SWALI: Ibnu taimiyyah

Hakika nimefanikiwa kusoma vitabu vingi vya Ibnu Taimiyya na Muhammad bin Abdilwahhabi na wala sikukuta kufru yoyote kwenye vitabu hivyo wala upotovu wa aina yoyote, bali nilicho kikuta ni wito wao na madai yao ni madai ya haki ambayo alitumwa nayo Mtume (s.a.w) na swali ni kama lifuatalo kwanini mwawazulia Mashekhe wawili hawa?  Na ikiwa nyinyi mko kwenye haki basi ni wajibu kwenu kuonyesha vitabu vyao na kuvidhihirisha kwa wasomaji na ni juu ya msomaji kuhukumu yeye mwenyewe.

Na amani iwe juu ya mwenye kufuata uongofu.

JAWABU: Ndugu mheshimiwa.

Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuhu.

Baada ya salam, tutakutajia badhi ya kauli zao zinazo julisha kuwa wako kwenye upotovu, na kuwa wanakwenda kinyume na kuwa wanapingana na uislaam wote, na ukihitaji nyongeza tutakupatia.

1- Itikadi ya Ibnu Taimiya kuhusu utangu wa aina fulani ya matukio kati ya vitendo na vifanya kazi vingine na kuitakidi kwake kuwepo kwa matukio yasiyokuwa na mwanzo jambo lipelekealo kuwepo kitu kingine cha tangu tofauti na Mwenyezi Mungu, na hiyo ni kufru.

 Rejea: Daru ta'arudhil-akli wannakil juzu 1\240 na 276-375, Sharhu hadithun-nuzuul 158, Sharhu hadithi amruwani Ibnu Husein 71, Ar-raddu alaa asaasit-taqdiis juzu 1\ 599.

2-Kauli ya Ibnu Taimiya juu ya kumalizika kwa moto, na hilo linapingana na ijmaai ya Waislaam.

Imetajwa na Ibnul-qayyim ambae ni mwanafunzi wa  Ibnu Taimiya katika kitabu chake (Shifaul-aliil: 431-451) na katika kitabu chake (Hawil-arwaah ilaa bilaadil-arwaah: 253- 277) na ametaja katika vitabu hivyo ya kuwa kauli ya kumalizika kwa moto ni kauli ya ustadh wake Ibnu Taimiya, na bwana Swafadiy katika kitabu (Al-wafiy bil-wafayaat juzu 7\ 26 amesema : Hakika Ibnu Taimiya anacho kitabu maalum kuhusiana na mas'ala ya kumalizika kwa moto.

3- Kauli yaIbnu taimiya na Muhammad bin Abdulwahhab au kuitaki kwao kuwa Mwenyezi Mungu ana kiwili wili (Tajsiim), na hii ni kauli iliyo mashuhuri kutoka kwao, na kauli yao hiyo wameitaja katika vitabu vyao vingi na kusema wazi kauli yao hiyo bila ya kificho chochote.

4- Ibnu Taimiya  na Muhammad bin Abdilwahhab kuwakufurisha kwo waislam wote . Rejea kitabu (Faslul-khitaab 28) cha Sulaiman bin Abdilwahhab nduguye Muhammad bin Abdilwahhab.

 5- Muhammad bin Abdilwahhab kuwanasibishia Mashia kauli ya kupinga kuwepo kwa kizazi cha Imam Hassan, na amesema: Na kauli hiyo imeenea kati yao na wote wamekubaliana juu ya hilo.

Rejea: Risaalatun fir-raddi alaa raafidhah: 29.

Na hakuna hata Shia mmoja apingae kizazi cha Imam Hassan (a.s) Al-mujtaba, bali Mashia wote wanathibitisha kuwepo kwa kizazi hicho.

 6- Kupinga kwa Ibnu Taimiya na Muhammad bin Abdilwahhab kuzuru makaburi na kutabaruku kwayo, na katika kauli yao hiyo waliwakhalifu na kuwapinga walio wengi na madhehebu nyingi za kiislaam.

Na jambo la muhimu kabisa unalo paswa kulifahamu na kulielewa ni kuwa maulamaa wakubwa wa madhehebu za kiislaam tangu Ibnu Taimiya na Muhammad Ibnilwahhab walipo tangaza kauli yao hiyo ya upotovu walibakia na msimamo wao huo na maulamaa hao kuandika vitabu vingi kupinga kauli yao hiyo na vingene kupinga rai zao za upotovu zinazo pingana na ijmai ya waislaam na zinazo kwenda kinyume na zinazo pingana na kitabu na sunna za wazi na uongo wao.

Na miongoni mwa uongo wa ibnu taimiya:

1-Kupinga kwake kuwa Ibnu Abbas alisoma kwa Imam Ali (a.s) (Minhajus-sunna juzu 7\ 537). Na kwa hakika amethibitisha bwana Al-manawiy ya kuwa Ibnu Abbas alisoma kwa Imam Ali (a.s) (Faidhul-qadiie juzu 4\ 357).

2- Kusema kwake ya kuwa hadithi isemayo (Úáí ãÚ ÇáÍÞ æÇáÍÞ ãÚ Úáí)

(Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali) ni ya uongo, na akadai ya kuwa hakuna mtu yeyote alie pokea hadithi hiyo (Minhajus –sunna juzu 4 \ 238).

Pamoja na ukweli kuwa hadithi hii imepokelewa na bwana Tirmidhi katika Sahihi yake na bwana Al-haakim katika Mustadrakul-haakim, na bwana Twabarany, na Al-khatwiib Al-baghdaady, na Ibnu Asakir, na wengineo…..

3- Kupinga kwake suala la kuunga udugu kati ya Mtume na Imam Ali (a.s) na kati ya Muhajirina wao kwa wao (Minhajus-sunna juzu 4\ 32, juzu 5\ 7-117 na 279).

Wakati ambapo hadithi hiyo ya kuunga udugu utaikuta katika kitabu cha Tirmidhi juzu 5\ 395 na katika Twabaqaatu cha Ibnu Saad juzu ya 2\ 60, na Mustadra cha Al-haakim juzu 3\ 16, na Maswabihus-sunna juzu 4\ 173, na vinginevyo…

Hadi Ibnu Hajar alimjibu Ibnu Taimiya katika suala la kuunga udugu katika kitabu chake Fat'hul-bariy juzu 7\ 217, na akasema: Haya ni majibu ya dalili (Nassi) kwa kiasi na kughafilika kuhusiana na hekima ya kuunga udugu, kama alivyo mjibu pia Zarqaniy katika Sharhul-mawahibu Alladunniyyah juzu 1\ 273.

4- kauli ya Ibnu taimiyya kuhusiana na hadithi isemayo

 (Çááåã æÇá ãä æÇáÇå æÚÇÏ ãä ÚÇÏÇå) kauli yake kuhusiana na hadihti hii: Ni uongo kwa kukubalia watu wenye maarifa ya hadithi (Minhajus-sunna  jzu 7\ 55).

Pamoja na ukweli kuwa hadithi hii imetolewa na Ahmad kwa sanadi sahihji na kutolewa na Ibnu Abi Shaiba na Ibnu Raahwaihi na Ibnu Jariir na Twabaraniy na Abu Naiim na Al-haakim na Khatib n.k…  

5- Kauli ya Ibnu Taimiyya kuhusiana na hadithi isemayo:

(ãËá Ãåá ÈíÊí ãËá ÓÝíäÉ äæÍ) (mfano wa Ahlil-baiti wangu ni kama mfano wa jahazi la Nuhu) kauli yake isemayo: Hadithi hii haina sanadi yoyote ifahamikayo hata ambayo si sahihi, na wala haipo kwenye vitabu vya hadithi nyenye kutegemewa (Minhajus-sunnah juzu 7\ 395).

Wakati ambapo hadithi hii imepokelewa na: Ahmad bin Hanbal na bwana Al-bazzaz na Abu yaaliy na Ibnu Jariir na Nasaiy  na Twabaraniy na Daaruqutniy na Al-haakim na wengineo…

6- Kauli ya Ibnu Taimiyya kuhusiana na hadithi ya ndege: Ni miongoni mwa hadithi za uongo zilizo pandikizwa (Minhajus-sunna juzu 7|371).

Wakati ambapo hadithi hii imepokelewa na: Al-haakim na Ibnu Saad na Ahmad bin Hanbali na Tirmidhiy na Al-bazzaz na An-nasaiy na Baihaqiy na Ibnu Hajar na Ibnu Asakir na Abu Hanifah na Twabariy na wengioneo…

Na ukitaka tukutajie opotovu zaidi wa Ibnu Taimiyya na Abdul-wahhab na kupinga kwao itikadi na hukumu ambazo Umma wa kiisalaam umekubaliana juu ya Itikadi na hukumu hizo, basi tutakutajia mamia kwa mamia na yote hayo yamechukuliwa kutoka kwenye vitabu vyao.

Na ukitaka tutakutajia mamia ya majina ya maulamaa wakubwa walio wajibu mabwana hawa wawili.

Mwenyezi Mungu atuongoze sisi na nyinyi.

Muulizaji: Muhammad Ali al-shamiy: