rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

21. TAWBA NI FARADHI BAADA YA KILA DHAMBI

Katika faradhi mojawapo za Muislamu ni kutubia mara moja pala anapotenda madhambi na hivyo ndivyo ilivyo wajibu. Iwapo atamwona mtu mwingine akitenda madhambi, basi amshawishi kutubu. Mfano, unapoketi mahala fulani na ukaona kuwa mtu mmoja anamtania na kumfanyia masikhara mtu mwingine basi ni faradhi kwako wewe kumkataza huyo wa kwanza aache utani wake dhidi ya mtu wa jpili na papo hapo atubu, na vivyo hivyo ni faradhi juu ya mtu huyo wa kwanza kukubali nasaha yako na atubu papo hapo na iwapo hatatubia basi uendelee kumkumbusha kila mara umnasihi zaidi.Kwani ni faradhi kwako wewe kumnasihi na kwake yeye kutekeleza. Iwap yeye hatakubali basi Aya hii itakuwa ikimzungumzia.

Quran inatuambia "Dhalimu ni nani?" Basi dhalim ni yule mtu ambaye amekwisha tenda madhambi na asiye tubu mbele ya Allah swt na wala asimwombe Allahs swt msamaha wa makosa yake.

22. TAWBA NI NURU YA MATUMAINI

"Ewe uliyekwisha tenda madhambi! Usikate tamaa kwa rehema za Allahs swt, rejeeni katika njia yake, na hataki muendelee kutenda madhambi vile mupendavyo na mutakavyo - tukidhani kuwa atatusamehe tu! La sivyo hivyo! Makusudi ya kutokata tamaa ni kwa wale waliokwisha tenda madhambi wakidhani kuwa hawana la kufanya kusamehewa hivyo wakaendelea na maasi yao, bali inawabidi waitambuw na waombe TAWBA na msamaha wa Allah swt. Hivyo wajue kuwa pale wanapotenda dhambi, waombe Toba mara moja. Inawezekana Allah swt akazikubalia TAWBA zetu.

23. KISA CHA KIJANA MWENYE MADHAMBI.

Ma'adh anasema: "Siku moja nilikuwa nkijiandaa kwenda kwa Mtume s.a.w.w. , na mara nikamwona kijana mmoja akilia mno, basi hapo nilimwuliza sababu ya kilio chake hicho. Huyo kijana alinibu kuwa yeye ni mwenye dhambi kubwa mno. Basi hapo nilimwambia aje pamoja nami kwa Mtume s.a.w.w. ili amwombee msamaha kwa Allah swt. Hapo huyo kijana alisema kuwa alikuwa akiona aibu kuja mbele ya Mtume s.a.w.w. kwa sababu ya dhambi zake." Hapo Ma'adh aliendelea na safari yake hadi kwa Mtume s.a.w.w. na kumwelezea yale yaliyotokea. Basi Mtume s.a.w.w.alimwambia akamlete yule kijana. Alipofikambele ya Mtume s.a.w.w. aliulizw, 'Je umekuwaje, walia kwa nini? Hapo huyo kijana akasema, "Ewe Mtume wa Allah swt! Dhambi langu ni kubwa mno!" Hapo Mtume s.a.w.w.aliendelea kumwuliza, "Je kosa lako kubwa au mbingu? " Akajibu, 'Kosa langu!' 'Je kubwa au dunia nzima? Akajibu, kosa langu! Je kosa lako kubwa au msamaha wake Allah swt? Hapo huyo kijana akasita na hatimaye kukubali kuwa 'Msamaha wa Allah swt ni mkubwa! Bassi hapo Mtume s.a.w.w. alimwuliza, sasa niambie kosa lako. Huyo kijana akaanza kusema: "Ewe Mtume wa Allah swt! Palitikea kufariki kwa binti mmoja mzuri mno wa kabila la ansaar, na mimi nilikwenda usiku ule kulifukua kaburi ili kutaka kuiba sanda aliyokuwa amevishwa huyo maiti, shetani alinighalibu na kunifanya nikatenda tendo la kinyama kwa maiti huyo, binti aliyekuwa uchi mbele yangu. Hapo ndipo maiti hiyo ilipota sauti ya masikitiko na kunilaani kwa kuniambia kuwa Allah sw ataniingiza motoni na kuniunguza humo kuteketea. Ewe mtume wa allah swt kwahakika, baada ya matamshi hayo ya maiti huyo, mimi nimekosa furaha ya kila aina na nimeingiwa na woga na nadhani nitaweza kuangamia katika hali kama hii iwapo itaendelea kunisumbua.Hapo mtume s.a.w.w. alimwambia huyo kijana:"Ondoka haraka mbele yangu kwani inawezekana moto wa Jahannam ukanikumba nami pia." Je kwa nini Mtume s.a.w.w. alisema hivyo? kwa sababu dhambi lilikuwa kubwa mno!

Kwa mujibu wa riwaya, kijana huyo baada ya kuambiwa hivyo, aliondika akiwa amesikitika mno na kuelekea katika milima ya mji wa madina, huko alikaa kwa muda wa siku arobaini akiwa akilia na kuomba Toba kwa Allah swt. Baada ya siku arobaini kupita, alisema: "Ewe Allah swt! Iwapo umeshakwisha kuikubalia Toba yangu, basi naomba unijulishe kwa kumpitia Mtume wako. Na iwapo bado haujaikubali Toba yangu, basi naomba uniteremshie miale ya moto kutoka mbinguni ili inichome na kuniunguza ili niteketee kabisa!"

Basi hapo iliteremka Aya ya 134 - 135 ya sura Ali Imraan (3):

"Na wale ambao, wanapofanya tendo la kuaibisha au kudhulumu nafsi zao,wakamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani awasamehee madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? Na ambao hawabakii (kwa kukusudia) katika yale waliyoyafanya maovu hali walikuwa wakiyajua hayo,"

Na kwa hao, malipo yao ni msamaha kutoka Mola wao na bustani chini yake kunapita mito, watamokaa milele; Na utukufu ni malipo ya wale watendao haki." (3:134-13)

Hapo Mtume s.a.w.w aliwauliza masahaba wake pale alipo huyo kijana mwasi wa Allah swt. Alijibiwa kuwa yupo katika mapango fulani ya milimani akiwa katika hali ya kufanya Toba na kuomba Allah swt msamaha wa dhambi yake. Mtume s.a.w.w. alimwendea huyo kijana na kumbashiria juu ya kukubaliwa kwa Toba yake.

Tuzingatie kuwa:-

Huyo kijana alijitenga na wengine akilia huko pangoni kwa muda wa siku arobaini akiomba Toba kwa dhati, ndipo alipokubaliwa Toba yake.

Sisi tusijipotoshe kwa kudhani kuwa tutakaposema mara tatu Astaghfirullah' basi Allah swt atatusamehe madhambi yetu na kuikubalia Toba yetu,

24.TOBA INAWEZA KUKUBALIWA KWA KUMTAWASULI IMAM HUSSEIN A.S.

Sisi huwa daima tunaomba, "Ewe Mola wetu! Tujaalie Tawfiqi ya Toba ili tuweze kusamehewa madhambi yetu na kiza cha moyo wetu kuondoka."

Wakati tuombapo, huwa hatujui iwapo dua yetu ni Tawbat Nasuuha au imekubalika kutufanya tusamehewe madhambi yetu yote. Hapo hapana haja ya kuhangaika kwani inatubidi kulia sana na vile vile kumtawasuli Imam Husseyn a.s. kwa kuomba msamaha wa madhambi yetu. Ipo riwaya isemayo kuwa,moyo wowote ule ulio katika hali ya kuhuzunika kwa mateso yaliyompata Imam Husseyn a.s na ahali yake na wafuasi wake, basi Allah swt huirehemu kwa baraka za Imam Husseyn a.s Imam Jaafer as-Sadiq a.s amesema:"Atakayemkumbuka Imam Husseyn a.s. na kutokwa na machozi walau kidogo sana, basi atapewa malipo yake kutoka kwa Allah swt na ataridhiwa Jannati (peponi)! (Thawabul a'amaal Na. 631 aya ya 2) Lakini kumlilia Imam Huseini a.s. peke yake haimaanishi kuwa ni uokovu, bali itatubidi kujibu maswali juu ya haki za watu,madhambi makuu hadi hapo tutakaponuia kwa moyo thabiti wa kuacha madhambi na kutenda mema ndipo tufanye Toba kamilifu.Baadhi ya riwaya zinadema kuwa madhambi yote yatasamehewa ila madhambi makuu. Madhambi hayo makuu kamwe hayataweza kusamehewa ila kwa Toba kamilifu.

Na hii ndiyo maana Allah swt amechukua ahadi ya TAWBA tu:

Kwa hakika, Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote kwa pamoja (Suraaz-Zumar,39:53)Na rejeeni kwa Mola wenu...(39:54)

Kwa hivyo kutokana na tawassul au Shifa'a kunaweza kusamehewa madhambi ili mtu asiseme kuwa yeye anayo madhambi mengi na hivyo ataingia Motoni tu, hivyo inambidi atambue wazi wazi kuwa kuomba msaada wa Imam Husseyn a.s.kutamfanya kusamehewa madhambi yake na hivyo inambidi awe mwenye kutegemea msamaha wake Allah swt.

Inambidi kila mtu ajiepushe na mapotoshi ya shetani kwa kila hali na hivyo tujitahidi kufanya Toba. Iwapo baada ya juhudi zetu hizi kutabakia kasoro zozote zile, basi Allah swt atatusamehe kwa msaada wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Ahali yake watukufu a.s.

Hapa nitapendekeza kusomwa kitabu kilichoandikwa katika lugha ya Kiswahili: 'UPOTOFU WA MADHEHEBU YA 'WAHHABI' NA HATARI ZAKE.' Kilichoandikwa na Khalifa M. Hamisi Mohammad na kinaweza kupatikana kwa anwani hii: Sherman Islamic Book Stall P.O.Box 5444 Dar es Salaam Tanzania E.A.

Katika kitabu hicho utaweza kusoma mengi pamoja na: Maana ya Wasila, Itsighatha (kuomba msaada kwa viumbe): Tawasul; kumzuru Mtume s.a.w.w. Madina; Mtume s.a.w.w. yu hai kaburini mwake; kuomba 'SHAFAA' (yaani kuombewa) siyo Shirki.

Vile vile ni muhimu kukisoma kitabu kiitwacho uchunguzi juu ya Uwahhabi kilichotolewa na Ahlul Bayt (a.s.) Assembly of Tanzania P.O.Box 75215 Dar Es Salaam – Tanzania. Kwa hakika kitabu hiki kinachambua masuala mengi mno na kwa undani.

Ama kuhusu Asili na kuenea kwa Uwahhabi jipatie kitabu hicho uweze kuelewa kwa undani kuhusu historia ya Mawahhabi.

Kwa hakika vipo vitabu vingi mno vinavyozungumzia upotoshi na mazushi ya Mawahhabi. Wasiliana na Bilal Muslim Mission of Tanzania P.O.Box 20033 DSM.

Ningalijaribu kuyadondoa machache hapa lakini itahitaji nafasi kubwa na si rahisi kuchukua machache kuyaacha mengi yaliyomo.