AL-KASHIF
Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

SWAHILI - JUZUU YA KWANZA TOLEO LA PILI (Vol-1)
 


YALIYOMO

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI ......i

DIBAJI iii

Kujilinda na Shetani....xxii

Shetani ni nani? ..xxiii

Hukumu.......xxiv

Mantiki ya Iblisi..xxiv

Bismillahi......xxx

AL-FATIHA (Sura ya Kwanza)....2

Aya 1-7: Kushuka...2

Majina yake ..

Kisa ....7

AL- BAQARAH (Sura ya Pili) .

Aya 1-2: Mianzo ya Baadhi ya Sura......10

Qur'an na Sayansi .......11

Aya 3-5: Wanaoamini Ghaibu ...17

Maarifa ...17

Ghaibu (yasioonekana) ......19

Dini na Elimu ..20

Aya 6-7: Ukiwaonya au usiwaonye .27

Njia ya Uislamu.....27

Mwenye kulazimiana na haki ...29

Aya 8-20: Wanafiki ......36

Ni nani Mnafiki? ....36

 

Aya 21-22: Mwabuduni Mola wenu .40

Tawi hufuata shina.......40

Tawhid....41

Maelezo..43

Aya 23-25: Leteni Sura......48

Siri ya muujiza wa Qur'an ..49

Kushinda ..50

Je Muhammad ana Muujiza mwingine zaidi ya Qur'an?....51

Aya 26-27:Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kupiga mfano wowote 54

Haya.54

Uongofu na upotevu.....55

Kuumba na kuweka sheria.61

Aya 28-29: Vipi mnamkanusha Mungu...63

Mwanadamu ni hoja.....63

Mauti na uhai mara mbili ....65

Ufufuo.....67

Yaliyo katika ardhi.68

Mbingu saba ...69

Aya 30-33: Mola aliwaambia Malaika.....71

Malaika...71

Khalifa ....72

Somo wazi ......74

Aya 34: Msujudieni Adam ..75

Aya 35-39: Adam Peponi....77

Hawa na ubavu wa Adam ..78

Mtaka yote hukosa yote .....78

Isma (kuhifadhiwa Mitume) .....79

Ahlul Bait ..83

Aya 40-46: Zikumbukeni neema zangu..85

Dhahiri ya maisha .85

Israil .86

 

Historia ya Mayahudi ...87

Muhammad na Mayahudi wa Madina....88

Aya 47-48: Wana wa Israil tena.92

Kukaririka katika Qur'an .....93

Shufaa....94

Aya 49-50: Na tulipowaokoa......97

Aya 51-53: Na tulipomwahidi....100

Aya 54-57: Musa alipowaambia watu wake.......103

Na jiueni ..103

Kumwona Mwenyezi Mungu ...107

Aya 58-59: Ingieni mji..109

Aya 60: Alipowaombea maji.....112

Ubepari na Ujamaa.....112

Aya 61: Na mliposema......116

Aya 62: Waumini na Mayahudi ......118

Aya 63-66: Tulipochukua ahadi......121

Mayahudi hawana mfano ..124

Aya 67-73: Mwenyezi Mungu anawaamrisha mchinje ngo'mbe.....129

Muhtasari wa kisa .......129

Aya 74: Kisha nyoyo zenu zikasusuwaa.....132

Tofauti ya hulka ...133

Aya 75: Je mna matumaini wataamini?......136

Aya 76-77: Wanapokutana na walioamini...138

Aya 78-79: Wako wasiojua kusoma.....139

Tafsiri na misingi na kanuni.....139

Aya 80-82: Walisema hautatugusa moto wa Jahannam...142

Mwislamu na Muumini ......144

 

Mwenye madhambi makubwa .146

Mayahudi tena .....147

Aya 83: Na tulipochukua ahadi ya kizazi cha Israil ..147

Kuwatendea wema wazazi wawili .147

Jamaa, Mayatima, Maskini......148

Kuchukulia sahihi.148

Aya 84-86: Hamtamwaga damu zenu...151

Mayahudi na Ukomunisti na Ubepari....155

Aya 87-88: Tulimpa Musa kitabu.....156

Mkweli na tapeli ...158

Aya 89-91: Kilipowafikia kitabu.160

Waliofanana na Mayahudi.163

Aya 92-96: Musa aliwajia na hoja...165

Maslahi ndio sababu ...167

Aya 97-100: Sema, anaemfanyia uadui Jibril.....168

Kuishi kwa amani.170

Aya 101: Walipojiwa na Mtume......171

Aya 102: Wakafuata yaliyofuatwa na mashetani......173

Aya 103: Lau wangeamini.178

Uchawi na hukmu yake.....178

Aya 104-105: Enyi mlioamini....181

Uzindushi.......181

Husuda na Hasidi .......182

Aya 106-107: Aya yoyote tunayoifuta....184

Kufuta....184

Aya 108-109: Je, mnataka kumuuliza Mtume.....188

Kuikhalifu haki .....190

Aya 110: Na simamisheni Swala.....191

Swala na vijana wa kisasa ......192

Aya 111-113: Na husema hataingia Peponi.......194

Ulanguzi wa Pepo.......195

 

Dini ya maslahi kwa Mayahudi na Wakristo.196

Waislamu vilevile wanakufurishana ......197

Kila mmoja avutia dini yake.....198

Aya 114: Kuzuia misikiti ya Mwenyezi Mungu....200

Hukumu za misikiti ......202

Aya 115-117: Na Mashariki na Magharibi...203

Mbunifu wa mbingu na ardhi ...207

Aya 118-120: Mbona Mungu hasemi nasi...209

Chenye kutolewa dalili ......210

Maadui wa dini na msingi wake.....213

Aya 121-123: Wakakisoma kama inavyostahiki..215

Mujtahid na Muqalid....216

Aya 124: Ahadi yangu haiwafikia waovu.....218

Uimamu na Isma..220

Aya 125-126: Na tulipoifanya nyumba..225

Mkosaji kukimbilia Haram .225

Aya 127-129: Na alipoinua Ibrahim kuta.....229

Historia ya Al-Kaaba ...229

Mashia na mababu wa Mtume ......231

Bishara ya Mahdi anayengojewa...233

Aya 130-134: Ni nani aliyejitenga na mila ya Ibrahim.......235

Haki ya mtoto kutoka kwa wazazi..237

Aya 135-138: Na wakasema kuweni Mayahudi au Manaswara.....240

Mjadala wa kimantiki...241

Aya 139-141: Sema, je mwahojiana nasi juu ya Mung.....245

Ushahidi ..249

Wenye kufanya Ikhlas.250
 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

Haki ya kunaikli imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987-427-06-5

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

Kimetafsiriwa na:

Sheikh Hasan Mwalupa

S.L.P. 88290, Mombasa / Kenya.

Email:mwalupa@hotmail.com

Kimehaririwa na:

Ustadh Abdallah Mohamed:

S.L.P. 1017, Dar-es-Salaam.

Email:info@alitrah.orq

Kupangwa katika Kompyuta na: Ukht Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: Februari 2003 Nakala: 5000

Toleo la Pili: Mei 2005 Nakala: 2000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation

P.O.Box 19701

Dar es Salaam, Tanzania

Simu:+255 22 2110640

Fax:+255 22 2113107

Email: info@alitrah.org

Website: www.alitrah.org

IX

Kaashif1-2.jpg

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

 UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilicho mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra hum na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana 'kwenda na wakati'.

Sifa kubwa ya pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo suala la madhehebu ni nyeti nchini humo,hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilmsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kiitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahibil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri,na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji

atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Ruhusa imetolewa kwa yeyote anaetaka kukichapisha upya kitabu hiki kwa sharti tu kwamba asibadilishe chochote bila ya kutujulisha, na atutumie nakala moja baada ya kukichapisha.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho, shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri,wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

Mchapishaji

XI

CHAPA YA PILI

Kutokana na maombi mengi ya wasomaji wetu wa Kiswahili, ambao ni wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu, walioko Afrika Mashariki na Kati, Uarabuni na hata nchi za Ulaya, tumeonelea kukichapisha tena Kitabu hiki ili kupunguza kiu yao kama si kuiondoa kabisa.

Tafauti iliyojitokeza katika chapa hii ya pili ni utaratibu mpya uliotumika, ambapo baada ya Aya kufasiriwa, maelezo yake yanapatikana moja kwa moja chini yake bila ya kwenda kwenye ukurasa mwingine, na utaratibu huu ndio utakaotumika katika chapa zote zitakazofuata.

Vilevile tumejaribu sana kusahihisha baadhi ya makosa ambayo kibinadamu yalikuwa yamefanywa katika toleo la kwanza.

Hatuna budi kuwashukuru wote waliotumia wakati na akili zao katika kufanikisha lengo hili adhimu, bila ya kuwasahau wafadhili na wasimamizi wetu. Mwenyezi Mungu awalipe kheri nyingi.

Vilevile tunawashukuru sana wasomaji wetu amabao waliotukosoa, hivyo kuchangia, kwa kiasi kikubwa, kuisahisha chapa hii. Na tunawaomba waendelee kufanya hivyo.

Mchapishaji

XII

DIBAJI

Sifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe. Baada ya hayo:

Mimi nimetunga mfululizo wa vitabu vidogo vidogo katika itikadi na misingi yake. Nimevitunga kulingana na mfumo na mantiki ya kizazi cha kisasa, ambacho hakiamini kitu ila kile kinachokitaka na chenye kuafikiana na malezi yake na maendeleo yake.

Alhamdulillah Mwenyezi Mungu amejaalia tawfiki na kufaulu kwa mfululizo huo na umerudiwa kuchapishwa mara nyingi.

Kimsingi ni kuwa kila kazi inayoafikiana na hekima na lengo inayolikusudia, Mwen-yezi Mungu huipa ufanisi na tawfiki. Hakika tawfiki inatokana na Mwenyezi Mungu, hakuna shaka, lakini Mwenyezi Mungu amekataa kupitisha mambo isipokuwa kwa njia yake na desturi yake.

Kuandika juu ya karatasi tu, sio sharti la kufaulu katika kitu chochote; isipokuwa kufaulu ni kumridhisha na kumpendeza msomaji kile atakachokisoma. Msomaji naye hawezi kuridhia kitabu chochote, isipokuwa kiwe kwa ajili yake na sio kwa ajili ya mwandishi. Na huko kuridhia kunampa nguvu mwandishi kuendelea. Hapo ndipo msomaji na mwandishi wanapoathiriana.

Kwa vyovyote ilivyo, kuenea kwa mfululizo huo wa vitabu vidogo vidogo kumenipa nguvu ya kutunga vitabu vikubwa na vipana; kama vile: Maalimu Falsafatil Islamiya, Alfiqhu Ala Madhahibil Khamsa, Fadhail Imam AN n.k. Mwenyezi Mungu naye akavifanyia vitabu hivi kama alivyofanyia vile vingine. Nikapata msukumo wa kutunga Fiqhul Imam Jaffar Assadiq katika juzuu sita kubwa; nacho kikawa kama vingine vilivyotangulia.

Kwa hiyo vikanipa msukumo wa kutunga kitabu kikubwa na kitukufu, Tafsirya Qufan ambayo nimeiita Tafsir Al -Kashif.

Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na nguvu Zake, vile vile kwa tawfiki Yake na fadhila Zake, imetimia juzuu hii ninayow-aletea. Ndani yake mna Sura mbili kamili za Al-Fatiha na Al-Baqara. Sijui kama uhai utaniruhusu nione natija ya lile nililojitolea mhanga, au kwamba kudra itafanya kinyume? Na kama ikitimia Tafsir Al-Kashif je, itakuwa na

XIII

mafanikio, kama ilivyokuwa kwa tungo nilizozitunga, ya kutoa matunda? Je, itazaa kitabu kingine baada yake kama ilivyokuwa kwa Fiqh?

Hayo ni maswali ambayo hapana ajuaye jawabu lake isipokuwa Mwenye tamko la kwanza na Mwenye uwezo wa juu.

"Na nafsi yoyote haijui itachuma nini kesho, wala nafsi yoyote haijui itafia ardhi gani." (31:34)

Hata hivyo kuamini kwangu ukweli huu hakunizuii kuendelea na juhudi zangu. Kwa sababu, vile vile ninaamini kwamba azma yangu ya kujitahidi ina athari kubwa katika kuhakikisha yale ninayoyataka. Imani hii inanipa msukumo wa kutoa juhudi zangu zaidi, kwa kuogopa kupoteza fursa.

Kwa hivyo basi, nitaendelea kuandika na kuwa na ndoto ya kutimia na kufaulu mpaka kufa. Yeye peke yake ndiye ambaye atasimamisha nishati yangu. Nami nitaendelea kutoa juhudi zangu muda wote ule ambao mauti yatakuwa yako mbali nami.

Natamani sana yanijie mauti huku nikiwa ninaandika kulingania kwenye haki na uadilifu. Bali mapendeleo yangu ni kuingia peponi ili niweze kusoma na kuandika, nikiwa sina mawazo mengine yoyote ya kunishughulishi, nitakuwa sina mawazo ya kushughulikia familia na kadhalika.

Mara nyingi sana hunijia swali hili: Kama nikiingia peponi nitakuwa mvivu? Je, itawezekana nisome na niandike? Halafu hujijibu: Ndio, huko kuna yanayofurahiwa na macho na yanayopendwa na nyoyo; hata kama moyo unapenda kusoma na kuandika. Kisha linanijia swali jingine: Nimwandikie nani na watu wote wa peponi ni wakamilifu?

Samahani kwa kuiachia kalamu iandike hayo; au kwa usahihi zaidi, kuiacha dhati yangu kujieleza. Kwa kweli mimi ni mtu wa kawaida tu, ambaye ni vigumu kumtenganisha na dhati yake na ambaye inakuwa vigumu kujizuia kuyaelezea yaliyo katika pango la moyo wake, wakati inapopatikana fursa ya kujieleza.

Kizazi cha kisasa

Kila kitu kina sababu ya kutokea kwake, ni sawa kiwe ni cha kimaumbile, kama vile tufani na tetemeko; au cha kijamii, kama vile ujinga na ufukara;

xiv

au kiwe ni katika mambo ya moyoni, kama vile imani na kufuru. Hakuna kitu chochote kinachotokea kwa sadfa bila ya sababu yoyote, au bila ya mipangilio yoyote. Nitayafafanua maelezo haya kwa swali na jibu lifuatalo:

Kwa nini kizazi cha sasa hakijishughulishi na misimamo ya kidini kama kilivyokuwa kizazi kilichopita? Vijana wengi wa kileo wameachana na ibada na mazingira ya kidini; bali imekuwa uzito sana kwao kusikiliza mawaidha na nasaha za kidini; hata msimamo mzuri wa kiutu - kama udugu, usawa, amani, kusaidiana, ukweli na uadilifu - haumo katika nyoyo zao kabisa. Inapotokea kuuzungumzia basi wanauzungumzia katika ndimi zao tu, sio katika nyoyo zao; ila ikiwa kuna manufaa ya kibinafsi.

Jibu ni kuwa, mataifa ya Kiislamu ya Kiarabu na yasiyokuwa ya Kiarabu yalik-uwa hayategemei misingi yoyote wala misimamo yoyote ila ile iliyotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), sio iliyotokana na ujamaa au ubepari, wala demokrasia au ubaguzi. Hakuna kitu chochote walichotegemea isipokuwa wahyi wa Mwenyezi Mungu. Humo ndimo mlimochukuliwa misingi ya itikadi, adabu, tabia na njia za taaluma. Vile vile kanuni na hukumu zinazotumiwa katika mahakama na mambo mengine ya kibinafsi na ya kijamii, yalitoka humo.

Kwa hiyo, ndio maana yakawa mafundi-sho ya dini yako wazi katika bongo za watu wengi; wakawa wanayajua yanayotakiwa na sharia na yanayokatazwa. Yule aliyekuwa akiishi maisha ya dini alikuwa ndio tegemeo la wote na ndio mahali pa amana zao. Na, yule mbaye hana dini hakuaminiwa au kutegemewa katika jambo lolote. Yaani misimamo ya kijamii ilikuwa ni misimamo ya kidini. Yeyote anayetoka katika msimamo huo, anakuwa ametoka katika usalama.

Kisha siku zikapita, yakatokea mapinduzi kutoka nchi za Kimagharibi, wakavamia miji ya Kiislamu. Kwanza kabisa walielekea kwenye sharia ya Quf an, wakaiondoa katika mahakama. Badala yake wakaleta kanuni za Kifaransa na za Kiingereza. Wakaondoa mafunzo ya kidini katika taaluma. Wakaanzisha majumba ya ufuska; kama vile mabaa, vilabu vya usiku pamoja na kila kitu ambacho waliona kingeweza kuondoa itikadi na maadili.

Kwa hiyo athari za Quf an na Sunna za Mtume zikafichika katika maisha ya kijamii. Hata lugha ya Kiarabu pia ilipatwa na kile kilichopatwa na dini. Ndio kikawa kizazi hiki hakijishughulishi na dini wala maadili mema. Hiyo ni natija ya ufisadi waliokulia na kulelewa nao. Na kama kawaida, hali hiyo ilienea.

xv

Kwa hiyo ni makosa kukitenga kizazi na jamii yake na malezi yake. Hawakukosea wale waliosema: "Panapofuka moshi hapakosi moto"

Dawa

Unaweza kuniuliza: Umeelezea ugonjwa, sasa dawa yake ni nini?

Kwa kweli jibu la swali hili si la kujibiwa na msomi mmoja tu; hapana budi zikutane akili kubwa zenye ikhlas. Kwa sababu, tabia na ada zikiingia katika kizazi na zikabaki kwa muda mrefu, huwa zimemea. kazi rahisi kuzing'oa. Kwa vile zinafanya kazi katika nafsi, kama zinavyofanya kazi athari za kisayansi. Kuzibadilisha kunahitaji juhudi najihadi ndefu, zenye mashaka; kama juhudi aliyoifanya Mtume (s.a.w.) katika kubadilisha ada za kijahiliya na itikadi zao. Kuna Hadith zinazoonyesha hayo; kama ile inayosema:

"Uislamu ulianza katika hali ya ugeni na utarudi katika hali ya ugeni, kama ulivyoanza."

Kwa hivyo, hauwezi kuepukana na ugeni wake na kutulia katika kurudi kwake, isipokuwa kwa kiongozi kama Mtume Muhammad (s.a.w.) na Masahaba kama Wahajiri na Ansari

Mwenyezi Mungu hashindwi kufanya Quf an, sharia yake na maadili yake kuwa ndiyo inayotawala leo. Lakini ni juu yetu kufanya juhudi kadiri ya uwezo wetu, wala tusingoje muujiza wa mbinguni.

Na kazi ambayo tunaiweza kuifanya, nionavyo mimi, ni: Kwanza, tuitilie mkazo dini katika mashule, hasa Quf an, kuisoma, kuihifadhi na kuifasiri. Kwani hiyo ndiyo msingi. Kama wasimamizi wakikataa kufundisha dini katika mashule na watakataa tu,basi ni juu yetu kuanzisha Shule za kibinafsi kwa ajili ya lengo hilo tu. Tuanzishe Shule hizi kutokana na mamillioni yanayotolewa sabili kwa wanavyuoni wakubwa na wengine Wala sijui kama kuna kazi nyingine bora zaidi ya kutumia pesa hizo kuliko kufufua na kuyaeneza mafundisho ya dini.

Pili, kila mmoja katika watu wa dini atekeleza wajibu wake kwa ikhlasi, baada ya kujiandaa kuwa kiongozi mwenye mwamko, anayejua namna ya kuwakinaisha vijana, kuwa dini ndio chimbuko la msimamo ulio sawa, ambalo litawapa maisha mema zaidi.

Tatu, kuufafanua uhakika wa dini, kuufanya mwepesi kufahamika na kuutangaza kwa vitabu, hotuba, makala na matoleo kadhaa. Tumthibitishie mjinga na mwenye shaka kuwa Uislamu kwa sharia na maadili yake, unatosheleza kabisa mahitaji ya mwanadamu ya kiroho na

xvi

ya kimaada; na unaweza kutatua matatizo yake; na kwamba una lengo la kumfanya afaulu katika dunia yake na akhera yake.

Msomaji atapata dalili ya hayo katika tafsiri hii ambayo inaunganisha dini na maisha, na ambayo imeshughulikia zaidi upande wa ubinadamu kuliko kushughulikia ufasaha wa maneno.

Mfasiri

Tafsiri, kilugha, ina maana ya kubainisha. Na, katika istilahi ina maana ya elimu inayotafiti maana ya maneno ya Quf an na yanavyohusika.

Ili mfasiri awe na ubainifu katika ambayo yanamstahiki Mwenyezi Mungu, hana budi kuwa na maandalizi yafuatayo:-

Elimu za kiarabu kwa nyanja zake zote, elimu ya Fiqh na Misingi (usul) yake, Hadith na elimu ya Tawhid. Na miongoni mwa maandalizi hayo, kama wanavyoona wengine, ni elimu ya Tajwid na elimu ya kisomo cha Qufan.

Kuna kitu kingine anachokihitajia mfasiri ambacho ni muhimu na kikubwa kuliko chochote katika walivyovitaja wafasiri katika utangulizi wa tafsiri zao. Kwa sababu, ndio msingi wa kwanza wa kufahamu maneno yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.); Wala sijamwona yeyote aliiyekielezea.

Kitu chenyewe ni kuwa, maana ya Qufan hawezi kuyafahamu na hatayafahamu kwa uhakika wake na kujua ukubwa wake, isipokuwa yule mwenye kuyahisi ndani ya moyo na akili yake. Pia imani yake ichanganyike na maana ya Qur'an pamoja na damu yake na nyama yake.

Hiyo ndiyo siri iliyo katika kauli ya Amirul Muminin, Ali (a.s.):

"Hiyo ni Qur'an iliyonyamaza na mimi ni Qur'an inayotamka."

Vile vile imenijia yakini wakati nikiendelea na tafsiri kwamba mfasiri yeyote asiyeleta fikra mpya, ijapokuwa moja tu, katika tafsiri yake yote, basi atakuwa hana akili ya mwamko, isipokuwa ana akili ya kusoma tu. Anamchorea mwingine yale anayoyasoma, kama inavyoonekana picha ya kitu katika kioo vile ilivyo kwa rangi na umbo. Hiyo ni kwa sababu maana ya Qur'an yako ndani sana kiasi ambacho yeyote hawezi kuyafikia kwa vyovyote vile atakavyokuwa na elimu na fahamu; isipokuwa atagundua yale ambayo maarifa yake yanayamudu. Atakaposimama mfasiri aliyetangulia pale alipofikia, kisha akaja mwingine akafuata nyayo zake bila ya kuzidisha chochote ijapokuwa

xvii

hatua moja tu, basi atakuwa ni kama kipofu kamili anayetegemea fimbo tu; anapoikosa anabakia pale alipo.

Nimepata rai nyingi na itikadi za hapa na pale wakati nilipokuwa nafasiri. Kwa kweli tafsiri imesahihisha fikra zangu nyingi za zamani. Nimekuwa na yakini kwamba hapana imani bila ya takua pepo haipati isipokuwa mwenye kujitahidi na akajitoa mhanga katika njia ya haki na kwamba hakuna msingi wowote katika misingi ya Kiislamu au tawi lolote katika matawi ya Kiislamu - katika kumwamini Mwenyezi Mungu au hukumu ndogo katika sharia - isipokuwa inafungamana na maisha.

Vile vile nimeyakinisha kuwa wengi wa wale ambao hawaujui Uislamu na makusudio yake ni wale wanaojinaki na Uislamu; na mengi ambayo atayakuta msomaji wakati wa kupekuwa kurasa za Tafsir hii, nimeyahusisha hayo katika vifungu mbali kwa vielelezo vyake.

Kwa kweli sijui kama kuna kazi ngumu na nzito kama kufasiri maneno ya Mwenyezi Mungu. Sio kazi rahisi kueleza matakwa yake Mwenyezi Mungu. Lakini jambo la kutia moyo, nikuwa mfasiri hufasiri maana ya Qur'an na makusudio yake kulingana na alivyofahamu yeye, sio kulingana na ilivyo hasa; sawa na mujtahid wa Fiqh ambaye hulipwa thawabu akifutu sawa na husamehewa akikosea, bali hupata thawabu, hata akikosea, kwa sababu ya juhudi yake na kutokuwa mvivu.

Mwito wa Qur'an

Mwenye kufuatilia Aya za Qur'an tukufu, akazingatia maana yake, atazikuta zina mfungamano mmoja tu katika kanuni zake zote na misingi yake. Vile vile katika sura zake na Aya zake. Mfungamano huu ni ule mwito wa kuwapa watu maisha mema yenye uadilifu, ustawi na amani.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Enyi mlioamini mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita katika yale yatakayowapa uhai."

(8:24)

Mwito wa Mwenyezi Mungu na Mtume kwenye maisha, una mfumo wake na nguzo zake maalum zinazousimamia

Mwenyezi Mungu ameupanga mfumo wa kulingania kwa kumwambia Mtume wake mtukufu (s.a.w.):

xviii

"Waite kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora."

(16:125)

Makusudio ya hekima na mawaidha mazuri ni kuuambia moyo na akili, na kuuonyesha viumbe vya aina yake na vya ajabu. Mwenyezi Mungu anasema:

"Tutawaonyesha ishara zetu zilizo katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli."

(41:53)

Vile vile kuwahadharisha wapinzani na mwisho mbaya, na huwaonyesha mfano wa umma uliotangulia; kama alivyofanya Nabii Shuaib aliposema:

"Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusiwapelekee kuwasibu kama yaliyowasibu watu wa Nuh au watu wa Hud au watu wa Swaleh. Na watu wa Lut si mbali nanyi."

(11:89)

Wakiendelea na inadi yao, na ikiwa hakuna dalili zaidi za kutoa, basi achana nao. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na kama wakikuhoji, basi sema nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu na walionifuata...."

(3:20)

"... Hakika ni juu yako kufikisha na ni juu yetu hisabu."

Ama nguzo za mwito wa maisha mema, ni hizi zifuatazo:-

(13:40)

XIX

1.        Hakika mtu hakupatikana kibahati tu, bila ya makusudio yoyote. "Na Mwenyezi Mungu amewaumba kisha atawafisha."

(16:70)

2.        Mwenyezi Mungu hakumwacha mtu bure bure tu, ajihukumilie kimapenzi yake, bali amemuwekea njia ya sawasawa, ambayo haijuzu kuikengeuka: Mwenyezi Mungu anasema:

"Hivi anadhani kuwa mtu ataachwa bure bure tu!"

(75:36)

"Naapa kwa Mola wako tutawauliza wote yale waliyokuwa wakiyatenda."

(15: 92-93)

3. Amani na kuchunga nidhamu. Mwenye kuiharibu na akafanya uharibifu katika nchi ataadhibiwa adhabu kali duniani, na katika akhera atakua na adhabu. Mwenyezi Mungu anasema:

4.

"Hakika malipo ya wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya uovu katika nchi, ni kuua-wa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao kwa mabadilisho au kuhamishwa katika nchi; hii ndio fedheha yao katika dunia na akhera watapata adhabu kubwa."

(5:33)

Amani na nidhamu haiwezi kuwako na wala haitakuwako ikiwa kila mtu hatachunga heshima yake na uaminifu wake. Kwa sababu jamii njema, kwa mujibu wa Qur'an, ni ile isiyokuwa na mbegu ya ufisadi hata moja. Mwenyezi Mungu anasema:

xx

5.

"Mwenye kumuua mtu bila ya yeye kuua mtu au kufanya ufisadi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote; na mwenye kumwacha hai basi ni kama amewaacha hai watu wote."

(5:32)

Hiyo ni kwamba hakika ya utu inakuwa kwa kila mmoja. Mwenye kumfanyia ubaya mmoja, atakuwa amewafanyia ubaya wote na mwenye kumfanyia wema mmoja, atakuwa amewafanyia wema wote.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Mwenye kuua mtu bila ya yeye kumuua mwingine au kufanya ufisadi katika nchi", ni kuonesha kuwa kila mtu ana heshima yake ya kiutu, mpaka aivunje mwenyewe kwa kufanya kosa litakalovunja heshima yake hiyo.

Utangamano kati ya watu unakuwa juu ya misingi ya kuchunga heshima kwa kila mtu bila ya kubagua kati ya mwanamume au mwanamke, mweusi au mweupe na tajiri au maskini, katika mila yoyote aliyo nayo. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameuthibitisha ubainifu huu kwa ibara fupi:

'Hakika tumemtukuza mwanaadamu..."

(17:70)

Mwenye kuidharau heshima aliyopewa na Mwenyezi Mungu, atakuwa amemdharau Mwenyezi Mungu na sharia yake.

6. Kuamini Mwenyezi Mungu, Utume wa Muhammad (s.a.w.), siku ya mwisho na mengineyo, ni katika misingi ya dini na matawi yake, wala sio kuwa ni bendera ya dini inayopeperushwa na Qur'an. Kila msingi katika misingi ya Uislamu na kila hukumu katika hukumu zake, zina matunda na amali yenye manufaa. Mwenyezi Mungu amekukutanisha kumwamini yeye na amali njema katika Aya kadhaa. Ama kuamini Utume wa Muhammad

XXI

(s.a.w.) ni kuamini utu na wema wake. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na hatukukutuma isipokuwa uwe rehema kwa walimwengu."

(21: 107)

Ama kuingia peponi, kunafungamana zaidi na jihadi na amali njema katika maisha haya. Mwenyezi Mungu anasema:

"Je mnadhani mtaingia peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigania jihadi dini ya Mwenyezi Mungu miongoni mwenu na kuwajua waliofanya subira?"

(3:142)

"Enyi ambao mmeamini mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita katika yale yatakayowapa uhai..."

(8:24)

Hii ni dalili wazi kwamba mwito wowote ambao hauna muungano wowote wa maisha, basi sio wa dini. Na mwenye kuunasibisha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atakuwa ameizulia uwongo dini.

Kwa misingi hii, ndipo nikajaribu kufasiri Aya za Qur'an tukufu na kuifafanua kwa ufafanuzi ufuatao:-

Njia

Makusudio ya njia hapa ni udhibiti anaokwenda nao mtungaji, bila ya kukengeuka. Kwani kazi yoyote ambayo haina njia ni shaghalabaghala tu, itakayoongozwa na migongano.

Njia niliyofuata katika tafsiri hii, inafungamana na kudhibiti mambo yafuatayo:-

xxii

1.        Nimeitazama Qur'an kwa mtazamo kuwa hakika yake na sera yake ni kitabu cha dini na uongozi, kutengeneza na kuweka sharia inayolenga kuwapa watu wote maisha yaliyo katika misingi iliyosalimika, inayoongozwa na amani na uadilifu na iliyojaa furaha na wema. Hayo nimetangulia kuyaeleza.

2.        Baadhi ya wafasiri wa kwanza walijishughulisha zaidi na lugha, wakarefusha maneno katika kubainisha siri ya matamko na wakaweka maswali; mfano: Kwa nini imetajwa wau na wala isitajwe fa au kwa nini amesema mafasiki na wala asiseme madhalimu, n.k. Kisha wakajibu majibu yasiyo na umuhimu. Mimi sikuingilia jambo hili.

Ikiwa kila tafsiri imepondokea upande fulani, basi mimi nimepondokea kwenye namna ya kumkinaisha msomaji kwamba dini kwa misingi yake yote na matawi yake pamoja na mafunzo yake mengine, ina lengo la kumpatia mtu heri na heshima na kwamba mwenye kukengeuka lengo hili, atakuwa ameikengeuka hakika ya dini na njia ya maisha yaliyonyooka.

Ili kuweza kulifikia lengo langu hili, nimejaribu kwa juhudi zangu zote kuleta ufafanuzi mwepesi na ulio wazi, atakaoweza kuufahamu msomaji kwa kiwango chochote atakachokuwa.

Kwa vile zama walizoishi wafasiri wa zamani hazikuwa zama za kudharauliwa dini, sharia yake na misimamo yake kama ilivyo sasa, ndio maana wafasiri hao walijishughulisha zaidi na fasihi kuliko kumkinaisha msomaji kuwa dini ni msimamo ulio sawa sawa. Kwa hiyo lugha ya tafsiri ya zama hizo sio ya zama hizi.

Hakika tafsiri ni fani kamili inayokwenda na wakati. Ndio maana mimi nimeielekeza tafsiri yangu katika kukinaisha kizazi cha kisasa kuwa dini inakwenda sambamba na maisha.

Lakini hiyo haimaanishi kuwa mimi nimeghafilika na upande wenye kunufaisha, ambao umeonyeshwa na wafasiri wakubwa, la! Isipokuwa nimeufupisha upande huo na kuuonesha kwa uwazi zaidi, hata nimeonyesha rai yangu ndani yake hasa katika masuala nyeti ya kifalsafa; mfano: Kulazimishwa watu au kuwa na hiyari, uongofu na upotevu, Uimamu na Isma ya Mitume. Pia shafaa, mwenye madhambi makubwa, hisabu ya kaburi na mengineyo.

Vilevile mara nyingi nimehusisha kifungu maalum cha lugha, kwa ajili ya kutafsiri misamiati ambayo si maarufu. Mara nyingine nimeweka kifungu kingine cha irabu kwa ajili ya kubainisha hukumu za Kinahw (sarufi) kwa

xxiii

tamko lenye utatanishi, ijapokuwa wafasiri wa kisasa hawakujishughulisha nalo, lakini mimi nimeangalia matakwa ya baadhi ya wasomaji wa nahw, ingawaje ni wachache.

Ama usanii wa methali za maneno, elimu ya usemaji, ulinganishaji na uunganishaji, nimemwachia Zamakhshari katika Kash-Shaf, Al-Andalusi katika Bahrul-Muhit, na wengineo.

Ili kuthibitisha kuwa lugha ya tafsiri inatofautiana kulingana na wakati, ninataja maneno ya Muhyiddin Ibn El-Arabi katika kitabu Futuhatil Makkiyya, Juzuu ya nne, mlango wa Hadhratul-hikma, kuhusu kuisoma Qur'an, ambayo yana maana ya undani kabisa na yanayoafikiana na nadharia za kisasa; hasa ile nadharia ya Uwiano (Relativity) ya Einstein, ambaye anazingatia kuwa wakati na mahali ndivyo vinavyosimamisha kitu. Anasema huyo Ibnul Arabi:

"Msomaji anasoma alichokihifadhi katika Qur'an, anakuta katika kila kisomo maana ambayo hakuyakuta katika kisomo cha kwanza pamoja na kuwa herufi zinazosomwa ni zile zile, isipokuwa matukio na hali ndivyo vipya. Kwa hivyo hapana budi maana hayo yawe mapya. Kwa sababu, wakati wa kusoma kwa kwanza sio kwa pili."

Hapa aliposema, "hapana budi kuwa maana hayo yawe mapya, maana yake ni kuwa, kitu kinakuwa kipya kwa kuwa kipya wakati ule."

Amesema kweli mwanafalsafa Rasil, aliposema: "Hakika watu wa zamani waligundua nadharia zilizothibitishwa na elimu kulingana na fikra na jitahadi zao; na zilikuwa ni rai za sawa; ambapo katika zama zao hizo hakukuwa na kitu zaidi ya jitihadi ya maoni."

3. Nimeangalia hadith zinazohusu Israil ambazo zimekuja katika baadhi ya tafsiri, nikazikuta ni vigano tu. Kitu kinachofahamisha zaidi uwongo wake, ni kuzinasibisha kwa Waisrail.

Vilevile nimejipurukusha na riwaya zilizoelezea sababu za kushuka, isipokuwa chache tu. Kwa sababu, wanachuoni hawakudhibiti mategemezo yake na kupambanua kati ya dhaifu na sahihi; kama walivyofanya kwa riwaya za hukumu. Hata hizo nazo hawakuangalia sana zile za Sunna na kuchunguza kwa makini, isipokuwa katika wajib na haramu. Bali wameweka utafiti mbali katika vitabu vya Usuul.

Vilevile sikujishughulisha na pia kumshughulisha msomaji, kutaja kufungamana au kunasibiana kati ya Aya na Aya nyingine; kama walivyofanya wafasiri wengine. Kwa sababu, Qur'an haikufunuliwa kwa Mtume (s.a.w.) kwa mpigo, bali iliteremshwa kwa nyakati maalum, mara

xxiv

nyingine kwa kufuatana na mara nyingine kwa kuchelewa; wala sura au Aya hazikupangwa kama tunavyozisoma hivi sasa.

Qur'an, tuliyo nayo hivi sasa, ilipangwa tangu siku za Mtume (S.A.W). Mpango huu haukufuata utaratibu wa kushuka sura, wala kuwa sura ni ya Makka au Madina; vile vile hakuna tarehe ya kushuka Aya. Hivyo tunakuta Sura ya Baqarah, Al-lmran na Maida ziko mwanzo wa msahafu baada ya Sura ya Fatiha, pamoja na kuwa zimeshuka Madina. Mara nyingine tunakuta sura iliyoshuka Madina ina Aya zilizoshuka Makka.

Mwenye tafsir ya Al-Manar, akimnukuu mwalimu wake, Sheikh Muhammad Abduh, katika Juzu ya pili, ukurasa 451, chapa ya pili, anasema: "Qur'an sio kitabu cha fani cha kuwa na mlango mahsusi na makusudio fulani; isipokuwa ni kitabu cha uongozi na waadhi, inamgurisha mtu kutoka hili mpaka lile.

Na mara kwa mara inarudia kwenye utafiti wa kusudio moja, kwa ibara nyingine na namna nyingine ya ubainifu, ili asichoke mwenye kupewa mawaidha na kuongozwa."

4. Kabla ya kitu chochote nimetegemea, katika kutafsiri Aya na kubainisha makusudio, Hadith zilizothibiti kwa Mtume (s.a.w.). Kwa sababu, ndizo zinazofasiri Qur'an na ni njia ya kujua maarifa yake.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Alichowapa Mtume jiepusheni nacho."

kipokeeni na alichowakataza

(59:7)

Ikiwa hakuna hadith, basi ninategemea dhahiri ya Aya na mpangilio wake. Kwa vile, msemaji mwenye hekima, ubainifu wake hutegemea yale anayoyafahamu yule anayemwambia kutokana na dalili zilizo wazi; kama ambavyo mwenye kuambiwa anachukua dhahiri hiyo tu, mpaka pale itakapothibitika kinyume.

Kama ikija Aya nyingine katika maana ya Aya ya kwanza na ikawa ina ubainifu na kuwa wazi zaidi, basi ninazitaja pamoja ili zifafanuke zaidi. Kwa vile chimbuko la Qur'an ni moja, inajitamkia yenyewe na kujiletea ushahidi.

XXV

Kama ikipingana dhahiri ya tamko pamoja na hukumu ya kiakili, basi ninaitafsiri kwa namna ambayo inaafikiana na akili, kwa kuizingatia hiyo akili kuwa ni dalili na hoja juu ya amali iliyo wajibu.

Ikiwa dhahiri ya tamko inapingana na Ijmai ya Waislamu katika nyakati zote kwenye masuala ya Kifiqh, basi huchukua Ijmai: kama kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Mnapowekeana deni kwa muda uliowekwa, basi iandikeni."

(2:282)

Ambapo neno iandikeni limefahamisha wajibu, lakini Ijmai imesimamia juu ya kuwa kuandika deni ni sunna. Kwa hiyo hapo nimechukua kuwa ni suna na sio wajibu.

Ama kauli za wafasiri, sikuzifanya ni hoja mkataa na dalili peke yake; isipokuwa kutilia nguvu njia mojawapo, ikiwa tamko linachukua maana nyingi.

Hata hivyo wafasiri wamefanya juhudi kubwa sana za kufafanua maana ya Qur'an na siri zake, na kuonyesha lugha inayofahamika na ngeni. Wamekitafsiri kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa juhudi ambayo haijapatikana mfano wake katika umma wa zamani au wa sasa.

Kwa hakika kuna wafasiri wakubwa na waliobobea katika fani mbali mbali za elimu ya Qur'an ambao walikuwa ni watu muhimu sana katika historia ya Kiislam. Kwa hiyo ingawaje kauli za mabingwa hao si hoja, kama kauli ya Masum, lakini zinaweza kuwa ni mwangaza juu ya maana yanayokusudiwa na kuuandaa njia ya kufahamu.

Makosa ya Chapa

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa Swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misrya mwaka 1935, Sura ya (2:146) Imeandikwa La

xxvi

Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya pili, Sura (2:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawmal qiyama". Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu Jabal amil 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: "Hatta idha balagha arbai'na sanah badala ya: Hatta idha balagha ashuddahu arbai'na sanah."

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: 'Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (AS): "Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu". Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyoyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani. (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH

XXVII

Najilinda kwa Mwenyezi Mungu na Shetani ALIYEFUKUZWA

Kujilinda na Shetani

Mwenyezi Mungu (S.W.T.) anasema:

"Unaposoma Qur'an jilinde kwa Mwenyezi Mungu na shetani aliyefukuzwa."

(16:98)

Amesema tena:

"Na kama wasiwasi wa shetani ukikusumbua basi jilinde kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni Mwenye kusikia mjuzi."

(7:200)

Maana ya kujilinda

Kujilinda huku kwa Mungu hakutoshi kwa kusema: Au'dhubillahi minash-shaytwanir rajim" tu, isipokuwa linalotakikana ni kumwamini Mwenyezi Mungu, kumtegemea na kumwogopa; hata kama mtu hakutamka hivyo.

Mwenye kutenda umuhimu wowote kwa kuitakidi kuwa nyuma yake kuna nguvu inayomsaidia kutenda amali njema; mwenye kupondokea kufanya haramu, lakini twaa ya Mwenyezi Mungu ikamzuia na mwenye kuchanganyikiwa akaifanya sharia ndio kipimo, wote hao ni katika wale wanaojilinda kweli kwa Mwenyezi Mungu na shetani aliyefukuzwa.

Hakuna kitu kinachofafanua zaidi 'kujilinda' kuliko mtu kumtegemea Muumba wake, kuwa na yakini kwamba mja mwingine hawezi kumdhuru wala kumnufaisha na kwamba kabisa hakuna kitu kitakachozidi hifadhi ya Mwenyezi Mungu.

Majaribio yametufundisha kwamba mwenye kumtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu, amedhalilika; na mwenye kutaka uokovu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ameruka utupu; na matarajio hayawezi kupatikana kwa kuwakimbilia viongozi, chama, wala kwenye hazina za matajiri, bali Mwenyezi Mungu tu peke yake ambaye hana mshirika.

XXVIII

Shetani ni nani?

Sisi hatujamwona Shetani ana kwa ana lakini ametolewa habari zake na wahyi. Kwa hivyo ni wajibu kusadiki kuwa yupo, na si wajibu kujua alivyo.

Mwenyezi Mungu amemtaja katika Qur'an kwa sifa ya kupoteza watu na kuwaepusha na twaa ya Mwenyezi Mungu na amali ya heri. Kwa hiyo kila wazo linalokupitia moyoni au mtu anayejaribu kukuhadaa kukuweka mbali na twaa na kheri ya Mwenyezi Mungu, kukuhadaa kuasi sharia na kuuvika uovu na ubatilifu nguo ya uongofu, basi huyo ni Shetani wa hisia au wa kimaana.

Jambo la kushangaza ni kuwa "mashetani watu" nao wanaomba walindwe na shetani, hali wao wenyewe ni mashetani lakini hawajijui. Ni sawa na mtu anayesoma Qur'an na huku inamlaani mwenyewe; kama ilivyoelezwa katika hadith.

Qur'an inamlaani mwongo aliye haini. Kwa hivyo huyo mwongo anapoisoma huwa amejitamkia laana yeye mwenyewe.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Hao malipo yao ni kushukiwa na laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote."

(3:87)

Hukumu

Kusoma Au'dhu... kabla ya kusoma Qur'an ni sunna, wala si wajib; ni kama vile kuosha mikono na kusoma Bismillah kabla ya kula. Lau hiyo Au'dhubillahi ingelikuwa ni wajibu ingeliwajibishwa katika swala, mahali pa fatiha na Sura. Wanavyuoni wote wamesema kuwa si wajib. Mwenye Miftaahul-Karaama amesema:"Hawakuhitalifiana katika hilo isipokuwa Ibn al-Junaid ambaye mafakihi wamemwita: 'aliyejitenga'."

Mantiki ya Iblis

Kwa mnasaba wa Au'dhu (kujilinda na Shetani) tutadokeza vigano alivyonasibishwa navyo Ibilisi. Kwa sababu ingawaje ni vigano, lakini vina picha wazi kwa watu wengi wa zama hizi; hasa wale wanaotaka kujinufaisha bila ya kuangalia maslahi ya wengine, kwa kufanya mbinu

XXIX

za kujaribu kila njia ya kucheza na maneno na kuficha haki. Tutayaonyesha hayo kwa matamkotu; bila ya kudhihirisha madhumuni.

Inasemekana kuwa Ibilisi alimwambia Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Haijuzu kuniadhibu kwa kuacha kumsujudia Adam." Mwenyezi Mungu akamuuliza, "Kwa nini?"

Akajibu: "Kama ungelitaka hasa nimsujudie ungenifanyisha kwa nguvu."

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamuuliza: "Wakati gani ulijua kwamba sikukutaka umsujudie Adam? Je ulilijua hilo baada ya kukuamrisha na kuasi amri yangu? Au kabla ya kukuamrisha kusujudu?"

Akasema: "Ni baada ya kuniamrisha".

Mwenyezi Mungu (s.w.t.). akasema: "Basi umejishinda. Kwa sababu ulihalifu kabla ya kujua kuwa Mimi niliyataka yale uliyoacha kuyafanya. Zaidi ya hayo kama ningekufanyisha kwa nguvu, basi isingelikuwa amri."

Utaona katika mantiki ya Ibilisi sura iliyo wazi kwamba Mwenyezi Mungu hawafanyishi wenye kuwajibikiwa na sharia kama vile anavyofanya katika kuumba kwa njia ya "kun fayakun" (kuwa, ikawa). Isipokuwa anawafanyisha kwa njia ya kuongoza matakwa ya mtu kwa sharia inayoelezwa ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Inasemekana kuwa siku moja Ibilisi alikutana na Mtume Muhammad (s.a.w.) akamwambia: "Hakika Mwenyezi Mungu amekusifu kwa jina la kiongozi, na mimi amenisifu kwa jina la mpotezaji. Lakini uongozi na upotezaji vyote vinatokana na Yeye, kwa hiyo wewe na mimi hatuna chochote."

Mtume akasema: "Hapana! Mimi hubainisha batili na kuikataza na kuitolea kiaga kibaya; hali wewe una unafiki na hadaa ya ubatilifu; na mtu ana uwezo, upambanuzi na hiyari. Kwa hivyo mwenye kufanya hiyari nzuri (akaongoka) anajifanyia mwenyewe, na mwenye kuifanya mbaya (akapotea) pia anajifanyia mwenyewe."

Imesemekana kuwa Ibilisi alimwendea Nabii Isa (a.s.) akamuuliza: "Si unadai kuwa wewe una daraja kubwa kwa Mungu? Basi hebu jitupe kutoka juu tuone, je atakuokoa?"

Masihi akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayemjaribu mja wake na sio mja kumjaribu Mola wake."

xxx

Imesemekana kuwa baada ya gharika na kukauka maji, Ibilisi alimwendea Nuh (a.s.) akamwambia: "Hakika wewe umenisaidia, kwa hiyo ninataka kukulipa."

Nuh (a.s.): Akasema: "Mungu apishe mbali! kumsaidia na kiumbe kama wewe."

Akasema Ibilisi: "Ndio hivyo."

Nuh (a.s.): Akasema "kwa nimekusaidia nini?

Akasema Ibilisi: "Umewaapiza watu wako ili waangamie wakaangamia, na nilikuwa nikijishughulisha usiku na mchana kuwapoteza kwa muda huo. Baada ya kuaangamizwa watu wako, sina kazi ya kufanya; sipati wa kumpoteza."

Nuh (a.s.) akasema: "Utanilipa nini?

Akasema: "Ninakunasihi usikasirike, kwa sababu hasira ya mtu inarahisisha kunifuata. Wala usihukumu kati ya watu wawili. Kama ukifanya hivyo, basi mimi nitakuwa wa tatu wenu. Wala usikae faragha na mwanamke kwani mimi hukuvutia kwake na yeye humvutia kwako."

Kutokana na mantiki hii ya kishetani, inaonyesha kuwa Shetani ndiye mchochezi, na kwamba yeye huzipongeza silaha zenye kuangamiza.

Inasemekana kwamba Mtume (s.a.w.) na sahaba zake walimpitia mtu mmoja akirukuu na kusujudu kwa unyeyekevu. Wakasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni uzuri ulioje wa swala ya mja huyu!" Mtume akasema: "Huyu ndiye aliyemtoa baba yenu peponi."

Lengo la hekaya hii ni kuwa haifai mtu kughurika na kuhadaika kwa zuhudi na ibada ya dhahiri.

Inasemekana kuwa Nabii Musa (a.s.) alikuwa akienda kuzungumza na Mola wake, ikatokea kukutana na Ibilisi, akamwambia "Unakwenda wapi ewe uliyezungumza na Mwenyezi Mungu?"

Nabii Musa (a.s.) akasema: "Ninakwenda kwa Mola wangu kupokea maneno kutoka kwake na niko tayari kukuombea akusamehe kama utaniahidi kuung'oa upotevu wako."

Ibilisi akasema: "Mimi sina haja ya kuombewa na wewe wala mwingine, bali ni juu Yake Yeye Mungu kutaka radhi yangu." (Mungu apishe mbali).

Musa (a.s.) akamwambia: "Kafiri mkubwa we Mwenye laana!"

xxxi

Ibilisi Akasema: "Kwani nina dhambi gani mimi? Mungu alinitaka nimsujudie Adam, na mimi kwa ilkhlas yangu, siwezi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Sasa tangu lini Ikhlas ikawa ni dhambi?"

Musa (a.s.) akamjibu: "Hii ni kuchezea maneno tu nako hakuwezi kukufaa wewe hata chembe, utaona yatakayokupata Kesho (Kiyama)."

Ibilisi akasema: "Na wewe utaona nitakavyofanya kesho." Akasema: "Utafanya nini?"

Ibilisi akajibu: "Nitamtaka Mwenyezi Mungu atimize ahadi Yake na nitamtolea hoja kwa kauli Yake:

"Na rehema yangu hukienea kila kitu."

(7:156)

"Nami ni 'kitu,' kwa hiyo ni wajibu rehema Yake inipate (inienee). Kama mimi si chochote, basi sitahisabiwa wala kuadhibiwa."

Akasema Musa (a.s.): "Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu inamwenea yule mwenye mwelekeo nayo, na wewe uko mbali sana nayo."

Ibilisi akasema: "Basi nitafanya njia nyingine. Nitawaita wafuasi wangu waliopotea na nitamtaka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) naye awaite wafuasi Wake waumini, halafu ipigwe kura. Hapo atajulikana nani mshindi mwenye sauti ya wengi. Kama Mwenyezi Mungu akikataa kura, nitafanya maandamano makubwa mpaka nipate ninayotaka."

Kigano hiki kina lengo la kwamba watu wa batili ni wengi zaidi kuliko watu wa haki, kwa sababu haki ni nzito na batili ni nyepesi; kama alivyosema Amirul Muminin, AN (a.s.): "Yapasa mwenye akili kutoangalia wingi kuwa ni kipimo cha haki, wala uchache kuwa ni kipimo cha batili."

Katika Nahjul-Balagha, amesema: "Hakika kundi kubwa ni watu wa batili hata wakiwa wengi; na kikundi kidogo ni watu wa haki hata wakiwa wachache."

Qur'an tukufu nayo inasema:

"Na wengi wao ni wenye kuchukia haki."

(23:70)

XXXII

"Lakini watu wengi hawajui."

(12:21)

"Lakini watu wengi hawashukuru."

(12:38)

"Na wengi wao hawatumii akili."

(5:103)

"Bali w engi wao hawaamini."

(2:100)

Kuna Hadith inayosema: "Wakikutana wasaidizi wa Ibilisi wanaweza kujaza Mashariki na Magharibi."

Ni kwa madondoo haya, na mengineyo mengi, ndipo Shia wakasema: Khalifa wa Mtume ni kama Mtume; huchaguliwa na Mwenyezi Mungu; siye yule anayechaguliwa na watu. Huyo anayechaguliwa na watu ni Mfalme wa watu; si Khalifa wa dini. Ama mkuu wa dini, kwa Shia, ni yule mwenye sifa zilizoelezwa. Sio yule anayechaguliwa na watu wala si yule anayewekwa na kiongozi wa kidunia.

Na kwa nini isiwe hivyo? Je, watu wenye matamanio ya dunia wanaweza kuaminika kuongoza dini ya Mwenyezi Mungu? Basi kama ni hivyo na wawachague na kuwapigia kura Mitume, na walifaradhishe hilo kwa Mwenyezi Mungu. Ametakata kabisa Mwenyezi Mungu na yale wayasemayo madhalimu.

Natija ya kimantiki ni kwamba Khalifa wa Mtume hawi, na hatakuwa, isipokuwa kwa usimulizi unaotokana na Mtume mwenyewe, na kwamba mkuu wa dini ni yule mwenye sifa zilizosimuliwa.

XXXIII

Mwenye kujipachika ukuu wa dini bila ya kuwa na sifa zilizotajwa, basi atakuwa amemzulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ameruka patupu mwenye kuzua.

Kwa hivyo basi, yote hayo yanafahamisha kuwa suala lolote haliwezi kuwa la kweli mpaka liwe limefuata haki; na kwamba mbinu za kucheza na maneno, haziwezi kuifanya batili iwe haki, au haki iwe batili, wala kisichoingia akilini kiingie akilini; hata kama hizo mbinu zitakuwa za hali ya juu kiasi gani. Tutakalolifahamu ni kuwa mwenye mbinu hizo ni mwanafunzi hodari wa Ibilisi katika kuificha haki, na kuifunika na moshi wa hadaa.

xxxiv

Kaashif1-3.jpg

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

BISMILLAH

Tamko hili tukufu ni nembo maalum ya Waislamu. Kwalo Wanaanzia maneno na vitendo vyao vyote; na iko kwenye daraja ya pili baada ya shahada mbili.

Ama wasiokuwa Waislamu, huanza: Kwa jina Lako ewe Mwenyezi Mungu Kwa jina Lake Mtukufu, kwa jina la Mwenye kuanza, na Mwenye kuishiliza au Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu n.k.

Huondolewa hamza katika neno ism katika Bismillahi, linapotamkwa na kuandikwa kwa sababu ya kutumiwa sana. Na, huondolewa hamza kwa kutamkwa, na sio kwa kuandika mahali pengine; kama vile sabbihisma rabbikal -aala na Uqsimu billah.

Tamko Allah (Mwenyezi Mungu) lina maana ya Mwenye kuabudiwa kwa haki, ambaye husifika na sifa zote za utukufu na ukamilifu, wala hakisifiwi kwa sifa hiyo kitu kingine chochote.

Inasemekana kuwa Mwenyezi Mungu ana jina moja Tukufu, na kwamba atakayelijua, basi atamiminikiwa na heri na atakuwa na miujiza. Lakini sisi tunaamini na kuitakidi kwamba kila jina la Mwenyezi Mungu ni tukufu; yaani huyo Mwenyezi Mungu ni Mtukufu. Kwa sababu haiwezekani kabisa kuu-fanya upande mmoja ni bora kuliko upande mwingine, kuboresha kutaleta ushirika na kuzidi; na ambaye hana mfano wa kitu chochote, hawezi kushirikiana na yeyote katika kitu.

Neno Rahman (Mwingi wa Rehema) ni sifa. Limechukuliwa kutoka katika Rahma (Rehema). Maana yake kwa upande wa Mwenyezi Mungu ni kufanya hisani na kwa upande wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lina maana ya upole wa moyo.

Limezoeleka kutumiwa kwa maana ya dhati yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.), likawa ni katika majina mema ya Mwenyezi Mungu.

xxxv

Mwenyezi Mungu anasema:

"Sema! Muombeni (kwa jina la) Mwenyezi Mungu, au muombeni (kwa jina la) Mwingi wa rehema; kwa jina lolote mnalomwita (itafaa), kwani ana majina mema".

(17:110)

Neno Rahim (Mwenye kurehemu) vile vile, ni sifa. Limechukuliwa kutoka katika neno Rahma. Wafasiri wengi wametofautisha kati ya matamko haya (Rahman na Rahim) kwamba Rahman ni rehema yenye kuenea kwa muumini na kafir; na Rahim ni rehema yenye kuwahusu waumini peke yao. Wakasema: Ewe Mwingi wa Rehema katika dunia na Akhera na ewe Mwenye Kurehemu akhera tu. Ama mimi nasema: Ewe Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu katika dunia na akhera.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Je, wao wanaigawa rehema ya Mola wako?"

(43:32)

Kwa ujumla maana ya "Bismillaahir rahmani rahim" ni kwamba wewe unaanza kitendo chako kwa kumtaka msaada ambaye rehema Yake imekienea kila kitu na kusajili katika nafsi yako kwamba unayoyafanya ni kwa jina lake, sio kwa jina lako wala kwa jina la mwingine yeyote asiyekuwa Yeye. Si kama vile anavyosema mtumishi wa serikali kuwaambia raia: "Kwa jina lataifa ninawaambia kadhaa..."

Bismillah inafahamisha kwamba kitendo unachofanya ni halali hakina shaka ya haramu. Kama kitendo ni haramu na ukakifanya kwa Bismillaah, basi utakuwa umeasi mara mbili kwa mpigo. Kwanza, ni kuwa kitendo chenyewe ni haramu. Pili, ni kuwa umesema uongo kwa kukinasibisha na Mwenyezi Mungu. Ametakasikia Mwenyezi Mungu na hayo kabisa.

Hukumu

Kwa upande wa Shia Imamiya, Bismillah ni sehemu ya sura na wamewajibisha kuisoma kwa sauti katika swala ambayo ni wajibu kusoma Alhamdu na sura kwa sauti; kama vile swala ya Asubuhi (Al-fajr)

xxxvi

na rakaa mbili za mwanzo za swala ya Maghrib na Isha. Ni sunna kusoma kwa sauti katika swala ambayo haisomwi kwa sauti kama vile swala ya Adhuhuri na Alasiri.

Hanafi na Maliki wamesema kuwa inajuzu kuiacha Bismillaah katika swala, kwa sababu si sehemu ya sura. Shafi na Hambali wamesema ni sehemu ya sura; ispokuwa Hambal wamesema kuwa isisomwe kwa sauti wakati wowote wa swala. Shafi nao kwa upande wao, wakasema isomwe kwa sauti katika swala ya Asubuhi (Al-fajr) na rakaa mbili za Maghribi na Isha. Hapa kauli ya Shafi na Hambal haziko mbali na kauli ya Imamiya.

Kwa ujumla ni kwamba herufi hizi za Bismillah zinatengeneza jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa Zake. Hutamkwa na kuandikwa kama maneno mengine, lakini lina heshima na hukmu mahsusi. Haijuzu kuliandika juu ya karatasi, au kwa wino, kalamu au kitu chochote kilicho najisi. Vile vile haijuzu kuligusa bila ya twahara.

Wataalamu wa Fiqhi wa Kiimamiya wamefutu kwamba mwenye kuutupa msahafu makusudi katika uchafu, kuupiga teke, kuupasua kwa dharau, au kuufanyia kitu chochote kinachoonyesha dharau, basi amekuwa kafiri aliyeritadi.

Msemaji mmoja amesema kuwa Sura ya Fatiha imekusanya maana yote ya Qur'ran, na kwamba Bismillah imekusanya maana yote ya Fatiha, na herufi Ba katika Bismillah imekusanya maana yote ya Bismillah. Hatimaye herufi Ba inakuwa imekusanya maana yote ya Qur'an.

Msemaji huyu ni kama yule anayejaribu kuuingiza ulimwengu pamoja na ardhi yake na mbingu yake katika yai bila ya kulikuza yai hilo au kuufanya mdogo ulimwengu!

Nembo ya Uislamu

Nilisoma makala katika gazeti la Al-Jumhuriyya la Misri la tarehe 21 Aprili 1967 yaliyoandikwa na Dhiyau Rayis, kwamba yeye alisoma makala katika jarida la fasihi la mwandishi mashuhuri wa Kiarabu akisema "(Huyo mwandishi) alipokuwa Uingereza, aliwahi kubishana vikali na msomi mmoja Mwingereza kuhusu Uislamu na Ukristo. Akasema yule Mwingereza kupingana na Waislamu wote: "Mimi ninaifupisha misingi yote ya Kikristo kwa neno moja tu, 'Upendo'. Je unaweza wewe Mwislamu kuleta tamko linalokusanya misingi ya Kiislamu?" Yule mwandishi akajibu: "Ndio neno hilo ni Tawhid'.

XXXVII

Baada ya Rayis kunakili mazungumzo haya akasema: "Jawabu halikuwa sawa." Akataja sababu kadhaa za kutomwafiki kwake, kisha akasema: "Lau swali hili ningeulizwa mimi, ningelijibu kuwa ni 'Rehema.' Akatoa dalili kwa Aya nyingi na Hadith nyingi, akianzia na Bismillahir rahmanir rahim mpaka Aya inayosema:

"Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu."

(21:107)

Amesema kweli Rayis kwamba jawabu la yule mwandishi halikuwa sawa. Lakini hata yeye Rayis pia jawabu lake halikuafiki, kwa kuchagua neno 'rehema'. Kwa sababu hakuzidisha kitu katika aliyoyasema Mwingereza. amechukua neno 'upendo' na kulifasiri rehema. Kwa hiyo Uislamu unakuwa hautofautiani na Ukristo.

Lau mimi ningelikuwa pamoja na yule mwandishi, ningelijibu kwa neno unyoofu'. (msimamo) Kwa sababu ni neno lenye kukusanya unyoofu katika itikadi tawhidi, vitendo, maadili, hukumu, na mafundisho yote yaliyo na rehema mapenzi na kusaidiana. Rehema ni moja katika misingi ya Kiislamu na sio Uislamu kamili; kama vile ambavyo tawhidi ni msingi katika misingi ya Uislamu na sio misingi yake yote.

Unyoofu ndio kipimo sahihi cha ukamilifu ambao mtu aweza kuufikilia wema wa dunia na Akhera. Ndio maana tunakariri katika swala zetu usiku na mchana: "Tuongoze njia iliyonyooka." Mwenyezi Mungu amesema kumwambia Mtume wake mtukufu (s.a.w.):

"Endelea na unyoofu kama ulivyoamrishwa, (wewe) na wale wanaoelekea (kwa Mwenyezi Mungu) pamoja nawe; wala msiruke mipaka. Hakika Yeye anayaona mnayoyatenda."

(11:112)

Amesema tena:

xxxviii

"Hakika wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakafuata unyoofu, hao Malaika huwateremkia (wakiwaambia): Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa."

(41:30)

Hakuna kitu kinachofahamisha zaidi kwamba unyoofu ni muhimu, kuliko neno la Ibilisi aliyelaaniwa:

"Basi nitawakalia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka..."

(7:16)

Kuna Hadith tukufu inayosema kuwa Sufyan Thaqafi alimwambia Mtume: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niambie neno ambalo sitamuuliza mtu mwingine baada yako milele." Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:"Sema nimemwamini Mwenyezi Mungu, kisha ufuate unyoofu (msimamo)."

Kwa ufupi maana ya unyoofu ni kuwa ndani ya mipaka ya Mwenyezi Mungu bila ya kukengeuka na haki kwa kuifuata batili na kuacha uongofu na kuwa katika upotevu. Vile vile kuwa kwenye njia iliyonyooka, njia ya (wale) ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, sio ya wale walioghadhibikiwa wala waliopotea.

xxxix

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

1 Sura Al-Fatiha

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

1 Sura Al-Fatiha

Al - Fatiha

(Ufunguzi) Sura ya Kwanza

Kushuka

Wametofautiana kuhusu mahali iliposhuka, imesemwa kuwa ni Makkah wengine wakasema ni Madina bali kuna kundi jengine linasema kuwa imeshuka mara mbili Makkah na Madina. Hata hivyo wafasiri wengi wamesema imeshuka Makkah.

Tofauti hii, kwa hakika, haina faida kwani surah hii tukufu haina Aya zozote zinazotofautiana kimaana kwa kutofautiana kushuka.

Majina yake

Wametaja majina mengi; yaliyo maarufu ni haya yafuatayo:-

Faatiha (ufunguzi): Kwa sababu ndiyo sura ya kwanza katika msahafu, na ni wajibu kuisoma mwanzo wa swala. Pia mafundisho, kwa ujumla, yalikuwa yakianzwa kwa sura hiyo.

Al-Hamdu: kwa sababu ndilo tamko la mwanzo katika sura hiyo.

Ummul-Kitab na Ummul-Qur'an (mama wa Qur'an): kwa sababu imetangulia sura nyingine, ijapokuwa ni kwa kimandishi tu. Kwani mama huwatangulia wanawe. Na kwa vile imekusanya misingi miwili; kutaja utawala wa Mungu na utumwa wa mja, na mambo mawili hayo ndiyo nguzo ya mafundisho ya Qur'an.

Sab'ul-Mathani (Saba mbili) kwa sababu ina aya saba, au ina Aya saba zinazorudiwa mara mbili katika swala, au ni kwa sababu inataja maambo mawili: Mola na mja wake.

Vyovyote iwavyo majina haya yana mwelekeo kidogo.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza Ayah 1-7

1.     Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

2.     Sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe (vyote).

3.     Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

4.     Mwenye kumiliki Siku ya Malipo.

5.    Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.

1 Sura Al-Fatiha

6. Tuongoze njia iliyonyooka.

7. Njia                ya                (wale)

uliowaneemesha; Sio ya (wale) waliokasirikiwa wala ya (wale) waliopotea.

(V) Cj

Sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe (vyote.)

Jumla hii ni habari kwa maana ya insha. Kwa sababu msomaji anakusudia kuleta sifa njema za Mwenyezi Mungu, wala sio kutoa habari za kuthibitisha sifa Zake njema.

Jumla hiyo ina maana ya mafunzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, jinsi watakavyomsifu Mwenyezi Mungu. Yaani: Semeni enyi Waja wangu! Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.

Maana ya sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, ni kumsifu kwa kukusudia kumwadhimisha katika hali zote, hata katika madhara. Amirul Muminin (a.s.) anasema katika moja ya khutba zake za Nahjul-Balagha:

3

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

1 Sura Al-Fatiha

"Tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa neema zake, kama tunavyomsifu kwa balaa."

Muhammad, Ahmad, Mahmuud na Hamdaan, ni majina yaliyochukuliwa kutoka katika neno Al-Hamdu. Neno Hamd linakuja kwa kukisifu kitu unachokiridhia.

Mwenyezi Mungu S.W.T. hapa anataja Mahmuud (chenye kusifika) akisema:

"Huenda Mola wako akakuinua cheo chenye kusifika"

(17:79).

Neno Rabb linaweza kutumiwa kwa maana ya 'Bwana' na 'Mwenye kumiliki'. Maana zote mbili zinasihi hapa, lakini maana ya 'Mola Muumbaji' ndiyo inayoelekea zaidi katika aya hii tukufu.

Makusudio ya Alaamin (viumbe) hapa ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo linaenea kwa viumbe vyote.

Maana ya Rabbil-Aalamin ( Mola wa viumbe vyote) ni Muumbaji wa kila kitu, na mwenye kupangilia vizuri. Na neno 'Mola' linafahamisha utukufu; yaani: Hakika mimi ninamsifu Mwenyezi Mungu kwa sababu Yeye ni Mola wa viumbe vyote.

Mwingi wa rehema mwenye kurehemu:

Maelezo yake yameshapita katika maelezo ya Bismillah

Miongoni mwa maneno ya Amirul Muminin katika kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema: "Ghadhabu haimshughulishi (asiwe) na rehema wala rehema haimshughulishi (asiwe) na mateso".

Nilivyofahamu jumla mbili hizi ni kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa waasi, na adhabu yao kesho, haimzuii Yeye kuwarehemu katika maisha haya wanayostarehe kwa neema yake na kwamba rehema Yake kesho haiwaondolei waumini balaa na maovu katika maisha haya.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                                 1 Sura Al-Fatiha

Mwenye kumiliki siku ya malipo

Neno Din lina maana nyingi; miongoni mwayo ni malipo. Na maana haya ndiyo yanayonasibiana na hapa, ambapo siku hiyo italipwa kila nafsi yale iliyoyachuma.

Neno Maaliki husomwa kwa alifu, kwa maana ya kuhusisha (umilikaji); kama inavyosemwa: Fulani ndiye mwenye kumiliki bustani hii (mwenye kuhusika nayo). Pia husomwa Maliki bila ya Alifu (kwa kutovuta) kwa maana ya 'mfalme', kama inavyosemwa: Mfalme wa Ugiriki, kwa maana ya Mtawala.

Visomo vyote viwili vinatumika, ingawaje cha kwanza ndicho kinachotumika zaidi.

Maana inayokuja haraka akilini, kwa kusoma namna zote mbili ni moja: Kuwa kila kitu kiko mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake, leo na kesho. Yeye ni Mola wa viumbe vyote, na Mola wa Siku ya malipo. Lengo ni kukemea watu na maasia na kuwavutia katika twaa.

Katika Nahjul Balagha Imam Ali (a.s.): amesema: "Hakika sisi hatumiliki chochote kwa Mwenyezi Mungu, wala hatumiliki isipokuwa kile alichotumilikisha. Alipotumilikisha kile ambacho Yeye amekimiliki huwa ametukalifisha nacho, na anapotuondolea huwa ametuondolea taklifa yake."

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.

Mja kumzungumzia Mola wake kwa dhamiri ya Mmoja (Wewe tu) ni kwa ajili ya kumtakasa katika Umoja wake, na pia kumtakasa na shirk. Kwa ajili hii, halinganiwi Mwenyezi Mungu kwa tamko la wingi. Ama dhamiri ya wingi (sisi) katika neno "tunakuabudu" na "tunakuomba msaada" ni ya mwenye kusema (mja) pamoja na mwingine, wala sio ya kutukuza.

Ibada inathibitika kwa Saumu, Swala, Hijja na Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu. Vile vile inathibitika kwa huduma yoyote ya kibinadamu ya kutekeleza haja za watu. Kuna Hadith inayosema: "Watu wa mema duniani ni wa mema Akhera. Bora wa watu ni yule mwenye kuwafaa zaidi watu."

Maana ya "Wewe tu tunakuabudu na Wewe tu tunakuomba msaada," sio kwamba Mungu ni wa kuabudiwa tu basi iwe imetosha. Bali vile vile Aya inafahamisha kuwa mtu ni kiumbe kitakatifu aliyekombolewa (aliyehuru) kutokana na utumwa na unyonge isipokuwa kwa haki tu, ambayo iko juu

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

1 Sura Al-Fatiha

ya kila kitu na wala haikaliwi juu. Kimsingi ni kwamba uhuru usiowekewa mpaka na haki, hubadilika na kuwa machafuko.

Katika maneno yenye faida niliyoyasoma, yanayohusiana na mlango huu, ni maneno ya Jean Paul Sartre, aliposema, "Hakika uhuru hasa ni akujilazimisha mtu kujitolea nafsi yake na uhuru wake katika kuwatumikia wengine."1

KISA

Kulikuwa na watu wawili wakitembea katika bustani. Mmoja alikuwa na fimbo akicheza nayo. Mara ikagusa ncha ya pua ya mwenzake. Alipomlaumu kwa kitendo hicho, yule mwenye fimbo akajigamba: "Nina uhuru bwana!" Mwenzake akamwambia, "Uhuru wako una mpaka; mwisho wake ni pua yangu!"

Mimi siupingi uhuru ikiwa mpaka wake ni kumwamini Mwenyezi Mungu na kumwabudu Yeye peke yake. Kwa sababu mwenye kuabudu haki tu atakuwa amejikomboa na batili; na mwenye kujikomboa na kuabudu haki, bila ya shaka atakuwa mtumwa wa batili. Haiwezekani kutofautisha katika mawili hayo isipokuwa kwa yule ambaye hana mpangilio; asiyeamini halali wala haramu, wala kuamini kitu chochote kingine isipokuwa nafsi yake peke yake.

Sartre mwanzo alikuwa na nadharia ya Existentialism (kuwako) akidai kwamba "kila mtu na lake, na hanasibiani na chochote isipokuwa kuwako kwake peke yake. Huko kuwako kwake hakuwezi kuthibiti isipokuwa kwa kuwa huru bila ya kuwa na kikwazo chochote au sharti lolote. Ama dini, misingi, na kuweka mambo katika vipimo, ni upuuzi. Hakuna heri isipokuwa heri ya mtu mwenyewe wala hakuna shari isipokuwa shari yake mwenyewe."

Kwa nadharia hii Satre anatoa dalili kuwa mtu amekuja kutoka katika ulimwengu usiojulikana.na anaelekea ulimwengu usiojulikana na kwamba yeye alikuwako kabla ya kanuni za kiakili na za kidini. Kwa hiyo, yeyote atakayejitia katika dini au katika msingi wowote, atakuwa amejifunga na kuuacha uhuru wake na kwa hivyo amejikanushia kuwako kwake.

Kisha akabadilisha falsafa yake hii akaingia katika falsafa ya Uhuru mkubwa, nao ni uhuru kwa ajili ya mamilioni; kwamba mtu anaichumia, nafsi yake, ikiwa atajiweka katika kuwahudumia wengine; kwamba 'mtu hasa ni yule anayelazimiana na misingi hii.'

Badala ya kuwa anazungumzia juu ya hali ya mtu mmoja peke yake, akawa Satre anazungumzia juu ya haki za watu wengi na kulitetea hilo!

6

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                                 1 Sura Al-Fatiha

Tuongoze njia iliyonyooka

Makusudio ya njia iliyonyooka si elimu tu, bali ni elimu pamoja na tawfiki katika vitendo (amali). Mwenye kukutakia uongofu amekutakia heri yote, na mwenye kukutakia elimu amekutakia baadhi ya heri.

Maajabu ni kuwa watu wengi wanakuwa wazito kuomba uongofu, hasa wanavyuoni na watu wakubwa, pamoja na kujua kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) alikuwa akikariri kuomba uongofu usiku na mchana katika swala zake na sehemu nyinginezo.

Sijui kama kuna uongofu na tawfiki bora na kubwa zaidi kuliko ile ya mtu kugundua aibu zake mwenyewe na kujilaumu, na kumchoma sana. Kwa kutambua hayo inawezekana mtu kuokoka. Mwenyezi Mungu atukinge na ghururi na maovu yake!

Njia ya (wale) uliowaneemesha; sio ya (wale) waliokasirikiwa wala ya (wale) waliopotea.

Imepokewa Hadith kwamba makusudio ya waliokasirikiwa ni Wayahudi, na waliopotea ni Wakristo. Lakini tamko la Aya ni la jumla, wala sio mahsusi au kuvuawengine (kubagua).

Kila mtiifu anaingia katika neema na rehema ya Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuasi ni mwenye kupotea na kughadhibikiwa.

Vyovyote iwavyo, lengo la Aya hii na sura nzima ya Fatiha, ni kuwa mja asimame mbele za Bwana wake akiwa ni Muumini mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, mwenye kushukuru, mwenye kumsifu, mwenye ikhlasi, na mwenye kuomba tawfiki kwa elimu na kwa vitendo.

Na kila mtu ataikuta amali aliyoitanguliza kwa Muumba wake. Ama maneno tu, hayana athari isipokuwa kujikurubisha na twaa, au kujiweka mbali na maasia.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Al - Baqarah

(Ng'ombe)

Sura ya Pili

Amesema mwenye Majmaul-Bayan kwamba sura hii yote imeshuka Madina, isipokuwa Aya ya 281.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1.    Alif Laam Miim

2.     Hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake; ni uwongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu.

3.    Ambao wanaamini ghaibu na wanasimamisha Swala na wanatoa           katika           yale tuliyowap

4. Na ambao wanaamini wj ıLUj yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako na akhera wana yakini nayo.

5. Hao wako juu ya uwongozi utokao kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

MIANZO YA BAADHI YA SURA Alif Lam Mim Aya 1-5

Wamehitalifiana wanavyuoni kuhusu makusudio ya mwanzo huu na ya mianzo ya sura nyingine inayofanana na hii mfano: Alif Laam Miim Raa, Kaaf Haa Yaa A'yn Swaad na Haa Miim.

Imesemekana kuwa herufi hizo ni katika elimu ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu hakuidhihirisha kwa yeyote. Lakini sidhani kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaweza kuwaambia watu jambo asilotaka walijue. Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu amewakemea wale ambao hawaifikiri vizuri Qur'an, aliposema:

"Je, hawaizingatii (hii) Qur'an au katika nyoyo zao kuna kufuli?

(47:24)

Pia imesemekana mianzo hii ni majina ya sura; vilevile imesemwa ni majina ya Mwenyezi Mungu, aidha ikasemwa kuwa ni ya Muhammad (s.a.w.) nk..

Lakini linaloelekea zaidi ni kauli inayosema kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya kuwaambia wapinzani walete mfano wa Qur'an, au sura kumi, au moja; na wakashindwa, ndipo akataja herufi hizi. Yaani, kitabu hiki ambacho ni muujiza, hutokana na herufi hizi ambazo hata watoto na wajinga pia wanazitumia, lakini nyinyi mmeshindwa.

Kwa hivyo kushindwa kwenu ni dalili wazi kwamba kuna siri, na siri yenyewe ni kuwa hii Qur'an ni wahyi wa kidini sio usanii wa kidunia.

QUR'AN NA SAYANSI

Kauli yake Mwenyezi Mungu: Ni uwongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu, ni dalili wazi kwamba Qur'an si kitabu cha elimu ya Historia, wala Falsafa, au elimu ya Fizikia au ya Hesabu; isipokuwa ni kitabu cha elimu ya uongofu wa mwana-adamu katika dunia na akhera, au sema Qur'an ni kitabu cha dini, maadili, itikadi na sharia.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kama utauliza: "Ikiwa Qur'an ni kitabu cha dini, mbona basi kuna Aya zinazohusu mambo ya kilimwengu; kama vile

"Na jua linakwenda mpaka kituoni pake; na mwezi tumeupimia vituo."

(36:38-39)

Jibu: Lengo la Aya hizi sio kutubainishia hali ya maumbile kwa undani wa kielimu - kwani hilo limeachiwa akili na majaribio yake - isipokuwa lengo la kwanza la kutajwa Aya hizo ni kwamba, kujua ulimwengu na nidhamu yake kutatuongoza kujua kuwa kuna Mungu, na kwamba huu ulimwengu haukupatikana kibahati tu bila ya kukusudiwa; kama wanavyodai watu wa kimaada. Bali ulipatikana kwa matakwa ya kihekima.

Mwenyezi Mungu amelibainisha hilo katika Aya isemayo:

"Tutawaonyesha ishara zetu zilizo katika upeo wa mbali na zilizo katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli."

(41:53)

Yaani, tutawafafanulia makafiri - kwa vile watakavyoufahamu ulimwengu kutokana na mipangilio mizuri ya Mwenyezi Mungu - kuwa wao wako katika upotevu.

Qur'an inapotoa mwito wa kuangalia ulimwengu, inasema kwa lugha iliyo wazi kuwa dalili za ulimwengu ni hoja ya kweli na ni dalili yenye nguvu zaidi juu ya kuwapo Mungu, kuliko kitu chochote. Baadhi ya wenye hekima wamesema: "Mwenyezi Mungu ana vitabu viwili: Kitabu kinachosomwa na kitabu cha akili, ambacho ni ulimwengu."

Ni kweli kuwa Qur'an inahimiza kusoma sayansi na kila elimu itakayompa binadamu ufanisi. Lakini kuhimiza ni kitu kingine na kuwa ni kitabu cha elimu hiyo ni kitu kingine.

Katika ambayo yanatia nguvu na kuunga mkono kwamba Qur'an ni kitabu cha uongofu, sharia, na maadili mema, na kwamba Qur'an imeteremshwa kwa lengo hili, ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

10

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Hizi (Aya za Qur'an) ni dalili zitokazo kwa Mola wenu na ni uongofu na rehema kwa watu wanaoamini."

(7:203)

Amesema tena:

"(Hiki) ni kitabu tulichokiteremsha kwako ili uwatoe watu katika giza uwapeleke kwenye num."

(14:1)

Na Mtume mtukufu (s.a.w.) anasema: "Hakika hapana jingine, nimetumwa kutimiza tabia njema". "Na amesema Amirul Muminin (a.s.) katika hotuba ya 174, ya Nahjul-Balagha: "Hakika Qur'an ni dawa ya ugonjwa mkubwa sana wa kufuru, unafiki na upotevu."

Kwa maneno haya tunapata tafsiri ya Aya isemayo:

"Na tunateremsha katika Qur'an yale am bay o ni ponyo na rehema kwa wanaoamini, wala hayawazidishi madhalimu ila hasara tu!"

(17:82)

Kama utauliza mara ya pili: Unasemaje kuhusu Aya hii. "Hatukupuuza kitabuni kitu chochote",

(6:38)

si inafahamisha kuwa katika Qur'an kuna elimu zote?

Jawabu: Kutosha kila kitu huwa ni kulingana na mahitaji. Ukisema: Nyumba hii ina kila kitu; itafahamika kwamba ina mahitaji ya mwenye kukaa humo. Kama ukisema: Kitabu cha Fiqh kina kila kitu, itafahamika kuwa mna masuala yote ya kifiqh. Qur'an ni kitabu cha dini. Kwa hiyo

11

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

pale Mungu aliposema. "Hatukupuza kitabuni kitu chochote, maana yake ni kila kinachoambatana na heri ya mtu na uongofu wake.

Swali la tatu: "Unasemaje kuhusu vitabu hivi vyenye majina kama: Qur'an na Sayansi, Uislamu na tiba ya kisasa, na vingenevyo?"

Jibu: Kwanza kabisa, kila anayejaribu kulinganisha kati ya uvumbuzi wa kielimu wa kisasa au wa kizamani na Qur'ani, atakuwa anajaribu jambo lisilowezekana. Kwa sababu elimu ya binadamu ina mpaka kulingana na nguvu yake ya kiakili; na Qur'an ni elimu ya Mwenyezi Mungu ambayo haina mpaka. Itakuwaje kitu kilicho na mpaka kiafikiane na kisichokuwa na mpaka?

Pili, elimu ya binaadamu inaingiliwa na makosa. Kwa sababu inakuwa ni dhana na makisio; inakosea na kupata. Mara ngapi tumewaona wataalamu wakikongamana juu ya nadharia fulani na kudai kuwa ni kweli mia kwa mia; kisha wao wenyewe au wale watakaokuja baada yao wanagundua kuwa ni makosa mia kwa mia? Qur'an ni yenye kuhifadhiwa na makosa. Itakubalika vipi kuoanisha chenye makosa na kile kisicho na makosa? Kisha je tuendelee kugeuza Qur'an kila yanapogeuka makisio ya elimu na nadharia zake? Hapana.

Ndio! hapana ubaya kujisaidia na ugunduzi wa kielimu katika kufahamu baadhi ya Aya, lakini kwa sharti ya kutoufanya huo ugunduzi kuwa ni kipimo cha ukweli na kusihi Qur'an, bali hata kutozifanya hizo elimu kuwa ndio nyezo za kufahamu siri ya Qur'an na kufahamu hekima ya baadhi ya hukumu zake.

Inawezekana kuwa hili ndilo lililowafanya watungaji kutunga vitabu kama: Qur'an na Sayansi n.k.

Vyovyote iwavyo, sisi tuna yakini kwamba tuna hoja zenye nguvu katika dini yetu, na tuna dalili za kutosha juu ya ukweli wake; hatuna haja kabisa na vilivyo kwa wengine. Bali tunaamini kwamba wengine ndio walio na haja kwetu katika hilo.

Kwa hakika historia ya binadamu haitapata dini yenye utengeneo zaidi ya dini ya Kiislamu, wala kitabu chenye kunufaisha zaidi ya kitabu chake, au Mtume mtukufu zaidi ya Mtume wake. Na yule ambaye hakuongoka kwa dalili za Qur'an na mwito wake wa maisha mema, basi hataweza kukinaishwa na ugunduzi wa kisayansi wa sasa au wa zamani.

12

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kuna kitu nilichokifikiria ambacho huenda kikapunguza machovu ya msomaji kuhusu majibu ya yule anayejaribu kuilinganisha Qur'an na ugunduzi wa sayansi; kama ifuatavyo:

Uzayr alipita katika mji uliokufa, akiwa na punda wake, chakula chake na kinywaji chake akastaajabu na kusema:

"Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu baada ya kufa kwake?"

(2:259)

Mwenyezi Mungu akataka kuuondoa mshangao wake. Akamfisha miaka mia. Chakula na kinywaji alichokuwa nacho, kilibakia katika hali yake bila ya kuharibika katika muda wote huo.

Kisha Mwenyezi Mungu akamfufua na akataka kumwonyesha miujiza yake ya ajabu, akamwambia:

"Tazama chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika"

(2:259)

Hebu angalia msomaji! Je, chakula cha Uzayr kilikuwa katika jokofu (friji)? Swali hili linamhusu mwenye kuilinganisha Qur'an na elimu ya kisasa. Hakuna anayetia shaka kwamba jokofu hili ambalo lilihifadhi chakula na kinywaji kwa muda wa miaka mia, pengine linaweza kuwa ni sampuli ya mwaka 2000, na wala siyo ya mwaka 1967.

Ndio! Inawezekana kulinganisha sayansi na kufahamu maana ya Qur'an tukufu; hasa kwa upande wa nadharia ya relativity (uwiano). Kwa vile kufahamu kunahusika na upande fulani katika maana yake, na kunatofautiana na hali ya anayesoma au anayesikiliza.

Kama mtu akisema kuwa tofauti hii haihusiki na Qur'an peke yake, kwa sababu nadharia ya uwiano ni ya jumla, isiyokubali kuhusishwa, tutajibu: Hiyo ni sawa, lakini maana ya Qur'an yamejiandaa na hilo. Na hili linatilia nguvu maelezo yetu kwamba mtu mwenye kuganda na kauli za wafasiri bila ya kuongeza kitu, atakuwa na akili ya kusoma tu, lakini sio akili ya mwamko.

13

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Basi twamuomba Mwenyezi Mungu azijaalie fahamu zetu katika Aya zake kuwa ni za mwamko na sio fahamu za kunakili.

Wamchao Mwenyezi Mungu

Maana ya neno kucha (takua) kilugha ni kujichunga na kitu chochote. Na maana yake kisheria ni kujikinga na hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu Yake, kujikinga na kuuacha wajibu na kutenda haram. Amesema Amirul Mumini Ali (a.s.): "Kumcha Mwenyezi Mungu ndio msingi wa tabia njema." Wengine wamesema kumcha Mwenyezi Mungu ni kuwa Mwenyezi Mungu asikuone na lile alilokataza na kutoacha alilokuamrisha.

Kumcha Mungu ndiko kunakomfanya mtu kuwa bora mbele ya Mwenyezi Mungu. Qur'an inasema:

"Hakika Mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchae Mungu zaidi."

(49:13)

Unaweza kuuliza, ikiwa wenye kumcha Mungu ni wenye kuongoka, basi wana haja gani ya kuongozwa? Je mwanachuoni anahitaji wa kumfundisha?

Jibu: Hakika mwalimu hufundisha wanafunzi wote wajinga na wenye akili, lakini wale wanaonufaika na mwalimu ni wale wenye akili wanaojitahidi ambao mwisho wao utakuwa ni kufaulu. Kwa hivyo ni sawa tukisema kuwa mwalimu ni wa wenye kufaulu. Vile vile Qur'an tukufu imewaeleza watu wote, lakini wanaonufaika nayo ni wale waumini wenye kumcha Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na wale wanaokubali kuongoka Mwenyezi Mungu anawazidishia uongofu."

(47:17)

Wanaoamini Ghaibu

MAARIFA

Inasemekana kuwa mwanachuoni mmoja mkubwa aliyekuwa na heshima na cheo kikubwa huku watu wakimzunguka kwa kumuuliza maswali na kumnyenyekea, alionewa kijicho na mpinzani wake mmoja.

14

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Akamuuliza swali la kutatiza kwa sauti kubwa, ili wote wasikie. Mwanachuoni akasema: "Sijui." Muulizaji akasema: "Mahali ulipo ni pa anayejua sio pa asiyejua." Akasema mwanachuoni: "Ole wako! Hapa ni mahali pa anayejua kitu sio kila kitu; anayejua kila kitu hana mahali."

Ndio! ni muhali kwa mtu kujua kila kitu. Mwenyezi Mungu anasema:

(17:85)

"Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu."

Hakuna mtu yeyote anayezaliwa na ujuzi, isipokuwa hupata maarifa muda baada ya muda, kutokana na sababu fulani; hata hilo jina lake pia halijui, isipokuwa baada ya kuitwa mara kwa mara.

Wajuzi wa fani ya maarifa wametaja sababu nyingi za maarifa ambazo ni:

1.     Kujua kutokana na hisia tano: Kujua rangi kwa kuona, sauti kwa kusikia, harufu kwa kunusa, ladha kwa kuonja na ugumu kwa kugusa. Vile vile kuna yale anayoyahisi mtu kwa hisia za kindani; kama njaa, shibe, mapenzi nachuki.

2.     Kupata maarifa kutokana na uchunguzi na majaribio.

3.     Kujua kwa misingi ya kikawaida; yaani kushirikiana na kukubaliana akili zote; mfano: Moja na moja ni mbili; na chenye kunufaisha ni bora kuliko chenye kudhuru. Au kujua kutokana na majaribio; kwa mfano kuamua kwamba kila kipande cha chuma ni kigumu, baada ya kujaribu kipande kimoja tu. Kwa hiyo hukumu inaenea kwa vyuma vyote lakini maarifa yametokana na majaribio ya kimoja.

4.     Kujua bila ya kupata maalumati yoyote ya hisia, majaribio au nguvu ya akili; bali kupata moja kwa moja. Hilo ni baada ya jitihadi ya kuitakasa nafsi na uchafu; kama wasemavyo masufi. Kwa ufasaha zaidi ni kwamba moyo mbele za msufi ni kama akili kwa wengine. Kama ilivyo akili kutambua baadhi ya vitu vingine kwa kujitahidi na kuangalia vizuri, basi hivyo hivyo moyo nao hutambua baadhi ya vitu bila ya

15

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

jitihadi ya nafsi; kama kuhisi mapenzi, na chuki. Na hutambua vitu vingine baada ya jitihadi ya nafsi; kama kujua kuweko Muumbaji.

Kwa hiyo jitihadi ya akili kwetu sisi inafanana na jitihadi ya nafsi kwa masufi. Wala hakuna yeyote anayeweza kubishana na sufi katika maoni yake na itikadi yake. Kwa sababu ukimuuliza dalili, atakujibu kwamba imani yangu na elimu yangu inatoka katika dhati yangu peke yake. Na kama ukimuuliza: Kwa nini imani na elimu hii haitokei katika dhati za watu wote? Atakujibu: Kwa sababu wao hawakupitia majaribio ya kiroho niliyoyapitia mimi.

Sisi tunajiweka kando na msimamo wa kisufi, bila ya kufungamana na upande wowote. Hatuwezi kuuthibitisha, kwa sababu tuko mbali na tunavyoelewa na tulivyozowea. Pia hatuwezi kuukanusha, kwa sababu mamia ya wanavyuoni katika kila zama hata katika zama zetu wanaamini kuwako nguvu ya usufi; na kutofautiana kwao kihali, kidini , na hata kilugha.

Hatuna hoja yoyote inayokanusha majaribio ya kiutu kabisa. Inawezekana kuwa majaribio ya kisufi yanafanana na vipindi ambavyo anapata ilham (anafunukiwa) mshairi na msanii, lakini jambo hili linamuhusu yeye peke yake; wala hana hoja kwa mwingine.

GHAIBU (yasiyoonekana)

Kuna vitu ambavyo hakuna njia ya kuvijua kwa hisia, majaribio au nguvu ya akili, kama vile Lawhin Mahfudh (ubao uliohifadhiwa), Malaika, Iblis, Hisabu ya kaburi, Pepo na Moto.Vile vile miujiza ya Mitume; kama fimbo kugeuka kuwa nyoka, kufufua watu, n.k. Akili haiwezi kugundua mambo hayo wala hatujayaona. Yote hayo ni makusudio ya ghaibu katika neno lake Mwenyezi Mungu: "wanaamini ghaibu".

Kwa hiyo ghaibu ni ile ambayo haijulikani isipokuwa kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia katika ulimi wa ambaye umethibitika Utume wake. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na kwa Mwenyezi Mungu ziko funguo za siri hapana azijuaye ila Yeye"

(6:59)

16

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa hali hii, inatubainikia kuwa kuamini ghaibu ni sehemu ya Uislamu, na kwamba asiyeiamini sio Mwislamu. Vile vile inabainika kuwa jambo ambalo halijulikani kwa kuona, majaribio au akili; au lisilosimuliwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu wala mapokezi ya Mtume, basi litakuwa ni katika vigano. Na vigano vingi vinatokana na mapokezi ya Mayahudi na mfano wao.

DINI NA ELIMU

Jambo la kushangaza ni kwamba hata wale wanaoamini kuwa ulimwengu umepatikana kibahati (sadfa), pia wanaamini ghaibu. Kwa sababu hakuna anayekataa kwamba kuamini sadfa ni ghaibu. Kwa vile hawakuiona hiyo sadfa kwa macho. Kwani wao wamepatikana baada ya kuja ulimwengu. Vile vile hawawezi kuijua kiakili; kwa vile akili bado haijaifanyia majaribio ya kukanusha au kuthibitisha.

La kushangaza zaidi ni kwamba wao wenyewe wanakadiria kuwa ulimwengu umepatikana kutokana na mada ndogo inayoitwa ether. Na hilo wanaliamini kwa imani isiyokuwa na shaka yoyote; kisha wanawakataza wengine wasiamini kupatikana nguvu yenye hekima yenye kupangilia vizuri mambo kwenye ulimwengu huu; ingawaje huku ndiko kuliko karibu zaidi na akili na moyo kuliko kufikiria kitu kipofu na kiziwi.

Kwa vyovyote iwavyo, ghaibu inajieleza kwa jina lake; inafahamika kwa wahyi tu, na sio kwa majaribio wala kwa nguvu ya kiakili. Sharti lake pekee ni kutopingana na akili, sio kutambuliwa na akili. Kwa hali hiyo basi, elimu ya sayansi haina nafasi ya kuwa juu ya wahyi.

Umuhimu wa elimu ya sayansi unakuwa katika kumsaidia binadamu kujua hali ya maumbile na kuyatumia, na ni jawabu la kujua ni nguvu gani zinazofanya asili ya vitu, mimea na wanyama na vipi tutaunda ndege zinazokimbia kuliko sauti.

Sayansi haitambui ni nani aliyesababisha kupatikana maumbile (Nature) na utaratibu wake. Ama dini inatuambia sababu za kupatikana, na inatupa funguo kuu za kumjua aliyeumba ulimwengu na kutuongoza kwenye lile tunalohitajika kulifanya katika maisha haya, ili tuhakikishe kufikia lengo letu la kiroho na la kimaada (kimwili.)

Viwanda au kilimo peke yake, au vyote kwa pamoja haviwezi kutekeleza matakwa yote ya binadamu na malengo yake. Kwa sababu mtu sio mwili tu; bali ni mwili, roho, mawazo na fikra. Katika mwili wa binadamu kuna

17

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

rehema yenye kuenea iitwayo utu, na nuru yenye kuenea iitwayo akili ambayo inaufanya ulimwengu mkubwa uwe mdogo mbele yake.

Mahitaji yetu ya hisia, kama vile kula kunywa na kulala yamekuwa ni lazima kwetu, wala hatuna hiyari ya kuyaacha. Kwa hivyo tutake tusitake ni lazima tuyahangaikie; wala hakuna tofauti katika hilo kwa mjuzi au kwa asiyekuwa na ujuzi, kwa Mtume au asiyekuwa Mtume. Lakini mahitaji ya kiroho yanatofautiana kulingana na watu. Mara nyingi sana mtu huvunja matakwa yake, mapenzi yake na ghadhabu - jambo ambalo ni bora kabisa - lakini mtu hawezi kuacha mahitaji ya mwili wake.

Zaidi ya hayo, lau ingekuwa mtu ni mwili tu, ungeliweza kuhukumiwa na wataalamu wa sayansi, kama wanavyohukumu maada. Na wangeliweza kujua siri za nafsi na undani wake. Vile vile wangeliweza kubadilisha ukafiri kuwa imani na imani kuwa ukafiri; mapenzi kuwa chuki na chuki kuwa mapenzi; uzee kuwa ujana na ujana kuwa uzee, na mengineyo ambayo yanaweza kujaza kurasa. Natarajia kulifafanua zaidi suala hili katika sehemu zake zinazohusika nazo.

Makusudio ya maelezo haya ni kuonyesha kuwa maudhui ya elimu ya sayansi ni mbali na maudhui ya dini na wahyi. Sayansi ni maudhui ya kimaada yenye kuganda au kukua; na lengo lake ni kugundua nguvu za kimaada. Ama dini ni maudhui ya maisha ya binadamu kwa pande zake mbili za kimaada na za kiroho. Ukipenda unaweza kusema: maisha ya kiroho na ya kimatendo. Na lengo lake ni kutaka watu wote waishi maisha ya kuridhisha yenye ufanisi.

Ndio! Uislamu unaheshimu akili na elimu yenye manufaa, na unahimiza kuitafuta; bali unaizingatia kuwa ni wajibu kwa mwanamume na mwanamke. Elimu inawainua watu kupanda daraja. Kwa ajili hiyo basi ni wajibu juu ya Mwislamu kuitakidi kwamba hakuna kitu sahihi katika elimu au akili kinachopingana na Uislamu, wala hakuna kitu katika hukumu za Kiislamu kinachopingana na elimu au akili. Lakini sio kuwa akili inaweza kujua hukumu zote za dini.

Unaweza kuuliza:"lmethibiti Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.) aliposema: "Msingi wa dini yangu ni akili." Je, hiyo si inaonyesha kwamba akili inajua hukumu zote za dini ya Kiislamu?"

Jibu: Uislamu unaanzia kwenye Uungu na Utume. Na kutokana na mawili hayo ndio yanachimbuka mafundisho yake na hukumu zake. Na njia ya kuyajua hayo ni akili. Kwa hivyo, maana ya Hadith tukufu ni kwamba Uislamu ambao misingi yake ni Uungu na Utume, unategemea

18

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

akili kuuthibitisha huo Uungu na Utume, sio kuigiza na kufuata kama kipofu tu, au kufuata hekaya na vigano.2

Na wanasimamisha swala

Mara nyingine serikali inaweza kumhukumu mtu kubaki katika mji fulani bila ya kutoka, na humlazimisha kupiga ripoti kituoni kwa ajili ya kuthibitisha kuweko kwake. Kama akihalifu basi atatakiwa kujibu. Uislamu umemwekea mumin sharti maalum, atakaloweza kwalo kuthibitisha imani yake kwa Mwenyezi Mungu Aliyeumba mbingu na ardhi kila siku mara tano, na kumfanyia ikhlas katika amali zake zote. Qur'an inasema:

"Hakika mimi nimeulekeza uso wangu kwa yule Aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimeacha dini zote za upotevu na mimi si miongoni mwa washirikina."

(6:79)

"Sema hakika swala yangu na ibada zangu (zote) na uzima wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote. Hana mshirika, na hayo ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa waislamu ."

(6:162-163)

Mwenye kuiacha swala kwa kuikana, basi ameritadi; na mwenye kuiacha kwa kupuuza atakuwa fasiki mwenye kustahili adhabu. Ndipo tunaikuta tafsiri ya Imam Ali (a.s.) katika Nahjul-Balagha "Hakika Mtume ameifananisha swala na chemchemi ya maji moto iliyoko mlangoni kwa mtu; akiwa anaoga katika chemchemi hiyo mara tano kila siku hawezi kubakiwa na uchafu wowote." Yaani kudumisha swala kunautakasa

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hujulikana kwa akili kutokana na njia ya ulimwengu. Na utume hujulikana kwa akili kutokana na miujiza.

19

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

moyo kutokana na kuritadi na ufasiki; kama unavyotakasika mwili kutokana na uchafu. Je, kuna uchafu unaoshinda ukafiri na ufasiki?

Na hutoa katika yale tuliyowapa

Kutoa hapa, kunakusanya yote anayoyatoa mtu katika njia ya kheri, iwe ni zaka au kitu kingine. Hakuna mwenye shaka kwamba kutoa kwa njia ya heri ni jambo zuri. Lakini je, kunapasa katika mali kutoa kitu kingine zaidi ya zaka na khums?

Zimepokewa Hadith kwa upande wa sunni; kama vile kutoka kwa Tirmidhi, na kwa upande wa Shia; kama ilivyopokewa katika Al-Kafi; kwamba katika mali, iko haki nyingine. Imam Sadiq (a.s.) ameifasiri haki hiyo kuwa ni kitu anachotoa mtu katika mali yake akitaka atoe zaidi au kichache kwa kiasi cha vile anavyomiliki. Ametoa dalili Imam, kwa Aya isemayo:

"Na ambao katika mali zao mna haki maalum (ya kupewa) masikini aombaye na anayejizuiya kuomba"

(70:24-25)

Wanavyuoni wengi wamelichukulia hilo kuwa ni sunna na wala sio wajib; isipokuwa Sheikh Saduq katika Shia. Imenukuliwa kutoka kwake kwamba zaidi ya zaka na khumsi, kuna haki nyingine iliyo ya lazima katika mali, inalazimika kuitoa kwa kiwango anachomiliki mtu; kingi au kichache.

Vyovyote iwavyo, jambo ambalo halina shaka ni kuwa kutoa mali kwa njia ya kheri ni kujitwaharisha na uchafu na kujiokoa na adhabu ya moto. Mwenyezi Mungu anasema:

"Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na kuwatakasa kwazo."

(9:103)

Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako

20

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad (s.a.w.). Makusudio ya yaliyoteremshwa kwako, ni Qur'an na Hadith. Kwa sababu, yeye Mtume (s.a.w.):

"Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi uliofunuliwa (kwake)."

(53:3-4)

"Na anachowapa Mtume kichukueni, na anachowakataza jiepusheni nacho"

(59:7)

Makusudio ya yaliyoteremshwa kabla yako, ni yale yaliyoteremshiwa Mitume waliotangulia; kama vile Zaburya Daud, Tawrat ya Musa na Injil ya Isa. Lakini hakuna athari yoyote hivi leo ya vitabu hivi kwa upande wa kiamali. Kwa sababu katika itikadi ya Waislamu ni kwamba, ama vitakuwa havipo au yale yaliyopo yamepotoshwa kabisa. Tuwaachie wenyewe wakristo mambo yanayofungamana na Injil.

Nimesoma katika kitabu kinachoitwa Voltar kilichotungwa na Johstone Lanson, na kufasiriwa na Muhammad Ghanimi Hilal ukurasa wa 193 chapa ya 1962. Ninamnukuu: "Inajulikana kuwa idadi ya Injili hizi ni hamsini na nne na Injili nne ziliandikwa baadaye na ya nne ya Luka, ndiyo ya mwisho."

Amesema Elias Najma katika kitabu Yaasu' Almasih (Yesu Masih) ukurasa 11 chapa ya 1962: Mitume (anakusudia wanafunzi wa Masih) walipoona kuwa ni dharura kukusanya mafundisho ya Mola na mafundisho mengine, ndipo wakaona waandike baadhi ya mafundisho, matendo na miujiza. Hiyo hasa ndiyo tunayoiita Injili iliyoandikwa. Kwa hivyo imekuja Injili moja katika sura nne."

Huku ni kukiri wazi kwamba Injili nne sio kiini hasa cha wahyi wenyewe na herufi zake; kama ilivyo Qur'an; isipokuwa ni kunakili kwa mapokezi kutoka kwa Masih (a.s.); kama vilivyo vitabu vya Hadith kwa Waislamu, ambao wamekusanya kauli za Muhammad (s.a.w.), matendo yake na miujiza yake. Tofauti ni kuwa wapokezi wa Injil ni wanne: Mathayo, Yohana, Marko na Luka. Wao ni wenye kuhifadhiwa na kufanya madhambi na makosa, kama

21

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wanavyodai wakristo na kwamba haifai kutia ila mapokezi yao. Lakini Waislamu hakuna (Isma) kuhifadhiwa na dhambi kwa wapokezi wa Hadith; bali haifai kuchukua na kutumia mapokezi yao ila baada ya kuchunguza na kuhakikisha.

Hakuna tofauti katika mantiki ya kiakili kati ya Injili nne na vitabu vya Hadith. Inawezekana kuvitoa makosa, madaamu tu ni kunakili kutoka kwa mtu. Ama tofauti ya Qur'an na Injil iko wazi. Kwa sababu vizazi mbali mbali vimeshindwa kuleta angalau sura moja tu iliyofanana na Qur'an.

Elias amejaribu kuzuia mushkeli huu kwa kauli yake katika ukurasa wa 12: "Kanisa linatolea ushahid Injili, na Injili inalishuhudia kanisa. Vyote viwili vinathibitishiana."

Ni wazi kwamba hivyo ni kuthibitisha madai kwa madai yenyewe. Ni sawa na anayesema: "Mimi ni mkweli katika madai yangu kwa sababu mtu fulani ananishuhudia kuwa mimi ni mkweli," kama akiulizwa, "Ni nani anayeshuhudia kuwa huyo mtu fulani ni mkweli? Atasema: "Mimi ninashuhudia kuwa yeye ni mkweli." Kwa maana hii anakuwa shahidi ndiye huyo huyo anayedai. Aina hii ya maneno wanafalsafa huiita 'mzunguko wa kubabaisha akili.'Kama vile Mshairi mmoja alivyosema:

Kigeugeu kutuka, Kati yangu na muhibu Lau si mvi kuzuka, Habiba singenighibu Na asingeniepuka, Mvi singeniswibu.

Ubeti wa mwisho, kama unavyouona, unafanana na kupagawa na akili. Kwa sababu, maana yake ni kuwa kuondoka mpenzi wa mshairi kumetokana na huyo mshairi kuota mvi; na kwamba huko kuota mvi kwake kumesababishwa na kuondoka mpenzi wake.

Kwa hivyo kuondoka na kuota mvi ni visababishi kwa wakati mmoja; kama kusema: Nimeshona nguo ili niivae na nimeivaa ili niishone.

6. Hakika wale ambao wamekufuru ni sawa wao ukiwaonya au

Katika gazeti An-Nahaar la Beirut la tarehe 12.7.1964 kuna makala ndefu yenye maelezo kwamba wataalamu na wakikristo wamethibitisha kwa majaribio na kwa kompyuta kwamba barua nyingi zinazonasibishiwa Paulo, mwasisi mkubwa wa ukiristo, ni uongo.

22

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza usiwaonye, hawataamini.

2 Sura Al-Baqarah

7. Mwenyezi Mungu amepiga muhun juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana kifuniko, basi watakuwa na adhabu kubwa.

NJIA YA UISLAMU

Aya 6-7

Ukiwaonya au usiwaonye

Yameshatangulia maelezo kuwa mafun-disho na misingi ya Kiislamu yapo aina mbili: Itikadi na amali; yaani mizizi na matawi; au itikadi na sharia: Vyovyote utakavyoita ni sawa. Maudhui ya kiitakadi yanaambatana na nafsi ya mtu na hisia zake, na maudhui ya sharia ni amali za mtu na vitendo vyake. Uislamu umetoa mwito wa kuuamini kiitikadi na kisharia.

Njia ambayo Uislamu umefuata kueneza mwito wake katika mambo yanayoambatana na itikadi, imebainishwa katika Aya hii.

"Waite kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka."

(16:125)

Makusudio ya hekima na mawaidha mazuri, ni kutegemea akili ambayo inaweza kuyafahamu, kama vile Uungu ambao binadamu anaweza kufikia kujua kwa kuangalia vitu na kupeleleza katika maumbile na maumbile ya mbingu na ardhi. Vile vile Utume wa Muhammad (s.a.w.) ambao watafiti wanaweza kuujua kutokana na sera yake na mfumo wa risala yake.

Ama njia ya Uislamu katika kujua yale ambayo akili pekee haitoshi kama vile ghaibu, basi inabidi kutegemea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu

23

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kupitia kwa Mtume ambaye Utume wake unathibitishwa na dalili za kiakili na ukweli wa yale anayoyaeleza kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Ama njia ya kuthibitisha sharia ni kitabu (Qur'an), Sunna (Hadith) na akili. Misingi mitatu hii inakusanyika juu ya masilahi na ufisadi, wema na uovu au uadilifu na dhuluma, vyovyote utakavyopenda unaweza kuita.

Mwenyezi Mungu anasema:

"...Na kuwahalalishia vizuri na kuwaharimishia vibaya na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao..."

(7:157)

"Wanakuuliza wamehalalishiwa          nini,          sema;

mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri..."

(5:4)

"...na tukawapelekea wahyi kufanya heri..."

(21:73)

"Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, na kufanya hisani, na kuwapa jamaa na anakataza uchafu na uovu na dhulma"

(16:90)

Kwa ufupi ni kuwa katika itikadi kuna yanayotegemea akili na yanayotegemea wahyi. Hukumu za sheria ziko katika masilahi na mambo ya uharibifu.

24

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Wameuitikia Uislamu na mwito wake walioamini yasioonekana, na wakatoa zaka; na wameyakataa hayo makafiri na wanafiki. Mwenyezi Mungu amewataja waaumini kwanza katika Aya zilizotangulia, pili ametaja makafiri na tatu anawataja wanafiki na sifa zao; kama zitakavyoeleza Aya zinayofuatia hizi.

Mwenye kulazimiana (kushikamana) na haki.

Watu katika kulazimiana na haki na kuacha kulazimiana nayo wako aina mbili: Wa kwanza ni yule anayelazilimiana nayo kwa njia ya haki, ni sawa iwe imeafikiana na lengo lake au imetofautiana nalo, bali yeye hana matakwa yanayotofautiana na haki; na kwa ajili ya haki anajitolea mhanga na kuvumilia mashaka, sawa na mgonjwa anayevumilia uchungu wa dawa na maumivu ya mkasi kwa kutaka afya.

Wa pili ni yule ambaye hajilazimishi na kitu chochote wala hakina thamani chochote mbele yake isipokuwa kile chenye kuafikiana na matakwa na mapenzi yake. Wala hajali ufafanuzi wowote hata kama uko sawa. Huyu mwenye kujipurukusha na haki atakuwa na moja ya mambo mawili: Ama atakuwa anajipurukusha na haki kwa ndani na nje (katika moyo na katika ulimi wake) au atakuwa anajipurukusha kwa ndani tu sio nje, basi huyu wa kwanza ni kafiri na wa pili ni mnafiki kama inavyojulikana katika Qur'an. Mwenye kulazimiana na haki anatofautiana na asiyelazimika nayo kwa njia nyingi. Miongoni mwa njia hizo ni kama hizi zifuatazo:

Mwenye kulazimiana na haki anatambua majukumu yake, lakini asiyejilazimisha, hayatambui.

Mwenye kushikamana na haki haamini kitu isipokuwa pamoja na dalili yenye kukinaisha, lakini asiyeshikamana nayo haamini kitu kinachoitwa dalili, hoja au mantiki yoyote. Jema kwake sio jema ila lile analolikusudia yeye. Hata kama akikosea hajirekebishi bali anaendelea kuliboresha lile alilolikosea.

Mwenye kulazimiana na haki anatoa nafasi kwa mpinzani, anamsikiliza na anakuwa tayari kujirekebisha akiona amekosea. Hiyo ndiyo maana ya neno lake Mwenyezi Mungu:

'Ambao husikiliza kauli wakafuata zile zilizo nzuri zaidi..."

(39:18)

25

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Lakini kwa mtu asiyelazimiana na haki kwake ni kama kisa cha 'Paa huruka'.4

Mwenyezi Mungu amewafananisha wale wanaokakamia kwenye upotevu wao kwa ibara ya undani na akaielezea katika Aya nyingi tukufu kama hii.

"Na wakasema; nyoyo zetu zi katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na katika masikio yetu mna uziwi na baina yetu na wewe kuna pazia, basi fanya (yako) na sisi tunafanya (yetu)"

(41:5)

Mwenye kushikamana na haki anasamehewa makosa yake kama akikosea baada ya kufanya utafiti na upekuzi, lakini mwengine hakubaliwi udhuru; na malipo yake ni laana na adhabu. Watu wengi zaidi hawaamini wala hawaridhii isipokuwa maslahi yao yanayowahusu tu kwa njia wanayoijua au wasiyoijua. Utamkinaisha vipi mjinga kuwa, mtukufu zaidi wa watu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemcha Mungu zaidi, na hali yeye mwenyewe anajitukuza kwa nasabu yake? Au utamkinaishaje mtawala kwa uadilifu wakati ambapo utawala wake umesimamia dhuluma? Au utawezaje kumkinaisha mlanguzi kwa uharamu wa ulanguzi wakati ukiwa huo ulanguzi ndio msingi wa utajiri wake?

Wote hao wanaoivunja haki ndio aliowakusudia Mwenyezi Mungu kwa kusema:

"Ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye hawatoamini."

Unaweza kuuliza, itakuwaje kuhusu wale ambao hawako katika kundi la wale wanaoshikamana na haki na wale wasioshikamana nayo, kama vile wajinga wanaodhania mambo tu, ambao wanafanya haraka kusadiki bila ya hoja wala dalili yoyote isipokuwa wanafanya hivyo kujilinda na kutaka usalama tu?

Inasemekana kuwa watu wawili waliona kitu kwa mbali, mmoja akasema : "Yule ni paa." Mwengine akasema: "Hapana ni kunguru" Baada ya muda kidogo yule kunguru akaruka. Yule aliyepata, akamwambia mwenzake, Waona?" Yule aliyekosa akasema: "Ah! ni paa tu ijapokuwa ameruka!" ndio ikawa ni mithali.

26

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                         2 Sura Al-Baqarah

Jibu: Hakika hao ni kama wendawazimu na wanyonge.

\                                                4

"Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe, Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwingi wa maghfira."

(4.99)

Swala la pili, kwa dhahiri kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao", ni kwamba amewazuia kuamini na kufuata haki. Kwa hivyo inakuwa kafiri amelazimishwa na hana hiyari basi hastahiki shutuma wala adhabu?

Jibu: Kila kitu ambacho hakina manufaa yoyote na wala hakitekelezi matakwa kinakuwa ni sawa tu, kiwepo au kisiwepo. Lengo linalokusudiwa kwa moyo ni kunufaika na kuongoka kwa dalili zilizo sahihi, kama vile ambavyo lengo la kusikia ni kunufaika na sauti zinazosikika, na lengo la macho ni kuona vinavyoshuhudiwa.

Kwa hivyo, zikiweko dalili za kutosha juu ya hakika na mtu akawa anaendelea kung'ang'ania upotevu wake, hiyo inamaanisha kuwa hakunufaika na moyo wake, na moyo wake haukunufaika na yale yanayotakikana kunufaika nayo; mpaka inakuwa kama vile ameumbwa bila ya moyo au kwa moyo uliofungwa, haufunguki kwa haki. Kwa hivyo, inajuzu kusifiwa mtu mwenye moyo uliosusuwaa kuwa yeye hana moyo. Mwenyezi Mungu anasema:

ü\

"Hakika katika hiyo mna ukumbusho kwa mwenye moyo au kwa ategaye sikio, naye mwenyewe yupo anashuhudia."

(50:37)

Ingawa moyo upo, lakini sio kitu maadamu uko mbali na uongofu. Kwa hivyo inakuwa kunasibishiwa Mwenyezi Mungu kupiga muhuri nyoyo zao ni kwa njia ya 'majazi' sio ya hakika. Hayo yanatiliwa nguvu na maelezo ya kifuniko, kwani tunaona hakuna kifuniko katika masikio na macho ya makafiri. Hivyo basi hakuna muhuri wa kikweli katika nyoyo. Ama yale masuala ya Jabr na Ikhtiyar (kulazimishwa na hiyari) kwamba je, mtu analazimishwa au ana hiyari, utakuja ufafanuzi wake Inshallah.

27

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

8.    Na kuna katika watu wasemao: Tumemwamini             Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.

9.    Wanataka             kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.

10.  Nyoyoni mwao mna maradhi na Mwenyezi                         Mungu amewazidishia maradhi, basi watakuwa na adhabu iumizayo kwa sababu ya kule kusema kwao uongo.

11.  Na wanapoambiwa msifanye ufisadi katika ardhi husema, bali sisi ni watengezaji tu.

12.  Hakika wao ndio wafisadi, lakini hawatambui.

13. Wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu, husema: Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu. Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawaju

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kvvanza

2 Sura Al-Baqarah

14.   Na wanapokutana na walioamini husema, tumeamini na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi tunawacheza shere tu.

15.   Mwenyezi Mungu atawalipa shere yao na kuwaacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo.

16.   Hao ndio walionunua upotofu kwa uongofu, lakini biashara yao haikupata faida wala hawakuwa ni wenye kuongoka.

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka            moto,            na

ulipoyaangaza yaliyo pambizoni mwake, Mwenyezi Mungu akaondoa nuru yao hiyo na kuwaacha katika kiza hawaoni.

18. Ni viziwi, mabubu (na) vipofu kwa hivyo hawatarejea.

19. Au ni kama mvua kubwa itokayo mawinguni, ndani yake mkawa na giza na radi na umeme, wakawa wanatia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, na kuogopa kufa.

29

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Na           Mwenyezi           Mungu

amewazunguka hao makafiri.

20. Unakaribia umeme huo kunyakua macho yao, kila unapowaangazia hutembea ndani yake na unapowafanyia giza husimama. Na lau Mwenyezi Mungu angetaka, angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.

WANAFIKI

 Aya 8-20

Kwanza Mwenyezi Mungu amewataja waumini, hao ni ambao wameifanyia ikhlas haki kwa ndani na nje. Kisha akawataja makafiri ambao wamefanya ukafiri ndani na nje.

Hivi sasa imekuja zamu ya wanafiki ambao wamedhihirisha Imani na kumbe sio waumini; kufuru ya hawa ni chafu zaidi ya ukafiri na ameichukia zaidi Mwenyezi Mungu; ndio maana Mwenyezi Mungu amewataja sana katika Aya kumi na tatu, wakati ambapo amefupiliza kuwataja makafiri katika Aya mbili tu.

Si hivyo tu, bali hata ameteremsha Sura maalum ya wanafiki. Aya hizi ziko wazi kabisa hazihitaji taawili wala ufafanuzi; ni kama Aya inayosema:

"Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu"

Kwa hivyo tutatosheka na maelezo haya yanayofuatia:-

(33:54).

30

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza Nl NANI MNAFIKI?

2 Sura Al-Baqarah

Kila mmoja wetu anataka awe anatajika katika watu; angalau watu wasimpinge katika mambo yake wala wasimtusi; hasa ikiwa maisha yake na kazi yake inategemea watu watakavyomwamini. Kwa hivyo basi mtu wa namna hii siku zote anakuwa na shaka hata kama halikutokea jambo la kumtilia shaka, ijapokuwa kuna kawaida ya kuchukulia usahihi juu ya kitendo cha Mwislamu.5

Kwa vyovyote iwavyo kila anayewaficha watu, na kujidhihirisha na mambo asiyokuwa nayo na akaogopa siri isifichuke, basi huyo ni mwongo, mnafiki, mwenye kujionyesha na mwenye hadaa; hata kama atapata kuaminiwa na watu wote, bali huko kuaminiwa kunazidisha kosa lake na ni balaa mbele za Mwenyezi Mungu na pia ni balaa mbele za watu siku siri ikifichuka.

Unaweza kuuliza, kama watu wakiitakidi kuwa kitu fulani ni haramu na mtu mwengine akaitakidi kati yake na Mwenyezi Mungu kuwa ni halali, akawa anakifanya kwa kujificha kwa kuogopa maneno ya watu je, atahisabiwa ni mnafiki? Je, ni wajibu awabainishie watu yale anayoitakidi? Je atakuwa ana lawama kama akinyamazia makosa yao?

Jibu: Hakuna ubaya wowote wa kufanya lile ambalo mtu anaitakidi kuwa ni halali; wala hawezi kuhesabiwa kuwa ni katika wanafiki maadamu roho yake imetulia.

Kwa sababu taklifa ya jambo hasa inafungamana na yeye sio watu, bali hata anasamehewa katika makosa. Kwani hakuna dhambi katika kufanya jambo kwa makosa bila ya kukusudia.

Ama kubainisha uhakika ni wajibu kwake kwa upande wa kuamrisha mema na kukataza mabaya; kwa sababu kosa liko katika hukumu sio katika maudhui.6

Maulama wa kifqh wana kawaida waliyoiita kuchukulia usahihi kitendo cha Mwislamu. Kwa mfano umemwona mtu anakunywa maji na hujui ni ya halali au haramu; au ulijua kuwa ni haramu, ukatia shaka je, anakunywa kwa ajili ya dawa au hajui kama ni haramu au anakunywa tu bila ya udhuru wowote? Basi ni lazima uchukulie usawa tu, mpaka idhihiri kinyume.

Ukimwona mtu anakula nyama ya nguruwe na yeye anajua kuwa ni nyama ya nguruwe, lakini hajui hukumu yake ya haramu, basi yakupasa umwongoze kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu. Hali hiyo ndiyo inayoitwa kutojua hukumu.

Ama akiwa anajua hukumu, lakini anaitakidi kwamba nyama hii anayoila ni nyama ya kondoo lakini kumbe ni nguruwe, sio wajibu juu yako kumbainishia, kwa sababu yeye ana udhuru. Wa kwanza huitwa asiyejua hukumu na wa pili huitwa asiyejuwa maudhui.

31

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Aya tulizonazo zinazungumzia wanafiki ambao iliwathibitikia hoja na haki ya Utume wa Muhammad (s.a.w.) lakini waling'ang'ania upinzani tu kwa inadi, kama ilivyokuwa kwa washirikina ambao walifanya inadi na wakapigana vita. Tofauti iliyopo kati ya washirikina na wanafiki, ni kwamba washirikina walitangaza upinzani wao na wakasema wazi:

"Hatuifuati haki kwa sababu mafukara wameifuata" Qur'an inasema:

"Wakasema: Je, tukuamini wewe, hali ya kuwa wanyonge ndio wanaokufuata."

(26:111)

Ama wanafiki wao waliikataa haki kwa sababu moja au nyingine lakini wao walifanya upinzani wakadhihirisha Uislamu kwa woga na hadaa, wakawa ni wabaya zaidi kuliko makafiri. Kwani makafiri udhahiri wao na undani wao ulikuwa sawa tu, kama vile mlevi anavyokunywa pombe njiani. Lakini wanafiki walificha yale yaliyo katika dhamira zao kama mwovu anayevaa nguo za watakatifu.

Hadaa hiyo inafahamisha kuwa mnafiki hana kizuizi chochote cha dini au akili, wala cha haki au uadilifu; dhamiri yake haishtuki maadamu yuko mbali na macho ya watu. Basi mtu wa namna hii ni vigumu sana kurudia kwenye heri.

Kwa hivyo ndio Mwenyezi Mungu amewataja wanafiki katika Aya hizi kwa sifa ya hadaa, kughafilika, maradhi ya moyo na upumbavu. Vile vile kughurika, kufuata matamanio, uchafu na kuendelea na upotevu.

Watu wanawaita kwa jina la wapelelezi, vibaraka waharibifu na wenye kujionyesha.

Watu hao wapo hivi sasa; kama walivokuwa wakati wa Mtume na kabla yake, na wataendelea katika vizazi vijavyo. Lakini ni wenye kulaaniwa popote walipo, hata wakiwa makaburini mwao. Kama wakifaulu basi ni kwa muda. Ama kufaulu kwa wakweli kunaendelea.

Ibara nzuri niliyoisoma kuhusu wanafiki ni kauli ya Muhyiddini maarufu kwa jina la Ibnul Arabi katika Juzuu ya nne ya kitabu Futuhatil-Makkiyyah.

32

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Ni uzuri uliyoje wa aliyoyasema Mwenyezi Mungu: Wanawastahi watu', ambao wana maumbile ya kusahau. 'Na wala hawamstahi Mwenyezi Mungu' ambaye hapotei wala hasahau, afadhali wangelifanya kinyume."

Maana ya ibara hiyo ni kwamba lau mnafiki angelikuwa anafikiria vizuri na akawa anafikiria kidogo na kuwa na akili, angelificha makosa yake kwa Mwenyezi Mungu - kama inawezekana - sio kwa watu. Kwa sababu watu hawawezi kumnufaisha wala kumdhuru. Ambaye ananufaisha na kudhuru ni Yeye (Mungu) peke yake. Kwani watu wanasahau uovu wanaouona; watamzungumzia mwenye uovu huo wakati fulani tu baadaye wanasahau na kunyamaza, kama vile hakukutokea kitu chochote. Tumeona wengi waliofanya madhambi makubwa makubwa yakawafedhehesha mpaka mtu akajificha kutokana na ubaya wa vitendo vyake, halafu baadaye mtu akajitokeza kwa watu, wakakaa naye, wakaamiliana naye kama mtu mwema. Tena pengine wakamtegemea na kumpa cheo kikubwa hata kuweza kusimamia mambo matakatifu ya kidini ambayo hakuyasimamia yeyote isipokuwa Mtume au wasii wake.

Mbali ya kuwa watu husahau pia wanasifu na kutusi kulingana na matakwa yao na matamanio. Kwa hiyo, mwenye akili atamwogopa Mwenyezi Mungu wala hataogopa watu, bali atajichunga yeye mwenyewe na kujiepusha na yale anayoyaonea haya. Na hakuna mtu mwoga kama yule anayefanya kwa siri yale anayoyaonea haya kuyafanya dhahiri.

21. Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amewaumba nyinyi na wale wa kabla yenu; ili mpate kuokoka.

22. Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko busati na mbingu kuwa paa na akateremsha kutoka mawinguni maji, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mwajua.

33

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

MWABUDUNI MOLA WENU Aya 21 - 22

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja waumini, makafiri na wanafiki kwa alama zao na sifa zao na yale yanayofafanua hali zao, aligeukia kuwaambia wote waliobaleghe wenye akili, wawe waumini au la, waliokuwepo wakati wa maneno na watakao kuwepo baadaye, wote aliwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake.

Amri hiyo kwa waumini ni kutaka uthabiti na kuendelea na imani na twaa. Kwa upande wa makafiri na wanafiki ni kuwataka watubie.

Unaweza kuuliza, kwa nini umewajumlisha watakaopatikana, wakati ambapo maneno ni ya ana kwa ana, hayawezi kumhusu asiyekuwepo?

Jibu: Kila jambo lina pande mbili: Upande wa nje ambao unahusika na yule aliyepo tu; kwa mfano kusema: "Ameangamia yule aliye katika jahazi." Upande wa pili ni wa maana ya undani; kama kusema: "Fanyeni uadilifu enyi watawala." Hapa amri itakuwa inafungamana na kila mtawala. Kwa hiyo Aya iko katika upande huu wa pili.

TAWI HUFUATA SHINA

Mwenye kufuatilia Aya za Qur'an na akazifikiria vizuri kwa undani ataona kuwa zikitaja msingi wowote katika misingi ya itikadi; kama Tawhid, Utume au Ufufuo, basi huuambatanisha na hoja na dalili, lakini kama zikitaja hukumu za sheria kama kuharamisha zinaa huwa bila ya dalili yoyote, je kuna siri gani?

Jibu: Kukithibiti kupatikana kwa Muumba na Utume wa Muhammad (s.a.w.) kwa hoja ya kiakili, basi kauli zao zinatosha kuwa ni hoja, wala haijuzu kuzikhalifu kwa hali yoyote. Kwa sababu kukhalifu kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume ni kupinga dalili ya kiakili juu ya Tawhid na Utume.

Yeyote mwenye kuamini na akakubali mashina haya mawili, basi ni juu yake kukubali kila lilothibitishwa na Qur'an na Hadith katika hukumu za sharia na tanzu zake bila ya maswali. Mwenye kuzikanusha hapana haja ya kujadiliana naye katika sharia na tanzu zake. Kwa ajili hiyo Qur'an imejihimu zaidi kuleta dalili juu ya Tawhid, Utume na Ufufuo (mambo ya msingi - shina). Imeanza kwa Tawhid kwa sababu ndio msingi mkubwa. Kwa hiyo anayeamini shina ni lazima aamini tawi la shina hilo.

34

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

TAWHID

2 Sura Al-Baqarah

Dini za Mwenyezi Mungu zote zinasimamia misingi mitatu: Tawhid, Utume na Ufufuo. Hakuna Mtume yeyote kuanzia Adam (a.s.) mpaka Muhammad (s.a.w.) ambaye hakusimamia mambo matatu haya. Yale yanayofuatia yanatokana na hayo. Kwa hiyo uadilifu, kudura na hekima zake ni sehemu ya Tawhid; Uimamu na Qur'an ni sehemu ya Utume; na hisabu pepo na moto ni sehemu ya Ufufuo.

Qur'an tukufu imeanza na msingi wa Tawhid na ikaongoza kwenye dalili Zake; ikiwaambia watu:

Mwabuduni Mola wenu ambaye amewaumba...

Kimsingi ni kwamba kumwabudu Mwenyezi Mungu kunataka kumjua kwanza kwa njia ya mkataa, sio njia ya kudhani kwa sababu dhana haiwezi kuitoshea haki na chochote; kwa ushahidi wa hiyo Qur'an yenyewe.7

Ni njia gani inayopelekea kumjua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa uwazi kabisa?

Wanavyuoni wanahitilafiana katika namna ya njia hii, kila mmoja amethibitisha kwa vile alivyoona ni sawa. Kuna wale waliotegemea dalili ya kilimwengu ambayo wameielezea kwa namna hii ifuatayo:

Hakika maumbile na matukio yake yenye kukaririka na yenye kutokea upya yanahitaji kuweko na sababu yake, na haiwezekani kuwa sababu iwe ni maumbile hayo yenyewe. Kama ingekuwa hivyo, basi ingelikuwa sababu na chenye kusababishiwa ni kitu kimoja; na huo ni mzunguko ulio batili kama tulivyoonyesha katika vifungu vilivyotangulia katika Aya ya 4 ya Surah hii.

Ikiwa sababu iko nje ya maumbile tutauliza; je, sababu hiyo ni natija ya sababu iliyotangulia au ni kwamba imepatikana yenyewe bila ya sababu? Kama kuna sababu, je na hiyo sababu nayo imepatikana na sababu ipi? Hivyo yataendelea maswali; na mlolongo huu wa maswali ni muhali.

Uislamu ni itikadi na Sharia. Itikadi ni kama kumwamini Mwenyezi Mungu na sifa zake; utume na isma yake, ufufuo na mengineyo katika mfano wake yaliyo katika ghaibu. Halithibiti jambo lolote katika masuala ya kiitikadi isipokuwa kwa njia ya mkataa: Ndio maana Ijtihad haiko katika itikadi. Ama sheria; kama vile ibada, mahusiano ya jamii.hukumu za makosa nk.inajuzu kuzithibitisha kwa njia ya dhana na ijtihad kwa sharti ya kuwepo dalili mkataa ya kusihi amali kwa njia hii hasa.

35

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa hiyo, inakuwa ni sababu ya pili ambayo ni kupatikana kwa dhati yake na kwake zinaishia na kukoma sababu zote; wala yenyewe haishilii kwa nyengine, nayo ni tamko la Mwenyezi Mungu, kukiambia kitu "kuwa kikawa" kun fayakun.

Dalili hii inasimamia kukubali nadharia ya sababu (Al-illiyyah) kwamba kila athari lazima iwe na mwenye kuileta athari hiyo na kila sababu ni lazima iwe na mwenye kuisababisha; kama vile elimu lazima iwe imetokana na mwenye elimu, na maandishi lazima yawe yameandikwa na mwandishi.8

Ili tuiweke wazi zaidi fikra ya ubatilifu wa mlolongo, na kulazimika kukomea kwenye sababu isiyokuwa na sababu, tutakupigia mfano: Hii michoro waliyoweka wahandisi wa michoro kwa ajili ya ndege, magari majengo, n.k. haina budi ikomee kwa mgunduzi wa kwanza ambaye ameweka huo mchoro; hata kama wengine wameuchukua kutoka kwake, na wala yeye hakuuchukua kutoka kwa mwingine. Lau tukikadiria kuwa hakuna mgunduzi wa kwanza wa mchoro, basi lazima kusingekweko na ugunduzi wala mchoro.

Kwa hivyo basi haifai kwa yeyote kusema na kuuliza: Mgunduzi wa kwanza aliuchukua wapi huu mchoro? Kwa sababu, maana ya ugunduzi ni kwamba, amegundua yeye mwenyewe bila ya kuchukua kutoka kwa mwingine. Hakika hii inajifahamisha yenyewe, kama linavyojifahamisha jua kwa mwanga wake.

Basi hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa Mwenye kuumba na Mwenye kuruzuku. Maana yake ni kuwa Yeye anaumba, lakini hakuumbwa, anaruzuku lakini haruzukiwi. Ndio ikawa Leibnitz anamwita Mwenyezi Mungu Mhandisi yaani mvumbuzi; Plato naye anamwita Mtengenezaji. Yote hayo ni kuonyesha kuwa yeye ni Muumbaji lakini si Mwenye kuumbwa.

Wengine wanatolea dalili ya kuweko Mwenyezi Mungu kwa nidhamu ya ulimwengu na kupangika kwake kunakaoendelea. Dalili hiyo inaitwa dalili ya ukomo 'Al-ghai'.

Mwanafalsafa mmoja wa Kiingereza anayeitwa Hume anakanusha misingi ya sababu kwa kusema: "Hakuna dalili kwamba kupatikana kitu lazima kuwe na sababu." Hatuna la kujibu kauli hii zaidi ya kusema kuwa kuondoa msingi wa sababu nikuondoa msingi wa akili za watu wote. Hakuna yoyote anayeweza kufikiria kupatikana kitu bila ya sababu.

36

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

MAELEZO

2 Sura Al-Baqarah

Wataalamu wengi wapya wa elimu ya maumbile wanaona dhahiri ya maumbile haifai kuifasiri kwa sababu ya ukomo wake, bali ni lazima kuifasiri kwa sababu za kiutendaji.

Jibu: sisi tunagundua kupatikana sababu ya kitendo kwa kupatikana sababu ya ukomo wake sawa na vile tunavyogundua seremala hodari kutokana na kupangika kitanda kifundi. Jibu linaweza kufunuka zaidi kutokana na maelezo yajayo.

Kuna wengine waliotegemea wataalamu wa elimu ya maumbile na wengineo katika kugundua hakika nyingi. Kutokana na makadirio haya ndio ikaja nadharia ya mvutano (Force of gravity) aliyogundua Newton kutokana na kuanguka tofaa juu ya ardhi. Kwamba makadirio yote yasiyokuwa mvutano ni batili na makadirio ya mvutano ni sahihi.

Ama kuifuatilia dalili hii juu ya suala tulilonalo, ni kwamba sisi tunashuhudia nidhamu ya ulimwengu na mshikamano wake unaoendelea; kila tunavyokadiria kuwa nidhamu hii imepatikana bila ya Muumba mwenye hekima, basi hayo ni makadirio ya kipuuzi yasiyokubaliwa na akili, wala haikubali akili isipokuwa lazima awepo Muumbaji mwenye hekima na kuwa yeye ndiye ambaye amepangilia. Hebu angalia mfano huu:

Kama ukiona jina lako limeandikwa angani kwa herufi za nuru; halafu usimwone mtu yeyote, huna budi kukadiria kuwa kuna mtu mwenye akili ana chombo kinachomwezesha kuchora herufi za nuru zenye kushikamana katika anga. Ni makadirio gani yasiyokuwa haya yanayowezwa kukadiriwa? Sadfa au kugongana gari mbili au kupatikana volkano, yote hayo yanakupeleka kwenye makosa. Akili yako haiwezi kutulia isipokuwa utakadaria tu kuwa kuna aliyefanya hivyo. Basi hivyo ndiyo ilivyo kuhusu ulimwengu.

Neno la kufikiria na lililo wazi zaidi ni lile la Voltaire aliposema: "Hakika fikra ya kuwepo Mwenyezi Mungu ni dharura. Kwa sababu fikra inayopinga hiyo ni upumbavu."

Nimesoma kitabu "Adhahiratul-Qur'aniyya" ukurasa wa 91 chapa ya 1958. "Kuna aina fulani ya sisimizi katika Amerika huondoka nyumbani mwao kabla ya kulipuka moto kwa usiku mmoja." Vyovyote utakavyokadiria katika makadirio yote na tafsiri zote, haiwezi kutulia nafsi yako milele isipokuwa kwa kukadiria kupatikana mwenye kuzingatia vizuri mambo, mwenye hekima aliyeipa kila nafsi mwongozo wake.

37

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Wengine wanategemea dalili ya kimaumbile na wanasema: "Lau si Imani ya kupatikana Mwenyezi Mungu yangeliangamia makadirio yote ya kimaumbile na kusingelikuwa na wa kuwaepushia watu shari wala kusingelikuwa na wa kuwafahamisha heri."

Dalili hii iko karibu zaidi na kukanusha kuliko kuthibitisha, kwani inaonyesha kuwa kumwamini Mwenyezi Mungu na hali hii ni wasila na sio lengo, kiasi ambacho lau ingekadiriwa kupatikana mtu anayefanya yale yanayotakikana kuyafanya na kuacha yale yasiyotakikana kuyafanya, basi asingelikuwa na wajibu wa kumwamini Mwenyezi Mungu. Hakuna mwenye kutia shaka kuwa kumfanya Mwenyezi Mungu ni chombo tu ni kubaya zaidi kuliko kumkanusha.

Wengine hutegemea dalili ya hisia ya moyo; nayo ni hisia za moyo moja kwa moja. Wanasema kuwa moyo wa mtu unapata kumjua Muumbaji moja kwa moja bila ya dalili yoyote, sawa na vile unavyohisi mapenzi na chuki. "Yamekw-ishatangulia maelezo kuhusu hayo katika tafsiri ya Aya ya 3, kifungu cha maarifa.

Njia bora zaidi ya zote ni ile aliyoitolea dalili Mwenyezi Mungu juu ya kupatikana Kwake. Kwa ufupi ni kuangalia na kufikiri katika kuumbwa mbingu na ardhi, mtu, mauti na uhai na neema kubwa. Na mengineyo yaliyokuja katika Qur'an tukufu, hadith za Mtume na Nahjul-Balagha.

Ingawaje dailili hii hakika yake inarudi kwenye dalili ya Kawni (kupatikana ulimwengu) na dalili ya Al-ghai (ya ukomo), lakini mpangilio wa maelezo unafahamika upesi na unaweka karibu zaidi kufahamu vitu mahsusi na vya kiujumla. Asiyekinaika na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa dalili za kupatikana Kwake alizozileta yeye mwenyewe, je anaweza kukinaishwa na mtu aliye mfano wake?

Ajabu ya maajabu ni kwamba anayemkanusha Mungu anaamini kabisa na kuitakidi kuwa shati alilolivaa - kwa mfano - limetokana na mbegu aliyoipanda mkulima kwa mpangilio; akaifuma mfanya kazi kwa umakini, akaiuza mfanya biashara kwa maarifa, baadaye mshonaji akaipasua na akaishona kwa kipimo kinachohitajika. Lakini haamini kupatikana aliyetengeneza vizuri huu ulimwengu na kila kitu.

Kwa kuongezea dalili ya kuweko Mwenyezi Mungu ambayo inaingia kwa ujumla, ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa kila mtu dalili ya kuwepo yeye Mungu inayomuhusu yeye tu bila ya kushirikiana na mwingine. Mtu yeyote, vyovyote vile atakavyokuwa, akikumbuka mambo na majaribio yaliyompitia, na kama akiyapeleleza ni lazima atakuta katika

38

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

maisha yake amepitiwa na vitu visivyo na maelezo yoyote isipokuwa matakwa ya Mwenyezi Mungu tu.

Mimi sikubali kabisa kuwa kuna mtu yeyote vyovyote alivyo, ijapokuwa ni kafiri, kuwa anaweza kuishi kipindi fulani cha maisha bila ya kupitiwa na kipindi kimoja katika maisha yake asiweze kumrejea Mwenyezi Mungu tena bila ya kukusudia wala kutambua. Atamwuelekea nani katika kipindi cha shida? Bila shaka atarudi katika maumbile ya Mwenyezi Mungu aliyowaumbia watu na yakapiga chapa kwa kila mwenye kuzaliwa, ambayo si baba anayeyajua wala mama.Mzandiki mmoja alimuuliza Imam Jafar Sadiq (a.s.): "Ni ipi dalili ya kuweko muumbaji?" Imama akamwambia: "Lau unapanda chombo na mabaharia wote wakafa ukabaki wewe peke yako, je utakuwa unataraji kuokoka?" Mzandiki akasema: "Ndio" Imam akasema:"Hakika muumbaji (Mungu) ndiye yule utakayemtarajia wakati huo."

Basi mimi ninampa nasaha yule anayetia shaka ya kuweko Mwenyezi Mungu asome dalili za wakanushaji na watu wa maada, bila shaka yoyote ataishilia kwenye kumwamini Mwenyezi Mungu; ambapo atakuta dalili ya kukanusha ni kwamba wao wanataka kumwuona Mwenyezi Mungu kwa macho na kumgusa kwa mkono na kumnusa kwa pua.

Nimetaja dalili nyingi sana katika maudhui haya katika kitabu Mwenyezi Mungu na akili na Falsafa ya mwanzo na marejeo ambacho nilikihusisha na kujibu Falsafa ya kimaada Vile vile katika kitabu Baina ya Mwenyezi Mungu na Mtu, Elimu ya Falsafa, Uislamu pamoja na Maisha, Uimamu wa AN na Akili na mengineyo katika vitabu na makala.

Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuombwa kuzitwaharisha nafsi zetu na shaka na kuzikinga kwa tawfiki yake na radhi zake.

Tumerefusha maneno katika msingi wa kwanza ambao ni Tawhid, ili uwe kama mdhibiti wa yote ambayo yatarudia kwake katika Aya zinazoambatana nao.

23. Na ikiwa mna shaka kwa (hayo) tuliyomteremshia          mtumwa

wetu, basi leteni sura moja iliyo mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu ikiwa

mnasema kweli.

2 Sura Al-Baqarah

24. Na msipofanya, na hamtafanya, basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, uliowekewa makafiri.

25. Na wabashirie walioamini na wakafanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito chini yake; kila mara watakapopewa matunda humo kuwa riziki, watasema: Haya ndiyo yale tuliyopewa mwanzo, kwani wataletewa hali yakuwa yamefanana na humo watapata wake waliotakasika; na watakaa milele humo.

LETENI SURA Aya 23-25

Kama ambavyo Qur'an imeongoza njia ya kujua kuweko Mwenyezi Mungu Mtukufu vilevile imeongoza njia ya kujua utume wa Muhammad (s.a.w.) miongoni mwazo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mtumwa wetu,

yaani Muhammad (s.a.w.).

Basi leteni sura moja iliyo mfano wake.

Makusudio yake ni kushindwa kuleta mazungumzo yaliyo mfano wa Qur'an, wakiwa wao ndio mabingwa katika fasihi na shughuli yao kubwa ni fasihi, lakini si lazima walete yale yanayolingana nayo kwa idadi na umbo. Walipewa hiyari, wakipenda walete yote; Sura kumi au Sura moja. Vile vile hawakulazimishwa kuleta mfano wa maana yake katika kanuni za tabia, misingi ya sharia na habari za ghaibu, bali walitakiwa walete

40

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wanayoyaweza katika maana yoyote na lengo lolote mradi tu ubainifu wake uwe kama wa Qur'an.

Matakwa haya, kama unavyoyaona yasingeliwashinda kama ingelikuwa Qur'an haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu wao hawakutakiwa wainue jabali au wakaushe bahari, isipokuwa walitakiwa maneno tu. Na wala hakuna kitu rahisi kama hicho kwao. Kwa hivyo kulipothibiti kushindwa kwao, imethibiti kwamba kuna siri fulani na wala hakuna tafsiri ya siri hii isipokuwa wahyi na Utume.Vilevile kila linaloshinda kutafsiriwa katika elimu halina budi kutafsiriwa na lile lililo juu ya maumbile.

Hakuna kitu chenye nguvu zaidi katika kufahamisha ukweli wa Qur'an kuliko mkatao huu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na hamtafanya ..." mpaka hivi leo hajafanya yeyote baada yao. Na mlango bado umefunguliwa kwa anayetaka kujaribu mpaka mwisho.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataja makafiri na adhabu ya moto waliyo nayo, amefuatisha kuwataja waumini, neema na thawabu; kama ilivyo desturi ya Qur'an, kukutanisha mapendekezo na vitisho na ahadi na kiaga kikali, kwa kusisitiza mwongozo na mawaidha.

Wafasiri wengi wamesema kuwa dhamiri katika neno, 'Mfano wake' inarudia Qur'an; yaani mfano wa Qur'an, kwa maana ya kuwa leteni sura iliyo na sifa za Qur'an na muundo wake.

Wengine wamesema, bali hiyo dhamiri inarudia mja wetu; yaani mfano wa mja wetu ambaye ni Muhammad (s.a.w.). Kwa maana ya kuwa mleteni Ummiy (mtu asiyesoma), kama Muhammad, aweze kuleta mfano wa Qur'an hii ambayo ameileta mtu huyu Ummiy.

Maana zipo sawasawa kwa kauli zote mbili ingawaje kauli ya kwanza ndiyo mashuhuri na dhahiri zaidi, ambapo Mwenyezi Mungu amesema: Ikiwa mna shaka kwa tuliyomteremshia... Na wala hakusema; ikiwa mna shaka katika Muhammad (s.a.w.). Hata hivyo kauli ya pili ina maana yenye nguvu, kwani lau yakadiriwa kuwa mtu mwenye uwezo analeta mfano wa Qur'an lisingelikuwa hilo ni ushindi. Kwa sababu wajihi wa kushinda unakuja kwa kuletwa na asiyesoma (Ummiy) sio kwa mjuzi mwenye uwezo.

Makusidio ya kuni ni chochote kinachowashiwa moto. Watu ni wale waasi, na mawe ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu washirikina.

41

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

SIRI YA MUUJIZA WA QUR'AN

2 Sura Al-Baqarah

Utume ni ubalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, anamhusisha nao anayemtaka katika waja wake ili awafikishiye yale wasiyoweza kuyajua; Mwenyezi Mungu amempa nguvu kila Mtume kwa ubainifu ulio wazi juu ya ukweli wa utume wake, ili iwe ni hoja kwa wale waliopelekewa Mtume. Sharti la msingi la ubainifu huo, ni kuwa uwe katika namna maalum inayodhihiri katika mkono wa Mtume na sio mwingine. Hiyo ni kwa kuchukuwa hadhari ya kutatizika kati ya Mtume na asiyekuwa Mtume.

Muhammad (s.a.w.) naye ana ubainifu na dalili juu ya utume wake. Miongoni mwa dalili zake ni hii Qur'an ambayo nakala zake zimeenea kila mahali na Aya zake zinasikika katika vipaaza sauti na katika idhaa za radio mashariki na magharibi, hata Israel.

Njia inayofahamisha kwamba hiyo Qur'an imeshinda, ni kuwa kila mkanushaji alishindwa na anaendelea kushindwa kuleta kitu kama Qur'an au kuleta Sura kama hiyo. Haijanakiliwa habari kuwa kuna mtu aliyeweza kuanzia zamani hadi sasa; ingawaje wapinzani na maadui wa Uislamu na Waislamu ni wengi. Kwa hiyo kimsingi kuthibiti muujiza ndio kuthibiti kwa Utume wa Muhammad (s.a.w.).

Baada ya wanavyuoni kuafikiana kwamba Qur'an ni muujiza wametofatiana katika njia ya muujiza wenyewe na siri yake. Je, ni maajabu na uzuri wa muundo wake? Au ni madhumuni yake mkusanyiko wa elimu, kanuni za sheria na kutolea habari mambo ya ghaibu, n.k.? Au ni mambo yote mawili pamoja?

Wamerefusha maneno katika kubainisha wajihi wa muujiza na kuweka vitabu mahsusi. Sitaki kurefusha yale yaliyosemwa, nafupiliza yale niliyoyaona yana mwelekeo. Kwa ufupi ni kwamba mtu anaweza kumwiga mtu aliye mfano wake kwa kauli na vitendo. Lakini kumwiga Muumba wake katika athari yoyote miongoni mwa athari Zake, ni muhali. Kwa sababu mtu hawezi kupetuka mpaka wake akiwa kama muumbwa, vyovyote atakavyokuwa na nguvu au mkubwa. Ni vizuri kufafanua kama ifuatavyo:

KUSHINDA

Tumedokeza kwamba Muhammad aliwashinda wapinzani kwa Qur'an. Hapana shaka kwamba ushindi unatimu na unakubalika ikiwa kitendo chenyewe anakiweza mtu aliyekusudiwa kushindwa; Kama kumtaka mwenye mkono mzima auweke juu ya kichwa chake, au aondoe unyayo

42

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

ardhini. Lakini ukimtaka asiyejua kusoma asome na asiyekuwa tabibu atibu au asiyekuwa malenga atunge shairi, haitakuwa ni kushindwa. Muhammad (s.a.w.) amewashinda wapinzani jambo wanaloliweza (maneno) likawashinda, na kushindwa kwao huko kumeongezea Qur'an sifa ya muujiza.

Unaweza kuuliza: Je, muujiza wa Qur'an ni kwa yule fasihi wa lugha ya Kiarabu au asiyejua Kiarabu au mtu dhaifu?

Jibu:Qur'an ni muujiza kwa kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu bila ya kumwangalia fasihi na asiyekuwa fasihi, isipokuwa tunajua kwamba ni muujiza kwa kushindwa mwarabu aliye na ufasaha; sawa, na tunapogundua bingwa wa kuogelea anaposhindwa kuogelea kwenye bahari ya mawimbi, kuwa ni kigezo kwamba mwingine asiye bingwa haiwezi bahari hiyo. Yaani ikiwa fasihi ameshindwa basi mwingine ndio kabisa. Kwa maelezo yetu sisi mafaqihi ni kwamba kushindwa kwa fasihi ni sababu ya kujua muujiza wa Qur'an na wala sio fungu au sharti lake.

JE, MUHAMMAD ANA MUUJIZA MWINGINE ZAIDI YA QUR'AN?

Wengine wanaona kuwa Muhammad (s.a.w.) hana muujiza mwingine isipokuwa Qur'an Ama mimi niko pamoja na wanaoamini kwamba miujiza yake haina ya idadi. K wa sababu hekima ya kiungu inapelekea kupatikana namna namna za miujiza kwa kutofautiana hali na watu; kama ilivyofanya hekima yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ya kuapizana Mtume wake na Wakristo wa Najran. Hayo ni ikiwa mwenye kutaka muujiza anautaka kwa kusadikisha.

Ama mwongo mkaidi asiyetoshwa na chochote, anatoshewa na Qur'an tu. Kwa sababu muujiza wa Qur'an ni msingi wa yote, si wa wakati fulani wala na kundi fulani au mtu fulani. Mara nyingine hekima inataka kutoonyeshwa mtu muujiza kabisa; kama vile kutosheka kwa utambuzi na hisia tu, au kwa kuapa Mtume tu.

Imekuja hadith kueleza kwamba mtu mmoja alimwambia Muhammad (s.a.w.): "Nina haja gani na muujiza?" Apa tu kwa Mwenyezi Mungu, kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mimi nitakuamini."

Mtume Akasema: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu." Yule mtu akasema: "Nashuhudia kwamba hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

43

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ambalo linatufahamisha kwamba miujiza ya Muhammad (s.a.w.) haina idadi, ni kwamba mtu wa dini zamani alikuwa akitoa dalili za Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.) kutokana na hadith za kusema na mawe, kujiwa na miti na kuchimbuka maji katika vidole vyake na watu walikuwa wakiyakubali wakati huo.

Ama leo ambapo watu wamejitokeza katika maisha bora (na teknolojia), sisi twatoa dalili Utume wake kwamba yeye alisimama pamoja na wanyonge na kuwapiga vita wadhalimu. Na kwa fadhila zake na fadhila za sheria yake yalivuliwa mataji kutoka katika vichwa vya wastakbari na kutupwa chini ya miguu ya wachunga ngamia na zikagawanywa hazina za wafalme kwa mafukara na maskini.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba miujiza yote ya Mtume mtukufu ni muhimu na mikubwa, lakini muhimu zaidi katika kukadiria kwangu ni mambo mawili:

Kwanza, sheria ya Qur'an ambayo imepanga haki za watu na ufungamano wa watu kati yao juu ya misingi ya uadilifu na kusaidiana. Nitaonyesha kila kitu mahali pake Inshaallah.

Pili, maapizano ya Mtume pamoja na ujumbe wa Najran, ambayo ameyataja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Sura ya Al-lmran (3).

Hakika maapizano haya ni dalili mkataa na ni mpaka wenye kupambanua, ambao unamweka mpinzani mbele ya adhabu na maangamizo ana kwa ana Maangamizo atakayoyateremsha Muhammad (s.a.w.) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa tamko moja tu linalotoka katika mdomo wake mtakatifu. Hakika ushindi huu hauna mfano wake katika historia ya binadamu. Utakuja ufafanuzi mahali pake Inshaallah.

Tumerefusha maneno katika msingi wa pili (Utume) ili uwe ni uthabiti wenye kuenea wa kila linaloambatana nao katika Aya. Nimetunga kitabu maalum kuhusu Utume nilichokiita Anubuwa wal-Aql (Utume na Akili), kimechapishwa mara nne.

26. Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kupiga mfano wowote wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walioamini, wao hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao; lakini wale waliokufuru husema: "Nini

44

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

analotaka Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?" Mwenyezi Mungu huwapoteza kwa mfano huo wengi na huwaongoza kwa mfano huo wengi na hawapotezi kwa (mfano) huo isipokuwa wale mafasiki.

27. Wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha kuifunga           na           kuyakata

aliyoyaamrisha             Mwenyezi

Mungu kuungwa, na kufanya ufisadi katika ardhi. Hao ndio wenye hasara.

HAKIKA MWENYEZI MUNGU HAONI HAYA KUPIGA MFANO WOWOTE

Aya 26 - 27

 HAYA

Haya ikinasibishwa kwa mtu maana yake ni kubadilika hali yake ya tabia kuwa hali nyingine, kwa sababu fulani. Haya ya mtu inaweza kuwa nzuri au mbaya. Nzuri, ni ile kuona haya mtu kufanya mambo maovu na machafu. Kwa hivyo ndio ikawa inasemwa kwa yule anayefanya uovu bila ya kujali: "Kama huoni haya fanya unavyopenda." Imam Jafar Sadiq (a.s.) amesema; "Hana haya asiyekuwa na Imani."

Ama ubaya wa haya, ni mtu kuacha kufanya yale yanayotakikana kwa kuogopa; kama vile mtu kuona haya kujifun-disha, kutafuta maarifa, n.k. Amirul Muminin amesema: "Woga uko pamoja na kushindwa; kukosa huletwa na haya, na wakati unapita kama mawingu (ya kiangazi)." Ilisemwa zamani: "Hakuna haya katika dini."

Hiyo ni haya kwa upande wa binadamu. Ama ikinasibishwa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), inakuwa makusudio yake ni kuacha kitendo.

45

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kama ilivyoelezwa katika hadith: "Hakika Mwenyezi Mungu anamuonea haya mzee, yaani anaacha kumwadhibu."

Makusudio ya kupiga mfano ni kuiweka wazi fikra na kuondoa mikanganyo. Makusudio ya ahadi ya Mwenyezi Mungu ni hoja iliyosimama kwa waja wa Mwenyezi Mungu; ni sawa iwe matokeo ya hoja hiyo ni maumbile na akili au kunakili kwenye kuthibiti kutoka katika kitabu chenye kuteremshwa au kutoka kwa Mtume.

Makusudio ya kufunga hapa ni kukata na kuhukumu. Ahadi kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu iliyopitishwa ni kumfanya peke Yake na kumfanyia ikhlas jambo ambalo linafahamika kutokana na akili na kuthibitishwa na sharia. Makusudio ya kukata aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa ni maamrisho yake na makatazo yake.

Kwa mujibu wa irabu za kinahaw (sarufi) inawezekana kuwa maana yake ni, "Hakika Mwenyezi Mungu haachi kujaalia mbu kuwa mfano". Pia inawezekana, kuwa maana yake ni, "Hakika Mwenyezi Mungu haachi kujaalia kitu chochote kuwa mfano, hata kama kitu hicho ni mbu".

UONGOFU NA UPOTEVU

Uongofu una maana nyingi; kama ifuatavyo:-

Kubainisha na kuongoza. Aya nyingi katika Qur'an zina maana hiyo; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Na hapana lililozuilia watu kuamini ulipowajia uongofu"

Vile vile kauli yake Mwenyezi Mungu:

(17:94)

"Hakika umewajia uongofu kutoka kwa Mola wao"

(53:23)

Yaani; wala hapana ubainifu wa Mwenyezi Mungu isipokuwa ule waliokuja nao Mitume au uliohukumiwa na hukumu ya wazi isiyokuwa na shaka.

Kukubali mtu nasaha na kunufaika nayo; kama asemavyo Mwenyezi Mungu:

46

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

"Sema: Enyi watu! Haki imekwisha wajia kutoka kwa Mola wenu, basi anayeongoka anaongoka kwa nafsi yake na anayepotea anapotea kwa nafsi yake."

(10:108).

Tawfiq na msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa njia mahsusi; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

"...lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye..."

Na kauli yake:

(2:272)

"...na hakika Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye..."

(22:16)

Yaani anamwafikisha kwenye amali kwa uongofu na kumwandalia njia ya kuendea.

Kimsingi ni kwamba uongofu kwa maana ya ubainifu tu haulazimishi kuwafikisha kwenye amali; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"Si juu yako uongofu wao."

(2:272)

yaani si juu yako wafanye amali kwa uongofu wako au wasifanye; isipokuwa ni juu yako kubainisha tu.

Thawabu; kama kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya Imani yao; itakuwa inapita mito mbele yao katika mabustani yenye neema."

(10:9)

47

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Yaani atawapa thawabu kwa sababu ya imani yao.

Mwenye Kuongoza na mwenye kubainisha, kwa kuangalia kwamba uongofu umepatikana kwa sababu yake. Hayo ndiyo makusudio katika Aya hii tunayoizungumzia. Amesema mwenye Majmaul-Bayan: Kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Huongoza wengi kwa mfano huo",

anakusudia wale ambao wameamini. Kwa kuwa uongofu umepatikana kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, basi umetengenezwa kwake.

Hukumu; kama kusema: "Kadhi amehukumu sawa sawa"; yaani amehukumu kwa uadilifu wake. Maana haya yanafaa kuyanasibisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Upotevu, nao pia una maana nyingi: Miongoni mwayo ni haya yafuatayo:-

Kutia mashaka, kuingiza katika ufisadi na kuizuilia dini na haki. Maana haya hayategemezwi kwa Mwenyezi Mungu kwa hali yoyote; bali hunasibishwa kwa Iblis na wafuasi wake; kama asemayo Mwenyezi Mungu akimzungumzia Iblis, Firaun na Samiri:

"kwa hakika nitawapoteza na nitawatamanisha..."

(4:119)

"Na Firaun akawapoteza watu wake na hakuwaongoza."

(20:79)

"...Na akawapoteza Samiri"

(20:85)

Adhabu, Aya nyingi katika Qur'an zimekuja kwa maana haya; kama vile:

48

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

(40:74)

"Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu huwapoteza makafiri "

âJI ill J-

"...Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu..."

(14:27)

"Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza aliyepita kiasi mwenye shaka"

(40:34)

Yaani anawaadhibu waongo, makafiri na madhalimu.

Kukusudiwa jina la mpotezaji, kama kusema "Amepotezwa na fulani" Ukikusudia kumnasibisha kwenye upotevu na kumzingatia kuwa ni katika wapotevu.

• • Kujitenga mtu na nafsi yake. Mwenye kumpuuza mtoto wake bila ya

malezi yoyote au usaidizi wowote, inafaa kuambiwa amempoteza mtoto wake.

• • Kupoteza kitu. Husemwa: "Fulani amepoteza ngamia wake". Maana

haya vile vile hayanasibishwi kwa Mwenyezi Mungu.

• • Majaribio na mitihani, kwa namna ambayo hupatikana upotevu

kwenye ubainifu ambao Mwenyezi Mungu humtahini mja wake. Mwenye Majmau anasema:"Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu anawatahini kwa mifano hii waja wake, kwa hiyo huwapoteza watu wengi na huwaongoza watu wengi."

MAELEZO

Maana yanayopatikana kutokana na Aya mbili hizi ni kwamba Mwenyezi Mungu haachi kupiga mifano kwa vitu ambavyo wajinga wanaviona ni duni; kama buibui, nzi, mbu na wengineo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Muumba na Mola wa kila kitu; kwake bawa la mbu na ulimwengu mzima ni sawa tu.

49

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Zaidi hayo kupiga mifano kunapatikana katika lugha zote ili kuziweka wazi fikra kwa kuzikutanisha na vyenye kuhisiwa. Kwa hivyo, kila linalohakikisha kupatikana kwa lengo hili linafaa kufanywa ni mfano, liwe dogo au kubwa; na kwalo inatimu hoja kwa kila mpinzani.

Mwenyezi Mungu amewatahini watu kwa mifano hii, kama alivyowatahini kwa mambo mengine miongoni mwa dalili na ishara. Wengi wakaitumia na wengi wakapinga. Wale walioitumia ni wale wema walio waumini na waliopinga ni wale mafasiki waliopotea.

Kumesihi kuutegemeza uongofu na upotevu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kuangalia kuwa Yeye ndiye aliyepiga mifano ambayo imekuwa ni rehema kwa aliyewaidhika na ni mateso kwa asiyewaidhika.

Ni vizuri kuleta mfano ili kufafanua fikra hii: Mwanachuoni alipata elimu na ikamwinua, halafu akahusudiwa na hasadi ikadhuru kiwiliwili na akili yake; kama alivyosema Imam Ali (a.s.) "Siha ya mwili ni husuda kuwa chache."

Inafaa kusema kuwa mwanachuoni huyu ndiye aliyemfanya hasidi kufanya uovu huu; au kama vile unavyosema: "Uzuri wa mwanamke fulani umeharibu akili ya mwanamume fulani." Pengine wawili hao hata hawajuani.

Kwa mtazamo huu ndipo umenasibishwa upotevu kwa Mwenyezi Mungu kimajazi. Kwa vile Yeye ndiye aliyebainisha hoja na kuziweka wazi, na mhalifu alipozikhalifu akapotea. Lau Mwenyezi Mungu asingelibainisha, basi kusingekuwepo na suala la utiifu na uasi na asingelikuwako mpotevu na mwongofu.

Mwenyezi Mungu amemwita yule asiyepata onyo kwa mifano: Fasiki, mvunja ahadi na mkataji wa yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ya ungwe, ambayo ni kufuatilia mambo ya heri na kuungana na watu wa heri na mengineyo ya kusaidiana kwenye heri.

KUUMBA NA KUWEKA SHARIA

Mwenyezi Mungu ana matakwa mawili: Matakwa ya kuumba ibara yake ni "Kun fayakun" (kuwa na ikawa). Kwa matakwa haya kinapatikana ambacho hakikuweko.

Matakwa ya pili, ni ya kuweko sharia ambayo yanakuwa katika ibara ya kuamrisha na kukataza na kulingania kwenye heri na kuacha shari. Mja

50

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

akifanya heri huifanya kwa matakwa yake na hiyari yake bila ya kulazimishwa. Vile vile akifanya shari na kuacha heri.

Ikiwa utekelezaji wa hukumu zote za dini unafungamana na matakwa ya wale wenye kukalifiwa na hukumu hizo na hiyari, wala kusiweko mwenye kuwachunga isipokuwa wao wenyewe, basi itakuwa ni kosa kusema kuwa dini imeathiri katika kuanguka wafuasi wake na wenye kunasibika nayo.

Ndio, lau wangeliitumia dini na wakaifuata kwa ukamilifu kwenye vitendo vyao, ingelifaa kufanywa dini ni kipimo cha kupanda na kuanguka kwao. Kwa hali hiyo basi ndio inabainika hasadi na chuki dhidi ya Uislamu katika kauli ya aliyesema; "Unyonge wa Waislamu ni dalili ya unyonge wa Uislamu na mafundisho yake."

Kutokana na matamko ya mkosaji, inajuzu kwetu kunasibisha katika dini ya Kikristo kila ufasiki, uovu, na kuvunjiana heshima katika Ulaya na Amerika. Vile vile kunasibisha uharibifu wa vita vyote vilivyoathiri dola za Kikristo katika Mashariki na Magharibi ya dunia mpaka kulipuka bomu la Atomiki katika Hiroshima, na mabomu yaliyotupwa Veitnam; na hata kubadili maumbile9 na kuongezeka idadi ya makosa na maovu siku baada ya siku katika Ulaya na Amerika mpaka kufikia hatua ya kuhalalisha ulawiti katika Uingereza kikanuni na kikanisa.

Je, yote hayo na mengi mengineyo yanafaa kunasibishwa kwa Masih (a.s.)? Hapana! Ametakasika na uchafu wote huu.

Kama tungechukulia uzushi wa huyo mzushi, angelikuwa Myahudi wa Yemen ni sawa na Myahudi wa New York na Mkristo wa Misri ni sawa na wa Paris kimaendeleo.

Kuacha kuendelea miji kuna sababu nyingi sana zisizokuwa za dini; hasa ujinga, Historia ya kubakia katika unyonge na matatizo ya mazingira, na kukosa kuchangayika miji iliyoendelea na ile isiyoendelea.10 Lau kama si kuchanganyika Waislamu wa kwanza na

Sehemu kubwa ya Hiroshima na Nagasaki zilizopigwa bomu la Atomiki ardhi yake haimei kitu, na watoto wengi hadi leo huzaliwa na kasoro mwilini kutokana na athari ya bomu hilo - Mfasiri

Dini ni sawa na baraza la kutunga sharia. Ama utekelezaji ni wa mwingine. Umoja wa mataifa umefeli katika maazimio yake mengi muhimu na baraza la usalama nalo likafeli kuyatekeleza. Vile vile haikufaulu mikutano ya uongozi wa siasa zisizofungamana na upande wowote na wengineo. Mara ngapi wameshindwa, lakini lawama halikuwa lao. Sasa itakuwaje Uislamu ulaumiwe kwa sababu ya wanaoitwa Waislamu.

51

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

mataifa mengine isingebaki athari yoyote ya maendeleo ya kiislamu. Naam! Uislamu ulikuwa ndio msukumo wa mchanganyiko huo.

Kwa ufupi sababu za kutoendelea hazitokani na tabia ya Uislamu wala ya Ukristo au wasiokuwa na dini, bali ni kutokana na hali za kijamii.

Tutarudia kufafanua zaidi tutakapofika kwenye Aya za maudhui ya Jabri na Tafwidh (kutenzwa nguvu na kuachiwa). Na hayo tumeyaelezea kwa ufafanuzi katika kitabu 'Maalimul Falsafatul Islamiya' na kitabu 'Maa'shiatul Imamiya'.

28.  Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akawafufua! Kisha atawafisha tena atawafufua, kisha kwake mtarejeshwa.

29.  Yeye ndiye aliwaumbia vyote vilivyomo katika ardhi tena akakusudia kuumba mbingu na akazifanya saba. Naye ni mjuzi wa kila kitu.

MWANADAMU KWA DHATI YAKE NI HOJA

Aya 28 - 29

Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu.

Kwa dhahiri ya mfumo wa maneno inaonyesha kwamba msemo katika Aya mbili hizi unaelekezwa kwa yule ambaye hanufaiki na chochote katika kupigiwa mfano, lakini ilivyo hasa msemo unamhusu kila anayemkufuru Mwenyezi Mungu pamoja na kuweko dalili hizi zisizokuwa na idadi ambazo ni pamoja na huyo kafiri mkanushaji. Kwani yeye kwa dhati yake ni dalili iliyo wazi ya kupatikana aliyemuumba. Kama si hivyo ni nani basi aliyemfanya katika nidhamu hii kali kabisa, akakiweka kila kitu mahala pake panapohusika, kuanzia chembe hai za ubongo na moyo mpaka kwenye utumbo na maini, kwenye usikizi na uoni na mpaka

52

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kwenye miishilio isiyokuwa na mwisho. Kila kimoja kinatekeleza umuhimu wake kwa uangalifu bila ya usimamizi wowote kutoka kwa kiumbe.

Vile vile ni kutoka wapi umekuja ufahamu huu na akili ambayo mtu analikurubisha lililo mbali, kulisahilisha zito na kukusanya yaliyo katika ardhi katika nyumba moja, kisha akaendelea zaidi na kuweka athari zake mwezini.

Je haya na mengineyo yamekuja kibahati na (kisadfa) tu? Je kuna vitu hasa vinavyoendesha mpangilio huo? Je Sayansi inaweza kujibu hayo? Na je majibu yatatokana na kuhusika na majaribio ya Kisayansi?(14:34)

Walijaribu wenye kujaribu kujibu, lakini yakajitokeza maelfu ya maswali. Sisi hatukanushi kabisa kwamba wataalamu wa kisayansi wamefikilia kwenye ukweli wa kushangaza katika tiba, ukulima na viwanda, lakini wataalamu wa uhai wameambulia patupu wakitafuta siri ya uhai na asili yake; na hawana chochote isipokuwa dhana tu, ambayo haitoshei haki. Kimsingi, kila Sayansi inaposhindwa kutafsiri jambo hulihukumia kwa kinyume chake.

Ikawa kupatikana mtu ni nguvu ya hoja kuhusu kuwapo Mwenyezi Mungu (s.w.t.), inakuaje hoja hii ipinge hoja inayolazimiana nayo? Vipi mtu aliye na fasihi aweze kupinga fikra ya fasihi na balagha? Basi hapo ndio inakuwa siri ya kustaajabisha katika kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

Vipi mnakanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akawafufua.

Yaani ni maajabu yaliyoje ya kumkanusha kwenu Mwenyezi Mungu na hali nyinyi kwa dhati kabisa ni dalili wazi ya kuwepo Mwenyezi Mungu. Vyovyote mtakavyokanusha, je, mnaweza kukanusha kwamba nyinyi hamkuwa kitu chochote kisha ndipo mkawa kitu kinachosikia, kuona, kuhisi na kutambua, pamoja na kusema na kutenda? Je, hiyo si dalili inayoeleza kupatikana nguvu iliyoumba?

Kweli kabisa. "Hakika binaadamu ni dhalimu mkubwa mwenye kukanusha mno!" Hakukuwa kumkanusha Mwenyezi Mungu isipokuwa ni kukanusha na kutojijua huyo mkanushaji.11 Na asiyejijua, basi ndio

Anasema Charlie Champlin, mchezaji sinema mashuhuri wa kimataifa, ambaye umashuhuri wake umezidi ule wa Gandi: "Katika mamlaka isiyojulikana kuna nguvu isiyokuwa na mpaka." Na anasema Kierkegaard "Hakika Mwenyezi Mungu

53

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

hamjui mwingine. Kwa hali hiyo ndiyo tunapata tafsiri ya hadith tukufu: "Anayejijua zaidi ni yule anayemjua zaidi Mola wake."

Unaweza kuuliza: Ni akili gani inayoweza kujikanusha yenyewe? Je hayo yanaingia akilini? Tunajibu: Hakika hoja inalazimiana na chenye kutolewa hoja; na kukanusha ulazima kunapelekea kukanusha chenye kulazimiwa. Kwa hivyo mwenye kukanu-sha dalili ya matamko, kwa mfano, kutokana na maana iliyowekwa, atakuwa ameyakanusha matamko yenyewe atake asitake, wala hakumfalii yeye kuyakubali wakati anakanusha dalili zake.

Hivi ndivyo ilivyo kwa mwenye kumka-nusha Mwenyezi Mungu. Kwani kuwapo kwake ni dalili ya kuwapo muumbaji, na kupatikana muumbaji kunatolewa dalili na kupatikana kwake yeye mkanushaji. Basi akikanusha chenye kutolewa dalili ndio amekanusha dalili yenyewe, ambayo ndiyo huyo mkanushaji kwa dhati yake bila ya kujijua wala kujitambua.

Hivyo ndivyo anavyofanya mjinga anayejiepusha na maumbile anayoishi nayo na kumpa uhai, kupinga dalili zilizo wazi na kuamini vigano na mambo ya kijinga.

MAUTI NA UHAI MARA MBILI

Makusudio ya kufa kwa kwanza kunak-oonyesha na neno "Mlikuwa wafu" ni kutokuwapo kwa mara ya kwanza, Na makusudio ya uhai wa kwanza, "Akawafufua" ni kuumbwa baada ya kutokuwapo.

Mauti ya pili, Kisha atawaua, ni mauti haya yaliyozoeleka; na kufufuliwa mara ya pili ni kufufuliwa kwa ajili ya hisabu na malipo.

TENA ATAWAFUFUA

Unaweza kuuliza, je roho inafarikiana na mwili baada ya kwisha nguvu zake za uhai, kwa namna ambayo lau nguvu zingebakia, basi roho ingelibaki na bina -damu milele? Au ni kwamba inawezekana roho kufarikiana na mwili hata ukiwa na nguvu za kuishi kwa ukamilifu bila ya kutokea uharibifu wowote mwilini?

Jibu: Watu wa kimaada wamechukulia kauli ya kwanza na wengine wamechukulia kauli ya pili. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

anajitokeza kwenye nafsi yenye kukata tamaa katika wakati mgumu wa kukata tamaa na katika lindi la makosa."

54

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"...Utakapofika muda wao hawatakawia (hata) saa moja wala hawatatangulia"

(7:34)

Inaweza kuchukuwa njia zote mbili. Kwani haikubainisha sababu ya kufika muda wao. Je ni kuharibika mwili au ni kitu kingine.

Kauli yake Mwenyezi Mungu:

"...ambao walitoka katika majumba yao nao walikuwa maelfu wakiogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia 'Kufeni'

(2:243)

Na kauli yake:

» -

"Akasema Mwenyezi Mungu atuuhuisha vipi (mji) huu baada ya kufa kwake? Basi Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia..."

(2:259)

Aya mbili hizo zinahusu matukio fulani tu. Haziingii katika matukio mingine.

Vyovyote iwavyo hatuna kitu kinachotuthibitishia, lakini tunayoshuhudia ni kwamba watu wengi wanafikiwa na mauti nao bado wabichi wakiwa na afya nzuri na kwamba wengi wanatembea na kufurahi nao wako katika umri mkubwa na magonjwa tele. Madaktari wengi mahodari wanamwambia mgonjwa utakufa baada ya saa chache tu, lakini akaishi muda mrefu!

UFUFUO

Ufufuo katika Uislamu ni msingi wa tatu baada ya Tawhid na Utume, misngi ambayo tumeshaielezea. Mwenyezi Mungu ameyatolea habari marejeo (ufufuo) aliposema: Kisha atawafufua kisha kwake mtarejeshwa.

55

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ametoa dalili au kuukurubisha uwezekano wa ufufuo katika Aya nyingi. Miongoni mwazo ni:

ill 01 Ij

"Je! hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi na hakuchoka kwa kuziumba, ana uwezo wa kuwafufua wafu?"

(46:33)

"Enyi watu! Kama mmo katika shaka juu ya ufufuo, basi kwa hakika tuliwaumba kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu..."

(22:5)

Hakuna anayetia shaka kwamba Mwenye kuumba kitu huwa rahisi kwake kuvikusanya viungo vyake baada ya kuwa mbali mbali; bali kukusanya ni rahisi zaidi kuliko kuumba tena. Mwenye kujenga jumba kubwa ni rahisi kwake kujenga kibanda.

12

Ninacho kitabu maalum nilichoandika cha maudhui haya kinachoitwa 'Al-akhira wal aql' kisha nikayalinganisha na kitabu 'Al-lslam wal aql' ambavyo vimechapishwa mara nyingi sana.

YALIYO KATIKA ARDHI

Baada ya Mwenyezi Mungu kumkumbusha mtu neema ya kupatikana kwake, anamtajia wingi wa neema alizonazo, ikiwa ni pamoja na kula na

Mnamo mwaka 1959 Mustafa Mahmud, Mmisri, alitunga kitabu Allahu Wal-insan (Mungu na mtu) katika kitabu hicho alikana Mungu na ufufuo, nami nikamjibu kwa kutunga kitabu Allahu wal-Aqli (Mungu na Akili) mpaka sasa kimechapishwa mara tano. Ilipofika tarehe 10.4.1967 nilimsomeya makala Mustafa Mahmud katika jarida la Ruz Al-Yusuf, inayosema: Imani yangu inashikilia kwamba mimi nilikuwako kabla ya maisha yangu haya kwa jina jingine, na kwamba mimi sitaisha baada ya kufa kwangu isipokuwa nitarudi kwenye uhai kwa namna nyingine, na maisha yanaendelea.

56

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kunywa, mavazi, vipando, mandhari na mengineyo katika starehe za ardhi na heri zake zisizohisabika.

Wametoa dalili mafakihi kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Yeye ndiye aliyewaumbia vyote vilivyo katika ardhi." Kwamba vitu vyote kabla ya kuja sharia ni halali, na kwamba haimfailii kiumbe kuharamisha kitu isipokuwa kwa dalili. Mwenyezi Mungu anasema:

"Sema: Je, mnaonaje zile riziki alizowateremshia Mwenyezi Mungu kisha mkafanya katika hizo (kuwa) haram na (nyingine) halali. Sema, Je, Mwenyezi Mungu amewaruhusu au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"

(10:59)

Pengine hutolewa dalili kwa Aya hii kwamba ardhi haimilikiwi. Kinachofaa kumilikiwa ni kile kinachozalishwa na ardhi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: "Amewaumbia vilivyomo ardhini na hakusema amewaumbia ardhi."

MBINGI SABA

Maana ya neno istawa hapa ni kukusudia. Kuzihusisha mbingu saba hakufahamishi kuwa ndio hizo hizo tu wala hakukanushi kabisa kuwapo nyinginezo. Wamethibitisha wanavyuoni wa elimu ya usul na lugha kwamba idadi sio ufahamisho, mwenye kusema mimi ninamiliki vitabu saba haimaanishi kwamba hamiliki vingine. Analitilia nguvu hilo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipomwambia Mtume wake (s.a.w.):

"Hata ukiwaombea msamaha mara sabini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe."

(9:80)

Mtume (s.a.w.) akasema : "Lau ningelijua kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe nikizidisha sabini ningelifanya."

Huenda ikawa sababu ya kutaja saba ni kwamba hizo saba zina mambo maalum yasiyopatikana katika mbingu nyingine.

57

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

30.  Na Mola wako alipowaambia Malaika mimi nitaweka Khalifa katika ardhi. Wakasema (Malaika) utaweka humo watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na kukutaja kwa utakatifu wako?" Akasema Mwenyezi Mungu: Hakika          mimi           nayajua msiyoyajua.

31.  Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika akasema: Niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnasema kweli.

32.  Wakasema: Utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundisha; hakika wewe ndiwe mjuzi, mwenye hekima.

33. Akasema: Ewe Adam waambie majina yake. Alipowaambia majina yake. Alisema (Mwenyezi Mungu): Sikuwaambia kwamba mimi ninajua siri za mbinguni na za ardhini; tena najua mnayoyadhihirisha                 na

mliyokuwa mkiyaficha.

58

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Aya 30 - 33

MOLA WAKO ALIPOWAAMBIA MALAIKA

Makusudio ya majina katika kauli yake Mwenyezi Mungu: Na Mwenyezi Mungu akamfundisha Adam majina ya (vitu) vyote, ni maana ya majina, nayo ni ya vitu vya ulimwengu na sifa zake. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Hakika majina bila ya maana hayana faida wala kuonyesha ubora wake."

Imam Sadiq (a.s.) Aliulizwa kuhusu hayo majina akasema: "Ni milima na mabonde." Kisha akaonyesha busati lililokuwa chini yake akasema: "Hili ni miongoni mwayo", yaani kila kitu mpaka busati hili pia.

MALAIKA

Hakuna njia ya kuwajua Malaika na hakika yao kwa hisia na majaribio wala kwa akili na kukisia au kwa kitu chochote isipokuwa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia midomoni mwa Mitume yake. Mwenye kukanusha wahyi kimsingi haifai kumzungumzia habari ya Malaika kwa hali yoyote. Kwa sababu wao ni tawi na wahyi ni asili (shina). Ikiwa hapana budi kulumbana naye basi ni lazima iwe ni kuhusu fikra ya wahyi na kuswihi kwake tu.

Hapa hatukusudii kulumbana na anayekanusha wahyi, kwa vile tumekwishafafanua; isipokuwa tunamwambia yule mwenye kukanusha: "Si haki kulazimisha rai yako juu ya yule mwenye kuamini wahyi; kama si hivyo basi ingelijuzu kwake kulazimisha rai yake kwako. Kama ukimwambia mwenye kuamini wahyi kuwa imani yake ni batili kwa vile yeye hategemei majaribio, atakujibu kwamba kuamini kwako kuwa wahyi ni batili vilevile hakukutegemea kwenye majaribio, kwa sababu kukanusha kwako na uthibitisho wa mwenye kuamini, maudhui yake ni mamoja, nayo ni wahyi. Ikiwa majaribio, hayathibitishi wahyi pia hayaukanushi.

Kwa maneno mengine kuamini kutokuwepo ghaibu ni sawa na kuamini kuwepo, yote mawili ni ghaibu katika ghaibu. Kimsingi ni kwamba ghaibu haifai kuipinga kwa ghaibu."

Sartre, mwandishi na mwanafalsafa mashuhuri wa Kifaransa akiwajibu wanao-amini maada alisema: "Nyinyi mnapokanusha kuwepo Mwenyezi Mungu ndio mnafafanua ghaibu kwa ukamilifu, kama wanaoamini mifano ambao wanakubali kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika yakini ya kimaada ya kukanusha ghaibu, inategemea dalili ile ile anayoitegemea

59

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

13

mwenye kuamini kuswihi ghaibu. Kwa hivyo basi imebainika kwamba imani ya kimaada inajipinga yenyewe.'

KHALIFA

Makusudio ya Khalifa katika Aya ni Adam, baba wa watu na kila mtu aliyeko na atakayekuwako katika kizazi chake wakati wowote na mahali popote. Wajihi wa kumwita Khalifa ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimpa nafasi ya kuchukua hatamu za uongozi wa ardhi hii na kutafuta yaliyomo ndani yake miongoni mwa nguvu na manufaa na kufaidika nayo.

Katika kauli ya Malaika:

"Utaweka humo watakaofanya uharibifu na kumwaga damu."

Inaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwafahamisha Malaika kwa njia fulani kabla ya kumuumba Adam, kwamba lau binadamu atakuwa katika ardhi hii angeliasi kwa ufisadi na kumwaga damu. Kutokana na hali hiyo ndio wakaona ajabu vipi Mwenyezi Mungu amlete ambaye atamuasi na wao wanamtukuza kwa sifa zake na kumtaja kwa utakatifu wake?

Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawabainishia hekima ya kuumbwa mtu na kwamba huko ni kuandaa kujulisha lile wasilolijua na uharibifu wake katika ardhi hauwezi kuondoa faida ya kupatikana kwake. Hapo Malaika wakatosheka na wakatii.

14

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumuumba mwanaadamu ili afanye maasi na maovu, bali amemuumba kwa ajili ya elimu na amali yenye manufaa na akamkataza ufisadi na madhara. Akikhalifu na kuasi basi huadhibiwa kadri anavyostahiki.

Aya hii inafahamisha kwamba elimu na yanayoambatana nayo, ina cheo kikubwa mbele za Mwenyezi Mungu na Malaika wake, kwa sababu Mwenyezi Mungu amefanya bora kumuumba mtu kwa ajili ya elimu na maarifa na alipowaonyesha hilo, Malaika walitoa udhuru kwa kusema: Utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundisha.

Angalia kifungu cha Sartre na madhehebu ya kimaada katika kitabu chetu Falsafatul-Mabdai Wal-Maad, tulichokitunga kuwajibu wenye Falsafa ya kimaada.

Inasemekana kuwa katika ardhi walikuwepo watu kabla ya Adam wetu, na kwamba wao walifanya uharibifu kisha wakaangamia wote na Malaika walikuwa wakilijua hilo.

60

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ikiwa lengo la kuumbwa mtu ni elimu na amali, basi mwenye kuiacha atakuwa ameivunja hekima ya kuwepo.

Naogopa kusema kuwa lau Malaika wakati huo wangejua athari ya mabomu ya kitonoradi (Nuclear) na mabomu ya sumu (Napalm) waliyotumia Wamarekani huko Vietnam, basi wasingelikinai kabisa...

Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu ambaye anajua vile tusivyovijua sisi wenyewe.

SOMO WAZI

Somo ambalo ni lazima tufaidike nalo katika majibizano ya Mwenyezi Mungu na Malaika wake, ni kwamba mtu, vyovyote atakavyofikia katika elimu, nguvu na ukubwa, hawezi kuepuka kufanyiwa majibizano, malumbano na kushauriwa. Mwenyezi Mungu mwenyewe tu aliye mtukufu alitoa nafasi kwa Malaika ajadiliane nao na kujibizana ambako kunafanana na upinzani; na wao hawakujizuia na hilo, bali walijitia ushujaa wa elimu. Mwenyezi Mungu akawachukulia upole katika kuwajibu na kuwabainishia dalili kwa upole wakakubali kwa kuridhia na kukinai, sio kwa kukemewa. Pia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akafungua mlango wa majibizano pamoja na Iblis mwenye laana ambaye alijibizana naye kwa kusema: "Umeniumba kwa moto na yeye umemuumba kwa udongo...", kama yatakavyokuja maelezo.

Basi ni juu ya wale wanaojiona kuwa hawawezi kupingwa wachukue faida ya somo hili la wazi. Wakijitoa na kujibiwa watakuwa wanajifanya juu zaidi ya Mwenyezi Mungu, bila ya kujua. Anasema Amirul Muminin Ali (a.s.):

"Msinich-anganye na watu wenye kujifanya wala msinidhanie kuwa nitaona uzito kwa haki niliyoambiwa wala kujifanya mkubwa. Kwani mwenye kuona uzito wa haki anayoambiwa au uadilifu atakaoonyeshwa, basi kuyafanya hayo mawili itakuwa uzito zaidi kwake. Msijizuwie na haki iliyosemwa au ushauri wa uadilifu."

34. Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni                          Adam,

wakamsujudia wote isipokuwa Iblis; alikataa na akajivuna; na

(Nahjul-Balagha, Khutba Na. 213)

61

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza akawa miongoni mwa makafiri.

2 Sura Al-Baqarah

MSUJUDIENI ADAM Aya 34

Mwenyezi Mungu aliwaamrisha malaika kumsujudia Adam kwa kudhihirisha ubora wake kuliko wao na kuliko viumbe vyake vyote. Hapana tafsiri ya ubora huu isipokuwa ubora wa elimu au ubora wa aliye nayo. Kwa sababu elimu, kama ilivyothibiti, ndiyo kipimo cha kila hatua anayopiga mtu ya maendeleo na ukamilifu; kama vile ambavyo ujinga ni msingi wa kurudi nyuma. Hawezi kuwa juu isipokuwa kwa elimu. Mwenye elimu siku zote hufuatwa, na mjinga siku zote hufuata. Kwa ajili hii Uislamu umewajibisha elimu kwa kila Mwislamu mwanamume na mwanamke.

Wafasiri wengi wamesema kwamba sijda ilikuwa ni ya ki-maamkuzi tu;

Kama kuinama na kuinua mkono. Kwa sababu kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu. Lakini haya sio kweli kwa mujibu wa mwenye tafsiri ya Majmaul-Bayan, kwani kama ingelikuwahivyo,basi, Iblis asingelikataa kumsujudia. Kimsingi sijda ilikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu sio kwa ajili ya Adam.

Amri ya kumsujudia Adam iliwahusu Malaika wote bila ya kumvua yoyote, hata Jibril na Mikail pia, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na tulipowaambia Malaika, msujudieni Adam. Basi wakamsujudia isipokuwa Iblis; yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake."

(18:50)

Hakuna njia ya kumjua Iblis, shetani na jini, isipokuwa kwa njia ya wahyi tu; kama ilivyo katika kuwajua Malaika. Maelezo yamekwishaelezwa katika Aya iliyotangulia.

Wafasiri wameonyesha utafiti usiokuwa na manufaa. Kwa hivyo tumeuacha kwa kufupiliza yale yanayofahamishwa na dhahiri ya maneno. Tumekwisha onyesha katika kurasa zilizotangulia baadhi ya yale yanayonasibishwa kwa Iblis katika vigano. Ni picha iliyo wazi ya

62

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

watu wengi wa siku hizi katika kuchezea kwao matamko, ambako hakutimizi elimu au fani yoyote zaidi ya kubobokwa tu.

35.  Na tukasema: Ewe Adam! kaa wewe na mkeo katika Pepo (bustani); na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, wala msiukurubie mti huu; msije mkawa miongoni mwa waliodhulumu (nafsi zao).

36.  (Lakini) Shetani akawatelezesha wote wawili na akawatoa katika ile hali waliyokuwa nayo. Tukasema: nendeni hali yakuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe kwa muda (maalum).

37.  Akapokea Adam maneno kutoka kwa Mola wake na Mola wake akapokea toba yake; hakika Yeye ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu.

38.  Tukasema: Tokeni humo nyote: Na kama ukiwafikia uongozi wangu basi watakaoufuata mwongozo wangu haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

39.  Na ambao wamekufuru na kukadhibisha ishara zetu, hao ndio watakaokuwa watu wa motoni, humo watadumu.

63

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

ADAMU PEPONI Aya 35 - 39

Mwenyezi Mungu aliamwamrisha Adam na Hawa kukaa peponi; akawahalalishia kula yaliyomo ndani yake isipokuwa mti mmoja tu, waliokatazwa kuula. Lakini shetani aliwahadaa kwa kuwataka waule. Walipokubaliana naye ilipita hekima yake Mwenyezi Mungu ya kuwatoa pepo ni kuwapeleka ardhini na akawatia mtihani kwa taklifa na kazi, uzima na ugonjwa, shida na raha, kisha mauti muda wake unapofika.

Adam alihisi msiba na akajuta. Akamwomba Mola wake kwa ikhlasi amtakabalie toba yake, akamkubalia na akamsamehe, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba Mwenye rehema. Nadhani

kwamba Hawa pia alitubia pamoja na Adam, lakini Mwenyezi Mungu hakuitaja toba yake. Hakuna tofauti kati ya Mwanamume na mwanamke. Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya amali njema, Mwenyezi Mungu atamuweka peponi, na mwenye amali mbaya atamwingiza motoni awe mume au mke.

Wamejiingiza wafasiri wengi kuelezea pepo aliyotoka Adam, ilikuwa wapi? Mti ulikuwa mtini au ngano? Kuhusu nyoka ambaye aliingia Iblis ndani yake, na mahali aliposhukia Adam, je palikuwa India au Hijaz? Na mengineyo yaliyokuja katika hadithi za Kiisrail. Qur'an haikudokeza lolote katika hayo; wala haikuthibiti katika hadithi kwa njia sahihi. Pia akili haiwezi kujua chochote katika hayo, na hayo hayaambatani na maisha kwa karibu au mbali. Hata hivyo hakuna budi kutanabahisha mambo yafuatayo:-

HAWA NA UBAVU WA ADAM

Imeenea habari kwamba Hawa aliumbwa kutokana na ubavu wa Adam, lakini hakuna maelezo sahihi ya kutegemewa. Na habari zilizoelezea hilo si za kutegemewa. Ikiwa tutazichukulia kuwa ni sahihi basi ni kwamba makusudio yake ni kuonyesha usawa na kukosa kutofautisha kati ya mume na mke, yaani mke ametokana na mume na mume naye ametokana na mke.

64

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Katika kitabu Malla yahdhur hul-faqih, imesemwa, Imam Sadiq (a.s.) wakati alipoulizwa usahihi wa uvumi huu, aliukanusha na akasema: "Mwenyezi Mungu Ametukuka na hayo kabisa. Je Mwenyezi Mungu alishindwa kumuumbia Adam mke isipokuwa kutokana na ubavu wake mpaka ikabidi Adam aoe sehemu yake ya mwili?"

MTAKA VOTE HUKOSA VOTE

Hekima ya Mwenyezi Mungu ilipitisha kuwa Adam akae na mkewe peponi wakati fulani, kisha atoke kwa sababu maalum ambayo wao wawili ndio walioifanya kwa matakwa yao na hiyari yao; lau si hivyo wangelibaki peponi milele wakistarehe bila ya taabu yoyote.

Vile vile hekima yake Mwenyezi Mungu ilipitisha kuwa Adam na Hawa wabaki katika ardhi hii mpaka watakapozaana na kupatikana koo na vizazi, wakati ambapo wataulizwa wote, kauli na vitendo walivyovifanya. Kama ilivyohukumilia hekima yake kurudi Adam na mkewe peponi baada ya kufa na wadumu humo milele.

15

Unaweza kuuliza: Kuna hekima gani ya kuingia Adam peponi na kutoka kuja ardhini, kisha kuitoka hiyo ardhi na kurudi tena peponi mara ya pili baada ya kufa?

Jibu: Huenda hekima iliyopo ni kuwa Adam apitie majaribio atakayonufaika nayo na kufaidika nayo, yeye na watoto wake, na kurudi kwenye pepo hii akiwa amejaa majaribio yenye kunufaisha. Yaani ni kwamba mtu hawezi kuishi milele bure bure tu vile anavyotaka na kwamba mwenye kuyachunga hayo majaribio kwa kuyamiliki matakwa yake bila ya kukubali kusukumwa na matamanio yake, basi ataishi maisha mazuri ya wema usiokuwa na mwisho. Na mwenye kuwa na msimamo hafifu na akawa mdhaifu mbele ya matamanio yake, atakuwa amepata aliyoyapata Adam majuto, kujaribiwa, taabu na mashaka.

ISMA (Kuhifadhiwa Mitume)

Wameafikiana Waislamu wote kwamba Adam ni katika Mitume, na Mitume kama inavyofahamika ni wenye kuhifadhiwa na madhambi na makosa. Sasa nini maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu; "Akawahadaa shetani katika hali waliyokuwa nayo?"

Kuna maelezo yanayosema kuwa Adam ana jina la kubandikwa peponi la Abu Muhammad kwa heshima na kutukuzwa, na hakuna mtu mwenye jina la kubandikwa peponi ispokuwa yeye tu.

65

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa ajili hiyo ndio wameonelea wanachuoni kuwa iko haja kubwa ya kufanya utafiti juu ya Isma ya Mitume; kisha kuifasiri Aya hii katika hali ambayo italeta natija. Nasi tunakusanya kauli juu ya hilo kama ifuatavyo ili iwe ni asili katika kila linaloambatana na maudhui haya.

Maana ya Isma ya Mtume ni kutakata na makosa katika kila jambo linaloambatana na dini na hukumu zake, kiasi ambacho atafikilia Mtume utakatifu na elimu na kumjua Mwenyezi Mungu na yale anayoyataka kwa waja wake; kwa hali ambayo inakuwa muhali kuikhalifu, iwe kwa makusudi au kwa kusahau.

Mwenye kuthibitisha Isma kwa Mitume kwa maana hayo na kwa mafungu yake yote yatakayokuja, ataifanyia taawil Aya inayopingana na dhahiri ya msingi huu, kwa kwenda na kanuni ya kiujumla ambayo ni wajibu wa kufanya taawil kwa kuafikiana na dhahiri ya akili. Na, mwenye kukanusha Isma kwa mitume, atabakisha dhahiri kwa dhahiri yake.

Wanavyuoni wa madhehebu mbali mbali wana kauli nyingi katika Isma, zenye kukhitalifiana kwa tofauti za mafungu yafuatayo:

1.    Isma katika itikadi na misingi ya dini; yaani kutakasika kwa Mtume kutokana na ukafiri na ulahidi. Hilo ni lenye kuthibiti kwa kila Mtume kimisingi na kwa maafikiano. Kwani haiingii akilini kuwa Mtume amkanushe yule aliyempa Utume.

2.    Isma katika kufikisha amri za Mwe-nyezi Mungu. Akisema, Mwenyezi Mungu anaamrisha hili na anakataza lile, basi amri itakuwa ile ile aliyoisema. Wameafikiana Shia Imamiya kuthibiti Isma hii kwa kila Mtume.

Kwa sababu lengo la kufikisha ni kuwachukua wale wanaokalifiwa na sharia kwenye haki. Akikosea mwenye kufikisha itakuwa lengo la kufikisha limebatilika. Hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:

li

"Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake)"

Na kauli yake:

(53:3)

66

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Na anachowapa Mtume kipokeeni na anachowakataza jiepusheni nacho."

(59:7)

Kwa maneno mengine Isma ya Mitume haiwezi kuepukana kabisa na kusema kuwa kauli yao, kitendo na uthibittisho wao ni hoja na dalili.

Baada ya Razi kusema katika tafsiri yake: "Wameafikiana Waislamu kwamba kukosea katika kufikisha hakujuzu kwa kusudi au kusahau," aliendelea kusema: "Wako watu wanaojuzisha hilo kwa kusahau." Sijui aliwakusudia watu gani.

3. Isma katika Fatwa; yaani Mtume kufutu kitu cha wote; kama kuharamisha riba na kuhalalisha biashara. Razi ametaja kifungu hiki katika tafsiri yake kwa kusema:

"Wameafikiana kwamba kukosea Mtume katika hilo hakujuzu kwa kuku-sudia ama kwa kusahau, wengine wamejuzisha na wengine hawakujuzisha."

Kifungu hiki kinarudi katika kifungu cha pili cha kufikisha. Inatakikana kifanywe kifungu cha tatu ni Isma katika hukumu sio fatwa.

16

Wameafikiana Imamiya kwamba Mtume ni mwenye kuhifadhiwa na makosa katika hukumu kama ilivyo katika kufikisha; pamoja na kwamba kwao wamenakili kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.) kwamba yeye amesema:

"Hakika mimi ninahukumu kati yenu kwa hoja (ushahidi) na yamini. Mimi ni mtu. Nyinyi mkiwa na ugomvi, huenda mmoja akawa mjanja kuliko adui yake - kwa hiyo nitahukumu kutokana na nilivyosikia kutoka kwake, basi kama mtu nikimpa haki ya ndugu yake asichukue; kwani ninamkatia kipande cha moto." Kama ni kosa hapo katika hukumu yake, imetokana na hoja au kiapo n.k. yaani katika kutegemea hukumu sio katika hakimu mwenyewe.

4. Isma katika vitendo vya Mitume na mwenendo wao hasa. Amesema Iji katika Mawaqif Juz.5; "Hakika Hashawiya wanajuzisha kwa Mitume kufanya madhambi makubwa; kama uwongo, kwa makusudi au kusahau; na wamekataa Ash'aira - yaani Sunni - kwa kusudi sio

Tofauti ya hukumu na Fatwa ni kwamba maudhui ya hukumu yanakuwa ni mahsusi kama kadhi kuhukumu mapatano yaliyopita kati ya Zaid na Bakari ni batili. Ama maudhui ya Fatwa yanakuwa ni kwa wote kama kuhalalisha biashara na kuharamisha riba.

67

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kusahau. Ama madhambi madogo inajuzu kwao hata kwa kusudi wachilia mbali kusahau."

Wamesema Imamiya: Hakika Mitume ni wenye kuhifadhiwa katika kila wanayoyasema na wanayoyatenda; kama vile ambavyo wamehifadhiwa katika itikadi na kufikisha. Ni muhali kwao kufanya madhambi madogo, wachilia mbali makubwa, na wala hayawezi kuwatokea kabisa, si kwa kukusudia wala kusahau, si kabla ya Utume wala baada yake.

Aya yoyote ambayo haiafikiani dhahiri yake na msingi huu, basi wameiletea taawil. Wakasema katika Adam kula tunda, kwamba kukatazwa kule hakukua ni kwa uharamu au kwa ibada, kama vile kukatazwa kuzini na kuiba, bali kulikuwa ni kimwongozo na nasaha tu; kama kumwambia mtu unayemtakia heri, 'usinunue nguo hii kwa sababu sio nzuri,' ikiwa hakukusikia, basi atakuwa hakufanya haramu wala hakumdhulumu mtu; atakuwa amejidhulumu yeye mwenyewe na amefanya jambo ambalo ilikuwa ni vizuri asilifanye.

Kimsingi kula tunda hakuambatani na kumdhulumu mtu yeyote isipokuwa kula tu. Kwa hivyo maana ya toba ya Adam inakuwa ni toba ya kuacha kutenda jambo lenye kupendekezwa na lililo bora. Na, jambo la toba ni jepesi sana, kwani mara nyingi Mitume na watu wema hulikariri neno "Namtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia."

Inatosha kuwa ni dalili juu ya hilo dua ya Imam Zainul-Abidin katika Sahifa Sajjadiyya yenye kujulikana kwa dua ya toba akisema: "Ninaomba msamaha kutokana na ujinga wangu."

AHLUL- BAIT

Amesema Muhyiddini anayejulikana kwa jina Ibnul Arabi katika kitabu chake Futuhatul Makkiya Juz. 1; Uk. 196 chapa ya zamani. "Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtoharisha Mtume wake na kizazi chake kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"...Mwenyezi Mungu anawatakia kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na kuwatakasa kabisa kabisa."

(33:33)

68

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Hakuna kitu kichafu zaidi ya dhambi kwa hivyo hakutegemewi kwa watu wa nyumba (ya Mtume) isipokuwa usafi na utohara, bali wao ni dhati ya utohara." Kisha akasema Ibnul Arabi kwamba Salmanul Farisi ni mwenye kuhifadhiwa na dhambi kwa ushahidi wa Mwenyezi Mungu, na imethibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amesema: "Salman ni katika sisi Ahlul Bait." Kwa hiyo Salman ni mwenye kuhifadhiwa na dhambi kwa ushahidi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Katika juzuu ya pili ya kitabu hicho hicho Uk. 127, amesema: "Hatabaki katika moto mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika waliotumwa na Mwenyezi Mungu, kwa sababu moto kwao unakuwa ni baridi na salama kwa baraka ya Ahlul Bait katika akhera. Ni utukufu ulioje wa baraka za Ahlul Bait!"

40.  Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema                               yangu niliyowaneemesha;                 na tekelezeni ahadi yangu nitatekeleza ahadi yenu; na niogopeni Mimi tu.

41.  Na aminini niliyoyateremsha ambayo                yanasadikisha mliyonayo wala msiwe wa kwanza kuyakataa, wala msiuze ishara zangu kwa thamani ndogo; na niogopeni Mimi tu.

42.  Wala msichanganye haki na batili, na mkaficha haki na hali mnajua.

43.  Na simamisheni swala na toeni zaka na inameni pamoja na wanaoinama.

44. Je, mnawaamrisha watu

69

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kutenda mema na mnajisahau, hali mnasoma Kitabu? Basi je, hamfahamu?

45.  Na takeni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.

46.  Ambao wana yakini kwamba wao watakutana na Mola wao na kwamba watarejea Kwake.

ZIKUMBUKENI NEEMA ZANGU Aya 40 - 46

Mwenyezi Mungu amewataja Mayahudi katika Aya nyingi za Qur'an tukufu. Zimebainisha Aya hizo neema za Mwenyezi Mungu na kuua kwao Mitume bila ya haki. Vile vile zimebainisha uadui wao kwa Musa na Harun (a.s.), kuabudu kwao ndama na kufanywa watumwa na Mafirauni, kisha kukombolewa. Vile vile Aya zimeeleza walivyookoka wasife maji na kuteremshiwa Manna na Salwa. Pia zimeelezea chuki yao hao Mayahudi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.), au njama zao dhidi yake na uadui wao mkubwa kwa Waislamu, kuchukia kwao haki na mengineyo ambayo yatakuja maelezo yake kwa ufafanuzi. Surah ya Ng'ombe, waliyemchinja, hii inaelezea kwa upana sifa na matendo yao.

DHAHIRI YA MAISHA

Aina nyingi za hali ya maisha wanayoishi watu ni natija ya Historia ndefu. Aina ya mavazi tunayovaa, mapishi ya chakula tunachokila na ujenzi wa nyumba tunazokaa, vyote hivi ni kutokana na usanifu wa waliotangulia. Hata meli zinazotumia mashine zimeundwa baada ya majahazi yanayotumia matanga, baada ya kupita vipindi vya maendeleo.

Hakika maigizo ya kihistoria yanafanya kazi kama desturi za kitabia.; sawa na mawimbi yanayotulia kutokana na msukosuko wa kupwa maji na kujaa.

70

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa hivyo matukio yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku na mfungamano tunaokuwa nao na watu wengine, mbaya au mzuri, ni natija ya yaliyopita zamani sana au hivi karibuni.

Hapa ndipo wanafalsafa wakasema: "Historia ni miongoni mwa njia za maarifa. Na Aya hizi ambazo Mwenyezi Mungu anawazungumzia Mayahudi, zina mfungamano mkubwa na Historia yao, kama tutakavyoona.

IS RAIL

Israil ni jina jingine la Yaqub bin Is-haq bin Ibrahim (a.s.), Khalilullah. Is-haq ni ndugu wa Ismail, babuye Mtume Muhammad (s.a.w.). Waarabu na Wayahudi wote wamekutana kwa Ibrahim. Mwenyezi Mungu amesema:

"Mila ya baba yenu Ibrahim."

(22:78)

Katika Majmaul-Bayan imesemwa kwamba Waarabu wote ni uzao wa Ismail; na wengi wasiokuwa Waarabu ni uzao wa Is-haq.

Maana ya Israil katika lugha ya Kiebrania ni Abdullah (mja wa Mungu) Isra ni mja il ni Mwenyezi Mungu.

Alitumia upole Mwenyezi Mungu katika kuwazungumzia Wayahudi kwa kuwategemeza na Mtume mtukufu Israil ili kuwakumbusha nasaba hii tukufu. Huenda wakahisi utukufu ikiwa umo ndani ya nafsi zao; sawa na kusema: "Ewe mtoto wa watu wema! Kuwa kama baba zako na babu zako".

Ama sababu ya kuitwa kwao Yahudi ni kwamba ukoo mmoja kati yao unatokana na Yahudha ambaye ni mtoto wa nne wa Nabii Yaqub. Sehemu ifuatayo tutaeleza kwa muhtasari historia ya Mayahudi kutokana na Aya tuliyonayo.

HISTORIA YA MAYAHUDI

Yatakuja maelezo katika Sura ya Yusuf kwamba Mtume Yaqub (a.s.) alihama na watoto wake kutoka Palestina kwenda Misri, alipo mtoto wake Yusuf (a.s.), akiwa waziri wa Firaun wakati huo. Firaun akawakatia kipande cha ardhi yenye rutuba kwa heshima ya Yusuf. Kikaendelea

71

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kizazi cha Yakub kwa muda kiasi. Lakini Mafiraun waliokuja baadaye waliwakandamiza na kuwapa adhabu na mateso; waliwachinja watoto wao wa kiume wakawaacha wa kike; na wakawafanya watumwa. Kisha Mwenyezi Mungu akawapelekea Mtume aliyekuwa mmoja wao ambaye ni Musa bin Imran, kuwak-omboa na dhulma na utumwa; akawataka warudi Palestina kupigana na akawaahidi ushindi. Wakakataa kwa woga. Mwenyezi Mungu akawapangia kutangatanga katika jangwa la Sinai miaka arobaini. Utakuja ufafanuzi Inshallah.

Katika kipindi hiki Harun alikufa kisha Musa pia akafa. Akachukua uongozi mpwawe Yashua bin Nun. Ilipofika karne ya 13 kabla ya kuzaliwa Nabii Isa (a.s.) walivamia ardhi ya Palestina wakiongozwa na Yoshua wakawafukuza wenyeji; kama kilivyofanya kizazi chao (Wazayuni) katika Palestina mwaka 1948.17 Baada ya Yoshua Mwenyezi Mungu alituma mitume wengi waliotokana na wao.

Mnamo mwaka 596 kabla kuzaliwa Nabii Isa (a.s.), Mfalme wa Babil Nebukadnezzar aliwashambulia akaondoa utawala wao katika Palestina, akawachinja wengi na kuwachukua mateka wengi.

Wakaendelea kuwa chini ya utawala wa Nebukadnezzar mpaka mwaka 538 kabla ya kuzaliwa Isa (a.s.) aliposhindwa na mfalme wa Fursi (Iran ya sasa), ndipo Mayahudi wakapumua. Wakaendelea kuwa chini ya utawala wa Fursi kiasi cha miaka mia mbili, baadaye wakatawaliwa na makhalifa wa Alexandria mkuu. Kisha wakawa chini ya utawala wa Roma.

Ilipofika mwaka 135 kabla ya kuzaliwa Isa (a.s.), Mayahudi walifanya mapinduzi kwa Warumi, lakini hayakufanikiwa. Walifukuzwa Palestina, wakakimbilia sehemu mbali mbali za mashariki na magharibi; wengine Misri na wengine Lebanon na Syria, wengine wakaenda Iraq na wengine Hijaz. Ama Yemen walikujua Mayahudi na kuhamia huko kwa ajili ya biashara tangu zama za Nabii Suleiman ambaye alimwoa Malkia wa Yemen, Bilqis (Malkia wa Sheba).

Neema za Mwenyezi Mungu kwao ambazo Mwenyezi Mungu amezitaja kwa kauli yake; Zikumbukeni neema Zangu nilizowaneemesha, ni nyingi; zikiwa ni pamoja na kuwachagua Mitume kutoka katika kabila lao; kama Musa, Harun, Yoshua, Daud, Suleiman, Ayub, Uzair, Zakaria, Yahya n.k. Ama Maryam, mama yake Isa pia ni Mwisrail, nasaba yake inaishia kwa

Tutaje mifano miwili: kwanza, Wazayuni waliwakusanya wanawake 25 wenye mimba katika kijiji cha Dair Yasin, wakawapasua matumbo yao kwa mabisu na mikuki. Pili, waliwakusanya watu wa kijii cha Zaituni msikitini, kisha wakawalipua kwa baruti.

72

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Nabii Daud (a.s.), lakini Mayahudi hawamkubali Masih mwana wa Maryam na wanadai kwamba Masih aliyetajwa katika Tawrat hajakuja bado.

MUHAMMAD NA MAYAHUDI WA MADINA

Mtume (s.a.w.) alipohamia Madina kutoka Makka, Mayahudi walikuwa na koo tatu: Bani Qaynuqa, Bani Quraydha na Bani Nadhir. Walikuwa wana vilabu vya pombe, madanguro na sehemu za kufugia nguruwe. Na walikuwa wakihodhi dhahabu na fedha, kutengeneza silaha na kufanya biashara ya riba. Kwa ujumla wao ndio waliokuwa wakuu katika mambo ya uchumi mjini Madina, kama walivyo sasa (duniani).

Alipofika Mtume (s.a.w.), Mayahudi walihisi hatari kwa faida zao na mapa to yao ya kibiashara, kwa sababu vijana wa Madina wasingekwenda kwenye maduka na mabucha yao na watu wa Madina wasingekula nyama za nguruwe. Maana yake ni kwamba mayahudi wangepoteza vitega uchumi vyote.

Kwa ajili hiyo wakawa wanamchimbia vitimbi Mtume mtukufu (s.a.w.) na kupanga njama pamoja na makafiri dhidi ya Waislamu, kama zinavyofanya leo nguvu za dola kubwa zinavyolinda maslahi yake.

Mtume naye ni kama aliyejua hilo pale alipoingia Madina, akataka kuwatafutia hoja na kuwaadhibu kwa kauli zao. Kwa hiyo akawachukulia upole, akawekeana nao mkataba: kwamba wao wana uhuru katika dini yao na Mahekalu yao kwa masharti ya kuwa wasimsaidie adui na kama wakiamua kupigana pamoja na Waislamu, basi watapata fungu katika ngawira. Ni juu yao kushirikiana na Waislamu, kuulinda mji wa Madina, kwa sababu mji ni wa wote sio wa kundi maalum.

Lakini walivunja ahadi upesi sana. Tangu lini ahadi ikasimama mbele ya maslahi? Je inaingia akilini usalama na hadaa kuwa pamoja? Vipi anaweza kuishi mbwa mwitu pamoja na punda kwa amani? Kutafaa nini kukumbushwa neema, hadhari na nasaha kama zikigongana na maslahi ya kiutu na mapatano ya kibiashara?

Imeelezwa katika kitabu Muhammad Rasullul-huriyya (Muhammad Mtume wa Uhuru) hivi: "Mtume aliwaambia wafanyabiashara wa Kiislamu waanzishe soko jipya mjini Madina, wakaanzisha; likawa na nguvu soko hilo; wafanyi biashara wageni wakawa wanaelekea huko, na soko la Mayahudi likaathirika. Kwa sababu biashara katika soko la waislamu ilikuwa ya uadilifu sana kwa muuzaji na mteja."

73

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Hiyo peke yake ilitosha kujaza nyoyo za Mayahudi hasadi na chuki kwa Muhammad (s.a.w.) na kuwafanya wavunje ahadi.

MAELEZO

Mwenyezi Mungu ameanza kuwaambia Mayahudi kukumbuka neema zake kwao. Miongoni mwa hizo neema ni kuwaletea Mitume wengi na kuwatukuza kwa Tawrat na Zabur. Vile vile kuwakomboa katika utumwa wa Firaun, kuokoka kwao kutokana na kufa maji, kuwateremshia Manna na Salwa, kuwapa milki na ufalme katika zama za Mtume Suleiman na mengineyo ambayo yanawajibisha kuamini na kushukuru na wala sio kukanusha na kukufuru.

Unaweza kuuliza: Kwa nini msemo unawaelekea Mayahudi wa Madina pamoja na kujua kuwa neema zinazoelezwa zilikuwa kwa baba zao na sio kwao?

Jibu: Neema kwa baba ni neema kwa watoto vile vile; ambapo mtoto anapata utukufu kutokana na baba yake. Zaidi ya hayo ni kwamba umma wote ni mmoja.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha neema zake aliwaambia: Tekelezeni ahadi yangu nitatekeleza ahadi yenu.

Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kuchukua yale yanayofahamiwa na maumbile na yale ambayo vimeteremshwa vitabu kwayo, ikiwa ni pamoja na kumwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake na kufanya amali kwa hukmu zake. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi katika Tawrat kwamba Yeye atawapelekea Mtume anayeitwa Muhammad. Fikra hii ndiyo wanayoielezea wafasiri wengi nayo ndiyo inayotolewa ushahidi na Qur'an."

Ama ahadi ya Mayahudi ni ile ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao. Na, kila mwenye kuamini akafanya amali njema basi Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu siku ya Kiyama.

Imesemekana maana yake ni kwamba kama wakimcha Mwenyezi Mungu, basi atawainua katika maisha haya ya duniani. Tutaeleza fikra ya malipo katika dunia mahali pake Inshaallah.

Kisha Mwenyezi Mungu amewaamrisha kuamini Qur'an na wasifanye haraka kuikanusha, kumkanusha Muhammad na kutaka maslahi tu. Na kwamba ni juu yao kuisimamisha swala na kutoa zaka ili wazitakase nafsi na mali zao.

74

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: "Je, mnawaamrisha watu kutenda mema na mnajisahau, hali mnasoma kitabu," inawaelekea viongozi na wakubwa, sio kwa watu wote, kwa sababu watu wengine ni wafuasi, na viongozi ndio wenye kufuatwa. Wao ndio wanaoficha haki na hali wanaijua na wanatoa mawaidha lakini hawayafuati.

Tunakariri tena kwamba mawaidha na nasaha haziendi pamoja na kutaka maslahi; na hayawezi kuacha athari yoyote isipokuwa katika nafsi isiyotaka maslahi na isiyokuwa na lengo lolote zaidi ya haki.

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) "Na takeni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali" Imeelezwa tena katika Aya ya 153 ya Sura hii, kwa hivyo utakuja ufafanuzi wake huko Inshallah.

47. Enyi wana wa Israil, ikumbukeni

Yangu

neema

niliyowaneemesha,                 na l£,

nikawatukuza kuliko viumbe

wengine.

48. Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa nafsi kwa lolote. Wala hayatakubaliwa                 kwake

maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa.

(£ A)

WANA WA ISRAIL TENA!

Aya 47 - 48

MAELEZO

Enyi wana wa Israil ikumbukeni neema Yangu.

Aya hii inatilia mkazo Aya iliyotangulia, na ni maandalizi kwa yatakayokuja baada yake. Tutaonyesha katika sehemu itakayofuatia hekima ya kukaririka. Makusudio ya kukumbuka hapa ni kushukuru; yaani zishukuruni neema zangu kwa usikizi na twaa.

75

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

Na nikawatukuza kuliko viumbe wengine.

2 Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha kuliko mataifa mengine ya wakati huo. Herufi lam katika neno Alamin ni ya kuenea kwa kawaida, sio kuenea kwa kiuhakika. Inatosha kuwa ubora ni katika upande mmoja na sio pande zote. Upande ambao Waisrail wamepambanuka na watu wengine ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwapelekea idadi ya Mitume; kwa mfano Musa, Harun, Yoshua, Zakaria na Yahya na wengineo. Wote hao ni Waisrail.

Vyovyote ilivyo, kuwa bora kwao kwa watu wa zama zao kwa upande fulani, hakufahamishi kuwa bora katika kila upande kwa watu wa wakati huo; wala sio kwamba mtu wao ni bora kuliko mtu mwingine. Bali kule kuwa Mitume wengi wamekuja kutokana na kabila lao ni hoja juu yao na wala sio hoja yao, kwa sababu hilo linafahamisha kwamba wao walikuwa katika upotevu sana, ikawa kuna haja sana wapate waonyaji na wahadharishaji.

Na ogopeni siku mbayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa lolote.

Yaani kila mtu na lake hakuna dhahiri wala batini, hakuna kusaidiana wala kuoneana huruma.

"Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake."

(80:34)

Wala hayatakubaliwa kwake (hiyo nafsi) maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa.

Yaani Kiyama ni sawa na mauti, haufai usaidizi wowote, haitafaa fidiya yoyote, hata ikiwa ghali, wala haitazuia nguvu yoyote hata iwe kubwa kiasi gani. Hakuna chochote isipokuwa Rehema ya Mwenyezi Mungu:

"Kama hataturehemu Mola wetu na kutusamehe, shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara."

bila

(7:149)

76

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

KUKARIRIKA KATIKA QUR'AN

2 Sura Al-Baqarah

Mara ya pili Mwenyezi Mungu anawaku-mbusha wana Israil neema Zake na amerudia baada ya Aya tano. Hiyo siyo Aya peke yake iliyorudiwa katika Qur'an, zimeka-ririka Aya nyingi hasa zile zinazofungamana na wana wa Israil pamoja na Musa (a.s.). Wengi hujiuliza sababu ya kukaririka Aya.Wameafikiana wafasiri kwamba hekima ya kukaririka ni kutilia mkazo.

Baada ya kupita siku, wakuu wa vyama, wanasiasa, wafanyibiashara na wenye mashirika wamegundua kwamba, kukar-irika jambo ndio njia nzuri ya kulipendekeza, kulikinaisha na kulifanyia propaganda. Kwa ajili hiyo ndio wakaweka mitindo mbali mbali ya matangazo, kukawa na watu maalum wa kuhusika nayo na yakawa ghali sana.

Gustave Lebon anasema katika kitabu chake kiitwacho The man and his work: "Mwenye kulikariri tamko mara kwa mara hulibadilisha kuwa itikadi.

Dr Gibson katika kitabu kilichotarjumiwa kwa kiarabu kayfa tufakkir"(Vipi utafikiri)" anasema "Ibara zina sumaku zinapokaririka mara kwa mara mbele ya macho yetu na masikio yetu, zinapumbaza akili zetu kabisa."

Kwa hivyo basi Qur'an inakariri kwa mfumo mwingine pamoja na kuzidisha makemeo na mengineyo kwa kiasi cha hekima inavyotaka.

SHUFAA (uombezi)

Hapana budi shufaa iwe na pande tatu: Mwenye kuombwa, mwenye kuombewa na muombezi ambaye anakuwa kati ya hao wawili, anaomba kwa yule wa kwanza ili amsaidie wa pili ni sawa apate idhini ya yule mwenye kuombwa au la. Hiyo ndiyo Shufaa kwa viumbe. Ama shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) maana yake ni msamaha na maghufira kwa mwenye dhambi; haitakuwa shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake.

Amesema mwenye Majmaul-Bayan "Shufaa kwetu ni yenye kuhusika na kuondoa madhara na kuondoa mateso kwa mumin mwenye dhambi."

Muutazila na Khawarij wamekanusha Shufaa ya Muhammad (s.a.w.) kwa wenye madhambi makubwa katika umati wake, kwa maana hii tuliyoinakili kutoka kwa mwenye Majmaul-Bayan, lakini Imamiya na Ash'aira wameithibitisha kwamba iko.

Akili haihukumu kutokea Shufaa au kutotokea, lakini haioni pingamizi yoyote ya kupatikana. Kwa hiyo, kusihi kwake na kuthibiti kwake

77

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kutategemea kunakili kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ambaye kumemthibitikia kunakili huko, basi ni wajibu kwake kuamini Shufaa, na kama hakuthibitikiwa basi atasamehewa. Kwa hali hiyo inatubainika kuwa shufaa si msingi wa dini na kwamba mwenye kuikanusha na huku anamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi huyo ni Mwislamu bila shaka.

Tukirudi kwenye Aya za Qur'an tunakuta nyingine zinakanusha; kama ile inayosema:

"...Siku ambayo hapatakuwa na bishara wala urafiki wala Shufaa (uombezi)...."

(2:254)

Hapo inaonyesha kukanusha Shufaa kabisa. Na Aya nyingine zinathibitisha kwa sharti; kama ile inayosema:

"....Hautafaa chochote uombezi (shufaa) wao isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia."

(53:26)

Tukiziunganisha Aya mbili hizi na tukazikusanya pamoja, natija itakuwa, Mwenyezi Mungu atakubali Shufaa kutoka kwa mwombezi baada ya kumpa idhini. Sio lazima kupatikana idhini ya Mwenyezi Mungu kwa jina la mmoja mmoja, bali inatosha tu kwa Mtume kujua kwamba Shufaa ni halali ikiwa yule mwenye kuombewa si katika wenye kuwakandamiza watu na kunyang'anya riziki zao; bali ni katika watu wa kawaida tu, ambao wanafanya madhambi ya kawaida.

Kwa maneno mengine ni kwamba makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu kwa Shufaa ni kumpa wahyi Mtume wake kwamba Mimi nimekuruhusu kuwaombea uwatakao katika Umma wako ambao wamefanya madhambi maalum. Hapo basi mambo ya hao wenye madhambi yatakuwa mikononi mwa Mtume (s.a.w.); naye atamwombea yule mwenye kustahiki kuombewa. Imethibiti kwamba yeye amesema:

78

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Nimeuweka akiba uombezi wangu kuwaombea wenye madhambi makubwa katika Umma wangu."

Sisi tuna yakini kuthibiti Shufaa katika Uislamu. Lakini hatujui kwa ufafanuzi; wakati huo huo tunaamini kwa imani ya mkato, kwamba mwombezi bora wa mtu ni matendo yake, na kwamba kitakachowaombea wenye dhambi ni toba. Hakika Mwenyezi Mungu haweki kizuizi kwa mwenye kutaka kuokoka akiwa na ikhlasi na akakimbilia kwenye ukarimu wa Mwenyezi Mungu hali ya kunyenyekea.

49. Na tulipowaokoa kwa watu wa Firaun waliowapa adhabu mbaya; wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike; na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu.

50. Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun na hali mwatizama.

NA TULIPOWAOKOA Aya 49 - 50 LUGHA

Neno Aal lina maana ya kurudi; kwa hiyo kila mwenye kurudiwa kwa nasaba, rai au itikadi basi yeye ni Aal wa wale wanaomrudia, kisha likawa linatumiwa zaidi kwa maana ya watu wa nyumba ya huyo mtu atakayetajwa, lakini hawezi kuitwa mtu Al mpaka awe na utukufu fulani.

Makusudio ya Al-Firaun hapa ni wafuasi wake ambao walikuwa wakiwatesa wana wa Israil kwa amri yake. Abu-Hayan Al-Andalusi (Mhispania) amesema: Katika tafsir yake kubwa Al-Bahrul Muhit;

79

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Firaun ni lakabu (msimbo) ya wafalme wa Misri wakati huo; kama vile Kisra wa Fursi, Kaizari wa Roma, Najashi wa Uhabeshi, Tubba wa Yemen na Khaqani wa Uturuki.

Lakini alhamdulillah misimbo hii yote imebakia kuwa ni vigano tu! MAELEZO

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha neema zake kwao kwa ujumla, sasa anawakumbusha kwa ufafanuzi. Bora zaidi ya neema aliyoidokeza ni kuwaokoa na Firaun na wafuasi wake ambao waliwapa Mayahudi adhabu kali. Mwenyezi Mungu ameifasiri adhabu hiyo kwa kusema:

wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike.

Yaani wanawaua watoto wanaume na kuwaacha wanawake waje kuwafanya watumishi.

■ 18

Zaidi ya hayo Wamisri walikuwa wakiwadhalilisha Wayahudi kwa kuwatuma kazi za kuvunja mawe, kuchimba mifereji na kazi nyinginezo za sulubu.

Msemo umewaelekea Mayahudi waliokuwepo zama za Mtume Muhammad (s.a.w.), kwa sababu wao walikuwa kwenye dini ya mababu zao na waliridhia amali zao. Na, mwenye kupenda amali ya watu wengine anakuwa ameshirikiana nao.

Na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu:

Yaani, Enyi wana wa Israil, Mwenyezi Mungu amewatahini katika shida na raha, ili ijulikane kuwa je mtapigana jihadi na kuwa wavumilivi katika shida? Na je, mtashukuru raha? Au mtasalimu amri katika shida na mkufuru katika neema?

Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamtahini mtu ili ajue, la! Yeye anajua lenye kuwa kabla ya kuwa; isipokuwa yeye anamtahini mtu kwa ajili ya kusimamisha hoja juu yake. Kwani hakuna madai kwa asiyekuwa na hoja, hata kama yenye kudaiwa yanathibiti katika elimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.).

Mwenye Majmaul Bayan anasema: Firaun aliota mambo yaliyomtisha. Wakamfasiria makuhani kuwa atazaliwa kijana wa kiume kutoka kwa wana wa Israil ambaye atakuja muua, ndipo Firaun akawafanyia hivyo wana wa Israil.

80

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu amewaonyesha Waisrail neema ya pili aliposema:

Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun

Yaani tulitenga bahari na tukafanya njia kumi na mbili kwa hisabu ya wajukuu. Wajukuu katika wana wa Israil ni koo katika kizazi cha Yaqub (a.s.)

Kwa ufupi Wayahudi walikuwa katika unyonge na udhalili wa hali ya juu; na adui yao alikuwa na nguvu za hali ya juu.

Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabadilisha hali hiyo kupitia mikononi mwa Mtume wake Musa (a.s.), wao wakawa ndio wenye nguvu; na adui yao akawa dhalili, hilo wakaliona kwa macho yao; kama inavyosema Aya: "Na hali nyinyi mnaangalia".

Mwenyezi Mungu alimdhalilishia yule aliyewadhalilisha na akamwangamiza yule aliyetaka kuwaangamiza. Kwa hivyo basi wamelazimiana na hoja na imewalazimu kuwaidhika na kuzingatia, wala wasiwafanyie wengine yale waliyofanyiwa na wengine.

Lakini hivi leo mfano ule ule waliokuwa wakifanyiwa na Firaun ndio wanawafanyia Wapelestina. Na waendelee hivyo, lakini wajue hali itakuja wabadilikia tu, na yatawafika yale yaliyompata Firaun. Na waangalie ilivyokuwa kwa Nebukadnezzar na Warumi; na kwamba shujaa huvuma kisha akaisha. Jambo la kustaajabisha sana kwa mtu ni kwamba anapokuwa kwenye shida, kisha akaokolewa na Mwenyezi Mungu, basi hupetuka mipaka akafanya uovu na kusahau kila kitu.

Wafasiri wengi wamesema, kwamba bahari iliyotajwa ni Bahari nyekundu (Red Sea).

51. Na tulipomwahidi Musa masiku &* i'.'           *           ■                °

arobaini mkafanya ndama (kuwa y Mungu) badala ya Mwenyezi liif'« Mungu mkawa madhalimu (wa nafsi zenu).

52. Kisha tukawasamehe baada ya '■' hayo ili mpate kushukuru.

81

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

53. Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi           ili           mpate

kuongoka.

NA TULIPOMWAHIDI Aya 51 - 53 LUGHA

Neno Musa kwa lugha ya Kiarabu lina maana ya kifaa cha kunyolea nywele kilichotengezwa kutokana na chuma; lakini maana yanayokusuduwa kwa Musa bin Imran siyo ya Kiarabu, bali ni ya Kikibti ambayo ni matamko mawili: Mu lenye maana ya maji na Sa lenye maana ya mti. Kwa hiyo maana ya Musa ni maji ya mti,

Ama maana ya kuitwa Maji ya mti, kama ilivyoelezwa katika Majmaul-Bayan, ni kwamba wajakazi wa Asiya(mke wa Firaun), walitoka kwenda kuoga wakakuta sanduku lililokuwa na Musa ndani yake baina ya maji na mti; wakawa naye.

MAELEZO

Baada ya Firaun kuangamizwa na Mwenyezi Mungu na waliokuwa pamoja naye, Waisrail Walipumua, wakarudi Misri wakiwa salama; kama livyoelezwa katika Majmau. Wakati huo, Tawrat ilikuwa bado haijateremshwa, wakamtaka Musa awaletee kitabu kutoka kwa mola wao. Basi Mwenyezi Mungu akamwahidi kumteremshia Tawrat na akamwekea wakati. Musa akawaambia:

"Hakika Mola wangu ameniahidi kitabu ambacho ndani yake mna ubainifu wa ambayo ni wajibu kwenu kuyafanya na kuyaacha."

Akawambia wakati wake ambao ni masiku arobaini, na masiku hayo -kama ilivyosemwa - ni mwezi wa Dhul-Qaada, na siku kumi za mwezi wa Dhul-Hijja.

Musa akenda kwa Mola wake ili awachukulie watu wake kitabu; ndugu yake Harun akawa naibu wake. Kabla ya kwisha muda wa kuja Musa,

82

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

walianza kuabudu ndama badala ya Mwenyezi Mungu, wakajidhulimu wao wenyewe.

Hayo ndiyo maana ya dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu ( wa nafsi zenu)."

Baada ya Musa kurejea kwa watu wake, walitubia na wakarudi kwa Mola wao; Mwenyezi Mungu akawakubali toba yao na hii ni neema ya tatu ambayo imeelezewa katika Aya: Kisha tukawasamehe baada ya hayo.

Ama neema ya nne ni kitabu cha Mwenyezi Mungu: "Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka." Kitabu chenyewe ni Tawrat; yenye kukusanya kila kitu kwa ajili ya kubainisha haki na batili, na halali na haramu.

Kunganisha kati ya neno, kitabu na kupambanua, ni kuunganisha sifa kwenye kile kinashosifiwa. Kwa muhtasari ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakumbusha Waisrail katika Aya zilizotangulia, neema nne. Kuwaokoa kuchinjiwa watoto wao wa kiume na kuachwa wa kike wawe watumwa, kuangamia kwa Firaun, kusamehewa na kuletewa Tawrat.

Maelezo mazuri zaidi niliyoyasoma kuhusu maudhui haya ni kauli ya Abu Hayan Al-Andulusi katika Tafsir Al -Bahrul Muhit; namnukuu:

"Tazama uzuri wa safu hizi ambazo zimepangika kwa mpango wa mtungo wa lulu na wa sayari katika falaki zake, kila safu katika hizo, yaani neema, imeishia kwa mnasaba wake na ikafikia daraja ya juu ya ufasaha ukitoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mdomoni mwa Muhammad mwaminifu wake, bila ya kusoma kitabu chochote kabla yake, wala kuandika kwa mkono wake."

Abu Hayan anaonyesha kuwa mpangilio huo wenye kupangika vizuri ni katika miujiza ya Muhammad; kwamba yeye anauelezea bila ya kujifundisha.

Mwenyezi Mungu awarehemu wahenga, awasamehe na awape neema nyingi. Kwani hakika wao hawakuona chochote chenye harufu ya kuitilia mkazo dini hii na Mtume wake mtukufu isipokuwa walikinyooshea shingo kwa pupa na shauku; wakafanya haraka kukisherehesha, kukifafanua na kukitolea dalili. Lakini tuko wapi sisi wanavyuoni wa sasa ambao twapupia zaidi dunia; hatuoni umuhimu wowote isipokuwa umuhimu wetu tu; wala matatizo isipokuwa matatizo ya watoto wetu tu! Tuko wapi

83

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

sisi na hao watukufu waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kuutukuza Uislamu na Mtume wa Uislamu? Mwenyezi Mungu awasamehe na awainue, na kila mwenye kuitumikia dini, kwenye daraja ya juu.

54.   Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejidhulumu kwa kufanya kwenu ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na jiueni; hilo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Basi akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba Mwenye kurehemu.

55.   Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu waziwazi. Ukawanyakua ukelele na hali mwatizama.

56.   Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

57.  Tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa: Kuleni katika vitu vizuri tulivyowaruzuku.                     Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu wenyewe.

84

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

MUSA ALIPOWAAMBIA WATU WAKE Aya 54 - 57 LUGHA

Manna ni kitu fulani kinachonata mithili ya asali, na Salwa ni tombo (aina ya ndege wa jamii ya kware, kama kuku).

MAELEZO

"Na Musa alipowaambia watu wake. Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mumejidhulumu kwa kumfanya kwenu Ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu."

Maana yoyote inayofahamika kwa kusikia tu haihitaji tafsiri, bali kuifasiri na kuisherehesha ni ufedhuli tu! Na Aya hii iko katika hali hiyo.

Na jiueni

Makusudio ya kujiua yako wazi, ni kujitoa roho: wala hapana haja ya kufasiri vingine, kwa maana ya kuhalifu mapenzi na kuidhalilisha nafsi kwa kukiri dhambi na makosa au kumwabudu sana Mwenyezi Mungu; kama ilivyosemwa. Makusudio ya kujiua hapa, ni baadhi wawaue wengine. Kwa hivyo yule ambaye hakurtadi dini yake kwa kuabudu ndama ndio atamuua yule aliyertadi dini yake. Sawa na kusema kwake Mwenyezi Mungu:

"...Mnapoingia katika majumba jitoleeni salamu...."

(24:61)

Na vile vile kusema kwake:"...Wala msijikejeli: yaani msikejeliane

(49:11)

Amesema Tabrasi katika Majmaul-Bayan kwa upande wa Shia, na Razi katika Tafsir Al-Kabir, kwa upande wa Sunni, kuwa Mwenyezi Mungu aliijaalia toba yao ni huko kujiua, sio kwamba wajiue baada ya kutubia. Hukumu hii ina mfano wake katika sharia ya Kiislamu, pale ulipozingatia kuua kuwa ni hadi na adhabu ya kosa la kurtadi. Hilo tutalieleza katika kifungu cha kurtadi kinachofuatia.

Zinaendelea Aya kueleza maovu ya Waisrail:

85

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpake tumwone Mungu waziwazi

Wakati Musa alipowaendea na Tawrat, baadhi yao walisema:

"Hatuamini kuwa kitabu hiki kinatoka kwa Mungu mpaka tumwone kwa macho; bila ya kizuwizi chochote kati yetu sisi na Yeye; na atueleze ana kwa ana kuwa Yeye amekutuma na kitabu hiki."

Sijui kama wale wanaokanusha kuwepo Mwenyezi Mungu wakati huu, kwa kuwa tu hawajamuona kwa wazi, wanategemea Waisrail na inadi yao? Au vipi?

Mayahudi walimwambia Musa: "Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu." Hawa wa sasa nao wanasema: " Hakuna chochote chenye kupatiana isipokuwa kile tunachoweza kukiona kwa jicho, kukigusa kwa mkono, kukinusa kwa pua au kukionja kwa mdomo." Hivyo ndivyo inavyokaririka historia ya picha ya upinzani wa haki katika kila kizazi.

Yakawanyakua mauti ya ghafla na hali mwalizania

Yaani adhabu kutoka mbinguni iliwapata wale waliomwambia Musa hatukuamini mpaka tumwone Mungu wazi wazi, wakaangamizwa mbele ya macho ya wale wasiopinga.

Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

Baadhi ya wafasiri kama vile Muhamad Abduh, katika tafsiri Al-Manar, amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuwarudishia uhai mara ya pili baada ya kuchukuliwa na ukelele; na kwamba makusudio ya kufufuliwa kwao ni kizazi chao kuwa kingi." Wengine wakasema kuwa sio hivyo, hayo hayafahamiki kutokana na dhahiri yake ilivyo, na kwamba waliorudishwa ni wale wale waliouliwa na ukelele. Na hii ndiyo sawa, kwani hapana sababu inayolazimisha taawil, madamu kurudishwa kuwa hai kunawezekana kiakili.

Na hilo lilimtokea Uzair, kama inavyofahamisha Aya:

"Akasema: Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu baada ya kufa kwake? Mwenyezi Mungu Akamfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua...".

(2:259)

Kimsingi, lililotokea haliwezi kuwa muhali. Kwa hakika inaonyesha kwamba makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Yakawanyakua

86

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

mauti ya ghafla," na kauli yake "tukawafufua" ni wale waliokuwa wakati wa Musa waliosema: "Mpaka tumwone Mungu waziwazi."

Kwa hiyo, kauli haiwahusu Mayahudi waliokuwa na mtume, msemo umeele-kezwa kwao kwa kuangalia kuwa wanatokana na kizazi kilichosema hivyo.

Tukawatilia kivuli cha mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa.

Hayo yaliyotokea wakati Waisrail walipotoka Misri wakahangaika katika jangwa la Sinai, kusikokuwa na majengo; wakamlalamikia Musa kwa joto la jua; Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa wingu lililowafunika na kuwakinga na joto la jua kali. Vile vile Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa Manna na Salwa ili wale. Yatakuja maelezo katika tafsiri ya Aya ya 60 kuwa maji yaliwabubujikia kutoka katika jiwe alilolipiga Musa kwa fimbo yake.

Inashangaza kuona baadhi ya wafasiri, wakifasiri yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu kuyabainisha; kama vile idadi ya waliojiua kwa toba ya kuabudu ndama, kuwa ni watu elfu moja; vile vile walionyakuliwa kuwa ni watu sabini.

Ama kuhusu Manna, wanadai kila mtu alikuwa akipata pishi moja na kwamba Salwa ilikuwa ikishuka kutoka mbinguni ikiwa moto moto huku ikifuka moshi, na mengineyo ambayo hayana kauli yoyote iliyopokewa au kudhaniwa. Imethibiti Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.): "Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia mambo si kwa kusahau, ni kwa kuwaonea huruma, kwa hiyo msijikalifishe nayo."

Katika Nahjul-Balagha amesema Imam AN (a.s.): "Hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhisha faradhi msizipoteze, na amewawekea mipaka msipetuke; na ameyakataza mambo basi msifanye; na ameyanyamazia mambo si kwa kusahau, basi msijikalifishe (nayo)."

Na hawakutudhulumu sisi, lakini wamejidhulumu wenyewe.

Kukanusha dhulma kwa Mwenyezi Mungu ni sawa na kukanusha kuwa na watoto na mshirika; yaani kumwepusha kabisa na hilo; sawa na kumwambia mseja kuwa hana mtoto.

Ama kujidhulumu kwa Mayahudi ni kwa sababu ya usafihi wao na kuzikanusha neema za Mwenyezi Mungu ambaye hanufaiki na twaa ya mwenye kumtii wala hayamdhuru maasi ya mwenye kuasi na madhara

87

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

ya uasi yanamrudia mwasi. Anasema Ali bin Abu Twalib (a.s.): "Ewe mwanadamu ukiona Mola wako anaendelea kukuneemesha nawe unamwasi, basi mhadhari."

Kwa ufupi Aya hizi zinaonyesha ibada ya Waisrail kwa ndama, kutubia kwao kwa kujiua na kutaka kwao kumwona Mwenyezi Mungu. Vile vile kuangamia kwao na kufufuliwa kwao, kufunikwa na kiwingu na kulishwa Manna na Salwa.. Tutaelezea kisa cha Nabii Musa na Waisrail katika surah ya Maida (5) Inshallah. Waliposema kumwambia Musa:

"...Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane sisi tutakaa hapa"

(5:24)

Hilo ni tamko linaloonyesha ukhabithi na uduni wa Mayahudi.

Wa kwanza waliogundua uhabithi na uduni wao ni watu wa Firaun ambao waliwachinja watoto wao wa kiume na kuwaacha wa kike.

Kumwona Mungu

Kutokana na Aya tukufu: "Mpaka tumwone Mungu waziwazi" tutaonyesha mzozo uliopo katika madhehebu ya Kiislamu na tofauti zao kuwa akili inajuzisha kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho au la!

Wamesema Ash'ari (Sunni): "Hakika kuonekana Mungu kwa macho kunawezekana kiakili, kwa sababu Yeye yuko na kila kilichopo kinawezekana kuonekana."

Imamiya na Mu'tazila wamesema; "Haijuzu kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho katika hali yoyote ile, si duniani wala akhera, kwa sababu Yeye si umbo hata akaonekana, wala haingii katika umbo wala upande fulani."

Baada ya akili kuthibitisha kutoonekana, wamechukulia kwamba ataonekana kiakili sio kwa macho na kwa hakika ya imani sio ya viungo vya mwili, kwa mujibu wa alivyosema mwanafalsafa mkubwa na mashuhuri, Muhammad bin Ibrahim Shirazi, maarufu kwa jina la Mulla Sadra.

Katika aliyoyatolea dalili Mulla Sadra kuhusu kutoonekana, ni kauli yake: "Kuhisi kitu ni hali inayozuka kwa kile kinachohisi kikikutanishwa na

88

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kinachohisiwa kilichozuka. Hivyo basi, kulazimisha kitu ambacho hakikuzuka kuwa kinahisiwa ni kama kulazimisha kitu kisicho na upande kuwa kina upande."

Kauli yake hii - kama ninavyoona - ni kwamba jicho haliwezi kuona kitu isipokuwa kwa sharti mbili: Liwe linaweza kuona na kiwe kile kinachoangaliwa kinaweza kuonekana kwa jicho. Hilo ni jambo la msingi; likikosa jicho uwezo wa kuona, au kikiwa kitu hakina uwezo wa kuonekana; itakuwa kuona hakuko. Jicho ni dogo na duni zaidi kuweza kuona dhati tukufu; kama vile ambavyo, Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kuonekana na jicho.

Nilipokuwa nasoma ibara hii, tukufu akili yangu ilienda kwa mwanafalsafa wa Kiingereza John Luk, anayesema kuwa: kitu kina sifa yake ya kwanza yenye kukithibitikia, ambayo haipambanuki nayo, ni sawa mtu aitambue au asiitambue; kama vile vitu vinavyosimamisha kitu hicho.

Vile vile kuna sifa ya pili ambayo haiwezi kuepukana na kuhisiwa au kujulikana; kama rangi, sauti na ladha. Rangi siyo sifa ya kitu, kama inavyoonekana, isipokuwa ni mawimbi ya kimwangaza yanayohusika kati ya kitu na jicho; kama wasemavyo wataalamu. Vile vile sauti ni mawimbi ya kihewa; na ladha isingekuweko kama si mdomo. Kwa hiyo ladha inahitilafiana kwa uzima wa mdomo na ugonjwa. Kwa ufupi anataka kueleza kuwa hakuna rangi bila ya jicho; wala sauti bila ya sikio; au ladha bila ya mdomo.

Hakuna mwenye kutia shaka kwamba nuru ya Mwenyezi Mungu imezidi mawimbi ya kimwanga na mengineyo. Kwa hivyo yakikosekana mawimbi haya, ndio kumekosekana kuona.

58. Na tuliposema: Ingieni mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea na semeni: "Tusamehe." Tutawasamehe makosa yenu na tutawazidishia wale wafanyao mazuri.

 

59. Wakabadilisha wale walio dhulumu kauli isiyokuwa ile

89

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

waliyoambiwa. Na ndipo tukateremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kubwa mbinguni kwa sababu ya ufuska waliokuwa wakiufanya.

INGIENI MJI Aya 58 - 59 Maelezo:

Na tuliposema: Ingieni mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo.

Mwenye Majmaul-Bayan amesema: Wamekongamana wafasiri kwamba maana ya mji hapa ni Bayitul-Maqdis: na kwamba hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Ingieni ardhi takatifu".

Na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea.

Yaani ingieni hali ya kuinamisha vichwa kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Katika tafsir Bahrul-Muhit ya Abu Hayan Al-Andalusi anasema: Makusudio ya mlango ni mmojawapo wa milango ya Baitul Maqdis unaoitwa "Hitwa" (mwanachuoni huyu wa Kihispania alikufa mwaka 754 Hijriya)

Na semeni: Tusamehe

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaamrisha kuingia kwa unyenyekevu, vile vile aliwaamrisha kuambatanisha kunyenyekea na kutamka kauli ya kujidhalilisha, mfano kusema astaghfirullah, ili kauli na kitendo vilingane; kama unavyotamka:"Subhana rabbiyal adhwiimi" katika kurukuu na; Subhana rabbiyal aala" katika kusujudu.

Ilikuwa si lazima kutamka neno lenyewe Hitwa kwa njia ya kuabudu kama walivyosema wafasiri wengi, wala sio kuwa makusudio ya "Hitwa" ni amali inayokata dhambi, kama ilivyo katika tafsiri ya Al-Manar kwa kunukiliwa Muhammad Abduh aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu hakuwakalifisha kutamka, kwa sababu hakuna kitu rahisi kwa binadamu kama hicho."

90

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Itakumbukwa kwamba Mwenyezi Mungu amewakalifisha waja wake kutamka maneno katika swala, amali za Hijja, kuamrisha mema, kurudisha salam na kutoa ushahidi, bali kuzitoa herufi kwa makhraji yake katika baadhi ya sehemu.

Wakabadilisha wale waliodhulumu waliyoambiwa.

kauli isiyokuwa ile

Yaani wao waliamrishwa waseme yale yanayostahiki msamaha na thawabu, lakini walikhalifu wakasema yale yanayostahili adhabu na mateso.

Nilishangaa kuona baadhi ya wafasiri wakubwa miongoni mwao ni wanafalsafa wawili! Razi na Mulla Sadra, wameingilia masuala ya kuganda kwenye dua na dhikri, kwamba je, inapasa kuganda kwenye herufi au inajuzu kubadilisha tamko kwa tamko pamoja na kuchunga maana? Na wala wasiingilie pale walipofasiri 'wakabadilisha wale waliodhulumu.' kuwa inawaelezea wale ambao wameifanya dini biashara, na hali wao ndio waliokabidhiwa dini ya Mwenyezi Mungu, lakini wakafanya hiyana na wakazibadilisha Aya na mapokezi, kama walivyofanya Maquraish.

Tukateremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni.

Mwenyezi Mungu ameinyamazia aina na hakika ya adhabu yake wala hakutubainisha kuwa ni maradhi ya tauni, kama walivyosema baadhi, au ni theluji, kama walivyosema wengine. Vile vile amenyamazia idadi ya wale walioangamizwa na adhabu. Kuwa je ni elfu sabini, zaidi ya hapo au chini ya hapo? Pia hakueleza muda wa adhabu yenyewe kuwa ni saa au ni siku nzima? Kwa hivyo nasi tunanyamazia yale aliyonyamazia Mwenyezi Mungu, Wala hatutajikalifu, kama wengine, kwa kutegemea kauli dhaifu au Hadith zenye kuachwa.

60. Na Musa alipowaombea maji watu wake, tukasema: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikabubujika humo chem chem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Kuleni na kunyweni katika riziki ya Mwenyezi Mungu wala msiasi

91

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza katika ardhi mkifanya ufisadi.

2 Sura Al-Baqarah

 

ALIPOWAOMBEA MAJI

Aya 60

Maelezo:

Na alipowaombea maji watu wake.

Hakuna maelezo katika Aya hii, kwani makusudio yake yanafahamika upesi, Razi amesema: "Wamesema kwa pamoja wafasiri, kwamba tukio hilo lilikuwa katika jangwa la Sinai." Vyovyote ilivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu baada ya kuwafunika na kivuli na kuwalisha Manna na Salwa, vile vile aliwanywesha maji akawapitishia chemchem kumi na mbili kulingana na koo zao, kila ukoo ukawa na chemchem yake ili kusitokee mzozo kwenye maji.

UBEPARI NA UJAMAA

Waisrail walipata kivuli, chakula na kinywaji bila ya taklifu wala mashaka yoyote; hakukuwa na tajiri wala maskini; wala mwenye njaa na mwenye kushiba; wala hakukuwa na mwenye kumiliki nyenzo za uzalishaji, wala hakuna ugawaji. Vile vile hakuna kuwa kila mtu atapata kutokana na nguvu zake; au kutokana na kazi yake. Hakukuwa na chochote isipokuwa usawa katika maisha bila ya kufanya kazi yoyote au kuwa na mali.

19

Hilo ndilo taifa la mwanzo na la mwisho kupata kuonekana kwa maisha kama hayo, pamoja na kuwa na umoja katika lugha, maendeleo na historia. Tutathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu alilifanyia taifa hilo mambo maalum kwa ajili yao tu na si kwa watu wote.

Ikiwa siyo sababu ya kiuchumi au ya kikabila inayoleta chuki na ufisadi, basi kwanini kuleta uharibifu na kumwasi mtoaji nasaha aliye mwaminifu, Musa bin Imran (a.s.)? Na vipi wachoke na maisha ya usawa katika utajiri na kusema, hatuwezi kungojea bali tunataka baadhi yetu

Katika yaliyoelezwa na baadhi ya tafsir na ya kushangaza ni kwamba aliyekuwa mtoto katika wao alikuwa akikua na nguo; yaani kila anavyokua na nguo nayo hukua naye kwa urefu na upana, Hayo yanawezekana, lakini hakuna dalili juu yake.

92

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wawaombe wengine; na wakaukabili mfululizo wa neema kwa ukafiri na uasi?

Wajamaa wanadai kwamba ubepari ndio kitovu cha uovu, na kwamba ujamaa ndio chimbuko la ubora. Mabepari nao wakasema umuhimu ni kuwa jinsi moja katika akili na sifa za kiroho...

Hitler anasema: "Hakuna kitu chochote isipokuwa watu wa aina ya Aria (Arian)" Lakini maadui wengi wa Hitler walikuwa (kama yeye) Aria; kisha nadharia yake hiyo ndiyo iliyoyaondoa maisha yake, ikidhalilisha taifa la Ujerumani na ikaangamiza mamilioni ya watu wengine. Pia ndiyo iliyovunja miji na maendeleo kwa ujumla.

Ama dola za kijamaa zimepita kiasi kwa kubishana. Mzozo wa Moscow na Beijing ulikata matumaini yote ya maafikiano; na kabla yake, kulikuwako na mzozo wa Stalin na Tito.

Hakika binadamu ana nguvu za ajabu zisizoweza kuhisabika, lakini hali ya mazingira yanayomzunguka kwa nje ni nyingi. Mwenye kujaribu kuyadhibiti hayo atakuwa ametafuta muhali, kila moja ina athari yake na kazi yake, na binadamu yuko kati ya kupwa na kujaa. Kwa hiyo kuchukulia kuwa athari inakuwa katika maada peke yake au katika roho peke yake, si sawa.

Ndio, ni kweli kwamba 'ufakiri unakaribia kuwa ni ukafiri' lakini hata hivyo binadamu akipata anayoyahitajia katika uhai wake, hautatimia kwake utulivu na upole mpaka aamini na kutegemea kwenye dini iliyo sawa itakayomhifadhi na makosa na dhambi.

20

KITU KUTOKA KUSIKO NA KITU

Unaweza kuuliza vipi mawe yachimbuke chemchemi? Je, muhali unaweza kuwa? Je, kinaweza kupatikana kitu kutoka kusiko na kitu? Au mtu anaweze kuchimba maelfu ya mita ardhini na yasitoke maji ikiwa hayapo pale palipochimbwa. Sasa vipi yabubujiike maji kutoka katika jiwe lisilo na chemchemi wala athari yoyote ya maji?

Hakuna maelezo kutoka katika Sayansi kwa hili kabisa, isipokuwa kwa miujiza tu, ambayo kawaida yake ni kukhalifu ada; na isipokuwa kwa

Katika mwaka 1936 Edward (VIII) alijiuzulu kiti cha ufalme wa Uingereza, ambao haukuchwewa na jua wakati huo. Alijiuzulu kwa sababu ya mwanamke aitwaye Wallis, ambaye alikuwa amekwishaolewa na kuachwa mara mbili. Akaamua aishi naye kama mkimbizi na kuhangaika katika miji akitafuta kazi. Hiyo yote ni kutokana na kuchukulia maisha yote kuwa ni ya kimaada tu!

93

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kauli yake ambaye umetukuka uweza wake: "Kuwa ikawa"; kama ilivyo katika kupasuka bahari na kusimama maji yake kama majabali, kushuka Manna na Salwa kutoka mbinguni na kuujalia moto kuwa baridi na salama kwa Ibrahim (a.s.). Vile vile kuzaliwa Isa bila ya baba, kufufua wafu, na kuumba ndege kutokana na udongo na mengineyo mengi.

Kwa hivyo mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na uweza wake atatosheka na haya, na mwenye kukanusha na akafanya inadi, itakuwa hakuna haja ya maneno katika matawi baada ya kukanusha shina.

Mimi nina yakini kabisa kwamba wale ambao wanataka maelezo ya kielimu na ya kiundani kwa kila kitu, kuwa katika maisha yao wanapitiwa na matukio kadhaa ambayo hawawezi kupata maelezo yake, isipokuwa katika ghaibu na matakwa ya Mwenyezi Mungu, lakini wao hawajui.

Inahakikisha hilo kauli ya Mulla Sadra21 mwanafalsafa mkubwa, ambaye wakati wake hakukuwa na vipimo vyovyote, aliposema katika kufasiri Aya hii: "Hakika asili ya maada haina sura ya kukoma kuendelea, kwa hiyo inawezekana baadhi ya sehemu ya jiwe kugeuka maji."

Ushahidi hapo ni kauli yake "Inawezekana kugeuka baadhi ya sehemu ya jiwe kuwa maji."

Hii inatilia nguvu nadharia ya kukua na kubadilika (evolution), ambayo aliibainisha kabla ya Darwin kwa karne tatu ambapo Darwin mwenyewe alihusisha nadharia yake kwa mnyama mwenye viungo tu, ama Mulla yeye amekusanya vitu vyote hata vitu vikavu, kama ulivyoona katika uwezekano wa kugeuka jiwe kuwa maji. Ni ukubwa ulioje wa uvumbuuzi huu. Lau Mulla angelikuwa ni mzungu, basi Einstein asingelikuwa na umaarufu wowote, lakini Einstein ni mtu wa Magharibi tena Myahudi na Mulla Sadra ni wa mashariki tena Mwislamu!

Ametangulia mtukufu huyu kuielezea nadharia ya kukua kwa upana. Na nadharia hii ilimzidishia imani juu ya kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Ugunduzi wake huu umeleta dalili mpya, kuweko Mwenyezi Mungu ambayo hakuwahi kuielezea yeyote mpaka akaitwa kiongozi wa wataalam wa kuthibitisha Mungu. Na ameleta nguvu ya hoja juu ya ujinga wa Gladstone na mamilioni ya wafuasi wake katika madai yao kwamba kuweko Mwenyezi Mungu, muumba wa ulimwengu huu, kumebatilika kwa nadharia ya kukua. Bali ni kinyume na hivyo.

Mulla Sadra ni katika wanavyuoni wakubwa wa karne ya kumi na sita (A.D.) na Darwin alikuwa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

94

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

61. Na mliposema: Ewe Musa: Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu, basi tuombee Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi miongoni mwa mboga zake, na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake.

Akasema: Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora? Nendeni kwenye mji, huko mtapata mlivyoviomba. "Na ikapigwa juu yao (chapa ya) udhalili na umaskini; na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na hayo ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu na wakiwaua Manabii pasipo haki. Basi haya ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupituka mipaka.

NA MLIPOSEMA Aya61

Na mliposema: "Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu."

Yaani walisema wahenga wenu walipo-kuwa katika kuhangaika, walipochoka kuendelea kula Manna na Salwa, waka-pendelea maisha yao ya mjini. Hakuna kosa hapa katika matakwa yao, kwani kila mtu anapendelea namna mbali mbali ya chakula, hali hiyo ndiyo inayoleta matamanio. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amehalalisha riziki njema kwa waja wake. Kwa hivyo Aya haiko katika mfumo wa kutusi bali ni

95

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kustaajabu kukataa kwao maisha yasiyo na tabu na kutaka maisha ya dhiki na usumbufu.

Akasema: Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora?

Herufi 'ba' (kwa) inaingia kwenye kitu bora, sio duni, Tunasema: Usibadilishe shaba kwa dhahabu, hatusemi: Usibadilishe dhahabu kwa shaba," lakini watu hufanya kinyume, kwa vyovyote itakavyokuwa muhimu ni kujua makusudio.

Nendeni kwenye mji; huko mtapata mlivyoviomba.

Yaani Musa ndiye aliyewaambia hivyo. Kwa dhahiri makusudio ya neno Misri ni mji kwa sababu Mwenyezi Mungu hakubainisha mji maalum.Na tafsiri ya Quran siyo ya kinahw ambayo itasahihishwa na Sibawayh na Naftawayh.

Na ikapigwa juu yao (chapa ya) udhalili na umaskini

Walikuwa watukufu walio hum; riziki ikiwajia maridhawa, wakakataa isipokuwa kulima, uhunzi na biashara. Yote hayo yanaleta mashindano na vita ambavyo vinaleta kuhemewa na kukosekana amani.

Na wakiwaua Manabii pasipo haki.

Kwa dhahiri kuwaua Manabii kunakuwa bila ya haki. Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu (s.w.t.) aliwasuta na kuwambia kwamba kuua, kwao hakukuwa kwa kukosea, bali ni kwa makusudi na inadi tu. Kwa hiyo hakuna geni kwa vitendo vya mayahudi, kwa sababu hiyo ndiyo asili yao.

62. Hakika wale ambao wameamini ; > na Mayahudi na Manaswara na Wasabai; yeyote atakayeamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akafanya vitendo vizuri basi watapata malipo yao kwa mola wao, wala haitokuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.

96

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

WAUMINI NA MAYAHUDI

Aya62

Lugha

Makusudio ya neno Hadu ni Yahudi kwa kunasibishwa kwa Yahudha mtoto mkubwa wa Yaqub. Israil ni jina la Yaqub, kama tulivyotangulia kueleza. Naswara ni wenye kunasibishwa na mji unaitwa Naswira katika nchi ya Palestina. Imepokewa Hadith: "Hakika wameitwa Manaswara kwa sababu Isa na mama yake Maryam (a.s.) wanatoka katika kijiji kinachoitwa Naswira katika mji wa Sham, Mara nyingi Bwana Masih (a.s.) huitwa Naswiri".

Wasabai ni watu wanaomkubali Mwenyezi Mungu, siku ya mwisho na baadhi ya mitume, lakini wanaitakidi kuwa baadhi ya nyota zinaathiri heri na shari na uzima na ugonjwa, miongoni mwao wanaishi Iraq hivi sasa. Neno Swabia lina maana ya kuchomoza; Yaani kuchomoza nyota. Watu wa kwanza kuabudu nyota ni watu wa Namrud ambao walipelekewa Mtume Ibrahim (a.s.); wao ndio watu wa dini ya zamani katika Historia.

MAELEZO

Katika maana ya Aya hii kuna karibu kauli nane za baadhi ya wafasiri. Zilizo sahihi zaidi katika hizo ni mbili.

Kwanza: Makusudio ya Aya ni kwamba Mwenyezi Mungu anataka kubainisha kuwa Yeye hatilii umuhimu majina kabisa. Ni sawa iwe ni aina ya Mwislamu, Mumin, Yahudi, Naswara au Msabai. Kwa sababu matamko hayadhuru kitu wala hayanufaishi, ispokuwa umuhimu mbele ya Mwenyezi Mungui ni itikadi sahihi na amali njema. Ufahamisho wa Aya ni yale yaliyoelezwa katika hadithi kwamba Mwenyezi Mungu haangalii sura isipokuwa huangalia vitendo.

Hapana shaka kwamba maana hii yenyewe ni sahihi, lakini tamko halitoi maana hiyo waziwazi. Wengine wamezowea kujipendekeza kwenye dini nyingine kwa kutolea dalili Aya hii kwamba hakuna tofauti kati ya Waislamu na wengine mbele ya Mwenyezi Mungu, na hali wao wanajua kwa yakini kwamba wao wanakanusha Utume wa Muhammad (s.a.w.) bali wanamzulia uongo na wanamnasibishia mambo yanayoweza kuitingisha ardhi.

Maana ya pili, ni kwamba watu ambao hawakumuwahi Muhammad (s.a.w.) lakini waliongoka kwenye imani ya Mwenyezi Mungu na

97

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wakaacha mambo ya haram; kama uwongo, kunywa pombe na kuzini, miongoni mwao ni Qas bin Saida, Zayd bin Amr na Waraqa bin Nawfal na wengineo; hao wanaitwa wenye kushikamana na dini sahihi. Kwa hiyo muulizaji aliuliza hukumu ya hawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ikajibu Aya kwamba hakuna ubaya kwao.

Vile vile Wayahudi, Wasabai na Wanaswara ambao hawakumuwahi Muhammad (s.a.w.) kupata ufafanuzi; hakika wote hao hawana hofu kwao, madamu walikuwa na Imani ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na matendo mema. Nasi tunapondokea kwenye maana hii.

Unaweza kuuliza kwamba maana ya Aya hii inafanana kuwa ni maana ya hayo kwa hayo. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mwenye kuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho", imekuja baada ya kusema: "Hakika wale ambao wameamini." Kwa kujaalia maneno kuwa: "Hakika wale ambao wameamini mwenye kuamini katika wao" ambayo ni sawa na kusema: "Hakika Waislamu mwenye kusilimu katika wao" na " waliosimama mwenye kusimama katika wao" basi nini jawabu?

Jibu: Swali hilo linaweza kuja ikiwa tutaif-anya herufi man ni ya mubtada (kuanzia) kwa kusema: Yeyote atakayemwamini.

Ama tukiifanya ni Badal (badili) ya namna tatu yaani katika Wayahudi, Wasabai na Manaswara atakayemwamini, basi itakuwa hakuna haja ya swali; yaani itakuwa maana yake ni: Hakika wale ambao wamemwamini Mwenyezi Mungu wasiokuwa Wayahudi, Wasabai na Wanaswara haitakuwa hofu juu yao; vile vile atakayeamini katika Wayahudi, Wasabai na Wanaswara haitakuwa juu yao hofu. Hukumu ya wote ni moja.

63. Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu: Shikeni kwa nguvu haya tuliyowapa na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate 0 ?) ^ kumcha (Mungu).

64. Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake, mngelikuwa miongoni         mwa         wenye

98

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza kuhasirika.

65.   Na kwa yakini mmekwisha jua wale miongoni mwenu walioivunja Sabato (Jumamosi). Basi tukawaambia: Kueni manyani wadhalilifu.

66.   Kwa hivyo tukaufanya (umma huo) ni onyo kwa waliokuwa katika zama zao na waliokuja nyuma yao, na mawaidha kwa wamchao Mwenyezi Mungu.

2 Sura Al-Baqarah

TULIPOCHUKUA AHADI

Aya 63 - 66

Na tulipochukua ahadi yenu.

Yaani tulipochukua ahadi kutoka kwa wahenga wenu kufanya amali kwa mujibu wa Tawrat. Walipoivunja ahadi, Mwenyezi Mungu aliwainulia jabali juu yao, akasema fanyeni la sivyo nitawaangushia jabali hili. Wakakubali na wakatubia; likatulia jabali mahali pake, lakini baadaye walirudia kuasi.

Ikiwa Wayahudi walikuwa hivi wakati wa Musa (a.s.) pamoja na kushuhudia waliyoyashuhudia katika miujiza, wala hakuna nguvu ya hoja kuliko kuona, basi si ajabu kwa mayahudi wa Madina kumkanusha Mtume (s.a.w.) na kuvunja mkataba naye.

Angalia kifungu cha Muhammad (s.a.w.) na Mayahudi wa Madina katika tafsir ya Aya 47.

Na lau si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake.

Yaani lau si kuwahurumia Mwenyezi Mungu, angeliwapa adhabu katika dunia na akhera.

99

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mulla Sadra anasema: "Hakika Aya hii ni katika Aya zinazotoa matarajio zaidi na yenye dalili ya nguvu zaidi ya rehema ya Mwenyezi Mungu na vile asivyopatiliza maovu ya waja wake waasi. Kwa sababu, kauli yake: "Lau si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu", ni baada ya kukithiri uovu wao, ukiwa ni pamoja na kuabudu ndama, kuikufuru neema, kuwakana Mitume na kuwaua, kuvunja ahadi iliyotiliwa mkazo, na mengineyo; inafahamisha ukamilifu wa upole wake na msamaha wake.

Kisha akanakili Mulla Sadra, kutoka Kuffal, yale yanayoeleza kwa muhtasari, kwamba baada ya kuwaondolea adhabu ya jabali waliibadili Tawrat wakadhihirisha maasi wakamkhalifu Musa, wakamfanyia kila adha. Mwenyezi Mungu alikuwa akiwalipa hapa duniani ili waweze kuzingatia kiasi kwamba baadhi yao aliwapoteza katika ardhi, wengine akawaunguza kwa moto na wengine wakaadhibiwa kwa tauni. Yote hayo na yasiyokuwa hayo yameandikwa katika Tawrat wanayoikubali, ambayo hivi sasa anaweza kuipata kila anayetaka.

Kisha waliofuatia wakafanya makosa kama waliyoyafanya waliopita; wakamkanusha Bwana Masih wakadhamiria kumuua. Kwa hivyo si ajabu kukanusha yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad (s.a.w.).

Na kwa yakini mmekwishajua wale miongoni mwenu walioivunja sabato (Jumamosi).

Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuacha kufanya kazi siku ya Jumamosi (sabato) akawaharamishia kuvua samaki siku hiyo. Wakawa samaki wanakusanyika siku hiyo kwa usalama na utulivu, lakini kundi jengine la Mayahudi lilifanya hila ya kuwazuia samaki siku ya Jumamosi, mahali wasipoweza kutoka na kuwachukua siku ya Jumapili, wakisema: "Mwenyezi Mungu ametukataza kuvua samaki siku hiyo, lakini hakutukataza kuwazuia na kuna tofauti kati ya kuzuia na kuvua."

Waongo hawa wenye hila wananikumbusha wale wanaoigeuza dini, ambao wanacheza na matamko; wanazivuruga haki ili waingize uwongo katika mitego yao. Jambo la kushangaza ni kwamba baadhi ya masheikh wametunga vitabu maalum vya kuifanyia hila sheria; kama kwamba Mwenyezi Mungu ni mtoto mdogo anayedanganywa, asiyewajua wakweli na waongo. Kama Mwenyezi Mungu hakuwabadilisha hawa kuwa manyani hapa duniani, kama alivyowafanyia Mayahudi, basi atawafufua kesho kuwa majibwa, manyani na nguruwe. Ikiwa waongo hawakugeuzwa hivi sasa kwa dhahiri, basi wamegeuzwa kwa ndani; na hakuna hoja yenye nguvu zaidi inayofahamisha hilo kuliko vitendo vyao vinavyofahamisha kugeuzwa nafsi zao.

100

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

Basi tukawaambia kuweni manyani madhalili.

2 Sura Al-Baqarah

Wamehitalifiana wafasiri kwamba je, kugeuzwa manyani kulikuwa kwa uhakika kiasi ambacho sura zao na mili yao ilikuwa ya manyani ama kulikuwa ni kugeuzwa kwa kitabia tu; kama vile alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Amepiga muhuri Mwenyezi Mungu juu ya nyoyo zao."

(2:7)

Au...

"Kama mfano wa punda anayechukua mizigo?"

Ambapo Aya hizi ni za majazi.

(62:5)

Wafasiri wengi wamesema kuwa walikuwa manyani wa kikweli kabisa, kwa kuchukulia dhahiri ya Aya ambayo haina haja kuiletea tafsiri nyingine. Kwa sababu kugeuzwa sura na kuwa sura nyingine ni jambo linalowezekana kihakika. Ikija Aya au hadith kuhusu jambo ambalo lawez-ekana, basi tutaipitisha kwa dhahiri yake bila ya kuhitajia tafsiri nyingine (Taawil).

Wafasiri wachache, kama Mujahid na Sheikh Muhammad Abduh wamesema kwamba mabadiliko yalikuwa katika nafsi si katika mwili. Anasema Sheikh Muhammad Abduh katika tafsiri yake ya Al- Maraghi: "Hakika Mwenyezi Mungu hambadilishi kila asi kumtoa katika umbile la mtu, kwa sababu hiyo siyo desturi yake katika kuumba kwake, na desturi ya Mwenyezi Mungu ni moja, analolifanya kwa karne ya sasa ndilo alilolifanya kwa karne iliyopita."

Sisi tunakubaliana na wale wa kwanza waliosema kwamba mageuzo yalikuwa ya uhakika. Ama kauli ya Abduh ni sahihi kama msingi wa mambo yalivyo na kama kawaida ya vyote, lakini kuna mambo mengine yasiyofuata kawaida ambayo yanatokana na hekima ya Mwenyezi Mungu, kama miujiza na mengineyo katika karama zake Mwenyezi Mungu. Vitendo vya Mwenyezi Mungu pamoja na mayahudi wakati huo,

101

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

ni katika mambo yasiyofuata desturi, kama itakavyobainika katika kifungu kifuatacho.

MAYAHUDI HAWANA MFANO

Mwenye kuangalia vizuri Aya za Qur'an tukufu zilizowahusu Waisrail hasa wale waliokuwa katika zama za Musa, atatoka na natija iliyo wazi kama jua. Nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwafanyia mambo yasiyokuwa na mfano wala hayafanani na kitu chochote ambacho watu wamekizowea. Sio mbali kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na nikawatukuza kuliko viumbe wengine", ni ishara ya muamala huo mahsusi.

Mwenyezi Mungu aliwakomboa kutoka katika ukandamizaji wa Firaun na utaghuti wake kwa kuipasua bahari, sio kwa jihadi wala kujitolea muhanga. Aliwalisha Manna na Salwa na kuwapa maji kwa muujiza bila ya taabu au kazi yoyote. Akawainulia jabali ili waweze kutii na kusikia. Akamfufua mtu wao aliyeuliwa, ili abainike muuaji. Yote hayo na mengineyo yanaonyesha dalili kwamba matatizo ya Mayahudi wakati huo hayakutatuliwa kwa njia ya kawaida iliyozoeleka, bali hata hawakufikiria kufanya kazi ya kuyatatua; kila walipo kuwa wakipata tatizo, basi husema; "Ewe Musa tuombee Mola wako afanye hivi na awache hivi," na Musa alikuwa akiwaombea na kukubaliwa.

Kwa hivyo basi inatufahamikia kwamba kukifananisha kizazi cha Waisrail cha wakati huo na vizazi vingine sio mahali pake; na kwamba kauli ya Sheikh Muhammad Abduh (analolifanya kwa karne ya sasa ndiyo analolifanya kwa karne iliyopita) ni sahihi katika watu wote isipokuwa watu hao tu!

22

Vile vile inabainika kwamba Mwenyezi Mungu aliwainulia jabali kutaka kuwalazimisha waifuate Tawrat, na kwamba kauli ya Sayyid Tabatabai katika tafsiri Al-Mizan: "Hakika kuinuliwa jabali hakufahamishi kulazimisha kwa sababu hakuna kulazimisha katika dini," kauli hii iko mbali na mnasaba wa watu wa Musa ambapo Mwenyezi Mungu aliwafanyia mambo yaliyo mbali na kawaida na desturi.

Mimi sina namna yoyote ninayoweza kutegemea kujua hekima ya Mwenyezi Mungu katika hilo. Huenda ikawa siri katika hilo ni kuwa

Qur'an na Injil zimewalaumu Mayahudi kwamba wao ni maadui wa utu, na historia yao inashuhudia ukweli huu. Kwa ajili hiyo wanajaribu kufanya kila njia ionekane kwamba hakuna tofauti ya ukabila wala ya dini; ndio wakatunga vitabu kwa makusudio hayo na wakaeneza propaganda na wakaanzisha taasis, miongoni mwa hizo taasisi ni ile ya 'Free Mason' ya kimtaifa ambayo wameivika nguo ya 'ubinadamu.'

102

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alitaka kupiga mfano kwa Mayahudi hao kwamba maisha hayawi mazuri ila kwa kutaabika na kufanya kazi. Na ni kutokana na hali hiyo tu, ndipo mtu anaweza kugundua mambo na kujua siri, na kupanda katika daraja ya juu ya kimaendeleo.

Lau binadamu angeliishi kivivu kwa kutegemea chakula kutoka mbinguni asingeliweza kutofautiana na mnyama aliyefungwa na kulishwa; wala asingelikuwa na haja ya akili na utambuzi. Hakika uvivu ni kuganda na ni mauti, ama ukakamavu ndio uhai.

Vyovyote iwavyo, historia ya Mayahudi kwa ujumla inaambatana na historia ya Wayahudi waliokuwa wakati wa Musa, wao ndio waliotangulia halafu ndio wakafuatiwa na wajukuu zao.

Kutokana na mazungumzo haya tutadokeza kuhusu jumuiya ya wazayuni wanaoishi Marekani katika mtaa uitwao Brooklyn mjini New York. Jina la jumuia hiyo ni Mashahidi wa Yehova ambayo lengo lake la kwanza na la mwisho ni kuleta vurugu na fitina za kidini katika pembe za ulimwengu hasa Uarabuni.

Wanatoa matoleo mengi sana ya vitabu kwa lugha zote, tena kwa majalada ya rangi ambayo yanamiminika kwa wingi katika miji yetu: Pia wanatoa jarida kwa jina la Mnara wa mlinzi. Miongoni mwa vitabu walivyotoa ni kile kinachomshutumu Mtume Muhammad (s.a.w.) na Qur'an. Jina la kitabu hicho ni Hal-khadama ddinul-lnsaniyya (Je, dini inahudumia utu). Vingine ni Liyakunillah-Swadiqan (Mungu awe ni mkweli), Nidhamu dduhuril-ilahiy (Nidhamu ya zama za kiungu), Al-haqqu Yuharrirukum (Haki itawakomboa), Al-Maswaliha (Masilahi), na vingine chungu mzima, ambavyo vyote vimechapishwa Beirut.

Serikali ya Misri iliwagundua baadhi ya wanachama wa jumuia ya Mashahidi wa Yehova wakiwa katika mikutano ya siri. Ikawashika na kuwashtaki mnamo mwezi wa April mwaka 1967.

Miongoni mwa mafunzo ya jumuia hii ni kwamba kulikuwa na mzozo mkubwa kati ya Mwenyezi Mungu na shetani, ambao ulidumu kwa muda wa karne sitini; kisha Mwenyezi Mungu akajitoa akamwachia mamlaka shetani afanye vile anavyotaka. Shetani akamwachia Mwenyezi Mungu umma wa Kiisrail. Kwa ajili hii Mwenyezi Mungu akamwambia Shetani:"Chukua watu wote na uniachie umma huu". Hivyo ndivyo yalivyotimia maafikiano kati ya Mwenyezi Mungu na Shetani, lakini mambo yatabadilika mwisho. Kwa sababu umma wa Kiyahudi utatawala kuanzia mto Naili (Nile) mpaka Furati (Euphrates) na kwamba Mitume wa Kiisrail watafufuka na kuchukua madaraka ya juu katika dola ya

103

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kiisrail; hatimaye ulimwengu wote utakuwa chini ya dola hii, Shetani atash-indwa na Mwenyezi Mungu atashinda.

Kundi hili lina wafuasi na wawakilishi katika Beirut, Oman, Baghdad, Damascus, Cairo, Saudia na Morocco.

Lengo la kuyaeleza yote hayo ni kuwatahadharisha watu na nyoka huyu, na kuwahadharisha na vidole ambavyo vinawatekenya baadhi ya waandishi wa vitabu na magazeti kwa kufanya njama za kuleta vurugu na uharibifu, na kuleta ukabila na fitina za kidini.

67.  Na Musa alipowaambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha                mchinje ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga.

68.  Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni ng'ombe gani? Akasema: Hakika yeye anasema kwamba ng'ombe huyo si mpevu wala si mchanga, ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyoamrishwa.

69.  Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie rangi yake ni ipi? Akasema: Yeye anasema ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imeiva sana, huwapendeza wanaomtazama."

70.  Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni vipi hali yake;          hakika         ng'ombe

104

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wamefanana na hakika sisi kama Mwenyezi Mungu akipenda (tutakuwa) ni wenye kuongoka.

71.  Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo             si              ng'ombe anayefanyishwa kazi ya kulima ardhi wala kutilia maji mimea, mzima, hana           kipaku. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja,          na walikaribia wasifanye.

72.  Na mlipoiua nafsi, kisha A mkahitilafiana kwa hayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

73.  Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha          wafu;          na anawaonyesha ishara zake ili mpate kufahamu.

MWENYEZI MUNGU ANAWAAMRISHA MCHINJE NG'OMBE Aya 67 - 73

 

MUHTASARI WA KISA

Aya hizi tukufu haziwezi kufahamika maana yake bila ya kufahamu tukio lililoteremshiwa. Kwa ufupi tukio lenyewe ni hili:

105

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mzee mmoja tajiri katika Waisrail aliuliwa na binamu yake kwa tamaa ya kurithi mali yake; kisha akadai kuwa ameuliwa na watu wengine, na wakatakiwa walipe fidia. Ukazuka ubishi mkubwa na wakamwendea Musa (a.s.).

Kwa vile hakukuwa na ushahidi wowote wa kugundua mambo walimtaka Musa- kama kawaida yao - kumwomba Mwenyezi Mungu awabainishie muuaji.

Ndipo Mwenyezi Mungu akampa wahyi kuwa wachinje ng'ombe na sehemu ya huyo ng'ombe wampige yule aliyeuliwa atafufuka na ataeleza yule aliyemuua.

Baada ya udadisi mwingi walifanya vile walivyotakiwa kufanya na yule aliyeuliwa akafufuka na akamtaja aliyemuua.

MAANA:

Wakasema: Je unatufanyia mzaha?

Yaani tunakuuliza kuhusu kuuliwa mtu nawe unatuamrisha kuchinja ng'ombe hakika huu ni mzaha.

Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga.

Yaani mimi sifanyi mzaha, hata katika mambo yasiyokuwa ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, sembuse hayo ya kufikisha neno la Mungu ambaye umetukuka msemo Wake?

Ilikuwa inatosha tu wamchinje ng'ombe yoyote, kwa sababu waliamrishwa wachinje ng'ombe tu; lakini kwa udadisi wao.

Wakasema: Tuombee Mola wako atupambanulie ni ng'ombe gani?

Wakajibiwa kuwa ni ambaye yuko katikati si mkubwa wala si mdogo, basi fuateni amri wala msingoje, lakini wakarudia tena kuuliza

Wakasema: Tuombee Mola wako atupambanulie rangi yake ni ipi?

Akasema ni wa manjano, lakini tena wakazidi kudadisi na kuuliza swali mara ya tatu, kwa sababu ng'ombe walio katika rangi hii na umri huu ni wengi. Akawaambia kuwa ni yule asiyefanyishwa kazi na asiyekuwa na kasoro yoyote.

106

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Wakamtafuta mpaka wakampata, wakamchinja; kisha wakampiga maiti kwa kipande cha nyama akafufuka na siri ikafichuka baada ya kumtaja aliyemuua.

Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuyisha wafu na anawaonyesha ishara zake ili mpate kufahamu.

Yaani huku kumfufua huyu aliyeuliwa ni ushaidi wazi na dalili wazi ya kufufuliwa watu baada ya kufa, kwa sababu mwenye kuweza kufufua nafsi moja hawezi kushindwa na nyingine. Je, baada ya ushahidi huu wa kuona kwa macho mnaweza mkakanusha na kutia shaka na kuasi? Lakini pamoja na hayo na yasiyokuwa hayo nyoyo zenu zimesusuwaa, bali zimesusuwaa zaidi na zimekuwa ngumu zaidi kuliko jiwe, kama itakavyoeleza Aya inayofuatia.

Baada ya maelezo tuliyoyaeleza kuhusu Mayahudi haiwezekani tena kuuliza swali lolote kuwa, kwa nini Mwenyezi Mungu hakumfufua yule aliyeuliwa tangu mwanzo, na hali Mwenyezi Mungu alikuwa anaweza kufanya hivyo? Vipi anaweza kufufuka mtu kwa kupigwa na nyama ya ng'ombe? Kwa nini ilikuwa lazima ng'ombe huyo? Kisha kuna faida gani ya kumpiga na ng'ombe huyo aliyeuliwa?

Maswali yote haya hayana nafasi baada ya kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu aliwafanyia Mayahudi mambo maalum wao tu; na kwamba Yeye kwa upande huu ndio amewafadhilisha juu ya watu wote.

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe mengine yanayobubujika mito ndani yake, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake; na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na mnayoyafanya.

107

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

KUWA NGUMU NYOYO

Aya 74

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo.

Yaani ilikuwa ni wajibu kwa wazee wenu - enyi Mayahudi wa Madina -wazingatie na zilainike nyoyo zao baada ya kushuhudia waliyoyashuhudia katika miujiza na maajabu; ambayo miongoni mwake ni kufufua aliyeuliwa, lakini, kwa ukhabithi wao, wakafanya kinyume na vile inavyotakiwa; wakafanya ufisadi na nyoyo zao zikasusuwaa kama kwamba zimetokana na mawe, bali baadhi yake ni ngumu zaidi kuliko mawe, kwani kuna mawe, mengine yanayobubujika mito ndani yake, na kuna mengine yanayopasuka yakatoa maji.

Unaweza kuuliza: Mito ni maji, sasa mbona yametajwa maji na mito? Inawezekana kutofautisha jengo na nyumba?

Jibu: Hakika Aya tukufu imegawanya maji kwenye mafungu mawili mengi ambayo ni mto, na machache ambayo ni chemchem. Ibara ya mgawanyiko imekuja kwa tamko la maji, kwa hivyo kumetajwa kububujika maji kwa maana ya wingi na kupasuka kwa maana ya uchache.

Vyovyote iwavyo, lengo la Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwa amefadhilisha aina za majabali na mawe kuliko nyoyo za Mayahudi, ni kwa sababu jiwe linaweza kupasuka likatoa maji, na kwamba jiwe mara nyingine huwa linatikisika likaondoka pale lilipokuwa. Lakini nyoyo za Mayahudi hazina hata chembe ya kheri wala hazitikiswi na uzuri wowote na hazielekei kwenye uongofu.

Unaweza kuuliza kuwa mawe hayana uhai wala utambuzi, kwa hiyo hayawezi kumwogopa Mwenyezi Mungu, sasa kuna wajihi gani katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu."

Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi, yaliyo karibu zaidi ni mawili: Kwanza, hayo ni makisio kwamba lau kama mawe yangelikuwa na fahamu na akili kama Mayahudi, yangelianguka kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mifano hii ni mingi sana katika maneno ya waarabu.

Jibu jingine, ni kwamba ni kawaida ya mawe kumnyenyekea Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyeumba maumbile yote.

108

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza Mwenyezi Mungu anasema:

2 Sura Al-Baqarah

"Zinamsabihi (zinamtakasa) mbingu zote saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, na hakuna chochote ila kinamsabihi kwa sifa Zake njema."

(17:44)

Utakuja ufafuanuzi tutakapofika Aya hiyo inshallah.

TOFAUTI YA HULKA

Anaweza kuuliza muulizaji: Je ndani ya binadamu kuna nguvu inayompa msukumo wa harakati; au yanayompa harakati ni matukio ya nje, kiasi ambacho ndani ni tawi lakini nje ndio shina? Au kila moja ni shina hiyo yenyewe peke yake, kwamba mtu mara nyingine hupata msukumo kutoka ndani na mara nyingine nje au mara nyingine ndani na nje? Kama tutafaradhia kuwa ndani ya binadamu kuna msukumo wa aina ya peke yake usioshirikiana na kitu kingine, Je msukumo huo ni wa aina moja kwa watu wote au kila mtu ana wa aina yake?

Jibu: Hakika mtu anakuwa mtu kwa silika yake na nguvu yake ya kiroho. Lau tunavitoa vitu hivyo au tanavizuia utendaji kazi wake, basi binadamu atakuwa ni kama ganda tupu au unyoya katika mavumo ya upepo.

Ndio! Ni kweli kwamba nguvu za kindani zinafanya kazi pamoja na matukio ya nje na kuathirika nazo, lakini kufanya kazi ni kitu kingine na kuathirika ni kitu kingine. Kwa mfano, silika ya kuchunguza inakuwa pamoja na mtu na ndio maana mtoto anakuwa mdadisi kwa umbile lake; bali silika hiyo ni katika mambo yanayomuhusu mtu. Kisha silika hii inakua na kukoma kwa kuona matukio ya nje vilevile kwa utafiti na uvumbuzi; na kwa kukua kwake binadamu anaweza kuathirika vitu vya nje kulingana na haja yake na matakwa yake. Kwa hivyo harakati za binadamu zinachimbuka kutoka ndani na nje, yaani kutoka katika nafsi yake na kutoka katika matukio.

Hapa kuna kifungu cha tatu ambacho nimekigundua kutokana na majaribio yangu maalum; Kifungu hicho nimekipa jina "Tawfik katika heri na kufaulu". Kifungu hiki hakitokani na nafsi wala matukio, bali kinatokana na nguvu iliyojificha ambayo iko katika ulimwengu uliojificha (usiojulikana), inawaandalia baadhi ya watu njia ya heri na inaingia katika kuwaelekeza watu kwenye lile linalomridhshia Mwenyezi Mungu bila ya mtu kutambua.

Ni kawaida kwamba hatanikubalia juu ya hili isipokuwa yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na hekima yake na kumpa cheo

109

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kinachomstahiki. Ninakiri kwamba mimi sina ufahamu wa ujumla wa kifungu hiki, isipokuwa nimekifahamu kutokana na majaribio yangu; kama nilivyotangulia kueleza.

23

Ama jawabu la kuwa je, watu wanakuwa na namna moja katika silika na sifa za kinafsi, linataka ufafanuzi.

Katika sifa za kinafsi kuna zile ambazo watu wanashir-ikiana; kama vile utambuzi wa kupambanua kati ya haki na batili, heri na shari, na kati ya baya na zuri.

Lau si ushirikiano huu isingeliwezekana kwa vyovyote vile kuthibitisha uovu na wema na isingelifaa kwetu kumlaumu au kumsifu mtu kwa kufanya jambo fulani. Vile vile kuna ushirikiano katika kujipenda na upendo wa mzazi na mwana, na mengineyo ambayo wanayo watu wote, ijapokuwa kuna tofauti ya wingi na uchache.

Kuna sifa nyingine za kinafsi, ambazo watu wanatofuatiana kama vile; ushujaa, woga, ukarimu, ubahili, ugumu wa moyo, ulaini wa moyo, udhaifu wa matakwa na nguvu yake na kupondokea kwenye heri au shari. Watu katika sifa hizi wanatofuatiana, kila mtu sio karimu au bahili, wala mwoga au mshari.

Unaweza kuuliza: Hakika kauli yako si inakhalifu kawaida maarufu iliyozoeleka, kuwa hakuna mtu yoyote isipokuwa ana pande mbili, mzuri na usiokuwa mzuri; na wewe umetilia mkazo upande mmoja tu, na ukaufinyia jicho upande mwingine?.

Jibu: Hakika uvivio wa heri ambao mara nyengine tunauona kwa baadhi ya watu wa shari, unakuwa umeingia kighafla tu, bila ya kukusudiwa; na kwamba suala la kuwa kila mtu ana pande mbili linawezekana kwa wasiokuwa Mayahudi. Kwa sababu, Mayahudi hawana lolote wao isipokuwa uovu tu; hawana wema kabisa. Ushahidi wa hayo ni Tawrat yao, Qur'an tukufu na historia sahihi. Vile vile vitendo vyao katika Palestina na kwingineko, mambo ambayo ni dalili wazi kwamba dini, maadili na mfungamano wote wa kiutu, kwao ni biashara na manufaa tu.

Jambo la kushangaza lilotokea kwa sadfa.Baada ya kuandika maneno haya nikasoma nakala fulani, kuwa kiongozi mmoja wa kijeshi wa Kiingereza maarufu sana anayeitwa Montgomery alijieleza kwa kusema: Hakika yeye ni askari mdogo chini ya uongozi wa nguvu kuu; na kwamba yeye hakushinda katika vita isipokuwa kwa matakwa ya kudra hiyo; na kwamba bila ya kuamini nguvu hii kubwa yenye akili, haiwezekani kushinda katika vita vya dunia vya pili. Yeye anaamini kwamba kuna nguvu iliyofichika ambayo iliwaandalia njia ya kumshinda Romel, ambaye alikuwa akiitwa mbweha wa jangwani, naye alikuwa amirijeshi mkubwa wakati huo.

110

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

Maudhui haya tutayarudia kila itakapolazimika.

75. Je mna matumaini ya kwamba

2 Sura Al-Baqarah

wataamini na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu kisha

wanayabadili baada ya kuwa (*-*J wameyafahamu na hali wanajua?

HAKUNA MATUMAINI

Aya75

MAELEZO

Kila mwenye ujumbe fulani huwa anapupia watu wauamini ujumbe huo. Kwa hivyo anaueneza kwa matumaini ya kupata wafuasi wengi, na anahimili taabu na mashaka katika hilo, kama alivyofanya Mtume (s.a.w.) na sahaba zake, waliueneza mwito wa Uislamu katika pembe zote kwa kutaraji kupata wafuasi.

Kulikuwa na mfungamano wa kijirani, kibiashara na hata kunyonyeshana watoto kati ya Ansar na Mayahudi. Hivyo wakawalingania kwenye Uislamu kwa amri ya Mtume. Wakawatolea dalili kwa hoja zinazoingia akilini na kwa mantiki mazuri, wakatumai kwamba nyoyo zao zitashtuka, hasa kwa kuzingatia kwamba wao ni watu wa Kitabu na kwamba sifa za Muhammad (s.a.w.) zimetajwa kwa uwazi katika Tawrat yao.

Walipoendelea Wayahudi kukaidi mwito wa Uislamu na kuendelea kukufuru na kuipinga haki, ndipo Mwenyezi Mungu alipomwambia Mtume wake kwa kusema: Je mnatumaini nyinyi Waislamu ya kwamba watawaamini hao Mayahudi, na hali wazee wao hawa Mayahudi walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa Nabii Musa (a.s.) pamoja na miujiza, lakini wakiyabadilisha na kuyageuza vile matamanio yao yanavyotaka pamoja na kujua kuwa hayo maneno ni ya haki?

Kwa hivyo, hali ya Wayahudi wa Madina ni kama hali ya wazee wao waliopita, ambao walibadilisha halali ikawa haramu na haramu kuwa

111

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

halali kwa kufuata matamanio yao na wakabadilisha sifa za Muhammad (s.a.w.) zilizopokewa katika Tawrat, ili isiweko hoja juu yao.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Katika Aya hii kuna dalili juu ya ukubwa wa dhambi ya kuibadilisha sheria. Na dhambi hiyo inapatikana katika kuleta Bid'a katika fatwa au hukumu na mambo yote ya kidini."

Kuongezea juu ya maneno hayo ya mwenye Majmau ni kuwa Aya hii ni dalili juu ya kuwa mwenye kufuata upotevu kwamba sio kuwa anajifanyia uovu yeye mwenyewe tu, bali athari yake inaenea kwa vizazi, kama ilivyoelezwa katika Hadith.

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao kwa              wao              husema:

"Mnawaambia                        yale

aliyowahukumia           Mwenyezi

Mungu ili wapate kuhojiana nanyi mbele ya Mola wenu? Je, hamna akili?

77. Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu                             anayajua

wanayoyayafanya siri na wanayoyadhihirisha?

WANAPOKUTANA NA WALE WALIOAMINI

Aya 76 - 77

MAELEZO

Baadhi ya Mayahudi walikuwa wakifanya unafiki na uwongo kwa Waislamu na wakisema: "Sisi tunaamini yale mnayoyaamini nyinyi na tunashuhudia kuwa Muhammad ni mkweli katika maneno yake, kwani tumekuta katika Tawrat sifa zake. Lakini wanafiki hao wanapochanganyikana na viongozi wao, basi viongozi wanawalaumu kwa kusema: "Vipi mnawahadithia wafuasi wa Muhammad yale aliyowahukumia Mwenyezi Mungu? Hivi hamfahamu kwamba huko ni

112

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kukubali nyinyi wenyewe kwamba mko katika batili na wao wako katika haki?"

Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya siri na wanayoyadhihirisha?

Yaani kwa vyovyote watakavyojaribu wanafiki, kuficha unafiki wao na viongozi wapotevu wanavyowaelekeza wafuasi wao, lakini kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakifichiki chochote. Basi nyinyi Mayahudi mnaficha njama zenu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamfahamisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) na anavifagia vitimbi vyenu.

78.   Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma; hawajui kitabu isipokuwa matamanio tu nao hawana isipokuwa kudhani tu!

79.   Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao. Kisha wakasema hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.

WAKO MIONGONI MWAO WASIOJUA KUSOMA

Aya 78 - 79

MAELEZO

Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma.

Yaani katika Mayahudi kuna wale waliokuwa hawakusoma; hawajui chochote katika dini ya Mwenyezi Mungu na kwamba mambo yao zaidi ni ya kudhania dhania tu, bila ya kutegemea elimu.

113

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kimsingi ni kwamba ingawa maelezo haya yamekuja kwa sababu ya Wayahudi, lakini shutumu inamwendea kila mjinga.

TAFSIRI INA MIS ING I NA KANUNI

Katika Aya hii kuna dalili wazi kwamba haifai kufasiri Qur'an na Hadith kwa kudhania na kukisia, bali hapana budi lazima mfasiri awe na elimu ya kanuni za tafsiri na misingi yake, na kuchunga kanuni hizi katika kubainisha makusudio ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kujihadhari na kuwazulia.

Sharti la kwanza la kufaa kufasiri ni kujua kusoma na kuandika; kisha hujua elimu za Kiarabu kwa aina zake zote, ambazo ni kujua msamiati, Sarfa, Nahw, Bayan, Fiqh na misingi yake. Vile vile kujua elimu ya Tawhid na kuongezea elimu nyingine ambazo zitamsaidia katika kufasiri baadhi ya Aya. Yote haya mfasiri anaweza kuyajua kwa kuwaendea wenye kuhusika nayo.

Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao.

Hapa Mwenyezi Mungu anamkemea kila anayemnasibishia yale asiyokuwa nayo kwa ajili ya kuchukua thamani kwa shetani. Si lazima thamani iwe ni mali (pesa) tu; inaweza kuwa ni kupata jaha au chochote katika anasa za kidunia.

24

Mwenyezi Mungu amekariri makemeo mara tatu katika Aya moja kwa kutilia mkazo kwamba kumzulia yeye Mwenyezi Mungu na Mtume ni katika maasi makubwa na yenye adhabu kali; kama alivyosema mahali pengine.

"Ole wenu msimzulie uwongo Mwenyezi Mungu asije akawafutilia mbali kwa adhabu. Na ameruka utupu anayezua uwongo."

(20:61) MWANACHUONI HAWEZI KUHUKUMU KWA MATUKIO

Tunadokeza kwa mnasaba huu kwamba mwanachuoni, kwa namna yoyote atakavyokuwa na elimu, ni juu yake kutomnasibishia chochote

Wamethibitisha wenye kuhusika na historia ya lugha na ada zake kwamba Tawrat ya sasa, ambayo Wayahudi wanaitakidi kuwa iliteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Musa, imetungwa. Watafiti wametoa hakika hii kutokana na muundo wa lugha ulivyo na ustawi wa kijamii na wa kisiasa ambao uko kinyume na Tawrat. Tutarudia kueleza maudhui haya kwa upana zaidi Inshallah.

114

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwamba kitu hicho kinatoka katika Lawh Mahfudh. Akitoa fatwa kwa uhalali au uharamu; au kuhukumia kitu kuwa ni haki; au kufasiri Aya au Hadith, basi ni juu yake kuifanya hukumu yake hiyo, fatwa yake au tafsiri yake kuwa ni rai yake tu. Inaweza kuwa ni makosa au sawa.

Hapo ndio atakuwa anakubaliwa msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu kama akijitahidi kadiri ya uwezo wake. Lakini kama hakujitahidi sana au amejitahidi sana, lakini akasema kuwa kauli yake hiyo ni kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi atakuwa ni sawa na wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uwongo, ajapokuwa ni mwanachuoni wa wanachuoni. Kwa sababu mwanachuoni hatoi fatwa ya kweli wala hukumu ya kweli, bali anaitikadi tu kuwa ni haki. Huu ndio msingi wa kwamba yeye sio maasum.

80.  Na walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu. Sema: Je, mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu Kwa hivyo hatakhalifu ahadi yake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msıyoyajua?

81.  Ndiyo, wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni; humo watadumu.

82. Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa peponi, watadumu humo.

115

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

WALISEMA HAUTATUGUSA MOTO WA JAHANNAM

Aya 80 - 82

Na walisema: 'Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu'

Mayahudi wanadai kwamba wao ni watoto wa Mungu na taifa lake teule na kwamba watu wote ni watoto wa shetani, isipokuwa wao tu, na ni mataifa yaliyotupiliwa mbali. Kwa hivyo ati Mwenyezi Mungu hatawaweka milele motoni, isipokuwa atawaadhibu kwa adhabu hafifu tena kwa muda mfupi, kisha atawaridhia. Yaani kwamba Mwenyezi Mungu anawaendekeza na kuuendekeza ukoloni wa kizayuni ambao unaikalia ardhi ya Palestina.

Sema: "Je, mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu."

Yaani waambie ewe Muhammad, kwamba madai yao haya ni porojo tu, na kama si hivyo, basi ni ahadi gani mliyowekeana na Mwenyezi Mungu? Madai yao haya, hayafahamishi chochote zaidi ya kudharau kwao madhambi na kufanya uovu.

Mtume mtukufu (s.a.w.) anasema: "Hakika mumini anaona dhambi yake ni kama jiwe anaogopa lisimwangukie na kwamba kafiri anaona dhambi yake ni kama nzi tu aliyepitia kwenye pua yake...". Anasema Amirul Muminin (a.s.):" Dhambi kubwa zaidi ni ile iliyodharauliwa na mwenye kuifanya."

Kauli yake Mtume mtukufu (s.a.w.): "Kama kwamba dhambi ni nzi anayepita juu ya pua ya mwenye dhambi." Inafanana kabisa na ya Mayahudi ambao wanadai kwamba wao ni watoto wa Mwenyezi Mungu wenye kutendekezwa. Huenda haya yakamnufaisha na kumzindua yeyote ambaye anapuuza dhambi kwa kutegemea utukufu wa nasabu.

Mwenye kujitegemea yeye mwenyewe tu wala asihisi makosa ya nafsi yake, na asikubali nasaha za mwingine, basi ni muhali kuweza kuongoka kwenye heri. Hakika mwenye akili hajiangalii mwenyewe tu kwa kujihadaa na ndoto zake, bali daima anakuwa na msimamo wa kujilaumu makosa yake na kupambanua yale aliyonayo na yale anayotakiwa awe nayo.

Vile vile huitoa nafsi yake na fikra za kitoto na mawazo ya kishetani. Kwa hali hii pekee ndio atakuwa anafaa kuitwa mtu kwa maana sahihi. Kuna hadith tukufu inayosema: "Mwenye kujiona kwamba yeye ni mwovu, basi ni mwema."

116

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ndiyo, wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni na humo watadumu.

Ubaya ni shirk na madhambi mengineyo, lakini makusudio yake hapa yanahukumu shirk tu! Kwa kulinganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu hao ndio watu wa motoni humo watadumu.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: "Makusudio ya ubaya kuwa ni shirk ndiyo yanayoafiki, kwa sababu dhambi nyingine yoyote haiwajibishi kudumu motoni."

Na wale walioamini na kutenda mema hao ndio watu wa peponi watadumu humo.

Aya hii tukufu inafahamisha kuwa kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu kesho kutatokana na imani sahihi ikiambatana na matendo mema. Hadith tukufu inasema: "Abu Sufyani Athaqafiy, alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niambie neno katika Uislamu ambalo sitamuuliza yeyote baada yako." Akasema Mtume: "Sema: Nimemwamini Mwenyezi Mungu, kisha ufuate unyoofu (msimamo)."

Katika hadith yake hii Mtume (s.a.w.) anaelezea Aya inayosema:

"Wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakawa na unyoofu hao huwateremkia malaika (wakawambia): Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa."

(41:30).

Makusudio ya kuwa na unyoofu katika Aya na Hadith, ni kuwa katika msimamo wa kufanya amali kwa mujibu wa Qur'an na hadith za Mtume (s.a.w.).

MWISLAMU NA MUUMINI

Mwislamu kwa kuangalia muamala wake na kuthibiti Uislamu wake, anagawanyika kwenye mafungu mawili:

Kwanza, kumkubali Mwenyezi Mungu kuwa ni mmoja na kukubali Utume wa Muhammad bila ya kuangalia itikadi yake na amali (matendo) yake.

117

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Lakini ni sharti asikanushe zile dharura za dini, kama ulazima wa swala na uharamu wa zinaa na pombe. Huyu ndiye anayejulikana kwa Waislamu kuwa yeye ni Mwislamu atafanya na kufanyiwa mambo ya Kiislamu; kama kurithi, kuoa, na kuzikwa kiislamu, ikiwa ni pamoja na kumwosha, kumtia sandani, kumswalia na kumzika katika makaburi ya Waislalmu, anafanyiwa hayo kwa vile amepiga shahada.

Pili, ni kuamini na kushikamana na Uislamu kwa misingi na matawi; hakanushi hukumu yoyote katika hukumu za Kiislamu, wala hafanyi uasi wa hukumu katika hukumu za sheria. Huyu ndiye Mwislamu wa kweli

(muumin) mbele ya Mwenyezi Mungu na watu, bali ni Mwislamu mwadilifu ambaye zimethibiti kwake athari zote za uadilifu wa Kiislamu duniani na akhera.

Athari za dunia ni kukubaliwa ushahidi wake, kufaa kuswalisha, kuchukua hukumu zake na fatwa zake akiwa ni mujtahidi. Ama athari za kiakhera ni kule kuwa juu hadhi yake na thawabu.

Mumin ni yule mwenye kukiri kwa ulimi na kusadikisha kwa moyo wake shahada mbili, wala haitoshi kukiri kwa ulimi tu au kusaidikisha kwa moyo tu, bali hapana budi yote mawili yaende sambamba. Kwa hivyo kila mumin ni Mwislamu, lakini si kila Mwislamu ni mumin.

Hapa inatubainikia kwamba amali njema haiitwi imani, kwa dalili kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ameleta kiunganishi baina ya imani na amali njema kwa maana ya kuwa ni vitu viwili tofauti. Hata hivyo amali njema inaingia katika ufahamu wa uadilifu kama tulivyoonyesha. Utakuja ufafanuzi wake mahali pake.

Mafaqihi wa kishia wanahusisha tamko la mumin kwa yule anayeamini Maimamu kumi na wawili, wakisema zaka inapewa mumin, na mwenye kuswalisha awe mumin, basi wanakusudia yule mwenye kuamini maimamu kumi na wawili tu. Istilahi hii wanahusika nayo mafaqih tu. Lakini hata huyo fakihi wa Kishia kama akizugumzia mumin katika mswala yasiyokuwa ya kifikihi, basi huwa anakusudia kila mwenye kukiri shahada mbili na kuzisadikisha kwa moyo; hata kama siye mwenye kuamini Maimamu kumi na wawili.

Kwa vyovyote ilivyo Uislamu na imani kwa maana tuliyoyaelezea, hautamuokoa mtu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kesho, isipokuwa uwe pamoja na unyoofu ambao ni kufanya amali kulingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake (s.a.w.).

118

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

MWENYE MADHAMBI MAKUBWA

2 Sura Al-Baqarah

Mafakihi wameyagawanya madhambi katika mafungu mawili: Makubwa; kama kunywa pombe. Na madogo kama kukaa mwenye meza ya pombe bila kunywa. Utakuja ufafanuzi wa madhambi makubwa na madogo Inshallah, katika Aya isemayo: "Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu; isipokuwa makosa hafifu..." 25

Wamehitalifiana Waislamu katika yule mwenye kukiri shahada mbili na akafanya madhambi makubwa, Je, yeye ni kafiri atakayebakia milele motoni au yeye ni mwislamu fasiki ambaye ataadhibiwa kiasi anachostahili, kisha atiwe peponi?

Khawarij wamesema kuwa atabakia milele motoni. Shia, Ash'ari, Masahaba wengi na Tabiin, wamesema atatolewa motoni. Mu'tazila wamezusha fikra ya tatu ya kuthibitisha mawili, yaani hatakuwa kafiri wala Mumin.

Allama Hilli ametoa dalili katika sherehe ya Tajrid juu ya ushahidi wa kauli ya kuwa mwenye madhambi makubwa ni fasiki hatokaa milele motoni, kuwa: "Lau atabakishwa milele motoni, ingelazimika mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu muda wa umri wake wote; kisha akamuasi mwisho wa umri wake mara moja tu, pamoja na kubakia na imani yake, aingie motoni milele, awe sawa na yule aliyemshirikisha Mwenyezi Mungu katika umri wake wote. Na hilo ni muhali na haliingii akilini."

Hapana mwenye shaka kwamba ovu moja haliwezi kuondoa mema yote, bali ni kinyume; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Kwa ajili hiyo basi, inapasa kulichukulia neno ubaya katika Aya (Na wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni, watadumu humo), kuwa na maana ya shirk. Kama ambavyo Aya inayofuatia hiyo (Na wale walioamini na kutenda mema hao ndio watu wa peponi, watakaa humo milele) inafahamisha kwamba mwenye kufanya madhambi makubwa ataingia peponi, wala hatakaa milele motoni. Kwa sababu Aya ile inamhusu pia mwenye kuamini na akafanya amali njema kisha akafanya madhambi makubwa na wala asitubie.

MAYAHUDI TENA

Madai ya Mayahudi kwamba wao ni watoto wa Mungu na taifa teule, ni kwamba dini na maadili yake, katika itikadi yao, ni kazi ya kibiashara na manufaa ya kiutu. Vinginevyo itakuwa ni bure tu.

119

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Unaweza kusema, hayo hayahusiani na Mayahudi tu, bali wako watu wa namna hiyo. Jibu, ndio, lakini tofauti iliyopo ni kwamba Mayahudi wana hasadi kwa watu wote isipokuwa wao.

83. Na tulipochukua ahadi na wana wa Israil: Hamtamwabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na maskini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni swala na toeni zaka.          Kisha mkageuka

isipokuwa wachache tu katika nyinyi na nyinyi mnakengeuka.

AHADI NA WANA WA ISRAIL

Aya 83

AYA HII IMEKUSANYA MAMBO YAFUATAYO

I. Kuwatendea wema wazazi wawili

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameikutanisha shukrani ya wazazi wawili na yake na akawajibisha kuwatendea wema na ku-wafanyia hisani; sawa na alivyowajibisha kuabudiwa kwake. Kuanzia hapa ndio mafakihi wamesema kwa kauli moja kwamba kuwaasi wazazi wawili ni katika madhambi makubwa, na kwamba mwenye kuwaasi ni fasiki hauwezi kukubaliwa ushahidi wake. Hadith tukufu inasema: "Hakika mwenye kuwaudhi wazazi wawili hatapata harufu ya pepo".

Makusudio ya kuwatendea wema wazazi wawili ni kuwatii na kuwachukulia upole.

Kuna kisa cha mwanamke mmoja aliyembeba baba yake mgongoni kutoka Yemen mpaka Makka. Akatufu naye katika Al-Ka'aba. Mtu mmoja akamwambia "Mwenyezi Mungu akulipe heri, umetekeleza haki yake." Akasema: "Hapana sijatekeleza; yeye alikuwa akinibeba huku akinitakia uhai (niishi) na mimi hivi sasa ninambeba huku nikimtakia mauti (afe)."

120

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza II.

 

Jamaa, Mayatima na Maskini

2 Sura Al-Baqarah

Aya imewajibisha muungano wa udugu kwa kuungana kwake na wazazi wawili. Pia imewajibisha kumchunga yatima na mali yake kwa yule ambaye atakuwa ni walii (msimamizi) au wasii wa yatima huyo. Vile vile Aya imemwajibishia fakiri fungu katika mali za matajiri.

III. Kuchukulia usahihi

Kama mtu akifanya amali yoyote au akisema kauli yoyote inawezekana iwe sahihi au isiwe sahihi. Sasa je, uchukuliwe usahihi juu ya kitu chochote au la; au ni lazima iweko dalili mkataa? Mfano kumwona mtu pamoja na mwanamke, hujui kama ni mkewe au ni mtu kando. Au usikie maneno nawe hujui kuwa msemaji alikusudia wewe au la.

Mafakihi wameafikiana kuchukulia usahihi katika hilo (afanyalo si kosa) na mfano wake. Wametolea dalili hilo kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na semeni na watu kwa uzuri."

Amirul Muminin Ali (a.s.) naye amesema: "Liweke jambo la ndugu yako juu ya uzuri wake."

Vile vile kwa kauli ya Imam Jafar Sadiq (a.s.): "Yakadhibishe masikio yako na macho yako kwa ndugu yako. Wakitoa ushahidi kwako watu hamsini kwamba yeye amesema kadhaa, na yeye akuambie sikusema, basi mwamini yeye na uwachukulie kuwa ni waongo wale watu hamsini."

Huu ndio msingi wa kiutu hasa. Kwa sababu unajenga heshima ya mtu na unatilia mkazo mfungamano wa kusaidiana na kuchukuliana upole kati ya watu, na unawaepusha na yale yanayoleta chuki. Kwa hivyo basi, inabainika kuwa Uislamu haujishughulishi na itikadi na ibada pekee, bali unajishughulisha na utu na heri zake na unaonyeshea njia itakayopelekea uhai wenye matunda ya kufaulu.

Lakini wale ambao wameiuza dini yao kwa shetani wameupoteza msingi huu wa kiutu, wakaenda kombo na malengo yake; na wakaboresha kazi ya uharamia na kuchukua riba.

Ilivyo hasa kama tulivyoonyesha ni kwamba msingi wa kuchukulia usahihi haufungamani na kazi ya unyang'anyi, ujambazi, kupoteza na mengineyo yanayofanana na hayo, ambayo tunayajua kwa yakini kuwa ni katika mambo ya haramu na yenye kuangamiza. Isipokuwa msingi huo tuliotaja unakuwa katika mambo ambayo yana uwezekano wa kuwa kweli au uwongo, usawa au upotevu.

121

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

84. Na tulipochukuwa ahadi yenu kuwa Hamtamwaga damu zenu, wala hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali na hali mnashuhudia.

85.  Kisha nyinyi hao hao, mnajiua wenyewe na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao, mkisaidiana dhidi yao kwa (njia ya) dhambi na uadui. Na wakiwajia                        mateka mnawakomboa na hali kumeharamishwa             kwenu kuwatoa. Je mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia, na siku ya Kiyama watarudishwa kwenye adhabu kali; na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda.

86.  Hao ndio walionunua maisha ya dunia kwa akhera, kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.

122

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

HAMTAMWAGA DAMU ZENU Aya 84 - 86 MAELEZO

Mazungumzo ya Mayahudi na matatizo yao hayajakwisha; na yanayokuja ni mengi. Kwa muhtasari wa Aya za Mayahudi, ni kwamba wao kila wanapopewa mwito wa uongofu na msimamo mzuri wanakakamia katika kueneza ufisadi duniani na wanaendelea katika upotevu, kama kwamba wao wameumbwa kumuasi Mwenyezi Mungu na kuikhalifu haki. Tawrat yao inawaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu, wao wanaabudu ndama; Musa anawaambia: Hii Tawrat kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wao wanasema; "Tuonyeshe huyo Mwenyezi Mungu wazi wazi". Tena Musa anawaambia: "Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwenu na mumwombe msamaha," wao wanafanya mzaha na stihizai.

Ikiwa Nabii Musa (a.s.) tu walimfanyia hivyo naye ni Mwisrail mwenzao, je mwingine watamfanyiaje? Mfalme Edward I aliwafukuza Uingereza na wakateswa na Hitler huko Ujerumani baada ya kuwajua walivyo. Wao wanastahili zaidi ya hayo. Tumekwishaeleza vile walivyofanyiwa na Fir'aun, Nebukadnezzar na Warumi.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba miongoni mwa ahadi alizozichukua Mwenyezi Mungu kwa Mayahudi katika Tawrat ni kutouana wenyewe kwa wenyewe wala wasimtoe yeyote katika nyumba yake. Na Mayahudi hawakanushi ahadi hizi, bali hawana nafasi ya kuzikanusha kwa sababu zinapatikana katika Tawrat ambayo wanaiamini kwa ukweli na kwamba hiyo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini pamoja na hayo yote waliikhalifu kwa makusudi, kwa hivyo ikawasimamia hoja.

MAANA

Na tulipochukuwa ahadi yenu kuwa hamtamwaga damu zenu wala hamtatoana majumbani mwenu.

Anarudia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwakumbusha Wana wa Israil ahadi walizoziweka kwa ulimi wa Musa na Mitume wengine waliokuwa baada yake. Miongoni mwa ahadi hizo ni kutomwaga damu na kutotoana majumbani mwao.

123

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                         2 Sura Al-Baqarah

Nanyi mkakubali na hali mnashuhudia.

Yaani mlikubali ahadi na kushuhudiana nyinyi wenyewe.

Unaweza kuuliza: Kukubali na kushuhudia ni kitu kimoja, sasa vipi ikafaa kuunganisha kitu kwa kitu chenyewe?

Jibu: Inawezekana kuwa ni katika upande wa kutilia mkazo. Vile vile inawezekana kuwa makusudio ya kukubali ni kukubali Mayahudi wa zamani na kushuhudia ni kwa watakaokuja. Kwa sababu wa zamani walikubali na wakakiri ahadi.

Kisha nyinyi hao hao mnajiua, na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao.

Yaani nyinyi baada ya kukiri kwenu ahadi, mnaivunja wenyewe, mwenye nguvu anamuua mnyonge na kumtoa katika nyumba yake.

Mkisaidiana dhidi yao kwa (njia ya) dhambi na uadui.

Aya inaonyesha kugawanyika Mayahudi na kusaidiana kila kikundi na Waarabu dhidi ya kikundi kingine cha Mayahudi.

Kwa ufupi kisa kilikuwa hivi: Aus na Khazraj ni koo mbili za Kiarabu zenye asili moja, kwa sababu Aus na Khazraj walikuwa ndugu. Koo mbili hizi zilikuwa na uadui na vita kati yao kabla ya Uislamu na walikuwa wakimshirikisha Mwenyezi Mungu, hawajui pepo wala moto wala Kiyama au Kitabu.

Na Mayahudi nao walikuwa na koo tatu: Bani Qaynuqa'a, Bani Quraidha na Bani Nadhir, nao walikuwa na uadui na vita kama ilivyokuwa kati ya Aus na Khazraj pamoja na kuwa hawa Mayahudi walikuwa katika asili moja na dini yao ni moja. Wote hao, Mayahudi na Waarabu walikuwa ni wakazi wa Madina.

Bani Qaynuqa'a walikuwa wakisaidiana na Aus dhidi ya Bani Nadhir na Quraidha; kama ambavyo Bani Nadhir na Bani Quraidha walikuwa wakisaidiana na Khazraj dhidi ya Qaynuqa'a. Vita vinapochacha Myahudi alikuwa akimuua ndugu yake Myahudi na kumtoa nyumbani kwake akiweza. Lakini kama Yahudi akitekwa na Mwarabu, basi Mayahudi hukomboana hata kama ni adui yake mkubwa.

Kwa ufupi ni kwamba Mayahudi hawaoni kizuizi kuwaua Mayahudi wenzao kiasi cha kusaidiana na Waarabu, lakini Mwarabu akimteka nyara Yahudi, basi Yahudi mw-enzake huingiwa na huruma na kutoa

124

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

fidia kumkomboa mwenzake ingawaje ni adui yake. Kwa hivyo Yahudi anahalalisha kumuua ndugu yake na kumfukuza, lakini asiwe mateka. Walikuwa wakidai kwamba Tawrat yao ndiyo inayowaamrisha kukomboa mateka wa Kiyahudi.

Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu kwamba Tawrat yao vile vile imewaamrisha kutouana na kutotoana majumbani; sasa vipi mmeiasi Tawrat katika kuua, na kuitii katika kukomboa mateka?

Hii ndiyo tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na wakiwajia mateka mnawakomboa na hali kumeharamishwa kwenu kuwatoa. Je mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi?

Walilolikataa ni kule kukatazwa kuua, kusaidiana katika dhambi na uadui na kutoana majumbani. Waliloamini, ni lile la kutoleana fidia mateka. Na hii ndiyo istihzai hasa na kucheza na dini.

Unaweza kuuliza, lenye kuharamishwa kwao ni kuua na kusaidiana na kutoana majumbani; kwa nini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana majumbani katika Aya hii? Jibu: Ndio yote ni haramu, lakini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana kwa kutaja mara ya pili kwa sababu ya kutilia mkazo tu. Kwa sababu kutoana majumbani huendelea, kinyume na kuua kama walivyosema wafasiri wengine.

Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya duniani.

Malipo yanaweza kuwa ya heri au ya shari; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Na malipo yao kutokana na vile walivyosubiri ni pepo na nguo za hariri."

(76:12)

"Na mwenye kumuua mumin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo atadumu..."

(4:93)

125

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Hao ndio walionunua maisha ya dunia kwa akhera; kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.

Mwenyezi Mungu hakuharamisha, katika Aya hii wala nyingine chakula kizuri na mavazi ya kifahari, isipokua anamkemea mwenye kuiuza dini yake kwa ajili ya dunia yake na akaishi maisha ya kidhulma na upotevu. Hakika Mwenyezi Mungu anakataza ufisadi duniani na sio vipambo na neema za dunia, bali hakika Yeye Mwenyezi Mungu amekanusha sana kuharamisha neema na ladha katika dunia hii; kama anavyosema:

"Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja wake. Na, vitu vizuri katika riziki? Sema: hivyo ni kwa walioamini...."

(7:32)

Yaani ni halali kwa aliyevichuma kwa njia ya halali na ni haramu kwa anayevitafuta kwa kunyang'anya, kuhadaa na utapeli.

Kwa ufupi ni kwamba misingi ya ki-Qur'an ni kuishi watu katika kusaidiana yale yaliyo na wema kwa wote. Ama misingi ya Kizayuni ya kikoloni, ni "Maadamu mimi ninaishi basi na uangamie ulimwengu" na kila mwenye kwenda na msingi huu, basi ni Mzayuni akijua au asijue; hana budi kukumbana na uadilifu wa mbingu na ardhi na kuteremkiwa na mateso na balaa.

MAYAHUDI NA UKOMUNISTI NA UBEPARI

Inadhihiri kutokana na Aya tukufu kwamba kugawanyika Mayahudi katika makundi mawili ni mambo waliyoyarithi kutoka kwa mababa na mababu zao ili wazidishe moto kuwaka kwa upande fulani na wapate masilahi yao kwa upande wa pili. Kama ilivyo kuwa kugeuka geuka kwao ndio asili yao na ada yao.

Kabla ya nusu karne walikuwa wakilingania ukomunisti na ndio wao leo wanaoulemea ubepari. Hawana lengo lolote isipokuwa kuugawa ulimwengu na kuanzisha vita na fitina ili watekeleze siasa zao za ukandimizaji na ukupe wa kunyonya jasho la watu.

126

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

87.  Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake; na tukampa Isa, mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi wazi, na tukamtia nguvu kwa roho takatifu. Kila alipowafikia Mtume kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlijivuna,          kundi          moja mkalikadhibisha na kundi jingine mkaliua!

88.  Na walisema: Nyoyo zetu A, zimefunikwa, bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini!

TULIMPA MUSA KITABU

Aya 87 - 88

LUGHA

Neno Maryam, lina maana ya mtumishi kwa lugha ya kiebrania. Kwa sababu mama yake Maryam aliweka nadhiri ya kumtoa awe mtumishi wa Baitul -Maqdis (Quds).

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake

Yaani tumempa Musa Tawrat; kisha tukawapeleka Mitume baada yake, mmoja baada ya mwengine. Inasemekana kuwa hazikupita zama kati ya Musa na Isa ambaye ndiye Mtume wa mwisho wa Kiisrail, isipokuwa kulikuwa na Mtume Mursal au Mitume tofauti wanaoamrisha mema na kukataza mabaya. Imesemwa katika Tafsirul Razi na ya Abu Hayan El-Andalusi kwamba Mitume hao ni Yoshua, Samuel, Sham'un, Daud, Suleiman, na Shiau. Vile vile Armiya, Uzayr, Ezekiel, Eliyas, Yunus, Zakaria na Yahya.

127

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Na tukampa Isa mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi wazi na tukamtia nguvu kwa roho takatifu.

Isa (a.s.) ndiye Mtume wa mwisho wa wana wa Israil, na kati yake na Musa kulikuwa na karne 14.

Ni kidogo tu wanayoamini

Yaani hawakuamini katika Mayahudi isipokuwa wachache tu, kama Abdallah bin Salam na wafuasi wake. Mwenye Majmaul-Bayan amechagua kusema kuwa maana ya: "ni kidogo tu wanayoamini" kwamba hakuamini yoyote katika wao, si wachache wala wengi; kama vile inavyosemwa ni nadra kufanya'. Kwa maana ya kutofanya kabisa. Lakini maana tuliyoyaeleza mwanzo ndiyo yaliyo sahihi zaidi, kwa kuangalia kauli yake Mwenyezi Mungu:

"...Na kwa kusema kwao nyoyo zetu zimefumbwa, bali Mwenyezi Mungu amezipiga mhuri kwa kufuru yao, basi hawataamini ila wachache tu."

(4:155).

MKWELI NA TAPELI

Inatakikana tuangalie tena kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: "Kila walipowafikia Mitume ..." mpaka mwisho. Hakika Aya hii tukufu pamoja na kuwa na madhumuni ya kumsuta mwenye kuwaasi Mitume na kuikataa haki, kama haikuafikiana na matakwa yake, pia vile vile ina madhumuni ya kumsuta mwenye kuwapuuza watu na asiwakabili kwa tamko la haki kwa kutaka kujipendekeza kwao kwa tamaa ya cheo nk.

Hakika mtengenezaji wa kweli anaizungumza haki wala haogopi lawama katika kazi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu lengo lake la kwanza na la mwisho ni kumridhisha Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa ajili hiyo ndio anajitoa muhanga na kufa shahidi kwa ajili ya kuwapelekea na kuwaonyesha haki umma.

Ama mharibifu aliye mwongo anakuwa na lengo la kuwaridhisha watu ili wanunue bidhaa yake: Imam Ali (a.s.) anasema: "Usimchukize Mwenyezi Mungu kwa kumridhisha yeyote katika viumbe vyake."

128

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

89.  Na kilipowajia kitabu kitokacho kwa         Mwenyezi          Mungu kisadikishacho yaliyo pamoja nao, na zamani walikuwa wakiomba ushindi juu ya makafiri. Lakini yalipowafikia yale waliyoyajua waliyakataa. Basi laana ya Mwenyezi Mungu ikojuu ya makafiri.

90.  Kibaya kabisa walichokiuzia nafsi zao ni kule kukataa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa kuona maya kuwa Mwenyezi                         Mungu amemteremshia fadhila zake amtakaye katika waja wake. Kwa hiyo wakastahili ghadhabu juu ya ghadhabu, na watakuwa nayo makafiri adhabu idhalilishayo.

91. Na wakiambiwa: Yaaminini V aliyoyateremsha          Mwenyezi

Mungu husema: Tunaamini j» yaliyoteremshwa juu yetu; na ^ hukataa yaliyo nyuma yake; na W hali yakuwa hii ndiyo haki inayosadikisha yaliyo pamoja & nao. Sema: Mbona mliwaua Mitume wa Mwenyezi Mungu hapo zamani kama mlikuwa mkiamini

129

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza KILIPOWAFIKIA KITABU

2 Sura Al-Baqarah

Aya 89 - 91 MAELEZO

Mayahudi wa Madina walikuwa wamejipa tumaini la kujiwa na Mtume na walikuwa wakimtaja Muhammad, wakiwaambia Aus na Khazraj: "Kesho atakuja Mtume ambaye sifa zake tumezikuta katika Tawrat na atawashinda waarabu na washirikina wote."

Mayahudi walikuwa wakifikiria kuwa huyo Mtume ni Mwisrail sio Mwarabu. Basi Mwenyezi Mungu alipomtuma Muhammad Mwarabu, waliona unyonge, wakaingiwa na ubaguzi na kuupinga Utume wake na kukanusha yale waliyokuwa wakiyasema kwa Muhammad. Ikawa baadhi ya Aus na Khazraj wanawambia: "Enyi Mayahudi, jana mlikuwa mkitutisha kwa Muhammad (s.a.w.) kuwa sisi ni watu wa shirk: mlikuwa mkimsifu na kumtaja kwamba yeye ni Mtume. Sasa mbona sisi ndio tunaomwamini na nyinyi mmegeuka na kurudi nyuma?

Wakajibu Mayahudi : "Hakutujia na kitu tunachokijua na wala yeye siye yule tuliyekuwa tukiwatajia". Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. Na kilipowajia kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kisadikishacho yaliyo pamoja nao.

Yaani ilipowajia Qur'an walikanusha. Qur'an waliyoikanusha ndani yake mna usadikisho wa yale yaliyo katika Tawrat yao iliyobashiri kuja Muhammad (s.a.w.). Kwa hiyo wanamfanya mwongo yule anayewasadikisha wao, bali wanajikadhibisha wenyewe.

Hili si geni wala si ajabu kwa yule anayefanya matakwa yake na mapenzi yake ndiyo kigezo cha kuhalalisha, kusadikisha na kukadhibisha. Kila mwenye kujihalalishia yale yaliyo haramu kwa wengine, basi anaingia katika mkumbo huu. Ewe Mwenyezi Mungu tukinge na shari ya kutojifahamu sisi wenyewe.

Na hapo mbele walikuwa wakiomba ushindi juu ya makafiri lakini yalipowafikia yale waliyokuwa wakiyajua waliyakataa.

Mayahudi kabla ya kuja Mtume Muhammad (s.a.w.) walikuwa wakiwaonya Aus na Khazraj kwa Muhammad. Lakini alipokuja mambo yaligeuka, Aus na Khazraj wakamwamini na wakamsaidia mpaka wakaitwa Ansar (wasaidizi) na Mayahudi wakamkanusha; wakaangamizwa na kufukuzwa na hao Ansar kupitia kwa Muhammad;

130

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kama vile walivyokuwa wao wakiwaonya Ansar. Namna hii wanapata wenye vitimbi vibaya, na balaa humshukia yule anayemtakia mwenzake hiyo balaa.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mayahudi waligeuza imani waliyokuwa nayo kwa Muhammad?

Jibu: Walikuwa wakiitakidi kwamba Mtume atakayekuja atakuwa Mwisrail kutoka katika kizazi cha Is-haq, kwa kufikiria wingi wa Mitume Waisrail. Walipomwona ni Mwarabu kutoka katika kizazi cha Ismail, walimkanusha kwa uhasidi na ubaguzi tu wa Kiyahudi. Na kila mwenye kuipinga haki kwa ubaguzi wa kikabila au vinginevyo, basi huyo ni sawa na Mayahudi hao ambao walikataa kumkiri Muhammad, si kwa lolote isipokuwa kwamba yeye ni Mwarabu tu.

25

Kibaya kabisa walichokiuzia nafsi zao ni kule kukataa alichokiteremsha Mwenyezi Mungu.

Qur'an tukufu mara nyingi hutumia tamko la kuuza na kununua na biashara, kuhusu amali njema na mbaya. Kwa vile mtu akiamini na akafanya amali njema, ni kama kwamba amefanya biashara ya nafsi yake na kuiokoa; na kama akikufuru na kuacha kunufaika, ni kama kwamba ameiuza nafsi yake kwa shetani kwa thamani duni kabisa. Kuziuzia nafsi zao hapa ni kwa maana ya kuwa Mayahudi wameziuzia shetani nafsi zao na wamejiangamiza; wala hapana thamani ya nafsi zao isipokuwa hasadi na ubaguzi wa Kiyahudi tu. Kwa hivyo ndiyo Mwenyezi Mungu akasema:

Kwa kuona maya kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila zake amtakaye katika waja wake.

Yaani walimkanusha Muhammad (s.a.w.) si kwa jingine isipokuwa wao walitaka kuhodhi wahyi na fadhila kwao tu peke yao. Hawakubali kutoka kwa Mwenyezi Mungu wala kwa mwengine isipokuwa yale yanayoafiki mapenzi na manufaa yao. Kwa hiyo wao wanastahili adhabu mara mbili, kwa kukanusha na kwa ubinafsi wao.

Haya ndiyo waliyoyataja wafasiri kwa kuangalia dhahiri ya Aya. Utakuja ubainifu wa sababu za hakika za kumkanusha kwao Muhammad (s.a.w.) katika Aya ya 91 ambazo ni manufaa na chumo lililotokana na uasherati, udanganyifu, riba, na mengineyo yaliyoharamishwa na Uislamu.

131

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Na wanapoambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu.

Yaani aminini wahyi kama ulivyo bila ya kuangalia utu wa mwenye kuufikisha wahyi huo. Kwa sababu Mtume ni wasila tu wa kufikisha. Ama sharti lenu la kuamini wahyi kuwa uteremshwe kwa taifa la Kiisrail tu, na kama ukiteremshiwa mwengine basi hamwamini, sharti hili linafichua kukosa kuamini wahyi kimsingi. Isitoshe, itakuwa nyinyi mnatoa hukumu kwa Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yenu. Maana yake nyinyi mnataka Mwe-nyezi Mungu awanyenyekee na mnakataa kumnyenyekea.

Husema: Tunaamini yaliyoteremshwa juu yetu.

Huku ni kukiri wazi kwamba wao hawaamini wala hawataamini isipokuwa kwa sharti la kuteremshwa wahyi kwao, na hawataamini wahyi utakaoteremshwa kwa mwingine, hata kama kutakuwa na dalili elfu.

"Sema: Mbona mliwaua Mitume wa Mwenyezi Mungu hapo zamani kama mlikuwa mkiamini."

Hakuna hoja yenye nguvu zaidi ya hii; yaani sema ewe Muhammad kuwaaambia Mayahudi: Nyinyi ni waongo katika madai yenu ya kuamini wahyi kwa kuuhusisha na taifa la Kiisrail, bali nyinyi hamwamini wahyi kabisa, hata ule uliowahusu nyinyi! Dalili ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu amepeleka Mitume kutoka kwenu na kwa ajili yenu na akawajibisha muwasadiki na kuwatii, lakini pamoja na hayo wengine mliwafanya waongo; kama vile Isa (a.s.) na wengine mkawaua kama vile Zakaria na Yahya. Hii inafahamisha uongo wenu na kugongana vitendo vyenu na maneno yenu na kujidaganya wenyewe.

Imekuwa sawa kuuelekeza msemo wa kuua kwa Mayahudi wa Madina pamoja na kuwa walioua ni mababu zao. Hiyo ni kwa sababu umma wao ni mmoja kwa kushiriki kuridhia kuua.

WALIOFANANA NA MAYAHUDI

Mayahudi walimkataa Muhammad (s.a.w.), kwa sababu alikuwa si Mwisrail; Naye Abu Sufian alimkanusha na kuongoza jeshi kumpinga kwa sababu Mtume ni katika ukoo wa Hashim. Alikataa kwa sababu ukoo wa Hashim utapata utukufu wa Utume kuliko ukoo wake yeye Abu Sufiani wa Umayya.

Vile vile Maquraish waliukana ukhalifa wa Ali (a.s.), kwa sababu walichukia kukusanyika Utume na Ukhalifa katika nyumba ya Hashim. Baadhi ya wasiokuwa Waarabu wanaona uzito kuwa Marjaa (Mufti) wa

132

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kwanza awe Mwarabu; kama ambavyo baadhi ya waarabu nao wanaona uzito kuwa Marjaa (Mufti) ambaye si Mwarabu. Mimi nawajua watu ambao wako tayari kubaki kwenye upotevu lau wanahiyarishwa kuifuata haki kwa wasiokuwa wao. Vile vile lau wanahiyarishwa kati ya kusikiliza sifa za mwingine, basi wangeona bora kusikiliza za Yazid.

Kwa ajili hiyo ndipo ukaona mtu anafanya juhudi ya kutafuta aibu ya mwenzake akipata chembe tu, huikuza na kuifanya jabali, na akiikosa huizusha.

Mwenye kuona fadhila kuwa ndio msingi, huikuza vyovyote iwavyo na njia yoyote itakavyokuwa na humwonyesha mwingine kama anavyoona yeye; bali hufanya kazi ya kuieneza. Ama mwenye kuikanusha, hutumia muundo huo ambao wameutumia Mayahudi kwa inadi.

92. Na aliwajia Musa na hoja zilizo wazi wazi, kisha mkafanya ndama baada yake na hali nyinyi ni madhalimu.

93. Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu: Kamateni kwa nguvu haya tuliyowapa na sikilizeni. Wakasema: "Tumesikia na tumekataa" na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ni kibaya kabisa kilichowaamrishia imani yenu; mkiwa ni wenye kuamini.

94. Sema: Ikiwa nyumba ya akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu nyinyi tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi ni wa kweli.

 

133

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

95.  Wala hawatayatamani    kabisa kwa sababu ya        yale yaliyotangulizwa na     mikono yao, na Mwenyezi     Mungu anawajua madhalimu.

96.  Na Utawaona wanapupia zaidi maisha kuliko watu wengine na kuliko wale wamshirikishao Mwenyezi Mungu. Kila mmoja katika wao anapenda lau angelipewa umri wa miaka elfu. Na huko kupewa kwake umri mwingi                         hakuwezi kumwondoshea adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda.

0) tJ

MUSA ALIWAJIA NA HOJA

Aya 92 - 96

MAELEZO

Aya hizi ziko wazi na zinayakariri yaliyotangulia. Kwa hiyo tutaeleza maana kwa ujumla.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake kujadiliana kwa uzuri na wapinzani. Maana ya kujadiliana kwa uzuri ni kuzungumza na moyo na akili. Hoja zote za Qur'an ziko namna hiyo; imewataka wakanushaji wajifikiriie wao wenyewe na kuumbwa mbingu na ardhi; akamwambia mwenye kumnasibisha Bwana Masih uungu, kuwa yeye Masih na mama yake walikuwa wakila chakula. Na inazungumza na nyoyo za Mayahudi kwa Aya hizi kwa kuwakumbusha neema ya Mwenyezi Mungu ya kuwapelekea Tawrat ambayo ndani yake mna uongofu na nuru; kama zilivyowakumbusha Aya zilizotangulia kukombolewa kwao kutoka kwenye minyororo ya Firaun, n.k.

134

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kisha Mwenyezi Mungu akawakemea kwa kuabudu kwao ndama wakaikufuru na kuipinga neema Yake, amekariri kutaja kuinuliwa jabali juu yao kutokana na uasi wao na mantiki ya kiakili ikayakadhibisha madai yao ya kuwa wao ni watoto na wapenzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba pepo inawahusu wao tu hataingia mwengine zaidi yao. Vilevile amewaamrisha kutamani mauti ikiwa wao ni wakweli. Kwa sababu mwenye kuitakidi kwamba pepo ni yake, basi atachagua mauti yenye raha kuliko kuwa na maisha ya balaa na mashaka.

Kisha Qur'an ikatoa habari kwamba wanapupia sana dunia na wana pupa zaidi kuliko wale wasioamini pepo wala moto. Bali hata mtu katika wao anaweza kutamani lau angeliishi miaka elfu. Lakini kurefusha kwake umri hakutamfaa kitu wala hakutamwokoa na adhabu.

Lengo la majadiliano haya ya kimantiki ya akili yaliyo salama ni kuwathibitishia Mayahudi hoja kwamba wao ni waongo wanavyodai kuwa wanaamini Tawrat, na kudai kwao kuwa wao ni taifa teule la Mwenyezi Mungu. Sheikh Maraghi katika tafsir yake anasema: "Imekuja Hadith kwamba Abdalla bin Rawaha alipokuwa akipigana na Warumi alikuwa akiimba:

Kwa hamu naitamani, Pepo ilokaribia

Yenye vinywaji laini, Vilo baridi jamia

Na Ammar bin Yasir katika vita vya Siffin alisema:

Hapo kesho twaazimu, Kukutana na wapenzi

Muhammad muadhamu, Na swahabaze wa enzi

Ikiwa Mayahudi hawatatamani mauti basi wao si wakweli wa imani. Hoja hii inawahusu watu wote. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuifanya hoja hiyo ni mizani watakayopimia madai yao ya imani na kusimamia haki za Mwenyezi Mungu. Wakiwa wanaona raha kujitolea roho zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, watakuwa ni waumini wa kweli, vinginevyo watakuwa kinyume na madai yao.

MASLAHI NDIO SABABU

Hatuna shaka kabisa kwamba suala la kumkadhibisha Muhammad (s.a.w.) sio suala la kuhusiana na ubaguzi tu. Isipokuwa sababu hasa ni maslahi yao ya kiutu na manufaa yao ya kimaada. Kwani wao wanaishi kwa utapeli, riba, na uasherati; na Muhammad (s.a.w.) anayaharamisha hayo. Vipi wataamwamini? Ushahidi wa hayo ni kwamba wao hawana

135

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

sababu nyingine isipokuwa pupa ya manufaa ya kibinafsi. Na kila mwenye kupupia manufaa yake, haumfai mjadala mzuri. Na kaui yake Mwenyezi Mungu:

"Na utawaona wanapupia zaidi maisha," inafahamisha hilo.

97. Sema: Anayemfanyia uadui *'**, ** Jibril Hakika yeye ameiteremsha Qur'an moyoni mwako, kwa Vj UJ \SjIa» İill üib ÜLİâ idhini ya Mwenyezi Mungu,                          o "          "

inayosadikisha yale yaliyokuwa  kabla yake, na ni uongozi na bishara kwa waumini.

98.  Anayemfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi Mwenyezi Mungu ni adui kwa makafiri.

99.  Na hakika tumekuteremshia hoja zilizo wazi; na hawazikatai ila mafasiki.

100. Je, kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa? Bali wengi katika wao hawaamini.

ANAYEMFANYIA UADUI JIBRIL

Aya97-100

LUGHA

Imesemekana kuwa maana ya neno Jibril ni mja wa Mungu (Abdullah) na Mikail ni mja mdogo wa Mwenyezi Mungu (Ubaidullah)

136

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza MAANA

2 Sura Al-Baqarah

Sema: Anayemfanyia uadui Jibril basi yeye ni kafiri, laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake."

Wamekubaliana wafasiri kwamba sababu ya kushuka Aya hii ni Mayahudi walimuuliza Mtume (s.a.w.) kuhusu Malaika anayemteremshia wahyi. Akawajibu: "Ni Jibril." Wakasema" "Ah! Huyo ni adui yetu, kwa sababu yeye huleta shida na vita na Mikail huleta amani na raha: lau angelikuwa Mikail ndiye anayekuletea wahyi tungelimwamini."

Wameufanya ushindani kwa dhahiri, kwanza kwenye ukabila wa Muhammad (s.a.w.) kwamba wahyi ushuke kwa mmoja wa Waisrail. Mwenyezi Mungu na Mtume wake alipowashinda kwa hoja, wakabadilisha ushindani kwa Jibril sio Muhammad tena. Hakika ilivyo hasa - kama tulivyoelezea mwanzo - sio sababu ya Uarabu na Uyahudi au Jibril na Muhammad bali ni maslahi yao tu; ni uasherati, ulevi, riba na utapeli. Na wao wanafanya unafiki na kuficha uwongo wao.

Kwa hivyo kwa upande wa malumbano na kuwapa hoja, Mwenyezi Mungu alisema:

Hakika yeye ameiteremsha Qur'an moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake:

Yaani uadui wenu kwa Jibril hauna msingi, kwa sababu yeye ni mpelekaji wahyi tu, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Muhammad. Na wahyi huo unasadikisha yaliyo katika Tawrat yenu, miongoni mwa sifa za Muhammad na bishara kwa wanaoamini. Kwa hivyo uadui wenu kwa Jibril ni uadui kwa Mwenyezi Mungu, wahyi, Tawrat, uongozi wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake na bishara kwa waumini.

Hakika tumekuteremshia hoja zilizo wazi na hawazikatai ila mafasiki

Yaani yaliyomjia Muhammad (s.a.w.) hayana shaka baada ya kuwa na hoja na dalili, na wala hayakanushi isipokuwa mwenye kukufuru Mwenyezi Mungu; mwenye kuipinga haki. Makusudio ya ufasiki hapa ni ufasiki wa itikadi yaani ukafiri sio ufasiki wa vitendo ambao unatendwa na mtu anapokuwa na imani.

137

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Je, Kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa?

Ahadi walizozitupa Mayahudi na kuzivunja ni nyingi; Kama ya kumwamini Muhammad, ya kuacha kuwasaidia makafiri, ya kuwaamini Mitume na kutowaua na kutomwabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, n.k. kwa hiyo wakamkadhibisha Muhammad na wakawasaidia washirikina, walio maadui wao na wa Muhammad. Vile vile huko nyuma waliwakadhibisha Mitume wakawa tayari kumsulubu Masih, na waliabudu ndama na mengine mengi.

Bali wengi katika wao hawaamini.

Yaani kuna kundi lililoabudu ndama na lililowaua Mitume, n.k; na wengi wao ingawaje hawakufanya hivyo, lakini bado ni makafiri, waovu.

Kwa ufupi ni kwamba asiyekuwa na haki anaweza kudai haki, na mwenye makosa anaweza kudai kuwa hana makosa. Wanayaweza hayo kwa mbinu za kusema. Lakini mara moja wanafedheheka zinapowashinda hoja na dalili ambazo hawawezi kuzikimbia; kama walivyofedheheka Mayahudi katika uwongo wao na madai yao kuwa wanafanya kama vile alivyoteremsha wahyi Mwenyezi Mungu.

Kuishi kwa amani na kumwamini mwenyezi mungu

Wenye kulingania amani wanakusudia kuwa watamaliza tofauti za wanaozozana kwa mikutano. Lakini tumejifunza kuwa mazungumzo ya amani na haja ya kuwa na amani, hayawezi kufaa kitu kwa watu wenye kuangalia manufaa yao. Wenye tamaa hawawezi kuacha tamaa zao isipo-kuwa kwa njia ya vikwazo na vitisho. Maisha ya amani yanahitaji akili iliyofunguka na tabia njema. Ni tabia gani tukufu itakayokuwa mbele za mtu asiyeamini isipokuwa maada, ulanguzi na kutaka utajiri wa haraka haraka? Na ni hoja gani zitakazomkinaisha mwenye tamaa?

Inasemekana kwamba mataifa mawili makubwa ya Mashariki na Magharibi yanadai amani kati yao, lakini wakati huo huo kila mmoja anajitengeneza silaha za hali ya juu na kujikinga kwa kumhofia mwenzake. Kwa hivyo amani wanayodai ni ya maneno na wala si ya vitendo.

Maumbile ya kiakili yanathibitisha kwamba kila taifa lina haki kamili katika kujiamulia mambo yake haliwezi kuingiliwa. Sasa je ni nani anayefuata misingi hii?

138

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Amani na haki haiwezi kupatikana kwa ukamilifu mpaka pande zote zinazohusika ziamini haki kwa njia ya haki. Ni muhali kuongoka kwenye heri na kutarajia heri yule asiyamini chochote isip-okuwa dhati yake na yule asiyejishug-hulisha na lolote zaidi ya manufaa.

101.Na walipojiwa na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao, kikundi kimoja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilikitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui.

WALIPOJIWA NA MTUME

Aya101

MAELEZO

Na walipojiwa na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Ambaye ni Muhammad (s.a.w.); aliyepelekwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote wakiwemo Mayahudi waliokuwa zama zake.

Mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nao.

Yaani kusadikisha yaliyo katika Tawrat miongoni mwa misingi ya Tawhid na bishara ya Muhammad.

Kikundi kimoja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu.

Nao ni wanavyuoni wa Kiyahudi.

Kilitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao.

Makusudio ya Kitabu, cha Mwenyezi Mungu, ni Qur'an. Imesemekana pia kuwa ni Tawrat, kwa sababu kumkana kwao Muhammad ni kuikana Tawrat ambayo imetoa bishara ya kuja Muhammad (s.a.w.). Hapa wanaingia wote Mayahudi na Manaswara. Kwani wote wamekipotosha

139

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kitabu, hasa sehemu zile zinazofungamana na bishara ya kuja Muhammad (s.a.w.); Bali hakuna tofauti kati ya Mayahudi na wale wanaoondoa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata mapenzi yao.

1O2.Wakafuata yale yaliyofuatwa na mashetani, katika ufalme wa Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu               uchawi               na

yahyoteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta, katika (mji wa) Babilon Wala hawakumfundisha            yeyote

mpaka wamwambie: Hakika sisi ni fitna (mtihani), basi usikufuru. Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na                            wanajifunza

yatakayowadhuru                wala

hayawanufaishi. Na kwa hakika wanajua kwamba aliyeyanunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na hakika ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wangelijua.

140

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

WAKAFUATA YALE YALIYOFUATWA NA MASHETANI Aya 102 MAELEZO

Wafasiri hapa wamerefusha maneno. Wengi wao hawana tegemeo lolote isipokuwa ngano ambazo hazikubaliki kiakili: Razi amechafua karibu kurasa ishirini katika kufasiri Aya hii, akazidisha mikanganyo. Mwenye Majmaul-Bayan naye akafanya hivyo hivyo. Ama Sayyid Qutb yeye ameingilia kuelezea mambo ya kuzugwa watu, ndoto, athari, n.k. Na huku hasa ndiko kukimbia.

Kwa hivyo nikabaki muda mrefu nikitafuta na kupekuwa vitabu na tafsir. Hakikutulia kiu changu hata kwenye tafsir ya Sheikh Muhammad Abduh na wanafunzi wake wawili - Al-Maraghi na mwenye Tafsir ya Al Manar, Bora zaidi ya niliyoyasoma katika mlango huu ni yale yaliyotajwa katika kitabu cha Annuwatu fi Haqli l-hayat cha Sayyid Ubaydiy, Mufti wa Musul (Iraq). Na haya ndiyo aliyoyasema ninamnukuu:

"Niliendelea kutofahamu maana ya Aya tukufu kiasi ambacho hakikunitosheleza kwa mfasiri yoyote, mpaka nilipotua kwenye historia ya Free Mason, ndipo nikajua maana yake.

Kutokana na kugongana wafasiri kiasi ambacho walionyesha kuwa Aya ina vitu viwili vyenye kutofautiana na kuingiza katika Aya hii ngano za watu wa kale ambazo sharia iliyowazi inazikataa, nimeona ni wajibu nikitumikie kitabu cha Mwenyezi Mungu kuthibitisha haya.

Ulipotukuka Ufalme wa Suleiman, mfalme wa Babiloni alikuwa na chuki na tamaa katika Palestine na Syria, na akaingiwa na hofu badala ya tamaa yake. Wakafanya msafara watu wawili walio wajanja na werevu wakitafuta mafunzo yatakayowawezesha kuuharibu ufalme wa Suleliman. Wakaingia dini ya Kiyahudi na kuonyesha utawa, kama kawaida wakapata wafuasi, wakawa wanaharibu fikra za watu na kuacha chuki kwa Suleiman mpaka wakamzulia ukafiri. Watu hawa walikuwa kama Malaika kwa wanavyoonyesha utawa. Lakini walikuwa ni mashetani na mafunzo yao yalikuwa kama uchawi kutokana na ufasaha, na mara kwa mara walikuwa wakitumia neno mfalme kwa mtu mwema, na neno shetani kwa mtu mwovu na neno uchawi kwa ibara ya fitina. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu kumzungumzia Yusuf, alivyozungumziwa.

141

Tafsir Al-Kash if: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"...Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu."

Na kauli yake:

(12:31)

"Mashetani katika watu na majini wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba kwa udanganyifu."

(6:112)

Vile vile kauli yake Mwenyezi Mungu akimzungumzia Walid:

"Hayakuwa haya ila ni uchawi ulionukuliwa, hayakuwa haya ila ni kauli ya binadamu."

(74:24-25)

Na kuna Hadith inayosema: "Katika ufasaha kuna uchawi."

Tumeelezewa historia ya Nebukadnezzar, mfalme wa Babelon katika vita vya Palestin baada ya Suleiman na alivyoiharibu Baitul Maqdis. Na tunaiona Qur'an inatilia nguvu matukio ya historia katika Aya isemayo:

"Na tukawafahamisha wana wa Israil katika kitabu: Hakika nyinyi mtafanya uharibifu katika nchi mara mbili na kwa yakini mtatakabari kutakabari kukubwa. Basi ilipofika ahadi ya kwanza yake tukawapelekea watumishi wetu wenye mapigano makali, mno wakaingia majumbani kwa nguvu, na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa."

(17:4-5)

Ukiyajua haya, basi tunasema: "Dhamiri katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), 'na wakafuata', "inawarudia Mayahudi wa Madina, ambao zimetangulia zaidi ya Aya sitini na mbili katika kuwaeleza wao tu. Utakapoyajua haya, kisha ukazingatia vizuri Aya zinazoambatana na Aya ya Suleiman, na ukafikiria kwa ndani kauli yake Mwenyezi Mungu juu ya ufalme wa Suleiman na madhumuni yake, utajua kwamba maana ya Aya tukufu ni kwamba Mayahudi wa Hijazi walikuwa wak-imfanyia

142

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mtume wa Kiarabu vitimbi na propaganda kwa kufuata nyayo za mab-abu zao ambao waliwasaidia wajumbe wa Babilon katika kuvunja ufalme wa Suleiman."

UFAFANUZI

Tutafasiri Aya kwa misingi ya alivyofahamu Ubaydiy. Wakafuata.

Yaani walifuata Mayahudi wa Madina waliokuwa zama za Mtume Muhammad (s.a.w.).

Yale yaliyofuatwa na mashetani

Makusudio ya mashetani ni wadanganyifu; miongoni mwao ni wale watu wawili wa Babilon ambao walijionyesha kuwa ni watakatifu kumbe ni maibilisi.

Katika ufalme wa Suleiman.

Yaani Mayahudi wa Madina walitumia dhidi ya Muhammad, sawa na vile walivyokuwa mababu zao Mayahudi dhidi ya ufalme wa Suleiman.

Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru.

Yaani kila walilomnasibishia Suleiman alikuwa yuko mbali nalo ulikuwa ni udanganyifu na uzushi wao, Wakiwafundisha watu uchawi. Yaani wanawafundisha watu mambo ya ubatilifu.

Na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili.

Yaani watu wawili wa Babilon waliodhihirisha utakatifu na ucha Mungu. Mak-usudio sio kuteremshiwa Wahyi wa Mitume, bali ni kiasi cha kupewa ilham na kufundishwa.

Wala hawakumfundisha, yoyote mpaka wamwambie: 'Sisi ni fitna (mtihani) basi usikufuru'

Walikuwa wakisema hayo kwa unafiki ili wawapumbaze watu kwamba elimu zao ni za kutoka kwa Mungu na kwamba wao ni watakatifu, wasafi wa nia; sawa na anavyosema mlaghai kumwambia yule anayemfundisha kuandika chuki na mapenzi: "Tahadhari kuandika hivi usije

143

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

ukawafarikisha waliooana kisheria, au kumfanya mke wa mtu kumpenda asiyekuwa mumewe."

Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe.

Yaani yale wanayofikiria kuwa yanaweza kutenganisha mtu na mkewe kama wanav-yochukua watu kutoka kwa walaghai, maandishi ya mapenzi na chuki.

Kwa ujumla ni kwamba Aya haifahamishi kuthibiti athari ya uchawi wala kuka-nusha. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu "Wakijifunza kwao ambayo waliweza", sio hukumu ya uhakika ya kutenganisha mtu na mkewe: Sawa na kusema kunywa kiponyesho, yaani kilichowekwa kwa ajili ya uponyeshaji. Kwa ufupi ni kwamba Aya haithibitishi wala haikanushi. Mara nyingi hekima ya kiungu hupitisha kubainisha kwa upande fulani na kwa ujumla kwa upande mwingine; hasa katika masuala yasiyo ya kiitikadi.

Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Yaani hawawezi kumdhuru yoyote vyovyote iwavyo kwa sababu ya kusoma na kuandika; kama akidhurika basi ni ku-tokana na sadfa tu, kwamba mtu amedhurika na sababu nyingine ya nje ikaon-ekana ni sababu hii. Makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu ni sababu ya nje iliyodhuru.

Na wanajifunza yatakayo wadhuru wala hayawanufaishi.

Ni kiini macho tu, na kiini macho hudhuru wala hakinufaishi.

Na kwa hakika wanajua kwamba aliyenunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera.

Wanajua wao kwamba mwenye kupendelea ulaghai hana fungu mbele za Mwenyezi Mungu.

Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao.

Yaani wamebadilisha kitu cha thamani kwa kitu duni. Imepita tafsiri yake katika Aya ya 61 ya sura hii.

144

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

il 3 I iial

a

(UT)

103.Na lau wangeamini na kuogopa, basi thawabu zitokazo kwa Mwenyezi Mungu zingekuwa bora kwao, laiti wangelijua.

LAU WANGEAMINI

Aya103

Maelezo:

Baada ya Mwenyezi Mungu kuyaorodhesha maasi ya Mayahudi na kampeni zao mbaya dhidi ya Muhammad (s.a.w.), amesema kuwa ukafiri wao huu na upinzani wao hautawafaa kitu. Lau wangelimwamini Muhammad, kama ilivyowaamrisha Tawrat yao, wangelistarehe na kupata daraja ya juu kwa Mwenyezi Mungu.

Amirul Mumini anasema: "Hakika kumcha Mungu ni ngome yenye nguvu na uovu ni ngome dhalili, haiwakingi watu wake wala haimhifadhi mwenye kuikimbilia. Fahamuni kuwa kumcha Mungu (takuwa) kunavunja uti wa mgongo wa makosa na hupatikana malengo kwa yakini".

UCHAWI NA HUKUMU YAKE

Mafaqihi wa Kishia wamezungumzia sana kuhusu uchawi, na wamerefusha maneno katika kuelezea maana yake, mafungu yake, yanayowezekana na yasiyowezekana. Pia wamezungumzia kuhusu kufundisha, kujifundisha na kuutumia.

Uchawi uliozungumziwa na Qur'an ni namna fulani ya udanganyifu na hadaa, kwa kuufanya uwongo uwe haki. Mwenyezi Mungu anasema:

"...Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake (Musa) zinakwenda mbio kwa uchawi wao."

(20:66)

"...Hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu"

(2:102)

145

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Imam Sadiq (a.s.) amesema kwamba uchawi uko namna nyingi; kama vile wepesi na haraka na kufanya hila, kwa sababu wenye hila wamegeuza uzima kuwa ugonjwa na maana kuwa hila.

Ama mambo ya kuandika, kuzungua na kutumia azima au kutabana na mengin-eyo ambayo yamesemekana kuwa yana athari, kama kufungwa mume wakati wa ndoa kiasi cha kushindwa kumwingilia mke. Vile vile mambo ya kuzidisha mapenzi, kutia chuki kati ya watu wawili na kuwatumia malaika na mashetani katika kupiga ramli na kutopoa, yote hayo, Shahidi wa pili ameyazungumzia katika Masalik mlango wa biashara akisema kuwa: "Wanavyuoni wengi wa Kishia wanaitakidi kwamba ni mambo ya kuwazia na dhana zisizokuwa na msingi wowote; na baadhi yao wanaona kuwa ni matukio ya kweli. Na yeye ni miongoni mwa wasemao kuwa ni hakika.

Bukhari amepokea katika Sahih yake J-4, mlango wa kisa cha Iblis na Askari wake, kwamba "Mtume alirogwa mpaka akawa anaonekana kama anafanya kitu na wala hakifanyi". Lakini hayo ameyakanusha mmoja wa Maimamu wa Kihanafi katika kitabu Ahkamul-Qur'an J-1; Uk. 55 chapa ya mwaka 1347 A.H. Vile vile Sheikh Muhammad Abduh amekanusha katika kufasiri Sura ya Falaq.

Sisi tuko pamoja na wale wanaouona uchawi kuwa hauna msingi wowote. Imam Sadiq anasema: Uchawi ni wenye kushindwa kabisa kugeuza aliyoumba Mwenyezi Mungu "...Lau mchawi angelikuwa na uwezo angelijizuwia asizeeke na pia angelijikiinga na maafa na magonjwa pia angelizuwia uzee, na ufukara. Na kwamba uchawi ni fitina inayotenganisha watu wanaopendana na kuleta uadui kwa wanaosikilizana."

Vyovyote iwavyo, wameafikiana mafaqihi wa Kishia kwamba adhabu ya mchawi ni kuuliwa akiwa ni Mwislamu. Akiwa si Mwislamu ni kutiwa adabu ya viboko na jela, kama atakavyoona hakimu.

26

1O4.Enyi mlioamini msiseme 'Raa'ina            bali            semeni

Mwenye kutaka ufafanuzi kuhusu uchawi na hukum yake asome kitabu Al-Jawahir mlango wa Biashara na mlango wa kisasi. Vile vile kwenye kitabu Makasib cha Sheikh Ansari. Mwenye Jawahir anasema :" sio kila Jambo geni ni uchawi, kwani elimu nyingi zina athari za ajabu; kama vile wanavyofanya wazungu wakati huu."

Hivi sasa ni mwaka 1967; miaka 121 imepita tangu alipokufa mwandishi huyu mkuu. Lau angelikuwako wakati huu asingeliona ajabu. Kwa sababu kila la ajabu hivi sasa litakuwa ni la kawaida wakati ujao.

146

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

'Undhurnaa' na sikilizeni; na makafiri wana adhabu iumizayo.

1O5.Hawapendi                waliokufuru

miongoni mwa watu wa kitabu wala washirikina mteremshiwe heri kutoka kwa Mola wenu. Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.

ENYI MLIOAMINI Aya 104-105 MAELEZO

Enyi mlioamini msiseme 'Raaina' bali semeni 'Undhurna' Mwenye Majmaul-Bayan anasema:

"Waislamu walikuwa wakisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Raina; Yaani tusikilize. Mayahudi nao wakalitumia neno hili kwa maana ya mpumbavu (katika lugha yao). Walipolaumiwa, wakasema tunasema kama wasemavyo Waislamu. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaka-taza hilo kwa kauli yake: Msiseme Raina na semeni: Undhurna. Makusudio ya Undhurna katika Aya ni kuangalia Mtume hali yao wakati anapozungumza; angoje ili wafahamu na waelewe maneno yote".

Uzindushi

Mwito wa kwanza katika Sura ya Baqara umekuja kwa watu wote na mwito wenyewe ni Uislamu na kumwabudu Mwenyezi Mungu; pale aliposema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya ya 21: "Enyi watu mwabuduni Mola wenu ambaye amewaumba..."

147

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mwito wa pili ulikuwa kwa wana Israil, taifa kubwa ambalo lilileta taifa la Kikristo. Mwito huu wa pili ulikuja kukumbusha kuondolewa mateso kwa waana wa Israil na kupatiwa neema; ni pale aliposema Mwenyezi Mungu katika Aya 40:

"Enyi wana wa Israil kumbukeni neema yangu niliyowaneemesha...". Mwito wa tatu umekuja kwa umma wa Muhammad (s.a.w.) katika Aya hii:

"Enyi mlioamini msiseme 'Raaina'", ambayo ni kuwafundisha Waislamu adabu za sheria baada ya kusilimu na kumwamini Mwenyezi Mungu.

Utaratibu huu wa miito hii mitatu ndio utaratibu wa kikawaida; yaani kuanza kuwalingania watu kwenye imani ya Mwenyezi Mungu, kisha kumtajia fadhila za Mwenyezi Mungu yule mwenye kumwamini Mungu kabla ya Utume tena kumfunza kuamini adabu za Mwenyezi Mungu yule mwenye kuamini Utume. Hii ni namna mojawapo ya ufasaha wa Qur'an.

Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa washirikina mteremshiwe heri kutoka kwa Mola wenu.

kitabu wala

Si ajabu kwa washirikina, Wayahudi na wakristo pamoja na makafiri, kuchukia yote aliyoteremshiwa Muhammad na vile alivyohusishwa na Mwenyezi Mungu kwa fadhila na hidaya na utengeneo; isipokuwa ajabu ni kutolichukia hilo.

Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye.

Amirul Muminin anasema: "Makusudio ya rehema hapa ni Utume."

 HUSUDA NA HASIDI

Husuda ni tabia za watu wengi, isipokuwa wale waliohifadhiwa na Mwenyezi Mungu, na wala haiko kwa washirikina, Mayahudi au Manaswara peke yao, bali iko pia kwa Waislamu wengi; hata kwa wanavyuoni wakubwa na baadhi ya wale wenye vyeo vya kuwa Marja (Mufti mkubwa) wa kidini ingawaje cheo hicho ndicho pekee kinachokurubiana na cheo cha maasum."

Mwenyezi Mungu, Mitume Maimamu na wenye hekima, wamezungumzia sana kuhusu hasadi. Miongoni mwa hayo ni kauli ya Imam Jafar Sadiq: "Hasadi asili yake ni upofu wa moyo na kukana fadhila za Mwenyezi Mungu, na hayo yote mawili ni mbawa za kufuru."

148

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Lugha fasaha zaidi niliyoiona katika kuisifu hasadi ni kauli ya bwana wa mafasaha na kiongozi wa wenye hekima, Amirul Muminin (a.s.) alipowaeleza kuwa ni mahasidi wa raha na wenye kutilia mkazo balaa. Akasema tena: "Inatosha kuwa ni shari kwa mahasidi kuhuzunika wakati unapofurahi."

Huenda itakuwa ni vizuri kunakili mfano huu kutoka kwa mwanahekima mmoja aliyesema: "Mfano wa hasidi ni kama mtu anayetupa jiwe kwa adui yake, kisha jiwe limrudie mwenyewe upande wa kuume na apandwe na hasira. Mara ya pili tena analitupa kwa nguvu kuliko kwanza, na limrudie upande wa kushoto na hapo ataingiwa na chuki na kisha alitupe jiwe kwa nguvu zote na hamasa halafu limrudie kichwani na limjeruhi na huku adui yake yuko salama."

Ni muhali kwa hasidi kuweza kutubu husuda yake, kwa sababu hasidi ni sawa na mwoga na bakhili. Atawezaje bakhili na mwoga kutubu? Ndio maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume kuwaambia mahasidi.

"...Sema; kufeni na ghadhabu zenu."

106.Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu?

107.Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni mfalme wa mbingu na ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

149

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

AYA YOYOTE TUNAYOIFUTA Aya 106-107

 KUFUATA

Kwanza tutaeleza maana ya kufuta kwa ujumla katika hukumu za sheria, kisha maana ya kufuta katika Qur'an.

Maana ya kufuta katika hukumu ya sheria ni kuja dalili inayofahamisha kuthibiti hukumu ya sheria kwa kudumu na kuendelea muda wote; baada ya kutumika hukumu hiyo kwa muda fulani, inakuja dalili nyingine ya kuthibitisha kwamba hukumu ile ilihusika na kipindi fulani tu; na kwamba masilahi yanahukumilia kutumika katika wakati fulani tu, sio kila wakati. Lakini hekima ya Mwenyezi Mungu ilidhihirisha kudumu na kuendelea. Sawa na Daktari ambaye anaona masilahi ya mgonjwa ni kutokula nyama kwa muda wa wiki moja tu, lakini akaona ni vizuri amfiche ule muda wa kumka-taza. Baada ya kupita wiki moja akamruhusu kula nyama. Kwa hivyo kufuta kunakuwa kwa maana ya kufuta yale yaliyoonekana kuwa ni ya kudumu na wala sio kuwa ni kwa sababu ya kutojua au kubadili mawazo.

Hakuna mwenye kutia shaka kwamba kufuta kwa maana haya kumethibiti katika sheria ya Kiislamu; kwani sheria imefuta baadhi ya hukumu zake zilizotangulia; kama vile sharia za Musa na Isa. Bali hukumu za Qur'an zenyewe zinafutana; kama vile kugeuza Qibla kuwa Al-Ka'aba (huko Makka) baada ya kuwa Baytul-Maqdis (huko Jerusalem).

Ama kufuta katika Qur'an kunawezekana kukugawanywa katika njia tatu:

1.    Kufuta Aya kisomo na hukumu, yaani kuondolewa tamko lake na hukumu yake.

2.    Kufutwa kisomo tu; kufutwa tamko na kubaki hukumu.

3.    Kufutwa hukumu tu, si kusomwa, yaani inasomwa lakini haichukuliwi dhahiri yake baada ya kutumiwa wakati fulani.

Lakini fungu la kwanza na la pili hayapo, kwa sababu yataleta upungufu na mageuzi katika Qur'an ambayo haifikiwi na batili mbele yake wala nyuma yake.

Ama fungu la tatu linawezekana na limethibiti; ndilo walilolikubali Waislamu wote na wafasiri wote, na limetungiwa vitabu mahsusi. Hivi

150

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

sasa kimetolewa kitabu kikubwa kwa jina "Annasikh wal-mansukh" (Inavyofuta na inayofutwa) cha Dkt. Mustafa Zaydi wa Misri.

Kwa ujumla inaonyesha kuwa hukumu ya sharia ikithibiti kwa njia sahihi haiwezekani kufutwa isipokuwa kwa Aya ya Qur'an au kwa Hadith mutawatir. Kwa sababu kufuta ni jambo kubwa na la muhimu. Kwa hivyo kufuta hakuwezi kuthibiti kwa habari moja. Kwa sababu kila umuhimu hauna budi kuenea na kutangaa midomoni. Mtu mmoja tu akinakili tukio kubwa au watu wengi, lakini bila ya kuenea, itakuwa ni uwongo. Kwani huoni kifo cha mtu mashuhuri kinanukuliwa na watu wengi! Vile vile mapinduzi! Lakini kifo cha mtu wa kawaida hunukuliwa na baadhi ya majirani na ndugu tu! Ufafanuzi zaidi uko katika Usulul-fiqh (elimu ya misingi ya Fiqh).

MAANA

Aya yoyote tunayoifuta au kuisahauliza, tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake.

Wafasiri wengi wanasema kwamba Mayahudi walikuwa wakisema kuwa: "Muhammad anawaamrisha masahaba zake jambo kisha anawakataza, leo anasema hili kesho anasema lile, lau anayoyasema kama yangelikuwa ni wahyi, kusingelitokea mgongano huu". Ndipo ikashuka Aya hii, kuwajibu.

Makusudio ya Aya, ni Aya za Qur'an tukufu, kwani maana haya ndiyo yanayokuja haraka kwenye fahamu. Amenakili Sheikh Maraghi katika tafsir yake kutoka kwa mwalimu wake, Sheikh Muhammad Abduh, kwamba makusudio ya Aya ni muujiza unaofahamisha utume wa Mtume; kwamba Mwenyezi Mungu anampa Mtume muujiza wa Mtume mwingine, kisha anauacha na kuumpa Mtume mwingine muujiza mwingine.

Maana haya yenyewe yako sawa, lakini mpangilio wa Aya unayakataa. Maana yanayoelezwa na wanavyuoni na kundi kubwa la wafasiri ni Aya za Qur'an.

Maana ya kufuta Aya ya Qur'an ni kubakia tamko na kisomo pamoja na kuacha hukumu iliyofahamishwa na Aya hiyo ambayo iliwahi kutumika wakati fulani.

Ama maana ya neno Nunsiha likisomwa bila ya harufi Hamza litakuwa lina maana ya kusahau; yaaani kuacha sio kwa kughafilika nayo yani twaiacha kama ilivyo bila ya mabadiliko. Kwani yafaa kusema kitu hiki

151

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

nimekisahau kwa maana ya kukiacha kama kilivyo. Na likisomwa kwa Hamza, litakuwa na maana ya kuchelewesha na kuahirisha yaani tunaacha kuiteremsha mpaka wakati mwingine.

Vyovyote iwavyo kupatikana herufi 'Ma' ya sharti haifahamishi kutokea kufutwa hasa, bali inafahamisha kuwa lau inatokea, basi Mwenyezi Mungu angelileta bora kuliko ile iliyofutwa.

Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu, hujui kwamba Mungu ni wake ufalme wa mbingu na ardhi?

Inasemekana kwamba msemo 'hujui' unaelekezwa kwa Mtume na makusudio yake ni Waislamu ambao walidhikika kutokana na upinzani wa Mayahudi na wengineo kuhusu kufutwa.

Ilivyo hasa ni kwamba msemo unaelekezwa kwa kila anayeona ajabu kufutwa au yule anayeumizwa na upinzani. Maana yake ni kuwa kufutwa sio jambo geni.

Kimsingi ni kwamba Mwenyezi Mungu anamiliki kila kitu na anapanga na kupitisha anavyotaka, iwe ni kufuta au kubakisha bila ya kufutwa. Ama kuhusisha kutaja mbingu na ardhi kunafahamisha kukusanya vitu vyote. Kwa sababu mbingu na ardhi zinakusanya viumbe vyote vya juu na vya chini.

Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Yaani msijali enyi waumini kwa anayepinga suala la 'kufutwa' au kitu chochote katika dini yenu; kiumbe hawezi kuwadhuru maadamu Mwenyezi Mungu ndiye anayetia nguvu na ndiye msaidizi.

Kwa ufupi ni kwamba kufuta ni haki, hakuna kizuwizi cha kutoka akilini au kwenye sharia, kinyume na wanavyofikiri wakanushaji na wapinzani!

108.Je mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, hakika amepotea njia iliyo sawa.

152

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

1O9.Wengi miongoni mwa watu wa kitabu wanatamani          lau

wangewarudisha nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nafsini mwao, baada ya kuwapambanukia haki. Basi sameheni na muwache mpaka Mwenyezi Mungu alete amri Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Ni muweza wa kila kitu.

JE MNATAKA KUMUULIZA MTUME WENU

Aya ya 108-109

MAANA

Je, mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani?

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaambia waumini msijali kwa kupingwa ufutaji wa hukumu za dini yenu, kwa sababu mambo yote yako chini ya uweza wake Mwenyezi Mungu, na Ndiye anayewachagulia lililo na maslahi kwa ajili yenu na wengineo; baada ya kuwambia haya, aliwaambia mwataka nini kutoka kwa Mtume wenu Muhammad (s.a.w.) na hali amewajia na dalili za kutosha? Mwataka kumdodosa kama walivyofanya Mayahudi kwa Musa kwa kumuuliza yasiyofaa kuulizwa? Mtu anaweza kuwa na shaka na akataka dalili ya kukinaisha kuondoa shaka yake. Ama kutaka jabali liwe dhahabu, hiyo itakuwa ni ukaidi na kiburi. Basi enyi waumini msiwe wakaidi wenye kutakabari.

Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, hakika amepotea njia iliyo sawa.

Kila mwenye kuwa na msimamo safi wa kutafuta dalili za kiakili kwa kutaka kuthibitisha haki, huyo ni muumini wa haki. Na kila mwenye kuwa na msimamo wa kiburi kudadisi na kutaka mambo yasiyoingia akilini basi huyo ni mpinzani wa haki. Na asiyetegemea aliyokuja nayo Muhammad

153

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

(s.a.w.) na kutaka zaidi, atakuwa amechagua inadi na kufuru juu ya imani.

Wengi miongoni wa watu wa kitabu wanatamani lau wangewarudisha nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nafsini mwao.

Kila mtu anapendelea watu wawe kwenye dini yake. Mwanafalsafa mmoja anasema: "Siku nzuri kwangu ni ile ninayomuona anayeniafiki yuko kwenye rai yangu." lakini Mayahudi walikuwa wakifanya juhudi kubwa ya kuwafitinisha Waislamu, kuwatoa kwenye dini yao ya Kiislamu na kuwarudisha kwenye dini yao ya kijahili ya kwanza, si kwa lolote bali ni kwa uhasidi. Ingawaje wao wanaweza kuwa Waislamu, kama walivyofanya wengine, lakini wao walihofia biashara zao na faida zao za pombe, kamari na uasherati.

Mayahudi walitaka kuwavunja Waislamu siku ya vita vya Uhud kwa kumlia njama Mtume. Imeelezwa kuwa baada ya tukio la Uhud walikuwa wakiwaita vijana wa Kiislamu majumbani mwao na kuwapatia pombe pamoja na kuwahadaa na mabinti zao, kama wanavyofanya leo na kila siku; kisha wanawatia shaka Waislamu kuhusu Qur'an na Utume wa Mtume mtukufu (s.a.w.).

Mtume alihisi mipango hii ya hatari akawakataza wasihudhurie kwenye vikao vya mambo ya upuuzi, akitilia mkazo kukataza zina, pombe, kamari na nyama ya nguruwe. Wakajizuilia Waislamu kwenda kwenye majumba ya Wayahudi waliyoyafungua kwa lengo lao hilo, ambayo hivi sasa yanajulikana kama Baa na Casino.

Baada ya kuwapambanukia haki.

Yaani Mayahudi walijaribu kuwarudisha Waislamu kwenye kufuru na upotevu pamoja na kujua Uislamu kuwa ndio dini ya haki na kwamba ushirikina na kuukana Utume wa Muhammad ni batili.

Haya si kwa Mayahudi tu, kwani wako watu wengi hukanusha haki na kuipinga sio kwa lolote isipokuwa ni kwa vile haiafikiani na tamaa zao. Kwa sababu ya kupelekwa na mapenzi na manufaa yake na wala sio kwa dini na akili. Amirul Mumini anasema: "Vita vya akili mara nyingi viko kwenye tamaa."

154

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Basi sameheni na muwache mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake.

Yaani achaneni nao hivi sasa wala msiwaingilie kuwatia adabu mpaka Mwenyezi Mungu awaamrishe hilo; kwani mambo yana wakati wake. Tafsiri nyingi zinasema kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwaamrisha Waislamu kuachana nao mpaka iliposhuka kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho..."

(9:29)

Na Aya nyenginezo za vita.

Razi amesema: "Imam Muhammad Baqir (a.s.) anasema: Hakika Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Mtume wake vita mpaka aliposhuka Jibril na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia."

(22:39)

KUIKHALIFU HAKI

Mambo yote ya maisha miongoni mwa kufuru, ulahidi, uovu, kuvunjwa heshima na ufisadi. Vile vile dhuluma, utaghuti, vita na ufukara, yote hayo yanasababishwa na kitu kimoja - kuihalifu haki. Lau watu wote, si kadhi peke yake, wangelichunga haki, wangeliishi wote kwa amani na raha. Kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Na nini kilicho baada ya haki isipokuwa upotevu?"

ni kuonyesha hakika hii.

(10:32)

155

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ni kweli kuwa haki haikosi watetezi wakati wowote ule, lakini ni wachache. Lau haki ingelipata watetezi kama ilivyo batili, basi ulimwengu wote ungelikuwa katika uzuri na amani. Bali lau kila mtu angeliitaka haki yake na akatekeleza wajibu wake, tusingeliona dhulma wala batili hata athari yake.

Mwenyezi Mungu ameisimamishia haki dalili za kuongoza kwenye hiyo haki. Hayo yanatolewa dalili na maumbile, kitabu chake Mwenyezi Mungu na kutokana na Mtume Mtukufu.Vile vile watu watakatifu wa nyumba ya Mtume aliowaweka sawa na Qur'an; kama ilivyoelezwa katika Hadith thaqalayn ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake. Mwenye kuipinga dalili hii hali anajua atakuwa amempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake; sawa na walivyofanya Mayahudi na washirikina.

110.Na simamisheni swala na toeni zaka, na heri yoyote mtakayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyafanya.

NA SIMAMISHENI SWALA

Aya 110

MAANA

Aya hii imekusanya mambo matatu:

1.    Kuamrisha kusimamisha swala

2.    Kuamrisha kutoa zaka

3.    Kuhimiza heri kwa ujumla

Katika Tafsir ya Al-Manar imeelezwa kwamba Aya ina madhumuni ya hukumu mahsusi ambayo ni kuamrisha swala na zaka. Kisha imetaja hukumu kwa ujumla ambayo iko peke yake, lakini ujumla wake unakusanya pia hukumu mahsusi iliyotangulia. Na huu ni katika mfumo wa Qur'an ambao ni wa aina yake.

156

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Mtaikuta mbele ya Mwenyezi Mungu Makusudio yake ni kukuta malipo yake na thawabu zake sio kukuta amali yenyewe, kama ilivyosemwa kwa sababu amali hazibaki.

Unaweza kuuliza: Tumeona Qur'an mara kwa mara inakutanisha amri ya swala na ya zaka; Je, kuna siri gani?

Limejibiwa swali hili kwamba swala ni ibada ya kiroho na zaka ni ibada ya kimali, mwenye kuitekeleza kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu inamuwia wepesi kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.

SWALA NA VIJANA WA KISASA

Vijana wengi wa kisasa wanapuuza dini na wanaoshikamana nayo; wengine wanasema wazi kuwa hakuna chochote zaidi ya hivi vitu vilivyoko." Wengine wanasema kuwa yuko mwenye kupanga mambo vizuri na mwenye hekima, lakini hakuwajibisha saumu wala swala. Aina zote hizo mbili za watu mbele ya Mwenyezi Mungu ziko sawa katika ukafiri. Kwa sababu mwenye kuacha swala kwa kuamini kuwa sio wajibu, huyo ni sawa na anayemkanusha Mwenyezi Mungu.

Na sisi wanavyuoni tunawaangalia vijana wa kisasa wakiendelea kupuuza dini na kuikataa haki, bila ya kufanya kazi yoyote au kuwakinaisha kwa namna yoyote ile.

Nikisema kazi, nakusudia kazi za ushirikano zenye kuleta matunda ambazo zinataka maadili na vikao vya kujadili namna ya utekelezaji kisha kufunguliwe shule na vyuo vya elimu ya Qur'an, Hadith, Falsafa ya Itikadi ya Kiislamu, Historia ya Kiislamu na elimu ya nafsi (Saikolojia).

Vile vile kuwe na mazoea ya kutoa mawaidha na ya kulingania kwenye dini kwa njia nzuri na ya kisasa. Ndio, wengine wamefanya juhudi zao zilizoleta natija ambazo zinafaa kutolewa shukurani. Lakini linalotakikana hasa ni kuzishirikisha pamoja juhudi hizo na kuwa na Ikhlasi katika nia na kujitolea mhanga katika yote. Lakini vipi zitashirikishwa pamoja juhudi na hali wenye kutaka kuchuma kwa jina la dini ni wengi ambao hawaoni umuhimu na haliwashughulishi lolote zaidi ya lile litakalowapatia jina na mali tu?

Kwa hiyo jukumu la kuwalea vijana ni letu sisi wanavyuoni wa dini, na tutaul-izwa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu; sawa na vile ambavyo wao nao watau-lizwa kutokana na kupuuza na kuacha kutafuta kujua dini ya haki na kutumia hukumu zake.

157

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

111.Na walisema: Hataingia peponi ila aliye Myahudi au Mnaswara (Mkristo). Hayo ni matamanio yao tu. Sema: Leteni dalili zenu kama nyinyi ni wasema kweli.

112.Si hivyo! Yeyote anayeuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake hali anatenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

113.Na Mayahudi walisema: Manaswara hawana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote na hali (wote) wanasoma Kitabu. Na hivi ndivyo wale wasiojua wasemavyo mfano wa kauli yao. Basi         Mwenyezi         Mungu

atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.

NA WALISEMA HATAINGIA PEPONI

Ayaya 111-113

LUGHA

Neno Hud linatokana na Haid lenye maana ya kutubia na kurudi kwenye haki. Na neno Naswara tumelifafanua katika kufasiri Aya ya 62.

158

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza MAANA

2 Sura Al-Baqarah

Na walisema: Hataingia peponi ila aliye Myahudi au Mnaswara (Mkristo).

Mwenye Majmau anasema: Hii ni kufupisha maneno: Kukadiria kwake ni kama kusema hivi: "Husema Myahudi: Hataingia peponi ila aliye Myahudi, na husema Mkristo: Hataingia peponi ila aliye Mkristo." Imekadiriwa hivi kwa sababu inajulikana kwamba Mayahudi hawakubali kuwa Wakristo wataingia peponi. Kwa hivyo tukafahamu kuwa yameunganishwa maneno kwa kufupiliza maneno bila ya kuharibu maana, kwani umashuhuri wa hali unatosha kuwa ni ubainifu.

ULANGUZI WA PEPO

Inadhihiri kutokana na Aya hii tukufu kwamba Mayahudi na Wakristo wanaamini nadharia ya ulanguzi tangu zamani na kwamba nadharia hiyo kwao inaingia pia kwenye neema za dunia na akhera.

Vile vile imedhihiri kwamba ulanguzi wa pepo unahusika na watu wa dini. Kwa misingi hiyo ndio likawa kanisa linauza cheki za msamaha kwa waasi na wenye dhambi kwa pesa. kanisa likachuma mali nyingi sana, lakini lilizidisha makosa na kueneza ufisadi. Miongoni mwa mambo yanayoandikwa kwenye cheki hiyo ya msamaha ni: "Unafungwa mlango ambao wataingia wenye makosa kwenye adhabu na mateso na unafunguliwa mlango wa kwenda kwenye pepo ya furaha; na hata ukiendelea kuishi muda mrefu neema hii itabaki bila ya kubadilika mpaka ifikie saa yako ya mwisho, kwa jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu."

Hayo ni matamanio yao tu.

Ni matamanio yao ambayo ni mengi sana. Miongoni mwayo ni kwamba Waislamu warudi kuwa makafiri na maadui zao waadhibiwe na kwamba pepo ni yao peke yao.

Sema: Leteni dalili zenu, kama nyinyi ni wasema kweli.

Madai yote huhitaji dalili na vile vile kila dalili ya kinadharia inahitaji dalili mpaka iishie kwenye asili yenye kuthibitika kimsingi. Maana ya kuthibiti kwake ni kuafikiana wote wenye akili kuhusu usahihi wake wala visipingane vitu viwili; kama ilivyo asili hii "Kila madai yanahitaji dalili" isipokuwa ikiwa madai yenyewe ni ya kimsingi, kwani mwenye kudai madai ya kimsingi yaliyo wazi hayawezi kuitwa madai; kwa sababu

159

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

madai huhitaji dalili; na madai ya kimsingi yanakuwa pamoja na dalili yake haiepukani nayo. Kwa hivyo huwezi kumuuliza dalili mwenye kusema: "Kumi ni zaidi ya moja."

Katika Tafsir Al-Manar anasema katika kutaja Aya hii kwamba wahenga wa Kiislamu walio wema walikuwa na asili hii ya kuonyesha dalili juu ya wanayosema na wakitaka dalili kwa watu kwa wanayoyadai. Lakini waliokuja baadaye walio waovu - kama asemavyo mwenye Al-Manar -wameifanya kinyume Aya; wamewajibisha kufuata tu na kuharamisha dalili ila kufanya kwa kufuata tu. Wamezuia kufanya amali kwa kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakawajibisha kufanya amali kwa kauli ya fulani.

Si hivyo! Yeyote anayeuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake hali anatenda mema basi ana malipo yake kwa Mola wake.

Hii ni kuyakomesha madai kwamba pepo ni yao peke yao. Maana ni kuwa kila anayemwamini Mwenyezi Mungu kwa kumsafia nia katika amali zake bila ya kuichanganya na shirk; wala ria, basi yeye ni katika wenye kutukuzwa kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye hapotezi malipo ya mwenye kutenda wema. Ama kauli yake na hali anatenda mema, ni ishara kwamba. Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kunatokana na amali njema sio mbaya, kwa sababu Mwenyezi Mungu hatiiwi pale anapoasiwa.

Na Mayahudi walisema: Manaswara hawana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote.

Mwenye Majmaul-Bayan amesema akimnukuu Ibn Abbas kwamba Wakristo wa Kinajran walibishana na Mayahudi mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) Myahudi mmoja akasema: "Hamna chochote nyinyi." Akajibiwa na Mkristo: "Mayahudi hawana chochote," ndipo ikashuka Aya hii ikisajili kauli ya vikundi vyote viwili.

DINI YA MASLAHI KWA MAYAHUDI NA WAKRISTO

Ni maarufu kwamba Wakristo wanaeleza kwa uwazi kwamba Mayahudi na kizazi chao ndio waliohusishwa na kumsulubu Yesu. Pamoja na hayo yote Baba mtakatifu wa Roma alifanya juhudi za kufa na kupona mnamo mwaka 1965 za kuwatakasa Mayahudi wa sasa na wa kizazi kijacho. Ikabidi kugongana na kanisa la Mashariki. Na gharama za mkutano zilifikia dola milioni ishirini.

160

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Lengo la kwanza na la mwisho la mkutano huo ni siasa tu ya kuipa nguvu dola ya Israil na kuyapa nguvu makao yake katika Palestina na siasa yake ulimwenguni. Kwa usahihi zaidi ni kuupa nguvu ukoloni na kuweka nguvu zake katika mashariki kwa ujumla na hasa katika miji ya kiarabu. Hii inafahamisha kwamba dini kwa baadhi yao ni manufaa ya kimaada.27

Na hali wote wanasoma Kitabu

Yaani Mayahudi wana Tawrat ambayo inaelezea habari njema za kuja Isa na kukubali Utume wake. Vile vile Wakristo wana Injil inayomtambua Musa na Tawrat yake. Kwa hivyo Mayahudi na Wakristo wako katika hukumu ya taifa moja, kwa sababu dini yao ni moja na kati ya Tawrat na Injil, ni fungu la kuitimiza nyingine. Lakini pamoja na hayo wamekufurishana.

WAISLAMU VILEVILE WANAKUFUISHANA

Ikiwa Mayahudi na Wakristo wako katika hukumu ya taifa moja, kwa sababu tu Tawrat inamtambua Isa na Injil inatambua Musa, basi bora zaidi ni Sunni na Shia wawe taifa moja kwa uhakika kabisa. Kwa sababu kitabu chao ni kimoja ambacho ni Qur'an moja wala sio viwili, na Mtume wao ni mmoja ambaye ni Muhammad sio Muhammad wawili. Sasa imekuwaje wengine wawakufurishe ndugu zao katika dini?

Na Mayahudi walisema: Manaswara ha-wana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote na hali wote wanasoma kitabu.

Lau tukiangalia maana tuliyoyabainisha ya Aya hii na wafasiri wote wakaafikiana; kisha tukaikisia na Mwislamu anayemkufurisha ndugu yake Mwislamu, basi hali ingelikuwa mbaya zaidi ya mara elfu kuliko Mayahudi na Wakristo.

Mayahudi waliwakufurisha Wakristo na Wakristo wakawakufurisha Mayahudi. Na hali wote wanasoma kitabu. Yaani Tawrat na Injil. Sasa itakuaje Mwislamu amkufurishe ndugu yake Mwislamu na hali naye anasoma Qur'an? Basi na wamwogope Mwenyezi Mungu wale wanaopinda ndimi zao kwa kusoma kitabu na nyoyo zao hazijui maana yake na makusudio yake.

Angalia kifungu cha "Masilahi ndio sababu " katika tafsir ya Aya 96 ya Sura hii.

161

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Na hivi ndivyo wale wasiojua wasemavyo mfano wa kauli yao.

Makusudio ya wasiojua katika Aya hii ni makafiri wa kiarabu kutokana na vile wali-vyosema, sawa na Mayahudi na Wakristo kwamba wao peke yao ndio watakaoingia peponi. Qur'an imewajibu, kwanza, kwamba haki haifungamani na watu fulani tu wala na majina, isipokuwa kuingia peponi kunatokana na imani njema.

Pili, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamjua mwenye haki na mwenye batil na yeye atamlipa kila mmoja kwa amali yake. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyohitalifiana.

KILA MMOJA AVUTIA KWAKE

Unaweza kuuliza kila watu wa dini na vikundi wanadai kuwa wao wako kwenye haki na wenzao wako kwenye batili; kama walivyodai Mayahudi, Wakristo na washirikina wa kiarabu. Sasa je, vipi tutamjua mwongo na mkweli?

Kabla ya kujibu, kwanza tunaanza kuelezea hakika hii: Kila mwenye kudai haki hana budi kuwa na moja ya mambo mawili: Ama kukubaliana kabisa na rai yake tangu mwanzo na kuendelea nayo na wala asione uwezekano wa makosa wala asifuate vingine vyovyote itakavyokuwa. Au awe anaitafuta haki kwa juhudi zake mpaka aone dalili ya kuitegemea kwa kuazimia kwamba akibainikiwa na haki kwa upande mwingine aifuate na kugeuza rai yake. Kwa sababu yeye anaitafuta haki popote na wakati wowote ilipo na itakavyokuwa.

Hapana budi kuwatofautisha wawili hawa. Wa kwanza hakuna njia ya kumkinaisha kwa hoja na mantiki ya kiakili, bali hana dawa isipokuwa kuachana naye.

Wa pili inakua wepesi kufahamiana naye. Kila mmoja wetu anajua kuwa kuna mambo ambayo yako wazi. Mfano, maisha mazuri ni raha, na ufukara ni balaa na mashaka, mapenzi ni bora kuliko kugombana, usalama ni wenye manufaa kuliko vita, elimu ni nuru na ujinga ni giza, uadilifu ndio haki na dhulma ni batili na kwamba kitu kimoja hakiwezi kuwa pamoja na kinyume chake, n.k.

Tukianza kuangalia hayo na kuyajua, kisha mtu akadai kwamba yeye ni mwenye haki kinyume cha mwingine tutampima na kumhukumu kwa hakika hizo, zikiafikiana naye atakuwa ni mkweli, vinginevyo atakuwa mwongo.

162

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa hivyo basi inatubainikia kwamba kauli ya mwenye kusema:"Kila mmoja anavutia dini yake nitatambua vipi iliyo sahihi?", ni ya hatari na duni yenye shabaha ya kueneza vurugu na ujinga. Lau ingekuwa ni kweli ingelipasa sehemu za kuabudu na vituo vifungwe, jambo ambalo halina msimamo wa kiakili wala kikanuni au kitabia.

La upuuzi zaidi ni kwamba kauli hiyo (nitajuaje ukweli) ni maneno ya kishairi yaliyokuja kutokana na mawazo yasiyo-kuwa na mantiki yoyote. Mwenyezi Mungu amesema kweli aliposema:

"Na washairi wanafuatwa na wapotofu. Je huoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? Na kwamba wao wanasema wasiyoyatenda?"

(26:224-226)

114.Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa humo jina lake na akajitahidi kuiharibu? Hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa; wana fedheha katika dunia na katika akhera wana adhabu kubwa.

KUZUIA MISIKITI YA MWENYEZI MUNGU

Aya ya 114:

MAELEZO

Aya hii ni katika Aya ambazo kauli za kuifasiri zimekuwa nyingi. Dhahiri yake inafahamisha makemeo na kiaga kwa asiyeiheshimu misikiti au sehemu yoyote ya kufanyia ibada na kuzuia kujengwa au kufanyiwa ibada ndani yake. Vile vile kuivunja au kuipuuza. Na kwamba wajibu wa kimungu na wa kibinadamu unafaradhishia kila mtu kuzitakasa sehemu

163

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

za kufanyia ibada na kuziingia kwa heshima na unyenyekevu, na hali ya kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu na kutaraji thawabu zake, sio kuzivunjia heshima na kuzidharau. Kwa sababu ziliwekwa kwa lengo la ibada.

Kisha Mwenyezi Mungu amebainisha kwamba mwenye kuziingilia sehemu za ibada kwa nia mbaya atamdhalilisha katika maisha ya dunia na kesho atamwadhibu adhabu kubwa.

Kwa ufupi Aya inabainisha kwamba mwenye kufanya jambo kadha atafanyiwa kadha. Na hilo ni suala la kijumla sio lililopita wala la wakati wa kushuka Aya au kungoja kutokea.

Lakini wafasiri wamesema kuwa ni suala maalum; kisha wakahitalifiana kwamba je suala lenyewe lilitokea kabla ya Utume wa Muhammad (s.a.w.) au baada yake?

Wale waliosema kuwa lilitokea kabla nao pia wamehitalifiana katika kulielezea tukio lenyewe. Kuna baadhi yao waliosema kwamba Aya inaelezea tukio la Titus wa Roma alipoingia Baytul-Maqdis baada ya kufa Masih kwa kiasi cha miaka sabini; akaiharibu kiasi ambacho halikubaki jiwe juu ya jiwe jengine; akavunja hekalu la Suleiman na akachoma baadhi ya nakala za Tawrat. Na Masih alikuwa amewehadharisha Mayahudi kuhusu hilo. Inasemekana kwamba Titus aliiharibu Baytul Maqdis, kwa kuhimizwa na Mayahudi ili awatese Wakristo.

Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Aya inaelezea matukio yaliyopita kuna wanaosema kwamba inaelezea yale aliyofanya Nebukadnezzar katika kuiharibu Baitul Maqdis.

Katika Tafsir Al-Manar anasema ninamnukuu: "Jambo la ku-shangaza ni kwamba Ibn Jarir amesema katika Tafsir yake kwamba Aya inaonyesha kuungana Wakristo pamoja na Nebukadnezzar wa Babilon kuiharibu Baitul Maqdis, ambapo tukio la Nebukadnezzar lilikuwa kabla ya kuja Masih na Ukristo kwa miaka mia sita na thalathini na tatu (633)".

28

Vile vile kuna wengine wanaosema kuwa Aya inatoa habari ya jambo lililokwisha tokea, kwamba imeshuka kwa ajili ya washirikina wa

ilitokea sadfa siku niliyosoma kosa hili la Tabariy, nikasoma makala ndefu katika gazeti la Al-jumhuriya la Misr la tarehe 5 May 1967, inayosema "...Tabariy bila shaka ni nguzo ya wanahistoria wa Kiislamu na kitabu chake ndio kiongozi cha tafsir...."

Tabari alikufa mwaka 310 AH yaani karibu miaka 1050 iliyopita. Ikiwa hali ya wanahistoria waliotangulia na wanaotegemewa ni hii, je, ategemewe nani?

164

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kiquraish waliomzuia Mtume na sahaba zake kuingia Makka katika kisa cha Hudaybiya.

Ama wale wanaosema kuwa Aya inatolea habari jambo linalongojewa kutokea, pia nao wamehitilafiana. Kuna wale waliosema kwamba Aya inaonyesha uvamizi wa Wakristo juu ya Baitul-Maqdis na miji mingine katika miji ya Waislamu. Wengine wanasema kuwa inatolea habari tukio la Wakaramet (Karmathians) la kuivunja Al-Ka'aba na kuwazuia watu kuhiji. Kisha kundi linalosema hivi likasema: "Hii ni katika miujiza ya Qur'an, kwa sababu ilitolea habari mambo yatakayotokea."

Hayo ndiyo kwa ufupi waliyoyasema wafasiri. Na sisi hatutegemei chochote katika kauli hiyo; kwani hakuna dalili ya kiakili au kauli itakayoweza kuituliza akili. Sisi tunategemea dhahiri ya Aya ambayo haipingani na akili wala hakuna kauli ya Hadith inayoeleza jengine. Dhahiri hiyo ni: Wajibu wa kuheshimu sehemu za kuabudu na kuharamisha kuziingilia na kwamba mwenye kukusudia uovu, atapata malipo yake.

HUKUMU ZA MISIKITI

Ni Sunna kujenga misikiti, kuiamirisha kwa sababu ya kutajwa Mwenyezi Mungu, kui-safisha na kuing'arisha, Ni haramu kuivunja, kuingia mwenye janaba na mwenye hedhi.

Ni Suna kuswali raka mbili za kuuamkia (kuusalimia) wakati wa kuingia. Ni makuruhu kujenga mahali palipo juu; kwa sababu Ali (a.s.) aliuona msikiti katika mahali palipo juu akasema: "Kama Sinagogi" yaani Hekalu la Kiyahudi. Kuna hadith inayosema: "Nyumba hujengwa mahali palipo juu na msikiti hujengwa mahali tambarare." Vile vile ni makruhu kutengeneza mihrabu ndani yake; kwa sababu Amiril-Muminin alipokuwa akiiona husema: "Kama kwamba ni madha-bahu ya Mayahudi." Makusudio ya ya Mihrabu hii iliyo makuruhu, ni ile inayotokeza ndani ambayo huwadhikisha wenye kuswali, bali jamaa wamesema kuwa ni haramu. Ama mihrabu inayojitokeza nje haina ubaya wowote.

29

115.Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahala

Amenakili mwenye Miftahul-Karama kutokana na wanachuoni umakaruhu wa kuiinua misikiti na wamesema, bali hujengwa kwa wastani; kama ambavyo imenukuliwa kutoka vitabu saba vya kifiqhi umakaruhu wa mihrabu yenye kutokeza. Mimi ninadhani kwamba Waislamu wanavyojihimu kujenga misikiti mikubwa ni kwa ajili ya kushindana na makanisa tu na kauli ya Amirul Miminin (kama sinagogi) inaashiria hilo

165

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

116.Na wanasema: Mwenyezi .>i Mungu amejifanyia mtoto. Ameepukana na hilo. Bali ni ^J vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamtii Yeye.

117.Mbunifu wa mbingu na ardhi; na anapotaka jambo basi huliambia tu kuwa, likawa.

NA MASHARIKI NA MAGHARIBI NI ZA MWENYEZI MUNGU

Aya ya 115-117.

LUGHA

Mashariki ni mawiyo ya jua na mwezi, na Magharibi ni machweo. Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja Mashariki na Magharibi tu bila ya Kusini na Kaskazini kwa sababu zinaingia sehemu zote, maana hakuna mahali kusiko chimbukiwa na jua na mwezi au kuchwea na jua. Kwa hiyo mgawanyo wa ardhi ni Mashariki na Magharibi tu.

MAANA

Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahali popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu.

Yaani ardhi na pande zote na vitu vyote ni vya Mwenyezi Mungu. Popote mtakapo-abudu na popote mtakapoelekea kwa kukusudia ibada na radhi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawatakabalia. Basi mwenye kuzuiliwa kufanya ibada ndani ya msikiti, na aabudu popote anapopata

166

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

na popote atakapoelekea, kwani ardhi yote ni msikiti na pande zote ni Qibla.

Mfasiri mmoja amesema kwamba Aya inahusika na upande tu, na sio mahali, yaani ni upande wowote tu, na wala sio mahali popote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema. "Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu". Lakini mfasiri huyu amesahau kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (na) Mwenye kujua" kwamba maadamu pande zote na sehemu zote ni za Mwenyezi Mungu, basi inasihi kumwabudu katika mahali popote na kuelekea pande zote kwa kuangalia kuwa kuenea kwa sababu ya kuhukumu ndio kuenea hukumu kwa kufuata sababu na kilichosababisha. Kwa maneno mengine ni kuwa, maadamu pande zote na mahali pote ni pa Mwenyezi Mungu, basi inasihi kuabudu popote na kuelekea upande wowote.

Unaweza kuuliza, hakika dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba Mukallaf ana hiyari katika swala yake kuelekea upande wowote, wala hana lazima ya kuelekea Al-Ka'aba, jambo hilo ni kinyume na Waislamu wote?

Jibu: Ni kweli kuwa dhahiri Aya inafahamisha hivyo na inakusanya swala ya faradhi na sunna katika hali zote, lakini imethibiti kutoka kwa Mtume, Maimamu na kwa Ijmai kwamba swala ya faradhi haiswihi kama mtu akielekea pengine ikiwa anaweza kuelekea Al-Ka'aba na swala ya sunna inasihi kwa kuelekea popote katika hali ya kupanda kwenye chombo cha kusafiria na katika hali ya kutembea kwa miguu. Vile vile inaswihi kuswali swala ya faradhi kwa kuelekea upande wowote kwa yule aliyeshindwa kujua Qibla.

Kwa hadith hizi na Ijmai tunaihusisha kauli yake Mwenyezi Mungu: "Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mungu", na swala ya sunna katika hali ya kwenda na kupanda na swala ya faradhi kwa mwenye kuchanganyikiwa. Vile vile kutokana na hadith na Ijmai tunaihusisha Aya 149 ya Sura hii inayosema: "Na popote wendako geuza uso wako kwenye msikiti mtakatifu (Masjidul-Haram)", na swala ya faradhi katika hali ya hiyari; na tunaihusisha na swala ya sunna katika hali ya kutopanda chombo cha kusafiria.

30

Kwa hali hii linabainika kosa na kuchanganyikiwa katika kauli ya mwenye kusema kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: "Geuza uso wako kwenye

Tazama tafsiri ya Aya inayofuatia 142 inayotimiza tafsiri hii katika kifungu cha kwa nini swala iswaliwe kwenye upande maalum.

167

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

msikiti mtakatifu", imefuta hukumu ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu". Kwa sababu sharti za kufuta ni kukanusha na kupingana kati ya yenye kufuta na yenye kufutwa; ambapo hali ya kuthibitisha na kukanusha inakuja katika maudhui moja.

Umeshajua kwamba maudhui 'elekeza uso wako kwenye msikiti mtakatifu', yanahusika na swala ya faradhi na sunna katika hali ya kutulia. Na maudhui ya 'popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu', yanahusika na isivyokuwa hivyo.

Na wanasema: "Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto"

Tumetangulia kueleza katika tafsiri ya Aya ya 113 kwamba Mayahudi, Wakristo na washirikina, kila kundi lilisema kwamba liko kwenye haki na wengine si chochote. Kwa hivyo dhamiri katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na wanasema" inarudia kwenye makundi haya matatu. Imeelezwa katika Qur'an kwamba Mayahudi wanasema: "Uzayr ni mtoto wa Mungu" Na Wakristo wanasema: "Masih ni mtoto wa Mungu" na Washirikina wa kiarabu walisema; "Malaika ni watoto wa Mungu." Kwa hiyo sio kosa kuwa wanazungumziwa wote.

Ameepukana na hilo.

Ni tamko la kutakasa. Katika Aya nyengine ni:

"...Ameepukana kuwa na mtoto..."

(4:171).

Kwa sababu kupatikana mtoto kwa Mwenyezi (s.w.t.). Kutalazimisha mambo mengi ya kujihadhari kama ifuatavyo:-

Kwamba ambaye huzaliwa hana budi kuwa katika jinsi ya huyo aliyemzaa ili aweze kuzaa; na Mwenyezi Mungu hana jinsi.

Kuzaa kunalazimisha udugu, na udugu unahitaji kuwa na mwili; na Mungu sio mwili.

Sababu inayowajibisha kuzaa ni kumuhitajia mtoto; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha na viumbe vyote.

168

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Ambaye anazaa hana budi kuwa amezaliwa; na Mwenyezi Mungu hakuzaliwa.

Amirul Muminin (a.s.) amesema: "Hak-uzaliwa akawa na mshirika katika utukufu", Yaani kushirikiana na baba yake katika utukufu. "Wala hakuzaa akawa mwenye kurithiwa kwa kufa". Yaani kuwa na mtoto atakayemrithi baada ya kufa. "Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo kabisa."

Jambo jengine ni kuwa kila kilicho katika mbingu na katika ardhi ni chenye kuu-mbwa na kumilikiwa na Mwenyezi Mungu; na chenye kumilikiwa hakiwezi kuwa mtoto wa Muumbaji. Wala Muum-baji hawezi kuwa ni baba wa mwenye kuumbwa mwenye kumilikiwa.

Kwa hali hiyo inatudhihirikia njia ya kutoa dalili juu ya kukanusha Mungu kuwa na mtoto katika kauli yake.

Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamtii Yeye.

Yaani vinamfuata Yeye na kumtii.

Unaweza kuuliza kwamba herufi 'Ma' hutumiwa kwa kisicho na akili na neno qaanituuna hutumiwa kwa aliye na akili.

Sasa imekuaje kitu kimoja mara nyingine kuwa katika ibara ya kisicho na akili na mara nyingine kuwa katika ibara ya kilicho na akili?

Jibu: Mbingu na ardhi inakusanya kuwa na akili na kutokuwa na akili; na, Aya imekusanya jumla mbili; ya kwanza imethibitisha ufalme wa vilivyokusanywa na mbingu na ardhi, na jumla ya pili imethibitisha kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wakati Mwenyezi Mungu alipotaka kuelezea kumiliki, alielezea kwa kisichokuwa na akili, na alipotaka kuelezea twaa ameelezea kwa aliye na akili, kwa sababu twaa huwa ni kwa mwenye akili na mwenye hiyari.

MBUNIFU WA MBINGU NA ARDHI

Neno Badiu (Mbunifu) lina maana ya mtengenezaji ambaye amtengeneza yeye mwenyewe bila ya kuchukuwa kwa mwengine ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu:

'Na utawa wameubuni."

(57:27)

169

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa hivyo maana yanakuwa: Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye mwanzilishi wa mbingu na ardhi, basi vipi anaweza kunasibishwa aliyemo ndani yake kuwa ni mwanawe?

Na anapotaka jambo, basi, huliambia tu: Kuwa, likawa.

Hili ni fumbo la ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uweza wake; kwamba Yeye kwa kutaka tu, basi jambo huwa, ni sawa kuwe hakuna kitu chochote halafu kipatikane kwa kutaka kwake; au kuwe na kitu, lakini akataka kukigeuza.

Tumeeleza katika kufasiri Aya ya 26-27 kwamba Mwenyezi Mungu ana matakwa aina mbili: Matakwa ya utengenezaji na matakwa ya kutoa sharia. Miongoni mwa matakwa ya utengenezaji ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

ill

"Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliyemuumba kwa udongo kisha akamwambia "kuwa, akawa".

118.Na walisema wale wasiojua: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au kutufikia ishara (tunazozitaka) Hivyo hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao (hii). Nyoyo zao zimefanana. Hakika sisi tumezibainisha ishara kwa watu wenye kuyakinisha.

119.Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji, wala hutaulizwa kuhusu watu wa motoni.

(3:59)

12O.Hawatakuwa radhi nawe

170

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu (hasa), na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokufikia, basi hutapata mlinzi yoyote wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.

2 Sura Al-Baqarah

MBONA MWENYEZI MUNGU HUSEMI NASI

Aya ya 118-120

MAANA

Na walisema wale wasiojua; mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au kutufikia ishara (tunazozitaka).

Wale wenye inadi walimwambia Mtume (s.a.w.): "Hatutakuamini mpaka Mungu atwambie ana kwa ana kwamba wewe ni Mtume; au atuletee malaika atakayetufahamisha hilo au atakayeleta hoja tunazozitaka sisi; kama vile alivyowazungumzia Mwenyezi Mungu aliposema:

Na walisema: Hatuwezi kukuamini mpaka utububujishie chemchemi katika ardhi... au upande mbinguni na hatutaamini kupanda kwako mbinguni mpaka ututeremshie kitabu tukisome..."

(17:90,93)

Mwenyezi Mungu amewajibu hilo kwa kauli yake:

Hivyo hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao (hii). Nyoyo zao zimefanana. Hakika sisi tumezibainisha ishara kwa watu wenye kuyakinisha. Yaani kung'ang'ania huku kwa mawazo ya ubatilifu hakuhusiki na waliyoyatoa kwa Mtume (s.a.w.) tu, kwani watu wa Nabii Musa walimwambia:

171

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"...Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi..."

(4:153)

Kwa hoja na dalili ambazo hazileti shaka katika nafsi isiyokuwa na shaka na wasiwasi, na kusafika kwa haki kwa njia ya haki. Mwenyezi Mungu amelifanya hilo na akabainisha dalili zenye kutosheleza juu ya Utume wa Muhammad. Ama kutaka zaidi ni kujitia mashaka na kutaka makubwa.

Kimsingi ni kwamba mpinzani mwenye inadi, haipasi kumjibu bali hupuuzwa na kuachiliwa mbali. Na watu wenye yakini ndio ambao wanatafuta yakini kwa njia yake.

CHENYE KUTOLEWA DALILI NA AINA YA DALILI

Tumetangulia kueleza katika kufasiri Aya ya 111: ("...Sema: Leteni dalili zenu, kama nyinyi ni wasema kweli") Kwamba kila dai linahitaji dalili na dalili inahitaji dalili mpaka iishie kwenye asili iliyo wazi ambayo haipingani. Katika kifungu hiki, tutazungumza aina hiyo ya dalili.

Dalili inatofautiana kwa kutofautiana tabia ya kitu. Kwa mfano tukitaka kujua vitu ambavyo vinatengeneza kitu katika vitu vya maumbile tutategemea majaribio na mtaalamu mtafiti. Tukitaka kuthibitisha kuwapo kwa mwenye kupanga mambo mwenye hekima, tutarudia akili.

Tukitaka kujua hukumu yoyote katika hukumu za sharia tutarudia Qur'an na Hadith. Kama tukitaka kujua lugha ya Kiarabu na matamko yake ni lazima kuwarudia wajuzi na istihali za Waarabu wa mwanzo:

Ikiwa kuna masuala ya kikanuni tutarudia kanuni au masuala ya kihistoria tuatawarudia wanaakiolojia na wapokezi wenye kutegemewa.

Hivyo ndivyo zinavyotofautiana dalili kutokana na yanayotakiwa kuthibitisha. Kwa hivyo haifai kwa yeyote, vyovyote alivyo kutoa maoni yake kwa namna ya dalili anayoitaka au kutaka uthibitisho zaidi baada ya kukamilika dalili zote zinazowajibisha yakini na kukinaisha.

Kwa hivyo dalili ya kutosha ikipatikana kisha mwingine akatoa maoni ya dalili nyingine au zaidi, basi huyo ni mwenye inadi na mwenye kutaka makubwa.

Mtume Muhammad (s.a.w.) amewashinda wenye shaka na wapinzani kwa Qur'an; kukathibiti kushindwa kwao na hoja ikatimu. Basi

172

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wanapotaka zaidi baada ya kushindwa huko kwenye kufedhehesha, itakuwa matakwa yao hayo ni inadi. Kwani lau kama kusudio lao ni haki, kama ilivyo, basi wangelikinai na wengeliikiri baada ya kuwadhihirikia kwa sura ya ukamilifu iliyo wazi.

Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji, wala hutaulizwa juu ya watu wa motoni.

Hiki ni kiwango cha kazi ya Mtume na jukumu lake na kwamba yeye ni mwalimu sio mtenza nguvu, na ni mwenye kubainisha haki sio mlazimishaji. Aya hii ni kama Aya inayosema:

"Na sema: 'Ni ukweli uliotoka kwa Mola wako, anayetaka na aamini na anayetaka na akufuru..."

basi

(18:29)

Aya hiyo ni kumuondolea uzito Mtume (s.a.w.) asipatwe na jaka moyo kwa sababu ya kufuru ya mwenye inadi na ya mwenye kufanya upinzani.

Hawatakuwa radhi nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila yao.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Mayahudi na Wakristo walimwomba Muhammad (s.a.w.) kupatana nao kwa muda kisha watamfuata wamwamini. Ndipo Mwenyezi Mungu akamkatisha tamaa. Hii inafahamisha kuwa haifai kuwaridhisha Mayahudi na Wakristo kwa hali yoyote iwayo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameambatanisha kuwaridhisha na kuwa Myahudi au Mkristo. Ikiwa haliwezekani hilo, basi haiwezekani kuwaridhisha.

Kwa hakika ni kwamba dini zote na vikundi vyote ni hivyo wala sio Mayahudi na Wakristo tu; bali baadhi ya watu hawawi radhi nawe mpaka uwe mtumwa kwao. Qur'an inapinga hali hii ya kuchukiza na ikatoa mwito kuishi kidini pamoja na dini zote, kuwatukuza Mitume wote na kuwataja kwa heri, na ikawajibisha kuamini Utume wao. Haya ndiyo yenye nguvu zaidi katika kuleta udugu kati ya watu wa dini na kusaidiana.

Mwenyezi Mungu amewahusisha kuwataja Mayahudi na Wakristo ili Mtume akate tamaa nao kuwa watamfuata kama alivyosema mwenye Majmaul-Bayan.

173

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu (hasa).

Tumetangulia kueleza katika tafsir ya Aya 26, kwamba neno Huda (uongofu) lina maana nyingi; kama vile kubainisha haki, kuwafikisha kwenye uongofu, thawabu na mengineyo. Hapa lina maana ya Uislamu ambao Mwenyezi Mungu amempelekea Mtume wake Muhammad (s.a.w.); usiokuwa huo ni upotevu sio uongofu. Maana yake ni, sema ewe Muhammad, niliyonayo mimi ndiyo haki na mliyo nayo nyinyi ni upotevu na batili, vipi niache, niifuate upotevu?

MAADUI WA DINI NA MSINGI WAKE

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemfahamisha Mtume wake mtukufu kwamba Wayahudi na Wakristo hawatamridhia mpaka afuate mila yao; pamoja na kujua kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) isma ya Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kwamba yeye hatafuata mapenzi yao kwa hali yoyote. Lakini amempa tahadhari hii:

Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokufikia, basi hutapata mlinzi yoyote wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.

Wafasiri wametaja kufaa hali mbili kutokana na tahadhari na katazo:

Kwanza, kwamba maasi yanawezekana kutokea kwa Mtume lakini anajizuia; yaani yeye anaacha maasi pamoja na kuwa anaweza kufanya; vinginevyo ingekuwa hakuna ubora wowote katika kuyaacha, na ndio yakaja makatazo na hadhari kwenye lile linalowezekana kufanyika bila ya kuangalia isma.

Pili, kwamba kwa dhahiri msemo unaelekezwa kwa Mtume, lakini ni kwa watu wote.

Mimi nimefikiria hali ya tatu, kwamba huenda Mtume ilimpitia kuwa Mayahudi watasogea na kuongoka au wamsaidie katika mambo ambayo yataleta heri au yatakayopunguza ugoigoi wao na kuzuia baadhi ya shari zao; ndipo akabainisha Mwenyezi Mungu kwamba maadui wa dini na msingi wake hawawezi kuridhia chochote kwao isipokuwa uache haki uliyo nayo na ufuate upotovu walio nao; kisha akamkataza kupatana nao na kukurubiana. Kwa sababu hilo litawasaidia na kuwapa nguvu; na kutia nguvu huko ni haramu kwako ewe Muhammad na mwingine kama ilivyo haramu kufuata dini yao.

174

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Zaidi ya hayo ni kwamba Mayahudi wana maumbile ya shari na ufisadi, kupinga haki na watu wake na kumfanyia uovu mwenye kufanyia wema; wala halifai kwao jaribio lolote la amani.

Jawabu bora ni kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kumwamuru na kumkataza masum; kama anavyoweza kumwamuru asiyekuwa masum kwa kuangalia utukufu wake na ukubwa wake.

Kisha makatazo haya na hadhari hii inawavunja wale wanaowabembeleza maadui wa dini wanaotoa udhuru kuwa wanafanya hivyo kwa masilahi ya Waislamu. Kwa sababu adui wa dini na wa nchi, hataki usalama wowote isipokuwa kwa biashara ambayo yeye daima atakuwa ndiye mwenye faida; na nembo yake pekee ni 'chukua wala usitoe, ukiweza chukua zaidi ya unavyotoa',

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amebainisha hakika hii ya wafanyi biashara hawa kwa ufasaha na uwazi aliposema:

"Na utawaona wana pupia zaidi maisha kuliko watu wengine na kuliko wale walioshirikisha"

121.Wale tuliowapa Kitabu wakakisoma kama inavyostahiki kukisoma,            hao            ndio

wanaokiamini.                         Na

wanaokikanusha, basi hao ndio wenye hasara.

(2:96)

122.Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema                                yangu

niliyowaneemesha na hakika îp nimewafadhilisha kuliko viumbe wengine.

123.Na ogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine,

175

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo; wala maombezi (shufaa) hayatafaa, wala hawatanusuriwa.

WAKAKISOMA KAMA INAVYOSTAHIKI

Ayaya 121-123

MAELEZO

Wale tuliowapa Kitabu wakakisoma kama inavyostahiki kukisoma, hao ndio wanaokiamini.

Baada ya Mwenyezi Mungu kumbainishia Mtume wake, Muhammad (s.a.w.) kwamba Wakristo na Mayahudi hawamwamini, bali hawatamridhia mpaka afuate mila yao, sasa anawavua wale wema wanaoichunga haki katika wao; wale ambao wamesilimu na wakamwamini Muhammad (s.a.w.) na akawaeleza kuwa ni wale ambao wanakisoma kitabu inavyostahiki.

Makusudio ya Kitabu ni kila kitabu alichokiteremsha Mwenyezi Mungu, kiwe ni Qur'an, Tawrat au Injil, kama vilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu. Kuacha kukihusisha kitabu maalum katika maelezo yake Mwenyezi Mungu ni dalili ya kuwa ni vitabu vyote alivyoviteremsha.

Maana ya kukisoma inavyostahiki, ni kuzingatia vizuri maana yake na kufuata amri na makatazo yake; sio kusoma vizuri, kudhibiti matamko, na kuzitoa herufi sawa sawa (tajwidi tu). Kwani hilo si chochote ikiwa hakuna kuzingatia vizuri na kuongoka. Kuna Hadith tukufu inayosema: "Hakuiamini Qur'an mwenye kuhalalisha yaliyoharamishwa."

Jumla ya maneno ni kwamba Tawrat na Injil vyote vimebashiri Utume wa Muhammad (s.a.w.); kama ambavyo Qur'an imefahamisha ukweli wake. Ndio maana wengi walisilimu miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara na Washrikina ambao walizingatia vizuri Aya na wakaifuata haki kama ilivyo.

Na wanaokikanusha, basi hao ndio wenye hasara.

Yaani mwenye kukanusha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ambayo yanalazimisha kumkanusha Muhammad (s.a.w.), huyo ni katika wenye

176

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kuhasirika, kwa sababu ni sawa na mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu. Ni wazi kwamba hapana hasara kubwa zaidi kuliko hasara ya akhera na neema yake yenye kubaki.

Enyi wana wa Israili! Kumbukeni neema Yangu niliyowaneemesha na hakika nimewafadhilisha kuliko viumbe wengine.

Tafsir ya Aya hii imeshatangulia katika Aya 40. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekariri kuwakumbusha Mayahudi neema yake katika Aya nyingi kwa lengo la kuwatahayariza kwa namna ya ufasaha zaidi na hekima; kama alivyotumia katika kauli yake: "Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine" ambayo pia tafsir yake imepita katika Aya 48.

MUJTAHIDI NA MUQALLID

Sheikh Muhammad Abduh alitoa mwito wa ijtihad (kujitahidi) na kuwakemea watu wa Taqlid wenye kufuata tu, na alikuwa na darasa ya kufasiri Qur'an alipofika kwenye kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Wakakisoma kama inavyostahiki."

Alisema: "Yule ambaye anasoma Qur'an kwa kusoma tu, mfano wake ni kama punda aliyebeba vitabu vikubwa, hana imani kwa sababu hafahamu siri yake wala hajui uongofu wa Mwenyezi Mungu ulio ndani yake. Kusoma matamko tu, hakuna faida yoyote, hata kama msomaji atajua maana ya hayo matamko. Kwa sababu itakuwa kama picha; na picha ni mawazo, yanakuja kisha yanapotea. Hakika fahamu sahihi ni kufahamu kwa imani na kusadikisha, kwa yule anayezingatia vizuri kitabu na kutaka kuongoka akijua kuwa anasoma Aya zake ili aongoke na kupata uongofu kutokana na maana yake."

Basi baadhi ya masheikh wa Taqlid wakamwingilia kati kwa kusema "Wanavyuoni wanasema: 'Qur'an ni ibada kwa kuisoma.' Sheikh Abduh akajibu: "Lakini Mwenyezi Mungu amesema: "Kitabu tumekiteremsha kwako.kilicho barikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wenye akili wawaidhike".

(38:29)

Na katika rai za Sheikh Abduh, kama ilivyo katika Tafsir Al-Manar ni kwamba, ni juu ya kila Mwislamu asome Qur'an au kuisikiliza yote ijapokuwa mara moja tu katika umri wake.

124.Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko, naye

177

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

akayatimiza.            Alimwambia:

Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu. Akasema: Na katika Kizazi changu (pia) Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.

2 Sura Al-Baqarah

AHADI YANGU HAIWAFIKII WAOVU

Aya ya 124

LUGHA

Makusudio ya kujaribiwa hapa ni kukalifishwa. Makusudio ya maneno ni amri na makatazo ikiwa ni pamoja na kukalifishwa kumchinja mwanawe. Makusudio ya kuyatimiza ni kutii.

MAANA

Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko naye akayatimiza.

Ibrahim Al-khalil (a.s.) ni baba wa Mitume. Dini tatu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi) zinakubali na kuthibitisha Utume wake. Washirikina wa Kiarabu wakijitukuza kwa kunasibika kwao na mwanawe Ismail (a.s.) na kwa kutumikia kwao Al-Kaaba, na kuihami, ambayo imejengwa na Ibrahim na mwanawe Ismail (a.s.)."

31

Mwenyezi Mungu anabainisha kwamba Yeye alimwamrisha Ibrahim baadhi ya taklifa, kama vile kumchinja mwanawe, akawa mwaminifu mwenye kutekeleza amri na kuitii. Mwenyezi Mungu amemsifu Ibrahim kuwa mtekelezaji aliposema:

"Na Ibrahim aliyetekeleza (ahadi)."

(53:37)

Mwenye Bahrul Muhit amesema: "Ibrahim ni babu wa thalathini na moja wa Muhammad; naye ni Ibrahim bin Tarih, bin Najur bin Sarugh, bin Arghu, bin Faligh bin Abir ambaye ni Mtume Hud. Naye alizaliwa katika ardhi ya Ahwaz."

178

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Akasema: hakika mimi nimekufanya Imam wa watu

Hii ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim, ya kumfadhilisha na Uimamu tangu mwanzo na bila ya yeye kuomba, ikiwa ni malipo ya Ikhlasi yake na utekelezaji wake, na pia kujitolea kwake mhanga.

Akasema na katika kizazi changu pia.

Haya ni matakwa na dua kutoka kwa Ibrahim (a.s.) kwamba Mwenyezi Mungu aneemeshe baadhi ya kizazi chake, kama alivyomnemeesha yeye. Kwa sababu neno 'katika' hapa ni kufahamisha baadhi. Hapa yanadhihiri mapenzi ya mzazi kwa mwanawe, kwa vile alivyotaka Ibrahim wema kwa baadhi ya kizazi chake na wala asijitakie yeye mwenyewe peke yake.

Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.

Kauli hii ni kumwitika Ibrahim maombi yake ya kufanywa Maimam baadhi ya kizazi chake kwa masharti ya kuwa wawe kama yeye; watekelezaji ahadi na wacha Mungu. Kwa sababu kazi ya Imamu ni kuzuia maasi, vipi awe yeye ndiye mwasi.

Sioni kauli inayofahamisha zaidi uadilifu wa Imamu na huruma yake kwa raia kuliko kauli ya Imam Ali (A.S) alipokuwa ni khalifa wa Waislamu:

"Umma hivi sasa unaogopa dhulma ya viongozi wake na mimi nahofia kuwadhulumu raia zangu."

Kiongozi anaogopa kuwadhulumu raia; mwenye nguvu anaogopa kuwadhulumu wanyonge; tena mtu mwenye nguvu ambaye hajali mauti. Yaani imekuwa yule mwenye utawala anahofia juu ya raia zake ambapo ingekuwa kinyume; kama ilivyozoeleka! Ni jambo ambalo si la kawaida.

UIMAMU NA FIKRA YA ISMA

Neno Imam (kiongozi) hutumika katika maana nyingi kama vile: njia, kwa sababu inamwongoza mwendaji kwenye makusudio yake. Pia lina maana ya anayoyafuata mtu kumwongoza au kumpotosha, Mwe-nyezi Mungu anasema:

179

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Na tukawafanya ni maimamu wanaoongoza kwa amri yetu..."

(21:73)

Katika Aya nyingine amesema:

"Na tukawafanya ni maimamu waitao katika moto..."

(28:41)

Mtu anakuwa Imam, ikiwa anafuatwa katika jambo fulani, na anakuwa Maamum ikawa yeye ndiye anayefuata.

Hayo ni kwa mujibu wa lugha. Ama kwa mujibu wa dini na sharia, ni kwamba neno Imam linatumiwa kwa anayeongoza swala, lakini katika maana hayo hutumiwa kwa kuunganishwa na neno jingine; kama vile Imam wa ljumaa na jamaa. Ikiwa ametajwa Imam tu, bila ya neno lolote jingine, basi litatumika kwa maana mbili:

Kwanza, kwa maana ya Utume. Hiyo ni daraja ya juu zaidi ya Uimamu. Pili, kwa maana ya Wasii wa Mtume.

Imam kwa maana ya Utume na Imam kwa maana ya wasii, anakuwa ni mwenye kufuatwa katika kila kitu, naye hamfuati yeyote wakati wa Uimamu wake. Uimamu kwa maana ya Utume unahitajia nukuu (nassi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Roho mwaminifu. Na Uimamu kwa maana ya wasii hauna budi kuwa ni kwa nukuu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa ulimi wa Mtume wake mtukufu. Sharti ya nassi hiyo ni kuwa kwa jina na kwa mtu maalum, sio kwa sifa na kwa tamko la ujumla; kama ilivyo kwa Mujtahid na hakimu wa sharia (kadhi). Bali ni lazima iwe ni kwa nukuu mahsus isiyokubali taawil au uwezekano wa kinyume.

Kuanzia hapa ndio inabainika kwamba kutumia neno Imam peke yake kwa asiyekuwa Mtume au Wasii ni jambo la kuangaliwa vizuri na sio mbali kuwa ni haramu, sawa na kutumia neno Wasii wa Mtume kwa asiyekuwa Imam Massum.

Vyovyote iwavyo, kauli ya Imam huyu - awe Mtume au Wasii - ni kauli ya Mwenyezi Mungu; uongozi wake ni wa Mwenyezi Mungu; hukumu yake ni hukumu ya Mwenyezi Mungu ambayo haina kinyume. Yeyote mwenye kudai kitu bila ya kuthibitisha kwa nukuu inayomuhusu basi huyo ni mzushi mwongo.

180

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Bora ya niliyoyasoma katika sifa ya Imam ni kauli ya Imam mtukufu Zainul-abidiin (a.s.) katika Sahifa Sajjadiyya: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika wewe umeitia nguvu dini yako kila wakati kwa Imam uliyemweka kuwaelimisha waja wako; na ni mnara katika miji yako baada ya kuiunganisha kamba yake na yako. Na ukawajaalia ni nyenzo ya radhi zako. Na umefaradhisha kutiiwa na ukahadharisha kuasiwa; umeamrisha kufuatwa maamrisho yake na kuachwa makatazo yake na kutotanguliwa na mtangulizi yeyote au kubaki nyuma naye yeyote. Yeye ni ngome ya wanaotafuta hifadhi na ni pango la Waislamu: Ni tegemeo la waumini na ni fahari ya Mola wa viumbe vyote."

Hizo ndizo sifa za ambaye amechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Imam kwa waja wake. Kimsingi ni kwamba Uimamu wa Utume na ule wa Uwasii unahitajia Isma (kuhifadhiwa na dhambi) haiwezekani bila ya hivyo, kwa sababu kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake. Mwenye uchafu na ambaye ana haddi (adhabu) hawezi kumfanyia haddi mwingine.

Wamelitolea daili hilo Shia Imamiya kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu.

Kwamba Uimam hauwi ila kwa kufanywa na Mwenyezi Mungu. Hilo linatiliwa nguvu na ombi la Nabii Ibrahim kwa Mwenyezi Mungu kufanywa Maimamu katika kizazi chake.

Ikiwa Uimamu ni kwa kufanywa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) utakuwa unatokana na nukuu kutoka kwake.

Vile vile wametolea dalili Shia, kauli Yake Mwenyezi Mungu: "Ahadi yangu haiwafikii madhalimu."

Kwamba ni wajibu kupatikana Isma kwa Mtume na Wasii. Njia ya kutolea dalili ni kuwa Mwenyezi Mungu amewabainishia wazi wazi kuwa Yeye hautoi Uimamu kwa dhalimu; na dhalimu ni yule aliyefanya madhambi katika maisha yake kwa namna yoyote ile, hata kama atatubia baada yake, lakini jina hili litakuwa limempitia. Kwa hivyo mwenye kuwa na hilo hawezi kuwa Imam.

Inatokea sadfa mtu mwengine asiyekuwa AN kukua katika malezi ya ushirikina na uchafu, kuabudu masanamu, kuzama katika uchafu wa kijahilia na wala asitamke shahada mbili ila baada ya kuyashiba masanamu na kuyasujudia.

181

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Kwa upande mwingine Mwenyezi Mungu akataka Ali bin Abi Twalib akulie katika malezi ya Mtume yaliyo na usafi; na Mtume amtengeneze kulingana na matakwa ya Mwenyezi Mungu na kuyaangusha masanamu kutoka kwenye hadhi yake na kuyatupa chini ya miguu ya Muhammad (s.a.w.)

Hapa kuna swali tunalolitoa kwa kila mwenye akili mwenye kuchunga haki, ili ajijibu yeye mwenyewe kwa akili yake; nalo ni hili:

Mtu asiyejua kutumia vizuri, amerithi mali kutoka kwa baba yake, ikabidi awe na msimamizi atakayemlinda na kumuhifadhia mali yake. Sasa kukawa na utatanishi wa kumpa usimamizi mtu ambaye hakuwahi kumwasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake, si kwa dhambi dogo au kubwa, au apewe usimamizi mtu aliyewahi kumwasi Mwenyezi Mungu kwa muda mrefu akiwa amekwisha baleghe, kisha akatubia; je tumchague yupi?

Inatosha kuwa ni dalili ya kuhifadhiwa na madhambi (Isma) kwa Ahlul Bait (a.s.) kutokana na alivyowatolea ushahidi Mwenyezi Mungu aliposema:

"Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kuwatakasa kabisa kabisa."

(33:33)

Tumezungumzia Isma kwa ufafanuzi katika kufasiri Aya ya 39 kifungu cha Isma ya Mitume na kifungu cha Ahlul Bait: Tafad-hali rejea, kwani kifungu hiki ni ukamilisho wa vifungu hivyo vilivyopita.

Fikra ya Isma (kuhifadhika na makosa) haihusiki na Shia tu. Masunni pia wameizungumzia, lakini wao wanaijaalia kwa umma, wakitegemea Hadith ambayo haikuthibiti kwa Shia, nayo ni "Umma wangu hauwezi kukusanyika juu yajambo la upotovu."

Wakristo nao wanasema Baba mtakatifu ana Isma. Wakomunisti wamesema Marx na Lenin pia wana Isma. Makabaila wa Syria nao wamesema iko Isma kwa Antony Saada, na wanachama wa Ikhwanul-Muslimin (ndugu wa Kiislamu) wamesema Hassan Al-Banna anayo Isma.

182

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Huko China, hivi leo ninapoandika tafsir hii ni mwaka 1967, mamilioni ya watu wanaamini kuwa Mao Tse Tung ana Isma na wanajizatiti kwa mafunzo yake.

Wakomunisti; tuliowataja wakitofautiana huwa wanatofautiana katika kauli za viongozi na makusudio, sio katika wajibu wa kuwafuata na kuwafanya viongozi; sawa na vile wanavyohitlafiana Waislamu katika tafsir ya Qur'an au Wakristo katika tafsir ya Injil.

Yeyote atakayeihuisha Isma kwa Mashia peke yao, basi atakuwa ni mmoja kati ya hawa wawili. Ama atakuwa ni mjinga mwenye kughafilika au mzushi mwenye njama.

125.Na tulipoifanya ile nyumba (Al-Kaa'ba) iwe mahali pa kuendewa na watu na mahali pa amani. Na pafanyeni alipokuwa akisimama (Maqamu) Ibrahim ni mahali pa kuswalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail kuwa: Itakaseni nyumba yangu kwa ajili ya wale wenye kutufu na wenye kujitenga huko kwa ibada na wanaorukuu na kusujudu.

126.Na aliposema Ibrahim: Ewe mola wangu! Ufanye mji huu uwe wa amani na uwaruzuku wakazi wake matunda, wale wanaomwamini           Mwenyezi

Mungu na siku ya mwisho katika wao. Akasema Mwenyezi Mungu: Na mwenye kukufuru nitamstarehesha kidogo; kisha nitamsukumiza katika adhabu ya moto napo ni mahali pabaya

183

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza kabisa pa kurejea.

2 Sura Al-Baqarah

NA TULIPOIFANYA ILE NYUMBA IWE MAHALI PA KUENDEWA

Aya 125-126

LUGHA

Nyumba ni nyumba yoyote, lakini ikisemwa nyumba tu, basi itakuwa ni Al-Kaaba, kutokana na kutumika sana hivyo.

MAANA

Na tulipoifanya ile nyumba (Al-Ka'aba) iwe mahali pa kuendewa na watu na mahali pa amani.

Aya hii inaungana na Aya iliyotangulia (alipomfanyia mtihani Ibrahim). Maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu ameijaalia nyumba yake ni mahali pa kuendewa na watu makundi kwa makundi kwa ajili ya kutekeleza ibada na baadaye warudi makwao; kisha yaje makundi mengine, n.k.

Vile vile ameifanya ni mahali pa kupata amani katika akhera. Kwa sababu mtu anapoifikia nyumba hiyo na akatekeleza ibada anajirudi na kutubia. Kwa hiyo nyumba ya Al-Kaaba inakuwa ni nyenzo ya kujitakasa na adhabu na mateso. Kama vile ambavyo ameifanya ni mahali pa amani katika dunia. Kwa sababu mtu mwenye kwenda mahali hapo anakuwa salama wala haingiliwi na yeyote kwa ubaya. Mtu anaweza kumwona mtu aliyemuua baba yake katika Haram (eneo la Al-kaaba) lakini akajitia hamnazo! Desturi hii imerithiwa tangu wakati wa Ismail (a.s.) mpaka leo.

MKOSAJI KUKIMBILIA HARAM

Katika kitabu cha Al-Jawahir ambacho ni tegemeo kubwa la Fiqh ya Shia Jafariyyah kuna maelezo haya, ninamnukuu: "Yeyote aliyekimbilia haram hapigwi haddi kwa kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)".

"Na mwenye kuingia humo huwa katika amani"

184

(3:97)

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Bali atapunguziwa chakula na atapewa kidogo tu kiasi cha kuzuwia tumbo ili atoke akapigwe haddi nje.

Imepokewa riwaya sahihi kutoka kwa Imam Jafar Sadiq (a.s.) kuhusu mtu ambaye amefanya jinai mahali pengine pasipokuwa Haram kisha akakimbilia kwenye Haram. Akasema Imam: "Hatapigwa haddi, lakini hatalishwa, hatapewa maji wala hatasamehewa, kwani akifanyiwa hivyo, kuna uwezekano wa kutoka nje ya Haram na apigwe haddi. Kama akifanya jinai ndani ya Haram atapigwa haddi ndani ya Haram, kwa sababu hakuihishimu Haram."

Abu Hanifa amesema: "Haifai kumwua aliyekimbilia kwenye Haram" ametoa dalili kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: "Na tulipoifanya ile nyumba (Al-Ka'aba) iwe mahali pa kuendewa na watu na mahali pa amani."

Na pafanyeni alipokuwa akisimama Ibrahim ni mahali pa kuswali.

Hiyo ni amri ya kuswali (Maqamu Ibrahim) mahali aliposimama Ibrahim. Mafaqihi wamekubaliana kuwa inatakikana kuswali hapo rakaa mbili za Tawaf ikiwezekana. Maana ya (Maqam Ibrahim) mahali aliposimama Ibrahim ni pale mahali maarufu ndani ya msikiti. Ama mwenye kusema kwamba makusudio yake ni msikiti wote, basi na atoe dalili ya kuthibitisha kauli yake hiyo.

Na tuliagana na Ibrahim na Ismaili kuwa itakaseni nyumba yangu kwa ajili ya wale wenye kutufu na wenye kujitenga kwa ibada na wanaorukuu na kusujudu.

Maana yake, tulimwagiza Ibrahim na Ismaili kuiheshimu Al-Ka'aba na kuiepusha na kila lisiloelekeana nayo; kama vile masanamu, najisi, upuuzi, uovu, majadiliano n.k. Na wawaamrishe watu hilo "Wanye kutufu ni wale wanaoizunguka, wanaojitenga kwa ibada ni wanaokaa humo msikitini au wanaokaa karibu kwa ibada, na wanaorukuu na kusujudu, yaani wanaoswali.

Na aliposema Ibrahim Ewe Mola wangu! Ufanye mji huu uwe wa amani.

Hii ni dua na matamanio kutoka kwa Ibrahim kwa Mwenyezi Mungu kuijaalia Makka tukufu kuwa ni mji wa amani, yaani watu wake wasiwe na vita, mitetemeko, vimbunga n.k.

Kuna kikundi cha wafasiri wamesema kwamba Mwenyezi Mungu ameiitikia dua ya Ibrahim, ambapo hakuna yeyote anayeikusudia Makka

185

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kwa uovu ila Mwenyezi Mungu humwangamiza, na mwenye kuikusudia kwa uadui basi uadui wake hauchukui muda mrefu.

Na uwape wakazi wake matunda wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Ibrahim alipomaliza kujenga nyumba hiyo katika ardhi kame isiyokuwa na maji wala mmea wowote, alimwomba Mwenyezi Mungu s.w.t. aipe amani ardhi hii na iwe na rizki, wala hakuainisha aina ya riziki wala kule itakapotoka isipokuwa umuhimu ni kufikiwa na riziki vyoyote itakavyokuwa na popote itakapotoka.

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliitikia maombi ya Ibrahim. Ikawa riziki ya namna namna inakuja Makka kutoka sehemu mbali mbali; ikawa Makka ni kituo cha wasafiri na cha biashara. Katika hali hii ndipo Mwenyezi Mungu akasema katika Aya hii:

"Je hatukuwakalisha mahali patakatifu na yanakoletwa matunda ya kila aina."

pa amani

(28:57)

Ibrahimu aliwahusisha waumini tu katika kutaka riziki, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikwisha mfahamisha kwamba katika kizazi chake kutakuwa watu madhalimu na Mwenyezi Mungu hakuuhaidi Uimamu kwa madhalimu.

Akasema (Mwenyezi Mungu nitamstarehesha kidogo.

s.w.t): Na mwenye kukufuru

Yaani Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim: Mimi vile vile ninawaruzuku makafiri na hata mafasiki. Kwa sababu riziki ni kitu kingine na Uimamu ni kitu kingine, kwani Uimamu ni uongozi wa kidini na wa wakati, nao unahitajia imani, uadilifu na Isma. Ama riziki inakuwa kwa mwema na mwovu; kama vile maji na hewa. Madhambi na maasi hayana dhara yoyote katika umri na riziki katika maisha haya, isipokuwa athari yake itadhirhirika kesho siku ya kiyama ambapo watu watapata malipo yao.

127.Na Ibrahim alipoinua misingi ya ile Nyumba (Al-Kaaba) na Ismail (wakaomba): Ewe mola wetu! Tutakabalie; hakika wewe ndiye

186

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza Msikizi Mjuzi.

128.Ewe mola wetu! Utufanye tuwe ni wenye kusilimu kwako. Na miongoni mwa kizazi chetu pia ufanye umma uliosilimu kwako. Na utuonyeshe ibada zetu na utukubalie toba. Hakika wewe ndiye mwenye kukubali toba mwenye kurehemu.

129.Ewe mola wetu! Wapelekee mtume anayetokana na wao, awasomee Aya zako, na kuwafundisha Kitabu na hikima na awatakase. Hakika wewe ndiye mwenye nguvu mwenye hekima.

2 Sura Al-Baqarah

NA ALIPOINUA IBRAHIM MISINGI YA ILE NYUMBA Aya ya 127-129

HISTORIA YA AL-KA'ABA

Wafasiri na wanahistoria wametofautiana katika historia ya Al-Ka'aba, kwamba je, ilikuako kabla ya Ibrahim, kisha ikaharibika ndipo akaijenga upya yeye na mwanawe Ismail kwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu; au yeye (Ibrahim) ndiye aliyeanza kuijenga?

Wafasiri wengi na wanahistoria wa Kiislamu wamesema kuwa ilikuwako kabla ya Ibrahim kwa miaka mingi. Baadhi wamesema ilianzishwa na Ibrahim (a.s.); wengine wamenyamaza na kusema: "Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. Nasi tuko pamoja na hawa. Kwani akili haina nafasi

187

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

hapa, na njia ya kujua itategemea athari au Aya za Qur'an au Hadith mkato.

32

Na mimi sikupata kauli yoyote ya watafiti wa athari na uvumbuzi, na Qur'an haikuelezea waziwazi historia ya Al-Kaaba, bali inaelezea tu kwamba Ibrahim na mwanawe Ismail waliijenga na kusaidiana. Na hii haifahamishi kuwa ilikuwako au haikuako kabla ya Ibrahim.

Na Hadithi mkato hakuna isipokuwa Hadithi Ahad (pwekesho).

33

Na Hadithi pwekesho ni hoja katika hukumu ya sheria tu.34

Kwa vyovyote iwavyo sisi hatutaulizwa na Mwenyezi Mungu mtukufu wala hatuna wajibu wa kuijua historia ya kujengwa Al-Kaaba au kujua wakati ilipoanzishwa.

Vile vile hatuna taklifa ya kujua kwamba hiyo ni sehemu ya pepo au ni ya ardhi na kwamba je, Adam na Mitume baada yake walihiji au la! Au kwamba hiyo Al-Ka'aba ilipandishwa mbinguni wakati wa Tufani kisha ikateremshwa ardhini.?

Pia hatuna taklifa ya kujua kwamba Hajarul-Aswad (jiwe jeusi) lililetwa na Jibril kutoka mbinguni au lilikuja pamoja na Adam kutoka peponi au lilibanduka kutoka Jabal Abu Qubays na kwamba je lilikua jeusi kwa sababu ya kuguswa na wenye dhambi. Na mengineyo ambayo hayana mapokezi yoyote isipokua Hadithi Ahad au visa visivyokuwa na ukweli.

Sisi hatutaulizwa vitu vyote hivyo wala hatuna taklifu yoyote ya kujua si kwa njia ya wajibu, wala sunna; si kiakili wala kisheria. Wala hakuna faida yoyote ya kidini au dunia katika kuifanyia utafiti. Utafiti huu ulikuako kisha ukaenda na upepo; na yeyote anayetaka kuufufua, ni sawa na yule anaejaribu kurudisha nyuma mishale ya saa.

Kitu ambacho tutaulizwa na kutakiwa kukifanya kuhusu Al-Ka'aba ni kuikusudia kwa ajili ya Hijja na Umra kwa anayeweza kuiendea. Na vile

Hadithi iliyokubaliwa na wote katika maana na matamshi.

Hadith ambayo silsila (mfuatano) ya upokezi wake imekatika au Hadith ambayo haikubaliwi na wengi.

La Kushangaza zaidi ya niliyoyasoma kuhusu maudhui haya ni kauli ya Sayyid Tabatabai katika Tafsir Al-Mizan J1 Uk 196 "Kukosekana kusihi mapokezi ya hadith hakuwajibishi kuitupa Hadith hiyo maadamu haihalifu akili au Hadith sahihi". Inajulikana wazi kwamba kutohalifu akili na Hadithi thabiti ni sharti la yasiyothibiti, kwa sababu kutothibitika kusihi mapokezi kunatosha kuitupa Hadithi bila ya kuongeza sharti jengine; kama si hivyo basi itabidi kuitumia kila Hadithi isiyokuwa sahihi mpaka itakapohalifu akili au hadithi thabiti.

188

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

vile kuiheshimu na kuitukuza na kuihami kwa kufuata nyayo za Mtume (s.a.w.) Ahlul Bait wake (s.a.w.), masahaba, wafuasi, wanachuoni na Waislamu wote. kwani hao wanaamini bila ya tashwishi yoyote kwamba kuiadhimisha nyumba ya Mwenyeezi Mungu ni kumwadhimisha Mwenyezi Mungu, na kuihami ni kuihami dini ya Mwenyezi Mungu.

Amirul Muminin amesema: "Amewawajibisha Mwenyezi Mungu kuhiji nyumba yake tukufu ambayo ameifanya ni kibla cha viumbe,wanaingia kama wanavyoingia wanyama na wanaingia makundi makundi kama njiwa. Ameijaalia Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni alama ya kumnyenyekea yeye (Mungu) na kuukubali Utukufu Wake. Ameijaalia ni alama ya Waislamu, na nikinga ya wenye kutaka hifadhi."

Ewe mola wetulTutakabalie

Hii ni dua kutoka kwa Ibrahim na Ismail ya kutaka thawabu kutokana na amali hii, kwa sababu maana ya kutakabaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kupata thawabu kutokana na amali atakayoikubali, kama vile ambavyo kukosa thawabu kunamaanisha kukataliwa amali. Hakuna mwenye shaka kwamba Mwenyezi Mungu ameitakabali dua yao na amewalipa thawabu kutokana na twaa hii. Kwa sababu yeye ndiye aliyefungua mlango wa dua, na hawezi kumfungulia mja mlango wa dua, hasa mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, kisha amfungie mlango wa kutakabaliwa, kama alivyosema Amirul Muminini.

Ewe Mola wetu! Utufanye tuwe ni wenye kusilimu kwako.

Makusudio ya kusilimu hapa ni kufanya ikhlas katika itikadi na amali (matendo). Hapana mwenye shaka kwamba mwema mwenye kusifiwa, ni yule anayemnyen-yekea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo yake yote.

Na miongoni mwa kizazi chetu (pia ufanye) umma uliosilimu kwako.

Ameikubali dua yao na akajaalia katika kizazi chao mamilioni na mamilioni ya waislamu.

SHIA NA MABABU WA MTUME

Shia wamehusika na kauli ya kuwa baba wa Muhammad, na mababu zake, mama yake na nyanya zake wote hawa-kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote na kwamba Muhammad tangu alipoumbwa alikuwa akigura (akihama) katika migongo mitakatifu mpaka kwenye

189

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

tumbo la mfuko wa uzazi mtakatifu na hadi ilipotimu saa ya kuzaliwa kwake.

Sheikh wa Shia mwenye kujulikana kwa jina la Sheikh Al-Mufid amesema katika sherhe ya Aqaid Aswaduq chapa ya mwaka 1371 A.H. uk 67: "Hakika mababa wa Mtume (s.a.w.) kuanzia baba yake Adam, walikuwa ni watu walio na imani, na Mwenyezi Mungu amemwambia Mtume wake Muhammad:

"Na mageuko yako kati ya wale wanaosujudu."

(26:219)

Mtume (s.a.w.) amesema: "Niliendelea kugurishwa katika migongo mitakatifu kwenda kwenye matumbo matakatifu mpaka Mwenyezi Mungu akanidhihirisha (kwa kuzaliwa) katika ulimwengu wenu huu." Kwa hiyo kauli ya Mtume inafahamisha kwamba mababu zake wote walikuwa wenye imani. Kwani lau baadhi yao wangekuwa makafiri isingelistahiki kusifiwa na utwahara kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Hakika washirikina ni najisi".

(9:28)

Mtume alipowasifu mababu zake kwa utakatifu imefahamisha kwamba wao walikuwa waumini

Utukubalie toba

Sio lazima kwa mwenye kutaka msamaha awe na dhambi hasa ikiwa mwenye kutaka ni Mtume au wasii. Kwa sababu watu watukufu hawa wanajiona hawajafikia kuitekeleza haki ya Mwenyezi Mungu sawa sawa kadiri watakavyojitahidi katika ibada ya Mwenyezi Mungu. Kwani wao ndio wanaojua zaidi utukufu wa Mwenyezi Mungu. Na kwamba ibada ya mtu, vyovyote itakavyokuwa haiwezi kutekeleza haki ya utukufu huo usiokuwa na mwanzo wala mwisho.

Ewe, Mola wetu! Wapelekee Mtume anayetokana na wao

Ombi hili alilikubali Mwenyezi Mungu kwa kuleta Mtume wa mwisho na bwana wa Mitume wote. Zimekuja Hadith kwa upande wa Shia na Sunni

190

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kwamba Mtume amesema: "Mimi ni ombi la Ibrahim na ni bishara ya Isa."

katika Qur'an Mwenyezi Mungu amesema:

"Yeye ndiye aliyemuinua Mtume katika wasiojua kusoma atokaye miongoni mwao anawasomea Aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hekima. Na kabla ya hayo walikuwa katika upotofu ulio dhahiri."

(62:2)

Amirul Muminin Ali (A.S.) amesema: "Alimpeleka Mwenyezi Mungu Muhammad kuwa ni Mtume na hakuna yeyote katika waarabu aliyekuwa akisoma kitabu au kudai Utume wala wahyi."

BISHARA YA MAHDI MWENYE KUONGTOJEWA

Kama walivyotoa Mitume bishara ya Muhammad, yeye naye alitoa bishara ya Mahdi kutoka katika kizazi chake. Mimi nimetunga kitabu juu ya suala hilo nilichokiita Al Mahdil Muntadhar Wal-aql (Mahdi mwenye kungojewa na akili) katika kitabu hicho nimenakili Hadith nyingi kutoka upande wa Shia na Sunni; na zimetoka nakala nyingi na kurudiwa na wachapishaji 'Daarul-malayin' pamoja na kitabu 'Allahu wal-aql', 'Al-akhira wal-aql' na 'Annubuwwat wal-aql'. Vitabu hivyo vinne vimekusanywa kuwa kitabu kimoja kwa jina Al Islamu wal-aql (Uislamu na akili).

Kitabu kilichokusanya zaidi kuhusu suala hili katika nilivyovisoma ni kitabu kinachoitwa Muntakhabul-athari fil - Imam thani ashar cha Sayyid Lutfillah Assafi kilichokuwa na kurasa zaidi ya 500, ambacho ni rejea bora zaidi.

Baada ya kuchapishwa kitabu 'Al-Mahdil muntadhar wal-aql' nilisoma maneno marefu ya Muhyiddin aliye mashhuri kwa jina la Ibnul Arabi, nanukuu sehemu ya maneno hayo. "Mwenyezi Mungu anaye Khalifa atakayetoka ikiwa nchi imejaa dhulma na jeuri ili aijaze uadilifu... na khalifa huyo ni kutoka katika kizazi cha Mtume (s.a.w.) kutoka katika kizazi cha Fatima (a.s.), jina lake linafanana na jina la babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu ...Atafanyiwa baia kati ya rukni na maqam,

191

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

anafanana na Mtume kwa umbo naye atakuwa na uso mwangavu mwenye pua ndefu... Atawaongoza watu kwa desturi ya Mtume (s.a.w.). Na babu yake alisema kumhusu yeye: Atafuata athari yangu bila kukosea na hiyo ndiyo Isma." Hayo yamo katika kitabu Futuhatil-Makkiyya kilichochapishwa na Darul-kutubil-Arabiya uk 327 na kuendelea.

130.Na ni nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu ? Na hakika sisi tulimtakasa (Ibrahim) katika dunia; na hakika yeye katika akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

131.Mola wake alipomwambia silimu; akasema Nimesilimu kwa Mola wa walimwengu wote.

132.Na Ibrahimu akawausia haya wanawe, na pia Yaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu.

133. Je, mlikuwapo yalipomfikia Yakub mauti, alipowaambia wanawe: Je, mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-haka; Mungu mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.

192

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

134.Huo ni umma uliokwisha pita. Utapata Uliyoyachuma nanyi mtapata mtakayoyachuma; wala hamtaulizwa              waliyokuwa

wakiyafanya.

NA NI NANI ATAJITENGA NA MILA YA IBRAHIM

Aya ya 130 - 134

MAANA

Na ni nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu?

Haya ni matahayarizo kwa Mayahudi na Manasara na washirikina wa Kiarabu ambao hawakumwamini Muhammad. Siri ya matahayarizo haya ni kwamba Mayahudi wanajifaharisha kwa kunasibika kwao na Israil: Na Israil ndiye Yaqub bin Is-hak bin Ibrahim; Manaswara nao wanajifaharisha kwa Isa na nasabu ya Isa kwa upande wa mama inaambatana na Israil vile vile. Ama washirikina wa Kiarabu wengi wao wanatokana na Adnani nasabu yao inarudia kwa Ismail bin Ibrahim kuongezea kwamba wao walipata heri wakati wa kijahili kwa baraka za nyumba iliyojengwa na Ibrahim.

Kwa hiyo wote wanajifaharisha kwa Ibrahim na mila ya Ibrahim na inajulikana wazi kwamba Muhammad (s.a.w.) anatokana na kizazi cha Ibrahim na yuko katika mila ya Ibrahim. Kwa hivyo mwenye kumk-anusha Muhammad na mila yake ndio amemkanusha Ibrahim na mila yake. Hapana shaka kwamba mwenye kukanusha matokeo ya utukufu na fahari yake, basi yeye ni safihi (mpumbavu) sawa na mwenye kufanya mambo ya kumwangamiza yeye mwenyewe.

Hakika sisi tulimtakasa (Ibrahim) katika dunia;

Yaani tulimfanya safi mwenye kutakata na uchafu; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

193

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na kuwatakasa kabisa kabisa."

(33.33)

Na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

Kwa uwazi kabisa ni kwamba yeye katika dunia yuko hivyo; kwa sababu Uislamu unaiunganisha akhera na amali za duniani; ambaye katika dunia atakuwa mwema na mwenye busara, basi huko akhera pia atakuwa hivyo na ambaye katika dunia atakuwa mwovu na kipofu basi huko akhera pia atakuwa hivyo.

Mola wake alipomwam-bia silimu akasema: Nimesilimu kwa Mola wa walimwengu.

Unaweza kuuliza, Je, Mwenyezi Mungu alimtaka Ibrahim asilimu (anyenyekee) kabla ya kumpa Utume au baada yake? Kwa sababu haiwezekani Mwenyezi Mungu kumpa wahyi asiyekuwa Mtume. Na pia hawezi kuteremsha wahyi kwa mtu ila baada ya kusilimu (kunyenyekea).

Jibu: Hakika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Silimu (Nyenyekea)" akasema nimesilim ni fumbo la kuwa Ibrahim ni msafi mwenye Ikhlas na kwamba yeye ndiye mwenye kuchukua utume na ujumbe kwa ukamilifu. Kwa hivyo makusudio yake ni kumsifu Ibrahim kutokana na Ikhlasi yake, twaa yake na kufuata kwake amri. Wakati huo huo ni matahayarizo kwa Mayahudi, manaswara na washirikina wa Makka ambao wanajifaharisha kwa Ibrahim, kisha wanamuasi na kumpinga yule aliyekuja kuhuyisha mila ya Ibrahim na kueneza desturi na itikadi yake.

Na Ibrahim akawausia haya wanawe na Yaqub pia: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu.

Yaani thibitini juu ya Uislamu mpaka kufa ili mfufuliwe juu ya Uislamu na mumkabili Mwenyezi Mungu kwa huo Uislamu.

HAKI YA MTOTO KUTOKA KWA MZAZI

Aya hiyo iliyotangulia inatambulisha kwamba mzazi ana jukumu kubwa na malezi ya mtoto wake na kumwongoza kwenye dini ya haki. Imam Zaynul-Abidin (a.s.). Amesema: "Ama haki ya mtoto wako ni kujua kuwa

194

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

anatokana na wewe na kwamba wewe una jukumu la kuitengeneza vizuri adabu yake na kumfahamisha kuhusu Mola wake Mtukufu na kumsaidia kumtii.

Basi mwamrishe amali ambayo anajua kuwa atapata thawabu kwa kufanya wema, na kupata dhambi kwa kufanya mabaya.

Je mlikuwapo yalipomfikia Yaqub mauti.

Kumfikia mauti ni wakati wa kufa, alipopata alama za kufa. Mwenye Majmau anasema: "Mayahudi wanadai kuwa Yaqub alipokufa aliwausia wanawe kushikamana na Uyahudi. Ndio Mwenyezi Mungu akabatilisha madai yao juu ya Yaqub; sasa vipi mnadai mambo ya uongo?"

Kwa hakika ni kwamba Yaqub aliwaambia wanawe: "Je mtaabudu nini baada yangu?"

Unaweza kuuliza kwamba neno 'nini' hutumiwa kwa kisicho na akili, sasa imekuaje hapa kutumiwa kwa mwenye kuabudiwa kwa haki?

Jibu: Wakati huo watu walikuwa wakiabudu masanamu, ndipo likaletwa swali kutokana na vile wanavyoabudu sio kutokana na uhaki wa kuabudu. Kwa hiyo maana itakuwa ni kitu gani mtaabudu?

Wakasema: "Tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu mmoja tu, na sisi tunasilimu Kwake."

Unaweza kuuliza Yaqub ni mtoto wa Is-hak, na Ismail ni ami yake (ndugu wa baba yake) sasa imekuwaje kumwingiza Ismail pamoja na mababa?

Jibu: Ami yuko katika daraja ya baba kwa sababu ni nduguye na anaadhimishwa kama anavyoadhimishwa baba. Iko Hadith ya Mtume (s.a.w.) inayosema; kuwa Mtume alisema:"Nirudishieni baba yangu" yaani ami yake Abbas.

Huo ni umma uliokwishapita. utapata ulioyachuma, nanyi mtapata mtakayoyachuma.

Aya hii inaashiria kawaida ya mambo, kwamba natija za amali zote na athari zake zitamrudia mwenye kutenda peke yake, hawezi kunufaika nazo mwenye nasaba naye na wala hazitamdhuru mwingine.

195

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Uislamu umethibitisha kawaida hii kwa mifumo mbali mbali ya maneno, kama vile anavyosema Mwenyezi Mungu:

"...Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine"

"Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya."

(6:164)

(53:39)

Pia Mtume (s.a.w.) amesema kumwambia mwanawe Fatima: "Ewe Fatima! Fanya amali wala usiseme mimi ni binti wa Muhammad, kwa sababu mimi sitakutoshea wewe na kitu chochote kwa Mwenyezi Mungu." Na mengineyo.

Kufafanua zaidi maudhui haya kutafahamisha kwamba mpaka leo sisi hatujui mambo yaliyo wazi kabisa.

135.Na wakasema:         Kuweni

Mayahudi au Manaswara ndio mtaongoka Sema:         Bali

(tunashika) mila ya Ibrahim Mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.

136.Semeni:               Tumemwamini

Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaqub na wajukuu na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao na sisi tumesilimu (tumenyenyekea) kwake."

137.Basi wakiamini kama mnavy-oamini itakuwa wameongoka.

1*3 LJİ J û

f r, \ l

J\ J\

196

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Basi Mwenyezi Mungu atakutoshea (na shari yao). Na yeye ndiye msikizi mjuzi.

138.(Huu ni) upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu. Na ni nani aliye mzuri kwa upakaji rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi tunamwabudu Yeye.

NA WAKASEMA: KUWENI MAYAHUDI AU MANASWARA

Ayaya 135-138

MAANA

Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo mtaongoka.

Dhamiri katika "wakasema" inawarudia watu wa Kitabu; maana yake walisema Mayahudi kuweni Mayahudi mtaongoka kwa sababu uongofu, wanavyodai wao, unatokana na wao tu peke yao. Na Wakristo nao walisema hivyo hivyo. Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake Mtukufu Muhammad (s.a.w.): "Sema bali (tunashika) mila ya Ibrahim." Yaani hatuwafuati Mayahudi wala Wakristo, bali tunafuata mila ya Ibrahim. Tumeyataja yanayoelekeana na haya katika Aya ya 111-113 ya sura hii.

MJADALA WA KIMANTIKI

Huenda mtu akasema: Mayahudi wamedai kuwa na haki, Wakristo nao wakadai kuwa na haki, na Muhammad (s.a.w.) naye aka-sema bali Ibrahim ndiye mwenye haki sio Mayahudi wala Wakristo; na kauli zote hizi ni madai. Sasa basi ikiwa itafaa kwa Mayahudi na Wakristo kutumia mantiki haya yasiyofaa, basi itakua haifai kuyafa-nanisha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake; Je, kuna njia gani?

Jibu: Makusudio ya: "Bali (tunashika) mila ya Ibrahim" ni kuyabatilisha madai ya Mayahudi na kuwanyamazisha, na wala sio kuthibitisha

197

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

uhakika hasa. Inawezekana mtu kuipinga hoja ya mtesi wake kwa kitu ambacho sio hoja yake bali ni hoja iliyo mfano wake; kama vile kuyavunja madai ya Wakristo kwa Adamu ambaye hana baba; pale waliposema kwamba Masih ni Mungu, kwa sababu hana baba. Na Adam naye hana baba, lakini hawamwiti Mungu. Aina hii ndiyo inayoitwa 'mjadala wa kimantiki.' Kwa hiyo njia ya kuwanyamazisha Mayahudi na Wakristo ambayo tunayo ni>

Mayahudi na Wakristo wanahitalifiana kidini na kiitikadi. Kila kundi linalikufurisha kundi jingine, lakini wakati huo huo wanaafikiana juu ya usahihi wa dini ya Ibrahim. Kwa dhahiri kabisa ni kwamba Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo bali aliacha dini za upotefu akashikamana na dini ya haki na hakuwa katika washirikina. Hakuwa Yahudi kwa vile hakusema kuwa Uzayr ni mtoto wa Mungu, wala hakumfananisha Mwenyezi Mungu; kama walivyodai kwamba Mwenyezi Mungu ni mzee mmoja mwenye mvi za kichwani na kidevuni. Vile vile Ibrahim hakuwa Mkristo kwa sababu hakusema Masih ni mtoto wa Mungu kwa vile hilo ni shirk.

Maadam Mayahudi na Wakristo wanaikubali dini ya Ibrahim, basi inawalazimu wawe ni wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, bali pia wanalazimika wahiji Al-Ka'aba tukufu; kama alivyokuwa Ibrahim akiitakidi na kufanya, na kama alivyoitakidi Muhammad na kufanya; na wao hawakumpwekesha Mwenyezi Mungu wala hawakuhiji. Kwa hiyo wao ni waongo; na Muhammad ni mkweli na mwaminifu juu ya dini ya Mwenyezi Mungu na mila ya Ibrahim.

Kwa maneno mengine ni kwamba kushikamana na lile lililoafiki ambalo ni dini ya Tawhid aliyokuwa nayo Ibrahim na aliyonayo Muhammad hivi sasa, ni bora kuliko kuchukua lile lenye hitilafu ambalo ni Uyahudi na kumfananisha kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Ukristo na utatu wake.

Semeni: Tumemwamini Mwenyezi Mungu. Yaani semeni enyi Waislamu. Na yale tuliyoteremshiwa ambayo ni Qur'an.

Na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim nazo ni sahifa za Ibrahim; Inasemekana zilikuwa kumi.

Na Ismail na Is-hak.

Hao ni watoto wa Ibrahim. Ismail ndiye mkubwa kuliko Is-hak; mama yake ni Hajar na mama wa Is-hak ni Sara.

198

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Yaqub ni mtoto wa Is-hak. Hao wote hawakuteremshiwa sahifa, isipokuwa ziliteremshwa kwa Ibrahim, lakini inafaa kusema kuwa zimeteremshiwa wote kwa kuangalia kwamba wao walikuwa wakiabudu na kulingania kutokana na sahifa hizi; sawa na vile inavyofaa, kwa sisi Waislamu kusema: tumeteremshiwa Qur'an, kwa vile tunaamini na kufanya amali kutokana nayo na tunailingania.

Na Wajukuu.

Hao ni wajukuu wa Yaqub kutokana na watoto wake kumi na wawili; Ni kama makabila ya Kiarabu katika uzao wa Ismail. Katika kizazi hicho kuna mitume wengi; kama vile Daud, Suleiman, Yahya, Zakariya. Vile vile waumini wengine ambao walifanya ibada kutokana na sahifa za Ibrahim (a.s.).

Na waliyopewa Musa na Isa

Ni Taurat na Injil na pia wengine waliyopewa Manabii. Kama Zaburi aliyoteremshiwa Daud.

Hatutofautishi baina ya yeyote katika hao.

Yaani tunawaamini wote, wawe na kitabu au la. Sisi sio kama Mayahudi na Wakristo ambao wanaamini baadhi na kukanusha baadhi, bali wote kwetu ni sawa katika kuukubali utume wao. Kimsingi ni kwamba kuwaamini wote ni wajibu kwa njia ya ujumla, na wala hatukukalifishwa kuwajua kwa upambanuzi ila baada ya ubainifu kutoka katika Qur'an, au Hadith.

Basi wakiamini kama mnavyoamini nyinyi itakuwa kweli wameongoka.

Yaani wakiamini imani sahihi ambayo ni Tawhid yenye kutakata na aina yoyote ya shirk, na pia wakiwakubali Mitume wote akiwemo Muhammad; kama vile wanavyofanya Waislamu kwa Mitume wote bila ya kuwabagua wengine, wakifanya hivyo, basi watakuwa wameongoka. Wala makus-udio sio kuwa waamini dini mfano wa dini ya Kiislam. Kwa sababu Uislamu hauna cha kufananisha.

Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu.

Yaani kila anayeipinga haki anakuwa amejitoa kundini na kujitofautisha.

199

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Basi Mwenyezi Mungu atakutoshea Kwani vitimbi viovu vinawapata wenyewe.

Kwa ufupi ni kwamba Uislamu unakataa ubaguzi, unatoa mwito wa kusaidiana kwa misingi ya kheri na uadilifu, unaikubali haki popote ilipo na unawataka wafuasi wake wafungue nyoyo kwa watu wote kwa mapenzi na Ikhlasi.

Huu ni) upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu.

Ni dini ya haki ambayo inautwaharisha moyo na akili kutokana na uchafu; na wala sio kuzama katika maji, (ya kubatiza) kama wanavyofanya Wakristo.

Muhyiddin Ibnul-Arabi katika tafsir yake anasema: "Hakika kila mwenye madhehebu na itikadi anapambika na itikadi yake, dini na madhehebu yake. Wenye kuabudu kutokana na mila wanapambika na pambo la kiongozi wao. Na wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wanapambika na pambo la Mwenyezi Mungu ambalo hakuna pambo zuri zaidi ya hilo na wala hakuna jengine baada yake!"

139.Sema: Je mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu? Na hali yeye ni Mola wetu na Mola wenu? Na sisi tuna vitendo vyetu, nanyi mna vitendo vyenu; na sisi tunamfanyia Ikhlas yeye.

140.Au Mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-haq na Yaqub na wajukuu (zake) walikuwa Mayahudi au Manaswara? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichaye ushahidi alio nao • utokao kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye

200

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

kughafilika            na

mnayoyafanya.

hayo

141.Huo ni umma uliokwishapita. utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma wala hamtaulizwa              waliyokuwa

wakifanya.

JE MNAHOJIANA NASI JUU YA MWENYEZI MUNGU?

Aya 139-141

MAANA

Yamekwishatangulia maelezo katika Aya ya 92-96 kwenye kifungu cha 'Maslahi ndio sababu', kwamba Mayahudi walimpinga Mtume kwa ajili ya masilahi yao na mali waliyokuwa wakiichuma kwa njia ya riba na utapeli.Vile vile pombe, kamari na mengineyo yaliyoharamishwa na Uislamu. Na walimwambia Mtume: "Wewe siye Mtume kwa sababu Mwen-yezi Mungu hapeleki Mtume asiyekuwa Myahudi". Yaani wanadai kwamba Mwenyezi Mungu ni wao peke yao na kwamba yeye ni Mungu wa kabila na sio Mungu wa Ulimwengu.

Vile vile viongozi wa kikristo na mamwinyi wa kiquraishi walimpinga Mtume kwa kuhofia vyeo vyao na masilahi yao. Wakatoa sababu za uongo, kama walivyotoa Mayahudi. Wakristo walisema kama ilivyoelezwa katika tafsiri mbali mbali: "Lau Mwenyezi Mungu angelituma Mtume, basi angelikuwa katika kabila letu sio mwarabu." Ama mamwinyi wa kikuraish, nao walisema: "Lau Mwenyezi Mungu angelipeleka Mtume kutoka katika kabila la Waarabu basi angelimtuma kutoka katika tabaka la kitajiri lenye nguvu; kama ilivyoonyesha Aya hii:

"Na walisema: Kwa nini hii Qur'an haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?". 36

(43:31)

201

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

"Au (mbona) hakuangushiwa hazina (ya mali); au (kwa nini) asiwe na bustani ale katika hiyo?

(25:8)

Kila kitu kinaweza kuwa na mjadala na hoja; hata kuweko Mwenyezi Mungu pia; isipokuwa kitu kimoja tu, hakiwezi kuwa na ubishani milele kwa wale wanaomjua Mwenyezi Mungu, nacho ni kuihusisha rehema ya Mwenyezi Mungu na neema Yake kwa watu fulani tu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Je wao wanaigawa rehema ya Mola wako?..."

(43:32)

Kwa hivyo ndio Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kuwaambia wale waliokanusha.

"Je mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu?" Na hali nyinyi mnajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi anayestahiki Utume na asiyestahiki! Basi msimwingilie Mola wenu, ni juu yetu sisi na nyinyi kuikubali hukumu Yake sio kufanya mjadala katika matakwa Yake na hiyari Yake. Hayo ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hali Yeye ni Mola wetu na Mola wenu."

Na sisi tuna vitendo vyetu; na nyinyi mna vitendo vyenu.

Kauli hii ni sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Mna dini yenu nami nina dini yangu".

(109:6)

Yaani athari ya ugomvi wenu katika khiyari ya Mwenyezi Mungu ya kunineemesha mimi, itawarudia nyinyi peke yenu; kama vile ambavyo madhara ya ukafiri yanamrudia kafiri na manufaa ya imani yanamrudia mumin.

202

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

Na sisi tunamfanyia Ikhlasi Yeye tu. Sio nyinyi kwa sababu mnamhukumu Mwenyezi Mungu na mnataka afanye vile mtakavyo nyinyi. Ama sisi mambo yote tunamwachia Yeye na tunakubali hukumu Yake.

Je mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Ishaq na Yaqub na wajukuu (zake) walikuwa Mayahudi au Wakristo.

Hayo yanaungana na "Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu?" Maana yake ni jambo gani kati ya mawili mnaloling'ang'ania? Je ni kusema kwenu kwamba Mwenyezi Mungu hamtumi Mtume mwarabu au ni kuwa mko kwenye dini ya Ibrahim na watoto wake na wajukuu zake? Mking'ang'ania jambo la kwanza basi Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi anapouweka ujumbe wake. Na kama mking'ang'ania jambo la pili, basi Ibrahim aliachana na dini zote za upotofu akashikamana na dini ya haki. Hakuwa Myahudi wala Mkristo. Kwani dini hizo zilizotokea baada yake na baada ya watoto wake na wajukuu zake. Kwa hiyo kauli yenu ni batili haina hoja.

Qur'an inatuongoza katika ubishani huu kwenye mfumo ambao unatakikana tuufuate kwa kutegemea mantiki ya kiakili yatakayowakinaisha wote wenye akili.

Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?

Tumetangulia kueleza kuwa Mayahudi na Wakristo, kila kundi lilisema ndilo linalostahiki utume; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume Wake Mtukufu kuwajibu kwa kauli Yake: Je nyinyi mnajua zaidi mahali alipouweka ujumbe Wake au ni Yeye? Ujumbe ni wa Mwenyezi Mungu na unatoka kwa Mwenyezi Mungu, vipi mnataka kumchagua nyinyi? Je, nyinyi ni mawasii wa Mungu? Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo kabisa. Je, kuna mjinga zaidi ya asiyejua kitu amwambie mgunduzi wa chombo cha anga za juu kuwa mimi ninajua zaidi kuliko wewe?

Sijaona kauli iliyo fasaha zaidi ya kumfanya mtu kuwa mjinga kuliko kauli hii ya Mwenyezi Mungu (Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?) Tunamtaka maghufira Mwenyezi Mungu na kumtaka hifadhi kutokana na wanayoyasema na wanavyofanya wabatilifu:

Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichae ushahidi alionao utokao kwa Mwenyezi Mungu?

Yaani enyi Mayahudi na Wakristo, ushahidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mmeusoma katika Tawrat. Nao ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

203

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza

2 Sura Al-Baqarah

atatuma Mtume mwarabu kutoka katika kizazi cha Ismail (a.s.), lakini pamoja na hayo mmeuficha ushahidi mkamkosea Mwenyezi Mungu kwa kukigeuza Kitabu chake kwa batili na kuipinga haki. Kwa hiyo mnapasa laana na adhabu.

Huo ni umma uliokwishapita. utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mtakayoyachuma.

Aya hii imekwishatangulia katika Aya ya 134 herufi kwa herufi. Huko imebainisha kwamba Ikhlas ya Ibrahim (s.a.w.) na utukufu wake hauwezi kuwafaa nyinyi na kitu chochote. Hapa imekuja kwa kubainisha kwamba amali ya Mayahudi na Wakristo haiafikiani na itikadi ya Ibrahim na amali yake. Kwa hiyo madai yao kwamba wao wako kwenye mila ya Ibrahim ni uwongo na uzushi. Hayo tumeyazungumza katika tafsir ya Aya ya 48.

USHAHIDI

Ni wajibu kwa kila mtu aliyebalehe mwenye akili kuitikia mwito wa kutoa ushahidi; wala haifai kwake kukataa bila ya udhuru. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na mashahidi wasikatae wanapoitwa".

(2:282)

Imam Jaafar Assadiq amesema: "Anapokuita mtu ili ushuhudie juu ya deni au haki yoyote usichelewe."

Jukumu la kuchukua ushahidi linawajibisha kuutoa na ni haramu kuuficha. Mwenyezi Mungu anasema:

"Wala msifiche ushahidi na atakayeuficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini..."

(2:283)

Amesema Imam Assadiq (a.s.) "Mwenye ushahidi asikatae kuutoa atakapotakiwa na atoe nasaha wala asilaumiwe".

204

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Ndio, inawezekana kuacha kutoa ushahidi kwa kuhofia madhara au kumhofia mwingine asiyekuwa na hatia. Kwa sababu hakuna kudhuriana katika Uislamu kutokana na Ijmai na Hadith mahsus.

WENYE KUFANYA IKHLAS

Uislamu unawahoji wabatilifu, unawalaumu kwa kiakili na dhamiri. Vile vile unawanasihi kwa uzuri na kuwaamrisha mema, lakini hauwachukulii hatua nyingine zaidi ya mawaidha mazuri isipokuwa kama wakipetuka mpaka, wakafanya uadui kuwapoteza watu wema na kuipoteza haki kwa uzushi na propaganda za uongo. Wakifanya kitu katika hivi itapasa kuwatia adabu. Ameyabainisha Mwenyezi Mungu hayo katika Aya nyingi, kwa mfano:

..."Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa madhalimu."

(2:193)

"Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotoka ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu yote ni kwa Mwenyezi Mungu; basi atawaambia mliyokuwa mkiyatenda."

(5:105)

="ltr">Aya hii imekwishatangulia katika Aya ya 134 herufi kwa herufi. Huko imebainisha kwamba Ikhlas ya Ibrahim (s.a.w.) na utukufu wake hauwezi kuwafaa nyinyi na kitu chochote. Hapa imekuja kwa kubainisha kwamba amali ya Mayahudi na Wakristo haiafikiani na itikadi ya Ibrahim na amali yake. Kwa hiyo madai yao kwamba wao wako kwenye mila ya Ibrahim ni uwongo na uzushi. Hayo tumeyazungumza katika tafsir ya Aya ya 48.

USHAHIDI

Ni wajibu kwa kila mtu aliyebalehe mwenye akili kuitikia mwito wa kutoa ushahidi; wala haifai kwake kukataa bila ya udhuru. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na mashahidi wasikatae wanapoitwa".

(2:282)

Imam Jaafar Assadiq amesema: "Anapokuita mtu ili ushuhudie juu ya deni au haki yoyote usichelewe."

Jukumu la kuchukua ushahidi linawajibisha kuutoa na ni haramu kuuficha. Mwenyezi Mungu anasema:

"Wala msifiche ushahidi na atakayeuficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini..."

(2:283)

Amesema Imam Assadiq (a.s.) "Mwenye ushahidi asikatae kuutoa atakapotakiwa na atoe nasaha wala asilaumiwe".

204

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza                                              2 Sura Al-Baqarah

Ndio, inawezekana kuacha kutoa ushahidi kwa kuhofia madhara au kumhofia mwingine asiyekuwa na hatia. Kwa sababu hakuna kudhuriana katika Uislamu kutokana na Ijmai na Hadith mahsus.

WENYE KUFANYA IKHLAS

Uislamu unawahoji wabatilifu, unawalaumu kwa kiakili na dhamiri. Vile vile unawanasihi kwa uzuri na kuwaamrisha mema, lakini hauwachukulii hatua nyingine zaidi ya mawaidha mazuri isipokuwa kama wakipetuka mpaka, wakafanya uadui kuwapoteza watu wema na kuipoteza haki kwa uzushi na propaganda za uongo. Wakifanya kitu katika hivi itapasa kuwatia adabu. Ameyabainisha Mwenyezi Mungu hayo katika Aya nyingi, kwa mfano:

..."Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa madhalimu."

(2:193)

"Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotoka ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu yote ni kwa Mwenyezi Mungu; basi atawaambia mliyokuwa mkiyatenda."

(5:105)

Na Aya nyingine ni hii tuliyonayo: "Na sisi tuna vitendo vyetu nanyi mna vitendo vyenu na sisi tunamfanyia Ikhlasi Yeye"

205