Isma'il ibn 'Abd al-Rahman, ibn Abi Karimah

Mfasiri mashuhuri, aliyejulikana kama Al-Suddi.

'Allamah al-Dhahabi ameandika katika kumwelezea Al-Suddi kuwa yeye alidaiwa kuwa Mshi'a na Husayn ibn Waqid al-Muruzi ametaja kuwa yeye amemsikia akiwalaumu Abu Bakr na 'Umar, lakini pamoja na kujua ukweli huu, Al-Thawri, Abu Bakr ibn 'Ayyash na wengineo wamezichukua na kuzipokea riwaya zake, na Imama Muslim, Tirmidhi, Abu Dawud, Ibn Majah, na Nasa'i wameziandika katika vitabu vyao vijulikanavyo kwa jina la Sahih kwa kuunga maoni yao.

Imam Ahmad (ibn Hanbal) amemchukulia yeye mwaminifu na Ibn 'Adi amemchukulia yeye kama msema ukweli wakati ambapo Yahya ibn Sa'id anasema:

"Nilimwona kila mtu akimsema vema Al-Suddi na wao wote wamezichukua na kuzikubalia riwaya kutoka kwake." Yeye alifariki mwaka 127 Hijriyyah.