SHIA NA HADITH

Majibu Na Maelezo

Abdilahi Nassir

UTANGULIZI

Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.

Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khututul Aridhwa kilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Misingi Mikubwa lliyojengewa Dini ya Ushia.

Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M. a(-Kbatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu Hadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. Na kama tulivyofanya katika kitabu chetu cha kwanza, Shia na Qur'ani, tumeyalinganisha hayo na yale yanayopatikana katika vitabu vya Kisunni.

Ni matumaini yetu kwamba, baada ya kukisoma kitabu hiki, itakudhihirikia kwamba hakuna hitilafu kubwa hivyo baina ya msimamo wa Sunni juu ya Hadith na ule wa ndugu zao, Shia, hata iwazuie wao kukurubiana na kuelewana kamaalivyopendelea Sheikh M. al-Khatib.   Kitu cha pekee kinachozuia ndugu wawili hao kuelewana ni zile chuki zinazojengwa baina yao na wale ambao watapata hasara lau ndugu hao watasikilizana na kulingana!

lli uweze kufaidika na majadiliano yaliyomo humu, na yale yaliyomo katika vitabu vyetu vingine katika mfululizo huu, ningependa uhakikishe kwamba:

(i)  unayo nakala ya hicho kitabu cha Sheikh M. al-Khatib tunachokijibu. Kama huna, jaribu kukipata kutoka mojawapo ya anwani hizi: S.L.P.70541; au 67971; au 48509: zote za Nairobi, Kenya.

Hivi vyetu, unaweza kuvipata kwa kutuandikia kwenyeS.L.P. 86260,     Mombasa, Kenya.

(ii) tunapotaja kwamba maneno fulani ya Sheikh M. al-Khatib yamo kwenye ukurasa fulani wa kitabu chake, hakikisha umefungua ukurasa huo na kuyakinisha kwamba tumeyanukuu maneno haya vilivyo.  Kamasivyo,

tafadhali tuandikie utukosoe ili tuweze kujisahihisha. Maana nia yetu si kumzulia marehemu S,heikh uwongo, bali ni kujenga umoja wa Waislamu kwa kujaribu kuondoa kutoelewana kulioko baina yao.

(iii) tunapotoa ushahidi wa vitabu fulani, ujaribu kuangalia ushahidi huo katika vitabu hivyo, kwa lugha unayoielewa. Kamahakuna kwa lugha hiyo, basi mwendee shekhe yeyote aliye karibu nawe, na ambaye hayuko upande wowote katika mzozo huu. umwombe akuangalilie katika nuskha za Kiarabu alizonazo yeye ili uhakikishe kwamba tulivyo nukuu ndivyo. Kama sivyo tafadhali usisite vile vile kutujulisha ili tuweze kuelekezana.

Mwisho, ningependa kurudia tena kwamba lengo letu katika kuandika majibu haya si kutafuta ubishi wala mizozo, bali ni kutaka tu kuonyesha kwamba vile vikwazo vya kuzuia uelewano na umoja baina ya Sunni na Shia, ambavyo Sheikh M. al-Khatib alidhania viko, haviko!   Kama tutafaulu kulithibitisha hilo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa maslaha ya Waislamu wote.

Ewe Mola! Tusaidie

ABDILAHINASSIR

Mombasa, Kenya RabiulAwwal, 1410 Oktoba, 1989

 HADITH KWA SUNNI

1. Katika uk. 29 wa kitabu chake, Sheikh M. al-Khatib amesema:

Hadith kwa Ahlil-sunnah ni tumbuko la pili la sharia, na ndizo zenye kuifasiri Qur'an tukufu.

Majibu:Hilo si kwa Sunni peke yao. Hata kwa Shia ni vivyo hivyo. Kwa mfano, unaposoma al-Kafi, Juzuu ya Kwanza, uk. 69-70 utaona Hadith zifuatazo:

(a) Imepokewa kwa Abu Abdillahi a.s. kwamba amesema: 'Kila kitu ni chenye kurejezwa kwenye Kitabu na Sunna; na kila Hadith ambayo haiwafikiani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi (Hadith hiyo) ni uwongo.'

(b) Imepokewa kwa Ibn Abi Umayr ... kwamba amemsikia Abu Abdillahi a.s. akisema: 'Yeyote anayekwenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Muhammad s.a.w.w., basi (huyo) amekufuru.'

(c) Imepokewa kwa Ali b. al-Husayn a.s. kwamba: 'Bora ya amali mbele za Mwenyezi Mungu ni ile iliyofanywa kwa kufuata Sunna, japo iwe ni kidogo.'

(d) Imepokewa kwa Amirul Mu'minina a.s. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: 'Hakuna maneno (yanayokubaliwa) ila kwa vitendo; na hakuna maneno wala vitendo (vinavyokubaliwa) ila kwa nia; na hakuna maneno wala vitendo wala nia (inayokubaliwa) ila yawafikiane na Sunna.'

(e)Imepokewa kwa Jabir kwamba Abu Ja'far a.s. amesema: 'Hakuna yeyote ila ana nishati na utulivu. Basi yule ambaye nishati yake imo katika sunna, huyo ameongoka. Na yule ambaye (nishati yake) imo katika bid'a (uzushi), huyo amepotea.'

(f) Imepokewa kwa Abu Abdillahi a.s. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: 'Kila Haki ina hakika, na kila la sawa lina nuru. Basi linalokubaliana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, lichukueni; na linalopingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, liacheni.'

(g) Imepokewa kwamba Abu Abdillahi a.s. amesema: 'Hadirth yoyote isiyowafikiana na Qur'ani ni uwongo.'

(h) Imepokewa kwa Abu Abdillahi a.s. kwamba Mtume s.a.w.w. alihutubu Minaa akasema: 'Enyi watu! Lolote tinalowajia kutoka kwangu, linalowafikiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi mimi nimelisema. Lakini linalowajia likawa linapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi hilosikulisema.

Kutokana na Hadith hizo, ambazo nimezitoa katika kitabu kimoja tu kati ya vitabu vingi vya Hadith vinavyokubaliwa na Shia, itadhihiri kwamba kamavile ambavyo Sunni wanaamini kwamba Sunna ya Mtume Muhammad s.a.w.w. ni 'chimbuko la pili la sheria' na ndiyo inayo ifasiri Qur'ani Tukufu, ndivyo vivyo hivyo wanavyoamini ndugu zao, Shia.

lli kuthibitisha hilokwa vitendo tazama, kwa mfano, jinsi Shia wanavyosali. Jee, wamepata wapi, kama si katika sunna, ile idadi ya rakaa za swala zao" Wametoa wapi kurukuu, kusujudu na kukaa tahiyatu? Wameipata wapi Allahu Akbar au Samiallahu Liman Hamida au Subhana Rabbiyal Adhimu Wabihamdihi au Subhana Rabbiyal A'alaa Wabihamdihi? Wamezipata wapi zote hizo hali hazimo katika Qur'ani? Bila shaka wamezipata katika Hadith za Mtume s.a.w.w. kama walivyozipata ndugu zao, Sunni. Kwa hivyo kama Shia hawakubali kuwa Hadith za Mtume s.a.w.w. ni chimbuko la pili la sheria na kwamba ndizo zinazoi fasiri Qui"ani Tukufu, bila shaka wasingekuwa na mambo yote hayo katika swala zao. lle kuwa wanayo yote hayo, na mengi mengine ambayo hatukuyataja, ni ushahidi tosha kwamba wanalikubali hilo

Juu ya yote hayo, mtu yeyote anayeweza kusoma na kukielewa Kiarabu natazame, katika tafsiri yoyote ya Shia ya O

Qur'ani Tukufu, jinsi Sura 4:80 16:44, 59:7 na nyingine kamahizo zilivyofafanuliwa ili aweze kuelewa vyema msimamo wa Shia kuhusu Hadith za Mtumes.a.w.w. kama chimbuko la pili Ia sheria ya Kiislamu.

Kutokhalifu Hadrth Sahihi

2. Akasema tena (katika huo huo uk. 29);

Na wala haifai kukhalifu hukumu za Hadithi yoyote iliyoswihi kutokamana na Mtume s.a.w.w.

Majibu: Hilo pia si kwa Sunni peke yao. Hata kwa Shia ni vivyo hivyo; na kama mtu atakataa au ataikhalifu Hadith yoyote iliyoswihi, basi huyo ni kafiri

Taz. Hadith Na. (b) katika uk. 3 humu.

Lakini hata hivyo, tunapotazama vitabu vya Kisunni tunaona kwamba matendo yao ni kinyume na madai ya Sheikh M. al-Khatib hapo juu. Wao huKhalifu hukumu za Hadith hizo; na hapa chini tunatoa mifano miwili mitatu tu:

(i) Talaka tafu: Tuhaposoma vitabu vya Kisunni vya l-ladith tunaona kwamba Bwana Mtume s.a.w.w., alipoendewa na mtu aliyemwacha mke wake talaka tatu katika kikao kimoja, alimwambia: 'Hiyo ni moja tu. Mrejee, ukipenda.' Lakini Umar b. al-Khattab, alipokuwa Khalifa, akahukumu kinyume cha hivyo. Yeye akasema talaka tatu ni tatu!

Ukitaka kuyaona hayo, tazama Mlango wa Talaka katika vitabu vya Kisunni vya Hadith k.v. Sahih Muslim, al-Mustadrak, Sunan Abi Dawud, na hata Bulughul Maram ya Ibn Hajar al-Asqalani inayosomeshwa sanamisikitini mwetu. Mote humo utaona imeandikwa kwamba talaka tatu zilikuwa ni moja katika enzi ya Bwana Mtume s.a.'w.w., na ya Abubakar, na miaka miwili ya kwanza ya Ukhalifa wa Umar. Lakini baadaye Umar akazifanya ni tatu! Na hivyo ndivyo ilivyo hadi leo katika madhehebu yote ya Kisunni!

Jee, hapo ndugu zetu wa Kisunni watakuwa wamefuata Hadith 'iliyoswihi kutokamana na Mtume s.a.w.w au watakuwa wamefuata sunna ya Khalifa Umar?

Kwa wale wanaojua Kiingereza nawatazame Hadith Na. 3491-3493 katika uk. 759 wa Juzuu ya Pili ya Sahih Musfim, na Hadith Na. 2193-2194 katika uk. 593 wa Juzuu ya Pili ya Sunan Abi Dawud.

(ii) Swala ya Tarawehe: Swala hii haikuswaliwa jamaa; bali ikiswaliwa kila mtu peke yake. Hivyo ndivyo ilivyokuwa zama za Mtume s.a.w.w., na hata zama za Ukhalifa wa Abubakar: mpaka alipofariki dunia mwaka 13H. Halafu akatawala Umar b. al-Khattab mwaka huo huo wa 13H, akafunga Ramadhan na asibadilishe chochote. llipofika Ramadhan ya mwaka 141-1 ndipo alipomteua Ubayy b. Ka'b aswalishe watu jamaa. Hata siku ya pili alipoona watu wakiswali hivyo akasema:'Bora ya bid'a (uzushi) ni hii!'

Tazama hayo katika 'Kitabus Sawm' Mlango wa 'Fadhl Man Qaama Ramadhan' katika Sahih Bukhari; pia 'Kitabu Swalatil Musafirina Waqasruha' Mlango wa 'at-Targhibu Fii Qiyami Ramadhan' katika Sahih Muslim. ^Kwa wale wenye tafsiri za Kiingereza za vitabu hivyo, nawatazame Hadith Na. 227 katika uk. 126 wa Juzuu ya Tatu ya Sahih Bukhari, Hadith Na. 1663 katika uk. 366 wa Juzuu ya Kwanza ya Sahih Muslim, na hata Hadith Na. 1366 katika uk. 358-359 wa Juzuu ya Kwanza ya Sunan Abi Dawud.

Na hilo la kuwa Umar b. al-Khattab ndiye aliyeizua tarawehe hivi iswaliwavyo na Sunni leo, linakubaliwa na wanazuoni wakubwa wakubwa wa Hadith wa Kisunni. Kwa mfano, ukitazama uk. 173 wa Juzuu ya Pili ya Subuhus Salaam (sherehe ya Bulughul Maram)utarrwona Imam as-Swan'ani asema: 'Ama hii tarawehe, ilivyozowewa sasa, haikuwa hivi zama za (Mtume) s.a.w.w. Kwa hakika aliyeizua ni Umar wakati wa Ukhalifa wake, akamwamrisha Ubayy aswalishe watu jamaa'.

Na kama hivyo ndivyo alivyosema Ibn Hajar al-qastwalani katika Irshadus Saari (sherehe ya Sahih Bukhari) alipofikia kile kipande cha maneno ya Umar b. al-Khattab kisemacho: 'Bora ya bid'a ni hii'. Yeye amesema: '(Umar) ameiita hiyo bid'a kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. hakuwawekea sunna hiyo, wala haikuwako zama za as-Siddiq r.a., wala mwanzo wa usiku, wala idadi hii...'

Kwa hivyo ni wazi hapa vile vile kwamba, kinyume na anavyodai Sheikh M. al-Khatib, sio wakati wote Sunni hufuata Hadith iliyoswihi kutokamana na Mtumes.a.w.w.

(iii) Ndoa ya muda (mut'a): Hii ni ndoa ya sheria iliyowekwa na Mwenyezi Mungu s.w.t. kama ilivyo katika Sura 4:34. Ndoa hii ilikuwa ikitendeka zama za Bwana Mtume s.a.w.w. Ikatendeka zama za Khatifa Abubakar mpaka akafariki dunia.  Ikaendelea katika enzi ya Umar b. al-Khattab mwanzo mwanzo; baadaye akaiharamisha! 'Na tangu siku hiyo ikawa ni haramu kwa Sunni hadi hii leol

Ukitazama Sahih Muslim, 'Kitabun Nikah', Mlango wa 'Nikahul Mut'a' utaona jinsi Jabir b. Abdillahi anavyosema kwamba walikioa mut'a zama za Mtume s.a.w.w. na Abubakar na Umar; mpaka Umar alipokuja kuizuia kwa .ajili ya Amr b. Hurayth. Pia tazama Musnad Ahmad, Juzuu ya Tatu, uk. 380..

Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 3249-3250 katika uk. 706 wa Juzuu ya Pili ya Sahih Muslim..

Kwa hivyo, na hapa pia, twaona sunna iliyowekwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake s.a.w.w., ikaondolewa na Umar; na Sunni nao wakajiharamishia hadi leo!

Kwa mifano mitatu hii (na kuna mingi mingine nimeiacha) itaonekana kwamba madai hayo ya Sheikh M. al-Khatib (yaliyomo Mk. 29 wa kitahu chake hicho) hayana mashiko!

Mustwalahul Hadith

3. Akaendelea kusema, hapo hapo uk. 29, kwamba:

 Na kwa ajili ya kuswahihisha hadith kuna misingi ambayo wanavyuoni wa Ummah wameafikana kuitegemea katika ilimu inayo julikana kwa jina la Mustwalahul Hadith.

Majibu:Elimu hiyo haiko kwa Sunni peke yao. Iko hata kwa Shia; na vitabu

inetungiwa k.v. ad-Diraya Fii llmi Mustwalahil Hadith 'cha zaynuddin b. Ali al-Amily, maarufu 'as-Shahiduth Thani',

Qawa'idul Hadith cha Muhyiddin al-Musawil Ghurayf, na vinginevyo (taz. uk. 8humu).i

Sharti ya usahihi wa Hadith

4.Akamalizia:

Na ndia ya kutimiza hilo ni kuhakikisha kushikamana sawa nyororo ya wapokizi wa Hadithi pasina kubagua kati ya waume na wake isipokuwa kukhusu kuhakikisha kuwa ushahidi ni wa uadilifu.

Majibu: Na vivyo hivyo ndivyo hasa ilivyo kwa Shia. Kwao wao vile vile Uislamu (sio madhehebu) na uadilifu wa mpokezi wa Hadith ni miongoni mwa sharti kubwa za kuhukumia usahihi wa Hadith yoyote. Kwa ajili hii utaona kwamba, pamoja na hitilafu zilizoko baina yao na Sunni, Shia huzikubali Hadith zilizopokewa kwa Sunni bora tu awe ni mwadilifu; kama anavyotweleza Sayyid Muhammad Taqiy al-Hakim katika uk. 219 wa kitabu chake kitwacho al-UsululAammah (chapa ya kw'anza):

Shia Imamiyya huzizingatia habari za wapinzani wao katika akida (imani) kuwa ni hoja inapothubutu kwamba (watu hao) ni thuqaat (wanao aminika); na habari zao hizo huziita muwath-thaqaat (zenye kuaminika). Nazo (habari hizo) katika kuwa ni hoja, ni kama habari nyinginezo (zilivyo). Na vitabu vyao (yaani Shia) vimejaa hayo.

Lakini, pamoja na yote hayo, tunapotazama vitabu vya Kisunni vinavyohusu sanad (nyororo za wapokezi) twaona kwamba wao wakati mwingine humtia ila a'bu) mpokezi kwa sababu za kibinafsi; sio kwamba si mwadilifu! Kwa nfano, ukitazama Tahdhibut Tahdhib chini ya jina la Abdullah b. Sa'd Abi Qudama as-Sarkhas), utaona kwamba Muhammad b. Yahya amekataa Hadith zake kwa sababu tu 'Muhammad aliingia kwake, naye (Abdullah b. Sa'd) akumsimamia'!

Kadhalika ukitazama katika kitabu hicho, chini ya jina la Sa'd b. Ibrahim b. bdulrahman b. Awf, utaona kwamba Imam Malik hakupokea Hadith zake na sababu 'alimwaidhi' kwa maneno yaliyomuudhi. Na vivyo hivyo ndivyo alivyosema Ibn Mu'in, humo humo, kwamba 'Sa'd alisema kitu juu ya nasabu ya Malik ndiyo (Malik) akaacha kupokea kwake'!'

Ukija kwenye Mizanul l'tidal, chini ya jina la Abdullah b, Dhakwan (maarufu 'Abuz Zanaad'), utaona Rabia anasema kwamba si thiqah (wa kutegemeka). Kisha inaendelea: 'Neno la Rabia kumhusu (huyu Abuz Zanaad) lisisikilizwe maana baina ya wawili hao palikuwa na uadui ulio dhahiri.' Haya! Hiyo ni mifano miwili mitatu tu. Mingine nimeiacha. Kutokana na mifano hiyo tunaona kwamba lile dai la Sheikh M. al-Khatib, kwamba sharti kubwa katika kutimiza usahihi wa Hadithi kuhakikisha uadilifu wa mpokezi, halitumiki wakati wote. Maana tumeona hapo juu kwamba kuna wapokezi ambao riwaya zao zimekataliwa kwa sababu za kibinafsi; sio kwamba si waadilifu! Jee, mambo yakiwa ni hivyo, tutakuwa na hakika gani kwamba Hadith nyingine hazikukataliwa kwa sababu hizo hizo za kibinafsi?

Tarekhe za wapokezi wa Hadith

5. Akaongeza shekhe wetu huyo (uk. 30):

Na kila mpokeaji wa Hadith ana tarekhe inayo julikana, na Hadith maalumu zenye

kudhibitiwa zilo swahihi au zilotaywa kwa kuwa si swahihi.

Majibu: Na hili pia ndivyo lilivyo kwa Shia. Wao, kamandugu zao Sunni. wana vitabu maalum vyenye tarekhe na habari za wapokezi wao wa Hadith pamoja na kudokeza usahihi au uwongo wa Hadith hizo. Miongoni mwa vitabu hivyo ni hivi vichache •tunavyovitaja hapa chini:

(i) at-Tustiri: Qamusur Rijal

(ii)  al-Ardabili: Jamiur  Ruwat

(iii) al-Khui: Mu'jamu Rijalil Hadith

(iv)  Mamqani: Tanqihul-Maqal

(v)' an-Najjashi: Rijalun Najjashi

(vi)Allama Hilli: Khulaswatur- Rijal

(vii) at-Twusi: Ikhtiyaru-Ma'rifatir Rijal

(viii) al-Muqmaqani: Miqyasul Hidaya

 (ix) al-Amili: al-Bidaya Fi  llmid Diraya

(x)  Hasan as-Sadr: Sharhul Wajiza ,

Kwa hivyo, wenye vitabu vya aina hjyo si Sunni peke yao; bali na Shia pia wanavyo.

Hadith ya mwongo au asiyejulicana

6. Mwisho Sheikh M. al-Khatib akafunga maneno yake hayo kwa kusema (ul 30):

Haikubaliwi Hadith iliyopokewa na mrongo au asiyejulikana, wala kwa yeyote kwa sababu ya ujamaatu au ya kizazi.

Majibu: Hilo li wazi mno; halihitajii hata kusemwa! Hakuna mtu yeyote, sikwamba Mwislamu, anayeweza kukubali habari iliyosimuliwa na mwongo;

seuze uwongo huo uwe amezuliwa Bwana Mtume s.a.w.w.!

Hata hivyo, tunapochunguza kwa makini baadhi ya vitabu vya Kisunni vya tarekhe za wapokezi wao wa Hadith tunaona kwamba, kinyume na alivyodai Sheikh M. al-Khatib, wanazuoni wa Kisunni hukubali Hadith zilizopokewa na waongo' na majhululhali (wasiojulikana hali zao)!!

lli kulithibitisha hilo, hapa chini nataja majina ya wapokezi kumi tu (ingawa tunayo zaidi ya hayo) walioelezwa hivyo katika Tahdhibut Tahdhib na / au Mizanul l'tidal; na wote hao wamo katika Sahih Bukhari na/au Sahih Muslim imbavyo'ndivyo vitabu sahihi mno kwa Sunni:

(i) Ash'ath b. Said al-Basry

 (ii) Suwayd b. Said Abu Mohammadal-Harawi

 (iii) Abdullah b. Swalih b. Muhammad b. Muslim

 (iv) Abdulrahman b. Nu'man b. Ma'bad

 (v) Abdulwahhab b. Ataa al-Khafaf

(vi) Ali b. Abdillahi b. Ja'far

 (vii) Muhammad b. lshaq b.Yasar

(viii), Nu'aim b. Hammad al-Khuzai

 (ix) Asbat Abul Yasa'

(x) Ismail b. Abdillahi Abi Uwais b. Abdillah'i al-Asbahi

Juu ya hao kuna watu kama:

(i) Ismail b. Sami' al-Kufi al-Hanafi ambaye, inaelezwa katika Mizanul tida/, kwamba alikuwa jirani na msikiti kwa miaka arobaini, lakini hakuonekana katika swala ya Ijumaa wala jamaa! Na bado mtu kamahuyo mna riwaya

zake katika Sahih Muslim!

(ii) Hajjaj b. Artwaat ambaye, kwa mujibu wa Imam Shafi, alikuwa akisema kwamba murua wa mtu hautimii mpaka aache kuswali jamaa! Pia, kwa mujibu wa al-Aswma'i, mtu huyo ndiye Kadhi wa kwanza kupokea hongo Basra! Na alipoulizwa kwa nini hahudhurii swala ya jamaa msikitini, alijibu: 'Nihudhurie msikitini kwenu ili wachukuzi na wauza mboga wasongamane nami?' Yote hayo yamo katika Mizanul l'tidal chini ya jina lake; na bado mtu kama huyo riwaya zake zimo katika Sahih Musliml

Jee, watu kama hao watakuwa ni waadilifu kwa kipimo gani?

Ewe ndugu yangu! Mpaka hapa nataraji ushaona kwamba yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib amewadaia Sunni kuhusu Hadith za Mtume s'.a.w.w. ndiyo yaliyoko kwa Shia. Kama kuna hitilafu yoyote (na ziko, kama tulivyokwisha kuona), basi hitilafu hiyo si ya kuzuia makundi mawili hayo kukurubiana na kushirikiana kwa maslaha ya Uislamu, kama Sheikh M. al-Khatib alivyokusudia kuonyesha kataika kitabu chake.

Sasa tuyajadili yale aliyowasingizia Shia katika uk, 30 wa kitabu chake hicho.

 Na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu s.w.t.

HADITH KWA SHIA

1. Katika uk. 30 wa kitabu chake, Sheikh M. al-Khatib amesema hivi:

Mashia hawazitegemei hadith zozote zisizo kutegemezwa kwa jamaa wa Mtume, na baadhi ya hadith za Watu fulani waliokuwa pamoja na Aliy (r.a.) kwenye vita vyake vya kisiasa, na wanazikataa nyinginezo.

Majibu: Si kweli kwamba Shia wanazikataa Hadith zisizotegemezwa kwa ahlulbayt (watu wa Nyumbani kwa Mtume s.a.w.w.) na waliokuwa pamoja na Imam Ali a.s. Ukweli ni kwamba wanazikubali bora tu ithubutu kwamba watu hao ni waadilifu na waaminifu. Likithubutu hilo, kama tulivyokwisha kuona uk. 7 humu, hapana tatizo. Na si kwamba huzikubali tu, bali huzipa daraja ya muwath-thaq (yaani 'zenye kutegemeka'), kama ilivyo wazi kwa yeyote anayesoma vitabu vya Kishia vya Mustwalahul Hadith.

Hata hivyo, ni kweli kwamba Shia huzipa uzito mkubwa, na kwa hivyo huzitegemea zaidi, zile Hadith zilizotegemezwa kwa ahul bayt na wale waliokuwa pamoja na Imam Ali a.s. katika vita vyake [1] . Na hilo ni kwa sababu zilizo wazi kueleweka kwa yeyote asiye na chuki.

Shia huwapa ahlul bayt uzito mkubwa zaidi kwa sababu:

(i) Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu (dhambi) na kuwatakasa kikamilfu, kama ilivyodokezwa katika Sura 33:33;

(ii) kabla ya Mtume s.a.w.w. kufariki dunia, aliwatangazia Waislamu kwamba anawaachia 'vizito viwili' ambavyo, wakishikamana navyo, hawatapotea baada yake kabisa: cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na cha pili ni ahlul bayt wake; [2] na

(iii) Hadith Iliyothubutu kwamba imetokana na ahlul bayt  kuwa haina mushkali kwamba inatokana na Mtume s.a.w.w. Maana imepokewa kwamba Imam Jar'faras-Sadiqi a.s.amesema; 'Hadith yangu ni Hadith ya babangu, na Hadith ya babangu ni Hadith ya babu yangu, na Hadith ya babu yangu ni Hadith ya Husayn, na ya Husayn ni Hadith ya Hasan, na Hadith ya Hasan ni Hadith ya Amirul Mu'minina, [3] na Hadith ya Amirul Mu'minina ni Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w., na Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. ni Neno la Mwenyezi Mungu aza wajalla.' (taz Bihar, Juzuu ya Pili,' Kitabul llm.')

Hizo ni chache tu kati ya sababu' kadhaa zinazowafanya Shia wazipe uzito mkubwa Hadith zinazotegemezwa kwa ahlulbayt.

Pia Shia huzipa uzito mkubwa Hadith zilizopokewa kwa wale waliokuwa ni Imam Ali a.s. katika vita vyake kwa sababu:

(i) Bwana Mtume s.a.w.w. amesema kwamba hampendi Ali isipokuwa mu'mini, na hamchukii isipokuwa mnafiki.

Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Muslim, 'Kitabul Iman', Mlango wa 'ad-Dalilu Alaa Anna Hubbal Answaar Wa Ali r.a, Minal Iman...' Na kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 141 katika uk. 46-4 wa Juzuu ya Kwanza.

Sasa basi, kama anayemchukia tu huwa mnafiki, jee anayechukua upanga na kumpiga vita huwaje? Jee aliyemlaani na kuamrisha watu wamlaani? Je aliyeuwa watu waliokataa kumlaani? Wote hao nini hukumu yao?

Na kama wanaompenda Imam Ali a.s. ndio mu'mini, jee wale waliojitolea kumtetea na kumkinga na maafa wa vipi? Na kwa nini iwe ni aibu au kosa kwa Shia kuzikubali Hadith zilizopokewa kwa wale waliomtetea Imam Ali a.s., hali Bwana Mtume s.a.w.w. amesema hivyo alivyosema, na isiwe aibu au kosa kwa Sunni kuzikubali Hadith zilizopokewa kwa wapinzani wake? Pengine watetezi wa Sheikh M. al-Khatib watapendelea kutweleza!

(ii) Bwana Mtume s.a.w.w. alimwonya Ammar b. Yasir kwamba atauliwa na tapo (kundi) la waasi'; na inajulikana katika historia kwamba sahaba huyo mtukufu iliuwawa katika Vita vya Siffin mwaka 36H alipokuwa pamoja na Imam Ali a.s. dhidi ya kundi la Muawiya b. Abi Sufyan.

Onyo hilo limetajwa katika uk,114 wa juzuu ya Pili ya Sirat Ibn Hisham; na hata katika uk. 52-53 wa Maisha ya Imam Aly a.s. .cha Sheikh Muhammd Kasim Mazrui, aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

Sasa basi, kama kundi lililomuuwa Ammar r.a.-ni 'kundi la waasi' (kama alivyotabiri Bwana Mtume s.a.w.w.), ni wazi kwamba lile kundi alimokuwamo yeye lilikuwa ni la watiifu; nalo ni lile la Imam Ali a.s. Na kama ni hivyo, kwa nini basi Shia walaumiwe kwa kuzitegemea Hadith zilizopokewa kwa kundi tiifu, wasilaumiwe wale wanaotegemea Hadith zilizopokewa kwa 'kundi la waasi'? Tungependa tuelezwe.

(iii) Bwana Mtume s.a.w.w, aliwaonya wake zake wasibwekewe na mbwa wa Haw'ab; na katika baadhi ya riwaya, alimwelekea mkewe, Mw. Aisha, hasa! Hata palipotokea Vita vya Ngamia (mwaka 36H), ambapo Mw. Aisha (akiwa juu ya ngamia mwenye nywele nyingi, kama alivyotabiri Mtume s.a.w.w.) aliongoza jeshi la kumpinga Imam Ali a.s, alifika mahali hapo paitwapo Haw'ab na akabwekewa na mbwa hao! Papo hapo akakumbuka lile onyo la mumewe (Bwana Mtume s.a.w.w.), na kwa kutambua kwamba hayuko upande wa haki, akataka aachwe arejee alikotoka!

Kisa hicho kimeelezwa katika vitabu vingi vya historia, k.v. Tarikh at-Tabari, al-lqdul Farid, Tarikh Abil Fidaa, na vinginevyo. Hata Sheikh Muhammad Kasim Mazrui, katika uk. 37-38 wa kitabu chake, Maisha ya Imam Aly, amekieleza.          

Kwa hivyo, kutokana na maelezo ya kisa hicho na jinsi Bwana Mtume s.a.w.w. alivyowaonya wake zake nacho, ni dhahiri kwamba kila aliyekuwamo katika kundi lililo bwekewa na mbwa hao, alikuwa katika kundi dhalimu kama ilivyoashiriwa na Bwana Mtume s.a.w.w. katika uk. 283 wa Juzuu ya Pili ya al-

lqdul Farid; uk. 237 wa Juzuu ya Saba ya Majmauz Zawaid; na uk. 334 wa Juzuu ya Kumi na Moja ya Kanzul Ummal.

Kwa hivyo, pale Sheikh M. al-Khatib anaposema (taz. uk. 30 wa kitabu chake) kwamba Shia huzitegemea 'baadhi ya hadithi za watu fulani waliokuwa pamoja na Ali (r.a.) kwenye vita vyake vya kisiasa...' amekusudia vita kamahivyo vya Siffin na Ngamia! Kwa maneno mengine, Shekhe wetu huyo anawalaumu Shia kwa kuzikataa Hadith za watu waliompinga Imam Ali a.s. na kumpiga vita hata baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kusema aliyoyasema! Basi mambo yakifika hapo, tusemeje? Bora mhukumu nyinyi, wasomaji watukufu

Lililo sawa, tukikumbuka maneno ya Bwana Mtume s.a.w.w. juu ya Imam Ali a.s., ni lipi? Ni kupokea Hadith zilizopokewa kwa watu kamaImam Ali a.s. na kundi lake, au zile zilizopokewa kwa wapinzani wake?

Hizo basi, vile vile, ni chache tu kati ya sababu nyingi zilizowafanya Shia wazipe uzito zaidi zile Hadith zilizopokewa kwa wale waliokuwa pamoja na

Imam Ali a.s., na Kuzikataa za wale wapinzani wake. Nyingine tumeziacha kwa kuogopa kukirefusha kitabu hiki.

Kwa nini kuchagua wapokezi

Wala hili la watu fulani kuchagua habari zao kwa wale wanaoaminika zaidi kwao haliko kwa Shia peke yao. Liko kwa madhehebu yote. Kwa mfano;

Ni jambo lijulikanalo, hata kwa wenye ujuzi mdogo, kwamba riwaya inayotegemeka mno ya Imam Malik ni ile ya Ibnul dasim na Ash'hab; lakini ya Abdullah b. al-Hakam na mfano wake huwa haina mashiko kwa wafuasi wa madhehebu hayo. Hali kadhalika tukija kwa Mahanafi; wao hawakubali riwaya ya Abu Hanifa isipokuwa ile iliyosimuliwa na Abu Yusuf na Muhammad b. al-Hasan. Kamakuna riwaya, kinyume cha riwaya ya hao, iliyopokewa kwa al-Hasan b. Ziyad al-Lu'lyi na wenziwe, basi Mahanafi huwa hawaikubali wala hawaitegemei.

Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Mashafi. Wao hutegemea riwaya ya al-Muzani na ar-Rabi' b. Sulayman al-Muradi. Lakini riwaya ya al-Khuzayma na al-Jurumi, na mfano wao; hawazitegemei.

Sasa basi, ikiwa mambo ni hivyo katika madhehebu ya kifiqhi tu, ambayo hushughulika na furuu' (matawi), jee inapokuja kwenye usul (mashina)? Kwa maneno mingine, ikiwa wafuasi wa madhehebu fulani hawakubali riwaya ya Imam wao ila iwe imepokewa kwa mtu anayeaminika kwao, kwa nini Sheikl-M. al-Khatib ataka Shia wapokee Hadith za Bwana Mtumes.a.w.w. kwa watu wasioaminika kwao? Lipi lililo muhimu zaidi kuhakikishwa? La Bwana Mtume s.a.w.w., au la kina Abu Hanifa na Shafi?

Kuswihi sanad

2. Akaendelea kusema (katika huo huo uk. 30):

Wala hawajishughulishi na kuswihi sanad (tegemezo) wala maelezo ya kiilimu! Kwani mara nyingi wanasema kwa mfano: 'Kumepokewa kwa Muhammad bin Ismail kutok kwa baadhi ya watu wetu, kutoka kwa mtu mmoja. kutoka kwake kwamba alisema...!!

Majibu:Si kweli kwamba Shia hawajishughulishi na kuswihi sanad y Hadith. Ukweli ni kwamba, kama ndugu zao Sunni, wanajishughulisha kama tulivyoeleza uk. 8 humu. Kamahawajishughulishi, kwa nini wawe na somo la mustwalahul Hadith [4] ? Kwa nini wawe na somo la al-Jar'h wat Ta'dil [5] ? Kw nini wawe na vigawanyo vya Hadith? Kwa nini wawe na Kutubur Rijal [6] ?

Na ni kwa sababu Shia huchunguza sana uadilifu na kutegemeka kwa watu ambao Hadith za Mtume hutegemezwa kwao ndio ikawa wao hawawatagemei watu kama Abu Hureira, [7] Ka'bil Ahbar [8] , Muawiya b. Abi Sufyan [9] , Abul Ghadiya Yasar b. Sab'i as-Sulamr [10] , Abdulrahman b. Muljam [11] , Imran b. Hittan [12] , Yazid b. Muawiya [13] , na wengineo kama hao ambao hutegemewa na nduguzao, Sunni!

                    

3. Akasema tena (ukurasa huo huo wa 30):

Na vitabu vyao vi tele hadithi ambazo haimkini kuthibitisha uswahihi wazo.

Majibu: Ni imani ya Shia kwamba, katika ulimwengu huu, hakuna kitabu chochote kilicho sahihi chote isipokuwa Qur'ani Tukufu. Vingine vyote, hata visifike kwa ukubwa wa kadiri gani, lazima viwe na ya kweli na ya uwongo ndani yake. Kwa sababu hii ndio ikapokewa kwa Maimamu wa Shia (taz. uk. 3—4humu) kwamba lolote lidaiwalo kwamba limesemwa na wao, na likawa ni kinyume na Qur'ani Tukufu, basi ni uwongo, Na ndio pia ikasemwa, kama tulivyoeleza katika uk. 16 wa kitabu chetu, Shia na Qur'ani, kwamba kati ya Hadith 16199 zilizomo katika al-Kafi (ambacho ni kitabu kikubwa cha Hadith kwa Shia) zaidi ya asilimia hamsini sisahihi.

Kwa hivyo, shekhe wetu M. al-Khatib hapo hakusema lolote jipya ambalo Shia wao wenyewe hawajalisema. La kushangaza ni kwamba alipoandika 'Hadithi kwa Ahlil-sunnah' (taz. uk.29-30wa kitabu chake), hakutaja kwamba na vitabu vyao pia 'vi tele hadith ambazo haimkini kuthibitisha uswahihi wazo'. Au hakulijua hilo?

Kama hakulijua hilo, basi hapa chini twazitaja baadhi tu ya Hadith za aina hiyo; na ni juu ya walio kiswahilisha hicho kitabu chake, kama hawakubaliani na sisi, watukinaishie usahihi wazo.

Kwanza tuanze na zile zinazowahusu mitume wengine wasiokuwa Mtume Muhammad s.a.w.w.:

Za Mitume wengine

1. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alisema kwamba Sulaiman b. Dawud, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alisema: Nitawajamii wake (zangu) sabini usiku; kila mwanamke kati yaoatazaa mtoto wa kiume atakayepigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Akaambiwa: Sema inshallah. Lakini hakusema. Basi akawajamii; lakini hakuzaa yeyote kati yaoisipokuwa mke mmoja tu, tena nusu mtu! Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akasema: Lau angalisema inshallah asingalishindwa, na hajayake ingalitimia.

Hiyo ni Hadith iliyomo katika Sahih Muslim, 'Kitabul Aymaani', Mlango wa 'al-lstithnaa Filyamini Waghayrihaa'. Kuna na Hadith nyingine mbili hapo hapo isipokuwa, badala ya wake sabini kama ilivyo katika Hadith tuliyoitaja hapo juu, zimetaja 'wake sitini' na 'tisini'!

Kwa wale wenye Sahih Muslim kwa Kiingereza, nawatazame Hadithi na. 4066,4067 na 4070 katika uk.880-881 wa Juzuu ya Tatu.

Vile vile Hadith kama hiyo unaweza kuipata katika Sahih Bukhari. 'Kitabu Bad'il Khalqi', Mlango wa 'Wawahabnaa Li Dawuda Sulaymana...'; pia 'Kitabun Nikah', Mlango wa 'Qawlur Rajuli La-atufannal Laylata Alaa Nisaaii';

na 'Kitabul Aymaani Wan Nudhuur', Mlango wa 'al-lstithnaa Fil Aymaani' isipokuwa humo idadi ya wake wa Nabii Sulaiman a.s. imetajwa kuwa 'sabini' na 'tisini' na 'mia'; na wote akawaingilia kwa usiku mmoja!!

Kwa wale wenye Sahih Bukhari kwa Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 635 katika uk. 421 wa Juzuu ya Nne. Hadith Na. 169 katika uk. 122-123 wa Juzuu ya Saba, na Hadith Na. 711 katika uk. 466-467 wa Juzuu ya Nane.

Ewe ndugu yangu! Tafadhali zizingatie kwa makini riwaya zote hizo, na ujiulize: kweli mwanamume, hata awe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaweza kuwaingilia wanawake wengi kama hao kwa usiku mmoja? Na kwa nini awe na uchu hivyo? Ataka kuonyesha nini? Miujiza ya kujamii?! Au jee, inawezekana Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama alivyokuwa Nabii Sulaiman a.s., akatae kusema inshallah hata baada ya kukumbushwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, kamariwaya nyingine isemavyo?

2. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Malaika wa mauti alimjia Musa a.s., akamwambia:

Mwitikie Mola wako. Musa a.s. akalipiga ngumi jicho la Malaika wa mauti, akalikoboa! Malaika akarejea kwa Mwenyezi Mungu s.w.t., akasema: Hakika Wewe umenituma kwa mja Wako ambaye hataki kufa; naye amelikoboa jicho langu! Mwenyezi Mungu akamrejeshea jicho lake, na akamwambia: Rejea kwa mja Wangu, na umwambie: Utakayo ni maisha? Kama wataka maisha, basi weka mkono wako juu ya mwili wa ng'ombe dume. Kadiri ya nywele ambazo mkono wako utazifunika, ndiyo idadi ya miaka utakayoishi: (Musa a.s) akasema: Kisha? (Malaika) akamjibu: Kisha utakufa....

Hadith hiyo, na nyingine kama hiyo, utaiona katika Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Fadhailu Musa a.s.'

Kwa wote wenye tafsiri ya Kiingereza ya kitabu hicho, nawatazame Hadith Na. 5851-5852 katika uk. 1264-1265 wa Juzuu ya Nne.

Pia tazama 'Kitabu Ahaadithil Anbiyaa', Mlango wa 'Wafaati Musa' katika Sahih Bukhari, na Mlango wa 'Man Ahabbad Dafna Fil Ardhil Muqaddasah' katika 'Abwaabil Janaiz.' Na katika tafsiri ya Kiingereza, tazama Juzuu ya Pili, uk. 236-237, Hadith Na. 423; na Juzuu ya Nne, uk. 409, Hadith Na. 619.

Na kwa mujibu wa Juzuu ya Kwanza ya Tarikhul Umami Wal Muluh' ya ibn Jarir at-Tabari, pale palipotaja 'Kifo cha Musa', imepokewa kwa Abu Hureira vile vile kwamba Malaika wa mauti alikuwa akiwajia watu wazi wazi;

mpaka alipomwendea Musa a.s., akampiga ngumi, akamkoboa jicho lake' Ndipo mwishowe, baada ya Musa a.s. kufariki, ikawa huwajia watu kwa uficho!

Haya! Hiyo ndiyo Hadith yenyewe. Jee, ewe ndugu yangu, waionaje? Si vituko hivyo?

Hivi kweli binadamu, hata awe ni mtume wa Mwenyezi Mungu, aweza kumpiga ngumi Malaika aliyepawa mamlaka ya kutoa roho za watu, na alikoboe jicho lake? Kwani Malaika huyo alikwenda kuifanya kazi hiyo kwa hiari yake, au ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu? Bila shaka, ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu. Maana, kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, malaika 'hawamwasi  Mwenyezi  Mungu kwa alilowaamrisha, na hufanya wanayoamrishwa.' (Sura 66:6). Kamailikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu, basi nini kosa la Malaika huyo hata ajeruhiwe hivyo? Kama hakuwa na kosa, basi si wazi hapo kwamba Nabii Musa a.s. alimdhulumu kwa kumpiga bure bure? Jee, Mtume wa Mwehyezi Mungu aweza kufanya dhuluma hivyo? Na jee, badala ya Mwenyezi Mungu kumwadhibu yule aliyemdhulumu mwenzake, ni sawa ampe bahashishi ya kuridhia kumwongezea umri?! Jee, huyo Malaika alipomwendea Musa.a.s., ilikuwa ajali yake ishafika au bado? Kama ilikuwa ishafika, kwa nini akaondoka bila ya kutekeleza wajibu wake hali Mwenyezi Mungu anatwambia katika Qur'ani Tukufu (Sura 7:34) kwamba 'inapowafikia ajali yaohawatachelewa (hata) saa moja, wala hawatatangulia'? Au ndiyo tuseme Musa a.s. ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikiogopa kufa? Hata baada ya kuambiwa na Malaika amwitikie Mola wake? Kweli inawezekana Mtumewa Mwenyezi Mungu awe asi hivyo?

Yote hayo ni maswali muhimu ambayo inataka, ewe ndugu Mwislamu ujiulize.   Na bila shaka majibu yatakayojitokeza, yatakudhihirishia wazi kwamba haiwezekani kuthibitisha usahihi wa Hadith hiyo. Au wale waliomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wataweza kututhibitishia hilo? Kama wataweza, tutashukuru.

3. Imepokewa kwa Abu hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Wana wa Israeli walikuwa na desturi ya kuoga uchi pamoja, wakitazamana nyuchi zao! Lakini Musa a.s. akawa huoga peke yake. (Wana wa Israeli) wakasema: Wallahi! Hakuna kinachomzuia Musa kuogi

pamoja nasi isipokuwa ni kwa sababu ana mshipa! Hata siku moja akaenda kuoga. Akaziweka nguo zake juu ya jiwe. Lile jiwe likakimbia na zile nguo zake! Musa a.s. akalifukuzia huku akisema: Nguo zangu, jiwe! Nguo zangu, jiwe! mpaka Wana wa Israeli wakautazama uchi wa Musa. Wakasema:

Wallahi Musa hana ubaya wowote. Jiwe likasimama baada ya (Musa) kuonekana (uchi wake). Hapo akazichukua nguo zake, na akalipigilia mbali lile jiwel Abu Hureira akasema: Naapa kwamba jiwe lenyewe likawa na kovu sita au saba kwa sababu ya kupigwa na Musa a.s.!

Hadith hiyo, na nyingine kama hiyo, utaiona katika Sahih Muslim kabla ya Hadith mbili tulizozitaja katika Na.2 hapo juu. Na kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na. 5849-5850 katika hiyo hiyo Juzuu ya Nne (uk. 1263-1264).

Katika Sahih Bukhari, Hadith hizo utazipata katika 'Kitabu Bad'il Khalqi' kwenye Mlango ulioko baada ya Hadith ya Khidhr, na katika 'Kitabul Ghusl', Mlango wa 'lghtasala Aryaanan'. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 277 katika uk. 169-170 wa Juzu ya Kwanza, na Hadith Na. 616 katika uk. 407 wa Juzuu ya Nne.

Haya! Bismillahil Jee, ewe ndugu Mwislamu, kabla ya hata kuuliza maswali yetu, waweza kukubali kuwa Hadith hizo ni sahihi? Mwenyezi Mungu aliamrishe jiwe (maana jiwe, kwa hiari yake, halina uwezo wa kufanya hilo) likimbie na nguo za Mtume Wake a.s. ili uchi wake uonekane na watu kwa sababu tu wajue kwamba hana mshipa? Au Mtume wa Mwenyezi Mungu afukuzane na jiwe uchi huku akisema nalo kama kwamba lasikia au laona? Na akilipata alipige, bado akiwa uchi, na watu wakiendelea kumtazama! Jee, Mtume huyo hakuwa na akili ya kubaki pale alipokuwapo na kupigia watu uketele wamletee ngub nyingine? Au jiwe limehiti nini hata lipigwe hali haliwezi kufanya lililofanya isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu?

Na hata kama Nabii Musa a.s. angekuwa na mshipa kweli, ndiyo nini? Ni aibu? Ni ila? Kwani ni aibu Mtume wa Mungu kuwa na maradhi? Kama ni hivyo, jee Nabii Shuaib a.s. hakupotea macho (Sura 12:84) Nabii Ayub a.s. hakuugua (Sura 21:83)? Sasa huo mshipa ungempunguzia nini Nabii Musa utume wake?

Mwisho, jambo la kushangaza ni kwamba Hadith hizo, katika Sahih Musiim, zimo katika mlango wa 'Fadhila za Musa a.s.' Sasa fadhila hapo ni ipi? Ni Nabii Musa a.s. kumpiga ngumi Malaika wa Mwenyezi Mungu na kulikoboa jicho lake? Au ni kuogopa kufa? Au ni kufukuzana na jiwe uchi? Au ni huko kulipiga na kulitia kovu?Twangojea majibu.

Mpaka hapa tushaona baadhi ya Hadith zinazohusu mitume wengine ambazo, kwa maoni ya Shia, 'haimkini kuthibitisha uswahihi wazo.' Sasa tutazame zile zinazomhusu Mtume Muhammad s.a.w w.

Za Mtume Muhammad s.a.w.w.

4. Abdullah b. Burayda alisema kwamba amemsikia Burayda akisema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alitoka kwenda katika baadhi ya vita vyake. Aliporejea, alikuja kijakazi mmoja mweusi. Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa nimeweka nadhiri kwamba, Mwenvezi Mungu akikurejesha salama, nipige dufu mbele zako na niimbe. Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akamwambia: Kama umenadhiria (hivyo), piga. Kamahukunadhiria, usipige. Akawa anapiga. Akaingia Abubakar, naye anapiga. Kisha akaingia Ali, akawa vile vile apiga. Kisha akaingia Uthman;

akaendelea kupiga. Kisha akaingia Umar; akaliweka lile dufu chini ya makalio yake, akalikalia. Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akasema: Hakika Shetani anakuogopa, ewe Umar! Mimi nilikuwa nimekaa, akawa anapiga. Abubakar akaingia, naye anapiga. Kisha akaingia Ali, naye anapiga. Kisha akaingia Uthman, naye anapiga. Hata ulipoingia wewe, ewe Umar, akaliweka dufu(lake)!

Hiyo ni Hadith Na. 3773 katika Mlango Na. 71 wa Sunan at-Tirmidhi. Hadith hiyo vile vile waweza kuiona katika uk. 353 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad.

Sasa, kama kupiga dufu na kuimba ni haramu (kamatuambiwavyo mara nyingi humu mwetu Afrika Mashariki), basi vipi itakuwa ni halali kwa nadhiri na Bwana Mtume s.a.w.w. aruhusu? Jee, inaingia akilini kwamba Bwana Mtume s.a.w.w. aweza kuhalalisha haramu k.m. kamari au kunywa pombe au uzinifu, kwa kuwekea nadhiri? Hasha!

Kama ni halali, au tujaalie ni haramu iliyohalalishwa kwa kuwekea nadhiri, basi kwa nini huyo mjakazi alifiche dufu lake chini ya makalio yake? Jee, halali hufichwa? Na kwa nini ifichwe alipoingia Umar tu? Kwani yeye peke yake ndiye aliyekiijua halali na haramu kuliko hao wengine? Kuliko hata Mtume s.a.w.w.? Na kwa nini Bwana Mtume s.a.w.w. aseme: Hakika Shetani anakuogopa, ewe Umar? Kwa nini, kama ni halali, amwite mwanamke huyo Shetani? Jee, mtu anayefanya kitendo cha halali huitwa 'Shetani'?

Mwisho, jee inaingia akilini Shetani kumwogopa Umar, na kumkimbia, na asimwogope Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. bali aendelee kupiga dufu

mbete zake na kumghania? Kweli inaweza Hadith hii kuwa sahihi? Twangojea majibu.

5. Imepokewa kwa Hudhaifa kwamba Mtume s.a.w.w. alifika kwenye jalala la watu fulani, akakojoa kwa kusimama!  'Kisha akasema aletewe maji. Nikamletea, akatawadha.

 Hiyo ni Hadith iliyomo katika 'Kitabul Wudhuu', Mlango wa 'al-Bawli Qaaimaa', katika Sahih Bukhari. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 224, uk. 144 wa Juzuu ya kwanza.

Katika kuieleza Hadith kama hiyo, Hammad b. Abi Sulaiman amesema kwamba Bwana Mtume s.a.w.w. 'alipanua miguu yake' akakojoa kwa kusimama! Taz. Musnad Ahmad, uk. 246 wa Juzuu ya Nne.

Jee, ewe ndugu Mwislamu, yawezekana Mtume wa Mwenyezi Mungu kusimama jalalani, apanue miguu yake kama mnyama (ambapo itambidi asege nguo zake), na akojoe hivyo? Mwache Bwana Mtume s.a.w.w., mtu wa kawaida tu, mwenye heshima yake na murua wake, aweza kufanya hivyo?

6. Imepokewa kwa Humaid b. Nafi' kwamba alimsikia Zainab binti Abi Salama akisema: Nimemsikia Ummu Salama, mke wa Mtume s.a.w.w., akimwambia Aisha: Wallahi, sipendi kuonekana na kijana ambaye ashaacha kunyonya. (Aisha) akasema: Kwa nini? Sahla binti Suhail alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w., akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungul Mimi naona (hasira) katika uso wa Abu-Hudhaifa pindi anapoingia Salim (nyumbani kwetu). Mtume s.a.w.w. akamwambia: Mnyonyeshe.(Sahla) akasema: (Yeye) ana ndevu!  Lakini (Mtume s.a.w.w.) akamwambia (tena): Mnyonyeshe, na (hasira) iliyomo juu ya uso wa Abu Hudhaifa itaondoka. (Sahla) akasema: (Nikamnyonyesha) na wallahi, sikuona (hasira yoyote) juu ya uso wa Abu Hudhaifa.

Hadith hii imo katika Sahih Muslirn. 'Kitabur Radhai', Mango wa''Radha'il Kabir'. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na. 3428 iliyoko uk. 742 wa Juzuu ya Pili.

Katika Hadith nyingine [14] iliyopokewa kwa Mw, Aisna, katika Mlango huo huo, inatweleza kwamba, alipoambiwa amnyonyeahe, Sahla aliuliza: Nitamnyonyeshaje naye 'ni mtu mzima? Mtume t.a.w.w. akakanya.

Akasema: Kwa hakika najua kwamba yu mtu mzima [15] ... Na kwa riwaya ya Ibn Umar: Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akacheka.

Na katika Hadith nyingine, katika Mlango huo huo tena, iliyopokewa kwa Ibn Abu Mulaika, [16] yeye (Ibn Abu Mulaika) akasema: Nimekaa mwaka (mzima) au karibu yake siitoi Hadith hii, kwa kuogopa.

Ewe ndugu Mwislamu! Hebu zisome tena riwaya zote hizo, na ujiulize: Kweli Mtume Muhammad s.a.w.w., au mtu yeyote yule, aweza kumwamrisha mke wa watu atoe ziwa lake iliamnyonyeshe mtu mzima mwenye ndevu zake? Na mwanamke anapoonyesha kushangazwa na amri hiyo, Mtume s.a.w.w. akenye/ acheke na kusema kwamba yeye ajua kuwa huyo yu mtu mzima? Hebu fikiria kama ni wewe uliyeamrishiwa mke wako hivyo, ungehisi vipi? Na kwa nini Ibn Abu Mulaika ajizuie kuitoa Hadith hiyo kwa mwaka mzima kamasi kwa sababu ya kuona aibu? Hivi Ibn Abu Mulaika alikuwa na haya zaidi kuliko Mtume s.a.w.w? Kweli wasaidizi wa Sheikh M. al-Khatib wanaweza kututhibitishia usahihi wa Hadith hii? Tunangojea majibu yaoinshallah.

Baadhi ya wanazuoni, ili isieleweke vibaya Hadith' hii, wamejaribu kutoa maelezo. Wengine [17] wamesema kwamba, sio amnyonyeshe ziwa, bali atoe tu hayo maziwa yake na amnyweshe! Na wengine [18] wamesema kwamba ni kumnyonyesha hasa; lakini hiyo ilikuwa ni amri maalum kwa huyo Salim peke yake! Lakini yote maelezo mawili hayo hayakubaliki, kwa sababu zifuatazo:

(i) ,neno ardhi'ihi lililotumiwa katika Hadith hizi ndilo lile lile alilotumiliwa mamake Nabii Musa katika Sura 28:7, na kwa maana hiyo hiyo ya kunyonyesha.

                                  

Kwa hivyo kulifasiri neno hilokwa maana ya 'mnyweshe' ni kulinyumbua mno [19] . Hapo, haliwezi kuwa na maana hiyo asilan!

(ii) kwa sheria ya Kislamu, mtu hawi maharimu ya mwanamke kwa kunywa maziwa yake nje ya ziwa lake. Huwa tu hivyo kwa kulinyonya hasa;na 

(iii) kama amri hiyo ilikuwa ni kwa Salim peke yake, mbona Mw. Aisha haonekani kuwa ameielewa hivyo? Maana tunaposoma Muwatta'a ya Imam Malik katika 'Kitabur Radha'i', Mlango wa 'Maa jaa-a Fir Radha'ati Ba'adal Kibari', tunaona kwamba Mw. Aisha, alipokitaka mtu awe maharimu yake, alikimwamrisha [20] dadake, Ummu Kulthum binti Abubakar, na binti ya ndugu yake (yaani Abdulrahman) wamnyonyeshe!! Jee, hiyo si fedheha nyingine?

Sasa tuzitazame Hadith zinazomhusu Mwenyewe Mwenyezi Mungus.w.t.

Za Mwenyezi-Mungu s.w.t.

7. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka alimwambia Adam kwa sura Zake, urefu wake ukiwa dhiraa sitini. Alipokwisha kumwumba, alimwambia: Nena kawaamkie kundi lile—nalo lilikuwa ni kundi la malaika Iimekaa—usikilize watakujibu nini. Maana hayo ndiyo yatakayokuwa maamkizi yako na maamkizi ya kizazi chako; Akaenda, akasema: Amani iwe juu yenu! Nao wakasema: Amani iwe juu yako, na rehema za Mwenyezi Mungu. Wakaongeza 'na rehema za Mwenyezi Mungu'. Kwa hivyo, kila atakayeingia Peponi ataingia kwa sura za Adam, urefu wake ukiwa dhiraa sitini. Na watu hawakwacha kupungua (urefu wao) baada yake, mpaka sasa.

Hadith hii unaweza kuiona katika Sahih Bukhari; Hadith ya kwanza katika 'Kitabul Isti'dhan'. Vile vile utaiona katika 'Kitabul Jannati Wasifatu Naiimihaa', Mlango wa 'Yadkhulul Jannata Aqwaamun Af-idatuhum Mithlu Af-iidatit Twayr' katika Sahih Muslim.

Kwa Kiingereza, tazama Hadith Na. 246, uk. 160-161 wa Juzuu ya Nane ya Sahih\ Bukhari; na Hadith Na. 6809, uk. 1481 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

Hata hivyo, kabla hatujasema lolote kuhusu Hadith hii, tafadhali ilinganishe na yale maneno ya MWANZO 1:27 katika Biblia yasemayo: Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.                  

Jee, inawezekana sura za Adam ziwe ndizo sura za Mwenyezi Mungu hali Qur'ani Tukufu inatwambia kwamba Yeye hana mfano? Hivi kweli Hadith hii ni sahihi?

lli Hadith hii isiwe imemfananisha Mwenyezi Mungu na kiumbe Chake, na kwa hivyo ionekane ni sahihi, baadhi ya wanazuoni husema kwamba dhamiri 'Zake' katika neno: alimwumba Adam kwa sura Zake, yarejea' kwa Adam. sio kwa Mwenyezi Mungu! Yaani Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa :   sura za Adam! Lakini taawili hiyo haikubaliki; maana tunapozitazama Hadithi  nyingine, zilizopokewa kwa yuyo huyo Abu Hureira, tunaona kwamba dhamiri "   hiyo inamrejelea

Mwenyezi Mungu, sio Adam! Kwamfano:

     (i) ukitazama uk. 491 wa Juzuu ya Kumi ya Irshaadus Saari, sherehe ya   Sahih Bukhari, utamwona Ihn Hajar al-Qastwalani anavyoirejeza dhamiri hiyo kwa Mwenyezi Mungu (sio Adam) kwa kuitaja Hadith nyingine iliyopokewa kwa Abu Hureira isemayo: Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa sura   za Rahman (Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema).  Na hiyo ndiyo sababu ikapokewa tena Abu Hureira kwamba

       (ii) 'Mmoja wenu anapopigana na ndugu yake najiepushe na (kumpiga)

uso; maana Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa sura Zake.' Taz. Hadith Na. 6325, uk. 1378 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Mustim (kwa Kiingereza). Na kwa Kiarabu, tazama 'Kitabul Birri Was-Swilati Wal Adab',        Mlango wa 'an-Nahyi An Dharbil Wajhi'.

 Hadith Na. (ii) itakufunukia zaidi unapoilinganisiia na:i:le

   (iii) ile iliyoko uk. 434 wa Juzuu ya Pili ya Musnad Ahmad isemayo: Yeyote ,  kati yenu anapompiga (mwenzake) najiepushe na uso: wala asiseme: Mwenyezi Mungu aufanye' mbovu uso wako, na uso wa anayeushabihi uso wako! Maana Mwenyezi Mungu amemwumba Adam kwa sura Zake. Jee, si wazi hapo kwamba sababu ya sisi kuzuiwa tusipigane nyuso, na tusigoane, ni kwamba nyuso zetu zimeshabihiana na uso wa Mola wetu?

Jee, Hadith hiyo bado yaweza kuwa ni sahihi?

Pia itakufunukia zaidi unapoilinganisha na ile iliyotajwa na Ibn Qutayba [21] katika uk. 280 wa kitabu chake, Ta'wilu Mukhtalafil Hadith, isemayo kwamba:

(iv) Musa a.s. alilipiga jiwe la Wana wa Israele likabubujika (maji). Akasema: Kunyweni, enyi punda, Mwenyezi Mungu akamteremshia wahyi (kumwambia): Umewatukana viumbe ni liowaumba kwa sura Zangu kwa kuwafananisha na punda...

Jee, siwazi hapo kwamba Hadith zote tulizozitaja hapo juu zathibitisha kwamba Adam aliumbwa kwa sura za Mola wake?! Bila shaka! Na hivyo ndivyo walivyoelewa hata wale waliofasiri Sahih Bukhan na Sahih Muslim;

maana wanapofasiri neno alaa (kwa sura Zake) huliandika in His image (kwa H kubwa, sio ndogo) ambavyo ndivyo inavyoandikwe kwa Kiingereza inapokusudiwa Mwenyezi Mungu.

Hiyo ni Hadith ya kwanza inayomhusu Mwenyezi Mungu, na ambayo, haiwezekani kuwa sahihi. Sasa tuiangalie nyingine:

8. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba watu walimwambia (Mtume s-a.w.w.): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee tutamwona Mola wetu Siku ya Kiyama? (Mtume s.a.w.w.) akasema: Jee mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku wa arbatashara [22] , panapokuwa hakuna mawingu? Wakasema: La, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Jee mnashida yoyote ya kuliona jua, panapokuwa hakuna mawingu? Wakasema: La, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Basi na nyinyi mtamwona Yeye Siku ya Kiyama kama hivyo (mnavyouona mwezi na jua). Mwenyezi Mungu atawakusanya watu Siku ya Kiyama, aseme: Yeyote aliyekuwa akikiabudu kitu, nakifuate. Basi aliyekiliabudu jua, atalifuata jua; aliyekiuabudu mwezi, ataufuata mwezi; na aliyekiwaabudu mashetani, atawafuata mashetani. Ubaki umma huu (wa Kiislamu) ukiwa na wanafiki (miongoni' mwao). Hapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atawajia kwa sura isiyokuwa sura Yake wanayoijua.   Aseme: Mimi ndiye Mola wenu.   Nao waseme: Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu na wewe. Tutakaa hapa mpaka Mola wetu atujie. Atakapotujia Mola wetu, tutamjua. Hapo, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atawajia kwa sura Yake wanayoijua. Aseme:

Mimi ndiye Mola wenu. Nao waseme: Wewe ndiye Mola wetu. Hapo wamfuate; na sirati (njia) itandikwe juu ya Moto. Mimi (Mtume s.a.w.w.), na umma wangu, niwe wa kwanza kupita; na siku hiyo hakuna atakayesema isipokuwa Mitume, na dua ya Mitume, siku hiyo itakuwa: Ewe Mola! Tupe salama, tupesalama...

Hadith hiyo utaipata katika Sahih Muslim, 'Kitabul Iman', Mlango wa 'lthbaatu Ru'yatil Mu'minana Rabbahum Fil Akhira'. Kwa tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na. 349, iliyoko uk. 115 wa Juzuu ya kwanza.

Na Hadith kama hiyo utaipata katika Sahih Bukhari, 'Kitabu Abwaabi Swifatis Swalaa; na 'Kitabur Riqaaq', Mlango wa 'as-Swiraatwi Jisri Jahann-ama Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 770 katika Juzuu ya kwanza (uk. 427-430);

NaHadith Na. 577 katika Juzuu ya Nane (uk. 374-375).. ;Na katika Hadith nyingine iliyopokewa kwa Abu Said al-Khudri, inasema:

'Baadhi ya watu, katika zama za Mtume s.a.w.w., walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee, tutamwona Mola wetu Siku ya Kiyama? Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akasema: Ndiyo, na akaongeza: Jee, mna shida yoyote ya kuliona jua adhuhuri, panapokuwa hapana mawingu? Na jee, mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku wa arbatashara, panapokuwa hapana mawingu? Wakasema: La, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Naye akasema: Hamtakuwa na shida ya kumwona Mwenyezi Mungu aliyetukuka Siku ya Kiyama kama msivyo na shida ya kuuona mwezi na jua.  Itakapokuwa Siku yaKiyama mtangazaji atatangaza: Kilaumma naukifuate kile walichokuwa wakikiabudu. Hapo hatobakia yeyote aliyekuwa akiabudu masanamu na mawe badala ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika (na mawi) isipokuwa ataangukia Motoni. Wabaki wale wema na waovu waliokimwabudu Mwenyezi Mungu, na baadhi ya Watu wa Kitabu. Hapo waitwe Mayahudi waambiwe: Nyinyi mlikuwa mkiabudu nini? Waseme: Tulikimwabudu Uzayr Mwana wa Mungu! Waambiwe: Mwasema uwongo; Mwenyezi Mungu hakupata kuwa na mke wala mtoto. Mnataka nini (sasa)? Watasema^ Tuna kiu, ewe Mola wetul Tunyweshe. Hapo wataelekezwa (upande fulani), waulizwe: Mbona hamchoti? Ndipo wasukumizwe Motoni (wautambue) kuwa ni mangati, [23] unakulana wenyewe kwa wenyewe, na wao waangukie humo. Kisha waitwe Wakristo. Waulizwe: Mlikuwa mkiabudu nini? Waseme: Tulikuwa tukimwabudu Masihi Mwana wa Mungu! Waambiwe:

Mwasema uwongo; Mwenyezi Mungu hakupata kuwa na mke wala mtoto. Mnataka nini (sasa)? WatasemaTuna kiu, ewe Mola wetu! Tunyweshe. Hapo wataelekezwa (upande fulani), waulizwe: Mbona hamchoti? Ndipo wasukumizwe Motoni (wautambue) kuwa ni mangati, unakulana wenyewe kwa wenyewe, na wao waangukie humo. Hata panapokuwa hapakubaki yeyote isipokuwa yule aliyekimuabudu Mwenyezi Mungu aliyetukuka, awe

.mwema au mwovu, ndipo Bwana wa viumbe vyote s.w.t. awajie kwa sura weliyokimjulia, aseme: Mnatafuta nini? Kila umma naukifuate kile walichokuwa wakikiabudu. Waseme: Ewe Mola wetu! Tulijitenga na watu duniani, japokuwa tulikuwa na haja nao sana; hata hivyo, hatukuandamana nao. Hapo (Mwenyezi Mungu) aseme:- Mimi ndiye Mola wenu. Na wao waseme: Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu na wewe! Hatumshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote. Watasema hivyo mara mbili au tatu hata wengine wakaribie kugeuka (na kurejea). (Mwenyezi Mungu) aulize: Jee kuna alama yoyote baina yenu na Yeye ambayo kwayo mtamjua? Watajibu:

Ndio. Hapo pafunuliwe muundi; na hapatabaki yeyote aliyekimsujudia Mwenyezi Mungu kwa hiari yake isipokuwa Mwenyezi Mungu atamruhusu kusujudu. Wala hapatabakia yeyote aliyekisujudu kwa kuogopa (watu) au kujionyesha isipokuwa Mwenyezi Mungu ataufanya mgongo wake kuwa tabaka moja; kila akitaka kusujudu, ataangukia mgongo wake.  Kisha watainua vichwa vyao, na Yeye atarudia sura Yake waliyomwonea mara ya kwaza! Awaambie: Mimi ndiye Mola wenu. Nao waseme: Wewe ndiye Molawetu...

Hiyo ni Hadith ya tatu, katika Sahih Muslim, baada ya ile tuliyoitaja kabla hapo juu. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 352 iliyoko uk. 117-119 wa Juzuu ya kwanza.

Na katik Sahih Bukhari, Hadith kama hjyo utaiona katika 'Kitabut Tafsir', Mlango wa 'lnnallaha Laa Yadhlimu Mithqaala Dharratin'.KwaKiingereza, ni Hadith Na. 105 katika Juzuu ya Sita (uk. 85-87).

Jee, Hadith hizo zaweza kuwa sahihi? Hadith zinazosema kwamba tutamwona Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama kama tunavyouona mwezi na jua panapokuwa hakuna mawingu! Swali hapa ni: vipi tutaweza kumwona hiyo bila ya Yeye kuwa na umbo? Na vipi ataweza kuwa na umbo bila ya kuwa na mipaka? Na jee, tunaweza kuamini kuwa ana sifa hizo na tukabaki kuwa Waislamu?

Au vipi Mwenyezi Mungu atatujia kwa sura mbalimbali—tunayoijua na tusiyoijua? Kwani ana sura ngapi? Na hiyo Yake hasa ikoje?! Na jee Mwenyezi Mungu ana muundi wenye alama? Yote hayo ni maswali yanayojitokeza katika Hadith hizo; na ni muhali kuyajibu bila ya kuingia kufuruni. Kwa hivyo haiwezekani Hadith hizo kuwa ni sahih ila ikiwa wasaidizi wa SheikhM.al-Khatibwatatuthibitishiahilo!

"9. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Mola wetu Aliyetukuka kila usiku, inapobaki thuluthi ya mwisho ya usiku huo, hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa, akasema: Ni nani atakayenilingana, nimwitikie? Ni nani atakayeniomba ni mpe? Ni nani atakayeniomba maghfira, nimghufirie?

Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Bukhari, 'Kitabud Da'awaat' Mlango wa 'ad-Du'a Nisful Layli'; vile vile katika 'KitabuI-'Kusufi', Mlango wa 'ad-Du'a Was Swalatu Min Akhiril Layli'. Na katika Sahih Muslim utaiona katika 'Kitabus Swalat', Mlango wa 'at Targhibu Fid Du'ai Wadh Dhikri Ri Akhiril Layli'.

Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 333 iliyoko uk. 225 wa Juzuu ya Nane ya Sahih Bukhari, na pia Hadith Na. 246 iliyoko uk. 136 wa Juzuu ya Pili. Na katika Sahih Muslim, ni Hadith Na. 1656 iliyoko uk. 365 wa Juzuu ya Kwanza

Na katika Jami'ut Tirmidhi, Mlango Na. 324 'Fii Nuzulir Rabbi Tabaraka Wata'ala llas Samaaid Dunyaa Kullu Laylatin' n wa Hadith (Na.445) isemayo:

Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Mola wetu Aliyetukuka kila usiku hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa, inapokuwa thuluthi ya kwanza ya usiku imepita akasema: Mimi ndimi Mfalme. Ni nani atakayenilingana, nimwitikie? Ni nani atakayeniomba, nimpe? Ni nani akakae niomba maghfira, nimghufirie? Basi huwa vivyo hivyo mpaka alfajiri iangaze.

Na katika Musnad Ahmad, Juzuu ya Kwanza (uk. 120) mna Hadith isemayo kwamba imepokewa kwa Ali a.s. kwamba amemsikia Mtunne wa Mwenyez Mungu s.a.w.w. akisema: Lau kwamba si kwa kuhofia kuwapa mashaka, umma wangu, basi ningaliwaamrisha kupiga mswaki wakati wa kila swala, na ningaliiakhirisha Ishaa ya mwisho mpaka thuluthi ya kwanza ya usiku. Maana inapopita thuluthi ya kwanza ya usiku, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa; na hubaki huko mpak alfajiri inapochomoza.

Hizo basi ni baadhi tu ya Hadith zinazohusu kushuka kwa Mwenyezi Mungu mpaka uwingu wa chini kabisa! Jee, ni sawa Mwenyezi Mungu kuharma kutoka mahali pamoja mpaka pengine? Hiyo sisifa ya mwili? Jee, Mwenye Mungu ni mwili?

Kisha isitoshel Ati Mwenyezi Mungu hubaki kwenye huo uwingu wa chini kabisa mpaka alfajiri inapochomoza!

Hilo,bila shaka, halikubaliki.   Maana kama tutalikubali, itamaanisha kwamba Mola wetu siku zote yuko kwenye uwingu huo. Maana, kwa mfano, alfajiri inapochomoza huku kwetu Afrika Mashariki, huwa bado haija wachomozea wenzangu walioko upande wa magharibi. Na inapowachomozea wao baada ya saa hivi, huwa bado haijawachomozea wengine walioko magharibi yaozaidi. Na ni vivyo hivyo mpaka iturejelee'sisi huku. Kwa hivyo kila wakati humu ulimwenguni huwa kuna jimbo lenye alfajiri yake. Na hili linamaanisha kwamba nyakati zote hizo Mwenyezi Mungu huwako kwenye huo uwingu wa chini kabisa. Jee, ni wakati gani ambao hupanda na kurejea kwenye uwingu iliko Arshi Yake?

Jee, baada ya maelezo na maswali yetu hapo juu, bado wale waliokiswahilisha kitabu cha Sheikh M. al-Khatib watatwambia kuwa Hadith hizo ni sahihi? Ukowapi hapo usahihi wake? Tunangojea majibu yao!

10. Katika 'Kitabul Iman' ya Sahih Muslim, mna Hadith k.w.k. zinazozungumzia Mwenyezi Mungu kucheka! Moja ni ile Hadith ndefu iliyomo katika Mlango wa 'Akhiru Ahlil Jannati Dukhulan al-Jannah' ambayo ina kipande kisemacho hivi..... Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atasema: Jee, hukutoa ahadi na mithaki kwamba hutaomba chochote kingine zaidi ya nilichokupa? Ole wako, ewe mwana wa Adam! U haini uliojel Naye atasema: Ewe Mola wangu! Sitakuwa mwovu wa viumbe Vyako! Hapo ataendelea kumlingana Mwenyezi Mungu mpaka Mwenyezi 'Mungu Aliyetukuka amcheke! Basi atakapochekwa na Mwenyezi Mungu, atamwambia: Ingia Peponi...'

Ya pili ni ile iliyomo katika Mlango wa 'lthbatus Shafa'a...' yenye kipande kisemacho: '...Mwenyezi Mungu atamwambia: Nenda uingie Peponi, maana utapata mfano wa dunia na mara kumi mfano wake, au utapata mara kumi mfano wa dunia.... (Yule mtu) atasema: Jee, unanifanyia maskhara, au unanicheka na Wewe ndiye Mfalme?...'

Ya tatu ni ile iliyomo katika Mlango wa 'Akhiru Ahlin Nari Khurujan' ambayo kipande chake cha mwisho chasema hivi; '...Ibn Mas'ud akacheka. Akasema: Mbona hamniulizi ninacheka nini? Wakasema: Unacheka nini? Akasema: Hivyo ndivyo alivyocheka Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w, (Masahaba) wakamwuliza: Unacheka nini, awe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: (Ninacheka) kwa ajlli ya kicheko cha Mola wa viumbe vyota alipoambiwa (namtaka Pepo); Jee, unanifanyia Dhihaki, na Wewe ni Mola' wa viumbe vyote? Naye ataeema: Mimi sikufanyii stihizai, ila ni Mweza wa kila kitu.

Yeyenne ni ile iliyomo katika mlango huo huo, yenye kipande kisemacho:

... Kisha atatujia Mola wetu, aseme: Mnamngojea nani? Watasema: Tunamngojea Mola wetu. Atasema: Mimi ndiye Molawenu. Naowatasema: Mpaka tukutazame! Hapo (Mwenyezi Mungu) atawatokea huku anacheka! Na ataondoka nao huku wakimfuata; na kila mtu miongoni mwao, awe mnafiki au mu'mini, atapawa nuru...'

Mbali nyingine nyingi tulizoziacha.

Hizo tulizozitaja hapo juu, katika Sahih Muslim kwa Kiingereza, ni Hadith Na.349(uk. 115-116), Na. 359 (uk, 120-121), Na. 361 (uk. 121-122), na Na. 367 (uk. 123-124) wa Juzuu ya Kwanza.

Jee, Hadith kama hizo zinaweza kuthibitishwa usahihi wazo? Mwenyezi Mungu kucheka?

Bila shaka hilohaliwezekani. Maana tunapozungumzia kucheka huwa tunazungumzia kukunjua uso na kufunua mdomo kwa namna ambayo, ghalibu, meno ya mchekaji yatadhihiri, na sauti ya kicheko chake kutokeza. Ikiwa ni hivyo basi, jee Mwenyezi Mungu anao uso na mdomo? Ukoje? Na jee, meno Yake yakoje? Astaghfirullah!

11.Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Pepo ilihojiana na Moto.   Moto ukasema: Mim nimeheshimiwa kwa kupokea wenye kiburi, na majabari.   Na Pepo ikasema: Nina nini mimi, hakuna aliayeniingia isipokuwa madhaifu na watu wa chini na wasiojiweza? Hapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka akaiambia Pepo: Wewe ndiye Rehema Yangu. Kwawe humrehemu nimtakaye kati ya waja Wangu. Akauambia na Moto: Hakika wewe ni adhabu. Kwawe humwadhibu nimtakaye kati ya waja Wangu. Na kila mmoja kati yenu atajaa Moto hautajaa mpaka Mwenyezi Mungu aweke mguu Wake (juu yake), nao useme: Basil Basi! Hapo utajaa na ushikamanishwe.

Hiyo ni Hadith unayoweza kuiona katika Sahih Bukhari, 'Kitabu Tafsiril Qur'ani, Mlango wa 'Surat Qaf'; na katika Sahih Muslim, 'Kitabul Jannati Waswifati Naimihaa Wa Ahlihaa', Mlango wa 'Jahannam A'adhanallahu

Minhaa'. Kwa Kiingereza, tazama Hadith Na. 373 iliyoko uk. 354 wa juzuu ya Sita ya

Sahih Bukhari; na Hadith Na. 6819 iliyoko uk. 1483 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

Jee, wale waliomsaidia Sheikh M. al-Khatib katika kukiswahilisha kitabu chake wanaweza kututhibitishia usahihi wa Hadith hiyo hapo juu? Mwenyezi

Mungu ana mguu? Umekaaje mguu huo? Tena auweke juu ya Moto ndipo Moto ujae! Nini hekima yake? Jee, Moto kuingiwa na wenye kiburi na majabari ni jambo la kujivunia? Kwa fadhila gani walizonazo watu hao, hali wao siku hiyo watakuwa chini ya waliochini (Sura 95:5)?

Au vipi Pepo itawadhania wale walioiingia kwamba ni watu wa chini na madhaifu hali wao ni 'miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha-manabii, masiddiki, mashahidi na watu wema' (Sura 4:69)?

12. Abu Hureira amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alinishika mkono wangu akasema: Mwenyezi Mungu aliumba mchanga siku ya Jumamosi. Akaumba na majabali humo siku ya Jumapili. Akaumba na miti siku ya Jumatatu. Akaumba vya kuendeshea maisha siku ya Jumanne. Akaumba na nuru siku ya Jumatano. Akaeneza wanyama humo siku ya Alkhamisi. Akamwumba na Adam a.s. baada ya alasiri, siku ya Ijumaa;

kiumbe cha mwisho, katika saa ya mwisho kati ya saa za Ijumaa: baina ya alasiri mpaka usiku.

Hadith hiyo utaipata katika Sahih Muslim, 'Kitabu Swifatil Qiyamati Waljannati Wannari', Mlango wa 'lbtidaul Khalqi Wakhalqi Adam a.s,' Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 6707 (uk. 1462) katika Juzuu ya Nne;

Sasa hapa tushike lipi? La Qur'ani kwamba mbingu na ardhi ziliumbwa kwa siku sita, au la Hadith hiyo kwamba ardhi (na vinginevyo visivyokuwa ardhi) viliumbwa kwa siku saba? Na jee, hapo zikiumbwa mbingu na ardhi, siku hizo zikijulikana kwa haya majina (ya Jumamosi na Jumapili) tuyajuayo sisi leo? Kila siku ilikuwa ni saa 24? Jua na mwezi vilikuwa vishaumbwa? Na jee, siku moja kwa Mwenyezi Mungu ni kama hii yetu, au ni 'kama miaka elfu' (Sura 22:47)?

Jee, usahihi wa Hadith hiyo unaweza kuthibitishwa? Tunangojea tuone.

Sasa tutazame ya vioja vingine.

Na vioja vingine

12. Abu Hureira amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Mtu mmoja alikuwa akimchunga ng'ombe aliyekuwa amembebea mizigo. Mara yule ng'ombe akamgeukia na kusema: Mimi sikuumbiwa hili (la kubeba mizigo) bali nimeumbiwa konde (kunyweshea mashamba). Watu wakasema kwa mshangao na fazaa: Subhanallahl Ng'ombe anasema?! Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akasema: Mimi naamini hilo, na Abubakar na Umar. Akasema Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alisema: Mchunga mmoja alikuwa akichunga mifugo yake.

Mara akaja mbwa mwitu akamchukua mbuzi wake mmoja. Yule mchunga akamfukuza yule mbwa mwitu mpaka akampokonya (yule mbuzi wake) Mbwa mwitu akamgeukia (yule mtu) na kumwambia: Ni nani atakayemwokoa (mbuzi wako) siku ambayo hapatakuwa na mchunga isipokuwa mimi?!  Hapo watu wakasema: Subhanallah!  Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w naye akasema: Mimi naamini hilo; mimi na Abubakar na Umar.

Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Bukhari, 'Kitabu Fadhailis Swahaba', Mlango wa 'Law Kuntu Muttakhidhan Khalilan'; na katika Sahih Muslim, 'Kitabu Fadhailis Swahaba' vile vile, Mlango wa 'Fadhaili Abibakar as-Siddiq'.

Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 15 iliyoko uk. 10-11 wa Juzuu ya Tano ya Sahih Bukhari; na Hadith Na. 5881 iliyoko uk. 1276-1277 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

Haya! Mambo hayo! Ng'ombe na mbwa mwitu wanazungumza Kiarabu' Tangu lini? Kwa kuthibitisha jambo gani hapo? Pengine tutaelezwa hapo tutakapojibiwa, na tuthibitishiwe usahihi wa Hadith hiyo inshallah.

13.Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Ayub alikuwa akioga uchi. Mara akaangukiwa na nzige wa dhahabu! Ayub akawakusanya katika nguo yake. Mola wake akamlingana: Ewe Ayub! Jee sikukukwasisha [24] na unavyoviona? Akasema: Kwani; kwa Utukufu Wako! Lakini mimi sikwasiki na baraka Zako.

Hadith hiyo utaipata katika Sahih Bukhari. 'Kitabul Ghusli', Mlango wa 'at-tasattur Fil Ghusli Indan Nasi Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 277 iliyoko uk. 170 wa Juzuu ya Kwanza.

Hapa hatukatai kwamba Mwenyezi Mungu hashindwi kufanya miujiza yoyote—ya kuumba nzige wa dhahabu, na zaidi ya hilo. Lakini ni sharti pawe na dharura ya kuleta miujiza kamahiyo. Jee, hapo pa Nabii Ayub a.s. kuoga faraghani peke yake, palikuwa na dharura gani ya kuteremshiwa nzige wa dhahabu? Awafanye nini?              

Hizo basi, tulizozidondoa hapo juu (uk. 16-32), ni baadhi tu ya Hadith nyingi zilizomo katika vitabu vya Kisunni (na nyingi yazo tumezitoa katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim) ambazo haiwezekani kuthibitisha usahihi wazo. Maana zinapingana na Qur'ani Tukufu, Hadith nyingine za Mtume s.a.w.w. zilizo sahihi, na hata akili. Kwa hivyo, sio vitabu vya Kishia peke yake vilivyo na Hadith kama hizo, bali hata vya Kisunni ni hali kadhalika.

Mwisho

Kutokana na majibu na maelezo yetu yaliyomo humu, tumeona kwamba wote wawili (Sunni na Shia) wanakubaliana kwamba:

(i) Hadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. ndilo chimbuko la pili la sheria ya Kiislamu, na ndizo zenye kuifasiri Qur'ani Tukufu. Yeyote asiyeamini hivyo ni kafiri;

(ii) haifai kukhalifu hukumu za Hadith yoyote iliyosihi kutokamana na Bwana Mtume s.a.w.w. Kufanya hivyo ni kukufuru vile vile;

(ili) katika kuthibitisha usahihi wa Hadith yoyote, ni lazima pathibitishwe ukweli na uadilifu wa kila mmoja kati ya wapokezi wake. Na hilo huwezekana tu kwa kupitia fani makhususi ya Mustwalahul Hadith.  Fani hii inakubaliwa na pande zote mbili, na kila upande umeitungia vitabu na kuvichapisha; na

(iv) Hadith yoyote iliyopokewa kwa mwongo au mtu asiyejulikana, haifai kukubaliwa.

Hata hivyo, pamoja na hadhari yote iliyochukuliwa kuhakikisha kwamba ni hadith sahihi tu zitakazochapishwa vitabuni:

(v) baadhi ya Hadith, ambazo haiwezekani kuthibitisha usahihi wazo, zimepenya na kuchapishwa katika vitabu vya pande zote mbili. Lakini ni uamuzi wa wote kwamba popote pale inapothibiti kwamba Hadith kamahizo si sahihi, basi zikataliwe.

Kwa hivyo, ikiwa mambo ni kama hivyo, kwa nini Sunni wazuiwe kukurubiana na kuelewana na ndugu zao,Shia? Ikiwa Wakatholiki na Waprotestanti, pamoja na kuwa Biblia zao ni tofauti, wanaweza kuku rubiana na kuelewana, kwa nini sisi Waislamu tusiweze hali yanayotuunganisha ni mengi zaidi kuliko yale yanayotutenganisha??

Majibu ninawaachia nyinyi, ndugu Waislamu, wa madhehebu yote.

Inshallah, katika kitabu kijacho, tutatazama msimamo wa Shia juu ya masahaba wa Mtume Muhammad s.a.w.w.


[1] Sheikh M. al-Khatib ameviita vita hivi "vya kisiasa"! Kwa kweli si vya kisiasa. Ni vya kidini hasa kamainavyoeleweka waziwazi kutokana na baadhi tu ya Hadith za Bwana Mtume s.a.w.w. tulizozidokeza humu (uk.12-13).

[2] Hadith ya "vizito viwili" imenakiliwa katika vitabu vingi sana vya Kisunni vya Hadith k.v. Sunan at- Tirmidhi, Kanzul Ummal, Mishkatul Masaabih, Majma'ui Zawaid, na vinginevyo ambavyo nafasi hapa haituruhusu kuvitaja vyote. Kwa wale wanaotaka maelezo kamili, watayapata katika kanda za hotuba zangu za "Majlis ya Muharram ya mwaka 1410" ziwezazo kupatikana kwa: Bilal Mualim Mission, S.L.P. 82608, Mombasa, Kenya.

[3] Makusudio hapa ni Imam Ali b. Abi Twalib a.s

[4]  Hii ni fani inayohusika na vigawanyo mbalimbali vya usahihi na udhaifu wa Hadith.

[5] Hili ni somo linalohusika na kuchunguza sifa na ila za wapokezi wa Hadith.

[6] Hivi ni vitabu ambavyo kwavyo hujulikana habari za wapokezi wa Hadith.

[7] Huyu ndiye aliyepokea Hadith nyingi za Mtume «.a.w.w. kuliko sahaba yeyote. Jumla ya Hadith zilizopokewa kwake ni 5374. Ukilinganisha idadi hiyo. na ile idadi ya Hadithi zilizopokewa. kwa mfano, kwa Khalifa Abubakar (142) au kwa Khalifa Umar (kiasi 50) au kwa Imam Ali (kiasi 50) au hata Mw. Aisha (2210). utaweza kuelewa kwa nini Shia wana wasiwasi na riwaya za bwana huyu—hasa inapokumbukwa kwamba muda aliowahi kukaa na Bwana Mtume s.a.w.w., tukimpa muda mrefu sana, ni miaka mitatu tu maana yeye alisilimu miaka mitatu tu kabla ya Bwana Mtume kufariki dunia! Pia unapotambua kwamba nyingi sanaya Hadith tulizozitaja katika uk. 16—31 humu zimepokawa kwake! Mbali sababu nyingine kadha wa kadha.

[8] Kabla ya kusilimu kwake, alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kiyahudi. Yeye hakuwa sahaba maana hakusilimu zama za Bwana Mtume s.a.w.w. Alisilimu zama za Ukhalifa wa Umar b. al-Khattab. Kupita kwake, Hadith nyingi za uwongo (israili'yyaat) zimepokewa!

[9] Huyu ndiye aliyempinga Imam Ali a.s. pale alipochaguliwa kuwa Khalifa, akasababisha roho za sahaba wengi sana wakubwa wakubwa kutilifu...Yeye ndily aliyetoa amri ya Imam Ali as. alaaniwe katika hotuba za Ijumaa na Idd, akawa huwapa tunzo wanaofanya hivyo au kuwaadhibu wanaokataa! Ndiye yeye aliye anzisha Ufalme katika Uislamu, baada ya Imam Ali a.s. kuuwawa, kwa kuwalazimisha waislaam wambai mwanawe, Yazid, kuwa Khalifa baada yake. Na ni  yeye aliemshawishi  mke wa Sayyidnal Hasan a.s. amtilie sumu kumuua! Mbali visa vya sahaba wengine k.w.k. walio uliwa na yeye.

[10] Huyu ndiye aliyemuaa Ammar b. Yasir ambae chake tumekidokeza katika uk. 12 1   humu.

[11] Huyu ndiye aliye muua Imam Ali as.

[12] Huyu alisherehekea kuuwawa kwa Imam Ali a.s. kwa kutunga shairi la kumsifu Ibn Muljim aliyetajwachini ya kidokezo Na.11 hapo juu.

[13] Huyu ni mtoto wa Muawiya ambaye habari zake zimeelezwa chini ya kidokezo Na. 9 hapo juu. Yeye ndiye aliyebandikwa kimabavu na babake kuwa Khalifa wa Sita (kwa kweli, ni Mfalma wa Pili) wa Waislamu japokuwa alikijulikana kuwa mlevi, mzinifu. mbali maovu mengine aliyokuwa nayo! Na ni yeye pia aliyepanga njama za Imam Hussein a.s. kuuwawa na kukatwa kichwa chake Hadithi zisizo sahihi ziko hata kwa Sunni

[14] Yaani Hadith Na. 3424.

[15] Neno la Kiarabu katika Hadith hii, tulilolifasiri kwa "mtu mzima", ni rajulun kabir. Jambo la kushangaza hapa ni kwamba, katika uk. 741 wa tafsiri ya Kiingaraza, neno hilolimefasiriwa kwa a young man badala ya a big man au a grown-up man au an adult. Hata kwenye kichwa cha Hadith hiyo, neno lililotumiwa ni a young (boy)l Sijui kosa hiloni kwa kughafllika au ni makusudi Allahu a'lamu!

[16] Hiyo ni Hadith Na. 3426 katika uk. 742.

[17] Kama Sheikh Abdul Hamid Siddiqi katika kidokezo Na. 1905 kilichoko mwisho wa uk. 741 wa hiyo Juzuu ya Pili ya Kiingereza ya Sahih Muslim.

[18] Kama Sheikh Muhammad as-Zurqani katika uk. 91 wa Juzuu ya Tatu ya sherehe yake ya Muwatta'a Walik.

[19] 19. Hata katika tafsiri ya Kiingereza ya Muwatt'a Malik badala ya kulifasiri neno hilo kwa neno suckle, kama lilivyofasiriwa ndivyo katika Sahih Mus/im, limefasiriwa kwa feed him with their milk. (Tai. mstari wa tano kutoka juu, uk. 275) Kufanya hivyo. kwa yeyote anayejua Kiingereza, ni kulinyumbua mno!

[20] Taz. Hadith Na. 1242 katika uk. 274 wa tafsiri yake ya Kiingereza.

[21] Kama ilivyonakiliwa katika uk.61 wa Abu Huraira ya Imam Abdul Husein Sharafuddin al-Musawi

[22] Huu ni usiku wa tarehe kumi na nne ambapo mwezi hung'ara sana.25

[23] Pia huitwa'mlenga'au'mazigazi'. Kwa Kiingereza mirage. 26

[24] "Kumkwasisha mtu" ni kumfanya atosheke na kitu fulani. 32