Jarir ibn 'Abd al-Hamid, al-Dabbi al-Kufi

Ibn Qutaybah katika kitabu chake Al-Ma'arif, amemhesabu yeye miongoni mwa Mashi'a waliojulikana vyema na Dhahabi amemtambulisha kwa vifupisho vya jina lake popote pale alipomtumia katika riwaya zake katika kitabu chake Mizan, inathibitisha vile alivyo mtu wa kutegemewa katika maoni ya waandishi wa vitabu vya Sahih.

Zaidi ya hayo, Dhahabi anasema katika kumsifu:

"Mtu msomi kutoka Ray, msema kweli, aliyechukuliwa na waandishi wa vitabu kuwa ni mtu wa aina yake pekee," naye ameelezea mwungano wa maoni kuhusu kutegemewa kwake.

Vile vile, kuna riwaya kutokea kwake katika Sahih al-Bukhari na Sahih al-Muslim ambazo yeye anazielezea kutoka Al-A'mash, Mughayrah, Mansur, Ismail ibn Abu Khalid na Abu Is-haq al-Shaybani na Qutaybah ibn Sa'id, Yahya ibn Yahya na 'Uthman ibn Abu Shaybah ni miongoni mwa watu ambao wamezieleza riwaya kutoka kwake.

Yeye amefariki huko Ray katika mwaka 187 H akiwa na umri wa miaka 77, Allah swt amrehemu.