rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

42. MSAMAHA NDIYO MALIPO YA ISTIGHFAAR.

Mfasiri mmoja wa Quran anasema:

a. Malipo ya TAWBA ni kukubaliwa kwake,

b. Malipo ya Istighfaar ni msamaha,

c. Malipo ya kushukuru ni kuzidishiwa neema,

d. Malipo ya Duaa ni kusikilizwa kwake,

e. Malipo ya sala ni kutimiziwa kwake,

f. Kwa kifupi Qurani inatuambia: Hakuna malipo ya wema ila wema

tu! (55:60)

Aya hiyo ya Qurani ipo inazungumzia kwa ujumla na wala si kwa kitu maalum si muumin au kafiri. Hata hivyo madhumuni ya aya hiyo ipo imeelezwa na Imam Jaafar as-Sadique a.s.:"Iwapo mtu anakutendea wema, basi na wewe pia umtendee wema tu hata kama yeye atakuwa ni kafiri."

Ulifika wakati mmoja huko mjini Kufa (Iraq) ambapo mvua ilikuwa haikunyesha na hali ya hatari ilidhihirika na ndipo wakazi wa Mji huo walipomwendea Imam Ali a.s. na kumwomba aombe dua ya kunyesha mvua. Na hapo Imam Ali a.s. alimwambia Imam Huseyn awaombee dua ya kunyesha mvua. Na baada ya kuomba Dua, mvua ilinyesha na wakazi waliweza kutumia maji mengi hata katika kilimo. Lakini wakazi hao hao wa mji wa Kufa walimfanyia nini kwa malipo hayo ya ihsani aliyokuwa akiwafanyia kila leo?

43. MAZUNGUMZO YA BAHATI.

Imam Jaafer as-Sadique a.s. amenakiliwa katika Usuli Kafi akisema:

Mcha Mungu mmoja na fisiqi (mwenye madhambi) mmoja waliingia Msikitini kwa kufanya ibada. Walipotoka nje mambo yakawa yamebadilika kabisa yakawa kinyume.Yaani yule fassiq alipoingia Msikitini alivutiwa na ibada za huyo Mcha Mungu na hivyo aliathirika mno moyoni mwake. Hapo allah swt alipendezewa mno na hali yake hiyo. Lakini yule Mcha Mungu aliyekuwa anayo ghururi (majivuno) alipomwona yule Faasiqi huyu amejiingiza humu Msikitini miongoni mwetu sisi wenyewe kufanya ibada bora?"

Katika hali hii ya kiburi na majivuno alijiona kuwa yeye yu bora kuliko wengine. allah swt hakupendezewa na tendo hilo la majivuno ya huyo mtu, na hivyo akajikuta amejipotezea malipo ya matendo yake mema kwa sababu ya kiburi.

Allamah Majlisi A.R. anaandika:"Katika ukoo wa Bani Israeli alikuwa mtu mmoja Faasiq aliyekuwa akiitwa 'Khalii' (mwenye madhambi au aliyeasi).Basi huyo fasiqi alimwendea mcha Mungu mmoja ili inaweza kutokea kuwa yeye akapona na kusamehewa na Allah swt kwa baraka za huyo mcha Mungu.

Huyo Mcha Mungu hakuwa Aalim (aliye elimika) hivyo alipojikuta yupo pamoja na faasiqi huyo alianza kujivunia.Kwa hakika huyo mcha mungu alifikia daraja la juu sana katika ibada hali kwamba kila kulipokucha kulimwijia kipande cha wingu likimkinga na jua na kumpatia ubaridi.Huyo Mfasiqi alipoyaona hayo yote alijiwa na hamuya laiti naye angalikuwa mcha mungu kama huyu basi naye angaliweza kufaidi hayo ambapo mwenyeji wake aliingiwa na majivuno mengi mno ya ibada zake.

Hali hii ya majivuno ya mcha mungu hayakumpendeza Mungu na badala yake alipendezewa na athari ya Mfasiqi.Ilipofika wakati wa kuagana kwaheri, huyo Mfasiqi aliondoka kwenda zake, na kumbe kile kipande cha wingu likaanza kumkinga yeye badala ya kumkinga mwenyeji wake mcha Mungu. Kwa kuyaona hayo, yalimshutusha mno huyo mcha Mungu na kujutia juu ya kosa lake asilolijua.

Basi Mtume wa zama hizo aliletewa ufunuo wa kumwambia kuwa Allah swt amemwondoshea hivyo kwa sababu ya majivuno na istikbari yake huyo mcha Mungu."

Basi haitupasi sisi kujivuna na kufa katika hali ya takaburi kwani aliyetukuka ni yule ambaye anayetukuzwa na Allah swt.Isije tukayapata yale tuliyoyasoma.

44. AYA YA QURANI ZIZUNGUMZIAZO TAWBA.

Sura na Aya zifuatazo zinazungumzia TAWBA Qurani: (Kwanza inatangulia nambari ya sura na kufuatiwa kwa nambari ya Aya).

2:37; 2:54; 2:187; 5:71; 6:54; 9:118; 20:83; 20:122; 25:70; 25:71; 28:67; 58:13; 73:20; 4:16; 2:160; 3:89; 4:146; 5:34; 7:153; 9:5; 9:11; 16:119; 24:5; 40:7; 4:18; 7:143; 46:15; 2:279; 9:3; 2:160; 22:4; 49:11; 3:128; 4:17; 4:26; 4:27; 5:39; 9:15; 9:27; 9:106; 9:102; 25:71; 33:24; 33:73; 9:74; 9:118; 85:10; 4:17; 5:74; 9:126; 2:128; 2:54; 11:3; 11:52; 11:61; 11:90; 24:31; 66:8; 40:3; 4:17; 4:18; 4:92; 9:104; 42:25; 66:8; 3:90; 66:5; 9:112; 2:27; 2:54; 2:160; 9:104; 9:118; 24:10; 49:12; 4:16; 4:64; 110:3; 2:222; 13:30; 25:71.

45. SIFA ZA WAMCHAO ALLAH SWT.

Ifuatayo ni Hotuba Na. 193 ya Imam Ali ibn Abu Talib a.s. kutoka Nahjul Balagha. (Sharh ya al- Hadid, Vol. 10, uk. 132-162)

Imeripotiwa na Sahaba wake Amir al- Muuminiin Ali ibn Abi Talib a.s. aliyekuwa akiitwa Hammam ibn Shurayh ambaye alikuwa mcha Mungu sana. Alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Amir al-Muuminiin, nielezee sifa za Muttaqiin (Wacha Mungu) kwa hali ambayo kama kwamba ninawaona wao." Imam Ali a.s. alijaribu kusita katika kumjibu na alimwambia, "Ewe Hammam, mwogope Allah swt na utende matendo mema kwa sababu Allah swt anasema katika sura ana-Nahl Aya 128: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wale wanaomcha, na wale wafanyao wema."

Hammam hakuridhika kwa hayo na alimfanya Imam Ali a.s. aseme zaidi. Kwa hayo Amir al-Muuminiin a.s. alianza kwa kumtaja na kumhimidi Allah swt na kumsalia mtume Muhammad s.a.w.w. na hapo alisema:

"Amma baad, Allah swt aliyetukuka, aliyeumba viumbe. Yeye aliviumba bila ya kuwa na mahitajio ya utiifu wao au kusalimika kwao kwa utendaji wa madhambi yao, kwa sababu dhambi afanyalo mtu yeyote haimdhuru yeye na wanaomtii wala haitamfaidia kitu chochote. Yeye amewagawia miongoni mwao riziki zao na amewaweka katika nafasi zao humu duniani.

Hivyo wanaomwogopa Allah swt, hao ni watu wapambanuao, mazungumzo yao yapo mahasusi (bila ya kuongezea au kubabaisha huku na huko) na mavazi yao ni ya heshima na mwendo wao ni wenye haya (nyenyekevu). Wao huwa wanafumba macho yao kwa yale yaliyoharamishwa na Allah swt kwa ajili yao, hutega masikio yao kwa elimu ambayo inamfaidia yeye. Wao huwa daima katika hali ya majaribio (hujitaabisha kwa ajili ya dini) hata kama wao huwa katika hali ya kustarehe. Iwapo kusingekuwa kumepangiwa wakati maalum wa kufariki, basi roho zao zisingekuwa zimebakia katika miili yao hata kwa kufumba na kufumbua macho kwa sababu ya hamu yao ya kutaka malipo yao (jazaa) na kwa khofu ya adhabu za Allah swt zenye kutisha mno.

Ukuu wa Muumba upo moyoni mwao na kwa hivyo, kila kitu kilichobakia huwa ni dogo machoni mwao. Kwao Jannat (peponi au Paradiso) ni kama kwamba wanaiona na kustareheka kwa neema zake. Kwao, Jahannam (motoni au Helo) ni kama kwamba wanaiona wapo wanataabika kwa adhabu zake.

Nyoyo zao zimejaa masikitiko, wamehifadhika na maovu, miili yao ni miembamba, mahitajio yao ni machache, na nyoyo zao zipo safi. Wao wamevumilia shida kwa kitambo kidogo na badala yake wamejipatia starehe za muda mrefu. Hiyo ni biashara iliyorahisishwa na Mola kwa ajili yao. Dunia inawatamani wao, lakini wao hawaitamani kamwe. Dunia iliwateka, lakini wao walijifanya huru kwa malipo. (nafasi zao)

Amma wakati wa usiku wamekuwa wakisimama kwa miguu yao wakisoma sehemu ya Qurani na usomaji wao huwa sahihi kimizania, wakifanyia majuto na masikitiko na kuomba kwa hiyo Qurani, matibabu ya magonjwa yao. Wanapopitia Aya juu ya Shauku (ya peponi) wao huichukua kwa pupa, na nyoyo zao huzigeukia kwa shauku, nao huhisi kama kwamba hivyo vipo mbele ya macho yao.

Nao wanapopitia aya zenye khofu (za Jahannam) wao huzizingatia kwa moyo na kuhisi kama sauti za Jahannam na milio yake yanaingia masikioni mwao. Migongo yao hukunjika, husujudu juu ya vipaji vyao, viganja, magoti na vidole vyake vya miguuni na huomba kwa Allah swt ukovu wao, wakati wa mchana wao huvumilia, wakiwaona waja wa kwelikweli ambao wanamwogopa Allah swt kwa wingi. Iwapo mtu yeyote akiwatazama, watawadhania kuwa wao ni wagonjwa, ambapo wao si wagojwa kama vile wanavyodhaniwa na vile vile husemwa kuwa wamerukwa na akili. Kwa hakika, khofu ya ziada zimewafanya wawe wendawazimu.

Wao hawaridhishwi na matendo yao yaliyo mema kwa uchache, na wala hawachukulii matendo yao makubwa kama ni makubwa. Wao huwa daima wakijilaumu na kuogopea matendo yao. Anapotokea mmoja wao akizungumzwa saidi, yeye husema: 'Mimi ninajielewa vyema kuliko vile wanielewavyo wengine, na Ewe Mola wangu! wanijua zaidi kuliko hata nafsi yangu. Ewe Allah! usinitendee kwa mujibu wa yale wayasemayo, na unifanyie mema zaidi kuliko vile wanifikiriavyo na unisamehe (zile kasoro) wao wasizozijua.'`

Alama yake ya kipekee ni kuwa utamwona yu mwenye nguvu katika Dini, mshupavu na mpole kwa pamoja, imani pamoja na kusadiki, juhudi katika (kutafuta) elimu kwa subira, ukiasi katika utajiri, upendo katika ibada, mwenye kushukuru katika njaa, mstahimilivu na mvumilivu katika hali ngumu, mapenzi katika kutafuta halali, raha katika mwongozo na chuki kwa uroho. Yeye huwa daima akitenda matendo mema lakini bado huwa mwenye woga. Ifikapo jioni huwa na shauku kubwa ya kumshukuru Allah swt. Huupitisha usiku katika khofu na huamka asubuhi katika furaha-khofu ya labda kuupitisha usiku katika hali ya usahaulifu, na furaha kwa neema na baraka alizotunukiwa na Allah swt. Ikiwa nafsi yake itakataa kustahimili kila kisichokipenda, basi naye hataikubalia ombi lake, kila kinachopendwa na nafsi yake. Macho yake yamepowa kwa yale yatakayodumu milele, ambapo vitu vya humu duniani visivyo vya kudumu, yeye hujiweka mbali navyo. Yeye huimarisha elimu pamoja na subira, na maneno yake kwa matendo.

Wewe utayaona matamanio yake ni mepesi, kasoro zake kidogo, moyo wenye khofu, nafasi iliyotosheka, chakula chake ni kidogo na cha kawaida, Dini yake ipo salama, matamanio yake yamekufa na ghadhabu yake imezimwa. Mema tu ndiyo yanayotegemewa kutoka kwake. Hapatakuwa na khofu ya kufikiwa nauovu kutoka kwake. Yeye atakuwa akihesabiwa miongoni mwa wale wanaomkumbuka Allah swt hata kama atakutwa miongoni mwa wale wanaosahau kumkumbuka Allah swt, na anapokuwa miongoni mwa wenye kumkumbuka Allah swt, hawezi kuhesabiwa miongoni mwa wenye kumsahau Allah swt. Yeye huwesamehe wale wote wasio waadilifu kwake, na humpatia yule aliyekuwa amemnyima. Yeye huwa na tabia njema hata kwa yule asiye na tabia njema mbele yake.

Kamwe hazungumzi mazungumzo yaliyo maovu, lugha yake ni laini, maovu yake hayo tena, mema yake yapo daima mbele na mizaha imeshamwondokea kwa kumgeuzia uso. Hutukuzwa pasi na kuhangaika katika maafa, mwenye subira wakati wa dhiki, na mwenye shukuru wakati wa faraja.Yeye huwa hamchukii yule anayembughudhi, na wala hatendi madhambi kwa ajili ya yule ampendaye. Yeye anakubalia yaliyo ya haki hata kabla hajatolewa ushahidi dhidi yake.Yeye hatumii kwa ubadhilifu kile kilicho mkononi mwake, wala hasahau kile atakiwacho kukikumbuka.Yeye kamwe huwa hawaiti watu kwa majina mengine yaliyo mabaya, wala huwa hawadhuru majirani zake, na wala huwa hafurahii maafa yawapatayo watu wengine, yeye kamwe hajiingizi katika ubatilifu na wala hatoki nje ya haki.

Anapokuwa kimya, ukimya wake huwa haumsikitishi na anapocheka, hapaazi sauti yake na anapotendewa mabaya, basi yeye huketi kimya akivumilia, hadi Allah swt hulipiza kisasi kwa niaba yeke.Nafsi yake inudhika naye, na watu wamesalimika naye kwa upole wake.Yeye anajitaabisha kwa ajili ya maisha ya ahera (ya milele), na huwafikishia raha watu kutokana naye.Kujiweka kwake mbali na watu ni kwa ajili ya uchaki na kujitakasisha, na ukaribu wake kwao ni kwa ajili ya upole na rehema. Kujiweka kwake mbali si kwa ajili ya upuuzi au kujiona mwenye fahari au takabari, na ukaribu wake kwao si kwa ajili ya kuhadaa au kudanganya."

Imeripotiwa kuwa Hammam ibn Shuray alipoyasikia hayo, alizimia na kufariki papo hapo kwa kuathirika na hotuba hiyo.

Hapo Imam Ali a.s. alisema: "Kwa kiapo cha Allah swt! Hayo ndiyo niliyokuwa nikiyakhofia kwake."

Aliongezea kusema: "Mawaidha kama haya ndiyo yanavyoathiri hadi akili nzuri."

Abdullah ibn al-Kawwa (mpinzani mkuu wa Imam Ali a.s.) alisema: "Ewe Amir al-Muminiin! Je, vipi wewe hauathiriki hivyo?"

Imam Ali a.s. alimjibu: "Ole wako! Ama mauti inayo saa maalumu iliyowekewa na wala haiwezi kuzidi au kuweza kubadilishiwa. Chunga sana,usitamke tena maneno kama hayo ambayo shetani ameyaweka juu ya ulimi wako."

46. DUA YA IMAM ZAYNUL AABEDIIN a.s. KATIKA KUOMBA TAWBA.

Ewe Mola wangu, ambaye sifa za kukusifu za wenye kukusifu haziwezi kutajika. Ewe mwenye mategemeo ambaye mategemeo hayawezi kwenda zaidi yako.Ewe ambaye kwako wewe malipo ya waja wako hayatapotea. Ewe unayeogopwa na waja wako. Ewe uliye khofu ya mja wako na hii ndiyo nafasi imemkuba ghafla kwa madhambi.

Ambaye amevutwa na zama za makosa na ambayo yameghalibiwa na sheitani.

Kwa hivyo ameshindwa kabisa kutimiza yale uliyokuwa umemwamrisha kuyafanya na yeye hakuyafanya.

Yeye amegang'ania tu katika yale uliyokuwa umeyaharamisha na kuyakataza kama kwamba haelewi uwezo ulionao juu yake.

Au kama yule anayekanusha ukarimu wako mtukufu kwake yeye hadi macho ya hidaya kufunguliwa kwa ajili yake na mawingu (kiza) cha upofu (wa hidaya) ulipoondolewa kutoka kwake, na alipotambua kwa ukamilifu vile alivyojidhulumu nafsi yake na kuyazingatia kuwa amemwasi Muumba wake.

Kwa hivyo ameyaona maovu yake kwa mapana vile yalivyokuwa, akaona ukubwa na uasi na upinzani wake ulivyo kupita kiasi, kwa hivyo amekurejea wewe kwa kutaraji msaada wako kwa kuona aibu mbele yako, akielekea kwako wewe kwa hali halisi kutokana na woga wake, shauku yake ya kutaka kuondolewa kila kitu na hofu zake, ila ni wewe tu ndiye mwenye uwezo wa kuyadonoa hivyo.

Hivyo amesimama mbele yako, akiomba.

Macho yake yakiwa yanatazama chini ardhini kwa utiifu, na kichwa chake chini kwa unyenyekevu wa Ukuu wako.

Katika hali ya kudhalilika ya nafsi anaungama kwako kwa siri zake zote ambazo wewe wazijua zaidi kuliko mimi mwenyewe na katika aibu amezihisabu madhambi yake ambayo wewe umeishakwisha kumhesabia.

(Yeye anakuomba wewe kumwokoa kwa kumtoa kutoka madhambi makubwa ambayo ameingia humo wakati wewe unajua na ambavyo imemwaibisha kabisa katika heshima yako ya maamrisho yasiyotimizwa naye, starehe ambazo madhambi yamemgeukia na kumhukumia adhabu ambayo itakayokuwa daima juu yake.

Yeye kamwe hakanushi uadilifu wako, Ewe Mola wangu! Iwapo wewe utamwadhibu.

Yeye anasadiki kuwa usamehevu kwako wewe ni jambo dogo. Iwap utamsamehe na kumhurumia yeye kwani wewe ni Bwana wa Hisani, ambaye hadhanii kuwa ni vigumu kwako wewe kumsamehe madhambi hata yakiwa makubwa kiasi gani.

Ewe Mola wangu! Kwa hivyo shuhudia! Mimi nipo hapa.

Nimekuijia wewe katika Ibada (kuomba), katika hali ya utiifu wa amri zako, nikitaraji utimizo wa Ahadi yako, ambamo wewe umeahidi kujibu. Kwani wewe umesema "Niombeni, nitakuitikieni" (40:26).

Ewe Mola wangu! Mbarikie Mtume Muhammad s.a.w.w. na Ahli Bayt yake toharifu.

Naomba unijaalie msamaha wako kama vile nilivyokuijia kwa kuungama na kukiri.

Naomba uniondoe kutoka vikwazo vya madhambi kwani nimeiwasilisha nafsi yangu mbele yako. Naomba unisitiri kwa usitiri wako kama vile ulivyoweza kuuchelewesha matimizo ya kisasi chako juu yangu.

Ewe Mola wangu! Naomba unithibitishie maazimio yangu ya kukutii wewe!

Unijaalie nguvu za fahamu zangu katika kukuabudu wewe.

Nijaalie rehema ya matendo ambayo yataweza kuosha na kutoa maambukizo ya makosa niliyo nayo mimi.

Naombanife katika Dini yako na katika Ummah wa Mtume Muhammad s.a.w.w.

Ewe Mola wangu! Mimi nafanya Tawba mbele yako katika hali hii ya madhambi yangu yaliyo makubwa mno.

Na yaliyo madogo.

Ya makosa yangu yaliyo dhahiri na yaliyofichika na yaliyotangulia kutendwa na ambazo zimetendwa hivi karibuni kwa Tawba ambayo yeye hata hawezi kuisimulia nafsi yake, kwa kutotii, na wala hawezi kudhamiria kurudia maasi.

Ewe Mola wangu! Kwa hakika wewe umesema katka kitabu chako (i.e. Quran) KItukufu kuwa unazikubali Tawba za waja wako, na unasamehe madhambi na unawapenda wale wafanyao Tawba (Qurani, 1:222), naomba ukubalie Tawba yangu kama vile wewe ulivyoahidi. Nisamehe madhambi yangu kama vile ulivyodhamini. Nijaalie mapenzi yako kama vile ulivyokubali. Ewe Mola wangu! Nakutolea ahadi yangu kuwa kamwe sitarudia katika kila kile ukichukiacho; na ni dhamana yangu kuwa kamwe sitarejea katika yale usiyoyataka; na ni maahadiano yangu kuwa nitayaacha matendo yote yale yenye kukuasi wewe.

Ewe Mola wangu! Kwa hakika wewe watambua na kujua vyema kabisa kila nilichokitenda. Kwa hivyo, naomba unisamehe yale unayoyajua. Kwa uwezo wako unirejeshe kwa kile ukipendacho mno.

Ewe Mola wangu! Mimi nipo chini ya ushurutisho nisioukumbuka na baadhi ambayo nimeshakwisha sahau, lakini vyote hivyo vipo wazi mbele ya macho yako ambayo kamwe hayawezi kulala na mbele ya Ilm yako ambayo kamwe haisahau. Kwa hivyo naomba ufidie yanayostahiki kutoka kwangu. Ondoa mzigo wa yale (faradhi) juu yangu. Yafanye wepesi uzito wao kwa ajili yangu. Nihifadhi kwa kutorejelea tena karibu na hayo.

Ewe Mola wangu! Kwa hakika mimi siwezi kuwa mwanifu katikaTawba yangu isipokuwa msaada wako wa kunihifadhi.

Wala siwezi kujizuia na madhambi isipokuwa kwa uwezo wako.

Kwa hivyo, naomba uniimarishe mimi kwa nguvu ya kutosha na naomba unilinde kwa uhifadhi wako unaotakiwa.

Ewe Mola wangu! Kiumbe chochote kile kinapofanya Tawba yako na ambaye, katika ukimu yako iliyofichika, ni lazima atakiuka viapo vyake vya Tawba na atarejea katika madhambi na maovu yake, kwa hivyo nahitaji hifadhi yako dhidi ya kutokea kwa hayo.

Hivyo, ifanye Tawba yangu iwe ni majuto ambavyo stakuwa na haja ya kutubu tena - Tawba ambayo tafuta yale niliyokuwa nimeyatenda na usalama kwa yale yaliyosalia.

Ewe Mola wangu! Najitetea (kutaka radhi yako) mbele yako kwa ujahili wangu.

Naomba msamaha wako kwa matendo yangu maovu.

Kwa hivyo, naomba uniingize katika hifadhi zako.

Nifunike kwa funiko zako za usalama na hisani zako.

Natubia kwako kwa kila kitu ambacho kinapingana na Amri yako au ambacho kimepoteza mapenzi yako kwa kutokana na mafikirio ya moyo wangu, maono ya macho yangu na matamshi ya ulimi wangu kwa Tawba ambavyo kila kiungo cha mwili wangu kisalimike kutokana na adhabu zako na kuponea kwa khofu ya maumivu ya ghadhabu zako kwa mwenye kuasi.

Kwa hivyo, nihurumie, Ewe Mola wangu, kwa unyenyekevu wangu mbele yako.

Juu ya roho yangu ambayo inadunda midundo ya kishindo kwa sababu ya khofu yako na

Juu ya maungo ya mwili wangu ambayo yanatetemeka kwa hofu yako, kwa hakika, Ewe Mwenye kutunuku riziqi, madhambi yangu yameniweka mbele yako katika hali ya kudhalilika, ili kwamba nitakapobakia kimya, basi hakuna mwingine atakaye sema badala yangu.

Iwapo nitajiombea uteteo, kwani mimi ni mtu nisiyestahiki hivyo.

Ewe Mola wangu! Bariki Mtume Muhammad s.a.w.w.na ahali Bayt yake a.s., rehema zako zinitetee maovu yangu. Yageuze maovu yangu kwa msamaha wako. Usinilipe adhabu yako kwa yale maovu yangu.

Unitandazie juu yangu kwa uarimu wako.

Nifunike kwa pazia yako.

Unitendee yale ambayo bwana mwema amfanyiavyo mambo ya huruma kwa mtumwa wake asiye na uthamini, ambaye anaomba huruma yake au mtu tajiri anapomsaidia mbele yake kiumbe chenye mahitajio.

Ewe Mola wangu! Hapana mwingine wa kunsitiri isipokuwa wewe tu, kwa hivyo Utukufu wako lazima unihifadhi. Hapana mwingine yeyote wa kunitetea kwako wewe. Kwa hivyo, huruma yako lazima inisuhulishie mimi. Kwa hakika makosa yangu yameniogopesha kupita kiasi, hivyo msamaha wako lazima yameniogopesha kupita kiasi, hivyo msamaha wako lazima unihakikishie hivyo. Kwa chochote kile nilchokwisha kukisema si kutokana na ujahili wa matendo yangu maovu, wala si kwa usahilifu wa kile kilichotangulia, cha tabia zangu zinazolaumiwa bali yasikilizwe na mbingu zako, na yale yaliyomo na ardhi yako na yale yaliyo juu yake, yanisikilize yale nilyokuambia wewe katika hali ya majuto na masikitiko na kwa Tawba ambayo naombea usitiri, nikitegemea labda baadhi yako, kwa kupitia rehema zako, zinihurumie, kwa kutokana na hali yangu isiyo nzuri au udhaifu ule kwa ajili yangu labda naweza kupata dua yake inayostahili kukubaliwa kuliko maombi yangu au mateteo yaliyo na nguvu kuliko nijiteteavyo mimi na ambavyo inawekekana ikawa ni sababu ya kuokoka kwangu kutokana na ghadhabu zako na mafanikio ya ushindi wa idhini yako.

Ewe Mola wangu! Iwapo majuto na masikitiko yanatosheleza kwa Tawba mbele yako, basi mimi ni mjutaji sana baina ya wale wanaojuta na kusikitika. Iwap kuacha kutokutii wewe ni uongofu basi ni mwachaji mkubwa miongoni mwao. Iwapo kukuomba msamaha kunaondoa madhambi, basi mimi ni miongoni mwa wale wanaokuomba msamaha wako!

Ewe Mola wangu! Kama vile Tawba, umedhamiria kuzikubalia, umetutia moyo wa kusali na umetuahidi kujibu; hivyo wabariki Mtume Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake a.s.

Nikubalie Tawba yangu.

Usinirejeshe nyuma kwa kutopatiwa niliyoyaazimia kutoka rehema zako.

Kwa hakika wewe ni Mkuu wa mkubaliaji wa Tawba za wenye madhambi na mhurumiaji kwa wenye kupotoka ambao wanarejea kwako.

Ewe Mola! Wabariki Mtume Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake toharifu a.s. kama vile ulivyotuamrisha sisi.

Wabariki Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake a.s. kwa baraka ambazo zitatutetea kwako siku "ya kufufuliwa na siku ya Mahitajio."

Kwa hakika wewe tu ndiye ulie na uwezo juu ya kila kitu na kila kitu ni saheli kwako wewe."

47. Mwongozo wa Dua zizungumziazo Tawba katika sahifai sajjadiyyah:-

1:21-23; 9:1-2; 11:3; 12:5,7,10,12; 15:2,4; 16:33; 31:16-10; 31:14-16; 31:19-20; 31:22; 31:26; 32:15; 32:19,20; 34:3-4; 37:14; 38:3; 39:13; 40:5; 43:6; 45:9-11; 45:45; 45:52; 45:54;46:16; 47:69; 47:72-73; 47:76; 47:103; 47:86; 47:126; 48:7; 49:15,50; 51:8; 52:7;52:9;53:4.