Isma'il ibn Aban, al-Azdi al-Kufi al-Warraq

Yeye alikuwa ni mmoja wa Mashekhe wa Bukhari.

'Allamah Dhahabi anaandika kuwa Bukhari na Tirmidhi wametegengeneza hoja zao kwa riwaya zake na vile vile kuelezea kuwa Yahya na Ahmad wamechukua riwaya kutoka kwake.

Bukhari anamwelezea kuwa ni msema mkweli.

Waandishi wengine wanasema kuwa yeye alikuwa ni mfuasi wa Madhehebu ya Kishia na alifariki mwaka 286 H.

Al-Qaysarani, hata hivyo, anaandika tarhe ya kifo chake kuwa ni 216 H.

na vile vile amechukizwa kwa kuwa Bukhari amechukua riwaya za Isma'il moja kwa moja kutoka kwake katika vitabu vyake mbali na Sahih.