rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

6. JE' TAWBATAN - NASUHA' NI IPI?

Katika kuisherehesha al-Kafi, Allamah Majlisi (A.R.) anawanakili mufassirina:

1.Kutubu kwa ajili ya furaha ya Allah swt kwa kujitakasa kuwa

khalisi, yaani kutofanya TAWBA kwa kuwa na khofu ya Jahannam

(motoni) au kwa tamaa ya Janati (peponi). Badala yake kuhuzunika

na kusikitika kwa matendo tuliyokwisha tenda na vile vile tujiulize

'Je, kwa nini nimefanya hivyo?' Muhaqqiq Tusi (A.R.) katika Tajiri

al-Kalaam anasema kuwa iwapo mtu atajuta na kujiepusha na

madhambi kwa khofu ya Jahannam, basi hiyo haitakuwa TAWBA!

2.Tufanye TAWBA kiasi kwamba wengine watuonapo wapate

fundisho, yaani tujitakasishe kwa TAWBA hadi mtu mwingine

mwenye madhambi atuonapo, naye ashawishike kufanya TAWBA au

tuwe ni watu wa kutoa nasiha kwa wengineo na vile vile mara kwa

mara tusijumuike pamoja na kundi la wenye madhambi duniani na

akhera.

3. Nasiha-khayyat yaani mtu aionaye dini yake inachanika basi aitu

mie TAWBA kama sindano ya kushonea machaniko hayo. Wafanyao

TAWBA pia wamekuwa wakisemwa ni watu walio miongoni mwa

Awliya- i-Allah swt.

4. Kila mwenye kufanya TAWBA, lazima awe na sifa za Nasuha yaani

mtu ajisihi mwenyewe kwa nia khalisi na kwa ukamilifu na hivyo

azimalize athari zote za madhambi yake na awe ni mwenye ridhaa

na kujipatia nuru ya imani na awe mwenye kutenda matendo mema

daima badala ya kutenda maovu hata yawe madogo kiasi gani.

Mwanachuoni mmoja mkongwe aeleza kuwa haitoshi kuufuta moshi mweusi uliotanda moyoni mwetu, bali inatubidi tuusugue, kama vile mtu anavyosugua chuma kwa ajili ya kutoa kutu iliyo juu yake. Hivi ndivyo tunavyopaswa kuangamiza mabaki ya maovu na kuanza kung'ara kwa nuru moyoni mwetu, kwani madhambi tuliyokwisha tenda yametia kiza nzito juu ya nyoyo zetu. Kwa hivyo inatubidi tujitakase kwa njia ya utiifu na ibada.

Kila tutakavyokuwa tukiongeza ibada zetu ndivyo moyo wetu utakuwa ukiingiwa na nuru. Kila mfanya TAWBA inambidi aweke madhambi yake mbele yake wakati wa kufanya TAWBA ili awe akitubu moja baada ya jingine bila ya kubakiza lolote kati ya maovu yetu tuliyoyatenda hapo awali.

Mfano, iwapo tulikuwa tukipendelea mno kutembelea na kusikiliza muziki na majumba yake, basi inatubidi tusikilize na kuisoma Quran, Hadithi na mawaidha mbalimbali ya dini.(Wakati wa kusoma Quran tufuate sharti la utoharifu). Iwapo tulibakia msikitini katika hali ya janaba basi inatubidi tufanye I'itikafu msikitini.Iwapo tulikuwa tukivitizama vitu ambavyo vimeharamishwa na Allah, basi sasa inatubidi tuvitazame vitu vyote vyema vyenye kuwa na malipo ya thawabu za ibada.Mfano kusoma Quran Tukufu, kuzitazama nyuso za wazazi wetu, kuwatazama wazee na watu walio wema na Masharifu na vile vile tujifunze kwa kuzitazama neema za Allah.

Baada ya kufanya TAWBA na baada ya kurejesha haki za watu, sasa tutoe sadaka kwa kiasi kikubwa kutokea mali yetu.Iwapo tulimsengenya mtu yeyote, basi baada ya kutubu, tumsifu huyo mtu kwa wingi kwani tulimsengenya na itatubidi tubainishe matendo yake yaliyo mema.Kwa kifupi, baada ya kufanya TAWBA,itatubidi tutende matendo yetu dhidi ya madhambi.Hivyo tuzidishe matendo yetu mema na tuongezee ibada zetu bila ya kujali upinzani utokao katika nafsi zetu kama vile daktari anavyomtibu mgonjwa ndani ya mwili wake na wala hapendi apasuliwe.Lakini daktari atafanya kinyume na kile atakacho mgonjwa kwa ajili ya faida yake.