Riwaya Za Waandishi Mashi'a Katika Vitabu Vya Sahih Na Musnad Vya Ahl as-Sunna

Kimetarjumiwa na : Amiraly M H Datoo

UTANGULIZI

Makala haya yafuatayo ni barua ambayo Sheikh wa Kisunni, Sheikh Salim al-Bishri, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, huko Cairo, Misri alimwandikia Sheikh wa Kishi'a katika karne ya ishirini na alianza majadiliano pamoja na Sheikh wa Kishi'a Mwanachuoni mashuhuri wakati huo, Sayyid 'Abd al-Husayn Sharaf al-Din wa Jabal 'Amil (upande wa kusini mwa Lebanon) ambaye aliizuru Misri katika mwaka 1329 - 1330 Hijriyyah muafaka wa 1911 - 1912 A.D. na walikutana pamoja. Sheikh Bishri hakuamini kuwa Ahl al-Sunnah wanazo riwaya[1] kutoka Mashi'a katika vitabu vyao vitukufu na hivyo alitaka uthibitisho pamoja na majina yao na iwapo kutakuwapo na kukiri kwa Masunni kuwa hao waandishi walikuwa ni Mashi'a. Barua ya maswala na majibu yametengenezwa kuwa kitabu kimoja mashuhuri sana kijulikanacho kwa jina la al - Muraja'at. Kwa hakika kitabu hicho kimewaathiri wengi mno waliojaribu kukisoma hasa miongoni mwa wasomi na Mashekhe. Na makala haya ni barua mojawapo tu ya jibu kwa Sheikh Salim kutoka kwa Sheikh Sharaf al-Din. Ni matumaini kuwa msomaji atafaidika na makala haya. Sheikh Sharraf al-Din anamwandikia majina 100 ya waandishi wa Kishi'a. Ombi la Majina ya waandishi wa riwaya na ahadith za Ahl al-Sunnah ambao walikuwa ni Mashi'a waliojulikana 'Allamah Sayyid 'Abd al-Husayn Sharaf al-Din, Assalaam 'Alaykum. Nimepokea barua yako ya hivi sasa. Yaani ina nguvu huku ikiungwa mkono kwa majibizano yako na maamuzi yaliyokomaa kiasi kwamba sijiwezi illa kukubalia kila neno ulilolisema. Lakini habari isemayo kuwa Ahl al-Sunnah kwa mara nyingi wamekuwa wakizichukua riwaya na Ahadith zao kutoka kwa waandishi wa Kishi'a, ni kiujumla na kwa maneno machache. Hivyo utoe maelezo zaidi juu ya swala hili. Itakuwa vema iwapo ungekuwa umetaja majina ya hao waandishi wa Kishi'a na vile iwapo Ahl al-Sunnah wakikiri kuwa hao ni Mashi'a. Natumai kuwa unaelewa aina ya majibu ninayoyahitaji. Pamoja na Salaam, Wako S Kwa Mawlana Shaykh al-Islam, Sheikh Salim al-Bishri, Assalaam 'alaykum. Ifuatayo ni orodha fupi ya waandishi wa Shi'a ambao riwaya na Hadith zao zipo zinapatikana katika vitabu vyenu vya Sahih na Musnad (musnad kutokea sanad, ikimaanisha mamlaka, ukusanyaji wa Hadith, mfano Musnad ya Ahmad ibn Hanbal). Orodha hii ipo kwa mujibu wa mpangilio wa herufi za Kiarabu.


Notes:[1] Kwa riwaya tutakuwa tukimaanisha mapokezi ya Ahadith na Sunnah za Mtume s.a.w.w. zilizowafikia Mashi'a kwa kupitia Ahl al- Bayt watukufu a.s.