'Aban ibn Taghlib, ibn Riyah

Qari (msomaji wa Qur'an), wa Kufah (Alikuwa mwanafunzi wa Imam Zayn al-'Abedin a.s. na Imam Muhammad al-Baqir a.s.) Yafuatayo yamenakiliwa kutoka Mizan cha Dhahabi:

'Aban ibn Taghlib wa Kufah; mfuasi halisi wa Shi'a, lakini hata hivyo alikuwa ni msema ukweli na kusadikiwa, na sisi tunachojihusisha naye ni ukweli wake tu, na swala la yeye kutokufuata dini zetu, basi hilo ni swala lake la kibinafsi.

[Dhabahi anaendelea:] Ahmad ibn Hanbal, Ibn Mu'in na Abu Hatim wanamwamini yeye kuwa ni mtu anayeaminiwa na kusadikiwa; na Ibn 'Adi anadokeza kusema kuwa yeye (ibn Taglib) alikuwa ni Mshi'a halisi; na Sa'di anaandika kuwa yeye alikuwa ni mtu mwenye kufarakanisha waziwazi ...... Miongoni kwa wale ambao wamemtegemea yeye ni Muslim na waandishi wa vitabu vinne (4) vya Sunan, tukiwataja Abu Dawud, Tirmidhi, Nasai na Ibn Majah kwa kidhibiti cha wao kutumia kifupisho cha jina lake. Zaidi ya hayo, unazo riwaya zake katika Sahih Muslim na vitabu vinne vya Sunan kutokea Hakim, Al-A'mash na Fudayl ibn 'Amr kama zilivyo rekodiwa na Muslim, Sufyan ibn 'Uyaynah, Sha'bah na Idris al-Awdi.

Yeye alifariki katika mwaka 141 Hijriyyah. Allah swt amrehemu.