rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

10.  SADAQAH   NA  MISAADA: 

WANANYUMBA WANAOSTAHIKI MALIPO

Wanaostahiki malipo ni mke ( wa ndoa ya kudumu ) mtiifu na watoto wake na watoto wa watoto wake na vile inavyoendelea kuteremka chini na ambao anahitaji msaada basi ni faradhi. Vile vile baba na mama na babu mzaa baba na mama mzaa mama na vile itakavyoendelea juu na iwapo wanahitaji msaada wake na watu wngineo basi na kwa kiasi cha uwezo wake kama anao na iwapo hatawapa basi atatazamwa miongoni mwa watu kama qata’ rahmi (mwenye kukata udugu). Na jambo hili limezungumziwa katika makala mengineyo.

1.1. SADAQAH ZILIZO SUNNAH

Zipo aina nyingi za malipo yaliyo Sunnah. Katika Ayah na riwaya nyingi  kumesisitizwa mno kuwa sadaqah itolewe hususan katika siku ya Ijumaa, Siku ya ‘Arafah, katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani itolewe kwa makhususi ya majirani, majamaa n.k. Vile vile Sadaqah ni dawa ya ugonjwa, huondoa balaa, huleta riziki, huzidisha mali na huepusha vifo vya kutisha kama kuungua moto, kuzama maji  na kuwazuia Majinni na kwamba huondoa balaa sabini. Kila utakavyotoa sadaqah zaidi basi matokeo yake pia yatakuwa ni mazuri zaidi. Wala haina kiwango kidogo, kiasi chochote mtu atakachokitoa kitatosha walau hata kama atatoa tembe moja ya tende basi itatosha !

1. 2. ZAWADI

Ni kitu ambacho mtu mmoja anampa mtu kwa ajili ya kuongezea urafiki ama awe masikini au tajiri. Na iwapo hivyo itakuwa kwa nia ya kutaka furaha ya Allah swt, basi itakuwa ni ‘ibada bora kabisa.

Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144  kuwa :

“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaqah.”

2. 3. UGENI NA UKARIMU

Zipo riwaya nyingi mno kuhusu kuwakarimu wageni na kwamba hiyo ndiyo tabia njema ya Mitume s.a.w. na Ipo riwaya moja kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia :

“Nasikitika mno na ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake.”

4.  HAKI ILIYO MAALUMU NA ISIYO MAALUM

Inatubidi sisi tuwe tumepanga viwango maalumu vya kila siku au kila wiki au kila mwezi katika mali zetu kwa ajili ya wale wenye shida na kwa ajili ya jamaa zetu ili kukidhi mahitaji yao.

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al- Ma’arij,   , Ayah 24 – 25 :

Kutoka kwa Al Imam Musa bin Ja’afer a.s.ya kuwa  imepokelewa riwaya kuwa  :

“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa na mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha  mustarehe wakati nusu ya umriuliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikin.

Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha  mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilofikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hiyo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake. Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikini na uwe na uhusiano mwema pamojanao. Na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

Mtu huyo alizingatia na kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika wakati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa :’Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha  mustarehe kama ilivyo sasa.’”

 5.  HAKI YA UVUNAJI

Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono mmoja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Quran: Surah 69, Ayah 141 :

Katika aina za Sadaqah, aina hizi mbili za sadaqah ni Sunnah kwani Ayah ya Qur'an Tukufu pamoja na riwaya nyingi zimezungumzia na kusisitiza na ndio maana zimezungumziwa mbalimbali.

6.  KUKOPA MADENI

Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaqah na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika  Al-Wafi :

“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt analihisabia deni hilo katika Sadaqah hadi kulipwa kwake.”

Kila mara mtu atakapokuwa akimpa muhula mdaiwa wake kulipa deni lake, basi Allah swt atakuwa akimwandikia kuwa ametoa Sadaqah kiasi hicho kwani yeye alikuwa na haki kamili ya kufanya na kulazimisha malipo lakini hakutumia nguvu kudai na badala yake amemwongezea muda mdaiwa wake, hivyo inamaanisha kuwa amemkopa mara mbili katika mali hiyo. Hivyo mtu huyo anakuwa mustahiki wa kupata thawabu za kutoa Sadaqah kwa mara ya pili.

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa :

“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidi katika Qur'an Tukufu  adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wanaodai kuwapa vitu vya nyumbani.”