rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

14. ISTIGHFAAR, KURUDIA TAWBA NA ALFAJIRI:

(d) Kusoma Istighfaar:

Kuhusu TAWBA inatubidi tusome sana Duaa zilizofundishwa na Mtume s.a.w.w.na Maimamu a.s. Khususan Sahifai Sajjadiyyah au Sahifai Kaamila (Dua Na. 31 ipo imewekwa humu mwishoni juu ya TAWBA) na asome 'Munajaati Khamsatashara (munajaat kumi na tano) za Imam Ali a.s. katika Mafatihul Jinaan (funguo za Peponi). Katika duaa hizo tutaona vile TAWBA inavyoombwa na vile tunavyoweza kujihisi kimoyo wakati tuzisomapo.

(e) Kurudia TAWBA na Istighfar:

Imam Jaafer as-Sadique a.s. amesema:

"Mtume s.a.w.w. alikuwa akitubu kila siku mara sabini, ilhali yeye alikuwa hana madhambi."

(Wasail, Kitabu Jihad, mlango 92. uk. 367)

Kwa mtu atakaye ongeza zaidi TAWBA , basi siku ya Kiyama matendo yake mema yatazidi kupendeza. (usuli Kafi. Kitabu cha Dua na Istighfaar).

Imam Ar-Ridhaa a.s amesema:

"Mfano wa Istighfaar ni ule wa majani ya mti, ambayo hutoa sauti kwa sababu ya upepo, kwamba mtu atakuwa amemfanyia Allah swt masihara (utani) kwani huku ameomba TAWBA wakati bado yupo ameyashikilia madhambi."

(Ulsuli Kafi, Kitabu Duaa, mlango wa Istighfaar).

Imam Jaafer as-Sadique a.s. amesema kuwa Mtume s.a.w.w. hakuondoka katika kikao hata kikiwa kidogo kiasi gani, ila amefanya Istighfaar mara ishirini na tano.

(Usuli Kafi, Kitabu Dua, mlango wa Istighfaar).

Ipo riwaya nyingine isemayo kuwa Mtume s.a.w.w. alikuwa akitamka 'astaghfurullah' mara sabini na 'Atubu Ilayhi' mara sabini.

Sayyid bin Taus, ameandika katika kitabu chake 'Nahjul ad-da'awaat' kuwa imepokelewa riwaya kutoka kwa Mtume s.a.w.w. kuwa "Apatwapo mtu na shida na dhiki, basi asome mara elfu thelathini: "Astaghfirullah wa Atub Illayhi.” Kwa hakika Allah swt atamwondolea shida na dhiki aliyonayo. Riwaya inaelezea kuwa hivyo imeshajaribiwa na ni yenye manufaa sana.

(f) Wakati wa alfajiri ni wakati bora kwa ajili ya Istighfaar:

Wakati wowote ni wenye manufaa sana kwa ajili ya TAWBA, lakini wakati wa Sahar (sehemu ya mwisho wa usiku hadi alfajiri ) huwa na athari ya ajabu kwa ajili ya TAWBA yaani madhambi yake yote yatasamehewa kwa pamoja.

Qurani inatuambia katika Sura ad-Dhaariyaat, Aya 17 na 18:

Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.Na wakiomba maghufira, (msamaha) nyakati za kabla ya alfajiri. (51:17-18)

Vile vile katika sura Ali Imraan, Aya 17:

.....na waombao maghufira saa za kabla ya alfajiri. (3:17)

Imam Ali a.s. amesema:

Allah swt anapotaka kuwateremshia adhabu watu wa ardhini, husema: "Iwapo wasingekuwa wale wanaonitukuza, na wanao imarisha na kudumisha misikiti yangu na ambao wanafanya istighfaar wakati wa alfajiri, kwa hakika ningewateremshia adhabu yangu."

(Wasail ash-Shia, Kitabu Jihad, mlango 94, uk. 374)

Mtukufu Luqman alikuwa akimwambia mwanamke: "Ewe mwanangu mpenzi! Angalia kuku asije akawa mbora kuliko wewe,kwani yeye akaamka alfajiri na kufanya Istighfaar, wakati ambapo wewe bado umelala!" (Mustadrakal- Wasail, katika Wisaya Laqman).

Zipo Hadithi na riwaya nyingi zizungumziazo fadhila za kukesha alfajiri.

Katika Qunut ya 'Witri (sala za Tahajjud au layl) ni kusema mara sabini 'Astaghfirullah' na kusema 'Al- afwu' mara mia tatu. Allah amemjaalia Mtume wetu Muhammad s.a.w.w. daraja la Mahmuud na hutimiza kila matamanio moyoni mwetu wakati wa alfajiri.

Kwa ufupi, wote wale waliotukuzwa na kupandishwa vyeo mbele ya Allah swt ni kwa sababu ya kukesha wakati wa alfajiri.

Kwa ufupi, wote wale waliotukuzwa na kupandishwa vyeo mbele ya Allah swt ni kwa sababu ya kukesha wakati wa alfajiri.