rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

2. UHAKIKA WA TAWBA.

Ipo Hadithi ya Mtume (S.A.W.W.) isemayo:

"Majuto na masikitiko baada ya kutenda dhambi ndiyo TAWBA."

Imam Muhammad Al-Baquir (a.s.) amesema:

"Kule kusikitika kwa mtu baada ya kutenda matendo,inatosha kwa kufanya TAWBA ........(Usuli Kafi)

Al-Imam Jaafer as-Sadique (a.s.) amesema:

"Hapana mtu ambaye asiyesamehewa na Allah swt baada ya kusikitika na kujuta kwa yale aliyoyatenda, na anapoomba msamaha na kutubu, basi hapo madhambi yake yote kwa pamoja husamehewa......."

Kwa sababu hiyo uhakika wa TAWBA ni kusikitika, kujuta na vile vile kujihisi mtu mwenye aibu kwa madhambi tuliyuoyatenda. Inambidi mtu aamini kuwa Allah swt atachukizwa kwa kosa langu hili kama vile mja anapofanya jambo kinyume na matakwa ya mmiliki wake huku akionwa na bwana wake, akiwa katika hali ya kumsahau Tajiri wake. Kwa kuwa kila mtu anaelewa na kuamini pia kuwa chochote kile akitendacho Allah swt anamwona, basi hapo kwa hakika atakuwa na majuto na masikitiko, na vile vile atakuwa amepatwa na aibu sana kama vile mfanyabiashara mmoja apatanapo na mtu na akampatia vyote alivyokuwa navyo na huku amebakia na deni adaiwalo, basi atasikitika mno kwa mapatano kama hayo. Hususan atasikitika zaidi pale iwapo atakuwa alishakanwa na kuzuiliwa na rafiki mpenzi. Mfano wake ni sawa na mgonjwa ambaye amekatazwa na daktari asile vitu fulani kwani vitamletea madhara mwilini mwake,naye kwa kupuuzia mashauri hayo, akavila, na hatimaye akaugua na kutaabika zaidi. Basi katika hali hiyo hakuna kitu kingine isipokuwa ni masikitiko na majuto matupu.