Ja'far ibn Ziyad, al-Ahmar al-Kufi

Abu Dawud anamwelezea katika maneno yafuatayo:

"Mtu msema ukweli na yu Mshi'a."

Juzjan anamwelezea yeye kama "anayetoka nje ya njia," yaani yeye ametoka nje ya njia ya Juzjan, na akaelekea katika njia ya Ahl al-Bayt a.s. Ibn 'Adi anasema kuwa "yeye ni mcha Mungu na ni Mshi'a." Mjukuu wake mwenyewe, yaani Husayn ibn 'Ali ibn Ja'far ibn Ziyad anasema: "Babu yangu, Ja'far, alikuwa miongoni mwa masharifu wa Kishi'a wa Khurasan." Abu Ja'far al-Dawaniqi anamwelezea yeye kama mfungwa aliyefungwa mkanda shingoni na kwa kamba ndefu, pamoja na Mashi'a wengineo.

Abu 'Uyaynah, Waki', Abu Ghassan al-Mahdi, Yahya ibn Bushr al-Hariri na Ibn Mahdi wamezieneza riwaya walizojifunza kutoka kwake, yaani ama yeye alikuwa ni mwalimu au mwongozi wao; na Ibn Mu'in na wengineo wanathibitisha ukweli wake, ambapo Ahmad ibn Hanbal anamsema hivi:

" Mwandishi mzuri wa riwaya." Dhahabi amemtaja katika kitabu chake cha Mizan na ameandika uhakika uliotajwa hapo awali kuhusu yeye na Tirmidhi na Nasa'i walitengeneza vifupisho vya jina lake, ambavyo inamaanisha kuwa wao walikuwa wakimtumia kwa mara nyingi katika kuziandika riwaya zake. Zaidi ya hayo, zipo riwaya nyingi kutokea kwake katika vitabu vyote vya Sahih kutokea Bayan ibn Bushr, 'Ata' ibn Sa'ib na wengineo.

Yeye alifariki katika mwaka 167 Hijriyyah, Allah swt amrehemu.