Isma'il ibn 'Abbad, ibn 'Abbas al-Taliqani

(Kwa umashuhuri alijulikana kama Sahib ibn 'Abbad)

Abu Dawud na Tirmidhi wamechukua riwaya kutoka kwake, kama vile ilivyoelezwa na Imam al-Dhahabi katika kitabu chake Mizan kwa kutoa maoni kuwa mtu adhimu kabisa wa uandishi wa mabarua na Mshi'a.

Hapana shaka kuwa kwake Mshi'a, na hayo ni kutokana na imani yake kwamba alikuwa Waziri Mkuu katika Utawala wa Buwayhiya.

Yeye alikuwa ni mtu wa kwanza kwa kupewa jina la Sahib, kwa sababu alikuwa mwenzie Mu'ayid al - Dawlah katika ujana wake na huyo ndiye aliyempatia heshima hiyo, na kwamba alikuja kujulikana kwa jina la Sahib na baada yake ilikuwa ni desturi kumwita Waziri Mkuu waliofuatia kwa jina la Sahib.

Yeye kwanza alikuwa ni Waziri wa Mu'ayid al-Dawlah, na baada ya kifo chake, ndugu yake Fakhr al-Dawlah, alimbakiza katika cheo hicho.

Wakati wa kifo chake (24 Safar, 385 H., akiwa na umri wa miaka 59) wakazi wote wa mji wa Ray (kwa sasa inajulikana kwa jina la Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) walifunga milango ya nyumba zao na walikwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu kushiriki katika mazishi yake, na Mfalme akiandamana na watu wote alishiriki kikamilifu katika mazishi yake.

Yeye alikuwa Mwanachuoni Mkubwa na mwandishi na mtunzi wa vitabu vingi pamoja na makala mbalimbali.