WALE WANAOPENDWA NA ALLAH SWT

Makala haya yametarjumiwa na kushereheshwa na:Amiraly M.H.Datoo

Hadithi hii ilisomwa na: Sheikh Akmal Hussein Taheri – Bukoba

1. Allah swt huwapenda wafanyao ihsani, Al-Qur’an Sura Al-Baqarah (2) Aya 195

‘Waahsinu Innaallaha yuhibbul muhsiniin

Hakika Allah huwapenda wafanyao wema

2. Allah swt huwapenda wafanyao Tawba, Al-Qur’an Sura Al-Baqarah (2) Aya 222

‘Innallaha yuhibbut tawwabiina wa yuhibbul mutatahhiriina

Hakika Allah huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa.

3. Allah swt huwapenda watimizao ahadi wazitoazo, Al-Qur’an Sura Aali Imran (3 ) Aya76

‘Balaa Man awfa biahdihi wat-Taqaa fainnallaha yuhibbul Muttaqiin

….. Allah huwapenda wajilindao

4. Allah swt huwapenda wafanyao subira, Al-Qur’an Sura Aali-Imran Aya (3), 146

‘Innallaha yuhibbus-Saabiriin

Na Allah anawapenda wafanyao subira

5. Allah swt huwapenda wenye nia halisi, Al-Qur’an Sura Aali-Imran (3), Aya 148

‘Wallahu yuhibbul Muhsiniin

Allah anawapenda wafanyao mema

6. Allah swt huwapenda wenye kufanya al-faaf, Al-Qur’an Sura Al-Maidah (5), Aya 42

‘Innallaha yuhibbul Muqsitiin

Bila shaka Allah anawapenda waadilifu.

7. Allah swt huwapenda wenye taqwa , Al-Qur’an Sura Al-Tawbah ( 9 ) Aya 4

‘Wa’alamu annallaha ma’al Muttaqiin

Allah anawapenda wanaomuogopa.

WALE WASIOPENDWA NA ALLAH SWT

1. Allah swt hawapendi wafasiqi, Al-Qur’an Sura Saffa’ (61), Aya 5

‘Wallahu la yahdil qawmal faasiqiin

Allah hawaongozi watu waovu

2. Allah swt hawapendi wafasidi, Al-Qur’an Sura Al-Maidah (5), Aya 64

‘Wallahu la yuhibbul Mufsidiin

Allah swt hawapendi waharibifu

3. Allah swt hawapendi wadhalimu, Al-Qur’an Sura Al-Tawba ( ) , Aya 19

‘Wallahu la yahdil qawma-dhalimiin

Allah hawaongozi qaumu dhalimu

4. Allah swt hawapendi wasaliti, Al-Qur’an Sura Al-Haj (22 ), Aya 38

‘Innallaha la yuhibbu kulla khawanina kafur.

Allah hampendi kila haini, asiyeshukuru

5. Allah swt hawapendi wenye kiburi, Al-Qur’an Sura An-Nahl (16 ), Aya 22

‘Innallaha la yuhibbul Mustakbiriin

Kwa hakika Yeye hawapendi wanaotakabari