AL-KASHIF

SWAHILI - JUZUU YA TANO - Vol:5

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya


YALIYOMO

AN - NISAA { Sura ya 4 }

Aya 24-25: Walioolewa.. 3

Ndoa ya Mut'a.6

Aya 26-28: Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia ..12

Aya 29-30: Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili. 15

Aya 31:              Madhambi makubwa .17

Aya 32-33: Na muombeni Mwenyezi Mungu Fadhila zake..21

Kumwomba Mwenyezi Mungu bila ya kufuata njia yake. 22
Aya 34-35: Wanaume ni wasimamizi wa Wanawake..26

 

Aya 36:             Kuwatendea wema wazazi wawili...32

Aya 37-39: Hufanya ubakhili na kuamrisha watu kufanya....35

Rafiki wa Shetani.....37

Aya 40-42: Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzani wa chembe.... 39

Aya 43:              Msikaribie swala mkiwa walevi....42

Mgonjwa na msafiri katika Tayammam..45

Aya 44-47: Hununua upotevu na kuwataka mpotee....50

Israil na nguvu ya shari ....50

Aya 48-50: Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika ...55

Dalili ya umoja na utatu.57

Aya 51-52: Wanaamini Sanamu na Taghut.61

Aya 53-55 Hawa wapi watu hata chembe.63

Aya 56-57: Kubadilisha Ngozi nyingine...66

Aya 58-59: Uaminifu na uadilifu..68Wenye mamlaka ni nani? ....71

Aya 60-63: Wanataka kuhukumiana kwa ubatilifu....79

Aya 64-70: Hatukupeleka Mtume ila Atiiwe.....83

 

Aya 71-73: Chukueni Hadhari.....88

Vita vya Jana na Leo...89

Aya 74-76: Wanaouza uhai wa dunia kwa Akhera....92

Aya 77:              Zuieni mikono yenu na simamisheni Swala.95

Aya 78-79: Popote mtakapokuwa yatawafika mauti ...98

Haiwezekani kuongeza zaidi ya ilivyo.99

Aya 80-82: Hatukukupeleka kuwa mlinzi juu yao..103

Mayahudi na Muujiza wa Qur'an....103

Aya 83:             Siri ya vita na kuvitangaza...105

Aya 84:              Haikalifishwi ila nafsi yako ..107

Aya 85-87: Kuunga Mkono na maamkuzi .....109
Njia mbalimbali za kuthibitisha marejeo (ufufuo) ..110

Aya 88-89: Imekuwaje kuwa makundi mawili katika habari ya  makafiri...113

Upotevu ... 114

 

Aya 91:              Mtawakuta wengine. 119

Hakuna kuuana wala vita katika Uislamu..119

Aya 92-93: Kuua kwa kutokusudia na kukusudia....122

Aya 94: Kuudhihirisha Uislamu kunatosha kuwa ni kuuthibitisha...125 Aya 95-96: Wenye kupigana Jihad na wenye kukaa..127

Ali na Abu Bakar....129

Aya 97-100: Ardhi ya Mwenyezi Mungu.133

Mafakihi na wajibu wa Hijra...135

Baina ya kuhama Mtume (s.a.w.) kutoka mji Mtukufu wa Makka na kuhama Wapelestina kutoka ardhi takatifu..136

Aya 101-103: Swala ya hofu..140

Aya 104:            Msilegee katika .kuwafuata.143

Aya 105-113: Kuwatetea wahaini..147

Aya 114-115: Siri ya kheri na ya usuluhishi..152

Inzi kufia kidondani ..155

Aya 116-122: Tena kukaririka katika Qurani ....158

 

Siasa ya Shetani na Sayansi ....159

Aya 123-124: Anayefanya uovu atalipwa...162

Mwanamume na Mwanamke..163

Aya 125-126: Nani mwenye dini nzuri..163

Aya 127:            Wanakuuliza kuhusu wanawake..167

Aya 128-130: Unashiza wa Mume...170

Aya 131-134: Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.....173

Aya 135-136: Kuweni imara na uadilifu....175

Baina ya dini na watu wa dini.175

Uadilifu...177

Aya 137-139 Hawathibiti kwenye ukafiri wala Imani ..179

Aya 140-141: Msikae nao mpaka waingie katika uzungumzi mwingine..182

Aya 142-143: Wanamhadaa Mwenyezi Mungu na atawalipa kwa kuhadaa kwao..186

Je watu wote hujionyesha...187

Aya 144-147: Msiwafanye makafiri kuwa marafiki .190

Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wa Imam Zainul Abdin..191
 

 


The .HTML version of this book is taken from
www.al-shia.com  and ebooked by
www.ShiaLibrary.com   and www.islamkutuphanesi.com  .
May Allah be pleased with all.

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 665 34 - 9

Kimeandikwa na:

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

Kimetafsiriwa na: Sheikh Hasan Mwalupa

P.O. Box 1017, Dar es Salaam/Tanzania. Email:mwalupa@hotmail.com

Kimehaririwa na: Dr.M.S. Kanju.

S.L.P 1017, Dar es Salaam. Email: drmkanju@yahoo.com Website: www.dartabligh.org

Kupangwa katika kompyuta na: Ukhti Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: September 2004 Nakala:5000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation P.O. Box 1017 Dar es Salaam, Tanzania Simu:+255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: alitrah@daiichicorp.com Website: www.alitrah.org

Kaashif5-2.jpgKaashif5-3.jpgKaashif5-4.jpg

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia waso-maji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaum-bele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kua-mua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi kari-buni Inshaallah).

ii

Kaashif5-5.jpgKaashif5-6.jpg

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inay-oifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalim-bali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

iii

Makosa ya Chapa.

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausame-heki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama" badala ya "Fawqahum yawamal qiyama". Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: " Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoy-akuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vime-jaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): "Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoy-apatia na kunisamehe niliyoyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH

iv

Kaashif5-7.jpg

v

Kaashif5-8.jpgKaashif5-9.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-10.jpg

1

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 24.Nawanawakewenyekuolewa

isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni Sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu. Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, kwamba Muwatafute kwa mali zenu kwa kuoa bila ya kufanya zina. Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyo lazimu. Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kili-chowalazimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye heki-ma.

25.Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waungwana waumini, basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume; na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi; Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kama ada - wawe ni wenye

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-11.jpg

2

2

Kaashif5-12.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa ..küjl'st¥hl'"si""waasherâti""waiâ"'

wenye kujifanyia mahawara.

Watakapoolewa                  kisha

wakafanya uchafu, basi itakuwa adhabu juu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa waung-wana. Hayo ni kwa mwenye kuchelea mashaka katika nyinyi. Na mkisubiri ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehe-mu.

WALIOOLEWA Aya ya 24-25

LUGHA

Neno Muhsanat limetoka katika neno Hisni (ngome) likiwa na maana ya Uislam, uhuru, ndoa, na kujistahi. Aya mbili tulizo nazo zinakusanya maana zote hizi nne, ufafanuzi unafuatia.

MAANA

Na wanawake wenye kuolewa isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.

Haya yanaungana na yale ya wanawake walio haramu katika Aya iliyotangu-lia. Yaani pia mmeharamishiwa wake wenye waume zao.

Yametangulia maelezo katika kifungu cha lugha kwamba neno Muhsanat katika Aya mbili hizi linachukua maana nne: Ndoa, kujistahi, uhuru na Uislam, Makusudio ya Muhsanat hapa ni wanawake walioolewa. Kwa sababu ndoa ni ngome ya mke inayomzuia kufanya yasiyotakikana na ni ngome ya mume,

Kaashif5-13.jpg

3

3

Kaashif5-14.jpgKaashif5-15.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'kwâ"sâbâbü"hİyo"hİyo7'"Hadİth"İnâsemâ: Wwenye"küöâ"âmeWfadWrtheîüthf mbili za dini yake."

Makusudio ya wale iliyowamiliki mikono yenu ni kutokea mwanamke kuwa

ni miliki ya mwanamume mwingine. Kwa maana ya kuwa mwanamke akiole-

wa ni haramu kwa mtu mwengine, ila kama atamilikiwa na Mwislam. Hapo

atakuwa halali yake yule (Mwislamu) aliyemmiliki hata kama ni mke wa mtu

mwengine.

Mwislam anaweza kummiliki mwanamke kwa sababu zifuatazo:

KWANZA: Kuwa mateka wake. Hilo linakuwa kutokana na vita vya kidini baina ya Waislam na washirikina na Waislam wawashinde washirikina. Hapo wake wa washirikina, watoto wao na mali zao, zinakuwa ngawira ya vita. Mwislam akipata mateka wa kike bila ya mumewe, basi mwanamke huyu atatenganishwa naye na awe si mumewe tena, kwa kongamano la madhehebu yote. Wakitekwa wote pamoja (mume na mke) hawatatenganishwa kwa mujibu wa madhehebu ya Hanafi na Hambal ama kwa Shia Imamiya, Shafi na Malik, (wamesema mume na mke hao makafiri) watatenganishwa.

Mwislam akitaka kumwoa mwanamke wa kishirikina aliyemteka, anaweza kufanya hivyo baada ya kuzaa, ikiwa alikuwa na mimba. Au atangoja aingie hedhi moja ikiwa hana mimba. Ikiwa hana mimba wala hatoki hedhi atangoja siku 45 ndipo amwingilie.

Hukumu hizi zilifuatiliwa katika ushindi wa waislam wa kwanza. Wengine wamezitafutia sababu kuwa ati zilikuwa ni kwa sababu ya kuuzuwiya na kuukataza ukafiri, na kuhimiza kukubali uislam. Ama sisi tunasema kuwa hizo ni hukumu za ki-ibada, hatujui hekima yake. Tunachojua ni kuwa zina mifano katika sheria, kuna baadhi ya dini nyengine zimehalalisha kuwaua wanawake na watoto. Lakini Uislam umeamrisha kuwafanyia upole mateka na watumwa wakiwa wa dini yoyote au madhehebu yoyote.

PILI: Mwislam kummiliki mwanamke ni kumnunua akiwa mjakazi. Hilo ni kuwa mtu awe ana mjakazi aliyemwoza mtumwa wake au mtu mwengine. Kisha akamuuzia mwengine; uuzaji huu utabatilisha ndoa ya mjakazi kwa mujibu wa madhehebu ya Shia Imamiya. Itamhalalishia mnunuzi kulala naye baada ya kusafika kwa kuzaa, hedhi au siku 45.

Sayyid Rashid Ridha mwenye Tafsir Al-manar anasema: "Baadhi ya masaha-ba kama Ibn Mas'ud wako kwenye rai hii wanayoitumia Mashia, lau si kwam-

4

4

Kaashif5-16.jpgKaashif5-17.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

ba ustadh Imam 1hakuichagua ingelikuwa kauli ya Shia Imamiya ni yenye nguvu zaidi kuliko madhehebu yote ya Sunni."

Sayyid Rashid anakiri kwamba kauli ya Shia ina nguvu zaidi kuliko madhehebu ya Sunni lakini pamoja na hivo anaikataa, si kwa lolote ila tu kwamba ustadh wake hakulisema. Ajabu ya watu wa mfano wa Sayyid Rashid ambaye ameilaumu Taqlid (kufuata) na wanaofuata, mpaka akawatoa katika dini sio katika elimu tu. Angalia tafsir yake ya Aya 165-167 ya Sura ya pili (Al-Baqara)

Kwa ujumla ni kwamba Uislam umehalalisha kwa Mwislamu kumwoa aliye na mume (aachike) akiwa ni mjakazi aliyemmiliki kwa kumnunua, au mshirikina aliyemteka katika vita vya kuupigania Uislam na kuulingania.

Unaweza kuuliza: Neno Muhsanat (wanawake walioolewa) ni wingi wa wanawake na maana yake yako wazi, sasa kuna faida gani ya Mwenyezi Mungu kusema katika wanawake

Jibu: Kwanza mara nyingi huwa ni kwa kufafanua na kuyatlia mkazo zaidi mfano "... Na kuwaua kwao Mitume pasi na haki ..." (3:181) pamoja na kuwa kuwaua Mitume daima huwa ni pasi na haki.

Pili: Huenda mtu akadhania kuwa makusudio ya Muhsanat ni wanawake waislam tu. Ndipo likaja neno katika wanawake ili kubainisha ujumla; na kwamba ndoa ni ya kuheshimiwa tu, iwe kwa mwanamke wa Kiislam au mwengine.

Ni Sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu.

Ni kutilia mkazo yaliyotangulia kuhusu walioharamishwa. Kwa maana ya kuwa uharamu wa aina zilizotajwa ni sharia inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenye kuikhalifu, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye atakayemhukumu na kumwadhibu.

Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipomaliza kubainisha walio haramu, anataja desturi ya kijumla, ambayo ni kwamba wasiokuwa wa aina zilizotajwa ni halali kuwaoa kwa sharti ya kuwa ndoa ifuate misingi iliyowekwa na sharia; kama kutoa mahari ya kisharia sio ujira wa ukahaba.

.Anamkusudia Sheikh Muhammad Abduh :

5

5

Kaashif5-18.jpgKaashif5-19.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Hiyo ndiyo maana ya kusem

kufanya zina. Neno kuoa linatosha bila ya kutaja zina, lakini limekuja kwa kutilia mkazo na kuonyesha kuwa mwenye mali anaweza kutoa mali yake kati-ka starehe zisizokuwa za haram. Kwa sababu Uislam kama ulivyoharamisha njia za chumo zisizokuwa za kisheria - kama riba, kughushi na kunyang'anya - pia umeharamisha kutoa mali katika mambo ya haram; kama vile zina au kuingilia uhuru wa wengine.

Sunni na Shia wameafikiana kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: Na mme-halalishwa wasiokuwa hao, inafahamisha kujuzu kuchanganya mtu na shangazi yake au mamake mdogo. Kwa sababu inavyojulikana katika njia ya watu wa sharia ni kutaja ya haram tu, kwa vile inawezekana kuyadhibiti. Ama yenye kuhalalishwa hayadhibitiki. Hivyo wanayaashiria kwa kusema: "Yasiyokuwa hayo." Lakini Sunni wamesema kuwa imethibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kwamba yeye amesema: "Haolewi mwanamke pamoja na shangazi yake wala khala (mama mdogo)."

Khawarij wamesema kuwa inajuzu kuwachanganya kwa hali yoyote, akikataa shangazi, mama mdogo au akikubali.

Shia Imamiya wametofautiana, kuna baadhi wanasema kama walivyosema Sunni. Wengi wao wanasema kuwa ikiwa mke wa pili anayetaka kumwoa ni shangazi au khala wa mke wa kwanza, anaweza kumwoa kwa hali yoyote. Lakini akimwoa shangazi au khala kwanza, haijuzu kuoa mpaka kwa idhini ya shangazi au khala. Wamelitolea dalili hilo kwa riwaya za Ahlul-bait (a.s.)

NDOA YA MUT'A

Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyo laz-imu.

Dhamiri ya 'nao' na 'wao' inawarudia wale ambao ni halali kuwaoa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:"... na mmehalalishiwa wasiokuwa hao." Maana - kwa maafikiano ya wafasiri - ni kwamba mwenye kutaka kumwoa mwanake katika wale walio halali kwake, basi ni lazima atoe mahari ambayo ni lazma, sio sadaka wala hisani.

Mjadala umekuwa mkubwa kuhusu Aya hii; Je, makusudio ni ndoa ya daima tu, au ndoa ya muda, au zote pamoja? Na kama makusudio ni Mut'a je Aya imekua mansukh (hukmu imefutwa) pamoja na ndoa yenyewe ya Mut'a?

6

6

Kaashif5-20.jpgKaashif5-21.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Katika vitabui vya Hadith, Fiqh na Tafsir ya Su

wameafikiana kwa kauli moja kwamba Uislam ulileta sharia ya Mut'a ya wanawake, na kwamba Mtume (s.a.w.) aliwaaamrisha sahaba zake hilo; kama inavyoeleza Sahih Bukhar Juz, 7 mlango wa Targhib fin nikah, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa katika jeshi la waislam akawaambia: "Mwenyezi Mungu amewapa idhini ya kufanya Mut'a, basi fanyeni ..."

Riwaya ya pili ya Bukhari inasema: "Mwanamume yeyote aliyeafikiana na mwanamke wanaweza kuishi pamoja siku tatu, wakipenda wanaweza kuzidisha au wakiamua kuachana wataachana."

Katika Sahih Muslim Juz. 2 mlango wa 'Nikahul-mut'a' Uk. 623 chapa ya 1347 A.H. Kuna Hadith iliyopokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillahi Al-ansary ame-sema: "Tulifanya M ut'a wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu; na wakati wa Abu Bakr na Umar." Katika ukurasa huo huo kuna Hadith nyengine kutoka kwa Jabir, amesema:

"... Kisha akatukataza Umar." Kuna Hadith kama hiyo katika Musnad Imam Ahmad bin Hambal. Juz. 3

Arrazi katika kufasiri, 'ambao mmestarehe nao' anasema: "Amesema Imran bin Al-hasin, ambaye ni katika mafakihi wa kisahaba na mbora wao: "Hakika Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya ya Mut'a na wala Aya hiyo haikufutwa hukmu yake na Aya nyingine; na Mtume akatuamrisha kufanya Mut'a wala hakutukataza. Kisha mtu mwengine akasema kwa maoni yake atakavyo. Hapo anakusudia kuwa Umar alikataza.

Riwaya hizi na mfano wake zinapatikana zaidi katika Sahih za Sunni na Tafsir zao na katika vitabu vyao vya Fikihi. Kwa hiyo basi mzozo wa kuwa je, makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ambao mmestarehe nao ..." Ni ndoa ya daima tu, au ndoa ya Mut'a tu, au zote pamoja unakuwa ni mzozo tasa usiokuwa na faida yoyote. Kwa sababu, natija inakuwa ni hiyo hiyo haitofautiani na chochote. Ni sawa tuseme kuwa Aya inaenea katika ndoa ya muda, au inahusika na ndoa ya daima tu. Kwa sababu linaloangaliwa ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ameamrisha ndoa ya Mut'a kwa kuafikiana Waislam wote. Na kwamba kila aliloliamrisha Mtume na Mwenyezi Mungu Mtukufu pia ameliamuru kama alivyosema: "Alichowapa Mtume, kipo-keeni na alichowakataza jiepusheni nacho." (59:7)

Baada ya kuafikiana Sunni na Shia kwamba Uislam umeweka sharia ya Mut'a, wamehitalifiana katika kufutwa sharia hiyo na kuwa haramu baada ya kuwa

7

7

Kaashif5-22.jpgKaashif5-23.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"halali....

Sunni wamesema imeharamishwa baada ya kuhalalishwa, Shia wanasema ilikuwa na itaendelea kuwa halali mpaka siku ya mwisho.

Kimsingi ni kwamba ni juu ya Sunni kuthibitisha kufutwa hukumu hiyo na uharamu wake kutoka kwa Mtume (s.a.w.). Kwa sababu wao wanadai kuon-doka kitu kilichothibiti kwa njia ya mkato na yakini. Ama Shia hawalazimiki kuthibitisha kuwa haikufutwa. Kwa sababu wao wanasema linalothibiti kwa yakini haliondoki ila kwa yakini. Mfano watu wawili wameafikiana kuwa fulani alikuwa hai mwaka uliopita, kisha wakatofautiana kuhusu kufa kwake. Hapo atakayetakiwa kuthibitisha ni yule anayedai kuwa amekufa. Ama yule anayesema bado ni mzima, hatakiwi kufanya chochote. Kwa kuwajibisha hukumu ya kubakisha lilokuwa kama ilivyo mpaka ithibiti kinyume.

Sunni wamekiri kwamba ni juu yao kuthibitisha, na wala sio Shia ndipo waka-toa dalili za kuthibiti kufutwa hukumu hiyo, kwa Hadith za Mtume (s.a.w.), ambazo Shia wamezijadili kwa matini na isnadi na wakathibtisha kwa mantiki sahihi kwamba Hadith hizo zimesingiziwa Mtume (s.a.w.) kwa dalili zifuatazo:

(i) Kwamba Sunni wenyewe wanakubali kuwa zinagongana na kupin-gana. Ibn Rushdi katika kitabu Al-bidaya Juz, 2 Masuala ya ndoa ya Mut'a anasema: "Baadhi ya mapokezi ni kwamba Mtume (s.a.w.) ali-haramisha Mut'a siku ya vita vya Khaybar; nyingine zinasema ni siku ya ushindi wa Makka; na nyingine zikadai ni siku ya vita vya tabuk; nyingine zikasema kuwa iliharamishwa siku ya Hija ya mwisho (Hijjatul-wadaa); nyingine siku ya kulipa Umra, nyingine katika mwaka wa Autas - jina la mahali katika sehemu ya Hijaz palipiganwa vita katika vita vya Mtume (s.a.w.) - kisha anaendelea kusema Ibn Rushdi -imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba yeye amesema: "Mut'a haikuwa ila ni rehema ya Mwenyezi Mungu aliyowarehemu umma wa Muhammad (s.a.w.) lau si kuikataza Umar asingelazimika kuzini ila mwovu."

(ii) Riwaya hizo za kufutwa hukumu si hoja, hata kama zitakuwa hazina migongano. Kwa sababu ni Khabarul-wahid. Na 'kufutwa hukmu' kunathibiti kwa Aya au Khabar Mutawatir tu, na wala sio Khabarul-wahid.*2

*2 Khabarul-mutawatir ni kupokea Hadith kundi lililofikia wingi ambao itakuwa vigumu kuafikiana uongo. Na khabarul-wahid ni ile isiyofikia kiwango cha mutawatir. Hata wapokezi wakiwa ni zaidi ya mmoja.

Kaashif5-24.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

(iij).Yâİİyöküjâ kwehyei Sahih"Musİİm'"kwâmbâ"w¥fsİâm"wâİİİfâny¥"Müt''â'

wakati wa Mtume na wa Abu Bakr. Kwa hivyo haya yanapingana na kuwa ilifutwa wakati wa Mtume. Vyenginevyo basi khalifa wa kwanza atakuwa ni muhalalishaji wa aliloliharamisha (alilolifuta) Mwenyezi Mungu na Mtume.

Ukweli zaidi unaofahamisha kuwa haikufutwa ni kauli ya Umar mwenyewe: "Mut'a mbili zilikuwako wakati wa Mtume na mimi ninazikataza na nitaadhibu kwazo ..." Kila nitakavyotia shaka, lakini siwezi kutia shaka wala sitatia shaka kwamba Umar, lau angelinya-mazia basi wasingelitofautiana hata Waislam wawili katika kujuzu Mut'a na uhalali wake mpaka siku ya kufufuliwa.

Unaweza kusema: Ni ajabu sana kuwa Umar amesema haya. Kwa sababu ni kuharamisha alilolihalalisha Mwenyezi Mungu; na ni kumpinga Mtume wa Mwenyezi Mungu ambaye 'hatamki kwa matamanio.'

Jibu: Ni kweli, ni ajabu ya maajabu kama ulivyosema: "kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake", lakini waislam wameafikiana kwamba Umar ameyasema hayo. Sijaona hata mmoja aliyekanusha. Bali kuna riwaya nyingine zinazosema kuwa Umar alikataza mambo matatu aliyoyaamrisha Mtume sio mawili. Anasema Al-qawshaji - mwanachuoni wa Kisunni - katika sherehe ya Tajrid mwisho wa utafiti wa Uimam: "Umar alipanda mimbar akasema: 'Enyi watu! Mambo matatu yalikuwako katika wakati wa Mtume na mimi ninayakataza na kuyaharamisha na kumwadhibu atakayeyafanya: Mut'a ya wanawake, Mut'a ya Hija na neno Hayya ala khairil amal."

Amepokea Tabari na Razi kwamba Ali amesema: "Lau si Umar kukataza Mut'a asingelizini ila mwovu." Yako mfano wa hayo soma Tafsir ya Thalabi na ya Suyuti.

Swali la pili: Je, haifai - kwa nafasi ya Umar - kuchukua kauli hii, kwamba ni riwaya ya Mtume (s.a.w.) na wala si rai ya Umar dhidi ya Mtume (s.a.w.) ?

Jibu: Ni kweli kabisa kuchukulia hivyo kunafaa sana, lakini kauli ya Umar: "... zilikuwako wakati wa Mtume na mimi ninazikataza ..." inakataa kuchukulia huku, Kwani yeye mwenyewe amenasibisha kuhalalisha kwa Mtume na kuharamisha kwake yeye. Lau kauli yake ingelikuwa ni riwaya na siyo rai, basi angelinasibisha kukataza kwa Mtume. Kwa sababu Mtume ndiye anayefaa zaidi kukataza.

9

9

Kaashif5-25.jpgKaashif5-26.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kwa ufupi haiwezekani kwa haliyoyotekuchanganyakaulimbili: "Kwamba Mtume alikataza Mut'a baada ya kuiamrisha na kauli ya Umar kuwa Mut'a ilikuwa wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mimi ninaikataza." Na ime-thibiti kwamba Umar ameyasema haya. Kwa hiyo ni wazi kwamba Mtume hakukataza Mut'a.

Haya ndiyo baadhi ya majibu ya riwaya za 'Naskh'(kufutwa hukumu) zilizolaz-imishwa kwa Mtume. Mwenye kutaka ufafanuzi na arudie Tafsir Alau-Rrahman ya Sheikh Muhammad jawad Al-balaghi; na Al-bayan Fi Tafsir Al-Qur'an ya Sayyid Khui, Naqdhul washi'a ya Sayyid Muhsin Al-amin na Juzuu ya tatu ya kitab Dalail s-swadiq cha Sheikh Muhammad Hassan Al-mudhaffar.

Kwa hakika ni kwamba hakuna tofauti kati ya ndoa ya daima na ndoa ya muda (Mut'a), kuwa haitimii bila ya mahari na Aqdi (kufunga ndoa); na katika uhara-mu unaoingia kwa ukwe; na katika wajibu wa urithi, kuwaangalia na kuwapa haki nyingine watoto; na katika wajibu wa eda ya mwenye kuolewa.

Katika kitabu chetu Fiqhul Imam Jaafar as-Sadiq (a.s.) tumetaja mambo kumi na tano yaliyo sawa katika ndoa ya daima na ya muda. Na mambo kumi yanayotofautiana.

Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kili-chowalazimu.

Ikipita ndoa kwa mahari maalum yaliyobainishwa wakati wa kufunga ndoa, basi yanakuwa ni haki ya mke; atayatumia kadiri atakavyo. Lakini hiyo haizuwii kuelewana mke na mume kusamehe mahari yote au baadhi hata kuzidisha. Vilevile halizuwii kuelewana juu ya aina ya matumizi ya mke na kiasi chake, au kuacha kabisa. Vile vile kuelewana kuhusu talaka, kurejeana baada ya talaka au baada ya kwisha muda wa Mut'a na mengineyo ambayo hayatoki katika mipaka ya sharia.

Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waung-wana waumini; basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.

Maana ni kuwa asiyepata mali ya kumwezesha kumwoa mungwana, basi aoe mjakazi mumini.

Na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi.

10

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'MâküsudTö"yâ"]manİ'"hâpâ"nİ"dİnİ'.' M¥ânâ"hT'küWa'Wâİtâkİk¥riİ"kwa"mümİn' kuona unyonge kumwoa mjakazi kwa sababu ya rangi yake na kabila yake. Kwa sababu watu wote wanatokana na Adam; na Adam ametokana na mchanga. Kuzidiana mbele ya Mwenyezi Mungu ni kwa takua tu, si kwa fahari na nasaba. Mjakazi anaweza akawa mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko muungwana kwa sababu ya wema wake na takua yake.

Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kama ada

Watu wao wajakazi, ni wale watu wanaowamiliki

Wawe ni wenye kujistahi si waasherati.

Yaani sio wazinifu kwa sura ya wazi, kama kahaba mzururaji.

Wala wenye kujifanyia mahawara

Yaani anayeizini kisiri siri.

Watakapoolewa kisha wakafanya uchafu basi itakuwa adhabu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa waungwana.

Yaani mjakazi akizini, adhabu yake ni nusu ya adhabu ya muungwana. Adhabu hiyo ni ile iliyotajwa na Aya hii: "Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume mpigeni kila mmoja wao mijeledi mia." (24:2)

Hayo ni kwa mwenye kuchelea mashaka katika nyinyi.

Mwenyezi Mungu hataki kuwapa mashaka waja wake wala kuingia katika fitna. Mwenye kuona kuwa ana haja na mke, basi aoe mungwana kama ana uwezo; na kama hana basi aoe mjakazi. Kama ataweza kuvumilia bila ya kuwa na mke na akawa salama na dini yake na afya yake, basi ni bora kuvumilia.

Na mkisubiri ni bora kwenu

Aya yote hii ndefu imeelezea hukumu ya mungwana kumwoa mtumwa, na adhabu ya mtumwa kama akizini. Sisi tumefupisha katika kuifasiri, kwa sababu maelezo ya utumwa na hukumu zao yamekuwa hayana umuhimu baada yakufutwa utumwa.

Ajabu ya maajabu ni kwamba dola ya kwanza kutangulia kuleta mwito wa kufutwa utumwa inawafanyia watu wa rangi nyengine kama wanyama nchini kwake na inazisaidia serikali za kibaguzi kila mahali na kufanya mambo ya kuutisha ulimwengu mzima, na mustakbali wa binadamu. Dalili wazi ya ukweli

11

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

huu, ni kushiriki kwake kuliunda taifala Kiisrail n a kuisadia kuzifanyia uadui nchi za Kiarabu na kuwafukuza wazalendo katika nchi zao ili kuzichukua . Ama kukusanya kwake mamia ya majeshi huko Vietnam na aina ya ukatili wa mauaji na uharibifu uliyoufanya, haina mfano katika historia . Naona kwamba njia pekee ya kuepuka uovu wa dola hii ni kila mtu wa Mashariki na Magharibi akatae lolote lile linalonasibiana au kuwa na athari na dola hiyo.

26.Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na kuwaongoza Mwendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi mwenye hekima.

27.Na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba na wale ambao hufuata matamanio wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa.

28.Mwenyezi Mungu anataka kuwahafifishia. Na mtu ameumbwa hali yakuwa ni dhaifu.

 

Aya 26 - 28: MWENYEZI MUNGU ANATAKA KUWABAINISHIA

MAANA

Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na kuwaongoza mwenendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kubainisha katika Aya zilizotangulia aina ya wanawake walio haramu kuwaoa kwa nasaba, ukwe na kunyonya na vile vile

Kaashif5-27.jpg

12

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

kubainisha walio halali, alien

na kuwabainishia ili mpate faida ya halali yake kutokana na haramu yake, na kwa twaa yake na maasi na mfuate nyayo za waliowatangulia katika kujie-pusha na yaliyoharamishwa na kufuata uongofu na imani. Vile vile aweze kujua mtubiaji hukumu alizoziweka Mwenyezi Mungu, aweze kujikurubisha kwake Mwenyezi Mungu na kuacha aliyoyakataza.

Imesemekana kwamba makusudio ya awatakabalie toba ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka sharia hizo ili awajue wanaotubia yale yaliyopita katika zama za ujahiliya na mwanzo wa Uislam - kuoa wake wa mababa, kuoa pamoja dada wawili na mengineyo ya haramu.

Vyovyote iwavyo ni kwamba mwenye kutubia na asiyetubia hawezi kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata hukumu zake ila baada ya kuzijua na kum'bainikia. Kwa hiyo ubainifu wa hukumu zake Mungu, ni hisani na neema kutoka kwake. Kwa sababu haamrishi isipokuwa lile lenye heri na masilahi; wala hakatazi ila lililo na shari na ufisadi. Na wala si lazima Mwenyezi Mungu atubainishie hekima ya kuamrisha Kwake na kukataza Kwake. Sisi hatukalifi-wi kujua au kufanya utafiti, letu sisi ni kufuata na kutii, tukiwa ni wenye kuami-ni kuwa hukumu zake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwa ajili ya heri yetu ya dunia na akhera.

Na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba. Na wale ambao hufua-ta matamanio wanataka mkengeuko mkengeuko mkubwa.

Wanaofuata matamanio ni wale wanaotoa mwito wa kujivua na mikazo ya dini na tabia njema, na hufuatana na matamanio ya mwili vyovyote yanavyoelekea. Hawa siku zote wapo; hata wakitofautiana wanatofautiana katika mfumo tu, kulingana na hali zao. Katika karne ya ishirini wamejibandika jina la uhuru na maendeleo. Wamepetuka mipaka katika kuamsha tamaa ya maingiliano ya wanawake na wanaume kwa njia ya filamu, vitabu na picha za uchi. Huu ndio mgeuko na kwenda kombo ambako ameashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kauli yake: "mkengeuke mkengeuko mkubwa."

Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekariri toba katika Aya mbili bila ya kuweko kitu kingine, pale aliposema: "Na awatakabalie toba ... na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba..." Je, kuna makusudio gani katika hilo?

Jibu: Toba ya kwanza imekuja kuwa ni sababu ya kubainisha halali na hara-

<ö> 13

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"rriu kwai "wanawake bila ya'kuâWğâlİâ'am7f'yâ'töb¥r'Âmâ"yâ"p]İİ"hl'"küeTe¥eia' amri yake Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwataka watu watubie kwa kuacha mambo ya haramu; mkabala wake ni matakwa ya mfuasi wa matamanio. Kwa mfano unaweza kumwambia mwanao: "Nimekununulia kitabu hiki ili ukisome basi kisome." Umetaja kusoma kwanza kwa kubainisha sababu zinazowa-jibisha kusoma, na ukarudia mara ya pili kwa sababu wewe unamtaka asome na huku ukimwamuru.

Mwenyezi Mungu anataka kuwahafifishia katika kuhalalisha walio halali katika wanawake; bali hata katika mambo mengine vile vile. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi hawatakii yaliyo mazito." (2.185) Wala hakuwawekea uzito katika dini. (22:78) Na kuna Hadith tukufu isemayo: "Nimewajia na dini nyepesi na ya kweli"

Na mtu ameumbwa hali ya kuwa dhaifu katika kukabiliana na mambo yanayosababisha ladha na starehe; hasa starehe ya mwili. Kwa ajili hiyo, ndipo Mwenyezi Mungu akahalalisha kustarehe na wanawake katika mipaka yake tuliyoielezea. Katika ngano la kale inaelezwa kuwa Iblis alimwambia Musa (a.s.): "Mwanamume hakai faragha na mwanamke ila mimi huwa sahibu yake."

Sijamuona yeyote aliyeleta picha ya udhaifu wa binadamu, katika nafsi yake na mwili wake, kuliko Imam Ali (a.s.) aliposema: "Akijiwa na matarajio, tamaa humdhalilisha; Akiingiwa na tamaa, pupa humwangamiza. Akimilikiwa na kukata tamaa, simanzi humuua. Akipatwa na hofu, hadhari humshughulisha. Akipatwa na masaibu, fazaa humfedhehesha na akipatwa na ufukara, mtihani humshughulisha."

Akaendelea kusema tena: "Masikini binadamu! Ajali (yake) imefichwa, ugonjwa (wake) umefunikwa, na amali (yake) imehifadhiwa. Anaumizwa na kunguni, au anauliwa na kikohozi na ananukishwa na jasho."

Kama ambavyo Imam ameleta picha ya udhaifu wa mtu; vile vile ameleta picha ya nguvu na ukuu wa mtu; kwa kusema: "Mtu anashiriki kufika mbingu saba zenye nguvu."

Yaani kipawa chake hakisimami katika mazingira yanayomzunguka tu, bali huvuka hadi mwezini, kwenye Zuhura na kwenye Merikh na sehemu nyengine-zo zilizomo ulimwenguni anazitumia kwa haja yake.

14

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Imam ameonyesha udhaifu wa binadamu ili as

kumhadaa akapetuka mpaka. Na akonyesha nguvu zake ili asisalimu amri kwa unyonge, akaacha kujitahidi na kufanya kazi. Mwenye akili ni yule mwenye kupigania huku akiwa na hadhari ya mambo yaliyofichika na yanayokuja ghafla.

29.Enyi ambao mmeamini!

Msiliane mali zenu baina yenu

kwa batili.

Ila itakapokuwa ni biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msi-jiue. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye rehema kwenu.

Kaashif5-28.jpg

30.Na atakayefanya hilo kwa uadui na dhulma, tutamtia motoni. Na hilo kwa Mwenyezu Mungu ni jepesi

Aya 29-30 MSILIANE MALI ZENU KWA BATILI

 

Enyi ambao mmeamini! Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili.

Jumla kama hii imekwishapita pamoja na tafsiri yake katika Aya ya 188 ya Sura ya Baqara. Tunaunganisha yaliyotangulia na Hadith iliyopokewa kutoka kwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.), kwamba Mwenye deni akiwa anayo mali, akaitu-mia katika haja yake bila ya kulipa deni, basi amekula mali ya batili bali ni juu yake kulipa deni; hata kama atahitajia sadaka." Inajuzu kwake kutumia mahi-taji ya siku moja tu na usiku wake.

15

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa "Ma"itakapokuwa 'n'İ 'b]âsh¥râ"kwâ"kUndhİânâ'b°aîha"yenüi...

Neno baina yenu ni ishara ya kwamba hapana budi kuridhiana pande mbili. Kusamehewa huku kunafahamisha kuwa biashara haishurutiwi kuwa bidhaa mbili za kubadilishana ziwe sawa sawa bila ya kupungua. Kwa sababu hilo linakurubia kuwa ni muhali. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemruhusu mnunuzi au muuzaji kula kinachozidi maadamu pande zote mbili zimekubaliana, lakini kwa sharti ya kutokuwapo kughushiana na kudan-ganyana.

Unaweza kuuliza: Kama mfanya biashara akiitangaza bidhaa yake na akaipamba; je itakuwa ni kughushi na kula mali ya batili?

Jibu: Hapana, lakini bei ikiwa ni kwa masharti ya sifa maalum; kisha ikawa kinyume, basi mnunuzi anayo hiyari ya kuvunja bei na kurudisha bidhaa kwa muuzaji, naye apewe pesa zake.

Wala msijiue yaani baadhi yenu wasiwaue wengine. Hapo pana ufahamisho wa umoja wa ubinadamu. Kuna Hadith tukufu isemayo: "Waumini ni kama nafsi moja."

Imesemekana kuwa maana ya msijiue, ni kuwa msijiingize katika majanga kwa kufanya mliyokatazwa na Mwenyezi Mungu. Maana hayo yako sahihi, lakini yanatofautiana na dhahiri ya Aya.

Na atakayefanya hilo kwa uadui na dhulma, tutamtia motoni.

Hilo ni ishara ya kujiua, kula mali kwa batili, uadui na kuipetuka haki. Inawezekana kutofautisha baina ya uadui na dhulma; kwamba dhuluma inakuwa kwa mtu mwenyewe kujidhulumu na kumdhulumu mwingine. Ama uadui ni kwa kumfanyia mwingine tu.

Kwa vyovyote ni kwamba, mwenye kusahau, kukosea au kulazimishwa, hasi-fiki na dhuluma wala uadui, isipokuwa mwenye kulazimishwa kuua. Kwa mfano: Dhalimu mwenye uwezo akimwambia mtu: 'Muue huyu au nitakuua wewe.' Hapo haijuzu kwa mtu huyo kuua hata kama ana hakika kuwa huyo aliyemwamrisha anaweza kumuua. Kwa sababu haifai mtu kujikinga kwa kumwingiza mwengine kwenye madhara. Kwa hiyo kama mtu huyo akitekeleza agizo la dhalimu na akaua, basi naye atauliwa na kulipiziwa kisasi, na yule dhalimu aliyeamuru mauaji atafungwa maisha.

16

Kaashif5-29.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

31.Mkijiepusha na (madhambi)

makubwa mnayokatazwa, basi tutawafutia makosa yenu (madogo) na tutawatia mahali patukufu.

Aya 31 MADHAMBI MAKUBWA

MAANA

Qur'an Tukufu imegawanya madhambi kwenye mafungu mawili: Makubwa na

madogo. Mgawanyo huu umekuja katika Aya kadhaa. Kama vile Aya hii tuliyo

nayo. Kwa sababu makusudio ya; basi tutawafutia makosa yenu ni yale

makosa madogo; kama walivyoafikiana wafasiri. Na maana yake ni mwenye

kujiepusha na madhambi makubwa hufutiwa madogo.

Aya nyengine zinazoyagawanya madhambi kwenye sehemu mbili ni kama hizi

zifuatazo:

a "Wale ambao wanajiepusha na madhambi makubwa na maovu isipokuwa

makosa madogo." (53:32)

a "Haiachi dogo wala kubwa ila hulihisabu." (18:49) a "Na amewafanya muuchukie ukafiri na ufasiki na uasi." (49:7)

Hapa inabainika kwa yaliyokatazwa ni mambo matatu: Ukafiri ambao ni ukanushaji na upingaji, ufasiki ambao ni kufanya madhambi makubwa na uasi ambao ni kufanya madhambi madogo.

Kwa hiyo inatubainikia kuwa kauli ya mwenye kusema: Dhambi zote ni kubwa wala hakuna ndogo, kwa vile kumwasi Mwenyezi Mungu katika jambo ni kukubwa, hata kama jambo lenyewe ni dogo, ni wazi kuwa kauli hii inakhalifu dhahiri ya Qur'an. Zaidi ya hayo, hata sharia za kutungwa pia zinagawanya makosa kwenye mafungu mawili: Kosa kubwa na dogo. Hata hivyo inawezekana kukanusha madhambi madogo kwa njia fulani tutakayoionyesha.

Kwa namna yoyote iwayo, ni kwamba Kitabu Kitukufu (Qur'an) hakikuweka mpaka wa kupambanua dhambi ndogo na kubwa. Kwa hiyo wametofautiana Mafaqihi katika maana ya dhambi kubwa. Kundi moja limesema kuwa kila lililokuja katika Qur'an kwa kukutanishwa na kiaga cha akhera hilo ni kubwa na

17

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

lisilokuwa hilo n i dogo; kauli bora ni ile ya aliyesema: kubwa hizo zenyewe - kama alivyosema mwenye kukanusha dhambi ndogo -isipokuwa zinagawanyika ndogo na kubwa kwa kulinganishwa na nyengine. Kwa mfano kumwangalia mwanamke wa kando kwa matamanio ni dhambi kubwa hilo lenyewe lakini ni dogo kulinganishwa na kumpiga busu, nako pia ni kudogo kulinganisha na kumwingilia. Au kula kwenye meza iliyo na pombe ni dhambi kubwa, lakini kwa kulinganisha na kunywa pombe yenyewe itakuwa ni dhambi ndogo.

Kwa hakika mtendaji dhambi na vivutio vyake vina athari kubwa katika kuifanya dhambi iwe kubwa au dogo; kama walivyosema Mafaqihi; na uhalifu au kosa la jinai; kama walivyosema wanasheria wapya. Kwa hiyo basi kabla ya kuichukulia dhambi kuwa ni ndogo au kubwa, ni lazima tumwangalie mtendaji kwanza, je amefanya aliyoyafanya kwa kutojua na udhaifu wa matakwa yake; kama vile kughilibiwa na mpotezaji mwenye dhambi; au alifanya kwa haja ya dharura; au ni kwamba yeye ana shauku ya kuwafanyia maovu watu; kama walivyo watu wengi. Zimekuja Hadith mutawatir kutoka kwa Mtume kwamba yeye amesema: "Hakika amali zote huzingatiwa kwa nia tu ..."

Hadith nyengine inasema: "Hakuna dhambi ndogo pamoja na kung'ang'ania, wala hakuna dhambi kubwa pamoja na kutubia."

Kutoka kwa Imam as-Sadiq anasema: "Hakika watu wa motoni watawekwa milele motoni, kwa vile nia zao ni kumwasi Mwenyezi Mungu katika dunia milele, kama wangebaki. Na hakika watu wa peponi watawekwa milele peponi kwa vile nia zao zilikuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu milele. Kwa hiyo ni kutokana na nia ndio wamewekwa milele hawa na wale." Tumefafanua athari ya nia katika kutafsiri Aya ya 144 Al-Imran.

Litakuwa ni jambo zuri tutaje Hadith iliyopokewa kutoka kwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) akielezea aina za madhambi makubwa. Imepokewa kwamba Amru bin Ubaid, alikwenda kwa Imam na kumwuliza kuhusu madhambi makubwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, naye akasema: : "Kubwa ya madhambi makubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika Mwenyazi Mungu hasamehi kwa kushirikish-wa" (4:48).

Na akasema: "Kwa hakika anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia pepo na makazi yake ni motoni. " (5:72)

18

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Dhambi kubwa jengine ni kukata

sababu Mwenyezi Mungu anasema: "Wala hawakati tamaa ya rehema ya

Mwenyezi Mungu ila watu Makafiri." (12:87)

Jingine ni kujiaminisha na hila (adhabu) za Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: "Hawajiaminishi na hila (adhabu) za Mwenyezi Mungu ila watu wenye hasara". (7:99).

Vilevile kuwaudhi wazazi wawili, kwa sababu Mwenyezi Mungu amekufanya kuwaudhi wazazi ni ujeuri na uovu katika kauli yake: "Na kuwatendea wema wazazi wangu wala hakunifanya niwe jeuri muovu." (19:32).

Pia kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu ila kwa haki, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahanam atadumu humo" (4:93).

Miongoni mwa madhambi makubwa ni kuwasingizia wanawake watakatifu kwani Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika wale ambao wanawasingizia wanawake wanaojiheshimu, walioghafilika (na zina), wamelaaniwa katika dunia na akhera; nao watapata adhabu kubwa." (24:23)

Jingine ni kula mali ya yatima; kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika wale wanaokula mali ya yatima kwa dhulma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao na wataingia motoni" (4:10)

Pia kukimbia vita, kwani Mwenyezi Mungu anasema: "Ambao wanakula riba; hawatainuka, ila kama ainukavyo ambaye amezugwa na shetani kwa wazimu." (2:275)

Na uchawi, kwani Mwenyezi Mungu anasema: "Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe ... Na hakika wanajua kwamba aliyenunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera." (2:102)

Pia zina, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: "... Wala hawazini; na atakayeyafanya hayo atapata adhabu. Na ataongezewa adhabu siku ya Kiyama atadumu humo kwa kufedheheka." (25: 68-69)

Vilevile dhambi kubwa ni kiapo cha kuzamisha *3 kwani Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawatakuwa na thamni yoyote akhera (3:77)

*3 Kiapo cha kuzamisha ni kiapo cha uongo ambacho kinamzamisha mtu motoni.

19

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Pia kufanya hiana, kwa sababu Mwenyezi M

kufanya hiyana, atayaleta yale aliyoyafanyia hiyana siku ya Kiyama (3:161)

Na kuzuia kutoa Zaka pia ni dhambi kubwa kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Siku (mali yao) itakapotiwa joto katika moto wa Jahannamu na kwayo vitachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao (waambiwe) haya ndiyo mliyolimbikizia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkiyalimbikiza." (9:35)

Pia kutoa ushahidi wa uongo na kuuficha ushahidi. Kwani Mwenyezi Mungu anasema: ".. Wala msiufiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini ..." (2:283)

Jingine ni kunywa pombe. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amelinganisha na kuabudu masanamu.

Kuacha Swala makusudi au chochote alichofaradhisha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: "Mwenye kuacha Swala makusudi atakuwa ameepukana na dhima ya Mwenyezi Mungu na dhima ya Mtume wake na atakuwa amevunja ahadi."

Na kuvunja udugu, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema:"... Na wanakata aliyoamuru Mwenyezi Mungu yaungwe na wanafanya uharibifu katika nchi; hao ndio watakaopata laana na watapata nyumba mbaya." (13: 25).

Hapo Amr bin Ubaid akatoka na kilio huku akisema: "Ameangamia anayese-ma kwa maoni yake na kubishana nanyi katika fadhila na elimu enyi watu wa nyumba ya Mtume!"

32.Wala msitamani aliyowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko baadhi nyingine. Wanaume wana fungu katika walichokichuma na wanawake wana fungu katika walichokichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Kaashif5-30.jpgKaashif5-31.jpg

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-32.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano '337N¥'Mİâ"wâtü"tüiifiewâwekeâ"wâ"'

kuwarithi yale waliyoacha wazazi wawili na jamaa na wale mliofungamana nao ahadi wapeni sehemu yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.

Aya 32 - 33: NA MUOMBENI MWENYEZI MUNGU FADHILA ZAKE

LUGHA

Neno Mawali ni wingi wa Maula. Neno hili lina maana nyingi; kama vile bwana aliyemwacha huru mtumwa wake; mtumwa aliyeachwa huru; na maana nyingine ni mwenye kurithi. Haya ndiyo maana yaliyokusudiwa katika Aya hii. Na neno Aymanikum ni wingi wa Yamini kwa maana ya kiapo au kwa maana ya mkono kwa sababu watu hupeana mkono wanapofungiana ahadi.

MAANA

Wala msitamani aliyowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko baadhi nyingine.

Dhahiri ya katazo hili inaonyesha kuwa haijuzu kwa mtu kutamani kile ana-chokiona ni kizuri kilicho kwa mwenzake; ni sawa iwe ni kwa husuda,yaani kutaka mwenzake aondokewe na neema hiyo; au hata kwa wivu mzuri, yaani kutaka asiondokewe na neema hiyo na yeye apate kama hivyo.

Lakini dhahiri ya Aya siyo makusudio, kwa sababu wivu mzuri hauna ubaya wala madhara. Ama hasadi ni haramu ikiwa kuna kuhusudiana au kuingilia hekima ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mtume Mtukufu (s.a.w.): "Ukifanya hasadi usiitokeze!" Yaani ukihisi katika nafsi yako kutaka mwenzako aondokewe na neema usiyokuwa nayo basi jizuiwe na usiitoe uipige vita isije ikad-hihirika nje kwa kauli au kitendo. Ukiweza kufanya hivyo, basi wewe huna jukumu lolote mbele za Mwenyezi Mungu, lakini ukishindwa kufanya hivyo basi wewe ni mwenye dhambi.

21

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Hali hii pekee n diyo inayokatazwa katika Aya. Kw

(s.a.w.) ni ubainifu na tafsiri yake. Ikiwa inajuzu kwa mtu kutamani mfano wa yaliyo kwa mwengine bila ya husuda, basi kutamani kheri kutakuwa kunafaa zaidi bila ya kuangalia aliyomfadhili Mwenyezi Mungu mtu mwengine. Mwenyezi Mungu anasema katika kusifu hayo: "Na miongoni mwao wako wasemao: Mola wetu tupe mema duniani na (tupe) mema akhera na utulinde na adhabu ya moto." (2:201)

Wanaume wana fungu katika walichokichuma na wanawake wana fungu katika walichokichuma.

Katika tafsir Majmaul-bayan, imeeleza hivi: Ulikwenda ujumbe wa wanawake kwa Mtume (s.a.w.) ukasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu siye wa wanaume na wanawake? Na wewe si ni Mtume wa wote? Basi kwa nini Mwenyezi Mungu anawataja wao tu, na wala hatutaji sisi? Tunahofia kuwa sisi hatuna maana yoyote na kwamba Mwenyezi Mungu hana haja nasi!" Hapo ikashuka Aya hii.

Maana ya dhahiri ni kuwa kila mtu atapata natija ya amali yake. Kwa hiyo haitakikani mtu kuishughulisha nafsi yake na husuda. Kwa sababu madhara yake yatamrudia mwenyewe duniani na akhera. Imam Ali (a.s.) anasema: "Msihusudiane, kwani husuda inakula imani, kama moto ulavyo kuni."

Amesema tena: "Siha ya mwili ni hasadi kuwa chache ." Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewataja wanawake kwa kukumbusha kuwa mke na mume ni sawa kila mmoja wao katika kupata alichokichuma. Mwenyezi Mungu amesema: "... Mimi sitapoteza amali ya mfanya amali miongoni mwenu akiwa mwanamme au mwanamke ni nyinyi kwa nyinyi." (3:195)

KUMWOMBA MWENYEZI MUNGU BILA YA KUFUATA NJIA YAKE

Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Kwa sababu hazina yake haishi, na neema zake hazihisabiki. Imam Zainul-Abidin katika baadhi ya dua zake anasema: "Ninajua- Ewe Mola wangu - kwamba mengi ninayokuomba ni mepesi kwako; na kwamba chungu ya mambo ninayokutaka unipe si lolote katika ukunjufu wako; na kwamba ukarimu haumdhikishi yeyote kukuomba; na kwamba utoaji wako ni zaidi ya wa yeyote."

Kuna Hadith isemayo: "Mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake na Mwenyezi Mungu hupenda kuombwa."

22

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Uriaweza küüîizâ kuwaamri ya"küömbâ"İnâs¥bâb]shâ"üİâzîmâ"wa'küjfb]wâ'n'â' inajulikana wazi kuwa watu wote au wengi wao wanaomba na kuomba, lakini hawajibiwi maombi yao?

Jibu: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kama alivyoamrisha kuomba dua, pia ameam-risha kujishughulisha na kujitahidi; na akasema: "Na kwamba mtu hatapata ila aliyoyachuma." (53:39)

Maana ya haya ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amedhamini kuitikia dua kwa njia ya kujishughulisha na amali, na wala hakudhamini kila ayawazayo mtu kwa kutaka tu na kuomba. Vipi isiwe hivyo? Lau angelifanya hivyo, ungeli-haribika ulimwengu. Kisha je, Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kuamuru au kuamriwa? Na atafanya nini kama atapokea maombi mawili yanayopin-gana wakati mmoja? Na mwisho utasemaje kwa yule anayeomba na hafuati njia yake?

Kwa hivyo basi amri yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ya kuomba fadhila zake, ni ibara ya pili baada ya amri ya kujitahidi na kufanya amali; na kwamba ni juu ya mtu kuelekea kwenye shughuli zake akimtegemea Mwenyezi Mungu peke yake na kutomwingilia mwengine katika shughuli zake, kutokana na fadhila ali-zopewa na Mwenyezi Mungu. Hakuna mtu yeyote aliye shughulishwa na mambo ya mwengine ila husongwa katika maisha yake, hudangana na kukosa namna katika mambo yake yote.

Kuna wanafunzi wenzangu fulani niliosoma nao huko Najaf, wakiwa werevu na wenye akili sana. Wakamaliza miaka mingi hapo Najaf, lakini pamoja na hayo hawakufaulu, si kwa lolote isipokuwa walishughulishwa na kuangalia mambo ya watu kuliko nafsi zao na masomo yao. Hakukosea aliyesema: "Mwenye kuchunguza mambo ya watu atakufa na kibuhuti." Tumezungumza kwa ufafanuzi kuhusu dua na kuitikiwa kwake katika kufasiri Aya 186 ya sura ya Baqara.

Na kila watu tumewawekea wa kuwarithi yale waliyoacha wazazi wawili na jamaa na wale mliofungamana nao ahadi wapeni sehemu yao.

Mwenyezi Mungu amewataja warithi wa aina tatu: (i) Wazazi wawili wakiwemo mababu na mabibi.

(ii) Jamaa wa karibu wakiwemo watoto, akina kaka na akina dada, ami, shangazi na wajomba na khala.

23

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

(iii).Mfühgâmâhömââiürri; ""kâma"'ViTe""ndbâr"umİİİkr"¥ü""mfühgamanö'

wakudhaminiana. Vile vile mfungamano wa kijumla ambao ni Uislam. Wote hawa wanaingia katika kauli ya Mwenyezi Mungu "Na mlio-fungamana nao ahadi."

Mfungamano wa ndoa ni maarufu. Ama mfungamano wa miliki ni mtu kummi-liki mtumwa, kisha akamwacha huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bila ya kutoa chochote au kuwa ni kafara. Mtumwa huyu huria akifa na akawa hana mrithi basi mrithi wake atakuwa yule aliyemwacha huru. Mfungamano wa kud-haminiana, ni kuafikiana wawili kila mmoja amdhamini mwenzake, au mmoja tu adhamini.

Yakikamilika maafikiano haya kwa masharti yaliyotajwa katika vitabu vya Fiqhi, basi ni juu ya mdhamini kumdhamini mwenzake na pia atamrithi mdhaminiwa ikiwa hana mrithi.

Ama mfungamano wa kiislam makusudio yake ni mafugamano ya kijumla baina ya Mtume na aliyemwamini. Mwislamu akifa na hana mrithi kabisa, basi atarithiwa na Mtume au atakayekuwa katika nafasi yake.

Imepokewa hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amesema: "Mimi ni mrithi wa asiye na mrithi" katika riwaya ya pili anasema: "Mimi ni msimamizi wa asiye na msimamizi." Na katika riwaya ya tatu: "Mimi ni bwana wa huria asiye na mrithi, ninamrithi mali yake na kumwacha huru."

Inatosha kuwa ni dalili ya hayo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Nabii ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao" (33:6)

Katika kitab Wasailu-Shia kuna Hadith kadhaa zisemazo kuwa Ali (a.s.) alikuwa akisema: "Mtu akifa na akaacha mali bila ya mrithi, wapeni mali (hiyo) watu wa mjini kwake." Hii haipingani na kauli ya Mtume. Kwa sababu Mtume aliwahi kuwapa haki yake hii mafukara wa mji wa marehemu.

Yamekwishatangulia maelezo kuhusu mafungu ya baba, mama ndugu mume na mke, katika Aya ya 12 ya sura hii.

24

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano '34\WaWaüme""h1""wâs'İmiamİzİ""wâ" wanawake, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhili baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali zao wana-zozitoa; basi wanawake wema ni wale wenye kutii na kujilinda hata katika siri, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde Na ambao mnaogopa unashiza wao, basi wanasihini na muwahame katika vitanda na wapigeni. Watakapowatii msi-watafutie njia.            Hakika

Mwenyezi Mungu ni mtukufu mkubwa.

4. Sura An-Nisaa

35.Na kama mkihofia ugomvi ulio baina yao, basi wekeni mwamuzi mmoja katika watu wa mume na mwamuzi mmoja katika watu wa mke. Wakitaka suluhu basi Mwenyezi Mungu atawawezesha,               Hakika

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari.

Kaashif5-33.jpg

25

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa .

Aya 34 - 35:WÂNÂÜMENİ'WÂSİMÂMÎZTWÂWÂNÂWÂKE

MAANA

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine.

Mwanamume na mwanamke ni nguzo mbili za maisha. Ni muhali mmoja wao kuwa bila ya mwingine. Maana ya haya ni kuwa kati ya mume na mwanamke kuna aina ya kutofautiana. Lau wangelikuwa sawa katika pande zote, basi wasingelihitajiana na ingelikuwa kuwako na kutakuwako ni sawa. Kwa hivyo basi mwito wa kuwa sawa katika kila kitu unahalifu mantiki ya maisha.

Huenda mtu akasema kuwa mwanamke na watetezi wake wanataka usawa katika haki na majukumu na wala hawataki usawa na mwanamume katika kila kitu; mfano kutunga mimba na kunyonyesha.

Jibu: Tofauti ya viungo inasababisha ulazima wa kutofautiana katika baadhi ya haki na mambo yaliyo wajibu, na hata katika baadhi ya matamanio ya kinaf-si. Kwa hiyo basi anayetaka usawa katika haki zote na majukumu yote, atakuwa ameenda mbali sana, sawa na yule anayetaka utofauti katika yote.

Ilivyo hasa ni kwamba mwanamume na mwanamke wanalingana sawa katika haki nyingi; za muhimu zaidi ni usawa mbele ya Mwenyezi Mungu, kanuni, uhuru wa matumizi ya mali, hiyari ya kuchagua mshirika wa maisha n.k. Na wanatofautiana katika baadhi ya haki.

Katika kufasiri Aya 228 Sura Baqara, tumetaja tofauti 14 baina ya mwanamume na mwanamke katika sharia ya kiislam. Ama Aya hii tuliyonayo inafa-hamisha mambo haya yafuatayo:

1.   Wanaume ni wasimamizi wa wanawake. Makusudio ya wanaume hapa ni kuwahusu waume wa ndoa; na wanawake, ni wake wa ndoa. Makusudio ya usimamizi sio mamlaka yote, kiasi cha kumfanya mume kuwa ni kion-gozi dikteta na mke kuwa ni mwenye kuongozwa asiyekuwa na matakwa au hiyari yoyote, la! Si hivyo, bali makusudio ni kuwa mume ana aina ya usimamizi. Mafakihi wameueleza usimamizi huo, ikiwa ni pamoja na kuifanya talaka iwe mikononi mwa mume, kumtii kitandani na kutotoka nyumbani mke ila kwa idhini ya mumewe. Zaidi ya hayo wako sawa.

2.   Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja sababu mbili za aina hii ya utawala wa

<ö> 26

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

..müme'kwâ'mke!"Âmeâsh]nasâbabü'yâ"kwâhzâ'kwâ

Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine. Na sababu ya pili kwa kusema: Na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa.

Tuanze na sababu ya kwanza: Dhamiri katika baadhi yao inawarudia wanawake na wanaume pamoja; na makusudio ya baadhi ya kwanza ni wanaume na baadhi ya pili ni wanawake.

Unaweza kuuliza kwanini Mwenyezi Mungu hakusema Alayhinna (juu yao wanawake) ambapo ingekuwa wazi zaidi?

Jibu: Lau angelisema hivyo ingelikuwa makusudio ni kufadhilisha wanaume wote juu ya wanawake wote; na hayo siyo makusudio yake. Kwa sababu hili liko mbali na hali ilivyo. Kuna wanawake kadhaa ambao ni bora kuliko wanaume elfu. Kwa hiyo ndio limekuja neno 'baadhi' peke yake kuashiria kwamba ubora ni wa jinsi fulani kwa jinsi nyingine bila ya kuangalia watu wote.

Mwenyezi Mungu ameficha aina ya ubora kwa kusema: Kwa sababu Mwenyezi Mungu amefadhilisha baadhi yao.

Wafasiri na wengineo wamesema kuwa mwanamume ana nguvu zaidi kuliko mwanamke katika mweko wake wa viungo na kiakili; na wakarefusha maneno na dalili katika hilo. Kuna miongoni mwao waliotunga vitabu mahsusi katika maudhui haya.

Tunayoyashuhudia ni kwamba kazi muhimu katika nyanja za elimu, dini, fani falsafa na siasa zote zinashikiliwa na wanaume na wala sio wanawake. Kama itatokea mwanamke, basi itakuwa ni nadra sana; na unadra unatilia mkazo desturi na sio kama unaikanusha.

Zaidi ya hayo tumeshuhudia mwanamke kabla ya chochote, akijishughulisha zaidi na vipodozi na mavazi ambayo yanaunda uke wake na kudhihirisha uchi wake na kujibadilisha kwa namna ambayo anaweza kumvutia mwanamume na kumwamsha hisia zake. Kwa hali hiyo ndio ukaona kuwa majumba ya mitindo ya mavazi ni kwa ajili ya wanawake tu. Wala hakuna tafsir ya kujishghulisha na uke wake; na mwanamume kujishughulisha na kazi muhimu katika nyanja za maisha ila ni kubainisha umbile na nafsi baina ya mwanamke na mwanamume.

Ama sababu ya pili ya ubora wa mwanamume ambao ameubainisha Mwenyezi Mungu kwa kusema: 'Na kwa mali zao walizozitoa', iko wazi kama tulivyoieleza katika sababu ya kwanza. Kwa sababu ambaye anachukua juku-

<ö> 27

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

mu la kuwakimu wengine, ha

lolote; hata kujikimu yeye mwenyewe tu.

Kwa hakika kauli yake hiyo Mwenyezi Mungu: Na kwa mali zao walizozitoa, imetosha kuwa mume asipomkimu mkewe, hawezi kuwa msimamizi wake; au mke anaweza kutaka talaka kupitia kwa kadhi; na ni juu ya kadhi kumwonya mume. Ikiwa mume ataendelea kumnyima matumizi, kwa kushindwa au kwa inadi, basi Kadhi atamwamrisha atoe talaka. Kama akikataa kutoa talaka, Kadhi atatoa talaka, kwa sababu Kadhi ni msimamizi wa anayekataa.

Hivi ndivyo asemavyo Maliki, Shafii na kundi la wanavyuoni wa Kishia akiwe-mo mwenye Urwatul-wathqa na Sayyid Muhsin Hakim. Nasi pia twaunga mkono rai hii. Suala hili tumeliwekea mlango maalum katika kitab Fiqhul-Imam Jafar as-Sadiq kwa kichwa cha habari 'Talaka ya kukosa kukimu.' Humo tume-onyesha dalili na kauli kwa ufafanuzi.

Wanawake wema ni wenye kutii na kujilinda hata katika siri, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde.

Mke mwema ni yule mwenye kuafikiana kinyumba na mumewe, mwenye kujichunga, kulingana na alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Hamwasi mumewe katika mambo aliyohalalishiwa na Mwenyezi Mungu, wala hamtii katika mambo aliyoharamishiwa na Mwenyezi Mungu.

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): "Mwanamke ni yule anayeku-furahisha ukimwangalia; anayekutii ukimwamrisha; na ukiwa mbali naye, hujichunga yeye mwenyewe na mali yako."

Maelezo ya unyumba hayaishi; wala hakuna yeyote anayejua siri iliyoko katika kauli ya asemaye: "Sioi tena hata mkinichinja;" isipokuwa yule aliyeoa tu. Baadhi ya wanawake ni saratani inayoua pole pole, Ikiwa kuna mtu aliye huru mwenye hiyari, basi mtu huyo ni kapera. Ama mwenye mke hana uhuru wala hiyari isipokuwa wachache sana. Baadhi ya dini zinasema kuwa kesho Mwenyezi Mungu hatawaadhibu kwa moto wala hatawapa thawabu kwa pepo, bali yule mwasi atamwoza kikongwe kilichojishia kinachomchukiza umbo na tabia, na ataozwa mtiifu msichana mzuri anayemfurahisha kiumbo na tabia!

Na ambao mnaogopa unashiza wao, basi wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni.

Makusudio ya unashiza ni kuacha kutekeleza haki za unyumba. Unashiza unaweza kuwa kwa mke tu, au mume tu, au wote pamoja.

<ö> 28

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Baada ya Mwen

mwanamke mwasi (nashiza); na akamuhalalishia mume kumwonya mkewe nashiza. Akiendelea amuhame kitandani. Akiwa bado anaendelea ampige kipigo hafifu cha kumtia adabu sio cha kumtesa-kipigo kisichoumiza wala kugeuza rangi ya ngozi;kama ilivyoelezwa katika vitabu vya fiqh.

Ieleweke kwamba; kutoa onyo, kususia kulala naye na kupiga ni ruhusa tu, sio wajibu. Mafakihi wote wameafikiana kuwa kuacha kupiga ni bora; na kwamba anayevumilia maudhi ya mke, wala asimpige ni bora kwa Mungu, kuliko anayempiga; kama walivyoafikiana kuwa kila itakapopatikana njia nyepesi zaidi, basi itumike na kuwa haramu kutumia njia ngumu.

Mtume (s.a.w.) amesema: "Asimpige mmoja wenu mkewe kama anavyompiga ngamia; anampiga mchana kisha analala naye usiku. Mbora wenu ni mbora wenu kwa familia yake, na mimi ni mbora wenu kwa familia"

Jambo la kushangaza ni kwamba Tabari ambaye anasifika kuwa ni Sheikh wa wafasiri, amesema katika kufasiri Aya hii kwamba ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mume, ikiwa mkewe atamuasi amfunge kwa kamba -kama amfungavyo ngamia - katika nyumba anayolala naye. lililomfanya kufasiri hivi ni kwamba Waarabu wanaiita kamba wanyomfungia ngamia 'Hijaria', kwa hivyo maana ya 'Uhjuruhunna' ni wafungeni kwa hiyo 'Hijara' ni kufunga na sio kuwahama.

Jibu zuri sana la tafsir hii, ni kauli ya Zamakhshari; "Na hii ni katika tafsiri nzito kufahamika."

Watakapowatii msiwatafutie njia katika zile njia tatu. Kwa sababu kuonya, kumwacha kitandani, na kipigo ni njia ya kutafuta utiifu. Kwa hiyo lengo lik-itimia hakuna haja ya njia.

Kauli yake hii Mwenyezi Mungu inaonyesha kuwa haifai kwa mume kutafuta sababu za uongo za kumuudhi mke; hata kama mke anamchukia mumewe. Maadam anamtekelezea haki zake za kisharia. Kwa sababu pendo na chuki viko nje ya uwezo wa mtu. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hahisabu wala kuad-hibu isipokuwa kauli inayodhihiri au kitendo kinachodhihiri.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu mkubwa

Arrazi anasema kwamba makusudio ya kauli hii ya Mwenyezi Mungu, kwa

ufupi ni:

Kwanza: Kuwatisha wanaume wasiwadhulumu wanawake.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Piİİ:.MWenyezl"Münğü'hâkâİ]f(shİ'lsîpbkuwâ'hâki"...

Tatu: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakalifishi lisilowezekana. Kwa hiyo ni juu ya mume kutowakalifisha wanawake wasioyaweza.

Nne: Mwasi hakalifishwi akitubia kutokana na uasi wake, basi nashiza aki-tubia, msimwadhibu.

Tano: Mwenyezi Mungu hafichui siri, kwa hiyo nyinyi ndio mnatakikana zaidi msifichue dhahiri ya hali ya mke; wala msitafute yaliyo moyoni mwake.

Arrazi ni katika Ashaira, wasemao kwamba Mwenyezi Mungu anamkalifisha mwanadamu asiloliweza. Naye ni mtetezi wa madhahebu haya kwa nguvu zake zote, ametetea katika sehemu nyingi kwenye tafsiri Al-kabir, hasa pale alipofasiri Aya isemayo: "Haikalifishi Mwenyezi Mungu nafsi yoyote ila uweza wake." (2:286)

Lakini hapa ameyasahau madhehebu yake na kurudia kwenye umbile safi ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia watu, Akasema: (Ninamnukuu) "Hakika Mwenyezi Mungu hawakalifishi msioyaweza. Kwa hiyo msiwakalifishe wanawake wawapende kwa sababu wao hawawezi hilo."

Na kama mkihofia ugomvi ulio baina yao, basi wekeni mwamuzi mmoja katika watu wa mume na mwamuzi mmoja katika watu wa mke.

Aya iliyotangulia imeonyesha uasi wa mke; na Aya hii inaonyesha uasi wa mke na mume kwa kutokutekeleza kila mmoja wao haki ya mwingine.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: 'Mkihofia ugomvi ulio baina yao' anakusudia kuhofia kuendelea ugomvi; na dhamiri katika 'mkihofia' na 'wekeni' inaelekezwa kwa makadhi. Amri ya kuwaweka waamuzi wawili ni ya sunna, siyo ya wajibu, lengo lake ni kupatikana suluhu, na kuhifadhi familia kwa kuhofia watoto wasipotee.

Ni sharti kwa mwamuzi awe na uwezo wa kusuluhisha. Kwa sababu (kuna msemo) 'asiye nacho hatoi.' Pia inafaa kuwa si katika jamaa; kwa sababu udugu si sharti katika uamuzi wala katika uwakili. Umetajwa udugu katika Aya kwa kuwa ni bora tu, sio kwa ulazima. Kwa sababu wao wanajua hali kwa undani zaidi, wenye huruma na wanaoweza kuficha siri.

Kazi ya waamuzi wawili ni kutafuta suluhu. Wakishindwa wampelekee Kadhi wamueleze hali ilivyo na maoni yao kwa masilahi ya pande zote mbili, wala

<ö> 30

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

hawana haki ya kuwatenganisha ila kwa idhini y wa ila kwa matakwa yake.

Wakitaka suluhu basi Mwenyezi Mungu atawawezesha.

Wametofautiana wafasiri katika dhamiri ya 'wakitaka' kuwa inawarudia kina nani?

Imesemekana kuwa dhamiri ya kutaka inawarudia waamuzi wawili, na dhamiri 'kuwawezesha' inawarudia mke na mume; na maana iwe: Waamuzi wakitaka suluhu, basi Mwenyezi Mungu atawawezesha mke na mume. Lakini hayo yako mbali kabisa. Kwa sababu ilivyo ni kuwa wanalotaka waamuzi ni suluhu, vinginevyo wasingekuwa waamuzi.

Pili: Ni kuwa waamuzi wanaweza kutaka suluhu na tawfiki isipatikane ambapo Mwenyezi Mungu anasema: Wakitaka suluhu atawawezesha, kuonyesha ni wajibu kupatikana Tawfiq (kuwezeshwa) mara tu baada ya kutaka suluhu kutoka kwa waamuzi.

Ilivyo hasa ni kwamba dhamiri zote mbili zinawarudia mke na mume. Maana yake ni ikiwa mke na mume wakiwa na nia safi, kwa kukusudia ndoa yao ien-delee na kuilinda familia, basi kazi za waamuzi zitaleta natija; na Mwenyezi Mungu bila shaka atawawezesha mume na mke. Kwani nia ikitengemaa mambo nayo hutengemaa. Na kama nia ya mume na mke ikiwa mbaya basi kazi ya waamuzi nayo haitafaulu, hata kama watakusudia usuluhishi kwa juhu-di zao zote.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja uasi wa mke; kisha uasi wa mume na mke na wala hakutaja wa mume tu. Lakini mafakihi wameliingilia hilo na wakase-ma: "Mume akimwasi mke na akaacha kumtekelezea haki zake atamuonya; akikubali sawa, la si hivyo hawezi kumwacha peke yake kitandani wala kumpi-ga, kama anavyofanyiwa yeye akiasi; hata kama ataona kufanya hivyo kutale-ta manufaa. Kwa sababu kufanya hivyo kunahitaji idhini ya sharia ambayo haiko kwa mke, isipokuwa lake la kufanya ni kwenda kumshtaki kwa Kadhi.

Na ni wajibu wa Kadhi kuthibitisha na kubainisha. Ikimthibitikia uasi wa mume, basi atamkataza, akirudia atamwaziri vile atakavyoona yeye; ikiwa ni kumshutumu au kumpiga au kumfunga gerezani.

Ikiwa ataacha kumtunza mkewe na ana uwezo, inajuzu kwa kadhi kuchukua mali ya mume na amlishe mke; hata ikiwa ni kwa kuuza kitu katika milki yake.

31

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Ikiwa hana kitu basi - kuna rai ya kuwa -

talaka, ikiwa mke atataka talaka. Hayo yametangulia kuelezwa nyuma.

36.Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote, na watendeeni wema wazazi wawili na jamaa wa ukoo na mayatima na maskini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na msafiri na waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia; Hakika Mwenyezi Mungu hapendi mwenye kiburi ajivunaye.

Aya 36 KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI

MAANA

Na mwabuduni Mwenyezi Mungu.

Hakuna kitu cha kumwabudu Mwenyezi Mungu kilicho bora zaidi kuliko kupi-gania na kufa shahid kwa ajili ya haki; uhuru na ubinadamu. Ama kutafuta elimu na kufanya kazi kwa ajili ya maisha, kusaidia mambo ya kheri na kupatanisha watu waliokosana ni bora kuliko Swala zote na Saumu zote; kama iliivyoelezwa katika Hadith.

Wala msimshirikishe na chochote.

Kuukana uungu ni ukafiri; na kumshirikisha Mungu kuko aina mbili; Kumshirikisha katika Uungu; kama vile kuamini kuwa mwenye kuumba na kuruzuku ni zaidi ya mmoja. Miongoni mwa ushirikina huu ni kuitakidi kwam-

Kaashif5-34.jpg

32

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

ba Mwenyezi Mungu ana mawaziri, wasaidizi na washauri.

Aina nyingine ya ushirkina ni katika utiifu; huko ni kuamini kuwa muumba, mwenye kuruzuku ni mmoja hana mshirika wala msaidizi, lakini ukawa unamwasi kwa kumtii kiumbe kwenye jambo ambalo halitamridhisha Mwenyezi Mungu, Vilevile miongoni mwa ushirikina ni kumridhia mtawala dhal-imu, waziri au naibu wake mwenye hiyana, na kadhi mjinga aliye mwovu, na yeyote anayesimamia mambo ya umma ambayo hana ujuzi nayo. Kuna Hadith isemayo 'Mwenye kuwaridhia watu kwa mambo wayafanyayo basi yu pamoja nao.'

Na watendeeni wema wazazi wawili.

Mara nyingi Mwenyezi Mungu hukutanisha wajibu wa kuabudiwa kwake na wa kutendewa wema wazazi wawili, katika Aya kadha; kama vile: "Na Mola wako amehukumu kuwa msimwabudu yeyote isipokuwa yeye tu, na kuwafanyia wema wazazi wawili; kama mmoja wao akifikiliwa na uzee naye, yuko kwako, au wote, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee na useme nao kwa msemo wa heshima." (17:23)

Aya nyingine ni ile isemayo:

"... kwamba unishukuru mimi na wazazi wako wawili; ni kwangu mimi mare-

jeo." (31:14)

Miongoni mwa dua za Imam Zainul-abidin kwa wazazi wake ni: "Ewe Mola wangu! Ni urefu ulioje wa kunishughulikia (wazazi) wangu kunilea! Ni tabu ilioje waliopata kunilinda! Na ni kujinyima kulikoje kwao kwa ajili ya kunitosheleza! Haiwezekani kwangu mimi kuwatekelezea haki zao, wala siwezi kutekeleza wajibu wangu kwao au kuwalipa huduma zao."

Na jamaa wa ukoo.

Hao ni kama ndugu wa kuzaliwa nao, ami n.k.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuwafanyia wema wazazi wawili, hapa ameamrisha kuwafanyia wema ndugu kisha ni mayatima na maskini. Hata kama si jirani kwa sababu yatima hana wa kumsaidia, yaani baba. Na kwamba maskini hawi sawa kijamii ila kwa kusaidiwa. Masikini anayehitajia kusaidi-wa, ni yule dhaifu asiyeweza kuchuma.

Ama kumsaidia mwenye kuweza kufanya kazi lakini akawa ni mvivu, ni kuchochea uduni uzembe. Kuna Hadith isemayo: "Hakika Mwenyezi Mungu

33

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"humperidârrijâ"'âWâyefâhyâ""kaz]""na"hümchukİâ'"mvlvü"v' Wahaifuhzi wal-' imwuliza Nabii Isa: "Ni nani mbora zaidi katika sisi" Akasema : "Mbora wenu zaidi ni yule anayefanya kazi kwa mkono wake na kula kwa chumo lake."

Na jirani wa karibu na jirani wa mbali na rafiki wa ubavuni na msafiri na waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia.

Rafiki wa ubavuni ni yule mwenzako safarini, unayekaa naye mjini, unayeso-ma naye darasani au unayefanya kazi naye n.k. Msafiri hapa ni yule aliye-haribikiwa safarini.Waliomilikwa na mikono ni watu ambao hawako hivi sasa(watumwa).

Kufanya wema sio lazima kutoa mali tu, bali ni pamoja na kufanyiana upole, unyenyekevu, kujishughulisha kutimiza mahitaji yao kushauriana na kuficha siri. Pia ni pamoja na kuzifumbia jicho aibu za watu, kutotangaza ubaya wa watu, kuazimana vifaa na mengineyo mfano wa hayo.

Kwa vyovyote ni kuwa amri ya kuwafanyia wema wote hawa ni Sunna si wajibu.

Hakika Mwenyezi Mungu hapendi mwenye kiburi ajivunaye.

Hili ni kemeo kwa mwenye kujitenga na jamaa zake walio mafukara na jirani zake.

37.Ambao hufanya ubakhili na huwaamuru watu kufanya ubakhili, na wakayaficha aliy-owapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake. Na tumewaandalia Makafiri adhabu yenye kudhalil-isha.

Kaashif5-35.jpg

34

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

38.Na wale ambao wanatoa mali

zao kwa kuonyesha watu wala hawamwamini            Mwenyezi

Mungu wala siku ya mwisho. Na ambaye shetani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-36.jpg

39.Na ingeliwadhuru nini lau wao wangelimwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakatoa katika aliyowaruzuku, na Mwenyezi Mungu anawajua.

Aya 37 -39 HUFANYA UBAKHILI NA KUAMRISHA WATU KUUFANYA

MAANA

Ambao hufanya ubakhili na huwaamuru watu kufanya ubakhili.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuamrisha kutoa na kufanya hisani katika Aya iliyotangulia, katika Aya hii anamkemea yule anayefanya ubakhili na akaamrisha wengine wafanye ubakhili. Kila bakhili huwaamrisha watu kufanya ubakhili; bali kila mwovu hupendelea kupata wafuasi, ili asiwe peke yake katika uovu na asisemwe vibaya. Kimsingi ni kwamba mwizi hukiboresha kitendo cha wizi na kukifanya halali, bali hata huongeza kukifanya.

Sijaona kitu kinachokubaliwa haraka na nafsi kama amri ya ubakhili na kuzuia kutoa. Kwa sababu mali ni tamu sana rohoni, wala si rahisi - mara nyingi -kutoa hata kidogo, isipokuwa kwa juhudi kubwa. Kwa hiyo amri ya kuzuwia inaungana na matamanio ya nafsi na kuitikiwa kwa haraka na ni nyepesi.

35

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Sheikh Muhammad Abduh katika ku

ubakhili wana nguvu ya kutia shaka, hata waliwahi kuniathiri; nikawa ninarud-isha pesa mfukoni baada ya kuzitoa. Kwa sababu wasiopenda kutoa walikuwa wakiniambia: Huyu hastahili kupewa na kumpa kitu ni kupoteza; kama utatoa mali mahali pengine itakuwa bora zaidi."

Ukweli ni tulioueleza kwamba amri ya ubakhili inamwathiri mtu anapoitikia matamanio ya nafsi yake, si kwa kauli ya wabakhili na shaka shaka zao. Kwani mtukufu ni yule anayeyashinda matamanio na nafsi yake na kuyalaz-imisha kukubali mambo mazito yakiwa na kheri na utengeneo. Imam Ali (a.s.) anasema: "Amali bora ni ile unayoilazimisha nafsi yako juu yake."

Hadith inasema: "Amali bora ni ile iliyo nzito zaidi."

Na wakaficha aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Yake.

Fadhila za Mwenyezi Mungu zinakusanya kila neema, ikiwemo mali na ilimu. Kuficha ilimu ni haramu na kuieneza ni wajibu, lakini kwa mfumo wa kuvutia sio wa kuchukiza na unaokurubisha sio kuweka mbali. Kwa sababu ilimu ni nyenzo na kuitumia ni lengo.

Baadhi ya maulama wamesema: "Tajiri akificha utajiri wake na akajifanya ni fukara mbele za watu basi atakuwa amefanya haramu." Wametoa dalili kwa Aya isemayo: "Na neema ya Mola wako izungumze." (93:11)

Kuna Hadith isemayo: "Mwenyezi Mungu akimneemesha mja neema yoyote hupendelea ionekane athari ya neema yake."

Na tumewaandalia makafiri adhabu yenye kudhalilisha.

Mfumo wa Aya unafahamisha kuwa makusudio ya Makafiri hapa ni wale ambao wameficha fadhila za Mwenyezi Mungu na neema yake. Imepokewa kutoka kwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) Kwamba yeye amesema: "kuz-izungumza neema za Mwenyezi Mungu ni kushukuru na kuacha kuz-izungumza ni kufuru." Mwenyezi Mungu anasema:

"Kama mkishukuru nitawazidishia, na kama mkikufuru basi adhabu yangu ni kali sana." (14:7)

Kwa hivyo basi kufuru katika Aya hii inachukuliwa kuwa ni kukufuru neema, sio kumkufuru Mwenyezi Mungu.

Na wale ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu wala hawaamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho.

<ö> 36

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                    4. Sura An-Nisaa

Imetangulia Aya kama hii na tafsiri ya

ufupi ni kuwa ambaye anatoa mali yake kwa ria (kujionyesha) na yule anayefanya ubakhili ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na huenda mwenye kujionyesha akawa na hali mbaya zaidi. Kwa sababu yeye ni kama kafiri ambaye hafanyi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

RAFIKI WA SHETANI

Kila kinachoshawishi kitendo cha uovu, kuhadaa kufanya ufisadi na upotevu, unaweza kukiita shetani; iwe ni mawazo, mtu au kitu chochote. Neno shetani ni nembo ya kila mpotevu aliye mpotezaji. Anaficha hakika yake chini ya nguo za watu wema. Kwa ajili hii ndipo tukawaona watu wengi wanasema na kuten-da kutokana na mwongozo wa kishetani na upotevu na wao wenyewe wanahisabu kuwa ni mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Aliye karibu zaidi na shetani ni yule ambaye watu humwamini kwa utakatifu wake, na hawajui hakika yake. Hayo ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Na ambaye shetani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya na kauli yake: "Na mwenye kufanya shetani ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi amepata hasara iliyo wazi." (4:119).

Kama ilivyokuwa shetani ni rafiki yake duniani, basi akhera pia ni rafiki yake vile vile. Kuna Hadith isemayo: 'Mtu yuko pamoja na anayempenda,'

Shetani anawagawanya wafuasi wake kwenye mafungu na kuwapa majukumu yao; kama afanyavyo kamanda wa jeshi. Wengine wanapoteza watu kwa kumwaga damu na kuyaingilia mataifa yenye amani; kama vile mataifa yaliy-otengeneza Israel na kuipa mali na silaha kwa ajili ya kuwachokoza Waarabu na miji ya Kiarabu, si kwa lolote ila wawatawale kisiasa na kiuchumi.

Wengine kazi yao ni kuhadaa kwa ufasiki na uovu na kuvunja heshima.

Wengine wanawaamrisha kuswali, kujivika nguo ya watu wema na wasiotaka mambo ya dunia, ili waweze kuwapata watu wema.

Ikiwa wameshindwa na wanaomcha Mungu na wakachoka na hila zao, basi huwa radhi kuwahadaa japokuwa kwa tamko la haki atakalolisema mtu kwa matakwa ya Iblis. Kuna riwaya kwamba Iblis alimwambia Isa bin Maryam (a.s.): "Sema: Lailaha illa Ilah," Isa akamwambia nitasema lakini si kwa matakwa yako, bali kwa kuwa ni neno la haki. Basi mlaanifu (Iblis) akawa dhalili. Hekaya hii inaonyesha kuwa imani haiwi kwa tahalili na takbira, wala kwa kufunga na Swala. Kwani yote hayo yanaweza kuwa ni mitego ya shetani

<ö> 37

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

hâ vitimbi vyake. Isipokuwa imani ya kweli hupimwa kwa namna ya kumjua Mwenyezi Mungu na hekima zake; na kujua milango ya shetani ambayo ina-haribu ikhlasi ya muumin na amali yake.

Na ingeliwadhuru nini lau kama wao wangelimwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakatoa katika aliyowaruzuku Mungu.

Mwenyezi Mungu ameunganisha baina ya kumwaini Yeye, kuamini Siku ya Mwisho na kutoa, kwa sababu bakhili anayeng'ang'nia amemtoa katika imani. Maana yake nikuwa kutoa ni dalili ya imani na ubakhili ni dalili ya ukafiri. Hilo ni kwa sababu muumini anayemtegemea Mungu kikweli kweli hutoa akiwa anaamini badali atakayopata. Na mwenye kuyakinisha badali hutoa bila ya pingamizi; kama alivyosema Imam Ali (as). Ama mwenye imani dhaifu hum-sikiliza shetani wake anayemwamrisha kuzuia na kumhofisha na ufukara kama akitoa.

Hata hivyo makusudio ya imani hapa ni imani ya utiifu na matendo sio imani ya itikadi; na ukafiri ni ukafiri wa utiifu na matendo sio wa kumkanusha Mwenyezi Mungu.

Miongoni mwa kauli za Imam Ali kuhusu ubakhili ni: "Namsatajabia bakhili anayeharakia ufukara alioukimbia na kuacha umpite utajiri alioutaka. Anaishi duniani maisha ya kifukara na akhera anahisabiwa ni tajiri." Maana ya kuwa tajiri anakimbilia ufukara ni kuwa yeye ana hali mbaya kuliko fukara. Kwa sababu tajiri huwa anahofia utajiri wake utamwondokea, lakini fukara huwa na matarajio ya kuondoka ufukara wake.

40.Hakika Mwenyezi Mungu had-hulumu (hata) uzani wa chem-be. Na liwapo (jambo) ni jema huzidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa.

Kaashif5-37.jpg

38

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 41.Basiitakuwajetutakapowaletea kila umma shahidi na tukakule-ta kuwa shahidi juu ya hawa.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-38.jpg

42.Siku hiyo watatamani walioku-furu na kumwasi Mtume ya kuwa ardhi isawazishwe juu yao, wala hawatamficha Mwenyezi           Mungu           na

mazungumzo (yao).

Aya 40 - 42 MWENYEZI MUNGU HADHULUMU HATA UZANI WA CHEMBE

LUGHA

Uzani ni uzito hata ukiwa mchache, na chembe ni zile zinazopatikana kwenye miili; na hapa zimekuja kufananisha uchache. Kwenye Aya nyingine uchache umefananishwa na hardali.

MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu (hata) uzani wa chembe.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha aabudiwe, kuwafanyia wema wazazi wawili na jamaa, kushutumu ubakhili na kutoa kwa ria na mwenye kuficha fad-hila za Mwenyezi Mungu na kuwapa kiaga marafiki wa shetani, baada ya hayo anabainisha tena kwa kutilia mkazo kwamba yeye hampunguzii yeyote katika malipo yake hata chembe, hata kama ni uzani wa chembe ya vumbi; bali huzidisha thawabu za wenye kufanya wema, akasema:

Na liwapo ni jema hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa.

Kusema 'kutoka kwake' ni ishara kwamba yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, humpa mwenye kufanya wema kwa wema wake kisha humzidishia bahashishi.

39

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Vİ/âriâfâİsâfa"waria kâüîikatikâ'hİîi"küwâ\"je7MweWyez]"Munğü"hümpaihiawabü' mtiifu kwa kuwa ni lazima anastahiki, kiasi ambacho kama hatampa, basi Mwenyezi Mungu atakuwa dhalimu - Mungu ametaka na hilo- au ni kwa njia ya fadhila na hisani tu?

Tuonavyo lililo karibu zaidi ni kuwa Mwenyezi Mungu hutoa thawabu kwenye wajibu kwa njia ya fadhila tu. Kwa sababu hakuna malipo wala shukrani kwenye tendo la wajibu. Ama mambo ya Sunna hutoa thawabu kwa kustahi-ki. Lakini kwa vyovyote ilivyo ni kuwa thawabu ziko hakuna shaka. Kwa hiyo mzozo wa kuwa sababu yake ni hisani au kustahiki ni mzozo tasa, maadamu sababu iko nje ya uwezo.

Basi itakuwaje tutakapowaletea kila umma shahidi na tukakuleta kuwa shahidi juu ya hawa?

Kesho Mwenyezi Mungu atawakusanya watu kwa ajili ya hisabu na adhabu. Kabla ya chochote ataushuhudiza kila umma na Mtume wao, kwamba ame-wafikishia ujumbe wa Mola wake na akawafundisha halali na haramu moja kwa moja; au kupitia sahaba zake, au wafuasi wao au wanavyuoni na mafak-ihi.

Kwa hiyo makusudio ya shahidi wa kwanza ni kila Mtume aliyemtangulia Muhammad na shahidi wa pili ni Muhammad (s.a.w.): Na neno 'hawa' ni umma wa Muhammad.

Umbali zaidi ni ule wa mwenye kusema kwamba neno 'hawa' ni Mitume wote waliotangulia na kwamba Muhammad atatoa ushahidi juu yao na wao watatoa ushahidi juu ya umma wao. Ameweka mbali msemaji huyu, kwa sababu ushahidi unajuzu kutolewa na kusikizwa juu ya ambaye anaweza kupuuza wajibu wake.

Tulipofasiri sura ya Baqara (2:143) tumetaja kwamba Muhammad (s.a.w.) ana-toa ushuhuda kwa maulama wa umma wake kwamba yeye amewafikishia Uislam na hukumu zake na ulama wa umma washuhudie kwamba wao wame-fikisha risala ya Uislam kwa njia yake.

Sheikh Muhammad Abduh, katika kufasiri Aya hii, amesema kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kesho atalinganisha baina ya itikadi ya kila umma, amali yake na hulka zake, na itikadi ya Mtume wake. Ikiwa ndiyo hiyo hiyo, basi umma utakuwa umeokoka, vinginevyo utakuwu umeangamia.

40

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Tâfsirİ hii hi miöriğöhi m^

haiko mbali sana na hali halisi. Kwani ulinganisho huu kama hautatokea mbele ya Muumba Mtukufu, lakini natija yake itapatikana tu.

Siku hiyo watatamani waliokufuru na kumwasi Mtume ya kuwa ardhi isawazishwe juu yao.

Yaani Makafiri watapofunuliwa pazia siku ya Kiyama, watatamani lau kwamba wao wasingeliumbwa, bora wangekuwa sawa na mchanga; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Siku ambayo mtu ataona kilichotangulizwa na mikono yake, na Kafiri atase-ma: Laiti ningelikuwa mchanga." (78:40)

Wala hawatamficha Mwenyezi Mungu na mazungumzo (yao).

Haya ni maneno yanayoanza upya, na maana yake ni kuwa wao hawataweza kuficha dhambi yoyote miongoni mwa dhambi zao walizozifanya na kufichika katika macho ya watu hapa duniani. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewazunguuka na amali zao. Na kwamba Malaika, masikio yao, macho yao, ndimi zao, ngozi zao, mikono yao na miguu yao, vyote vitashuhudia yale waliy-oyafanya: "Hata watakapoufikia (moto) yatashuhudia masikio yao na macho yao na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda." (41:20). " Siku ambayo zitashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyokuwa wakiyatenda." (24:24).

Ewe Mwenyezi Mungu mhurumie kwa uadilifu wako ambaye hana uwezo. Na mwokoe ambaye hana uokovu zaidi ya msamaha wako.

Unaweza kuuliza: Utaunganishaje baina ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala hawatamficha Mwenyezi Mungu na neno lolote" na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na siku ambayo tutawakusanya wote pamoja kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mliokuwa mnadai. Kisha hautakuwa udhuru wao isipokuwa kusema: Wallahi Mola wetu hatukuwa washirikina." (6: 22-23)

Jibu: Inawezekana kuwa makusudio yao ni kwamba wao katika itikadi yao hawakuwa washirikina. Tukutane wakati wa kufasiri Sura hiyo ya sita (An'am) inshaallah.

41

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 43.Enyi mlioamini, msikaribie

Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema; wala mkiwa na janaba - ispokuwa wapita njia - mpaka muoge. Na muwapo wagonjwa au mko safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe mwenye kughufiria.

Aya ya 43 MSIKARIBIE SWALA MKIWA WALEVI

MAANA

Enyi mlioamini, msikaribie Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema; wala mkiwa na janaba - ispkuwa wapita njia - mpaka muoge.

Hapa kuna masuala kadhaa

1. Msemo huu unaelekezwa kwa Waislamu kabla ya kubainishwa hukumu ya kuharimishwa pombe kulikoelezwa katika Sura ya Maida (5: 90 - 91) na katika A'raf (7:32). Zikiungana na Baqara (2:219) ambayo tumeyaelezea hayo kwa ufafanuzi kabisa. Pia tumeeleza hayo katika kitab Fiqhul-Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) mlango wa vyakula na vinywaji.

Kaashif5-39.jpg

42

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

...livyo hasa ni kwamba kukatazwa mtu kuswali hali ya

ufahamishi kwamba ni halali katika isiyokuwa Swala; kwa mfano ukisema: Usiwaangalie wanawake ukiwa unakwenda njiani hakufahamishi kuwa inafaa kuwaangalia ukiwa ukumbini.

Kwa maneno mengine ni kuwa Aya imefahamisha uharamu wa Swala katika hali ya kulewa, na kunyamzia hukumu ya kulewa mahali pengine.

2.   Wametofautiana (wafasiri) kuhusu makusudio ya Swala, je ni Swala yenyewe au msikiti ambao Swala iko ndani yake, kwa kuangalia desturi ya kutumia hali kwa mahali; kama kutumia jina la kahawani kwa maana ya mahali panaponywewa kahawa. Lakini wafasiri wengi wameelemea kwenye maana ya kwanza. Na hilo ni wazi zaidi kuliko kuwa ni msikiti.

3.   Wametofautiana vilevile kuwa je, makusudio ya kulewa ni kulewa pombe au usingizi?

Kwa dhahiri ni kulewa kileo sio usingizi.

4.   Baadhi ya wapokezi wamesema kwmba kundi la Maswahaba walikusanyi-ka kwa mmoja wao akawatengenezea chakula na pombe- Kabla ya kubain-ishwa hukumu ya pombe - Wakala na wakanywa. Walipolewa ukaingia wakati wa Swala; mmoja wao akawaswalisha; akakoroga Swala na akageuza Aya za Qur'an.

Sheikh Muhammad Jawad Balaghi*4 katika tafsir yake Alaurrahman amefu-atilia na kuthibitisha uongo wa riwaya hizi moja baada ya nyingine.

Kwa ufupi natija ya utafiti wake mkali ni kwamba Tirmidhi amepokea kuwa aliyewaita wenzake ni Abdul-rahman bin Auf na Ali ndiye aliyekuwa Imam. Abu Daud akapokea kuwa aliyealika ni mtu mmoja katika Ansari na Abdul-rahman alikuwa miongoni mwa waalikwa. Ibn Jarir Tabari amesema katika tafsir yake na Suyuti katika Durril-manthur wamesema kuwa Imam wa jamaa alikuwa ni Abdul-rahman bin Auf.

4Ni miongoni mwa maulama wakubwa wa kishia Imamia. Alikuwa akishinda na kukesha juu ya elimu, utafiti na kutunga. Alikuwa akijua lugha ya Kiibrania na akajua siri za Mayahudi na kufichua aibu zao. Ana vitabu kama Al-huda ila dinil-mustafa, A'ajibul-akadhib, Attawhid wa Tathlith na Rihlatul-madrasiya na vinginevyo.

Miongoni mwa mambo yake ya kutokuwa na ubinafsi na kumwelekea kwake Mungu peke yake, alikuwa haweki jina lake katika vitabu vyake alivyovitunga katika maisha yake. Alipoulizwa sababu yake akasema: "Huenda nikakosea katika baadhi ya niliyoyasema, akatusi - yule mwenye marad-hi moyoni mwake - taifa langu kwa sababu yangu, "Alikufa ulama huyu mwaka 1352 A.H.

43

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Vile vile katika Durril-manthur.. imesemwakuwa AyaimeshukakwaAbuBakr, Umar, Ali, Abdul-rahman na Saad, na kwamba aliyewaalika wenzake ni Ali. Katika Musnad ya Ahmad na Nassai kwamba Umar alisema: "Ewe Mola tubainishie kuhusu pombe;" ndipo ikashuka Aya hii.

Mbali ya kugongana riwaya katika mwalishi, Imam na Maamum, vile vile riwaya zimegongana na kupingana kuhusu Aya iliyovurugwa. Kuna riwaya inayosema kwamba Imam alisema: "Ninaabudu mnachokiabudu." Riwaya nyingine ikasema kuwa alisoma: "Sina dini."

Vile vile riwaya zimetofautiana kuhusu wakati wa kushuka Aya hiyo na sababu yake.

Zaidi ya hayo yote mwenye Alaurrahman amethibtishia kuwa mwenye riwaya ya kwanza, ambaye amesema kuwa Imam wa jamaa alikuwa ni Ali, alikuwa ni Kharij na ni katika madui wakubwa wa Ali.

Kwa vyovyote iwavyo ikiswihi kuwa kikundi cha maswahaba walikunywa pombe na kwamba Imam wao alikoroga Swala yake; basi watakuwa ni wale ambao waliwahi kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wakaabudu masanamu, wakanywa pombe na kula nyama za haramu katika ujahiliya waliokulia ndani yake na kulelewa,. Na Ali bin Abu Twalib hakuwa katika wao. Yeye alikulia katika malezi ya Mtume (s.a.w.), tangu utoto wake na akamrekebisha vile atakavyo.

Huenda mtu akasema: Kauli yako hii inatokana na mwongozo wa kiitikadi sio mwongozo wa matukio yalivyo.

Jibu: Hukumu ambayo inategemea makuzi ya mtu na malezi yake inatokana na mwongozo wa haki na matukio yalivyo. Sio mwongozo wa mawazo na itikadi.

Wala mkiwa na janaba - ispokuwa wapita njia - mpaka mwoge.

Imesemekana kuwa makusudio ya'mpita njia' ni msafiri; na kwamba maana yake, msikurubie Swala mkiwa mmelewa wala mkiwa na janaba ila katika hali ya safari. Ikumbukwe kwamba Aya imeeleza hukumu ya wasafiri pale ili-posemwa: "Na muwapo wagonjwa au mko safarini." Basi tukifasiri mpita njia kwa maana ya msafiri, italazimika kukaririka katika jumla moja bila ya dharura yoyote.

44

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

~ F^Tlf: İ--CIİJ ri sf * "HH sfcJTt Fi * ]^£ î İ Î ^f c3*fsTsllrî * "'rTrı p5>T"tsT * *ri j Î si * * "fc-vv^* * rrî eî sf rt *^* *y .s * "K:ili ff> it sî" VinTs î'hd îîıî Vi î Y l^vv eî rnrî—"

ba ni haramu kwa mwenye janaba kuingia msikitini, ila anayepita tu, isipokuwa Masjidul-haram (wa Makka) na Masjidun nabawi (wa Madina), haijuzu kabisa kuingia katika misikiti hiyo hata kwa kupitia.

Madhehebu mane yamesema kuwa mwili wote utakapoenea maji, basi litakuwa sahihi josho la janaba (janaba limeondoka), bila ya kuangalia kuanzia juu au chini.

Shia Imamia wameligawanya josho la janaba kwenye aina mbili; La mpango (tartib) na la kujivika (irtimasi), mpango kwao ni kujimiminia maji; wakawa-jibisha katika hali hii kuanza kichwa, kisha upande wa kuume na hatimaye kushoto. Lau atafanya kinyume, basi josho limebatilika.

Ama la kujivika ni kuuvika mwili wote ndani ya maji kwa mpigo mmoja; kama vile kuoga baharini, mtoni n.k.

MGONJWA NA MSAFIRI KATIKA TAYAMMAM

Na muwapo wagonjwa au mko safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni, au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayama-muni na mchanga ulio twahara, mpake nyuso zenu na mikono yenu.

Zimegongana kauli za wafasiri katika Aya hii, mpaka Sheikh Muhammad Abduh akasema: "Nimeangalia tafsiri ishirini na tano, sikupata cha kutesheleza wala kauli ya kuondoa taklifa." Alusy naye katika Rawhul-bayan akasema: "Aya hii ni katika Aya zinazotatanisha."

Na sisi tumerejea kiasi tafsiri ishirini za Sunni na Shia. Wengi wa wafasiri wake wamenakili tafsiri kadhaa, tukaona kama alivyosema Sheikh Muhammad Abduh, lakini hatukuona utatanishi wowote au mushkeli wowote, kama alivy-oona Alusy. Baada ya kutegemea maana yake na makusudio, tumejaribu kuifafanua kwa mfumo huu ufuatao:

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja katika Aya watu aina nne: Wagonjwa, wasafiri, waliotoka chooni na waliowagusa wanawake (makusudio ya kuwa-gusa wanawake ni kuwaingilia). Mwenyezi Mungu amewajibisha kwa wote hawa kuelekea kwenye tayammam wakati wa kuyakosa maji.

Katika mambo waliyoafikiana madhehebu yote ni kuwa dhahiri ya Qur'an haijuzu kuitegemea - hasa katika kutoa hukumu za sheria - ila baada ya kurudia kwenye Hadith za Mtume. Kwa sababu Hadith ni moja ya chimbuko la sharia;

$& 45

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'kâmâ âmbâ^

yenyewe:

"Analowapa Mtume lipokeeni na analowakataza, basi jiepusheni. Na mcheni

Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu." (59:7)

Ikiwa haikupatikana Hadith inayoichambua dhahiri ya tamko la Aya basi ni wajibu kuitumia dhahiri. Vinginevyo itawajibika kufanya amali kwa tutakavy-ofahamu kutoka katika Kitabu na Hadith kwa pamoja. Kwa sababu zinatoka katika chemchemi moja, ambayo ni Wahyi.

Tutazungumzia kila moja ya aina nne zilizotajwa na Aya. Hapo tutapata ufafanuzi wa jibu la swali hili: Kuwa je kuna Hadith inayopingana na dhahiri ya Aya katika moja ya aina hizi nne?

1. Mgonjwa: Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa yeye atatayamum akikosa maji. Wamekongamana kutumia dhahiri hii. Kwa sababu hata ambaye si mgonjwa atatayammum kwa kukosa maji.

Na mgonjwa akipata maji lakini akahofia kuyatumia je, atatayammum? Au atatumia maji hata akiwa anahofia madhara?

Wameafikiana mafakihi kwamba mgonjwa atatayammum hata ikiwa maji yapo akihofia kuyatumia. Wametoa dalili ya Hadith hii: "Hapana madhara wala kudhuriana." Na kwa isemayo kuwa sahaba mmoja alipatwa na jana-ba naye alikuwa na jeraha kubwa. Akawauliza wenzake wakamwamrisha kuoga alipooga akafa. Mtume aliposikia hilo akasema: "Wamemuua, Mungu awaue (nao)."

Kwa hiyo basi kauli yake Mwenyezi Mungu, 'kisha msipate maji; ni ya aina zote zilizotajwa katika Aya.

Haya ndiyo maana yanayopatikana kwa uasili wa Aya, sio kwa kufuatiza. Ama maana yanayopatikana kwa kufuatiza kwa kupatikana ambako mafaqi-hi na maulama wa Usul wanakuita 'ufahamu wa sharti'. Mafhumushart, ni kwamba unawajibisha kila mmoja katika aina nne kutumia maji akiyapata wala haijuzu kwake kutayamammu kwa hali yoyote ikiwa maji yapo; hata akidhurika kwa kuyatumia. Lakini umekwisha fahamu kutokana na yaliy-otangulia kwamba mafakihi wamekongamana na kwamba Hadith za Mtume, zimefahamisha kuwa mgonjwa atatayammam hata kama maji yapo ikiwa anahofia madhara kwa kutumia maji. Kwa hivyo basi hapana budi kumtoa mgonjwa na maana haya ya kufuatiza: na kubakisha aina tatu ambao ni

$& 46

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

wajibu kwao kutumia maji, yakiwapo, kwa mujibu wa ufahamu huu wa kufu-atiza.

Kwa ufupi ni kwamba wote wane watatayammam ikiwa wamekosa maji, hili halina shaka. Ama maji, yakiwapo basi atayatumia yule asiyehofia madhara ya kuyatumia. Ama yule anayehofia kuyatumia ataacha na atatayammam.

2.  Msafiri: Aya inafamisha kuwa yeye atatayammam akikosa maji, iwe safari yake ni ndefu au fupi. Hivyo ndivyo waliyoafikiana wote. Lakini wameto-fautiana katika asiyekuwa msafiri ambaye si mgonjwa. Je atayammam na kuswali au atasamehewa kuswali.

Abu Hanifa amesema: Swala itamwondokea. Kwa sababu dhahiri ya Aya ni kwamba tayammam inajuzu katika safari sio mjini.

Madhehebu mengine yote yaliyobakia wameafikiana kuwa mwenye kukosa maji ni wajibu atayammam na kuswali, ni sawa awe msafiri au nyumbani. Kwa sababu kujuzu kutayammam katika safari hakuzuwii kujuzu nyumbani. Zimekuja Hadith mutawatir, kutoka kwa Mtume (s.a.w.) amesema: "Hakika mchanga ulio twahara, humtwahirisha Mwislam hata akikosa maji miaka kumi."

Abu Bakr aliye maarufu kwa jina la Ibn A-arabi katika kitabu Ahkamul-Qur'an Juz, 1 Uk. 176 chapa ya mwaka 1331 A.H alisema: "Hakika Abu Hanifa mara nyingi huacha dhahiri na nukuu (nassi) kwa kukisia."

Unaweza kuuliza: Ikiwa msafiri na aliye mjini wana hukumu moja katika wajibu wa kuyatumia maji yaliyopatikana na kutayammam yakikosekana maji, kwa nini basi Qur'an imetaja safari hasa.

Wamejibu kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameitaja safari kwa sababu ndio aghlabu katika safari kukosa maji. Ama mtu akiwa mjini ni nadra. Hili ndilo jibu la kudhania na kuonelea ni vizuri katika kauli ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu halitegemei Aya au riwaya mutawatir au hukumu inayotokana na akili. Kwa hivyo sisi tunalinyamazia.

3. Au akiwa mmoja wenu ametoka chooni.

Ni kinaya cha kutokwa na mkojo, kinyesi au upepo. Basi mtu akitokwa na kimojawapo katika hivyo na akataka kuswali, ni juu yake kutawadha akipata maji na atatayammam akiyakosa. Hilo ni kwa kongamano la wanachuoni na Hadith (Ijmai na Sunna).

47

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'47ÂÜ mkâğüsaha nâ >wariawâ^

Qur'an, imetumia kwa kinaya katika hilo bila ya kueleza wazi; kama vile: "Basi sasa changanyikeni nao ..." (2:187) "Wala msiwakurubie." (2:222) "... Kabla hamjawagusa." (2:237)

Na Shafi amesema: "Makusudio ya kugusa katika Aya ni kule kugusana mwili." Kwa vyovyote iwavyo ni kwamba mwenye kuwa na janaba na akapa-ta maji ni juu yake kuoga akitaka kuswali. Akikosa maji atatayammam badala ya kuoga. Kila linalowajibisha kutawadha, mafakihi wanaliita hadath ndogo na kila linalowajibisha kuoga wanaliita hadath kubwa.

Basi tayammamuni na mchanga ulio twahara

Mchanga ni ardhi. Aya hii iko katika maana ya Hadith tukufu isemayo: "Nimeumbiwa ardhi kuwa ni msikiti na yenye kutwaharisha."

Mpake nyuso zenu na mikono yenu.

Madhehebu yote yameafikiana kuwa kutayammam hakuwi ila katika viungo viwili hivi; na wakatofautiana mpaka wa sehemu zinazopakwa mchanga katika uso na mikono miwili. Madhehebu mane yakasema: "Ni wajibu kupaka uso wote zikiwemo ndevu; sawa na ilivyo katika udhu. Katika mikono, Hanafi na Shafi wamesema ni wajibu kupaka mchanga mpaka kwenye vifundo vya mikono kama udhu."

Shia Imamia wamesema ni wajibu kupaka baadhi ya sehemu ya uso, sio uso wote. Kwa sababu herufi 'Ba' ni ya tabiidh (kufanya baadhi); sawa na ile iliyo katika udhu kuhusu vichwa. Kwa sababu kama isingekuwa ya tabiidh basi ingekuwa ya ziada; na asili ni kutokuwa ziada. Wakasema inafaa kupangusa viganja viwili tu. Ufafanuzi uko katika vitabu vya fiqh.

44.Je, huwaoni ambao wamepewa fungu katika Kitabu hununua upotevu na kuwataka mpotee njia?

Kaashif5-40.jpgKaashif5-41.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

45.Na Mwenyezi Mungu anawajua sana maadui zenu; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi, na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa msaidizi.

46.Miongoni mwa mayahudi wako ambao hugeuza maneno kutoka mahali mwake, na husema: tumesikia na tumeasi; na sikia bila kusikilizwa; na (husema) raina kwa kupondoa ndimi zao na kuitukana dini. Na lau kama wao wangesema: Tumesikia na tumetii na usikie na utuangalie, ingelikuwa heri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewaalani kwa kufuru zao, basi hawaamini ila wachache tu.

47.Enyi mliopewa Kitab! Aminini tuliyoyateremsha            yenye

kusadikisha mliyo nayo nyinyi, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tuliivy-owalaani watu wa Sabato (Jumamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima iwe ni yenye kufanywa.

Kaashif5-42.jpgKaashif5-43.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ..

Aya 44 - 47 HUNUNUA ■UPOTEVU NA KUWATAKA MPOTEE

ISRAIL NA NGUVU YA SHARI

Je huwaoni ambao wamepewa fungu katika Kitabu hununua upotevu na kuwataka mpotee njia.

Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa makusudio ya waliopewa fungu katika Kitabu ni Mayahudi ambapo amewasifu Mwenyezi Mungu kwanza kwa upotevu; pale aliposema hununua upotevu, na pili kwa upotezaji pale alipose-ma: na kuwataka mpotee. Kisha akawasifu kwa ugeuzaji maneno, pale aliposema: hugeuza maneno kutoka mahali pake.

Historia haikujua watu walio wapinzani zaidi wa haki na maadui wa kheri kuliko Mayahudi. Wamekuwa wapotevu, wapotezaji na wageuzaji maneno, pale walipokuwa madhalili waliotawaliwa. Ama leo baada ya dola dhalimu kuwa-tengenezea wao koloni, hawakuacha upotevu, upotezaji na kugeuza maneno. Bali wamekuwa ni nembo ya shari ya kimataifa na silaha na maangamizi aliy-onayo kila mkoloni mkandamizaji, na ni kipimo cha kupambanua nguvu ya shari na uhaini na ile ya heri na ukombozi. Hakuna dola yoyote ya kikoloni, wakati huu inayotaka kutawala watu, lazima itakimbilia Israel ndipo itaweza kutekeleza lengo lake. Taifa lolote dhalimu Mashariki na Magharibi lazima liombe msaada wa kuhami masilahi yake kwenye watu hawa dhalimu wenye dhambi.

Al-hamdulillah, dalili zimejionyesha waziwazi katika Vietnam za kumwandalia binadamu mpya atakayejua njia ya kummaliza adui wa haki na wa ubinadamu. Binadamu wa leo*5 katika Vietnam na binadamu wa kesho mahali popote, atatofautiana na binadamu wa jana.

Yeye anaweza kumtofautisha mwenye haki na uhaini bila ya utatanishi, hata kama atakinaishwa mara elfu na ataweza kumweka kila mmoja mahali pake. Hapo binadamu ataweza kuishi bila ya matatizo na mabomu.

Matukio yamethibitisha - hasa lile balaa la tarehe 5 June 1967- kwamba matatizo ya waarabu na waislam chimbuko lake ni kuweko watu wasiostahiki kuwa viongozi. Hili litakwisha kadiri siku ziendavyo.

*5 Hapo ilikuwa ni mwaka 1968

50

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Na Mwenyezi Mungu anawajua sana maadui zenu; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa msaidizi.

Mungu anajua na sisi tunajua vile vile kuwa Mayahudi na wanaowategemea ni maadui wa haki na ubinadamu, wala sio jambo lililojificha kwa yeyote kuwa dola ya Israel ni nembo ya uovu ya kimataifa, lakini wengi wetu hawawajui vibaraka wanafiki. Kwa sababu wao wanajificha kwenye nguo ya watu wema na kuwakanganya watu duni. Na iko siku watafichuka na Mwenyezi Mungu atawafedhehesha na kuing'oa mizizi yao kwa mikono ya waumini na wakom-bozi.

Miongoni mwa Mayahudi wako ambao hugeuza maneno kutoka mahali mwake.

Aya zilizo katika mwelekeo huo ni kama hizi zifuatazo:

"Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa ajili ya uongo wanasik-

iliza kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia; hugeuza maneno kutoka mahali

mwake." (5:41)

"... Wanasikia meneno ya Mwenyezi Mungu kisha wanayageuza baada ya

kuwa wameyafahamu ..." (2:75)

Ni sawasawa na walivyolifanyia azimio la Umoja wa Mataifa la ulazima wa Israel kuondoka sehemu za Waarabu wanazozikalia kwa mabavu walizozi-vamia tarehe 5 June 1967 na wakaliita wajibu wa ushirikiano pamoja na Waarabu6.

Maneno yoyote yasiyoafikiana na makusudio maovu wanayabadilisha na mahali mwake hata kama wakijua na kufahamu kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu . Mwanzo waliibadilisha Taurati; mahali pa Aya ya uadilifu na rehema wakabadilisha na kuwa unyang'anyi na dhuluma na kuwaua wanawake na watoto. Mwenye Tafsiri Al-manar, katika kufasiri Aya hii, amesema: "Wamethibitisha wanavyuoni kugeuzwa kwa vitabu vya agano la kale na jipya kwa ushahidi mwingi."

Katika kitab Idh'harul-haq cha Sheikh Rahmatullah (wa India) kuna ushahidi mia moja wa kugeuzwa kimaandishi na kimaana.

*6Maulama wa Kiislamu wametunga vitabu vingi kuhusu muujiza wa Qur'an na wakataja aina nyingi za miujiza, lakini hawakutaja jinsi Qur'an ilivyoeleza hakika ya Mayahudi, ambapo huo nao ni Muujiza

51

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kishaâkâtâjâ "mweriye 'W-mânâr"b¥âdh]"yâ"üshah]drhüb'kâWka'Jüz|5'Uk\'"141'' chapa 1328 A.H. Sheikh Jawad Al-balaghi naye akatunga kitabu madhubuti kilichokusanya maudhui haya, alichokiita Rihlatul-madrasiyya; na kimechapishwa mara kadhaa. Mtume (s.a.w.) aliwapa Mayahudi wa Hijaz (Madina) mwito wa kuifuata haki na kuacha kuyabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, lakini wakaendelea kuwa na inadi; na husema tumesikia; na tumeasi; na sikiza bila kusikilizwa; Yaani hutasikilizwa wala kuitikiwa mwito wako unaotulingania. Hilo si ajabu kwa watu wenye asili ya shari na chimbuko la ufisadi.

Na (husema) Raina kwa kupondoa ndimi zao na kuitukana dini.

Wafasiri wamesema kuwa Mayahudi walisema Raina wakiwa hawakusudii maana ya dhahiri ya tamko hili ya kuwachunga. Isipokuwa walikusudia ru'una yaani upumbavu. Na jambo hili ni kupotosha na kuitusi dini. Yamekiwshatangulia maelezo zaidi ya tamko Raina katika kufasiri Aya 104 ya Sura ya Al-Baqara.

Lau kama wao wangesema: Tumesikia na tumetii, na usikie na utuan-galie, ingelikuwa ni heri kwao na sawa zaidi.

Kwa kuwa kauli hiyo ni ya sawa zaidi na bora na salama zaidi ndipo wakaiacha na wala wasiiseme.

Katika kufasiri Aya hii, Arrazi anasema: Maana ya kwamba wao ni sawa lau wangelisema: Tumesikia na tumetii, badala ya kusema: Tumesikia na tumeasi. Kwa sababu wao wanajua ukweli wako. Na badala ya kusema: Na sikiza bila kuzikizwa, wangesema na sikia tu. Vile vile badala ya kusema kwao Raina waseme Undhurna; yaani tupe muda kidogo ili tukufahamu; lau wan-geliyasema yote haya ingelikuwa bora na sawa.

Lakini Mwenyezi Mungu amewalani kwa kufuru zao.

Na kuifanyia inadi haki na kung'angania batili, na laana ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake na machukivu yake.

Basi hawaamini ila wachache tu.

Tangu enzi na enzi watu kutoka mataifa mbali mbali na dini mbalimbali wameingia katika Uislamu kwa makundi, isipokuwa mayahudi tu. Walisilimu wachache sana; kama vile Abdillah bin salam na baadhi ya wafuasi wake. Bali wao mayahudi waliupiga vita uislam na waislam na bado wanaendelea kuu-

52

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

fariyia vitimbikwa "nyerizo"zöîe!'"'Hİİ"hT'daHiT'kübwa'küWâ"üİsîâmu"nİ"hâkT'n'â' kweli. Jambo la kushangaza ni kwamba viongozi wa uislam na wanaoutolea mwito, hawakuutolea dalili utukufu wa Uislam na utu wake kwa uadui wa Mayahudi waliosema; "Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba." (5:64)

Uadui wao ni kwa uilsam na kila mwenye kusema: "Lailahailla Ilah."

Enyi mliopewa Kitab! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha mliy-onayo nyinyi.

Kwa dhahiri msemo unawakusanya mayahudi na manaswara, kwa vile wote ni watu wa Kitab. Imesemekana kuwa msemo unawahusu mayahudi kwa kuan-galia mfumo wa maneno. Makusudio ya tuliyoyateremsha ni Qur'an tukufu, kwa sababu ndiyo inayosadikisha Taurat, kama ilivyoteremshiwa Musa (a.s.) na Injil, kama ilivyoteremshiwa Isa (a.s.)

Mtume (s.a.w.) aliwapa mwito, mayahudi, wa kuingia kwenye uislam kwa kuuzingatia kuwa ni haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Akawapa dalili na hoja kila mara. Lakini wapi! Haki na hoja zake si chochote kwa mayahudi. Dini yao ni faida na mali tu; na hawatapata faida ya haraka haraka katika uislam wala katika Taurat, isipokuwa faida na utajiri wa haraka haraka wataupata katika ulanguzi, riba, kunyang'anya, kughushi, utapeli, umalaya, kamari, kuleta fitina, vita na mengineyo.

Kwa ajili hiyo ndio wao wamekua msitari wa mbele katika uwanja huu; na

Mtume anajua fika hali hii, lakini aliwalingania ili kutimiza hoja tu:

"... Na sisi si wenye kuwaadhibisha mpaka tuwapelekee Mtume ..." (17:15)

Kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni.

Katika tafsir ya Aya hii, tumeona tafsir nne zenye kupingana. Yenye nguvu tuonavyo ni ile ya Sheikh Muhammad Abduh ambayo kwa ufupi ni kwamba kugeuza ni kinaya cha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawapofusha njia wasi-jue pa kuelekea kwenye makusudio yao; sawa na wale wanaorudi nyuma kila wanapotaka kwenda mbele.

Au tukawalaani kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi).

Watu wa Sabato ni watu miongoni mwa Mayahudi waliobadilisha dini na wakapetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu,. Kwa hiyo akawafedhehesha na kuwaadhibu duniani kabla ya akhera. Tumeyafafanua hayo katika sura Baqara. (2:65)

53

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Katika Aya"nil"Mwenyezi "Müriğü'anâwâkeme¥'küwâ'kâma"hâWâtâj]epushâ'n'â' upotevu, kupoteza na kubadilisha basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafedhe-hesha kama alivyowafedhehesha mababu zao.

Kwenye tafsiri nyingi ikiwemo Tafsiri ya Arrazi, Majmaul-bayan na Bahlul-muhit nimesoma jumla ninayoinukuu hapa: "Hapana budi wafutwe Mayahudi kabla ya Kiyama," Amin!

Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima iwe ni yenye kufanywa.

Hakuna wa kupinga hukumu yake wala kuvunja amri yake ambaye hukiambia kitu 'kuwa' kikawa.

Ewe Mwenyezi Mungu! Liharakishe jambo litakaloifanya dini yako iwe juu na watu wako wawe na nguvu.

48.Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika, lakini husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na mwenye               kumshirikisha

Mwenyezi Mungu hakika amezusha dhambi kubwa.

49.Je, huwaoni wale ambao huji-takasa nafsi zao? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, nao hawatadhulumi-wa hata kilicho kwenye uwazi wa kokwa ya tende.

50.Tizama jinsi wamzuiliavyo Mwenyezi Mungu uongo. Na latosha hilo kuwa ni dhambi iliyo wazi.

Kaashif5-44.jpgKaashif5-45.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ■'....

Aya 48 - 50MWENYEZİMÜNĞU"HMÂMEHrKÜFÂNYİWAMSHİRTKÂ

 MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika lakini husamehe yasiokuwa hayo kwa amtakaye.

Kabla ya kufasiri Aya hii tuanze na mambo mawili yanayoambatana nayo

sana:

1. Kushirikisha kunagawanyika kwenye aina mbili: Kushirikisha katika Uungu; kama kuitakidi kuwa kuna waumbaji wangi na wenye kutoa riziki. Na kushirikisha katika twaa; kama kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja kinadharia tu, lakini anamtii kiumbe katika kumwasi Muumba.

Ukafiri nao pia uko aina mbili: Kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumkanusha na kukufuru katika twaa; kama kuamini Mungu mmoja kisha kumwasi kwa kupuuza. Vilevile kukufuru neema na kuacha kumshukuru mwenye kuneemesha.

Makusudio ya kushirikisha katika Aya hii ni aina mbili za kwanza za kushirikisha na kukufuru; yaani kuamini waungu wengi na kutoamini kabisa.

2.Yakija maneno ya ujumla, yanahukumu kiujumla kwa watu na yakija tena maneno mahsusi, yanawatoa baadhi ya watu waliokuwa katika ujumla. Ikiwa meneno yote mawili yametokea katika chimbuko moja, basi tutauchukulia ule umahsusi kwenye ujumla; yaani tutawatoa wale waliofa-hamishwa na kauli mahsusi. Kwa ufafanuzi hebu tupige mfano:

Mwenyezi Mungu anasema: "Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni mikono yao." (5:38)

Hapa Aya imefahamsiha kwamba kila mwizi atakatwa mkono, hata kama ni siku za njaa. Kisha ikaja Hadith isemayo: "Mwizi hakatwi katika siku za njaa." Kwa hiyo kutokana na hali hiyo imepasa tuifunge Aya ya wizi na Hadith ya njaa na hukumu iwe kila mwizi atakatwa mkono isipokuwa siku za njaa.

Baada ya utangulizi huu sasa tuzikutanishe Aya tatu ambazo zitatupa ufafanuzi wa makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kufanyiwa mshirika."

Mwenyezi Mungu anasema: Sema: "Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi

<ö> 55

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

zenu! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu husamehi dhambi zote. Hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu." (39: 53)

Tamko la Aya hii linaonyesha ujumla, na maana yake yako wazi nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu husamehe kila dhambi hata ya kushirikishwa Yeye. Lakini Aya tuliyonayo 'Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika,' tamko lake ni mahsusi, na maana yake yako wazi vile vile, kwamba Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa, kwa hiyo imepasa kutoa kushirikisha katika Aya ya (39:53)

Tena ikaja Aya ya tatu isemayo; "Hakika mimi ni mwenye kusamehe sana kwa anayetubia na akaamini na akashika uwongofu." (20:82) Aya hii nayo, imemtoa mwenye kutubia kutoka Aya ya kutosamehewa mwenye kushirikisha; kama ambavyo nayo ilimtoa mwenye kushirikisha kutoka Aya ya kusamehewa dhambi zote.

Kwa hivyo basi, maana yanayopatikana kwa kuzikutanisha Aya tatu na kuzi-unganisha, ni kwamba mwenye kutubia ushirikina, Mungu humsamehe. Kwa sababu yeye amezikana dhambi zake; na mwenye kufa akiwa msirikina hana uokofu. Kwa sababu ameacha kuitumia nafasi yake na kwamba kusamehewa yeye ni kuchochea ushirikina na kuinyenyekea dhuluma.

Zaidi ya hayo kumsamehe mshirikina sio kuwa Mwenyezi Mungu atamwambia aliyefanya uovu: 'Ahsante sana' Mwenyezi Mungu ametakata na hayo kabisa.

Unaweza kuuliza, kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Lakini husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye, inafahamisha kuwa dhambi hiyo -isiyokuwa kushirikisha - mtu akiifanya, inawezekana Mwenyezi Mungu akam-samehe kabla ya kutubia. Kwa sababu kufutiwa dhambi pamoja na kutubia kumethibiti kwa Qur'an na Hadith. Kwa hiyo kauli ya Mwenyezi Mungu husamehe itahusika na muumin mwenye dhambi asiyetubia. Au kwa maneno mengine ni kwamba Aya inafahamisha kuwa kusamehewa dhambi muumin hakufungiki na toba tu, bali huenda Mwenyezi Mungu akasamehe dhambi za waumini bila ya kutubia?

Jibu: Wameafikiana waislamu kwamba mwenye kufa akiwa ametubia Mwenyezi Mungu humtakabalia toba yake, kulingana na Aya za Qur'an na Hadith za Mtume. Lakini wametofautiana kuhusu mwislamu mwenye dhambi akifa kabla ya kutubia.

56

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Khawanj wamesema: "Atabakishwa niilele rhötöhii"s¥wâ"nâ"Kâifin7'hT'sawâ' dhambi yake iwe kubwa au ndogo.

Kikundi kimoja cha Marjaa kinasema kuwa ataingia peponi bila ya kuadhibiwa, kwa sababu maasi hayadhuru imani wala twaa hainufaishi chochote ukafiri; kama wanavyodai.

Shia na Sunni wamesema hatabakishwa milele motoni, na dhambi zake zitaachwa na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Akitaka atamsamehe na kumwingiza peponi moja kwa moja; na akitaka atamwadhibu kiasi ana-chostahili, kisha amtie peponi.

Maoni yetu hayatofautiani sana na kauli ya Sunni na Shia, na tutaeleza kwa mfumo huu: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hataki kusamehe kwa michezo bila ya hekima inayosababishia hilo. Na hekima inayowajibisha kusamehewa, hai-fungiki na toba tu; inaweza kuwa ni shafaa au jambo jinginelo. Wala si dharu-ra kufahamu kwa ufafanuzi, bali inatosha kujua kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye hekima, basi.

Kwa hivyo, katika mtazamo wa kiakili, hakuna kizuizi cha kusamehewa dhambi kwa Muumin bila ya kutubia. Yametangulia maelezo yanayofugamana na utafiti huu katika kufasiri Aya (2: 81) kifungu cha Madhambi makubwa.

DALILI YA UMOJA NA UTATU

Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika amezusha dhambi kubwa.

Kwa sababu atakuwa ameamini lisilowezekana. Miongoni mwa dalili za kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na lau kungalikuwa na waungu wawili, basi ama atakuwa mmoja wao ni mweza zaidi wa kupangilia mambo ya ulimwengu, au asiweko.

Kwa hiyo akiwa mmoja ni muweza zaidi, basi wa pili atakuwa hana maana tena; na kama akitokuwapo muweza zaidi, basi hawezi kuwa Mungu, kwa kushindwa kwake kwa upande fulani na kutokuwa na faida ya kuweko kwake.

Dalili bora zaidi ya umoja wake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni ile aliyoieleza yeye mwenyewe juu ya umoja wa dhati yake, pale aliposema: "Lau wangelikuwako humo (mbinguni na ardhini) waungu wengine, isipokuwa Mwenyezi Mungu bila shaka zingeharibika. Ametakasika Mwenyezi Mungu Mola wa Arshi na yale wanayomsifu. (21:22)

$& 57

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Yaahi İâü kühğeliküvvakö "nâ'"Münğu'"mweWğİne'"kâîik¥"'mbİngu'"h¥'"afdhr asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi zisingelikuwa sawa na wangeliharibika waliomo na vilivyomo na kusingekuwako na nidhamu. Kwa vile kama kunge-likuwa na Miungu wawili angelikuwa kila mmoja ni muweza, na kawaida ya mwenye uwezo ni dhidi ya anavyotaka mwingine.

Kwa hiyo basi mmoja wao akitaka kuumba kitu na mwingine akitaka kinyume chake, hapo ama yatapatikana matakwa yao wote wawili kwa pamoja, jambo ambalo litalazimisha kupatikana na kukosekena kwa wakati mmoja na hilo ni muhali. Au yatapatikana matakwa ya mmoja wao kinyume cha mwingine, atakuwa huyu mmoja ameshindwa na mwingine. Kimsingi ni kwamba anayeshindwa hawezi kuwa Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto wala hakuwa pamoja naye mungu (mwingine). Ingekuwa hivyo basi kila mungu angeliwachukua aliowaumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu." (23:91)

Kuna mfano mashuhuri unaosema: "Fahali wawii hawakai zizi moja."

Amirul-mumin, Ali alimwambia mtoto wake Hassan (a.s.): "Jua ewe mwanan-gu, lau Mola wako angelikuwa na mshirika wangelikujia Mitume wake na ungaliona athari ya milki yake na ufalme wake na ungelijua vitendo vyake na sifa zake."

Unaweza kuuliza: Je kusema kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja katika asili tatu: Baba, mwana na roho mtakatifu ni katika umoja au ni katika kuwafanya miungu wengi

Jibu: Ikiwa makusudio ni sifa kama vile mwenye kurehemu, mwingi wa rehe-ma hizo ni katika kumpwekesha, lakini ikikusudiwa mtu basi huo ni Utatu.

Amesema Said Al-Khauri Ashartuni katika kitab Aqrabul-mawarid; "Neno Aqnnim (lililotumiwa katika kueleza utatu) maana yake ni asili na mtu." Kwa hivyo basi litakuwa katika kuwa waungu wengi sio mmoja. Hayo yanatiwa nguvu na neno baba na mwana ambayo yanahitajia kuweko na idadi na mabadiliko kwa mtu na dhati. Isitoshe, picha na sanamu zilizoko katika makanisa hasa ya bibi Maryam bikira (a.s.) zinaonyesha idadi ya waungu waziwazi, kwa sabaau anaonyesha amempakata mtoto ambaye ni Bwana Masih (a.s.)

58

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa Je, huwaorii wale"ambâö hujitakasâ riâfsi zâb!.....

Wafasiri wamesema kuwa Aya hii imeshuka kwa mayahudi. Ni sawa iwe ghu-ruri ya mayahudi ndio sababu ya kushuka Aya hii au la, lakini ni picha inayosadikisha madai yao ambayo hayana mfano katika uzushi na uongo.

Mfano kama wasemavyo: 'Sisi ni watoto wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake.' Au kusema: 'Hataingizwa peponi ila aliye myahudi.' Vile vile 'Sisi ni taifa teule la Mwenyezi Mungu.' Yaani kuwa Mwenyezi Mungu ni wao tu, peke yao, na kwamba Yeye amewaumba watu wengine wawe ni watwana wao. Hawakutosheka na haya, bali ujinga wao na ghururi yao iliwapelekea kusema: 'Mungu ni fukara na sisi ni matajiri.'

Kweli hakuna mtu anayewashinda kwa utajiri wa kuzusha na kutengeneza mambo yasiyokuwapo. Ni hivi majuzi tu walitangaza na kueneza uvumi, wakapiga kelele Mashariki na Magharibi kwamba waarabu wanajianda kuwashambulia, wakati ambapo wao na mabwana zao wakoloni wanapanga njama za kuvamia na kuwahujumu waarabu.

Baada ya kumaliza kupanga, wakatekeleza bila ya kutazamiwa, wakafanya dhulma na unyama uliowafanya watu wasahau aliyoyafanya Hitler na Jankis khan.

Haya ni madogo sana katika mifano ya madai ya mayahudi. Tumeyaleta kama mfano tu, lakini sio hali yao hasa. Je, inawezekana kuyamaliza yote ya mayahudi? Unaweza kuuliiza: Ikiwa hali ya Israil ni hivi imekuwaje wakaweza kusimamisha dola zaidi ya miaka ishirini sasa?

Jibu: Mataifa ya kikoloni ndiyo yaliyoitengeneza Israel kwa kuhami masilahi yao katika Mashariki ya kati. mayahudi hawana dola isipokuwa jina tu. Ama kubakia kwake mpaka leo, kunatokana na kubakia ukoloni ambao umeipigia hema la Oksijeni. Hivi sasa dola hiyo iko njiani kuisha; hata kama itachukua muda mrefu. Kimsingi ni kwamba mwenye kusimamia kitu huisha, mara tu kiishapo.

Ukiuliza vipi Mwenyezi Mungu amewashakiza mataghuti Makafiri kwa waja wake wanaompwekesha, jibu utalipata kwenye tafsiri ya 3; 138. Kwenye kifun-gu cha Ushenzi wa 5 Juni

59

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 'B¥lT'Mwehyezİ'Münğü'Kumtekâs¥'âmtakaye!..

Sio yule anayejishuhudia yeye mwenyewe. Kimsingi, Mwenyezi Mungu ham-takasi ila ambaye vitendo vyake vinashuhudia utakaso.

Ingawaje Aya imeshuka kwa mayahudi, lakini inamkusanya kila mwenye kuji-takasa kwa sababu tamko ni la kiujumla; na linalozingatiwa ni ujumla sio sababu ya kushuka. Majaribio yamethibtisha kuwa hakuna yeyote anayeji-tukuza ila ni kwa sababu ya ujinga wake na ghururi yake. Au kwa kasoro fulani anayojaribu kuificha, kwa ushahidi usiokubalika hata kwake yeye mwenyewe; kwa sababu anajua uongo wake.

Tizama jinsi wamzuliavyo Mwenyezi Mungu uwongo kwa kusema 'Sisi ni taifa teule la Mwenyezi Mungu', ni watoto wa Mungu na vipenzi vyake' na mengineyo mengi:

"... Na hatengenekewi mwenye kuzua uongo ..." (20:61)

51 .Je, huwajui ambao wamepewa fungu katika Kitabu wanaamini sanamu na taghuti na wakisema kwa ajili ya wale waliokufuru kuwa hao wameongoka zaidi katika njia ya haki kuliko walioamini.

52.Hao ndio waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu, na ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani, hatampatia wa kumsaidia.

Kaashif5-46.jpgKaashif5-47.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ....

Aya 51 -52VVÂNÂÂMİNİ SÂNÂMÜ NÂ TÂĞHÜT

 LUGHA

Neno Jibt linatumika kwa maana nyingi. Makusudio yake hapa ni anayeabudi-wa ambaye si Mungu (sanamu) Na Taghut ni aliyepetuka mipaka.

MAANA

Je, hawajui ambao wamepewa fungu katika Kitabu wanamini sanamu na taghuti.

Katika Aya zilizotangulia, Mwenyezi Mungu amewataja mayahudi kwa upote-vu, upotezaji, kuyaweka maneno pasipo mahali pake na kupindua maneno. Kisha katika Aya hii amewataja kuwa wao wanaamini sanamu na taghuti; yaani masanamu wanayoyaabudu Maquraish.

Unaweza kuuliza: Imekuwaje Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kusema kuhusu mayahudi kwamba wao wanaamini sanamu na inajulikana wazi kuwa wao hawaamini masanamu ya Maquraish.

Jibu: mayahudi hawaamini masanamu ya Kiquraish katika nafsi zao, bali waliyakubali kiunafiki kwa kudanganya na kwa ajili ya kubagua na kumfanyia inadi Muhammad (s.a.w.) na aliyemwamini. Wakawaambia waabudu masanamu: "Nyinyi mna njia ya uongofu zaidi kuliko waislamu." Iliyo sawa ilikuwa ni kwa mayahudi wawasaidie waislamu dhidi ya waabudu masanamu kwa sababu waislam ni watu wa Kitabu na wanaikubali Taurat kinyume na waabudu masanamu. Kwa hiyo mayahudi walikhalifu haki na wakasimama pamoja na washirikina, ndipo Mwenyezi Mungu akawataja kama waabudu masanamu.

Kwa hali hiyo ndipo tunapoipata tafsiri ya Hao wameongoka zaidi katika njia kuliko walioamini. Yaani mayahudi walisema: Washirikina ni waongofu zaidi wa njia kuliko waumini. Kwa hiyo jibu la swali liko ndani ya Aya yenyewe.

Kwa hali hii inatubainikia kuwa ishara ya hao ni ya waabudu masanamu na kwamba herufi lam katika neno Lilladhina ni ya kwa ajili; yaani waliyoyasema ni kwa ajili ya kuwaridhisha wale waliokufuru, ambao ni washirikina wa kiquraish na hawakusema kwa kuamini wayasemayo.

Hao ndio waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu nao ni mayahudi waliofanya unafiki wakasadiki masanamu kwa ukaidi na inadi kwa waislam wanaowasadi-

$& 61

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa kiMitume "yab"; karria'We'MusarDaudrsuieimanrWhya'na'Zakariya.'....

Na ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani, hatampatia wa kumsaidia.

Isipokuwa Amerika ambayo ilisheheneza Israil kwa silaha na kuisaidia tarehe 5 June; na Umoja wa Mataifa ukawatetea kwa namna ambayo mwarabu yeyote mwenye ikhlasi au mwislamu yeyote aliye muumin hatasahau hata ukipita muda gani.

Na sisi pamoja na majeraha tuliyo nayo, tunaamini kwa imani isiyo na shaka kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye msaidizi mwenye nguvu; na kwamba mwisho wa mambo utakuwa ni wa haki na uadilifu. Kwa hiyo ni juu ya wanaoitafuta haki kuvumilia, kutokuwa na pupa ya kuifikia, na kutotishwa na silaha ya adui kwa vyovyote atakavyokuwa na hatimaye kufaidika na majaribio.

53.Au wao wana fungu katika ufalme? Basi hapo wasingewa-pa watu hata kitobwe cha kokwa ya tende .

54.Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake? Basi tuli-wapa watoto wa Ibrahim Kitab na h ekima na tukawapa ufalme mkubwa.

55.Katika wao kuna walio mwamini na katika wao kuna waliojie-pusha naye; na Jahanam yatosha kuwaunguza.

Kaashif5-48.jpg

62

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ..

Aya 53-55: HAWAWAPi WÂTÜ HATACHEMBE

MAANA

Bado maneno yako kwa mayahudi. Mwenyezi Mungu katika Aya ya 44 ame-wataja kwa upotevu na upotezaji; katika Aya 45 uadui wao kwa waislamu katika Aya ya 46 kwa kugeuza maneno; katika Aya 49 kwa kujitukuza; katika Aya 50 kwa uzushi na katika Aya ya 51 kwa inadi, ukaidi na kuboresha ibada ya sanamu kwa unafiki.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawataja kwa ubakhili:

Au wao wana fungu katika Ufalme? Basi hapo wasingewapa watu hata

kitobwe cha kokwa ya tende.

Maana ni kuwa mayahudi hawana dola wala ufalme. Lau wangelikuwa na sehemu ya ufalme, wangeliwazuilia watu wote heri na wasingelimwachia yey-ote kitu; hata kiasi cha kitobwe cha kokwa ya tende kilicho kidogo sana kisi-chotumika.

Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. Walikuwa na wanaendelea kuwa hawawezi kuona neema ya Mwenyezi Mungu kwa mja yeyote miongoni mwa waja wake ila hujaribu kuiondoa kwa njama au kwa riba au kwa kudanganya kwa binti zao na wake zao. Na wakipata nguvu kidogo hunyang'anya na kumwaga damu.

Kuanzia siku walipovamia ardhi ya Palestina mwaka 1948, waliwatoa wazal-endo nchini mwao baada ya kuwachinja wanawake na watoto kila mahali. Na mnamo mwaka 1967 waisrail, kwa kusaidiwa na wakoloni, walivamia sehemu nyingine ya ardhi ya waarabu. Kikakaririka kitendo chao cha kwanza, cha kuua na kufukuza. Hili sio geni katika historia yao na tabia zao.

Waarabu wametawala na ukaendelea utawala wao miaka kadhaa; ukaenea mashariki na magharibi; na mayahudi walikuwa ni miongoni mwa raia zao; wakafanya uadilifu kwa wote na kuwafanyia wema mayahudi na watu wa dini nyinginezo; mpaka wakasema watunzi wa kimagharibi; kama vile Gustav Lebon: "Haikujua historia utawala wenye huruma zaidi ya Waarabu." Wameshuhudia kama hivyo wengineo "chombo humimina kilicho nacho" anasema Ibin Swafiy.

63

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Itakuwa ni vizuri kunakili aliyoyataja mwenye Al-amanarwakati wa kufasiri Aya hii, katika mwaka wa 60 wakati Palestina ilipokuwa katika utawala wa dola ya Uthmaniya, Ninamnukuu: "Maana yanayopatikana katika Aya hii, ni kwamba hawa mayahudi ni watu wachoyo na wabakhili sana, wanaona tabu kunufaika mwengine yeyote kutokana nao. Wakiwa na utawala wanawazuilia watu was-inufaike hata kidogo, japokuwa ni kitu kipuuzi tu. Basi kwa nini isiwe uzito kwao kutokea Mtume wa kiarabu (Muhammad) ambaye ana milki wakiwemo mayahudi?

"Sifa hii bado wanayo hadi leo. Ikiwa juhudi zao za kuunda serikali katika Palestina zitafanikiwa, basi watawafukuza waislamu na wakristo na hawatawa-pa hata kitobwe cha kokwa ya tende. Dalili ziko kwamba wanajaribu kumiliki ardhi takatifu na kuwazuia wengine na sababu zote za kupata riziki. Wameweka akiba ya mali nyingi sana kwa ajili ya hilo. Kwa hiyo ni wajibu kwa serikali ya Uthmaniya kutowapa nafasi mayahudi katika Palestina wala wasi-waache wakamiliki ardhi na kuhamia kwa wingi. Kwani hilo lina hatari kubwa."

Mwenye Tafsir Al-manar anasema Aya haithibitishi wala kukanusha kutawala mayahudi Palestina, isipokuwa inabainisha tabia watakayokuwa nayo lau watatawala Palestina.

Haya ndiyo aliyoyasema ulama katika maulama wa Kiislam kuhusu tafsiri ya Aya hii. Ameisema miaka arobaini kabla ya kupatikana serikali ya Israel katika Palestina. Hii haifahamishi kitu zaidi ya kufahamisha ukweli wa Nabii Muhammad (s.a.w.) katika Utume wake na ujumbe wake, pale alipotoa habari kwa Wahyi wa Mwenyezi Mungu kabla ya zaidi ya miaka 1300, kwamba mayahudi lau watamiliki na kutawala wangelikuwa na yale yaliyotokea mwaka 1948 na 1967.

Je, ambaye Mwenyezi Mungu ameufungua moyo wake kwa uislam akawa yuko katika nuru itokayo kwa Mola wake (ni sawa na mwenye moyo mgumu)? Basi adhabu kali itawathubutukia wale wenye moyo mgumu wasimkumbuke Mwenyezi Mungu. Hao wamo katika upotevu ulio wazi (39:22)

Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake?

Hii nayo ni sifa nyingine katika sifa za mayahudi, hasadi. Makusudio ya watu hapa ni Mtume Muhammad (s.a.w.) na waumini walio pamoja naye. Na hasadi yao mayahudi ni kutokana na dini ya haki aliyopewa Muhammad na waumi-

64

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

hiI ha"kunfiakinishwa katika ardhi.

Mayahudi waliposhindwa kuizuwia neema hii kwa waislamu, waliungana na washirikina dhidi ya waislam, wakaenezea propaganda dhidi ya uislamu na Mtume wake. Hatimaye uovu ukawazungukia wao na wakafukuzwa Hijaz kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

Basi tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa Ufalme mkubwa.

Makusudio ya Kitabu ni Zabur ya Daud, Taurat ya Musa na Injil ya Isa. Hekima ni Utume na elimu: maana yake kwa nini mnamhusudu Muhammad (s.a.w.) na waarabu kwa sababu ya Utume na kumakinika katika nchi? Mwenyezi Mungu amekwishawapa nyinyi mfano wa hayo katika waliopita; kama vile Yusuf, Daud na Suleiman.

Katika wao kuna waliomwamini na katika wao kuna waliojiepusha naye.

Wafasiri wametofautina katika dhamiri ya 'waliomwamini;' kuwa je ni kumwamini Muhammad (s.a.w.w.), au Ibrahim au Kitabu? Lenye nguvu zaidi ambalo linaafikiana na maana na kusaidiwa na kuzingatia ni kuwa dhamiri inamrudia kila Mtume aliyepewa Kitabu na hekima. Neno 'kila Mtume' hata kama halikutajwa katika Aya waziwazi, lakini linafahamika kutokana na mfumo wa maneno.

Kwa vyovyote iwavyo, hakuna tofauti kuwa maana ya Aya ni kwamba si jambo geni kwa hao na mfano wao kutomwamini Muhammad (s.a.w.). Kwani Mitume waliotangulia waliaminiwa na kikundi na wakakanushwa na kundi jingine. Na kundi la ukanushaji lilikuwa kubwa; kama asemavyo (s.w.t.): "... Wengine katika wao walikuwa waongofu na wengi katika wao walikuwa mafasiki." (57:26)

Jahannam yatosha kuwaunguza wale wapingao haki

65

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano '567H¥kıkâ'¥mbâö"wâmezTküifürİshâ"' Aya zetu tutawatia motoni; kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waonje adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na Mwenye hekima.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-49.jpg

57.Na ambao wameamini na waka-tenda amali njema, tutawaingiza katika pepo zenye kupita mito chini yake, ni wenye kudumu milele humo; wana humo wake waliotakaswa na tutawatia katika vivuli vya daima.

 Aya 56 - 57 KUBADILISHA NGOZI NYINGINE

Hakika ambao wamezikufuru Aya zetu tutawatia motoni; kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilisha ngozi nyingine.

Aya hii ni ubainifu wa mwisho wa Aya iliyotangulia. Na Jahannam yatosha kuwaunguza. Makusudio ya Aya hapa ni kila lililothibiti katika dini kwa dharu-ra; mfano ujuzi wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, Malaika, pepo moto na mengineyo yanayorudia kwenye misingi ya dini. Vilevile mfano wa wajibu wa kufunga, Swala, uharamu wa zina, pombe na mengineyo katika masuala ya kifiqhi na ya matawi ya dini.

66

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Hakuha"mweriyeshaka"kwamba"kük¥riüshâ"m"kukLi7ürüTWa je'kuWshak^'ni' kukufuru pia.? Hilo tumelifanyia utafiti kwa ufafanuzi, wakati wa kufasiri Aya 115 ya sura Al-imran kifungu 'mwenye kuacha uislam.'

Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni mwadilifu, hilo halina shaka. Anapoiunguza ngozi ya mwasi inaondoka na kuisha; kisha huumba ngozi nyingine mpya na kuiadhibu, je, huko si kuadhibui ngozi ambayo haikumuasi? Jambo ambalo halijuzu kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Imepokewa Hadith kutoka kwa Imam Jaffar as-Sadiq (a.s.) inayojibu swali hili: "Hakika ngozi ni hiyo hiyo, si nyingine. Akapiga mfano wa tofali unapolivun-javunja mpaka likawa mchanga, kisha ukalichanganya tena na maji na kutengeza tofali jipya. Hapo litakuwa ndio hilo hilo katika mada yake, lakini ni jengine katika sura yake.

Si mbali kuwa 'kubadilisha ngozi' ni fumbo la adhabu na uchungu wake. Katika hali zote ni kwamba linalopatikana kwetu ni kuamini uadilifu wa Mwenyezi Mungu na uweza wake. Ama ufafanuzi hatuna jukumu nao.

Ili waonje adhabu.

Yaani lililosababisha kubadilishwa ngozi ni kuhisi kwao adhabu ya kudumu. Aina hii ya adhabu inahusika na mkanushaji, na msihrikina na ambaye watu humwogopa kwa shari yake. Nasi daima, kufa na kupona, tuna imani ya Lailaaha illa illah, Muhammad rasuulu llah, na tunamfanyia uadui kila mwovu. Wanavyuoni wanasema: Watakaoingizwa motoni na wasitoke ni watano: Mwenye kudai uungu, kama vile Namrud na Fir'aun, mwenye kukanusha uungu moja kwa moja, mwenye kumfanyia Mungu washirika, mnafiki na muua-ji wa nafsi isiyo na hatia.

Kwa dhahiri ni kuwa mnafiki zaidi ni yule anayeleta vita kwa jina la mwenye kulinda amani; mwenye kuwafanya watumwa watu kwa jina la kuchunga uhuru; mwenye kunyang'anya chakula cha watu kwa jina la kunyanyua maisha yao na mwenye kueneza uovu kwa jina la maendeleo. Na ambao wameamini na wakatenda amali njema ...

Umetangulia mfano wa tafsir yake katika Sura Al-imran Aya 15. Kwa hiyo hai-hitaji tafsir.

67

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 58.Hakika Mwenyezi Mungu anawaamuru kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapo-hukumu baina ya watu muhuku-mu kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapa mawaidha mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia ni mwenye kuona.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-50.jpg

59.Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi. Na kama mkipingana katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake mkiwa mwamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hilo ni bora zaidi na mwisho mzuri.

 

Aya 58 - 59 UAMINIFU NA UADILIFU

Hakika Mwenyezi Mungu anawaamuru kurudishia amana kwa wenyewe.

Aya mbili zimekusanya wajibu wa kutekeleza amana na uadilifu katika huku-mu na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume na mwenye madaraka katika nyinyi. Zimekuja Hadith kadha na Aya kadhaa katika kuhimiza kuchunga amana na kuitekeleza kwa mwenyewe awe mwema au mwovu. Kwa sababu ni haki yake kama binadamu, sio kwa kuwa ni mwema au mwovu.

68

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi m

Mtume wala msikhini amana zenu ..." (8:27)

Mtume anasema: "Hana imani asiyekuwa na uaminifu, wala hana dini asiyekuwa na ahadi..." Lakini hakuna katika Qur'an wala Hadith - kwa tunavy-ojua - maelezo kamili ya amana. Tunavyofahamu ni kuwa amana ni dhamana iliyoko kwako kwa ajili ya mtu mwingine. Ni juu yako kuichunga na kuilinda na kuirudisha kwa mwenyewe anapoitaka kama ilivyo. Ukiizuia au kuirudisha pungufu, basi wewe ni mhaini wa hukumu ya Qur'an na Hadith.

Si lazima amana iwe ni kitu kinachoonekana, kama vile mali na kitabu, la inaweza kuwa ni siri, nasaha au kazi. Vilevile si lazima mwenyewe hiyo amana awe mtu hasa; inaweza kuwa ni dini au elimu, bali hata nafsi yako yenyewe ikawa ndiyo yenye amana.

Amana ya dini na elimu ni yale unayoyajua katika halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake na katika heri na shari. Amana hii itathibiti kwa kufanya unayoyajua. Ama amana ya nafsi yako iliyoko kwako, ni lile lililo la masilahi zaidi kwa dunia ya hiyo nafsi na akhera yake.

Kwa maneno mengine, mwaminifu ni yule anayetekeleza kwa ukamilifu bila ya upungufu, ni sawa aliyewajibisha wajibu huu ni dini, elimu, nchi, jamii au kitu chochote kingine.

Kwa hiyo basi amana sio muonjo ulio katika chakula au kinywaji hiki sio kile, au kuwa ni mwanamke huyu si yule wala sio wasifu unaowapendeza watu; kama upole, bali amana ni mshikamano wa maisha na msimamo wake ambao bila huo maisha hayaendi sawa.

Kwenye maana hayo Imam Ali (a.s.) ameishiria kwa kusema: "Amana ni nid-hamu ya umma"; yaani umma hautengenei mambo yake ila ikiwa kila mtu atatekeleza yanayotakikana kwake. Na amesema tena: "Ambaye siri yake haitofautiani na dhahiri yake na vitendo vyake havitofautiani na maneno yake, basi atakuwa ametekeleza amana na amewafanyia ikhlasi waja. Na mwenye kuipuuza amana akawa anafanya hiyana na wala asiepushe nafsi yake na dini yake kwa uhaini basi atakuwa amejiingiza katika fedheha duniani, na akhera atapata udhalili na fedheha. Na hakika hiyana kubwa ni kuuhaini umma, na fedheha kubwa ya utapeli ni kuutapeli umma."

Miongoni mwa dalili za kuutukuza uaminifu ni kauli ya mafakihi: "Mwenye kuu-tangazia vita uislamu na waislamu na akahalalisha damu zao na mali zao si

<ö> 69

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'kwa"chochote Via kwa küchükiâ'TâWhİd^basİ"m"hâ1'âll"mM'yake"nâ'dâmü'yake' wala haiwi halali amana yake."

Imam Zainul-abidin anasema: "Lau aliyemuua baba yangu angaliniwekea amana upanga aliomuulia, nisingelimuhini."

Mtu mmoja alimuuliza Imam Arridha; "Yahudi amenihini Dirham elfu; kisha faida yake ikaingia mikononi mwangu, Je, nimlipizie?" Imam akamjibu: "Ikiwa amekudhulumu usimdhulumu."

Katika riwaya nyingine amesema: "Ikiwa amekuhini usimuhini wala usijiingize katika aliyokufanyia." Siri katika hilo ni kwamba amana ni haki ya mwenyewe kwa sifa ya kuwa ni mtu sio kuwa ni mwislamu wala mshirikina au si mwema wala mwovu. Tutarudia kuelezea uaminifu tutakapofasiri Aya 72 ya Sura ya Ahzab.

Na mutapohukumu baina ya watu muhukumu kwa uadilifu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwajibisha kurudisha amana kwa wenyewe, amefuatisha wajibu wa uadilifu katika kuhukmu baina ya watu. Kwa sababu asiyechunga haki za watu, hana haki ya kuwa hakimu. Wajibu wa uadilifu siyo kwa hakimu tu, bali mtawala vile vile, na mtawala mwadilifu ni yule anayejishughulisha na nyanja zote za maisha; kama vile afya maendeleo, chakula na uhuru kwa wote.

Kabla ya kila kitu ni wajibu kutomwacha mtawala mwenye tamaa - mzalendo au asiyekuwa mzalendo - kutawala mambo ya watu. Matukio tuliyoyapitia yamethibitisha kwamba chimbuko la kwanza na la mwisho la matatizo yaliy-otufika ni kutokana na kuwarudisha wezi na wasiokuwa na ujuzi kwenye madaraka na vyeo vya juu.

Ama uadilifu wa hakimu unakuwa katika kuwafanyia kwake usawa watesi wawili katika kila kitu na kila mwenye haki kumpa haki yake, bila ya kuangalia dini yake na itikadi yake; urafiki wake na uadui wake au utukufu wake na uduni wake.

Katika Historia ya sheria hakuna sharia iliyojihimu na kulitilia mkazo hilo kuliko sheria ya Kiislam. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: "Mwenye kufanywa hakimu amechinjwa bila ya kisu." Anaonyesha kuwa wajibu wa hakimu ni mzito sana. Kwa sababu inabidi kupigana jihadi kwa nafsi yake na kufanya bidii ikiwa haki haiko. Na akasema tena: "Mahakimu ni watatu: waw-

70

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'İİİ'WâteküWâ"mötöm"nâ"mmoja'pepbni"..

Ama yule atakayekuwa peponi, ni yule aliyejua haki akaihukmu, na wale waw-ili wataokuwa motoni ni aliyewahukumu watu bila ya ujuzi na aliyekuwa anai-jua haki, lakini akahukmu kinyume chake."

Hakika mwenyezi Mungu anawapa mawaidha mazuri sana.

Makusudio ya mawaidha hapa ni amri ya kurudisha amana. Neno 'mazuri' linatambulisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) haamrishi ila ambalo ndani yake mna kheri na masilahi.

WENYE MAMLAKA NI NANI

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mam-laka katika nyinyi.

Maneno na mabishano yamekuwa mengi kuhusu makusudio ya 'wenye mam-laka' na sifa zao; kama ambavyo watawala wamejibandika nayo kuwa ni wajibu kuwatii au angalau kuwanyamazia.

Vile vile kundi la mafakihi limetoa dalili kwa Aya hiyo kuwa chimbuko la sharia na misingi yake linathibiti kwa mambo manne:

1.    Kitabu cha Mwenyezi Mungu; kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mtiini Mwenyezi Mungu."

2.    Hadith za Mtume; kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na mtiini Mtume."

3.    Ijmai; kutokana na kauli yake: "Na wenye mamlaka"

4 Kiyasi; kutokana na kauli yake: "kama mkizozana katika jambo basi lirud-isheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume." Wakadai kwamba maana lik-isieni lile lisilo na nukuu (nassi) kutoka katika Qur'an na Hadith. Utakuja ufafanuzi wa hilo.

Hakuna tofauti kuwa Qur'an na Hadith ni machimbuko ya msingi ya sharia. Ama Ijmai na Kiyasi wametofautiana katika hoja yake na katika ufahamisho wa Aya juu yake.

Yafuatayo ni madhumuni ya Aya na rai zilizosemewa Aya hiyo:

1. Hakuna waliotafoutiana katika waislam kwamba kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume kunakuwa ni kufanya amali kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na

$& 71

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

..Hadith za Mtume wake na kwa

Mwenye kumtii Mtume basi amemtii Mwenyezi Mungu. (4:80) Alichowaletea Mtume kichukueni na alichowakataza kiacheni. (59:7) Wala hasemi kwa matamanio; hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa. (53: 3-4)

Kuanzia hapo ndio wameafikiana waislam kwa kauli moja kukataa kila linalonasibishwa kwa Mtume (s.a.w.) kama linapingana na msingi katika misingi ya Qur'an na hukumu zake.

Unaweza kuuliza: Kwa nini kukaririka neno utiifu katika kumtaja Mtume na wala halikukaririka wakati wa kutaja wenye mamlaka?

Jibu: Ni kwa ajili ya kutanabahisha kwamba kumtii Mtume ndio asili kwa dhati yake; sawa na kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo ndiyo ikawa kauli ya kila mmoja wao ni chimbuko katika machimbuko ya sharia, lakini si hivyo katika kuwatii wenye mamlaka. Bali ni tawi la kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume. Hakika wenye mamlaka ni wapokezi wa Mtume.

2.  Neno miongoni mwenu, linafahamisha kwa uwazi wazi kwamba hakimu wa waislam anapasa awe ni miongoni mwao, wala haifai kabisa kuwa si miongoni

mwao. Hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu.

Na Mwenyezi Mungu hatawafanyia makafiri njia ya kuwashinda waumini. (

4:141)

3.   Wametofautiana katika makusudio ya wenye mamlaka baada ya kuafikiana kwao juu ya sharti la uislam; kuna waliosema: Ni makhalifa (Khulafau rrashidun). Na waliosema kuwa ni makamanda wa jeshi. Na wengine wakasema ni maulama wa kidini. Sheikh Muhammad Abduh amesema: Wao ni machifu watawala, maulama, viongozi wa jeshi na viongozi wengi-neo ambao watu wanawarudia katika haja na masilahi. Wakiafikiana hawa juu ya jambo, ni wajibu kuwatii kwa sharti ya kuwa wawe waaminifu na wasihalifu amri ya Mwenyezi Mungu wala Sunna ya Mtume wake. Na wawe na hiyari katika utafiti wao wa amri na kuafikiana kwao.

Shia wamesema kuwa Mwenyezi Mungu ameunganisha kwa herufi 'Wau' baina ya kuwatii wenye mamlaka na kumtii Mtume bila ya sharti lolote; na kuunganishwa kwa herufi 'Wau' kunahukumia kuchanganya na kushirikiana katika hukumu. Maana ya haya ni kuwa kuwatii wenye mamlaka ni kumtii

72

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Mtüme"h¥'kwâmba'iamn"yaö"hl"¥mri"yâke..

Hakuna mwenye shaka kwamba daraja hii tukufu haiwi ila kwa anayesifika na kustahiki twaa hii na hakuna kitu kitakachomfanya astahiki hayo isipokuwa kuhifadhika na makosa na maasi (isma). Ndiko pekee kunakokufanya kumtii yeye na kumtii Mtume kuwe sawa.

Arrazi amekiri waziwazi fikra ya Isma kwa kusema kuwa wenye mamlaka ambao ni wajibu kuwatii hapana budi wawe ni maasumin (waliohifadhiwa na dhambi). Na Arrazi - kama anavyojulikana - ni miongoni mwa maulama wakubwa wa kisunni; mwanafalsafa na mfasiri wao. Haya ndiyo aliyoyasema ninamnukuu;

"Jua kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu, 'wenye mamlaka inafahamisha kwetu kwamba Ijmai ni hoja. Dalili ya hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha kutiiwa wenye mamlaka moja kwa moja katika Aya hii. Na ambaye Mwenyezi Mungu anaamrisha atiiwe hapana budi awe amehifadhiwa na makosa. Kwa sababu lau asingelikuwa amehifadhiwa na makosa basi itakuwa anakadiriwa kufanya makosa, ambapo Mwenyezi Mungu ameamrisha afuatwe. Kwa hiyo hilo litakuwa ni kuamrisha kufanywa makosa; na inaju-likana kwamba kumfuata mwenye makosa kumekatazwa. Kwa hiyo imethibiti kwamba makusudio ya wenye mamlaka waliotajwa katika Aya hapana budi wawe wamehifadhiwa na makosa."

Hivi ndivyo walivyosema Shia katika kufasiri Aya hii. Tofauti iliyoko kati yao na Sunni ni katika kufuatilia na kumwainisha huyo mwenye kuhifadhiwa na makosa (maasum). Sunni wanasema kuhifadhiwa ni kwa umma. Wamefasiri umma kuwa ni watatuzi. Wengi wao wakasema ni baadhi ya watatuzi. Shia wamesema kuwa makusudio ya wenye mamlaka ni Ahlul-bayt ambao wametakaswa na makosa na kutwahirishwa na uchafu.

Kwa hiyo fikra ya Isma haihusiki na Shia tu, na wala sio waliosema peke yao, bali iko kwa Sunni; kama ambavyo iko kwa Shia. Hivyo kuchukulia kuwa shia tu ndio waliosema kauli hiyo ni kwa ajili ya ukaidi tu, na kueneza utengano.

Shia wametoa dalili juu ya Isma kwa Ahlul-baiti, kwamba ni kipawa cha Mwenyezi Mungu. Anawahusu watu anaowaridhia miongoni mwa waja wake. Haiwezekani mtu kuitafuta mwenyewe Isma kwa namna yoyote atakavyojitahi-di; kinyume na sifa nyingine. Kwa hiyo njia ya kujua Isma inajulikana kwa wahyi tu. Na imethibiti kauli wazi katika Qur'an na Hadith juu ya Isma ya Ahlul-

73

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

bait. Miongoni kwa hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu (Enyi) Ahlul-baiti na kuwatakasa kabisa kabisa." (33:33)

Pia kauli yake Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenye kunitii mimi ndio amemtii Mwenyezi Mungu; na mwenye kuniasi amemuasi Mwenyezi Mungu; na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, ndio amenitii mimi na mwenye kumwasi ameniasi mimi." Ameipokea Hakim katika Mustadrak na akasema: "Hii ni Hadith sahihi."

Vilevile ameisahihisha Dhahabiy katika Tal-khisu al-mustadrka. Katika kitabu hicho kuna hadith ya Mtume (s.a.w.) amesema: "Ali yuko pamoja na Qur'an na Qur'an iko pamoja na Ali, viwili hivyo havitatengana mpaka vinijie katika Birika."

Vile vile amepokea Tirmidhi katika Musnad yake, Hakim katika Mustadrak yake na Ibn Hajar katika Sawaiq yake kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.) kwam-ba yeye amesema: "Ewe Mola wangu izungushe haki pamoja na Ali popote aendapo." Pia Imam Ibn Hambal, Tirmidhi, Hakima na Ibn Hajar, wamepokea kauli yake Mtume (s.a.w.): " Mimi nawaachia vitu ambavyo kama mkishika-mana navyo hamtapotea baada yangu, navyo ni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-bait wangu."

Imekuwa mashuhuri Hadith kutoka kwa Mtume isemayo: "Hakika mfano wa Ahlul-bait wangu kwenu ni kama mfano wa safina ya Nuh, mwenye kuipanda ataokoka." Na Hadithi nyinginezo nyingi. Zote hizo zimeandikwa katika vitabu vya Hadith vya Sunni na sahih zao, na zimepokewa na wategemewa wao.

Shia wamezikusanya na kuziwekea vitabu maalum vya zamani na vya kisasa. Vya zamani ni kama Kitab shafi cha Shariff Murtadha, Tal-khisu shafi cha Sheikh Tusi, Nahjul-haq cha Allama Hilli na katika Hadith za Mujallad wa tatu katika A'yanusha Shia cha Sayyid Muhsin Amin. Vile vile Dalailus-swidq cha Sheikh Mudhaffir na Muraja't cha Sharafuddin.

74

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kwa ujumla ni kwamba Shia

msingi*7 Vile vile wameafikiana Shia na Sunni wengi kwamba wenye mamla-ka waliotajwa katika Aya wamehifadhiwa na dhambi. Pia wanaafikiana kwamba dalili ya kuhifadhiwa kwao ni kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha wati-iwe kama alivyowajibisha kutiiwa yeye Mwenyezi Mungu na Mtume. Lakini Sunni wakatofautiana na Shia kuwa makusudio ya wenye mamlaka waliohi-fadhiwa na makosa, ni watatutuzi wa mambo au ni Ahlul-bait?

Sunni wakasema ni watatuzi wa mambo. Shia wakasema ni Ahlul-bait. Kwa sababu Isma ni kipawa cha Mwenyezi Mungu, hakijulikani ila kwa kauli wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume. Na imethibiti kauli kutokana nao juu ya Isma ya Ahlul-bait. Kwa hiyo makusudio ya wenye mamlaka ni Ahlul-bait si wengineyo.

Kwa maneno mengine ni kuwa wenye mamlaka katika Aya ni wenye kuhifadhiwa na makosa kwa sababu ya wajibu wa kuwatii wao. Kwa sababu ambaye ni wajibu kumtii ni maasum. Vile vile kunathibiti kuhifadhiwa kwa Ahlul-baiti kwa kauli wazi na hakukukuthibiti kwa wengineo. Na ambaye kumethibiti kuhifadhiwa kwake, basi ni wajibu kumtii. Kwa hiyo natija ni kuwa Ahlul-baiti ndio wenye mamlaka si wengineo. Kama kusema: Msikilize mwenye kunasihi aliye mwaminifu, wala hakuna mwaminifu ila Zaid. Kwa hiyo natija ni msikilize Zaid.

Katika ambayo wameyatolea dalili Shia juu ya kutojuzu kuwafuata watatuzi katika mambo ya kidini ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Lakini watu wengi hawajui." Na kauli yake: "Na wengi wao hawaelewi." (5:103)

Maana ya haya ni kuwa haki haijulikani kwa kuangalia idadi ya watu, wawe wengi au wachache isipokuwa hujulikana kwa kuchukuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake na hukumu ya kiakili ya msingi ambayo hakuna wanaotofautiana, - Kwa kuongeza - ninaandika maneno haya katika mwezi Machi 1968 na uchaguzi wa wabunge wa Lebanon umeuma mchanga;

*7Fikra ya kuhifadhiwa na makosa (Isma) haihusiki na Shia wala Sunni. Wakristo pia wamesema kwamba Baba mtakatifu amehifadhiwa na makosa. Wakomunist wamesema ni Max na Lenin. Wachina wakasema ni Mao tse Tung. Ikhwanul muslimin wakasema ni Hassan Al-banna. Qaumiyyun wa Syira wakasema ni Anton Saada. Namna hii kila kikundi kinasema kuwa rais wake na mwasisi wake aliyeweka misingi anahifadhiwa na makosa (maasum). Tumezungumza kwa urefu kuhusu Isma katika kufasiri sura ya 2: 124.

75

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

watu wanasongamana kwenye masanduku ya kura ili wamchague aliyenunua sauti za watu baada ya mnada, au yule aliyewaahidi watu wake kutekeleza matakwa yao. Salaam zimfikie yule aliyesifu baadhi ya uchaguzi kwa kusema: "Mtu anaitikiwa pamoja na ukorofi wake. Mwengine anafuatwa kwa sababu ya udugu pamoja na maovu chungu nzima aliyonayo."

Mwengine akasema: "Ni wachungwa mazuzu wanaufata kila sauti ya mchun-gaji. Ni bendera wanafuata upepo. Hawakupata mwanga wa elimu wala hawakuegemea nguzo thabiti."

Na kama mkipingana katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Tumetangulia kusema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume - kwa maafikiano ya wote inafahamisha kushikamana na Qur'an na Hadithi; na kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu. Na wenye mamlaka katika nyinyi, inafahamisha - kwa shia - wajibu wa kuwatii Ahlul-bait; na kwa sunni wengi inafahamisha kuwatii watatuzi wa mambo. Sasa tuzungumzie kauli hii, 'Na kama mkipingana.' Je inafahamisha wajibu wa kutumia kiasi au iko mbali na hayo? Kabla ya jawabu tutupe swali hili:

Kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibisha kurudishwa mapingano Kwake na kwa Mtume tu, bila ya wenye mamlaka, ambapo Yeye amewajibisha kuwatii wote watatu?

Jibu: Kwa sababu mzozo huenda ukatokea katika kuwajua hao wenye mamlaka; kama ambavyo limetokea hilo. Sunni wakasema: Ni watatuzi wa mambo na Shia wakasema ni Ahlul-bait. Kwa hiyo katika mzozo huu inabidi kurudia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadith za Mtume wake. Kwa ajili hiyo ndio Shia wakatoa dalili Aya ya tat-hir *8 na Hadith.

Sasa turudie kwenye wajibu wa kutumia kiasi au kutotumia. (Qiyas), ni kutoa hukumu ya tukio iliyoelezwa wazi na sharia kwa tukio jengine ambalo hukumu yake haikuelezwa wazi; kwa kushirikiana matukio mawili katika sababu zilizotolewa na fakihi. Mfano sheria, imeeleza kuwa nyanya wa upande wa mama anarithi na wala isielezwe wa upande wa baba. Tukamrithisha nyanya wa upande wa baba kwa kuchukulia kiasi cha wa upande wa mama. Kwa sababu wote ni nyanya.

*8Aya (33: 33)

$& 76

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Sühhi wairo^

jambo lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume inafahamisha kusihi qiyasi; kuwa maana yake ni lirudisheni kwenye tukio alilolibainisha Mwenyezi Mungu hukumu yake; yaani linalofanana nalo.

Shia wamesema kuwa Aya iko mbali kabisa na qiasi wala haifahamishi zaidi ya kurudia Qur'an na Hadith katika masuala ya kidini inapotokea tofauti baina ya mafakihi. Na kauli za maimamu walio maasum zinaingia katika hadith. Kwa sababu ni riwaya kutoka kwa babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)

Ama njia yao katika ambalo halikuelezwa wazi katika Kitab wala Hadith ni kurudia kwenye hukumu ya akili ya mkato iliyo dhahiri ambayo haiwezi kuto-fautiana. Mfano ubaya wa mateso bila ya ubainifu; na ambayo wajibu hautimii ila kwalo, basi ni wajib. Kwa hiyo qiasi sio katika kauli hii.

Kwa sababu natija zake zote ni za kudhania; na dhana haitoshelezi kitu*9.

Katika waliyoyatolea dalili Shia kuhusu kubatilika kwa qiyas ni kwamba mambo ya kawaida, inasihi kuyafanyia qiyas. Kwa vile sababu zake ziko kwenye ukawaida. Ama hukumu za kidini haisihi kufanya qiyas. Kwa sababu sharia imekusanya pamoja vitu vinavyotofautiana; kama katika mambo yanayovunja udhu ambapo imeweka sawa kulala na kukojoa.

Mkiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Mwenye Majmau anasema: "Ni ubainifu wa uwazi ulioje wa kauli hii!" Nasi twasema: Ni uzuri ulioje wa tafsir wa hiyo!

Hilo ni bora zaidi na mwisho mzuri

Yaani kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, na kuirudisha hukumu ya kutofau-tiana kwa Qur'an na Hadith ni mwisho mzuri. Hii ni ikiwa tutalifasiri neno Taawil katika Aya hii kwa maana ya mwishilio.

Imesemekana kuwa makusudio ya neno Taawil hapa ni tafsiri ambapo maana yatakuwa ni tafsir ya Mwenyezi Mungu na Mtume katika mnayopingana ni bora na nzuri kuliko tafsiri yenu. Vyovyote iwavyo neno Taawil linachukua maana zote mbili.

*9 Haya ndiyo waliyo nayo Shia hivi leo. Lakini yaliyokuwepo wakati wa Amirul-mumin kwa Malik Ashtar, ni kwamba kurudisha kwa Mwenyezi Mungu katika Aya ni kuchukua kauli wazi katika Kitab cha Mwenyezi Mungu; na kurudisha kwa Mtume ni kuchukua Hadith zake ambazo Waislam wamekubaliana kuwa ni zake.

<ö> 77

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 60.Je, huwaoni wale wanaodai kuwa wao wanaamini uliy-oteremshiwa wewe na yalioteremshwa kabla yako, wanataka kwenda kuhukumiana kwa taghut na hali wameamr-ishwa wamkatae. Na Shetani anataka kuwapoteza upotevu wa mbali.

61.Na wakiambiwa njooni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume, utawaona wanafiki wanajizuia na kukupa mgongo.

62.Basi itakuwaje watakapopatwa na msiba kwa yaliyotangulizwa na mikono yao kisha wakakujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu (wakisema):         Hakika sisi

hatukupendelea ila wema na mapatano.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-51.jpg

78

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-52.jpg

63.Hao ni ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika nyoyo zao. Basi achana nao na uwape mawaidha na uwaambie maneno yatakayoingia katika nafsi zao.

WANATAKA KUHUKUMIANA KWA UBATILIFU Aya 60 - 63

Je, huwaoni wale wanaodai kuwa wao wanaamini uliyoteremshiwa wewe na yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka kwenda kuhukumiana kwa taghuti na hali wameamrishwa wamkatae.

Je huwaoni, ni msemo unaoelekezwa kwa Mtume (s.a.w.) kwa njia ya swali ukiwa na makusudio ya kustaajabia hali ya wanafiki, walioficha ukafiri na kud-hihirisha uislam na kuamini vitabu vya Mwenyezi Mungu. La kustaajabu ni kwamba wao wanajikadhibisha wenyewe; pale walipokataa kuhukumiwa kwenye haki na kwenda kwenye batili; pamoja na kuwa uislam umewaamrisha kujiepusha na upotevu na wabatilifu.

Mwenye Majmaul-bayan, anasema: aligombana yahudi na mnafiki katika waislam, yahudi akasema: "Tukahukumiwe kwa Muhammad." Kwa sababu alikuwa anajua kuwa Muhammad hakubali rushwa wala hafanyi dhulma. Mnafiki akasema: "Si yuko Kaabul-Ashraf," (yahudi) kwa sababu alijua kuwa Ka'ab anachukua rushwa na anadhulumu katika hukumu.

Pamoja na kuwa wafasiri hawathibitishi sababu ya kushuka Aya hii, hatuoni mfano unaofasiri makusudio ya Aya ulio wazi kuliko tukio hili aliolitaja mwenye Majmaul-bayan. Mnafiki alikataa kuhukumiwa na Mtume (s.a.w.), kwa sababu anamkanusha yeye na dini yake. Ama yahudi anaamini uyahudi, lakini pamoja na hayo alikataa kuhukumiwa kwa yahudi mwenzake na akataka kuhukumiwa kwa Mtume (s.a.w.) pamoja na kuwa anamkanusha yeye na dini yake, Siri ilikuwa ni manufaa tu. Dhahiri hii haihusiki na yahudi tu, yeyote mwenye kupata manufaa katika dini

<ö> 79

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

au msingi wowote, haitakikani kumtegemea wala dini yak

hani. Kwa sababu watu wengi wanakabidhiwa maelfu na kuishi vizuri, si kwa lolote ila kwa kuaminiwa tu. Huenda hao ndio wanaoambiwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Na miongoni mwa watu kuna wanaomwabudu Mwenyezi Mungu ukingoni. Ikiwafika kheri hutulia kwayo na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amepata hasara ya dunia na khera." (22: 11)

Imam Ali (a.s.) amesema: "Sifa ni baada ya misukosuko." Mtoto wake, Husein (a.s.) naye anasema: "Watu ni watumwa wa dunia, dini iko juu juu tu ya ndimi zao. Wakipatwa na misukosuko huwa wachache wenye dini." Mtume Mtukufu naye alikuwa akisema katika raha: "Sifa njema ni za mwenye kuneemesha mwenye kuzidisha." Na wakati wa shida husema: "Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa kila hali."

Akionyesha kuwa mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu yuko radhi kwa aliyokadiriwa hata katika hali hii; sawa na mtoto mwema anayebakia kumsafia nia mzazi wake hata katika hali ya kutiwa adabu. Na mjukuu wake Imam Zainul-abidin (a.s.) alikuwa akisema miongoni mwa anayoyasema anapopat-wa na shida: "Ewe Mola wangu! Ni ipi katika ya hali mbili ambayo nina haki zaidi ya kukushukuru? Ni ipi kati ya nyakati mbili ambayo ni bora zaidi kukusi-fu? Je ni wakati wa uzima uliponipa afya; au ni wakati wa ugonjwa uliponipa-ta? Ewe Mola wangu! Jaalia kutoka kwangu kwenye ugonjwa kuwa ni msamaha wako na kusilimika kwangu na shida hii kuwa ni faraja iliyotoka kwako."

Na shetani anataka kuwapoteza upotevu wa mbali.

Hii ni dalili ya wazi kwamba shari inatokana na shetani si kwa Mwenyezi Mungu. Na kila fikra inayokupelekea kufanya shari huitwa shetani. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Ambaye hutia wasiwasi katika nyoyo za watu katika majini na watu. (114: 5 - 6)

Na kuna Hadith isemayo: "Shetani akikwambia: Ni wingi ulioje wa swala yako! Mwambie, kughafilika kwangu ni zaidi. Na akikwambia ni wingi ulioje wa mema yako! Mwambie maovu yangu ni zaidi. Na akikwambia ni wingi ulioje wa waliokudhulumu mwambie: Nilio wadhulumu ni wengi zaidi." Kwa dhahiri ni kuwa nafsi ndiyo inayompa picha mtu kwamba yeye ni mfanya ibada sana, mtenda mema na mwenye kudhulumiwa. Wala hahadaiki kwa

80

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

übâtiİİfü hüü Îİa"mjfriğ'â'...

Na wakiambiwa njooni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume utawaona wanafiki wanajizuia na kukupa mgongo.

Kwa sababu wao hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Mtume wake wala kitu chochote isipokuwa dunia.

Basi itakuwaje watakapopatwa na msiba kwa yaliyotangulizwa na mikono yao.

Na msiba mkubwa zaidi kwa wanafiki ni kufunuka mambo yao na kufichuka siri yao hadharani, ambapo wanajulikana na watu kwa hiyana, uongo, vitimbi, hadaa, woga na utwevu.

Kisha wanakujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu (wakisema): Hakika sisi hatukupendelea ila wema na mapatano.

Wanamjia Mtume wakinyenyekea wakitoa sababu za uongo; na Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na watu wanajua kwamba wanafiki ni waongo na kwam-ba wao wanafanya viapo vyao ni ngao ya fedheha na kuadhibiwa.

Basi achana nao.

Yaani wapuuze, usiwakubalie udhuru kwa sababu wao wanachukulia kukubali kwako huku katika malengo yao. Wala usiwaadhibu kwa sababu wametoa udhuru japokuwa kwa dhahiri.

Na wape mawaidha na waambie maneno yatakayoingia katika nafsi zao.

Mtume (s.a.w.) alikuwa akiwaamuru kumcha Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo wanahisi kuwa wao ni wakosaji na kwamba ni juu yao kujisafisha kwa kutubia. Huu ndio msingi wa uislamu kwa kila mwenye makosa, haumfanyii haraka kumwadhibu wala kumkatisha tamaa, bali hutumia njia zote za kumten-geneza. Mwenyezi Mungu anasema:

"Nendeni kwa Firaun, hakika yeye amepetuka mipaka. Kamwambieni maneno laini huenda akawaidhika au ataogopa " (20: 44)

Imam, Amirul-muminin anasema: "Fakihi aliyekamilika ufakihi wake, ni yule asiyewakatisha tamaa watu na rehema ya Mwenyezi Mungu na asiyewavunja moyo kabisa na rehma ya Mwenyezi Mungu na kutowapa amani ya kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu."

Chimbuko la hekima hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu: "Sema enyi waja

<ö> 81

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

'w¥riğu"mTföjîdhü1'ümü"nafei"'zenü!" Mungu" (39:53).

64.Na hatukumpeleka Mtume ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi          Mungu          na

wakaombewa maghufira na Mtume,                wangelimkuta

Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakabali toba na mwenye kurehemu.

65.Naapa kwa Mola wako! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu katika yale wanayohitalifiana baina yao. Kisha wasione dhiki katika nyoyo zao kwa uliyohukumu na wanyenyekee kabisa kabisa.

4. Sura An-Nisaa

66.Na lau kama tungewalazimisha kuwa jiueni au tokeni katika miji yenu, wasingelifanya hilo isipokuwa wachache katika wao. Na lau kama wangelifanya yale waliyoagizwa, ingelikuwa heri kwao na uthibisho wa nguvu zaidi.

Kaashif5-53.jpgKaashif5-54.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-55.jpg

67.Na hapo tungewapa malipo makubwa kutoka kwetu.

68.Na tungewaongoza njia iliyony-ooka.

69.Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao (watakuwa) pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na wasadikishaji na mashahidi na watu wema. Na hao ndio marafiki wema.

70.Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na anatosha Mwenyezi Mjuzi.

Aya 64 - 70 HATUKUPELEKA MTUME ILA ATIIWE

Na hatukumpeleka Mtume ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza: Habari hii ni kama kufafanua ufafanuzi. Kwa sababu kumtegemeza Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenyewe kunafahamisha kuwa amepelekwa ili atiiwe, vinginevyo kutegemezwa kusingelikuwa na maana. Basi je ubainifu una makusudio gani?

Jibu: Makusudio ni kutoa hoja kwa wanafiki waliomwasi Mtume na kukataa kuhukumiwa naye. Hoja yenyewe ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ame-wabainishia wanafiki na wengineo katika Aya hii kuwa kumwasi Mtume sio kumwasi yeye hasa, bali ni kumwasi Mwenyezi Mungu. Ambapo amekataa

83

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

mambo yasipitie isipoku

kufikisha hukumu zake kwa waja wake kupitia Mtume atokanaye na wao.

Kwa hiyo basi mwenye kumpinga katika anayoyafikisha miongoni mwa hukumu za Mwenyezi Mungu, atakuwa amempinga Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo natija ni kuwa wanafiki na kila anayemwasi Mwenyezi Mungu wanastahili adhabu. Kwa sababu wanamwasi na kumkhalifu.Mwenyezi Mungu

Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakaombewa maghufira na Mtume, wangemku-ta Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakabali toba mwenye kurehemu.

Wamejidhulumu pale walipojiingiza katika adhabu na maangamizi kutokana na dhambi walizozifanya. Wamemdhulumu Mwenyezi Mungu vilevile kwa kupetuka mipaka yake na kuasi amri zake. Pia wamemdhulumu Mtume kwa kuwa wao wamekataa hukumu yake na kuridhia hukumu ya ubatilifu na kum-wonyesha kinyume na dhamira zao.

Pamoja na yote hayo bado Mwenyezi Mungu amewafungulia mlango wa toba. Ni juu yao basi kuuelekea na kutaka maghufira. Wakifanya hivyo atawaingiza kwenye rehema yake. Na wakitofanya, basi hawatapata wa kuwanusuru wala wa kumsaidia zaidi ya Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu, 'Na wakaombewa maghufira na Mtume; inapingana na misingi ya kiislam ambayo inapinga kuwe na wasita baina ya Mwenyezi Mungu na watu?

Jibu: Ni kweli kuwa hakuna wasita baina ya Mwenyezi Mungu na waja wake ila katika mambo yanayorudia kwenye haki yake Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumkosea Yeye. Ama kukosea haki za watu, basi amri ni yao; na msamaha wake unaombwa kwao si kwengine. Na wanafiki walimwudhi Mtume na kumkosea haki yake. Hivyo ikawa hakuna budi katika toba yao ila kudhihirisha majuto kwake na kumwomba msamaha. Na kila unayemdhihirishia kinyume cha dhamira yako basi umemdhulumu na kumkosea. Bali lau mtu fulani alikudhania sifa nzuri usizo nazo na akakuamini kisha ukamfanya mjinga na tena ukamkimbia, basi wewe ni dhalimu.

Naapa kwa Mola wako! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu katika yale wanayohitalifiana baina yao.

Kwa sababu hukumu zote anazozitamka Muhammad, hazitokani na yeye, isipokuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na yeye Mtume ni mse-

<ö> 84

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

maji wake.

Kisha wasione dhiki katika nyoyo zao kwa uliyohukumu na wanyeyekee kabisa kabisa.

Maana yake ni kuwa wao hawatakuwa waumini mpaka wajue kwa yakini kwamba hukumu yake ni hukumu ya Mwenyezi Mungu hasa, na anayekupin-ga wewe ndio amempinga Mwenyezi Mungu. Ni muhali kwa Muumin wa kweli kuhisi dhiki kwa hukumu anayojua kuwa inatokana na Mwenyezi Mungu.

Ndio ni kweli muumin anaweza kutaka baina ya nafsi yake kuwa kula mchana mwezi wa Ramadhan kuwe halali, lakini pamoja na hayo anafunga na kujizuil-ia kula kwa kuhofia adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo ni kali na ya masha-ka zaidi ya kufunga. Na huenda nafsi yake ikamshinda na maasi, lakini yeye anavumilia na kuilaani, kwa sababu itakuwa imepuuza haki. Hii ndiyo imani hasa.

Na lau kama tungewalazimisha kuwa jiueni au tokeni katika miji yenu, wasingefanya hilo isipokuwa wachache katika wao.

Hakika dini ya Mwenyezi Mungu ina wasaa, nyepesi na ni bora na ya uten-genefu. Haimkalifishi yeyote zaidi ya uwezo wake, bila ya manufaa yake ya kidini na ya kidunia. Mwenyezi Mungu anasema: "Wala hakuweka mambo mazito katika dini." (22: 78)

Na amesema tena: "Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika yatakayowapa uhai." (8:24)

Unaweza kuuliza: Ikiwa mambo ni hivyo, basi hakuna wajihi wa kauli yake Mwenyezi Mungu (Na lau kama tungewalazimisha kuwa jiueni...) kwa sababu hii ni amri ya lisilowezekana?

Jibu: Hii ni kiasi cha kukadiria tu, na ndio maana limekuja neno "lau" linalofa-hamisha kuzuilika jambo kwa kuzuilika jengine.

Makusudio ya kukadiria huku ni kubainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba wanafiki hawana udhuru kabisa katika kuzifanyia inadi hukumu zake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ambazo hakuna mashaka wala kujiangamiza, bali ni rehema kwao.

Lakini pamoja na haya yote waliasi.

Ikiwa wanafiki wameasi na kuzigomea hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu

85

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"pamoja ha"wepesi"üİ]bmbrbasl'"kâti'ka"Mâsâh¥bia"wa"Mtüme"(s\'â\'w.)..kuria"

ambao lau wangeliamrishwa kujiua wangelifanya. Nao Mwenyezi Mungu amewaelezea kuwa ni wachache. Miongoni mwa wachache hao ni Yasir na mkewe, ambao walikufa shahid katika adhabu kwa ajili ya Uislam. Hao ni wazazi wa Ammar aliyeuliwa na kikundi kiovu siku ya vita vya Siffin. Alikuwa katika munajat akimwambia Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Ewe Mola wangu! Hakika wewe unajua lau ikiwa mimi ninajua kuwa kukuridhisha ni kuki-ta upanga wangu huu kifuani mwangu na utokeze mgongoni mwangu, ningeli-fanya."

Na lau kama wangefanya yale waliyoagizwa, ingekuwa heri kwao na uthibitsho wa nguvu zaidi.

Makusudio ya waliyoagizwa, ni kumtii Mwenyezi Mungu katika amri zake na makatazo yake, "... Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amefanikiwa mafanikio makubwa." (33: 71)

Makusudio ya kuthibitisha ni kuthubutisha imani. Imam Ali (a.s.) anasema: "Katika imani kuna zilizo thabiti katika nyoyo na kuna zilizokaa kombo kwenye nyoyo kwa muda maalum."

Na hivi ndivyo alivyofasiri Imam as-Sadiq (a.s.) kauli yake Mwenyezi Mungu: "...Pako mahali pa kutulia pa kupita njia (6:98)

Na hapo tungewapa malipo makubwa kutoka kwetu.

Huu ndio ubainifu wa kheri katika kauli yake: "ingelikuwa kheri kwao" na kila malipo ya Mwenyezi Mungu na thawabu zake ni kubwa, hata yakiwa machache, sikwambii akiyasifu kwa ukubwa.

Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume basi hao (watakuwa) pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na wasadikishaji na mashahidi na watu wema. Na hao ndio marafiki wema.

Aya hii ni kutilia mkazo Aya iliyotanguilia na kuhimiza imani na wema ambao utamfanya mtu kuwa ni rafiki wa Mitume, mashahidi na watu wema.

NI NANI WASADIKISHAJI?

Sheikh Muhammad Abduh anasema: "Wasadikishaji ni wale walio na maum-bile matakatifu, kiasi kwamba wao wanaipambanua haki na batili, heri na shari kwa kuiona tu."

86

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kauli hii iko kâribü ria kis

nafsi yake ataijua haki bila ya kujifundisha. Ilivyo hasa ni kufasiri wasadik-ishaje kuwa ni Maasum (walio hifadhiwa na makosa) waliokamilika na wanaokamilisha, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewajaalia katika daraja ya pili kutoka Mitume bila ya kuweko kitu kingine. Na daraja hii haitakuwa kabisa kwa ambaye inajuzu kwake kukosea. Kwa sababu anayeweza kufanya makosa, hawezi kuwa mkamilifu wa mwengine kwenye ukamilifu wa uhakika. Bali atahitajia mkamilifu wa kihakika atakayemrudisha kwenye usawa. Na mkamilifu huyu ni Masum.

Kwa maneno mengine wasadikishaji wako aina mbili: Wa kwanza, ni yule asiyekusudia kusema uongo, lakini inawezekana kusema akakosa au kutatizika; kama mwenye kuelezea jambo mwenyewe akiamini ni mkweli katika anayoyaelezea, kisha ikabainika kwa habari yake si kweli. Hapo anakuwa mkweli katika makusudio yake na habari yake ni ya uongo. Haya hutokea mara nyingi.

Wa pili ni yule asiyekusudia uongo na wala hawezi kukosea, kiasi ambacho habari yake haikhalifu matukio kwa hali yoyote. Haya ndiyo makusudio ya wasadikishaji katika Aya hii na ya Wenye mamlaka katika Aya 59 ya sura hii. Kwa hiyo inakuwa makusudio ya wenye mamlaka na wakweli ni Ahlul -bait.

Vilevile Sheikh Muhammad Abduh amesema: "Makusudio ya mashahidi hapa ni watu wa uadilifu na wanaochunga haki, ambao wanaitilia nguvu haki kwa kuitolea ushahidi kuwa wao ni watu wa haki na kuwatolea ushahidi wabatili-fu kuwa wao ni wabatilifu."

Hii ni kulifanyia taawili tamko lililo dhahiri bila dalili yoyote. Kwani inavyofa-hamika mashahidi ni wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu na haki. Ni kweli kuwa iko Hadith isemayo: Wino wa maulama ni kama damu za mashahid. Na kwamba mwenye kufa katika njia ya haki, basi amekufa shahid, au ana thawabu za shahid, lakini kufa shahid ni jambo jengine na kuwa katika daraja ya kufa shahid ni jambo jingine.

Ama watu wema ni wale ambao imekuwa njema itikadi yao na amali zao. Imam Ali (a.s.) amesema; "Kwa imani yanafahamika matendo mema na kwa matendo mema inafahamika imani." Hakuna mwenye shaka kwamba kujua halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake kwa kujitahidi au kwa kufuata ni sharti la msingi katika wema. Kwa sababu kutojua huharibu itikadi na amali.

87

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

Hiyo"ri'f fadhila^^itökâyö kwa Mwenyezi Mürigü..

Ndio! Radhi ya Mwenyezi Mungu, na kuwa na urafiki na Mitume, wakweli, mashahidi na watu wema, ni kutengenekewa kwa kweli na ni fadhila za kudu-mu, sio hizi starehe ziondokazo.

71.Enyi mlioamini! Shikeni had-hari yenu. Tokeni vikosi vikosi au tokeni nyote pamoja.

72.Na hakika katika nyinyi kuna ambaye hukaa nyuma, na uki-wapata msiba husema: Mwenyezi Mungu amenineeme-sha kwa kutokuwa nao.

73.Na iwafikiapo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu, husema - kama kwamba, hapakuwa na mapenzi baina yenu na yeye -laiti ningelikuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makub-wa.

 

Aya 71 - 73CHUKUENI HADHARI

MAANA

Enyi mlioamini! Shikeni hadhari yenu

Aya hii ni miongoni mwa Aya za kuhimiza Jihad, zimetangulia Aya nyingi za namna hiyo na zijazo ni nyingi. Lakini Aya hii inawajibisha kutoka watu wote kwenye vita ikiwa iko haja. Umuhimu huu hasa unafahamisha maadui

Kaashif5-56.jpgKaashif5-57.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

waliokuwa nao Waislamu wakiw

na wahasimu wanaowafitini na dini yao. Mpaka leo uislamu na waislamu wanaandamwa na makafiri na mataghuti. Kwa hiyo ni kawaida kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwahimiza waislam wawe na hadhari na kujua nguvu za uadui na maandalizi yake ya silaha.

Tokeni, vikosi vikosi au tokeni nyote pamoja.

Tokeni, ni amri ya kutoka kwenda vitani; na kutoka kwa vikosi, ni vikosi maalum vya askari; na nyote pamoja ni jeshi pamoja na wengine kulingana na hali inavyotakikana. Makusudio ni kujiandaa kumkabili adui kwa nguvu zote na kutumia kila njia kuipinga dhulma na uadui; hata kama kujikinga kutapelekea umma wote kushiriki katika vita. Wakubwa kwa wadogo na waume kwa wake. Allama H—Iilli anasema: "Lau kuna haja ya kutaka msaada kwa wanawake basi itakuwa ni wajibu."

VITA VYA JANA NA LEO.

Zamani vita vilikuwa vya wanaume tu na kuandaliwa na askari na vikosi. Ama leo, sayansi ndiyo imekuwa nguvu katika nyanja zote. Na panga na mishale zimebadilika kuwa mabomu, mizinga nyambiz i, vifaru na meli za kivita. Vile vile silaha za sumu na mitandao ya upelelezi wa anga, bara na baharini*10 kiasi ambacho hajui isipokuwa Mwenyezi Mungu na mabingwa katika elimu ya kuharibu na kuvunja.

Biashara ya vita haikutosheka na uvumbuzi wa elimu wa vifaa vya kuvunja na kuharibu, mpaka wameanzisha vyuo maalum vya elimu ya kuharibu na upan-gaji wa njama za mapinduzi, kuleta fitina na chuki na kuleta ghasia. Vilevile kupanga namna ya kueneza hofu na wasiwasi, kupuuza maadili na misimamo na kuamini mambo ya uzushi, na mengineyo yanayoandaa nguvu za kuwatawala wanyonge.

Hii ndiyo aina ya silaha anayotupiga nayo vita adui wa dini na wa ubinadamu. Basi tutajikinga naye vipi? Je, ni kwa matusi na shutuma? Au ni kuomboleza na kulia? Au ni kwa chuki.

Hakuna jengine kwa tulivyo hivi sasa ila kumjua ni nani adui yetu na uwezo wake ukoje, na tujihadhari naye na mbinu zake; wala tusimwamini na cho-chote.

*10Hivi sasa kuna setilaiti karibu 40 katika ardhi za kufanyia upelelezi. Marekani peke yake ina vyombo 30 vya angani na vituo elfu moja vya kufanyia ujasusi.

<ö> 89

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'We vile tujifunze kutokana na mako

bidii mkono kwa mkono kwa nguvu zetu zote katika nyanja zote. Kwa namna

hii ndipo tutaweza kusimama kumkabili adui; angalau hali isiwe kama tulivyo

sasa.

Wavietnam waliweza kuwang'oa wamarekani pamoja na nguvu nyingi wali-

zozikusanya na mabilioni ya madola waliyoyatoa. Kabla ya Vietnam, Cuba ili-

jikomboa kutoka makucha ya wamarekani ingawaje ndilo taifa kubwa ulimwen-

guni. Na hivijuzi Korea ya Kaskazini imeteka nyara meli ya kijasusi na wala

Amerika haiwezi kuitikisa.

Siri ya hayo - kwa nionavyo - ni kwamba mataifa haya yalikuwa na mwamko

na

mipango na yalisahihisha makosa yake wakaikata mikono ya wahaini na kuwa-tenga na uongozi na sehemu muhimu. Pia mataifa hayo yaliamini haki yake na misingi yake na kupuuza maisha katika kuipigania.

Wala haiwezekani kwa nguvu za ulimwengu wote kutawala taifa lenye nid-hamu na mwamko, liwe la kivietnam au la kiarabu. Tofauti iko katika hali sio asili na katika mwamko na uthabiti katika wanachokiamini na kukiitakidi.

Na hakika katika nyinyi kuna ambaye hukaa nyuma.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaashiria kwenye kikosi cha siri ambacho kinajiin-giza katika safu za watu wema kwa makusudio ya kuharibu na kurudisha nyuma mapambano na uadui.

Unaweza kuuliza kuwa neno, 'katika nyinyi linaelekezwa kwa waumini, na wanafiki wako mbali zaidi na imani kuliko watu wengine. Sasa imekuwaje kuwafanya ni katika waumini?

Jibu: Kwa sababu wao wanahisabiwa kuwa ni katika waumini kidhahiri, na wanachukuliwa kuwa ni katika wao, sawa na mtu anayechukuwa uraia wa nchi akiwa ni kibaraka. Hawa wapo kila mahali na kila wakati.

Ukiwapata msiba husema: Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa kutokuwa nao.

Hii ni kuizungumzia hali ya mnafiki ambaye alikuwa akifurahi wanaposhindwa waislam katika vita ambavyo yeye hakuhudhuria pamoja nao. Kila mwenye kufurahi kwa kusalimika na balaa iliyompata ndugu yake katika njia ya Mwenyezi Mungu na kupigania kuinua dini, basi huyo ni mnafiki.

90

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Unaweza kuuliza kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu, amenineemesha, ni kukiri kuweko Mwenyezi Mungu, sasa imewezekanaje kumfanya ni katika wanafiki?

Jibu: Yeye ameufanya unafiki kwa kudhihirisha uislamu na kumwamini Muhammad (s.a.w.) na kuficha kukanusha utume wake. Na hili halipingani na kumkubali Muumba. Si kila anayemwamini Mungu anamwamini Muhammad (s.a.w.), Mwenyezi Mungu ameelezea kuwa kuna katika watu anayemwamini yeye Mwenyezi Mungu na wakati huo huo anamwamini mwingine, au atakayemkurubisha zaidi kwake.

"Na wengi wao hawamwamini Mwenyezi Mungu isipokuwa wao ni washiriki-na." (12:106)

Na iwafikapo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu, husema - kama kwamba hapakuwa na mapenzii baina yenu na yeye - laiti ningelikuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuelezea kuwa mnafiki hufurahi kwa kubaki kwake nyuma, kama waislamu wakishindwa, sasa anaeleza kuwa yeye anajuta kwa kuacha kujiunga nao wanapopata ushindi na ngawira. Kimsingi ni kuwa ambaye mambo yake ni hayo, si mwislamu kitu, hata kama anadai kuwa ni mwislamu. Na kama angelidhihirisha mapenzi baina yake na waislam angeli-tambua kwamba heri yao ni heri yake na shari yao ni shari yake. Imekuwa mashuhuri Hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): "Hakika waislam ni kama viungo vya mwili mmoja, na ni kama jengo moja, sehemu moja inasaidia nyingine; na kwamba asiyejishughulisha na mambo ya waislam si katika wao."

74.Na wapigane katika njia ya Mwenyezi Mungu ambao huuza maisha ya duniani kwa akhera, na mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, akauawa au akashinda, tutampa ujira mkubwa.

Kaashif5-58.jpg

91

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa katika wanaume na wanawake na watoto ambao husema: Ewe Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhal-imu, na tujaalie mlinzi kutoka kwako.

Kaashif5-59.jpg

76.Wale walioamini wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na waliokufuru, wanapigana katika njia ya shetani. Basi piganeni na marafiki wa shetani; hakika hila za shetani ni dhaifu.

WANAOUZA UHAI WA DUNIA KWA AKHERA Aya 74 -76:

Na wapigane katika njia ya Mwenyezi Mungu ambao huuza maisha ya duniani kwa akhera.

Uzuri wa yaliyosemwa katika kufasiri Aya hii ni haya yafuatayo: "Hakika Uislamu haupigani kwa ajili ya kupata ardhi au kuwatawala wakazi; haupigani kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda na masoko; au kwa ajili ya rasilmali zitakazozalishwa katika makoloni."

Uislam haupigani kwa ajili ya fahari ya mtu, nyumba, tabaka, dola, umma au watu fulani. Isipokuwa unapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwenye

92

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'ârdh'İ ha kumakihika hjiâyake'kâtl'ka"miâ]shâ"ha"]îi"Mü'¥fâ]dîke'Wâ"hjİâ"h'M'n'â' uadilifu baina ya watu huku ukimwacha mtu awe huru na mwenye hiyari kati-ka itikadi ambayo atakuwa nayo.'

Natamani wakati ninasoma jumla hii (Uislamu haupigani kwa jili ya malighafi ya viwanda) niunganishe na jumla hii: 'na wala si kwa ajili viwanda vipakwe damu ya wasiokuwa na hatia, wanawake na watoto.

Na mwenye kupigana katika njia ya Mungu. Akauawa au akashinda, tutampa ujira mkubwa.

Kila mwenye kuinusuru haki kwa njia ya haki na kufuata amri ya Mwenyezi Mungu peke yake, basi yeye ni mwenye kushukuriwa na mwenye kulipwa; ni sawa iwe ameshinda na akapata ngawira, au ameshindwa.

Wanahistoria, pamoja na kutofautiana misimamo yao, wameafikiana kuwa siri ya kuenea uislam ni itikadi ya Mtume (s.a.w.) na sahaba, kwamba wao ni wenye kupata faida katika hali yoyote, ya kuuliwa au kuua. Ikiwa ni kuuawa, basi mwelekeo ni peponi; au ikiwa ni kuua itakuwa tamko la haki limeinuka, na hili ndilo walilolitaka; kuongezea imani kwamba ajali yao ikifika haichelewi hata saa wala haizidi. Imani ya mtu ikifikia hatua hii hawezi kusimamishwa na kizuizi chochote.

Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa katika wanaume na wanawake na watoto.

Mtume (s.a.w.) alihama kutoka Makka kwenda Madina, na walihama pamoja naye wale walioweza na wakabakia wenye kushindwa, wakiwemo wanaume wanawake na watoto. Nao walikuwa wakipata adha kubwa kutoka kwa washirikina kwa ajili ya dini yao; na wala hawakuweza kujikinga wala kupata usaidizi. Kwa ajili hii ndio Mwenyezi Mungu akawaita 'wanaoonewa'. Walipokuwa hawana la kufanya, walimwelekea Mwenyezi Mungu na kusema: Ewe Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie mlinzi kutoka kwako.

Mwenyezi Mungu ameifanya misukosuko ya wanyonge ni njia ya kuwahimiza jihadi waislam kuwaokoa ndugu zao wa dini, jamaa wanyonge walibakia Makka mpaka mwaka wa ushindi Mtume alipoingia Masjidul-haram wakiwa washindi, vigogo vya ushirikina vikasalimu amri na masanamu yakavunjwa. Uislamu ukatukuka na akawaneemesha wale walio wanyonge katika Makka na kuwafanya watukufu.

<ö> 93

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Wale wâİİöâmİm^

furu wanapigana katika njia ya shetani.

Katika Aya 71 Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kutoka kwenda vitani vikosi au wote; katika Aya 74, ameamrisha kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; katika Aya 75, amewahimiza kuwakomboa wanaoonewa. Katika Aya hii amegawanya wapiganaji kwenye mafungu mawili; waumini wanaopigana kwa ajili ya haki na uadilifu, na makafiri wanaopigana kwa ajili ya kutawala, kunyang'anya, na kudhulumu. Hawa ndio wasaidizi wa shetani; na Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini wapigane na kuwatangazia vita na kuacha kufanya mapatano nao kwa namna yoyote ile. Kwa sababu kuwamaliza ndio heri na utengeneo wa ubinadamu, na kupatana nao ni shari na ufisadi.

Kwa ufupi ni kwamba Aya zote tulizozielezea na nyinginezo zinazohusu vita zina lengo moja tu, uimara na uthabiti katika kuwapiga vita wabatilifu na wenye kutaka kujichukulia faida. Aya za Jihadi zinatofautiana katika mfumo na ibara tu, lakini lengo ni moja.

Basi piganeni na marafiki wa shetani; hakika hila za shetani ni dhaifu.

Dhahiri ya Aya hii, ni kwamba wenye haki daima watawashinda wabatilifu, lakini aghlab hali inakuwa kinyume; je kuna siri gani?

Umetangulia mfano wa swali hili na jibu lake kwa ufafanuzi katika kufasiri Aya ya (3:137) kifungu cha Balaa la June. Lakini hapa tutajibu kwa mfumo mwingine, tuliojua kutokana na hotuba ya Imam Ali (a.s.) katika Nahjul-bal-agha.

Ufupi wa jibu ni kuwa vijasumu vibaya haviishi na kukua isipokuwa kwenye takataka na uchafu. Hivyo hivyo shetani hapati mahali pa kutekeleza hila zake isipokuwa penye jamii mbaya. Hapa maandalizi yake hupata nguvu na kujaza nguvu zake. Katika kauli yake Imam, inadhihiri kuwa umuhimu wa Iblis unafaulu pale wanapokuwa katika jamii mafukara wenye shida na matajiri wajeuri. Imam anasema hivi:

"Yafahamu vizuri haya! Ikiwa silaha ya shetani itakuwa na nguvu, vitimbi vyake vikaenea na uwindaji wake ukawa mwepesi tupa jicho lako popote unapotaka katika watu. Je, utaona zaidi ya fakiri mwenye mashaka au tajiri aliyebadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kuwa ukafiri au bakhili aliyefanyia haki ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio ubakhili! au jeuri ila ni kama kiziwi Wako wapi wabora wenu na wema wenu? Wako wapi waungwana wenu na watoa-

94

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

ji wenu? Wako wapi wanaochunga haki katika chumo lao? "- mpaka kufikia pale aliposema - "kwa hali hii ndio mnataka kuwa karibu na Mwenyezi Mungu katika nyumba ya utukufu wake, na muwe ni watukufu wa vipenzi vyake mbele zake? Awalaani Mwenyezi Mungu wanaoamrisha mema na kuyaacha, na wenye kukataza mabaya na huyafanya."

77.Je, huwaoni wale ambao wameambiwa: Zuieni mikono yenu, na msimamishe Swala na mtoe Zaka. Walipolazimishwa kupigana, mara kundi moja katika wao wakawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi; na wakasema: Ewe Mola wetu! Kwa nini ukatufaradhia vita usi-tuahirishie muda mchache! Waambie: Starehe ya duniani ni chache, na akhera ni bora kwa wenye kumcha Mungu wala hamtadhulumiwa hata kidogo.

Aya 77 ZUIENI MIKONO YENU NA SIMAMISHENI SWALA

MAANA

Mwanzo wa kulingania Mtume (s.a.w.) kwa Mwenyezi Mungu, alilingania akiwa Makka. Wenye nguvu wakamzuia, wakihofia masilahi yao. Wakamwita mwenda wazimu, mchawi na mwongo. Lau si ami yake Abu Twalib kumhami, wangelimmaliza. Waliposhindwa naye, waliingilia kuwatesa wanaomwamini. Na Mtume alikuwa akiwaamuru kuwa wavumilivu na kuizuia mikono yao, kwa sababu ya wingi wa adui na uchache wa wasaidizi.

Kaashif5-60.jpg

95

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Maudhi na vikwazo vya washirikina vilipoziidi kwa waumini wanyonge, kikundi kimoja kilisema kumwambia Mtume (s.a.w.) "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; tupe idhini ya kupigana na washirikina." Akasema: "Nimeamrishwa kufanya subira." Na Mtume alikuwa akiwapa matumaini sahaba zake ya kue-nea waislam na kuondoka utawala dhalimu.

Baada ya kupita miaka 13 Makka tangu kuanza mlingano, Mtume alihama kwenda Madina na wakahama pamoja naye wanaojiweza katika waislamu, wakiwemo wale waliotaka idhini ya kupigana na washirikina wa Makka. Idadi ya waislam ilipoongezeka wakawa wanaweza kujilinda. Mwenyezi Mungu akawaamrisha kupigana Jihadi na washirikina ili kujikinga na shari yao. Kwa sababu hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ilihukumia kupita mambo kwa desturi yake na sababu zake; na kutoenea dini yake ispokuwa kwa nyezo za kiubinadamu na kutolazimisha dini kwa nguvu za kiungu; kama inavyonyesha mvua na tufani.

Mambo yalipoiva wakaanza kuogopa wale waliokuwa na hamasa ya kupigana na washirikina walipokuwa Makka kabla hawajaruhusiwa vita. Hii ndiyo hali ya wanaopandwa na mori kwa hisia za mapenzi bila ya kufikiri na kuwaza, wana-pandwa na mori na hamasa ya kupigana mpaka wanarukwa na akili; ambapo utekelezaji wake ni kujiua. Lakini inapofikia haja ya kupigana na kuwa ni lazi-ma, basi huanza kurudi nyuma kwa woga.

Si lazima watu wa namna hii wawe ni wanafiki au wasiokuwa na uhakika wa dini yao. Wanaweza kuwa ni katika wanyonge wanaohofia mauti na kuathiri-ka na uhai kwa kuhofia kufa shahid katika njia ya haki.

Aya hii tuliyonayo imeonyesha kikundi cha waislamu waliokuwa na hamasa ya kupigana walipokuwa Makka kisha wakaogopa walipokuwa Madina. Tumetangulia kueleza utangulizi huo, kabla ya kuanza kufasiri Aya hii ili yawe wazi makusudio yake.

Je huwaoni wale ambao wameambiwa: Zuieni mikono yenu, na msi-mamishe Swala, na mtoe Zaka.

Makusudio ya, 'wale ambao; ni 'wale waliokuwa na haraka ya vita na hamasa walipokuwa Makka. Na kauli yake Mwenyezi Mungu "wameambiwa ..." ni ishara ya kwamba Mtume aliwaamuru kufanya subira na kujizuia kupigana, na kufanya lile waliloamriwa ikiwemo kuswali na kutoa Zaka.

96

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Walipolazimishwa kupigana, mara kundi moj

watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi.

Yaani, zilipokamilika sababu za waislam kupigana baada ya kuhamia Madina, na kukawa na haja sana waliamrishwa kufanya hivyo, lakini wale waliokuwa na haraka walichukia kwa kupenda uhai na kuwa na woga wa kukabiliana na adui na kuogopa kuteseka.

Kusema kwake na wakawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi ni fumbo la kuwa hofu imefikia kikomo.

Na wakasema: Ewe Mola wetu! Kwa nini ukatufaradhia vita, usitu-ahirishie muda kidogo.

Walitaka muda kwa kupenda sana anasa za dunia.

Na mwelekeo wao wa hili kwa kunyenyekea, unaonyesha kumwamini kwao Mungu. Ilivyo ni kuwa kuasi amri ya Mwenyezi Mungu kwa mauti, hakufa-hamishi kuwa ni ulahidi; kama ambavyo kuhiyari mauti kuliko kuwa dhalili hak-ufahamishi kumwamini Mungu.

Tumewaona walahidi wengi wakihiyari kufa kuliko kuishi na madhalimu; kama ambavyo tumewaona waislamu wengi wanajiingiza kwenye vifungo vya udhalili na utumwa, wao wenyewe na watu wao.

Waambie starehe ya duniani ni chache.

Makusudio ya uchache hapa ni kutodumu na kuondoka haraka. Na kila stare-he za dunia zitakwisha zaidi ya kuwa zimechanganyika na wasiwasi na machukivu.

Na akhera ni bora kwa wenye kumcha Mungu.

Akhera ndio mwisho wa yote; uchache wa neema yake ni bora kuliko neema za dunia zote; kama ambavyo uchache wa adhabu yake ni mkubwa kuliko adhabu ya dunia yote. Mwenye akili ni yule ambaye anathamini kitukufu cha kudumu, hata kama kitakuja baadaye, kuliko kitu duni kinachokwisha ingawa-je ni cha sasa hivi.

97

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

78.Popote mtakapokuwa yatawafi-ka mauti na hata mkiwa katika ngome madhubuti. Na liki-wafikia zuri wao husema: Hili linatokana na Mwenyezi Mungu. Na likiwafika baya husema: Hili linatokana na wewe, Sema: Yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi wananini watu hao hata hawakaribii kufahamu maneno.

79.Jema likufikalo linatokana na Mwenyezi Mungu na ovu likufikalo linatokana na wewe mwenyewe. Na tumekupeleka kwa watu kuwa ni mjumbe, na atosha Mwenyezi Mungu kuwa shahidi.

Aya 78 - 79 POPOTE MTAKAPOKUWA YATAWAFIKA MAUTI

MAANA

Popote mtakapokuwa yatawafika mauti na hata mkiwa katika ngome madhubuti.

Umetangulia mfano wake wakati wa kufasiri 3: 145 kifungu 'Ajali imeandikwa.' Likiwafikia zuri wao husema: Hili linatokana na Mwenyezi Mungu na liki—

Kaashif5-61.jpg

98

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa 'wafîka"baya7hüseiifiâ"hlM'lTnâtök¥ha"h¥wewe°.'.....

Kila alionalo mtu ni zuri, husema ni zuri na kulifuatishia na neno 'heri' ambalo mtu hulipendelea na kulitamani. Na kila alionalo mtu ni baya, husema ni baya, na kuliufuatishia na neno 'shari' ambalo mtu hujiepusha nalo na kulikataa.

Kheri inaweza kuwa ya watu wote; kama vile rutuba na fanaka ambayo haimhusu mtu au kundi pekee. Na mara nyingine huwa inamhusu mtu; kama ufanisi wa mtu baina yake na familia yake. Vilevile shari inaweza kuwa ni ya kiujumla; kama vile ukame na ughali wa vitu; au kuwa ni ya mtu binafsi; kama vile kuwa mke mwovu na watoto wake.

Makusudio ya uzuri katika Aya hii ni heri ya kimaumbile ambayo inaenea kwa wote; kama vile mvua na mfano wake. Na ubaya ni shari inayoenea kwa wote; kama vile kahati na mengineyo. Kwa sababu washirikina walipokuwa wakipa-ta neema; kama vile mvua, husema; Mwenyezi Mungu ametukirimu. Na wakipatwa na adhabu; kama vile kahati, husema: Hii imesababishwa na Muhammad; sawa na vile walivyokuwa wakisema wana wa Israil, ambao Mwenyezi Mungu amewaelezea kwa kusema: "Unapowafikia uzuri husema: Huu ni kwa ajili yetu. Na ukiwafikia ubaya humnasibishia ukorofi Musa ..." (7:131)

HAIWEZEKANI KUONGEZA ZAIDI YA ILIVYO Sema: Yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Hili ni jibu la anayenasibisha wema kwa Mwenyezi Mungu na uovu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kwani kahati, mvua, matatemeko na madini vyote hivi na vinginevyo ni katika athari na mambo ya lazima kwa maumbile. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ndiye aliyeleta maumbile. Kwa hiyo heri ya maumbile na shari yake inanasibishwa kwenye maumbile na kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kupitia kuleta kwake maumbile. Yeye, ambaye umetukuka utukufu wake, ndiye sababu ya sababu.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu hakuyafanya maumbile bila ya shari, kwa namna ambayo heri itatakata na kila tatizo na waja wapate raha, wasiwe na tabu?

Swali hili au mushkeli huu umetolewa tangu maelefu ya miaka iliyopita. Zaradasht amejaribu kulitatua kwa kusema kuwa kuna waungu wawili Mungu wa heri (Mozad) na Mungu wa shari (Ahriman).

<ö> 99

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Wengine wamesema: Hakika MwenyeziMunguameyaumbamaumbilehaya mkiwa ndani yake mna heri na shari, lakini wakati huo akaumba akili itakay-olinganisha maumbile haya kwenye heri yake na utengenevu wake. Ikiwemo huu ugunduzi ambao umefanya kitu cha mbali kiwe karibu, ukasahilisha jambo zito, yakatengenezwa mawingu ya mvua, na vimbunga vikajulikana kabla ya kutokea na mengineyo yasiyokuwa na idadi.

Amesema Abid Zahid: Hakuna budi na shari ili waasi waadhibiwe, lakini jibu hili linakanushwa na ushahidi uliopo na Qur'an. Kwa sababu desturi ya maumbile haimuhurumii muumin wala dhaifu na matetemeko ya ardhi hayamtengi mwema na mwovu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: Na iogopeni adhabu ambayo haitawasi-bu waliodhulumu nafsi zao katika nyinyi, peke yao. (8:25)

Kuna wengine waliosema: Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye na sisi hatujui kitu. Ashaira wamesema swali hili linarudishwa lilivyo. Kwa sababu vitendo vyake Mwenyezi Mungu Mtukufu, havisababishwi kwa malengo fulani. "haulizwi ali-fanyalo."

Katika kitab Asfar cha mwanachuoni mtukufu aliye mashuhuri kwa jina la Mulla Sadra kuna maelezo, kwa muhtasari: Ni jambo lisilowezekana kuweko ulimwengu usiokuwa na shari. Kwa sababu ulivyo ulimwengu wa kimaumbile kwa mujibu wa hali yake hulazimika kuweko na heri na shari, nguvu na udhai-fu na upole na ugumu. Vinginevyo isingewezekana kabisa kuweko ulimwengu; kama isivyowezekana kwa bingwa wa ujenzi kujenga ngome madhubuti kwa udongo tu.

Hilo ni kwamba ni muhali kuweko kitu bila kuweko na vitu vinavyopingana ambavyo daima vinakuwa katika mvutano na msukumano wa daima. Katika hali hii ndipo yanapatikana maumbile kama vile vimbunga, joto, baridi, mvua, ukame na mengineyo ambayo athari zake za kimaumbile ni heri yake na shari yake. Katika hali hii ndipo mambo lazima yawe katika hali mbili tu. Ama kusi-weko ulimwengu ama uweko ukiwa na heri yake na shari yake.

Hii ndio maana ya msemo mashuhuri: "Haiwezekani kuzidisha zaidi ya ilivyo," kama ambavyo inaafikiana kwa ukamilifu na kauli ya wanasayansi kuwa katika kila maumbile kuna sehemu ya nguvu ya sawa na ya kutengua.

Kwa hivyo basi, inatubainikia kuwa kauli ya mwenye kusema; Kwa nini Mwenyezi Mungu hakuumba ulimwengu usiokuwa na shari, ni sawa na

Kaashif5-62.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

mwenye kusema: kwa nini Mwenyezi Mungu hakuumba moto usiokuwa na joto, theluji isiyokuwa na baridi, akili isiyokuwa na utambuzi, uhai usiokuwa na harakati au mauti yasiyokuwa na kutulia. Kwa maneno mengine swali hili linafanana na mtu aliyepagawa anayesema: Kwa nini kitu kikawa hicho hicho na hakikuwa kingine. Katika hali hii ndipo tunapata siri ya undani katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi wana nini watu hao hata hawakaribii kufahamu maneno.

Kwa ufupi ni kuwa si Muhammad (s.a.w.) wala mwingineo mwenye athari yoy-ote, ya heri au ya shari katika maumbile. Iko riwaya mashuhuri kutoka kwa Mtume kwamba alisema wakati jua liliposhikwa, alipokufa mtoto wake Ibrahim: "Jua na mwezi ni alama katika alama za Mungu, zinakwenda kwa amri yake na kumtii yeye tu, hazishikwi kwa sababu ya kifo cha yeyote au uhai wa yey-ote."

Jema likufikalo linatokana na Mwenyezi Mungu na ovu likufikalo lina-tokana na wewe mwenyewe.

Unaweza kuuliza: Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya ya kwanza ameutegemeza ubaya na uzuri kwake Yeye tu, kwa kusema yote yatoka kwa Mwenyezi Mungu; na katika Aya ya hii ametegemeza mema kwake na mabaya kwa binadamu. Je kuna wajihi gani?

Jibu: Tumetanguliza kueleza katika Aya ya kwanza kwamba makusudio ya uzuri katika Aya ya kwanza ni heri ya maumbile na ubaya ni shari ya maumbile, na kwamba yote mawili ni dhahiri ya maumbile ambayo ni katika uten-genezaji wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo ikasihi kuyanasibisha kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mazingatio haya. Ama makusudio ya uzuri katika Aya ya pili ni kuokoka mtu katika maisha haya kidini na kidunia. Na makusudio ya uovu ni kutofanikiwa kidini na kidunia.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekunasibisha kuokoka - katika kuangalia ibara ya wema - Kwake Yeye kwa kuangalia kuwa yeye amempa uzima na utambuzi na akaamrisha kufanya amali kwa ajili ya manufaa ya duniani na akhera. Kwa hiyo akifuata na kufanya amali akafikia kufaulu, hunasibishwa kwake Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yeye ndiye aliyemwezesha na akampa ala za kufanyia kazi hiyo tena akamwamrisha. Ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Jema likupatalo linatoka kwake.

Vilevile inawezekana kunasibisha kuokoka kwa mtu. Kwa sababu yeye

Kaashif5-63.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

ameacha uvivu na kupuuza akajitahidi na kufanya. Haku kwamba mtu hana athari kabisa katika kufaulu kwake. Ama kupuuza na kufanya uvivu na asifikie popote kwa sababu ya kupuuza kwake na uzembe, hakuwezi kunasibishwa kwa yeyote zaidi yake yeye mwenyewe. Kwa sababu ni yeye aliyejiingiza kwa chaguo lake ovu la kupuuza. Kwa kuzingatia hivi ndipo Mwenyezi Mungu akasema: "Na ovu likufikalo linatoka kwako."

Wala haiwezekani kwa hali yoyote kutofaulu kwa mtu kunasibishwe na Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, amemwamrisha mtu kufanya na kumhimiza baada ya kumpa zana zote zihitajikazo.

80.Mwenye kumtii Mtume, basi amemtii Mwenyezi Mungu; na mwenye kukataa, basi hatukukupeleka kuwa mlinzi juu yao.

81.Na wanasema: 'Tunatii' na wanapotoka kwako kundi moja katika wao huenda njama usiku kinyume cha yale wayasemayo. Na Mwenyezi Mungu anaziandi-ka njama zao. Basi achana nao na mtegemee Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa ni mwenye kutegemewa.

82.Je, hawaizingatii Qur'an? Lau kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wangelikuta ndani yake tofauti nyingi.

Kaashif5-64.jpgKaashif5-65.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ■.

Aya 80 - 82 HÂTÜKÜKÜPELEKAKÜVVÂ'MÜNZİ JÜU YÂÖ

Mwenye kumtii Mtume, basi amemtii Mwenyezi Mungu.

Imetangulia tafsir yake katika Aya 59 ya Sura hii.

Na mwenye kukataa, basi hatukukupelekea kuwa mlinzi juu yao.

Kazi ya Mtume inaelezwa na tamko la jina lenyewe; kama ambavyo tamko la jua linavyoelezea maana yake. Ama hisabu ya mateso, ni kazi ya Mwenyezi Mungu, si ya Mtume: Hakika ni kwetu sisi marejeo yao. Kisha ni juu yetu sisi hesabu yao (88: 25 - 28)

Tumezungumzia kwa ufafanuzi maudhui haya katika kufasiri (2:270)

Na wanasema: 'Tunatii' na wanapotoka kwako kundi moja katika wao huenda njama usiku kinyume cha yale wayasemayo. Na Mwenyezi Mungu anaziandika njama zao.

Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa waislamu kwa ujumla wao walidhihirisha utii kwa Mtume (s.a.w.), lakini wao si wote waliokuwa na ikhlasi katika waliyoyad-hihirisha, Bali katika wao kulikuwa kuna kikundi kinachomhadaa Mtume na kula njama usiku kinyume na wanayoyadhihirisha. Aya hii ni jawabu tosha kwa wale wanaodai kuwa masahaba wote ni waadilifu na kwamba kusuhubiana na Mtume tu kunamfanya mtu awe msafi wa kila kitu.

Basi achana nao na mtegemee Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa ni mwenye kutegemewa.

Msemo unaelekezwa kwa Mtume, ukiwa na maana kuwa hekima inapelekea kutowafichua makafiri na kuwataja majina yao. Watafichuka wenyewe.

Mfano wa Aya hii ni kama Aya ya 63 ya Sura hii hii.

 MAYAHUDI NA MUUJIZA WA QUR'AN

Je hawaizingatii Qur'an? Lau kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wangelikuta ndani yake tofauti nyingi.

Katika kufasiri (2: 23-5) chini ya kifungu 'Siri ya muujiiza wa Qur'an; tume-onyesha siri hii kwa njia ya ujumla. Kwa sababu ufafanuzi utamaliza kitabu chenye ukubwa wa juzuu hii.

103

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Baada ya kwisha kufasiri tumegundua sîn zâ muujiza amb nazo wanavyuoni wa kiislam waliotangulia; hata wale waliotunga vitabu mah-sus katika muujiza wa Qur'an. Hiyo sio kama imetokana na uzembe, la! Isipokuwa maajabu na siri za Kitabu cha Mwenyezi Mungu haziishi.

"Sema lau bahari ingelikuwa ni wino kwa (kuandika) maneno ya Mola wangu, bila shaka bahari ingelikwisha kabla ya kwisha maneno ya Mola wangu. Hata kama tungelileta (bahari) kama hiyo kuongezea." (18:109)

Na amesibu kutokana na matamko haya kila mmoja kwa kadiri unavyomsaidia wakati wake na kipawa chake. Kwa sababu zama ni kiungo muhimu katika kufichua maana ya Qur'an na siri zake. Ibn Abbas anasema: "Katika Qur'an kuna maana yatakayofasiriwa na wakati."

Miongoni mwa maana hayo ni yale yaliyoonyeshwa na Aya ya 53 ya sura hii: "Au wao wana fungu katika Ufalme? Basi hapo wasingewapa watu hata kitob-we cha kokwa ya tende."

Tumetaja katika kufasiri Aya 46 utabiri wa Qur'an kuhusu fedheha ya Mayahudi na madhambi yao, wakipata Ufalme. Baada ya karne kumi na tatu utabiri huu umethibitika. Hii ni dalili ya mkato ya utume wa Muhammad (s.a.w.) na ukweli wa ujumbe wake. Huu ndio muujiza tulioukusudia kusema kuwa wanavyuoni na wafasiri hawakuzinduka nao. Kwa sababu Mayahudi wakati huo walikuwa wakitawaliwa, hawakuwa na chochote, si katika Palestina wala penginepo.

Katika jumla ya dalili za kuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Lau kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wangelikuta ndani yake tofauti nyingi."

Miongoni mwa tofauti hizi ni kutokuwepo mpangilio na kunasibiana katika maneno ya watu ki mfumo na kifikra. Hakuna mwanachuoni mwanafasihi au mtu yeyote ila kutakuwepo na kutofautiana nguvu na udhaifu katika ibara zake na fikra zake. Ama Qur'an iko katika daraja moja katika ufasaha wa mpangilio wake na ukubwa wa maana zake.

Siri ya hilo ni kuwa binadamu ana hali na matatizo yanayotofautina na kubadi-lika kwa nyakati mbali mbali bali hata kwa kitambo kidogo tu. Na yeye binadamu anafuatana nazo, wala hawezi kuepukana na hilo kwa hali yoyote ile. Kusema kwake Mwenyezi Mungu, ‘Tofauti nyingi,' ni ishara ya kuwa mageuzi ya binadamu kulingana na hali yake ni mengi sana yasiyo na idadi.

Kaashif5-66.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Töfâüti"hi) Jnatüfâsiriâ töfâüti"kMkâ"mfümo'wâ"bİhad¥mü'Wâ"fîkra yâke"....

Ama dhati takatifu ni moja katika kila kitu milele na milele, haibadiliki kwa hali wala kwa matatizo. "Vipi yatampita Mwenyezi Mungu yale aliyoyapitisha; na yamrudie yale aliyoyaanzisha; na yamzukie yale aliyoyazusha? Ingekuwa hivyo, basi dhati yake ingelitofautiana, na kuwa kwake kungegawanyika;" kama anavyosema Imam Ali (a.s.). Huyu ndiye anayetufasiria kufuatana na kunasibiana katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, madhumuni na utendaji kazi wake, kuanzia Alifu mpaka Ye.

83.Ikiwajia habari ya amani au ya hofu huitangaza. Na lau wangeirejesha kwa Mtume na kwa wenye mamlaka katika wao, wangejua wale wenye kuchunguza katika wao. Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngemfuata shetani isipokuwa wachache tu.

Aya 83: SIRI YA VITA NA KUVITANGAZA

MAANA

Ikiwajia habari ya amani au ya hofu huitangaza.

Walikuwepo katika Masahaba wa Mtume - kama ilivyo katika kikundi au kikosi chochote - wakweli na wanafiki, mashujaa na waoga, wenye nguvu na wad-haifu katika imani, na wenye akili wanaoangalia mambo kulingana na matukio, na wajinga wasiozingatia mambo wala kupima mwisho wake. Qur'an ime-waelezea hawa wote, mara nyingine kwa uwazi na mara nyingine kwa ishara.

Wafasiri wameafikiana kwamba Aya hii imeshuka juu ya wale waliokuwa wak-isikiliza habari za amani au za hofu, ambazo zilikuwa zikufungamana na nguvu za askari wa kiislam, basi huzitangaza kwa watu. Kisha wafasiri wakatofau-

Kaashif5-67.jpg

105

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

tiana katika kuwaelezea hao watangazaji: Je, ni wanafiki au ni wale waumini wa juu juu wadhaifu? Kila kikundi kikasema kutokana na vile ilivyotiliwa nguvu kwao.

Ama sisi haikuwa na nguvu kwetu kauli ya kukusudia wanafiki wala wanyonge. Kwa sababu yote yanayofahamishwa na dhahiri ya Aya ni kuwa miongoni mwa jamaa waliokuwa karibu na Mtume (s.a.w.), wakifikiwa na habari ya amani au vita, huizungumzia na kuifuchua kwa watu.

Hakuna kitu kinachodhuru amani ya ndani na ya nje kuliko kufichua siri za kiaskari, hasa ikiwa watangazaji wenyewe wamepata habari juu juu. Kwa sababu habari nyingi wanazitengeneza maadui na kuzisambaza kwa makusu-dio ya kufaidika nazo na kueneza fitina na hofu katika safu za waislamu.

Na lau wangeirejesha kwa Mtume na kwa wenye mamlaka katika wao, wangejua wale wenye kuchunguza katika wao.

Dhamiri ya 'wenye mamlaka katika wao' inawarudia waislam. Ama dhamiri ya 'wenye kupeleleza katika wao' wafasiri wametofautiana. Kuna mwenye kuse-ma kuwa inarudia wale waliotangaza habari ya amani au vita. Wengine wakasema kuwa inawarudia wenye mamlaka. Hilo ndilo lililo dhahiri. Makusudio ya wenye mamlaka ni wale ambao Mtume (s.a.w.) anaowaamini kwa ujuzi wao wa kidini na kielimu, na ambao Mwenyezi Mungu amewakusu-dia aliposema: "Yeya ndiye aliyekusaidia kwa nusura yake na kwa waumini." (8: 62)

Maana yake ni kuwa ingelikuwa bora kwa wale waliotangaza waliyoyasikia katika habari za vita kuacha kuziingilia habari zilizowafikia na wazielezee kwa Mtume na wenye ujuzi katika Masahaba wake, ni wao tu wanaojua habari za vita na mbinu zake na kuvitoa vitu kutoka katika machimbuko yake na kuvirud-isha kwenye mashina yake.

Kwa hiyo kauli yake wangelijua wenye kuchunguza katika wao, maana yake ni kwamba wenye ujuzi wanajua hakika ya habari za kutangazwa na lengo lake. Kwa sababu wao ndio wanaofichua hakika kutoka katika chimbuko lake la kwanza na kufanya lile linalowajibisha hekima na masilahi.

Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngem-fuata shetani isipokuwa wachache tu.

Makusudio ya fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake ni kuteremshwa Qur'an na utume wa Muhammad (s.a.w.); na maana yake ni, lau si Kitabu cha

Kaashif5-68.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake, mngelibaki juu ya ukafiri na upotevu isipokuwa wachache tu, katika nyinyi; Mfano Qas bin Saida, Waraqa bin Nawfal, Zaid bin Amr na wengine ambao walimwamini Mungu peke yake kwa hisia safi za ndani kabla ya Mwenyezi Mungu kumtuma Muhammad (s.a.w.). Aina hii ya waumini wanaitwa Hanafiya. Na Hanif, kwa Waarabu, ni yule aliye katika dini ya Ibrahim (a.s.)

84.Basi pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; haikalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulizi ya waliokufuru.

Na Mwenyezi Mungu ni mkali zaidi wa kushambulia na mkali zaidi wa kuadhibu.

Aya 84 HAIKALIFISHWI ILA NAFSI YAKO

MAANA

Kaashif5-69.jpg

Basi pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; haikalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize waumini.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja katika Aya 77 kuhusu wale walioogopa kupigana wakasema; "Ewe Mola wetu kwa nini ukatufaradhia vita..."

Na katika Aya ya 81 wakadhihirisha twaa na kuficha uasi wakasema 'Tunatii' na wakala njama dhidi ya yale waliyoyasema, Akataja katika Aya ya 83 wale waliotangaza habari za vita na siri zake. Baada ya kutaja yote hayo ndipo akamwamrisha Mtume wake kupigana jihadi, kuitetea haki na kuwahimiza waislamu kupigana jihadi pamoja naye na kuachana nao wale walioachana naye. Kwa sababu yeye hana jukumu wala kukalifishwa na matendo ya mwingine; isipokuwa matendo ya nafsi yake tu. Hii ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Haikalifishwi ila nafsi yako tu.

107 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Sîyö mââhâ yake kuwa piğari^

wewe yeyote; kama ilivyosemwa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amemkataza Mtume na waislam kupigana, wakati wa mwanzo mwanzo wa kutanganza dini; na aliwaamrisha wasubiri na kuvumilia maudhi ya washirikina walipokuwa Makka. Kwa sababu kupigana wakati huo kulikuwa ni sawa na kujiua. Na hakuwamrisha jihadi ila baada ya kuhama kwenda Madina; wakawa sasa wanaweza kukabiliana na adui. Sasa ikiwa hali ni hiyo, itakuwaje Mtume aam-rishwe kupigana akiwa peke yake.

Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulizi ya waliokufuru.

'Huenda' hapa ni ya uhakika, kwa sababu ni katika maneno ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu havunji ahadi. Makusudio ya 'waliokufuru' ni wakuu wa Kiquraish ambao wamemtoa Mtume (s.a.w.) Makka na kuandaa jeshi la kumpiga vita mara nyingi. Na Mwenyezi Mungu alitekeleza ahadi yake, alimnusuru mja wake na akavishinda vikosi vya washirikina akiwa peke yake.

85.Mwenye kuunga mkono jema, hupata fungu katika hayo, na mwenye kuunga mkono baya hupata hisa katika hayo; na Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.

86.Na mnapoamkiwa kwa maamkuzi, basi itikieni kwa yaliyo bora au mrejeshe hayo hayo; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila jambo.

Kaashif5-70.jpgKaashif5-71.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-72.jpg

87.Mwenyezi Mungu hapana Mola ila Yeye. Kwa yakini atawaku-sanya siku ya Kiama, halina shaka hilo na ni nani msema kweli katika maneno kuliko Mwenyezi Mungu?

Aya 85 - 87:KUUNGA MKONO NA MAAMKUZI

MAANA

Mwenye kuunga mkono jema hupata fungu katika hayo. Na mwenye kuunga mkono baya, hupata hisa katika hayo.

Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa kuuunga mkono jema ni kuhimiza kupigana, na kuunga mkono baya ni kuvunja moyo wa kupigana. Kila mwenye kuhimiza na mwenye kuvunja moyo ana malipo ya kampeni yake na athari zake. Hilo ni katika kila kuunga mkono jambo la heri na kuunga mkono jambo la shari. Kuna Hadith isemayo: "Mwenye kuanzisha desturi nzuri atakuwa na malipo sawa na ya yule anayeifanya na mwenye kuanzisha desturi mbaya atakuwa na malipo sawa na ya yule anayeifanya."

Uislamu unapongeza kila tendo zuri, liwe litafuatwa na mwingine au limefany-wa na mlahidi au hata bila ya nia ya kitendo chenyewe. La muhimu ni kuwa liwe linaweza kuitwa heri, bora, jema, zuri au mfano wa hayo. Tumelielezea suala hilo katika kufasiri 3: 144 kifungu 'Kila mtu ana alilolinuia,' Pia katika 3: 178 kifungu 'Kafiri na amali ya heri.'

Na Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.

Yaani ana uweza wa kutulipa kila mmoja anavyostahiki humpa thawabu mwenye kuunga mkono mema na kumwadhibu mwenye kuunga mkono maovu.

Na mnapoamkiwa kwa maamkuzi, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au mrejeshe hayo hayo.

109 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Üîslâmü ümeİİfâriyârîehö Tavvft/d^kuwa hi hemböya itikâdîyâ

Salaam kuwa ni maamkuzi yanayohusiana nao, kuonyesha kuwa mwelekeo

wake katika maisha ni kueneza amani (salaam) na kuusimamisha uadui.

Kuongezea kuwa maana ya neno lenyewe Islam ni kuusalimisha uadilifu na

wema na heri na amani. Zaidi ya hayo Salaam ni katika majina ya Mwenyezi

Mungu Mtukufu:

"Yeye ndiye Mwenyezi Mungu hapana mola isipokuwa Yeye tu; Mfalme,

Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha

mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Jabbar, Mkubwa. Mwenyezi Mungu

yuko mbali na hao wanaomshirikisha naye." (59:23)

Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuhisabu kila jambo.

Ana hisabu kuacha kuitikia salaam na mengineyo katika kuacha haramu na kutenda mambo ya wajibu.

Mafakihi wametoa dalili kwa Aya hii kuhusu wajibu wa kuitikia salaam, ama kwa mfano huo huo, yaani kumrudishia salaam aliyekuamkia kwa herufi hizo hizo bila ya kuongeza au kupunguza; kwa mfano kuongeza: Wa rahmatullah nk. Kuitikia salaam ni 'wajib ainy' (wajibu wa mtu mwenyewe) kama ikielekezwa kwa mtu maalum. Na 'wajibu kifaya', kama ikielekezwa kwa watu wengi; kwa maana kama baadhi wakiitikia, imetosheleza kwa waliosalia; vinginevyo wote watalaumiwa na kustahiki adhabu. Kuna Hadith isemayo: "Kuamkia ni Sunna na kuitikia ni wajib."

Wafuasi wa Abu Hanifa wamesema makusudio ya neno 'Tahiya' katika Aya ni kukirimiwa kwa mali. Mwenye kukupa zawadi kitu, basi ni juu yako kumpa zawadi ya kiasi alichokupa au zaidi*11

NJIA MBALI MBALI ZA KUTHIBITSHA MAREJEO (UFUFUO)

Uislamu umeipa kipaumbile misingi ya mwanzo ya uislamu na kuithibitisha kwa mifumo mbali mbali. Misingi hiyo ni kumwamini Mungu, Mitume na Siku ya Mwisho.

Katika kitabu cha kwanza cha Tafsir Kashif, umewekea kila moja misingi hiyo mlango: Wa kwanza, tumeuzungumzia kwa anuani ya Tawhidi katika kufasiri 2: 21, wa pili, tumeuzungumzia kwa anuani ya 'Leteni Sura mfano wake' katika kufasiri 2: 23, na wa tatu, tumeulezea kwa anuani ya 'vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu' katika kufasiri 2: 28.

*11 Rudia Kitab Ahkamul Qur'an cha Qadhi Abu Bakr Al-andalusi

Kaashif5-73.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Mweriyeküfûâtİİİâ Âyâ zâ Öür'ânı'yehye"Wekİmâ'zİnâzbele7eâ'uOuö7atâkütâ' aina nyingi, miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:

1.   Kutolea habari kutokea Kiyama:

"Siku itabadilishwa ardhi hii kuwa ardhi nyingine na mbingu; nao watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu mmoja, Mwenye nguvu." (14:48)

2.    Kuelezea pamoja na kusisitiza kwa kiapo na kuondoa shaka; kama ilivyo katika Aya hii tuliyo nayo:

"Kwa yakini atawakusanya siku ya Kiama, halina shaka hilo."

3.    Kutolea dalili uwezekano wa ufufuo kwa kuumbwa mbingu na ardhi:

"Je, hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu - aliyeziumba mbingu na ardhi na hakuchoka kwa kuziumba - Ana uwezo wa kuwafufua wafu? Ndio, hakika Yeye ni muweza wa kila kitu." (46:33)

4.   Kutoa dalili kwa kuumbwa mimea:

"Na Mwenyezi Mungu ndiye anayepeleka pepo ziyatimue mawingu na tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa na kwayo tukaihuisha ardhi baada ya kufa kwake; kama hivyo ndivyo kufufuliwa." (35:9)

5.   Kutoa dalili kwa kuumbwa kwa mara ya kwanza kwa binadamu:

"... Hapo watasema: Ni nani atakayeturudisha? Sema: Ni yule aliye-waumba mara ya kwanza ..." (17:51)

Kutoa dalili kwa ushahidi uliotokea. Miongoni mwa matukio hayo ni haya yafu-atayo: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwafisha jamaa katika wana wa Israel kisha akawafufua Qur'an yaeleza juu ya hilo

"Na mliposema : 'Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi,' Yakawanyakuwa mauti ya ghafla na hali mwaona. Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru." (2: 55 - 56)

Mtu mmoja katika wana Israel alifufuliwa baada ya kuuliwa: "Tukasema: Mpigeni kwa baadhi yake (huyu ng'ombe), Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anawaonyesha dalili zake ili mpate kufahamu." (2:73)

Vilevile Mwenyezi Mungu alimfufua Uzair baada ya kufa kwake:"... Mwenyezi Mungu akamfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua ..." (2: 259) Pia Mwenyezi Mungu aliwafufua ndege wane wa Ibrahim baada ya kuwakatakata na kuwaweka mafungu : " kisha waite, watakujia mbio ..." (2:

111

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

260)...

Na aliwafufua watu wa pangoni baada ya kuwafisha miaka 309: "... Namna hii tuliwafufua ili waulizane baina yao ..." (18: 19)

Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Na hakika tumewapigia watu mifano ya kila namna katika hii Qur'an ili wapate kukumbuka." (39:27)

Je, atakumbuka mjinga anayefahamishwa yule ambaye hashindwi na kitu cho-

chote na yule asiyeweza kitu chochote? Vipi ataamini mnafiki siku watakay-

otukuzwa wakweli na kudhalilishwa wanafiki? Wala sijui ni madhara gani

watakayopata jamii au watu kwa kuamini siku atakayopambanuliwa mwema na

mwovu na mahakama watakayokuwa sawa watu wote mbele ya haki na uadil-

ifu?

88. Mna nini nyinyi mmekuwa

makundi mawili katika (habari

ya) wanafiki, na hali Mwenyezi

Mungu amewageuza kwa yale

waliyoyachuma? Je, mnataka

kumwongoza                ambaye

Mwenyezi Mungu amemuacha

kupotea? Na ambaye

Mwenyezi Mungu amemuacha

kupotea, hatampatia njia.

89.Wanapenda lau mngekufuru kama walivyokufuru wao mkawa sawasawa. Basi msi-fanye katika wao marafiki mpaka wahame katika njia ya Mwenyezi Mungu. Wakikataa wakamateni na muwaue popote muwakutapo, wala msifanye katika wao rafiki wala msaidizi.

Kaashif5-74.jpgKaashif5-75.jpg

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano '9Ö7Mâ""wale""wâMöifünğâmanâ"'"nâ" watu ambao baina yenu na wao mna ahadi, au wakawajia hali ya vifua vyao vina dhiki kupigana nanyi au kupigana na watu wao. Lau Mwenyezi Mungu angelita-ka angewasaliti nao wakapi-gana nanyi. Watakapojitenga nanyi, wasipigane nanyi na wakawapa amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwafanyia njia ya kupigana nao.

Aya 88-90 IMEKUWAJE KUWA MAKUNDI MAWILI KATIKA HABARI YA MAKAFIRI

MAANA

Mna nini nyinyi mmekuwa makundi mawili katika habari ya wanafiki.

Aya hii ilishuka kuwahusu wanafiki waliobaki katika mji wa Makafiri na wala wasihame kwenda Madina, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mpaka wahame." Kwa sababu Hijra (kuhama) inakuwa ni kutoka mji wa ukafiri kwenda kwenye mji wa uislam tu. Na kabla ya kutekwa Makka, mji wa Madina pekee ndio uliokuwa mji wa uislam.

Dhahiri ya Aya hii ni wazi kuwa hukumu ya aliyekuwa mnafiki, akabaki katika mji wa ukafiri sio hukumu ya mnafiki anayekaa katika mji wa kiislamu. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kuuawa hao na kuwateka, kinyume cha hawa.

Kabla ya kushuka amri hii Masahaba walitofautiana, wakagawanyika makundi mawili kuhusu hukumu ya wanafiki ambao wamebaki kwenye mji wa ukafiri. Kundi moja likaonelea kuwa ni lazima kuvunja uhusiano nao na kuacha kuwa-saidia na chochote, tena kuwatangazia vita; sawa na aliyedhihirisha ushirikina na uadui kwa waislamu. Kundi jingine likaonelea kuweko kuvumiliana

Kaashif5-76.jpg

113 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"kuwasamehe ha"kuwafanyia müamâîa wa waisiamu.

Inaonyesha kuwa Mtume (s.a.w.) alinyamaza kuhusu tofauti hizi mpaka Mwenyezi Mungu alipompa ufumbuzi kwa kusema kwake: "Mna nini nyinyi mmegawanyika makundi mawili katika habari ya wanafiki."

Yaani haitakikani mtofautiane kuhusu mambo yao, bali ni juu yenu kuwa na kauli moja ya kutovumiliana nao kwa hali yoyote ile; na Mwenyezi Mungu akabainisha sababu ya hilo kwa kusema kwake: Na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa yale waliyoyachuma.

Yaani amewarudisha kwenye hukumu, ya makafiri wanaopiga vita, ya kujuzu kuwaua na kuwateka. Kwa sababu hao ni kama kafiri anayepiga vita tu, au wana madhara zaidi kwa kubakia kwao kwenye mji wa ushirikina ambao hana faida nao isipokuwa adui wa uislamu.

UPOTEVU

Je mnataka kumwongoza ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha kupotea.

Hii inafahamisha kwamba lile kundi lililotaka kuwavumila lilikuwa na matumai-ni ya kuwa hao wanafiki watarudi kwenye uongofu, Mwenyezi Mungu akaika-ta tamaa yao kwa kusema: Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea hatampatia njia.

Unaweza kuuliza: Kwanza Mwenyezi Mungu -uliotukuka usemi wake -ameeleza kwamba Yeye amewageuza hao wanafiki kwa sababu ya kuchuma kwao na kuchagua kwao kubaki katika mji wa makafiri, kisha tena anasema kwamba Yeye ndiye aliyewapoteza. Kwa hiyo upotevu ameutegemeza kwake baada ya kuutegemeza kwao. Sasa kuna wajihi gani katika kukusanya yote mawili?

Jibu: Makusudio ya aliyeachwa kupotea na Mwenyezi Mungu sio kuwa ni kuumba upotevu kwao, la isipokuwa ni kwamba mwenye kukengeuka na njia ya haki na uongofu kwa matakwa yake akifuata njia ya batili na upotevu kwa hiyari yake, basi Mwenyezi Mungu ataachana naye na atamwacha na mambo yake. Hapana mwenye shaka kwamba mtu anayeachiwa na Mwenyezi Mungu, hatapata njia ila ya upotevu. Maana haya ndiyo yanayooana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "... Na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa yale waliyoyachuma."

Kaashif5-77.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kwa ufasaha zaidi ni kwamba kila mwenye kufua

Mwenyezi Mungu anamwingiza katika usaidizi wake na kumchunga kwa taw-fiki yake: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wale wanaomcha na wale wafanyao mema." (16:128).

Usaidizi huu, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wanaomcha unaitwa uongo-fu, tawfiki, mapenzi na utegemezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kila mwenye kufuata njia ya upotevu, Mwenyezi Mungu huachana naye wala ham-rudishi kwenye uongofu kwa kumlazimisha. Kuachana naye huku kunaitwa upotevu, utwezaji na kugeuzwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa ibara moja ni kwamba upotevu kutoka kwa Mwenyezi Mungu maana yake ni ukombo sio usawa: na maana ya uongofu kutoka kwake Mwenyezi Mungu ni upole na upangaji wa mambo. Hapana budi kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) inapelekea upole kwa mja wake na kutoepukana naye; sawa na mama asivyoepukana na mwanawe. Ila itakapokuwa mja ndio sababu inay-owajibisha kuepukana na Mwenyezi Mungu kwa njia ya kumwasi; kama mama anavyoepukana na mtoto wake aliyezidi sana kumwudhi.

Wanapenda lau mngekufuru kama walivyokufuru wao mkawa sawasawa.

Kila mtu anapendelea watu wote wawe upande wake. Imetangulia tafsiri yake katika 2: 109.

Basi msifanye katika wao marafiki mpaka wahame katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya kuhama Mtume (s.a.w.) kwenda Madina. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwajibisha kuhama (Hijra) kwenda Madina kwa kila mwislamu ila akishindwa au kupewa idhini na Mtume kubaki kwa masilahi yanayowarudia waislam.

Miongoni mwa Aya zilizohimiza kuhama ni: "Na wale walioamini lakini hawakuhama hamna haki ya kuwalinda hata kidogo mpake wahame ..." (8:72)

Siri ya hilo - kama uonavyo - ni kwamba Waislamu walikuwa wachache kabla ya kutekwa Makka. Kama wakitengana huku na huko watakuwa wanyonge na maadui watavamia. Lakini kama wakikusanyika mahali pamoja karibu na Mtume (s.a.w.) watakuwa na nguvu na kuogopewa. Zaidi ya hayo kuna faida nyingi zinazotokana na kuwa pamoja na mshikamano. Kukaendela kuhama kwenda Madina ni wajibu mpaka ilipotekwa Makka na Mtume, Mwenyezi Mungu akamnusuru mja wake na maadui zake na kuingia watu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi, na kukawa hakuna sababu ya kuhama.

Kaashif5-78.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Mtüme wa Mwehyezi Muh^^ kutekwa (Makka)."

Wakikataa wakamateni na muwaue popote muwakutapo.

Yaani hao wanafiki kama hawatawacha mji wa ukafiri na kuhama kwenda Madina na kuungana na Mtume na waislamu, basi wakamateni na muwaue popote mtakapowapata. Wala msifanye katika wao rafiki wala msaidizi.

Yaani achaneni nao kabisa, msiwasaidie wala kuwalinda katika chochote. Unaweza kuuliza: Uislamu ni dini ya uhuru na kuvumiliana na vikundi vyote na watu wa dini zote na sharia yake, ikilinda maisha ya watu, tena watu wote, na haki zao za kimaana na kimaada, bila ya kuangalia rai, maoni yao na itikadi zao. Sasa imekuwaje hapa unaamrisha kuwateka wanafiki na kuwaua popote watapopatikana?

Jibu: Kuna tofauti baina ya makundi na watu wa dini, bali hata na walahidi wanaotangaza maoni yao na itikadi zao kwa watu na wasidhamirie uadui kwa watu wala wasipange njama au kuwasaidia wanaovunja haki; kuna tofauti kubwa sana baina ya hawa na wanafiki ambao wamedhihirisha uislamu na kufichika na neno la uislamu na wakabaki katika mji wa makafiri kwa makusu-dio ya kuwafanyia vitimbi waislamu, kuwafanyia njama na kuwasaidia maadui.

Kwa hiyo amri ya kuwateka na kuwaua ni malipo ya uadui wao na njama zao kwao. Ama kuvumiliana kwa uislamu na vikundi vingine na watu wa dini nyingine, kunafungamana na msingi wake katika kuuhami uhuru wa kila mtu na kuacha kulazimisha katika maoni na itikadi, iwe ya haki au ya batili, maadamu kila mtu ana mzigo wake, na watu wako katika amani.

Swali la pili lililotokana na jibu la swali la kwanza: Uislam unavumiliana na wanafiki; sawa na unavyovumilia na makundi mengine na watu wa dini nyingine kwa dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake kujipurukusha nao; kama ilivyotangulia katika Aya 63 ya Sura hii: "Basi achana nao na uwape mawaidha..."

Jibu: Aya hiyo ilishuka kwa wanafiki waliokuwa pamoja na Mtume (s.a.w.) Madina. Hawakuwa na wasaa wa kushirikiana na washirikina kwa kuwa mbali nao na kuwa karibu na Mtume na vile vile nguvu za waislamu. Na Aya tuliy-onayo (89) ilishuka kwa wanafiki waliong'anga'nia kubakia katika mji wa

Kaashif5-79.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'makaWi kw^

alimwamrisha Mtume kuwafanyia amani wanafiki wakati waislamu walipokuwa dhaifu wenye wasaidizi wachache. Kisha akamwamrisha kuwaua baada ya kuwa uislamu una nguvu na wasaidizi (Ansari) wengi; sawa na alivyowaamu-ru kuvumilia kule Makka na kupigana jihadi walipokuwa Madina.

Baada ya kuamrisha Mwenyezi Mungu kuadhibiwa hao wanafiki maadui, ali-wavua kutokana nao sehemu mbili:

Sehemu ya Kwanza ni wale aliowaashiria kwa kauli yake: Ila wale walio-fungamana na watu ambao baina yenu na wao mna ahadi. Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakusudia kwamba katika hao wanafiki mwenye kukimbilia kwa watu ambao wana mkataba wa amani na waislamu, basi mkim-bizi huyu hatatekwa wala kuuawa kwa sababu yeye - katika hali hii - anakuwa ana salama na waislamu, sawa na aliyekimbilia kwao. Kwa hiyo hawatamwingilia.

Ni vizuri hapa tumnukuu Razi, anasema: "Jua kwamba hii inadhamini bishara kubwa kwa watu wenye imani. Kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliondoa upanga kwa aliyewakimbilia waislamu, basi kumwondolea adhabu huko akhera aliyekimbilia kwenye mahaba ya Mwenyezi Mungu na mahaba ya Mtume wake ni zaidi."

Hapana mwenye shaka kwamba kuwapenda Ahlul bait wa Mtume ni kumpen-

da Mwenyezi Mungu na Mtume, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu

Mtukufu:

Sema: "Siwaombi malipo yoyote isipokuwa kuwapenda ndugu(kizazi changu)

." (42: 23)

Sehemu ya pili Mwenyezi Mungu amewaashiria kwa kusema. Au wakawajia hali ya kuwa vifua vyao vina dhiki kupigana na nyinyi au kupigana na watu wao.

Yaani wale ambao wanaona uzito kupigana na waislamu pamoja na watu wao washirikina au kupigana na watu wao pamoja na waislamu, na wakaja kwa Mtume (s.a.w.) kutaka awaridhie wawe katika msimamo usiofungamana na upande wowote, hawa vile vile wataachwa, hawatauawa wala hatatekwa yey-ote katika wao. Kwa sababu hao si wapiga vita. Mfano bora unaofasiri Aya hii ni ule uliokuja katika Majmaul-bayan kuwa jamaa katika Ashjai walikuja kwa Mtume (s.a.w.) wakamwambia: "Nyumba yetu iko karibu na yako na

117

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

tunachukia kukupiga vita na kuwapiga vita watu wetu; na tumekuja il tupatane. Akawakubalia na akapatana nao; wakarudi."

Hakuna nguvu na ukweli wa dalili ya kuwa uislamu ni amani kwa mwenye amani na inampiga vita mwenye kupiga vita, kuliko dalili hii.

Lau Mwenyezi Mungu angelitaka angewasaliti nao wakapigana nanyi.

Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hajiingizi kwa matakwa yake ya Takwin *12 Katika mambo ya watu isipokuwa anakusudia kwa kauli yake hii kuwakum-busha waislamu fadhila zake kwao na kwamba inawezekana kuwakusanya wote kwa maadui wa waislamu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwaondolea hilo kwa wao kuwa na msimamo wa kutofungamana na sehemu yoyote. Kwa hiyo kusema kwake Lau Mwenyezi Mungu angelitaka angewasaliti nao wakapigana nanyi, maana yake ni angeliwafanya wawashambulie na wala asingewajalia na moyo wa kupatana. Na hii si katika matakwa ya Takwin, bali ni matakwa yaTawfiki kama sikosei.

Watakapojitenga nanyi, wasipigane nanyi na wakawapa amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwafanyia njia ya kupigana nao.

"Hakika njia iko kwa wale wanaodhulumu watu na wakawafanyia jeuri katika ardhi pasipo haki ..." (42: 42)

"Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia hisani na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya dini wala hawakuwafukuza katika nchi zenu ..." (60: 8)

"Na wakielekea katika amani, nawe pia ielekee." (8: 61).

Na Aya nyinginezo zinatoa mwito wa mapenzi, udugu na usawa, vilevile kusaidiana katika kila jambo lenye masilahi ya watu kwa njia yoyote. Kuchunga zaidi kwa haki kuliko katika uislamu ni kwamba unazingatia kuutu-mikia ubinadamu kuwa ndio uti wa mgongo wa dini, bali ndio njia pekee ya kumwelekea Mwenyezi Mungu.

*12Tumezungumzia matakwa ya Mwenyezi Mungu 'Takwin' na Tashrii katika kufasiri (2: 26 - 27)

Kaashif5-80.jpg

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-81.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 91.Mtawakutawenginewanataka

wapate amani kwenu na wapate amani kwa watu wao; kila wakirejezwa kwenye fitna hudidimizwa                     humo.

Wasipojitenga nanyi na kuwapa amani wala kuzuia mikono yao, basi wakamateni muwaue popote muwakutapo; na hao ndio ambao tumewafanyia hoja zilizo wazi juu yao.

Aya 91 MTAWAKUTA WENGINE

HAKUNA KUUANA WALA VITA KATIKA U IS LAM

Aya zilizotangulia zimeonyesha namna mbali mbali za wale ambao Mtume (s.a.w.) alipata kutoka kwao aina za vitimbi na uasi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Aya hii inaonyesha sura nyingine ya kundi la watu ambao ni wengi kila wakati na kila mahali. Yaani wale wenye dhambi ambao hawana msimamo isipokuwa kugeukageuka tu; wanaamini msimamo fulani kwa muda tu; kisha wanaukanusha.

Sisi hatukatai kuwa binadamu anageuka kutokana na hali zake, hilo hutokea mara nyingi kama tulivyoeleza katika kufasiri 2: 143, kifungu cha 'Kubadilika hulka na fikra.' Lakini pamoja na yote haya tunaitakidi - kulingana na hali ilivyo - kwamba baadhi ya watu wana tabia ya kigeugeu wanabadilika kutoka hali hii hadi nyingine, hata kama wakiwa katika hali moja tu.

Kaashif5-82.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Mtawakuta wengine wanataka wapate

watu wao; kila wakirejezwa kwenye fitna hudidimizwa humo.

Makusudio ya kurejezwa ni kuitwa, fitna ni ukafiri na kudidizwa ni kuingia.

Maana yake ni kuwa kundi hili kila linapoitwa kwenye ukafiri na kurtadi wanakubali na kuwa wabaya zaidi ya kafiri uliyethibiti ukafiri wake. Maelezo mazuri hasa kuelezea hali yao, ni yale waliyoyasimulia baadhi ya wafasiri kuwa, wao walikuwa wanaporudi kwa watu wao, mmoja wao huambiwa sema kombamwiko (mende) ni Mungu wangu na nyani ni Mungu wangu, naye hukubali na kusema hivyo hivyo.

Kadiri wanavyofikia watu hawa katika hali ya kuporomoka, kukosa utu, na kigeugeu baina ya ukafiri na imani, lakini Uislam unawaacha tu na mambo yao, maadam hawajafanya uadui wala vita. Ikiwa watafanya uchokozi na wakapi-gana, basi uislam unaamrisha kupigana nao popote walipo, ikiwa watakuwa wanaendelea na vita. Haya ndiyo aliyoyakusudia Mwenyezi Mungu kwa kusema kwake.

Wasipojitenga nanyi na kuwapa amani wala kuzuia mikono yao, basi wakamateni muwaue popote muwakutapo.

Hii ni dalili miongoni mwa dalili kadhaa zinazoelezewa na Qur'an na Hadith za Mtume kwamba msingi wa dini ya Kiislamu ni kutoua wala kupigana vita ila kwa kumzuia mwenye kupigana na kueneza ufisadi duniani.

Kwa hivyo basi uislamu umeruhusu vita kwa namna ile ile iliyoruhusu sheria za zamani na za sasa na kukubaliwa na akili zote. Pamoja na dalili zote hizi, maadui wa uislamu bado wanang'ania kusema kuwa uislam ni dini ya upanga; sawa na yule aliyesema: "Ni mbuzi tu hata kama akiruka."

Angalia Aya iliyotangulia kisha uikutanishe na hii, utaona kila moja inatilia mkazo kuwa vita havikukubaliwa katika sharia ila kwa kujikinga na kuondoa ufisadi.

120 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

92.Wala haiwi kwa muumini kumwua muumini (mwenzake) ila kwa kukosea. Na mwenye kumwua muumini kwa kukosea, basi amwache huru mtumwa mwislamu na atoe diya kwa watu wake ila watakapoifanya sadaka.

Na ikiwa ni mmoja wa watu walio maadui zenu, naye ni muumin, basi ni kuacha huru mtumwa muumini. Na ikiwa ni katika watu ambao baina yenu nyinyi na wao pana ahadi, basi ni diya kwa watu wake na kumwacha huru mtumwa muumini. Na ambaye hakupata basi ni kufunga miezi miwi li yenye kufuatana. Ni kitubio kitokacho kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.

93.Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemughadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-83.jpg

121

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ■.

Aya 92-93KUÜÂ KWA KÜTOKÜSÜDİÂ NÂ KÜKÜSÜDIA

 MAANA

Wala haiwi kwa muumin kumwua muumin (mwenzake) ila kwa kukosea. Na mwenye kumwua muumin kwa kukosea, basi amwache huru mtumwa mwislamu na atoe diya kwa watu wake ila watakapoifanya sadaka.

Kuua kuko aina tatu:

1.  Kukusudia: Ni kudhamiria mtu mwenye akili aliyebaleghe kumwua mwingine moja kwa moja; kama vile kuchinja na kunyonga. Au kwa kus-ababisha; kama vile kutia sumu kwenye chakula au kumzuilia mtu asile mpaka afe na njaa.

Ukithibiti usawa wa muuaji na muuliwa kidini na kiungwana, na wala muuaji asiwe ni baba wa muuliwa, hapo msimamizi wa aliyeuliwa atakuwa na hiyari ya kumuua kwa kulipiza kisasi au kuchukua fidia ikiwa muuaji atakubali kuitoa. Hiyari ya kulipiza kisasi na kuchukua fidia ni ya msimamizi (walii) katika kuua kwa makusudi. Akichagua fidia, basi muuaji anayo hiyari ya kutoa fidia au ajitolee kuuawa. Kwa hiyo msimamizi hawezi kumlazimisha muuaji kutoa fidia wala muuaji hawezi kumlazimisha msimamizi kuchuka fidia.

Fidia ya kisheria ni Dinar elfu moja ambazo ni sawa na 3.529 Kg za dha-habu.

2.  Bila ya kukusudia: Ni kuwa muuaji amekusudia kitendo, lakini akakosea makusudio; kama kumpiga mototo kwa kumtia adabu akafa. Kuua kwa aina hii kunawajibisha fidia sio kisasi. Fidia yake ni Dinar elfu moja; kama fidia ya kukusudia. Tumezungumza kuhusu kuua kwa makusudi na shabihi -kusudio, katika kufasiri (2: 178 - 179)

3.Kukosea: Ni kuwa muuaji alikosea kitendo na makusudio; kama mwenye kupiga mshale mnyama ukampata mtu ukamuua. Hapo mtu siye aliyekusudiwa kufumwa wala kuuliwa. Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Na mwenye kumwua mwislamu kwa kukosea, basi amwache huru mtumwa mwislamu na diya kwa watu wake ila watakapoifanya sadaka."

122

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Qur'an na Hadith kwa pamojazimefahamisha kuwa mwenye kumuua mwis

kwa maksudi , basi ni wajibu kwake atoe kafara ya kumwacha huru mtumwa, kufunga miezi miwili yenye kufuatana na kuwalisha masikini sitini; atakusanya yote matatu. Hili ndilo linaloitwa kafara la kuchanganya.

Ikiwa kuua ni bila ya kukusudia au kukosea, basi atatoa kafara la kumwacha huru mtumwa; akishindwa afunge miezi miwili inayofuatana, akishindwa awal-ishe masikini sitini.

Fidia ya kuua kwa makosa mzigo wake utabebwa na walio baleghe wenye akili na walio na uwezo katika ndugu wa karibu wa upande wa baba; kama vile kaka, ami na watoto wao wanaume. Kiasi cha fidia ni 1000 Dinar. Fidia ni haki ya walii (wasimamizi) wa aliyeuliwa; wakipenda wataidai na wakitaka wataisamehe Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, "ila wakiifanya sadaka."

Mafakihi wanasema limewajibishwa kafara kwa mwenye kuua bila kukusidia ili kuwa ni onyo la uzembe na himizo la kuchukua tahadhari katika mambo yote. Imewajibishwa fidia kwa ndugu zake kwa kumuhurumia aliyekosea. Na kumewajibishwa kuchukuliwa kisasi kwa aliyeua makusdi, ili kumtia adabu kwa kukusudia haramu.

Na ikiwa ni mmoja wa watu walio maadui zenu, naye ni muumin, basi ni kuacha huru mtumwa muumin.

Makusudio ya watu walio maadui ni makafiri wenye vita na waislamu. Dhamiri ya 'naye' inarudia kwa aliyeuawa. Maana yake ni kuwa mwislamu akiua mtu kwa kuitakidi kwamba yeye ni kafiri, kisha ikabainika kuwa yeye ni mwislamu anayekaa kwa watu wake waliomakafiri, hapo hapatakuwa na chochote kwa muuaji zaidi ya kumwacha huru mtumwa; hakutakuwa na fidia. Kwa sababu watu wa aliyeuliwa ni makafiri, wakipewa fidia itawongezea nguvu kuwapiga vita waislamu.

Na ikiwa ni katika watu ambao baina yenu nyinyi na wao pana ahadi, basi ni diya kwa watu wake na kumwacha huru mtumwa muumin. Na ambaye hakupata basi ni kufunga miezi miwili yenye kufuatana.

Yaani ikiwa mwislamu aliyeuawa kimakosa anatokana na watu makafiri, lakini hawana vita na waislam kwa vile wana mkataba wa amani na waislamu, hapa itatolewa fidia kwa watu wake, hata kama ni makafiri, kwa sababu hukumu yao katika hali hii ni sawa na hukumu ya waislamu katika wajibu wa fidia.

123

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Na ni juu ya rTİüüaji k

afunge miezi miwli inayofuatana. Imewekwa sharia hii ya kafara kwa muuaji ili

iwe ni toba kwa aliyoyafanya.

Na mwenye kumuua muumin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemughad-hibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.

Tumeeleza mwanzo wa maelezo namba (1) kuhusu hukmu ya aliyeua makusudi na kwamba yeye atauwawa ila akisamehe walii. Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anataja kwamba malipo yake huko akhera ni kukaa milele motoni, ghadhabu na laana ya Mwenyezi Mungu na adhabu kubwa.

Adhabu zote hizi nne ni kutilia mkazo. Makusudio ya ukubwa wa adhabu kutokana na kosa hili ni kuwa ni kosa kubwa la kutisha na kwamba ni katika madhambi makubwa ambayo hayana mfano wake zaidi ya ukafiri. Baadhi ya mafakihi wamesema: Ni udhihirisho zaidi wa ukafiri na maana yake.

Utakuja ufafanuzi wa kuua nafsi kwa dhulma 'Inshaallah' katika kufasiri (5: 32). Na yemetangulia maelezo ya kudumu motoni katika kufasiri (2, 257) kifungu cha 'kudumu motoni.'

94.Enyi mlioamini! Mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakikisheni wala msimwambie mwenye kuwapa Salaam: Wewe si mwislam. Mnataka mafao ya duniani na kwa Mwenyezi Mungu kuna ngawira nyingi! Hivi ndivyo mlivyokuwa nyinyi hapo mbe-leni, na Mwenyezi Mungu akawafanyia hisani. Basi hakikisheni; hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyatenda.

Kaashif5-84.jpgKaashif5-85.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Aya 94 KUUDHIHIRISHA UISLAM KUNATOSHA KUWA NI KUUTHIBITISHA

MAANA

Enyi mlioamini! Mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakik-isheni, wala msimwambie mwenye kuwapa salamu: Wewe si mwislamu.

Wameafikiana wafasiri na wapokezi wa Hadith sababu iliyowajibisha kushuka Aya hii ni kuwa Mtume alituma kikosi katika Masahaba wakakutana na mtu mmoja mwenye mali; kama kondoo n.k. Wakamdhania ni kafiri; akatamka neno la kufahamisha uislamu wake, katika maamkuzi au tamko la shahada n.k. Baadhi wakaona hiyo ni kutaka kujiokoa na kifo, waka mwua.

Mtume alipolijua hili alihisi taabu na kumlaumu muuaji akasema: Hakika ame-hifadhika na kuuliwa kwa tamko hilo. Akamwambia - kama inavyoelezwa katika baadhi ya riwaya - "Huoni kuwa umeupiga mapande moyo wake!"

Matamshi ya Aya hayakatai maana haya. Kwani kauli yake, "mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi thibitisheni." Maana yake mtakapok-wenda kwenye Jihadi pelelezeni; msikimbilie kumua ambaye mnamtilia shaka katika dini yake na uadui wake; wala msimwambie mwenye kuwapa salamu wewe si mwislamu. Kwa sababu kila mwenye kudhihirisha uislamu anayo haki waliyonayo waislam; hasa katika mambo ya kuhifadhi damu na mali ama bati-ni yake inajulikana kwa Mungu peke yake.

Mnataka mafao ya duniani na kwa Mwenyezi Mungu kuna ngawira nyin-gi!

Inafahamisha kuwa lililowapelekea kuua ni tamaa ya mali aliyokuwa nayo. Hilo ndilo lililowafanya wawaze kuwa kudhihirisha kwake tamko la uislamu kulikuwa na makusudio ya kuokoka. Ni mara nyingi sana mtu kufikiria yale yasiyo ya uhakika. Inakuwa hali ilivyo ni vingine, hata kama anajua ndivyo hivyo. Haya ndiyo maajabu ya mtu. kwa hali yoyote Mwenyezi Mungu ame-watanabahisha makosa yao haya na kwamba wao wameharakia ngawira na ngawira za Mwenyezi Mungu na neema zake hazina idadi, ambazo atawabadilishia na mali ya aliyeuwa wa zaidi na zaidi.

Hivyo ndivyo mlivyokuwa nyinyi zamani.

Hili ni jibu lao na kukivunja kitendo chao kwa mantiki ya kiakili na ya hali hal-

Kaashif5-86.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

isi...Taarifa yake ni kuwanyinyiI hapo mwanzo mlikuwa wash

mkaingia katika Uislam kwa tamko lile lile alilolitamka yule aliyeuliwa; na Mtume alilikubali kutoka kwenu. Kwa tamko hili zimehifadhiwa damu zenu na mali zenu. Kwa hiyo ilikuwa ni juu yenu kumkubalia yule mliyemuua kama vile Mtume alivyowakubalia nyinyi. Hivi ndivyo walivyo watu wengi, wanataka wengine waridhie uchache, lakini wao wenyewe hawaridhii.

Na Mwenyezi Mungu akawafanyia hisani

Kwa kuwakubalia uislam na kuwafanya ni katika Masahaba kwa kutamka tu tamko la shahada, wala Mtume hakuyachunguza yaliyo nyoyoni mwenu. Kwa nini hamkufanyia mwingine vile alivyowafanyia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)

Basi hakikisheni; hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyatenda.

Yaani kuanzia sasa msifanye kitu mpaka muwe na uhakika nacho wala msimwadhibu yeyote kwa tuhuma au dhana. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa matukio yenu na ana hisabu kwa mnavyostahiki.

Mafakihi wameiingiza Aya hii katika Aya za hukumu *13 na wakatoa hukumu mbili za sharia.

Kwanza: Wajibu wa kuhakikisha katika kila kitu, hasa katika hukumu za kisharia na zaidi hasa katika damu na mali; ambapo wamewajibisha mafakihi katika mawili hayo kujichunga na kufanya ihtiyat na wakaongezea pia kuhu-siana na tupu.

Pili: Kila mwenye kutamka tamko la uislamu na akasema mimi ni mwislamu, basi hukumu yake ni hukumu ya waislam katika ndoa urithi na mengineyo ambayo yanafungamana na mtu akidhihirisha uislamu tu. Sio kwa undani.

13.Kila Aya inayotolewa hukumu ya kisharia, basi ni katika Aya za hukumu: Kama vile Aya za Hijja, Saumu, ndoa , urithi na vyakula vya haramu. Ziko karibu Aya 500. Mafakihi wa Kishia na Kisunni wameziandikia vitabu maalum. Miongoni mwa vitabu vya Sunni ni Ayatul-Ahkamul cha Al-Jiswas. Na miongoni mwa vitabu vya Shia ni Kanzul Urfan fi Ayatil-Ahkam cha al-Miqdad.

Kaashif5-87.jpg

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 95.Hawawi sawa waumini waliokaa

- wasiokuwa wenye madhara -na wenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Amewatukuza Mwenyezi Mungu katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa. Na wote Mwenyezi Mungu amewaahidi wema. Na amewatukuza Mwenyezi Mungu wenye kupigana Jihadi kwa malipo makubwa kuliko waliokaa.

96.Ni vyeo kutoka kwake na maghufira na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

WENYE KUPIGANA JIHAD NA WENYE KUKAA Aya 95 - 96:

Hawawi sawa waumini waliokaa - wasiokuwa wenye madhara - na wenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao.

Mwenye kubaki nyuma asiende katika jihadi kwa udhuru wa kisheria; kama vile upofu, ulemavu na mengineyo, basi amesamehewa, bali atapata malipo mema akiwa ni muumin mwenye ihlasi anayependa ushindi wa dini, na heri ya watu wake; na anayependelea lau angalikuwa mzima akashiriki na wanaopigana jihadi.

Kaashif5-88.jpg

127 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Küh'â"Hâdith iserriâyö:"Mtü yükö'pâmöjâ"nâ"anâyempehd^'v"Yâanİ7mwehye' kumpenda mwenye kupigana jihadi si kwa chochote ila kwa kuwa yeye ni mwanajihadi, basi naye ana malipo ya wapigania jihadi; mwenye kumpenda mkweli kwa sababu ya ukweli wake basi yeye yuko katika cheo chake; mwenye kumpenda dhalimu katika dhulma yake; basi yeye ni mshirika wake na mwenye kumpenda kafiri kwa ukafiri, basi ni kama yeye. Hii ndiyo hukumu ya wenye kukaa wasiokuwa na siha nzuri.

Ama wale wasiokuwa na udhuru katika wao wataangaliwa. Wakikaa bila ya kwenda kwenye jihadi ambayo wamewajibishiwa wao na wengineo; yaani kuwa vita ni vya wote. Hapo hawatasamehewa, bali watalaumiwa na ni wenye kustahili adhabu. Kwa sababu wao wameasi, kwa hiyo haifai kuwalinganisha na wapiganaji kwa hali yoyote kwa sababu kulinganisha ni kushirikisha; na hawa hawakushirikiana na wapigana jihadi katika kitu chochote; hata kama ikiwa jihadi ni faradhi kifaya (ya kutosheana), isiyokuwa na haja ya kushiriki wote, lakini bado wapigana jihadi ni bora kuliko waliokaa. Kwa sababu wao wamechagua uvivu - kujiuzulu na vita. Hawa ndio waliokusudiwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hawawi sawa waumini waliokaa ..."

Kwa hiyo maana yanakuwa ni hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu waliokaa, walio wazima na wale wapigania Jihadi ambao haikuwa jihadi ni wajibu kwao tu, bali ilikuwa wajibu kwa wote kwa njia ya kifaya, lakini wao ndio walioziba wajibu huu na wakautekeleza kwa ukamilifu na kuuondoa kwa waliobaki. Ni maana haya ambayo ameyakusudia Mwenyezi Mungu na kuyafafanua kwa kauli yake:

Amewatukuza Mwenyezi Mungu katika cheo, wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa.

Baada ya Mwenyezi Mungu kukanusha usawa baina yao na baina ya wale waliokaa anabainisha yale yaliyowapambanua wapigania Jihadi; ambayo ni ubora wao katika cheo kuliko waliokaa.

Kwa hiyo inakuwa kauli yake hii ni ufafanuzi baada ya kueleza kwa ujumla. Na siri ya kutukuzwa ni kama tulivyoeleza, kuchukua majukumu ya ulinzi peke yao; sawa na lau adui anashambulia mji, kukatokea kikundi kuwazuiwa kinyume cha kikundi kingine, hapo kimsingi kikundi cha kwanza kitatofautika na kikundi cha pili. Ingawaje kikundi cha pili hakitaadhibiwa baada ya cha kwanza kusimamia wajibu na kupatikana lengo lililotakikana.

128 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu waahidi wema.

Lakini tena akarudia kutilia mkazo na kuhimiza Jihadi kwa kusema:

Na amewatukuza Mwenyezi Mungu wenye kupigana Jihadi kwa malipo makubwa kuliko waliokaa.

Na akabainisha malipo haya makubwa kuwa Ni vyeo kutoka kwake na maghufira na rehema. Cheo kimoja tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko ulimwengu na vilivyomo ndani yake, je itakuwaje vyeo vingi! Ama rehema yake, hakuna kitu bora zaidi kuliko hiyo ila ambaye imetokana naye. Na inatosha kwa maghufira yake kuwa ni kusalimika na adhabu yake na machukivu yake.

Haya ndiyo maghufira, rehema na cheo kwa Mwenyezi Mungu. Mwenye kupa-ta moja tu, atakuwa katika walio juu, sikwambii atakayeyapata yote!

"Ewe Mola wangu! Hakika mimi nakuomba wepesi katika rehema yako na maghufira yako; na wewe wajua kuwa mimi naihitajia. Kwani itakuwaje kama utanineemesha na kunikwasisha? Kwani unahofia maghufira yako yatakwisha na hazina ya rehema yako (itakwisha)? Au ni nini ewe Mola wangu! Au ni kwa kuwa mimi nina dhambi? Ndio, lakini hujui kwamba mimi najua kuwa hakuna kimbilio ila kwako tu na kwamba kunanifurahisha mimi kunisamehe! Ewe Mola wangu! Ikiwa mimi ni muongo kwa niliyosema, basi nifanyie vile ninavyostahi-ki, na ikiwa ni mkweli kwa niliyoyasema, basi fanya vile unavyostahiki."

ALI NAABU BAKR

Amesema Razi (ninamnukuu): "Wamesema Shia kuwa Aya hii: Amewatukuza Mwenyezi Mungu wenye kupigana Jihadi kwa malipo makubwa kuliko wenye kukaa. Inafahamisha kuwa Ali bin Abu Twalib ni bora kuliko Abu Bakr. Kwa vile Ali alipigana Jihadi zaidi ya Abu Bakr..." Kipimo cha utofauti ni kuwa Ali alikuwa ni katika waliopigana Jihadi katika alivyomzidi Abu Bakr, na Abu Bakr alikuwa katika waliokaa. Ikiwa hivyo basi imewajibika kuwa Ali (a.s.) ni bora kuliko Abu Bakr."

Kisha Razi akawajibu Shia kwa kusema: "Tunawaambia: Kuua kwa Ali makafiri kulitokana na Mtume, kwa hiyo itawalazimu kwa hukumu yenu hii ya Aya, kuwa Ali ni bora kuliko Muhammad (s.a.w.). Na haya hayasemwi na mwenye akili. Kama mkisema: Kupigana Jihadi kwa Mtume pamoja na Makafiri ni kukubwa zaidi kuliko kwa Ali, kwa sababu Mtume alikuwa akipigana

Kaashif5-89.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'kutokaWa'na dMlTnâ'tö

hii ni kamilifu zaidi kuliko hiyo. Basi tunasema: Na sisi tukubalieni kuhusu Abu

Bakr kama mfano wake."

Huku ni ni kulala kabisa kwa mwanafalsafa wa wafasiri na wala siwezi kukuita kusinzia. Kwa sababu hizi zifuatazo:- Kwanza: kila mwenye kumlinganisha Muhammad (swa) na mmoja wa maswahaba zake, katika kuleta dalili na ubainifu, basi atakuwa ametoka katika uislamu, atake asitake. Kwa sababu Muhammad anatoa ubainifu kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu -kama tutakavyoeleza- na maswahaba wanatoa kutokana na mafunzo yake. Kwa hiyo basi cheo cha kwanza ni cha Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, cha pili ni cha Muhammad peke yake hana mwenzake na kuwamini wote waw-ili kuko daraja moja. Kwa vile kumwamina Mungu na mitume yake ni nguzo moja katika nguzo zinazousimamisha uislam, haitoshi moja peke yake. Ukhalifa na uswahaba ni matawi ya kumwamini Mungu na Mitume, na tawi haliwezi kufananishwa na shina.

Pili: Maana yaliyo wazi ya neno wenye kupigana Jihadi katika Aya, ni Jihadi kwa upanga, si kwa kingine kwa kukiri Razi katika tafsiri yake. Lakini yeye ameghafilika na aliyoyasema na akajipinga mwenyewe. Hebu tuiache dhahiri ya Aya na tafsiri zote, tumrudie yule ambaye Qur'an imeteremshwa kwenye moyo wake na tumwulize, ni yupi mbora wa watu? Tumsikilize atajibu nini.

Amepokea Muslim katika sahih yake, kwamba mtu mmoja alimwuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). "Ni nani mbora wa watu?" Akasema: "Ni mtu anayepigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake na mali yake."

Sote tunajua kuwa Ali alipigana zaidi Jihadi; kama alivyosema Razi, kwa hivyo anakuwa mbora wa watu, isipokuwa Mtume (s.a.w.); ambapo hakuna cho-chote zaidi ya daraja ya utume ila Uungu - kama tulivyobainisha - Na kila mmoja anajua kwa uwazi kwamba Jihadi kwa nafsi ni bora na kubwa kuliko Jihadi kwa mali. Kwa sababu mali hutolewa katika njia ya Jihadi kwa nafsi, lakini nafsi haitolewi katika njia ya mali.

Tatu: Hakika Mtume Mtukufu (s.a.w.) - kama tulivyotangulia kueleza - hakutoa dalili na hakubainisha,wala hakuondoa utatanishi yeye mwenyewe; bali yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alikuwa akimwelezea Muhammad (s.a.w.) naye akifikisha kwa kunukuu kwa herufi. Muhammad anaambiwa.

130

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Serhâ: Âtâihüisha yülei'MyeTümba'mâra'ya'kvvânzâ".".'.'"'(36:79)..

"Sema: Je, yuko katika washirika wenu aongozaye katika haki?" (10: 35)

"Sema: Hebu leteni Sura moja mfano wake na muwaite muwezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu mkiwa mnasema kweli." (10: 38)

"Sema: Je, mnawafanya wengine badala yake kuwa ni walinzi na hawajifai wenyewe kwa nafuu wala dhara" (13: 16)

Na Aya nyingine kadha. Jambo la ajabu ni kuwa Razi ameghafilika nazo baada ya kurefusha ufafanuzi na tafsiri zake. Ajabu ya maajabu ni pale ali-posema: "Basi na sisi tukubalieni kuhusu Abu Bakr kama mfano wake;" yaani kama mlivyomkubalia Muhammad. Hapana! tena hapana mara elfu! Si sisi wala mwislam yeyote atakayekukubalia wewe au mwengine kuwa Abu Bakr awe na mfano wa aliyo nayo Muhammad (s.a.w.) (katika kuleta dalili, hoja na kuondoa utatanishi na upotevu. Ila ikiwa Abu Bakr ni Mtume anayeteremshi-wa Wahyi.

Zaidi ya haya cheo cha Ali katika elimu hakikurubiwi na yeyote katika Masahaba. Inatosha kuwa ni ushahidi wa hilo. Hadith mutawatir iliyopokewa kutoka kwa Mtume inayosema: "Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake." Zimehifadhiwa turathi za kiislam kutokana na elimu ya Ali, kiasi ambacho hakikuhifadhiwa kutoka kwa Abu Bakr wala Sahaba mwengineo.

97.Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, wataambiwa: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa wanyonge katika ardhi. wataambiwa: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa pana mkahamia humo? Basi hao makazi yao ni Jahannam; nayo ni marejeo mabaya.

Kaashif5-90.jpgKaashif5-91.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

98.Isipokuwa wale wanyonge katika wanaume na wanawake na watoto (ambao) hawawezi kufanya hila yoyote wala kufua-ta njia.

99.Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe; na haki-ka Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa maghufira.

100.Na mwenye kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu atapata katika ardhi mahali pengi pa kukikimbilia na wasaa. Na mwenye kutoka nyumbani kwake ili kuhamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti, basi yamethibiti malipo yake kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

Kaashif5-92.jpg

132

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa "..

Aya 97 - 100A'FtD'H'l YA"MWENYEZl MÜNĞU Nİ PÂNÂ

 MAANA

Waislamu zama za Mtume (s.a.w.) walikuwa na Hijra mbili kutoka Makka. Ya kwanza ilikuwa ni ile ya kuelekea Uhabeshi (Ethopia), na ilikuwa miaka mitano tangu Mtume kuutangaza utume wake. Ya pili ilikuwa ile ya kuelekea Madina iliyokuwa miaka minane baadaye.

Wako Masahaba ambao walifanya Hijra mbili kama Jafar bin Abu Twalib ambaye maisha yake yaliishia kwa kufa shahid baada ya kukatwa mikono yake. Mwenyezi Mungu akamkirimu kutokana na mikono hiyo mbawa mbili atakazoruka nazo katika pepo; na ndio akatiwa 'Attwayyar' (Mrukaji).

Ama sababu ya Hijra (kuhama) ni kujiepusha na kuingia katika maangamivu, kukimbilia mahali pa amani kupanga mipango ya Jihadi na kuipinga batili. Kwa kutokana na Hijra (kuhama) na fadhila zake, uislamu umeshinda maadui zake. Lau si hiyo ungelizimika mwenge wake na kugeuka jivu linalopeperuka. Kwa ajili hii Hijra ikawa wakati huo ni fadhila kubwa na ni kitendo cha fahari cha kwanza ambacho hakikurubiwi na kitu chochote.

Mtume (s.a.w.) alihama kutoka Makka kwenda Madina na akawaamrisha waislamu wahamie huko. Wengi wakamwitikia na wengine wakabaki kwa kung'ang'ania mali zao na masilahi yao. Kwa sababu washirikina walikuwa hawamwachi mwenye kuhama kuchukua chochote katika mali yake.

Washirikina walikuwa wakimwudhi sana anayebaki hapo na kumzuilia na dini yake, akiwa hawezi kujitetea. Lakini alikuwa anaweza kujiepusha na vikwazo hivyo na kuisimamisha dini kwa njia za ukamilifu, kwa kuhama kutoka katika mji ulio na vita na waislam kwenda mji wa uislamu na amani (Madina) aliko Mtume na Sahaba. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu aliwatahayariza wale walioona kuwa ni heri kubaki katika nyumba ya ukafiri na kuipiga vita dini na watu wake. Aliwatahayariza na akawazindua kupitia Malaika kwa kusema:

Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao.

Kwa kuacha Jihadi na kuhama kwenda kwenye mji wa kiislamu, wakaridhia kubaki katika nyumba ya ukafiri, udhalili na kuharibu wajibu wa dini, Wataambiwa; mlikuwa katka hali gani? Yaani Malaika wa mauti watawaam-

Kaashif5-93.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

bia wale walioacha kuhama; mlikuwa vi

lawama na kusutwa. Ilivyo hasa ni kuwa lawama zinakuwa kwenye tukio maalum, ambalo hapa ni kule kukaa kwao nyuma ya ndugu zao wahamiaji ambao wamemtii Mtume katika kutekeleza mipango ya kuumaliza ushirikina na kuliinua neno la Mungu.

Akiuliza muulizaji; Je, makaripio haya na masuto kutoka kwa Malaika kwa wale waliorudi nyuma yalikuwa wakati wa kukata roho au ni baada yake?

Tutajibu kuwa ujuzi wa haya uko kwa Mola; yeye amelinyamazia hilo. Kwa hiyo na sisi tunalinyamazia vilevile. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia mambo si kwa kusahau, basi msijikalifishe nayo."

Watasema: Tulikuwa ni wanyonge katika ardhi.

Huu ni udhuru na kutafuta sababu kwa waliorudi nyuma. Maana yake ni kuwa waliorudi nyuma wanawajibu Malaika wanaowalaumu kwa uzembe wao katika mambo ya dini. Wanawajibu kwa kusema: Tulikuwa tumeshindwa,tunaonewa katika mji wa makafiri, kusimamia wajibu wa kidini. Kwa sababu washirikina walitukandamiza na kutuzuia kufanya tuliyokuwa tukiitakidi, Malaika wakajibu udhuru huu. Watasema: - Kwa kuwasuta - Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa pana mkahamia humo? Yaani mlikuwa mnaweza kuhamia mji wa kiislamu ambako mtaepukana na udhalili na kuweza kuitekeleza dini kwa uhuru; kama walivyofanya waislamu wengine.

Kama kuna kitu kinachofahamisha zaidi kuhusu malumbano haya, basi ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hamwadhibu yeyote ila baada ya kukamilisha hoja, bali ila baada ya kurundikana hoja kwake; kiasi ambacho kinamwacha mwenye dhambi asiwe na kimbilio ila msamaha wake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na rehema yake ambayo imeenea katika kila kitu, "... Ewe Mola wangu na mimi ni kitu zinienee rehema zako."

Basi hao - yaani waliorudi nyuma - makazi yao ni Jahannam, na ni marejeo mabaya. Isipokuwa wale wanyonge katika wanaume na wanawake na watoto (ambao) hawawezi kufanya hila yoyote wala hawawezi kufuata njia.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwakemea waliorudi nyuma, aliwavua walio na udhuru kwa ugonjwa au kukosa posho na akawaondolea takilifa ya Hijra. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakalifishi ila uweza wake.

Kaashif5-94.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Unaweza kuuliza kuwa kutolewa wanaume na wanawake wenye udhuru kuna mwelekeo maalum. Sasa kuna mwelekeo gani wa kutolewa watoto na inaju-likana kuwa watoto hawakalifiwi na kitu?

Swali hili limejibiwa kuwa maana ya neno Wildan ni watumwa na wajakazi. Ama sisi tunajibu kuwa watoto wengine wanaweza kuhama hasa vijana wado-go, bali baadhi yao wana uwezo zaidi ya watu wakubwa. Kwa ajili hii mtu anaweza akadhania kuwa kuhama ni wajibu kwa kila anayeweza. Hivyo Mwenyezi Mungu ameiondoa dhana hiyo na kubainisha kuwa Hijra ni wajibu kwa kila mwenye uweza ila akiwa ni katika watoto.

MAFAKIHI NA WAJIBU WA HIJRA

Mafakihi wameitolea dalili Aya hii kwamba mwislamu haijuzu kwake kukaa kwenye mji wa ukafiri ikiwa hawezi kuitekeleza dini, hata kama ni mji wake akiwa na milki na masilahi. Lakini hukumu hii siku hizi haina maudhui. Kwa sababu kila mtu katika kila mji anaweza kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa namna yoyote atakayo. Akiacha, basi yeye peke yake ndiye mwenye jukumu.

Unaweza kuuliza: Mtu akijua kuwa kukaa kwake katika mji usiokuwa wa kiis-lamu kunasababisha kuacha faradhi, si kwa kuwa mtu anamzuia, bali kwa udhaifu wa kukabiliana na msukumo; kama vile mchezo n.k. Je, inafaa kukaa katika mji huu?

Jibu: Akijua kwa yakini kwamba kwenda mahali popote, pawe ni mjini, kikao au sokoni ambako lazima kutamfanya aache wajibu au kufanya haram basi ni wajibu kwake kuepukana nako. Kwani sababu inayolazimu uharamu basi ni haramu. Mwenyezi Mungu anasema: "... Basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu." (6: 68)

Amirul Mumin (a.s.) anasema: "Hijra (kuhama) bado iko kwenye mipaka yake ya kwanza." Yaani, bado ipo hukumu yake ya wajibu kwa yule ambaye imekuwa uzito kutekeleza hukumu za dini yake ila katika mji wa waislamu. Ama kauli ya Mtume (s.a.w.): "Hapana Hijra (kuhama) baada ya kutekwa Makka," makusudio yake ni kuhama kutoka Makka. Hilo linafahamishwa na neno kutekwa Makka.

Na mwenye kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia na wasaa.

Riziki haziko nyumbani tu na kuhama hakuwajibishi kukosa. Miji ya Mwenyezi Mungu ni mingi, riziki yake ni pana na neema katika kila mji hazihisabiki, na

Kaashif5-95.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

kwambamafukara wengi wamejikusanyia mM küle w

cho walikuwa hawaoti kupata hata sehemu ndogo tu walipokuwa nyumbani

kwao.

Lau wale waliorudi nyuma wangelihama, wangelipata riziki na utukufu kiasi cha kuwadhalilisha washirikina waliowapa aina kwa aina za udhalili na vikwazo. Lakini waliorudi nyuma walilikataa hilo, wakachukua udhalili na utwevu kutoka kwa maadui wa dini yao, si kwa lolote ila ni kuwa shetani aliwatisha na ufukara iwapo watahama wakategemea vitisho vyake na wakaathirika kuacha maghu-fira ya Mwenyezi Mungu: "Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili; na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha utokao kwake na fadhila na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mjuzi" (2: 268).

Na mwenye kutoka nyumbani kwake ili kuhamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfikia mauti, basi yamethibiti malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.

Kila mwenye kukusudia kwa kujitahidi na kufanya ikhlasi kwa amali yoyote katika amali za twaa kisha akashindwa, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humwandikia thawabu kamili kwa fadhila na ukarimu kutoka kwake Mwenyezi Mungu. Tumelifafanua hilo katika kufasiri Aya (3: 144) kifungu, "kila mtu ana alilonuia."

Imepokewa kuwa Jundub bin Dhumra, aliposikia Aya ya Hijra aliwaambia wanawe; "Wallahi silali Makka mpaka nitoke, kwa sababu ninahofia kufa Makka;" naye alikuwa mgonjwa sana, wakatoka nae wakimchukua kitandani. Alipofika mahali panapoitwa Tan'im akafariki. Ndipo ikashuka Aya hii.

BAINA YA KUHAMA MTUME KUTOKA MJI MTUKUFU WA MAKKA NA KUHAMA WAPALESTINA KUTOKA ARDHI TAKATIFU.

Katika maajabu ya sadfa ni kuafikiana - bila ya kukusudia - kufikia kwangu kufasiri Qur'an kwenye Aya ya Hijra mwanzo wa mwaka 1388 A.H. na Israel inakalia ardhi yetu takatifu, watu wetu wanahama wakikimbia mateso na mauaji waliyoyafanya waisrael na wanayoendelea kuyafanya.

Sadfa hii imenifanya nilinganishe tukio la uchokozi wa washirikina katika Makka kwa waislamu na kutolewa kwao mijini mwao, na tukio la uchokozi wa waisrael; au kwa usahihi zaidi uchokozi wa kikoloni kwenye ardhi takatifu na kuwatoa wenyeji mijini mwao.

136

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kisha nikatoka kwenye mlinganisho huu kufikia Ib

na jihadi ya Mtume (s.a.w.) na waislamu katika kuhama kwao na kupanga mipango iliyowapeleka waislamu kwenye kilele cha ushindi kwa maadui zao, kuuvunja utaghuti na uchokozi wake na kuwasimamisha mamwinyi wa kiquraish, waliowatoa Makka mbele ya Mtume wakiwa madhalili, wenye kusal-imu amri wakimsikiliiza akiwaambia "Mnadhani nitawafanya nini?"

Baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa lengo la kwanza la Mtume na waislamu ni kuikimbiza tu dini yao kutoka kwa washirikina ambao waliwaingilia kwa kuwaudhi na kuwazuia kutekeleza nembo za dini yao na amali za kidini; sawa na anavyokimbilia Daruweshi msikitini ili aswali vizuri kwa kuepuka fujo na kelele. Hapana! Hijra ya waislamu ilikuwa mbali na kuwa na undani zaidi ya hilo. Dalili ya hilo ni natija na malengo yaliyotekelezwa na Hijra hiyo. Hijra hiyo zaidi ya kuikimbiza dini, ilikuwa na mipango iliyopangwa vizuri ya uandalizi wa vita; sawa na jeshi linapojitenga kutoka uwanja wa vita kwenda mahali pengine ili kujiandaa kwa shambulio kubwa la kummaliza adui.

Mtume (s.a.w.) baada ya kufika Madina aliwafanya ndugu Masahaba na akazichanganya pamoja nyoyo za mahasimu na akayeyusha vinyongo na vidonge walivyokuwa navyo.

Baada ya kukamilisha kazi hiyo aliwahimiza waislamu jihadi na kuwahimiza kulinda heshima yao na itikadi yao, na kumdhaminia pepo atakayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kupata utukufu na cheo duniani na akhera kwa atakayepona kifo.

Baada ya mafunzo haya kuwaingia, Mtume akaanza kuwaunganisha kijeshi na kuwazoesha vita vidogo vidogo akiwapeleka huku na huko; mara nyingi akiv-iongoza mwenyewe. Waislamu wakawa na amani na raha; na amani ya Maquraish ikaingia kwenye wasiwasi. Hatimaye vita vidogo vikageuka na kuwa vita vikubwa, huku waislamu wakijitolea roho zao na mali zao, mpaka ukaja msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi.

"... Na akalifanya neno la waliokufuru kuwa chini na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu ..." (9: 40). Nadhani ishara hii inatosha kuchukua ibra ambayo ni wajibu kunufaika nayo katika balaa letu na israel na wanaoisaidia .

Mtume (s.a.w.) alihama kutoka Makka kwa sababu ya uchokozi wa washirikina waliokuwa wakimfanyia yeye na masahaba wake. Na wapalestina nao wal-ihama kutoka ardhi takatifu kwa uchokozi wa kizayuni na kutaka kuwatawala

137

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

wao wanawake wao na watoto wao. Hijra ya waislamu wakati huo ilikuwa ni kujiepusha na maangamizo na kujitenga kutoka uwanja wa vita ili kukusanya nguvu na kujiandaa kwa shambulio la kummaliza adui.

Kwa hiyo basi ni wajibu kuwa kutoka kwa wapalestina mijini kwao kuwe ni kwa makusudio haya na kwa lengo hili; sio kwa kuwaachia wanyang'anyi Baitul-Maqdis waichezee.

Mtume alianza Hijra yake kwa kufanya udugu baina ya masahaba zake. Kwa hiyo ni juu ya viongozi wa kiarabu na waislamu, kuanza kufanyiana udugu na kusafiana nyoyo; wawe wamoja ili waweze kumkabili adui; sawa na alivy-ofanya Mtume kabla ya kukabiliana na washirikina. Mwenye kuepuka njia hii basi amekutana na waisrael na ametekeleza malengo yao, atake asitake.

Mtume alituma vikosi vidogo kubabaisha washirikina, alivipa vikosi hivyo mahi-taji yao. Ni wajibu kwa waarabu na waislamu kuwashujaisha wanaojitolea mhanga na wengineo na kusaidiana nao hadi mwisho, ili kuwatia wasiwasi waisrael.

Mtume aliwaandaa waislamu wote kwa vita vikubwa na kuung'oa ushirikina na mizizi yake baada ya kuota mizizi, karibu karne nzima, katika kila sehemu ya ardhi ya Bara Arabu. Na hivyo ndivyo inavyopasa kwa kila kiongozi wa waarabu na waislam.

Ikiwa hatutalizingatia somo hili kutokana na turathi zetu na Historia yetu na kuwa sote ni askari katika askari wa Mwenyezi Mungu na wa nchi, basi hatu-tastahiki jina la uarabu na warabu, wala la uislamu na waislam; hata kwa jina za binadamu na ubinadamu; baada ya kuwa hizi ni zama za kujitolea na kutekeleza; na kujikomboa na kila aina ya dhulma na unyonyaji.

Tumalizie kwa kuwapa salaam watoto wetu wapiganaji waliojitolea mhanga ambao wameonyesha mfano mzuri wa kishujaa katika nchi yetu iliyovamiwa, wakauthibitishia ulimwengu wote kwamba sisi tuko katika zama za kujitolea na kupigania uhuru na heshima.

138

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

101.Na mnaposafiri katika ardhi, si vibaya kwenu kama mki-fupisha Swala, ikiwa mnao-gopa kuwa wale waliokufuru watawaletea balaa. Hakika makafiri ni maadui wenu walio wazi.

102.Na utakapokuwa kati yao, ukawasimamishia Swala, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na washike silaha zao. Watakaposujudu na wawe nyuma yenu; Na lije kundi jingine ambalo halijaswali, waswali pamoja na wewe na washike hadhari yao na silaha zao. Wanataka wale waliokufuru lau kama nyinyi mwasa-hau silaha zenu na vifaa vyenu ili wawavamie mvamio wa ghafla. Wala hapana vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkiwa wagonjwa kuweka silaha zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ame-waandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.

Kaashif5-96.jpgKaashif5-97.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-98.jpg

103.Mtakapomaliza Swala, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kusimama na kwa kukaa na kwa          (kulala)           ubavu.

Mtakapopata amani, basi simamisheni Swala. Hakika Swala kwa waumin ni faradhi iliyoekewa wakati maalum.

SWALA YA HOFU Aya 101- 103: MAANA

Swala haiachwi kwa hali yoyote; hata kwa maradhi, vita, au safarini. Anaitekeleza kila mwenye kukalifiwa na sharia kiasi cha uwezo wake; iwe ni kusimama au kukaa; akishindwa ataitekeleza hali ya kulala ubavu. Hata bubu pia ni wajibu kwake kutingisha ulimi wake na kuishiria kwa mkono wake badala ya kutamka. Ufafanuzi uko katika vitabu vya Fiqh.

Na mnaposafiri katika ardhi, si vibaya kwenu kama mkifupisha swala ikiwa mnaogopa kuwa wale waliokufuru watawaletea balaa.

Aya hii imeshuka katika hukumu ya jihadi na hofu; sawa na Aya zilizotangulia, kwani mfumo wa zote ni mmoja. Uwazi zaidi wa kuwa mfumo mmoja ni kauli yake Mwenyezi Mungu: Ikiwa mtaogopa kuwa wale waliokufuru watawaletea balaa.

Kwa sababu makusudio ya balaa hapa ni kuua. Ama safari imekuja mahali pa aghalabu, sio kuwa ni sharti.

Ama kauli yake 'si vibaya kwenu' makusudio yake ni wajibu na lazima sio ruhusa na kuhalalisha. Kwa sababu Hadith zimefasiri ulazima; kama vile Aya ya Tawaf: "... Basi anayehiji katika nyumba hiyo, au kufanya umra, si vibaya kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili." (2:158) Kwa kuwa Aya imekuja katika Swala ya hofu si Swala ya kupunguza ya msafiri, basi makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu kufupisha Swala ni kupunguza idadi ya rakaa na

140 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'küğeüzâ üıfıbö la Swala, külihğariâ riâ dhârürâ iliyöpö....

Swala ya hofu ina sharti. Sharti lake muhimu ni kuwa upande wa maadui kuna nguvu zinazowawezesha kuhujumu na kuvamia. Ama aina yake, Shahid wa pili amesema katika Lum'a: ni nyingi zinazofikia kumi ... inasihi kwa jamaa na kwa mmoja mmoja.

Ifuatayo ni namna ya Swala ya hofu kwa mtu pekee aliyoielezea mwenye Kitab Ash-sharai: "Ama Swala ya hofu ni mfano wa hali ya kufikia kuuana. Ataswali kiasi atakachoweza, iwe ni kwa kusimama, kwenda au kupanda. Ataelekea Qibla kwa Takbira ya kuhirimia; kisha ataendelea ikiwezekana kuendelea, vinginevyo, ataelekea Qibla kwa itakavyowezekana kwake, na ataswali kwa udhuru wa kuelekea popote patakapomwezekania. Ikiwa hakuweza kushuka, ataswali akiwa amepanda na atasujudu juu ya kiti cha saruji yake; kama hakuweza basi ataashiria, kama atakuwa (anazidi) kuhofia basi ataswali kwa tasbih, bila ya kurukuu na kusujudu. Atasema badala ya kila rakaa "Subhanullah Wal-hamdulillaah wa Lailaha ilia Hah Wallahu Akbar."

Sura hii inatosha kuwa ni dalili kwamba Swala ni laizma, hasamehewi hata katikati ya mapigano na wala wakati wa kukata roho. Na kwamba mtu ataitekeleza kwa namna na hali yoyote atakavyoweza.

Na utakapokuwa kati yao, ukawasimamishia Swala, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na washike silaha zao.

Huu ni ubainifu wa Swala ya hofu ya jamaa. Maana yake, ukitaka Ewe Muhammad kuswali jamaa na wapiganaji, basi gawa makundi mawili: Moja liswali na wewe wakiwa na silaha zao; na la pili lisimame kulinda; kama ambavyo inaswihi jamaa pamoja na Mtume (s.a.w.); vile vile inaswihi pamoja na mtu mwingine.

Watakaposujudu na wawe nyuma yenu.

Yaani watakaposujudu wale wanaoswali na Mtume (s.a.w.), lisimame kundi linalolinda nyuma ya wenye kuswali.

Na lije kundi jingine ambalo halijaswali, waswali pamoja na wewe na washike hadhari yao na silaha zao.

Yaani baada ya kumaliza kundi la kwanza kuswali, kundi la pili lichukue mahali pa kundi la kwanza katika Swala na kundi la kwanza lichukue mahali pa ulinzi.

141

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Wanataka wale"vvâiîöküfürü"l¥ü"k¥m¥"hylnyİ"mwasahâü"sMaKa"zenü""nâ' vifaa vyenu ili wawavamie mvamio wa ghafla.

Huu ni ubainifu wa hekima iliyofanya kuwekwa Swala ya aina hii. Hekima yenyewe ni kutopata fursa adui ya kuwavamia wakati wanaswali.

Wala hapana vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkiwa wagonjwa kuweka silaha zenu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaamrisha walioswali kuchukua silaha, akawapa ruhusa ya kuziacha ikiwa wanaona uzito wa kuzichukua kwa sababu ya mvua au ugonjwa, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amewalazimisha wajilinde na wawe macho na adui asijewaingilia ghafla. Mtakapomaliza Swala, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kusimama na kwa kukaa na kwa (kulala) ubavu.

Makusudio ya Swala hapa ni Swala ya hofu. Maana ni kuwa kumtaja Mwenyezi Mungu ni vizuri katika hali yoyote si katika Swala tu. Imam Ali (a.s.) amesema: "Amefaradhisha Mwenyezi Mungu katika ndimi zenu dhikri na akawausia takwa na akaijaalia ndio mwishilio wa haja yake kwa viumbe vyake."

Anasema Ibn Al-arabi katika Futuhatil-Makkiyya J.5: "Mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu katika kisimamo chake kukaa kwake na kulala kwake, basi amekusanya yote."

Mtakapopata amani, basi simamisheni Swala; Hakika Swala kwa Waislamu ni faradhi iliyowekewa wakati maalum.

Yaani wakati wowote vita itakapotulia na hofu ikiwaondokea basi ni juu yenu kutekeleza Swala kwa wakati wake wala msipuuze.

Tumezungumzia kuhusu Swala na jinsi uislamu ulivyoipa kipaumbele, katika Aya zilizotangulia; kama vile (2: 238- 239).

Unaweza kuuliza: Aya imewajibisha Swala ya hofu, ambapo vita vilikuwa vya panga na mikuki. Lakini hivi sasa kuna maendeleo ya silaha za vita kiasi ambacho hatufahamu katika silaha za kuangamiza. Kwa hiyo si inapasa Swala ya hofu iondolewe kwa vile maudhui yake hayapo?

Jibu: Lililosababisha Swala hii ni hofu, bila ya kuangalia vita na ala zake, ziwe za zamani au za kisasa. Kwa hiyo ikipatikana kwa sababu zisizokuwa za vita, basi imejuzu kuifupiliza Swala kwa idadi ya rakaa na kwa aina.

Kaashif5-99.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

MwenyeAl-jawahirianasema: "Kukiwanahofu ya

moto au mengineyo, basi inajuzu kuswali Swala ya shida ya hofu. Kwa hiyo atapunguza idadi na namna. Kwa kukosekana tofauti katika sababu ya hofu iliyoruhusiwa. Kwani aliulizwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) kuhusu anayehofia wanyama au wezi ataswali vipi? Akasema: "Atapiga Takbira na kuashiria."

Tunasisitiza tena kuwa Swala haiwezi kumwondokea mtu kwa hali yoyote. Na kwamba kila mtu anaitekeleza kwa namna anavyoweza katika maneno na vitendo. Akishindwa ataashiria, akishindwa kuashiria ataleta picha ya Swala moyoni mwake.

104.Wala msilegee katika kuwafua-tia hao watu. Ikiwa mnaumia basi na wao wanaumia kama mnavyoumia nyinyi. Na nyinyi mwataraji kwa Mwenyezi Mungu ambayo wao haway-ataraji. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mwenye hekima.

 

Aya 104 MSILEGEE KATIKA KUWAFUATA

MAANA

Wala msilegee katika kuwafuatia hao watu. Ikiwa mnaumia basi na wao wanaumia kama mnavyoumia nyinyi. Na nyinyi mwataraji kwa Mwenyezi Mungu ambayo wao hawayataraji.

Lau kama Wahyi ungelishuka hivi sasa katika hali yetu na waisrael, basi usingezidi hata herufi moja ya Aya hii. Haja kubwa iliyopo sasa ya kupambana na adui huyu mwovu na fedhuli na kukomesha dhulma yake, ni kujifunga kib-

Kaashif5-100.jpg

143

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

webwe na kumtegemea Mwenyezi Mungu na sisi wenyewe na kutowasikiliza wakoloni wanaotaka kutunyonya; wanaofanya propaganda ili watudanganye tuache nguvu zetu.

Kumtetemekea adui tu kunampa faida na kunamsaidia, sikwambii kum-wogopa. Kwa ajili hii ndipo Mwenyezi Mungu akatukataza kumwogopa adui wa Mwenyezi Mungu na wa ubinadamu kwa hali yoyote ilivyo na itakavyokuwa; na kutuamrisha udhabiti katika kupambana naye. Vilevile ame-tuzindua kuwa tunamwumiza adui, kama anavyotuumiza, lakini sisi tuko zaidi kuliko yeye, kwa sababu sisi twamwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Ama Israel inawategemea wakoloni na ndugu zao mashetani walioitengeneza; wakawasheheni silaha na mali, wakawahimiza kufanya uchokozi na kuwa-saidia katika Umoja wa mataifa na katika Baraza la usalama.

Hapana shaka yoyote kuwa kama tukijitegemea na kuwa na msimamo imara wa ikhlasi na tukafanya juhudi zetu zote, kama alivyotuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ushindi utakuwa wetu tu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika Aya nyingine anasema: Wala msilegee na kutaka suluhu na nyinyi ndio mko juu na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi. (47:35)

Waislamu wako juu kwa itikadi yao historia yao na uwezo wao. Nguvu hizo haziendi wala hazitakwenda bure. Kwa hiyo hapana budi kuwa athari zake zitadhihiri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, iwe sasa au baadaye.

105.Hakika tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu; wala usiwe mtetezi wa wenye kufanya hiyana.

106.Na muombe maghufira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

Kaashif5-101.jpgKaashif5-102.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

107.Wala usiwatetee wale ambao wamezihini nafsi zao. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi aliye haini mwenye dhambi.

108.Wanajificha kwa watu wala hawajifichi kwa Mwenyezi Mungu, na yeye yu pamoja nao walipokula njama usiku kwa maneno asiyoyapenda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vyema muyatendayo.

109. Nyinyi ndio ambao mnawa-tetea katika maisha ya duniani, basi ni nani atakayewatetea kwa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama au ni nani watakayemtegemea?

110.Na mwenye kutenda uovu au akadhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-103.jpg

145

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

111.Na mwenye kuchuma dhambi, basi anajichumia mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi mwenye hekima.

112.Na mwenye kuchuma kosa au dhambi, kisha akamisingizia asiye na kosa, basi hakika amejitwika dhuluma na dhambi iliyo wazi.

113.Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, lingedhamiria kundi kati-ka wao kukupoteza; wala hawazipotezi ila nafsi zao; wala hawatakudhuru na lolote. Na amekuteremshia Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na amekufunza uliyokuwa huya-jui. Na fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako ni kubwa.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-104.jpg

146 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ...

Aya 105 - 113: KUWATETEA WAHAiNi

MAANA

Mwenye kufuatilia tafsir, akachunguza Aya hizi na kufikiri vizuri maana yake atakubali kuwa zilishuka kuhusiana na mwislamu mmoja aliyeiba bidhaa, akamsingizia mtu asiyekuwa na hatia; na kwamba jamaa wa mwizi walimwen-dea Mtume (s.a.w.) na kujaribu kumkinaisha kwa mbinu mbalimbali wamkinge mtu wao kumwepushia janga la wizi; na kama hakufanya hivyo, basi mtu wao ataangamia.

Karibu Mtume aitikie maombi ya wapotevu hao lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimlinda mchukuzi mwaminifu wa wahyi wake na mfikishaji wa sharia yake. Akamhifadhi na njama zao na kumfichulia uhakika. Akafichuka mwizi na kusal-imika yule aliyesingiziwa.

Inasemekana pia kuwa aliyesingiziwa alikuwa ni myahudi na mwizi ni ansari; na kwamba yeye baada ya kufichuka alikimbia na kujiunga na washirikina.

Dhahiri ya Aya inafungamana kabisa na tukio hili. Ufuatao ndio ubainifu wake:

Hakika tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu.

Tunasema - Tukimwomba msamaha Mwenyezi Mungu - kwamba msemo huu unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa Mtume wake mtukufu ukiashiria aina ya lawama. Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia: Nimekuchagua mimi mwenyewe, nikakuteremshia Qur'an ili uhukumu baina ya watu kwa lile unalojua kwa yakini kuwa ni hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Sasa wadanganyifu wamekurubia kukuhadaa, lakini Mwenyezi Mungu amekulinda na walivyokupangia - kumtia hatiani asiye na makosa - kwa kuku-fichulia uhakika na njama zao.

Hakuna linalofahamishwa na hali hii zaidi ya kuwa kuhifadhiwa na dhambi (Isma) si jambo la kulazimishwa; kama urefu na ufupi; isipokuwa ni wasifu unaomwepusha huyo maasum kufanya haramu, ingawaje anaweza kufanya, na kumpa msukumo wa kufanya wajibu, ingawaje anaweza kuuacha.

Aya hii ni jibu na kubatilisha kauli ya wasemao kuwa Mtume ana hukumu kati-ka baadhi ya masuala kwa ijtihadi yake. Aya inaonyesha wazi kuwa yeye

Kaashif5-105.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

hahukumu ila kwa wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hayo ni kwamba mwenye kujitahidi anapata na kukosa, na Mtume ni mwamuzi wa tofauti za wenye kujitahidi na kubainisha kosa la mwenye kukosea na usawa wa mwenye kupatia.

Wala usiwe ni mtetezi wa wenye kufanya hiyana.

Mtume hakuwatetea, na ni muhali kwa Mtume kuwatetea wanaofanya hiyana. Na kukatazwa kwake kutetea hakulazimishi kutokea hilo kwake, bali ni kwamba kukatazwa haramu kunatokea kabla ya kuifanya. Lau kungekuwa kunaku-ja baada ya kutokea lengo la kukatazwa basi litabatilika.

Unaweza kuuliza: Ikiwa kufanya haramu ni muhali kwa Mtume kutokana na kuhifadhiwa kwake na dhambi, kwa nini akakatazwa?

Jibu: Mwenyezi Mungu anaweza kuielekeza amri yake kwa Mtume wake kati-ka hali zote. Kwa sababu ni amri kutoka kwa aliye juu kwenda kwa aliye chini yake. Zaidi ya hayo, ni kwamba amri ya wajibu na katazo la haramu mara nyingi huelekea kwa Mitume kwa kuelewesha hukumu tu.

Na muombe maghufira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

Anasema Tabari katika Tafsir yake kuwa Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake kuomba maghufira ya kusamehewa dhambi za kumtetea mhaini. Na sisi tunaomba maghufira kutokana na tafsir hii. Kwani Mtume (s.a.w.) -kama tulivyotangulia kueleza - hakumtetea mhaini. Kwa dalili ya Aya itakay-ofuatia (113):

Ama amri ya kutaka maghufira ya dhambi hailazimishi kupatikana dhambi, Tafsiri ya Aya tunavyoiona ni kuwa Mtume (s.a.w.) kwa kuwa ni mtu, anaweza akadhania vizuri jambo lisilostahiki; ikamdhihirikia hakika kwa njia ya wahyi au nyingine kabla ya kuchukua uamuzi wowote wa dhana yake nzuri. Ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha kuomba maghufira kutokana na ile dhana nzuri iliyomtokea ambayo haikuwa mahali pake. Makusudio ni kujichunga na kujitoa shakani na kutotegemea lolote ila baada ya yakini.

Wala usiwatetee wale ambao wamezihini nafsi zao. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi aliye haini, mwenye dhambi.

Kwa dhahiri msemo unaelekezwa kwa Mtume (s.a.w.), lakini ulazima wake unamhusu kila aliye baleghe mwenye akili, hasa makadhi na mahakimu.

148 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Ama waliozihini nafsi zao ni wale waliofanya dham wengine wasio na hatia; na mwenye kuwatetea basi yeye ni kama wao. Maana ya mtu kujihini yeye mwenyewe ni kujibebesha mzigo wa adhabu kwa kuharibu mambo ya wajibu na kufanya haramu.

Tumetangulia kueleza kuwa Mtume (s.a.w.) hakutetea wala hatawatetea wahaini, na Aya hii inatilia mkazo kauli yake: Wala usiwe ni mtetezi wa wenye kufanya hiyana; Vilevile inabainisha kuwa mwenye kumdhulumu mwingine amejidhulumu yeye mwenyewe na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwadhibu kila haini, mwenye kujidhulumu na anayewadhulumu wengine.

Wanajificha kwa watu wala hawajifichi kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao walipokula njama usiku kwa maneno asiyoyapenda.

Mfanya makosa huficha makosa na kujificha gizani asionekane na watu kwa kutaka sifa au kuogopa shutuma zao. Ambapo ilikuwa afanye kinyume - aji-fiche na Mwenyezi Mungu - kama anaweza, na wala asijishughulishe na watu kabisa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kumiliki mad-hara na manufaa. Asiyekuwa Mwenyezi Mungu hawezi kumtosheleza binadamu na kitu chochote. Sifa za watu na shutuma zao ni maneno yanayok-wenda na upepo. Ikiwa kujificha na Mwenyezi Mungu hakuwezekani, basi kumtii ni lazima, sio pendekezo.

Nyinyi ndio ambao mnawatetea katika maisha ya duniani, basi ni nani atakayewatetea kwa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama au ni nani watakayemtegemeea?

Msemo unaelekezwa kwa watu wa yule mwizi mhaini. Kwa sababu wao peke yao ndio waliomtetea na kumgombea. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu - ambaye limetukuka neno lake - amewafahamisha kuwa kumtetea mhaini hakuwezi kumfaa mhaini siku atakayofichuliwa na Mwenyezi Mungu: "Na jitengeni leo enyi waovu" (36:59)

Na mwenye kutenda uovu au akadhullumu nafsi yake, kisha akaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu atamkuta Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

Huyo ndiye mwenye kutoka katika dhambi mwenye kuikiri na kutubia. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni mkali wa adhabu, basi pia ni mwenye kumghufiria mwenye kutubia, mwenye kumrehemu anayekimbilia kwake.

Kaashif5-106.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Küh'â"hâd'İthi irîâyösemâ: "Hakika'Mwehyezî'Müngu'hâchök]7mpâk¥'mcWökef mkiacha naye huacha."

Yaani mkiacha kutubia dhambi naye huacha kusamehe. Kwa hiyo la sawa kwa wale waliomtetea mwenye hatia, ni kumzindua kutokana na kosa lake na kumpa nasaha ya kutubia, kama wangelikuwa ni wanasihi waumin wa kweli.

Katika Aya hizi nne kuna maneno ambayo hapana budi kuyafafanua ili ieleweke tofauti yake ambayo kwa dhahiri inaonekana kama ni moja tu inayokaririka:

Neno la kwanza ni dhambi, lilioko katika Aya ya 107, 111 na 112. La pili na la tatu ni uovu na kujidhulumu, yaliyo katika 111. La nne ni kosa, lililotajwa katika Aya ya 112.

Maneno yote haya yanakusanya maana moja ambayo ni maasi. Tofauti ni kuwa uovu ni ule unaofanyiwa mtu mwingine, kujidhulumu ni kujiingiza katika madhara kwa kuacha wajibu au kutenda haramu na kosa ni lile linalofanywa bila ya udhuru wowote; kama vile mzembe asiyejua anayekosea kutekeleza wajibu kwa kutojua ingawaje ana uwezo wa kujifundisha. Hukumu yake ni kama hukumu ya mwenye kukusudia makosa. Kwa sababu amepuuza kufanya utafiti na kuuliza.

Na dhambi ni kufanya kosa pamoja na kujua na kung'angania kulifanya. Dhambi ni ujumla inakusanya uovu na kujidhulumu. Kwa hiyo maana yanakuwa: 'Mwenye kutenda uovu au akadhulumu nafsi yake... mpaka mwisho " ni kuwa mwenye kumfanyia uovu mwingine kwa kumtukana au kupi-ga na mengineyo au kuifanyia nafsi yake tu; kama vile yamini ya uongo kisha akatubia, Mwenyezi Mungu humkubalia toba yake; kama vile hakufanya uovu wowote au kudhulumu.

Na maana ya Mwenye kuchuma dhambi, basi anajichumia mwenyewe. Ni

kwamba mwenye kufanya dhambi, basi amejifanyia uovu mwenyewe, ni sawa awe amefanya uzembe kwa uovu huu yeye peke yake au alimfanyia mwingine.

Maana ya Mwenye kuchuma kosa au dhambi, kisha akamsingizia asiye na kosa, basi hakika amejitwika dhuluma na dhambi iliyo wazi, ni kuwa mwenye, kumsingizia mtu mwingine kwa kosa asilokuwa nalo, ataadhibiwa adhabu ya uzushi wa makusudi; ni sawa alifanya kosa hilo akamsingizia mwingine kwa makusudi, (hilo linafahamishwa na neno 'dhambi'), au hakuli-fanya yeye, lakini akamsingizia mwingine kabla ya kuthibitisha, (hilo linafa-

Kaashif5-107.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'hamishwa hâ hehö 'kösâyLehğö

mwingine jambo lolote, mpaka awe na yakini nalo kama jua.

Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, linged-hamiria kundi katika wao kukupoteza; wala hawazipotezi ila nafsi zao; wala hawatakudhuru na lolote.

Makusudio ya kundi ni wale waliomtetea mwizi; na dhamiri ya katika wao inawarudia watu wake na wasaidizi wake. Makusudio ya kukupoteza ni kukuhadaa kwa maneno ya makosa na masilahi. Wala hawazipotezi ila nafsi zao, kwa sababu kujaribu kupoteza kunalazimisha upotevu; na mwenye kupoteza ni mpotevu na ziada.

Maana kwa ujumla ni kuwa kundi katika wasaidizi wa mwizi na jamaa zake, walikula njama ya kukuhadaa na haki na kujaribu uwe upande wao katika kum-wokoa mtu wao nawe ulikaribia kuwakubalia kwa yale mazuri waliyokudhi-hirishia, lakini Mwenyezi Mungu akakuhifadhi nao; akakufichulia njama zao na kurudisha vitimbi vyao kwao.

Aya hii ni jibu la wazi kwa wale wanaodai kwamba Mtume (s.a.w.) aliwatetea wahaini. Kwani kauli yake Mwenyezi Mungu "Na rehema yake" na "Wala hawatokudhuru na chochote," hazikubali taawili yoyote na shaka yeyote kuwa Mtume hakumtetea mwizi na mhaini. Na kwamba aliyefanya haya ni mwingine.

Na amekuteremshia Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na amekufunza uliyokuwa huyajui. Na fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako ni kubwa.

Kitabu ni Qur'an na hekima ni utume. Ikiwa Mwenyezi Mungu amewajibisha Muhammad kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumfanya ni mwisho wa Mitume na bwana wa Mitume wote na kumfundisha asiyoyajua, basi ni wajibu kwa waarabu kumshukuru Muhammad kwa kuwa wamekuwa ni wenye kutaji-ka baada ya ujinga wao wa wajinga. Vilevile wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia mtukufu zaidi wa viumbe kuwa ametokana na wao sio kwa wengine.

151

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano ■|f4;Hâküna"'kherı'"kâtıka""sırİ'"zâö"'

nyingi, ila mwenye kuamrisha sadaka au wema au kusu-luhisha watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-108.jpg

115.Na mwenye kumpinga Mtume baada ya kumdhihirikia yeye uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya wenye kuamini, tutamwelekeza alikoelekea na tumtie katika Jahannam na ndio marejeo maovu.

 

Aya 114 - 115 SIRI YA KHERI NA YA USULUHISHI

MAANA

Hakuna kheri katika siri zao nyingi, ila mwenye kuamrisha sadaka au wema au kusuluhisha watu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja katika Aya zilizotangulia wale wanaokula njama usiku ya kauli asizoziridhia na kuwatetea wahaini, sasa katika Aya hii anasema siri zao nyingi hazina kheri. Kwa hiyo dhamiri ya 'siri' zao' inawaru-dia hao waliotajwa katika Aya zilizotangulia, kwa dalili ya dhahiri ya mfumo, lakini katika maana inaenea kwa watu wote. Kwa vile sababu inayowajibisha ni ya ujumla, haihusiki na watu maalum wala kundi maalum.

152

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Sâdâkâi'n'ikütöâ"rriâİİ kwa"mâs]ki'hl"wâMâjl7'Küw¥sü1'üWfshaWâtu'künâWâökb'â' na taabu nyingi na kuwaondolea matatizo. Na wema ni kila linalokubaliwa na akili na sharia kwa kuliona kuwa ni zuri. Ikiwemo elimu na mambo yote mazuri kama vile sadaka na kuimarisha udugu. Mwenyezi Mungu amehusisha kuy-ataja hayo mawili kwa kufahamisha umuhimu wake.

Arrazi anaema: "Mkusanyiko wa kheri zote umetajwa katika Aya hii." Na mku-sanyiko zaidi umetajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika mwanadamu yumo katika hasara. Ila wale ambao wameamini wakatenda matendo mema, wakausiana haki, wakausiana kusubiri." (103: 2 - 3)

Unaweza kuuliza: Watu huwa wakifanya siri za biashara, kazi, kilimo, na nyinginezo katika mambo ya maisha, sasa je siri hii ni katika mambo yasiyokuwa na kheri?

Jibu: Siri hiyo ni kheri maadam iko katika mipaka ya sharia, na katika yale ambayo ni wajibu kisharia, kikawaida na kiakili. Nayo ni yale ambayo maisha hayatimii bila hayo. Na Aya imeepuka aina hii ya siri na kuingilia wale wanofanya siri na kuwazungumzia watu; kama kawaida ya wasio na haki; hupoteza muda wao kwa porojo na kujishughulisha na yule ni zaidi na yule ni mchache. Tamko la nyingi katika Aya linafahamisha kuwa siri nyingi za watu hazina heri ila kama itawarudia faida na manufaa kwa namna fulani. Ama siri katika mambo ya maisha, Aya haikuelezea kwa uzuri au ubaya.

Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa.

Kuamrisha mema ni vizuri, hilo halina shaka. Lakini mwenye kulifanya kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu sio kwa kuchuma, na kutaka jaha ni bora kuliko ambaye anaamrisha mema na kuyaletea falsafa kubainisha mazuri yake na faida zake, lakini hayafanyi, bali itakuwa ni hoja yenye nguvu na ya fasaha zaidi kwake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika sisi hatupotezi ujira wa anayefanya vitendo vizuri." (18: 30) Wala hakusema mwenye kauli nzuri.

Kuamrisha mema kuyatolea mwito ni nyenzo na kuyafanya ndio lengo. Mwenye kuamrisha na yeye mwenyewe akafanya, atakuwa katika waliom-saidia Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: "Ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko alinganiaye kwa Mwenyezi Mungu na akafanya vitendo vizuri." (41: 33)

153

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Kwa hiyo kau

do. Zaidi ya haya ni kwamba kauli hata kama kwa dhahiri itaambatana na athari za kiislamu; kama vile ndoa na mirathi, haziwezi kufahamisha imani sahihi, ila vitendo vizuri. Amesema Imam Ali Amirulmuminin (a.s.): "Imani inafa-hamisha mambo mema na mambo mema yanafahamishwa na imani."

Na mwenye kumpinga Mtume baada ya kumdhihirikia yeye uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya wenye kuamini, tutamwelekeza alikoelekea na tumtie katika Jahannam na ndio marejeo maovu.

Upinzani ni uadui na kila mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu ni adui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Amirul-muminin (a.s.) anasema: "Hakika mpen-zi wa Muhammad ni mwenye kumtii Mwenyezi Mungu hata akiwa mbali naye (huyo Mtume) kwa nasabu, na hakika adui wa Muhammad ni yule mwenye kumwasi Mola hata kama akiwa karibu naye (mtume) kwa nasabu."

Adui wa Muhammad hapa ni kila ambaye imemdhihirikia haki, akaikana, akasi-mamishiwa hoja za kutosha, lakini pamoja na hayo akakanusha kwa inadi na kung'ang'ania mapenzi ya nafsi yake; kama anayejua kuwa uislamu ni haki au kuwa ni uongofu zaidi kuliko dini ya watu wake, lakini pamoja na hayo akang'a ng'ania dini ya mababu zake kwa kupupia masilahi yake ya kiutu au jaha.

Wafasiri wametaja kuwa Aya hii ilishuka kuhusu Bashir bin Ubairiq ambaye alisilimu kisha akartadi na kuungana na washirikina. Inajulikana kuwa ni des-turi ya wafasiri kujipachikia sababu za kushuka Aya. Wanataja tukio lolote linaloambatana na zama za kushuka Aya ikiwa linanasibiana nayo. Na Aya hii inafungamana na kurtadi kwa Bashir na kila mwenye kupinga baada ya kum-bainikia uongofu.

Maana ya Tutamwelekeza alikoelekea ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humtegemezea kila mtu kwenye lile alilolitegemea. Mwenye kujitukuza kwa mali, cheo, siha au ukoo, basi Mwenyezi Mungu huachana naye na kumwachia lile alilojitukuzia. Katika Hadiith Qudsi Mwenyezi Mungu anasema: "Naapa kwa utukufu wangu na enzi nitakatilia mbali matumaini ya kila anayem-tumainia mtu."

Aya hii inatujulisha yafuatayo:

i). Kauli yake Mwenyezi Mungu Tutamwelekeza alikoelekea ni wazi kuwa binadamu ana hiyari, si mwenye kuendeshwa.

154 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Ti).Kaüİı yakeMwehyezi Mühğü'Bâada'yâ'kümbâWkİâ"übhgofu'hidall'kwam-" ba mwenye kufanya utafiti wa ndani na usimbainikie uongofu basi huyo anasameheka; sawa na ambaye hakufikiliwa na mwito wowote, lakini kwa sharti ya kuwa awe ni mwenye kuelekea kuitafuta haki na kuitumia pale itakapomdhihirikia.

iii). Mtu ni mwenye kukalifiwa na yale anayoyafahamu kutokana na dalili, na wala hana jukumu la hali halisi ilivyo. Kinachotakiwa kwake ni kufanya utafiti tu, mpaka akate tamaa ya kupata dalili. Akipatia hali halisi baada ya utafiti huu, basi atakuwa na malipo mara mbili, na akikosea atakuwa na malipo mara moja; kama ilivyoelezwa katika Hadith.

iv).Yaliyoelezwa katika Tafsiri Razi kwamba Shafii aliulizwa kuhusu Aya ya Qur'an inayofahamisha kuwa Ijmai ni hoja? Akasoma Qur'an mara mia tatu mpaka akapata Aya isemayo: "Na akafuata njia isiyokuwa ya waumini."

Ambapo imefahamisha kuwa kufuata njia isiyokuwa ya waumini ni haramu, kwa hiyo basi kufuata njia ya waumini ni wajibu; na njia yao ni Ijmai yao juu ya jambo.

Hakuna linalofahamishwa na maelezo haya zaidi ya kuwa hakuna chimbuko la Ijmai katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa vile makusudio ya njia isiyokuwa ya waumini ni njia ya washirikina na wanafiki ambao wanampinga Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kuwabainikia wao uongofu. Kuongezea aliyoyasema Sheikh Muhammad Abduh: "Ijma wanayokusudia ni kuafikiana mujtahiid wa umma huu baada ya kufa Mtume wake na Aya imeshuka zama za Mtume sio baada ya zama zake."

NZI KUFIA KIDONDANI

Ametaja mwenye Tafsir Al-manar kisa cha anyeathiriwa na hawaa ya nafsi kuliko uongofu. Tutakinukuu kwa faida ya msomaji, anasema: "Mtu mwenye hawa ya nafsi anashawishika na manufaa ya kidunia kwa udhaifu wa nafsi yake. Kuna kisa kuwa Hajjaj aliandaa karamu ile ya 'nyote mwaalikwa'. Wakawa wanakula huku akiwaangalia, akamwona bedui mmoja anakula kwa umero sana. Lakini mara ilipokuja haluwa aliacha chakula na akairukia. Hajjaj akaamrisha muuaji wake atangaze kuwa atakayekula haluwa atakatwa shingo yake.

Ikawa bedui mara anamwangalia muuaji akipima uchungu wa mauti na ladha ya haluwa. Mara akamwelekea Hajjaj na kumwambia: "Nakuusia uwafanyie

Kaashif5-109.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

vizuri watoto wangu." (akiwa na maana kuwa atauliwa kwa kula haluwa) Akaishambulia haluwa kwa pupa sana kama mtu anayekula mlo wa mwisho maishani! Hajjaj akamwachilia mbali."

116.Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kufanyiwa mshirika, lakini humsamehi yasiyokuwa hayo kwa amtakaye.Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika amepotea upotofu ulio mbali.

117. Hamwabudu asiyekuwa yeye ila (Masanamu) ya kike na hawamwabudu ila Shetani Muasi.

118.Mwenyezi Mungu amlaani shetani. Naye alisema kwa hakika nitajifanyia katika waja wako fungu maalum.

119.Kwa hakita nitawapoteza na nitawatia tamaa. Na nitawaam-risha, watayakata masikio ya wanyama na nitawaamrisha wabadili umbile la Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya shetani kuwa mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu basi ame-hasirika hasara ya waziwazi.

120.Anawaahidi na kuwatia tamaa;

Kaashif5-110.jpgKaashif5-111.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

.na shetani hawaahidi ila udan-

ganyifu.

4. Sura An-Nisaa

121.Hao makazi yao ni moto wa Jahannam wala hawatapata pa kuukimbia.

122. Na wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, tutawatia katika pepo zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu, na ni nani msema kweli zaidi ya Mwenyezi Mungu?

Kaashif5-112.jpg

Aya 116 - 122TİENÂ KÜKÂRİRİKÂ KÂTİKÂ QUR'AN.

 MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kufanyiwa mshirika, lakini hum-samehe yasiyokuwa hayo amtakaye.

Imetangulia Aya hii na maelezo yake katika kufasiri Aya 48 katika Sura hii. Hakuna tofauti yoyote kati ya nukuu mbili ila katika kumalizia ambapo huko imesemwa: "Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amezusha dhambi kubwa," na hapa ikasemwa: "Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amepotea upotevu wa mbali," maana ni moja tu.

157 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ...

Tumezungumzia kukaririka Qur'an katika kufasiri Aya 2; 48; sasa tunaungan-isha na aliyoyasema mwenye Tafsiri Al-manar katika kufasiri Aya hii; "Qur'an sio kanuni wala si kitabu cha fani kinachotaja suala mara moja, bali ni Kitabu cha mwongozo. Inakusudiwa uongozi kwa kuyaleta maana yanayotakiwa katika nafsi katika kila mfumo wa maneno unaoukubali maana ya makusudio. Na hilo litatimia kwa kukaririka makusudio ya kimsingi; wala mwito wa kiujumla hauwi ila kwa kukaririka. Kwa hiyo ndio tunaona watu wa madhehebu za dini na wa siasa ambao wanajua desturi ya kijamii, tabia za watu na hulka zao, wanarudia khutba zao, malengo yao na makala zao wanazozisambaza katika magazeti yao na vitabu vyao."

Hawamwabudu asiyekuwa yeye ila( masanamu ) ya kike.

Waarabu kabla ya Muhammad (s.a.w.) walikuwa wakidai kwamba Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:

Je, Mola wenu amewachagulia watoto wa kiume, na mwenyewe akajifanyia watoto wa kike katika Malaika?" (17:40)

Itikadi yao hii iliwapelekea kufanya masanamu waliyowapa majina ya wanawake; kama vile Lata, Uzza na Manata. Wakiwatia alama za Malaika waliodai kuwa ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Mwanzo walikuwa wakijikuru-bisha kwa Mwenyezi Mungu kwa hayo masanamu. Baada ya kupita vizazi masanamu hayo yakageuka kuwa Mungu anayeumba na kuruzuku. Na hivi ndivyo kulivyogeuka kuzuru makaburu - kwa waarabu na watu wote - kutoka kuwa ni kutukuza alama za Mwenyezi Mungu na kutukuza misingi ambayo amekufia aliyemo kaburuni, na kuwa ni itikadi ya kuwa ni nguvu ya juu inay-oleta manufaa na kukinga madhara.

Na hawamwabudu ila muasi.

Yaani ibada ya washirikina kwa masanamu ilivyo hasa ni ibada ya shetani, kwa sababu yeye ndiye aliyewaamrisha hivyo, wakamtii. Yeyote mwenye kumtii mwingine na kufuata njia yake basi yeye ni mtumwa wake mwenye kuamrish-wa naye.

Mwenyezi Mungu amlaani. Naye alisema kwa hakika nitajifanyia katika waja wako fungu maalum.

Maana ni kuwa shetani alimwambia Mwenyezi Mungu Mtukufu; Mimi nina

Kaashif5-113.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

fungu katika waja wako u

"Na sikuumba majini na watu ila waniabudu." (51: 56). Na kwamba fungu hili

ni faradhi ya wajibu kwangu wanitii na kukuasi

Unaweza kuuliza: Dhahiri ya Aya yaonyesha kwamba shetani ni kiumbe hasa na kwamba yeye anamwambia Mwenyezi Mungu kwa nguvu na kujiamini. Je maneno yako kwenye dhahiri yake au kuna taawili?

Jibu: Mwenye tafsir Al-manar kutokana na ustadh wake Sheikh Muhammad Abduh anasema kwamba kila mtu ana maandalizi ya kufanya kheri na shari na kufuata haki na batili. Maandalizi hayo Mwenyezi Mungu ameyaashiria katika kauli yake: "Na tukamwongoza njia mbili." (90:10)

Na kwamba fungu la wajibu la shetani kutoka kwa bindamu ni kujiandaa kwake na shari ambayo ni moja ya njia mbili. Kwa hiyo tamko la shetani ni fumbo la uandalizi huu.

Tumezungumza kuhusu makusudio ya neno shetani katika juzuu ya kwanza maelezo ya Audhubillahi ... sio mbali kuwa kauli hii iliyokuja kwa lugha ya shetani, 'Nitashika fungu la lazima,' kuwa ni picha ya matukio ya waasi ambao maandalizi ya shari kwao yameshinda ya heri, na wala sio mazungumzo ya uhakika pamoja na Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

SIASA YA SHETANI NA SAYANSI

Mmoja aliwahi kusema kuwa fikra ya shetani ilitawala akili za watu pale elimu ilipokuwa ni mazungumzo tu yanayozungumzwa kwenye vikao vya kufundis-hana na misitari tu inayojaza kurasa za vitabu; wala haifikilii kwenye vitendo.

Ama leo fikra ya shetani imekuwa ni uzushi na ngano kwa tafsiri zake zote, baada ya kuwa elimu ni kipimo cha kila hakika, msingi wa kila hatua anayopi-ga binadamu, nguvu katika nyanja zote na uwezo unaokifanya chuma kipige marefu ya masafa ya mita katika ardhi, kuchimbua miamba ya dhahabu na kuruka angani mpaka mwezini na kwenye Merikh(mars) huku kikizungumza na watu wa ardhini wanoshuhudia safari yake.

Jibu: Hatudhani kuwa kuna yeyote anayeipuza elimu na faida zake na kwamba hiyo ni nguvu na ni utajiri vilevile na kuwa jinsi watu wanavyoihitajia ni sawa na vile mtu anavyohitajia maji na chakula. Lakini hakuna yeyote asiyejua kwamba elimu ni sawa na binadamu; ina maandalizi ya heri na shari na mara nyingine inaelekeza kwenye heri, ikazalisha chakula kwa walio na njaa, kuwavisha walio uchi na kuwatibu walio wagonjwa. Na mara nyingine

Kaashif5-114.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

inaelekeza kwenye shari; ikaua na kuvunja.

Shari ndiyo nguzo ya kwanza ya siasa ya shetani tunayemkusudia na leo elimu katika siasa, imekuwa inaelekeza kubomoa na kutawala na kunyonya. Fungu la shari au shetani - vyovyote utakavyoita - limezidi kwa maendeleo ya elimu (Sayansi). Zamani wasaidizi wa shari walikuwa na silaha ya nguvu na viungo, ama hivi leo baada ya elimu kuwafikia wakorofi, basi wanachama wa shetani wanatumia silaha za tonoradi, na mabomu na mengineyo yanayotetemesha ardhi kutokea chini.

Kuna mahali nimesoma kwamba Amerika imeweka mpango wa kuwanunua machipukizi wa elimu popote ulimwenguni na kwamba dalali wake anayetem-bea aliwahi kufika Uingereza katika baadhi ya ziara zake na kukubaliana na wataalamu mia saba wahamie Amerika. Mbinu hizi wanazitumia wanasiasa wa Amerika kutengeneza vifaa vya kupiga ulimwengu wote na kutawala nguvu zake. Hawa ndio shetani adui wa Mwenyezi Mungu na wa binadamu.

Ama mashule ya kisasa yaliyoenea kila mahali, mengi ni katika fungu la shetani hamna chochote chenye mwelekeo wa dini na maadili mema. Hivi ndi-vyo zilivyoitikia akili kubwa na ndogo mwito wa shetani alioutangaza kwa kuse-ma: Kwa hakika nitashika fungu la lazima katika waja waiko.

Kwa hakika nitawapoteza na nitawatia tamaa.

Shetani kumpoteza mtu ni kumpambia haki aione batili na kheri aione shari, au ampe dhana za kuwa hakuna haki wala heri katika kuwapo kwake wala haku-na pepo na moto na kwamba dunia ni ya mwenye kuimiliki, kama alivyosema Nietezshe*14. Kuna hadith isemayo: Ibilis ameumbwa na umbo la kupendeza.

Ama kutia tamaa kwa shetani ni kumpa mawazo ya kupata anayoyatamani kutokana na muda mrefu na kuokoka siku ya hisabu na malipo na mengineyo katika matamanio ya uongo na ndoto za uokofu.

Na nitawaamrisha, watayakata masikio ya wanyama na nitawaamrisha wabadili umbile la Mwenyezi Mungu.

*14Mwanafilosofia w Kijerumani (1844 - 1900)

Kaashif5-115.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Mâküsüdiö ya wariyama hi riğ^

Ujahiliya walikuwa wakiyakata masikio ya baadhi ya wanyama wao na kuyasi-mamisha kwenye masanamu halafu wanajiharamisha nao. Utakuja ufafanuzi wakati wa kufasiri (5: 103) Inshallah.

Baada ya kuwa shari au shetani akiwaamrisha wanachama wake wakati wa ujahiliya kukata masikio ya wanyama na kubadilisha umbile la Mwenyezi Mungu, hivi sasa amekuwa akiwaamrisha kutupa mabomu ya sumu (Napalm) kwa wanawake na watoto na kutupa mabomu ya Atomic huko Hiroshima na Nagasaki kwa ajili ya kumaliza viumbe vya Mwenyezi Mungu. Haya ni matokeo ya wanasiasa kutawala akili na elimu.

Na mwenye kumfanya shetani kuwa mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu yaani akimtii - basi amehasirika hasara ya waziwazi. Ambapo anakuwa ni mateka wa matamanio na hawaa za nafsi na vilevile mateka wa njozi na uzushi.

Anawaahidi na kuwatia tamaa; na shetani hawaahidi ila udanganyifu.

Ambapo amewawekea kwenye njia ya maangamivu baada ya kuwadanganya kuwa ni uokofu. Kwa mfano, mzinifu au mnywaji pombe anaweza kuwa yeye anastarehe kwa ladha na kumbe ilivyo hasa anajitwisha madhara makubwa ya kidunia na akhera.

Hao makazi yao ni moto wa Jahannam wala hawatapata pa kuukimbia.

Yaani wanachama wa shetani katika washirikina na wafisadi hawataokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja kiaga kikali, alifuatisha na ahadi kama ilivyo desturi yake ilivyozoelekea - kukutanisha himizo na kitisho. Anasema Mwenyezi Mungu:

Na wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, tutawatia katika pepo zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu; na ni nani msema kweli zaidi ya Mwenyezi Mungu?

Katika Aya hii kuna masisitizo matatu: Umiliki, ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli na ni nani mkweli zaidi. Lengo la kukaririka huku ni kufahamisha kuwa ahadi ya shetani ni ya uongo, tamaa inayokwisha na amri zake ni batili; na kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu ndiyo ya haki na ukweli na twaa yake ni heri na wema.

161

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                   4. Sura An-Nisaa

Unaweza kuuliza kuwa ahadi ya pepo mara nyingi katika Aya hukutani

kudumu milele (Abadan) ambapo Aya nyingi za kiaga cha moto hukutanishwa

na kudumu tu, je, kuna siri gani?

Jibu: Kudumu ni kukaa muda mrefu, inawezekana kuwa milele na inawezekana isiwe, mwenye kuingia peponi hatoki kwa hiyo inanasibu kusema milele. Ama mwenye kuingia motoni anaweza kukatikiwa na adhabu na kuto-ka humo kwa hiyo ndio haikukutanishwa adhabu na umilele ila katika hali maalum; kama vile ushirikina na kuua makusudi.

123.Si matamanio yenu wala mata-manio ya watu wa Kitabu. Mwenye kutenda uovu atalip-wa kwa ovu huo. Wala hataji-patia mlinzi wala msaidizi zaidi ya Mwenyezi Mungu.

124.Mwenye kufanya mema -mwanamume au mwanamke -hali ya kuwa ni mwenye kuami-ni, basi hao wataingia peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.

Aya 123 - 124 ANAYEFANYA UOVU ATALIPWA

:

MAANA

Aya mbili hizi zinaelezea msingi wa dhahiri ambao hakuna anayeweza kuu-tolea mjadala na kuuondoa au kuubadilisha mfumo wake kutokana na mabadiliko ya wakati au hali; wala pia hauhusiki na mwanamume peke yake au mwanamke tu. Msingi wenyewe ni "Mtu atalipwa amali zake ikiwa ni heri

Kaashif5-116.jpg

162

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

basi ni hen ha ikiwa ni shari bas

kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa mifumo mbali mbali; kama vile katika Aya

mbili hizi tulizo nazo.

Nyingine ni: "Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi yale iliyoyachuma ..." (14:

51)

"Ili awalipe wale waliofanya ubaya kwa yale waliyo yafanya" (53:31)

Si matamanio yenu wala matamanio ya watu wa Kitabu.

Wakanushaji waliwaambia wale wanaowalingania kwenye imani kuwa ni sawa tu muwe mmetupa mawaidha au la, haya ni mambo ya zamani tu sisi hatu-taadhibiwa. Mayahudi walisema hataingia ila aliye yahudi au naswara. mmoja katika waislamu alisema kuwa moto umeumbiwa wasiokuwa waislamu. Hivi ndivyo walivyo watu wote kufarahia dini waliyo nayo. Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema kwake: Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa uovu huo.

Vyovyote itakavyokuwa Mwenyezi Mungu hana nasaba wala sababu na yey-ote, isipokuwa ikhlas na amali njema. Dalili tosha ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

"... Hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchae Mungu zaidi katika nyinyi" (49:13)

Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) amesema: "Hatukuwa sisi ila ni watumwa wa ambaye ametuumba na kutuchagua, Wallahi sisi hatuna hoja yoyote kwa Mwenyezi Mungu wala hatuwezi kumwepuka. Sisi tutakufa na tutasimama (mbele ya Mwenyezi Mungu) na tutaulizwa. Mwenye kuwapenda Ghulat ame-tuchukiza na mwenye kuwachukia ametupenda. Ghulat ni makafiri na mufawadhaa ni washirikina*15 ."

MWANAMUME NA MWANAMKE

Mwenye kufanya mema - mwanamume au mwanamke - hali ya kuwa ni mwenye kuamini, basi hao wataingia peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.

t ni wale waliopetuka mpaka katika kumpenda Ali na kumfanya ni Mungu. Mufawawwidha ni wale wasemao kuwa vitendo vya binadamu viko chini ya uwezo wake sio wa Mwenyezi Mungu kinyume na Mujabbira waliosema kuwa binadamu analazimishwa na Mwenyezi Mungu katika vitendo vyake. Ama Ahlul-adl wanasema: Hakuna kulazimishwa wala kuachiliwa, lakini mambo yako baina ya mambo mawili.

Kaashif5-117.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

"Mââdâmunikeha mume vi/âkö sâvi/â kâtîkâ

basi inalazimika kuwa sawa katika malipo. Kama kuna tofauti kwa namna fulani, basi tofauti hiyo haisihi kwa hali yoyote katika malipo mema na mabaya. Yametangulia maelezo katika kufasiri (2: 228) kifungu 'Mwanamume na Mwanamke katika sharia ya kiislamu

Kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hali ya kuwa ni mwenye kuamini." Ni sharti la kuingia peponi; kama ilivyofafanuliwa katika Aya: "Basi hao wataingia peponi." Lakini sio sharti la malipo mengine ya amali njema. Kafiri akifanya amali njema kwa njia ya kheri kwa fahari au biashara, Mwenyezi Mungu atamlipa kwa sababu Mwenyezi Mungu ni mwadilifu hapotezi malipo ya mwenye kufanya amali njema. Kwa nini isiwe hivyo, na yeye ndiye aliyesema: "Hakuna malipo ya hisani ila hisan." (55: 60)

Si lazima malipo ya hisani kuwa ni pepo, inaweza kuwa malipo duniani au Akhera kwa kupunguziwa adhabu au kwa kutokuwa motoni wala peponi. Tumeyafafanua hayo katika kufasiri 3: 176 kifungu 'Kafiri na amali njema,' Pia katika kufasiri 4: 34.rejea

125.Ni nani mwenye dini nzuri kuliko yule aliyeusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu na akawa mwema na akafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim kuwa rafiki mwandani.

126.Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kukizunguuka kila kitu.

Kaashif5-118.jpgKaashif5-119.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ...

Aya 125 - 126 NÂNİ "MWENYE DİNI NZÜRI..

MAANA

Na ni nani mwenye dini nzuri kuliko aliyeusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa mwema.

Makusudio ya kusalimisha uso ni kusalimu amri, Maana ni kuwa, mkamilifu ni yule ambaye anamtarajia Mwenyezi Mungu wala hamtarajii asiyekuwa Mwenyezi Mungu na anafuata desturi alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa viumbe vyake katika maisha haya. Ni kwa hivi tu ndio mja atakuwa karibu na Muumba wake. Ama mwenye kuwanyenyekea waungu wa dunia kwa tamaa ya mali waliyonayo na jaha, basi hana chochote kwa Mwenyezi Mungu: hata kama atasimama kwa ibada usiku na kufunga mchana.

Na akafuata mila ya Ibrahim mwongofu.

Yaani akamfuata Ibrahim (a.s.) ambaye ameachana na kila yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu aliyewaambia watu wake:

"... Je, mnanimhoji juu ya Mwenyezi Mungu na hali yeye ameniongoza? Wala siogopi wale mnaowashirikisha naye ..." (6: 80)

Unaweza kuuliza Kwa nini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na akafuata mila ya Ibrahim na wala asiseme mila ya Muhammad?"

Jibu: Kwanza, mila ya Ibrahim na Muhammad ni kitu kimoja "Hakika watu wanaomkurubia zaidi Ibrahimu ni wale waliomfuata, na Mtume huyu na walioamini pamoja naye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa waumini." (3:68)

Pili, Utume wa Ibrahim umeafikiwa na dini zote, sio uislamu peke yake. Kwa hiyo kuutolea hoja kwa wasiokuwa waislam kutakuwa na nguvu zaidi, kama sikosei.

Na Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwandani.

Mwenyezi Mungu amemhusu Ibrahim kwa cheo kikubwa kinakurubia kuwa zaidi ya unabii na utume. Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim ni mja wake kabla ya kumfanya Nabii na akamfanya nabii kabla ya kumfanya mtume na akamfanya mtume kabla ya kumfanya rafiki mwandani."

165

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini.

Yeye ni mwenye kumiliki kila kitu mwenye kukiendesha kila kitu na mwenye kukizunguuka kila kitu.

Unaweza kuuliza kuwa maana haya yamekaririka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu mara nyingi, je kuna siri gani?

Jibu: Siri ni kumzindua binadamu na kubaki daima kukumbuka kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kuendesha ulimwengu, na kwam-ba amri yake ni yenye kupita humo na yeye binadamu daima yuko kwenye ujuzi wa Mungu, uweza na hekima yake. Nafsi itakapotambua hakika hii, itafanya matendo kulingana na aliyeiumba, kwa kufuata njia zake na kutii amri zake.

Zaidi ya hayo, kukaririka kunakuja kwa mnasaba unaohitajia, ambao mara nyingine wafasiri wanaweza kuutambua na mara nyingine wasiutambue. Nao hapa ni kwamba baadhi wanaweza wakafikiria kwamba Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim rafiki; kama vile sisi tunavyowafanyia marafiki. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akaondoa tuhuma hii, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumbaji mwenye kumiliki kila kitu na kwamba Ibrahim yuko chini ya milki yake, lakini yeye ni mja aliyechaguliwa, si kama waja wengine.

127.Wanakutaka fatuwa kuhusu wanawake,                  waambie

Mwenyezi Mungu anawapa fatuwa kuhusu wao na yale msomewayo humu Kitabuni kuhusu mayatima wanawake, ambao hamuwapi wali-choandikiwa, na mnapenda kuwaoa, na walio dhaifu katika watoto, na muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na heri yoyote muitendayo basi Mwenyezi Mungu anaijua

Kaashif5-120.jpgKaashif5-121.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ..

Aya 127:WANAKUUOZA KÜHÜSÜ WANAWAKE

MAANA

Mwanzoni mwa Sura Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja kidogo hukumu ya mwanamke na yatima, akafuatilia kwa kuwataja watu wa Kitabu, wanafiki na vita. Kisha akarudi tena kutaja mwanamke na yatima na kutaja baadhi ya hukumu zao kwa kukamilisha hukumu ya familia, aliyoianzia Sura. Hii ndiyo njia ya Qur'an kuelezea jambo kisha kuingiza jambo jingine tena kurudia jambo la kwanza kwa makusudio ya kuathiri katika nyoyo na mengineyo yanayohita-jia hekima na kuwachukulia upole waja.

Wanakutaka fatuwa kuhusu wanawake

Fatuwa ni kubainisha mushkeli. Yaani wanakutaka wewe Mtume wa Mwenyezi Mungu uwabainishie hukumu ya wanawake katika urithi, ndoa n.k.

Waambie Mwenyezi Mungu anawapa fatuwa kuhusu wao. Hii inafa-hamisha kwamba kuweka sharia ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake; Mtume hana zaidi ila kufikisha. Imethibiti kwamba Mtume alipokuwa akiulizwa jambo ambalo hajateremshiwa wahyi alikuwa hajibu mpaka ateremshiwe wahyi.

Na yale msomewayo humu Kitabuni kuhusu mayatima wanawake.

Yaani Mwenyezi Mungu anawapa fatwa kuhusu wanawake vile vile Qur'an inawapa fatwa kuhusu hao wanawake.

Unaweza kuuliza kuwa kufutu Qur'an ni kufutu kwa Mwenyezi Mungu hasa. Kwa hiyo kuunganisha kati ya mawili hayo ni kuunganisha kitu chenyewe.

Jibu: Makusudio ya kufutu kwa Qur'an hapa ni yale yaliyotangulia kubainishwa mwanzo wa Sura.

Na makusudio ya kufutu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni yale aliyoyabainisha hapa kukamilisha yaliyotangulia. Kwa dhahiri ni kuwa kuunganisha kunafaa ikiwa kutakuwa na tofauti za mwelekeo fulani kama vile kutofautiana wakati au mahali pa jambo moja.

Ambao hamuwapi walichoandikiwa.

167 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Yaarii MwehyeziMuriğü"Wâ'"<3ü?ân"l'h¥wâbâîri]sh]'a"hükumu'"y¥"wâWâwake' ambao mliwazuilia fungu lao la urithi na mahari. Waarabu wakati wa ujahiliya walikuwa wakimdhulumu mwanamke na kumfanya kama bidhaa au mnyama.

Na mnapenda kuwaoa. Mwanamume katika wao alikuwa akijichukulia yatima akiwa mzuri amempendezea humuoa, na kuila mali yake akiwa hakumpen-dezea humzuia asiolewe mpaka afe na achukue mali yake, mara nyingine humuua kwa lengo la kuchukua mali.

Na walio dhaifu katika watoto.

Yaani anawatolea fatwa pia kuhusu watoto wadogo ambao hamuwapi fungu lao la mirathi; na walikuwa hawamrithishi ila anayeweza kushika silaha. Ndipo Mwenyezi Mungu akalikataza hilo na akafanya fungu la mwanamume ni mara mbili zaidi ya mwanamke. Kwa hiyo hii ni kutilia mkazo ubainifu uliotangulia mwanzo wa Sura.

Na muwasimamie mayatima kwa uadilifu.

Yaani pia anawapa fatwa ya kuwasimamia mayatima kwa uadilifu wao wenyewe na mali zao. Kumpa kila mmoja katika wao haki yake kamili, awe mwanmume au mwanamke mdogo au mkubwa.

Na heri yoyote muitendayo - kuwatendea mayatima na wananwake - basi Mwenyezi Mungu anaijua.

Kwa ufupi maana ya Aya ni kuwa waislamu walimtaka Mtume kuwabainishia hukumu ya wanawake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia Mtume wake: waambie Mwenyezi Mungu amewabainishia sehemu ya hukumu hii na sasa anawabainishia sehemu nyingine, la muhimu kwenu ni kufanya uadilifu na kui-tumia hukumu hiyo. Kisha akawabainishia Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika Aya inayofuatia hukumu ya mwanamke, anayehofia unashiza wa mumewe na kuachana na mumewe.

168 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 'Y28Jkİwâ"'mke""âtahöifİâ"'mUmewe"'

kuwa nashiza au kumtelekeza, basi hapana vibaya juu yao kusikilizana kwa suluhu; Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa mbele uchoyo. Na mkifanya wema na mkajihi-fadhi, basi Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa myatendayo.

4. Sura An-Nisaa

129.Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake hata mkikamia. Basi msipon-dokee kabisa kabisa, mkamwacha (mwingine) kama aliyetundikwa. Na mkisik-ilizana na mkamcha Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu

130.Na               watakaptengana,

Mwenyezi Mungu a tam-tosheleza kila mmoja kwa wasaa wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye hekima.

Kaashif5-122.jpg

169 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ...

Aya 128 - 130 ÜNÂSHİZÂVVÂ ""MÜME

MAANA

Ikiwa mke atahofia mumewe kuwa nashiza au kumtelekeza.

Unashiza unaweza kuwa kwa mke kwa kumnyima unyumba mumewe au kuto-ka nyumbani bila ya idhini ya mume.Yametangulia maelezo ya unashiza wa mke katika kufasiri Aya ya 34 ya Sura hii.

Pia unashiza unaweza kuwa kwa mume kwa kumuudhi mke na kuacha kumpa matumizi au kumnyima siku akiwa na mke zaidi ya mmoja. Aya hii inaelezea hofu ya mke kwa unashiza wa mumewe au kumtelekeza. Makusudio ya kutelekeza ni kumwepuka kwake kunakoonyesha kumchukia. Ama kwenda kwenye shughuli zake na matatizo yake, lazima mke amvumilie na kumstah-milia madamu hamchukii.

Basi hapana vibaya juu yao kusikilizana kwa suluhu.

Ikiwa mke anahofia kuwa unashiza wa mumewe utasababisha talaka au kuwa katika hali ya kufungika - si kuwa na mume wala kuachwa, basi hapana ubaya kwa mume wala kwa mke kuafikiana wenyewe au kupitia kwa mtu. Waafikiane na kusikilizana, kuwa mume aache kumnyima haki zake, ili abakie katika hifad-hi yake na waishi maisha ya utulivu.

Na suluhu ni bora kuliko kutengana na talaka. Kuna Hadith isemayo: "Halali inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka."

Ni vizuri tueleze kuwa anachokitoa mke kwa ajili ya talaka si halali ila kwa kuridhia nafsi yake. Mwenyezi Mungu anasema: "... Kama wakiwatunukia kitu katika hayo mahari, basi kuleni kwa raha na kunufaika." (4:4)

Na nafsi zimewekewa mbele uchoyo.

Yaani uchoyo daima uko mbele katika nafsi haumwepuki hata wakati wa kutoa, ile hali ya jaka-moyo anayoihisi mtoaji na kuificha wakati wa kutoa ndio uchoyo wenyewe na makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu "na nafsi zimewekewa mbele uchoyo." Mke haiachi haki yake kwa urahisi wala mwanamume hasamehi badali. Tusisahau kuwa Aya tukufu imezungumzia matatizo ya

170 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

ühyûmbâ. Ârriaikiwa ühyüıfıbâ hâühâ mâtatizö^ h^

kutoa kitu bali hakuna kati ya mume na mke anayeona kuwa kitu ni chake.

Na mkifanya wema na mkajihifadhi basi Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa muyatendayo.

Huu ni mwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa mume na mke kufanya kila juhudi amfanyie wema mwenzake na ajichunge na sababu za kukosana na kutengana.

Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake hata mkikamia.

Kufanya uadilifu baina ya wake kuko aina mbili: Kuna kule kunakowezekana, kama kufanya usawa katika matumizi na mazungumzo mazuri. Na kuna ambako kuko nje ya uwezo wa binadamu, kama vile mapenzi ndani ya moyo na hata kujamii pia. Mume anaweza kusisimuliwa na mke, kiasi ambacho yule mwingine hamsisimui vile.

Uadilifu baina ya wanawake unaotakiwa ni katika matumizi ambao uko chini ya uwezo. Ama uadilifu katika mapenzi na mfano wake, mtu hakalifishwi nao. Na hii ndiyo inayotofautisha baina ya Aya hii na ile Aya ya tatu katika Sura hii ise-mayo: "

Na kama mkihofia kutofanya uadilifu, basi ni mmoja ..."

Imam Jafar as-Sadiq anasema: "Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: 'Mkihofia kutofanya uadilifu' anakusudia kutoa matumizi; na ama kauli yake; 'Hamtaweza' anakusudia mapenzi." Na sisi ni katika wale wanaoamini kabisa kuwa hakuna kitu kigumu kukipata kuliko uadilifu. Kwa hakika yake hasa na kiini chake ni kujikomboa na matamanio; kama ilivyoelezwa katika baadhi ya Hadith kwamba mwadilifu ni yule mwenye kuhalifu mapenzi yake na akamtii Mola wake. Wala hawi na haya ila aliyejitakasa.

Basi msipondokee kabisa kabisa. Kwa mke mnayempenda na mwingine mkamnyima haki zake.

Mkamwacha (mwingine) kama aliyetundikwa akawa si mke aliyeolewa anayepata haki zake, wala si mtalikiwa anayeweza kuolewa na mwingine anayemtaka.

Na watakapotengana, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake.

171

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

İriâtâkikâha kâbiâ yâ chöchöte"müme"nâ'mke"wajârİbü"küondoaTöfâüif zaö'n'â' mambo yanayosababisha kutengana. Kwa sababu suluhu ni bora. Ikiwa hai-wezekani, basi talaka ni bora kuondoa madhara zaidi; na fadhila ya Mwenyezi Mungu na riziki yake itawaenea wote, wawe pamoja au watengane. Mwenyezi Mungu anaweza kumpa mtalikiwa mume bora kuliko wa kwanza; na anaweza kumpa mtaliki mke bora kuliko wa kwanza.

Kwa ufupi ni kwamba yote yaliyotangulia yanazunguuka kwenye mzunguuko mmoja tu ambao ni "kushikana kwa wema na kuachana kwa wema." Kushikana ni bora ikiwa hakuna ufisadi na kuachana ni bora ikiwa kuna ufisa-di; kama ambavyo Mwenyezi Mungu ameumba dawa ya kuponesha magonjwa ya mwili, vile vile ameweka dawa ya maradhi ya kijamii.

131 .Ni vya Mwenyezi Mungu vilivy-omo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na hakika tuliwaamr-isha waliopewa Kitabu kabla yenu na nyinyi kwamba, mcheni Mwenyezi Mungu. Na kama mkikufuru, basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Mwenyezi Mungu ni mkwasi mwenye kusifiwa.

132.Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyo ardhini, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi.

133.Akitaka atawaondolea mbali, enyi watu alete wengine. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa hilo.

Kaashif5-123.jpgKaashif5-124.jpg

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-125.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

134.Anayetaka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona.

Aya 131 - 134 NI VYA MWENYEZI MUNGU VILIVYOMO MBINGUNI NA VILIVYOMO ARDHINI

MAANA

Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.

Katika juzuu ya kwanza na juzuu hii, tumezungumzia kuhusu kukaririka katika Qur'an. Sasa tutazungumzia kukaririka kwenye Aya hasa hii , kwa sababu ni Aya iliyotajwa na kurudiwa zaidi katika Qur'an . Kisha tutadokeza kukaririka kwa namna maalum ambayo imetajwa kwa kunakiliwa mara mbili katika Aya moja na kurudiwa mara ya tatu katika Aya inayoifuatia moja kwa moja bila ya kuweko kati kitu kingine.

Ama sababu za kukarika kwake kwa ujumla ni kwamba maudhui yake ni ulimwengu ambao pamoja na vilivyomo ndani yake unatolea dalili kuwapo Mwenyezi Mungu na sifa zake; kama elimu, uweza, matakwa na hekima. Ni dalili inayokusanya aina za dalili zote na vyenye kutolewa dalili. Kwa hiyo kukumbuka Aya hii ni kukumbuka kuwapo Mwenyezi Mungu na utukufu wake.

Ama kutajwa kwake hapa mara tatu, ni ishara ya faida tatu:

Kwanza: Mwenyezi Mungu katika Aya iliyotangulia amesema: "... Atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake" Kwa hiyo dalili hii imenasibiana na wasaa huu kuwa ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini.

Pili: Amesema: Kama mkikufuru basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.

Yaani yeye hamhitaji mwenye kukufuru kwa sababu vilivyomo mbinguni na

Kaashif5-126.jpg

4. Sura An-Nisaa

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

"ardhini hi vyake....

Tatu: Amesema Mwenyezi Mungu: Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi. Akitaka atawaondelea mbali, enyi watu na alete wengine.

Makusudio ni kwamba Yeye ni muweza wa kuwamaliza waasi na kuwaleta watiifu; kwa sababu ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Kwa hiyo kila moja katika mara hizo tatu ina sababu yake na kukutanishwa na faida mpya.

A nay eta ka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera.

Yaani malipo ya duniani na akhera yanawezekana kupatikana pamoja na imani na takua. Mwenye kudhani kuwa malipo ya duniani hayawi pamoja na takua, basi huyo amekosea. Kwa sababu hakuna kitu chochote kinachotengeneza vizuri maisha ya hapa duniani ila kitakuwa kinakubaliwa na dini bali kinaamr-ishwa na kuhimizwa na hiyo dini, lakini kwa sharti moja tu; kuwa kufanikiwa kwake kusiwe ni uovu kwa mwingine na utukufu wake usiwe ni utwevu wa mwingine.

Kwa hivyo malipo ya duniani na akhera hayagongani; isipokuwa kugongana kunatokea baina ya dhulma na malipo ya akhera - baina ya ghushi, hadaa na unyang'anyi na vilevile radhi za Mwenyezi Mungu, neema zake na pepo yake.

135.Enyi mlioamini! Kuweni imara na uadilifu mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi wawili na jamaa wa karibu. Akiwa ni tajiri au fukara basi Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Basi msifu-ate hawaa ili mfanye uadilifu. Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.

Kaashif5-127.jpgKaashif5-128.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-129.jpg

136.Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume wake na Kitabu alichokiteremsha kabla. Na mwenye kumkakataa Mwenyezi Mungu na Malaika Wake na vitabu vyake na siku ya mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.

KUWENI IMARA NA UADILIFU Aya 135 - 136

BAINA YA DINI NA WATU WA DINI

Sijaona Aya katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu inayoambatana na dini ila ninahisi umbali na tofauti iliyopo baina ya dini kama alivyoipanga katika Kitabu chake na dini kama tunavyoitekeleza sisi. Sisi tunazungumzia dini na kuitolea mwito kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba sisi hatuna lolote katika amri yake na ni watumwa wa dini, kama tulivyo watumwa wa Mungu. Hayo ndiyo tuyatangazayo na kuyaeleza. Lakini dini tunavyoitangaza na tabia zetu tunazodai ni za kidini ni wapi na wapi! Na ni kinyume waziwazi. Na hii haifa-hamishi chochote zaidi ya kuwa sisi, kwa hakika na hali halisi ilivyo, ni wanafi-ki. Ni sawa tutambue hivyo au tusitambue.

Lau kama tutaifasiri dini kuwa Mwenyezi Mungu amelipa uwezo baraza la dini litunge sharia za halali na haramu, kama wanavyodai baadhi ya watu wa dini, basi hapo ingelikuwa dini inakwenda sambamba na tabia zetu. Ama tukisema kuwa dini ni ya Mwenyezi Mungu na inatoka kwa Mwenyezi Mungu, kisha tusiende sambamba na hayo katika tabia na vitendo vyetu, basi huo ni unafiki hasa.

Enyi mlioamini! Kuweni imara na uadilifu mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi wawili na

175

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa jârrîââ wa karibii...

Katika Aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema: " Na msemapo semeni kwa uadilifu hata kama ni jamaa wa karibu, Na tekelezeni ahadi ya Mwenyezi Mungu ..." (6: 152)

Maana yake ni kuwa dini inatuhukumu sisi, baba zetu na watoto wetu; na kwamba ikitokea mgongano baina ya masilahi ya kiutu na dini, basi ni juu yetu kutanguliza ya dini; hata kama hili litapelekea kufa; kama alivyofanya Bwana wa mashahidi Husein bin Ali (a.s.)

Lau mtu atalinganisha hakika hii ya Qur'an na tabia zetu ataona kuwa sisi tunaathirika na masilahi yetu na masilahi ya watu wetu, kuliko masilahi ya dini. Na akiendelea kufanya utafiti zaidi ataamini kuwa kiini cha kwanza na cha mwisho cha dini kwetu ni masilahi na manufaa tu, si Kitabu cha Mwenyezi Mungu wala Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Hivi ndivyo tulivyo au ndivyo walivyo wengi katika sisi, lakini hatutambui hili wala kulizindukia. Kwa sababu ubinafsi umetawala akili zetu na ukatengan-isha hali halisi zetu na nafsi zetu na kutuziba macho tusione haki. Pia imetu-pa ndoto ya kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni masilahi yetu hasa, vinginevyo si chochote.

Nayasema haya si kwa kumwekea nongwa yeyote au kuwa na msukumo wowote. Kwani mimi, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, sina haja na yeyote katika viumbe vyake Mwenyezi Mungu. Lakini hivi ndivyo ninavyohisi na wanavyohisi wengine wachunga haki.

Mimi nionavyo ni kuwa hakuna budi kuweko na marekebisho ya hisia hii; kama ambavyo ninaitakidi kuwa hakuna dawa ya ugonjwa huu ila kujituhumu sisi wenyewe; na ninaitakidi kuwa sisi ni wa kawaida tu kama wengine tuna hawaa na mapondokeo ambayo ni lazima tujihadhari nayo na tuyahalifu. Ninasema haya nikijua kuwa ni kama kupiga kelele za kutaka msaada jangwani. Kwa sababu ni kilio kutoka kwa nafsi zetu kwenda kwa nafsi zetu, ambazo ndizo adui mkubwa katika maadui zetu.

Akiwa tajiri au fukara basi Mwenyezi Mungu anwastahiki zaidi.

Kila mtu katika wanadamu ana hali ya kukubali heri na shari wakati huo huo anaumbile la kuchagua heri kuliko shari, kiasi ambacho lau ataachwa na umbile lake, angelifanya lile analoitakidi kuwa ni heri; wala hawezi kuiepuka ila

176 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'kwia'sabâbü'zâ'nje"yâ'dhâTi'yâke'h¥'mâumb]1e"yâke.'...

Wanavyuoni wa elimu ya sifa za Mwenyezi Mungu wametolea dalili hakika hii kwamba mwenye akili lau atahiyarishwa baina ya kusema uongo apewe pesa, basi angelichagua ukweli kuliko uongo.

Kwa hiyo mwenye akili hasemi uongo ila kwa sababu; kama vile hofu, tamaa, kupendelea jamaa wa karibu, kuchukia adui, kuwahurumia mafukara au kujipendekeza kwa tajiri. Na amesema mkuu wa wasemaji; Akiwa - wenye kushuhudiwa - ni tajiri au fukara, basi Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Yaani kwamba yeye ni mwenye kurehmu zaidi mafakiri kuliko sisi na ndiye anayejua maslahi yake na maslahi ya tajiri. Sisi wajibu wetu ni kusema haki tu ni sawa iwe itawasaidia au la.

Ingawaje Mwenyezi Mungu hakutaja sababu zinazosababisha kupotoka zaidi ya kustahiki tajiri au kumuhurumia fakiri, lakini sababu ni ya kiujumla. Haki ina-paswa kufuatwa hata kwa maadui wa dini.

Basi msifuate hawaa ili mfanye uadilifu. Yaani, mtakuwa watu wa uadilifu kwa kuacha hawaa na kwenda kinyume nayo. Imesemekana kuwa tafsiri yake ni kukadiria kuchukia kwa maana ya msifuate hawaa mkaacha uadilifu. Yaani nyinyi mnafuata mapenzi kwa kuchukia uadilifu na kwamba Mwenyezi Mungu amewakataza hilo. Lakini tafsiri ya kwanza ndiyo iliyo karibu zaidi.

UADILIFU

Wamehitalifiana mafakihi katika maana ya uadilifu na wakarefusha maneno. Kuna katika wao mwenye kusema, ni dhahiri ya uislam bila ya kudhihirisha ufasiki, Mwingine akasema, ni tabia iliyomo ndani ya nafsi inayopelekea kufanya wajibu na kuacha haram, wa tatu akasema, ni sitara na kujistahi, wa nne akasema ni kuacha madhambi makubwa na kutoendelea na madogo.

Katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msifuate hawaa ili mfanye uadilifu." Ni kuonyesha kuwa uadilifu ni kuhalifu hawaa. Amirul-muminin Ali (a.s.) alimsifu ndugu yake, kwa Mwenyezi Mungu, katika aliyomsifu kuwa; "Alikuwa akijiwa ghafla na mambo mawili huangalia lipi lililo karibu zaidi na hawaa kisha akalikhalifu."

Na akasema: "Mwanzo wa uadilifu wake ulikuwa ni kukanusha hawaa ya nafsi yake."

Amesema Mjukuu wake, Imam Jafar as-Sadiq: "Ama katika mafaqih

177 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

atakayekuwa âhaîchûhğa riâfsr^

kukhalifu hawaa yake, mwenye kutii amri ya Mola wake basi ni juu ya watu

kumfuata."

Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo. Yaani msicheleweshe au kuacha kutoa ushahidi. Kisha akatoa tisho na kiaga kwamba mwenye kuyafanya hayo Mwenyezi Mungu anamjua na atamwadhibu.

Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume wake na Kitabu alichokiteremsha kabla.

Mtu anaweza kuamini Muumbaji na kukanusha utume na vitabu vya Mwenyezi Mungu. Na anaweza akakubali utume wa baadhi na baadhi ya vitabu; au kukanusha kuwapo Malaika au Siku ya Mwisho.

Aya hii imebainisha nguzo za imani ambazo ni wajibu kuzikubali kila mwenye kuacha shirki na ulahidi na kuziamini zote sio baadhi ya sehemu zake. Nguzo zenyewe ni kumwamini Mwenyezi Mungu na mitume yake yote, vitabu vyake na Malaika wake na pia Siku ya Mwisho.

Kwa hiyo makusudio ya neno 'wale walioamini,' ni wale walioacha ushirikina na ulahidi. 'Na wale walioamini' la pili ni imani ya uhakika, sio kudumu imani na kuthibiti kwenye imani kama walivyosema wafasiri, Makusudio ya Mtume wake, ni Muhammad (s.a.w.). Na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume wake ni Qur'an na Kitabu alichokiteremshia kabla, ni kila Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha kabla ya utume wa Muhammad (s.a.w.)

Na mwenye kumkakataa Mwenyezi Mungu na Malaika waake na vitabu vyake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.

Aya hii ni dalili wazi kwamba kuamini ghaibu ni nguzo katika nguzo za Kiislamu na kwamba asiyeamini si Mwislamu. Umetangulia mfano wa Aya hii pamoja na tafsiri yake katika sura 2: 285.

178 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

137.Hakika wale walioamini kisha wakakufuru kisha wakaamini kisha wakakufuru kisha wakazidi kukufuru, hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaghufiria wala kuwaon-gozea                                njia.

138.Wape bishara wanafiki kuwa wana adhabu iumizayo.

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-130.jpg

139.Ambao huwafanya makafiri ndio marafiki badala ya wau-mini. Je wanataka kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.

HAWATHIBITI KWENYE UKAFIRI WALA IMANI Aya 137 - 139:

LUGHA

Asili ya neno Bishara ni habari njema za kufurahisha ambazo zinadhihirisha furaha katika ngozi bashar (bashar) ya uso. Mtu akimwambia mwenzake nakupa bishara basi anajua kuwa kuna jambo la kufurahisha. Halitumiwi neno hilo katika jambo la kuchukiza ila pamoja na kukutana na neno jingine, kama

179 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

vile kauli yake Mwenyezi M iumizayo.

MAANA

Hakika wale walioamini kisha wakakufuru kisha wakaamini kisha wakakufuru kisha wakazidi kukufuru, hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaghufiria wala kuwaongozea njia.

Mtu anaweza kuamini dini yoyote miongoni mwa dini au itikadi yoyote katika itikadi. Hapo atashikilia na kujadiliana na watu wa dini nyingine au fikra nyingine kwa ajili ya dini yake. Kisha anasoma na kufanya utafiti ikambainikia makosa. Anaachana na fikra yake ya kwanza na kujiunga na watu wema ambao jana walikuwa ni katika maadui zake wakubwa.

Ni juu ya hawa kumkubali na kumpokea; wala hakuna haki yoyote ya kumwaibisha na kupinga mageuzi yake ya kufuata njia sahihi iliyomdhihirikia. Bali ni wajibu kumsifu na kumtukuza, kwa sababu mtu kuacha makosa ni utukufu na kuendelea nayo ni udhalilifu.

Hii ni ikiwa atathibiti na kudumu kwenye imani yake mpya. Ama akigeuka na kurudia sera yake ya kwanza, kisha akarudi tena, akarudia... Akafanya hivi mara nyingi. Huyu ni wajibu kumtoa na kumtupa. Bali ni wajibu kumwadhibu kwa adhabu kali. Hii ndiyo hali waliyokuwa nayo watu wa dini na wakuu wa madhehebu ya kisiasa tangu zamani na sasa. Kwa sababu kugeukageuka kwake huku kunafahamisha tu, kuwa yeye anafanya masihara na vitimbi na ni mzushi mwongo anayejiingiza katika ufisadi na upotevu na kuzidisha dhambi na upotevu kila anapoingia na kutoka.

Huyu na mfano wake ndio wanaokusudiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu ana-posema:

"...Walioamini kisha wakakufuru kisha wakaamini kisha wakakufuru kisha wakazidi kukufuru " Kwa sababu ya mchezo huu na kujigeuzagueza, Mwenyezi Mungu hakuwa ni mwenye kuwasamehe maadam wanayum-bayumba na kugeukageuka baina ya ukafiri na imani; wala kuwaongozea njia kwa sababu wamepotea njia kwa kuchagua uovu baada ya kuijua njia na kui-fuata.

Kwa ufupi ni kwamba muumin ni yule anayethibiti kwenye imani yake hata hali ikigeuka vipi. Ama yule anayertadi mara kwa mara, basi yeye ana hali mbaya

180 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'küîikö yüle âiiyethibitj kâtika ükâfiri ha üiâhîdi....

Wape bishara wanafiki kuwa wana adhabu iumizayo.

Razi anasema: "Mwenyezi Mungu ametumia neno 'bishara' kwa adhabu kwa istihzai sawa na msemo: 'salaam zako ni kipigo."

Ilivyo, ni kwamba mfumo wa Qur'an uko mbali na stihzai. La karibu zaidi ni kwamba makusudio ya bishara ni habari tu na inawezekana kulitumia neno hilo katika jambo la kuchukiza kwa kuambatana na jambo lenyewe; kama tulivyotangulia kueleza katika kifungu cha lugha.

Ambao huwafanya Makafiri ndio marafiki badala ya waumini. Je, wanata-ka kwao utukufu, basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.

Kila mmoja katika sisi anataka atajike katika maisha haya. Baadhi ya watu wanaweza kupupia kutaka umashuhuri kwa kufanya wema au kwa elimu. Lakini wengine hutaka utukufu na umashuhuri kwa kitu chochote kitaka-chokuwa; wanauza dini yao kwa shetani kwa ajili ya kupata umashuhuri; hum-fanya shetani ndio rafiki wa kumsikiliza na kumtii.

Ndipo hapa likaja swali la kusuta na kukanusha kutoka kwa Mola mtukufu kuwa je, wanataka utukufu kutoka kwa shetani na marafiki zake wadhalilifu. Je, utukufu unaweza kupatikana bila ya imani na takua? Uislamu kwa utukufu wake umedhalilisha dini zote, vipi utukufu utatafutwa kwa mwenye kuukanusha?

Waumini waliokusudiwa na Mwenyezi Mungu katika kauli yake "badali ya waumini" ni wale ambao uislamu umetukuka kwa ajili yao. Kwa sababu wao wameutukuza na kuuweka juu kwa jihadi yao na kujitolea kwao mhanga. Tumezungumzia kuhusu kuwafanya marafiki makafiri katika tafsir (3: 28)

181

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

Kaashif5-131.jpg

140.Na amekwisha wateremshia katika Kitabu hiki kwamba mtakaposikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na kuchezwa shere, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo hakika nyinyi mtakuwa mfano wao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanafiki na makafiri wote katika Jahannam.

141.Ambao wanawangojea mkipa-ta ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, huseme: Je hatukuwa pamoja nanyi. Na ikiwa Makafiri wamepata sehe-mu, husema: hatukuwa ni waweza wa kuwashinda tukawakinga na waumin? Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu siku ya kiyama na Mwenyezi                     Mungu

hatawafanyia makafiri njia ya kuwashinda waumini.

 

Aya ya 140 - 141MSIKAE NAO MPAKA WAINGIE KATIKA UZUNGUMZI MWINGINE

MAANA

Na amekwisha wateremshia katika Kitabu hiki kwamba mtakaposikia Aya

182

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na kuche pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengine.

Aya hii ilishuka Madina, inawakumbusha waislamu Aya iliyoshuka Makka ise-mayo: "Na unapowaona wale ambao wanaziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingie katika mazungumzo mengine; na kama shetani akikusahaul-isha, basi usikae baada ya kukumbuka pamoja na watu wadhalimu." (6:68)

Ama sababu ya ukumbusho huu ni kuwa baadhi ya Waislamu - kama ilivy-oelezwa Katika Tafsiri mbali mbali - walikuwa wakikaa katika vikao vya washirikina huko Makka waliokuwa wakingilia kumtukana Muhammad (s.a.w.) na kuicheza shere Qur'an. Waislamu wakati huo walikuwa wanyonge hawawezi kuwakanya; ndipo ikashuka Aya hiyo (6: 68), kuwahadharisha waislamu waepukane na washirikina na kuwaamrisha wasikae nao wanaposikia kufru na kuchezwa shere Aya za Mwenyezi Mungu.

Siku zikapita na waislamu wakahamia Madina; huko nako kulikuwa na mayahudi na wanafiki, waliodhihirisha uislamu na kuficha ukafiri. Baadhi ya waislamu wakarudia mwenendo wao wa kwanza, wakakaa na mayahudi na wanafiki waliokuwa wakiutusi uislamu na Mtume wake; ndipo ikashuka Aya hii, ambayo tunaifasiri, ili kuwakumbusha waislamu Aya ile iliyoshuka Makka na kuwaamrisha kujitenga nao.

Sababu yoyote ya kushuka Aya itakavyokuwa au wanaoambiwa, itakuwa Aya ni ya ujumla inayofahamisha wajibu wa kujitenga na kila mwenye kuingia katika mazungumzo ya batili. Wajibu huu hauhusiki na ambaye alikuwa akikaa na makafiri Makka au na wanafiki Madina tu, ingawaje iko katika kuhusika si kwa ujumla. Hadith inasema: "Upweke ni bora kuliko rafiki mwovu." Nyingine inasema: "Tahadharini na kukaa na maiti." Akaulizwa ni akina nani hao maiti? Akasema: ni kila mwenye imani potofu, dhalimu katika hukumu". Katika Nahjul Balagha imeelezwa: "Kukaa na watu wapuuzi kunasahaulisha imani na kumkurubisha shetani."

Hivyo hakika nyinyi mtakuwa mfano wao

Mwenye kuridhia ukafiri ni kafiri, na mwenye kurdhia dhambi naye ana dham-bi kwa namna yoyote atakayokuwa; kwa maafikiano ya mafakihi na Maulama. Imekuja Hadith Mutawatir isemayo: Mwenye kufanya dhulma, mwenye kum-saidia na mwenye kuiridhia ni washirika," hasa mwenye kuridhia ukafiri. Katika Nahjul-Balagha imeelezwa: "Mwenye kuridhia vitendo vya watu ni kama

183

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

mwenye kuingia ndani yake na kila mwen

bi ya kutenda na dhambi ya kuridhia."

Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanafiki na makafiri wote katika Jahannam. Ambao wanawangojea mkipata ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu husema; Je, hatukuwa pamoja nanyi? Na ikiwa makafiri wamepata sehemu, husema: hatukuwa ni waweza wa kuwashinda tukawakinga na waumin.

Aya hii inachora picha ya hali ya wanafiki wakati wa vita vya waislamu na washirikina. Kwa ufupi picha yenyewe ni kwamba wanafiki walikuwa wakitoka pamoja na waislamu katika kwenda vitani ili wakaharibu na kuchafua safu za waislam. Wakati huo huo wanajionyesha kuwa wao wametoka kuwasaidia waislam; na kungoja, ikiwa ushindi ni, waislamu wakisema 'sisi tuko pamoja nanyi kwa hiyo sisi na nyinyi ni washirika katika ngawira.' Ikiwa ushindi ni wa washirikina husema, "sisi tulikuwa majasusi" Basi yako wapi malipo? Wanaishika fimbo kati kati.

Ufasaha zaidi niliousoma kuhusu wasifu wa wanafiki, ni ule aliousema Amirul-mumiinin Ali (a.s.): "Wameiandalia kila haki batili, na kila msimamo upotofu, na kila mlango ufunguo, na kila usiku taa."

Hawa wapo kila siku na idadi yao inaongezeka katika miji ya kiarabu siku hadi siku, tangu ilipojitokeza dhahabu nyeusi (petrol). Wakafanya uzalendo kuwa ni nembo kama walivyojionyesha waislamu wakati wa Mtume. Wapigania ukombozi wakiwashinda wanyonyaji na walanguzi, wanafiki huwaambia: Je, hatukuwa pamoja nanyi? Na kama wanyonyaji wakifanikiwa huwaambia: Je, hatukuwazuia wapigania ukombozi wasiwafikie.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametumia ushindi kwa waislamu na kupata sehemu kwa makafiri?

Jibu: Ushindi wa waislam ndio ushindi wa haki ambao unadumu na kubaki maadamu watu wake wanafuata desturi ya Mwenyezi Mungu na amri yake katika kujiandaa. Kwa hiyo ikanasibu kuleta ibara ya ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ama ushindi wa batili ni ushindi wa muda usiodumu, unaondoka mbele ya watu wa haki, kama wakiungana kwa Jihadi. Walikwishasema zamani; "Dola ya batili ni saa moja na dola ya haki ni mpaka Kiyama."

184 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

Wala Mweriyeizii Mürigü hate

min.

Mafakihi wameitolea dalili Aya hii kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuweka sharia inayofanya mamlaka au usimamizi wa asiyekuwa mwislamu kwa mwislamu; Na wameitolea hukumu nyingi; kama vile kuwa baba wa mtoto akiwa mwislamu na mama yake sio mwislamu, mama hana haki ya kumlea. Kwa sababu mtoto hufuata dini iliyo tukufu zaidi anayoifuata mmoja wa wazazi wawili na hukumu yake ni hukumu ya waislamu.

Hukumu nyingine ni kuwa haijuzu kwa mwislamu kuwausia watoto wake wasi-mamiwe na asiyekuwa mwislmau; na akifanya hivyo basi wasia umebatilika. Hukumu nyingine waliyoitoa katika Aya hiyo ni kuwa, baba anakuwa na usimamizi kwa watoto wake kama wana dini moja. Ama wakiwa ni waislamu na baba si mwislam hatakuwa na usimamizi juu yao. Nyingine ni kuwa hukumu ya hakimu asiyekuwa mwislamu haitekelezwi kwa haki ya mwislamu, hata kama ni haki na mengine mengi.

142.Hakika wanafiki wanamhadaa Mwenyezi Mungu, na hali yeye ndiye menye kuwahadaa. Na wanapoinuka kwenda kuswali, huinuka kivivu. Wanajionyesha kwa watu

Wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.

143.Ni vizabizabina baina ya huku na huko. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea huwezi kumpatia njia

Kaashif5-132.jpgKaashif5-133.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                     4. Sura An-Nisaa

Aya 142 - 143 WANAMHADAAMWENYEZI MUNGUNAATAWALIPAKWAKUHADAA KWAO

MAANA

Hakika wanafiki wanamhadaa Mwenyezi Mungu, na hali yeye ndiye menye kuwahadaa.

Makusudio ya kuhadaa kwao ni kule kuonyesha imani kwa Mtume na kuficha ukafiri. Kwa sababu mwenye kumhini Mtume ndio amemhini Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika wale wanaokuunga mkono kwa hakika wamemuunga mkono Mwenyezi Mungu..." (48: 10)

Makusudio ya kuwa Mwenyezi Mungu anawahadaa ni kwamba yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaadhibu kwa hadaa yao na unafiki wao.

Na wanapoinuka kwenda kuswali, huinuka kivivu.

Wataichangamkiaje na wao wanaikanusha? Hawatarajii thawabu kwa kuiten-da wala adhabu kwa kuiacha; isipokuwa wanaitekeleza kwa kuwinda dunia tu na kuifanya ni nyanzo ya uchumi. Mwenyezi Mungu anasema: "Kwa hakika hiyo Swala ni ngumu isipokuwa kwa wanyenyekevu."(2: 45)

Unaweza kuuliza: Mtu akiswali kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na pamoja na hayo anapenda watu wamuone, ili wamhisabu katika watu wema au asituhumiwe kuwa aniipuuza dini. Je hii itakuwa ni ria?

Jibu: Hapana! Maadamu msukumo wa kwanza ni wa amri ya Mwenyezi Mungu na radhi zake; mengine yanafuatia tu, Imam as-Sadiq (a.s.) aliulizwa kuhusu mtu ambaye anafanya jambo la kheri, kisha akafurahi kwa kuonwa na mtu mwingine akilifanya jambo hili (nini hukumu ya mtu huyo)? Imam akajibu: "Hapana ubaya kwa hilo, ikiwa hakuifanya kwa hilo, kwani hakuna mtu asiyependa Mwenyezi Mungu amdhihirishie kheri mbele ya watu,."

Wanajionyesha kwa watu.

Kwa sababu wao huswali kwa ajili ya kuwinda na kupata faida.

Wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. Yaani wakati wa kujionye-sha kwa watu. Ama wakiwa peke yao, hawamtaji kabisa. Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) anasema: "Mwenye kujionyesha (ria) ana alama tatu: Anakuwa mvivu

Kaashif5-134.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

akiwa pekei yake, anachangamka akiwa ha w^ asilolifanya."

JE WATU WOTE HUJIONYESHA

Unaweza kuuliza: Hakuna yeyote anayedhihirisha ukweli wake kwa watu na kuwaambia kila analoitakidi. Ni nani anayeweza kumwambia kila mtu anayoy-ajua. Na akifanya hivyo, basi atahisabiwa katika wenda wazimu, bali ni nani ambaye - mara nyingine - hafanyi asiyoyapenda na kuyataka? Kisha utaziepu-ka vipi desturi na maadili ya jamii?

Je, unaweza kumwambia mtu uliyekutana naye, ambaye humpendi, akak-wambia 'natamani kukuona,' na wewe umwambie: nachukia kukuona? Na kama utamwambia hivyo je unavyoona wewe au waonavyo watu utakuwa uko sawa? Mwisho je watu wote wanafanya ria (kujionyesha), kwa sababu hawait-akidi yote wayasemayo; wala hawaamini yote wayafanyao?

Jibu: Kuna tofauti baina ya Ria na Mudarat. Ria ni kudhihirisha unafiki na uzushi ili uwe pamoja na wema na wewe si katika wao.

Na Mudarat ni kuwa mpole na kutowachukilia na kuamiliana na watu bila ya kulenga chochote zaidi ya kutaka kuishi nao katika uelewano na maafikiano. Ni kweli kuwa mara nyingine unafanya mambo kufuata desturi ya jamii; ukapongeza, kutoa rambi rambi au kutabasamu na kumheshimu mtu kwa jamala tu si kwa kuamini, lakini jambo hili ni salama halina tashwishi yoyote.

Wala halihisabiwi kuwa ni ria maadam kulifanya kwako kunaafikiana na jamii. Vilevile si wajibu juu yako kama utatokewa na kosa - hakuna maasum - kuli-tangaza kwa watu. Ndio ni wajibu kuwadhihirishia usafi sio makosa.

Vilevile ni kweli kuwa unasema uongo unapomwambia unayemchukia 'mimi nakupenda,' lakini ni uongo ulio katika masilahi na hulka njema. Mwenyezi Mungu anasema: "Na semeni na watu kwa uzuri" (2: 83)

Je hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri mizizi yake ni imara na matawi yake yako mbinguni." (14:24)

"Nendeni kwa firaun hakika yeye amepetuka mpaka. Kamwambieni maneno laini huenda akaonyeka au akaogopa. " (20: 44 - 45)

Kuna Hadith isemayo: "Tamko jema ni sadaka, hupewa thawabu alisemaye,

Kaashif5-135.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

thawabu za wenye fadhila na ihsan." Hadith nyigine inasema: "A

Mola wangu kuwachukulia watu upole (Mudarat), kama alivyoniamrisha farad-

hi (wajib)."

Wamekongamana mafakihi kwamba uongo ni wajibu ikiwa utakuwa ni kutetea nafsi isiyo na hatia na kuiepusha na maangamivu. Na kwamba ukweli ni haram katika ufitini na usengenyaji. Kwa hiyo mfitini ni mkweli na msengenyaji ni mkweli, lakini wanashutumiwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele za watu.*15

Baada ya yote hayo ni kwamba ria ya haramu ni ile ya kudhihirisha mambo asiyokuwa nayo mbele za watu; anajionyesha kuwa ana kheri ili apate hadhi ya watu wema na huku mwenyewe ni katika waovu wafisadi.

Ni vizabizabina baina ya huku na huko, Mara wanajidhihirisha wako pamo-ja na waislamu na mara wako pamoja na makafiri; na wao hasa ilivyo nikuwa: hawako kwa hawa wala hawako kwa wale bali wako kwenye manufaa yao na tamaa zao; wanabusu mkono wowote wenye manufaa kwao uwe mchafu au msafi.

Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea huwezi kumpatia njia.

Yaani Mwenyezi Mungu anamwepuka na kumwachia mwenyewe kwa sababu ya inadi yake na kupinga kwake haki. Na ambaye mambo yake yako hivi, basi hatarudi kwenye uongofu. Na hapana budi kuzingatia kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu inasababisha kutomuacha mja wake; kama ambavyo mzazi hamwachi mtoto wake. Ila ikiwa mja mwenyewe ndiye aliyesababisha kuachwa na Mwenyezi Mungu kwa njia ya kumwasi; kama ambavyo mama anaachana na mwanawe kwa sababu ya kumwudhi sana.

Imetangulia Aya kama hii, herufi kwa herufi katika Sura hii. Aya 88 na tumeizungumzia kwa ufafanuzi kama ambavyo tulifafanua mafungu ya uongofu na upotevu katika kufasiri (2: 26)

*15 Maandiko ya Qur'an na Hadith yako kwenye misingi ya kufanya lenye masilahi na kuacha lenye uharibifu. Penya masilahi ni amri na penye uharibifu ni katazo. Kwa hiyo ndio ikajuzu kuse-ma uongo pamoja na masilahi na ikawa haramu kusema ukweli pamoja na uharibifu wenye masengenyo na upeke peke.

188 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 144.Enyimlioamini! Msiwafanye Makafiri kuwa marafiki badala ya waumini. Je, mnataka awe nayo Mwenyezi Mungu hoja dhahiri juu yenu.

4. Sura An-Nisaa

145.Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini mtotoni. Hutakuta kwa ajili yao msaidizi.

146.Ila wale waliotubu na wakatengeza (mwendo wao) na wakashikamana na Mwenyezi Mungu na wakam-takasia Mwenyezi Mungu dini yao, basi hao watakuwa pamo-ja na waumini na Mwenyezi Mungu atawapa waumini malipo makubwa.

147.Mwenyezi Mungu ana haja gani ya kuwaadhibu kama mtashukuru na mtaamini na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kupokea shukrani Mjuzi.

Kaashif5-136.jpg

189 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano 4. Sura An-Nisaa ..

Aya 144 - 147:MSiWAFANYE MÂKÂFIRI KÜWÂ MÂRÂFİKİ

MAANA

Enyi mlioamini! Msiwafanye Makafiri kuwa marafiki badala ya waumini.

Imetangulia Aya hii pamoja na tafsir yake katika (3:28)

Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyowazi juu yenu?

Kila asiyekuwa na ubainifu wa dini yake au kupomoka na njia ya uongofu baada ya kumbainikia, basi yeye mwenyewe amempa Mwenyezi Mungu hoja nzuri juu yake mwenyewe.

Hebu tusome dua hii:"Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tunakiri kwamba wewe huadhibu ila baada ya kusimamisha hoja. Vile vile tunakiri kuwa hoja imetusimamia, bali tunagwaya na kutetemeka kwa kuhofia mashiko yako na tunataka hifadhi yake kwa msamaha wako na utukufu wako. Kwa hiyo haku-na haja ya kusimama mbele zako kwa kuhukumiwa na kuhisabiwa au kuchun-guzwa."

Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini motoni. Hutakuta kwa ajili yao msaidizi

Kwa sababu adhabu iko kwa kiasi cha kosa, na hakuna kosa kubwa kuliko unafiki ambao umekusanya ukafiri na uongo. Yote mawili ni mama wa maovu.

Ila wale waliotubu na wakatengeneza (mwendo wao) na wakamtakasia Mwenyezi Mungu dini yao; basi hao watakuwa pamoja na waumini. Na Mwenyezi Mungu atawapa waumin malipo makubwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutoa kemeo na kiaga cha adhabu kali kwa wanafiki, anawaongoza kwenye toba, njia ya uokofu na kuokoka, njia pekee ya kutaka nusura na shufaa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hilo liko mikononi mwao na katika uwezo wao. Mwenye kuzembea, basi na ajilaumu mwenyewe. Hii ni hoja nyingine kwa kila mwenye dhambi, anayoiongezea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye hoja zake sahihi ambazo hazina idadi.

Tumeweka mlango mahsusi wa toba na wenye kutubia wakati wa kufasiri Aya 18 katika Sura hii. Wafasiri wamerefusha maneno katika kubainisha tofauti katika viunganishi vilivyo katika Aya hii waliotubu, wakatengeneza (mwendo wao), wakashikamana na Mwenyezi Mungu na wakamtakasia Mwenyezi

Kaashif5-137.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Mütigü dirii yâö; Tüöhâvyö"sls]"nİ"kuwâ"nerib'Wbâ"1]haküsâny¥'slfâ"zHe"h]zr kwa ukamilifu wake; wala hatuoni tofauti ya kimsingi baina yao; isipokuwa yamekuja kwa kutilia mkazo kuonyeshwa yale waliyokuwa nayo wanafiki -kubabaika na kuasi, na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakubali toba yao wala hatawaingiza katika hisabu ya waumini ila wakiwa na uthabiti na kuen-delea na toba; na wao wakirtadi baada ya toba na wakatenda kama wanavy-otenda, basi kurtadi kwao kutaongezea ukafiri wao, uzushi wao na ubabaikaji wao. Hakuna malipo ya kurtadi ila kifo duniani na adhabu chungu huko Akhera.

MWENYEZI MUNGU NA UNYENYEKEVU WA IMAM ZAINUL ABIDIN

Mwenyezi Mungu ana haja gani ya kuwaadhibu kama mtashukuru na mtaamini?

Kabisa hana haja! Yeye anajitosheleza na kila kitu katika dhati yake na sifa zake vinginevyo basi asingeweza kuumba; isipokuwa anapatiliza na kuadhibu kwa malipo yenye kulingana. Wala hamhitajii kiumbe katika kupatikana kwake na kubaki kwake na katika harakati zake zote.

Sasa msomaji hebu tusikilize unyenyekevu na utukuzo ulio katika munajat huu utokao kwa Imam Zainul Abidin: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ni mtu duni na mawazo yangu ni mepesi; wala adhabu yangu haiongezi chembe katika milki yako. Lau adhabu yangu ingelikuwa inazidisha kitu katika milki yako, basi ningekuomba univumilie na ningependa iwe hivyo kwako, lakini ufalme wako ni mkuu zaidi usioweza kuongezewa kitu na utiifu wa wenye kutii au kupunguzwa na maasi ya wenye dhambi."

Munajat huu sio alama tu ya kuonyesha upeo wa mapenzi na shauku juu ya wema wa Mwenyezi Mungu na utakatifu wake; kama wafanyavyo masufi, wala sio dua tu ya kuhofia adhabu ya Mwenyezi Mungu hata kama dhahiri ya maneno inafahamisha hivyo, isipokuwa ni maelekezo kwa kila mwenye nguvu anayetaka kuwakaba wanyonge wasio na uwezo na kwamba lililo bora kwa uwezo wake juu ya wanyong e ni msamaha, na wala sio kuadhibu na kutesa. Nguvu haziwezi kuwa bora na kamilifu ila kwa kusamehe. Hakika kuhitajia au ukorofi ndio unaosababisha kumtesa asiyekuwa na kimbilio ila kwa mwenye nguvu. Na mwenye nguvu aliye mkamilifu hahitajii wanyonge, ni Mwenye kuji-tosheleza Mwenye kutakata na upungufu.

Baada ya yote hayo; hakika msamaha ni bora, sisi tuna haja nao na Mwenyezi

Kaashif5-138.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano                                                  4. Sura An-Nisaa

'Mühğü hi muweza"'naö"n¥'Wâİâ"hâkünâ"zâîdî"küİ]kö"Yeye" Kwâ hiyö basi' msamaha wake uko. Tunasema haya na sisi tukiwa miongoni mwa wanaom-wogopa Mwenyezi Mungu.

Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kupokea shukrani Mjuzi.

Anamjua mwenye kumtii na mwenye kushukuru na humlipa ujira wa watiifu wa wenye kushukuru. Tumemwamini Mwenyezi Mungu peke yake. Twanyenyekea tukimwambia Yeye s.w.t. atuwafikishe kumshukuru na kumtii.

192

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Tano

4. Sura An-Nisaa

193