rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

25. MOYO WA SHEITANI HUBABAIKA KWA ISTIGHFAAR ZA WATU

Iwapo mtu yeyote anataka kupigana na adui shetani, basi itambidi awe na silaha gani? Mtume Mtukufu s.a.w.w. anatuelezea amali mojawapo ambayo inaweza kumvunjia sheitani juhudi zake zote. Nayo ni

ISTIGHFAAR (kutubu) ambayo inamfukuzia mbali shetani. Je ni nani miononi mwetu ambaye hajawahi kumtii na kumfuata sheitani? Wingi wa wakati wetu wa magomvi huwa tunamtii sheitani, je hasira na ghadhabu zetu zisizo na msingi au kutokuwa na huruma, si vyote hivyo ni vishawishi vya shetani?

Njooni nyote tutubu madhambi yetu yaliyotangulia na tumtii Allah swt na tumsujudie kwa utiifu. Allah swt anasema: Sura an-Nisaa:69

"Hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu: Manabii, walio wa kweli (siddiqiina), na mashahidi na salihiina (walio katika haki), na watukufu ndio hao kama rafiki zao."(4:69)

Inawabidi wanawake wafuate maisha ya Bibi Fatema az-Zahra a.s., binti yake Mtume Mtukufu s.a.w.w. na vile vile wanaume wafuate maisha ya Sayyidina Ali a.s.

"Wanaume ambao si biashara wala kuuza kuliko wapotosha ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na kusimamiusha sala na kutoa Zaka: Wao waiongopa siku ambapo nyoyo na macho vitajinyonga kwauchungu." (24:37)

26. WENYE KUTUBU HAWATATOA USHAHIDI DHIDI YA MADHAMBI YAO.

Ni jambo la kusikitisha mno kuwa sisi na nyinyi tutasimamishwa kwa pamoja mbele ya Allah swt kwa ajili ya kutolewa uamuzi baina yetu kuhusu matendo yetu. Imam Jaafer as-Sadique a.s. katika Usuli Kafi, mlango wa TAWBA anatubashiria kuwa:

"Iwapo mtu atafanya Toba basi hilo jambo litambusuru siku ya Kiyama na wala halitapingwa na Malaika waandishi wa amali zetu. Na iwapo huyo mtu hakufanya TAWBA maishani mwake, basi ataambiwa aelezee hesabu yake kwa ukamilifu, ambapo kama yeye alifanya TAWBA maishani make, basi Malaika watasema 'Ewe Mola wetu! Huyu mtu alikuwa akitamka kila mara Astaghfurullah na alikuwa akiomba TAWBA kwako!"

Allah swt anatuambia katika Quran Tukufu sura Furqaan Aya ya 70:-

..Hao (waliotubia) ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema.......'(25:70)

Midomo ya watu wengine itabakia kimya wakati wa kuulizwa maswali na majibu kwani hataweza kujitetea, lakini midomo ya Muumin haitabakia kimya kwani daima husema: "Lailaha Illallah haqqan haqqa ta'abbudan wa riqqan Iimaanan wa tasdiiqan.'

Mwenyezi Mungu anatuambia katika sura Yaasin aya 65:

..Katika siku hiyo sisi tutaweka mihuri (tutaviziba) juu ya midomo yao ..... .(36:65)

Watu ambao daima walikuwa wakisema uongo na upotofu katika maisha yao,basi siku ya Kiyama ndimi zao zitakuwa bubu kwani watashindwa kutamka lolote na hapo viungo vyao vya mwili wao vitasema na kutoa ushahidi dhidi yao. Allah swt atujaalie tawfiqi (uwezo) wa kufanya Toba kabla ya kufariki kwetu! Aamin.

27. VIUNGO VYA MWILI VITATOA USHAHIDI DHIDI YA MADHAMBI YETU.

Baadhi ya Maulamaa wameelezea ushahidi utakavyokuwa wakati wa Qiyama ambapo sehemu zote na viungo vyote vya mtu vitatoa ushahidi.Allah swt anatuambia katika sura ar-Rahmaan, Aya ya 41:

"Wenye hatia (wenye madhambi) watatambulikana kwa alama zao, na wao watakamatwa kwa nywele za utosi wao na miguu yao." (55:41)

Mfano wake ni kwamba atakapotokea mtu ulimi wake umening'inia nje ya mdomo wake huku umebanwa na meno yake ya juu na chini na mdomoni mwake kunatoka miele ya moto, na huku damu na usaha unadondoka, basi atajulikana kuwa huyo alikuwa ni aalim (aliyepata elimu) aliyekuwa akizungumza maneno yenye nasiha kubwa kubwa bila ya yeye kuyatekeleza aliyokuwa akiyasema na vile vile alikuwa ni msema uongo. Vile vile ataonekana mtu mwenye tumbo kubwa mno kiasi kwamba hawezi hata kutembea, basi huyo atajulikana kuwa ni mwenye kupokea ribaa na kuifanyia biashara yake.

Allah swt anatuambia katika sura al- Baqarah, Aya ya 275:

Wale wanaokula ribaa, hawataweza simama (siku ya kiyama) ila kama yule aliyesimama ambaye ametunduwazwa na mguso wa shetani." (2:275)

Udhahiri wa mtu siku ya kiyama utaonyesha madhambi aliyokuwa akitenda akiwa humu duniani. Iwapo kipaji chake kitakuwa na nuru basi atajulikana kuwa huyu alikuwa ni mfanya sujuda nyingi wakati akiwa humu duniani. Wenye kusujudu watakuwa wakitokwa na miale ya nuru kutoka vipajini mwao, au yatatoa ushahidi wa kutenda kwao matendo yao katika mikono yao ya kulia, basi hayo yatatoa ushahidi wa kutenda kwao matendo mema.

Allah swt anatuambia katika Quran, sura Yaasin, Aya ya 65:

ituzungumzie mikono yao na itoe ushahidi miguu yao ..... (36:65)

Maulamaa wanasema kuwa ushahidi wao utatokana na viungo vyao na ushahidi huo (Ar-Rahmaan: 41) utakuwa,lakini ushahidi thabiti utakuwa ni ule ambao utatolewa na viungo vyao -mikono na miguu itasema. Na uthibitisho wake wa wazi ni Aya hii:

Na wao wataziambia ngozi zao: "Kwa nini mnashuhudia dhidi yetu?" Hizo zitajibu: " Ametufanya Mwenyezi Mungu tuseme, ambaye amekifanya kila kitu kiseme........." (41:21)

Wakati sehemu zote na viungo vyote vya mtu vitakapoanza kusema kila kitu bila ya kuficha, hapo huyo mtu masikini atasema,"Je kwa nini mnazungumza dhidi yetu?" Basi hapo hivyo viungo vitasema: "Sisi tumejaaliwa uwezo na Allah swt wa kuzungumza kama vile vilivyo jaaliwa vitu vyote viweze kuzungumza."