rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

9. DARJA ZA TAWBA

Mbele ya Allah swt, TAWBA ni kule kunapomfanya mtu ajirudi (kutoka maasi). Hivyo wafanyao TAWBA ni wa aina zifuatazo:

1.Kurudia Imani kutoka kufuru,yakini kutoka shaka, kuelekea utoshe

lezi kuacha kila akida za ubatili na kuingia katika haki.

2. Kuacha maasi na kuelekea katika utiifu na utekelezaji.

3. Kutoka katika maasi kuingia katika maarifa ya Allah swt na baada

ya kupata maarifa kuwepo na ongezeko katika ibada.Na kama

alikuwa ameghafilika, basi kuwepo na ongezeko la dhikiri. Nahivyo

inambidi achukie kila aina ya dhuluma na badala yake apendelee

uaminifu na utiifu.

Kwa mujibu wa vipengere hivyo hapo juu, imetuwia wazi kuwa TAWBA ni jambo lililo la lazima kwa kila mwanadamu kwa sababu inambidi awe katika hali ya kutokuwa na kulemewa na mzigo wowote wa madhambi.Na hii ndiyo hali ya maarifa na ibada ambapo mwanadamu huweza kujipatia daraja la juu mbele ya Allah swt.Ikiwa mwanadamu atajitahidi kwa kiasi gani kwa kujipatia maarifa, ibada na ushukuru, lakini bado tu hajaweza kujipatia maarifa kama inavyompasa. Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa mpenzi wa viumbe vyote, anasema: “Ewe Mola wangu! sikuweza kukujua vile ilivyokuwa ikinipasa kukujua na vile ilivyokuwa ikinipasa kufanya ibada yako, kiasi hicho sikuweza kukifanya!" Hayo ndiyo maneno ya Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa katika daraja la juu kabisa mbele ya Allah swt na mfanya ibada nyingi mno, mtoa shukurani mno, hata hivyo anaonyesha vile alivyokuwa akijihisi mbele ya Allah swt.Mtume s.a.w.w. alikuwa akijiepusha hata na vitu vilivyo karahishwa (makruuh) katika sheria na vile vile alikuwa akijiepusha na vilivyokuwa mubah (matendo yasiyo na madhambi wala thawabu).Alikuwa mbora katika matendo mema. Mtume s.a.w.w. alikuwa amekamilika katika uwema na ucha Mungu.Amenakiliwa akisema:"Mimi huwa nasema 'Astaghfirullah' mara sabini kila siku (pasi na kifani)!"