Ibrahim ibn Yazid, ibn 'amr ibn Aswad ibn 'Amr al-Nukha'i

Hakimu wa Kufah. Mama yake alikuwa malikah bin Yazid ibn Qays, naye kutokea Nukha'iyah; ndugu zake Al-Aswad, Ibrahim na 'Abd al-Rahman, wana wa Yazid ibn Qays, walikuwa kama wajomba zao 'Alqamah ibn Qays na Ubayya ibn Qays, Waislam thabiti na ushahidi wao ulikuwa daima ukisadikiwa kuwa ni wa ukweli kabisa.

Waandishi wa vitabu sita vya Sahih na wengineo wamechukua riwaya nyingi kutoka kwa hawa, wakijua waziwazi kuwa hao walikuwa ni Ma Shi'a.

Ama kuhusu Ibrahim ibn Yazid mwenyewe, Ibn Qutaybah katika Ma'arif anamtambulisha yeye kuwa ni Mshia kamili bila shaka yoyote ile.

Pamoja na hayo, Riwaya zake zipo zinapatikana katika katika vitabu vya Sahih i.e Bukhari na Muslim. Yeye vile vile amewaripotia riwaya kutokea kwa mjomba wa mama yake, 'Alqamah ibn Qays, ambaye ameripoti kutoka kwa Himam ibn al-Harith na Abu 'Ubaydah ibn 'Abdullah ibn Mas'ud, or from 'Ubaydah au mjomba wake kwa upande wa mama yake Al-Aswad ibn Yazid. Riwaya zake zinginezo zilizoko katika Sahih Muslim ni zile ambazo yeye amezichukua kutoka wajomba zake kwa upande wa mama yake, kwa kuwataja majina 'Abd al-Rahman ibn Yazid, na vile vile Sahm ibn Munjab, Abu Mu'ammar na 'Ubaydah ibn Nadlah, na 'Abis.

Riwaya zake zipo zimeripotiwa katika Sahih mbili kwa kupitia Mansur, Al-A'mash, Zubayd, Hakam na 'Ibn 'Aun; na katika Sahih Muslim kwa kupitia Fudayl ibn 'Amr, Mughayrah, Ziyad, Ibn Kulayb, Wasil, Hasan ibn 'Ubaydullah, Hamad ibn Abu Sulayman na Simak.

Ibrahim ibn Yazid alikuwa amezaliwa katika mwaka 50 Hijriyyah na alifariki mwaka 95 au 96 Hijriyyah, baada ya miezi minne kupita tangia afe Hajjaj ibn Yusuf.