Jabir ibn Yazid, ibn Harith al-Ju'fi al-Kufi

Dhahabi anaandika kuhusu huyu katika kitabu chake Mizan kuwa alikuwa ni mmoja wa Mashia waliosoma na anaandika kuwa Sufyan alisema kuwa alimsikia Jabir akisema kuwa ilimu ya Mwenyezi Mungu ilifikishwa na Mtume s.a.w.w. kwa Imam Ali a.s., na kutoka kwake kwa Imam Hasan a.s., na kutoka kwake kwa Imam Hussein a.s. na kuendelea, yaani kutoka kwa Imam mmoja hadi mwingine hadi kufikia kwa Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na kwamba yeye alijifunza riwaya nyingi kutokea Imam a.s. Muslim anasema mwanzoni mwa kitabu chake cha Sahih Muslim kutokea Jarrah kuwa Jabir alisema:

"Mimi kwa ujumla ninazo riwaya na Ahadith elfu sabini ambazo zote zimenifikia kutoka kwa Abu Ja'afar (yaani Imam Muhammad al-Baqir a.s.) kutokea kwa Mtume s.a.w.w." Mwandishi huyo huyo anasema kutokea Zuhayr kuwa Jabir alisema:

"Mimi ninazo Ahadith elfu hamsini ambazo sijazisimulia chochote," na hapo alisimulia Ahadith moja na kusema: " Hii ni mojawapo ya elfu hamsini.

" Dhahabi anaendelea kuelezea katika kitabu chake cha Mizan kuwa popote pale Jabir alipokuwa amezoea kusimulia Ahadith ya Imam Mohammad al-Baqir a.s., yeye daima alikuwa akianza kwa kusema:

"Hivyo ndivyo mrithi wa warithi (wa Mtume s.a.w.w.) alivyoniambia." Mwandishi huyu huyu anaandika kuwa wengi walimshutumu kwa kuamini katika raj'ah (marudio). Dhahabi anaelezea kwa mara nyingine tena kwa mamlaka ya Za'idah kuwa Jabir alikuwa rafidhi, na alikuwa akiwashutumu wapinzani wote wa Imam 'Ali a.s. Lakini pamoja na hayo yote, Nasa'i na Abu Dawud wamechukua riwaya zake kama vile riwaya yake kuhusu suju al-sahwa yaani kurekebisha kupitiwa wakati wa sala.

Sha'ba na Abu 'Awanah na washiriki wao vile vile wamechukua riwaya zake. Abu Dawud na Tirmidhi wanamchukulia yeye miongoni mwa waandishi wao waaminiwao na kuwategemea kwa usahihi.

Sufyan al-Thawri alimwelezea kama mwandishi mwenye imani ya riwaya na alisema: "Mimi kamwe sijamwona mtu yeyote aliye mwangalifu kuliko yeye," na Sha'bah anasema: "Jabir ni mwenyekuripoti aliye mkweli," na yeye pia husema: "Popote pale Jabir aliporipoti Hadith yoyote ile, basi mimi daima nimemwona yeye kuwa mwaminifu kabisa miongoni mwa watu.

" Waki anasema: "Lipo jambo moja ambalo mimi sina shaka nalo kwa vyovyote vile, nayo ni kwamba Jabir al-Ju'fi ni mtu wa kutegemewa na kusadikiwa.

" Ibn 'Abd al-Hakam alimsikia Al-Shafi'i akimwambia Sufyan al-Thawri: "Iwapo mimi ningalikuwa nikimshuku Jabir al-Ju'fi basi mimi nisingalitilia shaka yale uyasemayo wewe." Jabir alifariki ama katika mwaka 127 au 128 Hijriyyah; Allah swt amrehemu.