaniya hajawazuia,fanyeni hivyo kabla ya kubomolewa kwa Misikiti baina ya Naharwan na Naklistan. Fanyeni Hijja kabla mti huko Zurahaujang’olewa ambapo Mariamu alipata Mitende iliyoiva.Baada ya hapo nyinyi hamtaweza kutimiza Hijja kwa sababu ya kukosa uwezo wenu.”

 

Haya yatatokea baada ya mazao yenu kuharibika na kuenea kwa hali mbaya kabisa kote.Dunia nzima itaathirika kimapato.Watawala watakuwa waovu.Nyinyi nyote mtaathirika na kwa hali ngumu ya maisha, magonjwa hatari na vile vile uchokozi wa watawala.  Kila aina ya misukosuko ya dunia nzima itawakumba nyinyi. Enyi watu wa Iraq ninawasikitikia mno pale bendera kutoka Khurasan zitakapokuja kwenu.Teheran itasikitika kwa sababu ya kuingiliwa na Warusi na Iraq itapata misukosuko kwa sababu watu wa Teheran na maafa mengi yatakuja kutoka Shatt.

 

Sudair aliuliza:  “Ewe bwana wangu nini hiyo Shatt.”

 

Imam a.s. alimjibu:“Hayo ni jumuia. Masikio yao yatakuwa mafupi na watakuwa kama vyuma. Watakuwa na macho na ndevu zilizo tofauti, maneno yao ni ya kisheitani namwomba Allah swt aniepushe na michafuko yao. Hapo ndipo Allah swt ataIssaidia Din  hii na kuwapatia ushindi kwa kupitia Imam Mahdi a.s.”

 

Tanbihi: Kila neno la Hadith hii lina nukta ya kuzingatia.

 

1.Ulimwengu wa Kiarabu umejaa kwa machafuko na matatizo.Hususan imezungumziwa Iraq na Iran.Swala hili na mengineyo yamethibitisha kuwa Warusi watapitia Khurasan na kuiteketeza Teheran.Na baadaye wataiangamiza Iraq.

2.  Watawala wa siku hizi ni kwa wingi ni waovu.

3.  Dunia nzima ipo inaathirika kiuchumi.

4. Aina fulani ya jumuia itapita Shatt -Ghuba ya Uajemi inaonyesha kuwa Wachina wataingia Iraq kwa kupitia Ghuba ya Uajemi.  Riwaya zinginezo zimeelezea swala hili pia.

 

5.  Vikwazo juu ya Hijja ni jambo la kustaajabisha mno.Kuna Utofauti wa maelezo kuhusu Barjania baadhi ya watu wanasema kuwa hiyo ni Uingereza, na kwa mujibu wa wengineo, mambo mengine, hata hivyo kwa ujumla wote wanakubaliana kuwa njia zielekeazo Makka kwa ajili ya Hijja zitakuwa na vikwazo.

 

 

Imeandikwa katika Bihar-ul-Anwaar kuwa Kaab ibnul Hars anasema: “Mfalme Shaazan alikuwa ametingwa katika maswala fulani, hivyo alimwita mnujumi mashuhuri aliyeitwa Soteh.”

 

Kuwasili kwa soteh, Mfalme alitaka kwanza amjaribu na hivyo aliificha Dinar chini ya mguu wake na kumwita mnujumi huyo karibu yake na kumuuliza: “Niambie nimeficha nini?”

 

Soteh  alimjibu kwa ufasaha alisema:“Ninaapa kwa Ka’aba na Haram na ninaapa kwa Hajar  Aswad na ninaapa kwa usiku unaokuwa giza na ninaapa kwa kupambazuka na ninaapa kwa kila kilicho madhubuti na kila kilicho kimya, kuwa wewe unataka kujaribu ilimu yangu na kwa hivyo umeficha Dinar chini ya mguu wako.”

 

Kwa hayo Mfalme alifurahishwa sana.Naye alisema:“Ewe Soteh,je hii ilimu uliipataje?”

 

Soteh alimjibu: “Mimi nina ndugu yangu anayeishi pamoja nami, kila wakati. yeye ananipa ilimu hii na mimi ninaifanya ilimu hii ijulikane kwa wote.”

 

Mfalme aliuliza:  “Niambie kile kitakachotokea mbeleni.”

 

Soteh alimjibu:“Sikia ewe Mfalme utafika wakati ambao watu wema watatokomea humu duniani, wachokozi na waovu watatawala kwa wingi. Kutakuwapo na uzushi wa neno la Mungu, jambo litakalo zagaa kila mahali. Kukosa aibu heshima na huruma kutakuwa ni jambo la kawaida. Heshima watapatiwa watu ambao ni matajiri tu.Watu waovu watakuwa na nguvu kiasi kwamba watabadilisha mambo katika dini kwa mujibu wa matakwa yao na hivyo kufanya dini kukosa nafasi katika mioyo ya watu.

 

Yote haya yatatokea wakati ambao kutatokezea nyota moja ya kiajabu huko angani, nyota hiyo itakuwa na mkia. Watu wa nchi za Magharibi watakuwa wamezuzuliwa nayo, mvua zitakwisha na kutaongezeka mno kwa bei za vitu.Vinyozi wataingia Misri wakipanda mipando ya rangi ya njano.Kutatokezea mtu kutoka kizazi cha Sakhar.Kutokezea kwake kutabadilisha bendera nyeusi kuwa nyekundu.Yeye atahalalisha vilivyo haramishwa na kuvunja heshima na hadhi ya mwanamke kiasi kwamba hakutakuwa na heshima yeyote,huyu ndiye mtu atakayeteketeza Kufa, Wanawake warembo watabakwa kikatili kiasi kwamba hata migongo yao itavunjika na watakuwa wakitupwa barabarani.Waume zao watauawa.

 

Katika hali kama hiyo - atatokezea Imam Mahdi a.s. kutoka kizazi cha Mtume s.a.w.w. .Itatokezea hivyo wakati atakapouawa mtu mmoja huko Madina na ndugu yake atakapouawa katika hifadhi za Makka.Vitu vilivyofichika vitakuwa dhahiri.Watu weupe (Wazungu) watakuwa ni wenye nguvu sana na kutakuwa na mauaji na uporaji kila mahali.Kupatwa kwa mwezi na jua itakuwa ikitokea kila mara.Hapo ndipo vita vya kila aina vitazuka kutatokezea na mtawala huko Yemeni na rangi zake zitakuwa nyeupe kama pamba. Jina lake litakuwa ama ni Hassan au Hussein. Na kutokezea kwake ndipo kutakapotokomeza michafuko. Hapo ndipo Imam Mahdi a.s. atakuwa dhahiri. Yeye ataleta amani na raha duniani kote. (Imam Mahdi a.s.) Kiza cha Ulimwengu kitatokomezea kwa kuja nuru yake.Haki na ukweli itajidhihirisha yenyewe.Kugawiwa kwa mali kutakuwa kukifanyika kwa haki na uadilifu.Panga zitakuwa zimeisha pumuzishwa kutakuwa na amani na ukimya kila mahali. Watu wataanza kupata haki zao na ule moyo wa ukalimu utaanza kutokezea katika mioyo ya watu. Bwana huyu mkuu Imam Mahdi a.s. ataijaza dunia kwa amani, uadilifu na upendo. 

 

MNUJUMI WA KIIRAN AITWAYE JAMASP.

 

Kutokezea kwa Mfalme mkuu.

 

Imerekodiwa katika kitabu cha huyo bwana Jamasp kuwa Mfalme Ghustashp wakati mmoja alimuuliza huyo Jamasp:“Je lini kutakuwa na uokovu wa wanyama na wanadamu na dalili zake ni nini?”Bwana Jamasp alijibu:“Iwe bayana kwa Mfalme na mawaziri wake kuwa maisha ya mbele yatakuwa maovu kabisa na yenye kutisha.  Warusi kama mbweha wataivamia Iran kwa idadi kubwa sana.Watu wema watakuwa dhaifu. Viumbe vingi vya Allah swt vitauawa.Maisha hayatakuwa ya raha na yenye kuchosha. Uonevu na ukandamizwaji uliokithiri utazagaa duniani kote, kutazuka na vita vikali sana katika kingo za mto Furat na Tigris baina ya Wajerumani,Warusi, na Wazungu (Waingereza).Hapo ndipo Mfalme wa dini atakapotokezea na kutuliza ulimwengu mzima.Na baada ya kudhihiri kwake Allah swt atakuwa akizikubalia sara na dua za wanadamu. 

 

Ewe Mfalme, utafika wakati ambapo maovu na kila aina ya ubaya utakuwa umezagaa duniani kote.Wanaume watatafuta njia ya kujiridhisha kwa kuingiliana na wanaume wenzao na wanawake watajiridhisha kwa kuingiliana na wanawake wenzao, maafa ya ajali yataongezeka katika wakati huo kutatokezea kwa mtu mtakatifu kabisa.Msaada wake na maongozi yake ndiyo yatakayoondoa  uchafu na upotofu kutoka Iran.Dini ya ukweli itaenea kote. Wale watakao kataa na kukanusha kufuatia dini hiyo basi watateketezwa kwa mitetemeko ya ardhi.Kutakuwa na mitiririko ya damu kutoka mbinguni na kutakuwapo na ukame duniani kote.Baada ya hapo ndipo Allah swt atakapoineemesha dunia na kuirehemu.Ilimu kamili anayo Allah swt, na yeye tu ndiye aliye na ilimu ya kile tusichokiona au kukifikiria.

 

Jamasp ametabiri kuwa kutatokezea mtu mwenye jicho moja huko Bara la Arabia, kwanza yeye atajitangaza kama mtume na baadaye atajitangaza kuwa yeye ni Mungu yeye ataua watu wengi sana.Jitu hili linatambuliwa kama Dajjal katika riwaya za Kiislamu.

 

UTHIBITISHO WA KUWAPO KWA  IMAM MAHDI  A.S

KWA MUJIBU WA WANAZUONI WA AHLI SUNNA

 

Katika sehemu hii ya pili ninajaribu kuwaleteeni makala haya juu ya Uthibitisho wa kuwapo kwa Imam Mahdi  a.s. kwa mujibu wa Wanazuoni wa Ahli Sunna[13]  kwa sababu yatasaidia kutoa utata juu ya swala hili la kuwapo kwake kwani wengi wanazua kuwa mambo yote juu ya Imam a.s. yapo  yamezuliwa na Mashiah.

 

(1). HADITH YA KWANZA

 

Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume s.a.w.w. inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo:

"yeyote yule atakayekufa bila ya kumtambua na kumjua Imam wa zama zake basi mtu huyo atakufa mauti ya ujahili 

(yaani atakufa kifo cha ukafiri)."

 

Uzito wa Hadith hii itaeleweka vyema na umuhimu wake pia utakapoelewa kuwa mwana wa khalifa wa pili Abdullah bin Omar alipopata habari kuwa Abdul Malik amekuwa khalifa na hizo habari zilipomfikia akiwa Madina wakati wa usiku,basi aliondoka wakati huo huo na kumwendea mdhalimu huyo Hajjaj nyumbani mwake.Hajjaj alimwuliza sababu ya kufika kwake wakati huo wa usiku na hapo alimwambia kuwa amefika kumtolea  bay'a  (ahadi ya utiifu) ya baba yake Abdul Malik.

 

Hajjaj alimwelezea kuwa hakuwa na fursa wakati huo hivyo amwijie kesho yake.Hapo Abdullah bin Omar alisikitika mno na kusema "je nikifa usiku wa leo,basi nitakuwa nimekufa bila ya kufanya  bay'a ya imamu wa zama zangu na kwa mujibu wa  kauli ya Mtume Mtukufu s.a.w.w.,basi nitakuwa nimekufa mauti ya ujahiliyya ambavyo ni ukafiri.Hivyo vyo vyote vile,lazima chukua bay'a yangu."   

 

Hajjaj alimwita ndani (hivyo inamaanisha kuwa mtoto wa khalifa Omar alikuwa bado yupo nje) ya nyumba yake na kumwambia kuwa alikuwa anashughulika na hivyo mikono yake ilikuwa mashghuli hivyo atoe bay'a yake miguuni mwake. Hivyo huyo masikini mtoto wa khalifa Omar aliifanya  bay'a miguuni mwa Hajjaj kwa ajili ya utiifu wa Abdul Malik.Baada ya kufanya hivyo,alirejea nyumbani akiwa amefurahi mno.

(Sharh ya Nahjul Balagha - Ibn Abi al-Hadid,j.3,uk.362.Chapa ya Misri)

 

Jambo la kustaajabisha ni kwamba Abdullah ibn Omar katika zama za ukhalifa wa Amiral Muminiin Imam Ali ibn Abi Talib a.s. hakufanya bay'a na alikaa kimya na baada ya kupita miaka minne na nusu alipitisha kipindi hicho bila ya kumtambua  Imam  wa zama zake na wala hakuwa na khofu ya kufa mauti ya kafiri !

 

Vyema hadith hii inatuonyesha waziwazi kuwa katika kila zama kuna ulazima wa kuwapo kwa Imam wa zama hizo na ambavyo maarifa yake ni lazima yaelekee kwa kila mtu na vile vile katika zama zetu hizi pia yupo Imam ambapo inatuwia faradhi kuwa na ilimu na maarifa yake,ama sivyo atakayekufa bila ya kumjua na kufanya  bay'a yake atakufa kifo cha kikafiri.

 

Vile vile kuna wataalamu wa kuwapotosha watu kuwa wao wanadai kuwa neno  Imam linamaanisha  Quran Tukufu.Je watu kama hawa hawawezi kuelewa kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. hakulitumia neno la Imam  peke yake bali alitumia Imamu wa zama ?  Yaani kusudi lililopo hapa ni kule kubadilika kwa Imam katika kila zama yaani baada ya Imam mmoja atafuatia Imam wa pili na kuendelea. Jee na Quran imekuwa ikibadilika katika kila zama au jee kuna taarifa yoyote ya kuja kubadilika ?Jee baada ya Quran moja itafuatia ya pili na kuendelea ?.Kwa hakika sisi tusipotoshwe na wazushi kama hao kwa kutumia hila zao.

 

(2). HADITH YA PILI

Madhehebu yote ya Islam kwa pamoja yanaelezea Hadith ifuatayo na ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa Kiislamu na vile vile Sahih Bukhari na vitabu vingine vyote vya hadith pia vinaelezea kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema:

  "Baada yangu watakuwapo Maimamu kumi na wawili ambao watatokana na Maqureish."

 

Hadith zenye madhumuni kama haya yamepewa milango makhsusi katika vitabu vya Hadith. Na Hadith hii ipo yenye umuhimu mkubwa mno kwetu sisi kwani twaitegemea mno na kuweza kuelezea usahihi na ubatilifu wa Ukhalifa. Jambo lililowazi katika Hadith hii ni kuwa,iwapo kutapungua kwa idadi au kuzidi katika idadi ya  kumi na wawili  ama kutokea nje ya Qoeish  basi mfululizo huo wa makhalifa utakuwa si ule aliouelezea Allah swt kwa kupitia Mtume Mtukufu s.a.w.w..Kwani haiwezekani kamwe kuwa Allah swt alIssahau au kufanya kosa katika kuelezea idadi ya makhalifa wa Mtume s.a.w.w. na ambavyo kwa hakika idadi hiyo sivyo  au labda kwa ajili ya kufanya kubadili au labda inawezekana Mtume s.a.w.w. aliutoa huo ubashiri bila ya kupokea Wahyi (ufunulio kutoka kwa Allah swt). Haiwezekani kamwe kwa Allah swt kusahau au kutenda bila ya maarifa au kusema kwa Mtume s.a.w.w. bila ya kupokea wahyi ,basi itawezekanaje kwa idadi ya makhalifa aliyoielezea Mtume s.a.w.w. iwe imekosewa? Kwa hakika itatubidi tuyakini kuwa ijma',Istikhlaf,shuraa au taratibu zinginezo ambazo ndizo ziizotokezea utawala wa ukhalifa baada ya Mtume s.a.w.w. na ambao makhalifa wao hawakubakia katika idadi ya kumi na wawili au tawala hizo hazikuwa zile zilizopendwa au kubainishwa na Allah swt.

 

Kwa  kifupi, Mashiah wanayo fakhari kwa kuwa na Makhalifa kumi na wawili tu kama vile alivyothibitisha Mtume s.a.w.w. na vile vile alibashiri majina,idadi na kabila lao pia.

 

(3). HADITH YA TATU

Allamah Syed Jamal ud-Din Muhaddath ambaye ni mwachuoni mkubwa wa Ahli Sunna,anaandika katika kitabu chake Rawdhat ul-Ahbaab   kwa kumnakili Sahaba Ja'abir ibn Abdullahi Ansari wakati Allah swt alimfunulia Aya hii Mtume s.a.w.w.:-

 

"Enyi mlioleta Imani! Mtiini Allah swt na Mtume wake na vile vile mumtiini  'ulil Amr'."

 

"Basi mimi (anaendelea Bwana Jaabir) niliuliza "Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tunaelewa  Allah swt pamoja na Mtume wake.Lakini jee ni wakina nani hao ambao wanajulikana kama 'ulil Amr" ambao utiifu wao umefaradhishwa kwetu sisi?"

 

Hapo Mtume s.a.w.w. alitoa majibu haya yafuatayo:

"Wao watakuwa Makhalifa baada yangu na wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib na amfuataye atakuwa ni mwanae Hasan  na atamfuatia Hussein na baadaye atafuatia  Ali ibn al-Hussein na baadaye Mohammad ibn Ali na anatambulika katika Tawrati kwa umashuhuri wa jina la Baqir na ewe Jaabir! Karibu utafikia zama zake na hapo tafadhali naomba unifikishie salamu zangu. Baada yake atakuja Ja'afer as-Sadiq bin Mohammad na baadaye Musa ibn Ja'afer na baadaye Ali ibn Musa na baadaye Muhammad ibn Ali na baadaye Ali ibn Mohammad na baadaye Hasan ibn Ali na baadaye  Muhammad ibn al-Hasan  ambaye atakuwa juu ya ardhi hii kama  hujjatillah  na  bakiyallah  katika wamchao Allah swt. Huyo ndiye atakayepata ushindi wa mashariki hadi wa magharibi wa dunia hii. Na yeye mwenyewe ambaye atakuwa hayupo mbele ya wafuasi  (Mashiah) wake na wale wampendaye hadi kwamba hao hawatabakia katika itikadi ya Uimamu illa wale tu ambao Allah swt ameshawachukulia mitihani ya nyoyo zao."

 

Jaabir  r.a. anaelezea kuwa  "mimi sikusita kumwuliza Mtume s.a.w.w. "Ewe Mtume wa Allah swt! Je katika zama za Ghaibat,  wafuasi  (Mashiah)  wake wataweza kufaidika naye?"

 

Hapo Mtume s.a.w.w. alijibu:

 "Naam ! Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amenituma nikiwa Mtume wake,kuwa katika zama zake za  Ghaibat  ,Mashiah wake watang'arika kwa nuru yake na kufaidika kwa Ukhalifa wake kama vile  watu wanavyofaidika na jua hata kama litakuwa limejificha katika mawingu."

 

Hadith hii tukufu ambayo imenakiliwa na mwanachuoni mashuhuri wa Ahli Sunna kutokea kwa Sahaba Jaabir ibn Abdullahi ansari r.a. ambaye ni mmaarufu na mwenye kuheshimiwa katika Islam. Hivyo inatudhihirishia katika Hadith hizi tatu, wazi kuwa dunia haiwezi kubakia tupu illa kwa Makhalifa kumi na wawili na ni faradhi kwa kila Mwislamu kuwa na maarifa na ilimu yao na hao wote kwa pamoja wameshakwisha tambulishwa kuwa ni nani hao na kwamba Khalifa wa kumi na mbili hatakuwa akionekana machoni mwa watu  (atakuwa katika hali ya ghaibat) na kipindi hicho kitakuwa kirefu kiasi kwamba nyoyo zilizokwisha imtihaniwa,nyoyo zao zitakuwa salama na nyoyo zisizojaribiwa na zisizo na imani zitakuwa zikifanya mzaha na kuyapitisha kwa kicheko na Muumin watakuwa wakifaidika nae kama vile wanavyofaidika kwa jua hata kama litakuwa mafichoni.

 

Vivyo hivyo haiwezekani kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amekwishatubashiria juu ya Ghaibat bila ya kutubashiria juu ya dalili  na kudhihiri kwake [14]  Napenda kuwaleteeni baadhi ya hadith zinazozungumzia juu ya kudhihiri kwa Al-Mahdi a.s. na uthibitisho wa kuwapo kwake. Kwa hakika hadith zote ni mutawatir na hivyo hazihitaji dalili za ziada kwa sababu Shia na Sunni wote kwa pamoja wanaitikadi kuwa Imam Mahdi a.s. anatokana na kizazi cha Bi.Fatimah az-Zahra a.s na kwamba atadhihiri katika kipindi cha karibu na Qiyama.

 

(4). HADITH  YA  NNE

Imam bu Dawud ameandika katika kitabu chake  Sunan  na Imam Tirmidhi anaandika katika Sahih Tirmidhi  kwa kumnakili Abu Said Khudhri,kuwa:

 

" Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

' Mahdi anatokana nami na mwenye uso unaong'aa na pua yake iliyo ndefu ataijaza ardhi kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imeshajaa kwa dhuluma na ufIssadi, na atatawala kwa kipindi cha miaka saba.' "

 

(5). HADITH  YA  TANO

 

Imam Abu Dawuud katika  Sunan amendika kwa kumnakili Sayyidina Imam Ali a.s.:

 

"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa iwapo kwisha kwa dunia hata kama ni siku moja itakayobakia,hivyo pia Allah swt atamtuma mtu mmoja kutokana na Ahli Bayti yangu  (kizazi changu) humu duniani ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi."

 

(6). HADITH  YA  SITA

Imam Abu Dawud amemnakili Ummul Moominiina kufuatilia mfululizo huo wake kuwa:

Mtume Mtukufu s.a.w.w amesema kuwa

' Mahdi atatokana na Itrati  (kizazi) yangu,yaani atatokana na kizazi cha Fatimah az-Zahra a.s.'  "

 

(7). HADITH  YA  SABA

Imam Bukhari katika  Sahih Bukhari , Imam Muslim katika  Sahih Muslim  na Kadhi ibn Mas'ud Baghawi katika Tasnif Sharh al-Sunnah. Wote wanamnakili Abu Hurayrah akisema:

 

"Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

'Je hali yenu itkuwaje wakati Mtume Issa a.s. atakapoteremka kwenu na Imam wenu atakuwapo ametokea miongoni mwenu?'"

 

(8). HADITH  YA  NANE

 

Imam Tirmidhi katika  Sahih Tirmidhi  na Imam Abu Dawud katika  Sunan Abu Dawud  wanamnakili Abdullah Ibn Mas'ud akinakili riwaya:

 

" Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

kuwa dunia haitakwisha hadi hapo mfalme wa Kiarabu  hatatokea kutokana na kizazi changu,na ambaye jila lake litakuwa kama jina langu."

 

(9). HADITH  YA  TISA

Imenakiliwa na Maimamu wa Ahli Sunna katika Sahih  zao,riwaya ifuatayo:

Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

"Atatokezea mtu mmoja katika Ahli Bayti yangu,atakayetawala na jina lake litakuwa kama jina langu."

 

(10). HADITH  YA  KUMI

Imam Abu Is-haq  Tha'alabi katika  tafsir  yake anamnakili  Anas bin Malik kuwa:

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa

" Sisi wana wa Abdul Muttalib ni viongozi wa watu wa Jannah,yaani mimi , Hamza, Ja'afer  na Ali na Hasan , Hussein na Mahdi."

 

Dalili zote hizi zimefanya wazi kuwa Mtume s.a.w.w. ametuthibitishia nidhamu ya ukhalifa kwa urefu na undani katika maneno yaliyo wazi na yenye balagha na katika maelezo hayo yaliyokuwa na umuhimu zaidi ni juu ya Imam Mahdi a.s. na kipindi chake cha Ghaibat na vile vile kuhusu kudhihiri kwake.

 

Iwapo kutakuwa na watu ambao wataendelea kushuku kuhusu Hadith hizo,basi hapa chini ninawaleteeni shahada walizozitoa Wanazuoni na Maulamaa wa Ahli Sunnah kwa kuthibitisha itikadi ya Imam wa kumi na mbili yu bado hai na kwamba yupo katika Ghaibat na atadhihiri katika kipindi cha kabla ya Qiyamah Na itikadi hii inaaminiwa na Ahli Sunna na Mashiah.

 

(1). Allamah Abdul  Wahab Shu'arani

 

Ni mwanachuoni mkuu katika Ahli Sunna na ambaye amesifiwa mno na Shah Waliullah Dehlavi kuwa ni Sahabi Fadhail na Makarim Aarif Muhaqqiq Awliyaullah na kumshirikisha katika Irthani Rasulullah.

 

"Na miongoni mwao wapo Sheikh Saleh,Abid al-Zahid mwenye kashif sahih  na bwana adhimu Sheikh Hasan Iraqi,na umri wake ulikuwa kadiri ya miaka mia moja na thelathini,na mara moja mimi na Abul Abbas Harashi,tulimwendea,naye alituambia kuwa mimi ninataka kuwaambieni jambo moja ambalo nyie munaweza kuelewa hali yangu ya ujana hadi wakati ule (utakaouelezea)."

 

Sisi tulimwelezea kuwa atuelezee.Naye alisema kuwa "mimi wakati huo nilikuwa kijana kamili na huko Shaam (Damascus) nilikuwa nikijifunga nguo ya kujivika shingoni hadi miguuni  (abaa) na nilikuwa sijizuii katikakutenda madhambi(kwani nilikuwa nikijivunia juu ya nafsi yangu). Basi siku moja mimi niliingia katika chuo cha Bani Umayyah,na huko nilimwona mtu mmoja amekaa juu ya kiti akielezea juu ya Imam Mahdi a.s. na hali ya kudhihiri kwake. Basi hapo moyoni mwangu nilijawa na mapenzi yake Imam Mahdi a.s. na nikaanza kuomba duaa  kwa Allah swt kuwa anikutanishe naye Mahdi a.s. Ulipita kiasi cha mwaka mmoja hivi nikiwa nikiomba duaa hiyo,siku moja baada ya magharibi nilikuwa katika Msikiti wa Jamea na mara nilimwona kwa ghafla mtu mmoja wa makamo akiingia Msikitini akiwa amevaa kilemba cha kama Waajemi na amevaa jubba lililotengenezwa kwa ngozi ya ngamia,na akiwa amegusa mabega yangu,alisema:

 

"Je kwa nini unataka kuonana nami ?"

Nami nilimwuliza, 'Je wewe ni nani ?'

Alijibu, "Mimi ni Mahdi."

 

Basi mimi nilibusu mikono yake na nilimwomba aje nami hadi nyumbani kwangu,naye alinikubalia na kuwa mgeni wangu kwa muda wa siku saba na alinifundisha dhikiri ya Allah swt  na alinihukumu kuwa niwenikifunga saumu siku za katikati na kila siku niwe nikIssali sala za rakaa  mia tano na kwa ajili ya  kutaka kulala,nisiwe nikiuweka uso wangu hadi usingizi utakapokuwa ukinighalibu kabisa.Baadaye alitaka kuondoka,na kuniambia, "Ewe Hasan! Sasa baada yangu usiende kwa mtu yeyote yule na chochote kile ulichokipata ktoka kwangu kinakutosha kabisa na ujue kuwa kile walichonacho wengine ni kidogo na khafifu kuliko kile ulichonacho wewe,kwa hivyo usichukue hIssani za wengine zisizo na faida.Mimi nilisema sam'an wa ta'atan! ,na nilimshukuru na kumruhusu kuondoka na nilitaka kumsindikiza,lakini nilipofika mlangoni,alinizuia nisiendelee na kuniambia nirudie hapo. Basi mimi nilibakia katika hali hiyo kwa miaka.Nami nilimwuliza Imam Mahdi a.s.kuhusu umri wake,naye alinijibu,Ewe Mwana! Umri wangu kwa sasa hivi ni miaka 620."

 

Sheikh Hasan Iraqi anaelezea kuwa mazungumzo haya yamepita miaka mia moja iliyopita(yaani wakati huo umri wa Imam Mahdi a.s. ulikuwa wa miaka 720).

Allamah Abdul Wahab Sha'arani anaelezea kuwa mimi nilimwelezea hayo Ali Khawasi na ambaye aliwafikishia umri wa Imam Mahdi a.s. na ile ya Sheikh Hasan Iraqi."

 

Kutokana na kisa hicho cha hapo juu si kwamba tu Allamah Abdul Wahab Su'arani bali hata Sheikh Hasan Iraqi na Ali Khawasi,hawa wazee watatu wanatupatia uthibitisho wa Itikadi zao za kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. na mmoja wa watatu hao alibahatika kuupata ugeni wa Imam Mahdi a.s. na vile vile kupata fursa ya kuelimishwa na Imam Mahdi a.s. Vile vile Allamah Abdul Wahab Shu'arani ameandika katika kitabu chake mashuhuri Yanaqut wa Jawahir  katika sura ya sitini na tano juu ya dalili za kukaribia Qiyamah,anaelezea dalili ya kwanza ikiwa ni  kudhihiri kwa Imam Mahdi  a.s. na baadaye akielezea dalili zingine anaandika wakati ambapo Din itakapokuwa ikififia,basi:

"Wakati huo ndio unaotakiwa kumsubiri Imam Mahdi a.s. adhuhuri na huyo Imam a.s. atakuwa ni mtoto wa Imam Hasan al-Askari a.s. na alizaliwa tarehe 15 Sha'aban mwaka 255 Hijriyyah. Naye yu hai na ambaye yu bado hai hadi atakapoungana na Mtume Issa bin Maryam a.s. Umri wake wakati huu ni miaka 958,miaka 706 imeshakwisha."

 

(2). Mawlana Ali Akbar Mawdudi

Huyu ni miongoni mwa Maulamaa wakubwa mutakhirina naye ameandika,

yanayojulikana kwa jina la  Makashifat na mwandishi huyu katika kuelezea juu ya Ali ibn Sahil il-Isfihani,anaandika:

 

"Watu wanasema kuwa kutokufanya makosa katika hukumu au maamrisho ya Din ni sifa ya Mitume tu,lakini Sheikh r.a. amekhitilafisha jambo hili miongoni mwa watu katika Hadith ile ambayo imeshuka juu ya Mahdi a.s. akiyeahidiwa Babu yake  a.s..Baadaye katika sura ya arobaini na tano ameandika kuwa Sheikh Abul Hasan al-Shadhili r.a. amesema kuwa zipo dalili kumi na tano za Qutb - Shakhsiyya ya pekee kiongozi - mfano kwamba uthibitisho wake unatokana na ucha Mungu wake,kutokuwa na madhambi,rehema,ukhalifa na niaba na kudura huwa vinamsaidia na kudhihirisha waziwazi dhati yake na sifa zake na kadhalika,n.k."

 

Basi kwa kauli hii (kuwa katika Qutb kuna kuwapo na ile sifa ya kutokuwa na madhambi) inathibitisha kwa usahihi kuwa madhehebu ya wanaoamini kuwa wapo Maasum (wasio na madhambi) mbali na Mitume......kwa sababu kuwapo kwa utawala wa al-Mahdi Maw-ud  (aliyeahidiwa)  a.s. (yaani yeye ni Qutb baada ya baba yake Imam Hasan al-Askary a.s.  kama vile Imam Hasan al-Askary a.s. alivyokuwa Qutb baada ya baba yake hadi hapo huu mfulululizo unamfikia  Imam Ali  ibn Abi Talib a.s. ) inatuelezea ishara ya kuwa rutuba hii inakuwa makhsusi kwa ajili ya kizazi hiki tu(Baada ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Qutb hadi al-Mahdi al-Maw-ud a.s.,na wala si kabla ya Imam Ali s.a.).Hivyo yeyote yule atakayekuwa Qutb basi atakuwa ni katika niaba ya al-Mahdi  al-Maw-ud a.s. kwa sababu Imam Mahdi a.s. yupo ghaibu  mbele ya macho ya watu na papo hapo huwa anaonana na baadhi ya watu makhsusi na huwa sikatika hali ya ghaibu mbele yao...... Hivyo imekuwa ni lazima kuelewa kuwa kila Imam a.s. katika Ithna-Asheria ni Maasum (wasiye na dhambi)--- elewa faida hii !"

 

Kwa maelezo hayo,inatuwia waziwazi kuwa Mawlana Ali Akbar Mawdudi anamchukua Imam al-Mahdi al-Maw-ud  a.s. kuwa ni Qutb  wa zama baada ya Imam Hasan al-Askary a.s. na vile vile alikuwa akitikadi kuwa alikuwa Maasum (asiye na madhambi)  na vile vile alikuwa akisema daima kuwa Imam Mahdi a.s.alikuwa haonekani kwa wote illa wale walio makhsusi tu ndio walioweza kumwona.

 

(3). Mulla Jamiy  r.a.

 

Huyu ni Aalim mashuhuri katika Ahli Sunna na iwapo mtu atataka kumsifu yeye basi ni sawa na kutaka kuumulika jua kwa taa zetu,huyo anaeleweka kwa kuwa ni kitovu cha ilimu ya dhahiri na batini.Yeye ameandika katika tasnif yake mashuhuri Shawahid Nubuwwah kuwa al-Imam Mahdi a.s. ni Imam wa kumi na mbili na ameandika sura moja ndefu sana ambamo ameandika juu ya kiujiza na karama kabla ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi a.s. na wakati wa kuandika matukio yote .Vile vile ameandika kuwa mimba ya Imam a.s. ilikuwa haionekani na kuzaliwa kwake tu alisujudu na kusoma aya za Qurani Tukufu.

 

Naye alizaliwa akiwa amekwishakaa jando na hakuwa na ngozi ya utosini na katika bega lake kulikuwa kumeandikwa jaal haq wa zahaqal baatil,innal batila kana zahuqa  na pale alipokula chfya alisema alhamdulillahi rabbil aalamiin. Ameandika habari hizi na kama hizi kwa mapana na marefu sana na kwa kutoa maelezo marefu na baadaye ameandika hivi:

 

"Rawi (mwenye kuripoti)  amesema kuwa mimi nilikuwa pamoja na Imam Hasan al-Askary a.s. na nilimwambia  "Ewe mwana wa Mtume s.a.w.w. ! Je ni nani atakayekuwa Imam au Khalifa baada yako ?"

 

Basi Imam a.s. alikwenda ndani na alirejea akiwa na mtoto mikononi mwake. Mtoto huyo alikwa mfano wa mbalamwezi --- akipendeza na alijawa nuru---na umri wake ulikuwa kama miaka mitatu hivi.

Hapo akasema " Ewe Fulani ! Iwapo wewe usingalikuwa daraja la juu mbele ya Allah swt,basi mimi nisingalikuonyesha kamwe huyu mtoto.Jina lake ni jina la Mtume s.a.w.w. na kuniyah yake ni ile ya Mtume s.a.w.w.. Na huyu ni yule ambaye atakayeijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi."

 

Vivyo hivyo ipo riwaya nyingine isemayo Wakati  Imam  Hasan al-Askari a.s. alipomwonyesha mtoto wake na kusema: "Huyu ndiye Imam wenu !" na hapo Imam Mahdi a.s. aliteremka kutoka mapajani mwa Imam Hasan al-Askary a.s.. Abu Mohammad  a.s. alimwambia mwanae "Ewe mwana ! Uwe mafichoni (ghaibu) hadi wakati maalum" hivyo aliingia ndani ya chumba huku mimi nikimwona. Hapo Imam Hasan al-Askary a.s. aliniambia "inuka na ukamtafute huyo mtoto" .Nami nilikwenda kumtafuta huyo mtoto chumbani,lakini sikumwona mtu yeyote !

 

(4). Khwaja Muhammad Parsa

 

"Ilikuwa ni jambo lafuraha mno kwa masheikh na maulamaa kwa kukutana naye",anaandika katika kitabu chake Faslul Khitab :

 

Na wakati Abdullah Jaafer,mwana wa Imam Ali an-Naqi a.s. alipozusha habari kuwa ndugu yake Imam Hasan al-Askari a.s. alikuwa hana mtoto yeyote na hivyo yeye akiwa kama ndugu yake,basi uimamu ulikuwa umepatiwa yeye. Kwa hakika alikuja kuwa mashuhuri kwa jina la kadhib (mwongo) . Na mtoto wa Imam Hasan al-Askary a.s. ni Mohammad al-Mahdi a.s. na watu makhsusi walijua na wanajua.

 

Baadaye mwandishi anaendelea kuelezea kuwa ilipofika tarehe 15 Sha'aban mwaka 255,usiku huo Bi.Hakimah Khatun alikuja nyumbani mwa Imam Hasan al-askary a.s. naye hakumruhusu kuondoka na kulipokaribia wakati wa alfajiri,alizaliwa Imam Mahdi a.s. na baada ya hapo,mwandishi anaendelea kuandika:

 

"Hakimah Khatun anaelezea:

"Nilipomwijia Imam Hasan al-askary a.s. nilimwona mtoto aliyezaliwa na kuviringishwa katika kitambaa cha rangi ya kijani na us wake ulikuwa umejaa kwa nuru na furaha hadi kunifanya mimi nijiwe na mapenzi yake moyoni mwagu. Mimi nilimwambia Imam Hasan al-Askary a.s. 'Ewe Imam wangu ! Iwapo unayo ilimu yoyote  kuhusu huyu mwana mpenzi,basi naoma nami uniambie machache.'

Imam a.s. aliniambia,"Ewe dada yangu! Huyu ndiye yule Imam asubiriwaye ambaye tulikuwa tumeshakwishapata ubashiri wake." Bi.Hakimah Khatun anasema kuwa 'mimi papo hapo nilifanya sujuda ya kumshukuru Allah swt.Na nilikuwa nikienda daima nyumbani mwa Imam Hasan al-Askary a.s..Lakini siku moja nilikuwa sikumwona huyo mwana na papo hapo nilimwuliza Imam Hasan al-Askari a.s. 'Ewe Imam wangu ! Je umemfanya nini Imam wetu  al-Muntadhir  (aliyengojewa) ?"

 

Imam a.s. alinijibu, "Mimi nimeshampa katika hifadhi ya Allah swt ambaye alikadhibiwa Mtume Musa na mama yake katika hifadhi Yake (i.e.Allah swt). "

 

Ibara hii imekuwa ikitoa hidaya lakini vile vile imetuongezea uhakika kuwa Khwaja Muhammad Parsa pia ni muumin wa Imam al-Asr (Imam Mahdi a.s.) na vile vile juu ya ghaiba na pia alikuwa akiitikadi kuwa pale atakapotaka  Allah swt ndipo atakapodhihiri,hapo ndipo itakapotimia ubashiri wa Mtume s.a.w.w.

 

Vile vile katika kitabu hiki Khwaja Muhammad Parsa ameandika dalili za kudhihiri kwa Imam al-Muntadhar a.s.:

 

Na zipo Hadith nyingi mno zisizokadirika kuhusiana na maswala haya,na Imam Mahdi radhiyallahu Anhu (Imam-i-Zamana -- ambaye haonekani machoni mwa watu na ambaye yupo katika kila zama) anaelezewa mambo mengi mno yaliyo mema kabisa na vile vile zipo hadith zinazooana kuhusiana na swala la kudhihiri kwake na kusambaa kwa nuru yake. Yeye ataimarisha sharia ya Mtume s.a.w.w.na atafanya jihad kwa ajili ya Allah swt .Ataitakasisha  kwa kutokomesha najisi na maonevu juu ya ardhi ya Allah swt kutokea ncha moja hadi ya pili,zama zake zitakuwa ni zama za  muttaqiina  (wacha Mungu),masahaba wake hawatakuwa na mashaka au udanganyifu wa aina yoyote ile na vile hawatakuwa na aibu za aina zozote zile na watakuwa wakimfuata Imam wa zama na kutanda kwa mujibu wa hidaya zake na Allah swt atawajaalia maarifa ya Imam Mahdi a.s. Imam Mahdi a.s.ndiye atakaye khitimisha Ukhalifa na Uimamu  na kwamba yeye yu Imam kuanzia siku ile ambayo baba yake (Imam Hasan al-Askary a.s.) alipokuwa shahidi."

 

(5). Sibt ibn Jawzi

Huyu pia ni miongoni mwa Maulamaa wakubwa wa Ahli Sunna,naye katika kitabu chake mashuhuri Tadhkirt khawas al-ummah  fi ma'arifat il-Aimmah  anaandika kuhusiana na Imam al-Mahdi a.s.:

 

Yeye ni mwana wake Imam Hasan al-Askary a.s. na kuniyyah yake ni Abu Abdillah na Abul Qassim. Naye ni i Khalifa hujjat, Imam wa zama hizi,ni Qaim  na Muntadhar  na baqi  na yeye tu ndiye Imam-i-zamana (Imamu wa zama).

Je kunaweza kubakia chochote katika kuelezea kubakia hai na kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.?

 

(6).Abu Abdillah Muhammad ibn Yusuf bin Muhammad Ghibhi Shafi'i

 

Utunzi wake upo mashuhuri wa kifayat il-taalib  na vile vile ameandika kitabu kingine albayan ambacho ameandika khususa juu ya hali ya Imam Zamana a.s. kuzungumzia Uimamu,kuwapo kwake,umri wake mrefu na akiandika na kutoa maelezo juu ya kuwapo kwake  Imam al-Mahdi al-Maw-ud a.s.,anaandika:

 

Kuanzia ghaibat ya Imam Mahdi a.s. kuwapo hai kwake hadi leo kuna dalili moja ya kwamba si muhali kwake kubakia kwake hadi leo. Katika Maawliya Allah  wapo Mtume Issa  bin Maryam a.s. na Mtume Khizr a.s. na Ilyas  a.s. na hao wapo hai na katika maadui wake Allah swt wapo Dajjal na mal-un Iblis nao wote pia wapo hai. Na kubakia kwao hai na maisha yao yanaelezea katika Quran na Hadith na vinathibitishwa hivyo.

(Iwapo Allah swt anawaweka hai na baki shakhsiyyah zingine,jee itashindwa nini kumweka hai na baki Imam Mahdi a.s.?)

 

(7). Sheikh Nurdin ibn Sibagh al-Malik

 

Sheikh mashuhuri na mwenye kuheshimiwa katika Ahli Sunna,anaandika kwa marefu juu ya kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. katika kitabu chake Al-Fusul ul-muhimmah kama yafuatavyo:

' Sura ya kumi na mbili: Katika kuzungumzia mwana wa Imam Hasan al-Askary a.s. aitwaye Abul Qasim Muhammad hujjat Khalaf Saleh,naye ambaye ni Imam wa kumi na mbili,na kuelezea historia yake ya kuzaliwa na Uimamu wake na katika dalili zake na hali yake na ghaibat na muda wa kuwapo kwa autawala wake na katika kuelezea nasabu yake,kuniyyat na laqab yake. '

Katika sura hii kuna habari nyingine ielezewavyo,lakini tunanakili badhi ya habari kama  ifuatavyo:

Mwana wa Imam Hasan al-Askary a.s. aliyeitwa Abul Qasim alizaliwa tarehe 15 mwezi wa Sha'aban katika mwaka 255 Hijriyyah,katika mji wa Samarrah  huko Iraq .

 

Na hali hii inatudalilisha juu ya mtoto huyo aliyezaliwa ni Imam wa kumi na mbili na ambavyo ipo imebashiriwa na Maimamu watukufu a.s. Zipo riwaya nyingi kuhusu yeye na hadith nyingi zipo mashuhuri,nasi bila ya kufikiria tumefupisha maelezo yote yale na kuyaacha  na muhaddithiin wanaziandika hadith zile ambazo zimetolewa na wanatutaka sisi tuzikusanye hizo hadith ....

 

Maulamaa wa hadith wamesema kuwa Mahdi ni yule yule ambaye ni qaim al-Muntadhar  na kuhusu kudhihiri kwake riwaya zote zipo zinaoana na kuhusu nuru yake pia wanaafikiana na vile vile dhuluma zote zitaangamia kwa kuja kwake,na kwa kuja kwake hapatakuwa na kiza cha aina yoyote illa mng'aro kama vile usiku unavyobadilika katika siku, na ni karibu tu yeye atajitokeza kutoka ghaibu na nyoyo zote zitajawa kwa furaha tele.

 

(8). Shah Waliullah Dehlavi

 

Ahli Sunna wanamwita khatimil Aarifiin,Sayyidil Muhaddithiin,sanadil Mutakallimiin,Hujjatulahi ala-Aalamiin anaelezea kwa marefu mno katika tasnif yake Fadhlul Mubiin  juu ya Imam wa zama na kuwapo kwake na pia amekuwa mwenye kuamini juu ya Uimamu.Hivyo anaandika kwa kunakili hadith moja:

 

Mimi nimesema kuwa Ibn Akilah ameniruhusu kwa mdomo mambo yote ambayo riwaya zilikuwa zinaruhusiwa kwa ajili yake.Nami katika mfululizo wa Hadith niliikuta hadith moja mfululizo ambayo kila sehemu yake ilikuwa ikichukua upeke wa aina yake na ilikuwa na sifa adhimu ya watu wakuu,nayo ni kwamba Ibn Aqila alisema kuwa mimi niliarifiwa na Sheikh mkuu pekee wa aina yake katika zama zote Sheikh Hasan Ibn Ali Ajmiy,naye aliarifiwa na hafidh wa nyakati zake Bwana Jamalud-Din Babli aliarifiwa na mnakili na mtoa mawaidha,Bwana Muhammad Hajjazi naye aliarifiwa na Sufi  wa wakati huo Sheikh Abdul Wahab Shu'arani,naye aliarifiwa na Mujtahid wa zama zake Jalaludin as-Suyuti,naye aliarifiwa na zahid wa zama Imam Jamaluddin ibn Muhammad ibn Muhammad al-Jamal,naye amearifiwa na aliyekuwa Muhaddith  wa nchi za Uajemi Imam Muhammad ibn Mas'ud,naye amearifiwa  na Sheikh mkuu wa zama zake Sheikh Isma'il bin Mudhaffar Shirazi,naye aliarifiwa na Muhaddath wa nyakati zake  Abdus-Salaam bin Abu ar-Rabi'i Hanafi,naye  amearifiwa na Sheikh wa zama zake Abu Bakar Abdullah bin Muhammad Shaabur al-Kalamsi,naye amearifiwa na Imam wa wakati wake Abdul Aziz ibn  Muhammad Adami,naye amearifiwa na aliyekuwa mtu wa nadra wa zama zake Suleiman bin Ibrahim bin Muhammad bin Suleiman naye amearifu kuwa amemwarifu Ahmad bin Hashim Biadhuri ambaye amebainisha kuwa aliyekuwa hafidh wa zam zake aliambiwa na Imam al-Asr a.s. Muhammad ibn al-Hasan ibn Ali (aliye katika hali ya ghaibu kuwa mimi (Imam Mahdi)  niliambiwa na Baba yangu Imam Hassan al-Askary a.s., naye aliambiwa na Baba yake Imam Ali an-Naqi a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Muhanmadtaqi a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Musa al-Kadhim a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Muhammad al-Kadhim a.s. naye Imam Zainul Aabediin a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Syyidus-Shuhadaa, al-Husein ibn Ali ibn Abi Talib a.s. naye aliambiwa na Baba yake Sayyidil Awliya’a Ali ibn Abi Talib a.s. naye aliambiwa na Sayyidil Ambiya Mtume Mtukufu s.a.w.w. naye aliambiwa na Sayyidil Malaika Jibraili naye amesema kuwa Allah swt amesema “Mimi ni Allah na wala hakuna mwingine wa kuabudiwa ila ni mimi tu. Yeyote yule atakaye kubali na kusadiki upweke wangu basi atakuwa ameshaingia katika ngome yangu na yeyote yule atakaye kuwa ameingia katika ngome yangu, basi ameepukana na adhabu zangu.”

Katika riwaya hii tumeonyeshwa kuwa si Shah Waliullah Dehlavi tu bali Maulamaa kumi na sita wa Ahli Sunna ambao walikuwa na sifa pekee katika zama zao... ambao walikuwa akiamini juu ya Imam Mahdi Akhiruz-zamaan a.s. kuhusu jina lake na ukoo wake na hali yake ya ghaibat na kuwapo kwake akiwa Imam wa zama zetu kwani asingelileta riwaya kama hiyo iwapo mmoja wa waarifu wake angelikuwa hajulikani kwa utukufu wake mbele yake, hivyo aliwaheshimu wote waliotajwa kwa pamoja.

 

(9) Sheikh Abdul Haq Dahlavi

 

Ni miongoni mwa wale walio mashuhuri katika sunan, naye ameandika katika risala yake Munaqib wa ahwaal Aimma at-haar kuwa:

 

Na mwana wa Hasan al-Askary a.s. aliyeitwa Muhammad al-Mahdi a.s. alikuwa akijulikana na Sahaba makhsusi na kundi lililokuwa likiaminika tu.

 

Ipo riwaya kuwa Bi. Hakimah Khatun binti Imam Muhammad Taqi a.s. ambaye alikuwa ni dada wa baba yake Imam Mahdi a.s. na alikuwa akiomba mno kwa Alah swt amjaalie mtoto Imam Hasan al-Askary a.s. ili aweze kumwona kwa macho yake katika uhai wake. Na Imam Hasan al-Askary a.s. alikuwa amemchagua Bi. Nargis Khatun kwa ajili ya ndoa.  Ilipofika tarehe 15 ya mwezi Sha’aban mwaka 255 Hijriyyah, Imam Hasan al-Askary a.s. alimwambia Bi. Hakimah Khatun abakie nyumbani kwake usiku ule kwani kulikuwa na jambo moja mbele yao usiku ule.Basi kwa mujibu wa ombi la Imam Hasan al-Askari a.s. Bi. Hakimah alibakia nyumbani mwa Imam a.s. Ilipokaribia wakati wa alfajiri, hali ya Bi. Nargis Khatun ilianza kubadilika. Naye Bi. Hakimah alimkaribia ili kumsaidia lakini alimkuta anaye mtoto mzuri mno aliyezaliwa na akiwa amekwisha tahiriwa na kuogeshwa, nk. Alimchukua mtoto huyo na kumleta kwa Imam a.s. naye alimpapasa kwa mkono juu ya bega lake na macho yake na aliuweka ulimi wake mdomoni mwa mtoto huyo, na aliisema Adhaan katika sikio lake la kulia na aliisema Iqamah katika sikio la kushoto na baadaye alimwambia:“Ewe Bibi! Mchukue huyu mtoto kwa mama yake” Na hivyo Bi. Hakimah Khatun alimpeleka mtoto kwa mama yake.

 

Bi Hakimah Khatun anasema kuwa:“Baadaye nilimwona mtoto akiwa mikononi mwa baba yake akiwa amevishwa nguo za rangi ya kijani na akitokwa na nuru hadi mimi nilijawa na maenzi yake hadi hapo yalinitoka:‘Ewe Imam wangu!Je kuna chochote unachokielewa kuhusu huyu mtoto aliyezaliwa ili uweze kuniambia?”

 

Imam Hasan al-Askary a.s. alisema:“Ewe dada yangu!  Huyu mtoto ni yule ambaye alikuwa akisubiriwa (al-Muntadhar) na ubashiri wake tulikuwa tumeshaupata.”

 

Bi Hakimah Khatun anasema:“Mimi nilifanya sujuda juu ya ardhi kwa kutoa shukrani zangu kwa Allah swt. Na daima nilikuwa nikija nyumbani kwa Imam Hasan al-Askary a.s. Na siku moja nilipokuja sikumwona huyo mtoto, basi sikusita kuuliza,“Ewe Imam wetu!Je imemwia nini Sayyidil Muntadhar wetu?”

 

Hapo Imam Hasan al-Askari a.s. alinijibu kuwa alikuwa ameshamkabidhi yule ambaye alikabidhiwa na mama yake Mtume Musa a.s.

 

Na vile vile inapatikana riwaya isemayo kuwa aliulizwa jina la Qaim  wao litakuwa nini, alijibu kuwa:“Sisi tumehukumiwa kutotamka jina lake kabla ya kuzaliwa kwake.”

Je dalili zote hizo hazitoshelezi kuthibisha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s?

 

(10) Muhaddith Jamalud- Din

Huyu bwana anahesabiwa miongoni mwa walio mabingwa katika ilimu ya Hadith na vitabu vyake vinatazamwa kwa heshima kubwa. Yeye anadhihirisha itikadi yake katika kitabu chake mashuhuri kiitwacho Rawdhatil Ahbaab hivi:

 

Mazungumzo katika bayani ya Imam wa kumi na mbili: 

 

Mu’tamin Muhammad bin Hasan katika riwaya nyingi mno zinazooana zinaelezea juu ya kuzaliwa kwa Imam al-Mahdi a.s. ilikuwa ni tarehe 15 Sha’aba 255 Hijriyyah mjini Samarrah na mama yake alikuwa ni mtumwa aliyeitwa Sakil au Susan au Nargis. Majina ya Imam a.s. yalikuwa yakifanana na yale ya Mtume s.a.w.w. na vile vile al-Mahdi al-Muntadhar na Khalafi Saleh na Sahibu az-Zamaan. Kwa mujibu wa riwaya katika kzama za Baba yake (ambaye ni karibu na usahihi) alikuwa na umri wa miaka mitano na pengine labda ni miaka miwili ambapo Allah swt alipomjaalia hekima na alipatiwa daraja la juu la Uimamu kama Mitume Yahya a.s. Zakariyyah a.s. Imam wa zama a.s. katika kipindi cha Khalifa Mu’atamad na katika mwaka 265 au 266 Hijriyyah, inasadikiwa kuwa katika mji wa Samarrah, alikuwa ghaibu.”

 

(11)   Allamah Muhiddin bin’ Arabi

 

Kwa sasa tunawaleteeni ushahidi wa Allamah huyu wa Kisunni na ambavyo kauli yake hadi leo ipo mashuhuri kuwa:

 

   Hussein a.s. aliuawa kwa upanga wa Babu yake (Mtumes.a.w.w.) kwa sababu Bay’a ya Yazid ilikuwa imefanyika na Hussein a.s. alimwasi (huyu Yazid aliyekuwa imam wa haki). 

    (Je ni nani aliyekuwa juu ya haki:  Hussein au Yazid)?

 

Ni dhahiri kuwa iwapo Sheik mwenye msimamo mkali kama huo (kwani amethubutu kumwita Yazid kuwa ni Imam wa haki na kwamba Imam Hussein a.s. kuwa ni mwasi)!  Akianza kuelezea kuwa Imam Mahdi a.s. ameshazaliwa na yupo ghaibu na kufikia karibu na Qiyama atadhihiri na vile vile ni maasum na pia ameelezea kwa kinaga ubwaga sifa njema za Imam al-Mahdi a.s. na kumsifu katika kila hali, basi inathibitisha waziwazi kuwa haki daima huwa juu ya kila kitu.

Naye katika kitabu chake mashuhuri kiitwacho Futuhaati Makkiyyah katika sura ya 386 anaelezea kwa kirefu juu ya habari zinazomhusu Imam zamana na ametumia karatasi nyingi mno katika hayo, nanakuleteeni baadhi ya habari hizo juu ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s., zama zake na haki na mwanzoni mwake au zile zinazozungumzia sifa zake au kuhusiana kiilhamu au kiwahii na kuimarisha Din kwa mara ya pili na bayani ya uharifu wake, nk.

 

Hivyo tunakuleteeni madondoo yanayozungumzia juu ya majina yake, unasaba wake, kuzaliwa kwake na vile vile ghaibat:

 

Na muelewe kuwa kudhihiri kwa Imam al-Mahdi a.s. ni dharuri, lakini yeye hatadhuhuri hadi dunia itakapokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi, basi atadhihiri kwa kuijaza dunia kwa uadilifu na haki na ikiwa hata kama itabakia siku moja katika umri wa dunia, basi Allah swt atairefusha siku hiyo hadi hapo huyu Khalifa atatawala naye atatokana na kizazi chake Mtume s.a.w.w. na atakuwa katika wana wa Fatimah az-Zahra a.s. na babu yake ni Hussein ibn Ali ibn Talib a.s. na Baba yake mzazi ni Imam Hassan al-Askari ibn Ali an-Naqi a.s. (aliendelea kuelezea nasaba nzima hadi kumfikia Imam Amiral Muuminii Ali ibn Abi Talib a.s.) ...Vile vile mjue kuwa jina lake litakuwa likiaafikiana na jina la Mtume Mtukufu s.a.w.w. ...Na pia mujue kuwa wakati Imam Mahdi a.s. atakapodhihiri,  Waislamu wote kwa pamoja na wale walio makhususi watafurahi mno...Na sasa kipindi chake kimeshafika na kipindi hicho ndicho kipindi mulichomo. Naye atadhihiri katika karne ya nne ambayo ni kabla ya karne tatu zilizopita (yaani wakati wa suluhu katika kipindi cha Mtume s.a.w.w. ndicho kipindi cha kwanza, kipindi cha pili ni kile kilichofuatiwa cha tabiin na kipindi cha tatu ni kile cha tabaa Tabiin kilipita kipindi fulani baada ya vipindi vitatu hivi na kulizuka matukio mapya mapya mawazo na matamanio ya nafsi yalIssambaa kote na umwagikwaji wa damu ulitokea  naye huyo (al-Mahdi a.s.) alikuwa ghaibu kwa kipindi kirefu hadi ‘utakapotokezea’ wakati maalum wa kudhihiri.

 

12.  Kamaluddin bin Talha Shafi’i

 

Huyu  ni Aalim mmoja wapo miongoni mwa wale waliokuwa mashuhuri katika hali Sunna, na kauli yake inasadikiwa kuwa ni sahihi katika figh, Hadith na usul na katika kila fani, naye ametasnif kitabu kilichopo mashuhuri matalib il-usuul fi manaaqib Ali Rasuul humo katika sura ya kumi na mbili, Allamah huyu kubatilisha shaka za wazushi yaliyokuwa yakifanywa na wale waliokuwa dhidi yake. Tunawaleteeni baadhi ya habari kutoka kitabu chake, zinazozungumzia juu ya Imam Mahdi a.s. kuhusu jina lake,  nasaba yake na kuzaliwa kwake na vile vile ghaibat n.k:

 

 Sura ya kumi na mbili

Katika kuelezea juu ya Abul Qasim Muhammad Hujjat ibn Hassan Khalis (Askary) ibnAli Mutawakkil bin Muhammad (Taqi) Qania bin Ali ar-Ridha a.s. anaandika:

“.....basi alizaliwa (al-Mahdi a.s.) tarehe 23 Ramadhaan 258 Hijryyah katika mji wa Samarrah.  Lakini nasaba yake kwa upande wa Baba na mama yake ni Imam Hasan al-Askari a.s. (nasaba nzima hadi kufikia kwa Imam Ali a.s.)  na habari yake kamili ipo imeelezwa mwanzoni, na mama yake alikuwa mtumwa, aliyeitwa Sakiil na vile vile Hakimah pia aliitwa Muhammad, pia anatambuliwa kwa majina ya Abul Qasim, al-Hujjat, Khalaf Saleh na Muntadhar.”

 

Baadaye zinazungumziwa Hadith za Mtume Mtukufu s.a.w.w. juu ya Imam Mahdi a.s. zinazothibitisha kuwa sifa zote hizo (zilizopo katika Hadith) pamoja na majina yake zinapatikana katika Imam Hujjat a.s. kwa hivyo sasa inatubidi kuamini na kusadiki kuwa ni yeye tu al-Mahdi Maw-ud na kwamba atadhihiri pale patakapokuwa hukumu ya Allah swt Katika mazungumzo haya ameandika kurasa nyingi mno, na baadaye anaendelea kuandika kuwa:

 

Lakini umri wake unapohusika, ni kwamba yeye (al-Mahdi a.s.) alikuwa katika zama za Khalifa Mu’tamid Allah na alikuwa katika hali iliyojaa khofu na hapo ndipo alipokuwa ghaibu... Na kudra ya Allah swt ipo wasili (pana)  na amewajaalia rehema zake waja wake na iwapo mashekhe wakubwa wakubwa watataka kujua na kuelewa sababu za kudura na uhakika wa yale ayatendayo (Allah swt), basi hao mashekhe hawataweza kamwe kufanikiwa na macho yao yatachoka na watarejea wakiwa katka hasara na ndimi zao zitasema na kuchoka kwani Allah swt anatuambia katika Qurani tukufu:Hamkupewa ilimu isipokuwa kidogo. Na si jambo lenye kustaajabisha kuwa Allah swt kurefusha umri wa watu walio makhususi au kuwazidishia umri wao kwa ziada ya kipindi fulani.Je Allah swt hajawazidishia kundi moja umri wao ukawa mrefu.....na miongoni mwa maawliya na ma-asfiya na miongoni mwa waliokhilafuDin? Basi katika Maasfiyallah yupo Mtume Issa a.s. na pia humo yupo Imam al-Mahdi a.s. na katika Ambiya, wapo wengi ambao umri yao ipo mirefu hata kuzidi miaka elfu moja au wengineo wanaokaribia miaka elfu moja mfano Mtume Nuh a.s. na wengineo, na katika maadui wake Allah swt wapo Iblis na Dajjal[15] na vile vile kuna wengineo kama qaum ya Add[16] ambao walikuwapo watu waliokwisha fikisha miaka hata zaidi ya elfu moja, navyo vivyo hivyo yupo Bwana Luqman, na mifano yote hiyo inaletwa mbele yenu kwa kutaka kuwaonyesha kuwa ni uwezo wake Allah swt na ni amri yake kwa kutaka kwake anawazidishia umri mrefu wale awatakiao.Sasa itamwiaje vigumu kumrefushia umri mrefu al-Mahdi a.s. na je kuna ugumu au ukatazo wa aina gani kwa kufanya hivyo? Iwapo ni Allah swt mwenyewe akihitaji kufanya hivyo? Basi hadi yeye (al-Mahdi a.s.)adhihiri, tunaendelea kutekeleza maamrisho yake Allah swt, na kwa kuwa kauli imeshafikia hadi hapa na kalamu imeshafikia mwishoni mwake, basi sisi twamaliza uandishi wa makala haya kwa kalimah ya Alhamdu-lillahi rabbil Aalamiin kwani hiyo ndiyo kalimah tukufu ya waendao katika Jannah kwa kuridhiwa na Allah swt kwani ndiyo dua ya mwisho ya waendao Jannah.

 

MWISHO WA SEHEMU YA PILI

 

Sehemu ya tatu

KADIANI : MADHEHEBU YA MAAHMADIYA[17]

 

Miaka 150 iliyopita katika mji wa Kadyan, katika jimbo la Punjab, India,alizuka Gulam Ahmed Kadiani ambaye alijitangazia Utume na UMahdi. Wafuasi wake hata leo wako Indiana kwingineko. Baada ya kifo cha Gulam Ahmed wafuasi wake waligawanyika katika makundi mawili:MKadiani na Mmirzai. Gulam Ahmed alifanya daawa kubwa ya UMahdi. Vitabu vingi vimeandikwa na wanazuoni wa madhehebu yote, Shia na Sunni, kubatilisha dai lake na majadiliano yalifanywa kudhihirisha ubatili wa nadharia yake na madai yake ambayo yalikuwa kinyume cha dini.Kitabu hiki hakina lengo la kueleza marefu na mapana juu ya jambo hilo,lakini kuthibitisha ukweli wa Uimamu wa Hadhrat Mahdi (A.S.) suala limeguswa tu ili kuthibitisha ubatili wa dai la MaKadiani na maamrisho ya dini juu yake.

 

Gulam Ahmed Gulam Murtaza Atta Mohamed alifariki duniani 1908 akiwa na umri wa miaka 65. Yeye alikuwa Moghul kutoka Samarkand mwenye asili ya Kiajemi. Alifanya daawa nyingi; kwanza alitangaza kuwa yeye ni mwongozi wa dini, baadaye akawa Mahdi na hatimaye kajidai kuwa Mtume. 

 

Kwa kufanya daawa  ya UMtume yeye na wafuasi wake wameondoka katika Imani ya Islam kwa sababu Waislamu wote hukubaliana kwa kauli moja kwamba Mtume Muhammad s.a.w.w. ni Mtume wa mwisho.Katika 1898, Mirza aliwauliza maswali wanazuoni wa Kisunni na kutokana na majibu ya Uimamu wa kughibu na kutokeza kwa Imani Mahdi yalithibitishwa pasipo shaka. Hata hivyo, Mirza bado aliendelea kudai kuwa yeye ni Mahdi,Mtume Issa, Krishna na Mtume.

 

Munshi Mohamed Abdalla katika kitabu chake Shahadate Qur’any amechapisha maswali aliyoulizwa Mirza Gulam Ahmed Kadiani na majibu aliyopokea kutoka wanazuoni wa Kisunni.

 

“Suala: Kutokana na hadithi, wafuasi wa madhehebu ya Sunni huamini kwamba katika siku za mwisho wa dunia atatokeza Mahdi ambaye  atatokana na dhuria ya Fatima (a.s.) binti wa Mtume s.a.w.w. na ambaye atakuwa mrithi wa kweli wa Mtume s.a.w.w. Ikiwa mfuasi yeyote haamini hayo afikiriwe namna gani ? Suala hili lazima lijibiwe na wanazuoni na ulamaa wa dini. Tarehe 29 Desemba 1898, 15 Shaaban 1316 A.H. Mirza Gulam Ahmed”.

 

Jibu: “ Masunni wote hukubaliana katika imani yao kwamba katika siku za mwisho za dunia kutokana na dhuria ya Fatima (a.s.) binti wa Mtume s.a.w.w. atatokeza Mahdi. Yeye ataeneza Islam duniani kote na kuitawala dunia katika mambo yote ya kidini na kiulimwengu. Yeyote asiyeamini hayo atastahiki adhabu  kufuatana na aya ya Quran isemayo:“Na atakayemwasi Mtume ataingizwa Jahannam...”(4:115)Mtu huyo atakuwa amepotea njia, bila shaka amepotea njia kabisa.

 

Imetiwa saini na Abdul Haq Gazanwy (Mwanazuoni wa Kisunni) na baada ya hapo wanazuoni 19 wa Kisunni wakatuma majibu yao na baadhi yao walieleza bayana kwamba mtu asiyekuwa na “Imani hiyo” ataishia motoni.

 

Mwanazuoni wa Kisheria Janab Molvi Seyyid Ali Hainy amethibitishia ukweli wa jibu hilo kwamba mtu asiyekuwa na “Imani hiyo” ni kafiri.

 

Gulam Ahmed mwenyewe alikuwa Sunni na aliamini kwamba Mtume Muhammad s.a.w.w. alikuwa ni Mtume wa mwisho. Kama vile Waislam wote wanavyoamini kwamba Mtume Issa yupo hai mbinguni yeye vile vile aliamini na hata kuandika hivyo katika kitabu chake Barahine Ahmadia  baada ya kujitangazia UMahdi. Hatuna haja ya kuendeleza mada hayo, bali nia ni kueleza maneno machafu aliyotumia dhidi ya Islam, Quran na Imani za Kiislamu na vipi bishara zake alizotoa zikaonekana za uwongo.

 

IMANI ZA MIRZA GULAM AHMED

 

1. Baada ya kutoa ilani kuwa yeye ni Imam Mahdi, Mirza akachapisha kitabu kiitwacho Baharine Ahmadia na katika maelezo katika ukurasa 498 amearidhiwa kwamba: “Aya hii ni kwa ajili ya Mtume Issa ambaye atakuja  mara ya pili duniani”.

 

Zaidi ya hayo mwanae wa mrithi wake Mirza Mahmoud, katika gazeti la Kiurdu Afzal la tarehe 27 Juni 1916 amenakili kwamba:“Zamani ilikuwa itikadi ya Waislamu wote pamoja na viongozi wakuu kwamba Mtume Issa bado yu hai. Hata hivyo baba yangu Mirza Gulam Ahmed alikuwa na itikadi hiyo kwa muda wa miaka 10 hata baada ya (kudai) Mahdi na aliamini hivyo na kusisitiza kwamba Mtume Issa yu hai na yuko mbinguni.”

 

1. Kwa muda wa miaka 1300 Waislamu wote hata Mtume s.a.w.w. mwenyewe pamoja na Maimamu wote na Wanazuoni walikubali itikadi hii ya kwamba Mtume Issa yu hai. Lakini baada ya miaka kumi na kujitangaza kuwa Mahdi Mirza alipokea Wahyi kwamba Mtume Issa amefariki dunia na yeye amekuwa Mtume Issa ( kwa utanasukhi?) Amesema kuwa Mungu amemteremshia Wahyi: Yule Mtume Issa amefariki dunia wala hatarudi tena duniani na kwa hivyo yeye (Mirza) ni Mtume Issa, mwana wa Maria,alijitokeza.” Mirza mwenyewe alikuwa mwanazuoni na alifahamu hadithi vizuri sana. Baada ya kufahamu kote huko akadharau imani iliyokubaliwa kwa makini na Waislamu kwa miaka 1300 hata na yeye mwenyewe kwa muda mrefu na kujitangazia kuwa yeye ni Mtume Issa kinyume cha aya za Quran Tukufu na hadithi, bila kuwa na ushahidi au dalili  ya aina yoyote ya kuthibitisha daawa yake.

 

 2. Mirza aliaridhia katika gazeti la “Badar” katika toleo la 5 March 1908, kuwa: “Ni daawa yetu kwamba sisi ni Rasul au Mtume. Yeyote anayeteuliwa na Mungu lazima awe bora kuliko wengine kutokana na nasaba yake na sifa zake na awe mtu mwenye kutabiri mambo mengi na sisi tunazo sifa hizo.”

 

Katika kitabu cha Shahadate Quran ala kidhbe Krishna Kadiani kilichochapishwa Lahore Pakistan na Islamiyya Steam Press yafuatayo ni maoni yaliyotolewa na Mirza:

 

i) Mirza ameandika katika Izale Awham, ukurasa 689 kuwa:“Baadhi ya bishara zilizotolewa na Mtume Muhammad s.a.w.w. pia yamethibitika kuwa ni uwongo”.

 

ii)Katika  Barahine Ahmadia, Ukurasa 556 ameandika, “Mungu amemweka Hadhrat Muhammad s.a.w.w. chini ya uongozi wangu na kwa hivyo Mungu huniteremshia Wahyi kupitia kwake.”

 

iii)Katika kitabu cha Izala ukurasa 25, aliandika kuwa,“Mwenyezi Mungu ameteremsha Quran lakini kuna baadhi za aya ambazo ni kinyume cha ustaarabu na msikilizaji yeyote anayeweza kufahamu hizo aya atasema kuwa kauli ya aya hizo ni mbaya. Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri katika aya hizo. Maneno machafu yasiyoweza kutumika yamezungumzwa juu ya Walid bin Mugheira.”

 

iv) Katika kitabu cha Anjame Atham:, ukurasa 51,ameandika kuwa: Bibi Maryam (Bikira Maria) na mwane Mtume Issa hawawezi kuwa bora kuliko Kaushalya (mama yake mfalme Ramchandra)”.

 

v) Katika kitabu hicho hicho, ukurasa 80, ameandika kuwa: Waislamu wanaamini kwamba Mtume Issa atarudi duniani lakini Mungu amenijulisha kwamba Mtume Issa amefariki dunia na mimi ndiye Mtume Issa:.

 

vi) Kwenye ukurasa 691, katika Izalae Awhad  amewataja kuwa: “Mimi ni Mtume Issa mwana wa Maria, Wakristo ni Dajjal na gari moshi ni punda wa Dajjal.”

 

vii) Katika gazeti la kila mwezi la Al Hakam, Juzuu la iv, la 17 Juni 1900, amedai kuwa: “Baina yenu mimi ndiye Ali aliye hai na nyinyi mnaamini Ali aliyekufa.

 

viii) Anaendelea kusema katika Aine Kamalati Islam, kurasa 564-65 kuwa: “Nimejipatia maongozi ya Mungu kwamba mimi ni Mungu mwenyewe. Nafsi Mungu imeingia kwangu. Kwa sababu  Nafsi Mungu imeingia mwilini mwangu mimi ndiye niliyeumba dunia na mbingu”.

 

ix) Kuhusu Imam Hussein (A.S.) amesema: “Ninao Hussein kama hao kiasi cha elfu moja mfukoni mwangu”.

 

BISHARA ZA MIRZA KADIANI ZIMETHIBITIKA KUWA NI ZA UWONGO

 

Mirza amechapisha bishara nyingi katika kitabu chake Ilhame Mirza na karibu zote zimethibitika kuwa ni uwongo.

 

1. “ Mimi ninabashiri kwa ukweli kwamba Mungu amenisimulia kwamba nitamwoa binti mkubwa wa Mirza Ahmed Beg. Ubashiri huu ukithibitika idadi maalum ya makafiri watageuka kuwa Waislam na wengi waliopotoka watarudi kwenye njia ya haki”. (Amed Beg  alikuwa mtoto wa mjomba wake Mirza Kadiani).

 

Alituma ushenga kwa Beg amwoe binti yake,na kutishia kwamba ombi lake likikataliwa bidhaa yake itakuwa mbaya kwa ajili ya binti huyo na kama akiolewa na mwanamme mwingine, huyo mwanamme atafariki dunia katika muda wa miaka miwili na nusu na katika muda wa miaka mitatu baba mkwe vile vile atafariki. Zaidi ya hayo maafa makubwa yatakabili jamii ya Ahmed Beg. Hata hivyo Ahmed Bag hakujali vitisho hivyo; alimwoza binti yake kwa mtu mwingine.

 

Mirza alipoona ubashiri wake umekuwa udanganyifu tu akatoa ubashiri mwingine: “Mwenye Enzi Mungu amenijulisha kuwa: Hatimaye mimi nitamwoa Binti na hakuna hata mmoja ataweza kuzuia jambo atakalo Mungu na yeyote atakayekukashifu atadhalilika.”

 

Imetiwa saini na mnyenyekevu Gulam Ahmed, Gordapur, tarehe 10 Julai 1888 A.D.

 

Aliendelea kubashiri mengi juu ya jambo la ndoa na mwishowe katika kitabu chake Shahadatul Quran ukurasa wa 4, alitamka kwamba Ahmed Beg na mkwewe hawatakuwa hai baada ya 21 Agosti 1894. Mirza aliendelea kutoa vitisho dhidi ya huyo binti kwa muda wa miaka 20 eti kutokana na habari alizopewa na Mungu. Hatimaye Mirza  mwenyewe alifariki dunia. Licha ya kumkosa  huyo binti lakini yeye mwenyewe alifariki dunia,na huyo binti, babake na mumewe wote walikuwa hai wakiishi raha mustarehe.

 

2. Katika Ubashiri mwingine katika Jange Mukadas aliandika kwamba “Ikiwa Atham Shakhs hakufa na kuingia motoni katika miezi 15 mimi nipo tayari kupewa adhabu yoyote; mnidhalilishe, mnidharau, mnifunge kamba shingoni mwangu, mpake masizi usoni mwangu na mnilaani kuliko mashetani”. Hata hivyo, muda huo ulipita bila Atham Shakhs kufa.

 

3. Katika Kitabu chake Dafeul Bala  amearidhia kwamba: Kadiani haiwezi kukabiliwa na ugonjwa wa tauni kwa sababu Mtume wa Mungu huishi huko. Baada ya muda mfupi ugonjwa wa tauni ukaenea huko Kadiani na kusababisha vifo vya watu kwa maelfu wakiwemo na wafuasi wa Mirza.

 

4. Tarehe 15 Aprili 1907 Mirza akatoa kitabu ambamo anadai kuwa ikiwa daawa yake itathibitika basi mtu mmoja Mirza Sonullah (wa Amritsar) atakabiliwa na laana ya Mungu na atakufa katika  uhai wake (Mirza) kutokana na tauni au balaa nyingine. Akanadi kwamba Mweye Enzi Mungu atathibitisha ukweli wa daawa yake. Hata hivyo, Mirza mwenyewe akafa 26 April 1908 na wakati huo Molvi Sonullah alikuwa hai na licha  ya kuwa na afya njema lakini hakupata hata kuugua. Bishara nyingi za Mirza zimethibitika kuwa ni udanganyifu tu lakini hatuwezi kuandika yote hapa.

 

MIRZA KADIANI,KAMA MUNGU, MKE WA MUNGU NA MWANA WA MUNGU (MUNGU APISHIE MBALI)

1.“Mungu anatamani kukuona unaingia mwezini, au unanajisika. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu atakujulisha alama zake ambazo zitaendelea kukufikia.Wewe hupati hedhi lakini umezaa mtoto ambaye atakuwa na hedhi ya mwana wa Mungu”.(Hakikatul Wahyi, ukurasa 143, na Arbaeen, uk,12).

 

2.Mmoja wa wafuasi wake mwaminifu, Kadhi Yar Mohamed B.O.L.Pleader, ameandika katika chapisho lake “Islami Kurbani” Juzuu la 24/Riaz Hind Press, Amritsar: “wakati mmoja Masihi anayesubiriwa (Mirza) alisimulia kwamba anapoteremshiwa Wahyi (ufunuo) na Mungu hali yake hugeuka kuwa kama mwanamke na Mungu hutumia nguvu zake za kiume juu yake”. (Audhubillahi).

 

3. “Roho yake ilipulizwa mwilini mwangu kama alivyofanyiwa Mariyam na kwa mfano mimi nimekuwa mja mzito. Baada ya muda usiozidi miezi kumi mimi niligeuzwa kwa njia ya ufunulio, kutoka Maria kuwa Mtume Issa” (Kishtie Nooh ukurasa 47).

 

4. “Eh Mirza umetokana na maji yetu (manii) na wengine ni wa vitu vikavu.” (Arbaeen,toleo 2, ukurasa 390).

5. “Baadaye maumivu yakamkokota Mariyam, yaani miye,kwenye mti wa tende.” (Kishtie Nooh, ukurasa 47).

 

6. “Wakati wa ufunulio mwumbaji  huniita “sikiliza mwanangu” (Hakikatul Wahyi, ukurasa 79, na Arbaeen, uk.22).

 

7. “Niliota ndoto kwamba mimi ni Mungu na nina  hakika kwamba mimi ni Mungu” (Hakikatul Wahyi, ukurasa 64).

 

8. “Mungu ameniambia, “Wewe unatokana na mimi na mimi (Mungu) natokana na wewe”. (Hakikatul Wahyi, ukurasa 74).

 

Kwa hivyo Mirza amekuwa mwanamke Mariyam - baadaye mja mzito - tena mwana wa Mungu - baba wa Mungu na hatimaye Mungu mwenyewe. Ni mtu wa kushangaza mno! Hawezi kueleweka.

 

BABI, AZALI, BAHAI

 

Kama vile huko Punjab,Mirza alifanya daawa ya Utume na UMahdi, huko Iran, kabla ya miaka 100, yalizuka Madhehebu mapya ya Babi,Azali na Bahai. Wafuasi wa madhehebu hayo hadi leo wako Iran na India.

 

Katika kitabu kidogo kama hiki hayamkiniki kueleleza maisha ya Babi Azali na Bahai na ubatilisho wa madai yao. Hata hivyo, tutaeleza kwa muhtasari historia ya madhehebu haya.

 

Mwanzilishi wa Ubabi alikuwa Mirza Ali Mohammed Mirza Raza Shirazi. Vichepuko vya madhehebu ya Babi vikawa madhehebu ya Azali na Bahai yakimhesabu Baab kuwa Mtume na ishara ya habari njema kwa sababu alibashiria juu ya ndugu hao wawili.

 

Katika Mabahai, Baab hujulikana kuwa ni mtu mmoja tu aliyebaki hai kutokana na dhuria ya Mtume s.a.w.w. na Mirza Husseinali ni Mtume Issa wa pili anayesubiriwa.

 

Baada ya kifo ya Mirza Mohammed Baab, wafuasi wake hawakutambua au kumkubali Mirza Yahya Subhe Azal au Mirza Husseinali kama walivyomkubali Baah. Mirza alidai kwamba Baab alitangaza kuja kwake (Mirza Yahya).Mirza Husseinali Bahai mwanzoni alimkubali ndugu yake na kueneza madhehebu yake kwa niaba ya nduguye lakini baadaye akageuka na kutangaza kuwa madhehebu ya nduguye ni udanganyifu na kubatilisha madai yake kuwa ni ya uongo kuanza kueneza madhehebu yake mwenyewe ya Ubahai.

 

Kutoka na mafarakano baina ya ndugu wawili hao, damu nyingi ilimwagika. Wafuasi wa Mirza Yahya wakajitambulisha kuwa Maazali na wa Mirza Husseinali kuwa Mabahai.

 

Siku hizi Wamisionari wa Kibahai wameenea kote katika mabara ya Asia ,Ulaya na Afrika. Vipi mtu anaweza kuwa na daawa ya kuteremshiwa Wahyi wakati yeye mwenyewe amebadilisha dini yake mara tatu ! kwanza alikuwa Shia Ithnaasheri, baadaye akaungana na madhehebu ya Ubabi na baadaye kuwa misionari wa madhehebu ya nduguye Mirza Yahya Azali. Hatimaye  akawa mwanzilishi wa madhehebu yake na kujitangazia kuwa yeye  ni Mahdi anayesubiriwa. Madhehebu yake ni mchapuo wa madhehebu ya Ubabi.

Al-Bayan husemekana ni kitabu alichoteremshiwa mwanzilishi wa madhehebu ya Baab. Maadili kadhaa kutoka kitabu hicho yanaorodheshwa hapa. Itadhihiri kwamba maadili yote ni kinyume cha maagizo ya Quran na Hadith.

 

1. Sala ya jamaa hukatazwa.

 

2. Baada ya raka 17 za kila siku mtu asali rakaa tisa tu na kuna mabadiliko mengi katika hizo sala.

 

3. Kufunga katika mwezi wa Ramadhan kumekatazwa na badala yake mtu afunge siku 19 tu kuanzia tarehe 1 Machi (Asrarul Akaid, uk.830.

 

4. Kuoga tohara baada ya mtu kujamiiana na mwanamke au kutoka manii usingizini sio lazima.

 

5. Mwanamke yeyote, ila mama mzazi, huweza kufungwa naye ndoa.

 

Mwanzoni, mwanzilishi wa madhehebu ya Babi Mirza Mohammedali Baab alikuwa Shia Ithnaasheri. Alikuwa mwanazuoni wa kidini huko Najaf-Iraq. Baadaye alikwenda Iran na akaanza uombezi. Alikuwa akisimama kichwa wazi juani kwa muda mrefu. Mwishowe, akapotelewa  na akili na kujitangazia kila daawa.

 

Katika 1844 A.D. Mirza Ali Muhamad akaanza kutangaza dini yake. Akatangaza yeye ni mlango wa Mungu (huwezi kumfikia Mungu bila kupitia kwake),Mti wa Toor,Mahdi anayesubiriwa na mwishowe Mtume.

 

Katika majadiliano bayana na mwanazuoni wa Shia Ithnaasheri akatangaza “Kauli zangu ni bora na zenye ufasaha kuliko Quran. Madhehebu yangu hubatilisha Islam. Tahadharini mimi nitawaua wapinzani wangu wote”.

 

Aliwaamuru wafuasi wake kuongeza katika Adhana kauli ya kuwa: “Nitatoa ushahidi kwamba Ali Mohammed ni dalili ya Mungu na vile vile natoa shahada kwamba Ali Mohammed ni mlango wa Mungu”

 

Katika washabiki wakuu wa kueneza na kukubali madhehebu ya Babi alikuwa mwanamke mmoja, Kurratul Ayn, ambaye alikuwa binti wa mwanazuoni naye aliolewa na mwanazuoni. Alikuwa mwanamke mjanja, aliyeelimika na msemaji hodari. Jina lake la mwanzo lilikuwa Zarrin Taj na alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri sana. Kutokana na mafarakano na mumewe akaungana na madhehebu ya Babi ili alipize kIssasi dhidi ya mumewe. Kila alipopata fursa alionyesha umbo na uzuri wake kwa kuvua buibui lake hadharani.Siku moja alipanda juu ya mimbar mbele ya watu wengi, akavua buibui na kutangaza:“Marafiki na maadui! Kutokeza kwa madhehebu ya Babi kumebatilisha Islam.Amri zote kuhusu sala,saumu,kutoa sadaka na kadhalika zimetanguliwa. Tahadharini. Hadhrat Baab akaiteka dunia nzima na karibu hakutakuwa na dini yoyote duniani ila Ubabi na kwa hivyo kila mtu anawajibika kuungana nasi kwa wingi kadri iwezekanavyo.”Achilieni mbali buibui ambalo lawatenganisheni na wanawake. Mkumbuke kuwa mwanamke ni ua linalonukia la bustani la dunia hii. Hivyo, lichume na kulistaladhi. Ua huzawadiwa kwa marafiki.Tamaa mbele giza nyuma.Msikose kuwapa marafiki zenu,wake zenu na maana vikwazo kama hivyo vimekwishaondolewa katika madhehebu ya Ubabi. Staladhi raha zote za dunia maana hakuna lolote baada ya kifo.”

 

Mwenye akili hahitaji maelezo zaidi kuhusu imani ya madhehebu hayo.

 

UBAHAI

Ubahai ulianzishwa 1853 B.K. na mwanzilishi wake Husseinali ambaye hujulikana kama Bahaullah, huko Mazinderan Iran baadaya kuacha madhehebu ya Ubabi. Watu wengi waliuawa.

 

Mwishowe kwa amri ya Shah wa Iran, Nasiruddin,Bahaullah akafungwa jela na kufia huko gerezani 1886. Alirithiwa na mwanawe Abbas Effendi ambaye alistakimu katika jiji la Akka huko Palestina.

 

Professa Browne aandika kwamba Ubahai ni muundo mpya wa Ubabi. Kama vile Mababi humtukuza Ali Mohammed (Baab) kuwa mtukufu mno vivyo hivyo Mabahai vile vile humfikiria Mirza Husseinali Bahauddin kuwa mtukufu mno.

 

Mabahai huamini kwamba Ali Mohammed Baab alibashiri tu juu ya kutokeza kikamilifu kwa amri ya Mungu na hilo likafuatwa na kuzaliwa kwa Bahauddin kwa sababu Mirza Hussein Ali alikuwa kiwiliwili cha Mungu. Hata Bahaullah mwenyewe alipokuwa gerezani alitangaza kwamba “hakuna Mungu ila mimi mwenyewe aliyefungwa na kukandamizwa”.Mtu atamfikilia nini huyo Mungu aliyefungwa gerezani na anayekandamizwa ? Madhehebu hayo vipi huweza kuhesabiwa kuwa na uhusiano wowote na Islam ?

 

Kitabu cha kwanza cha Mabahai kilikuwa  Aykan Baada ya kujitangazia kama yeye mwenyewe ndiye Mungu akachapisha kitabu cha pili kiitwacho Aqdas ambacho kinadaiwa kuwa ni bora kuliko vitabu vyote vya dini. Katika humo imearidhiwa: “Mama zenu tu hamwezi kulala nao na ustaarabu tu tunakataza kutoa kanuni kuhusu kumfeli mtoto mwanamume mwenye sura ya kupendeza”. Hivyo, inamaanisha kwamba mtu anaruhusiwa kuingiliana na  kila mwanamke ila mama yake mzazi na vile vile kufeliana na mwanamume mwenzie.

 

Uchochezi wa Babi-Bahai ulIssababisha umwagaji mkubwa wa damu huko Iran. Wanazuoni,Mawaziri na mwishowe Shah wa Iran Nasirrudin Shah waliuawa.Idadi kubwa ya Mababi na Mabahai waliokuwa Iran na Mayahudi wa Hamadan,Kashan na Yazd waliokubali madhehebu hayo, na vile vile Maparisi wa Iran na India . Waislamu wachache mno walikubali madhehebu hayo.

 

Mmisionari Mkuu wa madhehebu ya Bahai,Mirza Hassan Niku, alikuwa mwanzilishi wa Abbas Effendi, mwana wa Bahaullah. Abbas ambaye alitunukiwa jina kuu la “Jibrael” na Mabahai. Jina lake la  Kiislam lilikuwa Abdulhussein Ayni naye alikuwa mfuasi mkuu wa madhehebu hayo. Hao wote pamoja na wamisionari wakuu wa madhehebu hayo wakatubu na kuandika vitabu dhidi ya Ubahai na kufichua mabaya ya madhehebu hayo.

 

Avarah katika kitabu cha Kashful Hiyal amechapisha kibayana picha zinazofichua siri za madhehebu hayo. Kwa sababu tu kuimarisha upinzani dhidi ya Islam huko Iran ndiyo Mayahudi na Maparisi walijiunga na madhehebu hayo.

 

Mdai UMahdi katika karne ya 13 na 14, Mirza Kadiani mwanzoni alikuwa mubalighi wa Kisunni. Pole pole, akaanza kudai UMahdi, UMtume na mwishowe Uungu. Vile vile, Mirza Mohammed Ali Baab wa Ubaabi na Husseinali Bahaullah wa Ubahai mwanzoni walikuwa Mashia-kila mmoja akaanzisha madhehebu mapya na wakadai kuwa ni wawakilishi wa Baab,Mahdi,Mtume na mwishowe Mungu.

 

Babu zake His Highness Agakhan walikuja India kutoka Iran wakiwa Shia Ithnaasheri na kuamini Maimam kumi na wawili, watukufu kumi na wanne na wakifuata sheria za kusali,kufunga Ramadhani na kanuni zote za madhehebu ya Shia. Siku za mwanzoni viongozi wa dini ya Agakhan walijulikana kwa jina la “Peer”. Jamatini watu wakiswali na kufunga Ramadhani.Quran ikisomwa na watu wakiamini Maimam kumi na wawili. Pole pole katika karne hii MaAgakhani ikaanza daawa ya UMahdi, uMtume na hatimaye kiwiliwili cha Mungu. Mwanzoni, wafuasi wa Agakhan wakijulikana kwa jina la Bhagat na Mashia Ithnaasheri Subhanya. Baadaye Wa-Agakhan wakajigeuza kuwa Maismaili na kitambo kidogo wamekuwa wakijitambulisha kama Shia Imami Ismailia.

Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa itikadi ya Shia Ithnaasheri,tangu kuja kwa Islam,Imani katika Quran, Maimam kumi na wawili,kuzaliwa kwa Hadhrat Mahdi(A.S.), kughibu kwake na kutokeza mara ya pili kumethibitishwa kutokana na Quran,Hadith na historia. Dalili madhubuti za uhakika huo na ufununuzi wake umeelezwa kikamilifu katika kitabu hiki.

 

Waliodai UMahdi ulijitokeza mmoja baada ya mwingine,na kueleza nadharia zilizokuwa kinyume na tofauti na maadili ya Islam kama ilivyoelezwa katika Quran na Hadith. Hapana shaka wadai wote hao hawawezi kuwa wakweli kwa sababu ubashiri uliopo ni wa Mahdi mmoja tu.

 

Hadithi maarufu ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. kwamba  watakuwa Maimam kumi na wawili baada yake na mwisho ni Hadhrat Mahdi (A.S.) imenakiliwa na wanazuoni maarufu wa Kisunni katika vitabu vifuatavyo:-

 

1. Kanzul Ammal,                        Juzuu la 6, uk.198

2. Sunan Abi Daud                      uk.558

3. Jama-e-Tirmizi                         uk.269

4. Sahih Muslim, Juzuu la pili, uk. 119

5. Sahihih Bukhari,Kitabul Fitan, Babul Istikhlaf,Juzuu la 29, uk.629

 

Bila shaka Mume Mtukufu s.a.w.w. alitangaza Hadith hiyo kuhusu Maimam kumi na wawili kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo, lazima wawe warithi 12 wa Mtume s.a.w.w. Basi imani yoyote kuamini warithi zaidi ya kumi na wawili wa Mtume s.a.w.w. haiwezi kuwa  na ridhaa ya Allah swt na Mtume s.a.w.w.

 

Ifuatayo ni orodha ya madai ya warithi wa Mtume s.a.w.w. :

 

1. Msururu wa kwanza ni wa Khulafa-ul-Rashiden ambao walikuwa wanne tu na sio kumi na wawili.

 

2. Msururu wa pili wa daawa  ya urithi ni kutoka nasaba ya Bani Umayyah ambao walikuwa kumi na wanne.

 

3. Msururu wa tatu ulikuwa wa Bani Abbasi ambao walikuwa 37 (thelathini na saba).

 

4. Msururu wa nne ulikuwa mchanganyiko wa watu wa Misri na Bani Abbas ambao walikuwa kumi na wanane. Halaku Khan alikomesha ukhalifa wa Bani Abbas huko Baghdad, na mfalme wa Misri alimtawaza mwana wa mfalme wa Bani Abbas kuwa Khalifa na kufanya idadi yao iwe kumi na wanane.

 

5. Msururu wa tano unatokana na Makhalifa wa Kituruki. Khalifa wa kwanza wa Kituruki Salim Sultan aliiteka Misri na kuanzisha  ukhalifa  wa Kituruki. Idadi ya Makhalifa hao ilikuwa thelathini, lakini alipokuja Mustafa kamal Pasha akakomesha ukhalifa huo; kwa hivyo, duniani sasa hayupo Khalifa wa Kusinni.

 

MADAI YA MADHEHEBU  MENGINE

1. Madhehebu ya Bab Azali bna Bahai,ambayo yamejitenga mbali na itikadi ya Islam, hayawezi kufikiriwa kwamba ni madhehebu ya Kiislam.

 

2. Vile vile U-Kadiani hupinga moja kwa moja imani ya Islam na kwa hivyo madhehebu hayo pia siyo ya Kiislam.

 

3. Hata hivyo waumini wa madhehebu ya Dawoodi Bohora ni Waislamu lakini huamini Maimam ishirini na mmoja na vile vile huamini hadi leo kuwa Imam wao wa mwisho, Imam Tayab amejificha hivyo, daawa yao huzidi idadi ya Imam kumi na wawili.

 

4.Waismailia, wafuasi wa Agakhan, huamini imam wao wa kipindi hiki ni wa 49; kwa hivyo idadi yao huzidi idadi iliyotajwa na Mtume s.a.w.w. zaidi ya mara nne.

 

5.Ni Shia Ithnaasheri pekee yao tu ndio wanawaamini Maimamu kumi na wawili, kama ilivyosimuliwa na Hadith ya Mtume s.a.w.w. . Imam wa kwanza ni Hadhrat Ali (A.S.) na wa kumi na mbili Hadhrat Mahdi (A.S.) kama ilivyoridhiwa katika vitabu vitano mashuhuri vya madhehebu ya Kusunni na kutajwa katika vitabu vingi vingine . Jina maalum la kila Imam (A.S.) lilitajwa na mwenyewe Mtume s.a.w.w.. Ukweli huu vile vile umethibitishwa katika vitabu maarufu vya Kisunni, k.m.

 

1. Mawaddatul Qurba uk. 34, kilichoandikwa na Allamah Seyyid Ali Hamdan, kilichochapishwa Bombay Press.

 

2. Arjahul Matalib , uk. 402, Lahore Press.

 

3. “Yanabiul Mawaddah”, uk. 445, kilichoandikwa na Allama Sheikh Suleiman Kanduzi,Sheikh wa Istanbul. Istambul Turkish Press.

 

4. Tarikhul rawzatul Ahbab ,Yanabiul Muwaddah Juzuu 3, uk.27.  Licha ya hivyo,kuna vitabu vingi vimetaja majina  halisi ya Imam Mahdi a.s.

 

5. Babu zake Agakhan wa siku hizo wakiamini Maimamu Kumi na Wawili kama ilivyoelezwa katika vitabu vyao ambavyo tumekwishavitaja.



[1] Katika maneno ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. tumepatiwa ishara tu.Moto na moshi vinaweza kumaanisha mabomu ambayo yanapolipuka hutoa moto na moshi.Moto undani  mwa Aden unaweza kusemwa kuwa moto katika matanki ya kuhifadhia  mafuta  ya petroli  au visima vya  mafuta vya Arabia. Tabaka za  chini ya ardhi za  Arabia yamejaa kwa mafuta.

 

 

[2] Habari hizi tazama Day of Judgement ,Sayyid Saeed Akhtar Rizvi,Bilal Muslim Mission of Tanzani,DSM,chapa ya pili,1978,uk.44.,naye amenakili kutoka Bihar-ul-  Anwar,j.III.

[3]  Kwa msomaji atakayependa kufanya utafiti zaidi juu ya swala hili juu ya  Ubashiri,anaweza kusoma Hotuba ya Imam Ali a.s. Al-Makhzun katika kitabu

   kiitwacho Basharatul-Islam,chapa ya Baghdad.

[4]  Leo duniani tunaona kuwa maendeleo ya sayansi yametudhihirishia kuwa kuna uwezekano wa kufikisha  Sauti na sura duniani kote hasa kwa kupitia satellites. Sasa  jee kuna ugumu gani kwake Allah swt kufanya  kudra zake?

[5]  Hivyo inamaanisha kuwa kutatokea matukio matatu katika mwaka mmoja  i.e. moja baada ya pili. Dunia hii  imekwisha shuhudia matukio mawili kama hayo katika  mwaka mmoja.

[6] Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!

[7]  Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya  mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya  misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.

[8]  Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6.30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza  k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.

Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.

[9] Tunajionea vile  nchi za Kiarabu zinavyopingana na kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya ushawishi wa nchi za Magharibi. Utengano miongoni mwao unatokana na kulaghaiwa na nchi za Magharibi ambavyo ni vyema kwa maslahi yao.

[10] moto huo utatokana na mlipuko wa bomu la kinyuklia au kitu kama hicho inadhaniwa kuwa bomu la Atomiki litatumika kwa mara ya kwanza huko Mashariki).

[11] (hali hii ni ya kawaida huku kwetu siku hizi, Waislamu wa Msikiti mmoja wanasali Sala ya Iddi na Waislamu wa Msikiti mwingine wamo katika saum, hakuna uelewano wala uhakika wa mambo yanavyoendelea).

[12]  Ufafanuzi zaidi juu ya Sahaba  na Ansaar  wa Imam Mahdi a.s.

Inawezekana kwa watu wenye nia khalisi wakajiona kuwa wao hawapo katika orodha ya wale Sahaba (wafuasi) wa Imam Mahdi a.s. hivyo wakavunjika moyo.

Lakini ufafanuzi halisi ni kwamba iwapo sisi hatutakuwapo miongoni mwa orodha ya Sahaba  lakini lazima tutakuwapo miongoni mwa Ansaar. Tofauti iliyopo baina ya makundi mawili hayo ni kwamba: Sahabah  walioorodheshwa ni watu 313 tu na ambao wamekwisha kutaarufishwa na Imam Ali a.s.

 

Ansaar  Hao ni wafuasi mukhlisi wenye adabu njema ambao watakusanyika huko Makkah pamoja na Imam Mahdi a.s. na watashirikiana bega kwa bega pamoja na Imam a.s. dhidi ya maadui wa Islam. Idadi yao haina mwisho kwa sababu kutakuwapo na Ansaar kiasi cha elfu kumi huko Makkah na vile vile kama nilivyokwisha elezea hapo nyuma kuwa Sayyid kutokea Iraq atakuja pamoja na wanajeshi elfu kumi na mbili.Kwa kifupi hakuna idadi maalum kwa sababu sisi tunasoma katika Duaa tulizofundishwa na Maimamu a.s. Katika Duaa hizo zinasema tumwombe Allah swt atujaalie miongoni mwa Wafuasi na Ansaar wa Imam Mahdi a.s. Hivyo wanaoomba ni mamilioni ya watu duniani kote.

 

 

[13] Katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki,tumezungumzia juu ya 'dalili za kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.kwa marefu na undani zaidi.Hivyo hii ni sehemu ya pili ya kitabu hiki juu ya uthibitisho wa kuwapo kwake.

 

Makala haya yametarjumiwa kutoka itmam-i-Hujjat  cha S.S.Akhtar Rizvi katika lugha ya Urdu na yamewahi kuchapishwa katika Sauti ya Bilal no.6  Juzuu XXII Novemba 1988.

 

 

[15]  Katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki,kuna habari kwa marefu na mapana kuhusu huyu Dajjal kwani anazungumziwa katika riwaya nyingi mno katika dalili mojawapo ya kuja kwa Imam Mahdi a.s.

[16] Kuhusu kusoma vIssa katika Quran unaweza kupata vIssa na masimulizi mengi mno katika kitabu nilichokitayarisha katika maudhui haya.

[17]  Makala haya katika sura hii ya tatu yametolewa kutoka Imam Zaman Hadhrat Mahdi  a.s. kilichoandikwa na Mulla Muhammadjaffer Sherif Dewji  na kutarjumiwa na Alhaj Zakirhussein M.S.Lakha, kilichotolewa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, P.O. Box 20033 Dar Es Salaam, Toleo la kwanza 1991.