Ahmad ibn Mufaddal, ibn al-Kufi al-Hafri

Abuy Zar'ah na Abu Hatam wamechukua riwaya kutoka kwake na kuunga mkono hoja zao, huku wakijua na kukiri kuwa huyo alikuwa ni Mshi'a halisi.

Hivyo, Abu Hatam anaelezea kwa kusisitiza katika kitabu chake Mizan : Ahmad ibn Mufaddal alitokana na watukufu wa Kishi'a na alikuwa ni mtu wa kusadikiwa na kuaminiwa.

Dhahabi vile vile amemwelezea katika Mizan na kumpatia vifupisho vya jina lake.

Abu Dawud na Nasa'i vile vile wamechukua riwaya kutokea kwake katika vitabu vyao vya Sahih kwa kupitia Al-Thawri naye ameripoti riwaya kutoka kwa Asbat ibn Nasr na Isra'il.