rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

TUSIWAITE WATU KWA MAJINA MABAYA AU MAJINA YA UTANI.

Tusiwe na tabia ya kuwaita watu kwa majina mabaya na yale yaliyokuwa ya utani au mzaha. Mfano, iwapo mtu mmoja alikuwa 'Myahudi' hapo awali na baadaye akawa Mwislamu, basi haifai kamwe kumwita 'ewe mwana wa Kiyahudi.' Vile vile usimwite mtu 'mlevi' wakati amekwisha kufanya toba.

Ni lazima kabisa kuwaita Waislamu kwa majina yaliyo bora kabisa. Ni haramu kumwita Muumin kwa jina au sifa mbaya. Mfano "Ewe mfupi kama nyundo! au ewe ''Mfasiqi' ni jina baya kabisa (kwa yeyote) baada ya yeye kuwa Muislamu.'''

Huyu mtu kwa sasa anayo imani na anatamka 'La ilaha illallah' Ole wenu iwapo mutamwita kwa kumnasibisha na kufuru. Laana ya Allah swt huwa juu ya watu wale wanaowasema waislamu kuwa ni makafiri!

Kumwita mtu au kumwambia mtu kwa jina la fasiq ni haramu, bali majina ya kujitungia ya kila aina pia ni haramu ambayo humhuzunisha kila asikiaye. Popote pale anapoitwa Mwislamu ni lazima aitwe kwa majina mema na heshima sana. Ipo rewaya mojawapo inyosema kuwa alitikezea mtu mmoja mbele ya Imam a.s. na Imam alikuwa halijui jina lake, hivyo alimwita "Ewe uliye na bahati njema, je haujambo?

Ni lazima kabisa kuwaita Waislamu kwa majina yaliyo borakabisa. Ni haramu kumwita Muumin kwa jina au sifa mbaya. Mfano "Ewe mfupi kama nyundo! au ewe mrefu kama mnazi, au ewe kiziwi, ewe kipofu n.k. Hakika katika zama zetu hizi tabia hii imeshamiri mno, Allah swt anatuambia katika Sura Hujurat Aya 11:

"Enyi mlioamini! Wasije watu (kikundi) wakawachekea (kikundi kingine cha ) watu (kwa dharau) ambao huenda wakawa ni bora kuliko wao; wala wasije wanawake wakawacheka wanawake wengineo ambao huenda wakawa bora kuliko wao na wala msitafutiane makosa miongoni mwenu na wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli); Mfasiqi ni jina baya kabisa (kwa mtu yeyote) baada ya yeye kuwa Mwislamu; na yeyote yule asiyetubu (kutubia kwa tabia yake hiyo),basi hao ndio walio wadhalimu." (49:11)