Talid ibn Suleyman al-Kufi

Ibn Mu'in ameandika kuwa yeye alikuwa akimshutumu mno 'Uthman.

Hivyo wa-'Uthmani walipoyasikia hayo, walimwua kwa kumpiga mshale uliovunja mguu wake.

Abu Dawud amemsema huyo kuwa ni rafidhi (yaani kafiri ilivyokuwa ikitumika kuwataja Mashi'a) na mshutumu mkuu wa Abu Bakr na 'Umar.

Lakini pamoja na kujua ukweli huo, Ahmad (ibn Hanbal) na Ibn Namir walijifunza riwaya na Ahadith kutoka kwake na Imam Ahmad alisema:

" Ingawaje Talid ni Mshi'a, lakini hakuna madhara kwa kuzipokea riwaya zake."

Kitabu kiitwacho Sahih al-Tirmidhi kinacho riwaya zake huyu Bwana.