USAFI WA MWILI NA

UTAKASO WA ROHO

Kimeandikwa na:

HUJJATUL ISLAM WALMUSLIMEEN ALLAMAH AL-HAJ SAYYID MUHAMMAD RIZVI

Kimetafsiriwa na:

         DR. MUHAMMAD S. KANJU

HISTORIA FUPI YA MWANDISHI

WA KITABU HIKI

Hujjatul Islam Wal Muslimeen Allamah Al-Haj Sayyid Muhammad Rizvi, alizaliwa katika familia ya Maulamaa mwaka 1957 huko India. Babu yake marehemu Ustadhul Ulamaa Sayedul Hukama Maulana Al-haj Sayyid Abul Hassan Rizvi (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alikuwa mmoja wa Maulamaa wakubwa wa India na mzazi wake ni Rai'sul Mubaligheen Ayatullah Allamah Al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi) ambae alikuwa kati ya Maulamaa wakubwa wa zama hizi katika ulimwengu mzima na hususan bara la Afrika.

Hujjatul Islam Rizvi alipata elimu ya msingi huko Tanzania ambako ni makazi ya mzazi wake Allamah Rizvi na katika mwaka wa 1972 alikwenda Qum-Iran kwa ajili ya masomo ya juu chini ya Ma-Ayatullah (Maulama'a) wakongwe mbali mbali mpaka mwaka wa 1982.

Katika mwaka wa 1983 alikwenda Canada kwa mwaliko wa Jumuiya ya Waislamu Shia wa british Columbia, Vancover ambako alikuwa Imam wa Jumuiya na kwa ajili ya kazi za Tabligh. Alianzisha Taasisi ya Vancover Islamic Education Foundation. Mwaka 1998 kwa utaalamu wake katika masomo ya Kiislamu na vitabu vyake vilivyochapishwa alichaguliwa katika Programu ya masomo ya kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Simon Fraser University ambako alipata Shahada ya M.A. katika Historia mwka 1991.

Kuanzia msimu wa kiangazi mwaka 1991, anaishi Toronto kama Mkurugenzi wa Islamic Education & Information Centre na Imam wa Jaffari Islamic Centre.

Hujjatul Islam Rizvi amesafiri nchi nyingi kwa ajili ya kufundisha (katika Vyuo na Hadhara mbali mbali) na amechapisha vitabu mbali mbali kwa ajili ya watu wazima na halikadhalika kwa ajili ya watoto pia. Kufikia sasa ameandika vitabu zaidi ya 30 kwa lugha ya Kiingereza. Muhimu zaidi ya vitabu hivyo ni "An Explanatory Trans­lation of the Holy Qur'an" ambacho juzuu zake tatu za mwanzo zimekwisha chapishwa na juzuu zingine ziko kwenye matayarisho. Vitabu vya Hujjatul Islam Wal Muslimeen Allamah Al-Haj Sayyid Muhammad Rizvi vinapendwa sana katika ulimwengu na Taasisi mbali mbali katika nchi ya India, Iran n.k. wanarudia kuvichapisha huko kwao na vile vile vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha ya Ki-Urdu, Ki-Hindi, Ki-Indoneshian, Ki-Thaii na Kiswahili.

Ni mtaalam wa lugha huandika. huzungumza na kutoa mihadhara kwa Kiingereza, Kiurdu, Kiarabu, Kiajemi. Vile vile anayo elimu ya Kiswahili, Kigujrati na Kifaransa.

Amepewa Ijaza (mamlaka) na Ma-Ayatullah wakongwe wa Qum na Najaf kwa simulizi ya hadithi (riwaya) kwa mambo ya hukumu kwa sharia na vile vile kushughulika suala lolote ambalo ruhusa ya Mujtahid ni muhimu. Mbali na ukubwa na upana (wa eneo) analoshughulikia, na ziara za mara kwa mara ndani ya Canada na Marekani, amezuru kama nchi 20 za Asia, Afrika na Ulaya.

DIBAJI

Kitabu kilichopo mikononi mwako, ni tafsiri ya Kitabu cha Kiingereza, kiitwacho, The Ritual &SpiritualPurity, kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu, Hujjatul Islam Wal Muslimiin Al-Haj Allamah Sayyid Muhammad Rizvi wa Toronto, Canada.

Katika Sura tano za mwanzo za kitabu hiki Mwandishi hakuelezea tu hukumu na taratibu za kujitoharisha kiibada katika lugha nyepesi, bali vile vile amewazoesha wasomaji vyanzo vinavyotumiwa na Mujtahid katika kufikia uamuzi wao juu ya mambo mbali mbali ya utakaso wa Kiibada. Amefanya hivyo kwa kunukuu aya za Qur'an Tukufu na hadithi zihusikazo - hadithi za Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.)

Sura ya mwisho ya kitabu hiki humpeleka msomaji katika utangulizi wa safari ya ulimwengu wa kiroho wa Kiislamu. Mwandishi anamwongoza msomaji katika safari hii kwa kuhusisha mambo mbali mbali ya utohara wa kiibada na utakaso wa kiroho. Kwa hakika itabadili namna unavyofikiria juu ya utohara wa kiibada wa Kiislamu.

Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu nzima na tayari kimetafsiriwa katika lugha ya Kiurdu na Kihindi. Watu wengi wametuomba kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili pia.

Tulimwomba Ndugu yetu Dr. Mohammad Salehe Kanju, Mwenyekiti wa Shia Centre, Bilal Muslim Mission, Tawi la Mkumbara, kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya Kiingereza. Tunamshukuru kwa kufanya kazi hii kwa moyo mmoja.

Mission inatoa shukrrani zake za dhati kwa mwandishi, kwa mfasiri na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awalipe malipo mema hapo Duniani na huko Akhera - amin.

Bilal Muslim Mission of Tanzania Dares Salaam

 


NENO LA MFASIRI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu

Najiona kuwa ni mwenye bahati kupewa jukumu hili la kutafsiri kitabu hiki. Namshukuru Sayyid Murtaza Rizvi ambaye amenikabidhi jukumu hili na kuwezesha tafsiri hii kuchapishwa.

Kama Mwandishi alivyoandika katika utangulizi wake kwamba, "Kitabu hiki huthibitisha matumizi ya maana kwa wale ambao wanataka kujifundisha kuhusu Uislamu." Ujumbe huu ulikuwa kwa wasomaji wa Kiingereza. lakini kwa vile sasa kitabu hiki kiko kwenye lugha ya Kiswahili. basi ujumbe huu unahusu vile vile kwa wasomaji wa Kiswahili.

Ni matumaini yangu kwamba mtanufaika na yote yaliyomo katika kitabu hiki.

Nawashukuru wale wote walionisaidia katika kazi hii ya kutafsiri. Allah (s.vv.t.) Amzidishie Mwandishi wa kitabu hiki Afya njema na umri aweze kuandika ili nasi tufaidike na elimu yake - Amin.

Wabillahi Tawfiq, Dr. M.S. Kanju


UTANGULIZI:

Kitabu: Katika mwaka wa 1984 nilichapisha safu zijulikanazo kama 'Kamusi za shari'ah' ambazo zilichanganya vijitabu juu ya utashi wa kuelezea kwa kutumia akili za kibinadamu kanuni za Sheri'ah, Ijtihad, Taqlid, Taharat, Najasat, Wudhu ghusl, na Khums. Vitabu hivyo vilipokelewa vizuri sana na wasomaji katika sehemu mbalimbali za ulimwengu, al-hamdu li '1-lah. Ta'asisi ya Imam Mahdi Bombay imetafsiri vijitabu vitatu vya kwanza katika Urdu na kuvitumia kama matini katika duru yake ya mipango ya kufundishia.

Katika mwaka wa 1987 wakati ulipofika wa kuchapisha kwa mara ya tatu vijitabu vya Taharat & najasat na Wudhu & Ghusl. niliamua kuchanganya viwili hivi katika kimoja. Lakini wakati nikiwa navichanganya, nilifikiria kuviandika tena upya vitabu viwili hivyo na kuongeza baadhi ya majadiliano ndani yao. Lakini uandikaji huo na mara ya pili uliachwa kwa sababu ya masomo yangu na harakati nyingine mbalimbali. Hatimaye, mwaka huu Allah amenibarikia fursa ya kuandika mara nyingine tena na kukimalizia kitabu hiki, na matokeo ni haya unayoyaona katika mikono yake. Vijitabu Taharat & Najasat na Wudhu & ghusl vilikuwa ni maelezo mepesi ya kanuni za matendo ya ibada ya kujitakasa katika Uislamu, katika kitabu hiki, nimenukuu kwa wingi sana aya za Qur'an zinazohusika, na hadithi. Aidha, nimeongeza mijadala mingine miwili mipya: Sehemu moja, juu ya "Mtazamo wetu juu ya najasat" ambayo hushughulika na suala ambalo ni muhimu sana kwa Waislamu, na ya pili ni sura "Kutoka matendo ya ibada mpaka kwenye roho" ambayo hujaribu


kuhusisha utakaso wa matendo ya ibada na utakaso wa kiroho. Sura hii ni katika kuitikia na kuikabali haja ambayo niliiona katika jumuiya za sehemu mbalimbali, ambazo kwanza nilikuwa nikifanya kazi nazo kwa muda wa miaka saba iliyopita. Kwa bahati nzuri, matendo ya ibada yanatekelezwa na wengi; lakini bahati mbaya yanachukuliwa kama ibada tu na si chochote zaidi. Nafikiria ni bora zaidi kwa Waislamu kujua namna ya kuzitumia ibada za kila siku za Taharat, Wudhu, Ghusl na Salat kwa ajili ya kuboresha roho zao. Sura mpya bado inaweza kupanuliwa kwa kuongeza maana ya kiroho ya Salat za kila siku, suala ambalo nililijadili katika khutuba kumi na mbili nilizotoa wakati wa Muharram wa mwaka huu. Lakini katika kitabu hiki nilitaka kujishughulisha zaidi na utakaso wa roho ambao ulihusiana na utakaso wa ibada. Na hivyo nimeacha mambo mengine ya kiroho kwa ajili ya vitabu vya baadae, Insha-Allah. Natumaini wasomaji wataona Sura hii ni yenye kuelimisha na yenye manufaa; na ninawahimiza viongozi, hususan wa vikundi vya Waislamu katika nchi za Magharibi kusoma sura hii na kujaribu kutekeleza mafundisho yake katika njia wanayoifikiria, kutenda na kushughulika na watu.

****

Chimbuko la Shari'ah: Hiki ni kitabu cha sheria za Kiislamu, zijulikazo kama Shari'ah. chimbuko la Sheria za ki-Islamu ni Qur'an na Sunnah. Kwa kusema Sunnah, tuna maana ya semi, matendo na kuthibitisha kwa kunyamaza kwa Mtume na Ahlul '1-bayt.

Qur'an huelezea hukumu za msingi tu na sunnah hufafanua juu ya hukumu hizo. Qur'an imemtambulisha Mtume wa Uislamu kama ifuatavyo:-

"Yeye (Allah) ndiye aliyeleta Mtume miongoni mwa watu wa kawaida, Mtume anayetokana na wao wenyewe, awasomee aya zake, kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hekima. " (62:2)


"Na tumeteremsha kwako wewe (Ee Muhammad) ukumbusho (yaani Qur 'an) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao na ili wapate kufikiri." (16:44).

Aya hizi mbili zinatosha kuthibitisha kwamba Mtume Muhammad (amani iwe juu yake) hakuwa mtu wa kuleta ujumbe tu ambapo kazi yake ilikuwa ni kufikisha tu kitabu kwetu. Alikuwa Mwalimu na mfasiri wa Qur'an. Hata matendo yake ni chimbuko la mwongozo kwetu:

"Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Allah, kwa mwenye kutegemea kwa Allah na siku ya mwisho, na kumtaja Allah sana. " (33:21) Utii kwa Mtume umechukuliwa kama uthibitisho wa kumpenda Allah, "Sema (Ee Muhammad): 'Kama mnampenda Allah, basi nifuateni (kamam mkifanya hivyo) Allah atakupendeni na kuwasamehe madhambi yenu. " (3:31) Qur'an inasema zaidi: Yeyote yule anayemtii Mtume hakika amemtii Allah... " (4:80).

Waislamu ambao walioishi wakati wa Mtume walikuwa na njia

rahisi ya kuzipata Sunnah zake. Je, vipi kuhusu sisi ambao tulizaliwa mamia ya miaka baada ya kifo cha Mtume? Naam, Waislamu wa siku za mwanzo walielewa umuhimu wa Sunnah za Mtume na wakaanza kuhifadhi misemo yake katika vitabu vya hadithi. Hata vitendo vya Mtume, vilivyoshuhudiwa na Masahaba vilihifadhiwa katika maandishi. Lakini utaratibu huu wa kuhifadhi Sunnah za Mtume haukuwa na kinga kutokana na makosa na hata kughushi. Misemo mingi ilibuniwa na kwa makosa makubwa ikahusishwa na Mtume wakati wa kipindi cha mwanzo cha historia ya ki-Islamu.

Kwa hiyo, ni muhimu kabisa kutafuta hadithi sahihi na wakati huo huo kutafuta vyanzo vyenye ujuzi na elimu kwa ajili ya Sunnah za Mtume. Wakati ukiwaangalia Waislamu wa wakati wa Mtume, huwezi kuona mtu yeyote ambaye anaweza kuwa na elimu zaidi, mjuzi muaminifu na karibu na Mtume kuliko Ahlul i-bayt, familia


ya Mtume. Mbali ya yote,   ni Qur'an ambayo huthibitisha utohara wao wa kiroho wa daraja la juu mno; kwa kusema:-

"Hakika Allah anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) (yaani Ahlul 'l-bayt) na anataka kukutakaseni kabisa kabisa. " (33:33) Changanya aya hii kuhusu utohara wa Ahlul i-bayt pamoja na aya ifuatayo:-

"Hapana aigusaye ila waliotakaswa na mabaya. " (56:79). Hii huonyesha kwamba Ahlul 'l-bayt wanaweza kuielewe Qur'an vizuri zaidi kuliko mfuasi yeyote wa muhammad (s.a.w.). Allah anasema: "Sema (Ee Muhammad) Siombi zawadi yoyote kutoka kwenu (kwa kuleta ujumbe huu) isipokuwa kuwapenda jamaa zangu wa karibu " (42:23).

Angalia kwamba, ni Allah ambaye ndiye anayemuamrisha Mtume Wake kuwataka watu kuipenda familia yake. Kama wasingekuwa waaminifu, wakweli na wabora wa kufuatwa, je Allah angetuamrisha sisi tuwapende?

Aya hizi chache zatosha kuonyesha kwamba wafasiri bora wa Qur'an na vyanzo sahihi zaidi kwa ajili ya Sunnah za Mtume ni Maimamu wa Ahlul 'l-bayt. Mtume mwenyewe alisema

"Ninakuachieni miongoni mwenu vitu viwili vizito. Muda mnashikamana navyo vyote, hamtapotea kamwe baada yangu. Moja ya viwili hivi ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Allah (ambacho ni kamba iliyoning'inia kutoka mbinguni mpaka ardhini) na kizazi changu, Ahlul'l-bayt, Vitu hivi viwili havitatengana kutoka kingine mpaka vinifikie katika (chemchem ya) Kawthar (Kesho akhera). Kwa hivyo angalieni namna mnavyonilipa kwa jinsi mnavyoshungulika nao. " Hapa sio mahali pa kujadili kuhusu usahihi wa hadithi hii, lakini nitamnukuu Ibn Hajar al-Makki mwanachuoni mashuhuri mbishani dhidi ya shi'ah. Baada ya kuandika


Hadithi hii hapo juu kutoka kwa masahaba wengi ambao wameisikia kutoka kwa Mtume katika sehemu mbali mbali na nyakati tofauti Ibn Hajar anasema, "Na hakuna kukinzana (Katika taarifa hizi nyingi) kwa vile kulikuwa hakuna cha kumzuia Mtume kutokana na kurudia (Maelezo haya) katika sehemu hizo mbali mbali kwa sababu ya umuhimu wa kitabu kitukufu na familia toharifu.[1]

Tunaweza kuhitimisha kutokana na aya hizi na hadithi zilizotajwa hapo juu kwamba Ahlul-'l-bayt ni sahihi zaidi na vyanzo bora zaidi kwa ajili ya Sunnah, na kwa hiyo tunawapendelea wao zaidi kuliko vyanzo vingine vyote. Wakati wowote tunaponukuu hadithi kutoka kwa Maimamu, kwa hakika sio kutoka kwao wenyewe, badala yake ni hadithi ya Mtume ambayo wameihifadhi kama makamu (warithi) wa kweli wa Mtume wa mwisho wa Allah. Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) anasema, "Hadith yangu ni hadithi ya baba yangu, hadithi ya baba yangu ni ile hadithi ya babu yangu, hadithi ya babu ni ile hadith ya al-Husein (bin Ali), hadithi ya al-Hasan ni ile ya Amiru-'l-Muuminin (Ali bin Abi Talib) (a.s.) hadith ya Amiru '1-Muumin ni ile ya Mtume wa Allah (s.a.w.) na hadithi ya Mtume ni maelezo ya Allah, mkubwa mwenye nguvu zote."[2]

Ijtihad & Taqlid: Baada ya Imamu wa kumi na mbili Imam al-Mahdi (a.s.) alipoingia kwenye ghaibah, jukumu la kuongoza Shari'ah katika mambo ya Shari'ah yakawa juu ya Mujtahidi, wanachuo wa dini waliosomea zaidi na kubobea katika sheria za ki-Islamu. Mujtahidi hutoa hukumu za ki-Islamu kutoka vyanzo viwili

vilivyotaja hapo juu. Hii inaweza ikaonekana rahisi sana, lakini sio hivyo. Hawafungui tu Qur'an na vitabu vya hadith, na kuanza kutoa fatwa. Kabla ya yote lazima kwanza waanze na utaratibu maalum (unaojadiliwa katika somo linalo julikana kama Usu'lu '1-fiqh). Katika utaratibu wao huu, wanaamua namna ya kuchunguza aya za Qur'an na hadith. Je? Yawabidi kutafuta ni aya gani imekuja kwanza na ipi iliyokuja ya pili katika suala hilo hilo? Je, aya ya pili itafuta ya kwanza au itaweka baadhi ya mipaka tu juu yake? Je, kila hadithi ichukuliwe kama sahihi? Kama sivyo, ni njia gani za kuthibitisha usahihi wa hadithi Iliyotolewa? Kama wakikutana na hadith mbili sahihi katika suala moja ambazo zenyewe hupingana, basi watafanya nini? Kama Qur'an na Sunnah zimenyamaza juu ya suala fulani ni njia gani itapasa kufutwa? Matatizo yote haya yanabidi kupata ufumbuzi wakati wa kutengeneza elimu ya utaratibu wa Ijtihad, na ni mpaka hapo tu, Mujtahidi kwa usahihi na kwa kuwajibika anaweza kutoa hukumu kutoka katika Qur'an na Sunnah.

Ni wazi kwamba sio wote wana uwezo au muda wa kujifunza na kuwa mabingwa katika kanuni na hukumu za shari'ah; na kwa hiyo kwa watu kama hawo ni muhimu kwao kufuata Mujtahid katika mambo ya shari'ah. Kanuni za juu ya ibada ya tohara iliyotolewa katika kitabu hiki zaweza kufuatwa na wafuasi wa Mujtahidi wa daraja za juu kabisa wa wakati wetu, hususan Ayatullah al-udhma Sayyid Abu '1-Qasim al-Musawi al-khui na marhum Ayatullah al-Udhma al-Imam Sayyid Ruhullah al-Musawi al-Khumayni. Kama kutakuwa na hitilafu miongoni mwa Mujtahidi wa sasa juu ya mambo ya ibada ya tohara ni katika kiwango cha makruh na mustahab, lakini sio katika kiwango cha wajib na haram. Wakati wowote ule hitilafu miongoni mwa Mujtahidi ikiwa katika haki kubwa mno, nimetoa maoni yao kwa kuyaweka mbali mbali.

Hadith katika kitabu hiki hazikuchanguliwa bila utaratibu, nimejaribu kwa uwezo wangu kuchunguza usahihi wao na kukubalika kabla ya kuzitumia.

Sababu moja ya kuandika aya zinazohusika, na hadith katika kitabu hiki ilikuwa ni kuwafanya wasomaji wawe wazoefu na baadhi ya vyanzo ambavyo Mujtahidi hutumia kufikia hitimisho zao. Hili, naamini vile vile litasaidia kuondoa mawazo yatolewayo na baadhi ya watu kwamba kanuni za Shari'ah si chochote bali ubunifu wa 'ulama"

Natumaini kitabu hiki huthibitisha matumizi ya maana kwa wale ambao wanataka hujifundisha kuhusu Uislamu; na ninaomba kwa Allah Subhanahu wa Ta'ala kukikubali kama mchango mdogo kwenye kuuhudumia Uislamu kutoka kwa mtumishi wake huyu mnyenyekevu mno.

Inna rabbi la Samiud- Du'a

Richmond, B.C.                      SAYYID MUHAMMAD RIZVI

Rabi'u'l-Awwal 14IO

October 198

SURA YA KWANZA

NAJASAT NATAHARA

A. Baadhi ya Istilahi muhimu.

"Najasat" (wingi: najasat) maana yake uchafu, vitu vichafu.

Katika sheria za ki-Islamu, najasat ni za aina mbili: ya asili na ya kujipatia. Kutofautisha kati ya mbili hizo ni: kitu ambacho ni cha uchafu wa asili hujulikana kama "ayn najis, " ambapo kwamba kitu ambacho uchafu wake wa kujipatia, hujulikana kama "najis". Kitu kisafi hupatwa na uchafu kwa kugusana na moja ya 'ayn najis'. Kwa mfano, damu huchukuliwa kama 'ayn najis', ambapo maziwa huchukuliwa kama kitu safi. Hivyo, kama tone la damu litadondokea kwenye glasi ya maziwa, maziwa yatakuwa najis kwa sababu ya damu ambayo ni 'ayn najis' Wingi wa 'ayn najis' ni "a 'yan najisah "

"Taharat" Ni kinyume cha "najasat, " ina maana ya usafi na tohara. "Tahir" ni kunyume cha  "najis, " ina maana ya kitu ambacho ni safi na tohara.

B. AYA NAJASAT A'YAN

        (Vitu najasat kwa asili yake)

Kwa mujibu wa sheria za ki-Islamu, 'ayn najisah' kwa idadi ziko tisa. 'Ayn najisah' zinaweza kugawanywa katika makundi manne kama ifuatavyo:

i. Sawa kati ya watu na wanyama:

1. Mkojo;

2.       kinyesi;

3.       Manii;

4.       Damu.

5.       Mayii

ii. Kwa wanyama tu:

6.    Mbwa

7. Nguruwe

iii. Kwa watu tu : 

8.    Kafir
iv.Vinywaji:

9.    Vinywaji vinavyo levya.

Maana ya sheria hii kwa Mwislamu ni kwamba aweze kujiepusha kutokana na a'yan najisah katika mambo matatu: Matendo ya ibada, chakula na vinywaji.

Katika sura zifuatazo, tutaelezea kanuni zinazohusiana na vitu tisa vichafu vya asili.

1. & 2.MKOJO NA KINYESI

Mkojo na kinyesi cha mwanadamu ni 'ayan najis. Watu wengi duniani huchukulia mkojo na kinyesi kuwa ni uchafu, lakini Uislamu umekwenda hatua moja zaidi kwa kutamka kwamba ni vichafu kiibada. Kwa mfano, katika mambo ya ibada ya Mwislamu ambaye amekojoa au amekwenda haja kubwa hawezi kusali hata baada ya kusafisha mwili wake kutokana na mkojo huo na kinyesi - ni lazima achukue au afanye Wudhu, josho dogo ambalo litajadiliwa katika sura ya 2.

Shariah ya Kiislamu imeelezea kanuni makhsusi juu ya jinsi mtu atakavyojisahfisha kutokana na mkojo na kinyesi.

1. Kiungo cha mkojo kinaweza kufanywa tohara tu kwa kumwaga maji juu yake mara mbili hivi. Ni bora kukiosha mara tatu.

2.  Kwa jinsi njia ya haja kubwa inavyohusika, mtu anaweza
kujisafisha kwa maji, au kwa vipande vitatu vya karatasi au
vipande vitatu vya matumbawe au mawe matatu. Makaratasi,


matumbawe na mawe yanaweza kutumika tu kama njia ya haja kubwa haikuchafuka  kupita kawaida.   Kama sehemu iliyochafuliwa ni kubwa, au kinyesi kimechanganyikana na. najasat nyingine kama damu, basi ni maji tu ndiyo yanayoweza kutumika kumtoharisha mtu.

Hata hivyo ni bora wakati wote mtu kujisafisha na maji, Wakati akiwasifia watu ambao walijenga Masjid Qubah, Allah anasema:

"Humo wamo watu ambao hupenda kujitakasa; na Allah huwapenda wale ambao hujitoharisha. " ( 9: 108). Wakati ilipoteremshwa aya hii, Mtume akawauliza watu- wa Quba, "Mnafanya nini mnapqjisafisha ambacho Allah amekusifuni nacho?" Wakasema, "Tunajisafisha na maji baada ya kwenda haja kubwa." [3]

3.      Katika kujisafisha mtu kwa vipande vya karatasi, matumbawe au mawe, ni wajibu kutumia vipande vyote vitatu hata kama
mwili umekuwa safi kwa kipande kimoja au viwili. Hata hivyo, kama mwili haukuwa safi hata baada ya kutumia vipande vyote vitatu, basi vipande zaidi lazima vitumiwe mpaka mwili uwe safi.

4.  Imependekezwa kwa wanaume kufanya "istibra"  baada ya kukojoa. "Istibra" maana yake ni kusafisha kitu, kuondokana na kitu.  Hapa ina maana kuondokana na matone ya mkojo kutoka kwenye uume. Namna ya kufanya istibra; Kamua kwa kidole cha kati chamkono wa kushoto kuanzia njia ya haja kubwa mpaka kinapo anzia kiungo cha mkojo mara tatu; kisha unashikilia kiungo cha mkojo kati ya dole gumba na vidole vya mbele, kamua mara tatu kuanzia kinapoanzia kiungo cha mkojo
mpaka kwenye kichwa; na kamua kichwa chenyewe mara tatu.

Faida ya istibra: Kama majimaji yatatoka kwenye kiungo cha mkojo baada ya kukojoa na mtu akatia shaka iwapo huo ni mkojo au kitu kingine, basi anaweza akachukulia kuwa ni tahir kama amefanya istibra. Lakini kama hakufanya istbra basi lazima aichukulie hiyo kuwa ni najis.

5.Katika vyoo vya kimagharibi (vya kizungu) hakuna maji, mnapatikana makaratasi tu. Kwa jinsi choo kikubwa  kinavyo husika, kinaweza kusafishwa na karatasi kama ilivyo elezwa hapo juu. Je, katika hali ya kukojoa, itatosha
kufuta sehemu inayohusika kwa karatasi? Hapana, kufuta kwa karatasi hakutatoharisha kiungo cha kukojolea. Pamoja na
hayo, katika hali kama hiyo, mtu yampasa kufanya istibra' na kufuta hicho kiungo kwa karatasi na baadae ikija wezekana lazima atoharishe kiungo hicho kwa maji. Faida ya istbra na kufuta kwa karatasi ni kwamba kiungo kitakuwa kikavu na hakitafanya nguo ya ndani (Chupi) au mapaja kuwa najis.

Hata hivyo, katika hali hiyo hapo juu, kama sehemu za siri za mtu zitatoa jasho, basi ni lazima atoharishe kwa maji kiungo hicho, sehemu zinazokizunguuka na nguo ya ndani. Ays bin al-Qasim alimuuliza Imamu Ja'afr as-Sadiq (a.s.) kuhusu mtu ambaye anakojoa sehemu ambayo haina maji na hivyo akakikausha kiungo cha mkojo kwa jiwe, lakini baadae akaanza kutoka jasho katika sehemu ile ile. Imam akasema: "Lazima aoshe kiungo chake cha mkojo na mapaja (kwa maji)."[4]

6. Wakati unajisaidia haja, ndogo au kubwa ni muhimu mtu kuficha sehemu zake za siri kwa watazamaji. Sharti hili huwezekana kirahisi katika vyoo vya kawaida, lakini mtu lazima awe muangalifu wakati wa kujisaidia katika sehemu za watu kwa mfano, wakati wa mandari au wakati wa safari n.k.

7.       Mwislamu yampasa vile vile aelewe kwamba hata katika kitu hafifu kama hicho, kama kutumia choo, Uislamu unasisitiza kwamba, ama uwe ni mwenye kumiliki choo hicho, au lazima
uwe na ruhusa ya mwenye choo hicho vinginevyo itakuwa haramu kwako wewe kutekeleza haja zako za kimaumbile katika
sehemu hiyo.

8.       Ni haramu kuelekea kibla ua kukipa Kibla mgongo wakati wa kujisaidia haja ndogo au kubwa. Kibla maana yake muelekeo wa Ka'abah (Makka).  Kwa hiyoMwislamu lazima awe na hakika kwamba choo cha nyumba yake hakikujengwa katika hali ambayo kwamba wakati akijisaidia ndani ya choo hicho, uso wake au mgongo huelekea upande wa Kibla. Kama hali inalazimisha kutumia choo ambacho ndani yake mtu ataelekea kibla au atakipa mgongo, basi itampasa kujiepusha kuelekea Kibla.

******

    Mkojo na kinyesi cha wanyama vile vile ni najis kama hutokana na wanyama (1) ambao nyama yao imekatazwa katika Uislamu na (2) ambao damu yao hutoka kwa nguvu wakati mshipa wa damu unapokatwa. Kwa hiyo, kama hali hizi mbili hazipatikani pamoja katika mnyama, mkojo wake na kinyesi sio najis. Kwa mfano, ingawa damu ya kondoo hutoka kwa nguvu, mkojo wake na kinyesi sio najis kwa sababu nyama yake haikukatazwa.

Hata hivyo, vinyesi vya ndege wote ni tahir. Je. mtu atafanya nini kama aliona kinyesi cha mnyama au uchafu utokanao na mnyama na hajui hutokana na mnyama wa aina gani? Katika hali zote za ujinga na mashaka, mtu anaweza akachukulia kwamba hutokana na mnyama ambaye mkojo au kinyesi chake ni tahir.

Abu Aghar an-Nahhas mtu mzoefu alimuambia Imam Ja'afar as-Sadiq (a.s.) "Nahudumia wanyama. Wakati mwingine huenda usiku (kuwa hudumia). Mnyama huenda amekojoa na kutoa kinyesi, na wakati akiruka juu ya uchafu, na mkojo wake wenyewe, ukaruka juu ya nguo yangu. (Nifanye nini?)" Imam akasema,'Hakuna kitu juu yako.'" Jibu hili linaweza kuelezwa katika njia mbili; Abu Aghar anaweza kuchukulia kuwa nguo yake bado ni safi (tohar) kwa sababu katika giza la usiku asingeweza kuwa na hakika ni nini kilichoingia katika nguo yake, au kwa sababu wanyama walikuwa mifugo ya nyumbani na hivyo kinyesi chao na mkojo sio najis.

3. MANII

Manii vile vile ni moja ya 'ayn najis'. Kuna hadithi nyingi juu ya suala hili, lakini hapa nitaelezea tukio la kihisitoria na kuhusiana kwake na aya ya Qur'an ambayo huthibitisha kwamba manii ni najis. Katika vita vya Badir Makafir wa Makka walipiga kambi karibu na chem chem ya Badir na ardhi katika sehemu ya kambi yao ilikuwa ngumu. Kwa upande mwingine Waislamu walikuwa mbali na chem chem na hivyo wakapata shida ya kupata maji, na ardhi chini yao ilikuwa ya kichanga ambayo ilifanya kusimama na kutembea kwao kuwa kwa tabu, kufanya mambo yawe mabaya zaidi, Waislamu wengi walitokwa na Manii wakiwa usingizini na wakanajisika. Kisha ukaja msaada wa Allah ambao unaelezewa na Qur'an kama ifuatavyo:

"Na (kumbuka) wakati alipowafunika na usingizi juu yenu kama ulinzi kutoka kwake (na hiyo mkalala kwa amani). Na, aliteremsha maji juu yenu kutoka mbinguni kuwatoharisheni kwayo, kuwatoleeni uchafu wa shetani, kuimarisha nguvu zenu na kuweka Miguu yenu imara kwayo (8:11).

Maneno yanayohusiana na somo letu ni:- "Aliteremsha maji juu yenu kutoka mbinguni kuwatoharisheni kwayo. " Kwa uchache ni kwamba aya hii huthibitisha kwamba manii ni najis, na kutoka kwake mtu hunajisika.

Abdullah ibn Ya'fur alimuuliza Imam Ja'afar as- Sadiq (a.s.) kuhusu nguo ambayo imeingiwa na manii. Imam akasema "Kama unajua sehemu makhususi ya nguo illiyoingiwa na manii, basi safisha sehemu hiyo tu; lakini kama sehemu hiyo huijui, basi safisha nguo yote." [5]

******

Wakati mwingine maji maji, mbali na manii na mkojo humtoka mtu; aina hii ya maji maji sio najis. Maji maji haya yako aina tatu:

1. Madhi          Mazi:    Maji maji haya meupe ambayo hutoka kwenye uume wakati wa mchezo kabla ya kujamiiana.

2. Wadh Wazi: Maji maji ambayo hutoka baada ya kutoa manii.

3. Wadi           Wadhi:   Maji maji ambayo hutoka baada ya kukojoa. Maji maji yote haya ni tahara.

4.  DAMU      Damu ya mwanadamu ni najis.

Damu ya wanyama ambao damu yao hutoka kwa nguvu vile vile ni najis. Lakini damu ya mnyama ambaye damu yake haitoki kwa nguvu ni tahir, kwa mfano, Damu ya samaki au maji maji yatokanayo na mbu.   Ibn Abi Ya'fur alimuuliza Imamu Ja'far as-Sadiq (a.s.), "Unasemaje kuhusu damu ya viroboto? " Imamu akasema, "Hakuna kipingamizi ndani yake." IbnAbi Ya'fur: "Hata kama ikiwa ni nyingi zaidi? " Imam, "Ndio, hata kama ikiwa zaidi."[6]

Baada ya mnyama kuchinjwa na kiasi cha damu cha kawaida kimetoka, damu inayobakia mwilini mwake ni tahir.

*****

 


Damu inayopatikana katika yai vile vile ni najis. Kama kuna damu katika nguo ya mtu au katika mwili wake na akatia shaka iwapo ni ya mnyama ambaye damu yake hutoka kwa nguvu au la basi itampasa afikirie kuwa ni tahir.

Kama maji maji ya njano yakitoka kwenye kidonda na mtu akatia shaka iwapo ni damu au kitu kingine, basi itampasa afikirie kuwa ni tahir.

Ingawa damu inafikiriwa kuwa najis, bado mtu anaruhusiwa kujitolea damu (kumpa mtu mwingine), au kuuza damu yake. Madakitari, wauguzi na wanasayansi wanaweza wakashughulika na kufanya uchunguzi na damu. Kitu kimoja muhimu ni kwamba katika wakati wa kusali, mwili wa mtu na nguo lazima ziwe tohara kutokana na najis hii.

5. MAYIT

Mwili wa Muislamu aliyekufa huwa najis baada ya kuwa baridi na kabla ya kuoshwa (ghusl mayyit).

Al-Halabi alimuuliza Imamu Ja-far as-Sadiq (a.s.) kuhusu mtu ambaye nguo yake imedondokea juu ya mwili wa mwanadamu aliyekufa.   Imam akasema, "Kama mwili wa mayit utakuwa umekoshwa josho la sheria (ghusl mayyit), basi hakuna haja ya kuosha nguo yake ambayo imegusa mayit; lakini kama mayit hajaoshwa josho la sheria, basi safisha sehemu ambayo nguo yako imegusana na mayit.[7]

Kafir ni najis nyakati zote wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake.

Kama sehemu ya mwili wa mwanadamu anayeishi au mnyama anayeishi ikikatwa, itachukuliwa kuwa ni najis. Hata hivyo sheria hii haihusu ngozi iliyokauka inayotoka kwenye midomo ya ngozi inayotoka kwenye kidonda kinachopona, au chunusi, mba n.k. Mimba iliyotoka vile vile ni najis.

"Mfu - Maytah" Katika hali ya vitu vya wanyama: mnyama yoyote ambaye amekufa kifo cha kawaida au alichinjwa katika njia isiyokuwa ya Kiislamu.

Mfu wa mnyama ambaye damu yake hutoka kwa nguvu vile vile ni najis isipokuwa sehemu zile ambazo hazina uhai (hisia) ndani yake wakati wa uhai, km. Nywele, kucha, mifupa mdomo wa ndege, pembe na meno. Naam, hakika sehemu hizi huwa najis kwa kuwa pamoja na mfu; hivyo baada ya kuzitenganisha kutoka kwenye mwili wa mnyama lazima zitoharishwe.

Mfu wa mnyama ambaye damu yake haitoki kwa nguvu ni tahir. Km. Samaki aliyekufa. Ammar as-Sabati anasema kwamba Imam Ja'far as-Sadiq aliulizwa kuhusu duduvule (mende) inzi, nzige, sisimizi na vitu vingine vya aina hiyo vinavyokufa ndani ya kisima, mafuta siagi au vitu vingine kama hivyo. Imam akajibu, "Hakuna pingamizi kuhusiana na vyote hivyo ambavyo havitoi damu kwa nguvu."[8]

****

Kama mtu akinunua nguo, mkanda, au pochi, nk. Iliyotengenezwa na ngozi ya mnyama na hajui kwa hakika iwapo mnyama amechinjwa Kiislamu au la, basi katika hali kama hiyo kuna uwezekano wa namna mbili:

1-Ama awe ameinunua kutoka kwa Muislamu au kutoka kwenye soko la Muislamu, basi anaweza kuchukulia kwamba mnyama huyo alichinjwa kwa mujibu wa Shari'ah.

2-Au ameinunua kutoka kwa kafir, katika hali kama hiyo kama kuna uwezekano kwamba ngozi hiyo imetokana na mnyama aliyechinjwa kwa mujibu wa Shari'ah, basi anaweza kuifikiria kuwa tahir na kuitumia. Hata hivyo, bado hawezi kutumia kitu hicho katika sala.  Na kama hakuna uwezekano huo, basi hawezi kuifikiria kuwa ni tahir, itapasa ifikiriwe kuwa ni najis.

6& 7 NGURUWE NA MBWA

Nguruwe na mbwa vile vile huhesabiwa kama 'ayn najis. Allah anasema katika Qur'an: "(Ewe Muhammad) Sema, sioni katika niliyoteremshiwa chochote kilicho katazwa kwa mtu kula isipokuwa (1) Kilichokufa chenyewe, (2) kilichosongelewa damu, (3) nyama ya nguruwe kwa vile ni chafu - na (4) kilicho chinjwa kwa jina lisilokuwa la Allah (6:145).

Ingawa aya hii inahusika kwenye chakula kilichokatazwa, lakini kwa uwazi hudhihirisha nguruwe kama mnyama mchafu. Khayran al-Khadim alimuandikia lmam Ali an-Naqi (a.s.) akimuuliza kuhusu nguo ambayo imegusana na kinywaji chenye kulevya na nyama ya nguruwe: "Je mtu anaweza kusali na nguo hiyo? Masahaba wetu wana maoni tofauti baadhi wanasema unaweza kusali nayo kwa sababu Allah amekataza kunywa vileo tu, ambapo wengine wanasema huwezi ukasali nayo." Imam akajibu, "Usisali na nguo hiyo kwa sababu ni najis."[9]

Abu Sahl al-Qarshi alimuuliza Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) kuhusu mbwa: Je? Mbwa ni haramu? Imam akasema, "Ni najis." Abu Sahl alirudia swali hili mara tatu na Imam mara zote akajibu "Ni najis." [10]

Kwa kutegemea juu ya mafundisho hayo, Mujtahidi wetu wamehukumu kwamba sehemu zote za nguruwe na mbwa, hata kucha, nywele, meno na mifupa na mate yao maziwa, mkojo na kinyesi vyote ni najis kwa hiyo, vitu vyote vinavyofanywa kutokana na mafuta ya nguruwe, ngozi, nywele, na sehemu nyingine za mwili wake (km. mkanda soksi za mikono, (gloves), jackets na viatu) ni najis. Halikadhalika bidhaa zote za chakula zinazotengenezwa kutokana na mnyama na mafuta ya nguruwe ni najis.

8. MAKAFIR

Nini maana ya "Kafir?" (Wingi - Kuffar) maana ya  kafiri, ni  asiyeamini kinyume na Muislamu, Muumini. "Muislamu" inaelezea kama mtu ambaye anaamini  umoja wa Mungu, Utume wa Mtume Muhammad na siku ya malipo. Mtu anayekataa moja ya kanuni hizi tatu ni Kafir.

Kwa mtazamo wa Waislamu, makafir wamegawanyika katika makundi mawili: Kafir dhimmi na Kafir harbi.

"Kafir dhimmi" ni kafir ambaye anaishi chini ya himaya ya Serikali ya Kiislamu.

"Kafir harb" ni kafir ambaye hana himaya hiyo. Lazima nitaje kundi la tatu, lakini kundi hilo la makafir huonekana mara chache sana: Murtad. "Murtad" maana yake aliyetoka kwenye dini; kuna aina mbili za murtadi: "Murtad fitri" mtu ambaye amezaliwa na mzazi Mwislamu lakini akatangaza kutokuamini kwake Uislamu. "Murtad Milli" mtu asiye Mwislamu ambaye ameikubali dini ya Uislamu na kisha akajitoa kwayo.

****

Wakati tunajadili utohara wa ibada au unajisi wa asiye Mwislamu, Mujtahid wamegawanya Makafir wote dhimmi, harbi, murtad fitri na Milli - katika makundi mawili yaliyo wazi: Mushrik na ahlul '1-kitab.

Mushrik (wingi-Mushirikina) maana yake mwenye kumshirikisha Mungu mtu ambaye huamini kwamba Mungu ana washirika. Hutumika vile vile kwa waabudu masanamu. Wafuasi wa uhindu wa dini za mashariki ya mbali zaidi huangukia katika kundi hili la mushrikina. Ahlul '1-Kitab maana yake watu wa kitabu; ni jina walilopewa wale ambao huamini  chochote kilichoteremshwa na Allah kabla ya Qur'an. Chini ya mfumo wa Kiislamu, Ahlu '1-kitab wana sifa ya upendeleo kulinganisha na wengine wasiokuwa Waislamu. Watu ambao kwa pamoja hukubaliwa na wote kuwa ni Ahlu '1-kitab ni Mayahudi, Wakristo na Wazoroastia.

****

Ama kwa washirikina, Mujtahid wanakubaliana kwa pamoja kwamba ni najis. Hivi ndiyo ilivyo kwa sababu Allah ametamka kwa uwazi kabisa katika Qur'an. "Enyi ambao mmeamini! Washirikina kwa hakika ni najis; kwa hiyo wasiukaribie huo msikiti mtukufu baada ya mwaka wao huu (i.e 9 A.H.) (9:28). Baadhi ya Waislamu hujaribu kutafsiri neno "najis" katika hali ya kiroho tu. Wamekosea kwa sababu mtu hawezi kupuuza maana halisi ya neno, vinginevyo iwe fuombo linaunga mkono kuondoka kutoka maana halisi kwenda kwenye maana ya kifumbo. Fuombo la aya hii haliachi nafasi kwa fumbo la kipekee au tafsiri ya kiroho ya neno "najis" Husema mara moja kwamba "Hawapaswi kuuendea Msikiti Mtukufu." Hii huonyesha usafi wa mwili. Hata hivyo tafsiri yetu haiondoi unajisi wa kiroho wa washirikina sambamba na mwili, na unajisi wa ibada.

Wakati tukiendelea juu ya Ahlul '1-Kitab, tunaona kwamba Mujtahid hawakubaliani kuhusu utohara wao au unajis. Kuna maoni tofauti aina tatu juu ya Ahlul '1-kitab.

1. Kundi la wachache wanasema kwamba Ahlul' 1-Kitab ni safi na tahir sawa kama Waislamu. Kundi hili ni la akina marehemu Ayatullah al-udhma Sayyid Muhsin al-Hakim at-Tabatabai (aliyekufa 1970) na marehemu Ayatullah ash-shahid Sayyid Muhammad, Baqir as-Sadiq (aliyekufa 1980).[11] (2) Maoni ya wengi husema kwamba Ahlu '1-kitab wanakuwa mafasidi katika imani zao na hawako tofauti na washirikina; kwa hiyo wao ni najis. Wale ambao wako katika kundi hili kuanzia Mujtahid wa saba ni: Ayatullah al-Udhma Sayyid Ruhullar al-Musawi al-Khumayni na Ayatullah al-uzma Sayyid Muhammad Riza al-Gulpaygani.[12] (3) Kundi la tatu ni la wale Mujtahid ambao kinadharia wanakubaliana na maoni ya kwanza lakini inapokuja katika kutoa fatwa kwa wafuasi wao, hufuata njia ya tahadhari na kuwa upande wa wengi. Aliye mashuhuri zaidi miongoni mwa kundi hili ni Ayatullah al-udhma Sayyid Abu '1-Qasim al-Musawi al-Khui.


Ayatullah al-Khui katika darasa zake juu ya fiqh anasema: "Ni dhahiri kutokana na mambo tuliyoyajadili hapo juu kwamba utohara wa Ahlul '1-Kitab ulichukuliwa kwa kuridhia tu na wasimuliaji wa hadithi mpaka mwisho wa zama za Maimamu wetu (yaani mpaka wakati wa ghaibat ndogo), na chochote kile walichowauliza Maimamu kuhusiana na kazi za Ahlul '1-kitab ilikuwa kwa sababu tu ya mashaka waliyokuwa nayo kuhusu najasat ya nje ambayo huenda ingewapata.

"Kwa hiyo ni vigumu kutoa fatwa juu ya msingi wa hadithi ambazo kidhahiri zinasema kwamba Ahlu '1-kitab ni najisi; hatahivyo, kwa upande mwingine kutoa hukumu juu ya msingi na hadithi ambazo husema kwamba wao (Ahlul '1-Kitab) ni tahir ni vigumu zaidi kwa sababu wengi wa Masahaba wetu, wanafikihi (fuqah), wote kuanzia siku za mwanzo na siku za baadae, wanaamini katika unajisi wa Ahlul '1-Kitab. Na hivyo hakuna njia ya kukwepa kutoka kwenye mfungo wa hatua za tahadhari juu ya suala hili." [13] Na kwa hiyo tunaona kwamba wakati akitoa fatwa kwa ajili ya wafuasi wake, Ayatullah al-Khui huandika ama kwa kitabi (Kafir) maoni yaliyo mashahuri husema kwamba ni najis; na ni tahadhari ya muhimu (kumfikiria kama hivyo)"[14]


Pamoja na sifa zote walizonazo Marja wa zama zetu, ningerudia tu mambo aliyosema juu ya suala lile Mujtahid Mashuhuri wa karne ya 10 ya Ki-Islamu, ash-Shahid ath-Thani Shah Zaynu 'd-Din al-Amili: "Kutenda kinyume na maoni ya wengi ni vigumu lakini kukubali maoni yao bila uthibitisho wowote wa kusaidikisha ni vigumu zaidi." [15]

Mbali ya maoni ambavyo kwayo mimi nimeelekea msomaji anashauriwa kufuata maoni ya Mujtahidi wake mwenyewe juu ya suala hili.

****

Kuna makundi mengine - Ghula't, Nawasib na Khawarij -ambao vile vile wanachukuliwa kuwa ni makafir na najis kwa mujib wa Shiah fiqh, pamoja na ukweli kwamba makundi haya yalikuwa vichipikizi (vitawi) vya Waislamu wakati wa hatua ya kwanza ya historia ya Kiislamu.

Ghulat (Ghali - Umoja) ni wale ambao hutangaza imani yao katika Uislamu, lakini huongeza chumvi katika imani zao kuhusu baadhi ya Mitume au Maimam, km. Wale ambao wanamini kwamba Imam amechukuwa umbo la Mungu (incarmation).

Hii ni kinyume na imani ya msingi ya Kiislamu kwamba Mungu hawezi kuingia ndani ya mtu yeyote au kitu chochote.

Nawasib (Nasib-umoja) ni wale ambao hutangaza imani yao katika Uislamu lakini huonyesha uadui kwa Ahlul-bayt (a.s.). Hii huenda moja kwa moja dhidi ya amri ya Qur'an:


"(Ewe Muhammad) Sema Siombi ujira wowote kwenu, kwa haya (yaani kwa ujumbe huu nilio waletea) isipokuwa mapenzi kwa jamaa zangu." (24:23).

Mtume alisema,"Yeyote yule atakaye kufa yu katika uadui kwa familia ya Muhammad atakufa kama kafir, Yeyote yule atakayekufa yu katika uadui na familia ya Muhammad hatainusa harufu nzuri ya pepo." [16]

Hata hivyo mtu lazima aelewe kwamba kama mtu sio Mwislamu wa madhehebu ya Shia haina maana kwamba na yeye vile vile anawachukia Maimamu wetu. Kuna Masuni wengi ambao hawaamini Maimamu wetu kama viongozi na makhalifa baada ya Mtume, Lakini wala hawawachukii, bali kinyume chake wengi wao huwaheshimu na hata pia huwapenda Maimamu wa Ahalul '1-bayt.

Khawarij (Khariji - Umoja) ni wale ambao waliasi dhidi ya Imamu Ali bin Abi Talib (a.s.) katika vita vya Siffin. Hatimae, Imamu Ali (a.s.) ilibidi apigane dhidi yao katika vita ijulikanayo kama naharwan. Waliamini kwamba Imam Ali (a.s.) amekuwa kafir kwa kukubali suluhu wakati wa vita dhidi ya Mu'awiyah. Aya na hadithi iliyotaja hapo juu kwa sawa sawa hutumika kwa Khawarij pia, na kwa hiyo wao vile vile ni Makafir na najis.

Kuna kundi moja zaidi la makafir. Mtu ambaye anakataa moja ya ibada zikubaliwazo kwa pamoja za Uislamu (Km. Wajibu wa Sala na haji), Vile vile huchukuliwa kama, kafir na najis. Mtu wa namna hiyo atakuwa kafir maadam anaelewa kwamba kukataa ibada kama hizo za Kiislamu ni sawa sawa na kuamini kwamba aya za Qur'an juu ya sala na hajj sio sehemu ya kitabu cha Allah, na hii itakuwa na


maana kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) hakuwa muaminifu katika kuutekeleza ujumbe wa Allah. Kwa ufupi mtu kama huyo huwa kafir kama tu huelewa matokeo ya kukataa kwake ibada zilizokubaliwa kwa pamoja za Uislamu. Hata hivyo, mtu lazima aangalie kwamba kuzembea na kukataa ni vitu viwili tofauti; hivyo kama mtu huamini ibada zikubaliwazo kwa pamoja za Uislamu lakini akazizembea, sio Kafir, atakuwa anafanya dhambi tu.

8. VINYWAJI VYENYE KULEVYA

Kila kinywaji kinacholevya ni najis.   Allah anasema katika Qur'an:

"Enyi ambao mmeamini! Hakika Pombe, Kamari, Masanamu na ramli ni uchafu wa shetani, hivyo jiepusheni navyo, ili mpate kufuzu." (5:90)

Neno uchafu katika aya hii, kwa kiasi pombe ihusikavyo, ina maana ya kiroho halikadhalika na ya kiibada kwayo; Na uchafu wa ibada ni neno lingine la najis. Aidha, jibu la Imamu Ali an-Naqi (a.s.) kwa barua ya Khayran iliyonukuliwa huko mbele kwa uwazi inasema kwamba pombe sio tu ni haramu bali pia ni najis.

Bia vile vile ni najis. Lakini vinywaji vyote visivyolevya vinavyotengenezwa kwa shairi ni tahir. Vileo visivyo vya maji maji ni haram lakini sio najis. Spiriti (Methyl alcohol, or wood alcohol, or wood spirit) ni tahir; inatumika sana viwandani kwa kusafishia na kwa ajili ya kutengenezea mipira bandia, kemikali, vifutio, wino, rangi, dawa za kuzuia kuganda barafu na bidhaa nyingine zinazofanana na hizo.


C. BAADHI YA HUKUMU ZA JUMLA

Kununua au kuuza najasat zifuatazo ni haram: aina zote za vileo vya maji maji, mfu, nguruwe na mbwa (isipokuwa mbwa atumikaye kwa ajiliyakuwinda).

Hata hivyo, mtu anaruhusuiwa kununua au kuuza najasat nyingine kama kuna manufaa yoyote halali ndani yake, km. Kununua au kuuza vinyesi kwa ajili ya mbolea. Vile vile inaruhusiwa kununua au kuuza sehemu za wanyama waliokufa (mbali ya mbwa na nguruwe) ambavyo havina hisia wakati wa uhai wao. Ni haramu kuuza zabibu au tende kwa mtu ambaye ananunua kwa ajili ya kutengenezea mvinyo.

Kama kitu safi (tahir) kiligusana na najasat yoyote, basi hakitakuwa najis mpaka kimoja ya vitu viwili hivyo kiwe na unyevunyevu.

Dawa, manukato, sabuni na nta zinunuliwazo kutoka nchi zisizo za Kiislamu zaweza zikachukuliwa kama tahir, vinginevyo labda mtu awe na hakika kwamba ni najis.

D. MUTAHHIRAT

(VITU VYENYE KUTAHARISHA)

Ulichosoma hapo juu kilikuwa kuhusu a'yan najisah, vitu kumi najis kiasili. Vile vile unapata kujua kwamba, vitu vingine vinaweza kuwa najis kiibada kwa kugusana na moja ya a'yan najisah kumi.

Je, inawezekana kutoharisha kitu najis? Ndio. Tunaweza kutoharisha kitu ambacho kimekuwa najis kwa kugusana na moja ya a'yan najisah. Je, inawezekana kutoharisha a'yan najisah? Baadhi ya a'yan najisah zaweza kutoharishwa kiurahisi, ambapo a'yan najisah nyingine zaweza kutoharishwa tu kwa kutumia utaratibu mrefu wa kubadili na kugeuza. Kitendo cha kutoharisha kitu hicho


hufanywa na Mutahhirat.

Mutahhirat ni wingi wa Mutahhir. Ina maana ya kitu au utaratibu ambao unaweza kiibada kutoharisha vitu najis na a'yan najis. "Mutahhirat" yaweza kutafsiriwa kwa kiswahili kama "Vitu vyenye kutoharisha" Mutahhirat ziko jumla kumi na moja. Mutahhirat zaweza kugawanywa katika mafungu matatu:-

i. Asili:

1.         Maji

2.    Arhi-udongo;

3.    Jua

ii. Badiliko la umbo:

4.         Istihalah (kubadilika kemikali);

5.         Inqilab (hubadilika asili);

6.    Intiqal kubadilika mahali);

7.    Zawali '1-ayni n-najasah (kutoweka kwa najasat);

8.         Istibra (karantini);
iii. Badiliko la Kiroho

9.         Uislamu

10. Taba'iyyah (kufuata);

11.    Ghaybatu l-Muslim (kutoweka kwa Muislamu)

Sio mutahhirat zote hizi zaweza kutoharisha kila najis au kila kitu kilicho 'ayn najis. Ni maji tu ndio mutahhirat zaidi kwa zote, ambapo nyingine zina mipaka katika upeo. Katika kurasa zifuatazo tutaelezea hukumu kuhusu mutahhirat hizi kumi na moja.

1. MAJI

Cha kwanza miongoni mwa mutahhirat ni maji. Qur'an inasema:

"Yeye (Allah) ndiye ambaye hupeleka upepo kama habari njema mbali ya rehema zake; na tunateremsha chini maji safi kutoka kwenye mawingu. " (25:48)


Hakika maji ni ya kawaida zaidi na hutumika kwa mapana sana kwa kutoharishia. Hata hivyo, njia ambayo maji yaweza kutoharisha kitu najis hutegemea juu ya aina yake na kiasi chake. Hivyo kwanza tutaelezea aina mbalimbali ya maji na kisha tueleze hukumu za kutoharisha.

Kwa mujibu wa Shari'ah maji yaweza kuwa ya aina mbili: Mutlaq na Mudhaf.

Mutlaq maana yake maji safi, maji ambayo hayakuchanganywa na maji maji mengine. Wakati tunatumia neno safi katika fuo hili, hatuna maana ya maji safi kisayansi, yaani H20, mchanganyiko wa maji wenye sehemu 2 za haidrojen na 16 za oksijeni. Kwa kusema Mutlaq tuna maana ya maji ambayo watu kwa ujumla hufikiria kuwa safi bila kuyatia katika vipimo vya kisayansi.

Mudhaf ni kinyume cha Mutlaq, ina maana maji ambayo yamechanganywa na baadhi ya maji maji mengine, km. Juisi ya machungwa, chai n.k.

Kwa ajili ya kutoharisha vitu najis, ni maji mutlaq tu ndio yanayoweza kutumika. Kwa hiyo maji mudhaf sio moj a ya Mutahhirat. Maji Mutlaq yanaweza kupatikana katika hali tano tofauti:

1-Mvua

2-Maji ya Kisima

3-Maji yanayo kimbia au kutiririka: km.   Mto,
kijito.   Maji yanayokimbia kutoka kwenye
mabomba ndani ya nyumba yana hesabiwa kama
maji yanayo kimbia maadamu yanakimbia.

4-Maji ya kur:  Dimbwi la maji ambalo limetulia
(hayatembei)   Ni lazima yawe angalu kilo 377


katika uzito au lazima yawe yamechukuwa nafasi angalau shibiri za cubic 27. Mfano wa maji ya kur: Bwawa la kuogelea, dimbwi, ziwa au bahari n.k.

5.  Machache kuliko kur: Dimbwi la maji ambayo ni machache kuliko kur.

Aina nne za kwanza za maji safi yanajulikana kama, maji kathir na qalil. Kathir maana yake mengi; qalil maana yake machache.

Maji yanaweza kufanya vitu najis kuwa tahir katika hali zifuatazo:

1-Ni lazima yawe Mutlaq;

2-Ni Lazima yawe tahir

3-Ni lazima yasiwe Mudhaf kwa kugusana na najasat;

4-Najasat   lazima   iondolewe   kutoka   kitu
kilicho najisika.

Kwa sababu ya kiasi chake, maji Kathir yamekingika kutokana na kuwa najis kwa kugusana na najasat, isipokuwa wakati najasat ikiwa na nguvu sana au nyingi mno kiasi kwamba inabadilisha ladha, au rangi au harufu ya maji. Wakati unaposafisha kitu najis kwa maji Kathir, inatosha kuosha mara moja baada ya kuondoa najasat.

Kinyume na ilivyo maji, Kathir, Maji qalil huwa najis mara tu yanapogusana na najasat. Wakati wa kusafisha kitu najis kwa maji qalil, ni muhimu kuosha mara mbili. Hata hivyo ni bora kuosha mara tatu.


Karibu vitu vyote vigumu ambavyo hupatwa na najis vinaweza kuoshwa mara moja kwa maji kathir au mara mbili kwa maji qalil. Mfano wa vitu vigumu: Nguo na viatu, mapazia na matandiko, mazulia na samani, matunda na mboga, vyombo vya chakula na vyungu.

Hata hivyo, kuna vitu vichache ambavyo hutakikana kuoshwa katika njia tofauti:-

1-Nguo ambayo imepatwa na najis kwa mkojo lazima ioshwe mara moja katika maji yanayokimbia au mara mbili kwa aina nyingine za maji, na lazima ikamuliwe baada ya kila safisho.

2-Chungu kilichorambwa na mbwa lazima kifutwe na udongo safi unyevunyevu kikamilifu; kisha, baada ya kuusafisha udongo, lazima kioshwe mara moja kwa maji kathir au mara mbili kwa maji qalil.

3-Chungu ambacho kimekuwa najis kwa kileo maji maji, lazima kioshwe mara tatu kwa maji kathir au qalil, hata hivyo ni bora kukiosha mara saba.

4-Chungu kilichorambwa na nguruwe lazima kioshwe mara saba kwa maji kathir au qalil.

Ama kwa vitu maji maji ambavyo vyaweza kupatwa na najis (km. maziwa), haviwezi kutoharishwa na maji. Njia pekee iwezekanayo kwa kutoharisha najis ya majimaji ni kwa kugeuka kabisa au kubadilika-njia ya kutoharisha ambayo itajadiliwa baadae.


2.   ARDHI

Ya pili miongoni mwa Mutahhirat ni ardhi. Hata hivyo, ardhi sio kitu cha kutoharishia vitu vyote kama maji, upeo wake wa kutoharisha una ukomo. Inaweza kutoharisha tu soli ya kiatu na unyayo wa mguu maadam iwe:

1-Kiatu au mguu umepatwa na najis kwa najasat katika ardhi;

2-Asili ya najis inaondolewa katika soli au nyayo kwa kutembea juu ya ardhi;

3-Ardhi iwe kavu na tahir;

3. JUA

Jua ni la tatu na la mwisho miongoni mwa "Mutahhirat asilia."

Jua vile vile ni Mutahhirat yenye ukomo kama ardhi. Linaweza kutoharisha vitu vifuatavyo vipatwapo na najis: Ardhi na vitu vyote visivyotembea juu ya ardhi kama miti, matunda juu ya miti, majani, n.k. Linaweza vile vile kutoharisha vitu visivyotembea vya nyumba kama kuta na milango.

Jua laweza kutoharisha vitu vilivyotajwa hapo juu maadamu:

1-Najasat iwe imeondolewa;

2-Sehemu iliyo najis, au kitu kiwe na unyevunyevu. Hivyo kama sehemu yenye najis au kitu, kimekuwa kikavu na unataka kuitoharisha kwa jua, basi utahitaji kumwagia maji juu yake na kuiacha ikauke moja kwa moja na miali
yajua.

3-Kitu kilichonajisika au sehemu lazima ikauke kwa miali yajua moja kwa moja.


4. ISTIHALAH

(Badiliko la kemikali)

Istihalah ni Mutahhirat ya nne. Istihalah maana yake kubadilika au sawa sawa zaidi ni, kubadilika kwa kemikali: Ni mutahhirat zaidi ya vyote katika fungu la "Kubadilika kwa umbo."

Ayn najis au kitu najis kinaweza kuwa tahir kwa kubadilika kuwa kitu tahir: Mkojo kugeuka hewa, kuwa mvuke na kisha kugeuka katika hali ya umaji umaji. Mwili wa mbwa kugeuka kuwa udongo. Mwili wa nguruwe uliotupwa kwenye mgodi wa chumvi na kugeuka kuwa chumvi. Mboji (mbolea) iliyotengenezwa kutokana na kubadilika kinyesi, katika utaratibu mrefu, kwenye majani na matunda.

Mifano michache ya vitu najis vibadilikavyo kuwa vitu tahir: Mti najis kubadilika kuwa jivu. Maji najis kubadilika kuwa mvuke na kuwa maji tena. Maji najis ambayo ng'ombe ameyanywa yakabadilika kuwa mkojo au maziwa.

5.INQILAB

(Kubadilika katika asili)

lnqilab kama istihalah maana yake kubadilika. Tofauti iko katika kiasi cha kubadilika. Katika istihalah, umbo na muundo vyote hubadilika; ambapo katika inqilab, ni asili tu hubadilika, lakini umbo halibadiliki lote. Mfano wake pekee ni mvinyo kubalika kuwa siki. Wakati kubadilika huku kukitokea, Siki huwa tahir.

6. INTIQAL

(Kubadilika mahali)

nyingine. vitu 'ayn najis fulani vyaweza kuwa tohora kiibada kwa kubadilika mahali pake (pa awali).  Kwa mfano, damu ya mtu, ni


najis. Sasa kama mbu akinyonya damu ya mtu, na damu ile ikawa 'damu ya mbu' basi inakuwa tahir. Hali kadhalika, kama kiungo cha Kafir kinapandikizwa kwa Mwislamu (na baada ya muda kiungo kile kinakuwa sehemu ya mwili wa Mwislamu). Basi kitakuwa tahir.

7. ZAWALUL 'L-AYNI N-NAJASAH

(Kutoweka kwa Najasat)

Zawalu'1-ayni 'n-najasah maana yake kutoweka kwa asili ya najis. Kujitoharisha huku kunatumika zaidi katika wanyama.

Kama kuna najis yoyote katika mwili wa mnyama, atakuwa tahir kwa kuiondoa au kuifuta tu, najis hiyo hutoka katika mwili wake.

Hivyo hivyo, sehemu za ndani za mwili wa mtu (kama ndani ya mdomo, pua na kope) huwa tahir mara tu najasat inapoondolewa humo: Hata hivyo, meno ya bandia hayahusiki katika hukumu hii kwa sababu yenyewe sio asili ya mdomo.

8. ISTIBRA'

Istibra maana yake kusafisha kitu kuondokana na kitu. Kutoharisha huku kuna ukoma kwa wanyama makhususi. Tayari unajua kwamba mkojo na kinyesi cha mnyama halali sio najis. Hata hivyo, wanyama kama hao hupoteza sifa yao ya tohara kama wakianza kula kinyesi cha mwanadamu. Na wakati hili likitokea basi njia pekee ya kuwafanya wawe tahir ni istibra:

Istibra; Katika fuo hili, maana yake kumtenga mnyama kutokana na kula kinyesi cha binadamu kwa muda maalumu wa siku. Idadi ya siku hutegemea juu ya aina ya mnyama: ngamia siku 40, ng'ombe siku 20, kondoo au mbuzi siku 10, bata au ndenge wa kufuga siku 5 au 7 na kuku siku 3.

9.UISLAM

Uislamu ni moja ya "kutoharisha cha kiroho." Moja ya a'yan na najisah ilikuwa ni kafir. Njia pekee ya kafir kuwa tahir ni yeye kuukubali Uislamu. Kwa kuukubali Uislamu mara moja atakuwa tahir. Hata hivyo kama mtu nguo zake zilikuwa najis, basi kukubali kwake Uislamu hakutatoharisha nguo hizo; itambidi kuzifanya tahir kwa maji.

10. TABAIYYAH

Tabaiyyah maana yake kufuata.

Katika fuo hili, ina maana kwamba kama kitu najis au mtu akiwa tahir, basi vitu inavyohusiana navyo moja kwa moja huwa tahir.

Wakati Kafir akiwa Mwislamu, Watoto wake wadogo huwa tahir moja kwa moja. Kama kisima kinakuwa najis, na kiasi cha maji yahitajikayo yakitolewa nje kukitoharisha basi kuta za kisima, ndoo na kamba vile vile vitakuwa tahir.

Wakati tunaosha kitu najis, mikono yetu huwa najis vile vile; lakini wakati kitu kile kikiwa tahir. mikono yetu vile vile moja kwa moja inakuwa tahir. Kama mvinyo ukiwa siki, kubadilika huku kutaifanya kuwa tahir, na chungu ambacho ulikuwamo mvinyo (huo uliobadilika kuwa siki) huwa tahir moja kwa moja.

Ubao wa mti au kibao cha saruji ambacho juu yake mwili wa Muislamu aliyekufa unaoshwa, halikadhalika na kipande cha nguo kilichotumika kufunikia sehemu zake za siri, na vile vile mikono ya mtu aliyemuosha mayiti huyo huwa tohara wakati josho la kawaida likikamilika.


11. GHAIBAITU'L - MUSLIM

(Kutoweka kwa Muislamu)

Ya mwisho miongoni mwa vinavyotoharisha ni ghaibatu '1-Musllm. Nimekuhesabu huku kama moja ya hutoharisha kiroho kwa sababu imetegemea juu ya mafundisho muhimu zaidi ya maadili ya Uislamu ambayo husema kwamba mtu awe wazi (asiwe na wasiwasi) katika kuwahukumu Waislamu wengine.

Ghaibatu '1-Muslim maana yake kutoweka kwa Muislamu. Katika fuo hili, ina maana ifuatayo: Iwapo mwili wa Mwislamu au chochote anachohusika nacho (Mwislamu ambaye ni makini katika kufuata Shari'ah) vikawa najis. Kisha mtu yule akaondoka mbele ya macho yako muda wa kutosha kwa yeye kujitoharisha (mwenyewe) au vitu vyake. Sasa, anarudi na unamuona anatumia kitu fulani kile, basi yakupasa ukifiria kwamba kitu kile ni tahir.

E. MTAZAMO WETU KUHUSU NAJASAT

Ni nini kinapasa kuwa mtazamo wetu wa jumla juu ya najis? Hili ni swali la muhimu sana kwa Mwislamu, hususan kwa wale ambao wanaishi katika jamii ambayo ukafir umezidi. Kwa hakika tunapata aina mbili ya majibu katika swali hili; kwa upande mmoja ni kundi ambalo limechukuwa mawazo ya wenye kupendelea mabadiliko (liberal) na husema kwamba hukumu ya Shari'ah hizo hazifai tena katika wakati wetu huu. Kwa hakika maoni haya hayaungwi mkono katika vyanzo vya Uislamu. Asili ya Uislamu ni kujisalimisha kwa hiari kwa Mungu na tabia ya wapendeleao mabadiliko ni kinyume na wazo hilo. Maoni ya wapendeleao mabadiliko kwa upande hutokea kutokana na ujinga kuhusu elimu ya nguvu yenye kuendesha na uchukuaji wa asili wa Shari'ah, ni matokeo ya kufikiria kimakosa muundo kwa kitu asilia; na kwa upande kutokana na ushawishi wa wapendeleao mabadiliko ya


mafundisho ya kimagharibi. Kwa upande mwingine, kuna kundi ambalo limechukuwa tabia ya utakatifu wa kujikweza zaidi na kusema kwamba ni lazima tujiepushe moja kwa moja kutokana na najasat katika maeneo yetu ya maisha. Maoni haya yanategemea baadhi ya mawazo potofu ya kupandikizwa kuhusu shari'ah na maoni ya ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla. Hupuuza au ni ujinga wa ukweli kwamba Uislamu yenyewe umeelezea shari'ah zake kama "Shari'atu 'n-Sahla" au "Shari'atu samha" Shari'a nyepesi, Shari'a ya huruma.

Wakati ambapo kila Mwislamu aliyesoma hutambua haja ya kupiga vita maoni ya wapendeleao mabadiliko, hivyo hivyo ni muhimu kupigana dhidi ya ushupavu wa wenda wazimu wa utakatifu wa kujikweza zaidi. Kundi la kwanza halipo bila lawama katika kuwasukuma Waislamu wengi wa kawaida kwenye hilo kundi linalojiita wapendeleao mabadiliko. Katikati ya ncha hizi mbaili kuna maoni ya Kiislamu, maoni ambayo yanaweza kuitwa kama njia iliyonyooka - njia ya wale ambao kwamba Allah amewaneemesha kwa baraka zake, sio ya wale waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea! Ni maoni haya ambayo nitajaribu kwa msaada wa Allah Subhanahu wa taa'la nitayaelezea hapa.

Hebu ngoja nianze kwa kuleta suala lifuatalo: Je, Tuanze kwa kufikiria kwamba kila kitu ni najis na haramu mpaka tuje tujue vinginevyo? Au tuanze na mawazo kwamba kila kitu ni tahir na halali mpaka tuje tujue vinginevyo?

Jibu langu kwa swali hili ni kwamba yatupasa kuanza na mawazo kwamba kila kitu ni tahir na halali mpaka tuje tujue vinginevyo. Mtu yeyote mzoefu wa kanuni za Shari'ah hawezi bali kukubaliana na mimi. Hata hivyo, kwa vile sheria zote za kawaida zinahitilafiana, maoni niliyoyachukuwa vile vile yana hitilafu moja. Nilichosema kinaswihi wakati wote isipokuwa katika bidhaa za wanyama zipatikanazo kutoka kwa watu wasio Waislamu, Ama kwa


bidhaa za wanyama zipatikanazo kutoka kwa Waislamu, bado tunaanza na mawazo kwamba ni tahir na halali. Ni katika bidhaa za wanyama tu zipatikanazo kutoka kwa makafir kwamba lazima tuanze na mawazo kwamba kila kitu ni najis na haramu mpaka tuje tujue vinginevyo. Maoni haya yanaungwa mkono kikamilifu na mujtahid wa zama zetu, wakiwemo Ayatullah al-Khui na ayatullah Sayyid Muhammad Kazim at-Tabatabai al-Yazdi Mujtahid, mashuhuri wa Kishia. Wa mwanzo kabisa wa karne hii ambaye kitabu chake al-'Urwatu'l-wuthqa kinatumiwa na Mujtahid wa nyuma yake kama kitabu cha darasa kwa ajili ya ijtihad zao.' Ayatullah al-Yazid anaandika:-

"(1) Vyombo vya kupikia vya mushrikina na makafir wengine ni vya kuchukuliwa kama tahir maadam haijulikani kwamba wamevigusa na ubichi unaochuruzika, almradi vyombo hivyo havikutengenezwa kutokana na ngozi, vinginevyo vitachukuliwa kuwa najis mpaka ijulikane kwamba mnyama (ambaye ngozi hiyo kutokana nayo) amechinjwa ki-Islamu au kwamba alikuwa akimilikiwa na Mwislamu (Kabla hajawa kwenye miliki ya kafir).

"(2) Halikadhalika, vitu vingine vinavyohitaji kuchinjwa ki-Islamu (Km., nyama na shahamu), kama vikionekana katika miliki ya kafir lazima vichukuliwe kuwa najis mpaka ijulikane kwamba mnyama huyo amechinjwa Ki-Islamu au kwamba alikuwa katika miliki ya Mwislamu (kabla ya kuwa katika miliki ya kafir).

"(3) Hata hivyo, kitu ambacho hakihitaji kuchinjwa kitachukuliwa kuwa tahir mpaka uwe na habari kwamba ni najis. Na ile dhana ya kwamba makafir huenda wameigusa na ubichi haitoshi (kufikiria kitu hicho kwamba ni najis).

"(4) Chombo ambacho mtu hana hakika nacho iwapo kimetengenezwa kwa ngozi ya mnyama, nyama au shahamu


ichukuliwe kama bidhaa isiyotokana na mnyama na tahir, hata kama imepatikana kutoka kwa kafir."[17]

Mujtahid wote wa zama zetu wamechukuwa na kueleza sehemu za al-'UrwatiTl-wuthqa na wote wamekubaliana na maoni ya hapo juu ya Ayatullah al-Yazid. Ingawa naqila ya hapo juu inatosha lakini kwa ajili ya ufafanuzi ningependa kumnukuu Ayatullah al-Khui. Katika juzuu ya kwanza ya Minhaju's-Salihina, chini ya sehemu ya najasat anaandika:-

"Kinacho patikana kutoka mikono ya makafir - kama mkate, mafuta, asali na vitu vingine kama hivyo, viwe katika maji maji au vigumu - ni tahir mpaka uje kujua kwamba wamevigusa na ubichi unaochuruzika. Hali hiyo huhusika pia kwa nguo zao na vyombo vya chakula. Na dhana kuhusu najasat (katika hali hiyo) haipaswi kuhesabiwa hivyo." [18]

Lakini anapojadili hukumu za vyakulana vinywaji, katika juzuu ya pili ya Minhaj, anaandika:

"Ngozi, nyama na shahamu ambavyo vimepatikana kutoka mikono ya kafir zichukuliwe kama najis hata kama akikujulisha kwamba amechinjwa Ki-Islamu." [19]

Walichosema Mujtahid wetu kwamba unaweza kuchukulia kila kitu isipokuwa bidhaa za wanyama zilizopatikana kutoka kwa kafir - kama tahir na halal mpaka uje ujue vinginevyo imetegemea juu ya miongozo ya wazi iliyotolewa na Maimamu wetu (a.s.).


Fuzayl bin Yasar, Zurah bin A'yan na Muhammad bin Muslim, Masahaba watatu hawa wanaoheshimika wa Maimamu wa tano na wa sita, walimuuliza Imam al-Baqir (a.s.) kuhusu kununua mnyama kutoka kwenye masoko ambapo hawajui wachinjaji walivyofanya wakati wa kuchinja wanyama hao. Imam akasema, "Kula kama inatoka kwenye soko la Mwislamu na usiulize kuhusu hiyo."[20]

Ahmad bin Muhammad bin Abi 'n-Nasr alimuuliza Imam Ali ar-Ridha (a.s.) kuhusu [ngozi] kiatu ambacho kimekuja katika soko la (Mwislamu) na mtu akanunua kiatu kile ambapo hajui iwapo kama (kimetokana na mnyama) aliyechinjwa Ki-Islamu au la. Unasemaje kuhusu kusali na kiatu kama hicho ambapo mtu hajui (iwapo kimetokana na mnyama aliyechinjwa)? Unaweza kusali nacho? Imam akasema, "ndio, mimi vile vile nanunua viatu kutoka kwenye soko, na vimetengenezwa kwa ajili yangu na ninasali navyo. Huhitaji kuuliza iwapo vinatokana na mnyama aliyechinjwa Ki-Islamu au la]."[21]

Al-Hasan ibn al-Jahm alimuuliza Imam Ali ar-Ridha (a.s.) swali kama hilo kuhusu viatu na aliposikia jibu lile lile, alisema: "Najizuia zaidi kuliko hivi [katika kushughulika na najasat]." Imam Ali ar-Ridha (a.s.) akasema, "Je, hutaki vile Abu '1-Hasan [yaani Imam Musa al-Kadhim] alivyokuwa akifanya?"[22]

Ali bin Abi Hamzah alimsikia mtu akimuuliza Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) kuhusu mtu ambaye alikuwa anasali na huku amechukuwa upanga - anaweza kusali nao? Imam akasema "Ndio" Kisha yule mtu akauliza, hata kama ala yake ilikuwa pengine imetengenezwa kutokana na mnyama ambaye huenda amechinjwa au hakuchinjwa ki-Islamu?  Imam akasema kama unajua kwamba inatokana na mnyama ambaye hakuchinjwa ki-Islamu, basi usisali nao."[23]


Kisa cha kuvutia kinasimuliwa na Mua'wiyah bin Ammar, mmoja wa Masahaba mashuhuri wa Imam wa sita. Mua'wiyah alimuuliza Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) kuhusu nguo ambayo imetengenezwa na Magi ambao sio tohara, ambao wanakunywa pombe na wanawake zao ni wa aina hiyo hiyo: "Naweza kuvaa nguo kama hiyo bila kuifua na kusali nayo?" Imam akasema, "Ndio." Baada ya pale, Mua'wiyah akakata kitambaa cha kanzu kilichonunuliwa kutoka kwa Magi kwa ajili ya Imam. Alitayarisha vile vile mkanda wa kiuno na joho kutokana na kitambaa hicho. Kisha siku ya Ijumaa kabla ya wakati wa adhuhuri alipeleka ile nguo kwa Imam. Alitaka kuona iwapo Imam ataivaa bila kuifua au la. Kwa maneno ya Mua'wiyah mwenyewe [anasema], "Inaonekana kama Imam alielewa makusudio yangu, na akatoka na nguo ile ile kwa ajili ya sala ya Ijumaa."[24] Swali namna kama hiyo aliulizwa Imam Mahdi (a.s.) kwa maandishi kuhusu kusali na nguo iliyotengenezwa na Magi bila kuifua. Imam Mahdi (a.s.) akajibu, "Hakuna matatizo katika kusali nayo."[25]

Abdullah bin Sanan anasimulia kwamba baba yangu alimuuliza Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.): "Niliazima nguo yangu kwa kafir dhimmi ambaye najua kwamba anakunywa pombe na kula nguruwe, na kisha akairudisha kwangu - je, itanipasa kuiosha nguo hiyo kabla ya kusali nayo?"

      Imam akasema "Sali na nguo hiyo na usiifue kwa sababu hiyo makhususi kwa sababu wakati unaiazimisha kwake, ilikuwa tahir na sasa huna hakika kuwa kwake (hiyo nguo) najis."[26]

Hadith nne za kwanza zimeweka wazi kwamba chochote unachopata kutoka kwa Mwislamu au soko la Mwislamu - iwe bidhaa isiyo ya mnyama au ya mnyama - unaweza kuchukulia kwamba ni tahir na halal, huhitaji hata kuuliza kuhusu bidhaa hiyo. Hadithi tatu za mwanzo zinaweka wazi kabisa kwamba chochote kisichokuwa bidhaa za mnyama unachopata kutoka kwa kafir ni cha kuchukuliwa kama tahir na halal mpaka ujue kwa uhakika kwamba ni najis na haramu.

Mipaka ya Mwislamu au soko la Mwislamu inayoonekana katika hadith tatu za mwanzo kwa uwazi huonyesha kwamba bidhaa za mnyama zaweza kuchukuliwa kama tahir na halali maadamu zinatoka kwenye soko la Mwislamu. Hufuatia moja kwa moja kwamba bidhaa za mnyama kutoka vyanzo visivyo vya Waislamu haziwezi kuchukuliwa kama tahir na halali mpaka tuje tujue vinginevyo. Hapa nitanukuu tu hadithi mbili zaidi juu ya suala hili la aina yake:-

Husayn bin al-Mundhir alisema kumwambia Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.): Sisi ni watu ambao mara kwa mara huenda milimani na umbali ni mkubwa kati yetu na milima. Kwa hiyo hununua wanyama kwa wingi kwa ajili ya chakula na tunawauliza wafugaji kuhusu dini yao na wanajibu kwamba wao ni Wakristo. "Sasa unasemaje kuhusu uchinjaji wa wanyama wa Wayahudi na Wakristo?"

Imam akasema, "Ewe Husayn! Uchinjaji wa Kiislamu unaweza kufanyika kwa jina la Allah tu na hakuna mtu anayeweza kuaminiwa kwa hilo isipokuwa watu wa tawhid (yaani Waislamu)."[27]

Siku moja Ibn Abi Ya'fur na Mu'alla bin Khumaya walikuwa wanasafiri katika mto Nile na wakakosa kuelewana wenyewe kwa wenyewe kuhusu kula nyama aliyechinjwa na Mayahudi. Mu'alla akala nyama ile ambapo Ibn Abi Ya'fiir alijizuia. Mwishowe walikuja kwa Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) na wakamweleza kutokukubaliana kwao. Imam akathibitisha uamuzi wa Ibn Abi Ya'fur na akaukataa uamuzi wa Mu'alla kula nyama ile.?[28]

Ningependa kumalizia sehemu hii kwa ufafanuzi wa kuvutia wa Ahmad bin Muhammad bin Abi 'n-Nasr al-Binzanti juu ya tabia ya utukufu wa kujikweza zaidi. Ahamad al-Bizanti alikuwa muaminifu sana na sahaba msomi wa Imamu Ridha (a.s.) na Imamu Muhammad at-Taqi (as). Ahmad bin Muhammad bin Isa alimuuliza Ahmad al-Bizanti kuhusu mtu ambaye ananunua joho la ngozi ambapo hajui iwapo linatokana na mnyama aliyechinjwa Ki-Islam au la - anaweza kusali nalo? Ni wazi kwamba swali hili linahusu kununua kitu katika jamii ya Ki-Islamu.

Ahmad al-Bizanti akajibu, "Ndio, na huhitaji kuuliza kuhusu hilo. Imam Muhammad at-Taqi (a.s.) amezoea kusema, Khawarij wameweka vikwazo mno juu yao wenyewe kwa sababu ya ujinga, wakati ambapo dini ni pana [katika mtizamo wake] kuliko hivyo." Maelezo kuhusu Khawarij yamesimuliwa pia kutoka kwa Imam Musa al-Kadhim (a.s.) na Sheikh as-Sadiq.[29]

   Ni katika kanuni hii ya Shari'ah kwamba Mujtahid wetu wametegemeza maoni yao kuhusu kuchukulia kila kitu -isipokuwa bidhaa za wanyama zipatikanazo kutoka kwa makafir -kuwa ni tahir na halali mpaka tuje tujue vinginevyo. Uislamu haututazamii sisi kujiepusha moja kwa moja kutokana na najasat, unatutaka tu tuondokane kutokana na najasat katika chakula chetu na vinywaji, na wakati wa salat.

SURA YA PILI

WUDHU

(josho Dogo)



11. WUDHU

A.UTANGULIZI

Wudhu na ghusli yote ni majosho ya ibada; la kwanza ni josho dogo ambapo la pili ni josho kubwa katika sheria za ki-Islamu. Wudhu huchukuliwa kuwa ni tendo la dini la ibada ambalo hufanywa kwa nia ya kutaka radhi ya Allah.

Tendo la Wudhu hujumlisha kuosha uso na mikono, na kupakaza kichwa na miguu. Sehemu hizi sita za mwili na mwanadamu - uso, mikono yote, kichwa na miguu yote - hujulikana kama " viungo vya wudhu."

Wudhu kwa wenyewe siku zote ni tendo lililopendezwa katika ibada za ki-Islamu, lakini huwa wajibu katika hali makhususi. Moja ya hali hizo ni ibada ya Salat za kila siku; na kwa ajili hiyo ni muhimu kwa kila Mwislam kujua namna ya kutawadha na hukumu zake:

Qur'an inasema:

"Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajiliya sala, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni.   (5:6). "

B. NAMNA YA KUTAWADHA

Namna ya kutawadha kama inavyoelezwa hapo chini imetegemea juu ya Qur'an na Sunna sahihi za Mtukufu mtume (saww) kama zilivyo simuliwa na Ahlul'1-Bayt wake (as) na Masahaba wake waaminifu zaidi. Aya inayohusika na hadith zitajadiliwa katika sehemu ya J.


Wudhuu unafanywa katika hatua nne zifuatazo:-

1.  KUOSHA USO: Baada ya kuweka nia, mwaga maji juu ya uso kutoka juu. Kisha kwa kutumia mkono wako wa kulia, futa uso wako kutoka juu mpaka chini, katika njia ambayo maji yanafikia
sehemu zote kwa urefu kutoka maoteo ya nywele mpaka kwenye kidevu, na kila sehemu kwa mapana kufikia ndani ya shibiri ya mkono kutoka kidole cha kati mpaka dole gumba.

Sio wajibu kuosha sehemu ambazo haziwi ndani ya kidole cha kati na dole gumba; Hata hivyo hakuna madhara kuchanganya sehemu hizo kuhakikisha kwamba sehemu zote muhimu zimeoshwa.

Sio wajibu kuosha sehemu za ndani za macho, midomo, kinywa, pua na kope. Kama mtu ana ndevu au mashumbu, inatosha kuosha nywele ambazo zinaonekana, sio muhimu kufanya maji yafike ndani ya nywele au ngozi. Hata hivyo kama nywele ni chache kiasi kwamba hazifichi ngozi, basi mtu itampasa afanye maji yafike kwenye ngozi.

Mtu mwenye kipara au wale wenye nywele zilizoondoka mbele itawapasa kuosha nyuso zao kama vile nywele zimeota kwa kawaida. Kama uso wa mtu ni mkubwa, au mdogo, kuliko kawaida, basi itampasa kuosha sehemu zinazokuwa ndani ya kidole cha kati na dole gumba.

2.  KUOSHA MIKONO:   Mwaga maji juu ya mkono wa kulia kuanzia kwenye kiko mpaka kwenye ncha za yidole; na ukitumia mkono wa kushoto, pakaza maji juu ya mkono kuhakikisha
kwamba sehemu zote muhimu zinapata maji. Kisha fanya hivyo hiyo kwa mkono wa kushoto. Kuosha lazima kufanywe kutoka kwenye kiko mpaka kwenye ncha za vidole na sio kinyume chake.


Maji lazima yamwagwe kuanzia juu kidogo ya kiwiko kuhakikisha kwamba mkono wote unaenea maji. Ni muhimu kuosha mkono katika njia hiyo ili maji yapenyeze kwenye nywele, kama zipo, na kufikia ngozi.

3.  KUPAKAZA KICHWA:   Kupakaza kichwa maana yake kupakaza kidole chenye unyevunyevu cha mkono wa kulia kuanzia utosini mpaka mwisho wa maoteo ya nywele. Kupakaza kichwa kunaweza kufanywa katika sehemu yoyote ya robo ya kichwa ambayo iko mbele ya kichwa.

Tendo la kupakaza laweza kufanywa na kidole kimoja tu, lakini inapendekezwa kutumia vidole vitatu kwa pamoja. Maji lazima yafikie mzizi wa nywele. Hata hivyo kama nywele ni fupi sana kiasi kwamba haziwezi kuchanwa basi inatosha kupaka nywele tu.

Wakati wa kupakaza kichwa, mkono wako usiguse paji la uso; vinginevyo, maji ya paji la uso yatachanganyikana na unyevunyevu wa mkono wake, na hii itafanya kitendo cha kupakaza mguu wa kulia kiwe batili. Kwa nini? Kwa sababu kitendo cha kupakaza lazima kifanywe na unyevunyevu wa mikono tu.

4.  KUPAKA MIGUU: Tena kwa kutumia unyevunyevu wa mikono, pakaza mguu wa kulia kwa mkono wa kulia, kisha mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto.

Katika kupakaza miguu, weka kiganja au vidole vya mkono juu ya ncha ya vidole vya mguu na kisha pakaza kuelekea juu kwenye fundo. Mtu anaweza kupakaza kuanzia kwenye fundo mpaka kwenye ncha za vidole. Katika kupakaza miguu, viganya lazima vipakaze miguu, haitoshi kuipitisha miguu kwenye viganja vyako.


B. BAADHI YA HUKUMU ZA JUMLA

C.  Uso na mikono: Tahadhari zaidi yapasa kuchukuliwa ili kwamba sehemu zote muhimu zinaoshwa; Wudhu utakuwa batili kama sehemu
yoyote (hata kama ikiwa sawa na ncha ya sindano) itaachwa.

Kupakaza kichwa na miguu: Kama ilivyotajwa mapema, kupakaza lazima kufanywe na unyevunyevu wa viganja, yaani baada ya kuosha mikono yote miwili, mtu haruhusiwi kulowesha mikono yake kwa maji mengine 'mapya' Halikadhalika, kupakaza kutakuwa batili kama unyevunyevu wa mikono unachanganywa na maji mengine kutoka viungo vingine vya wudhu.

Vipi kama mikono itakauka kabla mtu hajapakaza kichwa au miguu? Katika hali hiyo, mikono yaweza kufanywa unyevunyevu kwa maji kutoka kwenye ndevu, mashamvu, kope au viungo vingine vya wudhu. Vipi kama hali ya hewa ni joto sana kiasi kwamba uso wa mtu na mikono hukauka mara moja? Katika hali hiyo, mtu itampasa kufanya tayammamu badala ya wudhu.

Kama haiwezekani kupakaza kichwa na miguu kwa viganja kwa ajili ya majeraha, n.k. basi viungo vifuatavyo vinaweza kutumiwa (katika mpango wa kufuatana): Sehemu ya juu ya mikono na sehemu za ndani za mikono (sio viganja).

Kabla hujaanza kutawadha, hakikisha kwamba sehemu ya mbele ya kichwa chako na upande wa juu wa miguu yako ni kavu; vinginevyo wudhu wako hautakuwa sawa sawa kwa sababu maji yalioko kwenye kichwa chako au katika miguu ni "maji mapya" Hata hivyo ubichi kidogo au unyevunyevu, hauwezi kuleta madhara katika wudhu wako, labda mpaka iwe ni zaidi sana kiasi kwamba unyevunyevu wa viganja unachanganyikana mara moja unapopakaza kichwa au miguu.


D. MATENDO YA WUDHU YANAYO PENDEKEZWA

Uliyoyasoma juu yalikuwa yanahusu wajibu wa matendo ya wudhu. Sasa tutaelezea matendo ambayo yanapendekezwa (mustahaba Sunnat) wakati wa wudhu.

1.Kuosha viganja viwili mara mbili kabla ya kuosha uso.

2.Kusukutua mara tatu kabla ya kuosha uso.

3.Kuvuta maji puani mara tatu kabla ya kuosha uso.

4.Wakati wa kuosha uso na mikono, inapendekezwa kuosha kila sehemu mara mbili kabla ya kuendelea na hatua nyingine ya wudhu Mtu yampasa aelewe kwamba kuosha viungo hivi vya wudhu mara moja ni wajibu, ambapo huosha mara mbili kumependekezwa; lakini kuviosha kwa mara ya tatu ni haramu. Kuamua kwamba hii ni mara ya kwanza au ya pili ya kuosha hutegemea nia ya mtu mwenyewe binafsi. Na hivyo, inawezekana kwamba mtu anaweza kumwaga maji juu ya mkono wake wa kuume mara tano, na akafuta kwa kiganja chake cha kushoto mara mbili, na bado akahesabu kuosha huku kuwa ni mara
moja.

5.Inapendekezwa kwa wanaume kuanza kuosha mikono yao kuanzia sehemu za juu zinazoonekana za mikono, na kwa wanawake kuanza kuosha mikono yao kuanzia sehemu za ndani (za mikono yao).

6.Kusorna dua zifuatazo kama zilivyofundishwa na Imamu Ali (a.s.) Katika hatua mbalimbali za Wudhu:-

Mwanzo wa Wudhu:

Bis Mil-lahi wa bil-lahi; Wal hamdu lil-lahil ladhi ja'alal Ma'a tahiran wa lam yaj'alhu najisa= [Ninatawadha] kwa jina la Allah na kwa ajili ya Allah; Shukrani zote ni za Allah ambaye ameyafanya maji kuwa safi (tohara) na hakuyafanya kuwa machafu (najis).


Wakati wa kuosha mikono mara mbili kabla ya kuosha uso:

Allahummaj'alni minat tawwabiyna, waj'alni minal mutatah-hiriyn = Ee Allah! Niweke miongoni mwa wale ambao wanaomba msamaha na miongoni mwa wale ambao ni tohara.

Wakati wa kusukutua:

Allahumma laqqini hujjatiy yawma alqaka, Wat liq lisani bi dhikrika. = Ee Allah! Nifundishe mimi majibu sahihi kwa ajili ya siku nitakayokutana na Wewe, na fungua ulimi wangu kwa ajili ya kukushukuru.

Wakati wa kuvuta maji puani:

Allahuma la tuharrim 'alayya riyhal jannah, waj'alni min man yashummu riyhaha wa rawhaha wa tiybaha = Ee Allah! Usinizuie mimi kutokana na harufu ya pepo, na niweke miongoni mwa wale watakao inusa harufu yake, uzuri wake na uturi wake.

Wakati wa kuosha uso:

Allahumma bayyidh wajhiy yawma tus'wwadul wujuh; wa la tusawwid wajhiy yawma tub-yyadhul wujuh = EeAllah.'Nurisha uso wangu katika siku ambayo utaziaibisha nyuso; na usiuaibishe uso wangu katika siku ambayo utazinurisha nyuso.

Wakati wa kuosha mkono wa kulia:

Allahumma 'atiniy kitabi bi yaminiy, wal Khul-da fil jinani bi yasariy, wa hasibniy hisaban yasira = Ee Allah! Weke kitabu cha matendo yangu katika mkono wangu wa kulia na (cheti cha) kudumu katika pepo katika mkono wangu wa kushoto; na unifanyie hesabu iliyonyepesi.


Wakati wa kuosha mkono wa kushoto:

Allahumma la tu'tiniy kitabiy bi shimaliy wa la min wara'i dhahriy, wa la taj'alha Maghlulatan ila unuqiy; wa a'dhubika min muqatta'atin niyran = Ee Allah! Usiweke Kitabu cha matendo yangu katika mkono wangu wa kushoto wala nyuma ya mgongo wangu; na usikifanye kamba kuzunguka shingo yangu. Na najikinga kwako na moto mkali.

Wakati wa kupaka kichwa:

Allahuma ghash-shiniy bi rahamatika wa barakatika wa 'afwika = EeAllah! Nifunike na huruma (rehema) zako, baraka zako na msamaha wako.

Wakati wa kupaka miguu:

Allahuma thabbitniy 'alas-sirati yawmatudhillu fiyhil aqdam;Waj'alsa'iy fimayurziyka' anniy yadhuljalali wal ikram= EeAllah! Niweke imara juu ya njia yangu siku ambayo miguu itateleza; na fanya juhudi zangu (katika hiyo njia) ambazo kwamba zitakuridhia wewe - Ee Mola mwenye nguvu na utukufu.[30]

E. MUKHTASARI WA WUDHU

Ufuatao ni mukhtasari wa Wudhu. Matendo yaliyopendekezwa ya Wudhu yako katika herufi ndogo (italics).

1.  Kutia nia (niyyat) katika moyo wa mtu

2.           Kuosha viganja mara mbili

3.           Kusukutua mara tatu

4.           Kuvuta maji puani

5.           Kuosha uso mara ya kwanza na kisha mara ya pili.

6.           Kuosha mkono wa kulia mara ya kwanza na kisha mara ya pili


7.    Kuosha mkono wa kushoto mara ya kwanza na kisha mara ya pili.

8.    Kupakaza kichwa kwa kidole kimoja au kwa vidole vitatu kwa pamoja.

9.         Kupakaza mguu wa kulia kwa kiganja cha mkono wa kulia.

10.Kupakaza mguu wa kushoto kwa kiganja cha mkono wa kushoto.

F. MASHARITI YA KUSIHI KWA  WUDHU

Utekelezaji wa Wudhu hutegemea juu ya mashariti makhususi ambayo yanajulikana katika Shari'ah za Ki-Islamu kama "mashariti ya kusihi kwa Wudhu." Masharti haya yako kumi kwa idadi; tatu zinahusiana na maji; tatu kwa mtu; na nne kwa matendo ya wudhu wenyewe.

i. MAJI:

1.Maji lazima yawe Mutlaq. Mutlaq maana yake maji safi au yasiyo changanywa na chochote; katika fuo hili, huonesha kwenye maji maji ambayo watu kwa kawaida huyaita maji (hayahitaji kuwa safi kikemikali.) Kinyume cha mutalaq ni  "Mudhaf'     ambayo  huonesha maji  ambayo hayachukuliwi na watu kama maji safi, km. Maji ya machungwa (Juice).

2.Maji lazima yawe tahir (Safi kiibada, sio najis).

3.Maji lazima yawe Mubah (yamepatikana kihalali), yaani lazima uwe ni mwenye kumiliki maji hayo au lazima uwe na ruhusa ya kuyatumia.

Wudhu unaochukuliwa na maji mchanganyiko, najis au yasiyo mubah ni batil hata kama utafanywa bila kujua. Halikadhalika ni vigumu kuthibitisha kusihi kwa wudhu unaofanywa kwa maji ambayo yalikuwa katika chombo kilichotengenezwa kwa dhahabu au fedha.


ii. MTU:

4.Niyyat: Niyyat mana yake kusudio. Kwa vile wudhu ni kitendo cha ibada (ibadat), ni muhimu kuufanya kwa niyyat. Niyyat, katika fuo hili, ina maana kwamba mtu lazima awe na nia ya kutawadha katika kunyenyekea kwenye maamrisho ya Allah. Unyofu ni sharti muhimu kwa ajili ya niyyat; mtu yampasa achukue wudhu kwa kutaka radhi ya Allah tu, na katika unyenyekevu wa maamrisho Yake.   Kama mtu atachukuwa wudhu kwa makusudio mengine, km. Kujipoza wakati wa kiangazi, basi wudhu wake utakuwa batili.

Katika niyyat, sio muhimu kutamka maneno; ile nia tu ya kuchukua wudhu katika unyenyekevu kwenye maamrisho ya Allah inatosha; wala sio muhimu kutamka kwamba wudhu huu ni wajibu au mustahaba.

5.Viungo vya Wudhu lazima viwe safi (tahir) kabla ya kuviosha au kuvipakaza.

Mbali na usafi (tahirat) wa viungo vya Wudhu, lazima vile vile viwekwe wazi. Katika maneno mengine lazima kusiwe na kitu chochote juu yao ambavyo vyaweza kuzuia maji kufikia ngozi. Tahadhari maalumu lazima ichukuliwa na wanawake iwapo rangi ya mdomo, rangi ya kucha, kohl na wanja ni kiasi ambacho kwamba maji hayafikii ngozi. Kama uchafu kwenye kucha sio zaidi kuliko ilivyo kawaida, basi hautadhuru wudhu.

6.Utumiaji wa maji lazima uwe hauna madhara kwa mtu anayetaka kutawadha.   Kama mtu anahofia kwamba atapatwa na maradhi au maradhi yake yataongoezeka kwa kutumia maji ya baridi au ya moto katika wudhu, basi itampasa kufanya tayammamu.

7.Sehemu ya kutawadhia lazima iwe mubah (ya halali).

8.Katika hali ya kawaida, ni wajibu kwa mtu kutawadha mwenyewe, bila ya msaada wa wengine. Hata hivyo, msaada katika yanayoanza kama vile kutafuta maji kuweka maji (kwenye chombo), inaruhusiwa. Katika hali ya kutokuweza kwa sababu ya maradhi, nk., mtu mwingine yeyote anaweza kusaidia; lakini katika hali hiyo, ni muhimu kwa wote msaidizi na mwenye kusaidiwa kuweka niyyat.

9.Utaratibu wa sawa sawa (tartib):   Kila kitendo katika kuchukua wudhu lazima kifanywe katika utaratibu ulioelezwa: Kwanza kuosha uso, kisha mkono wa kulia, na kisha mkono wa kushoto, ikifuatiwa na kupakaza kichwa, kisha mguu wa kulia na mwishowe mguu wa kushoto.

10.Kufululiza (Muwalat):   Matendo ya Wudhu lazima yafuatane kila moja ili kwamba, kati hali ya hewa ya kawaida, wakati kila sehemu inapoanza kuoshwa sehemu zilizotangulia ziwe bado na ubichi.

G. KUBATILIKA KWA WUDHU

Baada ya kutawadha mara moja, ni muda gani mtu anaweza kuambiwa yuko katika hali ya tohara kiibada? Je Mwislamu anatakiwa kuchukuwa wudhu tofauti kwa kila sala yake, au Wudhu mmoja unatosha kwa siku nzima? Mara mtu anapochukuwa wudhu, anaweza kujiona mwenyewe katika hali ya tohara kiibada mpaka moja ya nawaqidh itokee. Nawaqidh maana yake vitu ambavyo hukomeleza ufunyaji kazi wa wudhu na kuufanya utenguke (batil).

Nawaqidh za wudhu ni kumi: Sita zinahusiana kutokwa na majimaji ambayo hutokea kwenye viungo vya uzazi, na nne huhusika na mambo ambayo husababisha ulemavu wa muda au wa kudumaa kwa akili:


i. Kutoka majimaji:

(a)Kulingana kat iya Wanaume na Wanawake:

1.Mkojo (na manii).

2.Choo Kikubwa.

3.Kujamba.

(b)Katika Wanawake tu:

4.Hedhi

5.Kutokwa na damu mara kwa mara

6.Damu ya baada ya uzazi (nifasi)

ii.  Mambo ya ulemavu wa akili:

7.Usingizi mzito (ambao mtu hawezi kusikia chochote).

8.Ulevi (kutokana na pombe au madawa ya kulevya n.k.).

9.Kuzimia

10.Wendawazimu.

Nawaqiz hizi zimeelezwa kutoka kwenye hadithi zifuatazo za Maimamu wa ahlul 'l-bayt (amani iwe juu yao wote):-

Zurarah bin A'yun ananukuu kutoka kwa Imam wa tano au wa sita kama ifuatavyo:

"Hakuna kitenguacho wudhu isipokuwa kile kitokacho nje ya pande zote [za viungo vya uzazi] au usingizi."[31] Katika hadith nyingine Zurarah aliwauliza Maimamu wote wawili, wa tano na wa sita "Ni nini kitenguacho wudhu?" Walijibu, "chochote kile kitokacho kwenye viungo vyako vya mwili kama, choo kikubwa, mkojo, manii au upepo; au usingizi ambao huzuia akili kufanya kazi .. ."[32]


Nawaqidh Sita za kwanza (yaani maji maji yatokayo kwenye viungo vya uzazi) huweza kuelezewa kwa urahisi kutoka kwenye hadith hizi mbili. Ukiangalia sentensi ya mwisho ya hadith ya Pili ("au usingizi ambao huzuia akili kufanya kazi"), huthibitisha kwamba usingizi umehesabiwa kama moja ya nawaqidh kwa sababu huzuia akili kufanya kazi. Hii kutoa kigezo mikononi mwa Mujtahid kuirefusha orodha kwa kuongeza vitu kulewa. Hadith inataja usingizi tu kwa sababu ni kitu cha kawaida kilicho wazi zaidi ambacho husababisha 'ulemavu' wa akili, naam, kwa muda tu.

Zaidi ya vitu vingine kumi vilivyotajwa hapo juu, hakuna kingine kinachobatilisha wudhu. Baadhi ya Waislamu wanafikiri kwamba kama mtu akimgusa mke wake au viungo vyake vya siri, wudhu wake hubatilika. Hii sio sahihi. Maimamu wa Ahlul 'l-bayt, ambao ni vyanzo zaidi vya kutegemewa kwa ajili ya Sunnah za Mtume na waongozi bora wa Qur'an, wameelezea kwa uwazi kwamba hakuna kitu kingine kinachoathiri wudhu kwa njia yoyote ile.

H.NI WAKATI GANI WUDHU HUWA WAJIBU?

Kama ilivyotajwa mapema, kuchukuwa Wudhu mara kwa mara ni kitendo kilichopendekezwa, lakini huwa wajibu katika hali makhususi, kuna hali tano ambazo kwazo wudhu huwa wajib; na wakati wowote Mwislamu akijiona mwenyewe yuko katika moja ya hali hizi, lazima achukue wudhu (atawadhe).

Hali tano ni kama hizi zifuatazo:-

1. Kwa ajili ya sala za wajibu km. Sala tano za kila siku. Wudhu sio wajibu kwa ajili ya sala za sunna; lakini kwa vile sala ziwe za wajibu au za sunna ni batili bila wudhu,


hivyo yatupasa kusali sala za sunna kwa wudhu. Kwa maneno mengine, kama hutachukuwa wudhu kwa ajili ya sala za sunna utakuwa hukufanya dhambi ingawa sala yako haitakuwa sahihi. Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) alisema:

"Haiwezekani kuwepo Sala bila wudhu."[33]

Salatu 'l-Mayyit (Sala anayosaliwa mtu aliyekufa kabla ya kuzikwa) ni ya aina yake katika hukumu hii; Salat hii ya wajibu yaweza kusaliwa hata kama mtu yuko katika hali ya hadathi (hali ya kutokwa tohara).

2.Kwa ajili ya tawaf ya wajib ya Kaabah katika hija. Ali bin Ja'far alimuuliza baba yake (Imam wa Sita) kuhusu mtu ambaye anafanya tawaf na kisha akakumbuka kwamba hakutawadha.   Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) akasema:  "Yampasa aache kufanya tawaf na asihesabu (chochote alichofanya kuwa sahihi)."[34]

3.Kwa ajili ya kugusa maandishi ya Qur'an.   Qur'an sio kitabu cha hivi hivi tu, ni ufunuo wa Mungu, ni neno la Mungu, na kwa hiyo ni kitakatifu.   Utakatifu wake unahitaji kwamba, kabla ya kugusa maandishi ya Qur'an, nilazima utawadhe. Allah anasema: "Hakigusi isipokuwa na wale walio tohara. " (56:79).

Kwa msingi wa maana hii ya nje ya aya hii na hadithi hizi, Mujtahid wamefikia uamuzi kwamba inakatazwa kushika maandishi ya Qur'an bila kuwa katika hali ya wudhu.

Hata hivyo hukumu hii ya Shari'ah haipaswi kuwa ni sababu ya kutosoma Qur'an.   Hakuna madhara katika kusoma Qur'an bila wudhu mradi mtu hagusi maandishi ya Kitabu Kitukufu, yaani shikilia tu jalada au mipaka ya kurasa. Siku moja Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) alimwambia mtoto wake Ismail kusoma Qur'an, Ismail akasema, "Siko katika hali ya Wudhu." Imam akasema "Usiguse maandishi, shika tu karatasi na soma kitabu."[35]


Halikadhalika, hakuna madhara katika kugusa tarjuma ya Qur'an, kwa sababu tarjuma haifikii sifa ya neno la Mungu. Wala si wajibu kuwazuia watoto kugusa maandishi ya Qur'an, mpaka kitendo hicho kionekane ni cha kukitweza kitabu Kitukufu - na hii hutofautiana kwa mujibu wa utamaduni na jamii ambayo kwayo Waislamu wanaishi.

    4.Kwa ajili ya kugusa majina na sifa za Allah. Inakatazwa kugusa majina na sifa za Allah katika Kitabuchochote, bila kuwa na wudhu.

Kwa kuangalia utakatifu ambao Mitume, Maimamu wa Ahlul 'l-bayt na vile vile Fatimah (bint wa Mtume) walioupata kwa ajili ya kuchaguliwa kwao na Allah, Mujtahidi wetu wamependekeza kwamba majina ya watu hawa watukufu vile vile hayapaswi kuguswa bila wudhu.

    5.Kwa ajili ya kuweka ahadi, kiapo na nadhiri ya kukaa katika hali ya Wudhu kwa kipindi makhususi cha wakati kama mtu atafanya ahadi au nadhiri kama hiyo, basi aitekeleze wakati masharti yake yamekamilika.   Kwa mfano, mtu anasema, "Kama nikifaulu mtihani wangu, nitakaa na wudhu siku nzima." Hivyo mtu huyu akifaulu mtihani wake, basi lazima akae na wudhu siku nzima
kamili.

1. WUDHU'U'L - JABIRAH

(Wudhu juu ya Kitata)

Jabirah Kilugha maana yake ni gango, banzi au kitata, lakini katika fuo hili, ina maana ya vifaa au dawa inayotumika kufungia kidonda n.k. Wudhu'u 'l-jabirah maana yake wudhu unaofanywa juu ya kitata (au kitambaa) ambacho kimefungwa juu ya viungo vya wudhu.

Kabla ya kuandika kuhusu wudhu'u 'l-jabirah, ni muhimu kutaja nukta mbili zifuatazo:-

1.Kama inawezekana kuosha kidonda kwa kukiondoa kitata, basi mtu itamlazimu kuchukuwa wudhu kama kawaida. Kama haiwezekani kuondoa kitata, basi itatosha kupakaza kwa kiganja kwa ukamilifu juu ya kitata.

2.Kama mtu ana kidonda ambacho hakikufungwa kitata, na hakuna madhara katika kukiosha, basi atachukuwa wudhu kama kawaida; lakini kama haiwezekani kuosha kidonda, basi mtu itampasa kuosha pembezoni mwa kidonda tu kama kawaida. Hata hivyo, katika hali hii, ni bora kupakaza kwa kiganja juu ya kidonda na kisha
kuweka kipande cha nguo juu yake na kupaza kiganja juu yake.

Yafaa isemwe kwamba Wudhu'u'l-jabirah ni sawa sawa tu katika hali ambapo utumiaji wa maji hauna madhara kwa mtu huyo. Kama utumiaji wa maji una madhara, basi mtu yampasa kufanya tayamamu.

Wudhu'u'l-jabirah unaweza kufanywa tu katika hali zifuatazo:

1.   Kama kitata kiko juu ya kidonda katika ngozi iliyo katika au kupasuka. Hivyo Wudhu'u'l-jabirah hauwezi kufanywa juu ya kitata ambacho kimefungwa tu kwa ajili ya maumivu au uvimbe - katika hali kama hiyo ima mtu atachukuwa wudhu kama kawaida kama inawezekana au kufanya tayamamu.


2.Kama ni gango (hogo) au banzi kwa ajili ya kiungo kilicho vunjika kukiweka katika hali ya sawa sawa.

3.Kama kitata au gango (hogo) halifuniki kabisa kikamilifu kiungo chochote cha wudhu. Hivyo kama kitata au gango (hogo) limefunika kikamilifu kimoja ya kiungo chochote cha wudhu, basi utaratibu ufuatao yapaswa ufuatwe:-

(a)Kama (gango au kitata) kimefunika mguu au
miguu  yote,   basi   mtu  itampasa  kufanya
tayammamu;

(b)Kama kinafunika mkono au uso, basi mtu itampasa kwa tahadhari kufanya vyote wudhu'u'l-jabirah na tayamamu. Utaratibu huu utahusu vile vile iwapo viungo vyote vya wudhu vimefunikwa na kitata.

J. WUDHU KATIKA QUR' AN NA SUNNAH

Kama ilivyotajwa mapema, wudhu ni kitendo kilicho na hatua mbili (1) Kuosha uso na mikono; na (2) kupaka sehemu ya kichwa na miguu. Hili ni kwa ushahid wa wazi kutoka aya 6 ya Surat 'l-Maidah:

"Enyi ambao mmeamini! Mnaposimama kwa ajili ya Sala (i)    Osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye kogwa mbili (ii)  Na pakazeni sehemu ya vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye fundo mbili".    (5:6)

Katika aya hii, aina mbili za amri zimetumika:

(i) "faqhsilu" ( ÝÛÓáæÇ) ambayo ina maana ya "Osha!"; na (ii) "Wamsahuu" (æãÓÍæÇ) ambayo in maana ya "'Pakaza!". Ni wazi kwamba aina ya amri ya kwanza ("Osha!") huonyesha kwenye vitu viwili ambavyo ni "uso wako" Wujuhakum=(æÌæåßã ) na "Mikono yako" {aydiyakum = ÇíÏíßã ) ambapo aina ya amri ya pili ("Pakaza!'') huonyesha kwenye vitu viwili ambavyo ni "Sehemu ya kichwa chako'" (bi ru 'usikíÑÄæÓßã) na "miguu yako" (arjulakum-


Neno "uso= æÌå (wingi - æÌæå )" maana yake sehemu ya mbele ya kichwa, kwa mwanaume inachukuwa sehemu baina ya juu ya paji la uso na chini kidevu (kwa urefu), na upana, kutoka sikio mpaka sikio. Katika ufafanuzi wake wa hukumu, kama ilivyoelezea katika hadithi za Maimamu wa Ahlu 'l-bayt. hujumlisha sehemu ya uso kwa urefu kuanzia maoteo ya nywele mpaka chini ya kidevu, na kwa mapana sehemu ambazo hufikiwa na shibiri ya mkono kuanzia kidole cha kati mpaka dole gumba.[36]

Neno "Mkono=  íÏni wingi - ÇíÏ " maana yake kiungo maalumu kwa ajili ya kushikia, na hujumlisha mkono baina ya bega na ncha za vidole. Hivyo tunaona kwamba kutokana na maoni ya lugha, neno "yad=íÏ' kwa kawaida ni kati ya mkono, kuanzia kwenye kongwa na kiganja. Wakati neno linapotumika kwa kawaida katika maana zaidi ya moja, inakuwa muhimu kwa mzungumzaji kuleta kihusisho (au fuo) kufafanua maana yake. Na hivyo tunaona maneno "ila 'l-marafiq=Çáí ÇáãÑÇÝÞ. Mpaka kwenye kongwa" Katika aya, maneno haya yalikuwa muhimu kufafanua sehemu za "'mikono =íÏ ambazo hutakiwa kuchanganywa katika wudhu.

****

Sasa tunakuja kwenye moja ya tofauti kubwa miongoni mwa Mashia na Masunni katika namna ya kuchukuwa wudhu. Masunni wanaosha mikono yao kuanzia ncha za vidole kwenda juu mpaka kwenye kongwa, na Mashia wanaosha mikono yao kuanzia kwenye kongwa mpaka kwenye ncha za vidole. Kama ilivyotajwa hapa juu maneno "Mpaka kwenye kongwa = Çáí ÇáãÑÇÝÞ.  " hayatuambii kwamba tuoshe kuanzia ncha za vidole mpaka kwenye kongwa au kinyume chake; maneno haya yapo tu kwa ajili ya kufafanua sehemu ya "ÇíÏ- mikono" ambayo inataka kuchangaywa katika wudhu.


Basi vipi tutaosha mikono yetu - kuanzia kongwa au ncha za vidole? Jibu la tatizo hili linatolewa na sunnah. Moja ya majukumu ya Mtume (saww) ilikuwa ni kuelezea maelezo ya kuonyesha kimatendo namna ya kufuata, hukumu, zilizoelezewa katika Qur'an. Na hakika, njia ya usahihi zaidi ya kujifundisha namna gani Mtume anavyofanya wudhu ni kupitia hadith za Maimamu wa Ahlul'1-Bayt (familia ya Mtume). Zurarah bin A'yan anasimulia hadithi ifuatayo:-

"Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) alisema, 'Je, nikuelezeni ninyi wudhu wa Mjumbe wa Allah?' Tukasema 'Ndio.' Wakati maji yalipoletwa, Imam aliosha mikono yake, kisha akafunua mikono yake. Akachovya kiganja chake cha mkono wa kulia katika chombo ... kisha akachota nacho akakijaza maji na akayamwaga juu ya paji lake la uso   aliyaacha maji  yatiririke juu mpaka mwisho wa ndevu zake na kisha akapitisha mkono wake juu ya uso wake na paji la uso mara moja.

"Kisha akachovya kiganja chake cha mkono wa kushoto (ndani ya chombo) akakijaza maji, akayamwaga juu ya kongwa ya mkono wake wa kulia kisha akapitisha, kiganja chake juu ya mkono wake mpaka maji yakachuruzika kwenye ncha zake za vidole. Kisha akakijaza maji kiganja chake cha kulia, akayamwaga juu kongwa yake ya mkono wa kushoto na kisha akapitisha kiganja chake juu ya mkono mpaka maji yakachuruzika kwenye ncha ya vidole vyake.


"Kisha akapakaza sehemu za mbele ya kichwa chake na sehemu ya juu ya nyayo zake kwa ubichi bichi uliokiwamo  kwenye kiganja chake cha kushoto na kulia."[37]

Katika hadith nyingine Imam Muhamad Baqir (a.s.) anasimulia namna hiyo hiyo ya kuchukuwa wudhu ambayo Amirul-muuminina Ali alionyesha wakati watu walipotaka kujua kuhusu namna ya Mtume anavyochukuwa wudhu.[38]

Amri ya "wamsahu =æãÓÍæÇ Pakaza" maana yake pakaza viganja moja kwa moja, nk. juu ya kitu. Wakati neno kama "wamsahu = æãÓÍæÇ " linatumika peke yake katika hali ya kitendo kisichotumika ila pamoja na kusudio (transitive form) huonyesha mambo mengi na ujumla wa kitendo; km., "Wamsaha ru'usakum =æãÓÍæÇ ÑÄæÓßã takuwa na maana "Pakaza kichwa chako chote." Lakini wakati wowote kitendo (vebu) hiki kinafuatiwa na herufi ya 'È =be huonyesha kisehemu; km. Wamsahuu "bi ru'usakum =æãÓÍæÇÈÑÄæÓßã itamanisha "mpakaza sehemu ya kichwa chako" Katika aya iliyotajwa hapo juu amri hii "Wamsahuu =æãÓÍæ  " imetumika pamoja na herufi uBe = È   " na hivyo tafsiri sahihi itakuwa "Pakaza sehemu ya kichwa chako."

Hapa tena tunakuta tofauti nyingine kati ya Mashia na Masunni; Masuni wanapakaza kichwa chochote ambapo kwamba Mashia hupakaza sehemu tu ya vichwa   vyao.

Ni sehemu gani ya kichwa inatakiwa kupakazwa katika wudhu? Qur'an imenyamaza juu ya hili; sunna imelielezea. Hadithi nyingi


kutoka kwa Maimamu wa Ahlul 'l-bayt zimeelezea kwamba "Sehemu ya kichwa" ni "sehemu ya mbele."[39]

Neno "arjulakum -ÇÑÌáßã" maana yake "nyayo, mguu." Kufafanua maana yake, ilikuwa muhimu kuongeza maneno "ila 'l-ka 'abayn = Çáí ÇáßÚÈíä. rnpaka kwenye fundo mbili." Neno arjulakum limeunganishwa kwenye bi ru 'usikum = ÈÑÄæÓßã sehemu ya vichwa vyenu kwa kiunganisho cha kunganisha "wa =æ  na." Na hivyo sentensi hii itakuwa na maana "Pakaza sehemu ya miguu yenu."

Hapa tena tunakuja kwenye tofauti mbili zaidi miongoni mwa Masunni na Mashia. Masunni huosha miguu yao yote katika wudhu ambapo kwamba Mashia hupakaza tu upande wa juu wa miguu unaonekana mpaka kwenye fundo. Kwa ambavyo Qur'ann na hadith za Ahlu 'l-bayt zinavyohusika, kupakaza sehemu ya miguu ndio tu tafsir sahihi ya aya ya wudhu. Na tafsiri hii imekubaliwa na mwanachuoni mashuhuri wa Kisunni Imam Fakhru-d-Din ar-Ridha katika kitabu chake "Tafsiri al-Kabair" [40]

Tegemeo kubwa la Massuni kuhusu rai ya "Kuosha miguu" ni baadhi ya hadithi zilizoandikwa kwenye vitabu vyao vya hadithi. Hadithi hizi haziwezi kukubaliwa kwa sababu:

Kwanza, ziko kinyume na hukumu ya Qur'an. Na Mtume (saww) alisema, "Kama hadith inasimuliwa kwenu kutoka kwangu, basi iwekeni mbele ya Kitabu cha Allah. Kama iko kwa mujibu wa Kitabu cha Allah, basi ikubalini, vinginevyo ikataeni."[41]

Pili, ziko kinyume na sunna ya Mtume (saww) kama ilivyoelezwa na Maimamu wa Ahlul 'l-bayt ambao wamekubaliwa kama waaminifu na Waislamu wote. Hata baadhi ya Masahaba wa Mtume wameelezea kwa uwazi kwamba ni makosa kuhusisha "kuosha miguu kwa Mtume kwa mfano Sahaba mashuhuri Abdullah bin Abbas alisema, "Allah ameamrisha kuosha (sehemu) mbili na kupakaza (sehemu) mbili (katika wudhu). Je, hamuoni kwamba wakati Allah anapotaja tayamamu, anaweka kupakaza sehemu mbili katika sehemu mbili za kuosha (za uso na mikono) na kuziacha sehemu za kupakaza (za kichwa na miguu)." [42]

Tatu, Hadithi za Masunni katika habari hii zinakingana. Baadhi ya hadithi hutaja "Kuosha miguu" kama zile za Humran zilizonukuliwa na Imam al-Bukhari[43] na za ibn Asim zilizonukuliwa na Imam Muslirn. Ambapo baadhi ya hadithi nyingine husema kwamba Mtume "alipakaza miguu yake" Kama ile ya Ibad bin Tamim ambayo husema kwamba, "Nilimuona Mtume akichukuwa wudhu, na alipakaza miguu yake." Hadithi hii ya mwisho imeandikwa katika kitabu cha Ta'rikh cha al-Bukhari, Musnad cha Ahmad ibn Hambal, Sunnan cha Ibn Shaybah, na Mujamu'l-Kabir cha at-Tabarani; na wasimuliaji wake wote wanahesabiwa kama waaminifu.[44] Na ni hukumu inayokubaliwa ya kanuni za sheria za Kiislamu, (us'ulu l-fiqih) kwamba kama kuna hadithi zinazokingana (kupingana), basi zile ambazo zinakubaliana na Qur'an hukubaliwa na nyingine zote hukataliwa.

Hivyo tunaweza kuhitimlsha kwamba njia sahihi ya kuchukuwa wudhu kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah sahihi za Mtume (saww), ni namna ambayo imeelezwa na Maimamu wa Ahlul'1-Bayt (as).

 

SURA YA TATU

GHUSL

JOSHOKUBWA

III GHUSL

A. UTANGULIZI

Ghusli ni josho kubwa kama ilivyo kinyume na wudhu ambao ni josho dogo. Katika Sheria za ki-Islamu, ghusl huhesabiwa kama tendo la ibada; ni tendo la kujitoharisha mtu kutokana na uchafu kiibada (najasat) uliosabishwa kwa kujamiiana, kutokwa na manii au damu, na kwa kugusa mwili uliokufa (mayiti). Josho la kiibada analofanyiwa Mwislamu aliyekufa kabla ya kuzikwa vile vile hujulikana kama ghusli.

Ghusl kwa kila sababu hizi ina majina tafauti:-

Kujitoharisha kutokana na najis iliyosababishwa na kujamiiana au kutokwa na manii, hujulikana kama ghusl janabat. Kujitoharisha kutokana na najis iliyosababishwa na hedhi, hujulikana kama ghusl haydh. Kujitoharisha kutokana na najis iliyosababishwa na kutokwa na damu mara kwa mara (ukeni) hujulikana kama ghusl istihadha. Kujitoharisha kutokana na najis iliyosababishwa na damu baada ya kuzaa hujulikana kama ghusl nifas.

Katika sheria za ki-Islamu, kifo vile vile huhesabiwa kama sababu kiibada ya najis ya mwili wa Mwislamu. Kwa hiyo, Mwislamu aliyekufa lazima aoshwe kiibada kabla ya maadhimisho ya kuzikwa. Josho kama hilo la kiibada kwa Mwislamu aliyekufa hujulikana kama ghusl mayyit. Kugusa mwili uliokufa, kabla ya josho la kiibada, vile vile humfanya mtu kuwa najis. Kujitoharisha kutokana na najis hii hujulikana kama ghusl mass mayyit.

Katika sura hii tutaelezea namna na hukumu kwa ujumla za ghusl. Katika sura ya 4, tutajadili hukumu za kuoga janabat. Majosho yanayohusiana na wanawake yamejadiliwa kwa mapana katika kitabu changu majosho ya kiibada kwa wanawake (Taharatu 'n-Nisa).


B. NAMNA YA KUKOGA - GHUSL

Kabla ya kuelezea hukumu za kutekeleza ghusl ni muhimu kutaja kwamba ghusl zote zinafanywa kwa namna moja, tofauti ni kwenye nia tu ya kila ghusl. Kwa mfano, kwa kujitoharisha mtu kutokana na najis ya kujamiiana, mtu lazima aweke nia kwamba anafanya ghusl janabat.

Ghusl ni josho la ibada; hujumlisha kuosha mwili wote. Kuna njia mbili za kufanya ghusl. Moja inajulikana kama ghusl tartibi' na nyingine inajulikana kama ghusl irtimasi.

1. GHUSL TARTIBI:

"Ghusl tartibi" maana yake utaratibu wa kuoga, hufanywa katika hatua tatu:

Baada ya kusafisha na kuondoa najis (km. Manii na damu) kutoka katika mwili na baada ya niyyat, mwili utaoshwa katika hatua tatu: Kwanza, kichwa mpaka chini kwenye shingo; kisha upande wa kulia wa mwili kuanzia kwenye bega mpaka chini ya mguu; na mwishowe, upande wa kushoto wa mwili.

Kila sehemu inapaswa ioshwe yote katika hali ambayo maji yanafikia ngozi. Tahadhari maalum yapasa kuchukuliwa wakati wa kuosha kichwa; nywele lazima zichanwe (km. Kwa vidole vyako) ili kwamba maji yafike kwenye mizizi ya nywele. Wakati wa kuosha upande wa kulia wa mwili, baadhi ya sehemu za kushoto lazima zioshwe pia, na vile vile, wakati wa kuosha upande wa kushoto wa mwili, baadhi ya sehemu za kulia lazima zioshwe.

2. GHUSL IRTIMASI

"Ghusl Irtimasi" maana yake kuoga kunakojumlisha kuzamisha mwili wote kwenye maji. Yafaa kusema kwamba ghusl kama hiyo yaweza kufanywa tu katika chombo cha maji km. Dimbwi, mto, ziwa na bahari.


Baada ya kusafisha na kuondoa manii au damu katika mwili na baada ya niyyat, mwili wote unapaswa kuzamishwa katika maji mara moja, sio kidogo kidogo. Mtu lazima ahakikishe kwamba maji yanafikia sehemu zote za mwili, pamoja na nywele za ngozi juu yake. Hata hivyo, ghusl tartibi hupendekezwa zaidi kuliko ghusl irtimasi.

C. MATENDO YANAYOPENDEKEZWA YA GHUSL

Yaliyotajwa hapo juu ni matendo ya wajibu ya ghusl, hapa tutaelezea mambo ambayo yanapendekezwa (mustahab, sunnat) Wakati wa ghusl. Matendo haya yaliyopendekezwa ni matano:

1.Kuosha mikono yote mpaka kwenye kogwa mara tatu kabla ya ghusl.

2.Kusukutua mara tatu.

3.Kupakaza mikono katika mwili wote kuhakikisha kwamba kila sehemu imeoshwa sawa sawa.

4.Kuchana nywele kwa vidole kuhakikisha kwamba maji yanafikia mizizi ya nywele.

5.(Kwa wanaume tu) kufanya istibra kabla ya ghusl janabat.
Istibra, katika fuo hili, maana yake "kukojoa" Faida ya istibra; kama maji maji yatatoka nje ya uume wa mtu baada ya kukamilisha ghusl, na akatia shaka iwapo ni manii au mkojo, Je, itampasa kurudia ghusl au la? Kama amefanya istibra kabla ya ghusl, basi anaweza akachukulia kwamba
maji maji hayo ni mkojo - hatahitajika kurudia ghusl; atachukuwa wudhu tu kwa ajili ya sala yake. Lakini, kwa upande mwingine, kama hakufanya istibra kabla ya ghusl, basi atachukulia kwamba ni mabaki ya manii – itmabidi kufanya ghusl tena.

Ubaydullah al-Halabi anasimulia kwamba mtu mmoja alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu mtu ambaye amefanya ghusl na kisha akaona matone (yenye kutia wasiwasi


kenye uume wake) ambapo alikojoa kabla ya kufanya ghusl. (yaani itampasa kufikiria yale matone kama mkojo au manii?). Imam akasema, "Itampasa kuchukuwa wudhu tu (kwa ajili ya sala yake) Lakini kama hakukojoa kabla ya ghusl, basi lazima arudie ghusl."[45]

Hukumu hii ya istibra inawahusu wanaume tu. Sulayman bin Khalid alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu mtu ambaye amekuwa najis kiibada kwa sababu ya kujamiiana na kisha akafanya ghusl bila kukojoa. Kisha akatokwa na matone. Imam akasema, "Lazima arudie ghusl."

Sulayman: "Vipi kama matone ya aina hiyo hiyo yakimtoka mwanamke baada ya kufanya ghusl?" Imam akasema, "Hahitaji kurudia ghusl." Sulayman: "Kuna tofauti gani baina ya wawili hawa?" Imam akasema, (Mwanamke hahitaji kurudia ghusl janabat) kwa sababu kinachotaka kutoka kwake kwa uhakika ni (mabaki ya) maji maji ya mwanaume." [46]

D. MUHTASARI WA GHUSL

Huu ni mukhtasari wa ghusl. Mapendekezo ya matendo ya ghusl yako kwenye hati ya italiki.

1.Ondoa najasat (manii, damu) katika mwili

2.Niyyat.

3.Osha mikono mpaka kwenye kongwa mara tatu

4.Sukutua mara tatu

5.Osha kichwa mpaka chini ya shingo; Pakaza mikono yako juuya uso na shingo na uchane nywele kwa vidole vyako.

6.Osha upande wa kulia wa mwili wako kuanzia kwenye bega mpaka chini ya nyayo, pamoja na baadhi ya sehemu


za kushoto vile vile.  Wakati unaosha, pakaza mwili kwa mkono wako.

7. Osha upande wa kushoto wa mwili wako kuanzia kwenye bega mpaka chini ya nyayo; pamoja na baadhi ya sehemu za kulia vile vile. Wakati unaosha, pakaza mwili kwa mkono wako.

E. MASHARTI YA KUSWIHI KWA GHUSL

Kuswihi kwa ghusl hutegemea juu ya masharti makhususi ambayo hujulikana kama "mashariti ya kuswihi kwa ghusl." Masharti haya yako kumi kwa idadi: Masharti matatu yanahusika na maji. Manne yanahusika na mtu na matatu katika matendo ya ghusl yenyewe.

i. MAJI:

1.          Maji lazima yawe mutlaq (safi, yasio changanywa  na chochote).

2.    Maji lazima yawe twahir (safi kiibada)

f. Maji lazima yawe mubah (ya halali) maelezo ya masharti haya yako sawa na masharti ya maji ya wudhu.

ii.MTU:

4.    Niyyat

5.          Sehemu zote za mwili lazima ziwe safi kutokana na najis
(km. Manii, damu) kabla ya kuanza ghusl.

6.          Utumiaji wa maji uwe hauna madhara kwa mtu ambaye anataka kufanya ghusl.

7.          Ghusl lazima ifanywe na mtu mwenyewe (maelezo yako sawa kama katika wudhu.)

iii.GHUSL:

8.          Sehemu ambapo ghusl inafanywa lazima iwe mubah (halal).

9.    Ghusl inapaswa ifanywe ima kwa njia ya tartibi au kwa


njiaya irtimasi.

10. Sehemu zote za mwili lazima zioshwe sawa sawa kama ilivyoelezwa hapo juu.

F. BAADHI YA HUKUMU ZA JUMLA

1.Kama ghusl zaidi ya moja inakuwa wajibu juu ya mtu, km. Janabat. mass mayyit, n.k. basi ghusl moja pamoja na niyyat ya yote itatosha. Zurarah bin A'yun anamnukuu Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kama ifuatavyo: "Wakati ukifanya ghusl (km., baada ya alfajir) ghusl hiyo moja
hutosheleza kwa (ghusl za) janabat, jum'ah, Arafah, nahr, halq, dhabibu na ziyarat. Wakati ghusl mbalimbali zikiwa wajibu juu yako, basi ghusl moja itatosha... Na hukumu hiyo hiyo ni kwa ajili ya mwanamke; ghusl moja itamtosha
kwa ajili ya ghusl ya janabat, ihram, jum'ah, na kwa ajili ya ghusl yake ya hedhi na Idd."[47]

2.Ghusl zote, isipokuwa ghusl kwa ajili ya "Istihadhah ya wastan" hutosheleza kwa aliyeifanya kwa ajili ya wudhu maadamu hakuna nawaqidh ya wudhu yoyote iliyotokea baada ya ghusl.   Hivyo mtu ambaye amekoga ghusl janabat, kwa mfano, anaweza kusali bila kuchukuwa wudhu. Zurarah anamnukuu Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) kuhusu njia ya kufanya ghusljanabatkamaifuatavyo:

"....hakuna wudhu kabla yake wala baada yake."[48]

3.Kama moja ya nawaqidh wudhu (km. kukojoa) ikatokea wakati wa ghusl janabat, basi mtu lazima afanye ghusl tena na katika hali hii inapendekezwa achukue wudhu baada ya ghusl. Kama moja ya nawaqidh za wudhu ikitokea wakati wa ghusl ya pili, basi ghusl haitaathirika; lakini mtu lazima achukue wudhu baada ya ghusl kwa ajili ya Salat.


4.Kama moja ya sababu za kufanya ghusl kuwa wajibu ikatokea wakati wa ghusl, basi kuna uwezekano wa namna mbili:   (a)  Imma sababu ni sawa na sababu
ambayo imesababisha ghusl ya wakati ule, basi mtu atafanya ghusl tena; (b) au sababu sio sawa na sababu ya ghusl ya wakati ule, basi itampasa kukamilisha ghusl na kisha afanye ghusl nyingine.

5.Kabla kuosha upande wa kulia wa mwili, kama mtu atakuwa na shaka iwapo ameosha kichwa na shingo, basi itampasa kuanza tena kuanzia mwanzo.   Lakini kama anatia shaka baada ya kuanza kuosha upande wa kulia, basi itampasa kupuuza shaka yake.   Wakati wa kuosha upande wa kushoto wa mwili kama mtu atatia shaka iwapo ameosha upande wa kulia au la, basi ataosha upande wa kulia kisha upande wa kushoto.

4. GHUSL 'L-JABIRAH:

Kama mtu ana kitata juu ya mwili wake, basi vipi atafanya ghusl? Mtu kama huyo atafanya Ghuslu 'l-jabirah. Ghusl Jabirah inaweza kufanywa kwa kufuata hukumu zilizotajwa katika wudhu l-jabirah; imma mtu ananyanyua kitata na kuosha kidonda kwa kawaida, au anaosha pembezoni mwa kidonda au juu ya kitata, n.k.


SURA YA NNE

GHUSLJANABAT (JOSHOKUBWA)

V. GHUSL JANABAT

A.UTANGULIZI

"Janabat" ni uchafu najis (najis) wa kiibada unaosababishwa na kutokwa na manii au kujamiina; na mtu ambaye kwamba ghusl Janabat huwa wajibu juu yake anajulikana kama "junub." Qur an inasema:-

"Enyi ambao mmeamini!

Msikaribie sala hali ya kuwa  ..................

junub   mpaka mkoge .... " (4: 43)

"Enyi ambao mmeamini! Mnaposimama, kwa ajiliya Salat.. na mkiwa najanaba, basi ogeni  ...."" (5: 6)

B. SABABU YA GHUSL JANABAT:

Kuna sababu mbili za janabat:

1. Kutokwa na manii, Hakuna tofauti yoyote iwapo kutokwa na maji maji (manii) haya ni wakati mtu akiwa macho au katika ndoto, kidogo au mengi kwa makusudi au vinginevyo, katika njia ya halali au ya haram (km. Punyeto): Katika hali zote hizi ghusl janabat huwa wajibu: Kama maji maji yatamtoka mtu (mume) na hajui iwapo ni manii au la, basi itampasa kuangalia alama tatu zifuatazo; (1) kutoka pamoja na ashiki; (2) maji maji yatokayo kwa nguvu; (3) kujisikia ahueni baada ya kutokwa na majimaji hayo. Kama alama hizi zikipatikana pamoja juu ya mtu, basi itampasa ayachukulie majimaji hayo kama manii, vinginevyo sio.

Kama majimaji yatamtoka mwanamke, basi ni tahadhari ya wajibu kwa ajili yake kufanya ghusl janabat

mradi imetokana na ashiki ya kujamiiana na alijisikia ahueni baada ya majimaji hayo kutoka. Lakini kama majimajai hayo yametoka bila ashiki ya kujamiiana au bila kujisikia hali ya ahueni baada ya maji hayo kutoka, basi sio najis na kwa hiyo ghusl sio wajibu juu yake.

2. Kujamiiana: Hakuna tofauti yoyote iwapo kujamiiana huko kulikuwa halali au haramu, na iwapo manii yametoka au la Katika sheria za Ki-Islamu, kujamiiana huelezewa kama kuingizwa kwa kichwa cha uume kwenye uke au tupu ya nyuma ya mwanamke. Hii ndio kusema, kwa ajili ya ghusl janabat kuwa wajibu sio lazima kwamba kupenyeza uume wote au kutokwa na manii kutokee. Katika hali ya kujamiiana, ghusul janabat huwa wajibu kwa wote mwanaume na mwanamke.

C. MAMBO ANAYOKATAZWA MTU MWENYE JANABA

Kuna vitu makhususi katika Uislamu ambavyo ni vitakatifu mno kiasi kwamba Mwislamu hawezi kugusana navyo mpaka awe tohara kiibada na msafi. Kutegemea juu ya dhana hii ya utakatifu, junub (mtu mwenye janaba) anakatazwa kugusana katika njia mbalimbali, na viwili kati ya vitu vitakatifu zaidi katika Uislamu: Qur'an na Msikiti.

Matendo manne yafuatayo ni haram kwa junub kabla ya ghusl. Mawili yanahusiana na Qur'an na mengine mawili yanahusiana na msikiti.

1. Kugusa maandishi ya Qur'an, majina na sifa za Allah, majina ya Mitume, Maimamu na Fatimah (bint wa Mtume). Hii imekwisha lezwa tayari katika ukurasa wa kitabu hiki.

2.Kusoma aya za Qur an ambazo kwayo Sajdah ni wajibu.
Ayahizi ni: Aya 15 yasuraya32. ayaya 15 yasuraya41,
aya ya 62 ya sura ya 53, na aya ya 19 sura ya 96. Ni bora kutosoma hata aya moja kutika sura hizi.

3.Kuingia au kukaa msikitini: Qur'an inasema:

"Envi ambao mmeamini!   wala (hamruhiisiwi kuingia msikitini)   kama mna janaba mpaka mkoge isipokuwa kama mnapita tu .... " (4: 43).

Kwa kutegemea aya hii na hadhhi sahihi, Mujtahid wamehitimisha kwamba junub anakatazwa moja kwa moja kukaa msikitini.

Naam, kama aya inavyosema mtu anaweza kupita msikitini (kwa kuingia mlango huu na kutokea mlango mwingine). Hata hivyo, ruhusa hii ya kupita moja kwa moja haihusiani na sehemu zifuatazo: Masjidu'l-Haram (Msikiti mtukufu wa Makkah), Masjidu'n-Nabi (Msikiti wa Mtume huko Madina) na ziara za Maimamu -junub hawezi hata kupita moja kwa moja sehemu hizo. Jamil alimuuliza Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) iwapo junub anaweza kukaa msikitini au la? Imam akasema, '"hapana! Bali anaweza akapita moja kwa moja katika Misikiti yote isipokuwa msikiti Mtukufu (huko Makka) na Msikiti wa Mtume (huko Madina) ,"[49]

 Bakir bin Muhammad anasimulia kwamba, siku moja yeye na rafiki zake walikuwa wanakwenda kuelekea nyumbani kwa Imam Ja'far as-Sadiq, wakati walipomkuta Abu Basir njiani. Wakati Abu Basir alipojua kwamba tulikuwa tukienda kumuona Imamu, aliungana nasi. Jinsi Bakir na rafiki zake walivyokuja kujua baadae, Abu Basir alikuw'a katika hali ya janabat katika wakati ule. Wakati walipoingia nyumba ya Imamu na kumsalimu, Imam alimuangalia Abu Basir na akasema, "Ee Abu

Basir! Hujui kwamba mtu junub hapaswi kuingia nyumba za Mitume?[50] Abu Basir mwenyewe vile vile alisimulia kisa hiki na anamnukuu Imamu kama ifuatavyo: "Hujui kwamba junub hapaswi kuingia nyumba za Mitume na watoto wao .. ..'"[51]

4.   Kuacha kitu ndani au kukichukuwa kutoka Msikitini.

****

Mabo yafuatayo ni makruh (ya kuchukiza) kwa junub: 1. Kula na kunywa ni makruh kwa junub isipokuwa baada ya kufanya wudhu au kusukutua au kusafisha pua. 2. Kusoma zaidi ya aya saba kutoka kwenye Qur'an Tukufu. Hii hufanyika kwa aya nyingine, isipokuwa zile zilizoko kwenye sura nne zenye wajib sajidah zilizo tajwa hapo juu. 3. Kugusa jalada la Qur'an. 4. Kulala isipokuwa baada ya kufanya wudhu.

D. MATENDO AMBAYO KUSWIHI KWAKE HUTEGEMEA JUU YA GHUSUL JANABAT

1.  Salat (sala) isipokuwa salatu'l-mayyit (sala kwa ajili ya Mwislamu aliyekufa) ambayo inaweza kusaliwa hata katika hali ya janabat.

2.          Wajib tawaf (kuzunguka Ka'abah katika hija) Allah anasema;
".... Na tulimwusia Ibrahim na Ismail kuitakasa nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka (kwa kutufu)  (2: 125, 22:26).

Sio vigumu kuona kwamba kama nyumba inataka isafishwe na kutakaswa kwa ajili ya tawaf basi watu ambao watafanya tawaf lazima vile vile wawe safi na waliotakasika. Tazama vile vile sehemu H. katika wudhu.

3.    Saumu (kufunga).   Kama mtu kwa makusudi akabakia kuwa junub mpaka asubuhi katika (mwezi wa) Ramadhani, Saumu yake
itakuwa batili.

****

SURA YA TANO

TAYAMMUM

            (BAADA YA KUTAWADH A)


V.TAYAMUM

A. UTANGULIZI

Tayammum vile vile ni kitendo cha ibada kinachofanywa kwa kupakaza (udongo) paji la uso na mikono miwili. Badala ya Wudhu na ghusul. Qur'an inasema:

"Enyi ambao mmeamini !  ............. Na kama mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka msalani (chooni) au mmewagusa wanawake wenu (yaani kujamiiana nao) na msipate maji, basi itakupaseni kufanya tayammum katika udongo safi, kwa kupakaza sehemu ya uso wako na mikono yako. (4:43 tazama vile vile 5:6)

B. NAMNA YA KUFANYA TAYAMMUM

Baada ya niyyat kwa ajili ya tayammum, fanya yafuatayo:-

1.          Piga viganja vyote juu ya ardhi.

2.    Pakaza viganja vyote pamoja juu ya paji la uso. Kuanzia maoteo ya nywele mpaka kwenye kope na juu ya pua.
"Juu ya pua" maana yake mpaka kwenye sehemu ya fupa ya juu ya pua (brige ofthe nose). Macho, Pua, naMashavu hayajumlishi. Je? Inapasa viganja vyote kwa ujumla vya mikono yote kupakaza paji la uso? Hapana, sio muhimu
kwamba viganja vyote vya mikono yote vyapaswa kupakaza pajhi la uso; kitu cha muhimu ni kuhakikisha kwamba paji lote la uso linapakazwa.

3.          Kisha pakaza kiganja cha mkono wa kushoto juu ya mgongo wa kiganja cha kulia, kuanzia maungio ya kiganja mpaka
'chini ya ncha za vidole.   Kisha fanya hivyo hivyo kwa kiganja cha kulia juu ya mgongo wa kiganja cha kushoto.

4.    Kisha piga tena viganja vyote juu ya ardhi.

5.          Kisha rudia vitendo vilivyotajwa katika na 3 hapo juu.
Namna hii ya kutayammum imetegemezwa juu ya hadithi ambazo zimeelezea juu ya maneno ya Qur'an ambayo husema:   "Fanya tayammam...kwa kupakaza sehemuya uso na mikono yako. "

C. VITU AMBAVYO JUU YAKE TAYAMMUM YAWEZA KUFANYWA

Aya ya tayammum iliyotajwa hapo juu, inasema kwa uwazi kwamba "fanya tayammum katika udongo safi. " Kwa kutegemea juu ya aya, hii na hadithi zinazoelezea, Mujtahid wetu wanasema kwamba tayammum yapasa kufanywa katika moja ya aina za udongo zifuatazo (katika utaratibu wa mpangilio):

1.          Udongo laini au mgumu

2.    Mchanga

3.          Changarawe au jiwe - mbali na madini au vito vya thamani.

Kama hakuna aina ya udongo inayopatikana, basi ni hapo tu mtu anaweza akafanya tayammum katika vumbi (ambalo limejikusanya katika sakafu, au ardhi, juu ya zulia au nguo). Kama vumbi halipatikani, basi tope laweza kutumika, lakini katika njia ambayo kwamba baada ya mikono kuwekwa juu yake, inapasa isafishwe kwa kuifuta yote pamoja.

Vifaa vyote vya kufanyia tayammum lazima viwe na hali zifuatazo:-

1.          Lazima kiwe kikavu kadri iwezekanavyo

2.          Lazima kiwe tahir

3.          Lazima kiwe mubah (halali)


4.  Sehemu ambapo vitu vilivyotajwa hapo juu vipo lazima nayo iwe mubah.

D. WAKATI GANI WA KUFANYA TAYAMMUM?

Tayammum inaweza kufanywa katika hali saba zifuatazo:-

1.  Kama maji ya kutosha hayawezi kupatikana kwa ajili ya wudhu au ghusl.

Kama kuna muda wa kutosha kwa ajili ya Salat, basi mtu itampasa angoje na asali wakati akifika sehemu ambapo maji yanapatikana.

Wakati maji havapatikani, Je, ni wajibu kuyatafuta? Kama mtu anajua kuwa maji hayapatikani, basi sio wajibu kwake kuyatafuta. Lakini kama kuna uwezekano wa maji kupatikana, basi ni wajibu kutafuta mpaka mtu awe na uhakika wa kutopatikana kwake. Katika hali ya mwisho, kama mtu yuko kwenye uwanda na nchi iliyo nyeupe, basi itampasa kutafuta kwa umbali wa hatua 400 katika pande mbili, kama atakuwa sehemu za milima au katika msitu, basi itampasa kutafuta kwa hatua 200 katika pande zote nne. Hata hivyo. kama mtu ana hakika ya maji kupatikana katika upande makhususi, basi sio muhimu kutafuta katika pande hizo.

2. Wakati maji yanapatikana lakini ni vigumu kuyafikia.

Haileti tofauti yoyote iwapo ugumu huu ni wa kimwili au vinginevyo. Kwa hiyo, kama kufikia maji kutahusisha hatari ya maisha, hesima au mali, basi mtu atafanya tayammum. Kwa mfano: Kwa ajili ya uzee au maradhi inakuwa vigumu kufikia maji, au katika mtu kwenda kwa ajili ya maji atakuwa katika hatari ya wanyama na wezi; au mmilikaji anahitaji bei mbaya kabisa kwa ajili ya maji n.k.

3.  Wakati utumiaji wa maji kwa ajili ya wudhu au ghusl una madhara kwa afya au maisha ya mtu.


Kwa mfano: Mtu ambaye anahofia kwamba utumiaji wa maji unaweza ukamfanya aumwe au kuzidisha maradhi yake, basi itampasa kufanya tayammum. Hata hivyo, kama utumiaji wa maji moto katika hali hiyo hauna madhara, basi tayammum haiwezi kuwa badala ya wudhu au ghusl.

4.       Kama maji yanapatikana lakini mtu anahofia kwamba kutumia maji hayo kutamfanya yeye mwenyewe, jamaa aliofuatana ano au mifugo yake katika hatari ya kiu.   Katika hali hiyo mtu itampasa kufanya tayammam badala ya wudhu au ghusl.

5.       Wakati muda wa sala ni mfupi mno kiasi kwamba mtu kama ataanza kuchukuwa wudhu au ghusl, sala yake itakuwa kadha ambapo kwa kufanya tayammum atasali sala yake katika wakati wake, katika hali hiyo mtu itampasa kufanya tayammum.

6.Wakati mwili au nguo pekee ya mtu ni najis; na akaona kwamba kama atatumia maji kwa ajili ya wudhu au ghusl, mwili wake au nguo yake itabakia kuwa najis; katika hali hiyo itampasa kwanza kutoharisha mwili wake au nguo yake kwa maji yalipo na kisha afanye tayammum.

7. Wakati utumiaji wa maji hutegemea juu ya vitu ambavyo vimekatazwa na Shari'ah. Km., Maji yamepatikana bila ya ruhusa ya mwenyewe, au yamo kwenye chombo ambacho hakikupatikana kihalali (ghasbi) au chombo kimetengenezwa kwa dhahabu au fedha ambamo kwayo mtu hawezi kufanya wudhu au ghusl. Katika hali zote hizi, mtu itampasa kufanya tayammum.

E.   MASHARTI KWA AJILI YA KUSWIHI TAYAMMUM.

Sawa na kama ulivyosoma katika wudhu na ghusl. kuswihi kwa tayammam hutegemea juu ya mashariti makhususi. Mashariti haya yako matano kwa idadi:-


1.  Niyyat.  Kama tayammam ni moja tu, basi sio muhimu kutaja iwapo ni badala ya wudhu au ghusl.

2.         Mfululizo (muwalat) Matendo ya tayammam lazima yafuatane moja baada ya jingine.

3.         Taratibu (tartib) Matendo yote lazima yafanywe katika utaratibu ulioelezwa hapo juu.

4.         Sehemu za mwili zinazohusika na tayammam (yaani paji la uso, na mikono miwili) lazima ziwe tahir na shariti kusiwe na aina yoyote ya kizuizi juu yao, km. Pete, rangi ya kucha, n.k.

5.         Katika hali ya kawaida, mtu lazima afanye tayammam mwenyewe. Lakini katika hali ya ulemavu, mtu mwingine yeyote anaweza kumsaidia.  Katika hali hii ya mwisho,
msaidizi itampasa kuchukuwa mikono (viganja) ya mwenye kusaidiwa na kuipiga juu ya udongo na kufanya tayammam; kama hii haiwezekani, basi msaidizi atapiga
mikono (viganja) vyake mwenyewe katika udongo na kisha kupakaza paji la uso na mikono ya mwenye kusaidiwa.

F. BAADHI YA HUKUMU ZA JUMLA

Kama bado kuna muda wa kutosha kwa ajili ya Sala, basi mtu haruhusiwi kusali kwa tayammam, mpaka awe na uhakika wa kutopatikana kwa maji.

Je, itakuwaje kama maji yatapatikana ambapo mtu anasali sala yake kwa tayammum?

Kama maji yatapatikana ambapo mtu anasali sala yake kwa tayammam, basi kutakuwa na hali mbili tofauti: (1) Maji yalipatikana baada ya kwenda rukuu ya kwanza-sala yake ni sahihi na hakuna haja ya kuirudia. (2)Maji ya mepatikana kabla ya kwenda rukuu ya kwanza - itambidi kurudia sala yake kwa wudhu.   Hukumu hii


imetegemea swali ambalo Zurarah alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.): Je, Mtu itampasa atafanye nini kama maji yakija ambapo amekwisha anza salat yake (kwa tayammum) Imamu akasema, "Ilimradi mtu hajakwenda rukuu, itampasa mtu kuacha salat yake na kufanya wudhu; lakini kama amekwenda rukuu, basi itampasa kuendelea na salat yake. Hakika tayammam ni moja ya tohora mbili."[52]

Itatokea nini kama maji yatapatikana baadaya mtu amekwisha sali salat yake kwa tayammam?

Kama maji yatapatikana baada ya salat kusaliwa, basi sio wajibu kurudia salat hiyo kwa wudhu.

Tayammam ni utakaso tosha; mtu ambaye amefanya tayammam anaruhusiwa kufanya vile vitu ambavyo kuswihi kwake hutegemea juu ya wudhu au ghusl km. Kuingia msikitini, kugusa maandishi ya Qur'an, n.k. Hii huswihi maadam muda maji hayapatikani; mara maji yanapopatikana, tayammum moja kwa moja huwa batili.

Kama ghusl zaidi ya moja ni wajibu juu ya mtu, basi tayammum moja pamoja na niyyat ya ghusl zote hizo hutosheleza. Mtu ambaye kwamba ghusl janabat ni wajibu itambidi kufanya tayammam moja badala ya ghusl; hanahaja ya kufanya tayammam nyingine kwa ajili ya wudhu. Lakini kama ghusl nyingine kuliko ghusl janabat ni wajibu juu ya mtu huyo, basi itambidi kufanya tayammam mbili: moja badala ya ghusl na nyingine badala ya wudhu.

****

SURA YA SI TA

KUTOKA (MATENDO YA IBADA) YA DHAHIRI MPAKA KIROHO (MINA 'Z-ZAHIR ILA 'L-BATIN)

VI. KUTOKA MATENDO YA IBADA MPAKA KIROHO

A. UTANGULIZI

Moja ya tofauti kubwa za wakati huu wa ustaarabu ni kwamba elimu imepata kuingia kwa watu wa kawaida katika usawa wa kutoweza kutofautisha. Mwendo wa kuwasilisha vitu katika njia nyepesi na katika lugha ya kawaida, na vyombo vya habari, umekuwa na jukumu muhimu la kufanya katika hili. Upatikanaji wa elimu umefanya watu wa kisasa wachunguzi zaidi kuliko huko nyuma kuhusu kila kitu, pamoja na kanuni za dini yake na matendo ya ibada. Katika familia kubwa ya wanadamu, Mwislamu wa leo vile vile amepata mgao wake wa uchunguzi huu wa ziada.

Tabia ya uchunguzi huu huvuta Mwislamu wa leo, kuhoji kwa kutumia akili kanuni na matendo ya ibada za Ki-Islamu. Hii, hakika, ni jambo zuri kwa sababu itaongeza ujuzi wake kuhusu upeo (na ubora) wa Ki-Islamu, na kumfanya imara zaidi katika maisha yake ya uchunguzi katika Uislamu. Wakati huu wa sasa, Mwislamu lazima apanue upeo wake na haimpasi kuungalia maelezo tu ya mambo ya kanuni za Ki-Islamu na matendo ya ibada kwa sababu mengi ya matendo hayo ni njia ya kuendea kwenye ulimwengu wa kiroho wa Ki-Islamu, ulimwengu ulio bado mgeni kwa Waislamu wengi. Aidha, lazima atumie gari sahihi la kupanda katika safari hii - Qur'an na sunnah.

Katika sehemu ya kitabu hiki, nakusudia kuchunguza utakaso wa nnje ili kugundua uhusiano wake na tohara ya kiroho

B. SWALI KUBWA

Je, matendo ya Ibada yana uhusiano wowote na utakaso wa kiroho? Jibu kwa swali hili litavuta akili za Waislamu walio wengi.


Wakati ukiulizwa, "Kwa nini wudhu na ghusl vimefanywa kuwa wajibu?" Au kwa nini vitu makhususi hufikiriwa kuwa ni ayn najis katika Uislamu?" Watu wengi watasema kwamba sheria kama hizo zilifanywa ili kwamba tuwe wasafi, na kwamba Uislamu ni dini ya usafi. Hili ni jibu unalopata kutoka kwa wote, Waislamu wenye akili za kawaida na vile vile Waislamu wenye mtizamo maridhawa (wenye kupendelea mageuzi-liberal).

Kwa bahati mbaya, msisitizo juu ya jambo hili la taharat na najasat unaoletwa na kundi la kwanza hutoa silaha kwa maoni maridhawa ambayo husema kwamba, sheria kama hizo zilifanywa kuwaweka safi waarabu wa majangwani na kwa hiyo hazituhusu sisi.

Sikatai kwamba Uislamu hutegemea kuwaona wafuasi wake wasafi kimwili, kwamba ni dini ya usafi, na kwamba hukumu za taharat husaidia katika kumuweka mtu katika hali ya usafi. Hakika, Uislamu ulikuwa umefanikiwa sana katika kuhimiza usafi wa mtu binafsi, sio tu wakati unapolinganishwa kwenye karne ya saba Arabuni, lakini hata ikilinganishwa na usafi binafsi wa wazungu nyuma sana kama karne ya kumi na tisa.

Will Durant anaandika: "Usafi katika zama za kati haukuwa wa pili kwa uchamungu. Ukristo wa mwanzo ulizishutumu hamamu (bafu) za Waroma kama visima vya upotofu na vya hovyo hivyo pasina utaratibu na upuuzaji wake wa jumla wa mwili kumefanya kutokuweka thamani juu ya usafi."[53]

Mt. Benedict alisema, "Kwa wale ambao ni wazima (wa afya), na hususan kwa vijana, kuoga kutarahusiwa mara chache."[54] Mwandishi mwingine anasema, "Vitabu vya kale vya mienendo ya kawaida ya kiungwana husisitiza juu ya kuosha mikono, uso na meno kila siku asubuhi, lakini sio juu ya kuoga ... Mfalme John alikoga mara moja kila baada ya juma tatu, na raia zake yumkini mara chache zaidi.[55]


Akielezea zama za mageuzi, Durant anasema, "Usitaarabu na usafi wa binafsi haukwenda pamoja na maendeleo ya uganga. Usafi binafsi haukuheshimiwa sana; hata mfalme wa Uingereza alikoga mara moja tu kwa juma, na wakati mwingine aliacha ."[56] Mwanahistoria huyo huyo, baada ya kuelezea tabia ya mavazi anaandika," Je, miili ilikuwa misafi vipi ndani ya mavazi ya madoido? Kitabu cha mwandishi wa karne ya kumi na sita 'Introduction pour les jeunes dames,' anazungumzia wanawake ambao hawana uangalifu wa kujiweka wenyewe wasafi isipokuwa katika sehemu zile ambazo zaweza kuonekana kubakia na uchafu ... ndani yao'; na methali ya ubezi huonyesha kwamba makahaba walikuwa ni wanawake pekee ambao waliosha zaidi ya nyuso zao na mikono yao. Pengine usafi uliongezeka pamoja na ufisadi, kwa vile wanamke walijitoa kujiuza zaidi wenyewe au kujionyesha, usafi ulipanua eneo lake."[57] Akiandika katika kitabu chake cha kupendeza "Clean and Decent" (Usafi na Adabu), anasema, "Tunaweza kujivuna katika njia nyingi za akina Elizabeth, lakini tunaona rejea chache kwenye kuoga au kuosha katika shakespeare."[58] Tukienda kwenye karne ya kumi na nane, tunaona kwamba vitabu vya mienendo ya kawaida ya kiungwana hushauri, "Kufuta uso kila asubuhi kwa kitambaa cheupe, lakini huonya kwamba sio vizuri sana kuuosha katika maji... "[59]

Mapema katika karne ya kumi na tisa Daktari alitamka kwamba


"Wanaume wengi katika London na wanawake wengine ingawa wana desturi ya kuosha mikono yao na nyuso zao, wanapuuza kuosha miili yao kutoka mwaka hadi mwaka."[60]

Katika 1812 Baraza la chini (Commo Council) lilikataa ombi kutoka kwa Lord Mayor wa London kwa ajili ya hamamu (bafu) tu katika Jumba la Lord Mayor "kwa sababu hoja hiyo haijawahi kulalamikiwa kwayo," na kama ana hitaji anaweza kutengeneza cha muda kwa gharama zake mwenyewe.[61] Katika ofisi ya Malikia Victoria katika 1817 kulikuwa hakuna hamamu katika Ikulu ya Buekingham.[62] Na si ajabu kwamba zama za wakati huo, "Maoni ya wenye akili walitambua kwamba kuoga mara kwa mara lazima kutaongeza homa ya baridi yabisi na matatizo ya mapafu ... mmoja wa Ma-Duke (Wafalme wadogo) wa Georgio alisema kwamba ilikuwa ni jasho ambalo humuweka mtu katika usafi,"[63] Kufikia mwisho wa karne ya kumi na tisa na mwanzo wa karne ya Ishirini, hofu ya maji ilianza kuondoka, "ingawa ilikuwa hivyo ilikuwa bado inafikiriwa kioja kuoga kwa aina yoyote bali kwa sababu za kiafya."[64]

Utafiti huu mfupi wa usafi na kuoga katika nchi za Ulaya huonyesha kwamba Uislamu ulikuwa umefanikiwa katika kuhimiza usafi binafsi wakati ukilinganishwa sio tu na zama za kati, bali hata nyuma kwenye karne ya kumi na tisa na mapema katika karne ya ishirini: Will Durant anaandika, "Moja ya vita vya msalaba ilikuwa ni kuanzishwa kwa mfereji wa kukogea huko ulaya katika mtindo wa Kiislamu."[65] Akielezea ustaarabu wa Othoman, mwanahistoria huyo huyo anaandika, "Usafi wa mtu binafsi ulikuwa jambo la kawaida. Katika mji wa Constantinopole na miji mingine mikubwa ya utawala wa Othoman hamamu za umma zilikuwa zimejengwa kwa marmar na mapambo ya kuvutia. Baadhi ya watakatifu wa Kikristo walijifaharisha wenyewe katika kujiepusha na maji, Mwislamu anatakiwa kutawadha kabla ya kuingia Msikitini au kusali salat zake; katika Uislamu usafi ulikuwa kwa hakika wa pili kwa uchamungu."[66]

LAKINI kusisitiza kwa upekee mambo ya hukumu za taharat ni sawa sawa na kupuuza sehemu nyingi za asili za matendo ya ibada ya Ki-Islamu.

Usafi wa mwili sio sababu kubwa ya msingi inayochukuliwa kwa ajili ya matendo ya ibada ya kutawadha. Kama Uislamu umeelezea wudhu, na ghusl kwa ajili ya usafi wa mwili tu, basi kwa nini basi ni muhimu kwa mtu ambaye mara tu ametoka hamamuni (bafuni) achukue wudhu kabla ya kusali salat ya Ki-Islamu? Kama matendo ya ibada ya kutawadha ni kwa ajili ya usafi wa mwili tu, basi tayammum ya nini? Tayammum ni badala ya wudhu na ghusl wakati maji hayapatikani; lakini inafanywa katika vumbi ("chafu") au udongo - na hii kwa njia yoyote haipelekei kwenye usafi wa mwili! Maswali haya yanatosha kuivunja hoja hii ya asili ya pekee.

C. MTAZAMO SAHIHI

Hivyo ni nini (hasa) uzito wa hoja ya matendo ya ibada ya kutawadha kama wudhu na ghusl? Kwa kuzichunguza aya mbili za Qur'an zihusikanazo na matendo ya ibada ya kutawadha, nimefikia hitimisho kwamba kuna randa mbili za utakaso:    Mwili na roho.

 

Ingawa wudhu na ghusl zinahusiana na utakaso wa mwili, lakini kuna sababu bora zaidi za msingi katika ibada mbili hizo za kutawadha- kuleta ukumbusho na njia ya kufikia utakaso wa kiroho.

Katika Surat '1-Baqara, baada ya kuzungumzia ghusl haydh, Qur'an inasema. "Hakika Allah huwapenda wale wamgeukiao mara kwa mara na huwapenda wale ambao hujisafisha wenyewe " (2:222). Katika aya nyingine, baada ya kuelezea hukumu za wudhu na ghusl Qur'an inasema, "Allah hataki kufanya uzito wowote kwenu, lakini Anataka kukusafisheni, na kwamba akamilishe neema zake juu yenu; kwafuraha mpate kuwa ni wenye kushukuru. " (5:6) Tunaona mambo mawili katika aya zote hizi mbili: Kwanza: Allah huwapenda wale ambao hujisafisha wenyewe, na kwamba hupenda kutusafisha. Pili: Hupenda kukamilisha neema zake juu yetu, na kwamba hupenda wale ambao mara kwa mara hugeukia kwake. Jambo la kwanza linahusikana na usafi wa mwili, ambapo jambo la pili linahusikana na utakaso wa kiroho.

Maneno katika aya ya kwanza yako wazi; huashiria kwenye usafi. Lakini nini kina maanishwa katika maneno ya aya ya pili? Nini maana ya "mara kwa mara hugeukia kwa Allah "? Kugeukia kwa Allah huonyesha kwamba mtu amegeukia mbali kutoka kwa Allah. Hii ina maana gani? Haya ni maswali ambayo nitayajadili

hapa chini:-

****

Katika muundo wa Kiislamu, roho ya mwanadamu ni kama mwanga wa bulb, kama bulb imehifadhiwa kutokana na vumbi na uchafu, itaangaza sehemu ile; lakini kama vumbi na uchafu vitaachiwa vijikusanye juu ya bulb, basi haitaweza kuangaza sehemu ile vizuri kama ilivyokuwa kabla. Halikadhalika roho ya mwanadamu inabidi kuhifadhiwa kutoka na 'uchafu' wa kiroho na kuchafuka, vinginevyo haitakuwa na uwezo wa kumuongoza mtu sawa kama ilivyokuwa mwanzo.


Allah muumba wa wanadamu anaelezea usahihi wa uumbaji wake katika njia ifuatayo:-

 Naapa kwa jua na kwa mwangaza wake.

Na kwa mwezi unapoliandama; na kwa mchana unapolilidhihirisha; na kwa usiku unapolifunika; na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza; na nafsi (roho) na aliyeitengeneza; na kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake; bila shaka amefaulu aliyeitakasa (nafsi yake); na bila shaka amejasiri aliyeiviza (nafsi yake).  (91: 1 - 10)

Baada ya kuapa kwa ishara zilizotukufu za uumbaji wake, Allah anasema kwamba roho safi ya mwanadamu ina uwezo wa kuelewa kipi ni kizuri na hipi ni kibaya maadam imetakaswa na bila kudhulumika. Aya hii huweka wazi kwamba roho ya mwanadamu, kama ulivyo mwili, ina uwezo wa kuwa najis na kuchafuka. Imamu Ali (a.s.) alisema, "Roho ya mwanadamu ni kito cha thamani; yeyote yule mwenye kuihifadhi huimarisha (uwezo wake), na yoyote mwenye kuipuuza huipunguzia (uwezo) wake. " [67]

Najis ambazo zaweza kudhulumu roho ya mwanadamu kwa pamoja hujulikana kama "dhambi" Mkusanyiko wa dhambi kwa hakika huiondolea roho ya mwanadamu uwezo na katika lugha ya

Qur'an 'huuteka moyo.' Allah anasema: "         Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao (maovu) waliyo kuwa wakiyachuma " (83:14) Kwa kutenda dhambi, sio tu roho ya Mwislamu itatekwa, bali vile vile kiroho anageukia mbali kutoka kwa Allah. Dhambi hufanya umbali kati ya Mungu na mtu.

Je, Mtu anaweza kuokoa roho yake kutokana na kutekwa na dhambi? Ndio hakika, mtu mwenye dhambi anaweza kiroho kurudi


kwa Allah. Kurudi kwa Allah maana yake kutubia na kuomba msamaha kwa ajili ya dhambi zako. Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) ameelezea jambo hili kama ifuatavyo:- "Kila muumini ana roho nyeupe, wakati akitenda dhambi, doa jeusi hujitokeza kwenye roho yake nyeupe. Kama akitubia, doa jeusi hutoweka. Lakini kama ataendelea kufanya dhambi, weusi utaongezeka mpaka ufunike roho yote-basi kamwe mtu hatarudi kuelekea kwenye mazuri. "[68]

Unaweza sasa kuelewa kwa urahisi kwamba kama ambavyo miili yetu yaweza kuwa michafu kwa najasat za mwili, roho zetu huwa chafu kwa dhambi. Kuiondoa miili yetu kutokana na najasat za mwili, tunatumia maji; halikadhalika, kuziondoa roho zetu kutokana na uchafu wa kiroho, tunatumia tawbah. Tawbaha kilugha maana yake "kugeuka" lakini hutumika katika istilahi ya Kiislamu kwa "Kutubia." Kwa maneno mengine, kwa kufanya tawbah mwenye dhambi "hugeuka kuelekea kwa Allah katika (kufanya) tawbah,"Na sasa itapasa iwe wazi kwako kwa nini nimechukuwa aya (2:222,) (Hakika Allah hupenda wale ambao mara kwa mara hugeukia hvake ") kama ukumbusho kwa utakaso wa roho. Dhambi hufanya roho ya mwanadamu kuwa chafu na kumchukuwa na kumweka mbali na Mungu. Tawbah hutakasa roho ya mtu na kumleta karibu na Mungu.

Kwa ufupi, roho ya mwanadamu ni madhulum; inadhulumiwa na dhambi; roho iliyodhulumiwa inaweza kutakaswa kwa tawbah. Kwa kutukumbusha sisi kwamba Anawapenda wale wafanyao tawbah katika aya ya ibada ya kutawadha, Allah anajaribu kutuweka hadhiri kwenye utakaso kiroho. Katika sehemu ifuatayo ya sura hii, nitajaribu kuelezea baadhi ya asili kubwa za uchafu wa roho, namna unavyo udhulumu roho na njia za kuitakasa roho kutokana na uchafu huo wa kiroho. Yote haya yatafanyika kwa kuunganisha utakaso wa matendo ya ibada kwenye randa ya roho. Kwa unyenyekevu naomba kwa Allah, subhanahu wa ta'ala, kunisaidia katika jukumu hili la kupendeza lakini wakati huo huo likiwa ni jukumu gumu.


D. KUUNGANISHA MATENDO YA IBADA KWENYE ROHO

1. KUTO KUAMINI - KUFR.

Moja ya najasat ni Kafir, asiye amini. Kwa hakika kama inavyotegemewa kafir anafikiriwa najis sio kwa sababu ya hali yake ya kimwili, bali kwa sababu ya hali yake ya roho - kafir, kutokuamini. Kwa kumtangaza kafir kama najis, Uislamu unataka kuhadharisha mawazo yetu kwenye ncha ya maradhi ya roho yajulikanayo kama kufr.

Kufr ni nini? Kufr kilugha maana yake mfuniko. Katika istilahi za Kiislamu, hutumika zaidi kwa mtu ambaye haamini Mungu; na hivyo "Kafir" maana yake mtu asiyeamini. Kwa kutumia neno "kafir" kwa ajili ya asiye amini, Uislamu unamaanisha kwamba asiyeamini ni mtu ambaye anafunika au anaficha ukweli. Ni kipi kinaweza kuwa kweli zaidi kuliko Mungu, Muumbaji? Vile vile humaanisha kwamba kafr ni mtu ambaye kwamba roho yake imefunikwa kabisa na giza.

Kufur - kumkataa Mungu - ni maradhi makubwa ya roho kiasi kwamba huathiri mwili mzima wa kafir na kuufanya najis. Hata kama kafir ajiosha sawa sawa mara mia moja na avae nguo zilizo safi Sana, bado atafikiriwa kuwa ni najis kiibada. Hakuna kinachoweza kuponyesha maradhi haya ya roho, hakuna kinchoweza kutakasa roho ya kafir isipokuwa Uislamu. Na kwa ajili hiyo, unaona kwamba


shari'ah huhesabu Uislamu kama moja ya Mutahhirat.

Je, inawezekana kweli jambo la kiroho kuwa na athari juu ya umbo la mwili wetu? Katika uwanja wa kiroho wa mtazamo wa ulimwengu wa Ki-Islamu, inawezekana. Kuifanya nukta yangyu wazi zaidi, nitatia mfano mwingine wa namna hiyo hiyo wa mambo ya kiroho lakini wa aina ya dhahiri. Umesoma katika sura ya kwanza ya kitabu hiki kwamba damu na Mayiti ya mwanadamu huchukuliwa kuwa ni najis kwa mujibu wa shari'ah. Hii ni hukumu ya ujumla, lakini kuna tofauti moja katika hukumu hii. Shari'ah inasema kwamba damu na mwili wa Shahidi sio najis. Shahidi ni uthibitisho unaoenyesha wa mtu kuwa tayari kutoa mhanga kila kitu kwa ajili ya Allah. Kufa shahidi ni kitendo kizuri cha sifa ya juu zaidi, na huathiri mwili wote wa shahidi. Na kwa ajili hiyo; Uislamu husema kwamba mayiti na hata damu ya shahidi ni tahir na safi. Sio mwili na damu tu lakini hata udongo wa kaburi la shahidi na kaburi lenyewe vimeathiriwa na kupata utukufu! Ni kwa sababu hii kwamba tumefundishwa kutoa heshima kwa mashahidi wa karbala kwa kusema: "Wazazi wangu na wawefidia kwenu! Mmekuwa wasafi na ardhi ambayo kwayo mmezikwa vile vile imekuwa safi. "[69]

Na hii ndio sababu kwa nini fiqh ya Shi'ah hupendekeza kwamba tufanye sajidah juu ya turbah, kidonge kilichotengenezwa kutokana na udongo wa Karbala.

Kwa ufupi, kama ilivyo tendo zuri la sifa ya juu zaidi kama kifo cha kishahidi kinavyoathiri mwili; damu na hata kaburi la shahidi huvifanya (vyote hivyo vilivyotajwa) kuwa safi na vitukufu, halikadhalika, aina ya tendo baya zaidi kama kufr huathiri mwili wote wa kafir na kuufanya najis.


Kwa nini Kufr ni jambo ovu kiasi hicho? Kwa kukataa imani ya Mungu, Kafir anapoteza sifa yake mwenyewe ya kweli. Baada ya kumkataa Mungu, ulimwengu huu huwa wa mwanzo na wa mwisho kwa maisha ya kafir; bila kuwa na imani ya akhera, unafanyakazi kwa ajili ya ulimwengu huu tu. Katika hatua hii, kama umuhimu wa kidini ukipoteza ushawishi wake, Kafir hufikiria kujiongezea uwezekano zaidi wa manufaa ya ulimwengu huu hata kwa gharama ya maisha ya watu wengine. Na anaanza kuuamini katika silika zake za kinyama tu na kunguuza mammbo yake ya kibinadamu. Wakati mtu akifikia hatua hii, anaanza kuhukumu matendo yake mwenyewe kama yale ya wanyama. Kwa mfano, kanuni ya ulimwengu wa wanyama ijulikanao kama "kupambana kwa ajili ya kuwepo" na "kuishi kwa mwenye nguvu" huwa ndio msingi wa ulimwengu wa mwanadamu. Wataalamu wengi wa mambo ya wanadamu (anthropologists) na wanasayansi wanachunguza tabia ya mnyama na kisha hawaelezi tu bali huthibitisha usahihi wa upotofu wa matendo ya mwanadamu. Ni kwa ajili ya watu kama hawa Allah anasema,

".... Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo na macho wanayo, lakini haoni kwayo na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika." (7. 179).

Halikadhalika shirk vile vile huchukuliwa kuwa ni ncha ya maradhi ya roho. Shirk maana yake mtu anayemuwekea Mungu washirika. Washirika hawa wanaweza kuwa mtu (watu), mnyama au kitu. Katika hali yoyote, Mushrik (mshirikina) ni muovu zaidi kuliko kafir kwa sababu wa kwanza hukataa tu dhana ya (kuwepo) Mungu ambapo wa pili huvinyanyua viumbe kwenye daraja ya Mungu. Mtu hawezi kuendelea kujidhalilisha mwenyewe hivyo kwa kumuinamia mwanadamu mwenzie au mnyama, au sanamu alilolitengeneza kwa mikono yake mwenyewe. Allah anasema:


"Hakika Allah hasamehi dhambi ya shirk lakini husamehe vingine vyote kuliko hicho. " (4:48)

Kwa kuwaita makafiri na mushrikina kama najis, Uislamu unataka kuhadharisha mawazo yetu kwenye umuhimu na ubora wa imani. Ni njia ya kupitia ya kusema kwamba katika uoni wa Allah kuonekana kupendeza kimwili na usafi hakuna thamani zaidi kuliko imani ambayo iko kwenye moyo wa muumini. Na vile vile hutueleza kwamba kama Uislamu uko makini hivyo kuhusu usafi wa matendo ya ibada, basi, vipi utakuwa makini kuhusu utakaso wa roho.

2. KIBURI - TAKABBUR.

Maradhi mengine ya roho yenye madhara zaidi au najasat' ni kiburi, hujulikana katika ki-Arabu kama takabbur. Ni hali ya akili ya mtu ambaye hujiona mwenyewe wa hali ya juu sana na kuwadharau wengine kwa kuwaona kuwa ni wa hali ya chini.

Katika mfumo wa mambo ya Ki-Islamu, kiburi kimelaumiwa kwa nguvu sana. Lakini ina nini cha kufanya na najasat na taharat?

Wakati natazama katika orodha ya najasat, vitu viwili visivyo husiana huonekana kushika mawazo yangu. Man'yi na mayti ya mwanadamu ni miongoni mwa vitu najis za kiibada. Man'yi (manii) hata hivyo huchukuwa mbegu ya mwanadamu - sanaa ya uumbaji wa Allah. Sasa kwa nini yaitwe najis?

Kwa nini mtu alazimike kujitakasa baada ya kutoa man'yi (manii)? Kwa nini Mwislamu achukuliwe najis baada ya kifo chake? Kwa nini ni lazima tujitakase kama tukigusa mayit kabla ya kuoshwa josho la ibada?

Baadhi ya watu wangeshawishika kuangalia sababu za kisayansi. Kwa ajili ya najasat ya man'yi na mayti. Sikatai uwezekano huo, lakini mawazo yangu hunipelekea kwenye uamuzi kwamba katika kutamka man'yi (manii) na mayti kama najis, Uislamu haupitishi hukumu juu ya mambo yao ya kimwili, badala yake


unajaribu kuleta akilini (mwetu) ujumbe mnyofu kuhusu kiburi.

Ngoja nieleze mwenyewe kwa kuuliza swali lifuatalo: Je, kuna uhusiano wowote kati ya 'Manii' na 'Mayti'? Ndio, manii ni mwanzo wa maisha ya mwanadamu na mayiti ni mwisho wake. Kwa maneno mengine, mtu huanza maisha yake kama manii na huishiliza maisha yake kama mayiti.

Kama mtu ataangalia kwenye uhusiano huu na kuelewa kwamba Uislamu umechukulia mwanzo wake na mwisho wake kama najis, atafikiria mara mbili kabla ya kuwa na kiburi!

Kama atakumbuka ubora wa ibada ya mwanzo na mwisho wake, kamwe hatapatwa na maradhi ya kiburi, haidhuru kiasi gani cha utajiri alionao au vipi amejipatia uwezo au nguvu. Kwangu mimi, manii na mayiti ya Mwislamu vimechukuliwa kama najisi kutukumbusha tu sisi asili yetu na kutukumbusha sisi kwamba kiburi sio haki yetu. Na kufikia katika uamuzi huu, nimetiwa moyo na usemi wa Imamu Ali bin Abi Talib (a.s.) ambao unasema, "Namshangaa mtu: mwanzo ni manii na mwisho ni mayiti, na kati ya mwanzo wake na mwisho wake ni mbebaji tu wa machafu - na bado ni mwenye kiburi."[70]

Kiburi ni miliki ya Mungu. Mtume Muhammad (amani iwe juu yake na kizazi chake) alisema kwamba Allah amesema:

"Kiburi ni joho langu na fahari ni mavazi yangu; kwa hiyo Yeyote yule anaye jaribu kuchukuwa lolote katika haya mawili kutoka kwangu, nitamtupa motoni."   Allah anasema katika Qur'an,

"Usitembee juu ya   ardhi kwa maringo, Hakika wewe huwezi kuipasua wala huwezi kufikia urefu wa mlima. " (17:37).

Vile vile anasema: "Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri) kwa upande mmoja wa uso, wala usiende katika nchi kwa maringo,


hakika Allah hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye. Na ushike mwendo wa katikati, na uteremshe sauti yako, bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko zote. " (31: 18-19).

Kiburi kinaweza kumsukuma mtesi (muathirika) wake kwenye dhambi nyingi na majinai. Hapa nitataja tu matukio mawili kutoka katika Qur'an kuhusu kiburi na matokeo yake.

Wale ambao ni wazoefu na kisa cha Adamu katika Qur'an wanajua kwamba kiumbe wa kwanza kuasi amri ya Allah ni Shaytan. Na kishawishi cha Shaytan kuasi ni kiburi, Qur'an inaelezea kisa hicho kama ifuatavyo:

"Hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni, sura, kisha tukawambia Malaika; Msujudieni Adamu; Basi wakasujudu isipokuwa iblisi hakuwa miongoni mwa waliosujudu. (Allah akasema kumwambia Shaytan) 'nini kilichokuzuia kumsujudia nilipokuamrisha? Akasema: 'Mimi ni bora kuliko yeye. (mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo; (Allah akasema) Basi shuka huko haikufai kufanya kiburi humo (haya) toka; hakika wewe ni miongoni mwa wadhalilifu. " (7: 11-13)

Katika sura nyingine, Qur'an inasema, " .... Wakamsujudia wote isipokuwa Iblis, akakataa na akajivuna (akafanya kiburi) na hivyo akawa mmoja wa Makafir. " (2: 34).

Hivyo kwa mujibu wa Qur 'an kiburi kilimtia mno upofu shaytan kiasi kwamba alisahau anavyojiita yeye wemyewe mkubwa kwa kuumbwa kutokana na Moto, kwamba alipewa yeye na Mungu huyo huyo ambaye alikuwa sasa akimuamrisha kumsujudia Adam.

Mfano mwingine kutoka katika Qur;an ni wa mwanadamu -firauni: Qur'an inaelezea kiburi chake kama ifuatavyo:

"Je, imekufika hadithi ya Musa?


Mola wake alipomuita katika bonde la Tuwaa (akambwambia) nenda kwa Firauni. Hakika yeye (amezidi katika jeuri zake). Umuambie: Je unataka kujitakasa? Nami nitakuongoza kwa Mola wako ili umche (hivyo Musa alikwenda kwa Firauni na) alimuonyesha ishara kubwa kubwa. Lakini alikadhibisha na akaasi. Kisha akarudi nyuma akaanza kufanya jitihadi. Basi akawakusanya (watu) akanadi: akasema Mimi ndiye Mola wenu Mkuu, Hapo Allah akamtia mkononi kwa adhabu. "  (79: 15-25)

Katika aya hizi, mtu anaweza kuona kwamba Allah humchukulia Fairauni kuwa ni mchafu kiroho na kwamba hiyo ndio sababu Mtume Musa anaambiwa amtake iwapo yuko tayari kujitakasa au la. Na kisha Allah anaelezea vipi kwa kiburi Firauni alivyodai kwamba, 'Mimi ndiyo Mola wenu Mkuu. Aya hizi ziko wazi kabisa katika kuelezea kwamba firauni alikuwa ana maradhi kutokana na uchafu wa roho ujulikanao kama kiburi. Firauni alikuwa ametawaliwa mno na kiburi kiasi kwamba wachawi wake mwenyewe walipotamka imani yao kwa Mungu wa Musa na Harun, alisema "Mmemuamini  yeye kabla sijakupeni ruhusa?! Tazama vipi kiburi kinavyoweza kufanya kwa mtu!

Lakini kama mtu siku zote atakumbuka kwamba mwanzo wake ni manii na mwisho wake ni mayiti, na vyote hivi vimechukuliwa kama najis na sheri'ah basi kamwe hatapatwa na maradhi ya uchafu wa roho wa kiburi. Mtu kama huyo hatakumbuka tu udhalilifu wake mbele za mola wake bali vile vile atajizuia kutokana na kuwadhalilisha wanadamu wengine, haidhuru ni kiasi gani walivyo 'chini' kimaisha.

Mbali na kukumbuka najasat ya manii na mayait, njia nyingine ambazo zaweza kumsaidia mtu kupambana na kiburi ni hizi zifuatazo: siku zote kuwa wa kwanza katika kusalimu wengine, kuhudhuria sala za jamaa na kwenda kuhiji. Sala za jamaa na hija ni programu ya mazoezi ya juhudi kumfanya mtu aelewe kwamba yeye si chochote


bali ni mtumishi wa Allah kama walivyo maelfu na mamilioni ya watumishi wake wengine ambao wako katika mataifa mbalimbali; wanazungumza lugha mbalimbali na sio muhimu kwao kuwa katika kipato kilicho sawa!

3. KUHESHIMU HAKI ZA WENGINE

Wanadamu wameumbwa kwa silka mbali mbali. Nyingi kwa mapana zaidi zaweza kuwekwa chini ya "Hawaa" (matamanio) na "hasira" vile vile hujulikana kama silka za chini zaidi au silka za wanyama. Hisia hizi hazikuumbwa bure, sio za kuzuiwa. Ni "hasira" ambayo hutuongoza kuepuka hatari na kujihami wenyewe. Na "hawaa" ambayo hutufanya tutafute chakula. Hata hivyo, silka hizi lazima ziwe chini ya miliki ya akili zetu au nafsi, ambayo hujulikana vile kama silka za hali ya juu ya silka za binadamu. Kwa mfano, kama matamanio ya mtu haya kudhibitiwa na akili, yatabadilika kuwa ulafi au choyo na kisha mtu huyo hatakuwa na heshima kwa hali yoyote ile kuhusu hisia au haki za watu wengine. Imam Ali (a.s.) alisema, "Allah amewapa Malaika uwezo wa akili lakini sio (silka za) matamanio na hasira; na amewapa wanyama silka hizi mbili bila uwezo wa akili; lakini amemtukuza mwanadamu kwa kumpa uwezo wa akili na halikadhalika silka za matamanio yake yakiwa chini ya amri ya akili yake, basi atakuwa bora kuliko malaika kwa sababu anafikia hatua hiyo (ukamilifu wa kiroho) pamoja na shida ambazo malaika kamwe hawazipati. " (kwa kusema "shida " maana yake ni matamanio na hasira.)

Lakini ili kudhibiti matamanio yake ya "kinyama" na kuyawekea chini ya uthibiti wa akili; mtu anahitaji kujenga uwezo wake wa kiroho. Elimu peke yake haitoshi. Mtu anahitaji mara kwa mara kukumbushwa kuhusu kuheshimu haki za wanadamu wenzake. Na ni katika ukumbusho huu wa mara kwa mara. Uislamu umefanikiwa zaidi kuliko mfumo mwingine wa maisha. Uislamu


umetumia matendo haya ya ibada ya kila siku kuimarisha baadhi ya kanuni muhimu za jamii na maadili katika akili za wafuasi wake.

Ukumbusho huo wa mara kwa mara umefanywa na hukumu zifuatazo za kujitakasa kiibada: (1) Bafu: lazima iwe mubah -yaani lazima uwe ni mwenye kumiliki bafu hiyo ni lazima uwe na ruhusa ya mwenyewe, vinginevyo inakatazwa kwako wewe kutekeleza haja zako za kimaumbile katika sehemu hiyo: (2) Maji na sehemu ya kuchukulia wudhu: Lazima viwe mubah (3) Maji na sehemu ya ghusl: lazima viwe mubaha (4)Udongo kwa ajili ya tayammam; ni lazima uwe mubaha na hata sehemu ambapo udongo upo lazima iwe mubaha. Sharia za aina hii hii zaweza kuonekana katika hukumu za ibada za sala za kila siku kuhusu nguo ambazo kwazo unasali nazo, sehemu ambayo unasalia, nk.

Kama Mwislamu atajifunga na hukumu hizi nyepesi za utaratibu wa kila siku, atalazimika kuhakikisha kwamba nyumba yake, maji, ardhi, nguo, n.k. ni mubah. Hii haitaongeza tu uimara na umuhimu wa kuheshimu haki za watu wengine, bali vile viile itaathiri njia ambazo hufanya maisha yake na jinsi ya kushughulika na watu wengine katika biashara. Atahakikisha kwamba kipato chake hakitokani na vyanzo haramu, vinginevyo utumiaji wa bafu, wudhu, ghusl na sala za kila siku katika nyumba yake haitakuwa sahihi. Maimamu kila mara wamejaribu kutufundisha kuhusu umuhimu wa kuheshimu haki za wengine. Imam Zainul 'l-Abidin (a.s.) alisema, "Naapa kwa yule ambaye amempeleka Muhammad kama Mtume wa Haki Hata kama muuaji wa baba yangu Hussein bin Ali, akaniaminisha upanga ambao kwao alimuulia baba yangu, hakika nitaurudisha kwake."

Katika hadithi nyingine, anasema, Allah atasamehe kwa ajili ya Waumini kila dhambi na kuwasafisha kwazo kesho akhera isipokuwa dhambi.mbili:   "Kuto kutekeleza taqiyyah pale ambapo


inapasa kutekelezwa, na kuvunja haki za ndugu yake katika imani. " Kwa hakika imekuwa bahati mbaya kwamba pamoja na mipango hii ya mafunzo katika Uislamu, Waislamu katika nchi nyingi hawaonyeshi kuguswa au kuheshimu haki za ndugu zao katika imahi. Ni kwa sababu gani baadhi ya Waislamu hawapati kunufaika kiroho na kimaadili kutokana na matendo haya ya ibada ni kwa sababu hawaunganishi matendo hayo ya ibada kwenye roho na mambo ya maadili. Kwao wao, haya ni matendo ya ibada na si kitu chochote kingine. Ni muhimu kwa Mwislamu kuunganisha matendo ya ibada ya Ki-Islamu kwenye roho yake, maadili na kanuni za jamii, na ni mpaka hapo tu ndio wataweza kujionyesha wenyewe kama umma bora katika ulimwengu wa sasa. Mfumo tayari uko pale, Waislamu wanatakiwa tu kuuelewa sawa sawa na kuutumia kwa ufanisi zaidi.

Uislamu sio dini ambayo kwayo uhusiano kati ya Mungu na mtu ni muhimu bali ni dini ambayo vile vile hutoa umuhimu mkubwa wa uhusiano kati ya wanadamu wenyewe. Katika Uislamu, huwezi kumridhisha Mungu kwa kutekeleza haki Zake, na kupuuza zile za wanadamu wengine.

Umuhimu wa kuheshimu haki za wanadamu wengine umeelezewa kwa uwazi sana katika Qur'an kwa kuchanganya kutaja pamoja Salat na Zakat. Katika zaidi ya aya 80, Allah amezungumzia kuhusu "Kusimamisha Sala na kutoa zakat. " Salat ni alama ya haki za Allah juu ya mtu, na zakat ni alama ya haki ya mtu ya wenyewe kwa wenyewe. Mtu bila wengine ni utekelezaji usio kamili katika Uislamu, hautathibitisha wokovu wa mtu kesho akhera.

Wakati tunazungumza kuhusu haki za watu, zaidi tunasisitiza juu ya vitu vyao na haki za kimwili, kuheshimu haki za wengine huchukuliwa zaidi na sisi kumaanisha kwamba yatupasa kujiepusha kutokana na kuwadhuru wengine kimwili au kuvunja haki za mali zao. Bali vile vile yatupasa kuzuia akili zetu kutokana na kutowaamini


wengine bila sababu zozote za msingi inaeleweka mara chache kwamba sio kwamba tunatakiwa tujiepushe na kuwadhuru wengine kimwili kuvunja haki zao za vitu, bali vile vile yatupasa kuepusha akili zetu kutokana na kutowaamini wengine bila sababu zozote za msingi. Uislamu unatufundisha kila siku kufikiria bayana kuhusu wengine.

Wakati mtu akianza kufikiria bayana kuhusu wengine, moja kwa moja atakuwa ameokolewa kutokana na matokeo ya uovu wa kuwaharibu wengine. Kwa matokeo haya sina maana ya kupeleleza kwenye tabia za watu wengine na 'kusengenya' Kufikiri bayana yapasa kuwa tabia yetu kuelekea wanadamu wote; lakini haswa zaidi kuelekea kwa Waislamu. Hata hivyo Waislamu wanachukuliwa na Allah kama kaka na dada kwa wenyewe kwa wenyewe. Na kama walivyo ndugu, yapasa kuaminiana na kuwa bayana kuhusu wengine. Qur'an inasema:

"Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu. Enyi mlioamini jiepusheni sana na dhana (mawazo kuhusu Waislamu wengine) kwani hakika dhana katika hali nyingine ni dhambi; wala msipeleleze (juu ya wengine) wala baadhi yenu msiwasengenye wengine. Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La. Hampendi. Na mcheni Mungu ni Mwenye kupokea toba na (na) Mwingi wa kurehemu. (49:   10; 12)

Wasiwasi hupelekea kwenye kupeleleza na kupeleleza hugeuka na kupelekea kwenye kusengenya. Uepukaji wa wasiwasi husaidia katika kujiepusha kutokana na kupeleleza juu ya wengine na hivyo na kusengenya (pia). Sio tu kwamba mtu, kama huyo ataokolewa kutokana na matokeo ya uovu wa kuharibu watu wengine, bali atakuwa na wakati zaidi wa kujikosoa mwenyewe ambako ni hatua ya kwanza ya utakaso wa roho.


Kuna mazungumzo ya kuvutia yaliyoandikwa na Allamah at-Tabrasi kati ya Imam Zaynul - Abidin (a.s.) na Muhammad bin Muslim az-Zuhri. Inaelekea kwamba az-Zuhri alikuwa hakai vizuri na watu. Alikuja kwa Imam na akalalamika kuhusu hali ya mazingira yake. Katika sehemu ya pili ya mazungumzo yao, Imam alitoa ushauri wa maana sana ambao unastahiki kukumbukwa na kila mtu na kila Mwislamu. Imamu alisema, "Na kama Shaytan, laana ya Allah iwe juu yake, akikufanya ufikiri kwamba una ubora juu ya mfuasi yeyote wa qibla, basi fikiria kuhusu mtu huyo; kama ni mkubwa kuliko wewe, basi sema, ' Amekuwa mbele yangu katika imani na matendo mema, kwa hiyo ni bora kuliko mimi? Kama ni mdogo kuliko wewe, basi sema, 'Nimekuwa mbele yake katika kuasi na madhambi, kwa hiyo ni bora kuliko mimi? Na kama ni makamo yako, basi sema, 'Nina hakika kuhusu dhambi zangu lakini nina mashaka kuhusu dhambi zake, hivyo kwa nini nipendelee shaka juu ya hakika'."[71] Soma hadithi hii tena na ifikirie inavyohusu. Angalia kama unaweza kufuata ushauri huu ambao, hakika, unastahiki kuandikwa katika herufi za dhahabu!

Kuonyesha umuhimu wa kanuni hii ya adabu, shari'ah imemhesabu ghaybatul'l-Muslim (kutoweka kwa Muislamu) kama moja ya Muhatahhi'rat. Yakupasa uchukulia kama tahir mwili au nguo za mtu ambaye alipatwa na najis mbele yako kwa sababu tu alitoweka mbele yako muda wa kutosha kwa yeye kujitoharisha mwenyewe au nguo zake. Hebu fikiria vipi Shari'ah inavyokutaka uwe bayana! Hili sio suala la kufikiria bayana kwa sababu hujui chochote kilichojificha kuhusu mtu huyo, bali ni hali ambapo unajua kwa hakika kwamba mtu au nguo zake zilipatwa na najis; bado unategemewa kufikiri bayana kuhusu mtu huyo.


4. UKWELI KATIKA NIA

Katika tathimini yetu wenyewe, tunamhukumu mtu kwa vitendo vyake. Hivi ndivyo ilivyo kwa sababu sisi, kama wanadamu, hatuwezi kujua makusudio ya mtendaji. Lakini, je, Allah anahukumu watu katika nia hiyo hiyo? Hapana katika siku ya malipo Allah hatahukumu kwa kuangalia katika matendo; atahukumu kwa kuangalia makusudio. Katika mfumo wa mambo ya Ki-Islamu, kusudio ni muhimu kama tendo lenyewe. Bali kwa mujibu wa Mtume, "Hakika matendo (hupimwa kwa mujibu wa) makusudio."[72]

Uislamu hufundisha wafuasi wake kufanya matendo mema kwa ajili ya kumridhisha Allah. Akielezea makusudio yetu ya maisha, Allah anasema,

"Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. " (51:56)

Kwa uhakika aya hii haina maana kwamba makusudio yetu ya kuumbwa si kufanya chochote bali kutekeleza sala za ibada. Hapana, sivyo hivyo kabisa. Kwa uhakika ina maana kwamba maisha yote ya Mwislamu yana pasha yawe ni tendo la kuabudu, yaani, unapaswa kwa.hadhiri kwa kumtii Allah. Maelezo bora zaidi ya dhana hii yanaweza kupatikana katika maneno ya Mtume yaliyonukuliwa katika Qur'an:

"Sema: Hakika sala zangu na ibada zangu, na uzima wangu, na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah, Muumba wa ulimwengu wote ... (6:162)

"Muislamu kamwe hataanguka katika shimo la ushirikina, kamwe hatafanya kitu chochote pamoja na makusudio ya kumridhisha mungu mwingine; lakini kuna baadhi ya najis za mawazo ambazo zinaitwa 'ushirikina uliojificha' dhidi yake ambazo lazima kwa nguvu sana ajilinde nazo. Kwa mfano, wakati mtu anamuabudu Allah, lakini wakati huo huo anataka watu wajue kwamba anamuabudu Mungu, basi anatenda dhambi ya ushirikina uliojificha, kwa sababu nia ya mwenye kuabudu sio safi, anataka kupendeza mabwana wawili kwa kitendo kimoja cha kuabudu: Mungu na 'watu'

"Sio ibada za sala tu, bali matendo yetu yote yanapaswa yategemee juu ya mapenzi ya Mungu.

Kwa mfano, tunapowasaidia ndugu zetu masikini, lazima tukumbuke kwamba unatoa mali ya Mungu kwa watu wanaomtegemea Mungu (yaani watu wa nyumbani kwa Mungu). Lazima kifanywe bila kivuli chochote cha makusudio ya kiulimwengu. Msaada unaotolewa pamoja na makusudio ya ulimwengu ni mwlli bila roho. Msaada unaofanywa kwa tamaa ya mtu kuimarisha msimamo wake wa kijamii huharibu mizizi ya msaada huo."[73] Allah anasema:

"Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia, kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu ..." (2: 264)

Kuna kisa mashuhuri cha Bahlul. Siku moja aliona Msikiti mkubwa unajengwa. Alikwenda kwenye eneo la jengo la Msikiti na akamuuliza (yule) mchangiaji mkubwa, "Kwa nini unajenga Msikiti huu?" Mfadhili: "Bahlul sio wazi kwamba Msikiti unajengwa kwa ajili ya kumridhisha Allah? Ni kwa ajili ya kitu gani kingine mtu atajenga msikiti? Bahlul akaondoka.

Akapata tofali kubwa la zege na akaandika 'Masji Bahlul' juu yake. Wakati wa usiku, aliliweka tofali lake juu ya mlango mkubwa wa Msikiti. Asubuhi yake, alimuona yule mfadhili amekasirika.

Kufanya tendo jema pamoja na nia safi ni hatua ya kwanza tu, kuliweka tendo hilo kama hesabu yako kwenye kitabu chako kwa Mungu ni vigumu zaidi. Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) anasema, "Kuweka tendo jema (katika daftari lako la matendo) ni vigumu sana kuliko kulifanya." Alipotakiwa kueleza anachomaanisha, Imam alitoa mfano: "Wakati Mtu akimsaidia ndugu yake akatoka pesa kwa ajili ya Allah ambaye hana mshirika, inaandikwa kwamba amefanya hivyo kwa siri (kwa ajili ya Allah), lakini kama atataja kitendo chake hicho kizuri (kwa mtu), basi kitabadilishwa daraja kuwa katika matendo ambayo ameyafanya kwa uwazi. Na kama akikitaja tena, kitapewa daraja ya kitendo kilichofanywa kwa ajili ya kuonyesha watu.

       Njia moja ambayo Shari'ah imechukuwa kuhadhirisha akili zetu kwenye fundisho hili muhimu la ki-Islamu ni kwa kulifanya sehemu ya ibada ambayo yatubidi kufanya katika msingi wa kila siku. Ninarejelea kwenye hukumu kuhusu niyyat katika wudhu; ghusl tayammum, Salat, n.k. Hukumu hizi, kama ninavyoelewa, haziko kwa ajili yao wenyewe, bali zinafanya kama ukumbusho wa kudumu kwamba makusudio yetu yanapaswa kuwa safi. Katika kufanya matendo mema.

Kumbuka, Allah haangalii kwenye matendo, Huangalia kwenye kusudio na nia ya mtendaji. "Hakika Allah hukubali (matendo mazuri) tu kutoka kwa watu wachaji. " (5:27)

5. DUA WAKATI WA WUDHU

Ningependa kumaliza sura hii kwa maelezo mafupi juu ya dua zilizotajwa katika sehemu 'D' ya sura ya pili. Kama mtu atahifadhi dua hizi na maana zake na akazisoma kila mara akichukuwa wudhu, nina hakika zitakuwa na matokeo ya maana sana katika roho yake. Dua hizi katika ibada ya kutawadha hufungua dirisha mmoja zaidi kuelekea kwenye ulimwengu wa kiroho wa Ki-Islamu.

Dua hizi katika mwanzo wa wudhu ni maelezo kuhusu usafi wa nia. Dua ya pili ni ukumbusho kwamba ibada ya kutawadha ni njia ya utakaso wa roho. Dua ya tatu inatuambia kuwa waangalifu katika kutumia ndimi zetu na vile vile hutukumbusha kuulizwa maswali siku ya hukumu. Dua ya tano hutujulisha kwamba mtu anaweza kukirimiwa au kuhasirika katika siku ya hukumu na hivyo yatupasa kujitahidi sana ili tupate kukirimiwa na sio kuhasirika. Dua ya sita na ya saba zinatukumbusha kwamba kama tunataka tupewe daftari la matendo yetu katika mikono yetu ya kulia, basi lazima tuwe wangalifu katika matendo yetu katika ulimwengu huu. Dua ya nane hutufundisha tusijitegemee sisi wenyewe tu, bali tutake msaada wa Allah vile vile. Na. mwishowe, dua ya tisa ni ukumbusho wa hali itakavyokuwa Siku ya Hukumu.

Ee Allah!

Utubariki na Mafanikio katika kukutii (wewe);

Utuweke mbali na madhambi; Ukweli katika nia zetu;

Kutambua mipaka (yetu); Na utubariki na mwongozo na uimarifu; ongoza ndimi zetu kwenye ukweli na hekima; Jaza nyoyo zetu kwa elimu na fahamu; Safisha matumbo yetu kutokana na haramu na (vitu vya) mashaka; Epusha mikono yetu kutokana na dhuluma na wizi; Angusha macho yetu kutokana na utovu wa maadili, adabu na kosa la imani; Funga masikio yetu kutokana mazungumzo ya kipuuzi na kusengenya

Ee Allah! Wabariki.

Wanachuoni wetu na uchaji na kuhubiri; Wanafunzi kwa moyo kufanya juhudi kubwa na kuvutika (katika

masomo yao); Na wasikilizaji kwa nguvu ya kufuata; Waislamu wagonjwa kwa shifaa na afueni; Wazee kwa sifa njema na subira, Vijana kwa utii na tawba;

Wanawake kwa adabu nzuri na usafi (wa matendo)

Matajiri kwa upole na ukarimu; Masikini kwa subira na kutosheka; Waislamu wapiganao kwa msaada wa ushindi; Wafungwa kwa kuachiwa huru na utulivu; Watawala kwa uadilifu na huruma; Raia kwa maadili mema na mwenendo mzuri; na uwabariki mahujaji kwa njia nzuri za kusafiria na masurufu.

****

MANENO NA MAELEZO YAKE

WAJIB: Wajibu muhimu, kupasa. Kitendo ambacho lazima kifanywe. Mtu atalipwa kwa ajili ya kukifanya na kuadhibiwa kwa ajili ya kukipuuza km. Sala za kila siku.

IHTIYAT WAJIB: Wajibu wa tahadhari: Maana yake ni sawa kama ile ya wajibu pamoja na tofauti kwamba popote ambapo Mujtahid anasema kwamba "hii ni wajibu ya tahadhari" Wafuasi wake wana hiari ya kuacha taqlid (kufuata) katika tatizo hili makhususi na kufuata fatwa ya mujtahidi bora wa pili maadam huyo mujtahid wa pili ana rai tofauti.

HARAM: Iliyokatazwa iliyozuiwa. Ni muhimu kujiepusha na vitendo ambavyo ni haram. Kama atafanya kitendo cha haram, ataadhibiwa ima na mahakama ya Ki-Islamu au kesho akhera au zote. Km. Kuiba. kula nyama ya nguruwe, n.k.

SUNNAT AU MUSTAHAB: Iliyopendekezwa, yenye kupendeza, bora. Huelekeza kwenye vitendo ambavyo vimependekezwa lakini visivyo wajibu. Kama mtu akivipuuza, hataadhibiwa; hata hivyo, mtu akivifanya, atalipwa. Km. Kuosha mikono kabla ya wudhu.

MAKRUH: Yenye kulaumika, kuchukiza, kutoshawishi. Hutumika kwa matendo ambayo yanachukiza lakini yasiyo haram. Kama mtu akifanya kitendo cha makruh, hataadhibiwa kwa ajili ya kitendo hicho; hata hivyo kama atajizuia kutokana nacho, basi atalipwa. Km. Kula kabla ya ghusl  janabat.

JA'IZ, HALAL, MUBAH: Iliyoruhusiwa, iliyokubaliwa, halali matendo au vitu ambavyo vinakubaliwa na halali: Hakuna malipo kwa kuvifanya wala adhabu yoyote kwa kukipuuza. Mubah hutumika;

kiujumla kwa vitu halali, sio kwa matendo yaliyokubaliwa. Km. Kunywa chai.

MUJTAHID: Mwanachuo wa kidini ambaye ni bingwa wa sheria za ki-Islamu, Shari'ah. Kwa kawaida, hutumika kwa Mujtahidina wenye daraja za juu mno, ambao hukumu zao hufuatwa na watu.

MARJA: Mujtahid wa daraja la juu mno ambaye anafuatwa na watu. Kwa maana halisi, ina maana sehemu, ya kurejelea. Mujtahidina wenye daraja la juu huitwa marja kwa sababu wao ni sehemu za kurejea kwa ajili ya watu katika mambo ya Shari'ah.

SHARI'AH AU SHARPAT: Kwa maana halisi ina maana ya mwenendo. Katika istilahi ya Ki-Islamu, ina maana ya sheria za Ki-Islamu.

MWISHO


[1]- Ibn Hajar al-Makki, as-Sawa' iqu' 1-Muhiriqah, Sura ya 11, sehemu ya 1. Kwa maelezo
zaidi juu ya suala hili, soma Uimamu cha Sayyid   Saeid Akhtar Rizvi; Sharafu
'd-Din,S. A. H., Al-Muraja'at na Jafri, S, M. H., The origin and Early Development

of Shi'a Islam.

[2] - al- Kulayin, Usulu 'l=Kafi, j. 2, sura 17, Hadith na. 14; ash-Sha'rani, at-Kubra
i-Kubra,j. 1, uk. 28; Abu Nu'aym, Hilyatu '1-Awliya, j. 3, uk. 193, 197.

[3] - at-Tabataba/i, al-Mizan,].9, uk.416; al-'Amili, Wasa'il). 1, uk.249-51; al-Kadhimi, Masalik, uk. 85.

[4]-Al-amili, Wasa’il, j 1, uk.247,1034.

[5] - Al-amili, Wasa’il, j.1, uk.1009. Masaalik, uk; al-ardibili, Zubdah,uk.31.

[6] - Wasa'il, j.1, uk. 1030

[7] - Wasa'il. l,uk. 1050

[8] - Wasa’il,j.1,uk.1051.

[9] - Wasa’il,j.1,uk.1055.

[10] -Ibid, uk. 1016.

[11] - al-Jannati, Taharatu 'l-kitabi, p. 22-3; as-Sadr, al-Fatawa al-Wadiha, uk. 221

[12] - al-Yazdi, al- Vrwah, uk. 24; al-Khumayni, Tahriru 'l-Wasilah, j. 1, uk. 118.

[13] - al-Gharawi, at-Tanqih fi Sharhi 'l-'Urwati 'I-Wuthqa (Lectures of Ayatullah al-Khu'i),

j. 2, uk. 64; pia angalia al-Jannati, Taharatu 'I-Kitabi, uk. 27

[14] - al-Khu'i, Minhaju s-Salihiyn,}. 1 (Beirut, Daru 'z-Zahra, 22nd ed.) uk. 111.

[15] - As quoted by Muhammad Jawad al-Mughniyya in Fiqhu 'l-lmam Ja'far as-Sadiq, j. l,uk. 28.

[16] - ar-Razi, Tafsir al-Kabir,]. 27, uk. 166.

[17] - al-Yazdi, al- 'Urwah, uk. 52. '

[18] - I6al-Khu'i,Minhaj, l,uk. 114.

[19] - Ibid, j.2:uk. 332.

[20]- Wasa'il,j. 16, uk. 294.

[21] - Wasa'il,'j l,uk. 1072.

[22] - Ibid, uk. 1073.

[23] - Ibid, uk. 1072.

[24] - Wasa'il,j. l,uk. 1093.

[25] - Ibid.

[26] - uIbid,uk. 1095.

[27] - Wasail j. 16, uk. 279-80.

[28] - tbid, uk. 285.

[29] - "Wasa'ihy l,uk. 1071.

[30] - Wasa'il,j.1.,uk. 282-3

[31] - Wasa'il,.j. l, uk. 177

[32] - Wasa'il j. l, uk. 177

[33] - Wasa'il, j. 1, uk. 256,483.

[34] - Ibid,j.uk.444.

[35] - Wasa’il,j.1,uk.269.

[36] - Wasa'il J. l,uk. 283-6 kifungu cha 17-19 sura ya Wudhu

[37] - Wasa'il,j. l,uk. 272.

[38] Ibid.

[39] - Wasa’il,j.1,uk.289.

[40] - 38 ar-Razi, Tafsir al-Kabir, j. 3, uk. 370.

[41] - Ibid, uk.371.

[42] - Muttaqi al-Hindi, Kanzu 'l-'Ummal.j. 5 uk. 103 (hadithi Na. 2213. Pia angalia
kwenye Musnad\bn HanbalJ. l.uk. 108.

[43] - al-Bukhari, Sahih,}. I (Beirut. Darul Arabia, n.d.) uk. 113

[44] - al-'Asqalani. al-'/.sabah,j. 1, uk. 193; piaangalia kwenyekitabuchake Tahdhib
at-Tahdhib.

[45] - Wasa'il j. 1, uk. 517

[46] - Ibid, uk. 482.

[47] - Wasa’il,j.1, uk. 526.

[48] - Wasa'il j 1, uk. 515; pia angaliauk. 503.

[49] - Wasa’il,j.1, uk.485

[50] - Wasa’il,j.1, uk.489

[51] - Ibid, uk. 489-90.

[52] - Wasa’il, j. 1, uk.991-2.

[53] - Durant, The Story of Civilization,). 4, uk. 835.

[54] - Wright, Clean and Decent, uk. 24.

[55] - Ibid, uk.39.

[56] - Durant, ibid/y 6, uk. 244.

[57] - Ibid, uk. 768.

[58] - Wright, ibid, uk. 75.

[59] - Wright, ibid, uk. 138.

[60] - Ibid.

[61] - Ibid.

[62] - Ibid, p. 139.

[63] - Ibid, uk. 138.

[64] - Ibid, uk. 158.

[65] - Durant, ibid,}. 4, uk. 835.

[66] - MDurant,/6W,j.4,uk.712-3.

[67] - al-Amudi, Ghuraru 'l-hikam, uk. 226.

[68] - al-Majlisi, Biharu 'l-Anwar,). 73, uk. 361.

[69] - Angalia "Ziyarat warithah" kwa Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.)katika Mafatihu 7-Jinan ya Shaykh 'Abbas al-Qummi.

[70] - as-Saduq, “Ilalu sh-Sharaya”, uk.101.

[71] - at-Tabarsi, al-Ihtijaj,}. 2, uk. 52.

[72] - Wasa’il, j.1, uk.33-5

[73] - Kwa mabadiliko kidogo kutoka Kitabu cha S.S.A. Rizvi Inner Voice, uk. 69.