SWALI: Hakuwa tajiri

Aya hii ilitelemka kwa ajili ya nani?

                                                                    (وسيجنبها الاتقى، الذي يؤتي ماله يتزك )

Jawabu: Mheshimiwa Muhammad Ali Ashujaiy. Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuhu.

Ama baada ya salaam, hakika aya hizo mbili ziko katika hali ya kubainisha matokeo na natija ya ucha Mungu na namna mwenye kujipamba na taqwa hiyo namna atakavyo epukana na moto na adhabu ya moto. Kwa hivyo basi matamshi ya aya hizo yako mutlaqa japo kuwa kuna rai tofauti katika kuzifasiri na kutoa taawili yake na kuitekeleza kwake (kupata vielelezo vyake), kwa mfano Ahli sunna wanazo rai mbili kuhusiana na sababu za kutelemka (kushuka) kwa aya hizo, wengi wao wanasema kuwa zimetelemka kwa ajili ya Abubakar, na wengine wao wanasema wazi kuwa zilitelemka kwa ajili ya Aba Dahdaah.

(Tafsiirul-qurtubiy na Tafsiri zinginezo).

Ama Shia hawaoni usahihi wa kushuka aya hizo kwa haki au kwa ajili ya Abubakar kwa sababu zifuatazo:

Kwanza: Hakika riwaya nyingi zinazo daiwa zinapingana na hadithi zilizo pokelewa zinazo julisha ya kwamba sababu ya kushuka kwa aya hizo ilikuwa ni kwa ajili ya Abu Dahdaah (zikimhusu yeye). Au riwaya zisemazo kuwa aya hizo zilishuka kwa ajili na zikimhusu Mtume (s.a.w) au zikimhusu na kwa ajili ya Amiril-muuminiin (a.s).

Pili: Hakika kauli isemayo kuwa Abubakar alikuwa tajiri na mwenye mali nyingi ni kauli isiyo kuwa na dalili, bali kuna dalili na alama au vithibitisho vingi vipingavyo kauli hiyo, vithibitisho vilivyo yazunguka maudhui haya, kwa mfano- ni kuwa:

Abaquhafah- baba yake Abubakar- alikuwa ni fukara sana hadi alifikia hatua ya kujiajiri kwa watu kwa ajili ya mambo yasiyo na thamani yoyote, (Musaamaratul-awaaili \ 88-Al-aghaniy juzu 8/ 329 na juzu 4/ 450 chapa ya Ihyaut-turaathi), je inaingia akilini baba kuwa katika hali hii wakati mtoto ni tajiri mkubwa?, je si vema kwa mtoto kumfanyia wema baba yake kabla ya kuwafanyia wema watu wengine?!!!, au kwa mfano vyanzo vya hadithi vyenye kuzingatiwa kwao vinanukuu kwamba yeye sikumoja alitoka nyumbani kwake akiwa pamoja na Omar akiwa na njaa kwa ajili ya kwenda kutafuta chakula (Sahihi Muslim juzu 3/ 1609 kitabul-ashribah H 3799- Iilaamun-nubuwwah cha Al-marudiy / 220 b 20), je hali hii inakubaliana na maneno yasemayo kuwa alikuwa tajiri wa kupita kiasi kama wasemavyo ?!!!.

Na kwa hakika ni kauli isiyo na dalili, kauli isemayo kuwa alimtajirisha Mtume (s.a.w) kwa mali yake, ni maneno ya uzushi na uongo na ni maneno ya batili, kwa sababu Mtume (s.a.w) alikuwa ni mwenye kujitosheleza kwa mali aliyo kuwa nayo yeye mwenyewe na kwa mali ya mlezi wake na Ami yake Abi Twaalib na mali ya Khadijah (a.s) alipo kuwa katika mji wa makka, na wakati alipo hama na kwenda Madinah akufungukiwa na milango mingi ya ukombozi na ngawira, sasa ni katika kipindi gani na wakati gani Mtume (s.a.w) alikuwa akihitajia utajiri na mali ya Abubakar?!!!.

Na huenda kutokana na kujikalifisha kupata dalili na kufanya majaribio ya kuambatanisha ushukaji wa aya hizo kwa ajili ya Abubakar kuliko daiwa kulimfanya asite bwana Alusiy katika kuyakamilisha maneno yake katika kuikubali dalili za Ibnu Abi Haatam alipojibu kauli ya Mashia kuhusianan na maudhui haya, pale mwisho aliposema:

…..Na akarefusha maneno-Ibnu Abi Haatam- katika hilo na akaleta maneno ambayo hayakuepukikana na kauli za  Qiila na Qaala (Inasemekana na imesemekana).

Na tunakutakia kila la kheri.