HIJAB

 

UTANGULIZI WA CHAPA YA KUMI
 

Wamekuja watu wa kimagharibi katika miji yetu ya Kiislam mitakatifu chini ya (sitara) funiko na maneno matamu.

Na haikuwa ila baadhi ya Waislam kuwafungulia mikono (miwili) na kuwakaribisha kwa kila aina ya ukarimu wakiwa ni wenye kughafilika na nia zao zenye chuki na malengo yao maovu.

Na wamejisahaulisha kauli ya Mwenyezi Mungu.

“Enyi mlioamini msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa wao ni marafiki.  Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki huo nao, basi huyo atakuwa pamona nao.  Hakika Mungu hawaongozi (njia ya kheri) watu madhalimu.”(5:51)

Na punde tu walizinduka Waislam mchezo (njama mbaya) weye kuhadaa, basi waliangalia Waislam katika mazingira yao wakaona katika miji yao imezama na ufisadi na machafu baada yake ilikuwa na hali tukufu kwa fadhila na utakatifu na wema.

Na wakaona (sheria) kanuni zilizopachikwa (za kijahilia) zachukua mahali pa (sheria) kanuni za Kiislamu (za Mwenyezi Mungu).

Kulifafanua kwa upande mwengine linavyozunguka katika akili (za watu) na namna jamii inavyofikiria mas-ala haya muhimu, mtungaji (wa kila kitabu) amejitolea kwa kuitikia mwito wenye kushukuriwa, basi wakajitoa hawa ndugu zetu na kujihusisha na mambo haya ya kidini yenye kusisimua kwa kuona umuhimu wa kutunga kitabu hiki na umuhimu vilevile wa kukieneza ili ipatikane faida kwa wingi, yalivyo matakwa ya taasisi hii kwa lengo la kukichapisha upya, na sisi tunatoa kazi hii mpya wala hatuna jengine isipokuwa shukrani kwa itakayemfikia, na makadirio yetu ni kwa taasisi zote za uchapishaji na uenezaji ambazo zilichapisha kitabu hiki katika chapa yake ya kwanza na hasa taasisi itakayojitolea, tukitaraji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mkubwa mwenye uwezo.

JUMBA LA FIRDAUS


Sifa njema ni zake (Yeye) Mola Mwenyezi Mungu Bwana wa ulimwengu na swala na salamu zimshukie Bwana wa viumbe vyote na mtukufu wa Manabii na Mursali (wote) Bwana wetu na Nabii wetu Muhammad (saw) na Ahli zake wa walio watukufu, watwahirifu ambao kawaodolea uchafu Mwenyezi Mungu na (kawatwahirisha) kawatakasa mtakaso mkubwa, akiwemo Khalifa wake na wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake na dalili yake kwa viumbe vyake, ambaye ni mwisho wa mawasii wa Mtume Imamu wa kumi na mbili Al-Mahdiy anayengojewa, swala za Mwenyezi Mungu zimshukie na aharakishe Mwenyezi Mungu kutokea kwake.

NENO LA MTUNGAJI

Kitabu ambacho kiko mikononi mwako ni katika vitabu ambavyo vinatoa uchambuzi kwa kirefu na kutoa mafunzo (maelezo) kwa kila kipengele kwa urahisi kabisa, tatizo moja muhimu katika jamii wa zama (wakati) hizi, nalo sijengine isipokuwa ni hijabu (kujihifadhi).  Na kufahamika (kueleweka) kimakosa kulikoenea na hapa mpaka sasa watu wengi wanafanya ili kulifanya (lienee) libakie katika jamii zetu za Kiislamu katika karne hii, na wakati zilipokutana tabia za kwanza na za pili na zenye kupenda kwa wingi na zenye kuathiri kwa haraka katika masoko (maneno ya watu) alitanguliza waandalizi katika ndugu zetu ili ajitolee.

Kulitokea maelezo yake Mungu awahifadhi walitarajia kwa uwezo wa Mungu kuweza kulitoa na je, wao wanataka hukumu za kijahilia (ya zile siku za ujinga kabla ya kuletwa Mtume)?   Na nani aliye mwema zaidi katika hukmu kuliko Mungu. (yanafahamika haya) kwa watu wenye akili”.

Na wakaona uharibifu wa upotofu wa fikra kasumba mbaya) zilizo na hatari (sumu) na tamaduni ya Kiarabu inayoangamia imeenea kama yanavyoenea maradhi ya kipindupindu katika jamii.

Na wakaona kuwa wao (watu wa kimagharibi) wamewaibia Waislamu utu wao na tabia (mwenendo) njema na matokeo yake wakawa ni wenye kupotoka na kuchanga (zao) zilizo na mambo machafu.

Wametupatia (watu wamagharibi) silaha zenye kuuwa na kuangamiza ambazo hazileti kheri (hata kidogo) hazibakishi wala haziwachi.

Wametulelea katika miji yetu mambo ambayo yanayotufikisha kwenye taabu na shida (ya milele), ili wazitume (hali hizo) pamoja na Waislamu wenye chuki (taasub) katika jela na kwenye vizuizi.

Ni kweli kuwa wametuletea mitambo na vyombo vingine vya kisasa na mfumo wa kisasa wa kimaisha, lakini ukweli ni kwamba pia wametunyang’anya utukufu na ucha Mungu na utulivu na badala yake wakatuvisha nyororo za udhalina na imani ya (kutomwamini Mungu) kimaumbile.

Hakika wao wametulelea sisi vitu vya kimaada, lakini wametunyang’anya vilivyo na manufaa, na hapana shaka kuwa vilivyo na namna ndivyo vilivyo na umuhimu na bora zaidi kuliko vyote vya kimaada.

Kwa hakika watu wakimagharibi kwetu sisi Waislamu, ni kama vile ng’ombe ambayo imetoa lita elfu ya maziwa, kisha ukampiga (yule iliompa maziwa Pigo la kumuuwa.

Na lau ingesalimika miji yetu na jamii zetu na katika mazingira yetu kutokana na vitimbi vya watu wa kimagharibi na upotofu wao, ingalikuwa hali zetusisi Waislamu ni tafauti na hali tulio nayo sasa. Lakini wapi! Ushatupia (tayari wakati) na hivyo basi tumetaka katika chini ya vivuli vya watu wa Magharibi miaka na miaka tukiwa katika maasi na maovu mazito yenye kuogopesha na kukatisha tamaa. Na sasa ndio mwanzo wameanza kugundua kidogo kidogo ya kuwa watu wa magharibi sio watu.  Wale watu sio wakweli katika mambo yao ya mito yao. Bali wao ni wafanyi biashara na wezi, lengo lao ni kupoteza jamii ya Kiislamu na kutoa neema za Waislamu na mema yao na badala yake wakapanda matatizo na shari na khufu wa kuogopesha katika miji ilio na amani.

Wamepata kutambua Waislamu kuwa wema (haupatikani) isipokuwa katika Uislamu utukufu na wala hakuna sio ukafiri wa kimagharibi wala wa kimashariki na ni juu yake arejee katika ridhaa ya Mwenyezi Mungu na silaha yake ni imani na thaqafa (utamaduni) wa kidini ili apambane na vita vipotofu.   

Na kwa hili, safari imeanza, safari ya kurudi kwa Mwenyezi Mungu, uongofu, kheri, utukufu na hijabu.

Na kwa njia hii maktaba ya Kiislamu zimeshuhudia kwa mshangao, mwanamke wa Kiislamu kujitokeza kwa sura ya Kiislamu yenye hamasa  na fikira ya kidini, imani, sahihi. Na kitabu hiki kwa mdogo wake,  lakini kwa mshangao kimepata wasomaji watukufu wengi, Alhamdulillah wamekifuatilia wanaume na wanawake, na maadui wa kitabu hiki wamekata tamaa haraka sana, na kimerudiwa kuchapishwa mara nyingi.

Mwisho mmoja akaniomba nikiongezee ili kunufaisha zaidi, na kichapishwe chapa ya kisasa, basi nikakkubali ombi, nikakiongezea baadhi ya mambo, hadith na n.k, basi nilipitia baadhi ya mambo yaliyo lazima.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe fadhila kwa kutukubalia, na amuongoze aliyepotea njia yake, hakika yeye ni mwongozi katika njia ya sawasawa naye ni mtegemewa.

10/Ramadhan tukufu/1407

Mohammad Ibrahim Al- Muwahid

UTANGULIZI

Hakuna shaka kuwa mwanamke ni nusu ya jamii, ama utukufu, na heshima yake kama mtu mwingine anayeishi katika dunia hii, na mwanamke sio kiumbe cha ajabu katika ulimwengu huu, na wala sio kizazi ajnabia katika maisha haya, bali yeye ni sehemu katika maisha.

Kwa kuwa Uislamu ni dini ya maisha, basi umeshampa mwanamke umuhimu mkubwa, umemujumuisha kwa hifadhi au upole, basi ukaweka hukumu zenye hekima na kanuni zenye  uadilifu kwa kutofautiana nyanja za maisha yake ya kipekee, kindoa, kifamilia, na ya kijamii, na ukamwachia wakati wa kumwezesha kuwa katika sifa za Malaika na kuweza kupanda daraja la juu Duniani na Akhera. Ili kujua kutoa mwanamke amepewa umuhimu tuangalie katika Qur’an tukufu utapata Sura nzima kwa jina la (wanawake) na katika sura zingine kama aya ambazo yanafungamana naye. Mfano: Hukmu, Kanuni na kumkamilishia kheri na raha, na zimemdhaminia wema duniani na akhera. Na ifahamike kuwa tabia ya mwanamke inatofautiana na tabia ya mwanamume katika upande wa kinafsi (saikolojia), kijamii na n.k. hakika ni kawaida na ni Hekima pawe na tofauti baina ya mwanamke na mwanamume katika baadhi ya hkumu na kanuni. Na haijawa tofauti hii isipokuwa tabia ya mwanamke kuafikiana na nafsi, na sehemu yake, na wala sio kuwa ana upungufu, kama walivyotuhumu maadui wa Kiislamu.

·            Na kanuni ya hijabu imekuja kuonyesha kanuni za kisheria ambazo Uislamu umeziafiki na kuzifaradhisha kwa mwanamke ili ziwe ni mdhamini wa wema wake, na kuhifadhi utukufu wake.

·            Na ina tubainikia kwake kutokana na aya za Qur’an ambazo zimekuja kwa hali ya kurudiwa, basi Mwenyezi Mungu (SW) ameshataja katika aya moja, pamoja n akujua kuwa Mwenyezi Mungu ameeleza mara nyingi hukumu na kanuni katika aya moja au nusu yake tu.

·            Hakika Mwenyezi Mungu (S.W.) alipohimiza na kurudia rudia inaonyesha umuhimu wa hijab na dharura yake katika maisha.

·            Ambacho linatakiwa kuangaliwa na kuzingatiwa ni kuwa kanuni hii ya hijab mara   nyingi inapigana na mambo yasiokuwa na maana, na upingamizi unatoka kwa maadui wa Uislamu, na kwa watetezi wa uharibifu na upotofu. Na imeshakuwa ndio ni lengo kwa kuandika kwao dhidi ya kanuni hii, basi wameanza kwa kusema kuwa ni kanuni iliyopitwa na wakati na wala sio maendeleo, na wanadai kuwa hijab ni ubaya kwa mwanamke na ni upungufu kwake katika maisha, na mengine mengi miongoni mwa tuhuma walizozipita.

·            Vile vile utaona serikali pamoja na kuwa ni masikitiko wanakuwa na msimamo mbaya ili waeneze uharibifu kwa wanawake wa Kiislamu.

·            Na  kila wakati tunasoma katika magazeti, au kusikia habari kuwa serikali fulani imetoa hukmu ya kuzuia wasichana wenye hijab wasiendelee na  masomo ya sekondari au ya chuo kikuu, na serikali nyingine imewajibisha kutovaa hijab ni sharti la kwanza kukubalika kuendelea na masomo kwa wasichana.

·            Nikuregea nyuma kidogo katika tarekhe ya Iran utapata kuwa serikali katika mwanzo          wa Maliki Al-baaid alitoa hukumu hasa ya kuzuia hijabu kabisa, kabisa katika nchi nzima, na wakasambazwa wanaume wenye kuangalia usalama, polisi katika mabarabara, masoko na hata katika vinjia vidogo, vidogo hiyo yote ni kwa ajili ya uadui wa hijabu, walikuwa wakichukua kitambaa cha  kichwani kwa kila mwanamke atakayeonekana amefunika kichwa chake.

·            Ni kwa sababu hii wanawake waumini waliona ni bora kubakia nyumbani bila ya kutoka nje, kwa muda wa miaka kadha, kwa tahadhari ila  wasishikwe na polisi kwa wao kuvaa hijabu.

·            Kwa nini vita hivi visiokua na maana dhidi ya hijabu?  Na kwa nini hawawafanyii vita hivi malaya?  Na kwa nini wasipinge madawa ya kulevya yanayo haribu ibada, na nchi, na kuangamiza vizazi? Mwenyezi Mungu (S.W) amesema: (Na wanapoondoka wanakwenda huku na huku katika kufanya uharibifu humo na kuangamiza mimea na roho, na Mwenyezi Mungu hapendi uharibifu). (Baqarah aya 205).  Ndio, wanatambua hekima ya kanuni hii, na falsafa yake, kimantiki, kiwakati,kiakili na athari zake nzuri, na wameona kuwa hijabu ni kizuizi kinachozuia mipango ambayo inapinga ambayo inapinga Uislamu ulio safi na kwa maana hii ndio hao wanapinga kanuni hii ya Kiislamu kwa kutumia njia tofauti, kupitia televisheni, radio,magazeti,majarida, sinema na n.k, na wanajaribu huondoa vitambaa vya kichwani kwa mwanamke Mwislamu, kumvua haya (aibu) na hijab na kumuelekeza katika uharibifu na uchafu.

·            Ni madamu amri ni hiyo, basi ni ukumbusho kwa mwanamke Mwislamu kushikana na hijab, na afanye kazi kubwa ya kueneza kanuni hii kwa wanafunzi wakike, wasichana na wanawake kuwalingania washikamane na hijabu.

·            Ni wajibu kwa mwanamke Mwislamu hasa katika hali hii na kwa Waislamu wote kuwapoteza fursa maadui, na wasiwachie nafasi ya kuweza kujihakikishia malengo yao ya kishetani ambayo yanadhuru Uislamu na Waislamu. Natarajia kitabu hiki kiwe ndio mwanzo wa kazi hii. Mwenyezi Mungu ni mwenye kuafiki na menye kutegemewa.

1/5/1400 H

Mohammad Ebrahim Al-Muwahid.

QUR’AN INAHIMIZA HIJAB

Hakika tumeshaeleza kuwa Qur’an tukufu imehimiza sana hijab na kutilia mkazo katika aya nyingi na hapa tunataja baadhi ya aya hizo:

1.     Amesema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) “Ewe Mtume: waambie wake zako na binti zako na wanawake wa Kiislamu (wengine wambie wajiteremshie uzuri nguo zao, kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa heshima) ili wasiudhiwe na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu). (Sura Ahzaab aya 59)

-         Katika aya hii tukufu Mwenyezi Mungu anamwamrisha Nabii wake Muhammad (S.a.w.) awaamrishe wanawake wa Waislamu, wake zao, binti zao na wanawake wa Waislamu kwa kujistiri na hijab likokamili. Na baadhi ya wafasiri wameeleza sababu ya kuteremka aya hii, kuwa wanawake walikuwa wakienda kusali katika  msikiti wa Mtume (s.a.w.) wakiwa nyuma, ya Mtume (s.a.w.), basi wakati wakwenda kusali sala ya magharibi na Isha, walikuwa na vijana ambao walikuwa wakiwazuia njiani na kuwaudhi, basi ikashuka aya  ikimwamrisha Mtume (s.a.w.) kuwa wajisitiri na hijab iliyokamili ili wasisumbuliwe na yeyote akasema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) “Ewe Mtume waambie wake zako.

2.     Binti zako.

3.     Na wanawake wa Kiislamu. Na hii inatuelekeza katika umuhimu wa hijab, ama kuhusu familia ya Mtume (s.a.w.) wanatakiwa washikamane na hukumu, kanuni hii kuliko watu wengine. Kisha akasema (s.w.t.): ( wajiteremshie uzuri nguo zao). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameshamuamrisha mwanamke awe karibu na hijab ili ajisitiri sawa sawa na ahifadhi mapambo yake ambayo Mwenyezi Mungu amemzawadia yeye.

-Hakika mwanamke amevaa hijab, lakini hijab lisilokamilika, kama tunavyo shuhudia hivyo mara nyingi, basi utamuona na amevaa kilemba, lakini shingo na nywele ziko wazi.

-Kwa kweli hijab hili haliwezi kuwa malengo alilokusudia Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na kwa maana hiyo amesema: (wajiteremshie uzuri nguo zao) basi ni jukumu la mwanamke Mwislamu kumtii Mola wake mwenye hekima, na kuvaa hijabu lilokamilika  ambalo linnamdhamiria kwa mkumsitiri, kuwa katika usafi, na usalama kutokana na watu wabaya. Hakika hijab linamfanya mwanamke apate sifa nzuri, basi atafahamika kwa kujisitiri, na uzurikatika jamii, kwa sababu  hijab linafanya wanawake wasiudhiwe  na watu wabaya, basi hijab linawekea hijab linafanya wanawake wasiudhiwe na watu wabaya, basi hijab linawekea mipaka  ili wasifikwe na matamanio ya wahalifu au waharibifu na kutodhalilishana. Mwanamke anapojisitiri vizuri na kusitiri mapambo na wale kusionekane kitu kwa wahalifu, hawakuzidhuriwa, na katika zama hii mwanamke ambaye hajisitiri anaonyesha mapambo ataudhiwa tu, lakini akisitiri hakika maharibifu atajua kuwa huyu ni mwanamke mwema na mwenye kuhifadhika, basi hawezi kumuudhi kwa baya, kwa sababu anajua kuwa akimsemesha hatajibiwa, bali huenda mwanamke akamtokea na kumdhalilisha mbele ya watu.

-         Kuna baadhi ya wafasiri wamesema kuwa hijab ni wajibu kwa wanawake huru tu, bila ya wanawake watumwa, na wala hakuna faida kutekelezwa kauli hii katika zama zetu hizi, kwa sababu siku hizi hakuna mwanamke watumwa wala  wanaume watumwa. Kwa kifupi: ni wazi aya hii tukufu inaonyesha kuwahijab ni wajibu, na linampa mwanamke sifa nzuri na kumhifadhi kutokana na uharibifu, na linamwepusha kutokana na shari ya waharibifu.

2.     Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema :  (Nanyi munapowauliza wakeze waulizeni ni nyuma  ya pazia kufanya haya kutasafisha nyoyo zenu na nyoyo zao)  (Sura Ahzaab aya 53)

-         Katika aya hii tukufu Mwenyezi Mungu anaamrisha Waislamu, wanapowauliza wake za Mtume (s.a.w.), basi wawauliza nyuma ya pazia, japo hapa wamekusudiwa wake za  Mtume (s.a.w.), lakini hukmu inajumuosha wanawake wote, kama walivyosema wajuzi, (wataalam) na wafasiri kuwa hukumu hii sio kwa wake za Mtume (s.a.w.) tu, bali ni kwa wanawake wote.

-         Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliposema waulize ni nyuma ya pazia, kisha akasema kufanya haya kutasafisha nyoyo zenu na nyoyo zao, yaani hijab ni kheri kwa wanaume na wanawake kwa pamoja.

-         Ama mwanamume anapomwangalia mwanamke kunaamsha shahwa, na hapo shaitani anamshawishi kufanya haramu na uharibifu.

-         Ama mwanamke bila ya hijab ataudhiwa utukufu wake na kuwa hatarini na maadui. Basi hijab ni usafi na kiepusho cha mwanamume na mwanamke.

-         Na faida ambayo tunaipata katika aya hii tukufu kuwa mchanganyiko baina wanaume na wanawake unasababisha kufanya uharibifu na fitina, kama ilivyotokea katika jamii za changanyiko na zisizovaa hijab.

-         Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameshakataza uharibifu wa kila aina.

Hapa kuna swali, kwa nini suali limeelekezwa kwa wake za Mtume (s.a.w.) bila ya wengine?

Jibu: ni kwa sababu ya daraja yao katika jamii, na wao ni mama wa waumini, basi kinachokusudiwa ni kuwa wake za Mtume (s.a.w.) washikamane na jukumu za Mwenyezi Mungu kuliko watu wengine na miongoni mwa hizo ni hijab, na kwa ajili hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema katika mwanzo wa aya (Enyi wakeze Mtume, nyinyi si kama yoyote tu katika wanawake wengine)

(Sura Ahzaab aya 32) na aya hii ni kama kumwambia mtu: Ewe mwenye utamaduni usiseme uongo, basi hii haina maana wengine waseme uongo, bali maana yake ni kuwa kusema ukweli ni jambo lilowajibu na kusema uongo ni jambo baya (haramu).

Wanawake walikuwa wakiwaendea wake za Mtume (s.a.w.) na kujifunza wanayo ya kushuhudia kwao kutokana na vitendo vyao. Basi ilikuwa ni dharura kwa wao kushikana zaidi na jambo ambalo Mwenyezi Mungu ameamrisha, na kama si hivyo basi aya hii isingejumuisha wanawake wote, kama ilivyo wazi.

3.     Mwenyezi Mungu amesema: (Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu, kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahilia (Ujinga, Ukafiri)

-         Mwenyezi Mungu amemtaka mwanamke akae nyumbani ili angalie mambo yake ya kinyumbani kama vile; mambo ya kindoa, familia na n.k. na ili apate nafasi ya kulea watoto wake malezi mazuri na kuwafunza dini na tabia njema. Kisha kuwakataza kwa bila ya hijab ni vibaya.

-         Basi Mwenyezi Mungu amesema (wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyo kuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za jahilia (Ujinga , Ukafiri) yaani msitoke nje bila ya hijab mkiwa mumejionyesha maana yake ni: Mwanamke kuonyesha mapambo yake mbele ya mwanamume ajnabia, na hii Mwenyezi Mungu anakataza na kuharamisha. Mpaka hapa inatudhihirikia katika aya hii tukufu kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anataka mwanamke Mwislamu awe tofauti na wanawake wengine kwa hijab kwa sababu wanawake wa Kiyahudi, Ukristo, na wakishirikina hawashikamani na hukmu hii yenye hekima, bali wanatoka hali wamejionyesha. Hakika Mwenyezi Mungu hataki wanawake Waislamu wajidhalilishe, bali anataka wawe na heshima.

-         Na hakuna maana kuwa mwanamke yoyote Mwislamu akiacha hijab na kujionyesha, basi yeye atakuwa kama wanawake wa Kiyahudi, Ukristo na Wakishirikina hawashikamani na hukmu hii yenye hekima, bali wanatoka hali wamejionyesha. Hakika Mwenyezi Mungu hataki wanawake Waislamu wajidhallishe, bali anataka wawe na heshima.

-         Na  hakuna maana kuwa mwanamke yoyote Mwislamu akiacha hijab na kujionyesha, hasi yeye atakuwa kama wanawake wa Kiyahudi, Ukristo na kushirikina ni kana kwamba anavua utukufu, na ukarimu ambao Uislamu umemtaka awe nayo, na atakuwa katika sehemu ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaichukia.

-         Na imekuja katika hadith: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemteremshia mmoja wa manabii wake waambie waumini: Wasivae vazi la maadui wangu, basi watakuwa maadui wangu, kama hao maadui wangu.

-         Ni wazi kuwa maneno haya yana lengo waumini wa kiume lakini yanajumuisha na waumini wa kike pia kama ilivyo hali katika aya nyingi na hadith.

-         Aya hizi tatu zimeshaelezea jambo la hijab na kuna aya zingine ambazo zinazungumzia maudhuu haya, hatujaziita kwa sababu ya kufupisha mambo.

FATMA ZAHRAH NI KIINGIZO CHEMA.

-         Fatma Zahra (AS) anachukuliwa kuwa ni mfano wa mwanamke katika uislam, na kiingizo chema kwa kila mwanamke anayetafuta wema katika maisha, basi ni bibi na mwanamke ulimwenguni na mwenye kuelewa katika Wahayi, ni mwenye kuelewa unabii na ujumbe, na amefikia daraja ya juu katika utukufu. Na baba yake amesema (S.a.w.) (Hakika Mwenyezi Mungu ameridhia kwa ridhaa ya Fatma na anakasirika kwa kukasirika kwake)

-         Mpaka hapa, hakika kila mwanamke ulimwenguni amchukue bibi huyu mtukufu kuwa ni kiizigo chake katika maisha, ili ajimulikie kwa uru yake na afuate njia yake ya uongofu kwa wema na kufaulu. Hakika bibi Fatma (AS) ni mfano wa kila fadhila, na kheri, mwanamke yoyote anayemfuata atapata wema, mwanamke yoyote atakayemwacha na kufuata mwingine atapata ubaya. Hakika bibi huyu mtukufu alikuwa katika daraja ya juu kabisa katika hijab, alikuwa hatoki nje isipokuwa amejisitiri mwili mzima, kuanzia kichwani hadi kwenye nyayo, alikuwa amechukiasana kujionyesha na kutova hijab, hakuwa akifanya hivyo ila Mwenyezi Mungu anachukia pia. Kwa sababu kutovaa hjab ni ufunguo wa kila madhalili ni njia ya uchafu na ni mwanzo wa kuanguka, bali ni kuanguka hasa

-         Na sasa hivi njooni tusome baadhi ya mafundisho ya hijab katika maisha ya bibi Fatma.

Ubora wa mwanamke ni nini? 

Tarekhe inatubia kuwa Mtume (s.a.w.) siku moja aliwauliza Sahaba zake suali (ni kitu gani bora kwa mwanamke)? Basi sahaba wakanyamaza, kwa sababuhawakuwa wanajua jawabu hasa au jawabu sahihi la suali hili,m wakaanza kufikiria! Ni kitu gani bora kwa mwanamke? Mali? Uzuri? Ndoa? Au nini? Bibi Fatma Zahra akasikia suali hili, basi akatuma mtu kwa baba yake ili akamwambie ubora wa mwanamke ni kutomwangalia mwanamume anaye kusudiwa hapa ni ajnabia. Na  sahaba wakabakia kumsubiri Mtume (s.a.w.) atasema nini? Kuhusu jibu la binti yake.

-         Basi Mtume (s.a.w.) akasema: amesema kweli na kusema hakika Fatma ni sehemu katika mimi. Ni vipi? NI vipi? Ni kwa sababu jawabu lake hili linatoka katika sehemu ya haki na ukweli wa imani. Na kwa jawabu hili Mtume (s.a.w.) ametangaza kwa kila mwanamke ulimwenguni kuwa ubora wa mwanamke ni hijab na shari yake ni kutovaa hijab.

Mazungumzo yenye Manufaa

Tarekhe inatuambia kuwa, bibi Fatma Azaharah (AS) alikuwa amekaa na baba yake (S.a.w.) na hapo alipaga hosi Ibn Ummu Maktum, naye alikuwa ni kipofu, na kabla hajaingia kwa Mtume (s.a.w.), bibi Fatma Azaharah akasimama na kuondoka, na alipoondoka Ibn Fatma (AS) akarudi kwa baba yake kwa mara nyingine, na hapa Mtume (s.a.w.) akamuuliza sababu ya yeye kutoka nje, pamoja na kujua kuwa Ibn Ummu Maktum haoni kitu, Mtume (s.a.w.) alikuwa akijua sababu hili, na ili tarekhe iandike mazungumzo haya ya kiimani yabaki kuwa mfano bora katiak maisha yote

-         Basai akasema (AS) : kama hanioni mimi, basi mimi namuona, naye ananusa harufu ya mwanamke. Basi Mtume (s.a.w.) akastaajabishwa na jawabu hili lenye utukufu kutoka kwa binti yake mwenye hikma, Mtume (s.a.w.)  hajawahi hata mara moja kumwambia Fatma ashikamane na hijab, bali amempa moyo na kumuunga mkono na kumwambia: nashuhudia kuwa wewe ni katika mimi. Bibi Fatma (AS) wakati alipotaka kutoa khutba katika msikiti wa Mtume (s.a.w.) walimwekea pazia msikitini, basi akakaa pamoja na wanawake wenzake katika upande wao, na waume wakaa upande mwingine, walikuwemo Muhajirin na Ansar.

-         Na pazia hii ilikuwa na maana nyingi:

Kwanza ni katika  upande wa kutekeleza kanuni ya hijab kwa kuwekwa pazia baina ya jinsia mbili.

-         Pili ni kupinga kitendo cha kuchanganyika wanaume na wanawake, kitendo ambacho wanakitaka maadui wa Kiislamu, ambacho kinasababisha upotofu. Na nyuma ya pazia bibi Fatma alianza kuhutubu khutba yenye manufaa ambayo imechukuliwa kama ni aya katika aya za Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa sababu ilikuwa na ujuzi, hekma, maana, fasaha na balagha. Ni vizuri kwa kila Mwislamu  mwanamume na mwanamke kusoma khutba hiyo, na kufikiria baadhi ya mmambo, ili apanukiwe na fikra katika ulimwengu wa elimu na imani. Ewe dada Mwiislamu: hii ni mifano mitatu katika maisha ya bibi wa mwanamke katika  Uislamu, na kiingizio chema, ni vizuri kwako kujifunza  mafundisho matukufu yenye kukupatia haya, na kukufanya unywe mwanamke mwema mwenye kushikamana na uislamu na hukmu za Qur’an tukufu.

KUJISITIRI NI UREMBO WA MWANAMKE

Amesema Mtume (s.a.w.): kujirembesha ni urembo wa mwanamke. Kuna aina mbili za mapambo.

1. Mapambo yasiyopo ya kweli        2. Mapambo ya kweli

Na mapambo yasiyo ya kweli ni ambayo hubaki daima mda mfupi na kama kumalizika bila kuongeza urembo wowote katika mwili.

Amma mapambo ya kweli ni ambayo hubaki daima dawamu na kumpatia mtu daraja ya mwanaadamu aliye kamilika. Na kwa mfafanuzi usio na shaka ni kwamba: marembo ya ukweli ndiyo yaliyo ya muhimu zaidi kuliko marembo mengine. Bali ndiyo shaba na inayo mlazimu mwanaadamu ashughulike kwa ajili yake. Na kama , na kama hana madh: yoyote (kwa mapambo) basi hatukuwa na kima cha mapambo yasiyo  ya kweli hatkuwa  na kima cha mapambo yasiyo ya kweli kamwe. Amma poda na manukato na mengineo kwa mapambo yasiyo ya hakika hayana kima chochote, hasa kama mwanamke amekosa stara ( hijab) . Hijab kuitupa (Hijab) uharibifu jina la la mwanamke na kuweka alama za kuwelesha juu ya utukufu na ukarimu wake wazi wazi, kwa mamia na maelfu ya machoni mwa watu. Na wala hatuwezi kujua ni mikono mngapi iliyoshikashika mikono na mwili wake kwa kutovaa hija?! Na jee mioyo hivyo hakika kutovaa hijab husababisha tuhuma na kashfa kwa mwanamke. Na amesema Ali (AS) atakaye tupa nafsi yake katika sehemu za jawana basi asimlaumu atakaye mdhania kwa mabaya. Usul Kafi 8 UK: 52 hakika mwanamke asiyevaa hijab hudhuru nafsi yake.

Kwanza: anadhalilisha sehemu yake mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kwa kuepuka amri ya Mwenyezi Mungu na kukhalifu kanuni zake. Na utasoma katika darasa lifuatalo na adhabu ya mwanamke siku ya kiyama. Amma jinsi anavyo poteza heshima zake katika jamii. Ni kwa sababu ya kujidhalilisha na kudhihirisha mapambo yake mbele ya watu na kuuza nafsi yake kwa macho ya ufisadi. Amma mwanamke aliye na hijab basi hufaid msimamo miwili kwa  pamoja

1. Kwa Mwenyezi Mungu           2. Katika jamii. Amma kwa upande faida anayopata kwa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na mwalii wake. Kwakuwa ni mtiifu wa Mwenyezi Mungu, akiingiza maamrisho ya Mwenyezi Mungu, kwani amemsitiri yaliyo yajibishwa na Mwenyezi Mungu kusitiriwa. Kwani hanyayui mguu wake illa rehma ya Mwenyezi Mungu hamfuata. Na Mwenyezi Mungu anaridhia marafiki wake na Malaika wake  wa mbinguni humuombea msamaha kama anavyosema Mwenyezi Mungu. “ LAKINI KILICHOKO KWA MUNGU NDICHO BORA NA KITABAKI”.  (AL QASAS 60.) Amma katika jamii kwani anaheshimiwa na kutukuzwa kwa kuwa amerembeka na hijab lake na mehifadhika na utukufu wake na anistiri uzuri wake aliopewa na Mwenyezi Mungu.

MAZUNGUMZO BAINA YA MSICHANA WA KIKRISTO

Kuna hadith : iliyo tamu iliyomtokea mmoja wa wanachuoni: wa kidini, alipo mjia mschana wa kikrito, na kumwambia: mimi najua mengi kuhusu Uislamu na nimestaajabishwa na sheria na desturi za dini hii  na nikazipenda sana, lakini kuna sheria moja tu iliyo nisababisha nisiwe muislamu na nimeuliza watu wengi lakini sijapata jawabu la kunitosheleza, basi kama utaweza kunibainishia hekima ya kanuni hii basi nitasilimu.

Akauliza Mwanachuoni: Na ni kanuni gani hiyo? Akasema msichana: Kanuni ya hijabu….. na ni kwa nini Mwenyezi Mungu alifaradhisha hijabu kwa mwanamke na kwa nini hakumuacha atoke bila hijabu kama mwanamume?

Mwanachuoni:  Je umewahi kuingia soko la bidhaa za thamani na dhahabu?

Msichana:  Naam.  Mwanachuoni: Je uliona kwamba bidhaa za thamani na dhahabu zimefungiwa katika sanduku la vioo?   Msichana :   Naam.

Mwanachuoni:  Mbona bidhaa hizo hazikuwachwa wazi ( mikono mwa watu) kwa nini likafungiwa katika sanduku la vioo.

Msichana: Ilikuepukana na waizi na mikono mibaya.  Mwanachuoni: Naam! Na hii ndiyo hekima ya hijabu, mwanamke ni kama bidhaa ya dhamana ni lazima ihifadhiwe kutokana macho ya iwe katika kitu kitakacho kusitiri kutokana na macho ya waovu kama inavyo hifadhiwa “Lulu”  katika ngozi yake ili isichukuliwe na watafutaji, na hijabu pekee ndiyo sitara yake na hifadhi yake.  Hakika mwanamke aliye na hijabu husalimika kutokana na khiyana za watu kwa kuwa mwili wake umefichwa, na uzuri wake umefichwa, kwa hivyo watu hawaoni chochote katika mwili wake wala hawamtamani hata kidogo, na wao huepukana nae na wala awawezi kumtamani kivyovyote vile, bali humuogopa na kumuonea haya. Hayo yote ni kwa sababu ya ya hijabu, kwa hivyo hijabu ni kizuizi chako na ni hifadhi ya utukufu wako na karama yako, ewe  msichana hiyo ndiyo hekima ya hijabu. Kisha ukatukuka uso wa msichana huyo na akasema:  Hivi sasa nimetosheka na hekma ya kanuni hiyo ya Kiislamu, na ninapendelea niwe Muislamu; kisha akatamka shahada mbili.

Haya ni mazungumzo mazuri ya kidini yanayotubainishia kwamba Uislamu unataka kuhifadhi utukufu na heshima za mwanamke, na unataka kusitiri jamii na kuilinda basi ikawajibisha kama sheria na sharti ya asli.

TOFAUTI YA MWANAMKE ANAYEVAA HIJABU NA ASIYEVAA HIJABU

Alinieleza mmoja wa marafiki zangu kuhusu kisa kilicho mtokea mmoja wa waumini, nacho ni kwamba alikuwa akitembea na mke wake aliye valia hijabu katika moja wapo wa sehemu kustarehe kwa watu wote. Alipojiwa na mmoja wa wadhihaka na mke wake asiyekuwa na hijabu na kunuuliza, kwa nini atoke amevaa hijabu.

Jawabu lake lilikuwa maridadi sana, alipomuuliza:  Je unajua tofauti baina ya mwanamke anayevaa hijabu na asiyevaa hijabu mdhihaka kwani kunatofauti gani.

Muumini: Ni ipi tofauti baina ya teksi na gari la kibinafsi?

Mdhihaka: Tofauti ni kwamba taksi ni gari la watu wote na lakibinafsi ni la mwenyewe pekee.

Muumini:  Basi hivyo hivyo mwanamke asiyevaa hijabu ni w awatu wote wanamtizama jinsi wanavyotaka mwili wake na mapambo yake na labda humfanyia uadui kama inavyotokea mara nyingi basi huwa gari la jamaa. Ama mwanamke amevaa hijabu, yeye huwa mtukufu, ni mume wake anayemuona wala haonekani ni mwengine wala haangaliwi niwaovu na wafisadi wala hafungui uso wake na mapambo yake kwa macho ya wana khiyana kwani anahifadhiwa katika hijabu, utukufu wake ukarimu wake mwili wake mapambo yake  yamehifadhiwa na mume wake, ametukuka kwa mume wake,kwa kuwa anamuamini na anajua ya kwamba ni wake pekee, wala hana uhusiano mbaya na wengine. Na hapa aliona haya (mdhihaka) kutokana na maneno haya ni ya kweli na mfano mzuri na mimi natubia kwa Mwenyezi Mungu kuwa yaliyopita.  Kisha mke wake akaruka na kusema:  Naam, na hapa kwa Mola wangu maneno hayo ni ya kweli na mfano mzuri sijawahi kuusikia na mtu yeyote mfano huo umeingia moyoni mwangu nami pia natubu.  Basi mume akarudi ili akamilishe maneno yake akisema: Hivi sasa naamini kwa hijabu na kutoka leo mwangu ataingia katika utukufu na ridhaa ya Mwenyezi Mungu, na wala hatatoka nyumbani bila ya kujihifadhi kwa hijabu na vazi la Imani kwa kuwa nafsi yangu inakataa mke wangu awe kwa watu wote.

MADAI YA WASIOVAA HIJABU YANAKUSUDIA NINI?

Baada ya masomo kwa muda mrefu ya maadui wa Uislamu, wameongezea mistari kadha wa kadha ya kuupinga Uislamu na Waislamu. Na moja wapo waingia walizozitumia kwa hiyo ni kulingana kwa kutovaa hijabu na ufisadi, chini ya maneno yaliyo wazi na ulinganifu ulio wa batili, na kwakutumia ujuzi na daraja za hali ya juu.  Basi adhabu ni kwa wanaolingania kwa ufisadi, na wanaolingania kwa uovu na kwa wanaodhalilisha dini ya Mwenyezi Mungu. Na baadhi ya Waislamu waume kuna wake wamedanganyika kwa maneno haya yanayovutia kwa uangamivu na upotovu . Wanawake wetu wa kiislamu na mabanati zao wametupa vazi la Kiislamu takatifu “Hijabu” Na kutoka katika nyumba ya imani na utukufu na kukimbilia mavazi ya kiyahudi na manasara yanayotoka nchiza kimagharibi na mashariki, na lengo la maadui wa Kiislamu tayari limefaulu….. jamii za Kiislamu zimetumbukia katika kisima cha upotovu na ufisadi na kugeuka hadi jamii za ufisadi baada yakuwa zimetakasika. Na kudhihirisha maovu yake na visa vya ubakiaji, ikadhihiri kwamba wao ndio wanaolingania kutovaa hijabu kwa mwanamke, kwa kweli humuita na kumuingiza katika maovu kwa kutovaa hijabu na kudhihirisha mwili wake na kumvuta hadi kichinjoni. Na kwa sababu wanataka kuvua utukufu wake, hivyo basi humbidi kufuata matamanio na lafdhi za kibatili; Ewe msomaji, ukitaka kuelewa maneno yangu vizuri uliza mmoja wa wazee wa zamani na mababu wanaokumbuka yaliyopita, waulize: Je hivi VISA VYA UBAKAJI na vitendo viovu, vilikuwepo katika zama zenu, kabla ya miaka ishirini na thalathini?  Kwa hakika jawabu utakalopata ni la “ Hakukupatikana  visa vya ubakaji”  Basi maovu haya yalitoka wapi?

Yasemekana: Yasemekana na mambo kadha; na miongoni mwa mambo hayo ni kutovaa hijabu na kudhihirisha mapambo yake.  Na hili ndilo jawabu lililo sawa.  Na ukitaka kuhakikisha zaidi waulize wana vijiji vidogo ambavyo bado vinashikamana na Uislamu na kanuni zake, waulize wanavijiji vidogo ambavyo bado vinashikamana na Uislamu na kanuni zake, waulize; Je katika kijiji chenu kunapatikana visa vya ubakaji kama vinavyopatikana mjini?  Watakwambia La…..La .

Kwa kuwa  bado jamii imehifadhika na Uislamu nasheria zake zilizo ongofu. Ama katika nchi zinazo dai kwa maendeleo, kwa upande wa machafu yanazidi kiasi cha kuhofisha. Inatulazimu kung’oa mizizi ya ufisadi kwanza mpka mabaya yajifiche na baada ya hapo yamalizike, kwa sababu maovu huzaliana katika vtuo vya ufisadi na machafu, kama sinema chafu na filamu zinazoteremsha utu wako  na picha za magazeti zilizo uchi na katika jarida na kutovaa hijabu na mapambo na mengineo, na hivi vituo vya ufisadi bado vipo, maovu na vita wala hauwezi kuzihukumu kwa sheria zilizo wazi.

NILIPI BORA?

Hivi sasa kuna mifano miwili katika jamii, wanawake wawili kila mmoja anatofauti na mwengine:

WA KWANZA

Mwanamke anayevaa hijabu vazi la Kiislamu na amerudi katika utukufu na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu na kupata daraja Peponi na huzidi kuogopewa na kutukuzwa na kujikataza yasiyo mfaa na kujiheshimu, wanaopenda kutizama wanawake, watamtizama  lakini hawataona chochote katika mwili wake, na wala hawatamtambua kuwa ni msichana au ni mwanamke mrembo au si mrembo?  Basi atamtizama kwa mtizamo wa kiheshima na wala hatamfanyia maovu au maudhi yoyote kwa kujua kwamba ni mwanamke anaye heshimika  na kushikamana na dini yake, na mwenye kuhifadhi utukufu wake, na ameshikamana na Uislamu kujionyesha atakuwa amejiepusha na ufisadi, upotevu, tabia mbaya na kujidhalilisha.

WA PILI

Mwanamke  asiyevaa hijabu amelivua vazi la heshima na kuondoa huruma na kuepukana  na Imani, kwa sababu haya kutokana na Imani,  na asiekuwa na haya basi hana Imani na ameupuuza hukumu za kwa mapambo ya wanawake wa mwanzo wa kijahili na akajifananisha na wanawake wakiyahiudi na kinasara na ameepuka utukufu wake na heshima zake kwa kuonyesha mwili na viungo vyake na kubadilisha uso wake na mikono yake na kubadilisha uso wake na mikono yake na kifua chake na kujibambua ili waovu wapate kumtizama na waliyo na khiyana wampigie makofi, na kutangaza mwili wake kama mfano wa bidhaa zilizo sokoni na pia humchezea na kumnyongesha na labda humfanyia uadui na kumzungumzia kwa kuwacha hijabu, Atakosa utukufu na kukuasirisha ukarimu wake na huwa amekatikiwa na kuishiwa kwa sababu ya shida na maovu na yote hayo ni kwa kutovaa hijabu. Hivi sasa umewajuwa wanawake wawili katika jamii, hebu karibu tujadili baina yao na kuhukumu kwa akili na mambo yalivyo. Na tujiulize swali hili: Ni yupi mbora kati ya wanwake hao wawili? Kati yao ni yupi anayeogopewa na kutukuzwa? Ni yupi aliye na rutuba na heshima? Kwa hakika mwanamke mwema anayevaa hijabu ni mbora na anadaraja  ya juu na gharama yake na utukufu wake ni wa juu zaidi.

KUTOVAA HIJABU NI HATARI KATIKA JAMII

Hakika mtizamo wa Kiislamu katika jamii ni kiheshima sana (Uislamu) hutaka kutengeneza jamii safi iliyotakasika, wala hautaki kuona mtelezo katika ufisadi. Na miongoni mwa vitu vinavyo tengeneza Imani katika jamii na utakasifu wake ni : Hijabu, Uislamu  uhifadhi na kusitiri jamii, na moja wapo wa hila za kutakasisha jamii ni kufuatakanuni za hijabu ni jambo lisilowezekana kusafisha jamii kutokana na za mwanamke asiyevaa hijabu na marembo yake, kwa sababu kutovaa hijabu ni kama ugonjwa wa kolera jinsi unavyoenea katika jamii, utakapoenea jamii utakomeka katika ufisadi na upotovu na kutumbukia katika maovu ya khiyana, hakika Uislamu umetaka kuung’oa mzizi wa ufisadi na maovu kwa njia kadha; na moja wapo ni umuhimu wa hijabu na kwamba Uislamu umepinga ufisadi na nyenendo zake, nazo ni marembo na kutovaa hijabu.

KUTOVAA HIJABU NA UFISADI

Hakika ubaya wakutovaa hijabu na athari zake ni:  Kuharibu vijana na kuwapoteza amesema Imam Ridhaa (as) “ Na mumeharamishiwa kutizama nywele za wanawake, na viungo vinavyosisimua wanaume kwa sababu ya ufisadi ya kuingia kwa ysiyo halali na wala asiyosifika nayo.

Hakika mwanamke anayetoka bila hijabu na kudhirisha mapambo yake na kuelekea barabarani na mitaani na huku akitizamwa ni wanaume, wakighafilika kwa msisimko wa kimwili, tizama nilipi litakalo tokeo ndio; inawaathiri miamko ya kimwili, na kutazama huku na kule kutafuta hali za kujitosheleza, basi wao hufanya nini? Kama si watu waloshikamana na dini au kijihimiza Uislamu, basi hukimbilia njia zifuatazo: Kuchezea sehemu zao za siri (ponyeto) kisha  zinaa na kuvunja kanuni za Mwenyezi Mungu. Na kwa maovu haya yote na kwa kughalifu sheria na kanuni  za Mwenyezi Mungu na dini yake basi huzalisha maradhi yaliyohatari na mabaya yanayo angamiza. Gadi kwamba imetolewa poti ya kwamba idadi ya hospitali za kutibu magonjwa ya zinaa ni 650 katika Amerika pekee.

Mwanamke asiyevaa hijabu anaye sababisha vijana kutumbikia katika haramu na machafu. Basi huisabiwa mshiriki katika maovu na adhabu, kwa kuwa amesisimua shahawa kwa mapambo yake yalio wazi, hii ndio hali ya vijana wasio na dini.

Na wakiwa ni wenye dini na kujihimiza Uislamu, basi huzimisha miamko yao ya kimwili katika undani undani wao na hupiga vita matamanio yao katika nyoyo zao na kujilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani na vitendo vyake na wao huvumilia maudhi yanayowapata. Kwa hivyo mwanamke asiyevaa hijabu ataulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kuwakera na kuwaudhi hao walio shikamana na dini yao.   

KUTOVAA HIJABU NA UBAKAJI

Katika ubaya wa kutovaa hijabu na athari zake mbovu ni ubakaji wa wanawake na kuwaingilia kimwili kwa nguvu na kwa kutopenda. Kwa kawaida mwanamke anaye dhihirisha urembo wake na uzuri wake usisimua shahawa za wanaume…….. na anafaa kutoa kodi ya nafsi yake na kwa mwili wake na kwa utukufu wake. Hakika mtizama wa wanaume wapotovu wasio  dini kwa mwanamke aliyedhihirisha mapambo yake ni kama mtizamo wa mbwa mwitu kwa kondoo au mtizamo wa paka kwa panya na mwindaji kwa mnyama wa mwituni, basi siajabu mwanamke kuingia katika shimo alilojichimbia mwenyewe au kuepukana na maadui wachafu, vyatokea visa vya ubakaji wa wanawake katika nchi za kimagharibi nchi zilizo chafuka na kuangamia kwa namna ya ushangaza!!!

 Hadi kwamba Gazeti la UINGEREZA la GURDIAN linaripoti likisema:  Hakika ripoti za polisi wa Amerika zaonye kuzidi visa vya ubakaji mwaka baada ya mwaka….. katika WASHINGTON, pekee visa vya ubakaji hutendeka kila baada ya dakika 15!!  Na katika mji mkuu wa Uingereza vimetokea visa tofauti tofauti 2095 za ubakaji ni : Kutovaa hijabu, nimesikia kwamba mmoja wa Maraisi katika nchi moja wapo nchi za Kiarabu kwamba: Mara kwa mara hutembelea vyuo vikuu na kuwatembelea wasichana na kuchagua aliye mbora na mrembo zaidi kati yao kisha ana kikosi cha raisi, huja hadi nyumbani mwa yule msichana na kuelezea babake kwamba: Hakika Raisi wa Jamhuri anapenda  kumaliza usiku waleo na huyu binti yako. Basi baba huona ya kwamba kiyama kimemfikia na familia yote kwa jumla kwa kuwa wanaelewa vizuri sana kwamba Raisi  huyu haishi na msichana ila kwa usiku mmoja!!

Na je wanaweza kukataa mwito wa Raisi? Na je wanauwezo wa kumaliza kwa haya maovu yanayo wasubiri?  Na ni yapi matokeo yake?  Hakuna nyengine ila ni kwamba msichana aende na maaskari hao hadi kwa mchafu na mdhalimu; amchafue kisha arudi kesho yake amekhasirika na kupoteza utukufu wake aona dunia imezunguka macho

Yake: Ewe ndugu msomaji wanao soma visa hivi au wanaozisikia, utawaona wakimlaani huyu Raisi muovu na kuonyesha kiwango cha machafu yanayomkumba lakini wacha tuzingatie kuhusu mizizi ya visa hivi, songea tutizame swali hili: Ni yupi muulizwa wa kwanza?  Si huyo baba siku aliyomruhusu binti yake kutoka nyumbani uso wazi na pia marembo, na kama angelimsitiri je yule Raisi muovu angemtamani na kumwinda? Baba ndiye atakayeulizwa?  Siku aliyonunua RUNINGA, huyo adui wa nyumbani aliye mchafu kwa kustarehesha jamaa zake na kushuhudia vipindi vya kimaendeleo siku aliyokuwa akiwapelekea jamaa zake sinema washuhudie picha chafu chafu.  Na mama pia siye atakaye ulizwa?  Siku aliyokuwa akiharakisha kutengeneza nywele za msichana wake na kumrembesha utadhani yuko katika usiku wa sherehe za harusi yake, kisha amtuma aende shuleni?! Siku aliyokuwa akimtafutia binti yake sketi (mavazi mafupi) yanayobana mwili. Na pia msichana ataulizwa kwa huu muelekeo mbaya alioukubali na kutovaa hijabu, hii ni njia mbovu iliyojawa na miba na mawe.

Naam hao ndio watakao ulizwa katika daraja ya kwanza na baada ya hayo mlaani Raisi!!

KUTOVAA HIJABU NA UTOAJI MIMBA

-         Hakika mabaya yanayotokana na kutovaa hijabu na athari zake ni pamoja na utoaji mimba, kumkatakata mtoto kwa kutumia vifaa na visu, kwa kuwa mwanamke mwenye kujionyesha – kama tulivyotaja mara nyingi hukumbana na vijana wahalifu, wanapompata basi huwa ni mazoea kwao, kinachofuatia ni kupoteza utukufu wake na ukarimu wake, na natija yake ni kubeba (kupata) mimba ya haramu, hapo ndio chanzo cha matatizo yatakayompelekea kutoa mimba.

-         Na hii imetendeka- na inatendeka-nchi za kimagharibi, ripoti hasa iliyotolewa.

-         Uingereza kwa idadi ya utoaji mimba imezidi kutoka 50 alfu katika mwaka wa 1969, mpaka kufikia 83 alfu katika 1970, na katika 1971 idadi yake inakaribia 200 alfu, ni katika Ufaransa inazidi pia mpaka kufikia baina ya 46 mpaka 143 ni utoaji mimba kwa kila mia mbili wanazaliwa, na katika muungano wa Soviet: Utoaji mimba umefikia milioni ni sita kwa kila mwaka.

-         Hakika idadi hii ya kuogopesha, si lingine isipokuwa ni natija ya mwanamke kutovaa hijabu na kuonyesha uzuri wake na mapambo yake, na hakuna kinga ya kuepukana na mabaya haya isipokuwa hijabu.

KUTOVAA HIJABU NA KUFANYA HIYANA KATIKA NDOA.

-         Siku moja imetokea kufanyiana hiyana katika ndoa baina ya wanawake wasiovaa hijabu, na idadi yake imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku.

Mara nyingi mwanamume huwa ni sababu yeye anaruhusu kwenda kwenye sherehe potofu na sinema chafu, na huko atafahamiana na wanaume hao, kwa hali ya kutabasamu na kuwapa mkono, kuwakaribisha kwa matunda peremende (sweet), kana kwamba yeye sio ajinabia wa wanaume hao.

Kadiri siku zitakapopita, ghafula mume anafahamu kuwa mke wake anahusiana wa kimapenzi na rafiki fulani na wanaume ajnabia pia.

Na hapa ndipo mapinduzi yatatokea na atalipuka kama volkano kwa mke wake, na   wakati  yeye ndio sababu ya mabaya haya, yeye ndio alimuongoza mke wake katika njia hii nyeusi, naye ndio ni chanzo cha dhambi hii.

-         Na hapa mwanamume atakuwa na mambo mawili

-         Ima aendelee kubaki na mke wake huyu mwenye hiyana na kuishi pamoja naye, maisha ya kuadhibika kiroho na uchungu wa kinafsi na kutokuwa na imani naye, au aende mahakamani ili amuandikie talaka na kuepukana naye.

-         Na mara nyingi talaka huwa ni chaguo la mwanamume, lakini ni baada ya fedheha na aibu katika jamii, na hapa familia ina vunjika, na kuvunjika maisha ya ndoa, na taabu zinakuwa ni za watoto, kwa sababuwanamkosa mama yao na wao bado ni watoto, basi wataanza kukosa mapenzi, malezi na watakuwa na hali upweke na kujihisi kuwa wamepungukiwa na kitu katika jamiii, na watabadilika na kujiunga na wezi na wahalifu.

-         Kweli hii imefanyika katika nchi potovu na imekuja katika gazeti la (Buraafidah) la soviet kuwa asilimia 80%  ni miongoni mwa hali zote za uvunjaji sheria ambazo wanazifanya wahalifu na asilimia hii 80% inaregea katika kuvunjika familia, na hakika hali kadiriitakavyoenda mwisho wake utaishia kwa talaka katika umoja wa soviet, na sababu hasa ya kujitokeza mambo haya ya kijamii huwa ni uchafu wa tabia na unywaji wa pombe. Ndio hii ni natija ya kutovaa hijabu.

Hakika Uislamu hauja haramisha kutovaa hijabu isipokuwa ni kinga kutokana na mabaya haya, na hauja faradhisha na mabaya haya n.k.

-         Magazeti yameandika kila siku na kutuelezea kuhusu kufanya hiyana katika ndoa, mambo ambayo yanatokea kwa sababu ya kutovaa hijabu na kujionyesha kunapelekea kupewa talaka au kuadhibiwa.

-         Basi ni mara ngapi tumesoma na kusikia kuwa mwanamume aemuacha mke wake na watoto wake kwa ajili ya kuoa msichana asiyevaa hijabu ambaye wamefahamiana katika bustani au sehemu nyingine.

-         Ni mara ngapi tumesoma kuwa mwanamke amemuacha mume wake kwa ajili ya kuolewa na kijana aliyemfahamu katika sinema au bichi.

-         Gazeti moja limeeleza kuwa mwanamume amemua rafiki yake ili yeye amchukue mke wa mwenzake ambaye alikuwa akijitokeza mbele yake bila ya hijabu, hali hii inapingana na aibu na hijabu.

-         Na linaendelea kutaja  kuwa mwanamke amemua mume wake kwa kushirikiana na rafiki yake na kumkatakata viungo vyake na kuvitupa katika shimo la uchafu, na hiyo ili aolewe na huyo rafiki yake.

-         Gazeti moja la Kiarabu limeelezea kuhusu kufanya hiyana katika ndoa- nayo ni swala la kusikitisha, kinachisikitisha zaidi kuwa jambo hili limetendeka katika moja ya nchi za Kiislamu lau lingetendeka katika nchi za kimagharibi ingekuwa ni sawa, kwa sababu ni nchi ambazo zimetolea ufisadi na ni sehemu za udhalili, lakini kwa nini katika nchi za Kiislamu zilizo safi? Zimeepukana na ufisadi.

-         Hakika hiyana na mabaya haya yanatokana na kutovaa hijabu, na hii ndio natija ya mwanamke kujionyesha na kutovaa hijabu, na mambo haya hayawezi kuishi isipokuwa kwa kuvaa hijabu, na mambo haya hayawezi kuisha isipokuwa kwa kuvaa hijabu na kujihifadhi, kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (S.a.w).

-         Ewe ndugu msomaji ningependa nikutajie kisa kimoja ili ufahamu umuhishimu wa kuvaa hijabu na mabaya ya kutovaa hijabu!

-         Wachezaji walienda katika moja ya nchi ili kumshangilia mmoja wa wanamieleka, na mmoja wao aliongozana na mke wake mzuri (asyevaa hijabu).

-         Na walipofika uwanja wa ndege wachezaji na wana mieleka wakamsalimia pamoja na mke wake kwa kumpa mkono, na katika uislamu ni haramu kwa mwanamke au mwanamume kumpa mwenzake mikono, na wakati walipokuwa wakimpa mke wake mikono walikuwa katika walipokuwa wakimpa mke wake mikono walikuwa katika hali ya uchangamfu na kitabasamu, na mmoja wao akampenda na akafikilia kumuoa akafanikiwa kumpata wakatafuta sehemu iliyojificha na akaanza kumdanganya kwa maneno ya kishetani.

Akamwambia:   Wewe na uzuri wako huu pamoja na mapambo haya unakuwa mke wa mwanamume huyu?

Hii ni dhuluma katika haki yako. Wewe unathamani zaidi, na mimi niko tayari kukuoa kwa sharti mume wako akupe talaka

-         Na kwa maneno haya yenye sumu mwanamke akandanganyika na kuafikiana naye akaombe apewe talaka na mume wake ili aolewe na mwanamume huyo baadaye.

-         Na haya yote yametendeka mume wake hajui kinachoendelea.

-         Na siku za ziara zilipoisha wakarudi na mume wake nyumbani, basi baada ya muda tabia ya mke wake ikaanza kubadilika, kabla ya hapo alikuwa akitabasamu na kumfariji mume wake, lakini sasa mambo yamegeuka kabisa, akamuuliza ni sababu gani iliyobadilisha tabia kuwa mbaya?

-         Akamjibu: Ni kwa sababu wewe umenidanganya.

-         Basi akamjibu kwa mshangao mkubwa!! Mimi? Ni vipi nimekudanganya?

-         Akajibu: Wewe haustahiki kwangu? Mimi ni mbora zaidi yako, na kuna ambaye anastahiki kunioa, na sasa hivi nataka talaka!!

-         Mwanamume akarukwa na akili kutokana na jambo hili na akakumbana na milipuko huu mkali; ambao amejiandalia yeye mwenyewe kwa nafsi yake, siku ambayo ameongozana na mke wake akiwa hajavaa hijabu mpaka katika nchi ya watu, akajaribu kumshawishi aache msimamo wake, lakini hakufaulu na mwisho akampa talaka kwa hasira na machukizo, na mwanamke akasafiri kwenda katika nchi aliyoko yule mwanamume, akiwa na ushahidi wa kupewa talaka ili akaolewe na yule waliyeafikiana naye.

-         Je! Ameishi na mume wapili?

-         Ni wazi kuwa ndoa za aina hii hazidumu ila chache, kwa sababu mwanamume hajamuoa ili waishi maisha ya ndoa, bali alimuoa ili amalize matamanio yake ya kijinsia basi.

-         Na alipomaliza haja yake na kushibisha matamanio yake ya kinyuma, akampa talaka ili arudi nyumbani kwao, akiwa amehadaika na mwenye huzuni, amesha mkosa mume wa kwanza ambaye alikuwa anaishi naye kwa kila aina ya mapenzi na mahaba.

-         Fikiria ewe msomaji hili ni tukio moja tu, kati ya matukio maelfu na maelfu ya kufanya hiyana katika ndoa, na tafuta sababu ili ikudhihirikie: Kuwa sababu yake ni kutovaa hijabu na kujionyesha, lau mwanamke huyo angekuwa amevaa hijabu, mwenye kusitiri uzuri na mapambo, je! Yangetokea mawindo haya?

-         Na je! Mwanamume yangempata  mabaya haya aliyoyaendelea mwenyewe?

-         Hakika malipo haya ni kwa mwenye kukhalifu kanuni za Kiislamu na hukumu za Qur’ani

JUKUMU LA SINEMA KATIKA KUTOVAA HIJABU NA UPOTOFU

Sinema zinafanya kazi kubwa zenye kuonekana katika  kuharibu jamii na kupoteza vijana katika njia ya haki na tukufu, na hiyo ni kwa kutumia filamu za kujamiana ambazo ni za uchi kabisa, na ndio ambazo zinaathiri matamanio ya wavulana na wasichana, zinawafanya wasiwe na aibu na imani na kuwaelekeza kufanya maovu, kujionyesha na kutovaa hijabu.

Na sinema hizi zinategemea sana wanawake ambao hawavai hijabu na kazi yao ni kwa uchio wa mnyama katika filamu, na maigizo yao, na mara nyingi hali ya kuwa uchi wa mnyama inazidi kwa kutumia wanawake wasiovaa hijabu ili wakajionyeshe mbele ya watazama na kuwazidishiwa matamanio na kufanya uchafu.

-         Hakika Mwenyezi Mungu(s.w.t) anajua idadi ya maovu na matukio ambayo yanatendeka na yanaendelea na malipo ya watu kuangalia filamu hizi, basi siku moja kijana mmoja aliangalia filamu ya kujamiana ikiwa uchi wa mnyama ikamuathiri, baada ya kumalizika filamu hiyo, kijana huyo alienda moja kwa moja nyumbani na kumwendea dada yake mdogo aliyekuwa amelala, jinsi alivyoona katika akamfanyia katika akamfanyia mshituko na mwisho ni kifo.

-         Hakika sinema hizi ni sehemu za usaliti ambazo zinawavulia wasichana wetu hijabu, na kuwaelekeza katika udhalili na uchafu, nayo pia ni sehemu za kuharibu vijana wetu na zinawabadilisha kuwa ni watumwa wa jamaa na kufuata matamanio, inawafanya wasifikirie maendeleo,ujuzi na kufikiria bali viwanda, elimu itakuwa ni ya  wasaliti peke yao. Na tunabakia sisi Waislamu wanyonge, tunawahitaji wao kwa kila dogo na kubwa, na wao wanakuwa ni viongozi kwetu, wameshatuonyesha mapanga yao na kutufanya si chochote kwao, wanatutumia wanavyotaka.

-         Na naona ni dharura kumuelezea kila Mwislamu ambaye anajihisi kuwa anajukumu la dini kupiga vita filamu hizi za uchi na kuwakata watu na kuwahadhari nazo, hakika zinatumika maslahi ya maadui na zinaharibu watoto wa Kiislamu kwa jina la ujuzi, elimu na uigizaji.

MADHARA YA KUCHANGANYIKANA

Kuchanganyikana maana yake ni:

Kukaa pamoja wanaume na wanawake bila ya kizuizi chochote,  na hii ndio hali ilivyo na katika sheria ya Kiislamu haijuzu na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ana chukizwa na hali hii.

-         Kwa nini?

Kwanza:  Ni kwa sababu ya kupinga kanuni ya hijabu ya Kiislamu, na kukaribisha ufisadi na mabaya yake.

Pili:    Inakuwa ndio ni mwanzo wa uhusiano wa kijinsia (mapenzi) yasioruhusiwa.

Tatu: Mara nyingi husababisha kubomoka kwa familia na kutoelewana.

Nne: Inasababisha majuto, na ufisadi kwa pande mbili.

Kwa hiyo mchanganyiko ni mtenganishi anaye kuwa katika jamii na anaingia ndani mpaka ahakikishe amevunja misingi yake.

-         Mchanganyiko ni maraadhi hatari ambayo yanahatarisha usalama na nidhamu ya familia, nayo ni kama maradhi ya saratani (kansa) na ni kama mdudu wa ziada ambaye hana usalama ila kuondolewa bila kubakizwa na kuondolewa kwake ni kuanzia kwenye mizizi yake.

-         Kwa hiyo leo hii  katika nchi ambazo kunapatikana mchanganyiko, ubakaji umezidi na ufisadi umekithiri kwa hali ya kuogopesha, na takarimu za ubakaji zinazidi kwa hali ya kuwa nusu uchi, na hasa katika vyuo (college) za mchanganyiko, imekuwa ni kwa kiwango cha juu, nayo ni kwa sababu kumekosekana ule utu wa asili, badala ya chuo kuwa ni sehemu ya utamaduni n aelimu, kwa leo imekuwa ni sehemu ya ufisadi na ya kuchukiza, ni kwa  sababu ya mchanganyiko usiokuwa na kizuizi ndani yake. Kama ilivyokuja katika ripoti ya kadhi mmoja wa Kiamerika ambaye ni “ Landisiy” kuwa asilimia 40% ya wasichana wa shule za mchanganyiko wanakuwa hawana bikira kabla ya kumaliza shule, na asilimia hii inazidi sana katika viwango vingine vya kujitunza. Kama ifuatayo:

-         Katika Uingereza uchunguzi uliofanyika katika mabegi (mifuko) ya wasichana wa shule ulionyesha asilimia 80% wana dawa za kuzuia mimba, hii inaonyesha kwamba wao wenyewe wako tayari kufanya mapenzi wakati wowote, na wao wanatumia dawa hizi ili kukimbia taabu nzito (ngumu)[1]

-         Baada ya kusoma uchunguzi huu mchache itafahamika hekima kubwa ya kuharamishwa mchangnyiko hakika Uislamu unataka tukuepushe jamii kutokana na ufisadi, na mabaya ambayo yanatokana na kutovaa hijabu.

Mpaka hapa… Hakika Uislamu unaharamisha mchanganyiko katika nyanja zote:

Katika shule, vyuoni sherehe na katika mikusanyiko ya pamoja… na hiyo sio kwa chochote ila kuzuia na kuhifadhi familia jamii

-         Lakini tunayo  ya shuhudia katika musimu wa hija, sehemu tukufu na  huseyiniyaati (sehemu ya kufanyia majilisi ya Huseini) kunapatikana mikusanyiko ya wanaume na wanawake katika sehemu moja, hiyo sio mkusanyiko ulio haramu, wala hakuna tatizo kwa sababu wanawake wamevaa hijabu, na hakupatikani ufisadi wa kutovaa hijabu.

-         Kuna baadhi ya nyakati tunasoma katika baadhi ya magazeti kuwa baadhi ya watu waliodanganyika na udanganyifu mkubwa wa watu wanatoa maoni yao binafsi katika baadhi ya kunieneza Kiislamu na katika mas’ala ya kisheria, na kuziweka katika mwangaza wa fikira zao za kibinafsi na katika viwango vyao maalum.

-         Kwa kifupi kanuni za Kiislamu ambazo ndio wanatimiza malengo yao na kauli zao, ni kanuni ya hijabu, kwa mfano utaona katika mwanzo wa gazeti kuwa: Mimi siko pamoja na hijabu kwa maoni yangu hijabu sio lazima! Na kuwa nusu uchi ni maendeleo! Sioni kizuizi cha kuchanganyikana!!  Na mengine mengi yasiokuwa na umuhimu.

-         Ni wajibu kumweleza huyu na wengine kama yeye.

-         Na wewe ni nani?

-         Wewe ni nani mpaka unaanza kutoa maoni yako katika desturi za mbinguni?

-         Na una thamani gani mbele ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na kanuni ya Kiislamu?!!

-         Je!  Kiislamu ni dini ya fikira nadharia mpaka kusema: Kwa maoni yangu ni hivi, na kwa maoni yangu ni hivi?

-         Kisha mimi namuuliza huyu msemaji!

-         Je! Wewe ni Mwislamu?!

-         Na kama kweli wewe ni Mwislamu, basi ni wajibu kwako unyenyekee amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake na kushikamana na hukumu za Kiislamu na kanuni zake ambazo miongoni mwa hizo ambazo ni muhimu ni kanuni ya “hijabu”, na kama wewe sio Mwislamu basi haistahiki kwako kuingilia mambo ya Uislamu na wala huwezi kuwajibisha maoni yako yenye kuadimika kwa Waislamu.

Na hapa uoga unanishika kutokana na majaribio haya kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na aitakuwa na uwezo, dhaifu mpaka kufikia kuingilia hukumu za Mwenyezi Mungu na kanuni za mbinguni kana kwamba hajui kauli ya Mwenyezi Mungu?!

((Na wasio hukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri)), (Madhalimu…..) ((Maasi…..)[2]

-         Hakika masuulia yao mbele ya Mwenyezi Mungu atawahesabia hesabu nzito… watalipa kodi (tax) maradufu kwa ajili ya kauli hizi za uongo na kupata adhabu kwa sababu wao wanatilia mkazo kutovaa hijabu na ufisadi na ubakaji.

-         Na hakika mimi naamini kuwa wao hawasemi hivi kwa nafsi zao, bali wao ni nyenzo za maadui ambazo zinapiga vita Uislamu  nyuma ya pazia, ili kuwavunja Waislamu kimoyo na kuwaharibu vijana na wasichana wao.

-         Na ambacho kinahitaji kutupiwa hicho tu!!

-         Kuwa kauli hizi zinarudiwa kila baada ya wakati katika magazeti na majarida na hasa ya Kiarabu, na sio kingine ila ni vikao vinavyofanywa na majaribio yenye makusudio, lengo la kuharibu jamiii yetu ya Kiislamu iliyosafi. Na kilicho muhimu kwa Waislamu waliohadaika, wazuie magazeti ambayo yamekuwa sila za maadui za kuwapiga Waislamu na Uislamu.

-         Kuathiri … kisha kuwa nusu uchi…. Na mwisho Ubakaji…. Utoaji mimba… Umalaya…. Kwa kumalizia kabisa ni kujiua.!

-         Na huu ndio ukweli uliopatikana katika nchi ambazo  zinajiita zimeendelea na wakati huo huo zinataka mwanamke atoke bila ya hijabu.

-         Ama nchi zetu za Kiislamu zimehatarishwa na hatari hizi ziko mbele yake huko… Magharibi na mashariki.

-         Kwa kweli wameonyesha ufisadi kwetu kwa jina la : (( fani) – ujuzi na ((elimu)).

-         Ama kuhusu ubakaji – katika nchi za Kiislamu siku hizi ni mchache sana ukilinganisha na ubakaji wa nchi zilizoendelea! Na sababu inaregea katika Uislamu mtukufu ambao unatatua matatizo kwa tabia njema, fadhila na kutupilia mbali ufisadi na uchafu.

-         Lakini bado ipo hatari….. na shari mbele ya nchi hizi….

-         Na sasa hivi tunaashiria baadhi ya mambo yanayo tendeka katika nchi ambazo hazitaki suala la hijabu.

1.     Takiribani filamu kumi za nchi kwa kila wiki zinachapishwa Uingereza, na zilizo nyingi wanazipeleka nje…. Takiribani filamu miatano (500) kila mwaka[3]

-         Hakika wajibu wa kisheria unawajibisha kila Mwislamu aelekee katika majaribio haya mabaya kwa kila nguvu iwe za kimali, nafsi,mpaka uadui usihakikishe lengo lake katika nchi za Kiislamu zenye nguvu, na mpaka nchi zetu zisigeuke kuwa ni ((Mapori ya wanyama)) kama zilivyo nchi za kimagharibi ambako imefikia mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke barabarani, ni kama wanavyofanya wanyama hivyo hivyo bila ya kuhisi chochote, hakuna aibu, utu, utukufu na ukarimu.

MADAI YA UOVU YAMEPATA NINI?

-         Na sasa hebu tuone:

-         Madai ya uovu yamepata nini?

-         Madai haya yamepata nini? Kuhusu uhuru wa mwanamke?

-         Ili kupata jibu la swali hili ni lazima kwanza tuangalie nchi za kimagharibi na jamii zake, na kuyapekua magazeti, majarida ambayo yanatoka huko,ilikufahamu hali ya dini anayoishi mwanamke asiyevaa hijabu huko, kwa sababu mas’ala hayaishi kutovaa hijabu tu! Bali imefikia kuacha uso wazi, miguu wazi kuathiri kifua wazi na kuvaa nguo za kubana

2.     Katika New York kuna mijumuiko ambayo inachanganyikana jinsia tofauti, na inafikia idadi yao 15 milioni wanaofanya mapenzi kinyume na jinsia.

3.     Katika 1961, polisi wa Uingereza walijaribu kumaliza umalaya na uchafu wa wanawake elfu mia moja (100,000) na mwisho polisi walitangaza kushindwa kumaliza jambo hili moja tu…..

4.     ((Na katika Roma (Italia) kuna madanguro mia tano (500) ya malaya, maelfu ya wanawake malaya wanaenda katika madanguro hayo wenyewe na kuwa pokea wanaume….))

-         Na hii ni chache sana yako mengi zaidi…

EWE DADA MWISLAMU

-Ni juu yako sasa ujifunze baadhi ya mambo ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu amekutaka ujifunze, ili ujiandae katika dunia na akhera…. Nayo ni mafunzo mazuri yanayokufanya uwe katika kiwango cha juu cha fadhila, Imani, Ukarimu, Utukufu, kuwa katika kheri na kufaulu…. Kwa sharti uyafuate haya na kushikamana nayo katika maisha!

1.     Hijabu kabla ya kila kitu kwa sababu ni hirizi ya amani ambayo inakulinda kutokana na ufisadi na wafisadi[4][5][6]  nalina kuhifadhi kutokana na ubaya na wabaya, nayo ni ngome inayokulinda kutokana na ubaya na wabaya.

-         Hakika hijabu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwako, basi mtii Mola wako, na utulekeze amri yake, na hiyo ni kwa sababu ya masilahi yako na kwa ajili ya kukuhifadhi.

-         Hakika muumba wako ni mpole kwako na hataki isipokuwa kukutakia wema na ameshasema (s.w.t.):

(( Wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahilia (ujinga), (ukafiri)

((Na waangushe shungi azo mpaka vifuani mwao, na wasionyesha mapambo yao)) Basi shauri yako ukikhalifu amri ya Mwenyezi Mungu utaangamia.

-         Hakika thamani ya mwanamke, katika mwili wake, aibu yake, na hakika hijabu ndio ufunguo wa dhahabu kwa hayo, basi ni juu yako ushikamane nayo.

-         Hakika kutovaa hijabu ni kujidhalilisha, basi hakuna budi kujiepusha, hakika  hijabu ni uzuri wa umbo na ni kinga kwako.

-         Hakika Mwenyezi Mungu anakurudia kuingia peponi kupitia hijabu, na shauri yako ukikhalifu njia hii itakuwa katika hasara kutopata radhi ya Mwenyezi Mungu na pepo yake.

-         Na hakika njia ya kuingia motoni na kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya kutovaa hijabu  basi shauri yako uifuate utaangukia ndani yake.

-         Hakika mwanamke ni mrehemu na wala sio kijakazi.

-         Kama alivyosema Amirul  Mumini Ali (AS) -     Basi ni wajibu kwako kufahamu uwezo wako wala usiwe mrahisi kuonyesha mwili wako na mapambo yako isipokuwa kwa mume wako tu.  Na amesema Mtume (s.a.w.) katika hadithakimsifu mwanamke mwema:  (( Mwenye kujionyesha kwa mume  wake, na amejihifadhi na wengine, nani ambaye asikia kauli ya mume anapomtaka kitu anakuwa tayari kumpa mume wake kitu anachotaka kwake.

-         Ni wajibu kwako kujisitiri kwa wanaume ajinabia, kwa hijabu ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ameifaradhisha kwako kwa kujali hali yako na utu wako.

-         Usionyeshe mapambo yako kwa wanaume, na wala usiwe kama bidhaa inayopelekwa sokoni na madukani.

2.      Usitumie powder, vitu vya kujirembesha, pafiumu (manukato) isipokuwa ukiwa nyumbani, kwa mume wako na jamaa (ndugu) zako …. Na kwa  tahadhari, tahadhari usitumie vitu hivi wakati wakutoka nje kwa sababu itasababisha hatari, uadui na itasababisha Mwenyezi Mungu kukukasirikia na kukulaani.

-         Amesema Mtume (s.a.w.):  Mwanamke yeyote anayetumia manukato kisha akatoka nje ya nyumba yake[7] basi atalaaniwa mpaka arejee nyumbani, hata kama atarejea saa ngapi?

-         Hakika mwanamke mwenye kizuizi anaepukana na kila kinacho washawishi wanaume kwake, kinyume ni kuwa mwanamke asiyekuwa na kizuizi, mwenye kujionyesha, basi hiyo itampeleka kufanya  yanayo washawishi wanaume kwake.

-         Miongoni mwa hizo ni kuvaa viatu vyenye visigino virefu ambavyo vinasababisha harakati zisizo za kawaida njiani kama vile sauti za farasi wennye kukimbia!

-         Hakika viatu hivi haviwezi vikaleta heshima na utulivu, bali vinathibitisha wanaume na kutoa tangazo kuwa huku kuna mwanamke na kwa ajili hii binadamu anayaona mengi- wakati anapokuwa njiani na kusikia sauti ya viatu na minenguo ya mwanamke anayetembea, na kama ni muovu, basi atarudi na kumwangalia, Je! Hii italeta heshima na kizuizi?

-         Kwa kuongeza kuwa viatu hivi ni vya upotofu vimekuja kutoka nchi chafu za kikafiri na kuletwa katika nchi safi za Kiislamu, basi kwa tahadhari usiwe nyezo ya uhalifu, kwa kujua au bila ya kujua![8] 

  3. Usijifahamishe na wanaume, katika mavazi n.k…… bali kuwa na msimamo katika maisha yako ya uke.

-         Amesema Mtume (s.a.w.), Mwenyezi Mungu amewalaani wale wanao jifananisha na wanawake

4.Usiwasalimie wanaume ajinabia kwa kuwapa mkono hata kama ni katika jamaa zako wa karibu kama vile, mtoto wa ami yako na mtoto wa mjomba wako…., kama mwanaume ajinabia akinyoosha mkono kwako ili akusalimie, basi jihadhari naye kwa kauli na kusema : Dini yangu na Mola wangu ananikataza kwa hili na wala usimchukulie yeye ni muhimu akikukasirikia, kwa sababu ridhaa ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko ya watu, na hakika kuwa na tahadhari ya kutokasirikiwa na Mwenyezi Mungu na kutofanya maasi yake ni bora kuliko kukasirikiwa na watu.

-         Katika hadithi: (( Mwenyezi Mungu alimpa wahayi Nabii Issa (AS) Ewe! Issa hakika mimi kama nitakukasirikia haitakufaa ridhaa ya mtu yeyote kwako, na kama nitakuridhia hatokudhuru yeyote miongoni mwa wakasirikao))[9] [10]

 

5.Usione aibu kuvaa hijabu, bali shikamana nalo kila wakati na uwe na msimamo, hata kama ukiwa katika familia isiojali, au shule au jamii ambayo watu wengi hawavaai hijabu, na kuwa na msimamo katika dini yako na kuwa thabiti msimamo wako, kama dini yako na kuwa thabiti katika msimamo wako, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):  Basi (Ewe Mtume) endelea na uongofu kama ulivyoamrishwa.

 Na amesema (s.w.t.) wale waliosema “ Mola wetu ni Mwenyezi Mungu, kisha wakaenda mwendo mzuri, hao huwateremkia Malaika msiogope wala msihuzunike na furahini na pepo mliyokuwa mkiahidiwa

-         Na wala usiwazingatie wale wanao kufanyia kejeli, - Ikiwa ni wanaume au wanawake – bali ni wajibu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) :  Kama nyingi mnatucheka nasi tutakuchekeni kama mnavyotucheka

-         Hakika tabia ya wahalifu ilikuwa na itaendelea kuwa ni kejeli kwa wenye Imani na fadhila, na hiyo ni kwa sababu hawana utu wala hawana tamko, dalili kwa upotovu wao na ukhalifu wao, kwa hili wanaelekea kushindwa kwa kusingizia, na wakati wao ndio wana ufasiki na uasi.

-         Kwa njia hii hii ya kushindwa walikuwa wakiwafanyia manabii, watu wema na waumini….. muda wote wa tarekhe

-         Amesema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) : Na hakuwafikia Mtume yeyote ila walimfanyia Istihizai

-         Hakika mjinga (kichaa) anajiona kuwa ni mwenye akili timamu na watu wengine ni vichaa, na mwenye kujidhalilisha anajiona anamaendeleo na wengine hawana maendeleo ni ((washamba)) na aliyefanyiwa mazingaumbwe anaona ukweli wa vitu kinyume chake …… kwa kweli mambo yako tofauti kabisa mia kwa mia (100%)[11] [12]  [13]

-         Kisha Mwenyezi Mungu amesema : Basi leo walioamini watawacheka waliokufuru, watakuwa juu ya viti vya fakhari wakitazama neema zao.

-         Hakika itakuja siku Mwenyezi Mungu na waumini watawafanyia kejeli hao wahalifu wenye kufanya kejeli.

-         Amesema Mwenyezi Mungu (s.w.t.): Mwenyezi Mungu atawalipa mzaha wao nao watapata adhabu iumizayo.

-         Lakini yakawazunguka wale waliofanya mzaha miongoni mwao yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

-         Moto utabambua nyuso zao nao watakuwa humo wenyekukennya meno yao kwa adhabu.

-         Hakika wameshakubali hao wenye kufanya kejeli kuwa walikuwa – katika dunia ni wabaya, wamepotea na ni wahalifu wenye kupotea.

-         Wajibu wa Mwenyezi Mungu limekuja kama kimbuga

-         Atasema Mwenyezi Mungu lizikeni humo, wala msinisemeshe (msiseme nami)

-         Lakini ni nyinyi mliwafanyia istihizai hatawaka kusahaulisheni kuni kumbuka na mlikuwa mkiwacheka.

-         Sasa ni juu yako ujifakharishe kwa hijabu, kwa sababu unamtii Mwenyezi Mungu(s.w.t.) katika kanuni hii tukufu, nawe unapata malipo na thawabu – katika hali ya kuwa umevaa hijabu katika kila hatua ambayo unatembea.

-         Na wakati huo huo mwanamke asiye vaa hijabu anapata dhambi na kuasi amri ya Mungu (s.w.t) katika kila hatua anayotembea naye akiwa hajavaa hijabu.

6.Uaminifu pekee yake hautoshi: Wapo wenye kusema mimi najiamini na anajihakikishia kuwa hawezi kufikwa na uhalifu na kutumbukia katika ufisadi, je! Ni wajibu wangu hijabu?              

Jibu:

Kwanza: Ndio ….. kwa sababu hijabu ni wajibu kwako kisheria katika kila hali, ikiwa ulikuwa unajia nini au hapana.

Pili: Hakika uaminifu peke yake hautoshelezi kwa sababu (( Kwa hakika kila nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu ameirehemu. Kwani  ni  wangapi miongoni mwa wasichana waliokuwa wanajiamini nafsi zao kisha wakaangukia kwenye ufisadi kwa sababu ya kutovaa hijabu!

Tatu: hakika kutovaa kwako hijabu kunasababisha kuamsha matamanio ya kimapenzi kwa vile anaye kuona, na inaweza kukupelekea kwenye ufisadi na mambo ya kuchukiza, Je! Hivi inajuza?

Nne: Hakika kutovaa kwako hijabu kunasababisha watu waanze kukuwinda, kukutega, na huenda ukasababisha uadui kwako- hakuna msamaha wa Mwenyezi Mungu,  Je:  uaminifu wako kwa nafsi yako unazuia chochote usidhurike??

7.     Uusijidanganyike na mambo ya kuiga ewe! Dada wa Kiislamu, hakika maadui wa Uislamu na maadui wa mwanamke wanapinga hijabu kwa njia nyingi, miongoni mwa hizo ni kuiga tabia mbaya na matamshi yasiokuwa na maana, ni juu yako uwe mwangalifu na mazungumzo yao, usidanganyike na matamshi yasiokuwa na maana yeyote ndani yake wala usidanyike na mitindo isiyofaa…. Na usijaribu kubugia sumu iliyochanganywa na asali na usiuze nafsi yako, dini yako na ukarimu wako kwa maadui wa Mwenyezi Mungu, kuwa Mwislamu kwa kauli na vitendo… na kuwa mbali na uchi za kimagharibi na ufisadi wake na uchafu wake.

-         Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na matangazo, maadui ambao lengo lao ni kuchafua jamii ya Kiislamu, hakika maendeleo  yapo kwenye hijabu, uhuru, maendeleo yote haya yanapatikana katika Uislamu na kanuni zake, na moja wapo ni hijabu.

-         Na  ujue kuwa:  uchafu, fedheha na ubaya hivi vinapatikana katika kanuni  ambazo zinapinga Uislamu miongoni mwa hizo ni kutovaa hijabu.

8.     Kuwa ni mwenye kulingania hijabu, elezea falsafa yake na hekima yake, kwa jamaa zako, rafiki zako….. shuleni, chuoni, ofisini, na katika njanja zote za maisha yako, kwa sababu kazi ya tablighi ya dini sio hasa kwa mwanaume bila ya mwanamke, bali kazi hii ni ya wote, kama ilivyokuja kwenye hadithi (( Nyote ni wachungaji, na mmoja ni masuula kwa watu wake)), na imekuja katika tarekhe :  Kuwa mtukufu Fatima Zahrah (AS), alikuwa akielezea baadhi ya mas’ala ya kisheria kwa wanawake katika Madinat – Munawarah na Sayidat. Zainabu binti wa  Amirul Muuminini (AS), alikuwa anafundisha wanawake tafsiri ya Qur’an katika mji wa Kufa.

-         Na ujue kuwa ukiweza kumshawishi msichana mmoja akakubali kushikamana na hijabu na akafuata haki kwa sababu yako basi Mwenyezi Mungu atakupa thawabu nyingi soma kwa kila msichana atakaye kubali kuongoka kwa sababu yako.

-         Na imekuja katika hadithi : Kuwa Mwenyezi Mungu amempa wahayi Nabii Musa(AS)… Ukimrudishia muovu kwenye mlango wangu au mpotevu ukamrudisha kwenye uongofu wangu ni bora kuliko ibada ya miaka mia moja, kufunga mchana na usiku kufanya ibada.

-         (*)   Mwenyezi Mungu akasema: Ni muovu aliyebobea         

-         Mwanamke asiye vaa hijabu anamuasi Mwenyezi Mungu, naye akiwa ni mwenye kutojali kanuni ya mbinguni; na kama atarudi katika kanuni ya Mwenyezi Mungu kwa juhudi zako na kushikamana na dini, na hijabu basi atakuwa na ujira mkubwa kwa Mwenyezi Mungu.

-         Na nini bora zaidi kuliko malipo na thawabu?!!  Kwa hiyo ni juu yako uwe mlinganifu katika dini, na hasa hijabu baina yako na wasichana na wanawake.

9.     Usikatae kuolewa wakati mtu anapotaka kukuoa, na uangalie mambo mawili ya msingi: dini na ana tabia na kama mume anafuata dini na ana tabia njema wala usisitesite kuolewa naye kwa sababu dinin na tabia njema ni ufunguo wa maisha mema,  kwa hiyo ni juu yako uulize vitu hivi na uvitafute, na wala usiulize utaifa wake, setifiketi yake, mshahara wake na mahari ambayo[14] atakupa, na wala usilete udhuru wa kujisingizia kuwa unakamilisha masomo, ili upate cheti cha kumaliza masomo n.k. na sababu zingine na maana na zinakusababishia mabaya na Mwenyezi Mungu hayaridhii kabisa.

(( Amesema Mtume (s.a.w.): Kama akiwajieni mtu mnaye mridhia tabia yake, dini yake muozesheni…. Na kutofanya hivyo kunaleta fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.

-         Hakika kuoa ni kiota cha dhahabu kwa ajili yake mmejistarehesha na kujifururahisha, nayo ni kinga  ya ufisadi nani ngome ya kujikinga na upotofu wa tabia, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakumuumba mwanamke aishi maisha ya upweke bali amemuumba aishi na mwanaume pamoja ili wapate familia na kuwa na jamii na kizazi kiendelee mpaka  awe mama wa kizazi kipya.

-         Mtume (s.a.w.) amesema : Enyi watu hakika Jibrail amenijia kwa Mwenyezi Mungu amesema: hakika wenye bikira, daraja yao ni kama matunda yaliyomo mtini na akiwahi matunda yake, basi hayachumwi na jua na upepo huwezi kuyaharibu, kwa hiyo wenye bikira wakiwali kama walivyo walii wanawake, basi hakuna dawa kwao ila kuolewa la sivyo hawawezi kuepukana na ufisadi kwa sababu wao ni viumbe.[15] [16]

-         Kisha akasimama mwanaume na kusema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tutawaozesha akina nani?

Mtume akasema : AL- Akifa’a

Mwanaume akasema : Ni waumini baadhi yao kwa wao ni al – akifa’a, Ikiwa posa iliyo tumwa kwako iliolewe kama mtu  huyo hafuati dini na tabia yake ni mbaya kwa mfano:  hesali, anakunywa pombe, na n.k, basi usikubali posa yake bila ya kusita sita, na wala usidanganyike na vitu alivyo navyo. Kwa mfano mali, cheo, kwa sababu maisha ya upweke ni bora kuliko kuwa na mume mpotovu katika dini au mwenye tabia mbaya hata kama awe ana mali kiasi gani na cheo cha juu.

- Ni juu yako kumuomba Mwenyezi Mungu iliakuwezeshe uolewe na kijana Mtukufu, Muumini, Mzuri wa usoi, dini n atabia, na ameshasema Mwenyezi Mungu: Niombeni nitawajibu.[17][18]

 EWE MUME MTUKUFU

1.      Ewe mume mtukufu: Hakika majukumu yako kuoa ni hatari mbele ya Mwenyezi Mungu…. Wewe ni mwangalizi wa tabia ya mke wako na matumizi (mahitaji) yake …. Hakika Mwenyezi Mungu amekufanya kuwa ni mlinzi kwake (mke).

(Amesema (s.w.t.), ( wanaume ni walinzi wa wanawake kwa yale waliyotoa), na anasema (s.w.t.): Enyi mlioamini jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe)

Ili ufanye wajibu wa kisheria na majukumu ya kadiri kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni juu yako kufuata mambo na mafunzo ya Kiislamu yafuatayo:

1.     Kwanza hijabu:

Ni wajibu kumwamrisha mke wako avae hijabu; Ikiwa yeye havai – ni bora umwelezee dalili za kutosha ili akinaike na avae  hijabu kwa kukinaika, kufahamu na kuwa na maarifa ya kanuni hii ya [19]  [20] Kiislamu na ukishindwa kumkinaisha basi mpeleke kwa a’alimu (mjuzi) wa dini ili akaelezewe ni nini falsafa, inayozungumzia hijabu

-         Imamu Ali (AS) anasema : Katika wasia wake kwa mtoto wake Mohammed bin Hunafiya (RA): hakika shida ya hijabu ni kheri yako.

-         Kutoka kwao nje sio tatizo sana, tatizso ni kuingiza mtu kwao usiye mwamini na ukiweza wasiingie yeyote ila wewe  basi fanya hivyo: Yaani  usimtambulishe kwa wanaume kwake kwa sababu kuna ufisadi na fitina.

2.   KUJIHADHARI NA SHEREHE ZA MCHANGNYIKO

Usiende naye kwenye sherehe za mchanganyiko na mtahadharishe sana na kucheza muziki na kuimba, migizo na sinema kwa sababu vinaharibu tabia yake, atakuwa hana haya na kupoteza  utukufu wake na kuwa katika hatari.

Mwanaume ambaye anataka mke asivae hijabu aende kwenye sinema na katika sherehe za[21]kucheza dansi basi yeye ni wa kwanza kumuhini mke wake nani muovu wa kwanza kwenye haki ya mke wake kwa sababu ametaka awe katika ufisadi na akamuongoza katika upotovu, na akamwelekeza kwenye uchafu, na mume huyu atakuwa ni wa kwanza kulipa kodi ya aliyoyatenda, na ataona malipo ya kitendo chake, wakati anapo muhini mkewe na kumuhusisha na uhusiano wa wanaume, uhusiano usio ruhusiwa.

-         Basi ni wajibu kwako ewe mume mtukufu uwe mbali na sehemu zote chafu na za kuchukiza, na uache kutembelea sehemu hizi potovu, ili uishi katika ridhaa ya Mwenyezi Mungu kwa uaminifu wa nafsi na utulivu.

3.   USIMTII MKE WAKO KATIKA MAASI

-         Ni wajibu kwako na familia yako muishi katika mazingira ya kidini na hukumu zake, na ujihadhari na kila aina ya upotovu, na kwa sababu mwanamke ni mnyonge, mdhaifu huenda akakuomba kitu ambacho Mwenyezi Mungu hakiridhii, na hapa …. Ni wajibu umwelezee haya kulingana na sheria na wala sio maoni yake, na haijuzu kwako umtii katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa sababu (( hakuna kumtii kiumbe katika maasi ya muumba))

-         Na sasa hivi soma hadith hii! Mtume (s.a.w.) amesema: (( Mwenye kumtii mke wake, basi Mwenyezi Mungu atatupia uso wake motoni))

-         Imeulizwa ni upi huo utiifu?

-         Akasema anapokuomba kwenda harusini kuogelea idd, akiwa amevalia nguo nyepesi.

-         Kwa hiyo ….ni juu yako usiniruhusu kwenda kuogelea katika sehemu za mchanganyiko, harusi za mchanganyiko, maigizo na sinema, na usimruhusu kuvaa nguo nyepesi zenye kushawishi wanaume ajnabia, kwa sababu katika kila ufisadi huo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) haridhii hayo.

4.    UWE  NA WIVU KWA MKE WAKO

-         Ni wajibu kwako ewe mume mtukufu, uwe na wivu kwa mke wako na jamaa zako, imepokewa katika hadith tukufu kutoka kwa Imamu Sadiq (AS) ansema: Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ana wivu na anampenda kila Mwenye wivu)

Kwa ajili ya wivu wake ameharamisha uchafu uliodhahiri na usio dhahiri[22]  [23]

-         Na ajili hii ni wajibu kwako kumuhifadhi mkw wako, dada zako, waepukane na upotofu wa kutovaa hijabu huvuta shari kwako na kwake, na inasababisha Mwenyezi Mungu kukukasirikia wewe na yeye; ameshasema Imamu Sadiq (AS) wasio kuwa na wivu wameharamishiwa pepo, kwa sababu wasio kuwa na wivu na wake zao wanawaridhia kutovaa hijabu na kujionyesha na wala hawamrishi hijabu.

-         Na akasema (AS) : ( Watatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya kiama wala hatowatoharisha, na watapata adhabu kali!

1.     Mzee mzinifu

2.     Asiye kuwa na wivu

3.     Mwanamke ambaye anafanya zinaa katika kitanda cha mume.

-         Kwa sababu ya wivu, basi mke wako, jamaa zako,na familia yako wasitoke wakiwa wametumia manukato, powder, na vitu vya kujirembesha,  kwa sababu hii inasababisha kuanguka utukufu wako na wake[24] na utaanguka kijamii na yeye pia, mwisho wa hayo ni ubaya.

-         Mtume (s.a.w.) amesema: (Mtu yeyote ambaye mke wake anajirembesha na kutoka nje, basi yeye hana wivu… Mwanamke anapotoka kwenye nyumba yake akiwa ametumia manukato na mume wake ameridhia kwa hilo, basi mume wake atajengewa nyumba motoni kwa kila hatua atakayo tembea mke wake.

-         Na Mtume (s.a.w.) amesema :  Aina kumi katika umma wangu hawaingii Peponi mpaka watubu. Miongoni mwa hao ni : Asiyekuwa na wivu ikasemwa: ni nani asiyekuwa na wivu?

-         Mtume (s.a.w.) akasema: ambaye hana wivu na mke wake)

-         Hakika nimeshashuhudia mara nyingi nikiona wanume wanakula chakula na wake zao katika Hoteli, na nimesikia watu wakisema pia wakiwa na kila aina ya uhuru, wake zao hawana hijabu au hawaoni umuhimu wake zao kuvaa hijabu, kama alivyo kithiri udhahiri huu mbaya katika matembezi na katika mabustani ya starehe[25]   [26] kiongozi mmoja wa hoteli anieleze kuwa kuna baadhi ya watu hawataki kula katika sehemu ambazo zimetengwa kwa ajili ya watu hasa, bali wanataka kula katika  sehemu zilizotengwa kwa ajili ya watu wote.

Enyi Waislamu! Hapa wivu uko wapi?

5.   MFUNZE SURAT NURU

     Ni suna kwako ewe mume mtukufu kumfunza mke   wako surat nuru na tafsiri yake, kwa sababu ina baadhi  ya  aya  ambazo zinamuhusu mwanamke na zinamtaka ashikamane na maarifa yake, ili aishi katika maisha ya usafi yasiokuwa na machukizo

-         Mtume (s.a.w.) amesema: Wafunzeni (wanawake) surat Nuru kwa sababu ina mawaidha

6. USIMUWEKE VYUMBANI

-         Mtume (s.a.w.) ameshakataza kumuweka mwanamke vyumbani, akiwaelezea wanaume: msiwaweke wanawake vyumbani).

-         Na ikaulizwa: Ni nini maana vyumba?

-         Jibu:  Maana yake ni vyumba ambavyo vinaangaliana na njia, barabara au soko n.k.

Kwa hiyo kauli ya Mtume (s.a.w.): ((msiwaweke wanawake vyumbani)) maana yake ni kuwa enyi wanaume msiwaweke wake zenu katika vyumba ambavyo vinaangaliana njia ya kupita watu[27] [28]

-         Na vile imekuja katika hadith kuwa miongoni mwa hatua za amani ambazo imamu Mahadi (AS) ataelekea njiani.

-         Na watauliza hekima yake ni nini?

-         Jibu: kwa sababu madirisha ambayo yanaelekea

Barabarani kunauwezekano mkubwa sana wa kufanya hiyana katika ndoa, na ufisadi wa familia kwa sababu yataonekana yaliyomo chumbani na hasa katika nyumba za gorofa ndefu kwa kiasi kwamba inaonekana ndani kwa walio nje, iwe wanaopita au wanaoishi katika nyumba inayoangaliano.

-         Na ufisadi una kuwa kwa pande mbili:

Mwanamke anayechungulia njiani, na mwanaume anayepita atamwangalia na huenda atampenda moyoni mwake…. Na huu utakuwa ni mwanzo wa uovu  na mwanaume anaposima dirishani  kuangalia chumba kinachoangaliana na chumba chake kwa kwaida mwanamke hatakuwa amevaa hijabu kwa sababu yuko kwake.

Mtume (s.a.w.) amesema mtu akichungulia uchi wa mwanaume au nywele za mwanmke au sehemu yeyote katika mwili, basi itakuwa  ni haki kwa  Mwenyezi Mungu kmuingizqa motoni pamoja na wanawake duniani, wala hatatoka duniani.

-         Mpaka Mwenyezi Mungu awafadhilishe na akhera ataonyesha uchi wake kwa watu.

-         Hakika hekima inasema (( Kinga ni bora, kheri kuliko kuponya)) ni wazi  mara nyingi kuponya hakufaulu na kinga ni dhamana (mdhamini) kuaminika.

-         Na inasikitisha kwa kweli jamii kuishi katika kutojua mafunzo ya kujikinga ya Kiislamu utaona mwanamke anatoka nje akiwa amevalia nguo za ndani akianika nguo kwenye kamba au  anaghafilika kwa anayoyavutia katika nafsi yake; na familia yake kutokana na mabaya na majuto.

-         Basi ni juu yako ewe mume mtukufu uzingatie mafunzo haya mazuri ya Kiislamu na uyafuate katika maisha yako ya ndoa pamoja familia yako pia, ili uishi pamoja na familia yako karimu kuwa mbali na fedheha za dunia na majuto ya akhera.

MAFUNZO YA KIISLAMU

-         Kwa munasibu mazungumzo yetu kuhusu jamii na nyezo za amani na ufisadi wake nimeona ni bora nikukumbushe ewe ndugu Mwislamu kwa baadhi ya mafunzo ya kujikinga ya Kiislamu ambayo lengo lake ni kumuhifadhi binadamu kutokana na ufisadi na upotofu.[29]

1.     USIMWANGALIE MWANAMKE AJINABIA 

Inachukuliwa kwa kumuangalia mwanamke ajinabia ni njia katika njia za ufisadi na upotovu wa tabia, nayo ni ufunguo wa shari, nini mwanzo wa ufisadi, kwa sababu inavutia mtu kuangalia kwa mara ya pili, na ya tatu…. Na mwisho ni kufanya uchafu na machukizo.

-         Anasema mwanashairi

-         Kuangalia, kisha kutabasamu,kisha salamu, kisha maneno, kisha ahadi na mwisho ni kukamilisha haja.

-         Kwa ajili hii uislamu unazuie ufisadi kuanzia mwanzo kwa kukata mizizi yake, basi Mwenyezi Mungu ameharamisha kuangalia mwanamke ajinabia na amehadharisha kuangalia mwanmke ajinabia na  amehadharisha hilo sana na amewamrisha waumini:  ((Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao hili ni takaso kwao bila shaka Mwenyezi Mungu anazo bahari za yote wanayoyafanya.

-         Na hakika kawaida ya ubinadamu kuna mvutano baina ya jinsia mbili. Mwanaume na mwanamke, kwa sababu ya kila mmoja kumwangalia mwingine, ni wajibu kuiweka kawaida hii mipaka kulingana na sheria ya Kiislamu.[30]

-         Na kama sio hivyo basi natija ( matokeo) yatakuwa ni mabaya na mwisho mbaya.

-         Imamu Sadiq (AS) anasema: Kuangalia baada ya kuangalia kunapanda shahawa katika moyo, na inatosha hiyo kwa mwenye kuangalia kuwa ni fitini).

-         Hakika mwangalio wa haramu ndio mwanzo wa uchafu, na kwa ajili hii imekuja katika hadithi: (( Kuangalia ni posta ya zinaa))  yaani mwanzo wa zinaa haiwezi ikawa ila baada ya mwanaume kumwangalia mwanamke na kustajaabishwa nayo, kana kwamba mwangalio wa haramu ni barua, mwito katika zinaa.

-         Basi mwanzo wa kila ubaya huu ni: Kuangalia mwanamke ajinabia.

-         Nabii Yahya bin Zakariya (AS) ameulizwa kuhusu mwanzo wa zinaa ni nini?

-         Basi akasema : ((Ni kuangalia na kuimba)).

-         Na hakuna ajabu kama ya kuja makatazo mahali ya kisheria kuhusu maudhuu haya, wala hakuna ajabu ikiwa katika akhera kutakuwa na adhabu kali.

-         Ima kuja katika hadithi tukufu: Mwenye kuangaza macho yake kwa mwanamke kwa haramu, Mwenyezi Mungu atawaunguza siku ya kiama kwa moto wa misumari, atawaunguza moto mpaka amalize kuhukumu watu, kisha atawaamuru waingie motoni.

-         Na imekuja katika hadithi nyingine: ((Mwenye kuangaza macho yake kwa haramu, Mwenyezi Mungu atajaza macho yake moto siku ya kiama, mpaka atubu.

 

Na miongoni mwa athari za kuangalia mwanamke ajinabia ni kupata adhabu ya kinafsi na kupata fikira nyingi

Hakika mtu ambaye hazui macho yake anaangalia kila anachotaka, atazidisha masikitiko na kuishi katika adhabu ya kinafsi na wasiwasi wa kifikira, huenda nafsi yake imeshikamana na aliyoyaangalia, basi yatashughulisha fikira zake hatapata usingizi na raha.

Na hadithi hii kwa sababu inazungumzia mambo yote kwa hiyo inajumuisha na kuangalia mwanamke ajinabia, bali ni ukweli unaojitokeza.

-         Imamu Sadiq (AS) anasema: (( Kuangalia ni mshale miongoni mwa mishale ya ibilisi yenye sumu na miangalio mingapi inayohuzunisha kwa muda mrefu .

-         Je! Umeona  mshaleunavyoingia katika mwili na kupasua mihipa?!  Huu ukiwa hauna sumu lakini ukiwa na sumu madhara yake ni makubwa zaidi na wakati mwingine husababisha kifo.

-         Vile vile kuangalia mwanamke ajinabia… ni mshale wenye sumu unapasua mwili mpaka kufika kwenye moyo wake huzuni ya muda mrefu!!!

Ndugu yangu mkarimu: ili Uwe ni mwingi wa ucha Mungu na kuwa mbali na mawindo ya shetani, hakika Uislamu unachukia kwako kuangalia nyuma ya wanawake.

Hakika unaona baadhi ya wahalifu wanaangalia mwanamke akiwa mbele hata akishampita anamgeukia kwa nyuma kumwangalia, kana kwamba wanazingatia mwenendo wake na mwili wake.

-         Abu Basiri amemuiliza Imamu Sadiq (AS):

Kwanini mwanamke anapopita, mwanaume humwangalia nyuma?

Akasema (AS): Je! Mnafurahishwa mtu kuangalia wake zenu na jamaa zenu?  Wakasema hapana.[31]

-         Akasema (AS) : basi ridhaa kwa watu wale wanaoridhia nafsi yako).

-         Na imekuja katika kisa cha Nabii Musa (AS), kwa kauli yake Mwenyezi Mungu kupitia kwa mmoja wa mabinti wa Nabii Shuaib (AS) (( Ewe baba yangu! Mkodi huyu awe anachunga wanyama wako badili yetu, bila shaka mbora uwezaye kumwajiri ni ambaye mwenye nguvu, mwaminifu.

-         Shuaib alimuuliza binti yake: Wewe umemjua Musa  kuwa ni mwenye nguvu kwa sababu alinyanyua jiwe, na kuwa yeye ni mwaminifu umemjulia wapi?

-         Binti yake akamjibu! Ewe baba, hakika mimi nilikuwa natembea mbele yake, basi (Musa) akaniambia nitembee nyuma yake,  na akasema kama akipotea njia, nimuonyeshe, halafu akasema : hakika sisi hatuangalii nyuma ya wanawake.

-         Nakatika kauli ya Mwenyezi Mungu: (( Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao))

-         Imamu Baqir (AS) amesema : Kijana wa Kiansari katika Madina aliangalia mwanamke – Kwa mbele, alipofanikiwa kumwangaalia, akafuata uchochoro na akawa anamwangalia akaona damu ikitiririka kifuani na nguoni mwake, akasema ni lazima nimwendee Mtume (s.a.w.) ilianieleze sababu, basi akamwendea na Mtume (s.a.w.) alipomuona akamwuliza nini hii?  Kijana akamwelezea yaliyompata, kisha Jibrail akateremka na aya hii (( Waambie Waislamu wainamishe macho yao…))

-         Imamu Sadiq (AS) amesema : hawasalimiki wale ambao wanaangalia nyuma ya wanawake, wake zao kuangaliwa pia.

-         Na katika hadithi nyingine : (( Jiepusheni na wake za watu, wake zenu watasalimika) na  hadithi ya tatu inasema (( Msizini kwani mkizini, wake zenu wataziniwa))

Na katika maudhui haya inasemekani kuwa kulikuwa na mtu ambaye kazi yake ilikuwa ni kupeleka maji kwa nyumba  ya muuza vito kwa muda wa miaka thelathini na wakati mwingine muuza vito alikuwa hashindi nyumbani, kwa hiyo mke wake ndio anamfungulia mlango mbeba maji ili aya hanishie katika viombo vingine, na kwa muda wote huwa miaka thelathini hapajatokea hiyana ya aina yeyote kwa mke muuza vito.

Siku moja mwanamke alipomfungulia mwenye maji mlango na hapo ndio akamshika  mwanamke mkono na kubusu…. Hapa mwanamke hakuwa na lingine ila kuvuta mkono kwa nguvu na kupiga kelele na kumfukuza ndani ya nyumba, kisha akaanza kufikiria – akiwa amestaajabu – kwa hiyana aliyofanyiwa na mbeba maji, baada ya kumwamini kwa muda wa miaka thelathini?!!

-         Na aliporudi mume wake akamuuliza  yaliyompata huko sokoni siku hiyo, akasema alinijia mwanamke kununua bangili na alipofunua mkono wake ili avae bangili nikaushika mkono wake na kuubusu!!  Basi mke wake akapiga kelele na kusema: Allahu akbar

-         Na yeye akamhadithia yaliyompata kwa mbeba maji.

-         Ndio … hakika kila mtu anapofanya mabaya kwa wake za wengine na mke wake, mama yake, dada yake na binti yake watafanyiwa hivyo hivyo.

-          Na katika hadithi Qudusi: (( Kama mnavyo fanya mtafanyiwa)), yaani utakayofanya kwa wengine nawe utafanyiwa, ikiwa ni kheri basi itakuwa ni kheri, na ikiwa ni shari basi itakuwa ni shari.

Ewe msomaji mtukufu:

Naregea katika hadithi ya  kuangalia mwanamke ajinabia… ninasema: hakika Uislamu ni dini ya upendo na hofu, ushujaa na tahadhari na kwa ajili  hii utaona Qur’an tukufu: Mwenyezi Mungu anapotajapepo na neema zake moja kwa moja hutaja moto na adhabu yake ili mtu kupenda neema na thawabu, kuogopa moto na adhabu yake na umeshasoma baadhi ya hadithi zilizo pokelewa kuhusu adhabu ya kuangalia mwanamke ajinabia athari zake na ubaya wake.

-         Na sasa hivi ni zamu ya hadith zinazozungumzia malipo mazuri ambayo yanatokana na hayo.

-         Mtume (s.a.w.) amesema:  Kuangalia mapambo ya wanawake ni mshale miongoni mwa mishale ya sheitani (Iblisi) na mwenye kuacha Mwenyezi Mungu atamuonjesha utamu wa ibada utakao mfurahisha.

-         Na Mtume (s.a.w.) amesema:  Kuangalia ni mshale wa sumu miongoni mwa mishale ya Iblisi, na Mwenye kuacha  kwa jili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atampa Imani itakayokuwa na utamu katika moyo wake)

-         Mtume (s.a.w.) amesema: Inamisheni macho yenu mtaona maajabu na Mwenyezi Mungu amesema: ((Waambie Waislamu wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao…)

-         Maajabu hayo ni yapi?

-         Hakuna shaka kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atampa mtu huyu kila baraka ambayo inastaajabisha, kwa sababu yeye haangalii mwanamke ajinabia.

-         Imamu Sadiq (AS) amesema:  ((Mtu akiangalia mwanamke, kisha akangalia juu au akafumba macho yake mpaka Mwenyezi Mungu atakapomuozesha hurul – aini))

-         Amesema (AS): Hakuna anayeweza kujiepusha kama anavyojiepusha kuangalia (kufumba macho), kwani kuamgalia hakufumbwi katika maharimu bali Mwenyezi Mungu atampata ushahidi mkubwa na utukufu.[32] [33]

-         Limebakia suali la mwisho nalo ni:

-         Ni vipi mtu anaweza kujiepusha na haramu hii pamoja na kuwaona elimu kuwa Kansa (saratani) ya kutovaa hijabu ni upungufu ulio wazi na kwa masikitiko zaidi – haya yako katika nchi za Kiislamu? ! Je! Itawezekanaje mtu kufumba macho ! ataonaje njia?

Jibu: Hakika umeshasoma baadhi ya aya na hadithi zilizotajwa – cha muhimu ni ((kufumba macho))  Utafumbaje? Ni kuangalia chini wakati wakutembea, basi mtu anapo muona mwanamke ajinabia ni juu yake kuangalia chini au kuangalia upande mwingine. Walahi Mwenyezi Mungu hapotezi malipo yake.

2.     USIMSALIMIE MWANAMKE AJINABIA KWA KUMPA MKONO

       Hakika Mwenyezi Mungu ameshakataza – ewe ngugu Mwislamu kumpa mkono mwanamke ajinabia.

       Mtume (s.a.w.) amesema :((Mtu akimpa mkono mwanamke ajinabia  ataharanishiwa, na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atamkasirikia.

        Na mwenye kumsikiliza mwanamke haramu kwake atafungwa na mnyonyoro wa moto pamoja na shtani, basi, watakuwa wakirukaruka motoni.[34]

3.   USIFANYE MZAHA NA MWANAMKE AJINABIA:

Hakika Uislamu umekataza mzaha na mwanamke ajinabia, kwa sababu mara nyingi husabisha ufisadi, chuki na athari za shahawa, mapenzi katika pande zote mbili:

-         Mtume (s.a.w.) amesema: (( Mtu akimfanyia mzaha mwanamke asiye halali kwake, Mwenyezi Mungu atamfanyia hesabu ya kila neno alilomsemesha katika dunia miaka elfu mija (yaani akhera)

4.    USICHELE KUOA

-         Ndugu yangu Mwislamu kuoa ni jambo la lazima ulifanye …….. basi mtu akifia umri wa kujiongoza, na akifikia  umri wa kubaleghe kisheria ni lazima kwake aoe…. Ili ahifadhi dini yake- kwanza – na kupata radhi ya Mwenyezi Mungu.

-         Pili:  anajihifadhi na mambo ya haramu na ufisadi, wa kijinsia.

-         Tatu: Hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu na kampa shahawa za kijinsia (mapenzi) amezifanya shahawa hizo kuwa ni zenye nguvu sana – zenye kudumu na kutoa kizazi…. Na kuoa ni kuzishibisha shahawa hizi kwa kufanya mapenzi kwa njia ya sheria tukufu.

-         Hakika kuchelewa kuoa kunamsababishia mtu moja ya mambo mawili:

1.     Kudhalilisha kijinsia na kukereka  kinafsi… kuvumilia taabu kwa ajili hiyo

2.     Kufanya ufisadi, haramu, punyeto, liwatu, na zinaa na ni wazi kuwa kila mambo wawili haya yanasababisha hatari kubwa ya kinafsi kwa mtu, utukufu wake na ukarimu wake.

-         Basi kujidhalilishana kukereka kunasababisha maradhi ya nafsi, ubnaya wa tabia na kujiadhibu kiroho, na kufanya haramu kunasababisha ubakaji na kukosekana utukufu na ukarimu…. Na mwisho mtu kuishia katika mahakama za wahalifu ….. baada ya hapo ni kwenda jela kuishi na waizi wa halifu.

-         Basi suluhisho ni nini?

-         Hakika kuoa  ndio ni suluhisho ambalo Uislamu unalitoa… na akili inaafikiana nalo, na hii ndio tiba peke yake kwa hilo.

-         Hakika kuoa kuna mkamilishia mtu wema wa kiroho,….. kustarehesha nafsi na tabia njema uupate uchangamfu na ladha (utamu) na wakati huo huo…. Kuoa kunamtosheleza mtu asifanye haramu, kujiepusha na ufisadi na inamhifadhi na chafu.

Hii … kwa kuongezea, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hajaumba mwanaadamu aishi maisha ya upweke bali amemuumba ili aishi na mke wake  muumini pembeni mwake ili wapate familia, kujenga jamii, na kulea watoto malezi mazuri.

-         Hakika upweke unamchukiza Mwenyezi Mungu (s.w.t.) … na hautakikani katika Uislamu… nani usumbufu kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

-         Mtume (s.a.w.) amesema: ((shari yenu ni upweke wenu))

-         ((Na udhalili wa mauti yenu ni upweke)).

-         Na imepokewa kutoka kwa Ghikaful – Hilaliy amesema :  (( Nilienda kwa Mtume (s.a.w.): akaniuliza: Ewe Ghikafu una mke?

-         Nikamjibu sina.

-         Akaniuliza una Jariya?  ((Yaani mtumwa wa kike))

-         Nikamjibu : hapana

-         Akauliza Je! Unauwezo wa kimali na wa kijinsia? (yaani nguvu za kiume))!

-         Nikasema : Ndio, al- hamdulilahi.

-         Akasema : Basi wewe ni ndugu miongoni mwa ndugu  za mashetani… ima uwe katika makasisi wa kinasarah au ufanye wanavyofanya Waislamu, na miongoni mwa suna zetu ni kuoa….

Mpaka akasema : Ole wako ewe Ghifaku oa…oa hakika wewe ni miongoni mwa wakosaji.

-         Nikamjibu : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) niozeshe kabla sijaondoka!!!

Basi, Mtume (s.a.w.), akamuozesha.

-         Na katika kutilia mkazo suala la kuoa…Mtume (s.a.w.) amesema: (( Hakuna jengo lilojengwa katika Uislamu lenye kumfurahisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kulitilia nguvu kama kuoa)).

Na amesema Mtume (s.a.w.) (( Hakuna kijana miongoni mwa vijana  ambaye anasa mwanzoni ujana wake ila atamuathiri, nakumkasirisha shetani, na Mtume atasema… ooh, huyu amejihifadhi nusu ya dini yake)) kisha akasema : (( Namuogopa Mungu katika nusu iliyobaki)) Yaani kuoa kunahifadhi nusu ya dini….. nami juu ya mtu kumuogopa Mungu katika nusu iliyobaki ….. na hii kama ikionyesha kitu basi inaonyesha umuhimu wa kuona athari yake  katika  tabia ya mtu na mienendo yake.

Na tunamalizia hadithi kuhusu kuoa- kwa hadithi ya Mtume (s.a.w.) ((Rakaa mbili anazo sali mwenye kuoa ni bora kuliko rakaa sabini anazo sali mwenye kuoa ni bora kuliko rakaa sabini anzo sali asiyeoa)).

ADHABU YA MWANAMKE ASIYEVAA HIJABU

-         Mwanamke asiyevaa hijabu adhabu yake ni nini akhera?

-         Hakika sisi tunajua kuwa Mwenyezi Mungu amewaahidi adhabu kali wale wanao Khalifu amri zake na wanafanya mambo ya haramu, wanaacha ya wajibu, basi na nini atakacho kipata  mwanamke asiyevaa hijabu akhera?

-         Ni adhabu gani ambayo Mwenyezi Mungu amemwandalia  mwanamke asiyevaa hijabu na kuchagua kutembea nusu uchi??

-         Jibu: Hakika kutovaa hijbu kunasababisha laana kwa mwanamke na kwa mbali na rehema na radhi ya Mwenyezi Mungu, na kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

-         Mtume (s.a.w.) ameshasema wazi kuwa:

(( Katika mwisho wa dunia, wake wa wanaume katika umma wangu watakuwa uchi, yaani kutositiri vichwa vyao na kuzifunga nywele kwa nyuma au utosini na kuzionyesha kwa wanaume, basi muwalaani hakika wao wamelaaniwa, na wala  harufu ya pepo.

-         Imamu Ali (AS) amesema : Itajitokeza zama katika mwisho wa dunia nayo ni shari ya nyakati, wanawake wataonyesha mapambo yao, wameachana na dini, watakuwa ndani ya fitina,  na wenye kufuata matamanio, wanakimbilia raha, wanahalalisha mambo ya haramu nawatakuwa motoni (Jahanamu abadani)  hawatoki humo.

-         Kuna  hadithi nyingi za Mtume (s.a.w.) : zinazohusu adhabu ya mwanamke asiyevaa hijabu, natunataja baadhi yake:

Imamu Ali (AS) amesema: Tuliingia mimi na Fatima Zahrah (AS)  kwa Mtume, basi tumemkuta analia sana, nikamuuliza:  Fadaaka abiy wa Umiy, nini kimakuliza?

-         Akasema :  Ewe Ali usiku niliopelekwa mbinguni nimeona wanawake wa umma wangu, wakiadhibiwa adhabu kali, basi nimechukizwa na hali zao na nimelia pale nilipoona shida ya adhabu yao kisha akaanza kuelezea jinsi alivyoona usiku huo wa miraji miongoni mwa aliyosema ni ((Nimeona mwanamke amefungwa kwa nywele zake na ubongo ukiwa unachemka, nimeona mwanamke amefungwa kwa ulimi wake na moto ukimwagiwa kinywani mwake, nimeona mwanamke anakula nyama ya mwili wake na moto ukiwakishwa chini yake, nimeona mwanamke amefungwa miguu yake na mikono yako pamoja na ameninginizwa juu ya majoka na mange nimeona, mwanamke, kiziwi, kipofu, sauti yake haisikii katika sanduku la moto, anatokwa na ubongo, ukitokea puani na mwili wake umekatika  katika  kutokana na mbalanga, nimeona mwanamke anakopesha nyama yake kwa wakopeshwaji)).

-         Basi Fatima Zahrah (AS) akamuuliza baba yake nieleze walichokuwa wakikifanya duniani mpaka Mwenyezi Mungu akawaweka kwenye adhabu?

-         Mtume (s.a.w.) amesema ewe binti yangu:

-         Ama aliyefungwa kwa nywele zake alikuwa hafuniki nywele zake kwa wanaume na mwenye kufungwa kwa ulimi wake alikuwa alikuwa anamuuzi mume wake.

-         Aliye kuwa ankula nyama yake alikuwa akirembesha mwili wake kwa ajili ya watu.

-         Aliye kuwa amefungwa mikono yake na miguu yake kwa  pamoja na kuninginizwa kwenye manyoka na mainge alikuwa hajitoharishi, nguo zake chafu, hajitoharishi kutokana na janaba, na hedhi na wala hajisafishi, na alikuwa msahalifu wa Sala.

-         Ama aliye kuwa kipofu, kiziwi…. Alikuwa anazaa watoto wa zinaa na kusema ni wa mume wake)

-         Na aliye kuwa ana kopesha nyama yake kwa wakopeshaji alikuwa akifanya umalaya na wanaume … mpaka mwisho wa hadithi.

(( Yaani alikuwa akijipeleka kwa wanaume bila ya kuulizwa.

-         Imeshadhihiri kwetu katika hadithi hii, hali za adhabu jinsi Mwenyezi Mungu alivyomwandali mwanamke asiyevaa hijabu kuwa atafungwa kwa nywele zake, na ubongo wake unachemka kwa sababu ya adhabu kali, moto ukimchoma pembezoni mwake, na hii ina maana kuwa kila  mwanamke asiyevaa hijabu atakumbana na adhabu hii kali sana….. ila akitubu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutokanan na kutovaa hijabu na akaamua kuvaa hijabu lililokamili, hakika Mwenyezi Mungu atakubali toba yake na kumsamehe.

-         Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: (( Naye ndiye anayepokea toba za watu wake na anasamehe makosa na anayajua yote mnayoyatenda)  ((Na hakika mimi ni mwenye kusamehe sana kwa anayetubia na kuamini na kutenda mema tena akashika uongofu bara bara)

HIJABU ISIYO KAMILI

-         Kuna baadhi ya wasichana ambao utawaona wamevaa hijabu, lakini hijabu isiyo kamili, utamuona amesitiri baadhi ya kichwa, na baadhi ya mwili na kuacha sehemu nyingine iko wazi mbele ya macho ya watu… au anasitiri kichwa chote lakini mikono na miguu yote iko wazi.

Kwa kweli… hijabu  hii lisilo kamilika halihisabiki kuwa  ni hijabu ambalo lina hakikisha lengo la hijabu, kama ilivyo,  halitekelezi amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.).[35] [36]

-         Na imeshatokea hali hii wakati wa Mtume (s.a.w.) kuwa baadhi ya wanawake walikuwa wakisitiribaadhi ya kichwa na kuacha baadhi pamoja masikio yakiwa wazi, basi Mtume (s.a.w.) akakatazana kuamrisha hijabu iliyo kamili ya kisheria.

Kwa sababu ya hijabu hii lililo kamili Mtume (s.a.w.) ameamria katika hadithi iliyotangulia ametaja neno walio uchi kwa maana  wanatoka wakiwa wamejionyesha ni vipi vitu hivi: ((Kujisitiri kujionyesha )) viwe pamoja?

Jibu:  Ishara hii inamlenga yule mwanamke ambaye anadhani kuwa amejisitiri mwili mzima!!

-         Mtume (s.a.w.) anaongezea kuwa vichwa vyao kama nundu ya ngamia, nundu hiyo ambayo inaonekana  wazi wazi.

-         Mtume (s.a.w.) : amefananisha nundu ya ngamia na wanayo yafanya baadhi ya wanawake  wakati wa kutoka nje kuwa wanazitengeneza nywele zao mfano wa nundu ya ngamia.

-         Kisha akasema muwalaani kwa sababu wao wamelaaniwa)) na hii inaonyesha kuwa kuna anaye walaani.

-         Na utauliza ni nani anaye walaani?

-         Jibu: imekuja katiak hadithi tukufu kuwa malaika wa mbinguni na ardhini wanamlaani mwanamke asiye vaa hijabu na anayevaa mfano wa hijabu kwa kila hatua anayo itembea mwanamke huyo, Hebu angalieni!!!

-         Kama mwanamke huyu angekuwa na masikio yasiyo haya ya kawaida angesikia kelel Malaika kutoka kila pembe wakimwambia: Laana ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)  iwe kwako, …. Laana ya Mwenyezi Mungu iwe kwako.

-         Mamilioni na mabilioni ya Malaika wakimlaani huyu mwenye kujionyesha!!

-         Hawafanyi hivi wenyewe, bali mwenye

-          (s.w.t.) anasema:  ((Hawamuasi mwenye

-          kwa yale waliyoamrisha, wanafanya wanayo amrishwa)).

-         Maana ya laana ni !

-         Kuwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu, wema na Tawfiqi.

-         Bilahi ghalikumu

-         Ni mwanamke gani ameridhia kulaaniwa na malaika wa mbinguni na wa ardhini?!

-         Mimi naamini kuwa mwanamke akijua hili itakuwa  ni vigumu kujichagulia kutovaa hijabu au rehema wala sio laana, anataka wema wala sio ubaya, ana maisha yamnyookee wala sio kinyume chake.

-         Mimi natilia mkazo kuwa hijabu iliyotiwa umuhimu na kuamrishwa ni kujisitiri kikamilifu kulingana na sheria iliyoepukana na mavazi yasiyofaa.

HIJABU KATIKA SHEREHE YA KIARABU

-         Umeshajua kuwa hijabu iliyowajibu katika dini na ni dharura kwa jamii, Uislamu umeamrisha hijabu kwa ajili ya kupenda mwanamke na kumhifadhi asiwe katika hali ya uchafu, na kumtoharisha kutokana na najisi.

-         Kwa sababu ya ukweli huu atakuwa na Imani na kufungiwa milango ya kiadabu ya kiumini, na ili ahakikishe ukweli huu kwa kufuata sheria, nayo ni kuonja adabu nzuri na kufuatilia kauli za waumini katika sherehe na mikusanyiko mingine.

-         Na amesadikisha aliyesema:  hakika katika shairi kuna hekima .

-         Na yafuatayo tunataja baadhi ya mifano ya wanamashairi katika maudhuu haya :

-         Kuwa katika utukufukwa kujisitiri

-         Najirembesha kwa kujisitiri na uache kujionyesha, kutovaa hijabu, kunasababisha kutofanikiwa, na mwishoni ni kuacha mambo ya kidini.

-         Msichana kujionyesha sio urembo.

-         Inasababisha kukosa utukufu, kwa hakika ni kulingania ujinga ((Ujahili)) ambao ni uwazi na vitimbi na fitina

-         Inahitaji kukataza udanganyifu ambao unaonekana kuwa ni uzuri.

-         Kama ungekuwa unajua makusudio na mwisho wa udanyifu na hatari zake, basi ungejihadhari na kuogopa.

-         Chache za moto zimewaka  pamoja  na kuwa kuna kizuizi na haziwezi kuzimika mara moja mpaka pawe na kinga) kwa kiasi cha kutosha kuzima mara moja, na iwe ni ngome ya kuhifadhi matunda ya kuliwa. Kwani kujitokeza kwake ni kuharibika.

-         Na kwa maana hiyo, dini: Inakuambia usijionyeshe kwa ajinabia ili uhakikishe lengo na ili ujiandae kujihakikishia kupata zawadi.

-         Lengo lenye kufanikiwa kwa mfano mizuri.

-         Na mwingine anasema : Kutovaa hijabu ni njia ya kufahamiana wavulana na wasichana, na kujionyesha kunasababisha mapindizi katika vifua wakati wake.

-         Miongoni mwa hali ambazo zinazuia ufisadi ni kuwa na ngome na kuwa na haya (aibu), na hii ni kama kutupa mshale wa kujizuia na wanaume wenye uchu na wanawake waumini, ni wangapi  waliokuwa wacha Mungu lakini wanasaka wasichana kwa hiyo vaa hijabu ewe binti ili uwe na kizuizi cha kukuweka katika daraja ya juu, na kukuepusha na macho ya wabaya kwa kukuangalia.

-         Kama ilivyo kuja: Kuangalia, kisha kutabasamu, kisha salamu, kisha mazungumzo, kisha kupeana ahadi na mwisho ni kukamilisha ahadi.

-         Hakika hijabu ni kinga ya mabaya yanayotokana  na kutovaa hijabu.

-         Na mwingine amesema:  Ewe binti yangu ukitaka uzuri ambao unapendezesha mwili na akili, basi tupilia mbali kabisa tabia ya kujionyesha.

-         Uzuri wa nafsi (Moyo) ni bora kuliko kujirembesha uso ili macho, basi ifanye heshima ya maisha kuwa hijabu, na tabia njema ni bara, ikinge nafsi yako kwa kuvaa hijabu, kwa sababu nguo zingine sio kinga kwako.

-         Na mwingine anasema :

-         Jitibu maradhi ya kutovaa hijabu, hakika hiyo wamesema kuwa ni dawa ya jicho kutoangalia msichana hali yake.

-         Maji yasipo hifadhiwa kwenye chombo.

-         Nani atakuwa masuulu wa wasichana baada ya kujionyesha?  Wanapo kuwa na uwezo hatari wa uchafu?

-         Na nani ambaye anakataza mtu mwenye kujua? Udanganyifu wa kila bikira mzuri asiyevaa hijabu kwa kujua kuna makatazo?

-         Basi elimu hajawekwa kuwa ni modeni (fasheni) ya mavazi au kuwa ni mafunzo ya wasichana wasiojisitiri.

Wamewatakia maisha yasio na hijabu - Na hiyo ni njia ya ufisadi

Ni vipi wasichana watahifadhiwa?  -  Na kila siku rafiki anamtembelea

Je ubikira hauwi ila kwa kuujengea? -  Na hali wao wanakizuizi imara

Basi nikipi kipya cha mudai?  -   Anacho kiona kuwa ni kigumu katika kujisitiri kwao?

Kila matokeo mwanzo wake ni kuangalia – Kkumbwa ni moto kuliko  shari ndogo

Miangalio mingapi inafika katika moyo wa mwenye kuangalia – kwenye macho yenye  kuwa hatarini.

Anayedhurika ni yule anayeongoza -  hakuna furaha inayorudi kwa mdhuriwa.

NENO LA MWISHO

-         Hakika umeshajua tuliyoyataja katika kitabu hiki – kuwa hijabu ni sheria tukufu, inatosheleza wema wa mwanamke, kuhifadhi familia,kutaharisha jamii, na kwa kuongezea kuwa ni jambo la kidini, hukumu ya kisheria, ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameitoa na Qur'an tukufu, Mtume (s.a.w.) na ahlu Baiti wake (AS) wametilia mkazo.

-         Na umefahamu pia kujionyesha, kutovaa hijabu, kunasababisha mabaya kwa mwanamke,familia kuvunjika na jamii kuwa na ufisadi, kwa kuongezea kuwa kukhalifu masilahi yote.

Kwa hiyo ni juu yetu sote kufuata kanuni hii na kuineza katika wanawake wa jamii, nyumbani, shuleni, chuoni, kazini,ofisini na katika nyanja mbali mbali za maisha, tukifanya hivi Mwenyezi Mungu ataridhia na kheri itakuwa kwetu duniani na akhera.

Na mwisho wa mazungumzo yetu, tuseme al – hamdulilahi rabil – ala’amini waswala llahu a’aalaa Muhammad wa’ali Muhammadi twayibiina twahirini.


YALIYOMO

-         NENO LA UJUMBE.

-         UTANGULIZA WA CHAPA YA KUMI.

-         UTANGULIZI.

-         QUR’AN INATILIA MKAZO HIJABU.

-         FATIMAH ZAHARAH (AS) NI KIGEZO CHEMA.

-         KUJISITIRI NI UREMBO WA MWANAMKE.

-         MAZUNGUMZO BAINA YA MSICHANA WA KIKIRISTO.

-         TOFAUTI BAINA YA ASIYEVAA HIJABU NA ANAYEVAA HIJABU .

-         MADAI YA WASIOVAA HIJABU YANAKUSUDIA NINI?

-         NILIPI BORA?

-         KUTOVAA HIJABU HATARI KATIKA JAMII.

-         KUTOVAA HIJABU NA UFISADI.

-         KUTOVAA HIJABU UBAKAJI.

-         KKUTOVAA HIJABU NA UTOAJI MIMBA.

-         KUTOVAA HIJABU NA HIYANA KATIKA NDOA.

-         JUKUMU LA SINEMA NA UPOTOFU KATIKA KUTOVAA HIJABU.

-         MARADHI YA KUCHANGANYIKANA.

-         UISLAMU SIO DINI YA NADHARIA (MAONI).

-         MADAI YA WASIOVAA HIJABU YAMEPATA NINI?

-         MADAI YA WASIOVAA HIJABU YAMEPATA NINI?

-         EWE DADA MWISLAMU.

1.     HIJABU KABLA YA KILA KITU.

2.     USITUMIE POWDER  (MANUKATO) ISIPOKUWA NYUMBANI.

3.     USIJIFANANISHE NA WANAUME.

4.     USIMSALIMIE MWANAUME AJINABIA KWA KUMPA MKONO.

5.     USIONEE AIBU HIJABU.

6.     UAMINIFU PEKE YAKE HAUTOSHI.

7.     USIDANGANYIKE NA VITU VISIVYOFAA (VISIONAMAANA).

8.     KUWA NI MWENYE KULINGANIA HIJABU.

9.     USIKATAE KUOLEWA.

 

EWE MUME MTUKUFU

 

1.         KWANZA HIJABU

2.         KUJIHADHARI NA SHEREHE ZA MCHANGANYIKO.

3.         USIMTII MKE WAKO KATIKA MAASI.

4.         KUWA NA WIVU KWA MKE WAKO.

5.         MFUNZE SURA YA NURU.

6.         USIMUWEKE VYUMBANI.

 

MAFUNZO YA KIISLAMU

 

1.     USIANGALIE MWANAMKE AJINABIA.

2.     USIMSALIMIE MWANAMKE AJINABIA KWA KUMPA MKONO.

3.     USIFANYE MUZAHA NA MWANAMKE AJINABIA.

4.     USICHELEWE KUOA.

 

-         ADHABU YA MWANAMKE ASIYEVAA HIJABU.

-         HIJABU ISIYO KAMILI.

-         HIJABU KATIKA SHERIA  YA KIARABU.

-         NENO LA MWISHO.

-         YALIYOMO

 

 



[1] Kitabu kuhusu mambo ya familia na kuoa

[2] Sura Maidah, Aya : 44,45,47.

[3] Jaridatul -Qubusil –Al- kuwaitiya- Idadi 18 – tarehe 13/3/1972

 

[4] Majalati – nahadwati-kuwaitiya – idadi 232.

 

[5] Kitabu – kuhusu familia na kuoa –U.k.130.

 

[6] Kitabu – kuhusu familia na kuoa – u.k. 145.

[7] Al-Kafiy J: 5, U.k: 324

[8] Biharul – Anwaari J : 103, U.k. 247

[9] Al- Kaafi: J : 5, U.k. 552.

[10] Al- Kafiy J : 8, U.k.138.

[11] Sura Hud aya 112.

[12] Sura Faswilati aya 30.

[13] Sura Hudi aya 38.

[14] Biharul – Anwaari J : 2 U.k. 4, Al –A’Abigi ni mtumwa mtoro.

[15] Al-Kafiy J : 5, U.k. 347

 

[16] Al-abukaari ni mabinti ambao bado wanahifadhi ubikira wao

 

[17] Al – Kafiy J: U.k 337 na Biharul – Anwaari  J: 130, U.k 371.

[18] Surati ghaafiri aya 60

[19] Sura Nisaah aya 34.

[20] Sura Taharimu aya 6.

[21] Nahajul – Balagha.

[22] Al – Kafiy J : 5, U.k 517.

[23] Al- Kafiy ya sheikhel – Islamu – Al – Kulainiy J : 5, U.k 535.

[24] Al – Kafiy J : 5, U.k. 537

[25] Biharul – Anwaari J : 103, U.k. 249

[26] Al – Mawaaidhiil –Al – ghadadiya U.k.223

[27] Al – Kafiy J: 5, U.k: 516

[28] Biharul – Anwaari J: 52,  U.k: 339

[29] Biharul – anwaari, J : 104, U.k.38

[30] Surat nuru, aya :30.

[31]  Biharul – anwaari J: 104, U.k: 40

[32] Mustadirikil- wasaail J : 2, U.k: 554.

[33] Biharul – anwaari, J : 104, U.k: 42.

[34] Biharul – anwaari, J : 103

[35] Surat Shurah aya 25

[36] Surat Taha aya 82