rudi nyuma Yaliyomo endelea

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo, naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

"Ewe Salman,

6. wakati huo watawala watakuwa wadhalimu

7. Mawaziri watakuwa waasi,

8. na wadhamini (wale waliopewa amana kwa kuaminiwa) watafanya hiana,

9. hakika wakati huo maovu yatakuwa mema na mema yatakuwa maovu,

10.  wale wafanyao hiana wataaminiwa na waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;na mwongo atasadikiwa,na msema kweli atahesabiwa mwongo.

11.  Wakati huo kutakuwapo na utawala wa wanawake XE "wanawake" ,

12.  Masuria watashauriwa,

13.  na watoto watakaa juu ya mimbar XE "mimbar" ,

14.  udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu

15.  na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini;na mateka ya vita (yaani mali ya ummah XE "ummah" ) yatakuwa kama ni mali ya mtu binafsi;na mtu atakuwa mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema kwa marafiki zake,

16.  na wakati huo kutatokea na nyota XE "nyota"  zenye mikia (comets)."

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?"

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

"Ewe Salman!

17.  wakati huo mwanamke XE "wanawake:mwanamke"  atakuwa mshiriki wa mumewe katika biashara,

18.  na mvua XE "mvua"  itakuwa moto XE "moto"  sana

19.  na watu wema watabaki katika huzuni;na masikini hawata heshimiwa;na wakati huo masoko yatakaribiana,

20.  Tena huyu atasema,"Mimi sikuuza chochote,na yule atasema, "Mimi sikupata faida yoyote." Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote asiyemlalamikia Allah swt.

"Ewe Salman!

21.  tena itatokea iwapo watu watawazungumzia watawala wao, watawaua, na ikiwa watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali yao, watanyimwa heshima zao,watamwaga damu XE "damu"  yao na mioyo ya watu itajaa woga;kisha hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga,mwenye khofu,ametishika na ameshstushwa”

"Ewe Salman!

22.  Bila shaka wakati huo mambo fulani yataletwa kutoka Mashariki

23.  na mambo fulani yataletwa kutoka Magharibi,

24.  Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) katika Ummah XE "Ummah"  wangu kutokana na hayo; Ole ya Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na huruma juu ya wadogo wao,wala hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa.Miili yao  itakuwa  ya wanadamu,lakini mioyo yao itakuwa ya mashetani."

"Ewe Salman!

25.  Wakati huo wanaume XE "wanaume"  watawaashiki wanaume,

26.  na wanawake XE "wanawake"  watawaashiki wanawake;

27.  na watoto wa kiume watapambwa kama wanawake;

28.  na wanaume watajifanya kama wanawake

29.  na wanawake wataonekana kama wanaume;

30.  na wanawake watapanda mipando

31.  Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt juu ya wanawake wa Ummah XE "Ummah"  wangu."

"Ewe Salman!

32.  Bila shaka wakati huo Misikiti XE "Misikiti"  itapambwa (kwa dhahabu n.k.) kama inavyofanywa katika masinagogi na makanIssa,

33.  na Qur’an XE "Quran"  zitapambwa (kwa nakshi na rangi za kupendeza n.k.)

34.  na minara (ya misikiti) itakuwa mirefu;na safu za watu wanaosimama katika sala XE "sala"  zitazidi,lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao yatatofautiana."

"Ewe Salman!

35.  Wakati huo wanaume XE "wanaume"  watatumia mapambo ya dhahabu;kisha watavaa hariri,na watatumia ngozi za chui."

"Ewe Salman!

36.  Wakati huo riba XE "riba"  itakuwako,

37.  na watu wata- fanyia biashara kwa kusemana na rushwa

38.  na dini itawekwa chini,na dunia itanyanyuliwa juu."

"Ewe Salman!

39.  Wakati huo talaqa XE "talaqa"  zitazidi

40.  na mipaka ya Allah swt hayatasimamishwa

41.  Lakini hayo hayatamdhuru Allah swt."

"Ewe Salman! 

42.  Wakati huo watatokea wanawake XE "wanawake"  waimbaji,

43.  na ala za muziki

44.  na wabaya kabisa watawatawala Ummah XE "Ummah"  wangu."

"Ewe Salman!

45.  Wakati huo matajiri katika Ummah XE "Ummah"  wangu watakwenda Kuhiji kwa matembezi,na walio wastani kwa biashara,na masikini kwa kujionyesha.

46.  Hivyo basi wakati huo watakuwapo watu ambao watajifundisha Qur’an XE "Quran"  si kwa ajili ya Allah swt na wataifanya Qur’an XE "Quran"  kama ala ya muziki.

47.  Na watakuwapo watu ambao watasoma dini si kwa ajili ya Allah swt 

48.  na idadi ya wanaharamu itazidi 

49.  watu wataiimba Qur’an XE "Quran" ,

50.  na  watu watavamiana kwa uroho wa kidunia."   

"Ewe Salman!

51.  Haya yatatokea wakati heshima zitakapo- ondoka,na madhambi yatatendwa

52.  na watu waovu watakuwa na uwezo juu ya watu wema,

53.  na uongo utaenea na mabishano (matusi XE "matusi" ) yatatokea

54.  na umasikini utaenea,

55.  na watu watajiona kwa mavazi yao

56.  na itakuwepo mvua XE "mvua"  wakati si wake

57.  na watu watacheza dama, kamari na Ala za muziki,

58.  na hawatapenda kuhimizana mema wala kukatazana maovu

59.  na kwa ajili hali itakavyokuwa hata itafikia wakati huo kuwa Muumin atakuwa na heshima ndogo kuliko hata mjakazi

60.  na wanaosoma na wanaotumia wakati wao katika kumwabudu Allah swt watalaumiana.

61.  Hao ndio watu watakaoitwa wachafu na wanajisi katika Ufalme wa mbinguni."

"Ewe Salman!

62.  Wakati huo matajiri hawataogopa chochote isipokuwa mtu masikini; hadi kwamba masikini wataendelea kuomba kati ya ijumaa mbili,na hawatamwona mtu yeyote wa kutia chochote mikononi mwao."

"Ewe Salman!

63.  Wakati huo itazungumzwa Ruwaibidhah."

Salman akauliza:"Ni nini Ruwaibidhah ? Ewe Mtume wa Allah swt, baba na mama yangu wawe fidia kwako."

Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akajibu:

64.  "Watu fulani watazungumza kuhusu mambo ya watu ambayo hayakuwahi kuzungumzwa namna hii zamani.

65.  Tena baada ya muda mchache machafuko yatatokea duniani,na kila nchi itafikiri kuwa machafuko yapo katika nchi yao tu."

66.  "Watabaki katika hali hiyo kwa muda ambao Allah swt atapenda wabaki;

67.  kisha ardhi itatapika vipande vya moyo wake dhahabu, fedha na madini mengineyo; (Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.) alinyosha kidole chake penye nguzo, na akasema: "Kama hizi (kwa ukubwa), lakini siku hiyo dhahabu wala fedha hazitamsaidia mtu yeyote. Na hii ndiyo maana ya maneno ya Allah swt 'Hakika dalili Zake zimekuja.'[100]

1684.   UBASHIRI WA IMAM JAAFER AS-SADIQ  A.S. 

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq a.s. ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam,Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi.Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran.

Imam a.s. alisema:

1 "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki XE "haki"  hawatapatikana.

5. Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.

6. Kufuata Qur’an XE "Quran"  kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.

7. Zitatolewa maana ya Aya za Qur’an XE "Quran"  kwa mujibu wa matakwa ya watu,hivyo mafhum ya Qur’an itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.

8. Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.

9. Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.

10.  Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.

11.  Ulawiti XE "Ulawiti"  utakuwa ni jambo la kawaida.

12.  Muumin  atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa

13.  Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.

14.  Huruma itakuwa imepotea kabisa.

15.  Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.

16.  Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume XE "wanaume"  wenzao.

17.  Wanawake watawaoa wanawake XE "wanawake"  wenzao.

18.  Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.

19.  Starehe, anasa na zinaa XE "zinaa"  zitashamiri.

20.  Zinaa XE "Zinaa"  itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.

21.  Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.

22.  Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.

23.  Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza  fitina na yale wanayozusha.

24.  Ushauri mzuri utakanwa.

25.  Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.

26.  Al-Kaaba XE "Kaaba"  haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.

27.  Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah XE "Makkah"  kuhiji.

28.  Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.

29.  Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake XE "wanawake"  watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.

30.  Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao.

31.  Na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara kuma zao.

32.  Wanawake wataunda vilabu vyao,mashirika na umoja wao.

33.  Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.

34.  Wanaume watajirembesha kama wanawake.

35.  Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli. Na Banu Abbas watalipia ulawiti.

36.  Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume XE "wanaume"  watakuwa hivyo hivyo.

37.  Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.

38.  Riba XE "riba"  ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.

39.  Ushahidi wa uongo utakuwa ukIssadikiwa mno.

40.  Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.

41.  Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.

42.  Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.

43.   Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.

44.  Rushwa XE "Rushwa"  ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.

45.  Wanaume wata walawiti wake zao.

46.  Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.

47.  Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawake XE "wanawake" .

48.  Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa XE "zinaa" .

49.  Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.

50.  Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.

51.  Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa  ulimini.

52.  Pombe XE "Pombe"  na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.

53.  Wanawake XE "wanawake"  wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri,ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.

54.  Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.

55.  Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.

56.  Usomaji na usikilizaji wa Qur’an XE "Quran"  utakuwa ni bughudha kwa watu.

57.  Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.

58.  Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.

59.  Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.

60.  Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.

61.  Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.

62.  Misikiti XE "Misikiti"  itarembeshwa kwa dhahabu.

63.  Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.

64.  Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.

65.  Kumwaga damu XE "damu"  ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.

66.  Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi XE "matusi"  mabaya ili kuwatishia watu wengine.Imam a.s. aliendelea kusema:

67.  "Watu watakuwa wakipuuzia sala XE "sala"  na kutojali.

68.  Watu hawatakuwa wakilipa zaka XE "zaka"  ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.

69.  Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.

70.  Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

71.  Watu watakuwa wakIssali katika mavazi ya kiajabu.

72.  Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.

73.  Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.

74.  Watu watasali kwa kuonyesha tu.

75.  Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.

76.  Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.

77.  Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali,watasifiwa kwa midomo tu.

78.  Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah XE "Makkah"  na Madina XE "Madina" .

79.  Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.

80.  Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.

81.  Matajiri wataigwa.

82.  Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.

83.  Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko,maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.

84.  Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.

85.  Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.

86.  Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume XE "wanaume"  wao.

87.  Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi,basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.

88.   Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.

89.  Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.

90.  Pombe XE "Pombe"  itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.

91.  Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.

92.  Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala XE "sala" .

93.  Misikiti XE "Misikiti"  itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.

94.  Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala XE "sala"  za jamaa'  na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

1685.     VIFO VYEUPE NA VYEKUNDU:

Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim a.s. kutatokezea kwa aina mbili za vifo XE "vifo"  - nyekundu na nyeupe.

Kwa nyekundu kunamaanisha damu XE "damu"  yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali.

Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafa XE "maafa"  ya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala."

Tanbihi: Kwa vifo XE "vifo"  vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damu XE "damu"  itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia.Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande.  Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n.k. yanavyoua watu kwa mamilioni.

UBASHIRI WA IMAM ‘ALI

1686.   Imam Ali ibn Abi Talib  a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake,

  1. Watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa.
  2. Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi.
  3. Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi.
  4. Waislamu wataanza kuchukua riba. XE "riba"  
  5. Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida.
  6. Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa.
  7. Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia.
  8. Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao.[101]
  9. Wanaume watawataka wanawake XE "wanawake"  ushauri na uongozi.
  10. Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu.
  11. Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida.[102]
  12. Mauaji na umwagaji wa damu XE "damu"  utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe.
  13. Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na  wadhalimu watakuwa wenye nguvu.
  14. Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu.
  15. Wasufi na wasomaji wa Qur’an XE "Quran"  watakuwa wapumbavu.
  16. Kutakuwa kukitolewa ushahidi  wa kughushiwa.
  17. Qur’an Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.
  18. Misikiti XE "Misikiti"  itakuwa ikijengewa minara mirefu.
  19. Watu waovu watakuwa wakiheshimwa.
  20. Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao.
  21. Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale.
  22. Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume XE "wanaume"  wao  kwa uroho wa mali.
  23. Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana.
  24. Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu
  25. Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa.
  26. Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji.
  27. Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi.
  28. Wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.
  29. Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke XE "wanawake:mwanamke"  (ajifanye mwanamke XE "wanawake:mwanamke" )na mwanamke XE "wanawake:mwanamke"  atapenda ajifanye kama mwanamme[103].
  30. Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea.
  31. Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.
  32. Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .
  33. Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko  kitu chochote kile.
  34. Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem. Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema "Ewe Bwana, naomba utwambie Dajjal XE "Dajjal"  atakuwa ni mtu wa aina gani?" Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal XE "Dajjal"  na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.
  35. Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota XE "nyota"  ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu XE "damu" . Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.
  36. Jua litakuwa pamoja naye.
  37. Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.
  38. Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,
  39. Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.
  40. Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal XE "Dajjal"  yatakauka hadi siku ya Qiyama XE "Qayama" ,
  41. Baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."
  42. Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.
  43. Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa XE "zinaa" ,
  44. Wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,
  45. Huyo Dajjal XE "Dajjal"  atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria XE "Syria" , atauawa siku ya Ijumaa mchana,
  46. Mtume Issa XE "Mtume Issa"  a.s. atasali nyuma ya Imam Mahdi XE "Mahdi"  a.s.
  47. Na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

UDONDOZI WA UBASHIRI

1687.   Kutoka dalili na mabashiri ya kudhihiri kwa Imam Mahdi XE "Mahdi"  a.s. hapa kuna madondoo machache ambayo yamechambuliwa:

1. Uasi wa Sufiani XE "Sufiani" ,

  1. kuuawa kwa Hasan,
  2. Ikhitilafu baina ya Bani Abbas kwa matakwa ya dunia.
  3. Kupatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani, ikifuatiwa na kupatwa kwa mwezi mwishoni mwa mwezi huo wa Ramadhani.
  4. Beda (mahala baina ya Makkah XE "Makkah"  na Madina XE "Madina" ) itadidimia ardhini,
  5. Ardhi katika upande wa Mashariki na upande wa Magharibi zitadidimia,
  6. Jua wakati wa asubuhi litaonekana liko papo hapo bila kutembea hadi wakati wa mchana na baadaye litachomoza kutoka Magharibi.
  7. Mcha Mungu atauawa nyuma ya msikiti wa Kufa XE "Kufa"  pamoja na watu sabini wengine.
  8. Mtu mwema kutoka ukoo wa Bani Hashim atachinjwa baina ya Rukn na Makam huko Makkah XE "Makkah"  XE "Makkah" .
  9. Kuta za Msikiti wa Kufa zitaporomoka.
  10. Bendera nyeusi zitatokezea huko Khorasan.
  11. Mtu kutoka Yemen XE "Yemen"  ataongoza uasi.
  12. Mtu atakayetokea nchi za Maghreb ataonekana huko Misri XE "Misri"  na ambapo atapata mamlaka makubwa.
  13. Warusi XE "Warusi"  watafika Bara la Arabia XE "Bara la Arabia" ,
  14. Wazungu XE "Wazungu"  watafika Palestina XE "Palestina" .
  15. Upande wa Mashariki kutaonekana kwa nyota XE "nyota"  yenye mkia. Mwanga wake utaonekana kama ule wa mwezi na ncha zake zote zitakuwa moja (zitaungana).
  16. Kutaonekana uwekundu mkubwa sana mbinguni.
  17. Kutazuka moto XE "moto"  mkubwa sana katika Mashariki ya kati ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu hadi saba.
  18. Wale wasio Waarabu watawafukuza Waarabu kutoka ardhi zao.
  19. Utawala wa kifalme utakwisha nchini Iran XE "Iran" .
  20. Wamisri watamuua kiongozi wao.
  21. Bendera tatu zitakusanyika Syria XE "Syria" .
  22. Kutazuka mizozo mikubwa na Syria itateketezwa.
  23. Bendera za Waarabu na Bani Qais zitatoka Misri.
  24. Bendera ya Banu Kinda itapepea Khorasan.
  25. Jeshi kubwa sana litapita Hira.
  26. Mabango meusi yatafika kutokezea Mashariki.
  27. Maji ya mito ya Furat yatafurika katika mitaa ya Kufa.
  28. Kutatokezea watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume.
  29. Sayyid kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imamu Mahdi
  30. Mtu mwenye heshima kubwa kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai karibu na Khankin.
  31. Kutajengwa na daraja katika Baghdad XE "Baghdad"  katika sehemu za Kharah.
  32. Kutakuwa na tufani ya upepo mkali katika Baghdad wakati wa asubuhi na kutafuatiwa na kupasuka kwa ardhi ambamo baadhi ya sehemu itadidimia ardhini.
  33. Mauti,vifo XE "vifo"  na maangamizo yatakithiri huko Iraq XE "Iraq"  kiasi kwamba watu watakuwa kama wamewehuka.
  34. Vikundi vitapigana mno huko Iran.
  35. Sura za jumuia zitachafuliwa.
  36. Watumwa wataanza kutawala nchi za Mabwana wao.
  37. Sura kama ya binadamu itaonekana karibu na jua.
  38. Makaburi yatafumuliwa na
  39. Waliokufa watapewa uhai.
  40. Kutakuwa na mvua XE "mvua"  itakayonyesha kwa mfululizo wa siku ishirini na nne ambayo itahuisha ardhi iliyokuwa imekufa.  Kwa hakika wakati huo ndio utakuwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s.

MUKHTASARI WA DALILI

1688.  

  1. Baghdad XE "Baghdad"  itateketezwa kabisa.
  2. Basra XE "Basra"  itazama.
  3. Waarabu watatawaliwa na mfalme wa ukoo mmoja tu kwa nguvu.
  4. Msikiti wa Borasa (baina ya Baghdad na Kazmain) utadhoofika.
  5. Kutakuwa na nchi nyingi za Kiislamu na kutakuwa na soko la kawaida
  6. Qum itakuwa ni kitovu cha mafunzo ya Kiislamu, kitakuwa ni kituo kipya kuliko kile cha Najaf (Iraq XE "Iraq" ). Na hapo ndipo kutakuwa kukitolewa ahkamu za dini.
  7. Kutakuwapo na reli kupitia katika nchi za Kiislamu.
  8. Azarbaijan itakumbwa na vita.
  9. Wanawake watakosa heshima kabisa.
  10. Duniani kote kutaenea sheria za kidemokrasia.
  11. Kutakithiri kizazi cha wanaharamu.
  12. Kutakithiri riba na rushwa.
  13. Kuzaliwa kwa wanawake waovu katika familia nzuri.
  14. Watu wenye hali ya chini wataweza kujenga majumba makubwa.
  15. Watu wema na waaminifu watakuwa wakiomba mauti ili waepukane na maudhi wanayoyapata.
  16. Watoto na majahili watapanda juu ya Mimbar, na watajulikana kama khatib.
  17. Wanazuoni watajiingiza katika mambo ya dunia.
  18. Madhumuni ya kutafuta Elimu itakuwa ni kutaka kutafuta pesa.
  19. Badala ya kusalimiana matusi ndiyo yatakayo kuwa yakitumika watu watakapokuwa wakikutana.
  20. Watu watatoka katika dini zao kwa sababu ya ulafi wa vitu.
  21. Dini ya Kiislamu itakuwa dhaifu.
  22. Mambo ya kuingiliana yatakuwa yakifanyika kidhahiri kama vile wafanyavyo wanyama.
  23. Wanawake watasuka nywele zao kama nundu za ngamia.
  24. Kupatwa kwa mwezi na jua na mitetemeko vitatokea Mashariki na Magharibi na baadaye katika Bara la Arabia XE "Bara la Arabia" .
  25. Kutakuwa na ongezeko katika kuzaliwa watoto wa kike.
  26. Ulawiti XE "Ulawiti"  na pombe XE "pombe"  vitakuwa ni vitu vya kawaida.
  27. Mitetemeko ya kila mara itaongezeka.
  28. Wanawake watakuwa na taasisi zao.
  29. Wanawake watafanya kazi pamoja na wanaumme katika kutafuta maisha yao.
  30. Usafiri utakuwa wa haraka sana.
  31. Kutakuwa na muongezeko wa ajali za njiani.
  32. Mavazi yatakuwa mafupi.
  33. Mwanamme na Mwanamke watajaribu kuonana sawa kijinsia
  34. Kutakuwa na ndoa za kuoa jinsia yake yaani mwanamme atamuoa mwanamme mwenzake na mwanamke XE "wanawake:mwanamke"  atamuoa mwanamke XE "wanawake:mwanamke"  mwenzake (na mambo haya hasa yanatokea katika nchi za Ulaya).
  35. Wakazi wa Kufa XE "Kufa"  na Najaf watakuwa wamekaribiana sana.
  36. Wakazi wa Makkah XE "Makkah"  na Madina XE "Madina"  wataongezeka.
  37. Hijab itakuwa imepotea (hijab, bubui).
  38. Maji yataanza kujaa katika ziwa Sawa.
  39. Kutakuwapo na nyota XE "nyota"  yenye mkia karibu na Capricorn.
  40. Watu wengi sana  watakufa kwa sababu ya kuenea kwa vita
  41. Misikiti XE "Misikiti"  na Qur’an XE "Quran"  itarembeshwa kwa dhahabu.
  42. Kutatokea  na moto XE "moto"  mkubwa sana katika mashariki na utaendelea kuwaka kwa siku saba.Na moto huo utatia khofu kubwa sana kwa mioyo ya watu.
  43. Kutakusanyika bendera XE "bendera"  tofauti tofauti huko Kufa na kusababisha mifarakano mikubwa.
  44. Utawala wa Kifalme utakwisha huko Iran XE "Iran" .
  45. Kutatokea na mivurugo katika nchi za Kiaarabu.  Kila nyumba ya mwarabu na nchi zote za Kiislamu zitahusishwa humo.
  46. Kukosa Imani kutaenea kote.
  47. Waislamu wataiga tamaduni na mila za maadui zao.
  48. Vifo vya ajali vitaongezeka.
  49. Ala za muziki zitaenea kiasi kwamba hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayesalimika kwa sauti zao.
  50. Watu wataanza kukataa kuwapo kwa Imam Mahdi XE "Mahdi"  a.s.
  51. Kutaonekana sura katika jua, na sauti zao zitasikika duniani kote.
  52. Mwanadamu atafika mwezini.
  53. Sufiani XE "Sufiani"  atatokezea na kueneza utawala wake wa vitisho.
  54. Sayyed Hassan atatokezea huko Iran.Na yeye atafika Multan kwa kupitia Kirman huku akiteka sehemu zote. Yeye atamfikia Imam a.s. Yeye atamfikia Imam Mahdi XE "Mahdi"  a.s. na kujIssalimisha mbele yake.
  55. Kutatokezea wazushi wa mtume sitini.
  56. Mtume Issa XE "Mtume Issa"  a.s.atateremka kutoka mbinguni.
  57. Maafa XE "maafa" , magonjwa ya kuambukiza na ukame utaenea kote.
  58. Nafsi ibn Zakia atauawa katika al- Khaaba (mtu mcha Mungu atauawa katika al-Kaaba XE "Kaaba" ).
  59. Jua litachomoza kutoka Magharibi kwa siku moja.
  60. Warusi XE "Warusi"  wataingia Bara la Arabia na watu weupe wataingia Bara la Parestina.Nao baadaye watapambana.
  61. Wachina XE "Wachina"  wataingia Bara la Arabia na kusababisha maangamio na maafa XE "maafa"  ambayo yatakuwa ni mambo ya kawaida.
  62.  Baadhi ya miji itateketezwa kwa sababu ya maafa na misukosuko.
  63. Sauti ya kutisha itasikika kutoka mbinguni.
  64. Kutokezea kwa Dajjal.
  65.  XE "Dajjal" Moto na moshi itakuwa kawaida duniani.
  66. Mvua zitatokezea pasipo na misimu yake.
  67. Kuongezeka kwa joto katika anga za juu.
  68. Kulipuka kwa moto XE "moto"  mkubwa katika Aden.
  69.  XE "Aden" Baadhi ya makundi ya wanaume yatakuwa yamegeuka maumbo.
  70. Kutatokea na mabadiliko ya ajabu katika sayari ya Capricorn
  71. Mkuu wa Dola ya Misri XE "Misri"  atauawa.
  72. Kutakuwapo na mvua ya mfululizo kwa muda wa siku ishirini na nne(24).Dunia nzima itakuwa imejaa michafuko, maafa na maangamizo n.k. 

1689.    Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo:

rudi nyuma Yaliyomo endelea