JANNAT na JAHANNAM

    ( Peponi na Motoni )

 

              Kitabu hiki kimekusanywa na kutarjumiwa na:    

             Amiraly  M.  H.  Datoo

                                            Bukoba – Tanzania                              

 

YALIYOMO

1. JANNAT.... 3

UTANGULIZI. 3

1. Imani na matendo mema. 11

2.  Taqwa.. 11

3.  Ihsani na matendo mema. 12

4.  Jihadi na kuwa shahidi... 12

5.   Kutokufuata nafsi yake. 12

6.  Kushindania katika kuleta Imani... 12

7.   Hijrah na Jihad.. 12

 

8.   Subira na Ustahimilivu wakati wa shida... 12

9.  Kuwa imara katika Dini.. 13

10.   Kumtii Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w... 13

11.  Ikhlas (Uhalisi ).. 13

12.  Ukweli.. 13

13.  Kujitakasisha mwenyewe... 14

14.  Kutoa katika njia ya Allah swt  na kuomba Tawba.. 14

15.  Hofu ya Allah swt. 14

16.  Tawalla na Tabarra.. 15

17.   Kudumisha Sala... 15

 

2.  JAHANNAM.. 16

1. Kufr na Nifaq.. 22

2. Kuwazuia wale wanaotenda kazi katika njia ya Allah swt.. 22

3.   Kutomtii Allah swt. 23

4.   Kudhihaki Ayah za Allah swt.. 23

5.   Kutotumia viungo vya mwili dhidi ya Allah swt.. 23

6. Kumtii na kumfuata Shaitani... 24

7.  Majivuno.. 24

8.  Kuwaomba msaada Wadhalimu.. 24

9.  Kuisahau Akhera.. 25

10.  Kuiabudu Dunia.. 25

 

11.  Kulimbikiza utajiri wa mali na mapesa. 25

12.  Kuikimbia Jihadi... 26

13.   Kumwaga damu ya mtu asiye na hatia. 26

14.  Kupuuzia na kutokusali Sala.. 27

15.  Kutokutoa Zaka.. 27

16.  Kudhulumu haki za yatima.. 28

17.  Kutoza na kupokea riba. 28

18.   Kutokushukuru neema za Allah swt.. 28

19. Kuibia katika  mzani... 29

20.   Kuzitafuta aibu za mtu na kumsengenya.. 30

21.   Ufujaji wa Neema za Allah swt... 30

 

 

22.  Kosa na Dhambi... 3123.   Kuvuka mipaka iliyowekwa na Allah swt. 31

Mtu kuchuma mali na kurundika.. 31

3.  ADHABU ZA KABURINI.... 33

     Marejeo kuhusu Jannat  na Jahanna         ..…….53

1. Qur’ani Tukufu. 53

2. Nahjul Balagha.. 53

3.  Sahifa-i-Sajjadiyah.. 53

4. ….. 53

NDOTO YA Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. 54

Ayah za  Qur'an Tukufu zizungumziazo Jannat.. 55

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

 

 

 


                                      1. JANNAT

                                                ( Peponi )

 

Sunday, February 03, 2002

UTANGULIZI

 

Ingawaje Qur’an Tukufu inatujulisha vya kutosha kuhusu Jannat (Pepo ) na  Jahannam ( Motoni ), vile vile tunapata habari zaidi kutoka Ahadith Qudsi zilizoletwa na Malaika Jibraili a.s. kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. ambaye ananakiliwa na Imam Ali a.s. na Maimamu Kumi na moja a.s. waliobakia. Mtume s.a.w.w. wakati wa Me’raj aliweza kuona na kutembea Peponi, kula matunda ndani mwake na kuangalia yale yaliyokuwamo. Vile vile alitembelea jahannam au Motoni ambamo aliweza kujionea vile wahalifu walivyokuwa wakiadhibiwa kwa madhambi yao.

 

Al Tirmidhi na Abu Daud wananakili Ahadith Qudsi ifuatayo kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w.:

Allah swt alipoumba Jannat na Jahannam, alimtuma Malaika Jibraili a.s. kwenda Jannat, akisema, “Angalia ndani mwake kile nilichokiwatengenezea wakazi wa humo.” Malaika Jibraili a.s. alikwenda akaangalia vizuri na kwa makini, na aliporudi kwa Allah swt alisema, “Kwa utukufu wako naapa kuwa hakuna atakayeisikia illa atatamani kuingia humo.” Kwa hayo Allah swt alizungushia vizuizi na magumu mbalimbali, na alimwamrisha Malaika Jibraili akaangalie vizuizi na magumu yaliyozungushiwa. Malaika Jibraili a.s. aliporudi baada ya kuyaangalia kwa makini, alimwambia Allah swt, “Kwa Utukufu wako, Naapa na kuhofu kuwa hakuna hata mtu mmoja ambaye ataweza kuingia ndani mwake.”  Allah swt alimwambia, “Sasa nenda kaangalie Jahannam na yale niliyowaandalia wakazi wake.” Malaika Jibraili a.s. alikwenda na kuona tabaka moja baada ya nyingine. Aliporejea akasema,”Kwa utukufu wako, hakuna hata mtu mmoja atakayetamani kuingia ndani humo atakapoisikia.” Hapo Allah swt aliamrisha kuzungushiwa vivutio na vipotoshavyo, na kumwamuru Jibraili a.s. kurudi kuangalia tena. Aliporudi Jibraili a.s. alisema, “Kwa kiapo cha Utukufu Wako! Hakika ninahofu kuwa hakuna mtu atakayeweza kujiepusha kuingia ndani humo.”

 

Sasa tujaribu kuchunguza na kuelewa zaidi kuhusu sehemu hizi mbili : Jannat na Jahannam

Article I.                        

1). Maelezo juu ya Jannat ( Peponi )

Jannat ni mahala ambapo kunatofautiana hali ya starehe, pema na furaha za kila aina. Si kama Jahannam ambapo ni shimo refu mno la moto mkali, Jannat ni eneo ( tambarare au imeinuka kidogo), kiasi kwamba hata mito yake haivunji kuta zake bali inabubujika vyema. Kuna Jannat  au Bustani zaidi ya moja. Ayah ya Qur’an ya Surah Al-Rahman (Sura 55 ) inatujulisha neno moja Mudhamutan ambayo inaelezea Bustani mbili zilizo za rangi zilizoiva za kijani, ambapo Ayah ya 62 ya Sura hiyo hiyo inatuambia “mbali na Bustani hizi mbili zipo Bustani zingine mbili,” zikijumlisha kuwapo kwa Bustani nne kwa ujumla katika Akhera. Bora ya Jannat ni  Bustani ya Eden, orjanat ‘adan.  Katika kitabu Lisan al-‘Arab, j.13, Uk. 99, sisi twaambiwa kuwa Jannat  inamaanisha : Bustani ya miche ya matunda mbalimbali.

Jannat ‘Adan imeelezwa katika :

AYAH

SURAH

 

AYAH

SURAH

72

Al-Tawbah , 9

 

31

Al-Kahf, 18

23

Al-Ra’d,  13

 

61

Al-Maryam, 19

31

An-Nahl, 16

 

76

Ta-Ha , 20

33

Al-Fatir, 35

 

50

As-Sad, 38

8

Al-Ghafir, 40

 

12

Al-Saff,  61

8

Al-Bayyinah, 98

 

 

 

 

Katika ukurasa wa 279, juzuu 13 ya kitabu Lisan al-‘Arab, twaambiwa kuwa Jannat ‘Adan inamaanisha kuwa “Mahala pa milele”, Bustani ya Kati (al-awsat).”  Kitabu hichohicho kinatutambulisha katika uk.427, juzuu ya 7 kuwa al-awsat inaweza kumaanisha kuwa : iliyo Bora.  Hakuna shaka kuwa tutaweza kuona na kupata maelezo na mafafanuzi zaidi juu ya Jannat ‘adan  kuliko kusema tu al-firdows, Jannat au Peponi, katika Qur’an Tukufu. Hali hii inatuacha sisi kwa kudadisi kuwa mahala bora kabisa, na iliyokuu, inayolengwa katika Jannat zote ni Jannat ‘Adan.

 

Peponi, au al-Firdows kama vile inavyoitwa katika Kiarabu, ni neno la kuazimwa. Waarabu aliowatokezea Mtume Muhammad s.a.w.w. walikuwa hawana itikadi ya maisha baada ya kufa, na Jannat na Jahannam. Na kwa hakika swala hili lilikua gumu kwake Mtume s.a.w.w. alipoanza kuhubiri. Sura-i-Yasin,36, Ayah ya 78 inatuelezea

Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake – akasema: “Nani atakaihuisha mifupa na hali imesagika ?”

 

Vile vile Qur’an inatuambia katika, Sura  Ya-Sin, 36; Ayah 79:

Sema: “Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya ) kuumba”

 

Hata mwandishi wa kazi nzuri kabisa za Kiarabu, Lisan Al-‘Arab, hanauhakika iwapo neno hili la Firdaws limeazimwa kutoka Kilatini au Kiajemi, au ni al-Majlisi, kama mwandishi huyo anavyokubali katika uk. 91, Juzuu ya 8 kati ya Juzuu 110 ya Encyclopedia – bila ya kuihesabu Juzuu ya Sifuri – ijulikanayo kwa jina la Bihar al-Anwar.  Wazo la tatu, ambalo linaweza kuwa sahihi zaidi ni kwamba inawezekana uasili wake ukawa Babilonia. Neno lingine lililotumika katika Qur’an Tukufu ni Jannat au Bustani. Lakini kwetu sisi Jannat inamaanisha sana kuliko kutaja Bustani au shamba la miti ya matunda. Waarabu kamwe hawakuwa na tabia ya kuishi katika mshamba yao ya miti ya matunda.

 

Majumba yao yaliyokuwa yamejengwa kwa udongo uliochomwa au uliokaushwa kwa jua, walikuwa wakiishi kwa kujumuika katika mashamba yao kama ilivyo katika swala la Jannat.  Kuwapo kwa Mayahudi wengi katika mji wa madinah ( walikuwa wengi zaidi kwa kutokana na hali ya hewa ) na wakazi wa Makkah waliwakubalia Mayahudi kuchangia katika baadhi ya maneno kama hayo. Jahannam linatokana na neno la Kihibrew Gehinnom (kwa mujibu wa Oxford English Dictionary (GED), jina lake kwa kikamilifu katika Kihibrew ni ge hen Hinnom, Bonde la mto wa L - Linnom, ikielezea mahala karibu na Jerusalem ambapo kwa mujibu wa Jeremiah 19 : 5, watoto walichomwa moto kwa kutolewa mhanga kwa Baal, mungu mwenye uwezo wa kuzalisha wa makafiri wa Canaaniti au kwa Molech (Moloch).  Kwa habari zaidi unaweza kurejea II Wafalme 23:10 na Jeremiah 32:35 katika Biblia ) (Kilatini Zehenna), Jahannam, ni lingine.

 

Swala hili linaweza kujitosheleza kuandika kitabu kikubwa sana ambapo si makusudio yetu hapa, hivyo kwa mukhtasari sana tuangalie milango yake ya kuingilia kama ilivyoonwa na Mtume Muhammad s.a.w.w. ambaye ananakiliwa katika Bihar al-Anwar j. 8, uk. 144, akielezea kama ilivyofikishwa na Abdullah ibn Mas’ud kama ifuatavyo :

“Wakati Allah swt aliponiruhusu kwenda Jannat, Jibrail a.s. aliniambia, “Mimi nimeamrishwa kukutembeza na kukuonyesha yote yaliyomo ndani mwa Jannat na Jahannam.”  Hivyo mimi niliiona Jannat na baraka na mema yote yaliyokuwamo na vile vile nimeiona Jahannam pamoja na mateso yote yaliyomo. Jannat  inayo milango minane, kila mlango inayo misemo minne, ambayo kila mojawapo ni bora kuliko ulimwengu mzima na kile ambacho kipo ndani mwake ni kwa ajili ya wale wanaotafakari na kufuatilia kwa kutenda kimatendo.  Na Jahannam inayo milango saba, na kila mlango inayo misemo mitatu, ambapo kila msemo ni afadhali kuliko dunia yetu hii na kilichomo ndani mwa kila msemo ni kwa ajili ya kutafakari na kuyatendea kazi. Malaika Jibraili a.s. aliniambia,  “Ewe Muhammad ! Soma yaliyoandikwa katika milango hizi !” Na hivyo mimi niliyasoma yote.

 

Milango ya Jannat

 

Katika mlango wa kwanza wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia riziki ni nnne : kutosheleka, kutumia katika njia sahihi, kukana kisasi na kufanya uhusiano pamoja na watu waliookoka yaani katika njia nyoofu.

 

Katika mlango wa pili wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia furaha katika maisha ya Aakhera ni nnne : Kuonyesha huruma kwa mayatima, kuwawia wema wajane, kuwasaidia wacha-mungu katika kufanikisha malengo yao na kuwaangalia na na kuwasaidia masikini na wasiojiweza.

 

Katika mlango wa tatu wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia siha njema katika maisha haya mafupi ni nne : Kuongea kwa uchache, kulala kidogo, kutembea kidogo na kula kidogo.

 

Katika mlango wa nne wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wageni wake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa jirani zake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wazazi wake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe ni mwenye kusema mema au anyamaze kimya.

 

Katika mlango wa tano wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; Yeyote yule ambaye hataki kunyanyaswa siku ya Qiyamah, basi naye asimnyanyase mtu yeyote; Yeyote yule ambaye hataki kusengenywa siku ya Qiyamah, basi naye asimsengenye mtu yeyote; Yeyote yule ambaye hataki kudhalilishwa siku ya Qiyamah, basi naye asimdhalilishe mtu yeyote; Mtu yeyote yule ambaye anataka kujishikiza kwa umadhubuti katika maisha haya mafupi na yale ya Aakhera, basi lazima atoe shahada kuwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi.

 

Katika mlango wa sita wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kaburi lake liwe pana na lenye nafasi ya kutosha (kutombana) basi ajenge Misikiti; Yeyote yule anayetaka wadudu na minyoo ya ardhini wasimle, aifanye Misikiti iwe nyumba yake ( yaani awe akiizuru kwa mara nyingi kama kwamba anaishi humo ); Yeyote yule anayetaka kubakia freshi, (yaani asipate shida na taabu za kiu katika maisha haya na ya Aakhera ambapo kila mtu atakuwa akitafuta hata tone moja la maji ) basi awe akifagia Misikiti; na yeyote yule amabye anataka kuiona nafasi yake hapo Jannat basi atengeneze sakafu na kuweka mazulia au mikeka katika Misikiti.

 

Katika mlango wa saba wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi.  Moyo halisi unapatikana kwa mema manne : Kuwatembelea wagonjwa, kutembea nyuma ya jeneza, kununua sanda kwa ajili ya maiti na kulipa madeni.

 

Katika mlango wa nane wa Jannat kumeandikwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kuingia katika milango hii basi lazima awe na sifa nne zifuatazo : Ukarimu, adabu njema, moyo wa kujitolea na kujiepusha katika kuwadhuru waja wa mungu.

 

Al-Majlisi, katika uk. 131, j. 8, ya kitabu chake kiitwacho Bihar al-Anwar, ananakili uk. 39, j. 2, ya AI-Kaisal,ambapo Ubayy anamnakili Sa’d anayemnakili al-Barqi akimnakili babake akimnakili na kuthibitisha kuwa ibn al-Nasr akimnakili ‘Amr ibn Shemr akimnakili Jabir ibn Abdullah al-Ansari akimnakili Imam Ja"fer al-Sadiq a.s. akisema, "Fikirieni kuhusu Allah swt kwa bora ya mawazo yenu, na mjue kuwa Jannat  inayo milango nane na upana wa kila mlango ni upana wa miaka arobaini.

 

Katika hotuba mbalimbali katika Nahjul Balagha, Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anazielezea kwa undani na mapana sana kuhusu Jannat  na Jahannam; hapa ninawadondosheeni machache vile anavyoelezea  Jannat :

“Kipeo cha furaha na mustarehe na pongezi au hongera inatofautiana sana baina ya mtu mmoja na mwingine au mahala moja na nyingine; starehe zake kamwe haziishi; wale waliobahatika kuingia na kuishi humo kamwe hawafukuzwi au kuhamishwa, na kamwe hawapatwi na uzee, na kamwe hakuna anayeambukizwa ugonjwa wa ubakhili  (Hotuba nambari 85). Wao hawajivuni wala kujigamba wala kamwe hawazaliani watoto. (Hotuba nambari 161).

 

Hakuna anayeingia Jannat isipokuwa wale ambao wanaouelewano mwema (na kufuata nyayo zao) pamoja na Ma-Imamu a.s. kutokea kizazi cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  na ambao ndio waliothibitishwa ndivyo katika Siku ya Qiyamah  (Hotuba nambari 152).

 

Iwapo utaingiwa na imani kwa  kile utakachoelezewa kuhusu Jannat, basi nafsi yako itajitoa mbali na mavutio ya macho na mapotoshi ya duniani humu (ambayo yanafurahisha macho tu ) utashangazwa kuona vile miti ilivyopangwa katika mistari na mizizi yao ikiwaimefukiwa katika marundo ya maski (mishki) katika mwambao wake. Matunda yao yanaweza kuchumwa kwa urahisi. Wakazi wake wanakarimiwa kila wakati kwa vinywaji vya asali halisi na mivinyo mbalimbali, ambayo haileweshi ulevi, wakazi wa humo watakuwa wakistarehe katika majumba yao ya fakhari. Itakuwa imeezekwa kwa ‘Arsh-i-Ilahi (mbingu ya Allah swt ); starehe zake ndizo nuru, na wakazi ndani ya Jannat huwa mara kwa mara wakitembelewa na Malaika wa Allah swt.

 

Raha na furaha kubwa kwa ajili ya wakazi wa Jannat  itakuwa ni kule kuwa karibu na Allah swt na watakuwa na mawasiliano naye kwa ukaribu zaidi. Allah swt atakuwa akiongea nao kama vile mwenyeji anapokuwa akizungumza na wageni wake.

 

Katika uk. 114, j. 8, ya kitabu chake Sahib, al-Bukhari anamnakili Ma’ath ibn Asad akimnakili Abdullah akimnakili Malik ibn Anas akimnakili Zayd ibn Aslam akimnakili ‘Ata ibn Yasar akimnakili Abu Sa’eed al-Khudri, Allah swt awe radhi nae, akimnakili Mtume wa Allah swt akisema kuwa Allah swt atawahutubia wakazi wa Jannat  kwa kusema : “Enyi watu wa Jannat ! nao watamjibu Allah swt kwa kusema, “Labbayk Mola wetu! Kwa furaha Yako!”

 

Na hapo ndipo atakapowauliza, “Je mmetosheka na kuridhika ?” Nao watamjibu, “Je kweli itawezekanaje sisi tusitosheke na kuridhika wakati ambapo ulichotupatia sisi haujawapatia viumbe vyako vingine ?”  Hapo atasema, “Mimi nitawapatieni mema zaidi ya hayo,” nao watasema, “Ewe Mola wetu ! Je ni jambo gani lililobora zaidi ya hayo ?”  Allah swt atasema, “Mimi nitawateremshieni rehema na baraka zangu ziwe juu yenu, na kamwe sitawaghadhabikieni.”

 

Mwandishi huyu huyu, katika Sura juu ya Tawhid, anamnakili Muhammad ibn Sinan akimnakili Fulayh akimnakili Hilal akimnakili ‘Ata ibn Yasar akisema kuwa siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema hadith na katika kikao icho alikuwapo bedui mmoja alikuwapo hapo. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema kuwa Bedui mmoja miongoni mwa wakazi a Jannat  alimwomba ruhusa Allah swt kwa ajili ya kutaka kulima ardhi, ambapo Allah swt alimwuliza, “je haukupata chochote kile ulichokihitaji (kutokea miti na mimea ya humu Jannat ?). ”

 

Mbedui huyo alijibu, “Naam (nimepata kila kitu nilichokuwa nimekihitaji, lakini bado ninapendelea kulima ardhi.”  Kwa hayo allah swt alimruhusu kufanya hivyo; basi alipanda mbegu ardhini na katika sekundi chache tu zikaota katika miti na kukomaa na kutoa matunda mengi mno kama milima.  Kwa hayo ndipo Allah swt alipomwambia, “Chukua, Ewe mwana wa Adam, kwani hakuna kinachoweza kukuridhisha wewe!”  Kwa kusikia hayo, yule Mbedui aliyekuwa ameketi anayasikia hayo, akainuka na kusema, “Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mtu huyo bila shaka alikuwa akitoka Quraish au kutokea Ansar, kwani wao ndio wakulima ambapo sisi Mabedui si wakulima.”  Kwa kuyasikia hayo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alionyesha tabasamu.

 

Tabia na shauku ya kukusanya na kulimbikiza ipo katika mishipa ya wanadamu, al-Tirmithi, katika uk. 89-90, J. 2, ya kitabu chake Jami’, anainakili hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambapo anawajulisha Ma-Sahaba kuwa wakazi wa Jannat  watakuwa wakijumuika kila mara humo katika karamu mbalimbali kama ukumbusho wao walivyokuwa wakizipitisha Ijumaa wakati wakiwa humu duniani, nao watakuwa wakienda bazaar (masoko au gulio) ambapo watakuwa wakijichagulia nguo, vito vya thamani au chochote kile watakachokuwa wakikitaka na kuvichukua katika makazi yao.

 

“Bustani ya Eden,” yaani Jannat ‘Adan, imetajwa katika Qur’an katika mahala pengi zaidi ya moja.  Kwa mujibu wa Ibn Mas’ud, ni sehemu ambayo iliyopo katikati ya  Jannat . Kwa mujibu wa al-Dhahhak, ni mji uliopo ndani ya mji, ambamo wakazi wake ni Mitume a.s., Mashahidi, na ma-Imamu a.s. watakuwa wakiishi huku wamezungukwa na wengine. Majengo yake yamejengwa kwa jawhari, Lulu, na vito vyenye thamani, dhahabu, almasi,fedha na kuvikwa kwa muski, na, kwa mujibu wa Muqatil na al-Kalbi, hewa nzuri na baridi itakuwa ikipepea kutokea ‘Arsh ikiitumbukiza katika (kama ukungu wa ) mushk nyeupe. Hata Ibilisi, shaytani, aliwaonea wivu wanaadamu kwa sababu ya Bustani ya ‘Eden.

 

Katika ukurasa wa  115 wa kitabu Al-Mahasin, Muhammad ibn Qays anamnakili Imam Abu Ja’fer al-Baqir a.s. akisema kuwa, “Siku moja Shaitani alimwona Mtume Nuh a.s.akisali, basi Shaitani alimwonea wivu Mtume Nuh a.s. na hakuweza kujizuia, akasema. “Ewe Nuh ! Allah swt aliyetukuka, Mkuu, amejenga mwenyewe Bustani ya Eden , akapanda miti na kutiririsha mito ndani mwake. Na kisha akaangalia mandhari hayo na kusema, “Kwa hakika waumini na waongofu ndio washindi ! La, Kwa Utukufu wangu ! Mtu mwenye utovu wa adabu (mwenye madhambi) kamwe hataingia kuishi humu.’”

 

Aina za vyakula na vinywaji vinazungumziwa na kutajwa katika Qur’an na Sunnah, na vile vile hur al-‘ayn wanawake wenye macho makubwa ndio watakaokuwa wake wa wale waliobahatika, lakini hapa mtu anaweza kujiuliza swala bila ya kujizuia : Je ni kitu gani kile kitakachowafurahisha mno wakazi wa Jannat ?  Je yatakuwa ni vinywaji, vyakula, sauti kama za muziki zitokanazo na matawi na majani ya miti ya Jannat , au nyimbo zitakazokuwa zikiimbwa na hawa hur al-‘Ayn ama mmoja mmoja au kimakundi, zitakazokuwa zikimsifu Allah swt na kumtukuza ? Katika Tafsiri ya Tafsir, al-’Ayyashi, kama ilivyoandikwa katika uk. 139, J. 8, ya Bihar al-Anwar, anamnakili Abu Baseer akimnakili Abu Abdullah Imam Ja’fer al-Sadiq a.s. akisema, ‘Wakazi wa Jannat watastarehe vyakula na vinywaji zaidi kuliko masuala ya kujamiiana.”

 

Katika ukurasa wa 438-439 ya kitabu cha Ali ibn Ibrahim Tafsir, kama ilivyonakiliwa katika uk. 120-121, J. 8, ya al-Majlisi Bihar al-Anwar, imeelezwa kuwa Ibn Abu ‘Umayr anamnakili Abu Busayr kuwa yeye alimwuliza mara moja Abu Abdullah Imam Ja’fer al-Sadiq a.s. kuchochea hisia zake za matamanio kuhusu Jannat , Imam a.s. alimjibu, “Ewe Abu Muhammad ! Je kunaweza kuhisiwa manukato mazuri kabisa ya Jannat  hata kutokea mwendo wa maelfu ya miaka, na makazi patakatifu katika Jannat  ni yale ambapo Majini  na wanadamu watakwenda; humo watahudumiwa vyakula na vinywaji vya kila aina bila ya kupungua au kuisha kwa kitu chochote kile.  Bora miongoni mwa wakazi za Jannat  ni yule ambaye, atakapoingia katika mabustani yake, ataona mabustani matatu ( na wala si bustani moja ) iliyojaa wanawake, wajakazi, mito na matunda ya kila aina ambayo yatafurahisha macho na moyo wake kwa furaha isiyoelezeka. Mtu huyo atakapokamilisha kumshukuru na kumtukuza Allah swt, yeye ataambiwa kukiinua kichwa chake kwa ajili ya kuiangalia Bustani ya pili, kwani kutakuwamo yale yasiyokuwamo katika Bustani ya kwanza. Kwayo, atamsifu na kumtukuza Allah swt na kumwomba, “Ewe Mola wangu ! Ninakuomba unipe Bustani hii (badala ya ile ya kwanza)!  Kwa hayo Allah swt atamwambia, Iwapo nitakupa Bustani hii, basi wewe utaanza kunitaka nikupatie nyingine badala ya hii !  Basi huyo mtu atasema, “Kwa hakika hii tu ndiyo ninayoihitaji, Ewe Mola wangu!”  Na wakati atakapoingia humo ndani, furaha zake zitaongezeka zisizo na kifani, na atamshukuru na kumsifu na kumtukuza Allah swt, na hapo ndipo milango itakapoamrishwa kufunguliwa na ataambiwa kuinua kichwa chake.

 

Pale Bustani ya milele itakapokuwa wazi mbele yake, yeye ataangalia mara kwa mara kama alivyokuwa ametaza hapo awali. Wakati furaha zake zitakapokuwa zimezidi kifani, atasema, “Usifiwe Ewe Mola wangu ! Kwa hakika sifa hazina kiwango cha kukusifu kwa yale yote uliyonijaalia : Bustani na kuniepusha na Jahannam ( Motoni ).”  Hapo, Abu Busayr hakuweza kujizuia kwa kuangua kilio, na alijikaza na akamwomba Imam a.s. amwelezee zaidi.  Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. akaendelea kumwambia, “Ewe Abu Muhammad! Katika kingo za mito ya Jannat kuna wanawake wanaowasubiri waume zao kama vile zilvyo miti iliyoota katika mstari. Pale atakapomchukua mmoja, basi mwingine atakuwa ameshawekwa kuziba pengo hilo.”

 

Abu Busayr akasema, “Niwe fidia kwako! Tafadhali sana naomba uniambie zaidi!”

 

Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. aliendelea kumwambia, “Mumin ataozeshwa kwa bikira mia nane, elfu nne tayyibs (ni wanawake waliokua ama hawakuolewa ambao ni wajane wacha-mungu wema au waliochiwa na waume zao) na hur al-‘Ayn wawili.”  “Bikira mia nane ?!” Abu Busayr alimwuliza Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. kwa mshangao mkubwa sana. “Naam. Yeye atawaona hivyo hivyo pale atakapojamiiana nao.”  “Maisha yangu yaweyametolewa kwa ajili yasko,” alisema Abu Busayr, “ Je hur al-‘Ayn wameumbwa kwa kitu gani ?” Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. alimjibu kuwa wameumbwa kwa mada ya Jannat iliyoumbwa, na kuongezea, “miguu yao itakuwa ikionekana hata kama kutavishwa mavazi sabini.”

 

Abu Busayr alimwuliza Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. ,”Maisha yangu yawe fidia kwako, je wanazungumza chochote huko ?”  Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. alimjibu, “Wao wanazungumza yale ambayo hakuna mwanadamu aliyewahi kuyasikia.”  Abu busayr aliuliza, “Je ni nini hayo ?”  Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. alimjibu, “ Sisi tutaishi milele na kamwe hatutakufa! Sisi ni wale waliobarikiwa, hivyo kamwe hatutahangaika na kutaabika ! Sisi ni wale tuishio na kamwe hatutatengana ! Sisi ni wale wenye furaha na kutosheka, hivyo kamwe hatuna mashitaka ! Habari njema kwa wale waliokuwa wameumbwa kwa ajili yetu, na habari njema kwa ajili ya wale tuliokuwa tumeumbiwa! Sisi ni wale ambao kama tungening’inia angani, basi nuru yetu ingeling’arisha kila sehemu .’”

 

Ibn Qawlawayh, na vile vile al-Majlisi ambaye katika uk. 143, J. 8, ya kazi yake Bihar al-Anwar, anamnakili Sa’d akimnakili Ibn ‘Eisa akimnakili Sa’ eed ibn Janah akimnakili Abdullah ibn Muhammad akimnakili Jabir ibn Yazid akimnakili Imam Abu Ja’fer al-Baqir (as) akiwanakili Mababu zake a.s. ( yaani ma-Imamu a.s.) wakisema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema, “Mitume yote imekatazwa kuingia Jannat kabla yangu, na mataifa yote yamekatazwa kuingia humo kabla ya waumini watufuatao sisi, sisi Ahlul Bayt a.s., kuingia ndani mwake.” Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amenakiliwa akisema, uk.139, J.8 ya Bihar al-Anwar, akisema, “Jannat  inayo milango sabini na moja ya kuingilia : Ahlul Bayt a.s. yangu na wafuasi wao wataingilia milango sabini, wakati ambapo watu wengine wataingilia mlango uliobakia.”

 

Furaha nyingine ya Jannat ni kwamba kule hakuna kuzeeka kwa wakazi wa Jannat , na kamwe hawatapatwa na maumivu ya aina yoyote yale, na kamwe hawatataka kujisaidia kwa choo ndogo au kubwa; na badala yake kile wakilacho kitatoka mwilini kama jasho lenye manukato mazuri mno. Hawatakuwa na ukiritimba wa aina yoyote ile na kamwe hawatanyimwa kitu chochote kile. Matamanio yao yatatimizwa, na furaha zao kamwe hazitaisha na kamwe hawatajisikia wanyonge wasio na raha. Tunamwomba Alah swt atuingize Jannat  bila ya kujali mema kiasi gani tufanyayo, kwani Yeye ndiye pekee wakutuhurumia na kutufanyia hisani. Yeye ndiye anayetujaalia moyoni mwetu moyo wa kufanya mema: Ni yeye pekee anayetuwezesha sisi kufanya mema, na ni Yeye pekee ambaye anakubalia mema yetu na kutulipa thawabu zake, kwani ni dhahiri kuwa sisi tusingaliweza kujifanyia mema kwa uwezo wetu wenyewe. Allah swt ndiye pekee chanzo cha wema na ndiye wema pekee.

 

Mwishoni, kila mtu anajawa na shauku ya kujiuliza vile Jannat  itakavyokuwa kwa ujumla. Kwa mujibu wa habari tulizozisoma hapo juu, kuhusu Jannat ‘Adnan  inaelezwa kuwa itakuwa ni mzunguko na Bustani ya Eden itakuwa katikati ikizungukwa na Bustani zinginezo za wale waliokuwa wafuasi na wapenzi wa ahlul Bayt a.s. ya wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuyafuata matendo yake,wakizungukwa na wale waliokuwa waaminifu kwao kwa maneno na vitendo, n.k. Iwapo utaendelea kutoka hoja hiyo, iwapo upeo wa matendo na malipo yako yatakavyokuwa kidogo, ndivyo atakapokuwa katika Jannat  na furaha zake. Ukiwa na daraja la juu basi utafaidika zaidi, na ikiwa daraja lako ni chini kidogo basi, na starehe za huko pia zitakuwa zimepungua kidogo. Uduara unamaanisha kudumu kwa milele. Bustani hiyo inadhaniwa kuwa ni duara, lakini Allah swt ndiye ajuaye zaidi.

 

Sababu zimfanyazo mtu kuingia Jannat   

1. Imani na matendo mema

Kwa hakika Imani na matendo mema ndiyo masuala bora kabisa na ambayo yanamletea furaha mtu na inasadikiwa kuwa ndiyo ufunguo wa Jannat   na baada yake sababu zote zitakazoendelea kuelezwa basi mutaona kuwa zote hizo ni matawi ya hoja hili na Allah swt pia anasema kuhusu Imani na Matendo mema kuwa mtu yeyote atakayetekeleza hayo humu duniani basi Allah swt lazima atamjaalia Jannat. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura  al-Baqarah ,2 , Ayah 82

Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio watu wa Jannat , humo watadumu.

 

2.  Taqwa

Taqwa inamaanisha kujiepusha yaani yale yote yaliyosemwa na Ahlul Bayt a.s. ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa ni halali basi ndiyo halali na yale yote yaliyosemwa ni haramu basi yawe ni haramu. Allah swt ametoa ahadi kuwa atakayeishi kwa Taqwa basi mahala pake patakuwa ni Jannat. Na hivyo ndivyo maana anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura  al-Maryam ,19 , Ayah 63 :

Hiyo ndiyo Jannat tutayowarithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu

 

Vile vile twaambiwa katika Qur’ani Tukufu , Sura  al-Hujurat ,49, Ayah 13 :

Enyi watu ! Hakika Sisitumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa na mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa  Allah swt ni  huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi….

 

3.  Ihsani na matendo mema

Yaani kuwafanyia watu mambo mema na matendo yetu yawe mema kwa ujumla na kwa hakika haya ndiyo mambo mema na bora kabisa na ndiyo sababu za kuingia Jannat. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maidah,5, Ayah 85 :

Basi Allah swt atawalipa, kwa yale waliyoyasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema.

 

4.  Jihadi na kuwa shahidi

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9, Ayah 111

Hakika Allah swt amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Jannat. Wanapigana katika Njia ya Allah swt – wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na  Qur'an. Na nani atimizae ahadi kuliko Allah swt ? Basi furahini kwa biashara yenu mliy fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

5.   Kutokufuata nafsi yake

Yaani mtu hafuati matamanio ya nafsi yake na badala yake anaikhilafu. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Naziat, 79, Ayah 40 – 41 :

Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt Mlezi, na akijizuilia nafsi yake na matamanio,

Basi huyo, Jannat itakuwa ndiyo makaazi yake !

 

6.  Kushindania katika kuleta Imani

Allah swt atuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al- Waqia, 56, Ayah 10 – 13 :

Na wa mbele watakuwa mbele.

Hao ndio watakao karibishwa

Katika Bustani zenye neema.

 

7.   Hijrah na Jihad

Tumeshaona kuwa Jihadi imeshatajwa hapo mwanzoni ( Jihadi na kuwa Shahidi, nam. 4 ) hapa Jihadi imekuja lakini pamoja na Hijrah. Yaani Hijra ni Jihadi mojawapo kwa ajili ya Mumin. Tumeona kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliiacha Makkah na kwenda Madina, hii ilikuwa ndiyo Jihadi mojawapo ambayo ndiyo kwa ajili ya Allah swt na Dini. 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9, Ayah 20-22 :

Wale walioamini na wakahama, na wakapigana Jihadi katika  njia ya Allah swt kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Allah swt . Na hao ndio wenye kufuz.

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu.

Watadumu humo milele. Hakika kwa Allah swt yapo malipo makubwa.

 

8.   Subira na Ustahimilivu wakati wa shida

Kufanya Subira na Ustahimilivu wakati mtu anapopatwa na shida na matatizo mbalimbali ama yakupoteza mali, kufiwa, kuugua n.k  Katika vitabu tunapata habari kuwa Mitume a.s na Maimamu a.s. pia wamepitia shida kali kali ambazo wao wamezifanyia subira na ustahimilivu kwa ajili ya furaha ya Allah swt . Qur’ani Tukufu , Sura al-Dahar, 76, Ayah 12 :

Na atawajaza Bustani za Jannat na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ra’d, 13, Ayah 24 :

Hao ndio watu wa Jannat, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.(Wakiwaambia) Assalamu ‘Alaikum ! amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno  malipo ya Nyumba ya Akhera.

 

9.  Kuwa imara katika Dini

Inambidi mtu awe madhubuti katika Dini kama ukuta wa Shaba yaani awe na uwezo wa kukabiliana na kila sura itakayojitokeza mbele yake kiasi kwamba kamwe hataweza kulega lega katika dini na kamwe hataweza kurudi nyuma katika msimamo wake wa Dini. Allah swt anasema katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ahqaf, 46,  Ayah 13 – 14 :

Hakika waliosema:Mola wetu Mlezi ni Allah swt ; kisha wakatengenea, hawatajuwa na khofu, wala hawatahuzunika.

 

10.   Kumtii Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Inatubidi sisi kumtii Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ili kuwa mustahiki wa Jannat . Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 13 :

…. Na anayemtii Allah swt na Mtume wake, Yeye atamtia katika Jannat zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

11.  Ikhlas (Uhalisi )

Iwapo kama hakutakuwapo na uhalisi katika kila jambo basi hakutakuwa na usahihi wa kitu au jambo hilo. Uhalisi lazima uwepo katika Imani, matendo na akili na fahamu zetu na kwa hakika huu ndio ufunguo wa kuingia Jannat  na ndivyo maana Allah swt ameweka sharti hili la kumwezesha mtu kuingia Jannat  na Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Safaat, 37, Ayah 39 – 43 :

Wala hamlipwi ila hayo hayo mliyokuwa mkiyafanya.

Isipokuwa waja wa Allah swt  walio khitariwa.

Haom ndio watakaopata riziki maalumu,

Matunda, nao watahishimiwa.

 

12.  Ukweli

Kwa hakika sharti hili ni la umuhimu wa aina yake kwani kila jambo tulifanyalo linahitaji ukweli na kama hakuna ukweli basi kila kitu kitaharibikiwa. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maidah,5, Ayah 119 :

Allah swt atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Allah swt amewawia radhi, nao awe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa.

 

13.  Kujitakasisha mwenyewe

Inambidi kila mtu atulie na kujitakasisha nafsi yake mwenyewe kwa kila jambo na hivyo alete mapinduzi ndani mwake. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ta-Ha, 20, Ayah 75– 76 :

Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu.

Bustani za milele zipitazo mito kati yake,wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.

 

14.  Kutoa katika njia ya Allah swt  na kuomba Tawba

Allah swt anatutaka sisi tule na tuwalishe wengine pia tuwe wakarimu na kamwe tusiwe mabakhili na tuombe Tawba kwa ajili ya madhambi yetu. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ali Imran, 3,   Ayah 133-136 :

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Jannat ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyowekwa tayari kwa wachamungu,

Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allah swt huwapenda wafanyao wema;

Na ambao pindiwafanyapo uchafu au wakjidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah swt na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao – na nai anayefuta dhambi isipokuwa Allah swt ? – na wla hawapendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.

Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mto kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.

 

15.  Hofu ya Allah swt

Kuna msemo kwamba Mwogopeni yule mtu ambaye hamwogopi Allah swt ! Na wala musimwogope yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt !  Kwa sababu yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt kamwe hatakudhuru nyuma yako na atakuwa akijua kuwa Allah swt hatafurahishwa na hatua yoyote ile ya kukuletea madhara. Ndiyo maana tunaambiwa kuwa tusiwaogope Waumini, tuongee nao waziwazi bila ya kuwa na hofu ya aina yoyote, lakini bila ya kuwatuhumu.  Lakini yule asiye na hofu ya Allah swt atatafuta kila hila na mbinu za kukudhuru wewe kwa sababu hana hofu ya Allah swt. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Rahman, 55,  Ayah 46 :

Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt atapata Jannat (Bustani) mbili

 

Vile vile nitapenda kuwaleteeni Hadith ya Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. amesema katika Majma’ul Bayan :

“Mtu yeyote ambaye anajua na kutambua wazi kuwa mimi nifanyapo jema au baya, basi Allah swt yupo anashuhudia matendo yangu haya, basi mtu kama huyu daima atakachokuwa akikifanya basi atakuwa mwangalifu mno katika matendo yake na atajiambia kuwa lau nitafanya kazi hii njema basi Allah swt atalipa mema kadha na kadha na lau nitafanya maasi na madhambi, basi Allah swt ataniandikia adhabu kadha wa kadha. Kwa hivyo watu kama hawa wamewekewa Bustani mbili katika Jannat.”

 

16.  Tawalla na Tabarra

Ama kuhusu mtu atakaye fuata masuala haya mawili basi Allah swt atamjaalia Jannat  na uthibitisho wake ni kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu , Sura al-Mujadilah, 58, Ayah 21 :

Allah swt ameandika : Hapana shaka Mimi na Mtume wang tutashinda. Hakika Allah swt ni Mwenye nguvu, mwenye kushinda.

 

Tawalla maana yake ni kuwa rafiki wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahl al-Bayt a.s. na Tabarra inamaana ya kujiepusha na kujiweka mbali na kutokuwa na uhusiano wowote pamoja na wale maadui wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja Ahl al-Bayt a.s.

 

17.   Kudumisha Sala

Katika maana yake ni kwamba inambidi kila Mwislamu awe akisali sala zote zilizofaradhishwa juu yake kwa kuzingatia umuhimu na nyakati zake. Zipo Sala nyingi ambazo tumefaradhishiwa katika Islam kwa mfano Sala tano za siku, Sala za matukio kama mitetemeko, kupatwa kwa jua au mwezi, n.k. (rejea vitabu vya fiq-hi). Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ma’arij, 70,  Ayah 22 -34 :

Isipokuwa wanaosali,

Ambao wanadumisha Sala zao,

Na ambaokatika mali yao iko haki maalumu

Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba;

Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,

Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.

Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo

Na ambao anahifadhi tupu zao.

Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi –

Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka.

Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,

Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,

Na ambao wanazihifadhi sala zao.

Hao ndio watakao hishimiwa Jannat.

 

 

 

 

 

 

 

 

                                 2.  JAHANNAM

                                               ( Motoni )

 

Maelezo juu ya Jahannam ( Motoni )

 

Waislamu wanatimiza nguzo ya Sumu kwa sababu waweze kuepukana na adhabu za Jahannam . Je Jahannam ni mahala pa namna gani na humo kuna adhabu za aina gani  ?  

 

Kumeandikwa vitabu vingi vikizungumzia swala hili. Qur’an Tukufu inayomaelezo ya kutosha yanayozungumzia mateso na adhabu za kiakili na kimwili kwa ajili ya wale watakaoingizwa humo kwa kutokana kwao kutoishi vile alivyotaka Allah swt, kwa sababu wao hawakutimiza ahadi yao pamoja na Allah swt alivyokuwa amewapa, ambao hawakutimiza makusudi ya kuumbwa kao yaani kumwabudu Allah swt na si mwingine.

 

Adhabu kama hizo zinaweza kuangaliwa na kurejewa katika Surah zifuatazo :

al-Baqarah,Aali-’Imran, alMaaida, al-An" am, al-A’raf, al-Anfal, Younus, Hud, al-Ra’d, al-Hijr, al-NahI, Maryam, Taha, al-Hajj, al-Muminoon, al-Noor, al-Furqan, al‘Ankabut, Luqman, al-Sajdah, al-Ahzab, Saba, al-Zumar, Ohafir, al-Tur, al-Hashr, al-Ma’arij, al-furuj, al-Fajr, al-Nisaa., Katika Surah nyingi, kwa hakika Qur’an imeteremka kuwaonya wanaadamu dhidi ya moto wa Jahannam  na kuwaelekeza katika furaha ya kudumu milele : Ufalme usiokwisha kamwe.

 

Je Jahannam  ina umbo gani la kuonekana ?  Tupitie Ayah ya Qur’an Tukufu Surah ya Al-Balad, 90, Ayah ya 19-20 zisemazo :

Lakini waliokanusha Aya Zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao.

 

“Kufungiwa inamaanisha kufunikwa; Jahannam  inaweza kulinganishwa kama mtungi, wenye kifuniko, juu ya jiko, kwamba chungu kinachomwa ndani na nje.  Maana itakuwa wazi zaidi tusamapo Ayah zifuatazo za Qur’ani Tukufu  Surah al-Humazah, 104, Ayah 5 – 9 :

 

Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika (Moto unaoitwa) Hutama.  Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini ( Huo Moto unaoitwa ) Hutama ? Ni Moto wa Allah swt uliowashwa (kwa ukali barabara ). Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) watafungiwa (wewemo ndani yake ). Kwa magogo marefu marefu

 

“Kufunikwa juu yao” inamaanisha sawa na vile ilivyo katika Ayah ya 90 : 20 hapo juu. Na mistari yake inaweza kumaanisha kwenda undani zaidi, na mistari hiyo  ‘inaongezeka,’ kiurefu, na kwa hakika Allah swt ndiye ajuaye zaidi. 

 

Je miale ya moto wa Jahannam  iko yenye ukubwa kiasi gani ? Jibu lake tunapewa na Muumba wetu na Jahannam  Qur’ani Tukufu  Surah al-Mursalat, 77: Ayah ya 32: "Hakika (Moto huo) hutoa macheche yaliyo kama majumba."

 

Milango ya Jahannam 

 

Katika mlango wa kwanza wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Yeyote yule atakayekuwa na matumaini katika Allah swt basi daima atakuwa mtu mwenye furaha na mafanikio; Yeyote anayekuwa na khofu ya Allah swt basi anajaaliwa usalama; mtu mwovu na aliyepotoka na mstahiki wa adhabu za Allah swt ni yule ambaye hana matumaini yoyote kwa Allah swt na wala hana khofu ya aina yoyote ile ya Allah swt.

 

Katika mlango wa pili wa Jahannam kumeandikwa yafuatayo: Yeyote yule asiyetaka kufanywa uchi Siku ya Qiyama, basi awavalishe nguo wale walio uchi humu duniani, Yeyote yule asiyetaka kupatwa na kiu Siku ya Qiyamah, basi awanywishe wale wenye kiu humu duniani, Yeyote yule asiyetaka kupatwa na njaa Siku ya Qiyamah, basi awalishe wale wenye njaa humu duniani.

 

Katika mlango wa tatu wa Jahannam kumeandikwa : Allah swt huwalaani wale wasemao uongo, Allah swt huwalaani wale walio mabakhili,  Allah swt huwalaani wale wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wanyong.

 

Katika mlango wa nne wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Allah swt humdhalilisha yule ambaye anaidharau Dini ya Islam,  Allah swt humdhalilisha yule anayewakashifu Ahl al-Bayt a.s. ya wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ; Allah swt humdhalilisha yule ambaye anawasaidia wadhalimu katika kuwadhulumu watu.

 

Katika mlango wa tano wa Jahannam kumeandikwa sentenso : Msiendekeze matamanio yenu, kwani matamanio yanapingana na tendo la kusadikisha;Musiyaongelee zaidi yale yasiyowahusu kwani mtaondoka katika Baraka za Allah swt; na kamwe msiwe wasaidizi wa madhalimu.

 

Katika mlango wa sita wa Jahannam kumeandikwa sentenso: Mimi nimeharamishiwa kukubalia Mujtahid (hawa ni wale ambao wamefikia upeo wa Ijtihad, uwezo wa kutoa fatwa. Rejea vitabu vya Fiqh ndipo utakapoweza kupata ilimu zaidi katika somo hili). Mimi nimeharamishiwa kukubalia wale wanaofunga saumu.

 

Katika mlango wa saba wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Ujihisabie mwenyewe matendo yako kabla hujafanyiwa hisabu ya matendo yako; ikaripie nafsi yako kabla wewe hujakaripiwa; na mwabudu, Allah swt aliye Mkuu na aliyetukuka, kabla ya wewe hujafika mbele yake na ambapo hautaweza tena kumwabudu na kumtukuza.

 

Kwa kuwa marejeo kuhusu Jahannam  yapo yanapatikana kwa wingi kutoka Qur’ani Tukufu, sisi sasa tutajaribu kurejea mapokezi na maelezo kuhusu Jahannam kutokea Ahadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. kuhusu adhabu,vitisho vya Jahannam , mahala palipojaa joto la hali ya juu yenye kuumiza, mahala ambapo moto wake unawekewa vipande vya kiberiti au mrututu ambayo kila moja ni kubwa kama milima mikubwa kabisa ulimwenguni. Zipo sehemu kubwa kabisa kama hizo ambapo wale waliokwisha adhibiwa hupelekwa kupoozwa na kugandishwa kama barafu. Kwa maneno mengine,  wanatolewa kutoka hali moja ya mto mkali kabisa na kupelekwa katika hali nyingine ya bariki kabisa. Katika sayari yetu kuna milima yenye theluji na milima yenye kutoa volkeno ambayo hutoa miyeyuko ya mawe kama lava; na hivyo ndivyo ilivyo hali ya Jahannam : kuna hali zote mbili za joto kali na baridi kali.

 

Katika uk.309 ya kitabu cha al-Selek, The Divine Traditions, mkusanyiko wa Ahadith al-Qudsi, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amenakiliwa akisema kuwa siku moja Jahannam  ilimlalamikia Allah swt kwa kusema, : “Ewe Mola! Hata sehemu zangu zinateketezana!” na kwa hayo Allah swt aliiruhusu kupumua mara mbili, mara moja katika majira ya baridi na mara nyingine katika majira ya joto kali. Kwa sababu ya kupumua kwake huku ndiko kumetokezea misimu hii miwili yenye joto kali na baridi kali. Iwapo Allah swt angalikuwa ameruhusu zaidi ya mara mbili basi kusingalikuwapo na maisha ulimwenguni humu.

 

Chakula cha watu wa Jahannam  na Jannat  

 

Wakati wakazi wa Jannat  watakuwa wakila kila aina ya matunda mazuri na yenye ladha tamu, wakazi wa Jahannam watakuwa wakila chakula kama miiba ambayo itakuwa ikiwasakhama katika koo zao, kamwe haitawafikia tumboni mwao, na wala hawataweza kutapika.  Na hii ndiyo chakula mojawapo ya watu wa Jahannam . Aina nyingine ya chakula kinachotayarishwa kwa ajili ya wakazi wa Jahannam  ni usaha wa majeraha ya wale wanaopata mateso katika Jahannam , na kuchemshwa katika joto la kupasua matumbo yao.

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amenakiliwa katika uk.145, J.1 ya al-Zamakhshari’s Rabee’ al-Abrar akiwa amemwuliza Malaika Jibrail a.s., “Je ni kwa nini mimi kamwe sijamwona Malaika Mikaili a.s. akicheka au kutabasamu?” Malaika Jibraili a.s. alimjibu: “Mikaili kamwe hakucheka wala kutabasamu kuanzia pale Jahannam  ilipoumbwa. ”  Anas, Allah swt airehemu rohoyake, amenakiliwa na al-Zamakhshari akisema kuwa mfano wa kiwango kidogo kabisa cha adhabu ya Jahannam  ni kama kwamba mtu anatengenezewa pea ya viatu ambavyo anapovaa bongo inachemka na kutokota. Habari zaidi kuhusu sehemu hii ya kutisha zinapatikana katika al-Zamakhshari, ambazo ni kama zifuatazo :

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, “Katika safari yangu ya usiku wa (‘Israa), mimi nilisikia sauti kubwa mno, hivyo nilimwuliza Malaika Jibrail a.s., ‘Je sauti hii kubwa ni ya nini, Ewe Jibraili ?’  Naye alinijibu, ‘Ni jiwe lililotupwa kutokea juu kuangukia ndani mwa Jahannam , na imekuwa ikianguka kwa muda wa vipindi sabini vya baridi, na sasa ndipo ilipofika chini.”

 

Abu ‘Asim ‘Ubayd ibn ‘Umayr ibn Qatadah al-Laythi, Hakimu wa Makkah (d. 68 A.H.), amesema, “Jahannam  hupumua mara moja kwa sababu yake Malaika na Mitume a.s. yote hutetemeka, kiasi kwamba hata Mtume Ibrahim a.s. hupiga magoti na kusema, “Ewe Mola wangu ! Nakuomba uniokoe!”

 

Abu Sa’eed al-Khudri amenakiliwa akisema, “iwapo milima itapigwa kwa rungu mara moja inayotumiwa na Malaika wa Jahannam , basi itavunjika vipande vipande na kuwa vumbi.”

 

Tawoos ibn Keesan al-Khawlani amenakiliwa akisema, “Wakati Jahannam ilipoumbwa, Malaika walishtushwa mno, na wakati nyie wanaadamu mulipoumbwa, basi walitulia.”

 

Al-Hasan ibn Yasar al-Basir amesema, “Kwa kiapo cha Allah swt! Hakuna hata mja mmoja wa Allah swt anayeweza kustahimili joto la Jahannam ! Tumeambiwa iwapo mtu atasimama Mashariki na Jahannam  ikawa upande wa magharibi na ikafunuliwa kidogo tu, basi bongo ya mtu huyo aliye Mashariki itachemka. Iwapo kama kiasi cha ndoo moja ya usaha wa Jahannam  ukimwagwa juu ya ardhi hii ya dunia, basi hakuna hata kiumbe kimoja kingalibakia hai.”

 

Hisham ibn al-Hassan al-Dastoo’i alikuwa hazimi taa wakati wa usiku, na wakati wananyumba yake walipompinga kwa kumwambia, “Sisi hatuwezi kutofautisha baina ya usiku na mchana !” Yeye aliwajibu, “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi ninapozima taa wakati wa usiku, hukumbuka kiza kikali cha kaburini, na hivyo sipati usingizi.”

 

Adhabu katika Jahannam   itakuwa kwa mujibu wa aina za madhambi zilizofanywa wakati wa maisha ya mtu humu duniani. Kwa mfano, Wale ambao walilimbikiza mapesa humu duniani bila ya kutoa Zaka na kodi zinginiezo za kidini, basi hao watachomwa kwenye paji la uso kwa yale waliyoyalimbikiza, pembeni mwao, na migongoni mwao. Kwa maneno mengine, sehemu zote za mwili wao.

 

Abu Zar al-Ghaffari, Allah swt amwie radhi, alikuwa akisema, “Waambieni wale ambao hupenda kulimbikiza utajiri wao kuwa watachomwa nayo juu ya paji la uso wao, pembeni mwao, na migongoni mwao hadi watakapokuwa wamejaa kwa mioto.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, kama vile tuambiwavyo katika uk.243, J.8, ya Bihar al-Anwar, “Hakuna Mja wa Mwenyezi Mungu mwenye utajiri au mali na hataki kulipa Zaka isipokuwa kwamba atachomwa kwa vipande hivyo vya mapesa vitakavyokuwa vimepashwa moto katika moto wa Jahannam  na kwamba watatumbukizwa katika adhabu hizo kuanzia juu ya vipaji vyao vya nyuso zao na migongo yao hadi pale Allah swt atakapokuwa amemaliza kupokea mahisabu na adhabu za waja wake Siku ya Qiyamah, muda ambao ni wa maelfu ya miaka kwa mujibu wa mahisabu yetu. Hapo ndipo watakapotumwa ama kuingia Jannat   au  Jahannam  .”

 

Abu Umamah anamnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akielezea aina na vinywaji watakaopewa wakazi wa Jahannam  . Anasema, “Italetwa mbele yake, naye atachukizwa nayo; na itakapoletwa karibu yake, itauchoma uso wake na kifuvu kitadondoka. Iwapo ataweza kunywa hata kidogo kutokamo, basi matumbo yake yatakatika vipandevipande na kutokezea sehemu za nyuma ya kutokezea choo.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameripotiwa akisema, “Sala za mtu anayekunywa pombe hazikubali kwa siku arobaini; na iwapo atakufa huku pombe ikawamo tumboni mwake, basi Allah swt atamlazimisha anywe sadiid, maji yatokayo kwenye sehemu za uchi wa malaya ambayo yatakusanywa katika birika huko Jahannam  na kupewa watu hawa, na kwayo matumbo na ngozi zao zitachomwa.”

 

Riwaya hii imeelezwa na Shu’ayb ibn Waqid ambaye anamnakili al-Husain ibn Zayd ambaye anamnakili Imam Ja’fer al-Sadiq a.s. kama ilivyoelezwa katika uk. 244, J. 8, ya  Bihar al-Anwar, “Wale wenye madhambi mbali na zinaa au mauaji, watapewa vinywaji vya risasi na shaba iliyoyeyushwa”, kama vile Ibn Mas’ud anavyonakiliwa katika Bihar al-Anwar akisema.

 

Mujahid anasema kuwa hayo yatakuwa ni usaha na damu za wale walioadhibiwa, ambapo Ibn Jubayr anasema ni ‘maji meusi; kwani Jahannam  ni nyeusi, miti yake ni meusi, na nyuso na miili ya wakazi wake pia inakuwa imegeuka kuwa nyeusi.

 

Hoja hii inachukuliwa na al-Dhahhak. Adhabu za ziada zitakazokuwa zikitolewa Jahannam  zitakuwa za nyoka na nge ambao makucha yao yatakuwa, kwa mujibu wa Ibn ‘Abbas na wengineo wanaripoti hivyo, makubwa na marefu kama minazi.  Nyoka watakuwa wanene kama tembo, na nge watakuwa wakubwa kama punda weusi. Na mara kwa mara wakazi wa Jahannam  watakuwa wakipigwa vipigo kwa makonde yao kama marungu: Iwapo wao watakuwa katika tabaka za juu za Jahannam  , basi vipigo hivyo vitawaangusha katika tabaka zinginezo, na kila tabaka litakuwa na joto na mateso makali kuliko tabaka lililotangulia, kwa muda wa miaka sabini. Mara watakapofikia tabaka la chini, miale mikali ya moto itawatupa tena, na vivyo hivyo itakavyokuwa ikiendelea. Hakutakuwa na muda wa kuomba msamaha kwa ajili yao.

 

Je ni mahala gani palipo pabaya zaidi katika Jahannam  ?

Ibn Mas’ud na Ibn ‘Abbas wamenakiliwa katika uk.241 – 242, J.8, ya al-Majlisi Bihar al-Anwar anasema kuwa wanafiki watawekwa katika tabaka la chini kabisa la Jahannam  ambapo kuna adhabu kali kuliko zote. Watafungwa katika vyumba kama majiko yaliyojaa mioto mikali.

 

Kwa sasa turejee Nahjul Balagha na tuangalie vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anavyotupatia picha ya Jahannam  , tumwombe Allah swt asitutumbukize humo :

‘Janga kubwa kwa mtu ni kule kutumbukia katika Jahannam ; yeye atajihisi kuwa anachemshwa mzimamzima, na ataona mateso yake yasiyona mwisho, na kiumbe fulani kinakoroma na kupumua, viumbe vyote vilivyo humo hukosa raha na kamwe hawapati fursa ya kupumzika, na kamwe hawatapata kupumzika kutokana na adhabu zake au mauti ya uhakika. Yeye hasinzii hata kidogo wala hakutakuwa na mapumziko katiko mateso yake : Kutakuwa na maumivu yakudumu kiasi ambacho tunamwomba Allah swt atunusuru na kutusaidia .’  ( Hotiba  83 ).

 

‘Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa kuliko sehemu yoyote ile, mahala ambapo mikono ya wakazi wake yanakuwa yamefungwa shingoni mwaio, na vichwa vyao vimefungwa na miguu yao kwa minyororo na mavazi yao yametengenezwa kwa  lami. Mashati yao yametengenezwa kwa moto wakati ambapo adhabu zao za moto usiozimika kamwe hazitakwisha kwamwe mahala ambapo mlango wake utakuwa umejazwa watu, katika moto mkali kabisa kiasi kwamba sauti zao zinasikitisha na kutisha, na miale ya moto ikipaa na kufikia kila sehemu na wala hakuna kujitoa kutoka humo na wala hakuna muda utakaokwisha,na wala haina mwisho wake kwa wale wanaotekeezwa na kuchomwa humo.’   ( Hotuba 109 ).

 

‘Joto lake ni kali mno, kufikia chini kwake ni mbali mno, sakafu yake ni chuma, vinywaji vyake ni usaha.’   (Hotuba 120 )

 

‘Siku ya Qiyamah, madhalimu wote wataletwa bila ya kuwapo na mtu yoyote wa kuwasaidia au kuwatetea, na hivyo watatumbukizwa katika moto wa Jahannam na humo atasagwasagwa kama vile machine za kusaga zifanyavyo, hadi hapo atakapojigonga kichwa katika sakafu ya chini kabisa.’ ( Hotuba 164 )

 

‘Iwapo Malik (msimamizi wa Jahannam) atakuwa mkali, husababisha sehemu yake moja kuminyana na sehemu zingine, anapogombeza, milango yake huruka juu na chini (hutema kama volkano). (Hotuba 183 )

 

Mazungumzo juu ya Jahannam yanatudhihirishia wazi kuwa umbali, mahala na nafasi ni vitu vya uhakika katika maisha yajayo kama vile yalivyo katika maisha yetu haya. Ushahidi wa kusema kuwa Jahannam  itasogezwa au kupelekwa sehemu moja kutokea sehemu nyingine, unapatikana katika Ayah ya 23 ya Surah al-Fajr (Surah namba 89 ) na katika Ayah zinginezo pia :

Basi Siku hiyo italetwa Jahannam. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini ?

 

Kwa hakika wale watakaokuwa wakiihamisha Jahannam  kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa Amri ya Allah swt, hawatakuwa wenfgine isipokuwa ni Malaika ambao sisi hatuwaoni duniani humu lakini punde tutakapo kufa, tutaanza kuwaona, naomba mazungumzo haya juu ya Malaika tuyaachilie hapa kwani yatahitaji kutungiwa kitabu kingine, na kwa sasa hivi somo hili litatuchukua mbali, Insha-Allah, tutaweza kuwatungieni kitabu kingine juu ya Malaika.

 

Lazima ikumbukwe kuwa picha yote iliyotolewa kuhusu Jahannam  hatujaelezea kuhusu mateso na adhabu yanayotokana kuwa pamoja na Mashetani, Pepo mbaya na Majini waliolaaniwa ambao wote hao watakuwa pamoja na wanaadamu waliolaaniwa. Tukiangalia mateso wanayopewa viumbe hivi, makelele yao, sehemu zao zikivutwa na kunyofolewa, na wakichunwa ngozi kutoka miili yao … yanatisha mno kama Jahannam  yenyewe. Kumbuka vile Allah swt alivyomwelezea mwanadamu kuwa ameumbwa kwa ubora wote. Wanaadamu watakaotumbukizwa katika Jahannam wataelewa vyema zaidi kuliko wengine, wakati ambapo wale watakaokuwa wameongoka watakuwa wamepona uhakika wa kuteswa.

 

Wale ambao wamesoma masimulizi ya Saint Joan of Arc (1412 – 1431 ), Mfaransa mashuhuri, mbali na umri wake wa kati, aliwaongoza Wafaransa katika ushindi dhidi ya majeshi ya Waingereza huko Orleans, kumbuka kuwa yeye alikuwa ni Pepo mbaya, na anapendelea kutembea juu ya miti iwakayo moto kutokea ncha moja ya dunia hadi nyingine kuliko kuangalia tu. Sasa hebu fikiria kuwa nao katika Pepo za milele. (Yeye haoni ajabu kutembea juu ya moto, je na wewe unaomsimamo kama huo…?)

 

Kwa kifupi hivyo ndivyo ilivyo Jahannam na adhabu na mateso yake. Kama tungaliweza kuangalia hata mara moja au kuwaangalia wakazi wake, basi kwa hakika tusingalijali kufunga saumu kila siku ya maisha yetu, na wala si katika mwezi wa Ramadhani tu, Mwezi wa Allah swt, mwezi  wa msamaha na baraka, lakini maisha yetu yote.

 

Sababu zimfanyazo mtu kuingia Jahannam     

1. Kufr na Nifaq

Hoja hii ipo ya kwanza katika mfululizo wa sababu za kumfanya mtu aingie Jahannam na sababu zote zifuatazo ndizo matawi ya Kufr na Nifaq na Allah swt amewafanyia makhususi Jahannam  watu wenye sifa hizi mbili. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4,  Ayah 140 :

Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Allah swt zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano waohao. Hakika Allah swt atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 ,  Ayah 145 :

Hakika wabnafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahannam , wala hutompata yeyote wa kuwanusuru.

 

2. Kuwazuia wale wanaotenda kazi katika njia ya Allah swt

Kuna watu wengi ambao wanatabia ya kuzua uzushi na kuwazuia kwa njia mbali mbali wale wanaofanya tabia na kutenda matendo mema kwa mujibu wa Sunnah na tabia ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahl al-Bayt a.s. kwa hivyo watu kama hawa ndio waliowekwa katika sababu ya kwanza ya kuingizwa Jahannam . Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4  ,  Ayah 55 :

Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.

 

3.   Kutomtii Allah swt

Leo kila mzazi anataka watoto wake wamfuate na kumtii vile atakavyo yeye mwenyewe akiwa kama mzazi na vile vile kila atengenezacho mtu hutegemea kuwa kitu hicho kitamfaa na kumfanyia kazi kwa makusudio ya kukitengeneza na ndivyo vivyo hivyo Allah swt ametuumba sisi pamoja viumbe vingine vyenye uhai na visivyo na uhai kwa sababu na makusudio maalumu, nayo ni utiifu kwa Amri Zake na kumfuata Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahl al-Bayt a.s.

 

Hivyo kwa kutomtii Allah swt na  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahl al-Bayt a.s. ni dhambi kuu na ndicho kitakachotutumbukiza Jahannam moja kwa moja. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Jinn, 72 , Ayah 23 :

….. Na wenye kumuasi Allah swt na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannam wadumu humo milele.

 

Vile vile twaambiwa na Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 115 :

Na anayempinga Mtume baada ya kudhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamwingiza katika Jahannam. Na hayo ni marejeo maovu.

 

4.   Kudhihaki Ayah za Allah swt

Kuna baadhi yetu tunayo tabia ya kuzifanyia dhihaka Ayah, amri na hukumu za Allah swt ambapvyo ni tabia ovu kabisa na hatimaye humtumbukiza Jahannam bila ya yeye kutambua athari mbaya ya tabia yake hiyo. Upeo wetu wa ilimu na maarifa ni mdogo sana kiasi cha kutufanya sisi tukajivunia na kufanya ufakhari mbele ya Allah swt  na tukajifanya hodari mbele ya maamrisho yake. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Kahaf, 18, Ayah 106 :

Hiyo Jahannam ni malipo yao kwa walivyokufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu.

 

5.   Kutotumia viungo vya mwili dhidi ya Allah swt

Tunaonywa kuwa tusivitumie viungo vyetu vya mwili kama macho, mdomo, masikio, miguu na mikono, n.k. dhidi ya Allah swt katika kutenda maasi na madhambi. Tunaelewa vyema kabisa kuwa Siku ya Qiyamah viungo vyote hivi vitatoa ushahadi wa kipekee kwa kila kilichotenda humu duniani na Allah swt amesema wazi waqzi katika Sura al-Ya-Sin kuwa Siku hiyo ya Qiyamah hakuna nafsi yoyote ile itakayolipwa mema au kuadhibiwa isipokuwa kwa yale waliyoyatenda tu.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-‘A’raf,  7,  Ayah 179 :

Na tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.

 

6. Kumtii na kumfuata Shaitani

Humu duniani watu wengi mno tumekuwa wafuasi na mashabeki wakubwa wa Shaitani kiasi kwamba hata Allah swt tumemsahau kama yupo na anayajua yale yote tuyafanyayo. Sisi tunayakimbilia kila yaliyo maovu bila hata ya kuyafikiria matokeo yao kama yatatunufaisha au kutudhuru. Na kwa hakika mambo mengi mno tuyafanyayo sisi kimatokeo ni kutudhuru tu. Kila aina za tabia mbaya sisi tunaongoza kama kunywa pombe, bangi, madawa ya kulevya, zinaa na uasherati wa kil aina, wizi, uongo, kudhulumiana na kufanyiana khiana, n.k. na hata wengi wetu kuthubutu kusema kuwa sala, saumu havina umuhimu wowote katika Islam na maisha ya mwanadamu. Kwa hakika tunakuwa tumejawa na kasumba za Kishetani ambazo zinatuangamizi moja kwa moja. Allah swt anasema katika Ayat ul-Kursi kuwa wale wanaokufuru na wanaomfanya Shaitani kuwa kiongozi wao, basi Allah swt huwatoa katika Nuru na kuwatumbukiza katika Kiza.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-‘A’raf, 7, Ayah 18 :

Akasema : Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

 

7.  Majivuno

Kwa hakika hii ni tabia mbaya kabisa katika maisha ya mwanadamu kwani anajiona yeye yu bora na afadhali kuliko watu wengine wote ama kwa kujivunia ilimu aliyoipata, uzuri, watoto, mali, siha, n.k. lakini yote yaho si ya kujivunia kwani vyote ni vitu vyenye kuangamia na kuisha pasi na sekundi hata moja. Mfano mtu kama huyo anaweza akaugua ugonjwa kwa muda mfupi atawehuka au akapoteza fahamu zake, hivyo akasahau yote aliyokuwa akiyajua. Vile vile mtu anayejivunia afya na mwili wake anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo, na akapooza mwili kiasi kwamba hata chakula analishwa akiwa amelala na anajisadia choo kidogo na kikubwa akiwa kitandani, hoi hawezi hata kujipangusa mwenyewe. Je majivuno yamekwenda wapi ? Na huu ni uatamaduni wa Shaitani ambao kwetu sisi ndio tunaouona kama ndio desturi nzuri. Mtu masikini akiketi karibu nawe, je utakuwa masikini au utajiri wako utamwendea huyo masikini ?

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura az-Zumar, 39,  Ayah 32 :

BASI NI NANI dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uwongo Allah swt na kuikausha kweli imfikiapo ?  Je! Siyo katika Jahannam makazi ya hao makafiri?

 

Na vile vile  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-A’raf, 7, Ayah 36 :

Na wale watakaokanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni atu wa Motoni; humo watadumu.

 

8.  Kuwaomba msaada Wadhalimu

Kwa kutaka misaada kutoka wadhalimu kunatupeleka katika Jahannam  bila kipingamizi kwani tunaelewa wazi kabisa kuwa mdhalimu (jina linajitosheleza kwa kujieleza ) ni mtu ambaye anamdhulumu mtu au watu hivyo hakuna kheri kwao kwani watataka kila mtu adhulumiwe tu kwa njia moja au nyingine. Na kwa kumwomba yeye msaada atajenga chuki na uhasama baina ya watu ili yeye aweze kunufaika. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Hud, 11,  Ayah 113 :

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Allah swt , wala tena hamtasaidiwa.

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maidah,5,  Ayah 2 :

…. Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui….

 

9.  Kuisahau Akhera

Kwa hakika sisi binadamu tunajitumbukiza katika maasi na madhambi basi tunasahau kuwa Allah swt yupo anatuangalia na kuyajua matendo yetu yote. Na katika hali hii sisi huwa tunasahau kuwa baada ya maisha ya humu duniani na kufa kwetu, kuna Aakhera. Na kuisahau huku ndiko kunakotutumbukiza Jahannam .

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Jathiyah, 45,  Ayah  24 :

Na walisema:Hapana ila huu uhai wetu a duniani – twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa dahar. Laini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadahani tu.

 

10.  Kuiabudu Dunia

Sisi tumepotea kiasi kwamba dunia hii tumeichukulia kama kwamba ndipo tutakapoishi milele wakati tunawaona watu wanakufa usiku na mchana, wote hawa wanaiacha dunia kwa mikono mitupu. Wapo humo wanaobahatika sanda au kuzikwa na wengine humo wapo ambao hata sanda hawabahatiki na badala ya kuzikwa wanaliwa na wanyama na kuoza kama vile kufa maji, kuchomwa moto n.k. Lakini haya yote tunayaona kama mzaha bila kuyatilia maanani kuwa nasi pia tuko njiani kwenda huko na tutayaacha yote humu humu duniani isipokuwa matendo yetu mema ndiyo yatakayotufaa katika safari yetu ya Aakhera. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema Safari ndefu lakini matayarisho ya safari ni madogo. Tukiwa watumwa wa dunia basi tutatumbukia Jahannam .

 

Hapa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema katika Mizanul Hikmah kuwa “Mapenzi ya dunia ndiyo chanzo chote cha kila aina ya madhambi.” Na vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- ‘Asra’, 17, Ayah 18 :

Anayetaka yapitayo upesiupesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannam ; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.

 

11.  Kulimbikiza utajiri wa mali na mapesa

Sisi wanaadamu tunayo tabia ya kulimbikiza utajiri yaani kulimbikiza mali na mapesa bila ya kujali haki zilizowekwa na Dini yetu Tukufu kama vile kutoa Zaka, Khums, Sadaqa, kuwasaidia jamaa na mayatima, wajane na wale wenye shida n.k. Kwa hakika Qur’ani Tukufu  inatuambia waziwazi kuwa sisi tunapenda kujiongezea tu hadi hapo tutakapofika makaburini, kamwe hatukinai wala kutosheka, na tufikapo makaburini ndipo tutakapoamka na kuzindukana na usingizi wetu huo wa upotofu.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Tawbah, 9,  Ayah  34 – 35 :

Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuiliz Njia za Allah swt. Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Allah swt. Wabashirie khabari ya adhabu iliyochungu.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya.”

        (Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile      

       ambamo zaka haijatolewa).

 

12.  Kuikimbia Jihadi

Hapa neno hili la Jihadi linamaana mbili : moja ya kupigana vita pamoja na nafsi yake mtu mwenyewe na pili kupigana vita kwa mikono yake dhidi ya makafiri na maadui wa Islam.

 

Katika uwanja wa vita badala ya kuwasaidia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Maimamu a.s. mtu anaweza kuacha wao vitani  na yeye akatoroka. Basi mtu kama huyu ataingizwa Jahannam  na Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Anfal, 8,  Ayah  15 – 16 :

Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo.

Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo – isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi – basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Allah swt . Na pahala pake ni Jahannam, na huo ni mwisho muovu.

 

13.   Kumwaga damu ya mtu asiye na hatia

Kwa kumwaga damu ya mtu asiye na hatia kutatufikisha katika Jahannam  kwani hii itakuwa ni dhuluma na ndiyo maana kuna mahakama na vyombo vya sheria vya kufuatilia masuala ya watu anapokumbwa na matatizo na watu wengine. Haifai kwa mtu kujichukulia sheria mikononi kwani inawezekana mtu mmoja akamwua mtu mwingine kwa kudhania tu pasi na ushahidi wa kutosha au bila kufikiria vyema kwani wakati huo mtu huyoanakuwa katika hasira na jazba. Katika Islam kuna uongozi sahihi umewekwa kwa ajili ya kufuatilia kila jambo na swala. Kwa kufuatilia maswala kwa uchunguzi na kufikia jibu au muafaka kunadumisha upendo na amani katika jamii zetu na kwa hakika haya ndiyo yanayomfurahisha Allah swt na ndipo hapo tunapojaaliwa baraka na rehema na neema Zake. Allah swt hataki mwenye nguvu na uwezo kuwadhulumu wanyonge na dhaifu. Haki ifuatwe ipasavyo.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maida, 5,  Ayah 32 :

Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika wakiwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa,4,  Ayah 93 :

Na mwenye kumuuwa Mumiin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam humo atadumu, na Allah swt amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.

 

Kwa hakika kwa mtu anayemwaga damu ya mtu asiye na hatia, huadhibiwa adhabu nne na huko Jahannam  atawekwa peke yake, daima ghadhabu za Allah swt zitakuwa juu yake, laana za Allah swt zitakuwa juu yake na adhabu kubwa kabisa itamwangukia. Habari hizi pia ziko katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ali Imran, 3, Ayah 21 :

Hakika wanaozikataa Ishara za Allah swt , na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.

 

14.  Kupuuzia na kutokusali Sala

Watu wa Jannat watawauliza watu wa Jahannam kile kilichowaingiza Jahannam. Nao watawajibu kuwa wao hawakuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Muddathir, 74,  Ayah 39 – 46 :

Isipokuwa watu wa kuliani.

Hao watakuwa katika mabustani, wawe wanaulizana

Khabari za wakosefu:

Ni nini kilichokupelekeni Motoni (Saqar) ?

Waseme : Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali.

Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.

Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu.

Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya malipo.

 

15.  Kutokutoa Zaka[1]

Katika maisha yetu Dini yetu imetuwekea masharti ya kutozwa kodi mbalimbali ambazo zimeelezwa vyema na kwa uwazi katika vitabu vya fiq-hi kwa ajili ya kutakasisha mali zetu.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Fussilat,41,  Ayah 7 :

Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa akhera.

 

16.  Kudhulumu haki za yatima

Duniani humu hakuna mtu ambaye anaomba watoto wake wawe mayatima na kutaabika kwa mateso yaliyopo humu duniani. Lakini kunapotokea hali ya watu wengine kuwadhulumu mayatima, basi hao hujishughulisha kwa kila hila na mbinu katika kufanikisha azma yao hiyo ya kuwadhulumu mayatima. Badala ya kuwa waangalizi wa mayatima, wao ndio wanawadhulumu na kuwafanyia maisha yao yakawa magumu kwani watoto hao watashindwa kusoma mashuleni, hawataweza kuvaa mavazi mazuri, hawataweza kuishi maisha mazuri na vile vile hawataweza kupatiwa matibabu mazuri kwa ajili ya hayo. Sasa jee haya ndiyo yanayomfurahisha Allah swt  au tunamghadhabisha na hatimaye atuadhibu ? Halafu tutasema kuwa Allah swt anatuonea.

 

Kwa kifupi sisi tunatakiwa tuwe walezi wa mayatima. Ipo Hadith tukufu kuwa Yatima anapotoa pumzi moja ya kusikitika, basi ;Arshi Ilahi inatetemeka na Malaika huangua kilio.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa,4,  Ayah  10 :

Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumoni mwao moto, na watingia Motoni.

 

17.  Kutoza na kupokea riba

Allah swt ameharamisha kutoza na kupokea riba kwa sababu riba inawadumaza watu kiuchumi na hatimaye hata kufilisika. Tunasikia kila mahala kunakuwapo na kilio kikubwa cha watu hata mashirika na hata nchi mbalimbali ikiwemo yetu, wote wakilia kilio cha kunyonywa kwa kutozwa riba ambayo inawawia ngumu kuilipa na hatimaye kutumbukia katika madeni makubwa makubwa ambayo kuyalipa tena ni vigumu mno.

 

Watu wengi wamewahi kuchukua riba lakini wameshindwa kurejesha

 

Unachukua mfuko mtupu na kuurudisha ukiwa mnono au unamchukua ng’ombe aliyekonda na kumrudisha akiwa amenona sana!

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- Baqarah, 2, Ayah 275 :

Wale walao riba riba hawasimami ila kama anavyosimama aliyezugwa na Shaitani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Allah swt ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Basi aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi,, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyokwisha pita, na mambo yake yako kwa Allah swt. Na wenye kurudia basi ao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

Allah swt huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka…

 

18.   Kutokushukuru neema za Allah swt

Sisi wanaadamu tunayo tabia na desturi ya kutoa shukurani kwa jema lolote tunalofanyiwa na watu wenzetu. Lakini ni ujeuri wetu sisi kwamba hatutoi shukurani ipasavyo kwa Allah swt amabye ametujaalia kila aina ya neema kama macho, miguu, mikono,siha, mali, watoto,  n.k. kwa hakika hatuwezi kuzihesabu neema za Allah swt (rejea Sura ar-Rahmaan ) hata tukizikalia pamoja na makompyuta zetu.

 

Allah swt pia anatarajia kuwa mja wake atakuwa ni mtu mwenye kumshukuru na kumnyenyekea kwa neeza zote anazomjaalia, lakini sisi badala ya kufanya hivyo, ndivyo tunavyozidi kuleta ufisadi na uchafuzi humu duniani kwa neema hizo hizo anazotujaalia Allah swt  kwa ajili ya mambo mema. Tunafanya kiburi na majivuno mbele ya Allah swt lakini tunasahau kuwa hatumpunguzii chochote Allah swt  na badala yake iwapo tutamshukuru basi Allah swt atatuzudushia katika maslahi yetu.

 

Hebu zingatia kuwa kuna masikini mwombaji mmoja akiwa mlangoni mwako, utampa chochote kile ili mradi umempa. Lakini kuna mwingine anakuja mlangoni mwako na kuanza kukusifu na kukutukuza na kukuombea dua nzuri nzuri, basi bila shaka huyu utampa mambo mazuri zaidi ya yule wa kwanza. Jaribu kusoma maana ya Ayah za Sura al-Fatiha (al-Hamdu ) utaona kuwa kunaanza kumsifu na kumtukuza Allah swt kwa mpangilio maalum na hapo katikati ndiko kunaanza sisi kujiombea maslahi yetu. Sasa katika hali kama hii Allah swt kamwe hawezi kutunyima kile tumwombacho.

 

Tujaribu kujifunza kutoka watoto wadogo hususan wanapoomba kitu utaona wanavyobembeleza.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ibrahim, 14,  Ayah 28 – 29 :

Hebu hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Allah swt kwa kukufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo ?

Nayo ni Jahannam ! Wataingia. Maovu yaliyoje makazi hayo !

 

19. Kuibia katika  mzani

Mwanadamu hujipatia malimbikizo ya mali kwa ilimu aliyonayo. Wengine wanapenda kufanya kwa uhalali wakati wengine wanafanya kwa kuibia katika mizani yaani wanapouza huuza kwa kupunguza, au huuza kitu kisicho sahihi au huiba katika vipimo vya uzito na urefu na upana, au huchanganya mali ili kufikisha ujazo kwa mfano kuongezea changarawe katika nafaka, maji katika maziwa, mafuta tofauti huongezwa katika mafuta ya aina nyingine au kumbandika mtu mali hafifu kwa kupokea malipo ya kifaa imara, n.k. Hivyo Qur’ani Tukufu inatukanya vikali mno pamoja na Ahadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Mutaffifiin, 83, Ayah 1 – 10 :

Ole wao hao wapunjao!

Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.

Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa

Katika Siku iliyo kuu,

Siku watapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote ?

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.

Unajua nini Sijjin ?

Kitabu kilichoandikwa.

 

20.   Kuzitafuta aibu za mtu na kumsengenya

Watu wanapokuwa hawana kazi au shughuli za kufanya, basi utawaona wengine kazi zao ni kuzitafuta aibu za wengine na kuanzisha mgumzo ya kuwasengenya watu. Kwa hakika tutambue wazi kuwa anayemsema mwinge vibaya mbele yetu basi atatusema sisi vibaya mbele ya wengine, hivyo inabidi kujiepusha na watu kama hawa. Je ni nani aliye humu duniani ambaye hana kasoro ? Basi huyo si mwanadamu bali ni Malaika ! Huyo anayezitafuta aibu za wengine, mwenyewe anazijua aibu zake, hivyo inambidi ajichungulie vyema unani mwake kabla ya kuwasema wengine.  Vile vile tutambue wazi kuwa Allah swt hatatusamehe madhambi yetu ya kumsema mtu vibaya hadi hapo huyo mtu atusamehe yeye mwenyewe kwa furaha yake.[2]

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Humaza, 104,  Ayah 1 - 5

Ole wake kila safihi, msengenyaji !

Aliyekusanya mali na kuyahisabu.

Anadhanim kuwa mali yake yatambakisha milele !

Hasha! Atavurumishwa katika Hutama

Na nani atakujuvya ni nini Hutama ?

Moto wa Allah swt uliowashwa.

Ambao unapanda nyoyoni.

Hakika huo utafungiwa nao

Kwenye nguzo zilionyooshwa.

 

21.   Ufujaji wa Neema za Allah swt

Kwa hakika mtu anapopata neema za Allah swt inambidi amshukuru kwa kila alichopewa lakini utaona watu kila wanapozidishiwa neema basi na ukafiri ndivyo unavyozidi kumwingia. Kwa kuwa sasa anao utajiri basi ataanza uasherati wa kila aina hata kuanzisha majumba ya kunywia pombe na kuchezea kamari na kuwaweka malaya ati ni kwa ajili ya starehe zake na marafiki zake. Kwa hakika hayo yote ni ufujaji wa Neema za Allah swt kwani utamwona mtu hatosheki kwa kidogo wala hakinai kwa kingi. Tusifuje neema za Allah swt na badala yake tuzitumie itupasavyo ili tuweze kujenga Aakhera yetu kwa Neema hiyo hiyo kama kutoa misaada kwa wenye kuhitaji, kuwasaidia mayatima na wajane na walemavu, kusaidia mahospitali, kuwachimbia watu visima kwa wenye shida  ya maji, kuwalipia karo wale wanaohitaji ili waweze kusoma na kuilimika, n.k.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Mumin,23, Ayah 43 :

Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Asra’,17,  Ayah 27 :

Kahika wabadhirifu ni ndugu wa Masheitani. Na Shaitani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi.

 

22.  Kosa na Dhambi

Sisi tunaponeemeka basi tunaona kuwa kuna vipingamizi vingi mno kupita kiasi katika maisha na starehe zetu, hivyo ndio mwanzo wetu wa kuanza kujifanyia vile tutakavyo, na kwa kufanya hivyo ndipo tunaanza kufanya makosa na madhambi moja baada ya nyingine. Tunafikia kiwango cha kusema kuwa bila madhambi maisha hayana raha. Allah swt atuepushe na hali kama hiyo, nyoyo zitakuwa zimekufa!

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Zukhruf, 43,  Ayah 74 :

Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannam

Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.

 

23.   Kuvuka mipaka iliyowekwa na Allah swt

Kila  Mwislamu inambidi afuate na kutekeleza kila amri ya Allah swt bila ya kuvunja hiki wala kile na kutokufuata itakavyo nafsi yake. Allah swt ametuwekea mipaka ya kila jambo.

 

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4,  Ayah 14 :

Na anayemuasi Allah swt na Mtume wake, na akaipindkia mipaka yake, (Allah swt ) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

 

MADHAMBI YAMFANYAYO MTU KUINGIA JAHANNAM

 

Makala haya yametarjumiwa na kushereheshwa na:

Amiraly M.H.Datoo  P.O.Box  838 Bukoba – Tanzania    (8/7/2000)

 

Hadithi hii ilisomwa na : Sheikh Akmal Hussein Taheri – Bukoba

 

Mwanadamu  yupo daima anatenda madhambi kutokana na nafsi yake mwenyewe. Malaika walipomwabia Allah swt kuwa mjumbe wake huyu atakuwa mtenda madhambi. Naye Allah swt akawaabia kuwa yeye ayajua zaidi kuliko wao.

 

 Mtu kuchuma mali na kurundika

Mtu yule ambaye atakusanya fedha na kuziweka mahala pamoja bila ya kufaidika yeye wala kuwasaidia wengineo ambapo wapo ndugu zake Waislamu wenye shida ambapo maisha yao yamewawia magumu. Mtume s.a.w.w. amesema kuwa “ufukara ni mbaya zaidi ya ukafiri”.  Vile vile Imam Ali a.s. amesema  Daima muchunge kuwa mwenye “shida masikini asikuijie bali ni wajibu wako wewe uwafikie”

 

Wakati mwingine mwanadamu hufikia wakati wa kukufuru ama kwa kukusudia au bila kukusudia. Siku moja mtu mmoja alikuwa akisafiri kwenda mji mwingine kwa ndege. Ndugu yake ambaye alikuwa akimsindikiza uwanjani hapo alimwuliza “Ewe ndugu yangu ! Je hautakuwa na shida ya fedha wakati ukiwa safarini ?”  Ndugu yake ambaye alikuwa akisafiri alimjibu “Naam Ndugu yangu ! Mimi sitakuwa muhtaji wa Allah swt kwa muda wa juma moja hivi.”  Ndege iliruka na katika muda wa nusu saa hivi kulipatikana habari kuwa ndege hiyo imeanguka na wasafiri wote wameuawa.

 

Hapa siwezi kusema kuwa watu wote hao wamekufa kwa sababu ya kuadhibiwa mtu mmoja aliyetoa maneno ya kashfa dhidi ya Allah swt. Na kwa maani hii ndipo tunapoambiwa kuwa sisi tusijihusishe na mahala ambapo panapotendeka maasi na madhambi kwa sababu inawezekana adhabu za Allah swt zikateremshwa hapo na wewe ukakumbwa pamoja humo.

 

Kisa cha kijana mwenye madhambi.

 

Ma'adh anasema:  "Siku moja nilikuwa nkijiandaa kwenda kwa Mtume s.a.w.w. , na mara nikamwona kijana mmoja akilia mno, basi hapo nilimwuliza sababu ya kilio chake hicho.  Huyo kijana alinibu kuwa yeye ni mwenye dhambi kubwa mno.  Basi hapo nilimwambia aje pamoja nami kwa Mtume s.a.w.w. ili amwombee msamaha kwa Allah swt.  Hapo huyo kijana alisema kuwa alikuwa akiona aibu kuja mbele ya Mtume s.a.w.w. kwa sababu ya dhambi zake."  Hapo Ma'adh aliendelea na safari yake hadi kwa Mtume s.a.w.w. na kumwelezea yale yaliyotokea.  Basi Mtume s.a.w.w.alimwambia akamlete yule kijana. 

Alipofikambele ya Mtume s.a.w.w. aliulizw,  'Je umekuwaje, walia kwa nini?  Hapo huyo kijana akasema,  "Ewe Mtume wa Allah swt! Dhambi langu ni kubwa mno!"  Hapo Mtume s.a.w.w.aliendelea kumwuliza,  "Je kosa lako kubwa au mbingu? "  Akajibu, 'Kosa langu!'  'Je kubwa au dunia nzima?  Akajibu, kosa langu!  Je kosa lako kubwa au msamaha wake Allah swt?  Hapo huyo kijana akasita na hatimaye kukubali kuwa 'Msamaha wa Allah swt ni mkubwa!  Bassi hapo Mtume s.a.w.w. alimwuliza, sasa niambie kosa lako.  Huyo kijana akaanza kusema:  "Ewe Mtume wa Allah swt!  Palitokea kufariki kwa binti mmoja mzuri mno wa kabila la ansaar, na mimi nilikwenda usiku ule kulifukua kaburi ili kutaka kuiba sanda aliyokuwa amevishwa huyo maiti, shetani alinighalibu na kunifanya nikatenda tendo la kinyama kwa maiti huyo, binti aliyekuwa uchi mbele yangu.  Hapo ndipo maiti hiyo ilipota sauti ya masikitiko na kunilaani kwa kuniambia kuwa Allah sw ataniingiza motoni na kuniunguza humo kuteketea.  Ewe mtume wa allah swt kwahakika, baada ya matamshi hayo ya maiti huyo, mimi nimekosa furaha ya kila aina na nimeingiwa na woga na nadhani nitaweza kuangamia katika hali kama hii iwapo itaendelea kunisumbua.  Hapo mtume s.a.w.w. alimwambia huyo kijana:  "Ondoka haraka mbele yangu kwani inawezekana moto wa Jahannam ukanikumba nami pia."  Je kwa nini Mtume s.a.w.w. alisema hivyo?  kwa sababu dhambi lilikuwa kubwa mno!

 

Kwa mujibu wa riwaya, kijana huyo baada ya kuambiwa hivyo, aliondika akiwa amesikitika mno na kuelekea katika milima ya mji wa madina, huko alikaa kwa muda wa siku arobaini akiwa akilia na kuomba Toba kwa Allah swt. Baada ya siku arobaini kupita, alisema:  "Ewe Allah swt!  Iwapo umeshakwisha kuikubalia Toba yangu, basi naomba unijulishe kwa kumpitia Mtume wako.  Na iwapo bado haujaikubali Toba yangu, basi naomba uniteremshie miale ya moto kutoka mbinguni ili inichome na kuniunguza ili niteketee kabisa!"

 

Basi hapo iliteremka Aya ya 134 - 135 ya sura Ali Imraan (3):

"Na wale ambao, wanapofanya tendo la kuaibisha au kudhulumu nafsi zao, wakamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani awasamehee madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu?  Na ambao hawabakii (kwa kukusudia) katika yale waliyoyafanya maovu hali walikuwa wakiyajua hayo,"       

 

 

                         3.  ADHABU ZA KABURINI

 

Sisi sote tunatambua kuwa kuwa kutakuwa na adhabu katika makaburi kwa ajili ya kila mmoja ikiwa ni Mwislamu au asiye Mwislamu. Lakini kunatofauti katika adhabu hizo baina ya makundi hayo mawili ya watu kwani makafiri, wanafiki na wasio wasio Waislamu itakuwa zaidi kuliko Waislamu. Lakini kuna baadhi ya Waislamu ambao wao wenyewe humu duniani wanapuuzia baadhi ya mambo na hivyo katika kituo cha kwanza cha safari ya Aakhera na ambacho ndicho baada ya dunia, watakumbana na magumu na mazito.

 

1.  Sababu za adhabu za Kaburini

 

Ninapenda kuwaleteeni Hadith ya kwanza kutoka Bihar al-Anwar, J.6, uk. 222 inayomnakili Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

1  Kuchonganisha na kufitinisha

“Kwa hakika adhabu ya kaburi ni kali mno kwa yule mtu ambaye ni mchonganishi(mambo na maneno ya hapa anayapeleka huko na ya kule anayaleta huku na kufitinisha )

 

2.  Kutojiepusha na vilivyo Najis

Sisi tunapuuzia mno na hatutilii muhimu Najis iwe katika katika hali yoyote ile kwa mafano mkojo, mavi ,damu na vitu vingi mno vinajulikana.

 

3.  Kutowawia wema wananyumba yake

Mara nyingi tunaona kuwa mtu anakuwa mchungu na mkali kwa familia yake na hata wengine huwadhulumu wake na watoto wake na kuwaonea na kuwanyanyasa. Na hii ndiyo sababu moja kubwa ya adhabu kali za kaburini. Hivyo inambidi mtu awe mwema na mpole na mwenye mapenzi kwa mke na watoto wake na inambidi kuwalinda na kuwatimizia mahitaji yao na kuwalinda.

 

Sa’ad ibn Ma’adh alikuwa ni Sahabah wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na alikuwa mwzuri sana na kwamba sanda na mazishi yake yalikuwa yamesimamiwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe na hata kuteremka katika kaburi lake aliteremka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa Malaika wengi mno walikuwa wameshiriki katika mazishi yake.

 

Mama yake alipopata habari hizo, alisema kuwa Allah swt amjaalie Jannat na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu, “Bila shaka ! Lakini atakuwa na adhabu kali mno kaburini !” Kwa kusikia hayo Masahaba waliuliza, “Je itawezekanaje hivyo wakati bwana Sa’ad alikuwa ni mja na Sahaba mwema ?”  Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwajibu, “Naam, alikuwa ni mtu mwema lakini alikuwa mkali kwa mke wake, na hivyo atapata adhabu kali humo kaburini.” Bihar al-Anwar, J.6, uk. 220

 

4.  Kuteketeza na kufuja Neema za Allah swt 

Yaani kutokutumia yema na ipasavyo neema za Allah swt alizomjaalia mwanadamu ziwe katika hali ya siha yake, watoto au mali. Ama mali ni kule kutumia kupita kiasi kinachohitajika au kutumia visivyo muhimu.

 

5.  Kunkatalia mume kujamiiiana

Kunawahi kutokea mara nyingi miongoni mwa watu kuwa mume anapohitaji kujamiiana na mke wake, mke humyima mume wake tendo hilo la kutimiza haja yake. Kwa hapa mwanamke kama huyu ndiye anatishio kubwa la adhabu kali za kaburini.

 

6.  Kupuuzia na kudharau Sala

Sisi tunatabia ya kupuuzia na kuidharau Sala tano za siku na zinginenezo zilizofaradhishwa. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , “Yeyote yule anayeipuuzia Sala, si miongoni mwetu.” Na vile vile amesema, “Mtu kama huyo hatapata nusura yetu Siku ya Qiyama.”

 

Vile vile Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema kuwa baba yake mzazi Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. amesema, “Wakati wake wa mwisho, alimwambia kuwa ‘mtu yeyote anayeipuuzia Sala basi hatapata nusura zetu Siku ya Qiyama.’”

 

7.  Kuwatetea wadhulumiwa

Mara nyingi tunaona kuwa wadhalimu wanawadhulumu watu wengine na sisi katika hali kama hiyo tukibakia kimya bila ya kujaribu kuwatetea hao wanaodhulumiwa, basi hivyo ndivyo itakuwa ndivyo sababu yetu ya kuadhibiwa kaburini.

 

8.  Kuwasengenya watu wengine

Siku hizi tumekuwa na tabia moja ya kujiburudisha na yo ni kuandaa mabaraza ya kukaa na kuwakejeli na kuwasengenya watu, kuchimbua aibu zao na kuongezea chumvi na pilipili katika maneno yetu ili kunogesha hadithi zetu. Tunasahau kuwa kufanya hivi sisi tunamharibia jina na sifa za mtu ambaye labda hakuyafanya hayo.

 

2. Sababu za kupunguzwa kwa adhabu za Kaburini

 

Kama vile tulivyokwisha kuona kuwa zipo sababu zinazosababisha adhabu za kaburini basi tusife moyo kuwa hakuna njia ya kupunguzwa au kuwa hafifu. La, si hivyo, daima zipo sababu za kupunguziwa adhabu hizo za kaburini na vile vile hali yetu ikawa njema zaidi humo kaburini.

 

1.  Sala za Tahajjudi au Salatil Layl

Inambidi mtu asali sala raka’a nane za salatil Layl na raka’a mbili za shufa’a na raka’a moja ya witri ambamo katika qunuti yake kunasomwa Astagh firullah wa atubu Ilaihi mara sabini. Basi zipo Ahadith zinazosadikiwa hususan kutokea kwa Al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. katika Safinatul Bihar,J.2, Uk.397 maudhui Kuhusu Kaburi kwamba : “Iwapo mja anasali raka’a nane za salatil Layl na raka’a mbili za shufa’a na raka’a moja ya witri ambamo katika qunuti yake kunasomwa Astagh firullah wa atubu Ilaihi mara sabini, basi hatakosa faida zake kama zifuatazo, atakuwa amepona fishar-i-kabr na ataepukana na Moto wa  Jahannam , umri wake utakuwa mrefu, Allah swt ataongezea baraka katika riziqi yake.” 

 

2.  Kutekeleza Rukuu na Sujuda kwa usahihi katika Sala

Kwa mtu ambaye anasali sala zake vile ipasavyo, basi hatakuwa na sababu ya kujibiringita kama kwamba anafanya mazoezi ya mwili, kumbe masikini anasali. Tunawaona wengi sana wakisali lakini kwa mbio kama kwamba wanashindana na katika hali kama hii hata usomaji na matamshi pia hayawezi kamwe kuwa sahihi. Tunasali ilimradi tu tumesali, sasa sala hiyo inamaana yoyote mbele ya Allah swt ?

 

3.  Kusali Sala zilizo Sunnah na kutoa Sadaqah

Tunasisitizwa mno kutimiza Sala zilizofaradhishwa na vile vile tupate muda wa kusali zilizo Sunnah na vile vile kusoma Dua kidogo na vyote hivyo kwa unyenyekevu na kwa moyo uliotulia. Sambamba na hayo tutoe sadaqah kuwasaidi masikini ambavyo kuna faida kwa pande zote mbili.

 

4.  Kusali Sala ya Wahshat

Anapokufa Mumiin basi inatubidi kusali sala hiyo usiku wa kwanza kuzikwa kwake kwani inamsaidia maiti huyo na vile vile iwapo tutawasalia wengine basi Allah swt atatujaalia watu wa kutusalia pale tutakapokufa ili nasi tufaidike na thawabu hizo ambazo zitatupunguzia adahabu zetu,

 

5.  Kwenda Makkah kwa ajili ya Kuhiji

Inatubidi sisi katika maisha yetu kwa mara moja kwenda Kuhiji, lakini kwa kutimiza masharti ya amri hiyo. Na tuwe na moyo kwa ajili ya hivyo. Wapo watu wengi ambao wanapuuzia swala hili ambalo ni faradhi kwao.

 

 

6.  Kifo katika usiku wa kuamkia Ijumaa au siku ya Ijumaa

Iwapo mtu atabahatika kufa katika usiku wa kuamkia Ijumaa au siku yenyewe ya Ijumaa, basi adhabu za kaburini zitapungua. Sisi hatutambui fadhila na Baraka za usiku huu na siku ya Ijumaa katika maisha yetu. Lau mtu atafanya utafiti kujua zaidi basi atashangaa kusikia au kusoma fadhila na baraka zake.

 

7.  Jariratain

Wakati wa kumzika maiti huwekewa matawi mawili yalio mabichi. Inasemekana kuwa mtu huyo hatakuwa na adhabu za kaburi kwa kipidi cha kubakia ubichi ka matawi hayo.

8.  Kumwagia maji juu ya kaburi

Ipo riwaya kuwa kwa kumwagia maji juu ya kaburi kutamfanya mtu huyo aliyezikwa humo asipate adhabu za kaburini hadi hapo kutapokauka maji juu ya kaburi hilo.

 

9.  Kusomwa kwa Surah maalum za  Qur'an Tukufu

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa , “Mtu yeyote atakayesoma Surah Al-Hakumu Takathur… atapona adhabu za kaburi.” Na vile vile Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa “Yeyote atakayeisoma Surah al-Nisaa kila siku ya Ijumaa basi huyo atapona adhabu za kaburi .” Safinat al-Bihar, J.2, Uk. 397

 

Na Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. amesema kuwa ,”Mtu yeyote atakayesoma Surah al- Qalam, hatapata adhabu za kaburini.” Na vile vile  iwapo atasma Sura Zukhruf au kusomwa kwa Sura al-Ya-Sin (ambayo inajulikana kama ndiyo moyo wa  Qur'an Tukufu ) ama wakati wa magharibi au usiku kabla ya kulala, hatapata adhabu za kaburi.”

 

Vile vile kusomwa kwa Ayah za mwisho katika Surah al-Baqarah, kutamwepusha na adhabu za kaburi, Ayah zenyewe ni :

Rabbana la tuakhidhna in nasina au akhta’ana. Rabbana wala tuhamilna ‘alayna isran kama hamaltahu ‘alal ladhina min qablina Rabbana wala tuhammilna ma la taqatalana bihi wa’afu ‘anna waghfirlana warhamna anta Mawlana fansurna ‘alal qawmil kafiriin.

 

10.  Kuuawa katika njia ya Allah swt

Iwapo mtu atafariki akiwa katika njia ya Allah swt kama katika vita , basi mtu huyo hana adhabu ya kaburi. Na hivyo ndivyoamesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran , Ayah 169 – 170 yaani ni kwamba wale wanaouawa katika njia ya Allah swt si watu waliokufa bali ni mashahidi na wapo hai.

 

11. Kumsalia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahlul Bayt a.s.

Na kwa kumsalia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja Ahl ul-Bayti a.s. kwa wingi kutamwepusha mtu na adhabu za kaburini.

 

Vile vile ipo katika riwaya kuwa mtu yeyote aanzaye dua yake kwa Bismillahir Rahmanir Rahiim na Salawati (Allahumma Salli ‘ala Muhammadin wa Ale (ahali) Muhammad )  na kumalizia kwa Salawati, basi kamwe dua yake hiyo haitarudishwa kwani salawati inakubaliwa na Allah swt. Sasa itawezekanaje mwanzo wa dua na mwisho wa dua vikakubaliwa na vya katikati vikatupiliwa mbali ?

 

12.  Mapenzi ya Ahlul Bayt a.s.

Tunaelewa waziwazi vile fadhila za Ahlul Bayt a.s. zilivyo na vile Allah swt pamoja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. walivyokuwa wakiwasifu hao na kutufaradhishia mapenzi yao juu yetu na hata kama salaikisaliwa bila ya kusomwa kwa salawati ndani yake basi sala hiyo itakuwa batili.

 

Kuwapenda Ahlul Bayt a.s. ni kuwapenda wafuasi na marafiki zao na kuwachukia na kuwalaani maadui wao. Je itawezekanaje adui wa kiongozi na mpenzi wako akawa rafiki yako ?

 

13.  Mwanamke kufanyia subira umasikini na shida za mume wake

Kwa hakika katika maisha yetu haya ya duniani kuna mambo mengi mno ambayo yanajitokeza katika maisha ya ndoa. Kuna wakati ambapo mume huwa ni masikini, hivyo inambidi mwanamke aumke kufanya subira na kustahimili shida zinazojitokeza na kumpata hima bwana wake ili sivunjike moyo bali aendelee na jitihada zake za kuondokana na umasikini. Vile vile kunawezekana kwa mume kuwa mtu mwovu ambaye hana matendo mema kama mlevi, mgomvi n.k.  Katika sura zote hizo na zinginezo, inambidi mwanamke afanye subira na kujaribu kustahimili katika mazingira hayo, na wla si kuamua kumpa talaka mume au kutoroka nyumbani. (Ingawaje talaka ni neema mojawapo ya Allah swt, hivyo isitumie vibaya ).

 

14.  Kusoma Ziyarah ya Imam Hussein a.s.

Imesisitizwa kuzuru kaburi la Imam Hussein a.s. usiku wa kuamkia Ijumaa na kusoma Ziyarah. Kwa hakika sisi tukiwa mbali mno, huwa tunasoma Ziyarah  ambavyo kwa hakika kutatuepusha na adhabu za kaburi.

 

15.  Kuzikwa Najaf

Iwapo mtu atazikwa katika maeneo yanayozunguka kaburi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. huko Najaf, basi hatakuwa na adhabu za kaburi.

 

16.  Kuwasaidia masikini na wasiojiweza

Kwa kutoa misaada kwa ajili ya kuwasaidia masikini na wasiojiweza na wale wanaohitaji misaada, kwa hakika kutamwepusha mtu na adhabu za kaburi. Inawezekana mtu akatoa hivyo katika uhai wake kwa ajili ya kupata thawabu yeye mwenyewe au akatoa kwa niaba ya wale waliokwisha fariki dunia hii, basi thatwabu hizo zitawafikia hao marehemu.

 

Siku moja alifariki mtu mmoja katika zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye alikuwa tajiri mno. Aliacha wusia kuwa mali zote zilizokuwa zimejaa mabohari yake zigawiwe sadaqah kwa masikini, baada ya kifo chake. Kwa hivyo, kwa mujibu wa wusia wake, baada ya kifo chake, mabohari yalianzwa kugawia vyakula kwa masikini. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwepo hapo na mwishoni wakati wanapitisha ufagio, waliokota kipande cha tende moja, na kwa kuiondoa hiyo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema, “Lau huyu mtu angalikuwa ametoa angalau hata kama mbegu moja kama hii ya tende katika uhai wake, basi mbegu moja ya tende ungali kuwa na thawabu ya mlima wa Abu Qobays (mlima mkubwa mno).”


                          Makala mchanganyiko

 

1.   SABABU ZINAZOFANYA NYOYO KUFA

 

Makala haya yametarjumiwa na kushereheshwa na:

Amiraly M.H.Datoo  P.O.Box  838 Bukoba – Tanzania

 

Hadithi hii ilisomwa na : Sheikh Akmal Hussein Taheri – Bukoba

 

Al – Imam Ja’afer as-Sadiq a.s  amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa mambo manne husababisha nyoyo za watu kufa ambazo ni:

 

1.Kutenda dhambi baada ya nyingine

Mwanadamu anapoanza kutenda madhambi nafsi yake inamzuia na kumtolea lawama ili asitende maovu. Lakini pindi anapoanza kukaribia madhambi, roho yake inaanza kuzoea na ile hali ya kujilaumu inaanza kupungua nguvu na hivyo ndivyo anavyojizoeza na hatimaye anahisi kuwa ni jambo la kawaida wakati wa kutenda dhambi. Kwa hivyo anatenda ovu moja na kuendelea kuyatenda mengine mengi bila ya kuhisi kuwa na dhambi na hata unafika wakati ambapo hajisikii vema hadi hapo anapokuwa ametenda madahmbi. Kwa kutoa mifano, ipo mifano mingi mno mbele yetu zilizo bayana. Mtu mmoja anapokaribia kunywa pombe, atakataa kata kata, lakini utaona akibembelezwa na kushurutishwa na marafiki zake walio waovu wenye kuwa ajaribu kidogo, na akishajaribu kidogo watamlazimisha anywe zaidi na zaidi. Na hali hii itakapoendelea bele hivi hivi, utaona mtu huyo ndiye wa kwanza kuagiza pombe na vile vile atakuwa akijiwekea nyumbani mwake. Heshima zote atakuwa amezipoteza na maovu yote yatakuwa yametundikwa shingomi mwake kwani atapoteza fedha, ataharibu siha yake, atawatukana wazazi, kaka, ndugu, majamaa na hata kuthubutu kuwapiga mke na watoto wake. Kwa kifupi familia nzima itakuwa imetumbukizwa katika janga kubwa.  Huyu pamoja na pombe ataongezea dhambi lingine la kuwatafuta malaya na kuvuta bangi na madawa ya kulevya. Haya ndiyo maangamizo makubwa kabisa.

 

Allah swt amewaamrisha Malaika kuwa: Mtu anaponuia kutenda jambo jema wamwamdikie thawabu. Na anapoanza kutembea katika kulifanya tendo jema basi hapo pia anaongezewa thawabu nyingi na pale anapolianza kutenda tendo jema basi huongezewa zaidi ya hayo na anapomaliza kulitenda tendo jema basi hapo analipwa thawabu nyingi mno zisizo na  hisabu.

 

Lakini mtu anaponuia kutenda dhambi basi hapo haandikiwi adhabu, na anajitoa kwenda kutenda dhambi napo pia haandikiwi kwa sababu inawezekana akarudia njiani na anapolianza tendo ovu pia kuna uwezekano wa kutolikamilisha na kwa masikitiko makubwa, anapolikamilisha basi kwa huruma zake Allah swt, huandikiwa dhambi moja tu.

 

 

2. Kuongea zaidi pamoja na wanawake

Islam haitukatazi kuongea na wanawake wasio wake zetu lakini kinachokatazwa ni ile hali ya watu kuongea mambo ambayo yanapita mipaka na huku ndiko kunapoanza kuteketea maadili. Utawasikia watu wakizungumza pamoja na wanawake mambo ambayo hayana heshima na kufanyiana dhihaka na hatimaye wanapozoeana katika tabia hii utakuta wanaanza  maneno ya kudalilisha kuwa wanapendana na wanahamu ya kuingiliana, na haya ndiyo yanayo tokea. Bwana Daud alimwusia mwanae kuwa ajiepushe na mazungumzo pamoja na wanawake kwani mwanamme anapokutana na mwanamke, katikati yao huwa yupo Sheitani kwa ajili ya kuleta madhambi.

 

Uislamu unamtaka mwanamke abakie katika hadhi na heshima aliyopewa na Allah swt. Hivyo mwanamke anapoongea na mwanamme inambidi asitoe sauti nyororo yenye kuvutia bali inambidi atoe sauti ambayo haitamfurahisha mwanamme na hivyo asitamani kuongea tena na mwanamke huyo. Na kwa misingi hii, mwanamme hatakiwi kumtolea salaam mwanamke ili asije akaisikia sauti yake. Lakini dunia hii imebadilika, leo katika maredio na televisheni utawaona wanawake hata wanasoma Qur’an kwa sauti za kuvutia.

 

Vile vile tusisahau kuwa kuwadokozea macho wanawake pia ni dhambi. Zipo zinaa za macho na midomo.

 

3. Kuzozana pamoja na mwehu

Yeye atasema na wewe utasema  bila ya kufikia maelewano baina yenu. Mutazozana kwa muda mrefu wakati ambapo watu watakaokuwa wakiwaona hawatajua tofauti baina yenu. Mwishoni hamtafikia jambo la kheri.

 

Hao ni watu ambao hawaongei katika mipaka ya ilimu, dini na adabu.

 

4. Kukaa pamoja na watu waliokufa

Kwa kukaa na kufanya mazoea ya urafiki pamoja na watu waliopotoka, kutatufanya na sisi pia tupotee na kutumbukia katika ujeuri, majivuno na takaburi mambo ambayo Allah swt hayapendi na anyachukia na kuyaadhibu. Qur’an inatuambia kuwa nyoyo zao zina magonjwa na Allah swt anawaongezea magonjwa baada ya magonjwa kwa kutokana na maovu yao yanavyoongezeka.

 

Kwa hayo Waislamu walimwulizaa Mtume s.a.w.w.  Je ni wakina nani waliokufa?   Mtume s.a.w.w. aliwajibu  Kwa waliokufa wanamaanishwa wale matajiri wenye takabburi na majivuno. Urafiki pamoja na watu kama hawa utakufanya wewe uwe na tamaa ya dunia na kujipatia mali ufahari na majivuno. Hao wanachokithamini ni kile kinachowaletea faida wao tu. Dharau majivuno ndiyo mavazi yao.

 

Hapa kuna aina nne ya watu: (1). Wale wanaokula na kuwalisha wengine  (2) Wale wanaokula na kuwanyima wengine  (3)  Wale hawali wenyewe na wala hawawapi wengine wale  (4) Wale wanaowanyan’ganya wengine ili wale peke yao.

 

Nasiha: Inatubidi sisi tujiepushe na mambo yote ambayo Allah swt hapendezewi na tufuate Hadithi na Sunna za Mtume s.a.w.w. pamoja na Maimamu 12 a.s. na vile vile tufanye tawba kwa yale tuliyokwisha ya tenda katika hali ya ujahili wetu na kamwe tusirudie kuyatenda. Allah swt ndiye Mwenye kuyaona, kuyasikia na kuyafamu yote.

 

25th June 2000

 

2.  MAADILI YA ISLAM

 

Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na

Amiraly M.H.Datoo  -  Bukoba  Tanzania

 

Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni fardhi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika ametambua Allah.”

 

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amebainisha kuwa: “Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

 

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:

 

Hapana shaka kuwa mwanadamu hana zaidi ya moja, lakini hii nafsi au roho inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama ‘nafsi ya kujilaumu’ ‘au nafsi ya kuamrisha’ ‘nafsi inayotosheka’ (kama vile vielezwavyo katika Qu’rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

 

NAFSI SAFI AU THABITI (nafsi au thabiti.)

 

Katika Qur’rani Tukufu, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-“Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo safi” (26:89)

 

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

 

Imenakiliwa kutoka kwa Imamu Sadique (a.s) kuwa: “Moyo ulio msafi- halisi ni ule   ambamo hakuna chochote kile ila Allhah (s.w.t) tu”

 

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allhah tu.

 

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Mtumfu (s.a.w.w.) ambamo twaambiwa: “Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba yake, mama yake, watoto wake mali yake na hata kuliko maisha yake.”

 

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah (s.w.t.) na wale wapendwao kwa ajili ya Allah (Mtume na Ahali yake)

 

NAFSI YENYE KUTUBU (al-Nafs al- Muniib).

 

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni ‘kutubu’ na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Mwenyezi Mungu.

 

“.. Na anayemuogopa ( Mwenyezi Mungu Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa m oyo ulioelekea ( kwa Mwenyezi Mungu).” (50:33)

 

Kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah (s.w.t) kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah (s.w.t.) imo ndani yake thabiti. Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Mwenyezi Mungu yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah na wala haitorudi kamwe kwa Allah.

 

NAFSI MWONGOZI (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur’rani inatuambia: (64:11).

 

“..Anayemuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake”

 

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah (subahana wa Tala), yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yale yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

 

NAFSI ILIYO RIDHIKA (al-Nafs al- Mutmaina)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni “kuridhika. Qur’an:

“ Sikiliza: Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. “(13:28)

 

Na vile vile mwishoni mwa sura al-Fajr twaabiwa (89:28)

“Ewe nafsi yenye kutua”!

“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika.”

 

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah (swt) tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza mghalimu na kumpotosha yeye.

 

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume mtukufu (s.a.w.w.) na ma - Imamu (a.s.), waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

 

AL-NAFS AL-MUTTAQI (nafsi ya tahadhari ya uadilifu):

 

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, (The virtuosly cautious self) nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na roho) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali  hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu:-

“...Anayezihishimu alama za (dini ya ) Mwenyezi Mungu, basi hili

ni jambo la katika utawala wa nyoyo. “(22:32)

 

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha “Taqwa” kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allhah (s.w.t.) na yele yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, sheriah, waumini wake Makka Ka’aba Tukufu n.k. kwa ufupi. Chochote kile kinachohusika na Mungu huwa kina kuwa na umuhimu na ta ‘adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya  ‘taqwa’

 

NAFSI NYENYEKEVU (al- Nafs al- Mukhbit)

 

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu (uvumilivu), yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah (swt)

 

Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Surah al Halj: (22:54)

“..waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao”

 

Kwa sababu nyoyo hizi hujiimamisha chini mbele ya Mungu na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allhah s.w.t  hawavunji kamwe maamrisho  ya Mwenyezi Mungu na wala hazisaliti au kuzipinga.

 

NAFSI HALISI (al-Nafs al-Zakiyyah):

 

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au roho iliyo mtakatifu (the pure self). Katika Qur’ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akisemea nafsi, anatuambia:

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)” (91:9 & 10)

 

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwakuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele. (The person whose self become purified is assured of salvation and bliss!)

 

NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (al-Nafs al- Lawwama).

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu  hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur’ani Tukufu inatuelezea:

“Naapa kwa siku ya Kiama. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”. (75:1-2).

 

Ni dhahiri kuwa iwapo Mwenyezi Mungu akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

 

NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (al-Nafs al-Mulham):

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Mungu. Twaambiwa kaika Qur’ani:

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake”  (91:8)

 

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- ‘Nafsi halisi si’ ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah (swt) yatafikia kikomo chake.

 

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

 

NAFSI YENYE MADHAMBI (al-Nafs al-Athima):

 

Iwapo roho au nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur’ani inazungumzia kulipa kwa amana:

“Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia

       dhambini.”(2:283)

 

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

 

NAFSI ILIYO SINZIA (al-Nafsal-Ghafil)

 

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah (swt). Anaelezea Mwenyezi Mungu katika Qur’ani Tukufu

 

“Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata

          matamanio yao.” (18:28)

 

NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (al-Nafs al- Matbu)

 

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho  ya kungwa, inatuambia:

“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao    kwasababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

 

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allhah (swt) hadi kudharau na kutokubali ujumbe wake na maamrisho ya Allah ambayo Mwenyezi Mungu ambazo amewekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo moyo wake unaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho Matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athali yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimiza kwa nafsi na kushindwa kwake.

 

NAFSI ILIYO POFUKA ( al-Nafs al- Amya):

 

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Qur’ani inatuambia kuwa:

“Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka. (22:46)

 

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah (swt) na hazimwoni Mwenyezi Mungu. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah (swt) na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

 

NAFSI YENYE MARADHI (al-Nafs al-Maridha):

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.”(2:10)

 

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Mwenyezi Mungu) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na akhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa avutiwa navyo kama kambwa ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi ilikwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

 

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika sala na kutii Sheria Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa huo moyo wake umeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kisita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur’rani Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga waa moyo, i.e.., wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), ili waweze kuitibu nafsi  ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

 

NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (al-Nafs al-Za’igha):

 

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.

 

Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakubwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Mwenyezi Mungu. I.e njia iliyo nyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu

 

Katika Qur’ani, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Mwenyezi  Mungu anatuambia:

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi.”(3:7)

 

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih au allegorical) wa aya za Qur’ani ili kuitumia Qur’ani kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

 

NAFSI YA MOYO MGUMU (al-Nafs al-Qasiya)

 

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili.

“..Na tukazifanye nyoyo zao kuwa ngumu” (5:13)

“..Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu” (57:16)

 

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

 

NAFSI WASIWASI (al-Nafs al-Murtaba):

 

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu iipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya dini ya Islam kama vile kushuka kuwapo kwa Allah (swt), akhera, Unabuwa na vile vile Uimamu (a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.

 

“Nyoyo zao zina shaka; kwahivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao.” (9:45)

 

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza hadi aya za Quarani na hadithi Tufuku za Mtume (s.a.w.w.) na ma -Imam (a.s.) na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

 

NAFSI ILIYOPATA KUTU (al-Nafs-al-Ra’ina):

 

‘KUTU’ ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha moyo ambavyo ni sehemu ya umuhimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza rudishwa iwepo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Mwenyezi Mungu.

 

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Mwenyezi Mungu kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Mwenyezi Mungu, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia (reflect ) kutoka na kwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa matilaba yake. Qurani ikiwa inatumbusha kuwa:

 

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.” (83:14)

 

Katika ‘aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba mara moja kwa  ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadithi Tukufu kuwa: “Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Kiama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Mwenyezi Mungu’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa Hivyo inambidi kila Mwislam mmoja wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Mwenyezi Mungu azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

 

NAFSI AMURU (al-Nafs al- Ammara):

 

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matnedo ya madhambi bila kiasi. Katika Qurani, kuhusu kisa cha Mtume Yussuf, Nafsi inasemwa:

“Nami sijitasi  Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu (12:53)

 

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Nabii Yussuf. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Yussuf alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile zidi ya Yussuf. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Yussuf au ni wote vyovyote vile, Qur’an inatuambia kuwa “Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. (12:53)

 

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na  ma’asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, iliramdi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na matilaba yake; na ile nafsi elimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na  kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

 

HATIMAYE: Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu  kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa ‘Nafsi halisi na  ‘Nafsi ridhika’ n.k.  na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya “kupigwa mihuri” au ‘zilizopofuka’ na ‘zenye maradhi’ zikiwa ni kama mifano.

 

Hali hii inadhihiridha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

 

     JE UMEJING’AMUA UNA NAFSI YA AINA GANI UNDANI MWAKO??

                                         (JITAHADHARISHE)!

 

 

 

3.  DHULUMA ZA AINA TATU

 

Makala haya yametarjumiwa  na:

Amiraly M.H.Datoo  P.O.Box  838 Bukoba – Tanzania

 

Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2, uk.330

“Zipo aina tatu za dhuluma: “Aina ya kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi.”

 

Ama dhuluma ambayo anaisamehe ni ile ambayo mtu huitenda baina yake binafsi na Allah swt. Na dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni kukufuru na dhuluma ambayo haipuuzii ni ile ambayo inatendewa dhidi ya haki za watu.”

 

Ufafanuzi:

Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

 

4.  MAKUNDI MANNE YA WATU

 

Imenakiliwa kutoka Jaafer ibn Muhammad naye kutokea Baba, naye kutokea kwa Babu yake naye kutokea kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kwamba Mtume s.a.w.w. alisema katika wasia wake.

 

Alisema Mtume s.a.w.w. “ Ewe Ali ! Kuna makundi manne ambamo watu wanapatikana wamegawanyika kwa mujibu wa matendo yao humu duniani.[3]

 

A. Kupanda daraja

 

1. Kutawadha wudhuu katika baridi

Kwa hakika ni jambo gumu mno kuamka na kujiweka tayari kwa ajili ya ibada za Allah swt hasa kama utakuwapo kazita sehemu ambazo kuna baridi kali ambapo hata kunakuwa na hatari ya watu wengine kuathirika kwa baridi kali. Wakati huyo unakuwa ndio wakati mzuri wa kujipatia usingizi mnono na nguvu za Shaitani zinakuwa zikitushawishi sisi tutoe visingizio mbalimbali ili mradi tusiamke na kufanya ibada za sala hususan za Alfajiri.

 

2. Kusubiri sala baada ya sala .

Mumin wa kweli kwa hakika anakuwa akiusubiri wakati wa sala kuwadia kwa ajili ya kutaka kusali sala kwa mara nyingine. Fursa hii anaisubiri kwa hamu kwa sababu anapata fursa kwa mara nyingine kumwabudu na kumshukuru Allah swt na ni wakati mwema kwa ajili ya kuomba Tawba ya madhambi yake na vile vile ni wakati mwingine wa kujipatia neema na baraka za Allah swt. Kwa kifupi mumin huyoo amabye anausubiri wakati wa sala uwadie anakuwa na hamu ya kujipatia bahati ya kuweza kujiweka mbele ya Allah swt.

 

Tukiangalia mfano wa kidunia, iwapo mimi nitaambiwa kuwa nimepewa kibali cha kumzuru Raisi wa nchi yetu nyakati fulani fulani kwa siku. Hivyo mimi baada ya kumzuru mara ya kwanza kwa siku, nitakuwa na hamu na shauku ya kuwadia kwa muda wa mara pili na hivyo hivyo kwa mara zote. Kwa hakika nitaiona saa ikienda pole pole mno.

 

Na hivyo ndivyo inavyokuwa hali ya Mumin kwa ajili ya kutaka kuwa mbele ya Allah swt kwa nyakati angalau mara tano kwa siku.

 

3. Kutembea usiku na mchana kwa miguu kuelekea Jamaa’

Mumin kwa hakika daima hupenda kujumuika pamoja na jama’a yake katika mambo yote ya jumuiya yake na sala za jama’a .

 

Mtume s.a.w.w. amesema:

“Kwa hakika Allah swt hawakutanishi Ummah wangu katika upotofu, na mkono Wake uko pamoja na Ummah huo, kwa hakika atakayejitoa humo basi atambue kuwa amejitoa kwa ajili ya Jahannam….”   Mizan al - Hikmah.

 

B. Kaffarah  ya madhambi.

 

1. Kutoa na kupokea salaam kwa unyenyekevu.

Mumin huwa daima mwepesi wa kutoa salaam na kujibu salaam anazotolewa. Kamwe hawi mtu mwenye dharau wala kutegea kutolewa salaam au mwenye kiburi.

 

Allah swt anatuambia katika Quran kuwa tutolewapo salaamu ni faradhi kuijibu ama kwa kurejea salaam hiyo hiyo au kuijibu kwa ubora zaidi.

 

Mtume s.a.w.w. alikuwa akiviziwa na ma Sahaba wake kwa kujificha kiasi kwamba wapate fursa ya kutangulia kutoa salaam kwa sababu Mtume s.a.w.w. alikuwa ndiyo daima mtu wa kutoa salaa kwa mara ya kwanza. Sasa sisi tunayo kiburi cha  nini ? Kwa hakika Allah swt anatuambia kuwa Salaam ni kauli itokayo Kwake.

 

2. Kuwalisha chakula wale wanaohitaji.

Mumin kwa hakika huwa na moyo wa huruma kiasi kwamba hawezi kula peke yake huku watu wengine wakiwa katika hali ya kubakia katika njaa. Na si hayo tu bali huwa na moyo wa kutaka kuwasaidia binadamu wenzake katika kila hali awezayo yeye.

 

Yeye huwa karimu na kamwe hawi bakhili ambaye yeye mwenyewe hula bila ya kuwapa wenzake.

 

3. Kusali sala za Tahajjud ( salat al - Layl au usiku wa manane ).

Mumin huwa anasali sala za usiku wa manane (Tahajjud ) wakati ambapo watu wanapokuwa wamelala usingizi mnono. Na husali kwa kutaka ridhaa ya Allah swt na wala si kwa kujionyesha kwa watu.

 

Kwa hakika sala hii huwa ikisaliwa na Mitume  a.s. na Ma-Imamu a.s. kila siku bila ya kukosa. Hii ni ibada ambayo mtu huwa anamnyenyekea Allah swt wakati ambapo anakuwa ametulia kiroho na kiakili. Huwa hana mawazo au mambo yanayomsumbua huku na huko. Hivyo inamaanisha kuwa ibada hii inafanyika kwa roho khalisi na mtu hukubaliwa ibada zake haraka zaidi katika sala hizi.

 

Imam Hussain a.s. siku ya Aashura alimwusia dada yake Bi. Zainab binti Ali ibn Albi Talib a.s. kuwa : “Ewe dada yangu Zainab ! Naomba usinisahau katika sala zako za usiku i.e. Salat al-Layl.”

 

C. Waangamio

 

1. Tabia mbovu

Wale watu wote wanaoingia katika kikundi hiki cha wenye tabia mbovu kwa hakika mwisho hao hujikuta kuwa wameangamia na kupoteza maisha yao. Yaani maji yameshakwisha mwagiga hayazoeleki tena. Tabia kama hizi zinamwigiza katika upotofu na kiburi na kujiona kuwa wao ndio watu waliostaarabika lakini kumbe ni kinyume na hali hiyo kwani Allah swt hawapendi wale wanaojifakharisha na kutakabari.

 

2. Kutii nafsi zao

Iwapo mtu ataitii nafsi yake katika kumpotosha basi atakuwa kwa hakika amepotoka na kuangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja.

 

Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.: “Yeyote yule atakayeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika amemtambua Allah swt.”

 

Vile vile amesema kuwa : “ Kwa hakika hodari kabisa ni yule ambaye ameighalibu nafsi yake.” Yaani nafsi yake haimpotoshi katika mambo mengi mno kama vile ulafi, uchoyo, ubakhili, uasherati, ukafiri, maasi  n.k.

 

Iwapo mtu atatawaliwa na nafsi yake basi atakuwa mtumwa wa nafsi yake.

 

Msomaji anaombwa kusoma makala niliyoyatoa katika Sauti ya Bilal , P.O.Box 20033 DSM juu ya maudhui Maadili ya Kiislamu - sura izungumziayo juu ya sifa 18 za nafsi,Juzuu XXXI, Na. 5, Rabiul Aakhar 1418, Septemba 1997. (Iliyochapwa katika sehemu mbili.)

 

3. Kujifakharisha

Kwa hakika mtu anapoambukizwa ugonjwa huu basi atambue kuwa ameangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja. Mtu anapenda kujionyesha kuwa yeye ndiye mtu bora zaidi kuliko  wengine kwa sababu ya kupata kwa mali zaidi au ilimu au wadhifa. Vitu vyote hivi ambavyo sisi tunavijua kuwa ni vyote vyeneye kuangamia na kupotea na tutaviacha humu humu duniani.

 

Mtu katika sura hizi anaanza kukufuru kwani anaanza kuwasema na kuwaona watu wenzake kama wanyama na waovu kiasi cha kuthubutu kusema ati wanamsumbua na kumpotezea wakati wake. Inambidi yeye kutambua kuwa Allah swt amemwingiza katika mtihani hivyo inambidi afanye mema ili aweze kufuzu.

 

D. Uokovu

 

1. Hofu ya Allah swt katika hali ya dhahiri na batini

Iwapo mtu atataka kupata uokovu inambidi awe na khofu ya Allah swt wakati akiwa peke yake na vile vile anapokuwa mbele ya watu. Isiwe kwamba mtu anapokuwa peke yake anaruhusiwa kufanya madhambi na wakati anapokuwa mbele ya watu kujionyesha kuwa ni mtu ambaye ana khofu ya Allah swt kupita watu wengine.  Kutenda madhambi katika hali yoyote yanayo adhabu kali.

 

2. Kusudio madhubuti katika umasikini na utajiri

Mtu inambidi awe na makusudio yake madhubuti bila ya kuyumbishwa katika hali ya umasikini na utajiri pia. Kwa sababu anapokuwa na moyo wa kuwasaidia watu wenzake katika ufukara asiupoteze katika hali awapo tajiri. Iwapo alikuwa msalihina awapo katika ufukara basi aendelee vile vile kwani asije akatoa kisingizio cha kukosa wakati katika utajiri na biashara zake.

 

Vile vile mtu anapokuwa katika umasikini inambidi awe madhubuti katika imani yake ili asije akakufuru na kushuku uadilifu wa Allah swt kwa shida azipatazo maishani mwake. Kila mtu anakumbana na misukosuko mbalimbali humu duniani hivyo inambidi kuimarisha imani yake.Huo pia huwa ni wakati wa mtihani kutoka kwa Allah swt, na inambidi ajaribu kufuzu.

 

3. Uadilifu katika shida na raha

 

Inambidi mtu awe daima katika mizani ya kauli yake asije akatamka maneno ambayo yatamkufurisha wakati anapokuwa katika shida au raha. Anapokuwa katika shida asije akasema kuwa Allah swt amemtupa au hamjali wala hazisikii duaa zake (Allah swt atuepushe na wakati huo) na pale anapokuwa katika utajiri na starehe asije akakufuru kuwa yeye hana shida ya kitu chochote au mtu yeyote kwani anacho kile anachokihitaji, hivyo kujifanya maghururi na mwenye takabbur. Kwa hakika Allah swt hawapendi watu kama hawa.

 

Kwa wale walio matajiri inawabidi wafanye mambo mema kwa kutoa misaada kwa misikiti,madrasa masikini na mahala pote pale penye kupata ridhaa za Allah swt na wale walio masikini na mafukara inawabidi wakinai kwa kile walichonacho na wamshukuru Allah swt kwa kile anachowajaalia.

 

Maneno yetu yawe yamepimwa vyema kabla ya kuyatamka kwani isije tukasema mambo ambayo yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa adhabu za Allah swt. Na wala tusiwaseme watu vibaya kwani na hayo pia yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa Adhabu za Allah swt.

 

Hadith  hii imesomwa na Sheikh Akmal Hussain kutoka Moshi, Tanzania.

 

Hadith hii imeshereshwa na:  Amiraly M.H.Datoo       8th May 1998

Article II.                     Marejeo kuhusu Jannat  na Jahannam  

1. Qur’ani Tukufu

Jannat   11:35, 3:112, 3:113, 10:15, 10:13, 3:111, 10:14, 9:354, 14:119, 15:205, 17:315, 18;375, 18:129, 19:9,   19:123,  19:124,  19:137,   20:218,   20:213,   20:399,   14:83,  14:83, 14:84, 4:18, 4:20, 8:117, 8:123   

Maana ya Jahiim  j 5 uk. 256;

Jahannam  : 11:20, 1:294, 14:357, 15:204, 17:232, 12:178, 18:130, 18:383, 19:141, 20:7, 20:412, 20:438, 8:350,   8:351,   8:352,   8:113,   8:114,    8:115,   20:9 

(Namba inayotangulia ni ya Juzuu na inayofuata ni nambari za ukurasa.)

 

 (Marejeo haya ni ya Al-Mizan fi tafsiril Qur’an, zipo juzuu 20. Chapa ya Intesharat Bayan, Teheran, Nasir khosru, Teheran. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran)

2. Nahjul Balagha 

Hotuba: 16; 27; 28; 64; 66; 79; 83; 157; 171; 167; 160; 75; 109; 106; 119; 120; 124; 128; 12; 144; 152; 156; 193; 176; 165; 183; 192; 191; 193; 199;

Msemo: 199;     

Barua: 17; 27; 31; 28; 41; 76;     

Wasia: 24     

Misemo ya hekima: 31; 368; 228; 349; 387; 429; 456; 131; 42

(Marejeo haya ni ya Chapa ya Sub-hi Salehe, Beirut. Libanon)

 

3.  Sahifa-i-Sajjadiyah   

4. ……………


 

NDOTO YA Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

 

Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia Msikitini na kuwaambia Ma-Sahaba, “Je niwasimulieni ndoto niliyoiota ?”

 


         Ayah za  Qur'an Tukufu zizungumziazo Jannat

 

Makala haya yemkusanywa na kutarjumiwa na

Amiraly M.H.Datoo  - Bukoba Tanzania

 

Utaratibu ufuatao umetumika kuandika Surah na Ayah za  Qur'an Tukufu : 5 : 119  hii ikimaanisha kuwa katika Surah ya 5 ya  Qur'an Tukufu Ayah ya 119.

 

 

No.

Maudhui inayozungumzwa

Sura namba na Ayah namba

1

Afya bora katika Jannat  

19 : 62

2

Ahadi na Jannat

25 : 16

3

Allah swt na Wakazi wa Jannat  

35 : 34,  36 : 58

4

Amani ya Wakazi wa Jannat

52 : 20

5

Bahati za Wakazi wa Jannat   

52 : 25

6

Baraka za Jannat  

2:25, 2:36, 10:10, 15:46, 16:31, 22:23, 22:24, 25:10, 43:71, 43:73, 47:12, 47:15, 52:17, 52:18, 52:19, 52:22, 55:48, 55:50, 56:23, 56:33, 56:37, 57:12, 69:23, 69:24, 76:20, 76:22, 77:43, 82:13, 85:11, 87:8

7

Batili katika Jannat

19 : 62

8

Bi. Hawa katika Jannat

7:19, 7:20, 7:22

9

Bustani ya Jannat  

 

13:23, 15:45, 16:31, 47:15, 61:12, 65:11, 66:8, 76:14,  85:11,98:7

10

Chakula cha Wakazi wa Jannat

8 : 74

11

Chakula cha watu wa Jannat  

56:21

12

Chemichemi ya Tasnim katika Jannat

83:27, 83:28

13

Chemichemi za Jannat  

15:45, 44:52,55:50, 76:17, 88:12

14

Daraja za Jannat  

17:21, 46:19, 55:62

15

Familia ya Wakazi wa Jannat  

52 : 21

16

Furaha  ya Wakazi a Jannat

7:43, 88:9, 101:1

17

Furaha katika Jannat   

37 : 58

18

Furaha za Wakazi wa Jannat

37 : 45

19

Habari njema za Jannat  

50 : 35

20

Hali za Jannat

35:35, 76:29

21

Hariri iliyofumwa ya Jannat

76:21

22

Heshima katika Jannat  

37 ; 42,  39 : 73

23

Heshima ya Wakazi wa Jannat  

36 : 56

24

Hotuba za Wakazi wa Jannat

88 : 11

25

Hour al-‘Ayn katika Jannat

37 : 48

26

Huruma za Wakazi wa Jannat   

44:53, 56:16

27

Huzuni katika Jannat

35:34, 35:35, 36:48

28

Imani katika Jannat  

36:55

29

Jannat katika maisha baada ya hapa ulimwenguni

2 : 25

30

Jannat kwa ajili ya wema

35: 33

31

Jannat Mlezi

37 : 42

32

Jannat na maisha ya baada ya hapa ulimwenguni

3 : 133

33

Jannat na wacha-mungu

50 : 31

34

Jannat ya wacha mungu

3 : 133

35

Jannat ya Wacha mungu

13:35

36

Jannat ya Wacha-mungu

38 : 49

37

Jinn katika Jannat  

55:46

38

Kauli njema za wakazi wa Jannat

56 : 25

39

Kazi katika Jannat

36 : 55

40

Kinywaji cha Wakazi wa Jannat

37:45

41

Kitulizo cha Wakazi wa Jannat  

18 : 31

42

Kituo cha karibu katika Jannat

83:28

43

Kuchekeshana kwa Wakazi wa Jannat  

52:23

 

44

Kuelekea Jannat    

5:119, 9:89

45

Kuingia katika Jannat  

2:214, 3:185, 4:13,15:45, 15:46, 18:31, 1963, 36:26, 40:8

46

Kuishi katika Jannat  

14:23, 15:47, 15:48, 76:16

47

Kuishi kifahari katika Jannat   

35:34

48

Kuisifu Jannat

25 : 76

49

Kujamiiana katika Jannat 

37 : 42

50

Kujamiiana kwa Wakazi wa Jannat

15 : 47

51

Kunyimwa kwa Jannat  

5:72, 7:40, 38:77, 70:39

52

Kuridhika katika Jannat

 92 : 21

53

Kuwastarehesha Wakazi wa Jannat  

3 : 198

54

Lungilungi ( ua) la Jannat

56 : 28

55

Maamkiano katika Jannat

14:23, 19:62, 33:44, 36:58

56

Maamkizi ya Watu wa Jannat  

13:23, 13:24, 14:23, 15:46, 56:26

57

Mafundisho ya Wakazi wa Jannat

7:43, 56:25, 78:35

58

Mahala ilipo Jannat

53 : 15

59

Mahala pa kupumzikia kwa ajili ya Wakazi wa Jannat

 25 : 24

60

Maisha ya Wakazi wa Jannat  

7 : 49

61

Majadiliano katika Jannat  

37 : 54

62

Majeruhi katika Jannat  

36 : 58

63

Makazi katika Jannat

9 : 72, 10 : 9

64

Makazi ya Jahannam na Jannat

7 : 50

65

Makazi ya Jannat na Jahannam

7 : 44, 7:54

66

Malaika wa Jannat

39 : 73

67

Malazi ya Wakazi wa Jannat   

55:54

68

Malezi katika Jannat

36:57, 37:42

69

Malezi ya Wakazi wa Jannat

19 : 62

70

Malipo ya Jannat

2:25, 9:89,  9:11

71

Maneno katika Jannat

22:24

72

Manukato ya Jannat

83:26

73

Mapambo ya Wakazi wa Jannat  

18 : 31

74

Mapenzi na usawa miongoni mwa Wakazi wa Jannat

10:23, 21:102, 21:103, 35:35, 50:34, 50:35, 52:23, 52:25, 55:54, 55:76, 56:12, 56:15, 56:20, 56:28, 56:31, 76:41, 88:15, 88:16

75

Mapokezi katika Jannat

25:75

76

Masharti ya Jannat

25 : 16

77

Mashujaa wa Imani katika Jannat

9:21, 9:98, 61:12

78

Matembezi katika Jannat

39 : 73

79

Matunda ya Jannat

 

44:55, 47:15, 55:52, 55:54, 55:68, 56:20, 56:28, 56:32, 69:23,  76:14

80

Mavazi ya Jannat  

76 : 21

81

Mavazi ya Wakazi wa Jannat  

18:31, 22:23, 44:53

82

Mazulia ya Jannat  

88 : 16

83

Mazungumzo na Wakazi wa Jannat

37 : 50

84

Mazungumzo ya kipuuzi katika Jannat

19 : 62

85

Mikusanyiko katika Jannat  

15 : 47

86

Miti ya Jannat

3:198, 4:57, 56:28, 56:29

87

Mito ya Jannat

88 : 15

88

Mito ya Jannat

2:25, 3:198, 4:57, 5:119, 7:43, 9:72, 9:89, 9:100,10:9, 58:22, 61:12, 65:11, 66:8, 98:7

89

Mtume Adam a.s. katika Jannat   

2:35, 2:36, 7:19, 7:20, 7:22,  20:118

90

Mtume katika Jannat

9 : 89

91

Mwanamwali mzuri wa Jannat kwa ajili Wacha-mungu

38 : 49

92

Mwito kuelekea Jannat  

2: 221

93

Neema za Wakazi wa Jannat  

52:22, 52:23, 77:43

94

Ombi katika Jannat

36:57, 41:31, 44:55

95

Sababu za Jannat  

19: 60, 57:21, 58:11, 58:22, 61:12, 66:8, 76:6, 76:12, 85:11

96

Shughuli za Wakazi wa Jannat

26:55, 83:25

97

Shukurani za Wakazi wa Jannat  

7:43, 10:10, 35:35

98

Sifa kwa ajili ya Jannat

3:136, 3:142, 5:65, 14:23, 20:75, 25:15, 25:75

99

Starehe za Wakazi wa Jannat  

36:56, 36:57, 52:18, 87:8, 89:26

100

Starehe za Wakazi wa Jannat

7:43, 15:47

101

Starehe za Wakazi wa Jannat

35:33, 36 :56, 37:58

102

Starehe zilizopo katika Jannat  

37:42, 27:45, 37:48, 39:32

103

Tafrija za Wakazi wa Jannat  

56 : 16

104

Uchovu katika Jannat

15:48, 35:35

105

Udugu wa Wakazi wa Jannat  

10 : 10

106

Ufalme wa Jannat

18:31, 52:20, 55:76, 56:15, 83:35, 88:13

107

Uhalisi wa Wakazi wa Jannat

7 : 43

108

Uhuru katika Jannat  

39:73

109

Uhuru wa Wakazi wa Jannat  

56:33

110

Ukaribisho kwa Wakazi wa Jannat

50 : 34

111

Ukarimu wa Wakazi wa Jannat

37:42

112

Ukuu wa Wakazi wa Jannat

41 : 40

113

Ukweli katika Jannat

5 : 119

114

Ukweli wa Jannat

39 : 32

115

Ukweli wa Wakazi wa Jannat

15 : 47

116

Umilele katika Jannat

2:25, 2:82, 3:136, 3:198, 4:13, 4:57, 4:122, 5:85, 18:3, 19:61, 25:16, 25:76, 35:35, 37:58, 39:73

117

Umilele wa Jannat  

43:71, 4:73, 44:56, 47:15, 48:5, 50:34, 56:33, 57:12, 64:9, 65:11, 76:11, 76:19, 98:8

118

Urafiki wa Wakazi wa Jannat  

52:25

119

Uroho wa Jannat  

70 : 36

120

Usahihi wa Wakazi wa Jannat

15 : 46

121

Usalama wa Wakazi wa Jannat

50:34, 52:18

122

Usalama wa Wakazi wa Jannat

15:46

123

Ushindani kwa ajili ya Jannat  

3 : 133

124

Usumbufu katika Jannat  

35 : 35

125

Utajiri wa Jannat

55 : 64

126

Utayari wa Jannat

3 : 133

127

Uthamini wa Jannat

9:89, 9:100, 13:24, 20:76, 44:57, 57:21

128

Utofauti katika Jannat  

17:21

129

Uuwezo wa Jannat  

12 3 : 133

130

Uwastani wa Jannat

76:13

131

Uwingi wa Jannat

55 : 62

132

Uzoefu wa Wakazi wa Jannat  

44:53, 56:16

133

Vijana wa Wakazi wa Jannat

56: 17

134

Vinywaji vya Jannat  

47:15, 56:18, 56:19, 76:16, 76:17, 83:26, 83:27, 88:14

135

Vito vya thamani katika Jannat   

22:23, 35:33, 76:21

136

Vitu vya fahari vya Wakazi wa Jannat

7 : 50

137

Vyakula vya Jannat  

83 : 26

138

Vyakula vya Jannat

7:50, 43:71, 47:15

139

Wafanya ‘ibada katika Jannat  

3:136, 16:31, 19:85, 38:49, 39:73, 44:55, 44:55, 47:15, 50:35, 52:17, 52:18, 52:19, 52:20, 52:21,54:54, 54:55, 78:32, 78:37

140

Wahamiaji katika Jannat  

9:21, 9:22, 22:59

141

Wahudumu kwa ajili ya Wakazi wa Jannat

52:24, 76:15

142

Wahudumu wa Jannat

52:24, 56:17, 76:19

143

Wakazi wa Jannat katika Jannat

22 : 24

144

Wakazi wa Jannat katika Jannat

22 : 24

145

Wakazi wa Jannat na Hour al-‘Ayn

37 : 48

146

Wakazi wa Jannat na marafiki zao

37 : 54

147

Wakazi wa Jannat na Wake zao

36 : 56

148

Walio okoka katika Jannat

76:6, 83:23, 88:10

149

Wanawake wa Jannat

56:36

150

Warithi  wa Jannat  

23 : 10

151

Washika Vikombe wa Jannat

76:15, 76:16, 83:23

152

Watenda mema katika Jannat

11:23

153

Watenda Usahihi katika Jannat

3:198, 10:9, 76:5, 77:44, 82:13, 83:23, 83:24

154

Watu wa Jannat

7:40, 7:43, 7:49, 25:15

155

Watu wa Vitabu na Jannat

2 : 111

156

Waumini katika Jannat

7:49, 9:22, 9:72, 9:100, 10:9, 11:23, 30:15, 40:81, 41:31, 43:70,48:5, 56:39, 57:12, 61:12, 64:9, 69:24, 70:35,76:22, 85:11, 98:8

157

Zawadi za Wakazi wa Jannat

18 : 3

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

                               

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

 


 

 

 


 



[1] Nipo ninakitayarisha kitabu juu ya maudhui haya.

[2] Iwapo utapenda kusoma habari zaidi juu ya maudhui haya ya Tawbah, jipatie kitabu nilichokitafsiri cha Syed Dastaghib Sirazi

   kinachozungumzia ka marefu na mapana kuhusu somo hili.

[3]  Ninajaribu kutoa maelezo machache ili kuwezesha kueleweka vizuri ili nawe msomaji uweze kuchangia mawazo na kuweza kupanua ilimu yako. Hata hivyo itawabidi kufanya utafiti zaidi ili kujua mafhum ya usia huu vizuri zaidi.