rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

10.HALI YA TAWBA KAMILIFU NA SUNNA ZAKE:

Kama ilivyokwisha elezwa kuwa TAWBA ya hakika ni ile ambayo inayotokana na hisia tokea moyoni mwa mtu na kumfanya kujutia matendo yake aliyokwisha tenda.Vile itakavyokuwa masikitiko na majuto ya mtu, ndivyo TAWBA yake itakavyokuwa na ukaribu wa kutakabaliwa. Ikiwa mtu atahisabu dhambi zake kuwa ni kubwa sana basi ndivyo hisia zake za masikitiko na majuto yatakavyokuwa makubwa. Mfano wake ni kama ule wa mtu ambaye amekusanya mali yake yote aliyoichuma maishani mwake na kuchoma kwa moto.

Kwa hakika atajuta sana kwa hasara hiyo ya daima.Matatizo yake yataongezeka na hivyo majuto na masikitiko yake pia yataongezeka. Hivyo ndivyo ilivyo hali ya mtenda madhambi ambaye anajichomea mwenyewe na wala hakuna mwingine wa kumsaidia kwani moto huo upo umeshawashwa na Allah swt kwa uwezo wake na ghadhabu zake. Imam Ali (a.s.) amesema:"Haya ni matikeo ambayo haiwezi kustahimili ardhi wala mbingu, na joto lake si sawa na joto la humu duniani."

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:"Iwapo mtu atatolewa kutoka Jahannam na kuwekwa katika tanuru lolote liwakalo humu duniani, basi humo ataishi kwa mustarehe kabisa kwa sababu kuungua kwa moto wa duniani si jambo la mushkeli, lakini hatuwezi kuustahimili moto wa Jahannam."