rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

18.TUYATEKETEZE MADHAMBI YETU KWA TAWBA

Allah swt anatuambia katika Sura Hujuraat, aya 11:-

Na wasiotubu, basi hao ndio madhalimu. (49:11)

Sehemu hii ya mwisho wa aya hii inatubashiria na kutuitia katika TAWBA hivyo tuitikie mwito huo na tufanye TAWBA.

Allamah Iqbal anasema:"Matendo ndiyo yafanyayo maisha ya mtu yawe ya Peponi au Motoni, huyu kiumbe si wa peponi wala motoni alipoumbwa."

Enyi Waislamu! Njooni nyote mliokwisha yatumbukiza maisha yenu katika madhambi. Allah swt ametuambia sisi (49:11) tusiitane kwa majina ya utani na majina mabaya, na sisi hatukuyafuata hayo, je ni nani aliye na utulivu moyoni mwao kuwa wao hawakuwatazama watu wengine kwa mitazamo ya dharau na wala hawakuwaita watu wengine kwa majina ya utani na ya kubughudhi? Basi iwapo hiyo ndiyo hali yetu basi tuombe: "Ewe Allah swt! Kwa utukufu wa mwezi wa Ramadhani, kwa madhambi yote yaliyotendwa na ulimi wangu, ewe Mola wangu! Naomba ihsani zako juu yangu, kwanza, unisamehe! Pili, wale wote walio na haki zao juu yangu naomba waniwie radhi kwani inawezekana wakanijia siku ya kiyama na kunikaba shingo huku wakinidai kuwa, je wakumbuka wakati fulani ulituita kwa matani au ulitunyang'anya haki zetu? Ewe Mola wangu! Nakuomba kwa utukufu wako, unisamehe iwapo nimemtesa au kumtania mtu yeyote yule katika maisha yangu na umfanye huyo muumin aniwie radhi juu yangu. Ewe Mola wangu!"

Tuelewe waziwazi kuwa Allah swt ni Mkarimu mno na hazina yake haipungui, iwapo hatutatubu, basi sisi ni wadhalimu, kwani yeye daima ametuwekea wazi milango ya rehema. Iwapo mlaji ni mvivu na akabakia njaa, basi mwenye chakula ana kosa gani?

Wale wasiotubu ni madhalimu! Njooni iwapo sisi hatukumbuki chochote (tulichokitenda) basi Allah swt anakumbuka vyote, iwapo hatujui, basi matendo yetu yote yameshaandikwa katika amali zetu. "Ewe Mola wangu! Iwapo nimetamka kwa ulimi wangu chochote kile chenye uchungu kwa muminiin au nimepoteza haki za Muumini au nimemkashifu, basi naomba msamaha wako kamilifu!"

Njooni tujitoe katika mipaka ya dhuluma na upotofu, na tusome dua ya Imam Zainul Aabediin a.s.:

(Dua hii imechapishwa kwa ukamilifu mwishoni)

Ewe Allah swt! Natubia kwako kwa kila kitu ambacho kinapingana na Amri yako au ambacho kimepoteza mapenzi yako kwa kutokana na mafikirio ya moyo wangu, maono ya macho yangu na matamshi ya ulimi wnagu, kwa TAWBA kutokana na adhabu zako na kuponea kwa khofu ya maumivu ya ghadhabu zako kwa walio asi..........."

Mtume Mtukufu Muhammad s.a.w.w. amesema: "Iwapo mtu yeyote atamdhalilisha au kumkashifu mtu yeyote yule, basi Allah swt atamkasirikia mno." Hatujui kila kitakachowafikia wale waliomtesa Imam Husseyn a.s. na wafuasi wake, mateso ya kila aina. Wao walimwambia Imam Husseyn a.s akiwa katika kiu kikali cha siku tatu:"Ewe Hussein!Hebu tazama vile mto Furati (Euphrate) unavyopiga mawimbi, lakini hatutakupatia hata tone moja la maji kwa ajili yako au wafuasi wako."

Tujue kuwa Imam Husseyn a.s. alikuwa si pekee hapo Karbala (Iraq) bali alikuwa pamoja na wanwake na watoto wadogo wadogo na jamaa zake.