SWALI: Aya ya mawaddah

Baadhi wanasema ya kuwa hadithi zote zilizo pekelewa kuhusiana na aya ya utwaharisho ya kuwa aya hiyo imeshuka kwa ajili ya Ahlul-baiti  wa Muhammas (s.a.w) zote zimepandikizwa, na sababu ni kwmba aya ya Mawaddah (kuwapenda Ahlul-baiti) iliyoko surati shuraa imeshuka Makka, na kwamba Imam Ali (a.s) na Fatima walioana baada ya vita vya Badri, kwa maana kuwa walikuwa madina basi jibu lenu juu ya kauli hiyo ni lipi?

Asanteni sana.

JAWABU:

Ndugu mheshimiwa Ahmad Jaafar

Asalaam alaikum warahmatu llahi wabarakatuh.

Ama baada ya salam.

Hakuna shaka wala shubha yoyote juu ya kupokelewa kwa habari (hadithi) zilizo tajwa kutoka kwa Mtume (s.a.w) na maimamu (a.s) zisemazo ya kuwa aya ya Mawaddah imethibiti  ihusianayo na  haki ya Ahlul-baiti (a.s) kwa ushahidi wa vyanzo na vitabu mama na vilivyo mutawaatir kama vile. {Ad-durrul-manthuur cha Suyuutwi juzu 6\ 7- Fadhaailu sahaba cha Ahmad bin Hanbal juzu 2\669- Al-mustadrak alaa sahihaini juzu 3\ 172- Shawaahidut-tanziil cha Haskaniy juzu 2\130- As-sawaaiqul-muhriqahcha Ibnu Hajar ukurasa wa 170- Tafsiirur-raziy juzu  27\ 166- Majmauz-zawaaid cha Haithamiy juzu 9\ 168- Al-kashaaf cha Zamakhshariy juzu 4\ 219- Dhakhaairul-uqbaa cha Twabariy ukurasa 25- na vinginevyo}.

Ama kuwepo kwa aya hiyo katika sura ya Makka hakudhuru maana ya aya hiyo-ni aya ngapi mfano wa hiyo kati ya aya zilizo telemka Makka lakini ziko katika sura ya Madinah na kinyume chake- Baada ya kuthibiti kwa walio wengi kati ya wanazuoni na Mufassiriina ya kuwa aya hii pamoja na aya zingine tatu baada yake kuwa zilishuka madina kama vile {Fathul-qadiir juzu 4\ 671- Ruuhul-maaniy cha Aalusiy juzu 20\10- Tafsiirul-qurtubiy juzu 16\1- Tafsiirul-khaazin juzu 4\ 49-. Natija ni kuwa kauli zisemazo kuwa riwaya hizi zimepandikizwa ni jambo ambalo halipaswi kufikiriwa kamwe seuze kuzungumzwa suala hilo.