SWALI: Aya ya wilaya

Ninataraji mtanipatia majibu yenye kukinaisha kwa mtu asemae ya kuwa ikiwa nyinyi mwaitolea hoja aya ya Wilaya isemayo (ÅäãøÇ æáíøßã Çááå æÑÓæáå )  juu ya Uimamu wa Ali (a.s) kwa nini Imam Ali (a.s) mwenyewe hakuitumia kama hoja kuthibitisha Uimamu wake?

JAWABU: Mheshimiwa ndugu Manar Ahmad.

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakatuhu.

Ama baada ya salaam tunapenda kukujibu kama ifuatavyo.

Kwanza: Hakika dalili zihusianazo na suala la uimamu wa Amiril-muuminiin (a.s) ni nyingi sana za kiakili na zilizo nukuliwa kiasi kwamba ni vigumu kufahamu idadi yake, kwa hakika kuna vitabu vilivyo tungwa kuhusu maudhui hayo na katika uwanja huu, lakini jambo ambalo inabidi kuliashiria na kulieleza hapa ni kuwa Imam (a.s) hakuwa na ulazima si wa kiakili wala kisheria kutoa hoja na kuthibitisha uimamu wake kwa kutumia dalili zote, bali ilikuwa inamlazimu kutoa kiwango kile tu cha dalili ambazo zitaweza kuthibitisha hoja kwa watu, na hili ndilo lililotokea baada ya kufahamu dalili alizo zitumia kama hoja ya kuthibitisha Uimamu wake (a.s) kama hadithi ya Ghadiir –dalili ambayo ndio yenye uthibitisho zaidi kuhusu suala hilo- na watu kuto kubali ukweli huu na haki hii iliyo wazi, je baada ya kutolewa ushahidi na dalili kama hii kuna matarajio ya kubakia nafasi ya kuathiri dalili nyingine kama aya ya Wilaya katika nafsi zao?!!!

Pili: Tujaalie kwamba kutoa hoja juu ya Uimamu kwa kutumia aya hii habari zake hazikutufikia , je hiyo inakuwa ni dalili ya kuwa hakuitumia kama hoja juu ya Uimamu?

Pamoja na kuwa tunayakini ya kuwa kunahabari na athari (riwaya) nyingi tangu mwanzo hazikutufikia na hasa zile ambazo zilikuwa zikipingana na maslahi ya makhalifa (watawala), kwani wao wameficha fadhila na sifa nyingi za Ahlil-baiti (a.s), na zilizo dhihiri na kuonekana ni tone moja katika bahari iliyo furika.

Tatu: Kisha kwa mara nyingine tujaalie kuwa Imam (a.s) ni kweli hakuitumia na kuitolea hoja, je hilo linatuthibitishia na kutwambia kuwa aya hiyo haithibitishi Uimamu wake (a.s)? hebu tufanye insaafu (tuwe ni watu wenye insaafu), ni ulazima gani huo?

Nne: Shubha hii asili yake inatoka kwa bwana Raziy katika kuifasiri kwake aya hiyo) rejea Tafsirul-kabir cha bwana Raziy juzu ya 12\ 28, na madhumuni ya kauli yake ni kuwa: Hakika Mashia hawakutaja kuwa Imam aliitumia aya hii kutoa  dalili juu ya kuthibitisha Uimamu kama ilivyo elezwa kutoa hoja kwake kwa kutumia hadithi ya Ghadiir.

Tunasema tukijibu ishkali hiyo ya bwana Raziy kuwa habari za kuitumia kwake kama hoja juu ya Uimamu zimepokelewa katika vyanzo vya hadithi vya kishia kama vile Al-ihtijaaj juzu ya 1\ 320, Al-aamal cha Tusiy juzu 1\ 343 na 2\159-166, Al-ikhtiswaali juzu ya 2\553, Al-ghadiir juzu 1\159, Buharul-anwaar juzu 8\ 325, na vitabu vinginevyo. Na baadhi ya hadithi zimeelezwa na kuashiriwa katika vitabu vingi vya Ahlisunna (kwa mfano Manaaqib cha Al-khawarizmiy\ 217-Manaaqib Ibnu Al-maghaziliy\112, Sharhu Nahjul-balagha cha Ibnu Abil-hadiid juzu 6\ 176, Lisanul-miizaan cha Ibnu Hajar juzu 2\156, Taarikhu Damashqi cha Ibnu Asakkir (Tarjumatu Amiril-muminiin )juzu 3\87).

Mwisho hakuna kilicho muhimu ila ni kuwa Mashia wanasema ya kuwa aya hii inathibitisha Uimamu wake (a.s) kama ilivyo elezwa mahala pake.

Tunakutakia kila la kheri.

SWALI:

PAMOJA NA MTUME KWENYE PANGO.

Ni yapi makusudio ya aya ya pango isemayo: Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi. Je yamhusu Imam Ali na Mtume (s.a.w) au Mtume na Abubakar?

Ikiwa iliteremka kwa ajili ya Abubakar je huhesabiwa hilo kuwa ni fadhila kwake au ni kinyume chake kiasi kwamba hakumuamini Mtume na hakuwa na matumaini nae ya kuwa mwenyezi Mungu atawahami na kuwalinda wote wawili? Nataraji mtatufaidisha kwa kutupatia jawabu na ufafanuzi, na tunamwomba Mwenyezi Mungu akuhifadhini na akufanyeni muwe akiba ya kueneza fadhila za Ahlul-baiti (a.s).

JAWABU.

Ndugu Ali Twaahir:

Assalaam alaykum.

Ama baada ya salaam:

Tuna kutumia mahojiano ya Shekh Mufid (Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake) aliyo yafanya na Omar katika ndoto na kutokana na mahojiano hayo utakuwa umepata majibu ya maswali yenu.

Imepokelewa kutoka kwa Shekh Mufid Abi Abdillah Muhammad bin Muhammad An-nuuman- Mungu awe radhi nae- amesema: Niliona katika ndoto katika mwaka mmoja wapo kana kwamba  nimevuka na kupita njia na kuona mkusanyiko wa watu wengi wakiwa wamekaa duara, nikauliza: Ni kitu gani hiki? Wakasema: Mkusanyiko huu ni kwa sababu kuna mtu anatoa mawaidha.

Nikasema ni nani huyo? Wakasema: Omar binil-khattab, hapo hapo nikawatenganisha hao na kukatiza kati yao na kuingia kwenye mkusanyiko huo na katika mduara ule wa watu, ghafla nikamwona mtu akiwazungumzia watu jambo ambalo sijawahi kulisikia na sikuwa nikilifahamu, wakati huo huo nikamkatiza mazungumzo yake.

Nikamuuliza ewe Shekh ni habarishe vipi aya hii ya Mwenyezi Mungu    (ËÇäÜì ÇËäíÜä ÅÐ åãÜÇ Ýì ÇáÛÇÑ) ni vipi yathibitisha na kutoa dalili juu ya fadhila ya swahiba wako Abibakar Atiq bin Abi Quhafah?

Akasema: Aya hii yathibitisha na kutoa dalili juu ya fadhila za Abubakar katika sehemu sita.

Sehemu ya kwanza ni kuwa: Hakika Mwenyezi Mungu alimtaja Mtume (s.a.w) na akamtaja Ababakar na akamfanya kuwa ni wa pili wake, na akasema:( ËÇäí ÇËäíä ÇÐ åãÇ Ýí ÇáÛÇÑ )

Sehemu ya pili: Amewasifia wote wawili kwa kukusanyika sehemu moja kwa kuwaunganisha kwenye aya  pale alipo sema (ÇÐ åãÇ Ýí ÇáÛÇÑ  )

Sehemu ya tatu: Hakika yeye alimdhifia kwake kwa kutaja usuhuba akawakusanya wote wawili kwa jambo lipelekealo kupata nafasi ya juu kabisa na akasema (ÇÐ íÞæá áÕÇÍÈå ).

Sehemu ya nne:Ni kuwa  ikielezea huruma ya Mtume (s.a.w) na upole wake kwake kutokana na nafsi yake kwake (mtume) na akasema (áÇ ÊÍÒä ) Usihuzunike .

Sehemu ya tano: Imeelezea kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja  nao wote sawa kwa sawa, akiwa ni Mwenye kuwanusuru wote wawili na mwenye kuwalinda wote wawili pale alipo sema: (Çä Çááå ãÚäÇ )  Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi.

Sehemu ya sita:  Hakika aya imeelezea kutelemka na kushuka kwa utulivu  kwa Abibakar kwa sababu Mtume (s.a.w) kamwe hakutengana na utulivu wake, akasema (ÝÃäÒá Çááå ÓßíäÊå Úáíå ) Akatelemsha utulivu wake  kwake.

Hizi ndizo sehemu sita zijulishazo juu ya ubora wa Abubakar katika aya hii tukufu ya pango, kiasi kwamba huwezi wewe wala wenzi wako kutia kasoro na illa yoyote kwenye aya hiyo.

Nikamwambia: nakushukuru kwa maneno yako katika kuthibitisha hoja zako na kumtetea sahiba wako kwa maneno yako hayo, na mimi kwa usaidizi wa Mwenyezi Mungu haya uliyo kuja nayo nitayafanya kama majivu yaliyo pigwa na upepo mkali siku ya tufani kubwa.

Ama kauli yako kuwa: Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amemtaja Mtume (s.a.w) na kumjaalia Abubakar kuwa ni mwenza na wa pili wake (kuwa pamoja nae), kwa hakika hilo ilikuwa ni kuelezea idadi tu, na nina apa kwa umri wangu kwa hakika walikuwa ni wawili, kwa hivyo basi katika hilo hakuna fadhila na ubora wa aina yoyote, kwa hakika sisi twafahamu bila shaka yoyote ya kuwa muumini na kafiri ni wawili pia, kwa hivyo basi sioni faida yoyote iliyopo kwako kulihesabu hilo na kulitegemea kama fadhila.

Ama kauli yako yakuwa: Amewasifu kwa kuwa kwao pamoja na kujumuika kwao katika sehemu moja, nayo ni kama ya mwanzo kwani sehemu au mahala hujumuisha watu wa aina tofauti, kati ya  Muumini na kafiri kama ambavyo idadi yaweza kujumuisha kati ya Waumini na Makafiri, pia msikiti wa Mtume (s.a.w) ni bora zaidi kuliko pango na tunaona ulikuwa ukijumuisha  Waumini na wanafiki (yaani ukiingiwa na watu hao) pia makafiri, na kuhusu hilo Mwenyezi Mungu alie takasika anasema: (   ÝãÇ ááÐíä ßÝÑæÇ ÞÈáß ãåØÚíä Úä Çáíãíä æÚä ÇáÔãÇá ÚÒíä)

   Basi imekuwaje wanaokufuru wanakujia kwa haraka. Vikosi vikosi kwa upande wa kulia na kwa upande wa kushoto. (suratul-maarij 36-37).

Pia ni kuwa: Hakika jahazi la Nuhu (a.s) lilikuwa pamoja na Nabii Nuhu mahala pamoja, Shetani na wanyama pia walikuwa, mbwa na nguruwe pia, na sehemu haimaanishi kuwa na ubora au fadhila kama ulivyo sema wewe, na kwa maana hiyo fadhila mbili hizo zina batilika.

Ama kauli yako isemayo kuwa: Hakika Mwenyezi Mungu alimdhifia kwake kwa kutaja usuhuba, hakika kauli hii na fadhila hii uliyo idai ni dhaifu zaidi kuliko hizo mbili za mwanzo kwa sababu jina la usuhuba linajumuisha kati ya Muumini na Kafiri, na dalili juu ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu: (ÞÇá áå ÕÇÍÈå æåæ íÍÇæÑå ÇßÝÑÊ ÈÇáÐì ÎáÞß ãä ÊÑÇÈ Ëã ãä äØÝÉ Ëã ÓæÇß ÑÌáÇ ð )(5)

Sahiba wake ali mwambia (alimuuliza) hali ya  kuwa akijibizana nae je umemkufuru yule ambae amekuumba wewe kutokana na udongo kisha kutokana na tone la manii (mbegu ya uzazi) kisha akakufanya kuwa ni mtu kamili). Suratul kahf 35.

Pili: jina la swahaba hutumika kwa mtu mwenye akili na pia hutumika kwa mnyama, na dalili juu ya hilo ni maneno ya waarabu ambayo Qur'ani ameteremka kwa lugha yao, na Mwenyezi Mungu alie takasika akasema:

(æãÜÇ ÃÑÓáäÜÇ ãÜä ÑÓÜæá ÅáÇ ÈáÓÇä Þæãå)

Hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake). Suratu Ibrahim aya 14.

Kwani wao walimuita punda kuwa ni swahiba na mshairi mmoja akasema: Åä ÇáÍãÇÑ ãÚ ÇáÍãíÑ ãØíÉ ÝÅÐÇ ÎáæÊ Èå ÝÈÆÓ ÇáÕÇÍÈ))

Na pia: kitu kisicho hai walikiita sahiba kikiwa na mtu hai, na wakasema kuhusu hilo, kuhusu upanga na wakatoa shairi kwa kusema:

( ÒÑÊ åäÏÇð æßÇä ÛíÑ ÇÎÊíÇäæãÚí ÕÇÍÈ ßÊæã ÇááÓÇä )  íÚäí: ÇáÓíÝ()

Sasa ikiwa jina la sahaba latumika kati ya Muumini na Kafiri, na kati ya mtu na kitu kisicho na akili, na kati ya wanyama na vitu visivyo na hisia, basi ni hoja gani uliyo nayo kuhusu sahiba wako katika hilo?.

Ama kauli yako ya kuwa: Mwenyezi Mungu alisema (áÇ ÊÍÒä) Usihuzunike, hakika hilo ni janga kwake na ni jambo la aibu kwake, na ni dalili juu ya ukosefu wake kwa sababu kauli yake isemayo (usihuzunike), hilo ni kemeo (katazo) na sura ya kukataza au kukemea ni pale mtu asemapo: usifanye jambo Fulani hapo tunapata moja kati ya maana mbili ya kwanza ni kuwa. Abubakar alipatwa na huzuni kwa ajili ya utiifu au uasi, ikiwa huzuni hiyo ni kwa ajili ya twaa (utiifu) basi Mtume (s.a.w) hawakatazi wala kuwakemea watu kunako kufanya jambo la twaa (utiifu), bali huwaamuru na kuwahamasisha kufanya hivyo  na huwahimiza kufanya twaa'a, na ikiwa alihuzunika kwa maasi, kwa hakika  Mtume alimzuia na kumkemea kufanya hivyo, na kwa maana hiyo aya imetoa ushahidi juu ya uasi wake kwa dalili kuwa alimkemea na kumkataza kufanya tendo hilo (kuhuzunika).

Ama kuhusu kauli yako isemayo kuwa: Yeye alisema hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi, hakika Mtume (s.a.w) alimfahamisha ya kuwa Mwenyezi Mungu yupamoja nae, na akajielezea yeye mwenyewe kwa tamko la wingi (jam'u), kama kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu isemavyo (Çä Çááå ãÚäÇ ) suratul-hijri aya 9, na pia imesemekana kuwa Abubakar alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu  huzuni huzuni yangu ilikuwa juu ya Ali bin Abi Twalib kutokana na yaliyo kuwa yakimkabili, Mtume (s.a.w) akamwambia: Usihuzunike kwa hakika Mwenyei Mungu yuko pamoja nasi). Yaani Mwenyezi Mungu yuko pamoja na mimi na ndugu yangu Ali bin Abi Twalib (a.s).

Ama kauli yako isemayo: Hakika utulivu ulimshukia Abubakar, hakika maneno hayo ni kwenda kinyume na uwazi wa maneno (dhahiri), kwani alie telemkiwa na utulivu ni yule alie ungwa mkono na kusaidiwa na Mwenyezi Mungu kwa majeshi, na huo ndio uwazi wa maneno na dhahiri ya maneno ya Qur'an isemavyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na Mwenyezi Mungu akatelemsha kwake utulivu wake na kumuunga mkono (kumnusuru na kumsaidia) kwa jeshi ambalo hamkuliona). Suratl-tawbah ya 4\.  (ÝÃäÒá Çááå ÓßíäÊå Úáíå æÃíÏå ÈÌäæÏ áã ÊÑæåÇ )

Ikiwa Abubakar ndie mwenye utulivu basi yeye ndie mwenye majeshi, na kwa kusema hivyo utakuwa umemtoa Mtume (s.a.w) kwenye utume na kwamba sehemu hii kama unge ificha na kuto muhusisha nayo sahiba wako ingekuwa bora zaidi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alitelemsha utulivu (sakinah) kwa Mtume sehemu mbili (pahala pawili), sehemu ambazo alikuwa na waumini na yeye kuwashirikisha katika utulivu huo, na kati ya mahala muwili humo alisema:

Basi ( Mwenyezi Mungu akatelemsha utulivu wake juu ya Mtume na juu ya waumini na kuwalazimisha kushikamana na neno la uchamungu).

( ÝÃäÒá Çááå ÓßíäÊå Úáì ÑÓæáå æÚáì ÇáãÄãäíä æÃáÒãåã ßáãÉ ÇáÊÞæì ) suratul fathi aya 26, na akasema mahala pengine:

                                 (ÃäÒá Çááå ÓßíäÊå Úáì ÑÓæáå æÚáì ÇáãÄãäíä æÃäÒá ÌäæÏÇð áã ÊÑæåÇ)

(Kisha Mwenyezi Mungu akatelemsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu yawaumini na akatelemsha majeshi ambayo hamkuyaona) suratu tawbah 12,  27, na alipofika mahala hapa alimuhusisha yeye tu na utulivu huo alio utelemsha, na akasema:

                                                                                        (ÝÇäÒá Çááå ÓßíäÊå Úáíå)

(Na Mwenyezi Mungu akatelemsha utulivu wake juu yake) lau kama ange kuwa na muumini yeyote ange mshirikisha nae katika utulivu ule kama alivyo washirikisha waumini tulio wataja kabla ya aya hii, kwa hivyo basi kumtoa kwake kwenye utulivu ikiwa ni dalili ya kuthibitisha kutoka kwake kwenye imani na hapo hakuwa na la kujibu na watu kutawanyika na mimi kuamka kutoka usingizini. Rejea kitabu Al-ihtijaaj juzu 2\ 499-501, Kanzul-fawaidi cha karajikiy juzu 2\ 48, Buharul-an'waar juzu 21\ 327 H I, na Al-kashkali cha Bahraniy juzu 2\ 5.

Tunakutakia kila la kheri.

SWALI:

Ni ipi kauli yenu kuhusiana na riwaya mbili hizi zilizoko katika kitabu Al-buhar juzu 35\ 297, na ambazo zinazungumzia kutumwa kwa Imam Ali (a.s) kwenda kufikisha ujumbe wa suratul baraa'a na Abubakar kurudishwa, (Abubakar akasema): Naapa kwa haki ya baba yangu na mama yangu! Je kuna jambo lililo tokea kiasi kwamba imebidi kuchukuliwa aya hizi kutoka kwangu?

Mtume (s.a.w) akasema: Hapana lakini Mwenyezi Mungu wa juu na adhim ameniamuru ya kuwa asichukue unaibu na kuniwakilisha mimi isipokuwa mtu atokanae na mimi, ama wewe kwa hakika Mwenyezi Mungu amekubadilishia kwa zile aya alizo kubebebsha na amekuamuru (amekukalifisha) kumtii na kwa kufanya hivyo utapata daraja ya juu na maratib matukufu, ama ikiwa wewe utaendelea kututawalisha sisi na ukatekeleza na kufika kwentu kwenye viwanjua vya kiama, watakutekelezea tuliyo kuahidi, kwa hivyo wewe ni katika mashie wetu wateule na watukufu wenye kutupenda na Abubakar kufurahi kwa kuyasikia hayo.

Na katika juzu  hiyo hiyo ukurasa 30 amesema Mtume (s.a.w) kumwambia Abubakar ….. je huridhii ewe Abubakar ya kuwa wewe ni sahiba wangu katika pango? Basi kutokana na maneno hayo ni ipi kauli ya wazi ya Mtume (s.a.w) kuhusiana na Abubakar? Je ni katika riwaya zilizo pandikizwa au ni nyongeza?

Asanteni.

JAWABU: Ndugu mheshimiwa Ahmad Jaafar

Assalaam alaykum.

Na baada ya salaam. Hakika msingi wa uhakiki kwa maulamaa wa kishia tofauti na maulamaa wengineo unawalazimisha kuzingatia kwa jicho la uchunguzi sanadi zote na kuweka pingamizi  za kielimu katika sanadi hizo, itakayo thibiti ukweli wake hukubaliwa na ambayo haikuthibiti basi wo hawafungiki na riwa hiyo na (kwa maana wako huru) kuhusiana na riwaya hiyo, na kutokana na kaida na kanuni hizi ( kanuni hizi)  si lazima kusema kuwa riwaya hizi zinahukumiwa kuwa zimepandikizwa  sehemu zake zote kwani pengine huenda kukawa na upandikizaji na upotoaji katika sehemu kadhaa za riwaya hizo, kwa sura ya ujumla kuhusu suala hili ni kuwa hadithi ambayo haikuthibiti usahihi wa sanadi yake kwa njia sahihi haiwezekani kujitegemeza kwayo katika kutoa dalili ya kuthibitisha suala Fulani.

Na kuhusiana na sehemu ya swali tunasema ya kuwa riwaya ya mwanzo imenukuliwa kutoka kwenye Tafasiri inasibishwayo kwa Imam Hassan Askariy (as) nani jambo lililo wazi kuwa Tafsiri hii haifahimiki chimbuko lake kama wasemavyo wahakiki, pamoja na kuongezea kuwa hakuna sanadi yenye kutegemewa ya riwaya hii yenyewe, ama riwaya ya pili nayo  imenukuliwa na kutoka kwenye Tafsiri Furat na Tafsiri hii japokuwa asili yake ni thabiti lakini hadithi iliyotajwa kwa ufafanuzi wake  haikupokelewa sanadi yake  sahihi na yenye kuzingatiwa kwa hiyo hukumu yake ni sawa na hukumu ya riwaya ya mwanzo.

Kisha ni kuwa katika sehemu kama hizi hadithi kama hizi kuwa katika vitabu Al-buhar – si ushahidi wa kusihi hadithi mbili hizo kwa sababu lengo la Al-majlisiy (Mungu mrehemu) mwandishi wa kitabu Al-buhar lilikuwa ni kukusanya hadithi bila ya kuangalia usahihi wake au udhaifu wake kwa hiyo kuweko riwaya katika kitabu  Buharul-anwaar si dalili uya kusihi kwa sanadi ya hadithi au dalili yake.

Na tukizifumbia macho sanadi za riwaya hizo ukweli ni kuwa riwaya hiyo ya kwanza haitujulishi juu ya fadhila maalum kutokana na kuingia sharti katika riwaya hiyo kama mlivyo litaja, (ikiwa utadumu na kuendelea….) na kama tunavyo fahamu kilicho shurutishwa huporomoka na kutoweka kwa kuporomoka sharti lake kama ilivyo wazi na hadithi hii mfano wake ni sawa na hadithi iliyo pokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) katika kulihamasisha na kulienzi shairi la Hassan bin Thabiti alilo lisoma siku ya Ghadiir akisema: Ewe Hassan utaendelea kuungwa mkono na roho mtakatifu kwa muda wote utakao endelea kutunusuru sisi kwa ulimi wako) aliyasema hayo kutokana na kufahamu kwake (s.a.w) kuwa Hassan atapotoka na kufuata njia nyingine  na kutomfuata Amiril-muuminiin (a.s) mwishoni mwa uhai wake, na hizi ni katika alama za utume kwani hiyo ni tanbihi kwa Abubakar ili asije kwenda kinyume na kukengeuka na kusahau ahadi mbali mbali alizo ziweka (s.a.w) juu yake na yeye kujisahaulisha ahadi hizo hapo baadae.

Ama riwaya ya pili haina fadhila yoyote bali ni usuhuba tu ulio elezwa humo na usuhuba huo hauna fadhila wala sifa yoyote  na hasa baada ya sisi kufahamu kuwa usuhuba huo haukuwa umepangwa na kufanyiwa maandalizi wala utafitri wala kukusudiwa hapo kabla , bali ulijitokeza baada ya Abubakar kufahamu kuwa Mtume (s.a.w) anatoka, napo ikabidi amchukue na kufuatana nae ili mtu yeyote asiweze kufahamu habari za kutoka kwake.

Tuna kutakia kila la kheri.

SWALI:

 Je Abubakar Swiddiq huzingatiwa kuwa ndie anae faa zaidi kuwa khalifa? wakati sisi twafahamu ya kuwa Mtume (s.a.w) alimuamuru kusalisha sala ya jamaa je tendo hilo lina maanisha ya kuwa Mtume alimuamuru kisheria Abubakar ya kwamba awe khalifa na Imam wa kwanza wa Waislaam?

JAWABU:Mheshimiwa ndugu Buhulufer Al-arabiy

Assalaam alaykum.

Na baada ya salaam, hakika riwaya ya sala ya Abubakar inakasoro katika sanadi yake na dalala yake, kwani wapokezi wake wote wanakasoro (wamejeruhiwa) kama wanazuoni wa fani ya jarhi walivyo thibitisha na kutoa ushahidi juu ya hilo au badhi ya njia za hadithi hiyo ni mursalah na si hoja kamwe. Ama dalala ya riwaya hiyo ni yenye kupingwa kwa njia nyingi kati ya njia hizo, hakika Abubakar alikuwa ameamuriwa kutoka pamoja na jeshi la usamah –kama vyanzo vya kihistoria visemavyo –mwenye kukiuka amri ya Mtume (s.a.w) huzingatiawa kuwa ni fasiki, sasa je ina ingia akilini Mtume atoe amri ya kumfuata mtu ambae ni fasiki?!!!

Pmoja na hayo ikiwa tutajaali kuwa hadithi hiyo ina kubalika, hakika kutoka kwake kwa ajili ya sala haikuwa ni kwa amri ya Mtume (s.a.w) pamoja na haya kama vile ilivyo pokelewa katika hadithi ya kuwa Mtume alipo sikia kutoka kwa Abubakar kwa ajili ya sala pamoja na hali ya maradhi aliyo kuwa nayo alitoka kwa kujitegemeza kwa Ali (a.s) na Abbas na kuwasalisha watu na kumweka kando Abubakar.

Twakutakia kila la kheri.

SWALI:

 Napenda kufahamu kuhusiana na baadhi ya matukio ambayo yalimtokea Maalik bin Nuwairah:

Kwa nini Maaliki bin Nuwairah alipinga kutoa zaka na kumpatia Abubakar?

Na je alikuwa ni mwenye kushikamana na wilaya ya Amiril-muuminiin Ali (a.s) kama inavyo semekeana?

Je ni kweli Maalik Bin Nuwairah alikataa kutoa zaka?

Na je mwenye kukataa kutoa zaka huhukumiwa kuwa ni kafiri?

JAWABU: Mheshimiwa: Ahmad Jaafar:

            Assalaam alaykum.

Ama baada ya salam, Ama kuhusu swali lako la kwanza tunasema: Hakika riwaya zetu zinasema ya kuwa Maaliki alikuja kwa Mtume wa Allash (s.a.w) mwishoni mwa maisha yake, akampatia habari ya kuwa Khalifa baada yake ni Amiril-muuminiin (a.s) kwa hivyo Walii wa kisheria kwa mtazamo w Maalik na kwa vitendo vyake alikuwa ni Amiril-muuminiin (a.s), na zaka hapewi yeyote isipokuwa Waliyul-amri, la sivyo ana haki ya kuitumia kulingana na vielelezo (vigezo) maalum vilivyo wekwa.

Ama kuhusu swali lako la pili, kwa hakika imebainika kutokana na jibu letu la swali la kwanza.

Ama kuhusu swali la tatu: Tuna sema: Ndio Maalik alikataa na kusema: Zaka tunawapatia mafukara wetu.

Ama kuhusu swali la nne, tunalijibu kama ifuatavyo: Mtu kama huyo hahukumiwi kuwa ni kafiri, kwa hali yoyote ile  iwayo.

Twakutakia kila la kheri.