rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

19. TUOMBE TAWBA KWA MADHAMBI TULIYOKWISHA TENDA

Haitupasi kamwe kumdharau mtu yeyote wala tusimfanyie masihara wala tusimdhalilishe kwani hatujui iwapo huyo mtu yu mwema nyuma ya pazia za macho zetu. Bali inatubidi tuseme, labda yeye anazo tabia njema kuliko tabia zangu ambazo mimi sinazo, inawezekana yeye anazo heshima zaidi mbele ya Allah swt. Vile vile inawezekana kuwa mambo yake usiyoyapendelea wewe yakawa ni mema:

Huenda wakawa bora kuliko wao.

Katika maisha yetu, yapo maovu mengi mno, kuwadhania watu visivyo (kwa mabaya) na vile vile kumshuku Allah swt. Leo ni siku ya Ijumaa na ni tarehe 15 ya mwezi wa Ramadhani (hiyo ni siku ambayo Shahid Mihrabu Ayatullah Dastaghib Shirazi, alikuwa akiwahutubia waumini) ambavyo vyote ni tukufu, hivyo sisi sote (wake kwa waume) tulie sana katika kufanya TAWBA ya madhambi yetu yote na vile vile tule kiapo thabiti cha kutorudia kutenda madhambi maishani mwetu. Leo ni muhula wa TAWBA, na tuombe TAWBA tu, mauti ipo inatupigia hodi petu. Insha Allah, madhambi yetu yatasamehewa na pale tutakapokwenda mbinguni hatutakuwa na mzigo mzito tuliojitwisha wa madhambi.

Katika masaa ishirini na manne (24) huwa tunatumia masaa mengi katika kutenda madhambi, hata wakati wa kupumua pumzi pia huwa tunatenda madhambi. Hatuelewi hali yetu itakavyokuwa kwani huwa tunamshuku hata Allah swt na viumbe vyake, uwezo wa kupangiwa na kupanga maamuru ya mwanadamu. (Qadhaa wa Qadr), kwa hakika sisi hatumtakidi Allah swt kwa kukamilifu na hili ndilo dhambi kuu kabisa. Njooni tujumuike kuomba toba ya madhambi yetu yaliyopita na tuombe kuepukana nayo na tuseme kwa moyo wetu wote kuwa kuanzia sasa sisi hatutashuku matendo ya Allah swt na tujisalimishe mbele ya hukumu zake kwa kikamilifu.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unayo majina mengi sana, na jina mojawapo lililo mashuhuri ni 'mwezi wa Toba.' As shaikh as-Sadduq A.R. ameelezea kuwa Mtume s.a.w.w. amesema:

"Mwenye kuupata (aliyekuwa hai katika) Mwezi wa Ramadhani, na asisamehewe (madhambi yake katika mwezi) humo, basi huyo hana msamaha wa Allah."

Hadithi hiyo inatuelezea wazi wazi kuwa iwapo mtu hatasamehewa madhambi yake katika mwezi huu wa Ramadhani, basi hakuna mategemeo mengineyo tena ya kupatiwa msamaha. Katika usiku na mchana wa mwezi huu mtukufu huteremka rehema na baraka za Allah swt. Leo ni Ijumaa na tena ni siku ya kumi na tano ya mwezi huu Mtukufu, ni siku ambayo alimozaliwa Imam Hassan a.s. Tufanye Toba kwa wasila wa Imam a.s. aliyeuawa kwa kupewa sumu. Tusome Duaa za Istighfaar za Imam Zaynul Aabediin a.s. Sinabudi kuwaleteeni machache tu:

"Ewe Allah swt! Mimi nakuomba msamaha (toba) mbele yako kwa madhambi yangu yote yaliyo madogo kwa makubwa, yaliyo dhahiri na batini na yale yote yaliyokwisha pita."