Isma'il ibn Khalifah, al-Mala'i al-Kufi

Jina la kiukoo ni Abu Isra'il na hili ndilo jina ambalo analotambuliwa kwa kawaida.

'Allamah Dhahabi ameandika katika kitabu chake Mizan al-I'tidal kuwa yeye alikuwa ni Mshia shupavu kabisa na daima akidai kuwa 'Uthman alikuwa kafiri na ameongezea maoni mengi kuhusu yeye.

Licha ya hayo, Tirmidhi na waandishi wengine wa Sunan wamezichukua riwaya kutoka kwake na Abu Hatam amezitambulisha riwaya hizi kama nzuri; Abu Zar'ah amemchukulia yeye kama mwandishi mkweli, ingawaje maoni yake yamekuwa yenye juhudi zaidi.

Imam Ahmad (ibn Hanbal) anachukulia riwaya zake kuwa ni zenye kuaminiwa Fallas anatoa maoni : yeye si miongoni mwa wale waliosema uongo na uzushi na riwaya zake zipo zinapatikana katika Sahih al-Tirmidhi ; na Ibn Qutaybah katika Ma'rif anamhesabu miongoni mwa Mashi'a mashuhuri.