rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA,KHUMS NA SADAQAH

Kimeandikwa na:SYED DASTAGHIB SHIRAZI

Kimetarjumiwa na kuhaririwa na: AMIRALY M. H. DATOO

UTANGULIZI

Hapa nitapenda kuzungumzia machache kuhusu sadaqah

Sadaqah inalipia madeni na kuongezea neema kwetu,

Sadaqah inatuepusha na mauti katika hali mbaya

Siku ya Qiyama kutakuwa na jua na joto kali mno, lakini Muumin atakuwa katika kivuli, nacho ni kivuli cha sadaqah aliyokuwa akiitoa.

Toeni sadaqah asubuhi na mapema, ili balaa na matatizo yasiwafikieni katika siku nzima.

Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa sadaqah

Kutoa sadaqah ni afadhali kuliko kumnunua mtumwa na kumfanya huru

Mtu mmoja alifiwa na watoto wawili, alibakia mmoja. Akashauriwa kutoa sadaqah.Toeni sadaqah kwa mikono yenu wenyewe kwani hamtakuwa na  kifo kibaya, na ba Ilaa zaidi ya 70 zitaepukwa na kujiepusha na mitego 70 ya Shaitani, kwani Shaitani yupo anasema, “Usitoe sadaqah.” Je tutamwitikia Shaitani ?

Toeni sadaqah hata kama ni tonge moja ya tende na kama hiyo pia hamuwezi basi toeni tembe moja ya tende.

Sadaqah inatuepusha na balaa 70 ambamo kuna magonjwa, madhara ya moto, kuzama maji, kuangukiwa na kufunikwa na majumba yanayoporomoka na kubomoka na kutokuwa masikini,

Unapokuwa na hofu ya kuibiwa, kuugua n.k. basi toa sadaqah.