AL-KASHIF

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

SWAHILI - JUZUU YA PILI (Vol-2)


YALIYOMO

AL- BAQARAH -(Sura ya pili)

Aya 142:  Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao .2

Kwa nini kuswali upande maalum .....2

Aya 143: Tumewafanya kuwa ni Umma wa wastani ...4

Ukamilifu na uwiano katika Uislamu ...6

Aya 144-145: Hakika tunakuona unavyogeuza uso wako......10

 

Ni wakati gani unapasa kuelekea Qibla..14

Watu wa Qibla.14

Uislamu na watu wenye upendeleo na dini zao ...16

Aya 146-147: Wanamjua kama wanavyowajua watoto wao ..18

Mimi na Mhubiri .18

Aya 148-152: Kila Umma ulikuwa na Qibla chake ....20

Katiba ya Uislamu .....24

Kumshukuru Mneemeshaji .....26

Aya 153-157: Jisaidieni kwa Subira ....26

Thamani ya Pepo ...30

Aina ya malipo ya wanaosubiri . . 32

Aya 158: Swafa na Marwa ...34

Aya 159-162: Wanaoficha yaliyoteremshwa .

36

Ubaya wa adhabu bila ya ubainifu 38

Hukumu ya laana katika sharia . 40



 

 

Aya 163-164: Na Mungu wenu ni Mungu

Mmoja 42

Mbingu .....42

Ardhi .42

Kuwapo Mungu ....44

Upi uliotangulia Usiku au Mchana 46
Aya 165-167: Wanafanya waungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) .46

Taqlid na Maimamu Wanne .....50

Aya 168-170: Kuleni vilivyomo katika Ardhi . . . .50

Kufuata na msingi wa itikadi . . . . 54

Aya 171: Mfano wa anayeita asiyesikia . . .58

Aya 172-173: Kuleni Vizuri .60

Mwenye dharura na hukumu yake 62

Aya 174-176: Wafichao aliyoyateremsha

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) .62

Mvutano kati ya Haki na Batili .....66

Aya 177: Anatoa mali akiwa aipenda .68

Wema katika ufahamu wa Ki-Qur'an 74


 

 

Aya 178-179: Kisasi cha waliouawa ..74

Aya 180-182: Wasia kwa wazazi ....80

Kuwausia warithi .....82

Aya 183-185: Mmelazimishwa kufunga ...84

Aya 186: Naitikia maombi ya mwombaji .....

88

Aya 187: Mmehalalishiwa Usiku wa Saumu .

90

Aya 188: Kula mali kwa Batili ...

92                            .

Hukumu ya kadhi fasiki ...

Aya 189
Aya 190 -193
Aya 194 – 195
Aya 196 – 203
Aya 204 – 207
Aya 208 – 210

Aya 211 – 212
Aya 213:
Aya 214:
Aya 215:
Aya 216 - 218:
Aya 219 – 220
Aya 221
Aya 222 – 223
Aya 224 – 227
Aya 228:
Aya 229 – 230
Aya 231 – 232
Aya 233
Ay a 234 - 235:
Aya 236 -237
Ay a 238 - 239:
Aya 240 – 242
Aya 243 – 244
Aya 245
Aya 246 - 252:

 

 

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 665 34 - 9

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

Kimetafsiriwa na: Sheikh Hasan Mwalupa

P.O. Box 1017, Dar es Salaam/Tanzania. Email:mwalupa@hotmail.com

Kimehaririwa na: Dr.M.S. Kanju.

S.L.P 1017, Dar es Salaam. Email: drmkanju@yahoo.com Website: www.dartabligh.org

Kupangwa katika kompyuta na: Ukhti Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: Februari 2004 Nakala:5000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation

P.O. Box 1017 Dar es Salaam, Tanzania Simu:+255 22 2110640 Fax: +255 22 2126757 Email: alitrah@daiichicorp.com Website: www.alitrah.org

Kaashif2-2.jpg

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wad-hifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana

i

Kaashif2-3.jpgKaashif2-4.jpg

hata kuweza kutoa kitabu kitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyan-si kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

Mchapishaji.

ii

Kaashif2-5.jpgKaashif2-6.jpg

Makosa ya Chapa.

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya Msahafu Mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswatu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama". Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: " Hatta idaha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidaha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakay-oyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefun-gua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu cho-chote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): "Watu wote ni wapun-gufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH

iii

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao               walichokuwa wakikielelekea?         Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

143. Na kama hivyo hivyo tume-wafanya kuwa umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu wote, na Mtume awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya Qibla uli-chokuwa nacho ila tupate kumjua yule anayemfuata Mtume na yule atakayegeuka akarudi nyuma . Na kwa hakika lilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale aliowaongoza Mwenyezi Mungu. Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwapotezea imani yenu. Hakika Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole Mwenye kurehemu.

Kaashif2-13.jpg

2

2

Kaashif2-14.jpgKaashif2-15.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

NINI KILICHOWAGEUZA KUTOKA QIBLA CHAO?

Aya 142:

LUGHA

Amesema Ibnul Arabi katika tafsiri yake: "Kila asiyejua hakika ya Dini ya Kiislamu huyo ni mpumbavu, kwa sababu yeye ana akili hafifu. Neno Qibla limechukuliwa kutoka katika neno Istqbal (kuelekea); yaani kila upande anaoulekea mtu.

MAANA

Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao walichokuwa wakikielekea?

Mitume waliotangulia walikuwa wakiswali kuelekea Baitul Maqdis. Na Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akitamani lau Qibla kinageuzwa kuwa Al-Kaaba. Mwenyezi Mungu aliyathibitisha matamanio yake, kama itakavyoelezwa.

Makusudio ya wapumbavu hapa ni Mayahudi, ndio waliowalaumu Waislamu kwa kuacha kwao kuelekea BaitulMaqdis.

Tamko Sayaqulu (Watasema) kwa dhahiri linafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu alimfahamisha Mtume wake Mtukufu kauli ya wajinga kabla ya kutokea. Ama yule anayesema kuwa neno Sayaqulu ingawaje kwa dhahiri linafahamisha muda wa mbele, lakini makusudio ni muda uliopita; na kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume wake baada ya kusema wajinga, sio kabla ya kusema; na kwamba limekuja kwa muda ujao, kwa vile yaliyosemwa yalikuwa yamekwisha kadiriwa, ama kwa hakika kauli hii ni kujaribu kutoa tafsir nyingine (Taawil) bila ya dharura yoyote na bila ya dalili yoyote inayofahamisha hilo.

3

3

Kaashif2-16.jpgKaashif2-17.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) kuwajibu wajinga hawa kwamba: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; humwongoza amtakaye katika njia iliyonyooka. Yaani pande zote ni za Mwenyezi Mungu:

Al-Kaaba na Baitul Maqdis ni sawa tu, lakini kwa hekima na masilahi mara nyingine humwongoza anayemtaka kwenye Baitul-Maqdis na mara nyingine kwenye Al-Kaaba.

KWA NINI KUSWALI UPANDE MAALUM?

Hili ni swali wanaloliuliza watu wengi kwa nini swala ni wajibu kwenye upande malum na haiswihi isipokuwa upande huo? Na hali yeye amek-wisha sema waziwazi:

Kaashif2-18.jpg

Na popote mnakoelekea (mtazikuta) radhi za Mwenyezi Mungu (2:115). Jibu: Kwanza Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema:

Kaashif2-19.jpg

"...Na elekeza uso wako upande wa msikiti Mtakatifu (Al-Kaaba); na popote mlipo zielekezeni nyuso zenu upande huo..." (2:144).

Aya hii ni ubainifu na Tafsir ya Aya 115 na makusudio yake ni kuelekea kwenye upande wowote katika swala ya Sunna na katika swala ya asiyejua Qibla kiko wapi. Makusudio ya Aya 144 ni kuelekea (Al-Kaaba) katika swala ya wajibu. Umekwishatangulia ufafanuzi wa hilo katika Aya 115.

Pili, kuswali swala kunategemea amri ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na

4

4

Kaashif2-20.jpgKaashif2-21.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

asili hii hapana budi tuangalie: Je inawezekana tuswali upande wowote tunaoutaka sisi au kwenye upande maalum. Ikiwa kauli ya kwanza ni sawa, basi itakuwa haiswihi swala isipokuwa kwenye upande ulioamrishwa tu; ni sawa iwe ni Al-Kaaba au Baitul-Maqdis au mahali pengine.

Pia ifahamike kwamba kufuata amri ni jambo j engine na kuweko radhi za Mwenyezi Mungu kila upande ni jambo j engine. Hakika ibada ni katika mambo yanayongoja ubainifu wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume wake, wala hakuna nafasi ya dhana na uwezekano; isipokuwa kwa kauli sahihi iliyo wazi. Na Mwenyezi Mungu aliaamrisha Waislamu kuswali kuelekea Baitul-Maqdis kwanza; lau wangeliswali kuelekea Al-Kaaba isingekubaliwa swala yao. Kisha Mwenyezi Mungu akawaamrisha kugeu-ka Al-Kaaba lau wangeling'ang'ania Baitul-Maqdis basi isingekubaliwa swala yao; pamoja na kuwa pande zote mbili ni za Mwenyezi Mungu. Hilo ni kwa sababu kipimo cha kusihi swala ni kuafikiana na sharti zote; kama vile ambavyo kuharibika swala ni kuhalifu amri.

UMMA WA WASTANI Ay a ya 143: LUGHA

Neno Wast lina maana ya kati kati na neno Wasat lina maana ya ubora, Mtume anasema Bora ya mambo ni wastani. Linakuja neno wasata. Kwa maana ya kulingana sawa (wastani). Neno wastani na ubora yanakuru-biana.

Makusudio ya Wasat hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameijaalia dini ya Waislamu ni ya wastani; yaani ni ya kati na kati katika itikadi na maadili. Kwa upande wa itikadi hakuna ushirikina wala ulahidi, bali ni Tawhid tu, na kwa upande wa maadili sio ya kimaada wala kiroho, bali ni pande zote mbili kwa sharti ya kulingana sawa na kukamilika.

Neno 'kurudi nyuma' ni istiara yaani kueleza mtu anayemkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa sababu mwenye kuacha imani yake yuko katika daraja ya asiyeendelea mbele.

5

5

Kaashif2-22.jpgKaashif2-23.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

MAANA

Tumewafanya kuwa umma wa wastani.

Jumla hii ni ubainifu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Kaashif2-24.jpg

Humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka." (2:213).

Njia ya kubainisha hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewa-neemesha wafuasi wa Muhammad (s.a.w.w) kwa uongofu. Linalodhihirisha zaidi uongofu huu ni kuwa Yeye amewajaalia wao kuwa katikati; yaani hawakuzidisha, kama vile kuwazidisha waungu, wala hawakupunguza; kama vile ulahidi (kumkana Mungu). Hayo ni upande wa kiitikadi. Ama upande wa kimadili wastani wake ni, kwa kuwa amewachanganyia mambo ya kiroho na ya kimwili katika mafunzo yake na maelekezo yake - sio ubahili wa kiroho wala ubadhirifu wa kimaada, bali kuna uwiano kati yao.

Baadhi wameifanya kauli hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Tumewajaalia ni umma wa wastani", kuwa ni dalili ya hoja ya Ijmai. Lakini hiyo ni kutoa dalili mahali pasipokuwa pake. Kwa sababu haikuja kubainisha Ijmai, kwamba ni hoja au sio hoja.

Wengine wamesema kwamba kauli hii ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) inafa-hamisha kuwa kila Mwislamu ni mwadilifu kwa tabia. Hii pia nayo ni batil kabisa. Kwa sababu uadilifu hauthibiti isipokuwa kwa kujua au kwa ushahidi.

UKAMILIFU NA UWIANO KATIKA UISLAMU.

Binadamu ni mwili uliotokana na mchanga unaokwisha na ni roho inayo-dumu inayotokana na siri ya Mwenyezi Mungu, kama alivyosema: "Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika mambo ya mola wangu." (17:85). Kwa vile vitu viwili hivyo (mwili na roho) vina mahitaji na

6

6

Kaashif2-25.jpgKaashif2-26.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

matakwa ndipo ikaletwa sharia ya Kiislamu kwa ajili ya kutoa maelekezo ya msingi na nidhamu ili visizidiane. Kwa maneno mengine binadamu ni sehemu mbili, kupuuza moja wapo ni kumpuuza binadamu mwenyewe.

Uislamu umekataza utawa na kuiepusha nafsi na maumbile ya kawaida, kama ambavyo umehalalisha starehe za maisha, kama kula, kuvaa vizuri nk.

Atakayeziangalia Aya za Qur'an atakuta kwamba dunia yote imeumbwa kwa ajili ya uhai wa mtu kwa namna inayokubalika kwa wote, lakini wakati huo huo kuipupia kuifanyia hiyana na kuwazuia watu wengine na hiyo dunia ni ufisadi na hatari kwa usalama wa jamii. Riziki bora kabisa katika Uislamu ni ile iliyotolewa jasho.

Anas anasema:

Siku moja tulikuwa na Mtume (saww) safarini wengine wakawa wame-funga na wengine hawakufunga. Tukashuka sehemu fulani ilikuwa ni wakati wa joto. Basi waliofunga wakaanguka wote, ikawa wasiofunga wanawahudumia waliofunga. Mtume (s.a.w.w) akasema.: Wasiofunga leo wamechukua malipo yote.

Huu ndio msingi wa uwiano katika Uislamu. Sio ibada itayozuia kuhangai-ka wala sio ulafi utakayozuia kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu.

Maana ya matamko haya yako wazi na maana ya kiujumla pia iko wazi. Lakini tatizo liko kwenye kuelezea sisi Waislamu ni mashahidi juu ya akina nani? Mtume (s.a.w.w) atakuwa shahidi kesho dhidi ya yule aliye-halifu miongoni mwetu, je sisi tutakuwa mashahidi dhidi ya wasiokuwa Waislamu ambao wamehalifu Kitabu na Sunna?

Kauli zimekuwa nyingi na kugongana juu ya hilo; nami sikupata ya kunit-uliza. Nionavyo mimi ni kwamba Ulama wa Kislamu wanawajibu wa kuu-fikisha ujumbe wa Muhammad (s.a.w.w) kwa watu wawe ni Waislamu au si Waislamu wasiojua au wawe wanajua. Mwenye kutekeleza wajib huu Mtukufu, basi atakuwa shahidi dhidi ya yule aliyemfikishia kuwa hakuya-tumia mafunzo. Na, atakayepuuza wajib huu na asiufikishe, basi

7

7

Kaashif2-27.jpgKaashif2-28.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Muhammad (s.a.w.w) atakuwa shahidi dhidi yake kesho mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amefanya hiyana.

Kwa ufafanuzi zaidi tupige mfano huu: Mtu ana mali na mtoto mdogo, alipohisi kifo chake kiko karibu akamuusia mtu anaye mtegemea kwa dini yake amlee mtoto wake kutokana na mali atakayoiacha. Akitekeleza yule aliyeusiwa na mtoto akafaulu, basi nisawa, lakini mtoto akifanya uasi na akakataa mfunzo, basi aliyeusiwa atakuwa shahidi dhidi ya mtoto na kama aliyeusiwa ndiye aliyezembea, basi mzazi atakuwa shahidi dhidi ya aliyeusiwa.

Vilevile sisi Ulama tuna majukumu makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ya kufikisha mwito wa Kiislamu kwa watu wenye dini mbali mbali kwa hekima na mawaidha mazuri. Na atakayezembea wajib huu kesho atashuhudiwa na bwana wa viumbe na atahukumiwa. Hii ni ikiwa amepuuza, sikwambii ikiwa yeye ndiye sababu ya kupatikana shaka katika watu wake?

Na hatukukifanya Qibla ulichokuwa nacho ila tupate kumjua yule anayemfuata Mtume na yule atakayegeuka akarudi nyuma.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwamrisha Mtume wake kugeuza Qibla baadhi ya watu walianza kutia shaka na kusema: mara huku na kesho kule. Na Mayahudi nao wakachukua fursa ya kuwatia shaka wajinga kuhusu Mtume. Hao Mayahudi walikuwa wamekuwa na wataendelea kuwa ni watu wa fitina na uvunjaji; wenye vitimbi na hadaha. Wanatengeneza matatizo na kumwekea vikwazo kila mwenye Ikhlas na wanajaribu kuzigeuza jamii kuzipeleka kwenye matatizo. Ndio tabia na maumbile yao.

Ndivyo ilivyo, mara nyingi maadui wa haki wanawatumia wadhaifu wa akili na kuwafanya ni chombo cha kufanya vitimbi, uharibifu na vurugu.

Imam Ali amewaelezea kwa ufasaha zaidi aliposema: Ni wanyama wasiokuwa na mchungaji wanamfuata kila atakayewapigia kelele ni (ben-dera) wanafuata upepo, hawakupata mwanga wa elimu wala hawana cha kutegemea."

Mwenyezi Mungu alimpa habari Mtume wake Mtukufu kwamba wale wanaotia shaka si waumini halisi na tumewapatia mtihani huu ili ufichuke

Kaashif2-29.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ukweli kwako na kwa wengine.

Na kwa hakika lilikuwa ni jambo gumu, ispokuwa kwa wale aliowaongoza Mwenyezi Mungu. Ambao ni wenye imani halisi sio imani ya kuazima.

Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua kila kitu kabla ya kutokea, sasa kuna wajihi gani kusema: ili tumjue anayemfuata Mtume?

Jibu: Lengo hapa ni kumdhihirisha mtiifu na asiyekua mtiifu na libainike hilo mbele za watu.

Wafasiri wengi wamesema kwamba Mwenyezi Mungu ana elimu mbili ya kujua kitu kabla ya kuwa ambayo ni elimu ya ghaib na elimu baada ya kuwa, ambayo ni elimu ya ushahidi na ndiyo iliyokusudiwa katika Aya hii, yaani Mwenyezi Mungu ametaka kujua baada ya kuwa, kama alivyo jua kabla ya kuwa.

Huku ni kucheza na maneno tu. Elimu ya Mwenyezi Mungu ni moja, elimu ya ghaib ndiyo hiyo hiyo elimu ya ushahidi .

Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kupoteza imani yenu. Hakika Mwenyezi Mungu kwa watu ni mpole mwenye kurehemu

Hii ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wale wenye uthabiti katika imani yao kwa Mtume (s.a.w.w) kwa shida na raha. Wanafuata amri yake na wanaacha makatazo yake.

Wafasiri wengi wamesema kuwa sababu ya kushuka Aya hii ni kwamba baadhi ya masahaba waliswali na Mtume kibla cha kwanza na wakafa kabla ya kugeuzwa kibla cha pili, akaulizwa Mtume kuhusu swala yao, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hiyo.

Sisi hatutegemei mapokezi ya sababu za kushuka Aya isipokuwa machache tuliyo na yakini nayo. Kwa sababu maulamaa hawakujishughul-isha sana na usahihi wake, kama walivyofanya kwa mapokezi ya hukumu.

9

9

Kaashif2-30.jpgKaashif2-31.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

144. Kwa hakika tunakuona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni;                    basi

tutakuelekeza Qibla ukipen-dacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu (Al-Ka'aba). Na popote mlipo geuzeni nyuso zenu upande huo. Na hakika wale waliopewa Kitabu wanajua kwamba huo ni haki itokayo kwa Mola wao; na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda.

145. Na hao waliopewa Kitabu hata ukawaletea hoja za kila namna, hawatafuata Qibla chako; na wala wewe si mwenye kufuata Qibla chao, wala baadhi yao si wenye kufuata Qibla cha wengine. Na kama ukifuata mata-manio yao baada ya kuku-fikia elimu, utakuwa miongo-ni mwa madhalimu.

Kaashif2-32.jpg

10

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

HAKIKA TUNAKUONA UNAVYOGEUZA USO WAKO

Aya 144-145:

MAANA

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Imepokewa kutoka kwa Imam Jaffar Sadiq (a.s.) kwamba: Kiligeuka Qibla baada ya kuswali Mtume (s.a.w.w), Makka kwa muda wa miaka 13 akielekea Baitul Maqdis. Na baada ya kuhamia Madina, aliswali miezi saba, kisha Mwenyezi Mungu akamwelekeza Al Ka'aba."

Sababu hiyo ni kwamba Mayahudi walikuwa wakimkejeli Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumwambia: "Wewe unatufuata sisi, unaswali kwenye Qibla chetu." Mtume akaingiwa na majonzi makubwa, akatoka usiku akawaana angalia pambizoni mwa mbingu, akingojea amri ya Mwenyezi Mungu kuhusu jambo hilo. Kulipokucha akaswali swala ya Adhuhuri katika msikiti wa Bani Salim, alipomaliza rakaa mbili alishukiwa na Jibril akamshi-ka na kumgeuza upande wa Al-Ka'aba, akamteremshia Aya hii: "Kwa haki-ka tunakuona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni", Mtume akaswali rakaa mbili kuelekea Baitul Maqdis na rakaa mbili kuelekea Al- Ka'aba.

Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti mtakatifu (Al Ka'aba).

Ameusifu Msikiti kwa utakatifu, ambapo ni wajibu kuutakasa na ni hara-mu kuuvunjia heshima. Al-Ka'aba ni sehemu ya Masjidul Haram (Msikiti Mtakatifu) nao ni sehemu ya Haram ambayo inakusanya Makka na mipa-ka yake, kama ilivyoelezwa katika vitabu vya Fiqh, katika mlango wa Hijja, katika masuala ya Ihram na kuwinda katika Haram.

Yanayojulikana katika Qur'an ni kwamba amri ya wajib yoyote ya kisharia inayoelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu inawahusu watu wote, mfano:

11

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-33.jpg

"Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana na mwanzo wa usiku." (11:114).

Haiwezekani kuwa amri ya wajib inahusika na yeye Mtume tu, ila kama kuna kitu kinachofahamisha hilo; kama Aya hii:

"Na katika usiku swali Tahajjud. (17:79).

Hiyo niSunna kwa ajili yako..."

Neno 'kwa ajili yako' linafahamisha kwamba taklifa hii haimuhusu mtu mwingine isipokuwa yeye.

Vile vile njia ya Qur'an ni kwamba taklifa zenye kuelekezwa kwa watu na Muhammad (s.a.w.w) pia huwamo, bila ya kuwako na tofauti hata ndogo ya mwelekezo huo kati yake na mwingine. Kwa hivyo umma unaingia katika kauli yake Mwenyezi Mungu: Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu (Al-Ka'aba).

Na popote mlipo geuzeni nyuso zenu upande huo.

Yaani popote mnapokuwa baharini au bara, kwenye tambarare au maja-balini, Mashariki au Magharibi, ni juu yenu kuelekea Msikiti Mtukufu kwa sehemu ya mbele ya mwili, wala haijuzu kuupa mgongo katika swala au kuuelekea kwa upande wa kuume au kushoto, nk.

Kutokana na hali hiyo Qibla kinahitalifiana kwa kuhitalifiana miji. Kwa ajili hii Waislamu wamejishughulisha sana na suala la Qibla na wakaweka elimu mahsus kwa jina la elimu ya "Qibla", Kinyume na Wakristo ambao wanalazimiana na upande wa Mashariki daima na Mayahudi nao ni upande wa Magharibi popote walipo, hata kama hilo litalazimisha kuipa mgongo Baitul Maqdis.

1

Swala za Sunna za usiku wa manane.

12

Kaashif2-34.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Unaweza kuuliza: Ikiwa Umma unaingia katika msemo unaoelekezwa kwa Mtume na msemo unaolekezwa kwa Umma unamhusu Mtume; sasa kwa nini kukusanyika misemo inayoelekea sehemu mbili katika Aya moja na maudhui moja tena bila ya kuwako kitenganisho. Yaani Mwenyezi Mungu anasema elekeza uso wako- ewe Muhammad - upande wa Msikiti Mtakatifu, na popote mtakapokuwa - enyi Waislamu - elekezeni nyuso zenu upande uliko Msikiti Mtakatifu.

Jibu: Kugeuka Qibla ni tukio kubwa katika Uislamu na kulikuja kutokana na raghba ya Mtume (s.a.w.w). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akataka kumbainishia hilo, na kulitilia mkazo kwa kulikariri.

Zaidi ya hayo ni kuwa kwa asili taklifa hiyo ni ya Muhammad (s.a.w.w), kwa sababu imekuja kwa raghba yake na kufuatilia umma wake.

NI WAJIB WAKATI GANI KUELEKEA QIBLA?

Al Ka'aba ni Qibla kwa aliye ndani ya Msikiti Mtakatifu ambao Al Ka'aba imo ndani yake, Msikiti ni Qibla kwa watu wa Haram; yaani watu wa Makka na pembeni mwake na Haram au upande wake ni Qibla kwa watu wa Mashariki na Magharibi.

Ni wajibu kuelekea Qibla katika swala za kila siku, swala ya ihitiyat, mafungu yaliyosahauliwa katika swala na sijda mbili za kusahau. Vile vile ni wajibu kuelekea Qibla kwa ajili ya swala yoyote ya wajibu, ikiwemo Swala ya tawaf, na Swala ya kumswalia maiti. Pia ni wajibu kumwelekeza Qibla mtu aliye katika hali ya kukata roho na wakati wa kumzika, na wakati wa kumchinja mnyama.

Ama katika swala za sunna ni wajibu kuelekea Qibla katika hali ya utulivu tu, na wala sio wajibu katika hali ya kutembea na kupanda chombo cha kusafiria.

13

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

WATU WA QIBLA

Watu wa Qibla, watu wa Qur'an, watu wa shahada mbili na Waislamu, yote hiyo ni misamiati iliyo katika maana moja. Ama lile jina la 'Wafuasi wa Muhammad' (Mohammedan), ni jina tulilobandikwa na maadui wa Uislamu, wakiwa na maana kwamba sisi ni wafuasi wa mtu na wala sio wa dini ya Mwenyezi Mungu; kama Mabudha ambao ni wafuasi wa Budha na Wazaradashti ambao ni wafuasi wa Zaradasht.

Kwa vyovyote vile lengo la kifungu hiki ni kuzindua kwamba umma wa Kiislamu, pamoja na kutofautiana miji yake, rangi na lugha, lakini unaku-sanywa na kuwa pamoja na misingi ya aina moja, ambayo ni ghali na yenye thamani zaidi kuliko uhai. Kwa sababu Waislamu wanadharau maisha kwa ajili ya misingi hiyo na wala hawawezi kuidharau misingi hiyo kwa ajili ya maisha. Misingi hiyo ni pamoja kumwamini Mwenyezi Mungu na kitabu chake, kumwamini Muhammad (s.a.w.w) na sera yake na kuswali kwa kuelekea Qibla. Basi mwenye kumkufurisha mwenye kuswali kwa kuelekea Qibla na akamtoa katika idadi ya Waislamu, atakuwa amei-dhoofisha nguvu ya Uislamu na atakuwa amelichana jina la Waislamu, na kusaidia maadui wa dini, atake asitake.

Na hakika wale waliopewa kitabu wanajua kwamba huo ni haki itokayo kwa Mola wao.

Makusudio ya waliopewa kitabu ni Mayahudi na Wakristo, na wala sio Mayahudi peke yao, kama ilivyosemwa. Kwa sababu neno linaenea, na wala hakuna dalili ya kuhusisha.

Wafasiri wametofautiana katika dhamiri ya neno Annahul-haqq kwamba je ni huo Msikiti au ni huyo Mtume? Sababu ya kutofautiana ni kwamba Mwenyezi Mungu nyuma amemtaja Mtume kwa kusema: "Kwa hakika tunakuona unavyogeuza geuza uso wako" na vile vile ametaja Msikiti Mtakatifu.

Sisi tuko katika upande wa wanaosema kuwa dhamiri inarudia Msikiti kwa sababu ndilo tamko la karibu zaidi, na dhamiri inarudia tamko la karibu zaidi.

14

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kwa hiyo maana yanakuwa, watu waliopewa kitabu wanajua kabisa kwamba Ibrahim (a.s.) ni baba wa Mitume na ni mkubwa wao ambaye alijenga Nyumba Tukufu (Al Ka'aba), lakini wao wameikataa kwa vile tu, iko mikononi mwa Waarabu ambao wanaitumikia na kuihami. Lau isingelikuwa mikononi mwa Waarabu, Mayahudi wangelikuwa wa kwanza kuitukuza na wangeliiheshimu sana.

Na hao waliopewa kitabu hata ukiwaletea hoja za kila namna hawata-fuata Qibla chako.

Yaani hawafuati mila yako, sembuse kufuata Qibla chao. Nao hawana hoja yoyote isipokuwa ujinga na ukaidi.

Na wala wewe si mwenye kufuata Qibla chao.

Huenda baadhi ya watu wa Kitab walitaraji kuwa Mtume (s.a.w.w) ataru-dia Qibla alichokielekea kwanza, ndipo Mwenyezi Mungu akawakatisha tamaa kabisa kwa kauli yake hiyo; kama alivyomkatisha tamaa Muhammad (s.a.w.w) kuwa wao hawatafuata Qibla chake.

Wala baadhi yao si wenye kufuata Qibla cha wengine.

Mayahudi wanaswali kuelekea Magharibi na Wakristo wanaelekea Mashariki, wala kundi moja haliwezi kulifuata kundi jingine, vipi wataweza kufuata Qibla chako ewe Muhammad? Bali hata hao Mayahudi wanatofautiana; kama walivyo Wakristo. Mauaji yaliyotokea kati ya Wakatoliki na Waprotestant, hayana mfano wa fedheha yake katika zama zote.

Na kama ukifuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu, utakuwa miongoni mwa madhalimu.

Ni muhali kuwa Mtume afuate matamanio yao, kwa sababu yeye ni masum (mwenye kuhifadhiwa na madhambi), lakini lengo la makatazo haya ni kumpa nguvu Mtume katika kuamiliana kwake na Mayahudi na kusimama nao imara, na kwamba hakuna heri yoyote ya kupatana nao wala hakuna,tumaini lolote kwao. Haliwezi kufaa jaribio lolote la kuwazuia na vitimbi na ufisadi wao. Kwa sababu wao wana maumbile ya shari.

15

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kupinga haki na kumfanyia uovu anayewafanyia wema. Yamekwishaelezwa maelezo zaidi katika kufasiri Aya ya 120.

UISLAMU NA WATU WENYE UPENDELEO NA DINI ZAO

Ni jambo lenye kuingia akilini kwamba wataalamu wanaweza kuhitilafi-ana katika aina yoyote ya masuala yasiyokuwa ya kidini. Baada ya kukumbushana na kudurusi, huafikiana katika lile walilohitilafiana. Hilo limekwishatokea.

Ama wakihitalifiana katika masuala ya dini mbali mbali, basi kuafikiana kwao ni muhali, hata kama zitakuwepo dalili elfu. Imethibiti kwa wataalamu wa elimu ya saikolojia, kwamba watu kubadili tabia yao ni rahisi zaidi tena sana kuliko kubadili dini yao. Hilo ni kwamba watu wengi hutegemea dini za mababa na mababu. Hakuna dini iliyojulikana kukataza kufuata mababu isipokuwa Uislamu ambao umetegemea akili peke yake katika kuthibitisha misingi yake. Mwenye kuangalia Aya za Qur'an na Hadith za Mtume ataziona zimetilia umuhimu kufuatilia akili kwa kiasi kile kile zinavyoitilia umuhimu kumwamini Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Imani hiyo haiepukani kabisa na nuru ya akili timamu katika kuongoka kwake.

146. Wale tuliowapa Kitabu wanamjua yeye kama wanavyowajua watoto wao. Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua.

147. Haki ni iliyotoka kwa Mola wako. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka.

Kaashif2-35.jpg

16

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

WANAMJUA KAMA WANAVYOWAJUA WATOTO WAO

Aya 146-147:

MAANA

Wale tuliowapa kitabu wanamjua kama wanavyowajua watoto wao.

Yaani wanavyuoni wengi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanajua kwa usahi-hi na uwazi Utume wa Muhammad (s.a.w.w); kama wanavyowajua watoto wao, kwa namna isiyokuwa na shaka yoyote. Kwa sababu Tawrat na Injil zimetoa bishara ya kuja kwake na zikamtaja kwa sifa zake na alama zake ambazo hazikupatikana kwa mwingine yeyote. Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-36.jpg

"...Wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurat na Injil..." (7:157).

Kaashif2-37.jpg

"Na aliposema Issa bin Maryam: Enyi wana wa Israil! Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katika Tawrat na kutoa bishara ya Mtume atakayekuja baada yangu ambaye jina lake ni Ahmad. Lakini alipowajia kwa hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi." (61:6).

17

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Abdallah bin Salam alikuwa ni mmoja wa maulamaa wa kiyahudi; kisha akasilimu. Miongoni mwa maneno aliyosema ni: "Mimi ninaujua zaidi Utume wa Muhammad kuliko ninavyomjua mwanangu." Alipoulizwa kwa nini, alisema: "Mimi sitii shaka kwamba Muhammad ni Mtume, lakini mtoto wangu, pengine mama yake amefanya hiyana."

Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua.

Ndio! wanaficha, hata kama wangeliona jina la Muhammad katika Lauhul Mahfudh, kwa sababu ya kupupia uongozi wa duniani na maslahi ya kibi-nafsi. Inadi hii ya kuficha haki haihusiki na Mayahudi na Wakristo tu. Kwani sababu ya kuficha haki ni ya kijumla. Tumekwisha waona baadhi ya Masheikh wanakana sifa za wenzao kwa sababu ya chuki na hasadi tu.

Haki ni iliyotoka kwa Mola wako, basi usiwe miongoni mwa wanao-fanya shaka.

Mtume (s.a.w.w) hawezi kutia shaka yale yaliyotoka kwa Mola wake na ni muhali kuyatilia shaka; na Mwenyezi Mungu anajua kuwa Mtume wake Mtukufu hawezi kutia shaka. Lengo la Aya hii ni kubainisha kwamba aliy-omteremshia Muhammad hayana shaka wala matatizo yoyote kabisa. Mtu akiyakanusha na kuyapinga basi atakuwa anafanya hivyo kwa inadi na ukaidi tu.

MIMI NA MHUBIRI

Tarehe 15-7-1963 alinitembelea mtaalamu wa mambo ya nchi za mashari-ki Mkristo kutoka Italia ambaye alikuwa akizungumza lugha ya Kiarabu vizuri. Basi tukawa na mjadala kwa mdomo na kwa maandishi. Miongoni mwa aliyosema ni "Qur'an inakiri wazi wazi kuhusu Injil, kwa nini Waislamu wanaikana?" Nikamjibu kuwa Qur'an inakiri Injil iliyobashiri Utume wa Muhammad (s.a.w.w); kama ilivyosema:

Kaashif2-38.jpg

"...Na mwenye kutoa bishara ya Mtume atakayekuja baada yangu ambaye jina lake ni Ahmad..." (61:6).

18

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

"...Wanamuona ameandikwa kwao katika Tawrat na Injil..." (7:157). Kisha Qur'an inaendelea kusema:

Kaashif2-39.jpg

"Hakika mfano wa Issa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia 'kuwa' basi akawa." (3:59).

Injil yenu inasema Issa ni Mungu, sasa vipi mnatutaka tuiamini na wakati huo huo tuiamini Qur'an?

Ikiwa Wakristo wanakataa kupingana na kukosana katika hukumu ya akili tu, na kukubali kuwa akili inaweza kupingana na kutoafikiana katika dini na itikadi, basi Waislamu wanaliona hilo ni muhali; haliwezekani kiakili na kidini na katika kila kitu. Kwa sababu misingi ya dini kwao inakuwa ndani ya akili tu.

148. Na kila mmoja ana mwelekeo anaouelekea. Basi shindaneni kufanya mema. Popote mtakapo-kuwa, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Kaashif2-40.jpg

19

Kaashif2-41.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

149. Na popote uendapo utakako kuwa elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu; na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako. Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoy-atenda.

150. Na popote utakapotoka utakokuwa elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu, na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande (uliko msikiti) huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale waliodhulu-mu miongoni mwao. Basi msiwaogope, niogopeni Mimi, ili niwatimizie neema Zangu na ili mpate kuongo-ka.

151. Kama tulivyomleta Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anayewasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima na kuwafundisha mliyokuwa hamyajui.

Kaashif2-42.jpg

20

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-43.jpg

152. Basi                 nikumbukeni

nitawakumbuka,              na

nishukuruni wala msinikufu-ru.

KILA UMMA ULIKUWA NA QIBLA CHAKE Aya ya 148-152:

MAANA

Na kila mmoja ana mwelekeo anaoulekea.

Alipotaja Mwenyezi Mungu Qibla ambacho amewaamrisha Waislamu kukielekea ambacho ni Al Ka'aba, na akataja kuendelea kwa Mayahudi na Manaswara kuelekea mielekeo yao, alibainisha kuwa siri ya kung'ang'ania huku kwamba kila umma ulikuwa na Qibla chake uliojichagulia kuelekea na wala haukiachi, hata kama ubaya wa mwelekeo wenyewe uko wazi kama jua. Kwa hiyo kauli Yake hii inafanana na kauli Yake:

Kaashif2-44.jpg

"...Kila kikundi kinafurahia kilicho nacho" (30:32).

Hayo ndiyo niliyoyafahamu kutokana na dhahiri ya tamko. Wafasiri wameleta kauli nyingi katika Aya hii; mwenye Majmau ametaja nne.

Basi shindaneni kufanya mema. Popote mtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja, hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

21

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Yaani achaneni na watu wa Kitab na washirikina walio wakaidi, na mfanye amali njema. Kwani marejeo yenu kesho ni kwake Mwenyezi Mungu, ambapo atalipwa thawabu mwenye haki na mwenye kufanya wema na kuadhibiwa mwenye batili mtenda maovu. Kama wanavyosema wafasiri maana ya: "Popote mtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamo-ja" ni ahadi ya thawabu kwa watiifu na kiaga cha adhabu kwa waasi. Ama kusema kwake: "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu" ni dalili na sababu ya kuwezekana kufufuliwa viumbe baada ya mauti.

Na popote uendapo elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu hapa amekariri kuelekea Msikiti Mtakatifu mara tatu na katika Aya ya 149 mara mbili; yaani amekariri mara tano mfululizo?

Jibu: Mwenye Majmaul-Bayan ametaja kauli tatu na Razi ameleta tano. Miongoni mwa kauli hizo ni lile jibu lililozoeleka linalorithiwa ambalo ni, kutilia mkazo na umuhimu. Nafsi yangu haikutulia kabisa katika kauli hizo. Na mimi sina chochote cha kusema isipokuwa huenda kukariri huku hapa ni kutokana na jambo lililohusu wakati huo ambalo hatulijui. Kuna mambo mengi ambayo hayaingii katika udhibiti na hisabu.

Inajulikana wazi kuwa mapokezi ya Aya na sababu zake yako ya kiujumla na mahsusi, na haifai kwa yeyote kutafsiri au kuleta taawili, kwa kutege-mea dhana bila ya kupata asili yake yoyote.

Ili watu wasiwe na hoja juu yenu.

Wafasiri wengi wamesema kuwa Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akiswali kuelekea Baitil Maqdis; Washirikina na Waarabu wakasema: "Vipi Muhammad anadai kwamba yeye yuko kwenye dini ya Ibrahim, na wala haswali kuelekea Al Ka'aba aliyokuwa akiswali Ibrahim na Ismail?" Na watu wa Kitab wakasema "Yaliyo katika Vitabu vyetu ni kwamba Mtume atakayeletwa katika kizazi cha Ismail ataswali kuelekea Al Ka'aba na wala sio Baitul Maqdis, sasa vipi tunaweza kuukubali Utume wa Muhammad. Kwa

22

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

hiyo wakaifanya kuwa hoja, wanayoitumia kwa dhana yao. Mwenyezi Mungu akambadilishia Qibla kuelekea Al Ka'aba na akaifanya ndio Qibla cha kudumu kwa Mtume na Waislamu wote mpaka siku ya malipo, ili hawa na wengine wasibakiwe na hoja yoyote.

Dhahiri ya jumla inafahamisha kwamba kuswali kuelekea Al Ka'aba kunavunja hoja ya wapinzani. Ama kuwa ni kina nani hao wapinzani, Aya haikubainisha. Inawezekana kuwa njia ya kukata hoja ya wapinzani ni kuwa Al Ka'aba imejengwa na Ibrahim (a.s.) na akaswali hapo. Hilo ni lenye kuafikiwa na wote na Muhammad atafuata mwendo wa Ibrahim

Isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao.

Yaani hakuna hoja yoyote juu yako ukiswali, isipokuwa kwa mpinzani asiye na haki ambaye hategemei dalili za kiakili katika upinzani wake wala uongozi wa kidini isipokuwa kung'ang'ania, na ukaidi.

Basi msiwaogope, niogopeni Mimi.

Yaani msiogope lawama katika haki, Mimi pekee ndiye ninayewamilikia manufaa na madhara. Ibnul Arabi katika tafsiri yake anasema. Maana ya niogopeni ni, jueni Utukufu Wangu ili makafiri wasijifanye watukufu kwenu.

Amirul Muminin (a.s.) anasema: "Amekuwa mkubwa Muumbaji katika nafsi zao akawa mdogo asiyekuwa yeye katika macho yao."

Na ili niwatimizie neema zangu na ili mpate kuongoka.

Yaani nimewaneemesha kwa Uislamu na nimewatimizia neema kwa kuwa-pa Qibla chenu kilichowafanyia umoja na kuwakusanya na kinachoeleke-wa na watu wa mataifa mbali mbali ya pembe zote za dunia, yenye maka-bila na lugha mbali mbali.

23

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

KATIBA YA UISLAMU

Mtaalamu mmoja anasema kuwa katiba ya Uislamu ina vipengele vitatu Mwenyezi Mungu mmoja, Kitabu kimoja na Qibla kimoja. Waislamu hukusanyika kutoka pembe zote za dunia kila mwaka ili wamwabudu Mwenyezi Mungu mmoja kwa sharia hiyo moja kwenye nchi mmoja, nchi ya mji wa kiroho. Hivi ndivyo ulivyokuwa umoja wa itikadi, sharia na mji, ili wakumbuke Waislamu kwamba wao hata kama wakitofautiana miji, lugha, rangi na nasaba, lakini wanakuwa wamoja kwa dini, wanaabudu Mwenyezi Mungu mmoja na ni wananchi wa nchi mmoja.

Kama tulivyomleta Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anayewa-somea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima na kuwafundisha mliyokuwa hamyajui.

Wanavyuoni wana maneno mengi na marefu katika maana ya neno hekima. Tunavyofahamu sisi ni kuwa kila kinachowekwa mahali pake pana-postahili, kiwe ni kitendo au kauli, basi ni hekima.

Hali yoyote iwayo, maana ya jumla ya Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaneemesha Waarabu kwa Qibla; kama alivyowa-neemesha kwa Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni katika wao na anatokana na wao. Amewapa umbo jipya; akawatwaharisha na uchafu wa shirk na tabia mbaya. Kwa hiyo, kwa fadhila zake, wakawa ni watu wa dini na sharia ya Mwenyezi Mungu ambayo misingi yake ni uadilifu na usawa; kama ambavyo wamekuwa na dola iliyopanuka, mpaka lugha yao ikawa kubwa na ikaenea kwa sababu ya Qur'an na fasihi yake.

Hapana mwenye kutia shaka kwamba lau si Muhammad na kizazi cha Muhammad, Waarabu wasingelikuwa na historia wala turathi zozote; wasingekuwa na chochote zaidi ya kuabudu masanamu, ujinga na kuwazi-ka watoto wa kike wakiwa hai, ili kuepuka gharama za kuwalisha. Bali Muhammad (s.a.w.w), Mwarabu, ni neema kubwa juu ya watu wote. Kwa sababu yake, watu wamepiga hatua za haraka katika nyanja za elimu na maendeleo. Uhakika huu wameukiri na kuusajili wataalamu wa

24

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kimagharibi wale wasiokuwa na ubaguzi, na tumeyanakili baadhi katika kitabu Al-Islam Wal-aql (Uislamu na Akili).

Kwa ajili ya neema hiyo aliyowaneemesha Waarabu, ndio Mwenyezi Mungu akawataka wamkumbuke na kumshukuru na akahadharisha wasije wakaikufuru neema na hisani, kwa kusema:

Basi nikumbukeni nitawakumbuka na nishukuruni wala msinikufuru.

Yaani nikumbukeni kwa utii nami nitawakumbuka kwa malipo na thawabu. Na mnishukuru juu ya neema ya Uislamu na Utume kwa Muhammad ambaye anatokana na nyinyi wala msinikufuru. Mahali pengine Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-45.jpg

"...Kama mkishukuru nitawazidishia, na kama mkikufuru basi adhabu yangu ni kali sana." (14:7).

Amirul Mumini Ali (a.s.) alisema: "Mwenyezi Mungu hawezi kufungua mlango wa shukrani na akafunga wa malipo." Anaendelea kusema: "Mkumbukeni sana Mwenyezi Mungu, kwani huo ndio ukumbusho mzuri, na kuweni na raghba katika aliyowaahidi wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwani ahadi Yake ni ya kweli sana."

KUMSHUKURU MNEEMESHAJI

Moja kwa moja akili inafahamu kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ni wajibu kwa kila aliye baleghe mwenye akili, hata kama isingeshuka Aya yoyote au kuja Hadith yoyote ya kuwajibisha kushukuru. Kwani Yeye Mtukufu ndiye Muumbaji Mwenye kuruzuku.

25

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Maana ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya kuitakidi kwamba Yeye ndiye mwanzilishi na kwamba Yeye ni muweza wa kila kitu ni kutii amri Zake na makatazo Yake na kutegemeza mambo kwake peke Yake.

Hayo ni kwa upande wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ama mtu akimfanyia wema mtu kama yeye, je inapasa, yule aliyefanyiwa wema kumshukuru aliyemfanyia wema, kiasi ambacho kama hakumshukuru kwa namna fulani atakuwa ni mwasi mwenye kustahiki adhabu?

Hapana mwenye kutia shaka kwamba kumshukuru aliyekutendea wema ni jambo zuri, bali hiyo ni alama ya watu wema. Ama kuwa ni wajibu au la, hakuna dalili juu yake. Kwa hiyo kila habari iliyokuja kuhusu kumshukuru mwenye kutoa neema asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Mtume au Ahlul Bait wake, ni pendekezo tu ya kuwa ni vizuri; kama alivyosema Ali (a.s.): "Ukiwa unammudu adui yako, basi ufanye msamaha ndio shukrani ya uwezo huo wa kummudu".

Kumsamehe aliyekufanyia ubaya sio wajib, lakini ni Sunna kwa Ijmai. Ama msemo unaosemwa sana: "Asiyeshukuru kiumbe ndio hamshukuru Muumba", hiyo ni hukumu ya kimaadili tu, siyo ya lazima.

Hata hivyo kukanusha neema na kumwambia aliyekufanyia wema: "Hukufanya wema" ni haramu, kwa sababu ni uwongo; na kumfanyia uovu ndio haramu kabisa, kwa sababu uovu ni haramu kwa dhati yake, hata kwa mtu asiyekufanyia wema. Lakini pamoja na hayo wajibu wa kushukuru ni jambo jingine na uharamu wa uwongo na uovu ni jambo jingine.

26

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

153. Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na swala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanao-subiri.

154. Wala msiseme kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui.

155. Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wa mali na wa nafsi na wa matunda. Na wape bishara wanaosubiri.

156. Ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na Kwake Yeye tutarejea.

157. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema, na hao ndio wenye kuongoka.

Kaashif2-46.jpg

27

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

TAKENI MSAADA KWA SUBIRA

Aya 153-157: SUBIRA

Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na swala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.

Mwenye Tafsiri ya Al-Manar anasema kuwa Subira (uvumilivu) katika Qur'an imetajwa mara sabini. Hiyo inafahamisha umuhimu wake, na Mwenyezi Mungu ameijaalia ni kitu cha kuusiana katika Sura Al Asr kwa kuikutanisha na haki, kwani mwenye kuilingania haki hana budi kuwa nayo."

Mwenye Bahrul Muhit ameiweka mbali sana aliposema: "Subira na swala ni nguzo mbili za Uislamu" Ameghafilika na Hadith inayosema: "Umejengwa Uislamu juu ya mambo matano: Kushuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga mwezi wa Ramadhan na kuhiji Makka kwa mwenye kuweza njia ya kuendea." Subira haimo katika nguzo hizo. Pia ameghafilika kuwa kuna taklifa za lazima ambazo Mukallaf anatakiwa kuzifanya na ataadhibiwa kwa kuziacha; kama, swala kulipa deni, n.k.

Na kuna taklifa nyingine ambazo ni za kimwongozo, zimekuja kinasaha, zinafanana na amri, lakini mukallaf hawezi kuadhibiwa kwa kuziacha; kama usafi, kuosha mikono kabla ya kula, kukatazwa kushiba sana, n.k. Sasa yako wapi haya na nguzo za dini, ambazo mwenye kuziacha anakuwa ametoka katika dini?

Kisha subira haisifiwi hiyo yenyewe hasa, isipokuwa inasifiwa ikiwa ni nyenzo ya kufikilia jambo kuu; kama subira katika jihad takatifu, subira juu ya ufukara na uhitaji, subira kwa ajili ya kuipata elimu na subira juu ya matatizo ya familia na kulea watoto.

28

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Vile vile subira juu ya kumwokoa mwenye kudhulumiwa, subira juu ya kauli ya mtu mpumbavu kwa kukinga shari, au kufanya subira kwa kumkosa mpenzi asiyesahaulika. Kwani kuendelea kufazaika ni kuzidisha msiba; kama alivyosema Amirul Muminin Ali (a.s.): "Mwenye kuyakuza masaibu madogo, Mwenyezi Mungu humwingiza kwenye makubwa."

Bazar Jamhar aliulizwa: "Kwa nini ewe mfalme mwenye hekima husiki-tiki kwa yaliyokupita wala hufurahi kwa yaliyopo?" Akasema: "Yaliyopita hayawezi kufutika kwa majonzi wala yaliyopo hayawezi kudu-mu kwa furaha." Mwingine alisema: "Siwezi kusema kitu kilichokwisha kuwa na tamani kisingekuwa au ambacho hakikuwa natamani kingekuwa.

Mara nyingine subira huwa mbaya; kama kusubiri juu ya njaa na uwezo wa kufanya kazi upo, na kusubiri juu ya ukandamizwaji. Katika hali hii subira nzuri ni kumkabili dhalimu.

Unaweza kuuliza, kuna uhusiano gani kati ya swala na subira mpaka zikakutanishwa pamoja katika Aya?

Jibu: Maana ya subira ni kutulizana moyo ingawaje una machungu. Hiyo inahitajia kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuamini kuwa Yeye "Yu pamoja na wenye kusubiri". Hakuna mwenye shaka kwamba swala inatil-ia mkazo mategemeo haya na ni hakikisho la imani hii, kuongezea kwamba kumwomba Mwenyezi Mungu kunapunguza machungu ya masaibu.

Wala msiseme kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai, lakini nyinyi hamtambui.

Mfano wa Aya hii ni kama nyingine isemayo:

"Wala usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu

Kaashif2-47.jpg

kuwa ni wafu, bali wa hai wanaruzukiwa kwa Mola wao." (3:169). Inajulikana kuwa kila anayefariki hurejea kwa Mola wake, awe mwema au

29

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

mwovu, shahidi au asiyekuwa shahidi; isipokuwa kwamba mwema anaon-doka kwenye maisha ya chini kwenda kwenye maisha ya juu na mwovu inakuwa kinyume chake.

Hapa imehusishwa kutajwa shahidi; ama ni kwa kueleza cheo chake mbele za Mwenyezi Mungu kwa kuhimiza ushahidi; au ni kwa kutokana na yaliy-onakiliwa kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Aya ilishuka kwa sababu ya waliouliwa katika vita vya Badr ambao ni Muhajirin kumi na nne na Ansar wanane; ikasemwa ameuawa fulani na fulani; ndipo ikashuka Aya hii. Haya hayako mbali, kwani kauli ya Mwenyezi Mungu: Msiwaite wafu, inafahamiisha hilo.

Vyovyote iwavyo, ambalo tunapaswa kuamini ni kwamba mwenye kufa shahidi kwa kuupigania Uislamu au kitu chochote kinachofungamana na haki, uadilifu na utu, atakuwa anahama kutoka ulimwengu unaoonekana kwenda kwenye ulimwengu usioonekana na huko atakuwa na maisha mema. Na kwamba yeye anatofautiana na aliyekufa kifo cha kawaida. Amirul Muminin anasema: "Naapa kwa yule ambaye nafsi ya mtoto wa Abu Twalib iko mikononi mwake, kupigwa mapigo elfu ya panga ni bora kwangu kuliko kufa kitandani."

Ama hakika ya maisha ya shahidi baada ya mauti na kuhusu riziki anay-oneemeshwa ni jambo tusilolijua na wala hatuna haja ya kulifanyia utafiti. Kwa sababu ni jambo tusilokalifishwa kulijua.

THAMANI YA PEPO

Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wa mali na wa nafsi na wa matunda. Na wapashe habari njema wanao-subiri.

Yeyote anayefuata haki ni lazima aigharimie kwa nafsi yake, watu wake au mali yake; na kila haki inavyokuwa kubwa, ndivyo gharama inavyokuwa kubwa, lau kama si hivyo wanaopigania haki wasingelikuwa na fadhla yoyote; na watu wote wasingelifuata haki. Kwa hali hiyo ndiyo tunapata

30

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

tafsiri ya Hadith hii tukufu: "Misukosuko amepewa mumin . . . na kwam-ba wenye misukosuko zaidi ni Mitume; kisha wanaowafuatia." Vile vile misukosuko ya Mitume inakuja kwa kadiri ya daraja zao. Mtume mtuku-fu (s.a.w.) amesema: "Hakuudhiwa Mtume kama nilivyoudhiwa mimi." Amirul Muminini amesema: "Hakika haki ni nzito lakini nzuri, na batili ni hafifu, lakini mbaya." Inatosha kuwa ni ushahidi kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mnadhani kuwa mtaingia peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa wale

Kaashif2-48.jpg

waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara. . ." (2:214).

Aya hii inafahamisha kuwa pepo haipati isipokuwa mwenye kujitolea mhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kujitolea mhanga hakuwi katika uwanja wa vita vya jihadi na watu wa shirk peke yake, bali machukivu yoyote anayoyavumilia mtu kwa ajili ya kuipigania haki na uadilifu ni kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ni thamani ya pepo; hata kama kupigania kwenyewe ni kwa neno la kumjibu dhalimu kumsaidia mwenye haki.

Baada ya kuingilia kuandika tafsiri, nimekuwa na yakini isiyo na shaka yoyote kwamba hataingia peponi isipokuwa yule aliyeudhiwa na akavumilia kwa subira, ijapokuwa ni ukandamizwaji na balaa katika njia ya haki na uadilifu. Kwa uchache ni kuifunga nafsi yake na yaliyoharamishwa au kufanya juhudi kwa ajili ya mwingine; hata kama ni mzazi au mtoto. Kipimo cha pepo ni kuvumilia mashaka kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu.

Ama kuingia peponi kutokana na "raha mstarehe" ni jambo lililo mbali sana.

Ambao ukiwapata msiba husema: 'Hakika sisi ni wa Mwenyezi

31

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mungu, na kwake Yeye tutarejea.

Maana ya, "hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu", ni kukiri ufalme na utumwa; na maana ya "kwake Yeye tutarejea", ni kukubali ufufuo baada ya mauti.

Kisha kujaribiwa kwa misukosuko ni mtihani ambao unadhihirisha hakika ya mtu. Mumin mwenye akili hayumbishwi na misukosuko; wala hawezi kupayuka payuka na maneno ya ukafiri na ufasiki na ujinga, bali anakuwa na subira; wala misukosuko haiwezi kumwondolea akili yake na imani yake.

Ama mwenye akili na imani dhaifu anatawaliwa na shetani, anafuata mwe-nendo wote wa kufuru na shutuma na hushuka chini kwenye udhalili. Kauli nzuri kuhusu haya ni ile ya bwana wa mashahidi, Hussein bin Ali, siku ya msiba wa Karbala "Watu ni watumwa wa ulimwengu na dini iko kwenye ndimi zao, wanaipeleka kule kwenye maisha yao wakijaribiwa na misukosuko, huwa wachache wenye dini."

Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao, na rehema.

Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni takrima na ni cheo cha juu; na rehema Yake kwa waja wake ni huruma yake kwao na kuwaongoza kwenye heri na kuwaneemesha.

Katika Hadith imeelezwa: "Hakuna Mwislamu yeyote aliyepatwa na masaibu, akakimbilia amri ya Mwenyezi Mungu kwa kusema: 'Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea. Ewe Mola wangu Wewe ndiwe unayeyatoshea masaibu yangu, basi nilipe katika masaibu hayo na unipe badali bora.' isipokuwa Mwenyezi Mungu humlipa na humpa badali bora."

AINA YA MALIPO YA WANAOSUBIRI

Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewapa wenye kusubiri aina nane za malipo na utukufu:

1. Mapenzi: Mwenyezi Mungu anasema:

32

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

"...Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao subiri." (3:146).

Kaashif2-49.jpg

2. Ushindi: Mwenyezi Mungu anasema:

"...Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanao subiri." (2:153).

Kaashif2-50.jpg

3. Ghorofa za peponi: Mwenyezi Mungu anasema:

"Hao ndio watakaolipwa ghorofa kwa kuwa walisubiri." (25:75).

Kaashif2-51.jpg

4. Malipo mengi: Mwenyezi Mugnu anasema:

"Hakika wanaosubiri watapewa ujira wao pasipo hisabu..." (39:10).

5. Bishara: Mwenyezi Mungu anasema: "Na wape bishara wanaosubiri." (2:155).

Kaashif2-52.jpg

6&7. Baraka na rehema: Mwenyezi Mungu anasema:

33

Kaashif2-53.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

"Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema."

Kaashif2-54.jpg

(2:157).

8. Uongofu: Mwenyezi Mungu anasema:

"Na hao ndio wenye kuongoka." (2:157).

Kaashif2-55.jpg

158. Hakika Swafaa na Mar-wa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguuka.                  Na

anayefanya heri, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani (na) Mjuzi.

SWAFA NA MARWA

Aya 158: LUGHA

Swafa na Mar-wa ni vilima viwili vilivyoko Makka karibu na Al Ka'aba. Mahujaji na wanaofanya Umra huenda Saa'y kati ya vilima hivyo.

Kaashif2-56.jpg

34

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

MAANA

Hakika Swafa na Mar-wa ni katika alama za Mwenyezi Mungu.

Ibada ziko namna mbali mbali na wakati mbali mbali. Kwa kuangalia wakati, kuna zile za kila siku ambazo ni swala, na nyingine ni za kila mwaka ambazo ni kufunga Ramadhani na pia iko ya mara moja tu, katika umri nayo ni kuhiji kwa mwenye kuweza.

Hijja ni moja ya nguzo tano zilizojengewa Uislamu, ambazo ni: Shahada mbili, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga Ramadhan na kuhiji Al Ka'aba. Umrah ni ada kama Hijja, lakini katika Umrah hakuna kwenda Arafa, wala kulala Muzdalifa au kutupa mawe Mina. Utakuja ufafanuzi wake Inshaallah katika Aya ya 196 na Sura nyingine zinazozungumzia hilo.

Kwa ujumla ni kwamba aina zote za ibada ikiwemo Hijja hazina nafasi ya kufanyiwa Ijtihadi wala kuelezwa sababu yoyote; isipokuwa inatosha nasi (nukuu) ya Qur'an na Hadith tu na kila ambalo litazidi hayo, Mungu (s.w.t.) hajaliridhia.

Linaloonyeshwa na Aya hii, ni kwamba Swafa na Mar-wa ni sehemu za kufanyiwa ibada kunakoonyeshwa na kauli yake:

Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au kufanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka.

Kuzunguka huku ndiko kunakojulikana kwa jina la Saa'y kati ya Safa na Mar-wa. Ama namna ya kufunya Saa'y na idadi ya mizunguko yake na kuanzia Safa, utakuja ubainifu wake mahali pake Inshaallah.

Unaweza kuuliza kufanya Saa'y kati ya Swafa na Mar-wa katika Hijja ni wajibu kwa Ijmai pamoja na kuwa ibara ya "Si kosa" inafahamisha kufaa jambo hilo na wala sio lazima na kwamba hakuna dhambi kuliacha.

35

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Jibu: Kauli yake Mwenyezi Mungu: "Si kosa" haikuja kubainisha huku-mu ya Saa'y kuwa ni wajibu au la, isipokuwa imekuja kubainisha kuwa Saa'y ni sharia na Uislamu unaikubali na kuithibisha. Ama maarifa ya hukumu yake na je, ni faradhi au ni sunna, hayo yanafahamishwa na dalili nyingine

Zimekuja Hadith mutawatir za Mtume na wamekongamana Waislamu juu ya wajibu wa kufanya saa'y katika Hijja ya Kiislamu. Katika Majmaul-Bayan anasema Imam Jaffar Sadiq amesema: "Waislamu walikuwa wakiona kwamba Swafa na Mar'wa ni mambo yaliyozushwa wakati wa Jahiliya, ndipo akateremsha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Aya hizi". Yaani anaziondoa dhana hizi na kubainisha kwamba Swafa na Mar-wa vinatokana na Uislamu tangu asili; washirikina wakivizunguukia huwa wanajikurubisha kwa masanamu, lakini Waislamu huwa wanavizungukia kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake.

Na anayefanya heri basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani (na) mjuzi.

Yaani anayefanya wema kwa kufanya Saa'y kati ya Safa na Mar-wa baada ya kutekeleza wajibu alionao, basi Mwenyezi Mungu atamlipa wema kwa wema wake. Shaakir (mwenye shukrani) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu na maana ya Mwenyezi Mungu kumshukuru mja wake mtiifu, ni kuwa radhi naye na kumpa thawabu kutokana na shukrani yake na utiifu wake.

36

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

159. Hakika wale wanaoficha tuliy-oyateremsha, katika ubainifu na uwongofu, baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu na wanawalaani wanaolaani.

160. Ila wale waliotubu na kujirekebisha na wakabain-isha, basi hao nitawataka-balia toba, na Mimi ni Mwingi wa kutakabali toba, Mwenye kurehemu.

161. Hakika wale waliokufuru, na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.

162. Humo watadumu, hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda.

Kaashif2-57.jpg

37

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

WANAOFICHA YALIOTEREMSHWA

Aya 159-162:

MAANA

Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika ubainifu na uwon-gozi, baada ya sisi kuyabainisha kwa watu kitabuni hao anawalaani Mwenyezi Mungu na wanawalaani (kila) wanaolaani.

Dhahiri ya Aya ni kwamba inaanzia habari nyingine isiyofungamana na yaliyo kabla yake. Makusudio ni kuwa kila mwenye kujua hukumu katika hukumu za dini ambazo ubainifu wake umekuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu au katika Hadith za Mtume wa Mwenyezi Mungu au katika hukumu ya akili na akaificha, basi yeye amelaaniwa mbele ya Mwenyezi Mungu na watu wa mbinguni na ardhini. Mwenyezi Mungu ameashiria hukumu ya akili kwa kusema "Uwongofu".

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Ubainifu ni dalili za kisharia na uwongofu ni dalili za kiakili..."

Laana haiko kwa watu wa Kitabu tu, bali inamhusu kila mwenye kuficha haki kwa vile:

1. Tamko la Aya halikufungwa na jambo lolote.

2. Lau tunakadiria kuwa mashukio ya Aya ni kutokana na waliyoyafanya watu wa Kitab ya kupotoa Tawrat na Injil, basi tutasema: mashukio hayafanyi hukumu iliyo shuka kuwa mah'susi; kama wasemavyo Wanafiqh, ambao wanakusudia kusema kuwa tukio mahsusi haliwezi kufanya tamko la kiujumla kuwa mahasusi.

3. Imethibiti katika elimu ya Usul kwamba kufungamana hukumu juu ya sifa kunafahamisha kuwa sifa ni sababu. Na hapa laana inafungamana na kuficha kwenyewe. Kwa hiyo inakuwa laana inaenea kwa kila chenye kufichwa.

38

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

4. Imekuja Hadith inayosema: "Mwenye kuulizwa elimu anayoijua, aka-ficha, atafungwa lijamu ya moto siku ya Kiyama.

Wameafikiana mafakihi kwa tamko moja kwamba kumfundisha asiye jua hukumu za dini yake ni dharura ya wajibu kifaya (wajibu wa kutosheana) kwa kila mwenye kuijua; wakiitekeleza baadhi basi jukumu limewaon-dokea wote; na wakiiacha wote, basi watastahili adhabu wote.

Maana ya laana kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ni kumtoa, mwenye kulaaniwa kutoka katika rehema Yake, na maana ya laana kutoka kwa Malaika na watu ni dua ya kutaka mwenye kulaaniwa atolewe katika rehema ya Mwenyezi Mungu.

UBAYA WA ADHABU BILA YA UBAINIFU

Jukumu la mwenye kukalifiwa na sharia aliye baleghe na mwenye akili timamu, mbele ya Mwenyezi Mungu hupimwa kwa kumfikia taklifa zenyewe na kuzijua, wala sio kupatikana taklifa. Kwa sababu kuacha kumfikia ni sawa na kutokuwepo.

Hata hivyo ni wajibu kwa kila mwenye kukalifiwa na sharia (makallaf) ata-fute na kufanya utafiti wa ubainifu na dalili za hukumu katika sehemu zinakopatikana na kuwaulizia wanaohusika katika dini na sharia, wala haifai kwake kufanya uzembe na kupuuza, kisha aje atoe udhuru kuwa hajui. Kwa sababu mwenye kuzembea ni sawa na mwenye kufanya makusudi, bali huo uzembe hasa ni makusudi, kwa vile mzembe anakuwa amekusudia kuacha kutafuta na kusoma. Kama akifanya bidii na asipate lolote, basi atakuwa hana jukumu, hata kama ubainifu uko.

Hakika huu ni msingi ulio wazi kiakili; ni akili gani inayoweza kumlaumu mwingine, ambaye hakufanya uzembe, kwa jambo asilolijua? Wanavyuoni wa Fiqh wamesema kwa pamoja kuhusu msingi huu na ume-thibitishwa na sharia katika Aya kadhaa; kama Aya hii tunayoizungumzia;

"Baada ya sisi kuzibainisha kwa watu." Pia Aya inayosema:

39

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-58.jpg

"...Na sisi si wenye kuwadhibu mpaka tumpeleke Mtume." (17:15).

Katika Hadith za Mtume iko inayosema: "Umeondolewa umma wangu yale wasioyoyajua." Tutayarudia maudhui haya kila tutakapofikilia kwenye Aya inayoyagusia Inshaallah.

Ila wale waliotubu na kujirekebisha na wakabainisha.

Yaani wale wanaoificha haki ni wenye kulaaniwa, isipokuwa wale waliotubu na kujuta kwa ikhlas katika toba kwa kuazimia kutorudia makosa; kisha wakayab- ainisha wazi wazi yale waliyokuwa wameyaficha mwan-zo. Kwani kutubia kwa mwizi hakutoshi maadamu hajarudisha haki ya wenye we.

Basi hao nitawatakabalia toba na Mimi ni Mwingi wa kutakabali toba Mwenye kurehemu.

Neno tawwab (mwingi wa kukubali toba) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Ameikutanisha rehema na kukubali toba, kwa kukumbusha kuwa sababu ya kukubali kwake toba kwa aliyemfanyia uovu ni rehema Yake kwa waja wake.

Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao wana laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.

Hata mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na akamkanusha, hukubaliwa toba yake akitubia na husamehewa na kurehemewa, wala hataadhibiwa isipokuwa yule atakayekufa akiwa ameng'ang'ania ukafiri na maasi, kwa sababu yeye katika hali hiyo anastahili laana ya watu wa mbinguni na wa ardhini.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu anasema: "Na ya watu wote" na inajulikana kuwa katika watu kuna wasio mlaani kafiri, hasa wale makafiri?

40

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Jibu: Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu; "Na ya Malaika wote na ya watu wote" ni kwamba huyo kafiri yuko mahali pa laana ya watu wa mbinguni na wa ardhini, iwe wamemlaani au hawakumlaani; hata kama ni makafiri kama wao, yeye ni wa kulaaniwa tu. Katika Qur'an inaelezwa kwamba makafiri kesho watalaaniana wenyewe kwa wenyewe.

Kaashif2-59.jpg

"...Kisha siku ya Kiyama baadhi yenu watawakufurisha wengine na baad-hi yenu watawalaani wengine..."                               (29:25).

Humo watadumu, hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa muda humu, ni humo mwenye laana.

Maana ya kudumu katika laana ni kukaa milele katika athari ya hiyo laana ambayo ni moto. Razi anasema: "Maana ya 'hawatapewa muda' ni kwamba wakiomba muda hawatapewa na wakilia kutaka kuokolewa hawataokolewa na wataambiwa: 'Nyamazeni wala msiseme'". Mwenyezi Mungu apishie mbali.

HUKUMU YA LAANA KATIKA SHARIA

Kumlaani mtu ni haramu na ni katika madhambi makubwa kwa sababu ni uadui sawa na kuingilia mali; katika Hadith inaelezwa "Hakika laana iki-toka kwa mtu, huzunguka, ikimkosa humrudia mwenyewe."

Ziko laana zilizoruhusiwa na sharia ambazo ni:-

1. Kafiri: Aya ni nyingi sana kuhusu kafiri, kama hii tunayoizungumzia. Ama Hadith zimepetuka kuwa Mutawatir. Miongoni mwazo ni ile iliyo katika kitabu Ahkamul-Qur 'an cha kadhi Abu Bakr Al-Muafiri, aliyoita-ja wakati wa kutafsiri (2:161), kwamba Mtume alisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika Amr bin Al-Aas amenikebehi na anajua kuwa mimi si mshairi, basi mlaani."

2. Dhalimu: Awe Mwislamu au si Mwislamu, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu "Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalim" (7 : 44)

41

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

3. Mwenye kufanya ufisadi.

4. Mwenye kufitini na kusababisha zogo.

Ama laana ya wasiokuwa hao waliotajwa kuna mushkeli na kuangaliwa vizuri. Ndio, ni kweli kwamba mwenye kudhihirisha maasia bila ya kujali inajuzu kumsengenya, lakini kusengenya ni kitu kingine na laana ni kitu kingine. Ama wanavyotumia watu kuwalaani wanyama, n.k. ni upuuzi, unaofaa kutupiliwa mbali.

163. Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja, hakuna Mungu isipokuwa Yeye, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

164. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kuhitali-fiana usiku na mchana, na vyombo ambavyo hupita katika bahari pamoja na viwafaavyo watu, na maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni, na kwa maji hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama, na mabadiliko ya pepo na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, ni ishara kwa watu wenye akili.

Kaashif2-60.jpg

42

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

NA MUNGU WENU NI MUNGU MMOJA Aya 163-164:

MAANA

Na Mungu wenu ni Mungu mmoja, hakuna Mungu isipokuwa Yeye.

Amirul Mumini katika kumuusia Mwanawe Hassan (a.s.) alisema: "Ewe mwanangu! Jua kwaamba lau Mola wako angelikuwa na mwenzake, basi huyo mwenzake angelileta Mitume yake na ungeliona athari za ufalme na usultani wake, na ungelijua vitendo vyake na sifa zake."

Maelezo ya kukanusha ushirika yatakuja katika kufafanua Aya ya (17:42) (21:22) na (23:91).

MBINGU

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi.

Katika mbingu kuna nyota zinazozidi chembe za mchanga kwa idadi; nyota iliyo ndogo zaidi miongoni mwazo, ni ile ambayo ni kubwa zaidi ya ardhi mara milioni. Kila kundi la nyota linakuwa katika mkusanyiko mkubwa unaoitwa 'Galaxy' unaokusanya zaidi ya nyota milioni mia moja. Idadi ya mikusanyiko hiyo ni zaidi ya milioni mbili. Kila mji uko mbali na mwingine kwa masafa ya simu ya upepo ambayo umbali wake kufiki-wa ni miaka milioni tatu, yaani mikusanyiko hiyo yote katika anga iliyo wazi ni sawa na nzi anayepotea katika dunia. Nyota zote hizo na sehemu zake zinakwenda kwa kipimo na utaratibu mzuri.

Huu ni mfano mmoja wa mamilioni ya mifano juu ya kudura ya Mwenyezi Mungu na ukubwa wake uliovumbuliwa na Sayansi. Na Qur'an tukufu bado inawaambia wavumbuzi hao:

"...Nanyi hamkupewa elimu ila kidogo."                          (17:85).

43

Kaashif2-61.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ARDHI

Ardhi ni tufe lililo hewani; inazunguuka mara moja katika kila baada ya masaa ishirini na nne, ambayo usiku na mchana unafuatana. Inaelea kan-doni mwa jua mara moja kwa mwaka ambapo vinafuatana vipindi vinne kwa mwaka. Ardhi inazunguukwa na mfuniko wa gesi yenye mchanganyiko wa gesi muhimu ya uhai; gesi hiyo inahifadhi kiwango cha nyuzi joto kinachowiana na uhai. Vile vile inachukua mvuke wa maji kuto-ka baharini na kuupeleka masafa ya mbali juu na hatimaye yanaanguka nakuwa mvua.

Lau kama upana wa ardhi ungelikuwa mdogo kuliko ulivyo sasa, ingel-ishindwa kuhifadhi uzani; na joto lingepanda kufikia mauti; na kama ungelikuwa ni mkubwa zaidi ya ulivyo ingelizidi mvutano wake, na ziada hiyo ingeliathiri maisha.

Vile vile, lau kama umbali wa ardhi na jua ungelipungua kuliko ulivyo hivi sasa, kiasi cha joto kingelipungua, na kama ardhi ingelikurubia zaidi jua kuliko ilivyo hivi sasa, basi joto lingezidi. Katika hali zote mbili maisha yangelikuwa magumu juu ya ardhi.

Kwa hivyo mduara wa ardhi, na kipimo cha sehemu wazi zinazoizunguu-ka, mzunguuko wake pembeni mwa jua, kuzunguukwa na mfuniko anga, kuwa mahali maalum na kuwa upana wake ni kiasi maalum, yote hayo yanaandaa sababu za kupata uhai wa mtu juu ya ardhi. Lau ingekosekana moja ya sifa hizi; kwa mfano upana wake kuwa mdogo au mkubwa, au kuwa mbali au karibu na jua au kukosa mfuniko anga, ingelikuwa vigumu mtu kuwa ni wa duniani, kwa ushahidi wa wataalamu.

Ni jambo lisiloingia akilini kuwa utaratibu huu uwe umepatikana kibahati tu. Bali yote hayo ni kwa hekima ya Mwenye hekima na mazingatio ya Mwenye kuzingatia.

KUWAPO MUNGU

Katika kufasiri Aya ya 21 na 22 za Sura hii, tumetaja dalili za kuwapo Mpangaji mambo, Mwenye hekima. Miongoni mwa dalili hizo ni dalili ya kufikia kikomo, na kwamba mpangilio wa ndani uliofanywa kwa hekima

44

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

kati ya mbingu na ardhi hauwezekani kuwa umepatikana kwa sadfa (kibahati) tu!

Wala hakuna tafsiri yenye kukinaisha isipokuwa kuwapo Muweza, Mwenye hekima. Qur'an imetegemea dalili hii na ikaionyesha katika Aya nyingi, kama vile Aya hii tuliyonayo.

Kwa kunasibiana kwake, tunarudia kutoa dalili ya kuwapo Mwenyezi Mungu, lakini kwa mfumo mwingine sio ule tuliofuata wakati wa kufasiri Aya ya 21. Kabla ya kitu chochote kwanza tunatanguliza haya yafuatayo:

Wamaada wameamua sababu ya elimu na maarifa ni kuona na kujaribu tu. Kila linaloaminika ni lazima kupitia majaribio, kila linaloitakidiwa kwa njia nyingine isiyokuwa na majaribio basi hawaliiti kuwa ni elimu bali ni itikadi. Kwa hiyo elimu na itakidi - katika istihali yao -ni vitu viwili tofau-ti katika matokeo yake. Mtu akipata msaada wa majaribio kwa kusihi yale anayoyaitakidi, basi yanakuwa yale yanayoitakidiwa ni elimu.

Kwa msingi wao huo, kunakuwa kuamini kuwapo Mwenyezi Mungu ni itikadi si elimu. Nasi tunawaambia: Lakini vile vile kuamini kutokuwapo Mungu pia ni itikadi si elimu, kwa sababu pia hakutegemei majaribio. Kwa hiyo itikadi zimekutana. Kwa maneno mengine, ni kwamba, kila yanayoambatana na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ikiwa ni kukubali au kupin-ga, basi ni katika mambo ya ghaibu (yaliyojificha). Ikiwa mwenye kuamini kuwapo Mungu anaamini ghaibu bila ya majaribio, vile vile mwenye kukanusha hategemei majaribio, bali hutegemea ghaibu. Kwa hiyo wote ni sawa.

Baada ya utangulizi huu tutaonyesha kauli ya wakanushaji - Wamaada, na tutaonyesha kauli ya wenye kuamini Mungu kisha tumwachie msomaji ajichagulie.

Wakanushaji wanasema: Kupatikana ulimwengu na yaliyomo ndani yake, miongoni mwa nidhamu, mtu, pamoja na hisia zake na akili, yote hayo hayategemei udhibiti wowote isipokuwa yamepatikana kibahati (sadfa). Kwa hiyo ulimwengu ulipatikana kibahati, kisha ukapatikana mpango kibahati na kila kitu kimechukua mahali pake panapostahili kwa kibahati

45

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

tu; na maada ndiyo iliyopatisha uhai na akili. Kwa maneno mengine, ni kwamba maada pofu ndiyo Mungu inayoweza kila kitu, lakini imepata uwezo hekima na kupangilia mambo kwa njia ya kibahati.

Ama wanaoamini kuwapo Mwenyezi Mungu wanasema: Ulimwengu na nidhamu yake, umepatikana kwa makusudio na kwa hekima, na mpangilio kutoka kwa Mola Muweza na Mwenye hekima.

Sasa msomaji jiulize swali hili: Ni nini chanzo cha ulimwengu, utaratibu na mipangilio? Je chanzo chake ni sadfa kama wasemavyo Walahidi? Au ni kwa makusudio na mipangilio, kama wasemavyo Waumini?

Jiulize swali hili kisha ujijibu kwa akili yako. Ama Voltaire amelijibu swali hili kwa kusema: "Fikra ya kuwapo Mwenyezi Mungu ni dharura, kwa sababu fikra ya kupinga ni upumbavu."

UPI ULIOTANGULIA: USIKU AU MCHANA?

Wataalamu wamehitalifiana kuwa je mwangaza umetangulia giza au giza ndilo lililotangulia mwangaza katika kupatikana? Wengine wanasema mchana ndio uliotangulia usiku kwa hiyo usiku wa siku ni ule unaokuja baada ya mchana.

Wengine wamesema usiku ndio uliotangulia mchana kwa hiyo usiku unakuwa ni usiku wa mchana utakaokuja. Watu wa kwanza walipendelea kauli hii; kwa hiyo usiku wa Ijumaa kwao ni ule usiku unaokuwa kabla ya alfajiri ya ijumaa na masiku mengine yote. Katika waliyoyatolea dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Na usiku ni ishara kwao; tunauvua humo mchana..." (36:37).

46

Kaashif2-62.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

165. Na katika watu kuna wanao-fanya waungu wasiokuwa Mwenyezi                  Mungu, wanawapenda kama kumpen-da Mwenyezi Mungu. Lakini wale walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu sana. Na lau waliodhulumu wangejua watakapoiona adhabu kwamba nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

166. Pindi waliofuatwa watakapo-wakataa wale waliowafuata, na hali yakuwa wamekwisha iona           adhabu           na yatawakatikia mafunga-mano.

167.  Watasema wale waliofuata: 'Lau kama tungeweza kurudi nasi tukawakataa kama walivyotukataa.' Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavy-owaonyesha vitendo vyao kuwa majuto juu yao; wala hawatakuwa wenye kutoka motoni

Kaashif2-63.jpg

47

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

WANAFANYA WAUNGU ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU Aya 165-167:

MAANA

Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu".

Yaani kuna baadhi ya watu wanamshirikisha Mwenyezi Mungu kwa sababu wao wamemfanya kuwa na mshirika katika baadhi ya mambo anay-ohusikana nayo; kama vile kunufaisha na kudhuru. Imam Baqir (a.s.) ame-sema: "Waungu ambao wamewafanya na kuwapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu ni maimamu wa dhuluma na wafuasi wao."

Imesemwa kuwa maana ya kumpenda Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kumpenda kwa ukamilifu, kwa sababu Yeye ni ukamilifu mtupu. Imesemwa pia: 'Ni kujua utukufu wake, uweza wake na hekima yake.' Na imesemwa: 'Ni kumwamini Mwenyezi Mungu kuwa Yeye ndiye mwanzil-ishi na mwenye kurejesha, na kwamba kila kitu kiko chini ya mamlaka yake'.

Sisi tuko kwenye njia ambayo tunakwenda nayo - kuchagua maana yenye kuafikiana ambayo yako wazi na yaliyo rahisi kufahamika. Kwa misingi hiyo tunasema: Anayempenda Mwenyezi Mungu ni yule asiyefuata mata-manio yake na akamtii Mola wake; kama alivyosema Imam Sadiq (a.s.) katika kumwelezea ambaye dini itachukuliwa kutoka kwake. Kwa maneno mengine, kumpenda kwako Mwenyezi Mungu ni kuacha unayoyataka we we na kufanya anayoyataka Yeye; kama ambavyo maana ya kumpenda Mtume (s.a.w.w) ni kufanya kulingana na Sunna yake.

Ama Mwenyezi Mungu kumpenda mja wake ni kumlipa thawabu. Imekuja Hadith inayosema: "Nitampa bendera kesho mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na anayependwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. " Yaani Ali anamtii Mwenyezi Mungu na Mwenyezi

48

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mungu atamlipa thawabu na Mtume anamtukuza na kumtanguliza.

Kwa hiyo basi, kila anayemtii kiumbe, huyo amefanya waungu wasiokuwa

Mwenyezi Mungu, atake asitake.

Lakini wale walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu sana.

Kwa sababu wao hawamshirikishi na yeyote katika twaa na humtegemea. Ama wale wasioamini wanawategema waungu wengi na wanamshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu katika twaa kutaka heri na kujikinga na shari.

Na lau waliodhulumu (nafsi zao) wangejua watakapoiona adhabu kwamba nguvu zote ni za

Mwenyezi Mungu.

Yaani lau washirikina ambao wamezidhulumu nafsi zao wanajua kwamba hakuna mwenye usultani katika siku ya haki na ya kupambanuliwa hukumu, isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye peke Yake ndiye Mwenye mamlaka ya kuwaadhibu waasi na kuwalipa mema watiifu, lau wangelijua hivyo, basi wangelikuwa na yakini kwamba atakayekuwa peke yake kesho katika kuendesha mambo ya akhera ndiye huyo huyo aliyepanga ulimwengu huu. Kwa hivyo jawabu la lau limeondolewa, linafahamika kutokana na mpangilio wa maneno.

Pindi waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu na kuwakatikia mafungamano.

Maneno bado yanaendelea kwa wale wanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu; wao ndio wanaoongozwa na ni wafuasi, na waungu ndio viongozi. Kesho pazia litakapofunguka, kiongozi atamkataa mfuasi wake kutokana na shida ya adhabu itakayotokea, na uhusiano kwao utakatika. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Zitaondoka zile sababu zote ambazo zinafungamanisha mapenzi, udugu, cheo mikataba ya umoja, n.k. na hilo ni mwisho wa kukata tamaa."

49

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Aya hii inafanana na Aya inayosema:

Kaashif2-64.jpg

"...Kila umma utakapoingia utawalaani wenzake, mpaka watakapoku-sanyika wote humo, wa nyuma wao watawasema wa kwanza wao: "Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza; basi wape adhabu ya moto maradufu! Atasema: 'Itakuwa kwenu nyote (adhabu) maradufu, lakini nyinyi hamjui tu'."          (7:38).

Na watasema wale waliofuata: 'Lau kama tungeweza kurudi nasi tukawakataa kama wanavyotukataa'.

Kesho atatamani kila muasi arudi duniani kutengeneza yale aliyokuwa ameyaharibu, hasa wafuasi wa watu wapotevu. Na hakuna kitu kilicho mbali zaidi ya matamanio haya, bali ni majuto yanayoichoma nafsi, sawa na moto unavyochoma mwili. Majuto hayo ni matunda ya kufuata matamanio na kupetuka mipaka.

Dhahiri ya tamko la Aya inafahamisha kwamba inahusika na makafiri, lakini kwa mujibu wa sababu ya hukumu, inamhusu kila mwenye kufuata na kusaidia dhuluma na ufisadi, na kila mwenye kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kunufaisha na kudhuru.

Vile vile mwenye kuchukua dini yake kutoka kwa wasio jua na wapotevu. Kwa hakika Aya hii inawahusu wote; hata mwenye kutamka shahada mbili, akaswali na kutoa zaka; isipokuwa asiyejua ambaye hakuzembea katika kujua uhakika wa mambo na kujua mambo yanayoweza kujulikana na akili yoyote iliyo timamu.

50

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

TAQLID NA MAIMAMU WANNE

Yamekuja maelezo katika tafsiri yaAl-Manar kwa kunakiliwa kutoka kwa Sheikh Muhammad Abduh kwamba, Maimamu wane: Abu Hanifa, Malik, Shafi na Bin Hambal wamekataza kufuatwa na kuchukuliwa kauli zao, na kwamba wao wanaamrisha ziachwe kauli zao na kifuatwe Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake. Baada ya kunakili kauli ya kila Imam katika hilo, akasema: "Lakini Karkhi - mmoja wa mafakihi wa Kihanafi- anasema wazi kwamba asili ni kauli ya Abu Hanifa. Kama Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake zitaafikiana na kauli ya Hanafi ni sawa; na kama si hivyo, basi ni lazima kauli ya Mwenyezi Mungu au Hadith ifanyiwe taawili ili iweze kuafikiana na kauli ya Abu Hanifa."

Maana yake ni kuwa kauli ya Abu Hanifa ndiyo inayohukumu na kuitan-gulia Qur'an na Hadith. Kauli hii kwa dhati yake ni kufru. Kuna kufru gani kubwa zaidi kuliko kuiacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa sababu ya kauli ya Abu Hanifa na wafuasi wake? Je, kuna tofau-ti gani kati ya mwenye kusema haya na wale waliotajwa na Mwenyezi Mungu aliposema:

Kaashif2-65.jpg

"Na wanapoambiwa; Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu huse-ma; "bali tunafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu..." (2:170).

Tutafafanua kwa upana zaidi suala la taqlid katika kufasiri Aya ya 170 ya Sura hii Inshaallah.

Kwa hiyo kufanya amali kwa kutegemea kauli za Maimamu wane ni kufanya amali bila ya ijitihadi wala taqlid, kwa sababu hao wane wamekataza kufuatwa.

51

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

168. Enyi watu! Kuleni vilivyomo ardhini halali na vizuri, wala msifuate nyayo za shetani. Hakika yeye kwenu ni adui aliye dhahiri.

169. Hakika yeye anawaamrisha tu maovu na machafu, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.

170. Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; husema: Bali tutafu-ata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.' Je, hata kama baba zao walikuwa hawafa-hamu chochote wala hawakuongoka?

KULENI VILIVYOMO KATIKA ARDHI

Aya 168-170 LUGHA

Halali ni kila ambalo halikuthibiti kukatazwa katika sharia; na haramu ni lile lililothibiti kukatazwa. Makusudio ya uzuri hapa ni lile ambalo linapendelewa na nafsi na kuburudika nalo kwa sharti ya kutokuwa ni

Kaashif2-66.jpg

52

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

lenye kukatazwa. Na ovu ni lile ambalo mwisho wake ni uovu. Enyi watu! Kuleni vilivyomo ardhini halali na vizuri.

Msemo huu unawahusu watu wote; ni sawa awe mtu amejiharamishia mwenyewe baadhi ya vyakula au asiyejiharamisha; ni sawa awe ni Mumin au kafiri. Kwa sababu kafiri atazuiliwa neema za akhera tu sio starehe za dunia. Kuna Hadith Qudsi isemayo: "Mimi ninaumba na anaabudiwa mwingine na ninaruzuku na anashukuriwa mwingine."

Katika vyakula kuna vya halali na haramu. Kula ambacho hakikukatazwa na sharia ni halali. Hadith inasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amenya-mazia vitu sio kwa kusahau. Kwa hivyo msijikalifishe navyo; ni rehema kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu." Mara nyingine uharamu unao-tokana na sababu iliyozuka; kama vile mali iliyochukuliwa kwa riba, utapeli, rushwa au wizi.

Wala msifuate nyao za shetani. Hakika yeye kwenu ni adui aliye dhahiri.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuhalalishia watu halali anawahadharisha kuifanya haramu. Ibara ya tahadhari hii ameileta kwa kukataza kumfuata shetani na tashwishi zake ambazo zinampambia mtu yale yasiyokuwa halali kwake na kila ambalo linamhadaa, ili afanye mambo ya haramu; kama vile kunywa pombe, zinaa, uongo na ria. Au kumhadharisha kufanya wajibu; kama vile kutia hofu ya ufakiri ikiwa mtu atatekeleza haki aliyon-ayo kwa kutoa mali au madhara ikiwa atafanya jihadi au kusema haki. Yote hayo ni katika mawazo ya shetani. Mwenyezi Mungu ameuelezea usemi wa shetani aliposema:

Kaashif2-67.jpg

"Na kwa hakika nitawapoteza na nitawatia tamaa..." (4:119).

53

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-68.jpg

"...Basi nitawavizia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka kisha nitawafikia mbele yao na nyuma yao na kuumeni kwao na kushotoni kwao; wengi katika wao hutawakuta wenye kushukuru." (7:16-17).

Hakika yeye anawaamrisha mambo mabaya na machafu, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.

Huu ni ubainifu wa athari na natija zinazotokana na kufuata mwito na nyayo za shetani, nazo ni tatu: Kwanza, ubaya ambao ni kila kitendo ambacho mwisho wake ni ubaya. Pili, uchafu nao ni aina mbaya ya maasi. Tatu, kumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua kwamba yeye ana washirika na watoto, kuhalalisha haramu, na kuharamisha halali. Vile vile kufanya amali kwa kukisia na kupendelea katika kutoa hukumu ya sharia.

Na wanapoambiwa! Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu huse-ma: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.

Dhamiri ya wanapoambiwa inamrudia kila anayefuata mwingine bila ya hoja wala dalili, na kuacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume, kwa sababu ya kauli ya mababa. Makusudio ya aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ni kila yale yaliyo na dalili na hoja na yakaingia katika akili zilizo timamu.

Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?

Yaani wanafuata baba zao hata kama hawafahamu chochote katika mambo ya dini. Makusudio sio kukanusha kufahamu kila kitu, ijapokuwa kwa

54

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

dhahiri Aya hii inaonyesha hivyo. Bali makusudio ni kukanusha kufa-hamu, kwa vile maneno yanahusikia na mambo ya kidini.

Tutaonyesha katika kifungu kifuatacho kwamba Aya hii inafahamisha ubaya wa kufuata mambo ya upotevu. Ama kufuata ya uongofu, hilo ni katika kufuata mwendo mzuri.

KUFUATA NA MSINGI WA ITIKADI

Kufuata (Taqlid) kulivyo hasa si kuzuri wala si kubaya kwa ujumla, bali kunatofautiana kwa aina zake zifuatazo:

1. Kufuata mkumbo, ambako kwa binadamu na wanyama ni sawa sawa; kama vile kuwika kwa jogoo anapomsikia mwenzake amewika na kulia kwa punda anapomsikia mwenzake. Hali kadhalika kwa upande wa binadamu, mmoja anaweza kupiga kofi kwa ajili ya hotuba, basi wengine wote wanaigiza bila ya kutambua, hata kama hawakufahamu kitu katika yaliyos-emwa. Au mtu anaweza kuangalia upande fulani basi kila anayemuona naye huangalia huko bila ya kukusudia. Huku ndiko kufuata ambako si kuzuri wala kubaya. Kwa sababu kuko nje ya hisia na matakwa.

2. Kufuata mitindo na desturi fulani ya jamii; kama vile namna ya mavazi na mengineyo katika mambo ya jamii ambayo yamefanywa na wakub-wa na wadogo, na wajuzi na wasiokuwa wajuzi. Hii ni katika aina ya kufuata ambako kunaweza kuwa kuzuri au kubaya kulingana na mtazamo wa watu.

3. Asiyejua kumfuata mtaalam katika mambo ya kidunia; kama vile utabibu, uhandisi, kilimo, ufundi, n.k. Huku ni kufuata kuzuri bali ni muhimu sana katika ustawi wa jamii. Lau kama si hivyo, basi utaratibu ungeharibika na kazi zingelisimama. Kwani mtu hawezi kujua kila kitu na kupata kila anayoyahitajia peke yake. Mtu alikuwa na ataendelea kuwa na haja ya kusaidiana na kubadilishana huduma.

55

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

4. Mujtahid kumfuata mujtahid mwenzake katika mambo ya kidini. Huku kunakataliwa na akili na ni haramu kisharia. Kwa sababu, aliyoyajua ni hukumu ya Mwenyezi Mungu katika haki yake, haijuzu kuyaacha kwa sababu ya kauli ya mtu mwingine. Na ni mjuzi gani anayeacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake aliye Masum na kutegemea kauli ya anayekosea?

5. Asiye na elimu kumfuata mujtahid mwadilifu katika masuala tanzu ya kidini, kama vile hukumu za ibada, halali na haramu, twahara, najisi na kusihi muamala, n.k. Kufuata huku ni wajibu kisheria, kwa sababu ni kumfuata aliyechukua ujuzi wake kutokana na hoja na dalili; sawa na mgonjwa kumfuata daktari. Asiyejua anakalifiwa na hukumu, na haku-na njia ya kuzifuata isipokuwa kumrudia mjuzi.

Kaashif2-69.jpg

"...Basi waulizeni wenye kumbukumbu (wajuzi) ikiwa nyinyi hamjui." (16:43).

Hata hivyo, asiyejua akiswali na kufunga kwa kufuata baba zake na mfano wao, sio kwa kufuata mujtahid mwadilifu, na ibada zake zikaafikiana na fat-wa za mujtahid, hizo zitakuwa sahihi na kukubaliwa. Kwa sababu kufuata (taqlid) si sehemu wala sharti la yanayoamrishwa, isipokuwa ni nyezo tu ya kufikilia kwenye amri. Hata inaweza kusihi maamiliano yake kama yakiwa ni sawa sawa.

Kuhusu kauli ya anayesema kuwa ibada inahitajia nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kwamba nia hiyo haithibitiki ila kutokana na mujtahid au mwenye kumfuata, kauli hiyo ni madai tu. Kwa sababu, maana ya nia ya kujikurubisha ni kutekeleza yaliyoamriwa kwa nia safi yenye kutakata na kila uchafu wa kidunia. Hapana mwenye kutia shaka kwamba hayo yanaweza kupatikana bila ya mujtahid. Kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"...Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala kuon-goka?" Inafahamisha kuwa ikiwa baba alikuwa kwenye uongofu na aka-

56

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

fuatwa na mtoto, itasihi.

6. Kufuata katika misingi (itikadi) ya dini kama kumjua Mwenyezi Mungu na sifa Zake, Utume wa Muhammad isma yake na ufufuo. Wanavyuoni wengi wa Kisunni na Kishia wameikataza aina hii ya kufuata, wakasema kuwa haijuzu (haifai). Kwa sababu kufuata (taqlid) huko ni kufuata bila ya dalili. Na huo ndio ujinga hasa; yaani mwenye kusema juu ya kuweko Mwenyezi Mungu kwa kufuata tu, ni sawa na mwenye kusema Mungu hayuko.

Wanavyuoni hawa wamesema: "Tumejuzisha kufuata katika matawi ya dini na masuala ya kuamiliana, lakini sio katika misingi ya kiitikadi. Kwa sababu linalotakiwa katika matawi ni amali tu kwa kufuata kauli ya mujtahid, jambo ambalo linawezekana, lakini kwa misingi ya kiitikadi, linalotakikana ni elimu na itikadi."

Wahakiki katika Sunni na Shia wamesema kuwa kufuata kukiafikiana na uhakika ulivyo ni sahihi, kwa sababu hilo ndilo linalotakikana; na ijtahidi sio sharti wala fungu la imani na kusadikisha, isipokuwa ni njia tu.

Hii ni kweli kabisa, kwa sababu linalozingatiwa katika misingi ya itikadi ni imani sahihi yenye kuafiki. Kwa ajili hii ndio Mtume (s.a.w.w) akakubali Uislamu wa kila mwenye kuuamini na ikatulia nafsi yake kwa ukweli wake na Utume wake bila ya kufanya ijtahidi na kuangalia. Ama Aya zilizokuja kukemea wanaofuata mababa, mfumo wake unafahamisha kuwa makusudio ni kufuata batili na upotevu, sio haki na uongofu. Hakika hii inadhihiri kwa kila mwenye kufikiria kwa undani maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-70.jpg

"Na wanapoambiwa: Njooni katika hukumu alizoteremsha Mwenyezi Mungu na (anazozisema) Mtume' husema: 'Yanatutosha yale tuliyowaku-ta nayo baba zetu' ..." (5:104).

57

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-71.jpg

"Hata kama nawaletea yenye mwongozo bora kuliko mliyowakuta nayo baba zenu." (43:24).

Kaashif2-72.jpg

"Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala kuongo-ka?" (2:170).

Ufahamisho wa Aya zote hizi ni kwamba, kama mababa zao wangelikuwa na desturi yenye uongofu ambao umeteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume, basi ingelifaaa kuwafuata mababa hao. Kwa sababu linalotakiwa ni kufuata aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu! Wakiyafuata, basi wamefuata amri na wametii, na hawataulizwa kitu kingine baada ya twaa.

Kwa ufupi ni kwamba kila anyefuata kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume, atakuwa amefuata haki yenye kuthibiti kwa dalili, ni sawa awe amejua dalili hiyo au la. Inatosha kujua kwa jumla kwamba kuna dalili sahihi waliyoifuata wahusika wanaofanya ijtihadi. Bali mwenye kufuata haki bila ya kuijua kwamba hiyo ni haki, hataadhibiwa kwa kuacha kuji-fundisha hata kama hastahiki thawabu na kusifiwa. Hayo yanafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Kaashif2-73.jpg

"Na (wazazi wako) wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, usiwatii ..." (31:15).

58

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-74.jpg

Hiyo vile vile inafahamisha kuwa wakikushurutisha kumwamini Mwenyezi Mungu na ukawatii bila ya kuwa na elimu nayo, basi hapana ubaya kwako.

Tumefafanua kuhusu kuwafuata (taqlid) Maimamu wane katika kufasiri Aya ya 167 ya sura hii, mwenye kutaka na arudie.

171. Na mfano wa wale walioku-furu, ni kama mfano wa anayempigia kelele asiyesikia ila wito nasauti tu; ni viziwi, mabubu, vipofu kwa hivyo hawafahamu.

MFANO WA ANAYEITA ASIYESIKIA.

Aya 171:

MAANA

Mwenyezi Mungu katika Aya hii anawapigia mfano makafiri ambao wameng'ang'ania dini ya mababa, akawafananisha na wanyama na akam-fananisha na mchungaji, yule anayewalingania kwenye haki. Kama ambavyo wanyama hawafahamu chochote katika maneno ya mchungaji isipokuwa sauti wanayoizowea baada ya kuzoweshwa; vile vile makafiri hawafahamu haki wala manufaa ambayo wanalinganiwa. Kwa hakika wao ni kama viziwi japo wanasikia; ni kama mabubu japo wanasema, na ni kama vipofu japo wanaona.

Aya nyingi za Qur'an hazimtofautishi kiziwi asiyeweza kusikia kabisa na yule anayeisikia haki wala asiitumie; kama vile Aya hii tuliyo nayo:

59

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Asiyesikia ila wito na sauti tu

Na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-75.jpg

"Wanaokubali ni wale wanaosikia ..." Na kauli yake Mwenyezi Mungu:

(6:36).

Kaashif2-76.jpg

"Wala msiwe kama wale wanaosema: Tumesikia, na kumbe hawasikii." (8:21)

Unaweza kuuliza kuwa dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewafananisha Makafiri na Mchungaji wanyama sio wanyama; kwa vile amesema: Na mfano wa wale waliokufuru nikama mfano wa yule anayemwita asiyesikia. Inavyoelekea nikuwa anayeita ni mchungaji na asiyesikia ni mnyama, sasa imekuwaje?

Jibu: Hapa kuna kukadiriwa maneno ambako ni hakika mfano wa wanaowalingania makafiri kwenye haki ni kama mfano wa anayemwita asiyesikia. Hili limefahamika kutokana na mfumo wa maneno ulivyo.

60

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-77.jpg

172. Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyowaruzuku                na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa mnamwabudu Yeye tu.

173. Hakika amewaharamishia mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichosomewa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi aliye-fikwa na dharura bila kuta-mani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, Mwenye kurehe-mu.

KULENI VIZURI

Aya 172-173

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwaambia watu wote kwa kauli yake "kuleni vilivyomo ardhini" amerudia kusema tena, lakini akiwahusisha waumini:

"Enyi mlioamini! kuleni vizuri tulivyowaruzuku."

Ili awabainishie kwamba imani sahihi sio kujizuia na vitu vizuri, kama wanavyofanya baadhi ya watawa, makasisi na wengineo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametuhalalishia kustarehe na maisha na neema

61

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

za kimwili na akatuamrisha kuzishukuru; na maana ya kuzishukuru ni kuz-itumia katika njia inayotakikana.

Amirul Muminin Ali (a.s.) anasema: "Uchache zaidi wa yanayowalazimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kutozitumia neema zake kwa kumwasi." Huenda wale wenye jaha na utajiri, wakapata onyo kutokana na hekima hii iliyo fasaha ili wasizame katika anasa iliyoharamishwa na kuwa na kiburi na kupetuka mipaka.

Hakika ameharamshia mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilisomewa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Hakuna mwenye shaka kwamba makusudio ya uharamu hapa ni uharamu wa kitendo ambacho ni kula sio uharamu wa kitu chenyewe. Kwani kitu hakiwezi kutajwa kwa uhalali na uharamu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja , katika Aya iliyotangulia, uhalali wa vinavyoliwa, hapa anatupa aina nne ya vilivyo haramu kuliwa:

1. Mfu: Ni kila mnyama aliyekufa bila ya kuchinjwa kisheria.

2. Damu: Makusudio ni damu iliyojitenga na nyama, kwa sababu iliyo pamoja na nyama inasamehewa.

3. Nguruwe: Nyama yake, mafuta yake na mwili wake wote, kinyume na anavyosema Daud Dhahiri aliposema: "Ni haramu nyama ya nguruwe tu, sio mafuta yake," kwa kuchukulia dhahiri ya tamko, eti Aya imetaja nyama tu. Ilivyo ni kwamba imetajwa nyama kwa sababu ndio inay-otumika zaidi.

4. Kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu: yule aliyetajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni sawa kuchinjwa kwa ajili ya masanamu matambiko, mazindiko au vitu vingine.

Hekima ya kuharamishwa aina tatu za kwanza ni kiafya ambayo watabibu wanaijua. Ama hekima ya kuzuia kile kilichotajiwa aisyekuwa Mwenyezi Mungu, ni ya kidini yenye lengo la kuchunga Tawhid na kumwepusha Mwenyezi Mungu na ushirikina.

Kwa ujumla ni kuwa ni wajibu kumtaja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wakati wa kuchinja. Mwenye kuacha kufanya hivyo kwa makusudi, basi alicho-

62

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

kichinja ni haramu, ni sawa iwe aliacha kwa kujua au kutojua. Ama aki-acha kwa kusahau, basi haiwi haramu. Inatosha kutajaAllahu Akbar au Al-hamdulillah au Bismillah au Lailaha illa Ilahu, n.k. Ufafanuzi zaidi unaweza kuupata katika vitabu vyetu vya Fiqh; kama vile kitabu chetu cha

Fiqh Imam Jaffar Sadiq (a.s.)

Unaweza kuuliza; Dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba hakukuharamish-wa isipokuwa aina hizi nne tu za vyakula, kwa sababu neno tu linafaa-hamisha mambo mawili:

Kwanza, kuthibitisha yale yanaelezwa ambayo hapa ni kuharamishwa vitu vinne.

Pili: Kukanusha ambako hapa ni kutoharamishwa vitu vingine ispokuwa vitu hivi vine tu; na ilivyo ni kuwa kuna vyakula vingine vilivyoharamish-wa; kama mbwa, wanyama wanoshambulia, wadudu, baadhi ya samaki. n.k.

Jibu: Ndio dhahiri ya Aya inafahamisha hivyo, lakini halitumiwi hilo baada ya kongamano la wanavyuoni na kuthibiti Hadith za Mtume. Hii siyo Aya pekee ambayo dhahiri yake imeachwa na kongamano la wanavyuoni kutokana na Hadith.

MWENYE DHARURA NA HUKUMU YAKE

Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi.

Mwenye dharura ni yule ambaye anahofia nafsi yake kufa ikiwa hatakula kitu cha haramu, anayehofia kuzuka maradhi au kuzidi maradhi, kuhofia madhara na adha juu ya nafsi nyingine yenye kuheshimiwa; kama vile mwenye mimba kuogopea mimba yake au mwenye kunyonyesha kumhofia mwanawe; au mwenye kulazimishwa kwa nguvu kula au kunywa kitu cha haramu, kwa namna ambayo kama hakufanya hivyo atapata adha ya nafsi yake au mali yake au utu wake.

Yote haya na mifano yake ni katika mambo yaliyosamehewa katika kutu-mia kitu cha haramu, lakini kwa kiasi kile tu kinachoweza kuondoa madhara. Kuanzia hapo ukawa mashuhuri msemo wa mafaqihi: "Dharura

63

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

hupimwa kwa kiasi chake". Hilo linafamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi." Mwenye kutamani ni yule anayefanya haramu bila ya dharura, na mwenye kupitisha kiasi ni yule anayepitisha kiasi cha haja.

174. Hakika wale wafichao aliyoy-ateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto:         wala

Mwenyezi                   Mungu

hatawasemesha siku ya Kiyama, wala hatawatakasa; na wao wana adhabu chungu.

175. Hao ndio walionunua upotevu kwa uongofu, na adhabu kwa maghufira. Basi ni ujasiri ulio-je wa kuvumilia Moto?

176. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ame-teremsha Kitabu kwa haki, na wale waliohitalifiana katika Kitabu (hiki) wamo katika upinzani ulio mbali.

Kaashif2-78.jpg

64

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

WAFICHAO ALIYOYATERMSHA MWENYEZI MUNGU.

Aya 174-176:

MAANA

Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo.

Inasemekana kuwa Aya hii imewashukia wale walioficha sifa za Muhammad (s.a.w.w) na Utume wake.

Kwa vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya, makusudio yatakuwa ni kwa kila mwenye kujua kitu chochote katika haki akakificha kwa kuleta tafsiri nyingine au kubadilisha kwa manufaa yake binafsi; awe ni Myahudi, Mkristo au Mwislamu. Kwa sababu tamko ni lenye kuenea na linalozingati-wa ni kuenea tamko si kuhusika sababu za kushuka kwake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtisha mpotevu huyu katika Aya nyingi; miongoni mwazo ni zile zilizotangulia (Aya ya 146 na 159) na zitakazofu-atia katika Sura Al-Imran, Nisa, Maida na Aya hii tuliyonayo. Zote hizo ni hasira za Mwenyezi Mungu na kiaga kikali cha adhabu na mateso.

Kwa sababu ni wajibu haki itukuzwe na kutangazwa kwa kila njia na kuon-doa mikanganyo yote ya kutofahamika. Vile vile kumpiga vita mwenye kuipinga kwa nguvu zote na kujitoa mhanga kwayo. Kwani hakuna msi-mamo wa dini, wala nidhamu au uhai isipokuwa kwa haki.

Hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto.

Yaani adhabu wanayostahili katika moto. Hiyo ni katika kuelezea kina-chosababishwa ambacho ni moto na kinachosababisha ambacho ni kula haramu. Ametaja matu-mbo, ingawaje inajulikana kuwa kula hakufanywi isipokuwa kwa ajili ya tumbo, ili kuonyesha kuwa linalowashu-ghulisha wao ni kujaza matumbo yao tu.

65

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya Kiyama.

Ni fumbo la kuachana nao na kuwakasirikia wala hatawatakasa na mad-hambi kwa kuwasamehe.

Hao ndio walionunua upotevu kwa uongofu.

Upotevu ni kufuata matamanio na uongfu ni kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu. Kubadilisha upotevu kwa uongofu ni kuathirika na batili kuliko haki.

Basi ni ujasiri ulioje wa kuvumilia moto?

Huku sio kuelezea ujasiri wao kwa moto wala sio kustaajabu kunakotokana na kutojua sababu ya jambo, hilo haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kwani anajua kila kitu. Isipokuwa makusudio hapa ni kuonyesha namna ya kujitia ujasiri kwao kwa kuacha hukumu zake na mipaka yake, na kufuata upotevu na batili.

Kwa hiyo makusudio ni kuleta picha ya hali yao hiyo na kufananisha mare-jeo yao ambayo haiwezekani kuyafanyia ujasiri kwa vyovyote. Razi anase-ma: "Walipojiingiza kwenye lile linalowajibisha moto, wamekuwa kama wenye kuridhia adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwa majasiri wa adhabu hiyo; sawa na kumwambia yule anayejiingiza kwenye lile linalo kasirisha serikali: Ni ujasiri ulioje wako kufungwa jela?

Unaweza kuuliza: Tumejua hiyo ndiyo hali ya yule mwenye kuijua haki na akaificha; sasa ni ipi hali ya asiyejua chochote katika yalivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, lakini pamoja na hayo anasema: Hii ni haramu na hiyo ni halali, na wala hana chochote cha kutegemea isipokuwa dhana na kuwazia tu?

Jibu: Huyu ana hali mbaya zaidi kuliko yule anayeijua haki na akaificha. Kwa sababu yeye amejiweka daraja ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kuji-fanya ndio msingi wa sharia, wa kuhalalisha na kuharamisha.

66

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

MVUTANO KATI YA HAKI NA BATILI

Mwenye tafsir ya Al-Manar amemnakili Sheikh Muhammad Abduh kwamba amesema katika kuifasiri Aya hii:

"Katika Waislamu kuna wanaoficha yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa kugeuza na kuleta taawili, sawa na wanavyofanya Mayahudi kuficha sifa za Mtume. Waislamu hawa wanatambua mivutano miwili inayopingana mvutano wa haki waliyoijua na mvutano wa batili waliy-oizoweya. Hayo yanawatingisha na kuwaathiri, na haya yanawapa kiburi na chuki. Akili zao zimeshinda yale waliyoyajua na nyoyo zao zimeshin-da yale waliyoyazowea, wakathibiti kwenye yale waliyoyazua; wakawa katika vita kati ya akili na dhamiri. Wakifikiria kesho (akhera), starehe za sasa (duniani) zinawatokea puani, lakini wanapoonja utamu wa wanay-ofanya wanasahau yatakayokuja. Je, huku kuhisi kuitweza haki na kui-nusuru batili sio moto unaowaka mbavuni mwao? Je thamani ya haki wanayoila si miti ya miba ambayo hainenepeshi wala kuondoa njaa?"

Hayo ni sahihi kwa upande wa baadhi ya wale wanaojitilia shaka katika dhamiri zao na kujilaumu, wakiwa wanafanya dhambi. Lakini wengine wamezoweya batili mpaka ikawa ni tabia yao, na kuliona adui kila lenye harufu ya haki na utu.

Wakati ninapoandika maneno haya ni mwezi June 1967. Katika mwezi huu ulio na shari, Israil imevamia baadhi ya sehemu za miji ya Waarabu kwa msaada wa Uingereza na Marekani, na wamewatoa watu majumbani mwao, wakawafukuza zaidi ya watu laki mbili na nusu (250,000), wakawachoma wake kwa waume na watoto kwa mabomu ya Napalm.

Wengi wameunga mkono fedheha hii na kufurahishwa nayo; wanatamani lau Israil ingeendelea na uovu wake. Mapenzi ya nafsi yamezidi akili na dhamiri zao mpaka zikaisha zote bila ya kubaki athari yoyote, wakawa sawa na wanyama. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaita kuwa ni watu wasio na akili; wasiofahamu na kwamba wao ni wanyama, bali ni wapotevu zaidi kuliko wanyama.

67

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki.

Hayo ni ishara ya adhabu itakayowashukia wale wanaoficha haki. Na, kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu", ni kubainishwa sababu za adhabu ambazo ni kuthubutu kwao kuwa wajasiri wa kuihalifu haki iliyokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Na wale waliohitalifiana katika kitabu wamo katika upinzani ulio mbali.

Wafasiri wamehitalifiana katika makusudio ya kauli hii. Wafasiri wengi, aki-wemo mwenye Majmaul Bayan wamesema ni makafiri; na namna ya kuhi-talifiana kwao hao makafiri ni kwamba kuna katika wao waliosema kuwa Qur'an ni uchawi, wengine wakasema ni utenzi na wengine wakasema ni vigano vya watu wa kale.

Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya waliohitalifiana ni Waislamu, kwamba wao baada ya kuafikiana kuwa Qur'an inatoka kwa Mwenyezi Mungu, wamehitilafiana katika kuifasiri na kuleta taawili; wakagawanyika kwenye vikundi. Ilitakiwa wao wawe na tamko moja kwa vile Qur'an ni moja.

Inawezekana kuwa makusudio ni makafiri, lakini sio kwa kuwa wengine walisema kuwa Qur'an ni uchawi, utenzi au vigano, bali ni kwamba wao ndio sababu pekee ya kuhitilifiana, kupigana na kuacha kuafikiana na tamko la haki kati yao na wale walioamini Qur'an.

68

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

177. Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu, lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na malaika na Kitabu na man-abii; na akawapa mali, akiwa aipenda ,jamaa na mayatima na masikini na mwananjia na waombao, na katika ukombozi wa watumwa; na akasi-mamisha swala na akatoa zaka; na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wanaokuwa na subira katika shida na dhara na katika wakati wa vita. Hao ndio waliosadikisha na ndio wenye takuwa.

Kaashif2-79.jpg

69

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ANATOA MALI AKIWA AIPENDA

Aya 177 LUGHA

Kila amali ya heri ni wema. Mwananjia ni msafiri asiyesafiri kwa maasia, akaishiwa na mali asiweze kurudi kwake. Madhara ni kila linalomdhuru mtu, iwe ni maradhi au kumkosa mpenzi, n.k.

MAANA

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameyataja mambo aliyoyazingatia kuwa ni nguzo ya wema, uchaji Mungu na imani ya kweli. Mambo hayo kuna yanayofungamana na itikadi, yanayofungamana na kutoa mali, yanayofungamana na ibada na yale yanayofungamana na akhlaq. Kabla ya kufafan-ua ameanza kwa kusema:

Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu.

Maneno haya waanaambiwa watu wote, hata kama sababu ya kushuka ni mahsusi. Kwa sababu, la kuzingatia ni hayo maneno kwa ujumla sio sababu za kushuka kwa Aya.

Makusudio ni kuwaambia waumini na wanaoswali, kwamba kuswali tu upande maalum, sio heri ya dini iliyokusudiwa. Kwa sababu swala imewekwa kwa ajili ya kuwa mwenye kuswali amwelekee Mwenyezi Mungu peke yake na kuachana na wengine.

Baada ya utangulizi huu, ameingilia kubainisha misingi ya itikadi ambayo ndiyo nguzo ya wema, na ameikusanya katika mambo matano ambayo yamekusanywa na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na Malaika na kitabu na Manabii.

70

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kumwamini Mwenyezi Mungu ndio msingi wa amali njema inayo sababisha kumtii Mwenyezi Mungu katika yote aliyoyaamrisha na kuyakataza. Kuamini Malaika ni kuamini wahyi ulioteremshwa kwa Mitume; na kuwakana Malaika ni kuukana wahyi; Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-80.jpg

"Ameiteremsha Roho mwaminifu juu ya moyo wako, ili uwe miongoni mwa waonyaji." (26: 193-194).

Kuamni Kitabu ni kuamini Qur'an na Manabii na kuamini sharia zao.

Mambo yote haya matano yanarejea kwenye mambo matatu; Kuamini Mwenyezi Mungu , Utume na siku ya mwisho. Kwa sababu kuamini Utume kunachanganya kuamini Malaika na kitabu.

Baada ya hayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaashiria taklifa za kimali kwa kauli yake:

Na akawapa mali akiwa aipenda

Imesemekana kuwa dhamiri katika kupenda inamrudia Mwenyezi Mungu, kwa vile limetangulia jina lake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika kauli yake: "Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu" Na imesemekana kuwa dhamiri inarudia mali na inakuwa kama kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-81.jpg

"Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda..." (3:92).

71

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Vile vile kauli yake:

Kaashif2-82.jpg

"Na huwalisha chakula masikini na mayatima na mateka na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda." (76:8).

Kauli hii ndiyo iliyo dhahiri zaidi, kwa sababu dhamiri inamrudia wa karibu zaidi, sio wa mbali. Kisha makusudio ya kutoa mali hapa sio zaka ya wajibu, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameunganisha na kutoa zaka na kuunganisha kunahukumilia kubadilika.

Aya imetaja aina sita za wale ambao inatakikana kuwapa: 1. Jamaa - Nao ni jamaa wa mwenye mali, kwa sababu wao ndio wenye haki zaidi ya kuwatendea wema. Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-83.jpg

"Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutoawapa akra-ba" (24:22).

Ni wajibu kumlisha jamaa aliye karibu, ikiwa ni mzazi na mtoto, ikiwa wanashindwa kujilisha. Ama wasiokuwa hao inakuwa kuwapa ni Sunna sio wajibu, kama wanavyosema Mafaqihi.* 2

*

2

Hanafi wanasema : Ni wajibu mtu kuwalisha jamaa zake wa karibu asioweza kuwaoa. Hanbal wamesema: Ni sharti mlishaji awe ni mrithi wa anayelishwa.

Malik wanasema: Si wajibu kulisha isipokuwa baba, mama na watoto wa kuwazaa tu, sio ndugu wengine. Shia Imamiya na Shafii wanasema: Ni wajibu kuwalisha wazazi, mababu na kuendelea juu na watoto, wajukuu na kuendelea chini.

72

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

2. Mayatima - ambao hawana mali wala mlezi wa kuwatunza. Kwa hiyo itakuwa ni wajibu kwa wenye uwezo kuwalea, ikiwa hakuna hazina ya Waislamu (Baitul-maal).

3. Maskini - wale wenye haja ambao hawawanyooshei watu mkono wa udhalili (hawaombi).

4. Mwananjia - Yule ambaye ameishiwa safarini asiyeweza kurudi kwao bila ya msaada.

5. Wenye kuomba wale ambao wanawa-nyooshea watu mikono ya udhalili. Jambo hilo limeharamishwa kisheria isipokuwa kwa dharura ya hali ya juu; sawa na dharura ya kula mfu. Dalili tosha ya uharamu wake ni kwamba ni udhalili na utwevu, na udhalili huo wenyewe ni haramu uwe umetokana na mtu mwengine au na yeye mwenyewe.

Kuna Hadith inayosema: "Si halali kupewa sadaka tajiri na mwenye nguvu aliye mzima wa mwili."

6. Watumwa- Yaani kununua watumwa na kuwaacha huru kwa kuwakom-boa utumwani. Lakini maudhui haya hayapo siku hizi kutokana na kutokuwepo utumwa.

Kwa ujumla aina hizi sita alizozitaja Mwenyezi Mungu ni kwa njia ya mfano, sio kwamba hizo ndio zote. Yako mambo mengi ambayo ni vizuri kuyatolea mali; kama kujenga shule, vituo vya mayatima, mahospitali, kuilinda dini na nchi na mengineyo yanayohusu Umma kwa ujumla.

Ikiwa heshima ya mtu itavunjika isipokuwa kwa kutoa mali, basi ni wajibu kuitoa kwa mwenye kuweza; na lolote ambalo wajibu fulani hauwezi kutekelezeka isipokuwa kwa kufanya jambo hilo, basi ni wajibu kulifanya.

Mwenyezi Mungu ameashiria nguzo ya kutenda wema ya kiibada kwa kauli yake:

73

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na akasimamisha Swala na akatoa Zaka.

Swala ni ya kutakasa nafsi, Saumu ni ya kutakasa mwili na zaka ni ya kutakasa mali.

Ameashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye nguzo ya maadili kwa kuse-ma:

Na watekelezao ahadi zao wanapoahidi.

Ahadi inayopaswa kutekelezwa iko namna mbili. Ya kwanza, ni ile inayokuwa kati ya mja na Mola wake; mfano Yamini Nadhiri na ahadi kwa sharti zilizotajwa katika vitabu vya Fiqh. Hayo tumeyafafanua katika Juzuu ya tano ya Kitabu Fiqhul-Imam Jaffar Sadiq (A.S).

Ya pili, ni aina ya ahadi ya muamala unaopita kati ya watu. Ni wajibu kuitekeleza; kama vile bei, ajira, deni n.k.

Mumini mwema anatekeleza mambo yote yanayomlazimu; hata kama hakuna uthibitisho wa kulazimisha kutekeleza. Ama kutekeleza kiaga sio wajibu kisheria, bali ni Sunna Kifiqh

Miongoni mwa tabia nzuri zenye kusifiwa ni subira (uvumilivu) ambayo ni katika nguzo za wema, yenye kuonyeshwa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na kuwa na subira katika shida na dhara na wakati wa vita.

Shida ni ufukara, na dhara ni maradhi, n.k. Makusudio ya kuvumilia ufukara na maradhi sio kuyaridhia, kwani Uislamu umewajibisha kuhangaika na kufanya juhudi kwa kadri iwezekanavyo, ili kujitoa katika ukata, maradhi, ujinga, na kila linalorudisha nyuma maendeleo.

Makusudio yake hasa ni kutosalimu amri kabisa katika shida na kuwa na mshikamano na kufanya kazi kwa uthabiti na bidii ili kujikwamua na yaliy-owapata. Baadhi ya wafasiri wanasema: "Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja uvumilivu katika mambo matatu: (ufukara, maradhi na vita), pamo-

74

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ja na kuwa uvumilivu unatakiwa katika hali zote, kwa sababu hali hizo tatu ni miongoni mwa balaa na mitihani mikubwa. Mwenye kuvumilia hayo, basi anaweza kuvumilia mengine.

Hao ndio waliosadikisha na ndio wamchao Mungu.

"Hao" ni ishara ya wale ambao wamekusanya mambo yote haya yaliyota-jwa - misingi ya itikadi, kutoa mali, kutekeleza ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na tabia nzuri. Hakika hao ni wakweli katika imani yao, wenye kuogopa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake.

Ama wale wanaosema kwa vinywa vyao tu, kuwa tumeamini na wala wasitoe wanayoyapenda wala kutekeleza yanayowalazimu na kuvumilia katika shida. Wote hao wako mbali na wema.

WEMA KATIKA UFAHAMU WA KIQUR'AN

Aya hii imeonyesha mambo matano: Itikadi, taklifa za kimali, ibada, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida. Haya mambo mawili ya mwisho ni katika mambo ya kimaadili.

Kwa dhahiri ni kwamba ibada, kama swala na saumu ni athari ya imani na ni alama yake isiyoepukika nayo. Kwa sababu asiyeamini kuwapo Mungu, hawezi kumwabudu.

Ama kutoa mali, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida, hayo yanapatikana kwa anayemwamini Mwenyezi Mungu au kwa anayemkanusha. Kwani wengi wanaomwamini Mungu wanasema wasiyoyatenda, ni wabahili; hata kwenye nafsi zao na wanasalimu amri mbele ya shida. Lakini mara nyingine mkanushaji Mungu huweza kujitolea mhanga katika kupigania uadilifu na utu, anakuwa imara katika shida na kutekeleza anayoyasema.

Kwa hivyo, kidhahiri, inaonyesha kuwa imani hailazimiani na tabia njema wala kufuru hailazimiani na tabia mbaya. . . lakini ilivyo hasa hakuna imani bila takuwa (kumcha Mungu).

75

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Lakini Aya hii (sio wema ...). Imezingatia imani kuwa pamoja na tabia njema bila ya kutengana, kwa maana yakuwa sio kumwamini Mungu pekee ndiko kutakakomfanya mtu kuwa mwema; wala tabia nzuri bila ya imani haiwezi kumfanya mtu awe mwema, bali hapana budi kumwamini Mwenyezi Mungu, kuwa na tabia njema na kumwabudu. . . Kwa hivyo basi 'mwema' anavy-oelezwa katika Qur'an ni Mumin mwenye kufanya ibada, mtekelezaji ahadi, mkarimu na mvumilivu.

178. Enyi                     mlioamini!

Mmeandikiwa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesame-hewa na ndugu yake cho-chote, basi ni kufuatana kwa wema na kulipa kwa ihsani. Hiyo ni tahfifu itokayo kwa Mola wenu na rehema. Na atakeyeruka mipaka baada ya hayo, basi ana yeye adhabu iumizayo.

179. Mna uhai katika kisasi, enyi wenye akili, ili msalimike.

Kaashif2-84.jpg

76

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

KISASI CHAWALIOUAWA

Aya 178 - 179

MAANA

Wanavyuoni wa sharia ya Kiislamu wamepanga namna tatu za adhabu:

1. Haddi; kama kukata mkono wa mwizi, kupigwa mawe hadi kufa kwa mzinifu aliye na mke, kupigwa viboko kwa mnywaji pombe, n.k. Utakuja ufafanuzi mahali pake Inshallah.

2. Diya (Fidia): Hiyo ni adhabu ya kimali.

3. Kisasi - kufanyiwa yule aliyefanya jinai kwa makusudi sawa na vile alivyomfanyia yule aliyemuua, au aliyemkata kiungo au aliyemjeruhi. Ama kupiga hakuna kisasi. Mafaqihi wameweka maelezo maalum kwa kila namna ya adhabu hizo tatu, na Aya hii inaingia katika kisasi.

Enyi mlioamini! mmeandikiwa kisasi katika waliouawa.

Wakati wa ujahiliya (kabla ya Uislamu) watu walikuwa hawana sheria yenye mpango; wanauana kidhulma na kiuadui, na kulipiza kisasi kwa watu wasiokuwa na hatia na wala sio kwa yule aliyekosa. Mtu wa kawai-da akiuawa, basi watu wake wataua idadi kubwa ya watu wa muuaji. Na, kama mwanamke akimuua mwanamke mwenzake, basi mahali pake pat-achukuliwa na watu wa ukoo wake au kabila yake; wanaweza kuua hata watu kumi kwa mmoja tu.

Dhuluma hii ilisababisha vita vya kikabila; watoto na wajukuu wakarithi uadui na chuki. Ndipo Mwenyezi Mungu akaweka sharia hii ya kisasi ambayo inafahamisha usawa na kisasi kiwe kwa yule aliyeua kwa hali yoy-ote awayo na wala sio watu wasiokuwa na makosa, na pia kusiweko na ziada au upungufu; kinyume na ilivyokuwa zama za ujahiliya. Na kwa sharti ya kuwa kuua kuwe ni kwa kukusudia sio kwa kukosea au bila

77

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

kukusudia.*

Katika maana Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"...Nafsi kwa nafsi..."

(5:45).

Kaashif2-85.jpg

"...Lakini hiyo asipite kiasi katika kuua..."

(17:33).

Kaashif2-86.jpg

"Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na huo..." (42:40).

Kaashif2-87.jpg

"...Basi anayewachokoza mchokozeni kwa kadiri alivyowachokoza..." (2:194).

Muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke.

Maana yake yako wazi hayahitaji ufafanuzi. Hiyo ni ibara ya usawa katika kisasi kati ya muuaji na aliyeuliwa katika uhuru, utumwa na jinsia.

Kuua kwa makusudi ni kukusudia kitendo na kuua; kama mtu kumchoma kisu mwengine kwa kukusudia kumchoma na kumuua au kakusudia kitendo cha kuua tu, kama kukusudia kumchoma katika moyo wake lakini bila ya kukusida kuua. Hayo ni mauaji ya kukusudia. Ama kuua kwa makosa, ni kukosea katika kusudio lake na kitendo chake; kama mwenye kukusudia kumfuma mnyama akampata mtu, hapo mtu siye aliyekusudiwa kufumwa wala kuuliwa. Kuua bila ya kukusudia ni kukusudia kitendo, lakini sio kuua; kama anayempiga mtoto kumtia adabu, akafa; hapo tendo la kupiga limekusudiwa, lakini mauti hayakukusudiwa. Katika hali hizi mbili (Kuua kwa makosa na kuwa bila ya kukusudia) hakuna kisasi isipokuwa fidia tu.

78

Kaashif2-88.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Unaweza kuuliza kuwa: Ufahamisho wa mfumo wa tamko unaonyesha kuwa muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa. Na kama mwanamume akimuua mwanamke hauawi, Je wameafikiana Mafaqihi?

Jibu: Hakika Aya imeonyesha aina tatu tu ambazo ni muungwana kumuua muungwana, mtumwa kumuua mtuwa na mwanamke kumuua mwanamke, na haikueleza aina ya nne ambayo ni muungwana kumuua mtumwa au mtumwa kumuua muungwana na mwanamume kumuua mwanamke au mwanamke kumuua mwanamume.

Aya imefahamisha kwa matamko yake kwamba kisasi kimewekwa katika aina tatu za kwanza; na hayo wameafikiana Mafakihi, kwa sababu katika dhahiri ya Qur'an hakuna kuhitalifiana. Vile vile Aya haikukanusha au kuthibitisha kisasi katika aina nyingine, si kwa kimatamko wala kiufa-hamu. Kwa hiyo hapana budi kurejea kwenye dalili nyingine ya Hadith au ijmai.

Mafaqihi wamehitalifiana katika hilo:

Malik, Shafii na Hambal wanasema: Muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa.

Abu Hanifa anasema: Bali atauawa muungwana kwa kumuua mtumwa wa mtu mwingine, lakini hauawi kwa kumuua mtumwa wake. Wameafikiana wote wanne kwamba mwanamume atauawa kwa kumuua mwanamke na kinyume chake.

Shia Imamia wamesema: "Muungwana akimuua mtumwa hauawi, bali atapigwa kipigo kikubwa na kutoa fidia ya mtumwa. Na mwanamke akiua mwanamume, watu wa aliyeuawa wanayo hiyari ya kuchukua fidia, kama huyo muuaji akikubali au kumuua. Kama wakichagua kuua, hapo watu wake hawatatoa chochote. Kama mwanamume ndiye aliyemuua mwanamke, basi watu wake wanayo hiyari ya kuchukua fidia kama muuaji akikubali au kumuua kwa masharti ya kuwapa warithi wa yule aliyeua nusu ya fidia ya mwanamume ambayo ni Dinar mia tano (500).

79

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na anayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwa wema; na kulipa kwa ihsani.

Neno "chochote" linafahamisha kwamba walii wa aliyeuawa, akisamehe chochote kinachofungamana na muuaji, kama kusamehe kumuua na kuridhia kuchukuwa fidia, basi inatakikana muuaji aukubali msamaha huu kwa wema. Imesemekana pia kuwa neno chochote linafahamisha kuwa, kama warithi wakiwa wengi na mmoja wao akamsamehe muuaji, basi hakuna kisasi, hata kama waliobakia watang'ang'ania kutaka kisasi.

Vyovyote iwavyo, hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kwa walii wa damu iliyomwagwa haki ya kisasi kutoka kwa aliyeua kwa makusudi. Haifai kum-lazimisha muuaji atoe fidia ikiwa mwenyewe anataka kuuliwa, wala muuaji hawezi kumlazimisha walii wa aliyeuawa kuchukua fidia ikiwa mwenyewe anataka kulipiza kisasi cha kuua.

Inaruhusiwa kwa wote wawili kuafikiana kwa kufanyiana suluhu ya kiasi cha mali ya fidia, kiwe kichache au kingi, ili kiwe ni badala ya kisasi. Maafikiano hayo yakitimia basi itakuwa ni lazima kutekelezwa na wala haiwezekani kubadilisha.

Ni juu ya walii wa aliyeuawa kumtaka muuaji badala ya kisasi kwa wema, bila ya kumtilia mkazo wala kumdhikisha au kuomba zaidi ya haki yake. Na ni juu ya muuaji kutoa mali kwa wema, bila ya kuchelewesha, kupunguza au kufanya hadaa yoyote.

Hiyo ni tahfifu itakayo kwa Mola wenu.

Yaani hekima ya kuwekwa fidia badala ya kisasi ni tahfifu na rehema

kwenu.

Na atakayeruka mipaka baada ya hayo, basi yeye ana adhabu iumiza-

Walikuwa baadhi ya watu wakati wa ujahiliya, wanaposamehe na kuchukua fidia, kisha wanapompata muuaji baadaye humuua. Hapo

80

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu akakataza kupetuka mipaka huku na akamwahidi adhabu iumizayo mwenye kuyafanya hayo.

Baadhi ya wafasiri wanasema: Hakimu atamhukumu kuuliwa aliyemuua muuaji baada ya kupita msamaha; hata kama atatoa fidia na kuridhia walii wa aliyeuliwa. Lakini kauli hii ni ya kuonelea uzuri hivyo tu, na wala Aya haifahamishi hilo si kwa karibu wala mbali.

Mna uhai katika kisasi enyi wenye akili.

Hii ni sababu ya kuwekwa sharia ya kisasi na kubainisha hekima, na kwamba katika hukumu hiyo kuna kulinda kufanyiana uadui. Kwani mwenye kujua kwamba yeye atauliwa baada ya kuua, ataogopa. Ama kutoa mali sio kuzuia kuua, kwani watu wengi wangeliweza kutoa mali kwa sababu ya kuwakomoa maadui zao.

Wafasiri wamerefusha maneno katika kubainisha ufasaha wa Aya hii na kuilinganisha na msemo unaosema; "Kuua ni kinga ya kuua." Baadhi yao wametaja njia sita, Alusi ameongeza mpaka kufikia kumi na tatu na waliokuja baada ya Alusi nao wakaongeza zao. Njia zote hizo zinarudia kwenye utafiti wa matamshi tu.

81

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

180. Mmeandikiwa, mmoja wenu anapofikwa na mauti kama akiacha mali, kuwausia kitu wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri inayokubalika. Ni haki haya kwa wenye takua.

181. Na atakayeubadilisha (wasia) baada ya kuusikia, basi dham-bi yake ni juu ya wale watakaobadilisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.

182. Mwenye kuhofia mwusiaji kwenda kombo au dhambi, akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira Mwenye kurehe-mu.

WASIA KWA WAZAZI

Aya 180-182 LUGHA

Neno "Khayri" lina maana ya kinyume cha shari, na makusudio ya neno Khayr hapa ni mali. Inasemekana kuwa kila linapokuja neno Khayr kati-ka Qur'an linakuwa makusudio yake ni mali; kama ilivyo katika Sura

Kaashif2-89.jpg

(11:84 ) (24:33), (100:8), , n.k.

* 4

82

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

MAANA

Mmeandikiwa, mmoja wenu anapofikiwa na mauti kama akiacha mali, kuwausia wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri inayokuba-lika.

Aya hii ni miongoni mwa Aya za hukumu, na inaingia katika mlango wa wasia. Kauli za mafaqihi na wafasiri zimekuwa nyingi na kugongana kuhusu Aya hii. Miongoni mwa kauli hizo ni kama zifuatazo:-

• Ikiwa mtu ana mali na akaona dalili za mauti, basi ni wajibu kwake kuu-sia kitu katika mali yake kwa wazazi wawili na ndugu wa karibu, hata kama wao ndio watakaoirithi; atawakusanyia urithi na wasia.

• Wasia ni wajibu kwa jamaa zake wakiwa sio warithi.

• Wasia kwa akraba ni sunna tu, na wala si wajibu.

• Kuwausia warithi haki yao na viwango vyao vya kurithi. Kwa hivyo Aya itakuwa inapita mapito ya Aya inayosema:

"Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu; fungu la mwanamume

Kaashif2-90.jpg

ni kama fungu la wanawake wawili." (4:11).

• Wasia utakuwa ni wajibu kwa jamaa ikiwa mali ni nyingi.

• Aya ni Mansukh (haitumiki hukumu yake) kwa Aya ya urithi. Na mengineyo zaidi ambayo hayategemewi kabisa.

Kauli hii nimeikuta katika baadhi ya vitabu vya tafsiri nilivyonavyo, lakini inaping-wa na Aya inayosema:"Aya yoyote tunayoifuta au kuisahauliza tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake ..."(2 : 106) Ambapo hapa kuna neno Khayr lililotumiwa kwa maana ya Aya iliyo bora sio mali.

83

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

KUWAUSIA WARITHI

Sunni na Shia wametofautiana katika kuswihi wasia kwa warithi. Wakaafikiana madhebu mane kuwa hauswihi, wakitegemea hadith ise-mayo: "Hakuna wasiya kwa warithi". Shia Imamia wameafikiana juu ya kuswihi wasia kwa warithi na wengineo, kwa kutothibiti Hadith hiyo kwao, na kwamba dalili ya kuswihi wasia inachanganywa kwa ujumla na wasia kwa warithi; kuongezea riwaya mahsusi kutoka kwa Ahlul Bait (a.s.). Dalili yenye nguvu ya kuswihi wasia kwa warithi ni Aya hii tuliyo nayo. Allama Hilli katika kitabu At Tadhkira anasema:

"Wasia kwa warithi unafaa kwa kauli za wanavyuoni wetu wote, ni sawa warithi wamekubali au la. Hilo ni kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye Aya hizi tulizo nazo.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amewajibisha kuwausia wazazi wawili, kwa sababu wao ndio akraba (jamaa wa karibu) zaidi wa maiti, kisha akasema kutilia mkazo wajibu huo: "Ni haki haya kwa wenye takua" yaani anamwambia yule ambaye hayaitakidi haya, kuwa si katika wamchao Mungu. Tena akatilia mkazo kwa mara ya pili kwa kauli yake: "Na atakayeubadilisha baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha." Mwisho akaitilia mkazo jumla hii kwa kusema: "Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mjuzi".

Unaweza kuuliza: Shia wamesema, inajuzu kuusia, na wala hawakusema ni lazima, pamoja na kuwa Aya mmeandikiwa kwa maana ya imesema mmewajibishiwa, kwa hivyo basi Shia wameihalifu Aya kama walivyoi-halifu Sunni kwa kusema kuwa hauswihi wasia kwa warithi?

Jibu: Wameafikiana Waislamu wote kwamba kutoa hukumu ya sharia katika Qur'an, hakufai ila baada ya kuangalia Hadith za Mtume, na baada ya kufanya utafiti wa Ijmai vile vile. Kama hakuna Hadith wala Ijmai katika maudhui ya Aya, basi inajuzu kutegemea dhahiri ya Aya.

Imethibiti katika Hadith na Ijmai kwamba wasia kwa akraba sio wajibu, kwa hivyo hapana budi kuichukulia Aya kuwa ni Sunna katika wasia na wala sio wajibu, na yanakuwa maana ya "Ni haki kwa wamchao Mungu",

84

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

kwamba Sunna hii ni yenye kuthibiti kwa haki, kwa sababu maana ya haki ni kuthibiti.

Makusudio ya "Namna nzuri inayokubalika"

Ni kuwa kitu chenye kuusiwa kinanasibiana na hali ya mwenye kuusia na mwenye kuusiwa; kisiwe kichache cha kudharaulika, wala kisiwe zaidi kuwadhuru warithi; yaaani kisizidi theluthi ya mali itakayoachwa na mare-hemu. Kuna Hadith inayosema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewapa theluthi ya mali yenu wakati wa kufa kwenu."

Na atakayeubadilisha baada ya kuusikia.

Yaani atakayebadilisha wasia na kuugeuza na hali anajua. Basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha;

Yaani dhambi ya kubadilisha, itamwangukia yule mwenye kubadilisha, awe ni mrithi, walii, hakimu, wasii au shahidi. Hii ni dalili kwamba mwenye kufanya dhambi ni juu yake mwenyewe peke yake. Ikiwa mare-hemu alimuusia mtu ambaye anamwamini kuwa atamtekele-zea haki ya Mwenyezi Mungu au ya watu aliyonayo, halafu aliyeusiwa akafanya uzembe au hiyana, basi maiti hana dhambi yoyote isipokuwa dhambi iko juu ya yule aliyeusiwa.

Razi anasema: "Wanavyuoni wameitolea dalili Aya hii, kwamba mtoto mdogo hawezi kuadhibiwa kwa ukafiri wa baba yake. Na haya ni katika mambo yaliyo wazi kiakili ambayo Qur'an imeyathibitisha kwa mifumo mbali mbali; kama Aya inayosema:

"Wala hatabeba mbebaj i mzigo wa mtu mwingine." (35:18).

Mwenye kuhofia muusiaji kwenda kombo au dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi.

Kupata dhambi hapa kuna maana ya kukusudia dhulma. Aya hii inavua hukumu ya Aya iliyotangulia; yaani mwenye kubadilisha wasia atakuwa na

85

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

dhambi, isipokuwa kama mwusiaji amekosea katika wasia wake. Hapo ita-juzu kwa wasii au walii au hakimu kubadilisha batili kuiweka kwenye haki, sio kubadilisha haki. kwenye batili

Hayo ndiyo waliyoyataja wafasiri kuhusu maana ya Aya; nayo ni sahihi hayo yenyewe, lakini yale tunayoyafahamu kutokana mfumo mzima wa Aya, na kuyathibitisha mwenye Majmaul-Bayan, ni kwamba mtu akitoke-wa na dalili za mauti na akausia mambo ambayo ndani yake mna dhuluma; kama kuwapa wengine na kuwanyima wengine, na katika wasia huo wakahudhuria watu wenye akili na waumini, basi itakuwa hakuna dhambi kwa yule aliyehudhuria kumwonyesha haki mwusiaji na kusuluhisha kati yake na warithi wake, ili wote wawe wameafikiana na kuridhia, wala usizuke baina yao ugomvi na migongano baada ya kufa mwusiaji.

183. Enyi                    mlioamini!

Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuwa na takua.

184. Siku maalum za kuhisabika. Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi, au yuko safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine. Na wale wanaoweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha maskini.         Na

atakayefanya heri kwa kuji-tolea, basi ni bora kwake. Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.

Kaashif2-91.jpg

86

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

185. Ni mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa katika mwezi huo Qur'an, kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi.                   Basi

atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge; na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi wala hawatakii yaliyo mazito, na mkamilishe hisabu hiyo, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongoza, na ili mpate kushukuru.

MMELAZIMISHWA KUFUNGA

Aya 183 -185

MAANA

Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu.

Saumu ni miongoni mwa ibada muhimu, na ni katika dharura za dini, kama ilivyo wajibu Swala na Zaka. Katika Hadith imesemwa: "Uislamu ume-jengwa katika mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwam-

Kaashif2-92.jpg

87

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ba Muhammad ni Mtume wake (shahada), kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga mwezi wa Ramadhan na kuhiji Makka kwa anayeweza.

Mafaqihi wametoa fatwa kwamba yeyote mwenye kukana wajibu wa saumu, basi amekuwa murtadi (si Mwislamu tena) na ni wajibu kumuua. Na mwenye kuamini kuwa saumu ni wajib, lakini akaiacha kwa kupuuza ataaziriwa kutokana na vile anavyoona hakimu wa sharia. Kama akirudia ataaziriwa mara ya pili. Akirudia tena atauawa, wengine wamesema atauawa mara ya nne.

Saumu ni ibada ya zamani aliyoifaradhisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa watu waliotangulia, kwa namna inayotofautiana na yetu sisi Waislamu, kwa kiasi chake namna yake na wakati wake. Kufananishwa hapa kumekuja kwa uwajibu tu, bila ya kuangalia sifa, idadi ya siku na wakati wake. Na kufananisha kitu sio lazima kiwe sawa kwa njia zote.

Ili mpate kuwa na takua.

Wafasiri wengi wamesema kuwa jumla hii inaonyesha hekima ya saumu ambayo ni mazoezi ya mwenye kufunga kuweza kuthibiti nafsi, kuacha matamanio ya haramu na kuwa na subira (uvumilivu). Hadith inasema: "Saumu ni nusu ya subira." Imam Amirul Mumini (a.s.) anasema: "Kila kitu kina zaka (utakaso) na zaka ya mwili ni kufunga." Amesema tena: "Mwenyezi Mungu amefaradhisha saumu kwa majaribio ya ikhlasi ya viumbe..."

Kimsingi, ni kwamba kila maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake ni majaribio ya ikhlasi ya viumbe, lakini saumu ina taklifa kubwa, kwa sababu kuna kushindana na nafsi na kupambana, kuweza kuidhibiti na mambo inayoyapendelea ambayo ni chakula, kinywaji na matamanio ya kimwili.

Kwa siku maalum za kuhisabika

Hizo ni siku za Ramadhan, kwa sababu Mwenyezi Mungui hakutufarad-hishia zaidi ya Ramadhan.

Kaashif2-93.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi, au yuko safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine. Na wale wanaoweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha maskini.

Mwenyezi Mungu ametaja katika Aya hii mambo matatu ya kuruhusiwa kufungua Ramadhan ambayo ni Maradhi, Safari na Uzee.

Maradhi anayoruhusiwa mtu kufungua ni kuwa mtu ni mgonjwa ambaye kama atafunga maradhi yake yatazidi, au kuzidi siku za ugonjwa. Au pengine ni mzima, lakini anaogopa kama atafunga atazukiwa na maradhi mapya. Ama udhaifu tu, hauwezi kumruhusu mtu kufungua, madamu anaweza kustahmili na mwili wake uko salama. Ikiwa mgonjwa atang'ang'ania kufunga pamoja na kuthibitika madhara, basi saumu yake itakuwa batili na ni wajibu kwake kulipa sawa na aliyefungua bila udhuru.

Imethibiti kwa upande wa Sunni na Shia kwamba Mtume (s.a.w.w) ame-sema ; "Si wema kufunga safarini", Katika Tafsir Al-Manar imekuja Hadith mashuhuri iliyopokewa kutoka kwa Mtume mtukufu: "Mwenye kufunga safarini ni kama mwenye kufungua akiwa nyumbani."

Katika waliotaja Hadith hii ni Ibn Maja na Tabari. Razi anasema: "Wanavyuoni wa kisahaba wamesema kuwa ni wajibu kufungua kwa mgonjwa na msafiri kwa hali yoyote ile kutokana na kutokuwepo amri ya kufunga. Na hiyo ndiyo kauli ya Ibn Abbas na Ibn Umar. Vile vile Daud bin Ali Al-Asfahani.

Kutokana na hali hiyo, kufungua safarini ni wajibu na wala sio ruhusa tu, Yaani haifai kufunga kwa msafiri kwa hali yoyote ile kutokana na kutokuwepo amri ya kufunga. Dalilli yenye nguvu zaidi juu ya hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewajibisha kulipa kwa safari kwa namna ile ile aliyowajibisha kwa maradhi, pale aliposema: Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au yuko safarini, basi (atimize) hisabu katika siku nyingine

Na wala hakusema ukitaka fungua (utimize ) hisabu katika siku nyengine.

89

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na kukadiria hivyo ni kinyume na dhahiri; wala hakuna haja ya kukadiria mambo mengine ikiwa maana yanasimama bila ya kukadiria.

Ama ruhusa ya tatu ya kufungua, ni uzee. Mwenyezi Mungu ameonyesha hilo kwa kauli yake: "Na wale wanaoweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha masikini."

Hukumu hii inamhusu mzee aliye dhaifu kwa sababu ya ukongwe awe mume au mke. Kuweza kwa shida ni kufanya kitu kwa shida na mashaka sana. Huyu anahiyarishwa kati ya kufunga au kufungua pamoja na kutoa fidia ambayo ni kuwalisha maskini. Kuna Hadith sahihi kuhusu hilo kuto-ka kwa Ahlul Bait (a.s.)

Na atakayefanya heri kwa kujitolea basi ni bora kwake.

Yaani mwenye kuzidisha kulisha zaidi ya maskini mmoja au kumlisha masikini mmoja zaidi ya kiasi cha wajibu, basi ni bora kwake. Anayo hiari ya kumwita maskini muhitaji amlishe mpaka ashibe au ampe chakula cha unga au nafaka anachokula, kiasi kisichopungua gramu mia nane (800gm). Inaruhusiwa kumpa pesa zenye thamani ya chakula kwa sharti ya kumwambia: "Ifanye ni thamani ya chakula chako."

Na kufunga ni bora kwenu.

Yaani mzee mume au mke walio wakongwe, ingawaje wana hiyarishwa kati ya kufungua na kufunga, lakini wakihiyari kufunga, ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kufungua na kutoa fidia.

Ni mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa katika mwezi huo Qur'an.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Mwenyezi Mungu alipohusisha kufunga katika mwezi wa Ramadhan, amebainisha kwamba hekima katika hili ni kuwa Qur'an, ambayo juu yake ndio kuna mzunguuko wa dini na imani, iliteremshwa katika mwezi huo.

90

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kisha akanakili mwenye Majmaul-Bayan kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwa njia ya Sunni na Shia kwamba: Sahifa za Ibrahim (a.s.) ziliteremshwa siku ya tatu ya mwezi wa Ramadhan, Tawrat ya Musa (a.s.) siku ya sita, Injil ya Isa (a.s.) siku ya kumi na tatu , Zaburi ya Daud (a.s.) siku ya kumi na nane na Qur'an ilimshukia Muhammad (s.a.w.w) siku ya ishirini na nne.

Unaweza kuuliza: Hakika kauli yake Mwenyezi Mungu. "Ni mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa katika mwezi huo Qur'an" kwa dhahiri inafahamisha kuwa Qur'an imeteremshwa yote katika mwezi wa Ramadhan na inavyojulikana ni kuwa Qur'an iliteremshwa kwa vipindi katika muda wote wa Mtume ambao ni miaka ishirini na tatu?

Jibu: Makusudio ni kwamba kushuka kwake kulianza katika mwezi wa Ramadhan, sio kwamba imeteremshwa yote katika mwezi huo. Na usiku ambao ilishuka Qur'an unaitwa Laylatul-Qadr, yaani, usiku wa cheo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

"Hakika sisi tumeiteremsha (Qur'an) katika usiku uliobarikiwa ..." (44:3).

Zaidi ya hayo ni kwamba msahafu unaitwa Qur'an na sehemu yake pia inaitwa Qur'an.

Ama kauli ya anayesema kwamba Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'an kutoka Lawhil-Mahfudh, iliyoko juu mbingu ya saba, na kuileta katika mbingu ya dunia kwa mkupuo mmoja katika usiku wa Laylatul-Qadr, kisha akaiteremsha kwa Muhammad (s.a.w.w) kwa vipindi, kauli hii haina dalili yoyote.

Kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi.

Upambanuzi ni kupambanua kati ya haki na batili na kati ya heri na shari.

91

Kaashif2-94.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Tumekwishaeleza maana ya uongozi katika kufasiri Aya ya pili, na kwam-ba Qur'an si kitabu cha Falsafa, Historia au elimu ya maumbile, isipokuwa ni ufumbuzi, uongozi na rehma. Na kauli yake Mwenyezi Mungu "kuwa mwongozo kwa watu" inafahamisha kuwa mawaidha, hekima na viaga na yote ambayo yako katika Qur'an, yanafahamiwa na watu wote wala hayahusiki na kufahamiwa na mujtahidi au watu mahsusi.

Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na aufunge.

Yaani mtu ambaye hayuko safarini katika mwezi huu ni wajibu kwake kufunga, wala haifai kwake kufungua bila ya udhuru wowote. Linalofahamisha kuwa makusudio ya neno shahida ni kuwa mjini, ni kauli yake Mwenyezi Mungu inayofuatia isemayo:

"Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini basi atimize hisabu katika siku nyingine."

Amerudia kutaja ugonjwa na safari kwa kutilia mkazo kwamba katika mwezi wa Ramadhan kunajuzu kufungua, ili kuwajibu wale wanaoshikilia kwamba kufungua hakujuzu kwa hali yoyote.

Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi wala hawatakii yaliyo mazito.

Kwa dhahiri ya mfumo wa maneno ulivyo, ni kwamba jumla hii ni sababu ya kujuzu kufungua katika hali ya ugonjwa, safari na uzee, lakini kwa uhakika ni sababu ya hukumu zote. Imekuja Hadith isemayo: "Wafanyieni wepesi (watu) wala msiwafanyie uzito na wapeni habari za furaha wala msiwafukuze."

Mwenye kusema kuwa kufungua ni amri na wala sio ruhusa atakuwa ame-fasiri kauli yake Mwenyezi Mungu: "Anawatakia yaliyo mepesi", kwamba Mwenyezi Mungu anawatakia mfungue katika safari na hataki mfunge. Na mwenye kusema kuwa kufungua ni ruhusa na wala sio amri atakuwa amefasiri kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawataka muwe na wasaa

92

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

katika mambo yenu na kuchagua lile ambalo ni jepesi kwenu. Ikiwa kufungua ndio wepesi kwenu sawa; au ikiwa kufunga ndio kwepesi sawa. Ikiwa yule ambaye inakuwa wepesi kwake kufunga katika mwezi wa Ramadhan na kuona uzito kulipa, basi kufunga ni bora. Hakuna anayetia shaka kwamba kuzingatia dhahiri ya tamko kunatilia nguvu maana haya. Lau si Hadith sahihi kutoka kwa Ahlul Bait kutokana na babu yao (s.a.w.) tungelisema kwamba kufungua katika safari ni ruhusa na wala sio amri.

Na mtimize hisabu hiyo.

Hii ni sababu ya kulipa alikowajibisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kauli yake: "Basi (atimize) hisabu katika siku nyingine." yaani ni juu yenu kulipa saumu kwa idadi ya siku mlizofungua katika mwezi wa Ramadhan, kwa sababu ya maradhi na safari, ili itimie idadi ya siku za mwezi kamili ambazo mara nyingine huwa thelathini au ishirini na tisa.

Na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongoza na ili mpate kushukuru.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametubainishia hukumu za dini Yake, ili tumtukuze na tumshukuru. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Makusudio ya kumtukuza Mwenyezi Mungu, ni takbira za Idd baada ya swala ya Magharibi ya usiku wa Idd, Isha na Asubuhi, na vile vile baada ya swala ya Idd kwa mujibu wa madhehebu yetu; yaani takbira inayokariri-wa baada ya swala ya Idd ambayo husomwa hivi:

"Allahu Akbar, Allahu Akbar, Lailaha illa llahu Wallahu Akbar, Allahu Akbar wa lillaahilhamd; Allahu Akbar alaama hadaana. "

Maana yake ni: Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi, Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi, hapana Mola mwengine isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi kwa aliyotuongoza.

93

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-95.jpg

186. Na waja Wangu watakapoku-uliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba; Basi na waniitikie na waniami-ni, ili wapate kuongoka.

NAITIKIA MAOMBI YA MWOMBAJI

Ay a ya 186:

MAANA

Inasemekana kuwa Bedui mmoja alimwendea Mtume na kumuuliza: "Mola wetu yuko karibu ili nimnog'oneze? au yuko mbali nimpigie kelele?" Ndipo ikateremshwa Aya hii kuwa ni jawabu la Bedui.

Kama ni sawa kauli hii, au sio sawa lakini inanasibiana na maudhui.

Dua ni katika ibada bora na imehimizwa sana katika Qur'an na hadith. Kwa sababu ni dhihirisho la utumwa wa mtu kwa Mwenyezi Mungu na kumhitajia kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Hayo tumeyazungumzia kwa urefu katika kitabu Bainallah wal-insan.

Unaweza kuuliza: kauli yake Mwenyezi Mungu: "anaponiomba" baada ya kauli yake: "naitikia maombi ya mwombaji" ni jaribio la kupata ambacho tayari kipo, kwa sababu inafanana na kauli ya mwenye kusema: "Mwangalie mkaaji akiwa amekaa na msikilize msemaji akiwa anasema?"

Jibu: Makusudio ya "anaponiomba", ni dua inayotoka katika moyo wa mwenye ikhlasi na mkweli katika maombi yake, sio dua ya ulimi tu. Hiyo inafanana zaidi na kauli ya mwenye kusema "Mtukuze mwanachuoni

94

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

akiwa ni mwanachuoni", akimaanisha mwanachuoni wa kikweli kweli sio mwenye jina tu la wanachuoni.

Swali la pili ambalo ni maarufu na mashuri ni: Dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu "naitikia maombi ya mwombaji", na kauli yake; "niombeni nitawaitikia" ni kwamba Mwenye zi Mungu anamwitikia kila anayemwomba; wakati ambapo mtu anaweza kuomba sana na kun-yenyekea, lakini haitikiwi maombi yake?

Wafasiri wamelijibu swali hilo kwa majibu mbali mbali, baadhi yao wakafikia majibu sita. Wote wameafikiana kwamba Mumin, mtiifu kwa Mwenye zi Mungu, huitikiwa maombi yake, kinyume cha mwingine. Lakini kauli hii inabatilika kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliitika maombi ya Iblis

Kaashif2-96.jpg

"Akasema: Nipe muda mpaka siku watapofufuliwa (viumbe), Akasema (Mwenyezi Mungu): Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda." (7: 14 - 15)

Vyote iwavyo jibu la swali hilo linahitaji ufafanuzi kwa njia zifuatazo:

1. Mja kumwomba Mola wake mambo yanayopingana na desturi, kama vile kutaka riziki bila ya mihangaiko yoyote, elimu bila ya kujifundisha na mengineyo ambayo ni ya kutaka masababisho bila ya sababu, na kuingia nyumba kwa ukutani wala sio mlangoni. Hiyo siyo dua, au ni dua ya asiyemjua Mwenyezi Mungu na hekima zake na desturi yake. Kwani Mwenyezi Mungu ana desturi kwa viumbe vyake.

Kaashif2-97.jpg

"... Wala hutapata mabadiliko katika desturi wa Mwenyezi Mungu." (48:23).

95

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

2. Kutaka tawfiq na uongofu katika hukumu za dini kwa kufanya amali za heri, kutekeleza wajibu na kuacha maasi na mambo ya haram,

Kaashif2-98.jpg

"Tuongoze njia iliyonyooka" (1:6)

Vile vile dua ya kuomba kujiepusha na shari na maafa:

Kaashif2-99.jpg

" Sema najilinda kwa Mola wa asubuhi. Na shari ya alichokiumba" (113:1

- 2)

Pia kuna dua ya kumwomba Mwenyezi Mungu sababu za kufaulu katika riziki, elimu na afya:

"Ewe Mola wangu! nikunjue kifua changu. Na unifanyie nyepesi kazi yangu."

Hayo yote ni kwa sharti ya kuwa mwombaji awe na ikhlasi na kumtege -mea Mwenyezi Mungu peke Yake. Hayo ndiyo maombi ya Mitume na watu wema na ndio makusudio ya dua zao.

3. Kabla ya yote inatakikana kwanza tujue na wala tusiipuuze hakika hii ambayo tunaona na kushuhudia kwa macho, nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humpa anayemwomba na asiyemwomba kwa rehema na ukarimu kutoka kwake. Na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu humpa ufalme anayemtaka na humzuilia ufalme anayemtaka, Humdhalilisha anayemtaka na humwinua anayemtaka na humpa nguvu anayemtaka bila ya dua.

96

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kwa hivyo basi maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba," sio kwamba Yeye hatoi isipokuwa kwa dua. Wala hakuna maana katika kauli yake:

Kaashif2-100.jpg

"Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wanaofanya wema." (7:56)

Kuwa rehema ya Mwenyezi Mungu iko mbali na waovu. Hapana si hiyo! Hakika rehema Yake imeenea kila kitu.

"... Na kutoa kwa Mola wako hakuzuiliki." (17:20)

Zimekuja baadhi ya riwaya za dua ya maumivu ya tumbo, nyingine za maumivu ya mgongo, ya jicho, ya meno, n.k. Hadith hizo, ama zitakuwa zimewekwa tu, kwa sababu haziendi na hali halisi wala hazifai chochote; au pengine makusudio ni kujibidiisha kufanya matibabu pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Inasemekana kwamba Amirul Muminin (a.s.) alimpitia Bedui, aliyekuwa na ngamia mwenye ukurutu karibu yake.

Imam akamwuliza Bedui: "Kwa nini humfanyii dawa?"

Akajibu: "Kwa nini ewe Amirul Muminin! Ninamfanyia,"

Imam akauliza: "Dawa gani?"

Bedui akajibu: Dua

Imam akasema: "Pamoja na dua tumia dawa ya utomvu."

Basi na waniitikie na waniamini

Razi katika Tafsiri yake anasema: "Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

97

Kaashif2-101.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

anamwambia mja wake: Mimi ninaitikia maombi yako pamoja na kwamba Mimi sikuhitajii kabisa, basi nawe vile vile uwe ni mwenye kuitikia maombi yangu pamoja na kwamba wewe ni mwenye kunihitajia kwa kila hali. Ni ukubwa ulioje wa ukarimu huu!"

187. Mmehalalishwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi lenu na nyinyi ni vazi lao. Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe. Basi sasa changanyikeni (onaneni) nao na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku wakati wa alfajiri. Kisha timizeni saumu mpaka usiku. Na wala msichanganyike nao na hali mko katika itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha ishara Zake kwa watu ili wapate kumcha. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiikurubie. Namna hii Mwenyezi Mungu anabainisha ishara zake kwa watu ili wapate kuwa na takua.

Kaashif2-102.jpg

98

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

MMEHALALISHIWA USIKU WA SAUMU

Aya 187

LUGHA

Usiku wa saumu ni ule anaoamkia mtu akiwa amefunga. Kwa asili neno Rafath lina mana ya uchafu makusudio yake hapa ni kumwingilia mke. Vazi ni nguo ya kuvaa, lakini makusudio katika Aya hii ni kuchanganyi-ka.

Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu.

Yaani inafaa kwa mwenye kufunga kumwingila mkewe katika usiku wa kufunga. Usiku wa kufunga unakusanya siku zote za Ramadhan na wala hauhusiki na usiku fulani, au sehemu fulani tu ya usiku.! Hilo limefa-hamika kutokana na kuachiwa neno bila ya kufungwa na kitu kingine.

Mwenyezi Mungu amefumba kuwaingilia kwa neno rafath (uchafu) kwa ajili ya kuitakasa ibara; kama vile ambavyo amefumba katika Aya nyingine kwa maneno kama: Kugusa, kuingiliana na kukurubiana. Ibn Abbas anasema: "Mwenyezi Mungu ni mwenye staha hufumbia ana-chotaka."

Wao ni vazi lenu, na nyinyi ni vazi lao.

Baadhi ya wafasiri wanasema; vazi hapa ni fumbo la kukumbatiana. Razi anasema: Rabia amesema ni kuwa wao ni tandiko kwenu na nyinyi ni shuka kwao. Haya ni sawa na tafsiri ya Mustashriqina wanaosema: Wao ni suruali kwenu na nyinyi ni suruali kwao. Ilivyo hasa ni kuwa neno Libas ni matokeo ya neno Labis kwa maana ya kuchanganyika kuvaanas.

Makusudio kwa ujumla ni kubainisha hukumu ya kuruhusiwa kuingiliana na wanawake usiku wa saumu; kwani mke na mume wakiwa pamoja na kutangamana, basi inakuwa uzito sana kwa mume kuvumilia.

99

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe.

Msemo unawaelekea baadhi na wala sio wote. Hilo tunalifahamu kutokana na neno hiyana, kutakabali toba na msamaha.

Wafasiri wengi wanasema kwamba Mwenyezi Mungu alimhalalishia mfungaji tangu mwanzo wa sharia, kula na kunywa na kujamiiana na mkewe usiku wa saumu kwa sharti la kutolala au kuswali swala ya Isha. Kwa maana ya kuwa akilala usiku au kuswali Isha, basi ni haramu juu yake kula, kunywa na kujamii mpaka uingie usiku unaofuatia. Na kwamba sahaba mmoja alivunja sharti hili; hivyo akamjamii mkewe baada ya kuamka; kisha akajuta sana na akakiri makosa yake kwa Mtume (s.a.w.w.); ndipo ikashuka Aya hii.

Vyoyote iwavyo ni kwamba nafsi ina mambo ambayo inakuwa vigumu kujizuwiya nayo. Kwa hiyo mtu huishibisha kwa kujificha au kwa kuasi dini ya Mwenyezi Mungu. Basi lililo bora ni kuhalalisha lile linalopen-delewa ikiwa kuna njia yoyote ya kuhalalisha, ili mtu asivutwe kwenye maasi mara kwa mara, hatimaye kuwa mwenye dharau na kutojali dini na hukumu za Mwenyezi Mungu.

Na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu.

Ambayo ni kustarehe na wanawake wakati wa usiku wa saumu, jambo ambalo hapo mwanzo lilikuwa haramu.

Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainike weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku.

Yaani mmehalalishiwa kujamiina kuanzia mwanzo wa usiku mpaka machimbuko ya Alfajiri.

Imepokewa Hadith ya Mtume (s.a.w.w.): "Alfajiri ni mbili: Ama ile ambayo iko kama mkia wa mbwa mwitu hiyo haihalalishiwi kitu (swala)

100

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

wala kuharimishiwa (kula). Ama iliyo katika umbo mstatili ambayo inae-nea pambizoni, hiyo ni halali kuswali ndani yake na ni haramu chakula".

Kisha timizeni saumu mpaka usiku.

Mwanzo wa saumu ni kuanzia Alfajiri na mwisho wake ni unapoanza usiku. Usiku unaingia kwa kutua jua, lakini kutua kwake hakuwezi kuju-likana kwa kufichika machoni tu, bali hujulikana kwa kutoweka wekun-du upande wa mashariki kwa sababu mashariki ndiyo inayochomoza magharibi. Kwa hivyo wekundu wa mashariki unakuwa ni akisi ya mwan-ga wa jua, na kila linavyozidi kujificha zaidi jua ndipo akisi hii inavy-opotea

Ama yale wanayotuhumiwa Shia kwamba wao wanachelewesha swala ya Magharibi na futari ya Ramadhan mpaka zitokeze nyota, huo ni uongo na uzushi. Imam Sadiq (a.s.) aliambiwa kuwa watu wa Iraq wanachelewesha swala ya Magharibi mpaka zitokeze nyota. Akasema. "Hiyo ni kazi ya adui wa Mwenyezi Mungu Abul Khatwab."

Na wala msichanganyike nao, na hali mko katika itikafu msikitini.

Katika vitabu vya Fiqh kuna mlango mahsus unoitwa mlango wa itikafu. Aghlabu mafaqihi huutaja baada ya mlango wa saumu. Maana ya itikafu katika sharia ni kukaa mtu katika msikiti wa jamaa sio chini ya siku tatu, kwa masiku mawili, kwa mwenye kufunga; kwamba asitoke msikitini isipokuwa kwa haja muhimu na kurudi mara moja anapomaliza.

Ni haramu kwa mwenye kukaa itikafu kuingiliana na mwanamke usiku au mchana; hata kubusu na kugusa kwa matamanio. Kukatazwa hapa, kuna-fungamana na kuvaana na mwanamke kwa hali yoyote; iwe ni ndani ya msikiti au nje. Mwenye kukaa itikafu akitoka msikitini na akajamiiana na mwanamke usiku, hata kama atakoga na kurudi msikitini, atakuwa ame-fanya haramu; na itamlazimu kutoa kafara ya mwenye kufungua makusu-di katika mwezi wa Ramadhan - kumwachia huru mtumwa, au kufunga miezi miwili mfululizo au kulisha maskini sitini.

101

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-103.jpg

188. Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili na ku-zipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua.

KULA MALI KWA BATILI

Aya 188

MAANA

Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili.

Msemo unaelekezwa kwa wote wenye kulazimiwa na sharia. Maana ya msile mali zenu, ni sawa na kauli yake. Mwenyezi Mungu; "Msijiue" yaani msiuane. Hiyo inafahamisha umoja wa utu, na kwamba utu ni kama kiwiliwili kimoja na watu ni viungo vyake, lilopata kiungo kimoja linafikia kiungo kingine.

Makusudio ya kula, ni kutumia mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali. Neno "kati yenu" katika Aya linahusisha mali iliyotokana kwa mabadilis-hano ya haramu, kama riba; au mali iliyosimama kwa haramu, kama pombe, nguruwe ambayo hayathibitishwi na sharia. Mfano wa hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-104.jpg

"... Msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana...."(4:29)

102 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Ama uharamu wa mali iliyochukuliwa kwa unyang'anyi, wizi kiapo cha uongo, n.k. hayo yanafahamika kwa dalili nyingine. Kwa ajili hii, ndipo mafaqihi wakatoa dalili kwa Aya mbili hizo juu ya kubatilika kila muamala (mapatano) alioharamisha Mwenyezi Mungu.

Aya hii inafahamisha wazi wazi kwamba Uislamu unakubali mtu kumiliki chake. (mali ya mtu binafsi.)

Na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi.

Haya yanaungana na kula. Makusudio ya dhambi hapa ni rushwa, kwa kuangalia mfumo wa maneno ulivyo. Maana yaliyokusudiwa ni kukataza kutoa rushwa kwa mahakimu kwa ajili ya kula mali za watu.

Na hali mnajua.

Yaani msifanye dhambi hii na hali mnajua ubaya wake. Hakuna mwenye kutia shaka kwamba kufanya jambo ovu na huku mtu anajua, ni uovu zaidi kuliko kufanya na shaka shaka. Kuna hadith isemayo: "Kujizuia na shaka shaka ni bora kuliko kujitia katika maangamizo." Basi itakuwa ni bora zaidi kujizuia ikiwa mtu anajua uharamu.

Rushwa ni katika mambo makubwa yaliyoharamishwa, hata katika huku-mu ya haki. Mwenyezi Mungu ameilaani rushwa na mwenye kuitoa, mwenye kuipokea na mwenye kuwaunganisha wawili hao. Imepokewa Hadith inayofahamisha kuwa rushwa ni kumkufuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na riwaya nyingine inasema ni shirk.

HUKUMU YA KADHI FASIKI

Hanafi anasema kuwa hukumu ya Kadhi fasiki inafaa, hayo yameelezwa katika kitabu kiitwacho Ibn Abidin chapa ya mwaka 1325 hijriya., mlango wa Hukumu. Ninamnuukuu; "Fasiki ni mtu wa kutoa ushahidi, kwa hiyo anaweza kuwa Kadhi."

103 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na katika kitabu Fat-hul Qadir J5 uk. 454 mlango wa hukumu amese-ma; "Ilivyo ni kuwa hukumu ya kila mtawala inafaa, hata kama ni mjinga tena fasiki, na hayo ndiyo yaliyo wazi katika madhehebu yetu."

Shia Imamiya wamesema kwa kauli moja kwamba fasiki hawezi kuhuku-mu, na hukumu yake haifai kutekelezwa, hata awe na elimu kiasi gani.

Wamelitilia mkazo hilo kundi la mafaqihi wa Kiimamiya waliposema kuwa mwenye haki haijuzu kupeleka madai yake kwa kadhi asiye mwadil-ifu, hata kama ikibidi kuwa haki yake hawezi kuipata isipokuwa kwake, kwa namna ambayo lau si kadhi huyo, basi haki yake itapotea.

Akihalifu mwenye haki yake, basi haijuzu kuchukua chochote kili-chohukumiwa hata kama ni haki; kwa kuchukulia kauli ya Imam Jaffar As Sadiq (a.s.): "Anachokichukua ni haramu, ijapokuwa ni haki yake iliy-omthibitikia."

Mafaqihi wengi wa kiimamiya wamesema kwamba mwenye haki anaweza kumtaka msaada asiyekuwa mwadilifu katika kupata haki yake ikibidi, ikiwa hawezi kupata njia nyingine, bila ya kutofautisha kuwa haki yenyewe ni deni au mali. Kwa sababu kuzuia madhara ya nafsi kunajuzu, bali mara nyingine huwa ni wajibu, ikiwa hakutimii isipokuwa kumrudia asiyekuwa mwadilifu. Ama dhambi na haramu iko juu ya mwenye kuizuia haki sio mwenye kuchukua haki yake.

HUKUMU YA KADHI HAIBADILISHI UHAKIKA WA MAMBO

Hakimu mwadilifu akiwahukumu watu wawili na akampa haki asiyekuwa na haki kwa kushindwa kutoa ushahidi mwenye haki, basi haijuzu kuchukua ali-chohukumiwa. Kwa sababu hakimu hageuzi uhakika. Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Mimi ni mtu kama nyinyi isipokuwa napewa wahyi tu, na nyinyi mnapokuja kutaka hukumu kwangu, huenda mwingine akawa fasaha zaidi kwa hoja kuliko mwenzake. Nikihukumu kutokana na niliyosikia, basi ninayemhukumia kitu katika haki ya nduguye, (ajue) nimehukumia kipande cha moto."

104

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Lakini Abu Hanifa amesema kinyume cha hivyo. Akinukuliwa na mwenye TafsirAl- Manarkatika kuelezea Aya hii, Abu Hanifa amesema: "Kadhi aki-hukumu kuvunjika ndoa kati ya mume na mke kwa ushahidi wa uongo, itakuwa haramu kwao kuishi maisha ya ndoa. Na kama shahidi akitoa ushahidi wa uongo kwamba fulani amemuoa fulani na hakimu akahukumu kuwa ni sawa, basi ni halali kwa mwanamume kumwingilia bila ya ndoa, kwa kutosheka na hukumu ya Kadhi ambayo anajua kuwa sio haki."

189. Wanakuuliza kuhusu ya miezi. Sema: 'Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hijja. Wala si wema kuin-gia majumba kwa nyuma yake, bali mwema ni aliye na takua. Na ingieni majumba kupitia milangoni mwake, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.

WANAKUULIZA KUHUSU MIEZI

Aya 189

MAANA

Wanakuuliza kuhusu miezi.

Swali hili linawezekana kuwa pande mbili, ikiwa hatukuangalia jibu lake linalofuatia: Kwanza, nikuwa ni swali la kutaka kujua sababu za kisayan-si; kutokana na tofauti inayoonekana - kuanzia mwezi mwandamo, kisha mwezi mkamilifu, tena unarudi kama ulivyokuwa. Pili, kuwa ni kuuliza hekima yake, sio sababu za kisayansi.

Kaashif2-105.jpg

105 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Tukiliangalia swali pamoja na jibu lake: "Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu", litakuwa ni swali la hekima tu, na wala sio la sababu za kisayansi. Hili ndilo lenye nguvu zaidi.

Ama kauli ya anayesema kuwa wao waliuliza kuhusu sababu za kisayansi na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.). akamwamrisha Mtume wake kuwa-jibu kwa kubainisha hekima kuonyesha kuwa swali lao haliko mahali pake, kwa sababu wao wameshindwa kufikia kwenye sababu za kisayansi ambazo zinahitaji darasa ndefuna zenye undani na utangulizi mwingi wa kielimu; na ilivyotakiwa wao waulize hekima na faida ya kutofautiana miezi, jambo ambalo wao wanaweza kulifahamu. Kauli hiyo haitegemei dalili yoyote isipokuwa kuonelea kuwa ni vizuri hivyo tu.

Unaweza kusema kuwa dalili iko; nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Wala si wema kuingia majumba kwa nyuma". Kwamba kuuliza kwenu sababu za kisayansi, ni sawa na kutaka kuingia nyumba kwa nyuma; lakini kuuliza kwenu hekima yake, ni kama anayetaka kuingia nyumba kwa mlango wake.

Jibu, kwanza hiyo ni Ijtihadi ya kuleta taawili ya tamko na wala sio kutafsiri dhahiri ya tamko.

Pili, imethibiti kuwa jumla hii imeshuka kutokana na waliyokuwa wakiyafanya wakati wa kijahilia, ya kuingia nyumba kwa nyuma. Ufafanuzi ni kama ifuatavyo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake kuwajibu kuwa hekima ya kutofautiana miezi ni kuyawekea wakati maslahi yao na mambo yao ya kidunia, kama vile madeni na kukodisha; na mambo yao ya kidini, kama vile Hijja na saumu. Kwa maneno mengine ni jibu linapitia katika kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t)

Kaashif2-106.jpg

": ...Ili mjue idadi ya miaka na hisabu..." (10:5) Wala si wema kuingia majumba kwa nyuma yake.

Bali mwema ni yule anayemcha Mwenyezi Mungu. "Na ingieni majumba kupitia milangoni mwake". Wafasiri wengi wasema wakati wa

106

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

kijahiliya mtu kuwa anapohirimia Hijja, hutoboa tundu ya kuingilia au hutengeneza ngazi ya kupanda sakafuni; na akiwa ni katika Mabedui hutoka nyuma ya kibanda.

Baadhi ya waislamu nao walikuwa wakifanya hivyo hapo mwanzo mwanzo, ndipo ikashuka Aya kuwabainishia kwamba wema ni kum-wogopa Mwenyezi Mungu, kufanya amali za heri na kujiepusha na maasi na machafu, sio kuingia majumba kwa nyuma na mengineyo ambayo hayaingii akilini wala kuwa na lengo la dini na imani.

190. Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga, wala msi-chokoze. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wachokozi.

191. Na wauweni popote muwapa-tapo na muwatoe popote walipowatoa; na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtukufu mpaka wapi-gane na nyinyi huko. Wakipigana na nyinyi basi nanyi pia wapigeni. Namna hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.

192.  Lakini kama wakikoma, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufi-ra, Mwenye kurehemu.

Kaashif2-107.jpg

107

Kaashif2-108.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

193. Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina, na dini iwe ya Mwenyezi Mungu. Na kama wakikoma, basi usi-weko uadui ila kwa madhal-imu.

NA PIGANENI KATIKA NJIA YA MWENYEZI MUNGU

Aya 190 -193

LUGHA

Neno Fitna lina maana ya balaa na misukosuko, na makusudio yake hapa ni ukafiri, yaani kuwaharibu watu na dini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kutokana na kulinganganisha na neno "Na dini iwe ya Mwenyezi Mungu peke yake."

MAANA

Katika Majmaul Bayan imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipotoka yeye na sahaba zake katika mwaka ambao wal-itaka kufanya Umra wakiwa watu elfu moja na mia nne (1400), walipofi-ka Hudaybia, Washirikina waliwazuia wasiingie Al Ka'aba. wakachinja wanyama hapo Hudaybia;* 5 kisha wakafanya suluh na washirikina kurudi, na waje mwaka ujao.

Mwaka ulipofika Waislamu walijiandaa kutekeleza Umra, lakini wakao-gopa kupigwa vita na Washirikina. Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zake wakachukia kupigana na washirikina katika mwezi mtukufu tena ndani ya Haram (sehemu takatifu ya Makka).

5

Hayo yalikuwa mwezi wa Dhul-qada (mfunguo pili) mwaka wa sita wa Hijriya. Na Hudaybia siku hizo ilikuwa na maji mengi na miti, lakini leo imegeuka na kuwa jangwa kama nilivyoiona mwaka 1964 A.D.

108

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii, na kuidhinishwa kupi-gana. Baadhi ya jamaa wamesema hiyo ndiyo Aya ya kwanza kushuka kuhusu vita.

UISLAMU UNAPIGA VITA DHULMA NA UFISADI

Baadhi ya ambao wana ghera juu ya Uislamu na kujaribu kuugombea Uislamu kwa kila njia, hata kama itapigana na misingi ya Qur'an, wamesema kuwa Uislamu hauruhusu kupigana na yeyote isipokuwa mchokozi; na vita vya Kiislamu, katika zama za Mtume, vilikuwa ni vya kujikinga sio hujuma na walitoa dalili kwa aya kadhaa miongoni mwazo ni Aya hii tuliyonayo sasa na Aya nyingine inayosema:

"...Na piganeni na makafiri nyote kama wao wote wanavyopigana nanyi nyote" (9:36)

Lililowafanya kuugombea hivyo Uislamu, ni madai ya maadui wa Uislamu kwamba Uislamu ni dini ya vita, sio dini ya amani, kwa kisin-gizio cha vita vya Mtume (s.a.w.w.).

Ilivyo hasa ni kuwa Uislamu umeruhusu kupigana kwa sababu zifuatazo: Kujikinga

Kupigana na madhalimu;

Kaashif2-109.jpg

Mwenyezi Mungu anasema: "Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni, likiwa moja la hayo linadhulumu jengine, basi lipigeni lile linalodhulumu mpaka lirudie kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." (49:9)

109

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kumaliza ukafiri wa wanao mkufuru Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-110.jpg

"Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho, wala hawaharimishi alivyoviharimisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala hawafuati dini ya haki miongoni mwa waliopewa kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe kodi kwa hiari yao, hali wametii." (9:29)

Mtume amesema: "Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka waseme hapana Mungu isipokuwa Allah. Kama wakisema, basi imehifadhika nami damu yao na mali zao."

Lakini kupigana kwa aina hii hakuruhusiwi isipokuwa kwa idhini ya Masum au naibu wake kuepuka vuruga.

Kujuzu kupigana kwa kujikinga, hakuna maana kuwa hakuna idhini ya kupigana kwa malengo mengine, kama vile kumaliza dhulma na ukafiri. Uislamu umeruhusu kupigana kwa ajili ya kupatikana dini ya haki na uadilifu, kwa sababu ukafiri wenyewe ni uadui katika Uislamu. Lakini Uislamu umeharamisha kupigana kwa ajili ya kutawala watu na kuwapokonya uwezo wao na kutawala uchumi wao.

Uislamu umejuzisha kutumia nguvu kumaliza maovu na madhambi na kupigania haki za binadamu, uhuru wake na heshima yake. Wakoloni walianzisha vita wakaleta machafuko na kumwaga damu, wakatafuta elimu kwa ajili ya kuua na kunyonya, na kuiweka juu dhulma na uadui

A 6

ju 6

Mnamo mwaka 1957 kilitolewa kitabu huko Amerika, kinachohusu Mustakabali wa nguvu za nuklia cha Torry Tony. Anaeleza mtungaji kwamba maendeleo ya elimu yame-teremsha bei ya kumuua Mtu. Mwanzo bomu la Atomic lilikuwa likigarimu pauni nyingi baadaye ikagarimu pauni moja na baada ya bomu la haidrojeni kumua mtu kukawa kunagharimu shilingi moja tu.

Kaashif2-111.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Hilo ndilo jawabu la wale wanaojaribu kuutweza Uislamu na Nabii wake, kwamba Uislamu ni dini ya vita na upanga. Na kweli Uislamu ni dini iliyokamilika. Inampiga vita kila asiyefuata haki na uadilifu na anayele-ta uharibifu na ufisadi katika ardhi. Na kumkufuru Mwenyezi Mungu ni dhulma na ufisadi katika dini ya Kiislamu na sharia yake.

Kulingana na suala hili hatuna budi kudokeza kuwa mafaqihi wa mad-hehebu zote za Kiislamu wameafikiana kwa kauli moja kwamba mwenye kuvunja miko ya Mwenyezi Mungu kwa kuihalalisha na kwa kumwaga damu na kunyakua mali, basi yeye ni mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu; hata kama akiswali na kufunga na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu; bali huyu ni mwovu zaidi kuliko yule mwenye kukufuru, lakini akazuia umwagikaji damu na kunyakua mali na akijizuia kuwaudhi watu.

Ndio, wote wawili ni makafiri, lakini kafiri mwingine ni mwovu kwa Mwenyezi Mungu na kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Bora ya watu ni yule mwenye kuwanufaisha zaidi watu, na mwovu zaidi wa watu ni yule ambaye watu wanahofia shari yake."

Tunasema tena kila mwenye kukanusha hukumu ya kisharia iliyothibitika kwa dhahiri ya dini na Waislamu wote, basi huyo ni kafiri hata kama amezaliwa na wazazi Waislamu na akatamka shahada mbili.

Wala msichokoze.

Yaani, msipigane kwa ajili ya manufaa ya kiutu, bali piganeni kwa lengo la heshima ya utu binafsi na kwa lengo la kuihami dini na haki msiwaue watoto, wazee na wagonjwa. Vile vile msiharibu majengo na kukata miti. Mafunzo yote haya na mengineyo yamekuja katika Sunna za Mtume.

Waueni popote muwapatapo.

Yaani waueni makafiri wakati wowote na mahali popote walipo

111

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

isipokuwa kwenye Msikiti Mtukufu, kwa sababu kupigana hapo ni hara-mu isipokuwa wakianza humo

Unaweza kuuliza: Katika Aya ya mwanzo kumeamrishwa kupigana na anayepigana na Waislamu, lakini kwenye Aya hii kumeamrishwa kupigana tu, bila ya kufungamanishwa na kitu kingine. Je, Aya hii imefuta hukumu ya hukumu ile?

Jibu: Hapana kufutwa hukmu. Hivi punde tumeonyesha kwamba kujuzu kupigania nafsi hakufahamishi kuwa hakuna ruhusa ya kupigana kwa malengo mengine; kama vile kumaliza ukafiri na dhulma. Kama ukimwambia mtu 'wewe ni mtu mzuri' haina maana kuwa mwingine si mtu mzuri.

Basi hivyo hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu: 'Piganeni na wanaowapiga' haina maana msipigane na wasiowapiga. Ndio, kama angelisema msipigane isipokuwa na wanaowapiga, hiyo ingefahamisha kufunga huko ni kwa kukanusha.

Na muwatoe popote walipowatoa.

Washirikina wa Makka walimtoa Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zake hapo Makka, si kwa lolote isipokuwa tu masahaba hao wameamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake na Waislamu wakirudi Makka wakiwa washindi, wamtoe hapo kila asiyemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; sawa na vile walivyofanywa na washirikina 'malipo yenye kulingana.' Inasemekana Mtume aliwatoa washirikina ulipokuja msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi kwa kuchukulia Aya hii.

Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua.

Hii ni sababu ya kujuzu kuwaua washirikina. Makusudio ya fitina ni ushirikina. Maana ya kuwa mmeruhusiwa kuwaua washirikina, ni kuwa dhambi ya shirk ni mbaya zaidi kuliko dhambi ya kuua.

112

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Baadhi ya tafsiri zinasema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekusudia katika kauli yake hiyo, kuwa Washirikina wa Makka hapo mwanzo wa mwito wa Uislamu walikuwa wakimfitini mwenye kusilimu kwa kumuudhi kumwadhibu na kumtoa mjini kwake. Na hiyo ni fitina mbaya zaidi kuliko kuua. Kwa ajili hii ndio kukaruhusiwa kuwaua na kuwatoa mijini mwao.

Vyovyote iwavyo makusudio ya neno Fitna katika Qur'an sio ya kufanya umbeya na udaku kama wanavyofikiria wengi.

Wala msipigane nao karibu na Msikiti mtukufu mpaka wawapige huko.

Hili ni sharti la kujuzu kupigana katika Haram tukufu ambayo ame-haramisha Mwenyezi Mungu kupigana ndani yake isipokuwa kama ikivunjiwa heshima kwa kupigana.

Wakipigana nanyi basi nanyi pia wapigeni. Kwa sababu wao wameanza na wakauvunjia heshima Msikiti mtakatifu na mwenye kuanza hakudhulu-miwa, isipokuwa yeye ndiye dhalimu.

Lakini kama wakikoma, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, Mwenye kurehemu. Kulingana na mfumo wa maneno ulivyo, unahuku-mia kuwa maana yake ni, basi nanyi jizuieni nao na muwasamehe, kwa vile sababu iliyolazimisha kupigana nao ni kuanza kwao vita; wakijizuia basi sababu imeondoka.

Wafasiri wengi wamesema kuwa maana yake ni, wakitubia kutokana na ukafiri na wakamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa sababu kafiri hawezi kusamehewa na Mwenyezi Mungu kwa kuacha kupigana tu, bali husamehewa kwa kuacha kufuru. lakini huku ni kumuhukumia Mwenyezi Mungu(s.w.t.) kwa sababu Yeye anaweza kumsamehe anayemta-ka, hata kama ni kafiri. Ni kweli kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kumwadhibu mwema kabisa, sababu Yeye ni Mwadilifu, lakini anaweza kumsamehe mkosaji kwa namna yoyote ya uovu itakavyokuwa, kwa sababu Yeye

113

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

ni Karimu, Mwenye huruma.

Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina na dini iwe ya Mwenyezi Mungu.

Yaani Jihadi ni kwa ajili ya imani ya Mwenyezi Mungu. Kumaliza ukanushaji (wa kumkanusha Mwenyezi Mungu) ni wajibu maadam duni-ani kuna athari ya shirki na ulahidi. Kama yakiondoka haya na watu wote wakaamini, basi wajibu wa Jihadi utakuwa umeondoka.

Kwa ujumla ni kwamba wajibu wa Jihadi kwa ajili ya kuueneza Uislamu una sharti ya kupatikana idhini ya Imam mwadilifu na wala hai-juzu kwa hali yoyote bila ya amri yake. Ama Jihadi ya kuihami dini na nafsi, wajibu wake umeachwa bila ya kuwekwa sharti lolote.

Na kama wakikoma basi usiweko uadui ila kwa madhalimu. Yaani kama wakiacha ukafiri na wakasilimu basi si halali kuwaua isipokuwa kwa sababu zinazowajibisha kuua, ambazo ni moja kati ya mambo matatu: Kukufuru baada ya kuamini, kuzini baada ya kuwa na mke na kuua mtu bila ya haki yoyote.

194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu; na vitu vitakatifu vina kisasi. Basi wanaowa-chokoza, pia nanyi wachokozeni kwa kadiri walivyowachokoza.          Na

mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha.

Kaashif2-112.jpgKaashif2-113.jpgKaashif2-114.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

195. Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu, na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi                Mungu

huwapenda wafanyao wema.

MIEZI MITAKATIFU

Aya 194 - 195

MAANA

Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu.

Miezi mitakatifu ni minne; mitatu inafuatana, nayo ni Dhul-Qaada, Dhul Hijja na Muharram (mfunguo pili, mfunguo tatu na mfunguo nne). Na mwezi mmoja uko pekee na ni (Rajab). Miezi hii imeitwa mitakatifu kwa sababu ya kuharamishwa kuuana ndani ya miezi hiyo. Katika wakati wa ujahiliya na wa Uislamu, ilikuwa mtu anaweza kukutana na mtu aliye-muua baba yake katika miezi hiyo na asimfanye chochote.

Yameshatangulia maelezo kwamba Mtume na sahaba zake walitaka kufanya umra katika mwezi wa dhul-Qaada (mfunguo pili) mwaka wa sita (6 Hijriya), wakazuiwa na washirikina na wakatupiwa mishale na mawe; kisha waka-fanyiana suluhu kuwa Waislamu warudi mwaka utakao-futia. Lakini Waislamu wakaogopa washirikina wasije wakaanza kupigana katika mwezi mtakatifu; ndipo Mwenyezi Mungu akawapa idhini ya kupigana na washirikina na akabainisha kuwa lenye kukatazwa ni kuanza uadui wa kupigana na sio kujikinga.

Kwa hivyo maana ya mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu ni kwamba mwenye kuihalalisha damu yenu enyi Waislamu katika mwezi huu, basi nanyi ihalalisheni damu yake katika mwezi huo huo.

115

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na vitu vitakatifu vina kisasi.

Yaani mwenye kuvunja heshima ya Mwenyezi Mungu atalipizwa kisasi na atafanywa kama alivyofanya. Hiyo ndiyo asili kwa ujumla inayoondoa kila udhuru wa mwenye kuvunja heshima. Mwenye kuhalalilisha damu za watu, mali zao na heshima zao, naye atahalalishwa kwa kiasi kile ali-chowafanyia. Heshima kwa mtu mwingine inatokana na heshima ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kama akivunja heshima ya mwingine. Hapo itakuja haki ambayo daima inakuwa juu na wala haikaliwi. Hapa ndipo tunapata tafsiri ya:

Anayechokoza pia nanyi mchokozeni kwa kadiri alivyo wachokoza.

Sharti la kulipiza ni kuwa sawa na kosa la aliyeanza bila ya kuzidisha au kupunguza. Hicho ndio kisasi hasa kilivyo.

Unaweza kuuliza: Mwenye kuchokoza , yeye ni mchokozi bila ya wasi-wasi wowote, lakini mwenye kulipiza kisasi bila shaka siye mchokozi.

Kwa hiyo kuna wajihi gani kwa Mwenyezi Mungu kusema: Mchokozeni

Jibu: Makusudio ya kuwafanyia uchokozi, sio uchokozi hasa kwa maana yake, isipokuwa makusudio ni malipo ya uchokozi uliofanywa kwa kipimo chake bila ya kudhulumu. Hayo ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu(s.w.t.):

Kaashif2-115.jpg

"Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo..." (42:40) Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Kutoa katika njia yake Mwenyezi Mungu kunakuwa ni kwa masilahi ya umma; kama vile shule, hospitali na nyumba za kulea mayatima. Vile vile jihadi, sadaka kwa mafukara na masikini na kuwalisha watu wa nyum-bani. Bora zaidi ya kutoa ni kule kunakohusika na kutia nguvu na kuieneza dini, kuthibitisha haki na kuibatilisha batili.

Wala msijitie, kwa mikono yenu, katika maangamivu

Kaashif2-116.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu ametumia neno mikono kwa maana ya mtu kujiingiza mwenyewe. Kama tukiangalia jumla hii peke yake tu bila ya kuangalia mfumo mzima wa maneno, ingelikuwa maana yake ni kuwa haijuzu kwa mtu kufanya lolote ambalo lina madhara na bila ya kuwako manufaa kwa ujumla. Lakini tukichunga mfumo wa maneno na kuja kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu" baada ya kusema: "Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu", basi maana yanakuwa, toeni katika mali zenu sio kwa ubahili wala ubadhirifu, kwa sababu yote hayo mawili yanaleta uangamivu. Kwa hivyo Aya kwa maana haya inakuwa kama ile Aya isemayo:

Kaashif2-117.jpg

"Na wale ambao wanapotoa hawafanyi ubadhirifu wala ubahili, bali wanakuwa katikati ya hayo."(25:67)

Inasemekana pia kwamba maana yake ni: Msijitie kwa mikono yenu kwenye maangamivu kwa kuacha kupigana jihadi na maadui wa dini na kutoa mali kwa ajili ya kuwaandaa wapigania jihadi, kwa sababu hilo litawaogopesha na atawaweza adui; muangamie na mdhalilike.

Haya ndiyo yaliyothibitishwa na majaribio waliyoyapitia Waislamu. Wamekosa uhuru wao na heshima yao tangu walipoacha jihadi na kutoa mali kwa ajili ya kuinusuru haki na uadilifu. Hivyo akapata tamaa kila mnyang'anyaji na mnyakuzi; hata Wazayuni, vibaraka wa ukoloni, nao waliivamia Palestina mnamo 1948. Baada ya Waarabu kunyamaza na wasi-fanye jihadi. Baada ya miaka ishirini wakateka Sinai na ukanda wa Gaza Magharibi mwa mto Jordan; wakazikalia sehemu hizo kwa msaada wa Amerika, Uingereza na Ujerumani Magharibi. Wakawaua wanaume na kuwafukuza wanawake na watoto. Lau Waislamu wangefanya jihadi kabla yake, wangeliokoka na maangamizo haya na udhalili huu, na wala dola ya Israel isingekuwepo kabisa.

Na fanyieni wema Kwa jihadi na kujitolea mali katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kila njia inayomridhisha Mungu na yenye sifa nzuri.

Kaashif2-118.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

196. Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuili-wa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machin-jioni mwao. Na ataka-yekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana adha kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnya-ma. Na mtakapokuwa sala-ma, basi mwenye kujistarehe-sha kwa kufanya Umra, kisha akahiji, achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporudi; hizo ni siku kumi kamili. Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Kaashif2-119.jpgKaashif2-120.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

197.  Hijja ni miezi maalumu. Na anayejilazimisha kufanya Hijja katika miezi hiyo, basi hakuna kuchafua wala ufuska wala mabishano katika Hijja. Na heri yoyote mnay-oifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masu-rufu, na hakika masurufu bora ni takua; na nicheni Mimi, enyi wenye akili.

198. Si vibaya kwenu kutafuta rizi-ki ya Mola wenu. Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril-Haram: Na mkumbukeni kama            alivyowaongoza, ijapokuwa zamani mlikuwa miongoni mwa waliopotea.

199. Kisha miminikeni kutoka mahali wanapomiminika watu (wote), na mumwombe Mwenyezi Mungu maghufira; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria Mwenye kurehemu.

Kaashif2-121.jpgKaashif2-122.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

200. Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu; bali mtajeni zaidi. Na kuna baadhi ya watu wase-mao: Mola wetu! Tupe duni-ani; nao katika Akhera, hawana lolote.

201.  Na miongoni mwao kuna ase-maye; Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema Akhera, na utulinde na adhabu ya Moto.

202.    Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

Kaashif2-123.jpg

120

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-124.jpg

203. Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazo-hisabiwa. Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusany-wa Kwake.

TIMIZENI HIJJA NA UMRA

Aya 196 - 203

MAANA

Aya hizi zimeonyesha baadhi ya hukumu za Hijja, Mafaqihi wameweka vitabu maalumu vinavyohusu Hijja, nami nimetunga kitabu kwa jinaAl-Hajj ala Madhahabil-Khamsa; kisha nikakiunganisha katika kitabu Al-Fiqh ala Madhahabil Khamsa wakati kiliporudiwa kuchapishwa kwa mara ya tatu. Vile vile nimeizungumza kwa urefu katika Juzuu ya pili ya kitabu Fiqh ul-Imam Jaffar Sadiq (a.s.)

Hijja imekuwa maarufu tangu zama za Nabii Ibrahim na Ismail (a.s.) na iliendelea katika zama za ujahiliya; na Uislamu ukaithibitisha baada ya kuisafisha na mambo machafu, na kuongeza baadhi ya ibada.

Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Maana ya Hijja kilugha, ni kukusudia, na kisharia ni ibada maalum katika mahali na wakati maalum. Umra kilugha ni ziara yoyote; na kisheria ni

121

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

ziara katika Al-Ka'aba kwa namna maalum,

Hijja ni wajibu katika Qur'an, Hadith na Ijami. Bali wajibu wake umethubu-tu kwa dhahiri ya dini. Na mwenye kuikanusha sio Mwislamu, sawa sawa na aliyekanusha wajibu wa Saumu na Swala. Shia Imamiyya na Shafii wamesema Umra ni wajibu, Hanafi na Malik wamesema ni Sunna.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu" Yaani Hijini na fanyeni Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake na sio kwa makusudio ya kidunia. Kwani Waarabu walikuwa wakikusudia kuhiji kwa ajili ya kukutana, kujifaharisha, kutafuta mahitaji na kuhudhuria soko. Ndipo Mwenyezi Mungu akaamrisha Hijja iwe ni kwa makusudio yake Yeye kwa ibada safi yenye kutakasika na makusudio yoyote mengine.

Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana.

Yaani ikiwa mmeherimia Hijja, kisha mkazuilika kukamilisha ibada kwa njia yake ya kisheria kutokana na maradhi au adui na mengineyo, basi ni juu yenu kuchinja mnyama atakayepatikana kwa urahisi; kwa uchache awe ni mbuzi, wastani ni ng'ombe na wa juu zaidi ni ngamia.

Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao.

Msemo unaelekezwa kwa wale waliozuilika ambao hawakuweza kutimiza Hijja au Umra. Wao hawatakuwa wametoka katika ihram yao (miko ya Hijja) mpaka wajue kwamba mnyama amefika mahali pake pa kuchinjwa. Na mahali pa kuchinja ni Mina ikiwa ni Hijja; na kama ni Umra basi ni Makka. Hayo ni itakapokuwa kizuizi ni maradhi. Ama ikiwa kizuizi ni adui, basi mahali pa kuchinja ni pale mahali palipotokea kizuizi. Kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) alichinja mnyama katika Hudaybiya, alipozuiliwa na washirikina kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu (Al Ka'aba).

122 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana adha kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnyama.

Yaani ikiwa mwenye kuhirimia atanyoa kichwa chake kwa dharura, basi ni juu yake kutoa kafara, atakuwa na hiyari baina ya kufunga siku tatu, kuwalisha masikini sitini au kuchinja mnyama; kwa uchache awe ni mbuzi.

Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha akahiji, achinje mnyama aliyemwepesi kupatikana.

Yaani mtu asiyekuwa na kizuizi, akafanya Umra kisha akahiji baadae katika mwaka huo huo, basi ni juu yake kuchinja mnyama. Hii ndiyo aina ya Hijja inayojulikana kwa jina la Haj Tamattui (Hijja ya starehe) ambayo ni wajibu kwa wasiokuwa watu wa Makka. Imeitwa Hijja ya starehe, kwa sababu mwenye kuhiji baada ya kumaliza amali za Umra anatoka kwenye miko ya Umra mpaka aje ahirimie Hijja.

Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporu-

di; hizo ni siku kumi kamili . Imam Jaffar Sadiq (a.s.) amesema; Mwenye kufanya Hajj Tamattu, asipopata mnyama atafunga siku tatu katika Hijja; siku ya saba, ya nane na ya tisa katika Dhul-Hijja (mfungu tatu) wala hakuna sharti la Iqama na siku saba atafunga atakaporudi kwa watu wake. Hizo ni siku kumi kamili za kutosheleza mnyama.

Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na msikiti mtakatifu.

Mwenye Majmaul Bayan amesema kuwa hayo yaliyotangulia kutajwa katika Tamattui ya Umra kisha Hijja, sio kwa watu wa Makka na walio karibu yake. Isipokuwa ni kwa ambaye hayuko Makka, yule ambaye yuko mbali na Makka kwa zaidi ya maili kumi na mbili (12) kwa kila upande.

Mafaqihi wa Kishia Imamiya wamesema Hajj Tamattui ni wajibu kwa walio mbali na Makka, wala haijuzu kwa aliyembali na Makka kuhiji Hijja Qiran na Ifrad, kwani hizo ni wajibu kwa watu wa Makka na wa kando kando yake; na wao haijuzu kwao kuhiji Hajj Tamattui. Kwa ufafanuzi zaidi angalia vitabu vya Fiqh.

123 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Hijja ni miezi maalumu. Nayo ni kuanzia Shawwal, Dhul-qaad na kumi la mwanzo la Dhul-Hijja. (mfunguo mosi, mfunguo pili na mfunguo tatu) Mwenye kuhirimia kabla yake Hijja yake haitaswihi na mwenye kuhirim-ia ndani ya miezi hiyo itaswihi na ataleta amali zilizobakia.

Na anayejilazimisha Hija katika miezi hiyo, basi hakuna kuchafua wala ufuska wala mabishano katika Hijja.

Makusudio ya uchafuzi hapa ni kujamii. Mtu akimjamii mkewe na huku amehirimia Hijja, basi Hijja yake imeharibika, sawa sawa na aliyejamii au kula huku akiwa amefunga. Kwa hiyo atakamilisha Hijja yake, kisha aje alipe mwaka ujao; kama ilivyo kwa mwenye kuiharibu Saumu. Makusudio ya ufuska, ni uongo na kutukana.

Ama kuhusu kubishana riwaya za Ahlul Bait zinasema, hilo ni kusema mtu; "Hapana wallahi au "Kwa nini, wallahi n.k."

Si vibaya kwenu kutafuta riziki ya Mola wenu

Kwa vile wakati wa ujahilia watu walikuwa wakifanya biashara na kuchu-ma siku za Hijja, kukadhaniwa kuwa ni haramu, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.), akaondoa tuhuma hii na akabainisha kwamba kuchuma hakupin-gani na ikhlasi katika amali za Hijja.

Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'arilHaram.

Arafa ni mahali maalum. Kumiminika kutoka Arafa ni kuondoka, Mash'aril-Haram ndipo pale panajulikana kama Muzdalifa na kutua hapo ni wajibu; kama ilivyo kwa Arafa.

Kisha miminikeni kutoka mahali wamiminikapo watu (wote)

Inasemekana kuwa Maquraish walikuwa hawatui Arafa pamoja na watu wengine kwa kiburi tu, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume

124

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

wake kutua hapo na kutoka pamoja na watu ili abatilishe waliyokuwa wakiyafanya Maquraish.

Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu zaidi.

Imepokuwa kutoka kwa Imam Baqir baba wa Imam Sadiq (a.s.) kwamba watu walikuwa wanapomaliza Hijja wanakusanyika huko na kuwataja wazazi wao kwa fahari, ndipo Mwenyezi Mungu akawaamrisha kuliacha hilo na badala yake wamtaje Mwenyezi Mungu na jinsi alivyowaneeme-sha. Kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuwaneemesha wao na mababa zao.

Na baadhi ya watu kuna asemaye: Mola wetu! Tupe duniani; nao kati-ka akhera hawana lolote. Na miongoni mwao kuna asemaye: Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera, na utulinde na adhabu ya moto. Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu.

Watu katika Hijja zao wako aina mbili. Aina ya kwanza ni yule asiyetaka lolote isipokuwa starehe ya dunia na hana makusudio yoyote isipokuwa dunia tu, na anapomwabudu Mwenyezi Mungu humwabudu kwa ajili ya dunia. Hawa ndio wenye kunyimwa neema ya Akhera. Ama aina ya pili ni yule anayetaka heri ya dunia na akhera na anafanya amali kwa ajili ya dunia yake na akhera yake. Huyu ndiye mwenye radhi mbele ya Mwenyezi Mungu kesho kwa kulipwa amali yake njema.

Mwenye Tafsiri Rawhul Bayan amenukuu kutoka kwa Imam Ali bin Abi Twalib (a.s.) kwamba wema katika dunia ni mwanamke mwema na katika akhera ni Hurulain. Ama adhabu ya moto makusudio yake ni mwanamke muovu.

Iwe ni sahih Hadith hiyo au la, lakini mimi najua kuna watu wanaohisi kwamba lau wao wangekuwa katika Jahanam kisha wakahiyarishwa kutoka katika Jahanam na warudi kwa wake zao waliokuwa nao duniani au wabaki Jahannam, basi wangelichagua kubaki katika Jahannam kuliko kuishi tena na

125 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

wake zao hao.

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabiwa.

Makusudio yake ni siku tatu za Tashriq nazo ni; Tarehe kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu katika mwezi wa Dhul-Hijja (mfungo tatu).

Si wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina usiku wa kumi na tatu, lakini kwa sharti ya kuwa atoke Mina siku ya kumi na mbili baada ya kupinduka jua na kabla ya Maghrib na awe hakuvunja mwiko wa kuwinda au kujamii. Kwa hali hiyo ndipo tunapopata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake kwa mwenye takua.

Yaani mwenye kuacha kuwinda na wanawake katika ihram yake.

Ikiwa amevunja mwiko wa kulala na mke au kuwinda au alichelewa na jua siku ya kumi na mbili akiwa yuko Mina, basi itakuwa wajibu kwake kulala usiku wa kumi na tatu na kutupia mawe vikuta vitatu (shetani).

126

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

204.  Na katika watu kuna ambaye kauli yake inaku-pendeza katika maisha ya duniani,                      naye humshuhudiza Mwenyezi Mungu kwa yaliyo moyoni mwake na hali ni hasimu mkubwa kabisa.

205.  Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi, na huangamiza mimea na viumbe, na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.

206.  Na anapoambiwa. Mche Mwenyezi Mungu, hupand-wa na mori wa kufanya dhambi. Basi Jahannam inamtosha, napo ni makao mabaya mno .

207.  Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja.

Kaashif2-125.jpg

127 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

KAULI ZAO ZINAKUPENDEZA

Aya 204 - 207

MAANA

Baadhi ya wafasiri wapya wamejaza kurasa kwa maneno matamu katika kufasiri Aya hizi, lakini hawakuzidisha chochote zaidi ya kuwagawanya watu kwenye wema na uovu. Kwa dhahiri haya yanajulikana na wote, hayahi-taji ubainifu wowote, sikwambii tafsiri ndefu tena.

Unaweza kuuliza; Ikiwa kugawanyika watu kunajulikana na wote, basi kubainisha kunakuwa ni maelezo ambayo tayari yameshaelezwa na kufafanua lililofafanuliwa na yapasa kuyachukulia maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) vizuri?

Jibu: Inawezekana kuwa makusudio ni kuongoza na kuelekeza kwamba mwenye akili anatakikana kutohadaliwa kwa mambo ya nje wala asimwami-ni mwenye kutegeneza maneno matamu. Kwa sababu wafisadi ni mabingwa wa kazi hiyo na kazi ya ria. Kwa hivyo ni juu yetu kutomtegemea yeyote isipokuwa baada ya kufanya majaribio na kupatikana dalili ya ukweli wake na usafi wake.

Hiyo ndiyo asili ya ujumla inayoenea katika hukumu nyingi za dini na za kidunia; kama kuchagua Hakimu, Kadhi, Naibu, Kadhi, Mufti na kila anayesimamia masilahi ya Umma.

Ajabu ya maajabu ni kutakiwa shahada ya kielimu tu kwa mwenye kuji-tokeza kwa kazi muhimu ya mji au nchi na inayogusa maisha ya watu. Lakini haulizwi uaminifu wake na tabia yake, pamoja na kuwa hayo ndio msingi. Wengi wenye shahada wanazitumia kuwa ni zana za kuibia.

Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza hapa duniani, naye humshuhudia Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali ni hasimu mkubwa kabisa.

128

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Yaani wanadhihihirisha mapenzi na heri na hali wao ndio maadui zaidi wa heri na watu wa heri.

Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi.

Wamehitaliafiana wafasiri kuhusu neno Tawalla. Je makusudio ni kuon-doka na maana yake kuwa ni, anapoondoka kwa yule aliyemdanganya, 'huhangaika katika ardhi kwa ufisadi'. Au kwamba makusudio ni kutawala na usultani, na maana yawe, 'na atakapokuwa mtawala atafanya wanayoyafanya watawala waovu ya kuangamiza mimea na viumbe?'

Mwenye Tafsir Al manar amenakili kutoka kwa Ustadha wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba ameyapa nguvu maana ya utawala kwa kuun-ganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi." Kwa maana ya kuwa mtawala mkaidi anakuwa na kiburi kuongozwa kwenye maslahi au kupewa tahadhari ya mambo ya ufisadi, yeye hujiona yuko juu ya haki; kama vile alivyo juu ya watu wake anaowatawala, basi itawezekanaje kwa mtu kumwambia amwogope Mwenyezi Mungu.

Na huangamiza mimea na viumbe.

Mimea ni kilimo na viumbe ni wanyama. Makusudio ni maslahi yote ya kiuchumi katika kilimo, viwanda na ufugaji, mali ghafi, na mengineyo yanayohusika na uhai wa watu na maisha yao. Mwenyezi Mungu amehu-sisha kutaja kilimo na ufugaji kwa vile viwanda wakati huo havikuwa na umuhimu wowote kama ilivyo sasa.

Uharamu wa mambo hayo kwa mtazamo wa Uislamu ni sawa na uharamu wa kumwaga damu; na mwenye kukusudia ubaya katika vitu hivyo, ndio amekusudia ubaya wa utu hasa; hata kama vitu hivyo ni milki ya adui anayepiga vita Waislamu. Mtume (s.a.w.w.) amekataza kukata miti, kuharibu mimea na majengo na kutia sumu miji ya washirikina siku za vita, n.k. Lau tunailinganisha sharia ya Kiislamu na mambo yanayofanywa

129

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

leo na dola za kikoloni na vita vyao vya silaha za kemikali kwenye mimea, watu na wanyama, na kuitia sumu anga kwa mabomu ya Atomic na kuyatupa kwa wanawake na watoto, lau hayo yote tunayaunganisha na Uislamu, basi tutajua huruma, uadilifu na utu wa Uislamu na unyama wa dola za Magharibi na jinsi zilivyopetuka mipaka katika dhulma na unyang'anyi.

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hapendi ufisadi.

Hakuna uharibifu mkubwa zaidi kuliko kuzusha vita na kutumia silaha zenye kubomoa ili kuwatawala watu na kuwanyang'anya chakula na matunda ya jasho lao.

Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu hupandwa na mori wa kufanya dhambi.

Mtu mwema wenye ikhlasi anakubali masahihisho na nasaha, bali huz-itafuta na kuzikaribisha, kwa sababu yeye hana lengo j engine zaidi ya haki, wala hatafuti sifa; kwa sababu amali yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) sio umashuhuri. Imam Amirul Muminin (a.s.) anasema katika maneno anayowasifu wanaomcha Mwenyezi Mungu:

"Hawaridhii na amali zao chache wala hawakioni kingi kilicho kingi; wao wanajituhumu na wao ni wenye kunyenyekea katika amali zao."

Katika hotuba yake siku za ukhalifa wake alisema: "Mtu hata kama ana cheo kikubwa katika haki na fadhila kubwa katika dini hawezi kuwa hahitajii kusaidiwa katika aliyobebeshwa na Mungu katika haki zake; wala si mwenye kutaka kujitukuza; wala mtu hata kama nafsi zinamfanya mdogo na kudharauliwa na macho sio kuwa hawezi kusaidia au kusaidiwa... Wala msinidhanie kuwa mimi ni mzito katika haki nitakayoambiwa, kwani mwenye kuifanya nzito haki atakayoambiwa au uadilifu atakaoonyeshwa, basi kwake kuitumia haki na uadilifu ni kuzito zaidi."

130

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Hivyo ndivyo anavyotakikana mwanac-huoni mwenye ikhlasi ya kweli. Ama mnafiki mwenye hiana, haki inakuwa nzito juu yake kwa sababu itamfedhehesha; na hununua sifa kwa thamani kubwa ili azibe upungufu wake na uovu wake.

Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu.

Yaani baadhi ya waumini wanaikabili Jihadi na wanapenda mauti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. sawa na wale wengine wanaopenda uhai. Hawana lengo jengine isipokuwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu Zake.

Razi katika kutafsiri Aya hii anasema kuhusu sababu za kushuka kwake kuwa kuna riwaya tatu; Mojawapo ni kwamba Aya hii imeshuka kwa sababu ya Ali bin Abi Twalib (a.s.) alipolala kwenye kitanda cha Mtume wakati wa Hijra, alisimama Jibril kichwani mwake, Mikail miguuni mwake na Jibril: Pongezi! Pongezi! ewe Ali akisema: Mwenyezi Mungu anajionea fahari kwako, mbele ya Malalika.

*7 Sheikh Mudhaffar katika kitabu Dalailu Swidq J2 anasema; "Wale ambao wamenakili kuwa Aya hii imeshuka kwa haki ya Ali, ni Razi, Thaalabi na mwenye Yanabiul-Mawadda, Abu Sadak katika Fadhail itrati twahira, Ghazali katika Ihyai, Hakim katika Mustadrak na Ahmad bin Hanbal katika Musnad. Zaidi ya hizo kuna riwa nyingine zilizopokewa kwa upande wa shia.

131

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

208. Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote, wala msifuate nyayo za Shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

209. Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye heki-ma.

210. Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu na Malaika, na liishe jambo; na mambo yote         hurudishwa kwa

Mwenyezi Mungu.

Kaashif2-126.jpg

132

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

INGIENI KATIKA USALAMA NYOTE

Aya 208 - 210:

MAANA

Enyi Mlioamini! Ingieni katika usalama nyote.

Imesemekana kuwa makusudio ya neno Silmi hapa ni Uislamu, na kwamba msemo unawaelekea wanafiki ambao wameificha kufuru na kudhihirisha Uislamu. Na imesemekana kuwa msemo unawaelekea wenye kumwamini Mwenyezi Mungu katika Ahlul Kitab ambao hawakusilimu. Na ikase-mekana kuwa unawaelekea Waislamu wote kwa hivyo maana yake yanakuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea katika hukumu Zake zote sio baadhi. Na pia imesemekana maana yake ni suluhu kwa maana kuwa ingieni katika suluhu nyote.

Tuonavyo sisi ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemwamrisha mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, kwa imani sahihi kuingia katika lile ambalo lina salama yake ya dunia na akhera. Na njia ya usalama ina-julikana na wote, nayo ni kusaidiana, kuungana, na kuacha vita na uhasama. Vile vile kuyashinda matamanio na kuwa na ikhlasi katika kauli na vitendo.

Makusudio ya maana hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:'Wala msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni aduiwa wazi, Aliyoileta mara tu, baada ya kusema. 'Ingieni katika usalama nyote'.

Hapo Mwenyezi Mungu amezingatia kuwa nyayo za shetani kinyume chake ni usalama; na amemweka mtu mbele ya mambo mawili tu, haku-na la tatu; Ama kuingia katika usalama au kufuata nyayo za shetani ambazo ndio dhati ya uovu, ugomvi, shari na ufisadi.

133 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuingia katika usalama na kukataza kufuatwa nyayo za shetani, amemhadharisha yule atakayehalifu amri yake na makatazo yake na akatishia kwa kusema: "Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima." Mwenye nguvu, hashindwi katika amri Yake wala hakimzuwii chochote kwa alilokusudia kulifanya. Mwenye hekima, humlipa mema mtiifu na humwadhibu mwasi.

Razi anasema: "Huo ndio ukomo wa kiaga kwa sababu ni kuhofisha bila ya kutaja adhabu. Huenda mzazi akamwambia mtoto wake: "Ukiniasi basi wewe wanijua na wajua uwezo wangu kwako", basi maneno hayo yanakuwa ni makemeo ya ufasaha zaidi kuliko kutaja kipigo na mengineyo.

Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu na Malaika.

Maana kwa ujumla ni kwamba wale wenye kukadhibisha na wakaasi watajiwa na adhabu kwa ghafla wala hawataokoka. Aya iko katika mwelekeo wa Aya inayosema:

Kaashif2-127.jpg

"Na hawangoji ila saa ya Kiyama kiwajie kwa ghafla...?" (47:18).

Na lishe jambo; na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu.

Mauti ambayo hapana budi nayo, yakija na Kiyama kikija, kila kitu kitakuwa kimekwisha na hapatabakia mbele ya wenye makosa isipokuwa hisabu na mateso.

134

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

SIRI NA MATUKIO YA GHAFLA

Hakuna yeyote ajuaye yatakayomtokea mbele na siri ya wakati, heri au shari. Hawezi kuyajua hayo vyovyote atakavyokuwa na elimu au imani:

Kaashif2-128.jpg

"Na nafsi yoyote haijui itachuma nini kesho." (31:34)

Mara nyingi mtu hujiwa na heri kwa ghafla wakati yeye anatazamia kupa-ta shari; na hujiwa ghafla na shari wakati anapotazamia heri. Hakuna kitu kinachotia uchungu kama hicho cha kupata shari wakati wa kutazamia heri; kama vile ambavyo hakuna kitu kitamu kama kupata heri wakati wa kutazamia shari.

Mwenye akili hawezi kughurika na alivyo navyo, bali hufikiria mzun-guko wa zama; kama vile ambavyo hakati tamaa na lolote linalompata; kwani dunia inageuka milele; ndio maana ikasemwa; "Kudumu hali ni muhali na faraja inakuja kutokana na dhiki." Imam Ali (a.s.) anasema: "Baada ya dhiki ni faraja.

Anaendelea kusema Imam: "Hakika Musa bin Imran alitoka kuwatafutia watu wake moto akasemeshwa na Mwenyezi Mungu na akarudi akiwa Mtume." Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-129.jpg

"...Hawakati tamaa ya rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri." (12:87).

Kaashif2-130.jpg

Na amesema tena: ... Hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye hasara." (7:99).

135

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Imeelezwa katika vitabu vya Historia na Sera kwamba Ibn Ziyat alikuwa waziri na mtu wa kutegemewa na Mu'utasim, naye alikuwa ni katika mataghuti wa hali ya juu na dhalimu mkubwa. Alitengeneza tanuri la chuma alilolijaza misumari yenye ncha pambizoni mwake. Anapomkasirikia mtu humtupa ndani, kila anavyojitingisha ndivyo misumari inavyomwingia mwilini mwake.

Mutawakkil alipotawala alimshika Ibn Ziyat na akamfunga kwa chuma mikononi mwake na miguuni mwake kisha akamtupa katika tanuri hilo, na baadaye akafa. Kabla ya kufa alisikika akiimba shairi hili:

Sifazake tulia, hebu nenda pole pole, Kigeugeu dunia, huenda nyuma na mbele.

211. Waulize wana wa Israil, ishara ngapi zilizo wazi tulizo-wapa? Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

212. Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani, na wanawafanyia maskhara wale walioamini. Na wale wenye takua watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu hum-ruzuku amtakaye bila his-abu.

Kaashif2-131.jpg

136

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

WAULIZE WANA WAISRAIL

Aya 211 - 212

MAANA

Waulize wana wa Israil, ishara ngapi zilizo wazi tulizowapa?

Makusudio ya waulize hapa sio swali hasa la kihakika, kwa sababu Mtume (s.a.w.) anajua hali zao, wala makusudio sio kuelezea hali waliyokuwa nayo; kama ilivyo katika Aya ya 49 na inayofuatia. Isipokuwa makusudio hasa ni kuwa Waislamu wazingatie na wapate funzo na hali ya Waisrail.

Njia ya kupata funzo ni kuwa Waisrail walijiwa na Mtume Musa (as)kwa miujiza na hoja ambayo ni mkono kuwa mweupe, fimbo kugeuka nyoka na kupasuka bahari. Vile vile kufunikwa na wingu, kuteremshiwa Manna na Salwa na jabali kutoka maji. Pamoja na hayo yote waliasi na kukhali-fu, ndipo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa madhila na utwevu katika dunia na adhabu iumizayo katika Akhera.

Na Waislamu nao wamejiwa na Muhammad (s.a.w.w.) kwa miujiza na hoja zinazofahamisha ukweli wa Utume wake na kuswihi sharia yake; naye akawafikilizia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa waaingie katika Uislamu wote, kwani humo watapata heri na utengeneo wao; kama wakiasi kama walivyofanya Waisrail, basi yatawapata yaliyowapata Waisrail.

Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. Makusudio ya neema hapa ni dalili za haki, kwani hizo ni katika neema kubwa. Kwa sababu ndani yake mna uongofu na kuokoka na kuhiliki na upotevu. Makusudio ya kuzibadilisha ni kuziasi na kuziharibu. Kwa hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia" ni sawa na kauli yake:

137

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-132.jpg

"Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu..." (2:209).

Vile vile kusema kwake:

"Basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" ni sawa na kusema:

Kaashif2-133.jpg

"Kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima." (2:209)

Maana ni moja na lengo ni moja.

HAPANAIMANI BILA TAKUA (UCHA MUNGU)

Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani.

Hapana tofauti kati ya mwenye kukanusha kuwapo Mwenyezi Mungu na yule mwenye kuamini kinadharia tu, lakini matendo yakawa ni tofauti. Hapana tofauti kati ya wawili hao. Kwa sababu kila mmoja ameathiriwa na dunia na vipambo vyake, ameathirika na kitu cha sasa hivi kuliko cha muda ujao; heri na manufaa ameyapima kwa kiwango cha manufaa yake, wala hakupima na mambo aliyoharamisha Mwenyezi Mungu wala na msi-mamo wa kibinadamu.

Mimi kila ninavyozidi kuzama katika tafsiri ya Qur'an na kuangalia kwa undani Aya zake, basi huwa na yakini zaidi kwamba imani bila ya ucha Mungu haina maana yoyote; na kwamba kila anayeiangalia dunia kuwa ndio makusudio yake yote, basi atakuwa ameiweka mbali sharia ya haki na dini, atake asitake.

138

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Imekuja Hadith Mutawatir kutoka kwa Mtume Mtukufu akisema: "Dunia na akhera zina madhara" yaani zinadhuriana kuhujumu moja yao nikuiacha nyingine. * 8

Imam Ali (a.s.) anasema: "Hakika dunia na Akhera ni maadui wawili wanaotofautiana, na ni njia mbili tofauti. Mwenye kuipenda dunia ataichukia akhera na kuwa adui yake; zote mbili ni kama Mashariki na Magharibi, mwenye kutembea kati yao huwa mbali na nyingine kila anapokaribia moja wapo."

Na wanawafanyia maskhara wale walioamini.

Ni kawaida wale wanaozichezea Hoja za Mwenyezi Mungu na hukumu zake wakihalalisha damu na mali ya haramu kuwadharau na kuwachezea wale wanaojilinda na maharamisho na kuvumilia tabu na mashaka kwa ajili ya kumridhisha Mungu.

Na wale wenye takua watakuwa juu yao siku ya Kiyama.

Amesema wenye takua wala hakusema wale walioamini, kwa sababu imani bila takua si lolote; kama tulivyobainisha. Maana yako wazi ni kuwa makafiri wakiwadharau waumini hivi sasa, basi mambo yatabadilika kesho. Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-134.jpg

Hakika hizaya na ubaya leo itawafika makafiri." (16:27).

Kaashif2-135.jpg

"Basi leo wale ambao wameamini wanawacheka makafiri."(83:34)

*8 Kuna Hadith nyingine inayosema: "Si mbora wenu yule mwenye kuacha dunia kwa akhera, wala akhera kwa dunia lakini mbora wenu ni yule atakayechukua hii na hii . Mumin mwenye nguvu ni bora kuliko dhaifu.".

139

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hisabu.

Riziki ni mbili ya dunia na riziki ya Akhera. Riziki ya dunia inajulikana na riziki ya Akhera, ni neema isiyokatika na isiyokuwa na chembe ya huzuni au hofu. hataipata yeyote isipokuwa kwa imani na amali njema: Anasema Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-136.jpg

"Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa Peponi, humo watakaa milele." (2:82).

Kila mtu anaweza kupata riziki duniani, awe ni kafiri au Mumin, mwema au mwovu, na anayehangaika au asiyehan-gaika; kama vile urithi, zawadi, wasiya, n.k. Vile vile inaweza kupatikana kwa njia ya halali, au haramu, kama vile kunyang'anya, kughushi na utapeli.

Mwenye Tafsir Al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba, amesema wakati wa kutafsiri Aya hii, kwamba riziki bila ya kuhangaika inaweza ikapatikana kwa baadhi ya watu. Ama kwa Umma ni muhali kujitosheleza isipoku-wa kwa kuhangaika na kufanya kazi. Huo ni ukweli ulio wazi kabisa.

140

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

213. Watu wote walikuwa wa mila moja.         Basi Mwenyezi

Mungu akapeleka Manabii watoao bishara na waonyao. Na pamoja nao akawa-teremshia kitabu kina-choshikamana na haki ili kihukumu baina ya watu katika yale waliohitilafiana. Na hawakuhitilafiana katika hayo ila wale waliopewa Kitabu, baada ya kuwafikia ubainifu, kwa sababu ya uha-sidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu akawa-ongoza kwenye haki walioami-ni katika yale waliyohitilafiana kwa idhini yake.         Na

Mwenyezi Mungu humwon-goza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

WATU WOTE WALIKUWA MILA MOJA

Aya 213:

LUGHA

Mwenyezi Mungu amelitumia tamko Umma katika kitabu chake, kwa maana nyingi, kama vile Mila Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-137.jpg

141

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-138.jpg

"Hakika mila yenu hii ni mila moja." (21:92)

Au kwa maana ya kundi - Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-139.jpg

"Na katika wale tuliowaumba wako watu wanaoongoza kwa haki tu... (7:181).

Pia limekuja kwa maana ya muda; kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

Kaashif2-140.jpg

"Na kama tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwisha hisabi-wa..." (11:8).

Vile vile kwa maana ya Imam anayefuatwa - Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-141.jpg

"Hakika Ibrahim alikuwa mfano (wa kufuatwa) mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu..." (16:120).

142 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Ama makusudio ya neno Umma katika Aya hii tunayoifasiri, ni mila.

MAANA

Kauli za wafasiri zimegongana katika kuelezea maana ya aya hii. Razi ameifafanua kwa kiasi cha kurasa saba. Ama mwenye Tafsir Al - Manar ameifaf-anua kwa kurasa ishirini na mbili na kumwacha msomaji wa kawaida patupu, bila ya kuambua chochote. Na sisi, kama kawaida yetu, tumo katika njia yetu ya kumfanyia wepesi yule msomaji wa kawaida, kwa kiasi kile kitakachoafikiana naye. Kwa hivyo ufafanuzi wake ni kwa uwazi na ufupi, ili aweze kuangalia vizuri Aya za Mwenyezi Mungu kwa wepesi na kuathirika nafsi yake. kama kunakuwa na maudhui muhimu, tunayaeleza katika kifungu cha peke yake.

Watu wote walikuwa mila moja.

Yaani walikuwa wa umbile ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia watu na ambalo Mtume (s.a.w.w.) ameliashiria kwa kusema: "Kila anayezali-wa huzaliwa kwenye fitra (umbile la usawa)." Mwenye Majmaul Bayan anasema: "Masahaba wetu wamepokea kutoka kwa Imam Abu Jaffar al Baqir, kwamba kabla ya Nuh watu walikuwa mila moja ya umbile alilowaumba Mwenyezi Mungu - si wenye kuongoka wala kupotea; Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume. Kwa hivyo maana yake ni kwamba wao walikuwa ni wenye kuabudu kulingana na akili zao bila ya uongofu wa Mitume wala sharia."

Kisha wakajiliwa na mawazo na fikra ambazo ziliwapeleka katika tofauti ya itikadi na rai, hatimaye kwenye uadui. Kwa hivyo wakagawanyika vikundi vikundi baada ya kuwa ni wa mila moja. Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume na kitabu kinachosema kweli na kinachohukumu mizozo yao. Haya ndiyo maana yaliyo wazi ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

* 9 Imeelezwa katika Tafsiri Rawhul-bayan kwamba baina ya Adam na kupewa Utume Nuh kuna kiasi cha miaka themanini (80)

143 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Basi Mwenyezi Mungu akawaleta Manabii watoao bishara na waonyao.

Na pamoja nao akawateremshia kitabu kilichoshikamana na haki ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitalifiana."

Hapa inatubainikia kwamba katika maneno kuna jumla iliyokadiriwa ambayo ni : "Watu walikuwa wa mila moja kisha wakahitalifiana"

Linalofahamisha hilo ni kauli inayosema: "Ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitalifiana." Na hilo linatiliwa nguvu na kauli hii:

Kaashif2-142.jpg

"Na watu hawakuwa isipokuwa wamila moja; kisha wakahitalifiana.. ."(10:19).

Na hawakuhitilafiana katika hayo ila waliopewa kitabu, baada ya kuwafikia ubainifu, kwa sababu ya uhasidi baina yao.

Yaani: Watu ambao walikuwa ni umma mmoja, kisha wakahitalifaina na Mwen-yezi Mungu akawapelekea Mitume, watu hao pia walihitalifiana katika Mtume alieyepelekwa; wengine waliamini na kusadiki na wengine wakakufuru na kukadhibisha baada ya kusimama hoja na dalili wazi za mkato. Hakuna sababu yoyote ya kukadhibisha huku isipokuwa uhasidi na kuhofia manufaa yao ya kibinafsi na uadui.

Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongoza kwenye haki walioamini katika yale waliyohitalifana kwa idhini yake.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewafikisha wenye nia njema kwenye imani ya haki aliyokuja nayo Mtume; na imani hiyo ni kwa amri yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Kwa hiyo makusudio ya idhini ni amri. Na Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye kwenye njia iliy-

144

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

onyooka.

Katika kufasiri Aya ya 26 ya Sura hii kifungu cha uongofu na upotevu, tumetaja maana ya uongofu ambayo miongoni mwake ni: Kukubali mtu nasaha na kuzitumia; na hayo ndiyo makusudio yake hapa. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawaafikisha watu wema kukubali nasaha na kufanya vitendo vya haki na heri.

TOFAUTI KATI YA WATU

Kulipatikana kutofautiana kati ya watu tangu Qabil alipomuua nduguye Habil; kunaendelea hadi leo na kutabaki hadi siku ya mwisho. Kutofautiana hakuhusiki na watu wa dini tu; kama wanavyodai wasio-jua hakika ya mambo. Kwani tunaona kutofautiana kusikokuwa kwa dini kumefikia kugeuka maneno na kuwa vita vya kumalizana. Ugomvi kati ya dola za kibepari kumepelekea vita vya Atomic. Bomu lilitupwa Hiroshima kwa wanawake na watoto na dola ya kibepari dhidi ya dola nyingine ya kiberi pia. Na kugawanyika mwelekeo kwa dola za kijamaa kunaeleweka. Vile vile dola za Kiafrika na Kiesia zinatofautiana kulingana na upande wa wanyonyaji wanaozinyonya. Ama kutofautiana kwa dola za Kiarabu matokeo yake ni kupatikana Israil ndani ya nchi yao na hati-maye kusalimu amri mnamo tarehe 5 June, 1967.

Hali yoyote iwayo, kutofautiana kuna sababu nyingi, kama vile: Kutofautiana katika malezi na maendeleo, katika tabia na akili na kutofautiana kunakotokana na mgongano wa masilahi na manufaa ya kiutu.

Tofauti inayotokana na maendeleo, akili na tabia inaweza kurekebishwa kwa kufanya yale yanayoafiki misingi iliyothibitishwa na elimu na majaribio. Lakini tofauti zinazotokana na kugongana kwa manufaa ya kiutu hazina dawa isipokuwa kumzuwia adui kwa nguvu.

Maelezo yetu haya, ni kukamilisha tuliyoyasema katika kufasiri Aya ya 113 kifungu cha "Kila mmoja anavutia dini yake."

145 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-143.jpg

214. Au mnadhani kuwa mtaingia Peponi na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara, na wakasukwasukwa hata akase-ma Mtume na wali-oamini pamoja naye: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu.

KUINGIA PEPONI

Aya 214:

MAANA

Au mnadhani kuwa mtaingia peponi na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara.

Hakika Aya hii tukufu inamwelekea kila mwenye kuamini haki, akaitu-mia na akailingania. Inasema waziwazi kwamba desturi ya Mwenyezi Mungu kwa wanaoinusuru haki, ni kuitolea thamani yake wao wenyewe, watu wao na hata mali zao. Vile vile kuvumilia adha na kuwa na subira juu ya masaibu na shida. Waliokuwa kabla yenu walipambana na aina za maudhi wakasubiri; Je, nanyi mtasubiri kama walivyosubiri? Au nyinyi mnataka kuingia peponi bila ya kuilipia thamani. Na mwenye pepo hiyo amekataa isipokuwa thamani yake iwe ni imani, ikhlas na kuvumilia hofu, njaa na upungufu wa mali na nafsi!

146

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Yamekuja maelezo katika khutba mojawapo ya Nahjul Balagha: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akisema: 'Hakika pepo imezungukwa na machukivu na moto umezungukwa na anasa; na jueni kuwa hakuna katika twaa ya Mwenyezi Mungu isipokuwa huwa machukivu na hakuna katika maasi ya Mwenyezi Mungu isipokuwa anasa.'"

Kwa faida zaidi ni vizuri msomaji arudie tuliyoyataja katika kufasiri Aya ya 155 kifungu 'Thamani ya pepo.'

Na wakasukwasukwa hata akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini?

Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini, ni swali kutoka kwa Mtume na waumini, linaloleta picha ya misukosuko na shida walizozipata kutoka kwa maadui wa haki na makundi ya batili

Maana kwa ujumla ni kwamba walionusuru haki, waliotangulia, walipatwa na shida na wakaingia katika misukosuko mpaka wakadhani kwamba nusura imechelewa, hivyo wakaitaka ije haraka kwa kusema: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini? Mwenyezi Mungu naye akawajibu kwa kusema:

Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu.

Aya hii iko katika mwelekeo wa Aya isemayo:

Kaashif2-144.jpg

"Hata Mitume walipokata tamaa, wakadhani ya kwamba wamekadhibish-wa, msaada wetu uliwajia..." (12:110)

147

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-145.jpg

215. Wanakuuliza watoe nini? Sema:           Kheri yoyote

mtakayotoa ni kwa ajili ya wazazi wawili na akraba na mayatima na masikini na mwana njia. Na kheri yoyote mnaoufanya         Mwenyezi

Mungu anaujua.

WATOE NINI? Aya 215:

MAANA

Wanakuuliza watoe nini?

Msemo unaelekezwa kwa Mtume (s.a.w.w.).

Sema: Kheri yoyote mtakayotoa ni kwa ajili ya wazazi na akraba na mayatima na masikini na mwananjia. Makusudio ya neno kheri hapa ni mali. Wazazi wawili ni baba, mama, babu na bibi, kwa sababu wao wanaingia katika jina la wazazi wawili. Ndugu ni akraba wa karibu wa mtoaji, yatima ni asiyekuwa na baba na mwana njia ni yule aliyeishiwa njiani na kushindwa kufika kwa watu wake na wala hana chakula.

Unaweza kuuliza kuwa dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa watu waliuliza aina ya kitakachotolewa sio nani wa kumpa. Na jibu ni la matumizi sio la aina, sasa je, imekuwaje?

Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya jawabu ni kumzindua

148

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

muulizaji kwamba yeye anatakikana kuuliza nani wa kumpa, sio nini atoe. Razi amemnakili Qafal kwa jibu jingine; nalo nikuwa hata kama swali liko kwa tamko la Ma (nini) lakini kilichoulizwa ni nani wa kumpa sio cha kutoa, kwa sababu cha kutoa kinajulikana.

Sheikh Muhammad Abduh ameyatilia mkazo hayo kwa kauli yake: "wasomi wa fani ya mantiki ndio waliosema, swali la Ma linahusika na aina na jinsi..." Lakini waarabu wanatumia kwa aina. Qur'an haiko kati-ka mfumo wa Aristotle na mantiki yake, isipokuwa iko katika mfumo wa lugha ya Kiarabu ulio waziwazi. Jibu hili lina nguvu kuliko la kwan-za ingawaje natija ni moja.

Swali la pili: "Je kuwapa waliotajwa katika Aya hii, ni wajibu au sunna?

Jibu: Ni wajibu kwa wazazi kuwalisha watoto, na watoto kuwalisha wazazi ikiwa upande mmoja una uwezo na mwengine hauna uwezo wa kujilisha wenyewe. Kutoa huku hakuhisabiwi kuwa ni zaka. Ama may-atima na wasa-firi, inajuzu kuwapa kutokana na zaka ya wajibu; kama vile ambavyo inajuzu kuwapa wote sadaka ya sunna.

Na sadaka ya suna hupewa kila mwenye kuhitajia, awe Mwislamu au si Mwislamu, kwa sababu kuna malipo katika kumnywesha kila mwenye ini la joto (kiu); kama ilivyoelezwa katika Hadith.

149

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

216. Mmeandikiwa kupigana (vita) nalo ni (jambo) la kuchukiza kwenu. Na huen-da mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

217. Wanakuuliza juu ya kupigana (vita) katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita katika (miezi) hiyo ni (dhambi) kubwa. Na kuzuilia watu na njia ya Mwenyezi Mungu na kumkufuru na (kuwazuilia) Msikiti Mtakatifu na kuwa-toa humo wenyewe ni kukubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni kubwa zaidi kuliko kuua. Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika dini yenu, kama waki-weza. Na yeyote katika nyinyi atakayertadi, kisha akafa hali ya kuwa kafiri, basi hao zimepomoka amali zao duniani na akhera. Na hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele.

Kaashif2-146.jpg

150

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-147.jpg

218. Hakika wale walioamini na wale           waliohama na

wakafanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu           ni

Mwenye kughufiria, Mwenye kurehemu.

MMEANDIKIWA KUPIGANA VITA

Aya 216 - 218:

MAANA

Mmeandikiwa kupigana vita.

Mmeandikiwa hapa ni kwa maana ya mmewajibishiwa zilivyo Aya kad-haa zenye neno hilo.

Mwenyezi Mungu amewajibisha vita kwa Waislamu si kwa kuwa vita vinapendeza au vinatakiwa mara kwa mara. Pia si kwa ajili ya kupanua nchi na kutawala au kunyonya mataifa mengine, isipokuwa au Mwenyezi Mungu amewajibishia kwa ajili ya kuinusuru na kuitetea haki.

Kwa sababu haki pekee, ni fikra na nadharia tu. Ama kuifuatilia na kulaz-imiana nayo kunahitaji kazi ngumu, ambayo kwanza ni kuilingania kwa hekima na kwa njia iliyozoeleka. Kama haikuwezekana, basi ni wajibu kuitekeleza haki kwa nguvu. Nadharia yoyote isiyotegemea nguvu za kiutekelezaji, basi kuwepo kwake na kutokuwepo ni sawa.

Ni kwa ajili hii ndipo Mwenyezi Mungu akawajibisha, katika Aya hii na nyinginezo, kupigana jihadi na kila adui wa haki, ikiwa hakuna faida

151

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

kwake kumwamrisha mema na mawaidha mazuri. Lau si nguvu za kiutekelezaji, basi nguvu za kisheria zingekuwa ni maneno yanayosemwa mdomoni na kuandikwa tu.

Nalo ni (jambo) la kuchukiza kwenu. Na huenda mkachukia kitu nacho ni heri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamujui.

Wafasiri wanasema kwamba masahaba wa Mtume walichukia vita, kwa sababu ni tabia ya mwanaadamu kuona uzito kujiingiza katika jambo litakalomwangamiza. Lakini wakati huo huo wanaitikia amri ya Mwenyezi Mungu kwa kutaka radhi Yake; sawa na mgonjwa anayekunywa dawa kwa kutaka kupona. Na Mwenyezi Mungu akawazindua kwa kauli yake: "Huenda mkachukia kitu nacho ni heri kwenu" kwamba matunda ya vita na jihadi yanawarudia wenyewe na sio Mwenyezi Mungu.

Huu ndio ufupi wa waliyoyasema wafasiri. Na dhahiri ya Matamshi inak-ubaliana nayo, lakini tukiwaangalia masahaba wenye ikhlasi na ushujaa katika jihadi, kujitolea kwao kwa ajili ya dini na jinsi dini ilivyotawala hisia zao. Vile vile jinsi walivyopuuza uhai kwa kutaka kufa mashahidi mpaka ikawa anayeokoka vitani na kurudi salama anajiona ni mwovu tukiangalia yote haya na kuyatia akilini mwetu, wakati wa kufasiri Aya hii, tutaona kuwa, haielekei kwa masahaba kuchukia vita, na kwamba hapana budi kufasiri Aya kwa maana nyingine itakayochukuana na matamko.

Kwa ufupi maana ni kuwa masahaba walikuwa wakiogopa kuwa Uislamu utamalizwa na washirikina kutokana na idadi yao kuwa kubwa na ya Waislamu kuwa ndogo; kwamba wao wataangamia kusibakie atakaye-unusuru Uislamu, na mwito wa Kiislamu uende bure.

Kwa hiyo walikuwa wakihofia Uislamu, sio nafsi. Ndipo Mwenyezi Mungu akawabainishia kuwa vita mnavyoitiwa na kuvichukia ni bora kwenu na kwa ajili ya Uislamu, na kwamba kukaa tu, kutapelekea kumalizwa nyinyi na Uislamu; na nyinyi hamjui hakika hii, lakini

152 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Mwenyezi Mungu anajua, kwa sababu kwake halijifichi lolote. Aya iko katika mwelekeo wa kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-148.jpg

"Ewe Mtume! Wahimize walioamini waende vitani. wakipatikana kwenu watu ishirini wanaosubiri watawashinda mia mbili. Na kama wakiwa watu mia moja kwenu watawashinda elfu moja ya wale waliokufuru, maana wao ni watu wasiofahamu." (8:65)

"Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana (vita) katika (miezi) hiyo ni dhambi kubwa.

Yamekwishapita maelezo katika kufasiri Aya ya 192 na inayofuatia hiyo.

Na kuzuilia watu na njia ya Mwenyezi Mungu na kumkufuru na (kuwazuilia) msikiti mtakatifu na kuwatoa humo wenyewe ni makub-wa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Waarabu walikuwa wakijizuilia kupigana katika miezi mitukufu ambayo ni Dhul-Qaada, Dhul-Hijja, Muharram na Rajab (mfunguo pili, mfunguo tatu, mfunguo nne na mfunguo kumi). Mtume naye akaithibitisha ada hii, kwa sababu inapunguza shari na umwagikaji damu. Kwa ujumla Uislamu umethibitisha kila ada nzuri au isiyokuwa mbaya iliyokuwa wakati wa Jahilia.

Hata hivyo Waarabu waliokuwa wakiitukuza na kuitakasa miezi hii, walivunja miiko yake na wakatangaza kupigana vita na Mtume katika mwaka wa sita Hijriya; wakamzuwia pamoja na masahaba zake kuzuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kumfitini mwenye kusilimu;

153 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

wakawa wanamwadhibu kwa aina aina ya adhabu kwa muda wa miaka kumi na tatu; kama walivyofanya kwa Bilal, Suhaib, Khabbab na Ammar bin Yasir pamoja na baba yake na mama yake.

Lakini Waislamu wanapotaka kujikinga au kulipiza kisasi kwa washiriki-na, basi washirikina huanza kupiga mayowe kwa propaganda za upotevu, kwamba Waislamu wamevunja miko. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawabainishia kuwa makosa waliyoyafanya wao kwa Waislamu ni makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kupigana katika miezi mitukufu. Na kwa ajili hii Waislamu wamehalalishiwa kupigana na washirikina mahali popote na wakati wowote watakapowapata kwa kuchukua kisasi.

Na fitina ni kubwa zaidi kuliko kuua.

Yaani kuwafitini Waislamu na dini yao, mara nyingine kwa kuwaadhibu na mara nyingine kujaribu kuwatia shaka katika nyoyo zao, ni mbaya zaidi kuliko kupigana katika miezi mitukufu.

Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika dini yenu, kama wakiweza.

Lengo la washirikina ni kutobakia athari yoyote ya Uislamu duniani. Na ni kwa ajili hii tu, ndio wanapigana na Waislamu, na wanaendelea kupigana nao.

Basi kama Waislamu wakichukia kupigana na washirikina, lengo la maadui litatimia.

Roho hii ya kikafiri ya kiadui, inaendelea mpaka leo popote pale penye harufu ya Uislamu; inaendelea katika nafsi za wengi katika mashariki na magharibi. Sababu ya kwanza ya uadui kwa Uislamu ni utu wake, uadili-fu wake na kuzuia kwake dhulma na ufisadi. Kwa sababu hiyo ndio wanawakusudia na kila shari na kuwapiga vita kwa nyenzo mbalimbali. Vile vile kuwafitini kulingana na hali ilivyo. Kwa hiyo ni juu yetu kuzin-duka na maadui hawa na kuwapiga vita kwa silaha ile ile wanayotupiga nayo.

154

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Na yeyote katika atakayertadi, kisha akafa hali yakuwa kafiri, Basi hao zimepomoka amali zao katika dunia na Akhera . Na hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele.

Hii ni hadhari kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa mwenye kuwaitikia maadui na kutoka dini yake, basi mtu huyo amepata hasara ya duniani na akhera na mwisho wake ni Jahannam ambayo ni marejeo mabaya.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Kisha akafa hali yakuwa kafiri," inafa-hamisha waziwazi kwamba mwenye kurtadi (kutoka) katika dini, akitubia kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu huikubali toba yake na huondokewa na adhabu; na akili inakubaliana na hilo. Lakini mafaqihi wa kishia wame-sema: Ikiwa ni mwanamume na kutoka kwake kukawa kunatokana na kuzaliwa; kisha akatubia, basi ataondokewa na adhabu ya akhera tu, ama ya duniani ambayo ni kuuliwa itakuwapo. Kama kukiwa kutoka kwake kunatokana na mila basi hatauawa.* 10 Katika ufafanuzi huu wametege-mea riwaya za Ahlul bait (a.s.).

Maana ya kupomoka amali zao katika dunia ni kuwa wao watafanyiwa muamala wa kikafiri kuongezea kustahiki kuuawa. Ama kupomoka amali zao huko akhera, ni adhabu na mate so.

Hakika wale walioamini na wale waliohama na wakafanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kutarajia rehema ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutaja hali ya washirikina na waliotoka katika Uislamu na kutaja adhabu yao, amefuatishia kutaja waumini na malipo yao.

* 10 Kuzaliwa ni kuwa mwislamu na wazazi wake au mmoja wao ni Mwislamu na mila ni kuwa wazazi wake ni makafiri, kisha yeye akasilimu baadaye akatoka kwenye Uislamu.

155 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

waliohama (Muhajirina) ni wale kutoka Makka kwenda Madina pamo-ja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na waliofanya jihadi ni wale waliotoa juhudi zao katika kuunusuru Uislamu na kupigana na maadui zake.

IBADAYAMWENYE KUTUBIA BAADA YA KURTADI (KUTOKA KATIKA UISLAMU)

Mwenye kutoka katika Uislam (murtadi) akitubia na akarudi katika Uislamu kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu humkubalia toba yake kwa huku-mu ya kiakili na kwa dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Kisha akafa hali yakuwa kafiri" alipounganisha kupomoka amali na kufa katika hali ya kafiri.

Hapo basi yanakuja maswali mawili: Swali la Kwanza: Je, ibada zake kama vile swala, Hijja, Saumu na Zaka, zitasihi baada ya kurudi kwenye Uislamu?

Mafaqihi wa Kisunni wameafikiana kuwa zinasihi na kukubaliwa. Mafaqihi wa Kishia wameafikiana kwamba zinazokubaliwa ni za yule wa mila, na wamehitalifiana katika wa kuzaliwa. Wengi wao wamesema hazisihi kwa hali yoyote na kwamba Uislamu wake baada ya kuutoka, haumfai na chochote katika dunia kabisa, bali atatendewa muamala anao-fanyiwa kafiri;isipokuwa Uislamu wake utamfaa akhera tu, kwa kuon-dokewa na Adhabu. Lakini wahakiki wa mambo katika Shia wamesema, bali zinasihi ibada zake, na utamfaa Uislamu wake na atafanyiwa muamala wa Kiislamu. Nasi tuko pamoja nao.

Swali la Pili: Je, Murtadi akirudi katika Uislam atalazimika kulipa ibada zake alizozifanya wakati alipokuwa Mwislamu kabla ya kurtadi.

Hanafi na Maliki wamesema, atalazimika kulipa. Na Shafii amesema hatalazimika.

156

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Ama Mafaqihi wa Kishia wamesema kuwa zinasihi ibada za mwenye kutubia baada ya kurtadi, wao wanasema mtu halipi chochote alichok-ifanya wakati ni Mwislamu, isipokuwa atalipa yaliyompita wakati wa kutoka Uislamu (kurtadi).

KUPOMOKA

Mu'utazila wamesema kuwa thawabu za Mumin mtiifu zinaanguka zote kwa maasi yatakayofuatia; mfano hata mwenye kuabudu umri wake wote, kisha akanywa tama moja tu la pombe, basi ni kama ambaye hakumwabudu Mwenyezi Mungu kabisa. Vile vile twaa inayofuatia inaon-doa madhambi yaliyotangulia; na hayo ndiyo maana ya kupomoka amali.

Shia Imamiya na Asha'ri wameafikiana kuwa hakuna kuharibika; wakasema kila amali ina hisabu yake inayoihusu; wala twaa haifungamani na maasi, nayo hayafungamani na twaa, bali atakayefanya wema (hata) uzani wa sisimizi atauona. Mwenye kufanya uovu na wema akiwa muumini Mwenyezi Mungu ataupima wema wake na uovu wake. Ikiwa wema utazi-di, atakuwa kama ambaye hakufanya uovu, kwa sababu wingi unafuta uchache. Ikiwa yote ni sawa, basi atakuwa kama ambaye hakutokewa na lolote.

Kupomoka kuko mbali sana na maana haya; maana yake hasa ni mwenye kufa akiwa kafiri baada ya kuwa Mwislamu, ukafiri wake huu utakuwa unafichua amali zake alizokuwa akizifanya wakati wa kusilimu, kuwa hazikuwa katika njia inayotakikana tangu mwanzo; sio kwamba alistahiki thawabu kisha zikafutwa, bali hili ni katika upande wa kuzuwia sio kuon-doa; yaani thawabu hazikuwepo.

157

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

219. Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo mna madhara makub-wa na manufaa kwa watu, na madhara yake ni makub-wa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Vilivyowazidia. Namna hii Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya mpate kufikiri.

220.  Katika dunia na akhera. Na wanakuuliza kuhusu maya-tima.                        Sema: Kuwatengenezea ndiyo heri. Na kama mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu. Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadi na mtengenezaji. Na kama angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwatia katika dhiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu,Mwenye hekima.

Kaashif2-149.jpg

158

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

ULEVI NA KAMARI Aya 219 - 220: LUGHA

Limetumiwa neno Khamri, lenye maana ya kufunika, kwa maana ya ulevi, kwa sababu ulevi unafunika akili. Na limetumiwa neno May sir, lenye maana ya wepesi, kwa maana ya kamari, kwa sababu chumo la kamari linakuwa j epe si bila ya j asho.

MAANA

Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari.

Waliuliza baadhi ya Waislamu kuhusu hukumu ya ulevi na kamari katika Madina; yaani zaidi ya miaka 13 tangu ulipoanza mwito wa Kiislamu. Hiyo inafahamisha kuwa hukumu ya pombe ilikuwa imenyamaziwa muda mrefu, kama zilivyonyamaziwa baadhi ya hukumu za haramu mpaka wakati wake maalum, kulingana na masilahi. Mara nyingine kubainisha hukumu kunataka hekima ya kuchukulia mambo pole pole.

Inasemekana kuwa ubainifu wa hukumu ya pombe ulikuwa hivi, kwa sababu Waislamu walikuwa wameizoweya wakati wa Ujahiliya (kabla ya kuja Uislamu); lau wangelizuiliwa mara moja tu, ingelikuwa uzito kwao. Bali Mwenyezi Mungu aliwakumbusha Waislamu walipokuwa Makka kwamba katika j umla ya neema zake ni kwamba wao wanafanya ulevi na kupata riziki kutokana na tende na zabibu. Anasema Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-150.jpg

"Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri..." (16:67)

159

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Waliuliza baadhi ya Waislamu kuhusu hukumu ya pombe na kamari, Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwajibu: Katika hivyo madhara makubwa na manufaa kwa watu na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Jawabu hili peke yake halitoshi kuwa ni dalili ya uharamu wa ulevi. Kwa sababu hakusema kuwa ni haramu; linafahamisha kawaida ya kujikinga na madhara ni bora kuliko maslahi, na muhimu inatanguliwa na muhimu zaidi.

Lakini tukiangalia Aya isemayo:

Kaashif2-151.jpg

"Sema: Mola wangu ameharimisha mambo maovu yaliyodhihirika na yaliyofichika na madhara na uasi pasipo haki..." (7:33)

Tukiiunganisha Aya hiyo na hii tunayoizungumzia tutapata dalili ya kuharimishwa ulevi waziwazi na kwa mkato. Kwa sababu natija inay-opatikana ni kuwa ulevi ni madhara na madhara ni haramu, kwa hivyo ulevi ni haramu.

Hiyo ni pamoja na kuongezea Aya inayosema:

Kaashif2-152.jpg

"Enyi mlioamini! Hakika ulevi na kamari na masanamu na mishale ya kuti-zamia (ramli) ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili

160

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

mpate kufaulu. Hakika Shetani anataka kuwatilia uadui na bughudha baina yenu kwa ulevi na kamari kuwazuilia na kumkumbuka Mwenyezi Mungu na Kuswali. Basi je, mtaacha?" (5:90 - 91)

Kwa hiyo kusema jiepusheni navyo ni amri ya kujiepusha, na amri inafa-hamisha wajibu. Na kusema basi je mtaacha! Ni kukataza, na kukataza kunafahamisha uharamu. Ndipo Waislamu waliposikia Aya hii wakasema: "Tumeacha."Ama ile Aya inayosema:

Kaashif2-153.jpg

"Enyi mlioamini msiikurubie swala hali mmelewa..."(4:43)

ilishuka kabla ya Aya (5:90-91), ambazo zina uzito mkubwa. Tumeeleza kwamba huenda ilikuwa ni hekima ya kuchukulia mambo pole pole katika kubainisha uharamu, kwa vile kutoikurubia swala hali mme-lewa haina dalili yoyote ya kuonyesha uhalali wa pombe katika isiyokuwa swala. Tutafafanua Inshaallah tutakapofikia Aya hizo.

Zaidi ya hayo Waislamu wote tangu mwanzo hadi hivi leo wamekonga-mana kwa kauli moja tu! Kuwa ulevi ni katika madhambi makubwa, na kwamba mwenye kuuhalalisha siye Mwislamu. Na mwenye kuinywa kwa kupuuza ni fasiki na atapigwa (Had) viboko themanini.

Imekuja Hadith Mutawatir kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba ame-laaniwa mwenye kupanda mti wa (hiyo pombe), mwenye kuigema, mwuzaji, mnunuzi, mwenye kuhudumia wanywaji na mnywaji. Na imeelezwa katika baadhi ya hadith kwamba hakuna sharia yoyote ya mbinguni ila imekataza ulevi.

Tumeyaeleza kwa ufafanuzi zaidi maudhui haya katika juzuu ya nne ya kitabu "Fiqhul Imam Jaffar Sadiq " katika mlango wa vyakula na viny-waji.

161

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Makusudio ya ithm hapa ni madhara. Madhara ya pombe yanadhihirika kati-ka mwili, akili na mali na vile vile kuacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kugom-bana na kufanya mambo yaliyoharamishwa.Wanahistoria wanasema kwamba baadhi ya walevi walizini na mabinti zao.

Abbas bin Mirdas, alikuwa kiongozi wa watu wake, katika zama za Jahiliya (kabla ya Uislamu) alijiharimishia pombe yeye mwenye tu kwa maumbile yake. Alipoulizwa sababu, akasema: "Siwezi kuchukua ujin-ga kwa mkono wangu nijiingize mwenyewe, wala siko radhi asubuhi niwe bwana mkubwa wa watu na jioni niwe mpuzi wao."

Daktari mmoja mashuhuri wa Kijerumani alisema: "Fungeni nusu ya mabaa na mimi ninawadhaminia kuwa hamtahitajia nusu ya zahanati na mahospitali na majela."

Ama kamari inaleta uadui na chuki na inazuia kutajwa Mwenyezi Mungu; kama ilivyoonyesha Aya tukufu, inaharibu tabia kwa kuzoeya uvivu na kutafuta riziki kwa ndoto tu! Pia inavunja majumba na inamtia mtu kwenye umasikini ndani ya saa moja tu. Inatosha kuwa haramu kamari, kule kuchukua mali bure bure tu.

Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Vilivyowazidia.

Yaani: Toeni vilivyozidi haja zenu na za familia yenu.

Amri ya kutoa hapa ni ya suna sio ya wajibu, isipokuwa inakuwa wajibu

kutoa kama zikithibiti sharti za khumsi na zaka. Tutaelezea kwa ufafanuzi,

Inshaallah.

Aya hii ni kama Aya isemayo:

162 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-154.jpg

"Wala usifanye mkono wako ni wenye kufungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo utakuwa ni mwenye kulaumiwa mwenye kufil-isika." (17:29)

Imeelezwa katika Hadith kwamba mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na kibonge cha dhahabu kama yai, akamwambia Mtume: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu chukua hii ni sadaka Wallah sina chochote zaidi ya hiyo." Mtume akaachana naye; kisha akamfuata tena na kuru-dia kumwambia, kisha Mtume akakichukua na kumrudishia mwenyewe akisema: "Mtu ananijia na mali yake naye hana kitu kingine chochote; kisha aombe watu! Hakika sadaka inatokana na kujitosha; chukua mwenyewe hatuna haja nayo."

Iko Hadith pia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiiwekea familia yake matumizi ya mwaka mzima.

Namna hii anawabainishia Mwenyezi Mungu Aya mpate kufikiri katika dunia na akhera

Yaani Mwenyezi Mungu anawabainishia hukumu yake katika pombe na kamari, na hukumu yake katika vile ambavyo tunatakikana kuvitoa sadaka katika mali zetu kwa misingi ya maslahi yetu. Yeye haamrishi isipokuwa lile ambalo lina maslahi ya kidunia na askhera, na wala hakatazi isipokuwa lile lenye uharibifu.

Yatupasa kuuzingatia na kuuchunga uhakika huu tusimwasi Mwenyezi Mungu katika jambo lolote miongoni mwa amri na makatazo yake. Kwa hivyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mpate kufikiri katika dunia na akhera" ni kwamba tufanye amali kwa ajili ya zote mbili (dunia na akhera) bila ya kuacha moja.

Na wanakuuliza kuhusu mayatima.

163 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Wakati wa ujahilia (kabla ya Uislamu) watu walizowea sana kunufaika na mali za mayatima; pengine mtu aliweza kumwoa yatima au kumwoza mtoto wake kwa tamaa ya mali yake tu. Ulipokuja Uislamu, Mwenyezi Mungu alimterem-shia Mtume wake Aya hizi:

Kaashif2-155.jpg

"Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhulma, hakika wanakula moto matumboni mwao..." (4:10)

Kaashif2-156.jpg

"Wala msikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya wema kabisa..."(6:152)

Basi ziliposhuka Aya hizo waliacha kuchanganyika na kuwasimamia mayatima. Hapo maslahi yao yakaharibika na maisha yao yakawa mabaya. Ndipo baadhi ya Waislamu wakauliza kuhusu hali hiyo. Likaja jawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

Sema: Kuwatengenezea, ndio heri.

Maana yake msijizuilie na kuchanganyika na mayatima na kuzikurubia mali zao, kama mnataka kuwatengenezea uzuri katika malezi yao, adabu zao na kusimamia mali zao. Bali hilo lina malipo na thawabu. Lenye kuharamishwa ni kuzifuja na kuzila mali zao.

Na kama mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu.

Kundi la wafasiri limesema: "Hii ni idhini kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa anayesimamia yatima kumshirikisha pamoja na familia yake katika kula na kunywa ikiwa hilo ni sahali kwa msimamizi na achukue kutoka katika

164

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

mali ya yatima kiasi kile cha malezi

Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadi na mtengezaji.

Fisadi ni yule anayesimamia yatima ili afuje mali zake: Na mtengezaji ni yule anayesimamia mali ya yatima kwa maslahi ya yatima kwa dhati. Kwa hivyo kauli yake hiyo Mwenyezi Mungu ni kemeo kwa mwenye kutaka kufuja na kufanya ufisadi.

Na kama Mwenyezi Mungu angelitaka angeliwatia katika dhiki.

Makusudio hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu amehalalisha kuchanganyika yatima na familia ya msimamizi na kuchukua katika mali ya yatima thamani ya kile alichompatia posho, ili yasipatikane mashaka na uzito. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anawatakia watu wepesi wala hawatakii uzito.

Hapa inaonyesha kuwa si lazima kuwe na usawa wa kutopungua hata kidogo kati ya kile alichokula yatima pamoja na familia ya msimamizi na kile atakachochukua badali kutoka katika mali ya yatima. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) husamehe tofauti ndogo isiyoepukika, bali msimamizi anaweza hata kula katika mali kwa wema akiwa fukara. Hayo ni kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-157.jpg

"...Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe, na atakayekuwa mhitaji basi ale kwa kadri ya ada. (4:6)

165 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

221. Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina hata akiwa-pendeza. Wala msi-waoze wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina hata akiwapen-deza. Hao wanaita kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaita kwenye Pepo na maghufira, kwa idhini Yake. Naye hubainisha Aya Zake kwa watu ili wapate kukum-buka.

MSIWAOE WANAOMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGU Aya 221

MAANA

Aya hizi ni miongoni mwa Aya za hukumu, na zinaingia katika mlango wa ndoa.

Kabla ya kuingilia madhumuni ya Aya, kwanza tutajaribu kufasiri neno.

Nikah, Mushrikina, Amah,

Neno (Nikaha) lina maana mbili: Kufunga ndoa na kumwingilia mwanamke. Neno Mushrikina (washirikina) imesemekana kuwa ni kila

Kaashif2-158.jpg

166

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

asiyeamini utume wa Muhammad (s.a.w.w.). Kwa kauli hii watakuwa wanaingia watu wa Kitabu ambao ni Mayahudi, na Wakristo. Na inase-mekana kuwa Qur'an haikusudii watu wa Kitabu, japo wanasema kuwa Issa ni Mwana wa Mungu na utatu wa Mungu. waliosema haya wametoa dalili kwa Aya hizi:

Kaashif2-159.jpg

"Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu wala washiriki-na... "(2:105)

Kaashif2-160.jpg

"Hawakuwa, wale ambao wamekufuru katika watu wa Kitabu na washiririkina..." (98:1)

Katika Aya hizo kuna viunganishi kati ya watu wa kitabu na washirikina, na kiunganishi kinafahamisha tofauti. Kwa sababu kitu hakiwezi kuungan-ishwa na kitu hicho hicho.

Neno Amah (mjakazi) na Abd linatumiwa kwa mtumwa na hata aliye-huru. Unaweza kumwambia aliyehuru: "Ewe mjakazi wa Mwenyezi Mungu," vile vile mtumwa kwa sababu binadamu wote ni watumwa wa Mwenyezi Mungu.

Maana ya Aya ni kuwa enyi Waislamu msioane na washirikina, bali oaneni na wanaotokana nanyi hata kama sio bora kama washirikina kwa umbo na tabia au kwa j aha na mali.

Hao wanaiita kwenye moto.

Yaani hao washiikina. hikima ya kukataza kuoana ni hiyo ya mwito wa motoni, na kwamba muungano wa kuiondoa unapelekea uharibifu wa itika-

167

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

di na dini. Kwa ufupi unapelekea ufasiki na kupuuzwa hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Tunashuhudia hivi leo vijana wetu wengi wako katika hali mbaya kuliko makafiri na washirikina, kutokana na kudharau kwao, kuipuuza dini na kujivua kabisa katika athari za dini. Wanawalea watoto wao malezi yasiyokuwa ya dini wala ya tabia njema. Lau sikuwa walishuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake, basi tungeli-wafanyia muamala wa walahidi na washirikina.

Lakini kwa sababu ya tamko hili tu (la shahada), ndilo limehifadhi damu, mali na kusihi kuoana na kurithiana nao hata kama haya yanatokana na njia za taqlid na kurithi.* n

Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye pepo na maghufira.

Hapa kuna miito miwili:

• Mwito wa kwanza

Ni wa wanaoshirikisha - kufanya yale yanayoingiza motoni na kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

• Mwito wa pili

Ni wa Mwenyezi Mungu - kufanya yanayoleta maghufira na kuingia peponi. Miongoni mwa hayo ni kuoa mwenye kuamini na wala sio mwenye kushirikisha. Hapana mwenye shaka kwamba wanaoamini ndio wanaoitika mwito wa Mwenyezi Mungu na wanapata maghufira yake na hatimae kuingia pepo Yake kwa idhini Yake; yaani kwa uongofu na tawfiki yake.

KUOA MWENYE KITABU (AHLUL-KITAB)

Wameafikiana Waislamu kwamba haijuzu kwa Mwislamu kuoa au kuolewa na asiyekuwa na kitabu; kama vile kuoa wale wanaoabudu masanamu, jua na moto, n.k. kwa ufasaha zaidi yule asiyeamini.

* " Ndoa na mirathi zinakuwa kwa dhahiri ya Uislamu, sio kwa Uislamu halisi. Hayo tumeyafanyia utafiti katika kitabu Usulul-ithbat sehemu ya madai na kuhalifu sharia.

168

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Vile vile haijuzu kumuoa au kuolewa na Majusi, hata kama imesemwa Majusi ni shabihi ya wenye kitabu.

Wameafikiana madhehebu manne ya Ahli Sunna juu ya kusihi kumuoa mwenye kitabu, na wamehitalifiana Mafaqihi wa Kishia. Wengi wao wamesema kuwa haijuzu kwa Mwislamu kumuoa Yahudi au Mkristo. Na wengine wamesema inajuzu. Miongoni mwa Ulamaa wakubwa waliose-ma hivyo ni Sheikh Muhammad Hassan katika Jawahir, shahidi wa Pili katika Masalik na Sayyid Abul Hassan katika Wasilah, wamesema inajuzu. Na sisi tuko pamoja na rai hii kwa dalili hizi:

1. Dalili zinazohalalisha ndoa zimemtoa Mwislamu mwanamume kumwoa Mshirikina, na Mwislamu mwanamke kuolewa na mshirikina na mwenye kitabu. Kwa hivyo inafahamisha kuwa wasiokuwa hao ina-juzukuoa.

2 Kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-161.jpg

"Leo mmehalalishiwa kula vilivyo vizuri na chakula cha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na wanawake wasafi waumini na wanawake wasafi katika wale waliopewa kitabu kabla yenu..." (5:5)

Kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa (zenu)," makusudio ya makafiri hapo ni washirikina sio wenye Kitabu. Kwa sababu Aya iliwashukia wanawake waliosilimu na kuhama na Mtume wakiwaacha waume zao washirikina; na mfumo mzima wa Aya unafahamisha hivyo. Aya yenyewe ni hii:

169

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-162.jpg

"Enyi mlioamini! Watakapowajia wanawake walioamini wanaohama, basi wafanyieni mtihani; Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi imani yao. Mkiwajua ni waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Hawa si halali kwa hao (wanaume makafiri) wala wao (wanaume makafiri) si halali kwao. Na warudishieni (waume zao) (mahari) waliyotoa. Wala kwenu si vibaya kuwaoa ikiwa mtawapa mahari yao (hao wanawake) kwenu. Wala msiwaweke katika kifungo cha makafiri..."(60:10)

Pia ziko Hadith sahihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) katika kusihi kumuoa mwanamke katika wenye kitabu, na haya tumeyafafanua zaidi katika juzuu ya tano ya kitabu. Fiqhul Imam Jafar Sadiq. Mlango yaliy-oharamu, kifungu cha kutofautiana dini

170

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

222. Wanakuuliza kuhusu hedhi; waambie ni udhia. Basi jiten-geni na wanawake wakati wa hedhi wala msiwakaribie mpaka watoharike. Wakisha toharika basi waendeni pale alipowaam-risha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao-tubia na huwapenda wa-naojitoharisha.

223. Wake zenu ni mashamba yenu.         Basi yaendeeni

mashamba yenu mpendavyo, na tangulizieni nafsi zenu; na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba mtakutana Naye, na wape habari njema wenye kuamini.

HEDHI

Aya 222 - 223

MAANA

Baada ya kumuuliza Mtume mtukufu (s.a.w.w.) kuhusu miezi mitakatifu, ulevi, kamari watakachotoa na mayatima; kisha walimuuliza kuhusu hedhi. Amesema Razi: "Imepokewa habari kuwa Mayahudi na Majusi walikuwa wakikaa mbali sana na wanawake wakati wa hedhi; Wakristo walikuwa wakiwaingilia bila ya kujali hedhi; na watu wa zama za Jahiliya (kabla ya

Kaashif2-163.jpg

171

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Uislamu) walikuwa hawali, hawanywi, hawakai kitanda kimoja wala hawakai nyumba moja na mwanamke mwenye hedhi; kama walivyokuwa wakifanya Majusi na Mayahudi.

Wanakuuliza kuhusu hedhi; waambie ni udhia. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.

Swali linahusu kuchanganyika na wanawake wakati wa hedhi, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake mtukufu kuwajibu wauliza-ji kwamba wajitenge na wanawake siku za hedhi; yaani wasiwaingilie. Imekuja Hadith inayosema; "Fanyeni kila kitu isipokuwa kuingilia tu."

Makusudio ya neno 'Adha' (udhia) ni madhara kwa kuwa ni uchafu na najisi.

Wala msiwakurubie mpaka watoharike.

Wamehitalifiana juu ya makusudio ya kutoharika kuwa je, ni kukatika damu tu bila ya kuoga au ni pamoja na kuoga? Yaani inajuzu kuingili-wa kabla ya kuoga au la?

Wamesema Shia inajuzu kumwingilia hata kabla ya kuoga kwa vile ndio ufahamu wa tamko Tuhr watoharike. Ama kujitoharisha hiyo ni kazi ya wanawake ambayo inakuwa baada ya tohara (kwisha damu).

Amesema Malik na Shafii: Haijuzu ila baada ya kuoga. Na wanasema Hanafi: Ikiendelea damu kwa muda wa siku kumi, inajuzu kumkurubia kabla ya kuoga, lakini ikakatika damu kabla ya siku kumi haijuzu mpaka aoge. Mwenye tafsiri ya Al Manar ameelezea juu ya ufafanuzi huu kwa kusema: "Huu ni ufafanuzi wa kushangaza."

Wakishatoharika, basi waendeeni pale alipowaamrisha. Mwenyezi Mungu.

Neno pale ni uhakika wa mahali, kwa maana ya tupu ya mbele, kama inavyofahamika. Masuala ya hedhi na hukumu zake tumeyazungumzia kwa ufafanuzi zaidi katika kitabu Fiqhul Imam Jaffar Sadiq na kitabu Al Fiqhu ala Madhahibil Khamsa

Wake zenu ni mashamba yenu. Basi yaendeeni mashamba yenu

172 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

mpendavyo.

Neno "Anna " Kulingana na sarufi (nahw ya Kiarabu) lina maana ya vyovy-ote, wakati wowote au popote. Zimekuja kauli nyingi kuhusu maana ya neno hilo Anna katika Aya hii: Kuna mwenye kusema: Ni kwa maana ya wakati wowote; yaani muwaendee (muwaingilie) wakati wowote usiku au mchana. Wengine wakasema ni kwa maana ya popote yaani mna hiyari ya kuwaingilia popote tupu ya mbele au nyuma. Vile vile kuna mwenye kusema ni kwa maana ya vyovyote; yaani hali yoyote kukaa, kulala, n.k.

Limesema kundi la wafasiri, miongoni mwao akiwa ni mwenye Tafsiri ya Al Manar ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni na mwenye Tafsiri ya Bayanu Ssada ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wa Kishia, kwamba Neno shamba linafungamana na mazao na ni tupu ya mbele tu, ndiyo ambayo inaweza kuoteshwa mazao (Mtoto ). Kuongezea kuwa kuendea tupu ya nyuma ni udhia.

Sisi tunaiunga mkono rai hii kwa sababu mbili: Kwanza, mazao hayap-atikani isipokuwa kwa kupitia tupu ya mbele tu, kama walivyotaja wafasiri hao. Pili, kauli yake Mwenyezi Mungu "Waendeni pale alipowaamrisha Mwenyezi Mungu" inaonyesha makusudio yake ni mbele baada ya kufasiri hayth kwa maana ya mahali.

Kuna baadhi ya Mafaqihi wa Kishia wanaojuzisha kumwendea mke nyuma lakini kwa makuruhu makubwa sana.

Wengine wamedai ati kuwa hayo yanahusika na Shia tu! Na kwamba hawaafikiani na yeyote katika hilo; na inajulikana kuwa Razi (mwanachuoni wa kisunni) amenakili katika kuifasiri Aya hii kwamba, Ibn Umar na Malik walikuwa wakisema:

"Makusudio ya Aya ni kujuzisha kuwaendea wanawake nyuma." Na Al-Hafidh Abu Bakr Al-Andalusi wa madhehebu ya Kimalik (Sunni) - aliyek-ufa mwaka 542 Hijriya - katika juzuu ya kwanza ya kitabu Ahkamul Qur'an ukurasa 73 chapa ya mwaka 1331 A.H.; alisema hivi ninamnukuu: "Wamehitalifiana wanavyuoni katika kujuzu kumwendea mke nyuma, wengi wamejuzisha."

Ameyaeleza hayo Ibn Shaban katika Jimau nnis-wan wa Akhkamul Qur'an.

173 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Sunni Na akategemeza, riwaya nyingi kujuzu kwake, kwenye kundi tukufu la masahaba, na Tabiina na kwa Malik. Bukhari ametaja kutoka kwa Ibn Aun, kutoka kwa Nafi kwamba Ibn Umar alikuwa akisoma Sura ya Baqara mpaka alipoishia 'Anna shiitum' alisema: "Je unajua imeteremka kwenye nini?" Nikasema: "La." Akasema: "Imeshuka katika kadha na kadha"; yaani tupu za nyuma za wanawake.

224. Wala msimfanye Mwenyezi Mungu ni pondokeo la viapo vyenu, (ili) mfanye mema         na         mumche (Mwenyezi Mungu) na muwe wema kati ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

225.    Mwenyezi Mungu hata-washika kwa sababu ya kuapa kwenu kwa upuzi upuzi, lakini atawashika katika yaliyokusudiwa na nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghu-fira Mpole .

226.  Kwa wale ambao wanaapa kujitenga na wake zao ni kungojea miezi minne. Na kama wakirejea basi Mwenyezi         Mungu ni Mwenye              maghufira Mwenye kurehemu.

227.  Na wakiazimia talaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Kaashif2-164.jpg

174

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

YAMINI

Aya 224 - 227

Wala msimfanye Mwenyezi Mungu ni pondokeo la viapo vyenu

Mwenyezi Mungu amekataza kutangulizwa katika kila jambo kwa kuapa sana. Kwa sababu mwenye kukitaja kitu sana amekijaalia ni pondokeo lake. Mwenyezi Mungu ameshutumu kuapa sana kwa kauli yake.

Kaashif2-165.jpg

"Wala usimtii kila mwenye kuapa sana aliye dhalili." (68:10)

Mwenye kuapa sana haiba yake hupungua, huzidi dhambi zake na atatuhu-miwa uongo.

(Ili) mfanye mema na mumche (Mwenyezi Mungu) na muwe wema kati ya watu.

Hili ndio sababu ya kukatazwa kuapa; maana yake Mwenyezi Mungu anawakataza kuapa bila ya dharura, ili muwe wema wanaomcha Mungu, wenye kufanya wema duniani na wala sio wenye kufanya ufisadi.

Mwenyezi Mungu hatawashika kwa sababu ya kuapa kwenu kwa upuzi upuzi.

Baada ya kukataza Mwenyezi Mungu kuapa bila ya dharura amebainisha kwamba mengi yanayowapitia watu katika ulimi mfano 'Wallahi vile' au 'sio hivyo Wallahi', n.k. hayo siyo viapo vya uhakika isipokuwa ni mchezo tu unaokuja kwenye ulimi bila ya kukusudia, wala hayana athari yoyote. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu hakuwajibisha kafara katika dunia wala hakuna adhabu katika akhera.

175 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

Lakini atawashika katika yaliyokusudiwa na nyoyo zenu.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu Ambaye umetukuka utukufu wake, haan-galii sura na kauli, bali huangalia nia na vitendo, kama anavyosema:

Kaashif2-166.jpg

"Mwenyezi Mungu hatawashika kwa viapo vyenu vya upuzi, lakini atawashika kwa viapo mlivyoapa kwa nia mliyoifunga (barabara). Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mna-chowalisha watu wa majumbani mwenu au kuwavisha, au kumwacha huru mtumwa. Asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu. Hiyo ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa...." (5:89)

Mtu aliyebaleghe, mwenye akili timamu mwenye kukusudia na aliye na hiyari, akiapa na akakhalifu, basi itampasa kutoa kafara ya kumwacha huru mtumwa au kuwalisha au kuwavisha maskini kumi. Akishindwa hivyo ata-funga siku tatu. Tumezungumzia zaidi kuhusu kiapo, sharti zake na hukumu zake katika juzuu ya tano ya Fiqhul-Imam Jaffar Sadiq.

Kwa wale ambao wanaapa kujitenga na wake zao ni kungojea miezi minne. Na kama wakirejea basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. Na wakiamua talaka basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Kuapa kujitenga katika sharia ni kuapa mtu kuwa hatamwingilia mkewe. Mafaqihi wa Kishia wameshartiza kuwa mke awe ameingiliwa; kama si

176

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

hivyo hakitakuwa kiapo; na kuwe ni kuapa mume kuacha kumwingilia mkewe muda wa maisha yake au muda unaozidi miezi minne, kwa sababu mke anayo haki ya kuingiliwa angalau mara moja kila miezi minne kwa uchache.

Wamesema: Kama atamwingilia kabla ya miezi minne atatoa kafara na kizuizi kitaondoka; kama vile hakikuwa kitu, na ikipita zaidi ya miezi minne wala asimwingilie; kama mke akisubiri na akaridhia, hiyo ni juu yake wala haifai kwa yeyote kumpinga. Na kama akishi-ndwa atamshta-ki mume kwa hakimu wa sheria. Baada ya kupita miezi minne atalaz-imishwa kumrudia au kumwacha, akikataa atafungwa mpaka achague moja wapo ya mambo mawili; wala si haki kwa hakimu kumwachisha kwa nguvu. Kama mume ataamua kurudi, basi atatoa kafara iliyotajwa.

228. Na wanawake waliopewa talaka wangoje tohara tatu wala si halali kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa             wanamwamini

Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki zaidi ya kuwaru-dia katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu. Nao (wanawake) wanayo haki sawa na ile iliyo juu yao kwa sharia. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Mwenyezi Mungu ana nguvu, Mwenye hekima.

Kaashif2-167.jpg

177

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

WALIOTALIKIWA

Aya 228: MAANA Na wanawake waliopewa talaka wangoje tohara tatu.

Tamko la waliopewa talaka kwa dhahiri ni lenye kuenea kwa yeyote yule aliyepewa talaka, awe anatoka hedhi au amekoma, muungwana au kijakazi mwenye mimba au asiyekuwa nayo, mkubwa au mdogo asiyetimiza miaka tisa. Lakini dhahiri hiyo siyo makusudio yake. Kwa sababu baadhi ya wanaotalikiwa hawana eda, kwa tamko la Qur'an;

Kaashif2-168.jpg

"Enyi mlioamini Mtakapowaoa wanawake wenye kuamini kisha mkawa-pa talaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayaoihis-abu... "(33:49)

Pia aliyekoma. Mafaqihi wa Kishia wanasema kwamba hana eda hata kama ameingiliwa na mume; vile vile mtoto mdogo chini ya miaka tisa. Na kuna wanawake wanaokaa eda kwa tohara mbili kama mjakazi. Wengine wanakaa miezi mitatu sio tohara tatu; huyo ni yule ambaye yuko katika rika la kutoka hedhi, lakini hatoki; kama ambavyo mwenye mimba muda wake

Kaashif2-169.jpg

wa kukaa eda unaisha wakati atakapozaa. Mwenyezi Mungu anasema; "...Na wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa..." (65:4)

178

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Kwa hivyo basi makusudio ya waliopewa talaka katika Aya, ni yule aliyeingiliwa akiwa na umri wa zaidi ya miaka tisa, asiwe na mimba na awe mwenye kutoka hedhi.

Wamefasiri Shia, Malik na Shafii neno Qurui kwa maana ya tohara na makusudio ya tohara ni siku za kutoharika baina ya hedhi mbili. Kama akiachwa wakati wa mwisho mwisho wa tohara yake, itahisabiwa pia katika eda na atakamilisha tohara mbili. Ama Hanafi na Hambal wamefasiri neno Qurui kwa maana ya hedhi tatu.

Wala haijuzu kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao.

Ili kufahamu hakika ya jumla hii itabidi kuanza kueleza haya yafuatayo: Mafaqihi wa Kisunni wameigawa talaka kwenye mafungu mawili: ya sunna na bid'a (uzushi). Hebu tuwaachie wenyewe tafsiri ya 'Sunna' na Bid'a (talaka ya kawaida na uzushi)

Katika kitabu Al-Mughni cha Ibn Quddam Juzuu 7 Uk. 98 chapa ya tatu anasema : "Maana ya talaka ya sunna ni talaka ambayo inaafiki amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake, nayo ni talaka katika hali ya tohara asiyomwingilia." Na katika kitabu hicho hicho Uk. 99 amesema: "Hakika talaka ya Bid'a ni talaka katika hali ya hedhi au katika hali ya tohara aliyomwingilia. "Amesema Razi katika tafsiri ya Aya ya 1 katika Sura ya 86; "Utohara katika talaka ni lazima, vyinginevyo haitakuwa ya sunna."

Kwa hali hiyo basi, kupewa talaka mke katika hali ya hedhi au katika hali ya utohara ambapo mke ameingiliwa, siyo talaka ya kisheria, bali ni Bid'a (uzushi) na kila uzushi ni upotevu na kila upotevu ni motoni.

Ama kumtaliki mke katika tohara asiyoingiliwa na mumewe, inakuwa ndiyo talaka iliyofuata sharia ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapo ndio inafafanulika siri ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "wala haijuzu kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao." Kwa

179

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

sababu maarifa ya kutokea talaka kwa njia ya kawaida au uzushi ndiyo yatakayofahamisha hali ya mwenye kuachwa, na kwamba je ana hedhi au yuko tohara.

Kimsingi njia ya kujua sifa mbili hizi (tohara na hedhi) inamtegemea mwanamke mwenyewe. Kwa hivyo itabidi aaminiwe maadamu haujajuli-wa uwongo wake. Imam Jaffar Sadiq amesema; Mwenyezi Mungu amewachia wanawake mambo matatu: Tohara, hedhi na mimba." Katika riwaya ya pili imeongezewa eda.

Shia wanaafikiana na Sunni kwamba talaka ikiwa katika hedhi au katika tohara aliyoingiliwa, inakuwa ya uzushi na ikiwa ni katika tohara ambayo hakuingiliwa inakuwa ni ya sharia ya Mtume (s.a.w.w.). Lakini Shia wame-sema Talaka ya uzushi sio talaka kabisa; yaani si sahihi. Na talaka sahihi inayomtenganisha mume na mke, ni talaka ya kawaida; yaani inayotokea katika tohara asiyoingilwa. Sunni wanasema hapana; talaka ya uzushi ni sahihi na inahusika na athari zote za talaka, isipokuwa tu yule mwenye kuacha atapata dhambi.

Hiyo ni kusema kuwa Sunni hawatofautishi kati ya talaka ya kawaida na ya uzushi katika kusihi kwake, isipokuwa wanatofautisha katika kupa-ta madhambi na uasi tu. Ama Shia wametofautisha kati ya hizo mbili, kwa upande wa usahihi, na si upande wa dhambi.

Ikiwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Hii ni kuogopesha na kuweka utisho kwa wenye kuficha yaliyo tumboni na wala sio sharti la kuwajibisha kusadiki. Kwa sababu maana yake ni kwamba imani inazuwiya uongo; kama vile kumwambia mtu: "Ikiwa unamuogopa Mwenyezi Mungu usiseme uongo."

Tumetangulia kueleza kuwa mwenye kutalikiwa ndiye atakayeamini-wa katika tohara, hedhi na mimba. Maana yake ni kuwa itakayotegeme-wa ni kauli yake katika kubaki eda na kwisha kwake. Ilivyo ni kwamba haki ya mume katika kurejea, itategemea kutokwisha kwa eda; kama

180

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

ambavyo muungano (wa nasaba mtoto) unaambatana na utohara na hedhi. Vile vile kusihi talaka na kutosihi kwa upande wa mafaqihi wa kishia. Akiwa na hedhi na akasema kuwa ni tohara, basi talaka haitakuwa, na atabaki ni mke wa mtu; kama akisema eda yake imekwisha kwa tohara na kumbe bado, haki ya mume ya kurejea itafutika. Lakini akiolewa katika hali hiyo atakuwa mzinifu. Kwa sababu hii na nyinginezo, ndio Mwenyezi Mungu akawakataza wanawake kuficha vilivyo katika matumbo yao na akawakemea kwa hilo.

Na waume zao wana haki ya kuwarudia katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu.

Kauli yake Mwenyezi Mungu "katika muda huo" ni ule muda wa kungo-jea (muda wa eda). Maana yanayopatikana ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya kubainisha wajibu wa eda, ametaja haki ya mwenye kutaliki kumrejea mtalaka wake katika muda wa eda ikiwa ni talaka rejea.

Hiyo ni haki yake awe mke hakuridhia au ameridhia; wala kurejea mke hakuhitaji kufunga ndoa tena na mahari, kama vile ambavyo hakuhitajii ushahidi kwa mafaqihi wa Kishia. Utakuja ubainifu wake zaidi kwenye Sura ya Talaka (65).

Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu "kama wakitaka kufanya suluhu" ni suluhu kati ya mume na mke bila ya kukusudia madhara katika kurejea.

Unaweza kuuliza: Kama mume akimrejea mtalaka wake ndani ya eda kwa kukusudia madhara sio suluhu, je kurejea kutakuwa sahihi au la? Jibu: Kutaswihi kurejea, lakini mume atapata dhambi, kwa sababu kukusudia suluhu ni hukumu ya taklifa ambayo ni kuhalalisha kurejea na wala sio sharti ya maudhui yenyewe ya kurejea na kuswihi kwake.

Nao (wanawake) wanayo haki sawa na ile iliyo juu yao kwa sharia.

181

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Makusudio ya kufanana haki hapa sio ya kufanana kijinsia, kwamba yanayostahiki kwa mume kama vile mahari na posho, basi na mke pia naye atoe, la; isipokuwa makusudio hapa ni kuwa sawa wajibu na yanayostahiki. Mafaqihi wanasema haki ya mume kutoka kwa mkewe ni kutiiwa kitandani, na haki ya mke kutoka kwa mume ni kumlisha na kumvisha. Mwenye tafsiri Al Manar anasema haki ya mume kwa mke na haki ya mke kwa mume ni ile kawaida ya mambo ya watu, isipokuwa yale yaliyoharimishwa katika sharia. Linaloonekana kikawaida kuwa ni haki kwa mke na mume, basi litakuwa ni sawa mbele za Mwenyezi Mungu.

Yanayodhihirikia kutokana na mfumo wa Aya ni kwamba haki iliyo kwa mke ni eda, ukweli katika kuitolea habari eda na kuacha kupinga kurejea kulikokamilisha masharti. Na iliyo juu ya mume ni kukusudia suluhu katika kurejea na usuhuba mzuri na wala sio madhara. Ama haki nyingine za mume na mke ziko mbali na Aya hii.

Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.

Wamehitalifiana wanavyuoni na wafasiri katika makusudio ya daraja hii inayomtofautisha mwanamume na mwanamke. Ikasemwa kuwa ni akili na dini; ikasemwa ni mirathi na pia ikasemwa kuwa ni ubwana; yaani inam-pasa mke kumtii mume na kumsikiliza.

La kushangaza ni kwamba wengine wamefasiri daraja ya juu kwa maana ya ndevu; kama ilivyoelezwa katika kitabu Ahkamul-Qur'an cha Abu bakr Al-Andalusi.

Sio mbali na maana kuwa makusudio ya daraja ni kuijaalia talaka na kurejea mikononi mwa mume na wala sio mwa mke.

MWANAMUME NA MWANAMKE KATIKA SHARIA YA KIISLA-

MU

Uislamu umezitangulia sharia na kanuni zote katika kumkomboa mwanamke na kuzithibitisha haki zake, baada ya kuwa mwanamume alim-tumia mwanamke kama bidhaa tu, akamfanya kama mnyama, ambapo mpaka hivi karibuni Ulaya na Marekani walikuwa wakifanya hivyo.

182 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Uislamu unapomtofautisha mwanamke na mwanamume unamtofautisha kwa tofauti za kimaumbile au maslahi ya jamii. Ni jambo lisiloingia akili-ni wala uadilifu kufanya usawa katika kila kitu kati ya yule mwenye kujishughulisha zaidi na magauni, mitindo ya mavazi, kuchana nywele, n.k.; na yule anayehisi majukumu ya mwenzake (mkewe) na watoto na kustahamili mashaka kwa ajili yake (mke) na kwa ajili yao wote.

Mafaqihi wa Kiislamu wamezitaja tofauti kati ya mwanamume na mwanamke katika hukumu za kisharia kama ifuatavyo:

1. Fidia ya kuuliwa mwanamke ni nusu ya mwanamume.

2.    Kutoa talaka na kurejea kuko mikononi mwa mume sio mke.

3.    Haijuzu kwa mke kusafiri, na kutoka nyumbani kwake isipokuwa kwa kukubali mume, lakini mume anaweza kufanya hivyo.

4.    Si wajibu kwa mwanamke kuswali Ijumaa, hata yakitimia masharti.

5.    Haijuzu mwanamke kutawalia jambo wala kuwa Kadhi, isipokuwa kwa Abu Hanifa anasema inafaa katika haki za watu lakini sio za Mungu.

6.   Hawezi kuwa Imam wa swala ya wanaume, lakini mwanamume anaweza kuwa Imam wa wanawake.

7.   Ushahidi wake haukubaliwi katika mambo yasiyo husiana na mali; hata akiwa pamoja na waume, isipokuwa katika maswala ya uzazi, unakubaliwa akiwa pamoja na waume kwa kuchukulia kuwa ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na wa mwanamume mmoja.

8.    Katika mirathi mtoto wa kike anapata nusu ya fungu la mtoto wa kiume.

9.   Ni lazima ajifunike mwili wake wote - hata nywele - mbele za waume wasio maharimu, lakini kwa mwanamume mbele za wanawake wajibu wake ni kustiri tupu mbili tu.

10. Hapigani jihadi wala hatoi kodi wala hauliwi vitani iwapo hajapigana.

11. Mama hashirikiani na baba katika usimamizi (uwalii) wa mtoto mdogo au katika matumizi ya mali yake (mtoto).

12. Haifai kushindana mashindano ya farasi na kulenga shabaha.

13. Mafaqihi wametoa fatwa kuwa fidia ya aliyeuawa kimakosa inachukuliwa na ndugu zake wa karibu kwa upande wa baba tu; kama vile kaka, ami na watoto wao lakini sio wakike.

14. Mwanamke akimuua mwanamume, atauliwa bila ya kutoa fidia,

183 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

lakini kama mwanamume akimuua mwanamke, basi hawezi kuuliwa mpaka walii wa mwanamke atoe nusu ya fidia kwa warithi wa muua-ji.

229.  Talaka ni mara mbili; kisha ni kushika kwa wema au kuacha kwa ihsani. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa, isipokuwa wakiogopa (wote wawili) ya kwamba hawataweza kusi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkio-gopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwa hapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiipetuke. Na watakao-ipetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhalimu.

230.  Na kama amempa talaka ( ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine. Na akimwacha, basi hapo si vibaya kwao kurejeana waki-ona kuwa watasi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wajuao.

Kaashif2-170.jpg

184

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

TALAKA NI MARA MBILI

Aya 229 - 230

MAANA

Talaka ni mar a mbili.

Waarabu katika zama za Ujahiliya (kabla ya Uislamu) walikuwa na talaka, eda na kurejeana katikati ya eda. Lakini talaka haikuwa na idadi maalum. Mtu aliweza kumwacha mkewe mara mia na kumrudia. Kwa hivyo mwanamke anakuwa ni kitu cha kuchezewa mikononi mwa mwanamume.

Kuna riwaya inayoeleza kuwa mtu mmoja alimwambia mkewe: "Sitakukur-ubia milele, na pamoja na hivyo utabaki kwangu tu, hutaweza kuolewa na mwingine." Mke akauliza: "Itakuwaje hivyo?" Mume aka-jibu: "Nitakuacha mpaka ukikaribia muda wa kwisha eda nikurudie, hala-fu nikuache tena, n.k." Mwanamke akamshtakia Mtume (s.a.w.w.). Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii: "Talaka ni mara mbili" yaani talaka ambayo mnaruhusiwa kurejea ni talaka ya kwanza na ya pili tu! Ama ya tatu si halali kurejea, mpaka mke aolewe na mume mwingine; kama alivyosema Mwenyezi Mungu; "Na kama amempa talaka si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine."

Kisha ni kushika kwa wema au kuacha kwa ihsani

Mume akimwacha mkewe mara ya pili ana hiyari kati ya mambo mawili akiwa katika eda. Jambo la kwanza ni kumrejea kwa kukusudia kupatana na kutangamana. Huku ndiko kumweka kwa wema. Jambo la pili, ni kumwacha mpaka ishe eda yake, amtekelezee haki yake asimtaje kwa ubaya baada ya kutengana wala asimkatishe anayetaka kumwoa baada yake. Huko ndiko kumwacha kwa ihisani.

Unaweza kuuliza, wafasiri wengi wamefasiri kumwacha kwa ihisani ni talaka ya tatu na wakatoa ushahidi wa Hadith ya Mtume (s.a.w.w.). Sasa

185 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

imekuwaje wewe kuipinga kauli yao na kufasiri kuacha, kuwa ni kupuuza kumrejea katika muda wa eda?

Jibu: Neno kumwacha, kwa dhati yake linawezekana kuwa ni talaka ya tatu na linawezekana kuwa ni kumnyamazia mtalaka na kuwacha kumrejea. Lakini kwa kuchunga mfumo ulivyo, maana ya neno inarudia maana ya pili; yaani kuacha kurejea, kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu "Kama amempa talaka basi mwanamke huyo si halali kwake baada ya hapo." Inatokana na kumweka; maana yake yanakuwa ni akimwacha baada ya kumweka na akamrejea katikati ya talaka ya pili itakuwa talaka ni ya tatu wala si halali kwa mwenye kuacha kumwoa mpaka aolewe na mume mwingine. Kwa hivyo haiwezekani kuwa imetokana na kumweka kwa maana ya talaka ya tatu, kwa sababu maana itakuwa alimwacha mara ya nne baada ya kumwacha mara ya tatu. Na ilivyo ni kwamba hakuna talaka ya nne katika Uislamu. Ama Hadith iliyofasiri kumweka kwa maana ya talaka ya tatu si thabiti.

TALAKA TATU

Madhehebu manne ya Kisunni yameafikiana kuwa atakaye mwambia mkewe: Nimekuacha talaka tatu au akisema: Nimekuacha, nimekuacha, nimekuacha, basi itakuwa ni talaka tatu na itakuwa haramu mpaka aolewe na mume mwingine. Shia wamesema itakuwa ni talaka moja tu, na ni halali kumrejea, maadamu yuko katika eda.

Katika tafsiri ya Al Manar imepokewa kutoka kwa Ahmad bin Hambal katika Musnad yake, na Muslim katika Sahih yake kwamba talaka tatu zilikuwa moja katika zama za Mtume (s.a.w.w.), za Abu Bakr na baad-hi ya miaka ya ukhalifa wa Umar, lakini Umar ikamdhihirikia fikra nyingine akasema; "Hakika watu wamefanya haraka katika jambo lililokuwa na upole kwao, lau tungelipitisha."Basi akapitisha (kuwa kuse-ma talaka tatu ni tatu).

Kisha amenakili mwenye tafsiri Al Manar kutoka kwa Al Qayyim kwamba masahaba wote walikuwa wakikubali kwamba talaka tatu hazikutokea

186

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

kwa pamoja tangu mwanzo wa Uislamu mpaka miaka mitatu ya ukhalifa wa Umar. Vile vile walifutu hivyo jamaa katika masahaba, Tabiina (waliokuwapo baada ya maswahaba) na waliokuja baada ya hao Tabiina (Tabii-Tabiina), na kwamba fatwa juu ya hilo inaendelea kila wakati hata baadhi ya wafuasi wa Maimamu wanne walifutu hivyo.

Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa.

Katika mlichowapa hapa ina maana kiwe kingi au kichache; yaani ikiwa mume ndiye asiyemtaka mke na akapendelea kumpa talaka, basi si haki kwake kuchukua vile alivyompa zawadi mke au mahari. Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-171.jpg

"Na kama mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke na hali mmoja wao mmempa rundo mali, basi msichukue chochote katika hiyo. Je, mnachukua kwa dhuluma na kwa dhambi iliyo wazi" (4:20)

Hiyo ni ikiwa mume ndiye asiyemtaka mke. Ama ikiwa mke ndiye asiyemtaka mume, basi hapana kizuwizi cha mke kumpa mume kile kinachom-ridhia ili amwache, ni sawa chenye kutolewa kiwe ni kiasi cha mahari au kichache au zaidi ya mahari. Talaka hii inaitwa Khul'u (kujivua); na mume katika talaka hii hana haki ya kumrejea katika eda maadamu anaendelea kulipwa. Isipokuwa kama huyo mke atabadilisha katikati ya eda.

Kuhusu talaka hii ya khul'u Mwenyezi Mungu anasema: Isipokuwa wakiogopa (wote wawili) ya kwamba hawataweza kusi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwa hapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke. Hii ni kuelezea uwezekano wa kuchukua kitu kutoka kwa mke. Mipaka ya Mwenyezi

187

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Mungu ni haki na wajibu wa kila mmoja kwa mwenzake (mke na mume). Maana yake: Enyi waume! Msichukue kitu kutoka kwa watalaka wenu kwa sababu yoyote ile, isipokuwa sababu moja tu, ambayo ni ikiwa mke ndiye anayemchukia mume, wala hawezi kuishi naye, kiasi ambacho hali itapelekea kumwasi Mwenyezi Mungu katika kutia dosari haki za unyumba, na huenda mume naye akaogopa kumkabili mke kwa uovu. Katika hali hii, itafaa kwa mke kudai talaka kutoka kwa mume na kum-lipa ridhaa; kama vile ambavyo inajuzu kwa mume kuichukua ridhaa hiyo.

Imekuja Hadith kwamba Thabit bin Qays alikuwa amemuoa bint wa Abdulla bin Ubay. Naye alikuwa akimpenda, lakini mke hampendi mume. Na alikuwa amempatia shamba. Mke akaja kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Mimi na Thabit kichwa changu hakipatani na chake." Thabit akasaili: "Na lile shamba?" Mtume akamwambia bint Abdulla: "Unasemaje?" Akasema: "Ndio, tena na ziada nitampa." Mtume akasema: "Hapana, shamba tu," Basi wakafanyiana khul'u.

Linakuja swali katika aya hii: Kwa nini ikaja dhamiri ya wawili katika "Isipokuwa wakiogopa (wote wawili) ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu." Kisha ikaja dhamiri ya wengi kwa kusema: "Na kama mkiogopa". Kwa nini dhamiri zisiafikiane katika jumla mbili?

Jibu: Dhamiri ya wote wawili ni ya mke na mume na dhamiri ya 'mkiogopa' ni ya mahakimu na wasuluhishi; yaani wakiogopa, mahakimu na wasuluhishi kuacha kusimamishwa mipaka ya Mwenyezi Mungu. Makusudio hasa ni kuondoa hofu ya kutoa na kuchukua kwa wote.

Swali la pili: Kwa nini ikaja dhamiri ya wawili katika: Si dhambi juu yao (mume na mke), na tunajua kuwa anayepokea ni mume tu. Jibu: Hapa inaonyesha kuwa si vibaya kutoa na kuchukua; kwa kufahamu kuwa kujuzu kutoa kunalazimisha kujuzu kupokea.

Swali la tatu: Ikiwa mke na mume wameridhiana kufanya khul'u, mke akatoa mali ili aachwe; lakini uhusiano wao ni mzuri, je, itaswihi khul'u

188

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

na itafaa mume achukue fidia?

Madhehebu zote nne zimesema khul'u itafaa na itafungamana na athari zote za khul'u.

Shia Imamia wamesema haiswihi hiyo khul'u wala mtaliki hawezi kumi-liki fidia, lakini talaka itaswihi na itakuwa ni talaka rejea kwa sharti zake. Wametoa dalili ya kuharibika khul'u na kutojuzu kuchukua fidia kwamba Aya imeshartisha kujuzu hilo kwa kuogopa kuingia katika maasi, kama ndoa ikiendelea. Ama Aya inayosema:

Kaashif2-172.jpg

"Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni zawadi, kama waki-watunikia kwa ridhia ya nafsi zao, katika hayo (mahari) basi kuleni kwa raha." (4:4)

Makusudio ya Aya hiyo ni kwamba anachotoa mke hapo ni zawadi tu, sio badali ya talaka. Hivyo Aya iko mbali na khul'u.

Swali la nne: Kama mume akifanya makusudi ubaya ili apate mali kuto-ka kwa mke, na mke naye akatoa mali na ikatolewa talaka kwa misingi hii; je, khul'u itakuwa halali? Na je, ni halali kuchukua mali?

Abu Hanifa anasema: "Khul'u ni sahihi, mali ni lazima itolewe na mume ana dhambi."

Shafi na Malik wamesema: "Khul'u ni batili na mali irudishwe kwa mke, kwa sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

189

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Kaashif2-173.jpg

"... Wala msiwataabishe ili mpate kuwanyang'anya baadhi ya vile mlivy-owapa..." (4:19)

Hayo yamo katika kitabu Al- Mughni, cha Ibn Quddama Juz 7, Uk 55 chapa ya 7.

Shia Imamia wamesema: "Haiswihi khul'u, ni haramu kuchukua mali, lakini itakuwa ni talaka rejea kwa kukamilika sharti zake."

Ama sisi tuko katika fikra ya kuwa talaka hiyo ni upuzi tu, sio khul'u wala talaka rejea. Kwa sababu kinachojengeka kwa uharibifu ndio kimeharibi-ka chote. Hayo tumeyafafanua zaidi katika kitabu Fiqhul Imam Jaffar Sadiq Juz 6 mlango wa khul'u kifungu cha Hukumu za khul'u.

Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine. Na akimwacha (mume wa pili), basi hapo hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watasi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Maana ni kuwa mwenye kumwacha mkewe mara tatu, basi si halali kwake kumwoa tena mpaka aolewe na mume mwingine kwa ndoa sahihi tena amwingilie. Imekuja Hadith inayosema:

"Si halali kwa mume wa kwanza mpaka wa pili amwonje (amwingilie)."

Huyu mume wa pili ndiye anayeitwa muhallil (mhalalishaji); Ni lazima awe ni baleghe, na ndoa iwe ya daima sio ya Mut'a. Zikitimia sharti; kisha mume wa pili akatalikiana naye kwa mauti au talaka na ikaisha eda, basi itafaa kwa mume wa kwanza kufunga ndoa naye tena.

190

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita

5. Sura Al-Maidah

231.  Na                mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema. Wala msiwaweke kwa kudhuriana mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo,amejidhulumu mwenyewe. Wala msiz-ifanyie mzaha Aya za Mwenyezi Mungu. Na kum-bukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na Kitabu alichowateremshia na heki-ma, kwa kuwaonya. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

232.  Na                mtakapowapa wanawake talaka na wakafikia muda wao, msi-wazuie kuolewa na waume zao, ikiwa wamepatana kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule, miongoni mwenu, anaye-mwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni mazuri mno kwenu na safi kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

Kaashif2-174.jpg

191

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

MNAPOWAPA TALAKA WANAWAKE

Aya 231 - 232

MAANA

Na mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema. Msemo huu unaelekezwa kwa waumini wote au kwa watu wote; ni kama vile Mwenyezi Mungu ametaka kusema: Enyi waumini! Atakapompa talaka mmoja wenu mkewe.

Baada ya kubainisha Mwenyezi Mungu kwamba mwenye kupewa talaka ni lazima akae eda, kwamba anaweza kurudiwa na mumewe zikikamili-ka sharti, kwamba ni haramu baada ya talaka ya tatu mpaka aolewe na mume mwingine, na kwamba si halali kuchukua kitu kwa mke kwa ajili ya talaka, isipokuwa ikiwa mke ndiye asiyemtaka mume, baada ya kuyabainisha yote hayo, anatubainishia vile tunavyotakiwa kuchunga haki ya anaekaa eda.

Kuchunga haki kutathibitika kwa kuazimia mwenye kuacha moja kati ya mawili: Kumrejea mtalaka wake wakati inapokaribia kumalizika eda, kwa kukusudia usuluhishi na utangamano mzuri. Na huku ndiko kurejea kwa wema. Au kumwacha bila ya kumtaaradhi kwa ubaya pamoja na kumtekelezea kila analostahiki. Na huku ndiko kumwacha kwa wema.

Kwa hivyo inatubainikia kuwa makusudio ya Aya iliyotangulia siyo makusudio ya Aya hii tuliyonayo. Aya ile iliyotangulia inabainisha kuwa kurejeana ni talaka ya kwanza na ya pili na siyo ya tatu. Na hii inabainisha vile tunavyotakiwa kuwafanyia waliopewa talaka; kama ambavyo makusudio ya kufikilia muda wao ni kukurubia sio kufika hasa.

Wala msiwaweke kwa kudhuriana mkafanya uadui.

Yaani msiwarudie kwa kukusudia kuwaudhi au kuwafanyia ubaya; muware-

192 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

jee tu kwa makusudio ya kutekeleza haki za unyumba na kusaidiana yale yaliyo na maslahi kwa wote.

Unaweza kuuliza kwa nini imesemwa kudhuriana, ambapo makusudio ni kuepusha madhara ya mume kwa mke?

Jibu: Kumdhuru mke kunasababisha kudhurika kwa mume pia, kwa sababu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu yake, shutuma za watu kwake, na mke kulipiza kisasi. Hapo ndio unyumba unageuka kuwa Jahannam kwa mume na mke na huenda moto ukaenea kwa jamaa na ndugu. Ndio maana Mwenyezi Mungu anasema: Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu mwenyewe. Yaani si kumdhulumu mke peke yake.

Wala msizifanyie mzaha Aya za Mwenyezi Mungu. Hiki ni kiaga na kemeo kwa yule mwenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu katika haki za unyumba. Njia ya kuzifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, ambaye limetu-kuka neno lake, ni kwamba kila mwenye kudai kumwami-ni Mwenyezi Mungu na hakufuata dini kwa sharia zake, halafu akapuuza hukumu zake, halali yake na haramu yake, basi atakuwa amefanya mzaha, atake asitake. Sawa na anayem-uahidi mtu kitu hali akiwa na niya ya kutotekeleza. Baadhi ya wahenga wamesema: "Mwenye kutubu dhambi na huku anaendelea nayo ni kama mwenye kumcheza shere Muumba wake."(Mungu apishie mbali!)

Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu.

Miongoni mwa hizo ni kuwa Mwenyezi Mungu ametuumbia wanawake ili tupate utulivu kwao na tusaidiane nao katika yale yenye utengeneo wa famil-ia. Ikiwa tunamwamini Mwenyezi Mungu na tunafuata amri zake kweli, basi ni juu yetu kufanya lile litakaloleta lengo hili na kujie-pusha na kila linalole-ta uovu katika familia na kuchafua usafi wa maisha ya ndoa.

Na mtapowapa talaka wanawake na wakafikia muda wao, msiwazuie kuolewa na waume zao.

193 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

Makusudio ya kufikia muda katika Aya iliyotangulia ni kukaribia kwisha eda na makusudio yake hapa ni kwisha kabisa hiyo eda.

Katika Aya hii kuna mielekezo miwili ya misemo (mnapowapa talaka, na msiwazuie) ambayo wafasiri wamehitilafiana; kwamba, je yote inaelekezwa upande mmoja au pande tofauti?

Kuna wenye kusema kuwa unaelekezwa kwa upande mmoja tu wa waume; na maana yake ni: Enyi waume, mnapowapa talaka wanawake na eda yao ikaisha, basi msiwazuwie kuolewa na waume wengine wanaowaridhia. Kwa sababu mwanamume alikuwa akimhukumu mtalaka wake na kumzuia, kuolewa na mume mwingine baada yake.

Wengine wanasema: Msemo wa kwanza Mtakapowapa talaka, unaelekezwa kwa waume, na wapili msiwazuie, unaelekezwa kwa mawalii; kwa maana ya: Enyi waume, mnapowapa talaka wanawake, basi nyinyi mawalii msiwazuwie watoto wenu kurudiana na waume zao wa kwanza, ikiwa eda imek-wisha. Wanaosema hivi wametoa ushahidi wa Hadith ya Mu'ukil bin Yasir.* u

Inaeleweka kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mtakapowapa talaka wanawake na wakafikia muda wao msiwazuwie" ni jumla ya pamoja iliyo na sharti, na jawabu lake ni msiwazuie.

Ikiwa sharti ya mwenye kumwambia ni mwingine na jawabu liwe kwa mwingine na maana yawe ni: Enyi waume mtakapowapa talaka wanawake basi nyinyi mawalii msiwazuie, hapa kutakuwa na mkorogano ambao hau-paswi kuwapo katika maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Usahihi hasa ni misemo miwili (sharti na jawabu lake) inaelekezwa kumoja tu kwa waumini wote;

* 12 Imepokewa kutoka kwa Mu'ukil bin Yasir kwamba yeye amesema: "Nilikuwa na dada aliyeolewa na binamu yake kisha akampa talaka wala asimrejee mpaka ikaisha eda, wakataka kurudiana nikamzuia; ndipo ikashuka Aya hii."

194

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Sita                                            5. Sura Al-Maidah

sio waume peke yao wala mawalii tu, wala pia sio kwa wote, bali ni kwa waumini. Hali hii inakuja mara nyingi katika maneno yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na maana yanakuwa: Enyi mlioamini mmoja wenu akim-pa talaka mkewe, eda ikaisha na akataka kuolewa na mume mwingine au kurudiwa na mumewe wa kwanza, basi msimzuie kama wakipatana kwa wema; yaani wakiazimia kuoana.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu: Ikiwa wamepatana kwa wema inafa-hamisha kuwa mke anaweza kujioza yule anayemridhia, bila ya kumngoja walii.

Unaweza kusema: hakika Aya imeuondoa uwalii (usimamizi) kwa wanawake walioachwa tu, na wala haikuutaaradhi usimamizi kwa wengineo. Kwa hivyo kuuondoa usimamizi kwa wanawali kunahitajia dalili.

Jibu: Kuthibitisha usimamizi ndiko kunakohitajia dalili; ama kuondoa, dalili yake ni ya asili kwamba kila aliyebaleghe mwenye akili mume au mke ni huru katika mambo yake wala hatawaliwi na yeyote, kwa vyovyote atakavyokuwa isipokuwa tu kama atakiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Hayo anawaonywa nayo yule, miongoni mwenu, anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Hayo ni ishara ya hayo aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika hukumu zake. Anaonywa nayo, yaani wanaonyeka nayo wenye imani sahihi. Ama wengineo katika wenye imani mbovu, masikioni mwao mna vizuwizi, hawasikii mawaidha ya Mwenyezi Mungu na hukumu Zake wala uongozi Wake.

Aya hii ni dalili ya wazi kwamba hakuna imani bila ya ucha Mungu na imani sahihi haiepukani na mawaidha, na asiye waidhika wala kunufaika na amri za Mwenyezi Mungu hana hata chembe ya imani.

Hayo ni mazuri mno kwenu na safi kabisa.

195 <

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Hayo ni ishara ya mawaidha na kutumia hukumu ya Mwenye-zi Mungu katika maisha ya ndoa kwa ujumla na hasa katika waliopewa talaka. Hakuna mwenye shaka kwamba ndoa yenye lengo la utu na kusaidiana katika heri, inaleta ongezeko na usafi katika riziki, usafi wa tabia, heshima na ufanisi kwa watoto. Ama makusudio yakiwa mabaya, basi mwisho wake ni ukafiri, uharibifu, balaa na mashaka katika maisha ya wazazi na watoto.

Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

Makusudio sio kutupa habari kuwa Yeye ni mjuzi au mjuzi zaidi, hapana. Hilo liko wazi halihiitaji mafunzo wala ufafanuzi. Makusudio hasa ni kutilia mkazo na kuhimiza kutekeleza hukumu Zake Mwenyezi Mungu; hata kama haikutubainikia njia ya manufaa yapatikanayo katika hukumu hiyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hekima yake, haamrishi isipokuwa lenye heri na maslahi na wala si lazima tuijue heri hiyo kwa ufafanuzi; bali inatosha tu kujua kuwa Mwenye kuamrisha na Mwenye kukataza, ni Mjuzi Mwenye hekima, halijifichi lolote Kwake liwe ardhini au mbinguni. Kwa ujumla ni kuwa kuna tofauti kati ya mumin na asiyekuwa mumin. Mumin anaabudu kulingana na kauli ya Mwenyezi Mungu na anafanya amali katika hali ya kuyakinisha kupatikana manufaa, hata kama atashindwa kuyafahamu kwa ufafanuzi.

Ama asiyekuwa mumin hafanyi kitu mpaka ajue au adhani kuwa kuna manufaa anayoyajua yeye mwenyewe kwa akili yake au aongozwe na kiumbe kama yeye, ambapo mara nyingi anaruka patupu na kubainikiwa na kinyume, lakini mumin anakuwa katika amani ya Mwenyezi Mungu na hifadhi Yake.

196

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

233. Na wazazi wa kike wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kukamilisha kun-yonyesha; na ni juu ya aliyezaliwa mtoto huyo (baba) chakula chao na nguo zao kulingana na desturi. Wala haikalifishwi nafsi yoyote ila kwa uweza wake. Mzazi (Mama) asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala aliyezaliwa mtoto (baba) kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha (kunyonya) kwa kuridhiana na kushau-riana, basi si kosa juu yao. Na kama mkitaka kuwapa-tia watoto wenu Mama (wengine) wa kuwanyoye-sha, basi haitakuwa vibaya juu yenu kama mkitoa mli-chowaahidi, kwa desturi. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona mnayoya-tenda.

Kaashif2-175.jpg

197

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

MAMA WANYONYESHE

Aya 233

MAANA

Na wazazi wa kike wawanyonyeshe watoto wao.

Wafasiri wamehitilafiana katika makusudio ya tamko la wazazi wa kike. Je, ni waliopewa talaka tu, au ni walio kwa waume zao tu, au wote pamo-ja? Wengi wanasema kwamba tamko hilo linawakusanya wote kwa kuan-galia kidhahiri; wala hakuna dalili ya kuhusisha upande mmoja tu. Na sisi tunaelekea upande huu. Kwa sababu kunyonyesha kunamtegemea mama kwa hali yoyote awayo, sio kwa kuwa na mume wala kwa kuwa ni mtalikiwa.

Wawanyonyeshe watoto wao: ni amri ya mapendekezo tu, sio lazima; kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

"... Na kama mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee (mwanamke) mwingine." (65:6)

Maana yake ni kuwa akina mama wanayo haki ya kuwanyonyesha watoto wao kuliko watu wengine.

Unaweza kuuliza kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na ni juu ya baba chakula chao na nguo zao" inatilia nguvu kuwa makusudio ya Wazazi watakao nyonyesha ni wanawake walioolewa au walio katika talaka rejea tu; na wala sio walioachwa ambao imekwisha eda yao. Kwa sababu mtalikiwa, chake ni malipo ya kunyonyesha tu sio chakula; kwa hiyo Aya haiwahusishi waliopewa talaka.

198

Kaashif2-176.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Jibu: Hapana kizuizi kwa tamko moja kuenea kihukumu kwa upande mmoja na kuhusika upande mwingine pamoja na kupatikana dalili. Iko hadithi na wamekongamana wanavyuoni kuwa mwenye kupewa talaka hana posho isipokuwa malipo ya kunyonyesha; kwa hiyo hakuna dalili iliyohusisha upande fulani, basi tunafuata kuenea kwa wote.(aliye katika ndoa na mtalikiwa)

MIAKA MIWILI KAMILI.

Hapa kuna maswali mawili: Kwanza: Je, inafaa mama kunyonyesha mtoto zaidi ya miaka miwili?

Jibu: Ndio, hasa ikiwa mtoto anahitajia ziada. Kuwekwa kiwango cha miaka miwili kuna faida tatu:

1. Mama asidai malipo zaidi ya miaka miwili.

2. Ukitokea mzozano kati ya baba na mama kuhusu muda wa kunyonyesha mtoto, basi hukumu itakuwa ya Mwenyezi Mungu: 'Miaka miwili kamili.'

3. Kunyonyeshwa mtoto baada ya miaka miwili na mtu kando hakuwezi kusababisha uharamu kati ya mnyonyeshaji na mtoto: Hivyo ndivyo walivyosema Shia na Shafii. Ama Abu Hanifa yeye amesema hiyo ni mpaka baada ya miezi thelathini.

Swali la pili: Je, inafaa kupunguza muda wa miaka miwili?

Jibu: Inafaa kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha.

Na pia kauli yake: Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kur-idhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao

Je, tutarudia sharia katika kiwango cha chini cha muda wa kunyonyesha,

au tutaangalia hali ya afya ya mtoto?

Mafaqihi wengi wamesema uchache wa muda wa kunyonyesha ni miezi

199

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

21 kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-177.jpg

"... Na kubeba mimba kwake na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini..." (46:15)

Tukitoa miezi tisa ambayo aghlabu inakuwa ya mimba, inabakia miezi ishirini na moja.

Kwa vyovyote ilivyo, umuhimu ni kuchunga afya ya mtoto na maslahi yake ambayo yanatofautiana kwa kutofautiana miili. Na utafiti huu ulikuwa na umuhimu hapo zamani ambapo hakukuwa na lishe ya kutosha. Ama hivi leo ambapo lishe zimejaa tele, suala hili halina maudhui tena.

Na ni juu ya aliyezaliwa mtoto huyo (baba) chakula chao na nguo zao kulingana na desturi.

Kwa dhahiri ulazima wa kulea uliotajwa hapa ni kwa mke na aliye katika eda ya talaka rejea. Kimetajwa chakula na mavazi kwa sababu ya umuhimu wake.

Makusudio ya desturi ni kuangalia hali ya matumizi ya mke katika jamii yake. Ama kuangalia hali ya mume kimali, Mwenyezi Mungu anasema:

Haikalifishwi nafsi yoyote ila kwa uweza wake.

Tafsir wazi ya jumla hii tunaweza kuipata katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

200

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-178.jpg

"Mwenye uwezo atoe kadiri ya uwezo wake; na yule ambaye amepun-gukiwa riziki yake, atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yoyote ila kwa kadiri ya alichom-pa..."(65:7)

Imam Jaffar Sadiq (a.s.) alikuwa na marafiki wengi, mara nyingine walikuwa wakichelewa kuondoka nyumbani kwake mpaka unafika wakati wa chakula, basi huwaletea chakula; mara huwaletea mkate na siki na mara nyingine huwaletea chakula kizuri kabisa. Mmoja akamuuliza sababu ya kufanya hivyo. Imam akamjibu: "Tukiwa na nafasi tunawapa cha nafasi na tukiwa na dhiki tunawapa cha dhiki."

Mzazi (Mama) asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala mwenye kuzaliwa mtoto (baba) kwa ajili ya mwanawe.

Inapasa kuangalia vizuri Aya hii, kwa sababu makadhi hivi sasa wanatoa ushahidi sana kwa Aya hii katika hukumu zao na kuifasiri kuwa baba asimd-huru mama kwa sababu ya mtoto. Ama watu wa tafsiri wanakurubia kuafikiana kwa pamoja kwamba maana yake ni kinyume na hivyo; kwamba mama asikatae kumnyonyesha mtoto wake na kumdhuru kwa kutaka kumkasirisha baba yake kwa hilo.

Mwenye Majmaul Bayan anasema: "Mama asiache kumnyonyesha mtoto wake kwa ajili ya kumuudhi baba yake." Sasa haya yako wapi na ushahidi wa makadhi kwamba baba asimdhuru mama kwa sababu ya mtoto?

Na sisi tunasema, baada ya kuitia akilini Aya bila ya kutegemea zaidi maneno ya mafaqihi na wafasiri, kwamba mara nyingi kunapotokea kutengana kati ya mtu na mkewe, humfanya mtoto ndio chombo cha kukasirishana, na matokeo yake mtoto hudhurika kwa kumfanya mtoto

201

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

ndio kafara la ugomvi wao.

Mfano mama anaweza kukataa kumnyonyesha mtoto, hata kama iko haja, ili amuudhi baba. Au baba anaweza kumnyang'anya mama mtoto na kumpatia mtu mwingine amnyonyeshe, hata kama mamake anataka kumnyonyesha.

Mwenyezi Mungu amekataza kudhuriana kwa namna yoyote ile, iwe kwa mtoto, baba au mama kwa sababu ya mtoto. Haya ndiyo yanayokuja haraka kwenye fahamu katika kauli yake Mwenyezi Mungu. Wala hayapingani na kauli ya wafasiri, isipokuwa yanayopingana ni kutolea ushahidi makadhi; ingawaje kauli yao yenyewe ni sahihi, lakini makosa yako katika kutolea ushahidi.

Na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo .

Wamehitalifiana kuhusu makusudio ya mrithi, je ni mrithi wa baba au mrithi wa mtoto?

Mfumo wa maneno unatilia nguvu kwamba ni mrithi wa mwenye mtoto (baba), lakini maana hayasimami sawa. Kwa sababu mtoto na mama ni katika jumla ya warithi wa baba na kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu mfano wa hivyo inaonyesha ni wajibu kwa mrithi wa baba kutoa posho ile iliyo wajibu kwa baba.

Kwa hivyo inamaanisha posho ya mama ni wajibu kwa mama, kwa mtoto wake na kwa warithi wengine wakiwepo. Inavyo-julikana ni kuwa posho ya mama si wajibu kwa yeyote ikiwa huyo mama anauwezo; ni sawa uwezo huo uwe umetokana na kumrithi mume, au la. Kwa hivyo basi hakuna maana kusema kuwa ni wajibu kujilisha kutokana na mali yake.

Kama tukifasiri mrithi kwa maana ya mrithi wa mtoto, basi itakuwa tunahi-talifiana na dhahiri kwa upande mmoja; pia tutakuwa tunahitilifiana na hali ilivyo kwa upande mwingine. Kwa sababu posho ya mama si wajibu kwa anaye mrithi mtoto. Ni kweli kuwa Mama anaweza kuchukua ujira wa kun-yonyesha kutoka katika mali ya mtoto wake (anaye mnyonyesha), ikiwa anayo mali, lakini ujira wa kunyonyesha ni kitu kingine na posho ni kitu kingine kwa maana yake sahihi.

202

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Ilivyo hasa ni kwamba Aya hii ni miongoni mwa Aya za mifano zenye kuta-tiza ndio maana Malik akasema kuwa ni Mansukh (iliyoachwa hukumu yake) kama alivyonakili Abu bakr Al-maliki katika kitabu cha Ahakamul Qur'an. Baadhi ya wafasiri wameiruka na wengine wameinakilia kauli zisizo kuwa na nguvu.

Kutatiza kwake kama tulivyobainisha ni ikiwa itabaki dhahiri ilivyo, maana hayatasimama sawa; yaani tukifasiri mrithi kwa maana ya mrithi wa baba na kufasiri mfano wa hivyo kwa maana ya posho ya mama. Na kama tukifasiri mrithi kwa maana ya mrithi wa mtoto na mfano wa hivyo kwa maana ya malipo ya kunyonyesha, maana yatakuwa sawa lakini tutakuwa tunahitalifi-ana na dhahiri ya matamko mawili (mrithi na mfano wa hivyo). lakini hakuna njia nyingine zaidi ya kuhitalifiana na dhahiri ya tamko na kulifasiri kimaana (taawili). Sio mbali kuwa Hadith zenye kupokewa katika kunyonyesha na malipo yake, ni mfano wa dalili ya kuswihi taawili hii.

Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha (kunyonya) kwa kuridhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao.

Yaani baba na mama kwa kushauriana wanaweza kumwachisha mtoto kabla ya miaka miwili au baada yake kwa maslahi ya mtoto; bali inajuzu kwa baba kumpa mnyonyeshaji mwingine; Mwenyezi Mungu ame-lionyesha hilo kwa kusema:

Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu Mama (wengine) wa kuwany-onyesha, basi haitakuwa vibaya juu yenu kama mkitoa mlichowaahidi kwa desturi.

Msemo 'mkitoa mlichowaahidi,' unaele-kezwa kwa akina baba. Maana yake ni enyi akina baba! Hakika mama ana haki zaidi ya kumyonyesha mwanawe kuliko mtu wa kando; naye mama anastahiki malipo ya kawaida. Ikiwa mumempa haki hii na mkamdhamiria kumpa malipo ya kunyonyesha ya kawaida, lakini akataka zaidi, basi si vibaya hapo kuwapatia watoto wenu wanyonyeshaji wengine. Imesemwa kuwa maana yake ni mkiwapatia wanyonyeshaji wa nje malipo ya kawaida si vibaya kwenu.

Vyovyote iwavyo, ni juu ya baba kumpatia haki (malipo) yake kila mmoja, awe mama au mama wa kunyonyesha tu.

203

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

234. Na wale wanaokufa miongo-ni mwenu na kuacha wake (hao wake) wangoje miezi minne na siku kumi. Na wanapofikilia muda wao, basi si vibaya kwenu kwa yale            wanayojifanyia,

yanayoafiki ada.         Na

Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

235. Wala si vibaya kwenu kuonyesha ishara ya kuwa-posa wanawake, au kutia azma katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakum-buka. Lakini msifanye nao ahadi kwa siri; isipokuwa mseme maneno yaliy-oruhusiwa na sharia. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda uliofaradhiwa ufike. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo katika nafsi zenu, basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufi-ra, mpole.

Kaashif2-179.jpg

204

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

EDA YA KUFIWA

Ay a 234 - 235:

MAANA

Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake; wangoje miezi minne na siku kumi.

Mafaqihi wote wameafikiana kwamba eda ya mwenye kufiwa na mume ni miezi minne na siku kumi. Awe mkubwa au mdogo; mwenye kutoka hedhi au aliyekoma, mwenye kuingiliwa au la. wamelitolea dalili hilo kwa Aya hii.

Ama akiwa na mimba, madhehebu manne ya kisunni yamesema: Eda yake itakwisha kwa kuzaa; hata kama ni muda mchache tu, baada ya kufa mumewe, kiasi ambacho anaweza kuolewa hata kabla ya kuzikwa mumewe, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-180.jpg

"... Na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapo-zaa..." (65:4)

Mafaqihi wa Kishia wamesema: Eda yake ni ule muda utakaorefuka zaidi; yaani ikipita miezi minne na siku kumi kabla ya kuzaa atangojea mpaka azae; au akizaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi, atakaa eda ya miezi minne na siku kumi. Wametoa dalili juu ya hilo kwa ulazima wa kukusanya Aya mbili; "Wangoje miezi minne na siku kumi" na "Eda yao ni mpaka watakapozaa."

Aya ya kwanza imejaalia eda kuwa ni miezi minne na siku kumi, nayo inakusanya mwenye mimba na asiye na mimba; na Aya ya pili imeifanya eda ya mwenye mimba ni kuzaa, nayo inakusanya mwenye kuachwa na mwenye kufiwa na mumewe. Kwa hivyo kutakuwa na mgongano kati ya

205

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

dhahiri ya Aya mbili kwa mwanamke mwenye mimba ambaye atazaa kabla ya miezi minne na siku kumi: Kwa mujibu wa Aya ya pili itakuwa eda imekwisha na kwa mujibu wa Aya ya kwanza itakuwa bado haijaisha kwa sababu miezi minne na siku kumi haikutimia.

Vile vile utapatikana mgongano ikipita miezi minne na siku kumi, akiwa bado hajazaa; kwa mujibu wa Aya ya kwanza eda itakuwa imekwisha kwa sababu muda wa miezi minne na siku kumi umekwisha; na kwa mujibu wa Aya ya pili itakuwa eda bado haijaisha kwa sababu hajazaa. Na maneno ya Qur'an ni mamoja ni lazima yaafikiane.

Kwa hivyo tukiziunganisha Aya mbili na kuzikusanya katika jumla moja, zikawa hivi; "Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake; wan-goje miezi minne na siku kumi. Na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa." Tukizikusanya hivi, maana yake yatakuwa ni: Eda ya mwenye kufiwa na mumewe ni miezi minne na siku kumi, kwa asiyekuwa na mimba; na mwenye mimba ambaye atazaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi. Na itakuwa eda ya mwenye kufiwa, mwenye mimba ambaye atazaa baada ya kupita miezi minne na siku kumi, ni kuzaa. Kama akiuliza mwulizaji: Vipi Shia wamefanya eda ya mwenye mimba, aliyefiwa na mume, ni muda utakaorefuka pamoja na kwamba Aya "Na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa", iko wazi kwamba eda inaisha kwa kuzaa?

Shia naye anaweza kujibu kwa kusema: "Vipi madhehebu manne ya Sunni yakasema kuwa eda ya mjane mwenye mimba inaweza kuwa hata miaka miwili kama ikiendelea mimba pamoja na kuwa Aya "Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuwaacha wake, (nao wake) wakae wan-goje miezi minne na siku kumi" iko wazi kwamba eda ni miezi minne na siku kumi?"

Kwa hiyo hakuna j engine lolote la kuchukulia Aya mbili isipokuwa kuchuku-lia kauli ya muda utakaorefuka zaidi.

206

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na wanapofikia muda wao, basi si vibaya kwenu kwa yale wanayoji-fanyia, yanayoafiki ada Mwenyezi Mungu anazo habari mnayoyaten-da.

Yaani kama ukisha muda wa eda ya mjane, basi hapana dhambi kwenu enyi Waislamu kwa mwanamke kufanya yale aliyozuiliwa wakati wa eda; kama kujipamba na kuonekana, na wanaotaka kuwaoa kwa njia ile iliyo maarufu kisheria. Hapa Mwenyezi Mungu anawaambia Waislamu wanaume, kwa sababu ni juu yao kuwazuia wanawake wanapopetuka mipaka ya kisheria. Wameafikiana mafaqihi kwa kauli moja kuwa mjane aliyefiwa na mume wakati wa eda ni wajibu kwake kujiepusha na kila linalomfanya kuonekana mrembo wa kutamanika.

Wala si vibaya kwenu kuonyesha ishara ya kuwaposa wanawake.

Mwenyezi Mungu ameharamisha ndoa katikati ya eda ya namna yoyote, bali ni haramu pia kwa mwanamume kumposa mwanamke akiwa katika eda yake, iwe ni eda ya kufiwa na mume au ya talaka bain, lakini Mwenyezi Mungu anahalalisha kufanya ishara ya posa bila ya kudhi-hirisha, katika isiyokuwa eda ya talaka rejea. Kwani mtalaka katika eda hiyo bado yuko mikononi mwa mume we.

Au kutia azma katika nyoyo zenu.

Kila linalopita akilini na kuazimiwa na moyo halina ubaya kwa Mungu, kwa sababu liko nje ya uwezo wa mtu; lililo kwenye uwezo wa mtu ni zile athari. Kwa hivyo mtu akiazimia kuoa mke aliye edani, sio dhambi. Lakini akiidhi-hirisha azma yake hii akamposa, basi atakuwa ni mwenye dhambi. Kwa sababu kuazimia kuko nje ya uwezo na kudhihirisha kuko ndani ya uwezo wa mtu. Iko Hadith inayosema: "Ukiwa na donge moyoni usilitekeleze." Hapo amekataza kufanya, ambako ni athari ya hilo donge, lakini hakukataza kuwa na donge kwa sababu hakuzuiliki.

Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka.

Kwa hivyo ndio akawahalalishia kuonyesha ishara, lau angeliwazuia basi

207

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

mngeliona mashaka.

Lakini msifanye nao ahadi kwa siri.

Hiyo ishara ya kuoa pia haifai kuionyesha kwa siri wakati wa eda katika faragha. Kwa sababu faragha kati ya mwanamume na mwanamke inale-ta mambo asiyoyaridhia Mwenyezi Mungu. Iko Hadith inayosema:

"Hakai faragha mwanamume na mwanamke isipokuwa shetani huwa watatu wao." Hasa ikiwa mume anamtamani aliyekaa naye faragha, isipokuwa ikiwa mume ana yakini kwamba faragha haitaleta haramu katika maneno wala vitendo, hapo ndipo itajuzu kusema naye yale ambayo si mabaya, hata kusema kwa dhahiri. Ndio Mwenyezi Mungu akalegeza kido-go kwa kusema; "Isipokuwa mseme maneno yaliyoruhusiwa na sharia."

Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda uliofaradhiwa ufike.

Yaani msifunge ndoa ndani ya eda mpaka ishe.

NDOA KATIKA EDA

Baada ya kuafikiana Waislamu wote kwamba kufunga ndoa na kuposa wazi wazi katikati ya eda, ni katika mambo ya haramu, na kwamba ndoa itakuwa batili baada ya kuafikiana hivi, wakahitalifiana juu ya uharamu wa waliofunga ndoa ndani ya eda. Je mwanamke atakuwa haramu milele au inawezekana kufunga ndoa tena baada ya kwisha eda?

Hanafi na Shafi wamesema hakuna kizuizi cha kumwoa mara ya pili. Hayo yamo katika kitabu Bidayatul Mujtahid.

Shia wamesema: Akifunga naye ndoa na hali anajua kuwa yuko katika eda, basi atakuwa haramu kwake daima, iwe amemwingilia au hakumwingila. Na akifunga naye ndoa bila ya kujua kuwa yuko kwenye eda, basi hatakuwa haramu, isipokuwa kama amemwingilia, na anaweza kumwoa tena baada ya eda kama hakumwingilia.

Hii ndio hukumu ya kufunga ndoa katikati ya eda. Ama kuposa hakuna athari yoyote isipokuwa dhambi tu.

Maajabu niliyoyasoma katika suala hili ni yale yaliyo katika kitabu Ahkamul

208

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Qur'an cha Abu Bakr Al Andalusi wa madhehebu ya Malik, pale aliposema: "Akimposa katikati ya eda, kisha akafunga naye ndoa baada ya eda, basi ni lazima amwache talaka moja, kisha aanze upya kumchumbia na kufunga ndoa."

236. Si vibaya kwenu kama mkiwapa wake talaka ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari. Na wapeni cha kuwali-waza, mwenye wasaa kadiri aweza-vyo na mwenye dhiki kadiri awezavyo. Kiasi cha kuwali-waza, cha kawaida. Ndio haki kwa wafanyao mema.

237. Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa na mmekwisha wakadiria mahari, basi ni nusu ya hayo mahari           mliyokadiria.

Isipokuwa          (wanawake

wenyewe) wasamehe au asamehe ambaye kifungo cha ndoa kiko mikononi mwake, na kusamehe ndiko kuliko karibu zaidi na takua. Wala msisahau fad-hila baina yenu; hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyafanya.

Kaashif2-181.jpg

209

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

TALAKA KABLA YA KUINGILIA

Aya 236 -237

MAANA

Si vibaya kwenu kama mkiwapa wake talaka ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari

Yaani hamlazimiwi na mahari. Kwa ujumla maana yake ni kwamba mwenye kufunga ndoa na mwanamke wala asimtajie mahari katika ndoa, kisha akamwacha kabla ya kumwingila, basi hana ulazima wa kutoa mahari; isipokuwa mwanamke anastahiki kupewa kiasi cha kumliwaza tu. Kiasi hicho ataangalia mume uwezo wake; kwa mfano tajiri anaweza kutoa mkufu wa thamani ya shs. 1000, mtu wa kawaida akitoa bangili ya Shs. 500 na masikini akatoa nguo ya Shs. 20. Katika haya Mwenyezi Mungu anasema:

Na wapeni cha kuwaliwaza mwenye wasaa kadiri awezavyo, na mwenye dhiki kadiri awezavyo. Kiasi cha kuwaliwaza, cha kawaida. Ndio Haki kwa wafanyao mema.

Wale ambao wanazifanyia wema nafsi zao kwa kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa na mmekwisha wakadiria mahari, basi ni nusu ya hayo mahari mliyokadiria.

Ikiwa amefunga ndoa akataja mahari kisha akamwacha kabla ya kumwingilia, basi anastahiki nusu ya mahari.

Isipokuwa (wanawake wenyewe) wasamehe.

Yaani haifai kumzuilia mwanamke nusu ya mahari au kitu chochote, isipokuwa kama akisamehe mwenyewe kwa radhi yake.

Au asamehe ambaye kifungo cha ndoa kiko mikononi mwake.

Mume ndiye ambaye kifungo cha ndoa kiko mikononi mwake. Makusudio ni kwamba mwenye kupewa talaka kabla ya kuingiliwa hastahiki zaidi

210

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

ya nusu ya mahari yaliyotajwa isipokuwa kama mume atampa yote au kumpa zaidi ya nusu.

Na kusamehe ndiko kuliko karibu zaidi na takua.

Msemo unaelekezwa kwa wote, mume na mke, kuwahimiza kusameheana.

238. Angalieni sana swala, na ile swala ya katikati. Na sima-meni kwa unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

239. Na kama mkiwa na hofu, basi ni hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda.                     Na

mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyowafunza yale mliyokuwa hamyajui.

SWALA YA KATIKATI

Ay a 238 - 239:

Angalieni sana Swala na ile Swala ya katikati

Kuziangalia sana ni kuzitekeleza kwa nyakati zake na njia zake. Mwenyezi Mungu ameihusisha hii kwa kuipa uzito na umuhimu; kama umuhimu wa Jibril na Mikail katika Malaika alipowahusu wao, baada ya kuwakusanya na Malaika wen-gine katika kauli yake:

Kaashif2-182.jpg

211

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-183.jpg

Ambaye ni adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail..." (2:98)

Wamehitalifiana kuhusu swala ya katikati, mpaka kufikia kauli kumi na nane; kama ilivyonakiliwa katika kitabuNaylul Awtw ar. Kauli iliyo mashuhuri zaidi ni ile inayosema kuwa ni swala ya Alasiri, na kuna riwaya katika hilo. Imesemwa kwamba imeitwa swala ya katikati kwa sababu iko baina ya swala mbili za (Maghribi na Isha) na swala mbili (Asubuhi na Adhuhuri). Ama sababu ya kutajwa kwake ni kwamba inakuwa wakati ambao aghlab watu wanashughulika.

Mwenye tafsir ya Al Manar amenakili kutoka kwa Ustadh wake, Sheikh Muhammad Abduh, kwamba yeye amesema: Lau si kuwako kongamano juu ya tafsiri ya Wusta kuwa ni moja ya swala tano na wala sio tano zote, basi yeye angeliifasiri kwa swala bora; na Mwenyezi Mungu amehimiza na kutil-ia mkazo swala bora nayo ni ile ambayo moyo unakuwapo ndani ya hiyo swala, nafsi kuwa na mwelekeo wa kuwa na ikhlas kwa Mwenyezi Mungu na kuzingatia maneno Yake. Sio swala ya kujionyesha au ya mwili tu, lakini moyo haupo.

Haya ndiyo maelezo mazuri zaidi niliyosoma katika tafsiri ya Aya hii, nayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Kaashif2-184.jpg

Wamefuzu waumini ambao katika swala zao huwa ni wanyenyeke-vu."(23:1-2)

212

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na simameni kwa unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Yaani mumuombe Mwenyezi Mungu katika swala zenu kwa unyenyekevu wa kuhisi ukubwa na utukufu wake, hali ya kuachana na mambo yanayoushughulisha moyo.

Na kama mkiwa na hofu basi ni hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda.

Swala haisamehewi kwa hali yoyote ile. Mtu akiwa anashindwa kufanya baadhi ya vitendo vyake, basi atatekeleza vile atakavyoweza. Akishindwa kufanya vitendo vyote, basi ataswali kwa kutamka na kuashiria. Ikiwa hivyo pia atashindwa, basi ataleta picha ya swala moyoni.

Hapa anaashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba mtu anaweza kufiki-wa na wakati wa Swala naye yuko vitani akiwa amekabiliana na adui, n.k. basi ataswali kadiri atakavyoweza, kwa kwenda au akiwa amepanda kitu; kwa kuelekea Qibla au bila ya kuelekea.

Mwenye Majmaul Bayan anasema: "Swala ya kuhofia adui ni rakaa mbili iwe ni safirini au nyumbani, isipokuwa Maghrib tu, hiyo ni rakaa tatu.

Imepokewa Hadith kwamba Imam Ali (a.s.) katika usiku wa vita vya Harir aliswali kwa kuashiria na ikasemwa ni kwa takbir, na kwamba Mtume (s.a.w.w.) siku ya vita vya Ahzab aliswali kwa kuashiria.

Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyowafunza yale mliyokuwa hamyajui.

Yaani hofu ikiondoka basi swalini swala ya kawaida ile mliyofundishwa mwanzo.

213

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

KUACHA SWALA KUNAPELEKEA UKAFIRI

Tumezungumzia swala katika kufasiri Aya iliyotangulia na sasa tunaun-ganisha kifungu hicho na haya yafuatayo:

Majaribio yamethibitisha kwamba kuacha swala mara nyingi kunapele-ka ukafiri na athari zake. Hiyo ni kwamba kafiri hajali kufanya haramu, basi hivyo hivyo mwenye kuacha swala anafanya mambo ya haramu bila ya kujali. Popote penye ukafiri pana uovu na uchafu. Hali hiyo inaletwa na kuacha swala.

Dalili kubwa zaidi inayoonyesha hakika hii ni ufisadi katika zama zetu hizi. Haya mabaa, madanguro na ma casino katika miji yetu. Na pia huku kutembea nusu-uchi kwa mabinti zenu na tabia mbaya za watoto wetu (kuiga wazungu), yote hayo ni natija ya kuacha swala; kwa dalili ya kuwa haya yote hayakuwako wakati wa swala ilipokuwa imezoeleka kwa watoto wetu wa kiume na wa kike. Hiyo ndiyo tafsir ya Hadith tukufu inayose-ma:

"Tofauti kati yetu sisi na nyinyi (makafiri) ni swala; mwenye kuiacha amekufuru."

Haitamtosha mtu kusema: Mimi ni Mwislamu au kutamka shahada mbili (kushahadia) tu, maadamu amali zake ni za kikafiri na kilahidi.

Hakika mlahidi haoni haya wala kigegezi chochote kuacha swala, na hafichi hilo, bali hutangaza hasa, kwa sababu hafuati dini. Basi hivyo hivyo vijana wetu wa kileo wanaona fahari kujulikana kuwa hawaswali, bali wanamdharau mwenye kuswali na swala yenyewe. Kwa hivyo haku-na tofauti kati yao na walahidi.

Si vibaya kama tukinukuu mawaidha mazuri kutoka katika kitabu Al-Islam Khawatir wa Sawanih cha Mfaransa, Comte Henry Descarte kilichofasiri-wa kwa Kiarabu anasema:

214

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

"Nilisafiri katika jangwa la jimbo la Hawaran nikiwa na wapanda farasi the-lathini, wote wakinihudumia mimi. Wakati tukiendelea na msafara, mara sauti ikanadi kwamba wakati wa swala ya Alasiri umefika. Wapanda farasi wote wakashuka haraka; mara wakajipanga safu za swala ya jamaa, nikawa ninawasikia wakilikariri neno Allahu Akbar kwa sauti ya juu. Likawa jina hilo la Mungu linaniingia akilini zaidi kuliko nilivyoingiwa akilini na somo la elimu ya Mungu. Nikahisi kukosa raha kuliko sababishwa na haya na kuhisi kwamba hao wapanda farasi ambao walikuwa wakinitukuza muda mchache uliopita, hivi sasa wakiwa katika swala yao, wanahisi kwamba wako katika makao ya juu zaidi na wenye nafsi tukufu zaidi kuliko mimi. Lau ningeitii nafsi yangu ningeliwapigia kelele kwa kusema: Mimi pia ninamkubali Mungu na ninajua Swala.

Ni uzuri ulioje wa mandhari ya watu hao katika swala yao na huku farasi wao wako pembeni mwao wakiwa wametulia kimya kamba zao zikiwa chini, kama kwamba wao nao wanainyenyekea swala; farasi aliyekuwa akipendwa na Mtume kwa mapenzi ambayo yalimpelekea Mtume kuifuta pua yake kwa shuka yake.

Nilisimama pembeni nikiwaangalia wan-aoswali na kujikuta mimi niko pweke kabisa nikionyesha alama ya kukosa imani, kana kwamba mimi ni mbwa tu, aliye mbele ya wale wanaomkariria Swala Mola wao kwa unyenyekevu unaotoka katika nyoyo zilizojaa ukweli na imani.

215

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

240. Na wale wanaokufa miongo-ni mwenu na wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi ya mwaka mmoja bila ya kutolewa. Wakiondoka, basi si vibaya kwenu kwa yale waliyojifanyia wenyewe, yanayofuata desturi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

241.  Na wanawake waliopewa talaka wapewe cha kuwali-waza kulingana na desturi; hiyo ni haki kwa wenye takua.

242. Namna hiyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya Zake ili mpate kufahamu.

Kaashif2-185.jpg

216

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

NA WALE WANAOKUFA Aya 240 - 242

MAANA

Ilikuwa ni ada ya Waarabu kabla ya Uislamu kwamba mtu akifa, mkewe hapati urithi wowote isipokuwa posho yake ya mwaka mmoja tu; kwa sharti akae eda katika nyumba ya mumewe. Akitoka kabla ya mwaka, basi hana posho. Aya hii ni uthibitisho wa hayo, na yalikuwapo katika mwan-zo wa Uislamu.

Wafasiri na mafaqihi wote wameafikiana kwa kauli moja kwamba Aya hii ni Mansukh hukumu yake (haitumiki tena) na imenasikhwa na Aya mbili:

Kaashif2-186.jpg

1. "Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake, wangoje miezi minne na siku kumi..."(2:234)

2. "...Nao (wake zenu) watapata robo ya mlivyoacha, ikiwa hamna mtoto, lakini ikiwa mnaye mtoto basi wao (wanawake) watapata thu-muni..." (4:12)

Kwa maana kuwa atajilisha mwenyewe kutokana na fungu lake.

Pamoja na kwamba Aya hii haitumiki kabisa hukumu yake katika sharia, lakini tutaifasiri kama walivyofanya wafasiri.

217

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Na wale wanaokufa miongoni mwenu na wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi ya mwaka mmoja.

Ilikuwa kabla ya kutotumika Aya hii ni wajibu kwa wale ambao wanadhi-hirikiwa na alama za mauti kuusia kwa ajili ya wake zao wazuiliwe majumbani kwa kupewa posho.

Bila ya kutolewa.

Yaani posho itakuwa wajibu kama wakitaka kukaa katika nyumba ya bwana aliyefariki. Ama wakitoka, basi si wajibu. Kwa hivyo ndio akaashiria Mwenyezi Mungu kwa kusema:

Wakiondoka basi si vibaya kwenu.

Yaani hamna jukumu kuwapa posho. Kwa maneno mengine posho ni wajibu kwa kubaki nyumbani, wakitoka hakuna posho.

Kwa yale waliyojifanyia wenyewe, yanayofuata desturi.

Mwanamke akitoka nyumbani kwa mumewe aliyefariki, anaweza kuji-pamba na kuposwa katika mipaka ya sharia; yaani mwanamke aliyefiwa na mumewe ana hiyari kubaki nyumbani kwa mume kwa muda wa mwaka mmoja na kupewa posho au kutoka asipewe posho.

Na wanawake waliopewa talaka wapewe cha kuwaliwaza kulingana na desturi; hiyo ni haki kwa wenye takua.

Kutoa ni lazima kuangalia hali ya mtoaji; kama ilivyokwishaelezwa katika Aya ya 236. Tamko la wenye kupewa talaka linawakusanya wataliki-wa wote ambao wanagawanyika sehemu nne.

1. Mwenye kupewa talaka akiwa amekwishaingiliwa na amekwisha bainishiwa mahari, huyu atapata mahari yote, kama ilivyobainishwa katika Aya ya 229.

218

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

2. Mwenye kupewa talaka bila ya kuingiliwa na amekwisha bainishwa mahari; yeye atapata nusu ya mahari; kama ilivyoelezwa katika Aya ya 237.

3. Mwenye kupewa talaka akiwa ameingiliwa, lakini hakubainishiwa mahari; yeye atapata mahari kiasi cha makisio ya desturi yao. Hilo wameafikiana Waislamu wote.

4. Mwenye kupewa talaka, bila ya kuingiliwa na bila ya kubainishiwa mahari. Huyu hana mahari, isipokuwa atapewa cha kumliwaza tu; kama ilivyoelezwa katika Aya ya 236.

Kwa ufupi ni kwamba cha kuliwaza hupewa yule mwenye kupewa talaka bila ya kuingiliwa na bila ya kubainishiwa mahari wakati wa ndoa. Ama wengine hakuna ulazima wa kuwapa bali ataachiwa mwenyewe aliyetoa talaka akitaka atampatia cha kuliwaza, asipotaka ni basi. imesemwa kuwa ni sunna kumpatia.

Namna hiyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake ili mpate kufahamu.

Yaani mpate kujua. Kwa sababu ambaye haonyeki na kuacha kutumia hukumu za Mwenyezi Mungu, basi yuko katika daraja ya wasiokuwa na akili.

219

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

243. Je, hukuwaona wale waliotoka majumbani mwao nao walikuwa maelfu wakio-gopa mauti? Mwenyezi Mungu           akawaambia:

Kufeni; kisha akawafufua. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

244. Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.

KUOGOPA MAUTI

Aya 243 - 244

MAANA

Wafasiri wamerefusha maneno kuhusu Aya hii, wengi wao wameonyesha kuwa ni kisa cha kihistoria na kuchafua kurasa katika kukielezea kisa hiki. Baadhi yao wamesema hivi:

Watu katika Waisrail waliamrishwa kupigana jihadi dhidi ya adui zao. Wakaogopa kupigana ili wasife, wakayakimbia majumba yao kwa kuogopa kufa. Mwenyezi Mungu akawaua ili kuwafahamisha kwamba hakuna kitu

Kaashif2-187.jpg

220

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

chochote kinachoweza kukinga mauti; kisha akawafufua ili wazingatie na wamalize umri wao uliobakia.

Ya kushangaza zaidi niliyoyasema katika tafsiri ya Aya hii ni kwamba mmoja wa wafasiri anasema: "Mauti ni namna mbili: Mauti ya mateso, nayo ni yale ya ambayo mtu huhuishwa baada ya kufa hapa hapa duniani. Na mauti ya ajali ambayo mtu atafufuliwa akhera."

Wengine wamesema walikimbia maradhi ya Tauni, lakini sio kwa kupigana jihadi.

Muhyiddin bin Arabi ameifasiri Aya hii kwa tafsiri yake ya Kisufi kwa kusema: "Mwenyezi Mungu aliwaua kwa ujinga akawafufua kwa elimu na akili."

Sheikh Muhammad Abduh ameichukulia Aya hii ni tamthiliya ya mazinga-tio na maonyo na wala sio tukio la kweli, na kwamba lengo la ishara hii ni kubainisha desturi ya Mwenyezi Mungu katika umma mbali mbali, na kwamba umma ambao unapigana jihadi na kulinda haki yake, utakuwa na maisha mema; na umma ambao una woga na kusalimu amri kwenye dhulma, utaishi maisha ya udhalili.

Kwa hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu kufeni ina maana ishini kwa kutawaliwa na kukandamizwa kwa ajili ya woga wenu, kwa sababu mfano wa maisha kama hayo ni mauti sio uhai. Na kauli yake akawahuyisha; ina maana aliwahuyisha kwa maisha ya uhuru na utukufu kwa sababu ya jihadi yao na kupigania haki yao.

Huu ni muhtasar mfupi sana wa rai ya Sheikh Muhammad Abduh ambayo ameifafanua kwa urefu sana. Na rai hiyo, kama unavyoiona, ni ya kimwamko lakini haitokani na dalili ya tamko la Aya. Rai yake yenyewe ni sahihi bila ya shaka lakini iko mbali na dalili ya tamko. Huenda ikad-haniwa kwamba ni ya karibu kuliko zile kauli nyingine za wafasiri kwa upande huu. Kwa sababu kauli zao zinategemea riwaya za Kiisrail na ngano tu. Na kauli ya Sheikh ina lengo la kuhamasisha, kupinga dhulma na

221

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

kujitoa mhanga kwa ajili ya uhuru na heshima ya mtu, jambo ambalo lina mwelekeo.

Vyovyote iwavyo Aya hii inawezekana kuwa na maana mbali mbali, ndio maana kauli zikawa nyingi; wala hakuna kitu katika tamko la Aya kina-chofahamisha kuswihi kauli kwa dhati.

Hata hivyo, kauli ya Sheikh Abduh ndio yenye nguvu zaidi ya kauli zote kwa kuangalia mwelekeo, kama tulivyokwisha eleza. Pia inasaidiwa na mpangilio wa maneno, pale alipofuatishia Mwenyezi Mungu moja kwa moja na Aya inayosema: "Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na jueni kwam-ba Mwenyezi Mungu ni msikizi, mjuzi."

245. Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, ili amzidishie ziada nyingi? Mwenyezi Mungu ndiye anayezuia na hukunja na hukunjua na kwake mtarejezwa.

NI NANI ATAKAYEMKOPESHA MWENYEZI MUNGU Aya 245

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kupigania haki katika Aya iliy-otangulia, katika Aya hii anahimiza kutoa mali ya kuwaandaa wapiganaji. Kwa sababu vita, kama vile vinavyohitajia watu, pia vinahitajia mali.

Mwenye kusoma bajeti ya vita, ya madola makubwa hivi sasa, hana budi kupotewa na tarakimu. Baadhi ya Dola za kimagharibi zimefikia zaidi ya

Kaashif2-188.jpg

222

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

elfu mia nne milioni. Lakini bajeti yote hii inahusika na kufanya uadui, kutaka ukubwa kutawala kimabavu, kuwakandamiza watu na kuwatawala katika mambo yao yote. Ama jihadi aliyoihimiza Mwenyezi Mungu katika kitabu chake ni jihadi kwa ajili ya kupigania haki na kujikinga na maadui.

Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri.

Ilivyo hii ni amri ya kujitolea. Imekuja kwa njia ya swali ili kuilainisha mioyo ya waumini, waweze kuona wepesi kujitolea kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu mkopo mzuri ni kuonyesha kuwa mali itakayotolewa ni lazima iwe ya halali sio ya haram na kujitolea kwa radhi na kukusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Atimize sharti hizo, ili Mwenyezi Mungu amzidishie ziada nyingi.

Imam Jaffar Sadiq (as) anasema: Iliposhuka Aya hii:

Kaashif2-189.jpg

"Atakayefanya wema atapata jaza bora kuliko huo ..." (28:84).

Mtume alisema:"Ewe Mola wangu nizidishie", Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii:

Kaashif2-190.jpg

"... Atakayefanya wema, atalipwa mfano wake mara kumi ..." (6:160)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: "Ewe Mola wangu nizidishie" basi Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii "IliMwenyezi Mungu amzidishie ziada nyingi." Na wingi mbele ya Mwenyezi Mungu hauna idadi.

223

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Na Mwenyezi Mungu hukunja na kukunjua.

Yaani hudhikisha na kufanya wasaa, kwa maana kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuwahimiza waja wake kutoa kwa kuwa ana haja; hapana, Yeye ni mkwasi, na wao ni wahitaji. Lengo hasa ni kuwaongoza kwenye amali ya heri.

Na Kwake mtarejezwa.

Ili mwema alipwe kwa wema wake na mwovu kwa wovu wake.

246. Je, Hukuona wakubwa wa wana wa Israil baada ya Musa walipomwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika njia ya Mwenyezi Mungu. (Mtume wao) akasema: Je, haielekei kuwa               hamtapigana

mtakapoandikiwa kupi-gana?                Wakasema:

Itakuwaje tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na hali tumetolewa nje ya majumba yetu na watoto wetu? Walipoandikiwa kupigana,          wakageuka

isipokuwa wachache mion-goni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhal-imu.

Kaashif2-191.jpg

224

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

247.  Na Nabii wao akawaambia: Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia Talut kuwa mfalme. Wakasema: Vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema:               Hakika Mwenyezi Mungu amem-teua juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa elimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme Wake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mjuzi.

248.  Na Nabii wao akawaambia: Hakika alama ya ufalme wake ni kuwajia lile san-duku ambalo ndani mna kit-ulizo na mabaki ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na wa Harun, wakilibeba Malaika. Hakika katika hayo mna dalili kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.

Kaashif2-192.jpg

225

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

249. Basi Talut alipoondoka na jeshi, alisema: Mwenyezi Mungu atawafanyia mtihani kwa mto. Basi atakayekuny-wa humo si pamoja nami na asiyekunywa atakuwa pamoja nami; ila atakayeteka fumba kwa mkono wake. Wakanywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi walipovuka, yeye na wale walioamini pamoja naye walisema:         Leo

hatumwezi Jalut, na Jeshi lake. Na wenye yakini ya kukutana na Mola wao walisema: Makundi man-gapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wafanyao subira.

250. Na walipotoka kupambana na Jalut na jeshi lake walisema: Mola wetu, tumiminie subira na uisimamishe imara miguu yetu na utasai-die tuwashinde watu makafiri.

Kaashif2-193.jpg

226

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

251. Basi wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; na Daud akamuua Jalut, na Mwenyezi Mungu akampa ufalme na hekima na akam-fundisha aliyoyataka. Na kama Mwenyezi Mungu asingeliwazuia watu, baadhi yao kwa wengine, ingeli-haribika ardhi; lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya viumbe vyote.

252. Hizo ni Aya za Mwenyezi Mungu, tunakusomea kwa haki; na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume/

KISA CHA TALUT

Aya 246 - 252:

Tumekwishaeleza katika tafsiri ya Aya ya 2 kwamba Qur'an ni kitabu cha mwongozo na dini, na ni kitabu cha kueleza tabia njema na sharia; sio kitabu cha visa na Historia au Filosofia na Sayansi, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akielezea tukio la Kihistoria hulieleza kwa ajili ya mawaidha na kuwataka watu wazingatie; na wala haileti kisa chote kwa upambanuzi katika pande zake zote. Hilo limeelezewa katika Aya kadhaa; kama vile:

Kaashif2-194.jpg

227

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-195.jpg

"Kwa hakika katika visa vyao, kuna fundisho kwa wenye akili (12:111)

Kaashif2-196.jpg

"Zimepita desturi kabla yenu, basi tembeeni katika nchi na muone ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha." (3: 137)

Sheikh Muhammad Abduh anasema; "Kujaribu kuifanya Qur'an kuwa ni kitabu cha Historia ni kuhalifu desturi ya Qur'an na ni kuziepusha nyoyo na mawaidha yake, na pia ni kulipoteza lengo lake na hekima yake. Lililo wajibu kwetu ni kufahamu yaliyomo ndani yake na kuzitumia fikra zetu katika kutoa mafundisho, tujivue na yale yanayoitusi na kuikebehi Qur'an, na tujipambe na yale yanayoisifu Qur'an na kuiweka vizuri.

Mwenyezi Mungu amekidokeza kisa cha Talut katika Aya hizi (246-252), Nasi tutakitaja kama vile yanavyofahamisha matamko ya Aya hizi; kisha tutaidokeza sehemu za mafundisho na mawaidha.

Baada ya kufa Musa (a.s.) walikuwako makhalifa wake katika Manabii waliokuwa wakiendeleza amri za Mwenyezi Mungu katika Waisrail. Miongoni mwa makhalifa ni Mtume aliyeelezwa katika Qur'an bila ya kuta-jwa jina lake, isipokuwa alikuwa wakati wa Nabii Daud (a.s.), kama zinavy-ofahamisha Aya. Wafasiri wengi wanasema alikuwa akiitwa Samuel.

Siku moja kikundi cha Waisrail kilimwendea na kumwambia" "Tuwekee mkuu wa jeshi ambaye tutafuata rai yake katika kupanga vita, na tupigane pamoja naye katika njia ya Mwenyezi Mungu,"

228

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Mtume wao akawaambia - na alikuwa amekwisha watahini - "Mimi naona mtamwacha kama vita vikianza na mkiitwa kwenye jihad,"

Wakasema: "Tutamwachaje ikiwa adui ametutoa katika majumba yetu; na kutuweka mbali na watoto wetu?"

Basi Nabii wao akamtaka shauri Mwenyezi Mungu kwa yule atakayefaa kuongoza vita, Mwenyezi Mungu akampelekea wahyi kwa kusema kuwa "Mimi nimewachagulia wao Talut kuwa mfalme," Inasemekana - aliitwa Talut kwa sababu ya urefu wake; kutokana na neno la Kiarabu Tul (urefu),.

Mtume alipowapa habari hiyo kwamba Mwenyezi Mungu amemchagua Talut walisema: "Atakuwaje mfalme wetu na wala hatokani na ukoo wowote mtukufu tena ni maskini?" Mtume akasema: "Kiongozi hahitaji ukoo isipokuwa awe na ushujaa na maarifa ya kuendesha mambo. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa Talut uwezo wa kielimu na ki-umbo na nyenzo nyingine za kiongozi,"

Wakasema: "Basi tunataka alama itakayofahamisha uwezo wake huu."

Akasema: "Alama ni kurudishiwa kasha; litaletwa na Malaika kwa amri ya Mwenyezi Mungu," Inasemekana kasha hilo lilikuwa na mabaki ya mbao za Musa, fimbo yake, nguo zake na baadhi ya sehemu ya Taurat. Na walikuwa wamenyang'anywa na Wapalestina katika vita fulani. Pia ime-semwa kwamba Mwenyezi Mungu aliliinua kulipeleka mbinguni baada ya kufa Musa. Lilipowajia kasha kutoka kwa Mwenyezi Mungu waliamini uon-gozi wa Talut.

Talut akawaongoza kwenda kupigana na adui yao; akawafahamisha kuwa watapitia kwenye mto ambako watatahiniwa kuangaliwa ikhlasi yao. Ambaye atakuwa na subira hatakunywa isipokuwa kiasi cha kitanga chake cha mkono. Atakayefuata ndiye msafi mwenye kutegemewa. Ama ambaye atakunywa mpaka amalize kiu, sio wa kutegemewa katika vita na jihadi. Walipopitia kwenye mto waliasi kama kawaida yao, wakanywa isipokuwa kikundi kidogo tu, kilithibiti kwenye ukweli na uaminifu.

229

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Yalipokutana makundi mawili, Waisiralil wakiongozwa na Talut (Sauli) na Wapalestina wakiongozwa na Jalut (Goliat), Waisrail wengi waliogopa na kumwambia Talut; "Hatumuwezi Jalut na jeshi lake," Waumini wachache ambao hawakunywa maji wakasema : Makundi mangapi madogo yameshin-da makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu," Wakam-womba Mwenyezi Mungu awape subira uthabiti na ushindi. Mwenyezi Mungu akawatakabalia dua yao baada ya kujua nia yao, azma yao na ukweli katika nia. Daud akamuua Jalut na maadui wakahsindwa vibaya sana. Daud akawa maarufu mwenye kusikika sana baada ya kumuua Jalut. Baada ya hapo Mwenyezi Mungu akampa Utume, akamtremshia Zabur na akamfundisha kutengeneza deraya na elimu ya dini na upambanuzi wa maneno; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: Mwenyezi Mungu akampa ufalme na heki-ma."

Huu ndio muhtasari wa zinavyofahamisha Aya tukufu. Ama Daud kum-woa binti ya Talut na kujaribu kufanya vitimbi vya kumuua kwa kumuoza binti yake, teo ya Daud na mawe yake, na kisa cha Daud na wanyama wakali mwituni, na mfano wa hayo yaliyomo katika vitabu vya Tafsir, vyote hivi ni visa ambavyo havina tegemeo lolote la mapokezi isipokuwa mapokezi ya Kiisrail.

Ama somo la kisa hiki ni anayefaa kuongoza ni yule mwenye uwezo wa kielimu na kiumbo na wala sio yule mwenye nasaba na fahari au mwenye jaha na mali; na kwamba ushindi utakuwa pamoja na subira na imani na wala sio kwa wingi wa watu; na njia ya kumjua mwema na mwovu ni kwa majaribio na mitihani.

Baada ya kuelezea muhtasari wa kisa na somo lake, sasa tunaingilia kufasiri j umla za maneno.

MAANA

Je, hukuona wakubwa wa wana wa Israil baada ya Musa.

Kwa dhahiri msemo unaelekezwa kwa Mtume, na katika maana unaelekezwa

230

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

kwa wasikilizaji wote; na tamko linaelekezwa kwa mwenye kukijua kisa na asiyekijua pia. Unaweza kumwambia mtu; "Je hujui fulani amefanya nini," wakati huo unataka kumfahamisha aliyoyafanya.

Walipomwambia Nabii wao; Tuwekee mfalme ili tupigane katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Inasemekana Nabii waliyemwambia hayo ni Samuel.

(Mtume wao) akasema; Je, haielekei kuwa hamtapigana mtakapo andikiwa kupigana!

Yaani; je mambo yako kama ninavyoona kuwa miongoni mwenu kuna watakaojitoa na kuacha kupigana kama mkifaradhiwa vita?

Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na hali tumetolewa nje ya majumba yetu na watoto wetu?

Walikanusha kuwa na chochote kitakacho wafanya waache jihadi; na wak-abainisha sababu itakayowafanya wapigane ambayo ni kutolewa majum-bani mwao na kutenganishwa na watoto wao.

Walipoandikiwa kupigana waligeuka, isipokuwa wachache miongoni mwao.

Watu wengi wana sifa hii; wanathibitisha na wanaazimia kufanya mambo, lakini wakati ukifika wanajificha mvunguni. Ufasaha zaidi wa yaliyosemwa kuhusu mambo hayo ni kauli ya Bwana wa mashahidi Hussein bin Ali (a.s.); "Watu ni watumwa wa dunia na dini wameilamba kwa ndimi zao tu, inachukulika yanapokuwa mazuri maisha yao. Wapatwapo na misukosuko, wenye dini wanakuwa wachache.

Na Mtume wao akawaambia; Hakika Mwenyezi Mungu amewachag-ulia Talut kuwa mfalme. Wakasema: Vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, naye hakupewa

231

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

wasaa wa mali?

Mantiki hii haiwahusu Waisrail tu, bali watu wengi walikuwa na wanaen-delea kuwa na mawazo kwamba cheo ni cha mwenye mali na jaha. Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-197.jpg

"Na wanapokuona hawakufanyi ila ni mzaha tu (wanasema); 'Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu aliyemtuma kuwa Mtume?' "(25:41)

Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amemteua juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa elimu na kiwiliwili.

Yaani uongozi haui kwa sababu ya mali na nasaba, bali ni kwa elimu na ikhlasi. Makusudio ya ukunjufu wa kiwiliwili ni kutokuwa na maradhi, kwa sababu maradhi yanamzuwia kiongozi kutekeleza wajibu wake.

Inasemekana kuwa Talut alikuwa mrefu zaidi kuliko mtu wa kawaida kwa kiasi cha dhiraa moja ya mkono.

MATAKWA YA MWENYEZI MUNGU NA KIONGOZI MWOVU Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni Mfalme wa wafalme, humpa ufalme amtakaye na humvua amtakaye; humtukuza amtakaye na humdhalilisha amtakaye; heri imo mikononi mwake na Yeye ni muweza juu ya kila kitu. Hapana shaka katika hilo; lakini, Yeye ambaye hekima yake imetuku-ka, ni Mwadilifu, hamdhulumu yeyote na hafanyi mambo kiholela. Vipi isiwe hivyo na hali Yeye amesema:

232

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Kaashif2-198.jpg

"Na kila kitu kwake ni kwa kipimo."(13:8)

Yaani kwa nidhamu na sababu, sio kwa sadfa au kiholela; hata mali ya haramu na utawala wa dhulma una sababu zake za kijamii.

Unaweza kuuliza: Je utawala mwovu na utajiri wa unyanga'nyi unatege-mea matakwa ya Mwenyezi Mungu?

Jibu: Hapana, Mwenyezi Mungu ameharamisha dhulma na unyanga'nyi. Na Yeye hajiingizi katika mambo ya kijamii kwa njia ya Kun fayakun (kuwa ikawa). Mwenyezi Mungu hamzuwii kwa nguvu dhalimu kutokana na dhulma yake isipokuwa anamkataza kwa kisheria na kimwongozo na anamuhad-harisha na kumtolea viaga. Atakapohalifu atamwadhibu siku ya malipo iliyo kubwa. Kama angelitaka kumzuwia angelifanya, lakini anaacha mambo yapite kwa sababu zake na desturi zake.

Huenda ikawa huu ndio mwelekeo wa kumnasibishia Mwenyezi Mungu ufalme kwa jumla. Kwa hivyo yanakuwa maana. "humpa ufalme wake amtakaye" ni kwamba Mwenyezi Mungu lau angelitaka kuuzuwia kwa nguvu ufalme kwa asiyeustahiki, angelizuwia na wala asingelifikia kwenye ufalme mtu dhalimu pamoja na kuwepo sababu zake za kikawaida.

Vyovyote iwavyo utajiri wa mtu na ufalme wake unakuja kutokana na natija yakijamii anayoishi. Ama kuunasibisha na matakwa ya Mwenyezi Mungu moja kwa moja bila ya sababu yoyote ni makosa kabisa.

Na Mtume wao akawaambia: Hakika alama ya ufalme wake ni kuwa-jia lile sanduku.

Sanduku hilo lilikuwa la Musa alilokuwa akiwekea Taurat. Mwenyezi Mungu alikuwa amelipaza mbinguni baada ya kufa Musa kwa kuwakasirikia Mayahudi kama ilivyosemwa.

233

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

Ambalo mna ndani kitulizo.

Yaani kitulizo cha nyoyo zenu ambapo sanduku lilikuwa na jambo tuku-fu la kidini kwa Wana wa Israil.

Na mabaki ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na wa Harun.

Mwenyezi Mungu hakubainisha ni mabaki gani hayo. Watu wa Musa na wa Harun ni Mitume ambao walilirithi sanduku hilo.

Wakilibeba Malaika.Yaani kwa miujiza. Basi Talut alipoondoka na jeshi, alisema: Mwenyezi Mungu atawafanyia mtihani kwa mto, basi atakayekunywa humo si pamoja nami, na asiyekunywa atakuwa pamo-ja nami; ila atakayeteka fumba kwa mkono wake.

Imepokewa kwamba Talut aliwaambia Waisrail: "Asitoke na mimi kwenye jihadi mzee, mgonjwa, aliyejenga jengo ambalo hajalimaliza, mwenye kushughulishwa na biashara, au mume aliyeoa mke ambaye hajamwingilia." wakakusanyika jamaa wenye sifa zinazotakiwa, na ulikuwa ni wakati wa kiangazi na joto kali, wakafuata njia isiyokuwa na maji. Walipolalamikia kiu, Talut aliwaambia: "Mwenyezi Mungu atawapa mtihani katika utii na uasi kwa mto mtakaoupitia. Atakaye kunywa katika mto huo si katika wafuasi wangu waumini, isipokuwa akinywa kidogo kiasi cha kiganja.

Wakanywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao.

Inasemekana idadi ya waumini ilikuwa ni 313 kama idadi ya watu wa vita vya Badr. Hakika wema walikuwa na wanaendelea kuwa ni nadra sana kupatikana.

Basi alipovuka yeye na wale walioamini pamoja naye walisema: Leo hatumwezi Jalut na jeshi lake.

Aliendelea mbele Talut pamoja na wale waliomtii baada ya kuvuka mto mpaka wakakutana na Jalut na jeshi lake. Walipoona wingi wa adui yao,

234

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili                                            2. Sura Al-Baqarah

waligawanyika makundi mawili; kundi lilisema hatumwezi Jalut na kundi likasema:

Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wafanyao subira.

Ambao wamejizatiti kwa kupigana jihadi na kujitoa mhanga kwa ajili ya maisha mema yaliyo bora ambayo ni kuishi huru katika nchi iliyo huru na kujitosheleza kwa chakula na wataalamu katika nchi iliyoendelea. Ama kuvu-milia udhalili na umasik-ini ni uchafu katika kazi ya shetani.

Na walipotoka kupambana na Jalut na jeshi lake walisema: Mola wetu, tumiminie subira na uithubutishe miguu yetu, na utusaidie juu ya watu makafiri.

Waumini walipojiona ni wachache na maadui zao ni wengi walikimbilia kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kuomba na kunyenyekea kwa ikhlas; na Mola wao akawatakabalia dua.

Na Daud akamuua Jalut. Na Mwenyezi Mungu akawapa ushindi waumini dhidi ya makafiri. Ikathibitika, kwa fadhila Zake na rehema Zake, dhana ya waliosema: "Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu."

Na Mwenyezi Mungu akampa ufalme na hekima na akamfundisha aliyoyataka. Yaani Mwenyezi Mungu alimtawalisha Daud mahali pa Talut baada ya kufa kwake. Hekima ni ishara ya Zabur. Mwenyezi Mungu anase-ma:

"...Na tukampa Daud Zabur." (4:163)

235

Kaashif2-199.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Na akamfundisha kutengeneza deraya (mavazi ya vita), Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-200.jpg

"Na tukamfundisha (Daud) kutengeneza mavazi kwa aj ili yenu ili yawahi-fadhi katika mapigano yenu ..." (21:80)

Na kama Mwenyezi Mungu asingeliwazuia watu baadhi yao kwa wengine ingaliharibika ardhi. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya viumbe vyote.

Yaani jamii yoyote ambayo ndani yake hamna utawala (serikali) basi itakuwa na vurugu. Na kwamba akili na sharia bila ya nguvu ya utekeleza-ji haiwezi kuleta amani na nidhamu. Imam Ali (a.s.) anasema "Mfalme ni msaidizi wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake... " Lakini mara ngapi wafalme wameiharibu ardhi na watu wake. Pamoja na hivyo, lakini hawa-tengenei watu wasiokuwa na mwendeshaji.

Hizo ni Aya ya Mwenyezi Mungu, tunakusomea kwa haki; na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.

Mwenyezi Mungu alimsomea Mtume wake Aya zake na Mtume akatu-somea ili tuzingatie hakika yake na tuzifanye ndizo desturi za vitendo vyetu vyote ili tuwe na maisha mema yenye utulivu.

Kaashif2-201.jpg

"Sema mimi nawaonya kwa wahyi na viziwi hawasikii mwito wanapoony-wa." (21:45)

MWISHO WA JUZUU YA PILI

236

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

="ltr">Na Mwenyezi Mungu akampa ufalme na hekima na akamfundisha aliyoyataka. Yaani Mwenyezi Mungu alimtawalisha Daud mahali pa Talut baada ya kufa kwake. Hekima ni ishara ya Zabur. Mwenyezi Mungu anase-ma:

"...Na tukampa Daud Zabur." (4:163)

235

Kaashif2-199.jpg

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

Na akamfundisha kutengeneza deraya (mavazi ya vita), Mwenyezi Mungu anasema:

Kaashif2-200.jpg

"Na tukamfundisha (Daud) kutengeneza mavazi kwa aj ili yenu ili yawahi-fadhi katika mapigano yenu ..." (21:80)

Na kama Mwenyezi Mungu asingeliwazuia watu baadhi yao kwa wengine ingaliharibika ardhi. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya viumbe vyote.

Yaani jamii yoyote ambayo ndani yake hamna utawala (serikali) basi itakuwa na vurugu. Na kwamba akili na sharia bila ya nguvu ya utekeleza-ji haiwezi kuleta amani na nidhamu. Imam Ali (a.s.) anasema "Mfalme ni msaidizi wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake... " Lakini mara ngapi wafalme wameiharibu ardhi na watu wake. Pamoja na hivyo, lakini hawa-tengenei watu wasiokuwa na mwendeshaji.

Hizo ni Aya ya Mwenyezi Mungu, tunakusomea kwa haki; na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.

Mwenyezi Mungu alimsomea Mtume wake Aya zake na Mtume akatu-somea ili tuzingatie hakika yake na tuzifanye ndizo desturi za vitendo vyetu vyote ili tuwe na maisha mema yenye utulivu.

Kaashif2-201.jpg

"Sema mimi nawaonya kwa wahyi na viziwi hawasikii mwito wanapoony-wa." (21:45)

MWISHO WA JUZUU YA PILI

236

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili

2. Sura Al-Baqarah

237