rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

4. TOBA KAMILIFU:

Mtu mmoja alitamka 'Astaghfirullah' mbele ya Imam Ali a.s. Hapo Imam alimwambia: "Ole wako! Je wajua kuwa istighfar ni nini? (Kwani huyo mtu alikuwa akitubia mdomoni tu, wakati moyoni mwake alikuwa hana hisia za kutubu) Istighfar inayo daraja la juu kabisa na ni mojawapo ya mambo bora kabisa mbele ya Allah. Ama katika maana ya Istighfar, ni lazima kuwepo kwa mambo kwa mambo sita katika utekelezaji wake, ndipo itakapokuwa Istighfar kamili:

1. Kujutia na kusikitikia matendo tuliyokwisha tenda.

2. Tuazimie kwa nia moja kutotenda madhambi tena maishani mwetu

na vile vile kuwa tutajiepusha nayo kwa uwezo wetu wote.

3. Kutimiza haki za watu ili tutakapokufa tuwe tumekufa bila ya haki

ya mtu mbele ya Mola wetu (Tusiwe na mzigo wa mtu).

4. Tuzilipe amali zote tulizoziacha na ambazo tulifaradhiwa.

5. Kuugeukia mwili wetu, kusikitika na kujuta katika hali ya TAWBA,

hadi nyama yote ilikuwa kwa sababu ya kula vilivyo haramu ikauke

kiasi kwamba ngozi igusane na mifupa. Baada ya TAWBA, nyama

inaweza kukua kwa mara nyingine tena.

6. Tuuonjeshe mwili wetu taabu na shida za ibada kama vile

tulivyokuwa tukiufurahisha wakati wa kutenda madhambi tukiwa

katika starehe mbali mbali.

Basi utakapokuwa umejitahidi na umetekeleza hayo mambo sita, ndipo useme 'astaghfirullah'