HADITHI YA SHUKA

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

KIMETARJUMIWA NA : SALIM NG’ANG’A MWEGA

DIBAJI

Kama vile yanavyobadilika yaliyomo ulimwenguni, vile vile maumbile ya binadamu hupatwa na mabadiliko. Tofauti zipatikanazo baina ya binadamu na binadamu mwingine husababisha tofauti pia katika tabia na nyenendo, kwa mfano katika unyenyekevu, kiburi, usahaulifu, kumbukumba nzuri, hisia ya kutaka hifadha, n.k.

Kwa hivyo, ikiwa katika jamii baadhi ya itikadi, desturi na sheria, hazina misingi thabiti, na ikiwa watu wanaosimamia jamii hii sio waamimifu, bila shaka zitapatwa na mabadiliko na ulegevu, na hata mwishowe kutoweka kabisa. Hili ni jambo la hakika lililothibiti kwa njia ya uchunguzi na ujuzi.

Ili kuepuka hatari hii na kuuhifadhi uislamu –
(dini tukufu ya milele) – Mtume Mtukufu (s.a.w.a.) aliwaachia maswahaba wake maandiko matukufu yenye mfumo mzima wa maisha pamoja na viongozi waaminifu, ili kuwaongoza katika njia iliyonyooka. Aliwausia waislamu kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran tukufu) na Ahlul bait (kizazi chake kitukufu) na kuwasihi kutoviacha kamwe vitu hivi viwili. Huu wasia wake mtukufu umenakiliwa na wapokezi wa hadithi wa kisunni na wa kishia. Ulamaa wengi wa madhehebu tofauti tofauti wameelezea ya kwamba hii ni hadithi ya Mtume Mtukufu (s.awa) iliyo sahihi.

Mtume Mtukufu (s.awa.) amesema ya kwamba:

(اني تارك فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلّوا بعدي احدهما اعظم من الآخر كتاب الله حبل ممدود من السماء الى الارض و عترتي اهل بيتي و لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروا كيف تخلفوني فيهما)[1]

“Hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kitukufu kuliko cha pili navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu (ambacho ni) kamba iliyonyooshwa toka binguni hadi ardhini na kizazi changu, (ambacho ni) Ahlu baiti wangu na wala havitatengana kamwe hadi vitakapo nikuta kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni vile mtakavyo vitendea baada yangu. (Sunanut Tirmidhi hadithi ya 3788.)

1) QURAN TUKUFU

Quran tukufu ndio chemchemi ya misingi na mafunzo ya kiislamu na uthibitisho wa kuwa kwake Kitabu cha Allah (ambacho ni muujiza) na pia ni uthibitisho wa utume wa Mtume Mtukufu wa uislamu. Quran tukufu ni neno la Allah, lililofunuliwa kwa Mtukufu Mtume(s.awa.) na kwa kupitia kwake liliwafikia wanadamu. Quran tukufu inawapa wanadamu ujuzi wa kielimu na kivitendo, ambao kwa kuutumia ipasavyo, binadamu anaweza kufanikiwa kuchuma mema, amani na mafanikio humu duniani na huko akhera. Lengo hasa la Quran tukufu ni kuwaongoza wanadamu ili kupata maendeleo na mafanikio.

Inawapa wanadamu elimu kwa njia nzuri, nyepesi na ya dhahiri, kuhusiana na itikadi zilizo sahihi, tabia njema na matendo mema ambayo ni muhimu sana katika maisha ya kila mmoja, na vile vile katika maisha ya jamii.

Allah (S.B.) amesema katika Quran tukufu.

((ونزّلنا عليك الكتاب تبياناً لكل شيء و هدىً و رحمة و بشرى للمسلمين))

“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kielezacho kila kitu na ambacho ni uongofu na rehma na khabari za furaha kwa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu) waislamu” (AN NAHL: 89)

2) AHLUL BAIT

“Ahlul bait” kilugha kama ilivyo katika kamusi ya kiarabu ni jamii yote ya nyumba” k.m. mke, mwana, binti na watumwa. Yaani wote wanao mtegemea mwenye nyumba. Wengine wamepanua zaidi maana yake ili kuwaingiza pia, jamaa wa karibu k.m. mama, baba, dada, kaka na watoto wake ami na shangazi (dada ya mama) pamoja na watoto wao. Lakini kulingana na Quran tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.a), hizi tafsiri mbili hazitumiki kwa “Ahlul bait” wa Mtume (s.a.w.a).

Kulingana na hadithi za Mtume (s.a.w.a), ambazo zimenakiliwa na wapokezi wengi, “Ahlul bait” ni neno tukufu linalomaanisha watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume, ambao ni Imam Ali (a.s.) Bibi Fatima(a.s.), Imam Hasan (a.s.), na Imam Husein (a.s.). Hawa ndio wale watu watano watukufu – (Ahlul kisaa, yaani watu wa shuka) – ambao, hakuna shaka kuwa ndio “Ahlul bait”.

Kwa hivyo, Jamii nyingineyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.a) haiingii katika maana, ya ‘Ahlul bait’. Hata Bibi Khadija (a.s.) mke wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a). aliye heshimika sana, na aliye kuwa mama yake Fatima (a.s.), binti mpendwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a.). Vile vile, Ibrahim mwanawe Mtukufu Mtume (s.a.w.a.), pamoja na cheo chake kitukufu, haingii katika ‘Ahlul bait’.

Bila shaka kulingana na ukweli wa hadithi nyingi ambazo zimekuwa zikinakiliwa na wapokezi wa hadithi mara kwa mara watu watano watukufu – (Yaani watu wa shuka) – na Maimamu tisa watukufu, ambao wanatokana na kizazi cha Imam Husein (a.s.) wanaingia katika ‘Ahlul bait’. Na kwa Ibara nyingine ni kuwa “Ahlul bait” ni kumi na wanne, katika idadi, na ndio wanaoitwa “Maasumin kumi na wanne”.

Kulingana na aya ya utakaso (Suratul Ahzab 33;33) ‘Ahlul bait’ wana cheo kitukufu cha ucha Mungu na umaasumu (utakasifu), kwani hawakuwahi kutenda dhambi na wala hawatendi.

Katika hadithi ifwatayo, Mtukufu Mtume ameonyesha utukufu wa ‘Ahlul bait juu ua maswahaba wake wote; na kwa maneno na vitendo vyake alifafanua maana ya aya ya utakaso. Alisema ya kwamba “Mimi na Ahlul bait wangu tumetakaswa kutokakana na madhambi.” Aliwatangazia watu haya akiwa msikitini. Kila alipokuwa akienda msikitini kwa sala ya alfajiri alikuwa akipita nyumbani kwa Imam Ali (a.s.) na Bibi Fatima (a.s.) na kusema;

((السلام عليكم اهل البيت و رحمة الله و بركاته – الصلاة – رحمكم الله – انما يريد الله ليذهب عنكم الرجس اهل البيت و يطهركم تطهيراً – انا حرب لمن حاربتم، انا سلم لمن سالمتم))

“Amani ya Allah, rehma na baraka zake ziwashukieni, enyi ‘Ahlul bait’. (Wakati wa) swala (umewadia), Allah awarehemuni”. Kisha alikuwa akifuatilizia kwa aya ya Quran, “Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa.” Kisha aliongeza, “Mimi ni mwenye kumpiga vita kila anayekupigeni vita (na) mimi ni mwenye kumpa amani kila anayekupeni amani” (Majmauz Zawaid, Juzu yaq, na Tafsirus Suyuti, Juzu ya 5).

Katika Sahihu Tirmidhi, Musnadu Ahmad, Musnadu Tialasi, Mustadrakus Sahihain, Asadul Ghaba na katika tafsiri za Tabari, Ibn kathir na Suyuti, Anas bin Malik Khazraji (aliyedai kuwa alibaki katika uswahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a) kwa muda wa miaka kumi. Alifariki huko basra akiwa na umri wa miaka tisiini) amenakiliwa akisema ya kwamba, Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alikuwa akipita karibu na mlango wa Fatima Zahra (a.s.) kwa muda wa miezi sita akisema. “Enyi watu wa nyumba! Wakati wa swala umewadia!!” kisha aliongeza kusema, “Enyi watu wa nyumba!…..”.

Hawa ndio “Ahlul bait” ambao Imam Shafii, mmoja kati ya maimamu wanne wa dhehebu la kisunni katika kuwasifu amesema. “ Enyi ‘Ahlul bait’ wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a), kuwapenda ni faradhi iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu katika Quran tukufu. Kwa hakika yatosha kuwa fakhari kubwa kwenu kwamba asiye waswalia nyinyi (katika swala yake), basi

swala yake hubatilika!!” (Almuhaddithul Qummi, Alkuna wal Alqab, Shablanji, Nurul Absar, ukurasa wa 104).

Vile vile Zamakhshari na Razi, katika tafsiri zao za Quran tukufu wameinakili hadithi ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a.) ifwatayo;

Amesema (s.a.w.a.):

((من مات على حب آل محمد مات شهيداً، الا و من مات على حب آل محمد مات مغفوراً له، الا و من مات على حب آل محمد مات تائباً، الا و من مات على حب آل محمد مات مؤمناً مستكمل الايمان...... الا و من مات على بغض آل محمد مات كافراً، الا و من مات على بغض آل محمد لم يشم رائحة الجنة.))

“Anayekufa akiwapenda Aali (kizazi) zake Muhammad hufa shahidi. Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa akiwa amesha samehewa (madhambi yake). Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa (kifo cha) aliyetubia. Tambueni kuwa anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad, hufa akiwa muumini, aliyekamilika imani (yake) ……… Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad, hufa akiwa kafiri. Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad hatoipata harufu ya pepo” (Zamakhshari, Tafsirul Kash-shaf juzu ya 4, tafsiri ya sura Ash-shura, 42; 32, na Fakhrud Din Arrazi, Tafsirul Kabir, Juzu ya 26, Ukurasa wa 165 – 166).

Tutamalizia kwa misitari ya shairi moja la mwanashairi maarufu wa kiirani aitwaye Sa’adi.

سعدى اكر عاشقى كنى و جوانى **** عشق محمد(ص) بس است وآل محمد

“Ewe Sa’adi! Ikiwa watamani kupata furaha ya mapenzi na ukamilifu wa maisha usiokuwa na kikomo, basi yakutosha kumpenda Muhammad na Aali zake Muhammad”.

Hakuna malipo bora na furaha zaidi ya humu duniani kuliko kuwapenda kidhati “Ahlul bait” na kuwafwata kwa vitendo.

بِسم الله الرَّحمن الرَّحيم

عِنْ جَابِرِ بنِ عِبْدِاللهِ الاَنْصَارِيِّ عَنْ فَاطِمَةَ الزَّهْرَاءِ عَلَيْها السَّلامُ بِنْتِ رَسُوْلِ اللهِ(صلى الله عليه وآله وسلم) قَالَ سَمِعْتُ فَاطِمَةَ(عليها السلام) اَنَّهَا قَالَتْ دَخَلَ عَلَيَّ اَبِيْ رَسُوْلُ اللهِ(ص) فِي بَعْضِ الاَيَّامِ فَقَالَ السَّلاَمُ

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Jabir bin Abdullah Al-ansari anahadithia kutoka kwa Bibi Fatimatuz Zahra (a.s.) ya kwamba, “Nilimsikia Fatima (a.s.) akisema ya kwamba”; Siku moja baba yangu (mpendwa) Mtume wa Allah, alinizuru nyumbani kwangu na kusema;

“Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Fatima” Nami nikamjibu

عَلَيْكِ يَا فَاطِمَةُ فَقُلْتُ وَعَلَيْكَ السَّلاَمُ قَالَ اِنِّي اَجِدُ فِيْ بَدَنِيْ ضُعْفاً فَقُلْتُ لَهُ اُعِيْذكَ بِاللهِ يِا اَبَتَاهُ مِنَ الضُّعْفِ فَقَالَ يَا فَاطِمَةُ إئتِيْنِيْ بِالْكِسَآءِ الْيَمَانِيِّ فَغَطّيْني به فَاَتَيْتُه بِالْكِسَاءِ الْيَمَانِيِّ فَغَطَّيْتُه بِه وَ صِرْتُ اَنْظُرُ اِلَيْهِ وَ اِذَا وَجْهُهُ يَتَلأْلأُ كَاَنَّهُ الْبَدْرُ فِيْ لَيْلَةِ تَمَامِهِ وَكَمَالِهِ فَمَا

“Nawe pia amani ya Allah iwe juu yako”.

Kisha akasema; “(Mwanangu) ninahisi mwili wangu ni dhaifu”

Nikamwambia; “Allah Akulinde kutokana na udhaifu, ewe baba”.

Akasema, “Ewe Fatima, niletee ile shuka itokayo Yemen, na unifinikie, kwayo”.

Basi nikamletea ile shuka ya Yemen na kumfunika kwayo”.

Nilipokuwa nikimwangalia niliona kuwa uso wake unameremeta, kama mwezi katika usika wa (mwezi) kumi na tano

كَانَتْ اِلاَّ سَاعةً وَّ اِذَا بِوَلَدِيَ الْحَسَنِ قَدْ اَقْبَلَ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكِ يَا اُمَّاهُ فَقُلْتُ وَعَلَيْكَ اَلسَّلاَمُ يَا قُرَّةَ عَيْنِيْ وَ ثَمَرَةَ فُؤَادِيْ فَقَالَ يَا اُمَّاهُ اِنِّيْ اَشَمُّ عِنْدَكِ رَائِحَةً طَيِّبَةً كَاَنَّهَا رَائحَةُ جَدِّيْ رَسُوْلِ اللهِ فَقُلْتُ نَعَمْ اِنَّ جَدَّكَ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَاَقْبَلَ الْحَسَنُ نَحْوَ الْكِسَاءِ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكَ يَا جَدَّاهُ

Baada ya muda mfupi mwanangu Hasan (a.s.) aliingia na kunisalimu : “Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa)” nami nikamjibu, “Amani ya Allah, pia, iwe juu yako ewe kiburudisho cha macho yangu! na tunda la moyo wangu!”

Akasema, “Ewe mama, hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya baba yangu, Mtume wa Allah (Amani ya Mwenyezi iwe juu yake)”.

Nikamwambia, “Na’am, hakika babu yako yuko chini ya ile shuka”.

Basi Hasan (a.s.) aliikaribia ile shuka, na kusema, “Amani ya Allah, iwe juu yako, ewe babu!

يَا رَسُوْلَ اللهِ اَتَاْذَنُ لِيْ اَنْ اَدْخُلَ مَعَكَ تَحْتَ الْكِسَاءِ قَالَ وَ عَلَيْكَ السَّلامُ يَا وَلَدِيْ وَ يَا صَاحِبَ حَوْضِيْ قَدْ اَذِنْتُ لَكَ فَدَخَلَ مَعَهُ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَمَا كَانَتْ اِلاَّ سَاعَةً وَّ اِذَا بِوَلَدِيَ الْحُسَيْنِ قَدْ اَقْبَلَ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكِ يَا اُمَّاهُ فَقُلْتُ وَ عَلَيْكَ اَلسَّلاَمُ يَا قُرَّةَ عَيْنِيْ وَثَمَرَةَ فُؤَادِيْ

ewe Mtume wa Allah. Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka niwe pamoja nawe?”

Naye akamjibu, “Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe mwanangu!, ewe mwenye kuimiliki hodhi yangu (ya kauthar siku ya Qiyama) nimekuruhusu”.

Basi akaingia chini ya shuka pamoja naye.

Baada ya muda mfupi kupita, naye mwanangu, Husein (a.s.) akaingia na kunitolea salamu. “Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa)”

Nami nikamjibu , “Amani ya Allah pia, iwe juu yako, ewe mwanangu! Ewe kiburudisho cha macho yangu! Na tunda la moyo wangu!”.

فَقَالَ لِيْ يَا اُمَّاهُ اِنِّيْ اَشَمُّ عِنْدَكِ رَائِحَةً طَيِّبَةً كَاَنَّهَا رَائحَةُ جَدَّيْ رَسُوْلِ اللهِ فَقُلْتُ نَعَمْ اِنَّ جَدَّكَ وَ اَخَاكَ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَدَنى الْحُسَيْنُ نَحْوَ الْكِسَاءِ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكَ يَا جَدَّاهُ يَا رَسُوْلَ اللهِ اَتَاْذَنُ لِيْ اَنْ اَدْخُلَ مَعَكُمَا تَحْتَ الْكِسَاءِ فَقَال وَ عَلَيْكَ السَّلامُ يَا وَلَدِيْ

Akaniambia, “Ewe mama! Hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya babu yangu, Mtume wa Allah”.

Nikamjibu, “Naam, babu yako na ndugu yako wako chini ya ile shuka”.

Basi, Husein akaikaribia ile shuka na kusema; “Amani ya Allah, iwe juu yako ewe uliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu (kuwa Mtume wake). Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka, niwe pamoja nanyi”.

Akasema, “Amani ya Allah, pia iwe juu yako ewe mwanangu! Ewe

وَ يَا شَافِعَ اُمَّتِيْ قَدْ اَذِنْتُ لَكَ فَدَخَلَ مَعَهُمَا تَحْتَ الْكِسَاءِ فَاَقْبَلَ عِنْدَ ذلِكَ اَبُو الْحَسَنِ عَلِيُّ بْنُ اَبِيْ طَالِبٍ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكِ يَا بِنْتَ رَسُولِ اللهِ فَقُلْتُ وَ عَلَيْكَ اَلسَّلاَمُ يَا اَبَا الْحَسَنِ وَ يَا اَمِيرَالْمُؤْمِنِيْنَ فَقَالَ يَا فَاطِمَةُ اِنِّيْ اَشَمُّ عِنْدَكِ رَائِحَةً طَيِّبَةً كَاَنَّهَا رَائحَةُ اَخِيْ وَ ابْنِ عَمِّيْ رَسُوْلِ اللهِ

muombezi wa umma wangu (mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama). Nimekuruhusu”.

Basi akainga chini ya shuka, (akawa) pamoja nao.

Wakati huo huo, Abul-Hassan Ali bin Abi Talib (a.s.) akaingia na kutoa salamu, “Amani ya Allah iwe juu yako ewe binti ya Mtume wa Allah!”.

Nami nikamjibu, “Amani ya Allah, pia, iwe juu yako, ewe babake Hasan! Ewe Kiongozi wa waumini!”

Akasema “Ewe Fatima, hakika ninaipata harufu nzuri sana kutoka kwako kana kwamba ni harufu ya ndugu yangu na binami yangu, Mtume wa Allah”.

فَقُلْتُ نَعَمْ هَا هُوَ مَعَ وَلَدَيْكَ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَاَقْبَلَ عَلِيٌّ نَحْوَ الْكِسَاءِ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ عَلَيْكَ يَا رَسُوْلَ اللهِ اَتَاْذَنُ لِيْ اَنْ اَكُوْنَ مَعَكُمْ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَقَالَ لَهُ وَ عَلَيْكَ السَّلامُ يَا اَخِي وَ وَصِيِّي وَ خَلِيْفَتِيْ وَ صَاحِبَ لِوَآئِي قَدْ اَذِنْتُ لَكَ فَدَخَلَ عَلِيٌّ تَحْتَ الْكِسَاءِ ثُمَّ اَتَيْتُ نَحْوَ الْكِسَاءِ وَ قَلْتُ اَلسَّلاَمُ

Nikamwanibia “Na’am, yuko pamoja na wanao chini ya ile shuka”.

Basi, Ali akaikurubia ile shuka na kutoa salamu, “Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah, je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?”

Akamjibu, “Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe ndugu na wasii wangu na khalifa wangu, na mbebaji wa bendera yangu, nimekuruhusu”.

Basi Ali akaingia chini ya shuka, kisha mimi nami nikaikurubia ile shuka na kusema, “Amani ya Allah iwe juu yako ewe baba (mpendwa), ewe Mtume

عَلَيْك يَا اَبَتاهُ يَا رَسُوْلَ اللهِ اَتَاْذَنُ لِيْ اَنْ اَكُوْنَ مَعَكُمْ تَحْتَ الْكِسَاءِ قَالَ لَهُ وَ عَلَيْكِ السَّلامُ يَا بِنْتِيْ وَ يَا بَضْعَتِيْ قَدْ اَذِنْتُ لَكِ فَدَخَلْتُ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَلَمَّا اكْتَمَلْنَا جَمِيْعاً تَحْتَ الْكِسَاءِ اَخَذَ اَبِيْ رَسُوْلُ اللهِ بِطَرَفَيِ الْكِسَاءِ وَ اَوْمَىءَ بِيَدِهِ الْيُمْنى اِلَى السَّمَاءِ وَ قَالَ اَللّهُمَّ اِنَّ هؤُلاَءِ اَهْلُ بَيْتِيْ

wa Allah, Je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?”.

Akajibu, “Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe binti yangu, na ewe kipande cha mwili wangu, nimekuruhusu”.

Basi nikaingi chini ya shuka.

Tulipokuwa tumekusanyika sote chini ya shuka, babangu mpendwa, alizishika ncha mbili za ile shuka na kuuinua mkono wake wa kulia, akiulekeza binguni na kusema;

“Ewe Allah! Hawa ndio Ahlul bait wangu, wasiri

وَخَاصَّتِيْ وَحَامَّتِيْ لَحْمُهُمْ لَحْمِيْ وَ دَمُهُمْ دَمِيْ يُؤْلِمُنِيْ مَا يُؤْلِمُهُمْ وَ يَحزُنُنِيْ مَا يَحزْنُهُمْ اَنَا حَرْبٌ لِّمَنْ حَارَبَهُمْ وَ سِلْمٌ لِّمَنْ سَالَمَهُمْ وَ عَدُوٌّ لِّمَنْ عَادَاهُمْ وَ مُحِبٌّ لِّمَنْ اَحَبَّهُمْ اِنَّهُمْ مِّنِّيْ وَ اَنَا مِنْهُمْ فَاجْعَلْ صَلَوَاتِكَ وَ بَرَكَاتِكَ وَ رَحْمَتَكَ وَ غُفْرَانَكَ وَ رِضْوَانَكَ عَلَيَّ وَ عَلَيْهِمْ وَ

wangu na wasaidizi wangu. Mwili wao ni mwili wangu, damu yao ni damu yangu. Huniumiza kinachow- aumiza na hunihuzunisha kinacho wahuzunisha. Ninampiga vita kila ananyewapiga vita, na ninampa amani kila anayewatunuku amani.

Mimi ni adui kwa mwenye kuwafanyia uadui, na humpenda yule awapendaye. Hakika wao wametokana nami, nami nimetok- ana nao. Basi niteremshie amani yako, baraka zako, rehma zako, msamaha wako, na radhi yako, mimi pamoja na wao. Na uwaondolee uchafu na kuwataka sa kabisa kabisa”.

اَذْهِبْ عَنْهُمُ الرَّجْسَ وَ طَهِّرْهُمْ تَطْهِيْراً فَقَالَ اللهُ عَزَّ وَجَلَ يَا مَلاَئِكَتِيْ وَ يَا سُكَّانَ سَمَاوَاتِيْ إِنِّيْ مَا خَلَقْتُ سَمَاءً مَّبْنِيَّةً وَّ لاَ اَرْضاً مَّدْحِيَّةً وَّ لاَ قَمَراَ مُّنِيْراً وَّلاَ شَمْساً
مُّضِيْئَةً وَّ لاَ فَلَكاً يَّدُوْرُ وَلاَ بَحْراً
يَّجْريْ وَلاَ فُلْكاً يَّسْرِيْ اِلاَّ فِيْ مِحَبَّةِ هؤُلاَءِ الْخَمْسَةِ الَّذِيْنَ هُمْ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَقَالَ الاَمِيْنُ

Basi, Mwenyezi Mungu, Mshindi na Mtukufu Akasema “Enyi malaika wangu! Enyi wakazi wa mbingu zangu! Hakika mimi sikuiumba mbingu madhubuti wala ardhi iliyotandaa, wala mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuangaza, wala sayari yenye kuzunguka, wala bahari yenye mwendo wa mawimbi, wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa kuwapenda hawa watano, walioko chini ya shuka”.

Hapa, malaika mkuu, Jibrail akasema, “Ewe Mola

جَبْرَائِيْلُ يَا رَبِّ وَ مَنْ تَحْتَ الْكِسَاءِ فَقَالَ عَزَّ وَجَلَّ هُمْ اَهْلُ بَيْتِ النُّبُوَّةِ وَ مَعْدِنُ الرِّسَالَةِ هُمْ فَاطِمَةُ وَ اَبُوْهَا وَ بَعْلُهَا وَ بَنُوْهَا فَقَالَ جَبْرَائِيْلُ يَا رَبِّ اَتَاْذَنُ لِيْ اَنْ اَهْبِطَ اِلى الاَرْضِ لاَكُوْنَ مَعَهُمْ سَادِساً فَقَالَ اللهُ نَعَمْ قَدْ اَذِنْتُ لَكَ فَهَبَطَ الاَمِيْنُ جَبْرَائِيْلُ وَ قَالَ اَلسَّلاَمُ

wangu! Na ni nani walioko chini ya shuka?”

Allah, Mshindi na Mtukufu akamwambia, “Hao ni watu wa nyumba ya utume, na asili ya ujumbe.

Wao ni Fatima na babake na mumewe na wanawe”.

Jibrail (a.s) akasema, “Ewe Mola wangu! Je unaniruhusu kuteremka ardhini ili niwe wa sita pamoja nao?”.

Allah Akamjibu na kusema, “Na’am nimekuruhusu”.

Jibrail (a.s) akateremka ardhini na kusema, “Amani

عَلْيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ اَلْعَلِيُّ الاَعْلى يَقْرَئُكَ السَّلاَمَ وَ يَخُصُّكَ بِالتَّحِيَّةِ وَ الاكْرَامِ وَ يَقُوْلُ لَكَ وَ عِزَّتِيْ وَ جَلاَلْي اِنِّيْ مَا خَلَقْتُ سَمَاءً مَّبْنِيَّةً وَّ لاَ اَرْضاً مَّدْحِيَّةً وَّ لاَ قَمَراَ مُّنِيْراً وَّلاَ شَمْساً مُّضِيْئَةً وَّ لاَ فَلَكاً يَّدُوْرُ وَلاَ بَحْراً يَّجْريْ وَلاَ فُلْكاً يَّسْرِيْ اِلاَّ لاَِجْلِكُمْ وَ مَحَبَّتِكُمْ وَ قَدْ اَذَنَ لِيْ

ya Allah, iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah. Mkuu wa wakuu Anakutolea salamu, na kukustahi na kukutukuza, na Anakujulisha ya kwamba “Naapa kwa Ushindi na Utukufu wanga ya kwamba sikuiu- mba bingu madhubuti, wala ardhi iliyotandaa wala, mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuzunguka, wala bahari yenye mawimbi wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa ajili yenyu na mapenzi yenyu”.

اَنْ اَدْخُلَ مَعَكُمْ فَهَلْ تَاْذَنُ لِيْ يَا رَسُولَ اللهِ فَقَالَ رَسُوْلُ اللهِ وَعَلَيْكَ السَّلاَمُ يَا اَمِيْنَ وَحِيِ اللهِ اِنَّهُ نَعَمْ قَدْ اَذِنْتُ لَكَ فَدَخَلَ جَبْرَائِيْلُ مَعَنَا تَحْتَ الْكِسَاءِ فَقَالَ لاَبِيْ اِنَّ اللهَ قْدْ اَوْحى اِلَيْكُمْ يَقُوْلُ اِنَّمَا يُرِيْدُ اللهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ اَهْلَ الْبَيْتِ وَ يُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيْراً فَقَالَ عَلِيٌّ لاَبِيْ

Na ameniruhusu kuingia pamoja nanyi. Basi, ewe Mtume wa Allah, unaniruhusu kuingia?”

Mtume wa Allah (s.a.w.a.) akasema, “Amani ya Allah, pia, iwe pamoja nawe, ewe mwaminifu juu ya wahyi (ujumbe) wa Allah, na’am nimekuruhusu.”

Basi Jibrail (a.s) naye akaingia nasi chini ya shuka na kumwambia babangu, (mpendwa). “Hakika Allah amewateremshia wahyi, na kusema, “Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya utume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa”.

Ali (a.s.) akamwambia babangu

يَا رَسُوْلَ اللهِ اَخْبِرْنِيْ مَا لِجُلُوسِنَا هذَا تَحْتَ الْكِسَاءِ مِنْ الْفَضْلِ عِنْدَ اللهِ فَقَالَ النَّبِيُّ(صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَ الِهِ) وَ الَّذِيْ بَعَثَنِيْ بِالْحَقِّ نَبِيّاً وَّ اصْطَفَانِيْ بِالرِّسَالَةِ نَجِيّاً مَّا ذُكِرَ خَبَرُنَا هذَا فِيْ مَحْفِلٍ مِّنْ مَّحَافِلِ اَهْلِ الاَرْضِ وَ فِيْهِ جَمْعٌ مَّنْ شِيْعَتِنَا وَ مُحْبِّيْنَا اِلاَّ وَ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ الرَّحْمَةُ

(mpendwa) “Ewe Mtume wa Allah! Hebu nijulishe, kikao chetu hiki chini ya shuka kina fadhila gani mbele ya Allah.”

Mtume (s.a.w.a.) akamwambia, “Naapa kwa Yule Aliyeniteua kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba, itaka- pokumbukwa habari yetu hii, katika hafla yoyote ya watu wa ardhini na ikawa ikati yao kuna shia wetu na wapenzi wetu, basi Allah atawateremshia rehma yake na malaika watawahudhuria na

وَ حَفَّتْ بِهِمُ الْمَلائِكَةُ وَ اسْتَغْفَرَتْ لَهُمْ اِلى اَنْ يَّتَفَرَّقُوْا فَقَالَ عَلِيٌّ عَلَيْهِ السَّلاَمُ اِذاً وَّاللهِ فُزْنَا وَ فَازَ شِيْعَتُنَا وَ رَبِّ الْكَعْبَةِ فَقَالَ اَبِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَ الِهِ يَا عَلِيُّ وَ الَّذِيْ بَعَثَنِيْ بِالْحَقِّ نَبِيّاً وَّ اصْطَفَانِيْ بِالرِّسَالَةِ نَجِيّاً مَّا ذُكِرَ خَبَرُنَا هذَا فِيْ مَحْفِلٍ مِّنْ مَّحَافِلِ اَهْلِ الاَرْضِ

kuwaombea msamaha hadi watakapotawanyika”.

Ali (a.s.) akasema, “Basi wallahi tumefuzu na (pia) shia wetu wamefuzu”.

Kisha babangu, Mtume wa Allah (s.a.w.a.) akasema, “Ewe Ali! Naapa kwa Yule Aliyeniteua kwa haki kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba itakapotajwa habari yetu hii katika hafla yoyote ya watu wa ardhini na ikawa kati yao kuna

وَ فِيْهِ جَمْعٌ مِّنْ شِيْعَتِنَا وَ مُحْبِّيْنَا وَ فِيْهِمْ مَّهْمُوْمٌ اِلاَّ وَ فَرَّجَ اللهُ هَمَّه وَلاَ مَغْمُوْمٌ اِلاَّ وَكَشَفَ اللهُ غَمَّه وَلاَ طَالِبُ حَاجَةٍ اِلاَّ وَ قَضَى اللهُ حَاجَتَهُ فَقَالَ عَلِيٌّ عَلَيْهِ السَّلاَمُ اِذاً وَّ اللهِ فُزْنَا وَ سُعِدْنَا وَ كَذلِكَ شِيْعَتُنَا فَازُوْا وَ سُعِدُوْا فِي الدُّنْيَا وَ الاخِرَةِ وَ رَبِّ الْكَعْبَةِ

shia wetu na wapenzi, na ikawa kati yao kuna mwenye huzuni, basi bila shaka Allah atamuondolea huzuni yake, na mwenye ghamu, Allah atamuondolea ghamu yake, na mwenye haja, Allah Atamtek- elezea haja yake”.

Ali (a.s.) akasema, “Basi, wallahi tumefuzu na tumebarikiwa na kadhalika shia wetu wamefuzu na kubarikiwa, humu duniani na huko akhera, naapa kwa Bwana wa Kaaba”.

Ewe Allah mrehemu Muhammad na Aali zake Muhammad.

(اِنَّ اللهَ وَ مَلائِكَتَهُ يُصَلُّوْنَ عَلَى النَّبِيِّ يا أيُّهَا الَّذِيْنَ آمَنُوْا صَلُّوْا عَلَيْهِ وَ سَلِّمُوْا تَسْلِيْماً)

اَللّهم صَلِّ عَلى مُحَمَّدٍ وَّآلِهِ فِي الاَوَّلِيْنَ وَ صَلِّ عَلى مُحَمَّدٍ وَّآلِهِ فِي الآخِرِيْنَ وَ صَلِّ عَلى مُحَمَّدٍ وَّآلِهِ فِي النَّبِيِّيْنَ وَ الْمُرْسَلِيْنَ اَللّهُمَّ اعْطِ مُحَمَّداً صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ وَ سَلَّمَ الْوَسِيْلَةَ وَ الشَّرَفَ وَ الْفَضِيْلَةَ وَ الدَّرَجَةَ الْكَبِيْرَةَ اَللّهُمَّ اِنِّيْ آمَنْتُ بِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ وَ سَلَّمَ وَ لَمْ اَرَهُ

DUA

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake katika waliotangulia, na mrehemu Muhammad na Aali zake katika watokaokuja, na mrehemu Muhammad na Aali zake katika wakazi wa mbinguni, mrehemu Muhammad na Aali zake katika Mitume na Wajumbe wako.

Ewe Allah! Mpe Muhammad (s.a.w.a.) wasila, na utukufu na fadhila na cheo kikubwa (mbele yako).

Ewe Allah! Hakika mimi nilimwamini Muhammad (s.a.w.a.) bila ya kumwona,

فَلاَ تَحْرِمْنِيْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ رُؤْيَتَهُ وَارْزُقْنِيْ صُحْبَتَهُ وَ تَوَفَّنِيْ عَلى مِلَّتِهِ وَ اسْقِنِيْ مِنْ حَوْضِهِ مَشْرَباً رَوِيّاً لاَّ ظَمَأَ بَعْدَه اَبَداً اِنَّكَ عَلى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرٌ اَللّهُمَّ اسْتَعْمِلْنِيْ بِسُنَّتِهِ وَ تَوَفَّنِيْ عَلى مِلَّتِهِ وَ ابْعَثْنِيْ فِيْ شِيْعَتِهِ وَ احْشُرْنِي فِي زُمْرَتِهِ وَ اجْعَلْنِيْ مِمَّنْ يَّتْبَعُهُ وَ لاَ تَحْجُبْنِيْ عَنْ رُّؤْيَتِهِ وَ لاَ تَحْرِمْنِيْ مُرَافَقَتَهُ حَتّى تُسْكِنَنِيْ فِيْ جَوَارِهِ بِرَحْمَتِكَ يَا اَرْحَمَ الرَّاحِمِيْنَ.

basi usiniharamishie kumuona siku ya Qiyama, na uniruzuku kuwa pamoja naye, na unifishe katika dini yake, na uninyweshe katika hodhi yake (ya kauthar) kinywaji ambacho kitanifanya nisione kiu tena kamwe. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu.

Ewe Allah! Nijaalie kuzifuata sunna zake na unifufue katika kikundi chake, na unijaalie kuwa miongoni mwa wamfuatao, wala usinizuie kumwona (siku ya Qiyama) na usiniharamishie usuhuba wake, kisha unijaalia kuwa jirani wake (huko peponi) kwa rehma zako, ewe Mbora wa kurehemu.

ORODHA YA MADONDOO KATIKA

VITABU VYA KISHIA

1.Al-Ihtijaj cha Allamma Tabarsi.

2.Amalu Ibnush Shaikh.

3.Biharul Anwar cha Allama Majlisi.

4.Kashful Haqq cha Allama Al-hilli.

5.Fadhailu Ibnu Shadhan.

6.Kanzu Jami’ul Faraid.

7.Luhufu cha Seyyid ibnu Taus .

8.Almajalis (Al-amali) cha Shaikh Mufid.

9.Al-majalis (Al-amali) cha Shaikh Saduq.

10.Tafsirul Furat cha Ali ibnu Ibrahim Alkufi.

11.Tafsiru Majma’ul Bayan – cha Allama Tabarsi.

12.Al-umda cha Ibnu Batriq.

ORODHA YA MADONDOO KATIKA VITABU VYA KISUNNI

1.Al-isaba Jz3, uk 489

2.Ibnu A’sakir 5/1/16 B

3.Il-isti’ab Jz2, uk597

4.Jami’ul usul Jz10, uk101

5.Kanzul ummal Jz7, uk103

6.Khasaisun Nasai uk4.

7.Majma’’uz Zawaid Jz9, uk 167

8.Maqtalul khawarzmi Jz.2. uk 61

9.Mushkilul Athar Jz1, uk335

10.Musnadu Ahmad bin Hambal Jz4, uk17

11.Musnadu Tiyalasi Jz8, uk274

12.Almustadraku A’las Sahihain Jz.2, uk416

13.Mustadrakul Hakim Jz3, uk 147

14.Riyadhun Nadhrah Jz2, uk 248

15.Sahihu Muslim Jz7, uk13

16.Sahihu Tirmidhi Jz12, uk85

17.Sunanu Baihaqi Jz2, uk 14q

18.Tafsiru Durrul Manthur Jz5, uk198

19.Tafsiru Ibnu Kathir Jz3, uk485

20.Tafsirut Tabari Jz 22, uk.7

21.Tafsiruth Tha’alabi Jz3, uk228

22.Tahdhibut Tahdhib Jz2, uk297

23.Tarikhu Baghdad Jz9,uk 126

24.Tarikhut Tabari Jz5, uk31

25.Tafsirul Wusul Jz3, uk297

26.Asadul Ghaba Jz5, uk521

27.Zakhairul uqbah Uk24

28.Tarikhu Jum-ah isti’ab Uk637


[1] - سنن الترمذي، حديث 3788.