Isma'il ibn Musa, al - Fazari al-Kufi

'Allamah al-Dhahabi ameandika kuhusu huyu bwana katika kitabu chake Mizan al-I'tidal kuwa Ibn 'Adi alikuwa na mazoea ya kusema kuwa yeye alikuwa akilaumiwa kwa kuwa Mshia shupavu.

Abdan anaelezea kuwa "Hannad na Ibn Abi Shaybah walichukizwa mno na kwenda kwetu kwake na daima walikuwa wakituambia sisi tusiende kwa huyo mtu mwovu ambaye anawalaumu vikali viongozi wetu watukufu." Lakini pamoja na hayo, Ibn Khuzaymah, Abu 'Arubah na wengi mno walijifunza Ahadith na riwaya kutoka kwake na yeye alikuwa na wadhifa na elimu ya waalimu kama Abu Dawud, Tirmidhi na wengineo.

Wao wote wamechukua Ahadith na riwaya kutoka kwake na kuziingiza katika Sahih zao.

Nasa'i amesema kuwa hakuna ubaya katika kuuchukua Ahadith na riwaya kutoka kwake.

Yeye alifariki mwaka 245 H.

Baadhi ya waandishi wanadai kuwa yeye alikuwa ni mjukuu wa Al-Suddi kwa upande wa mama.