SWALI: Aya ya maapizano

Tunakushukuruni kwa juhudi zenu hizi mzifanyazo, na tunakutakieni mafanikio na tawfiq inshaa allah.

Kuhusu aya ya maapizano, tunataraji mtatoa ufafanuzi kwa muhtasari kuhusiana na utukufu na fadhila za Ahlul-baiti (a.s) kupitia ayah ii tukufu.

Mwenyezi Mungu awawafikishe kwa yote yenye kheri.

Jawabu: Mheshimiwa Salies

Assalaam alikum warahmatullahi wabarakatuhu.

Baada ya salaam, hakika aya ya mapizano ilishuka ikiwahusu Mtume (s.a.w) Ali Fatuma Hasan na Husein (a.s) katika ujumbe wa watu wa Najrani, habari hiyo imepekelewa na bwana Suyut kwa njia nyingi katika Tafsiri yake ya Durrul-manthuur juzu ya 2/ 230, na bwana Naisaburiy katika njia tisa juzu 1/ 155, na bwana Ibnu Kathiir amepkea pia katika tafsiri yake juzu ya 1/484 kutoka kwa Jabir.

Kwahakika Mtume (s.a.w) kuwaita Ahlul-baiti wake (a.s) na kuwatumia kumuomba Menyezi Mungu katika maapizano(kumuelekea kwa maapizano) ni tendo libainishlo ubora wao na ukaribu wao na daraja yao mbele ya Mwenyezi Mungu, na kumuapia Mwenyezi Mungu kupitia kwao ili awalaani waongo, ni dalili ya kuwa wo wanayo daraja ambayo hakuna aijuae isipokuwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu kiapo kina daraja mbele ya mwenye kuapiwa, na maapizano ya Mtume (s.a.w) kwa kuwatumia wao (a.s) inamaana ya kuwatumia wao kama hoja juu ya wakiristo, watu ambao ni hoja na dalili juu ya ukweli wa Mtume (s.a.w) na kuwa ametumwa kweli na Allah.

Kama ambavyo maapizano kama yalivyo yana maana kuwa Mtume (s.a.w) aliwafanya watu hawa aliotoka nao kwa ajili ya maapizano kuwa ni washirika katika wito wake, jambo linalo maanisha kuwa majukumu ya daawa (wito) yako mabegani mwao. Pia kutokana na wao kuwa hoja na kutokana na daraja yao, na ikiashiria kuwepo kwao ni kwa kusaidiana na kugawana kwao kazi kati yao na kati ya Mtume (s.a.w) na kama cheo cha harouna kwa Mussa litujulishavyo hivyo isipokuwa ni kwamba hakuna utume baada yangu.

Dhakhaairul-uqbaa: ukurasa 63,  kwa hivyo basi cheo chake (a.s) ni sawa na cheo cha Harouna na hiyo ni sifa ya kuwa kwake hoja na kushiriki kwake katika wito wake kama Harouna alivyo shirikiana na Mussa katika wito wake, kwa hivyo kufananishwa huku katika maapizano pamoja na Mtume (s.a.w) ni dalili juu ya kuwa kwao hoja na kushiriki kwao pamoja nae (kushirikiana nae) katika kufikisha ukweli wa utume wake (s.a.w). Haya ndio yaliyo bainishwa na aya ya maapizano kutokana na nafasi yao na daraja yao (a.s)

Tunakutakia kila la kheri.