MLANGO 10

MCHANGANYIKOWAMAMBO   MUHIMO

(A) MADHAMBI MAKUBWA

Twalieleza mbele kwamba jambo muhimu na la kwanza katika 'Amal' vitendo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ni Taqwa' (Kujitenga na yaliyo haramishwa).

Tusisahau kuwa adabu na Adhabu ya kila dhambi katika mwezi huu, tukitenda huwa mara mbili. Kwa hivyo kwa kuwasaidia wasomaji wetu, tunaeleza hapa orodha ya madhambi  makubwa (ambayo Mwenyezi Mungu ameahidi kumtia motoni mtendaji), nayo ni haya: (1) (Ash-Shirku Billaah) Kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika. (2) (Al-Ya'su min Rawhil-Laah) Kukata tamaa na rehema za Mola. (3) (Al-Amnu min Makril-Laah) Kutoogopa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. (4) (Uquu-Qul-Waa-lidayn) Kukosa radhi ya wazee na kuwaudhi. (5) (Qatlun-nafsil-muhtarama) Kuua. (6) (Qadhful-Muhsina) Kumsingizia mwanamke kwa kuzini. (7) Kula mali ya yatima kwa dhuluma. (8) Kukimbia kwenda kupigana Jihadi. (.9) Kula riba. (10) Kuzini (11) Kulawiti (12) Kutenda mambo ya uchawi. (13) Kuapa kiapo cha uwongo, juu ya jambo au kumkosesha haki ya mtu kwa kuapa uwongo. (14) Kukataa kutoa zaka iliowajibu kutoa. (15) Kushuhudia uwongo. (16) Kuficha na kukanusha ushahidi. (17) Kulewa (kunywa mvinyo wa aina yoyote) (18) Kuacha kusali sala ya fardhi au jambo lolote la fardhi makusudi. (19) Kuvunja ahadi. (20) Kukosa kumsaidia jamaa yako kwa jambo lolote la kheri. (21) Kukaa au kuhamia mahala ambapo utakosa mambo ya dini na Imani. (22) Kuiba. (23) Kukanusha mafundisho au jambo lolote la Dini. (24) Kusema uwongo, uwongo wa namna yoyote hasa juu ya Mwenyezi Mungu, Mitume na Awsiyaa (warithi) wa Mitume. (25) Kula maiti (nyama ya halali aliyekufa au kachinjwa bila kutajwa jina la Mwenyez'i Mungu au hazikutimizwa shuruti za kumfanya mnyama aliyechinjwa awe halali kula). (26) Kula damu namna yoyote. (27) Kula nyama ya nguruwe. (28) Kucheza kamari, (29) Kula thamani ya uchafu. Maiti, mvinyo, ulevi, malipo ya uzinzi, mirungura, mtabiri (mpiga ramli), kazi kwa mdhalimu, malipo ya kwimba mwanamke, Staranji (chess). (30) Kupunja (Kutoa kasoro kwa kipimo au mizani). (31) Kuzuia haki za watu pasipo na taabu. (32) Takabari (kuwa na kiburi). (33) (Al-Is-ra-fu) Kutumia kwa fujo. (34) Kudharau kwenda kuhiji Maka. (35) Kushughulika, au kwenda kwenye ngoma, muziki na kwenda sinema. (36) Kucheza ngoma (dance). (37) (Al-Gheebah) kumsema mwenzio. (38) (At-Tuhma) Kutuhumu. (39) An-Na-Meemah) uchongezi. (40) Kuwadhihaki Mumineen, kuwaudhi na kutoa siri ya wenzio. (41) Kumchungulia mke au mwanamke yeyote asiyekuhusu, na vile vile mwanamke kumtazama mwanamme yeyote asiyemhusu au kutoka wanawake nje bila ya kujifunika. (42) Kuvaa mwanamume pete au kitu chochote cha dhahabu, na hariri safi. (43) Kuficha vyakula vya mahitajio ya watu na kukataa kuuza wakati wa dhiki kutaka faida nyingi.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani:

Êöáúßó ÍõÏõæÏõ Çááøåö ÝóáÇó ÊóÞúÑóÈõæåóÇ

(Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie). Hakika hizi hukumu za faradhi, haramu, halali, na suna, ndizo mipaka ya Mwenyezi Mungu na ukingo kati ya haki na batili; basi msikaribie kwa kukanusha na kuhalifu. Katika hadithi ya Mtume (s.a.w.) amesema, "Hakika kila mfalme anao ulinzi, na ulinzi kwa Mwenyezi Mungu ni kujilinda na yaliyoharamishwa, basi mwenye kwenda karibu nazo ipo hatari ya kuanguka ndani yake".

Mwenyezi Mungu amesema:

 Åöä ÊóÌúÊóäöÈõæÇú ßóÈóÂÆöÑó ãóÇ Êõäúåóæúäó Úóäúåõ äõßóÝøöÑú Úóäßõãú ÓóíøöÆóÇÊößõãú æóäõÏúÎöáúßõã ãøõÏúÎóáÇð ßóÑöíãðÇ (4:31)

"Kama mkijiepusha na maovu makubwa mnayokatazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo na tutakuingizeni mahali patukufu kabisa (Napo ni Peponi)". Hapa inasema tukijiepusha na ile midhambi mikubwa tuliyo itaja juu, Mungu atatusamehe vile vile vijidhambi vidogo vidogo. Lakini usiendelee nao wala tusiyadharao kuwa ni vidogo; kwani ukifanya hivyo unatenda dhambi kubwa.

(B) ITIKAFU

Itikafu ni kutia nia mtu kukaa msikitini muda usiopungua siku tatu na zaidi, kufanya ibada kama sala, dua, na kadhalika, na hufaa kufanya Itikafu kati ya mwaka mzima siku ambazo hujuzu kafunga saumu. Bora kabisa na ambayo ina thawabu nyingi ni kufanya Itikafu katika mwezi wa Ramdhani na hasa siku za mwisho. Hukaa humo msikitini   isipokuwa  kwa jambo la dharura  sana  kama kwenda chooni, kuoga janaba, na vile vile anaruhusiwa kwenda kumzuru mgonjwa, kumwosha na kumvalisha sanda maiti, na kumsalia maiti. Basi muda huo wa kuwa katika Itikafu hapana ruhusa kuingiliana na mkewe japo kuwa huo muda wa kwenda chooni.

Mwenyezi Mungu amesema:

æóáÇó ÊõÈóÇÔöÑõæåõäøó æóÃóäÊõãú ÚóÇßöÝõæäó Ýöí ÇáúãóÓóÇÌöÏö

 Wala msichanganyike nao (msiwaingilie) na hali mnakaa Itikafu (msikitini).

(c) Alama na thibitisho za kuanza na kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani

(1) Ramadhani hudhihirika unapo andama mwezi, na humalizika kwa kuonekana mwezi wa mfungo mosi (Shaw-wal). Mwezi wa Ramadhani ukionekana tu, kifungo huwa ni wajib kwa wote wanaotakiwa kufunga. Mwezi wa mfungo mosi (Shawwal) ukiandama tu, Ramadhani humalizika. Mtume (s.a.w.) alisema, "Su-muu li-ru-yati-hi wa af-tirou li-ru-yati-hi fa-in khafiya fa, ak-miluu id-data sha-ban thala theena yaw-man".

"Fungeni mkiona mwezi na mfunguwe mtapoona mwezi; lakini ukifichika, imalizeni Shabani kwa siku thelathini, vile vile ikiwa mwezi wa Shawwal haukuonekana kwa sababu ya hali mbaya ya hewa, Ramadhani iwe thelathini"

Njia za kuthibiti mwezi ni tano

(1) Mtu   binafsi   auone   mwezi.   Hapo   itamlazim (Wajib) afunge ikiwa ni mwezi wa Ramadhani, na itampasa )wajib) afuturu (asifunge) ikiwa ni mwezi wa Shawwal itapokuwa mtu mwingine hakuuona mwezi.

(2) Zipite siku thelathini kamili kwa mwezi wa nyuma basi ikiwa imetimia siku thelathini ya Shabani, ni wajib afunge hata kama hakuona mwezi, na ikiwa zimefika siku thelathini za Ramadhani basi lazima siku baadaye afuturu (asifunge) hata kama mwezi hakuuona.

(3) Washuhudie   wanaume wawili   waadilifu   kuwa wameuona mwezi  kwa macho yao;  (lakini hao  waadilifu wasiwe wanahitalifiana  katika maelezo  ya kuona  mwezi, kwa mfano mmoja aseme umekaa hivi, na mwembamba sana, na wa pili aseme ulikuwa juu sana na mnene; basi hapo shahada hizo hazithibiti).   Hapo ni wajib afunge ikiwa ni mwezi wa  Ramadhani, na  itampasa kufuturu (asifunge) ikiwa ni mwezi wa Shawwali.

(4) ASH-SHI-YAA. Kikundi cha watu au makundi ya watu washuhudie kwamba mwezi wameuona, na wewe kwa

ushuhuda huo upate yakini ndipo itakulazimu kufunga au kufuturu; lakini ikiwa kwa ushahidi huo hukupata yakini basi huwezi kufunga au kufuturu.

(5) Akihukumu Mujtahid  (Mwanachuoni)   mwadilifu kwamba kesho ni mwezi mosi na unao uhakika wa maelezo ya kuandama mwezi aliyoyapata sahihi (thabiti) basi ni wajibu watu wote wafuate.

Mwezi kuwapo juu sana au kuwa ni mkubwa au kuchelewa kuzama haiwi dalili na thibitisbo ya kuwa usiku wa jana ilikuwa usiku wa mwezi mosi, na leo mwezi pili. Mwezi hauthibiti kwa kuandikwa magazetini au kwa kusemwa na wenye elimu ya nyota (Metreology). Haithibiti mwezi kwa shesria. ikiwa wameona wanawake tu, wala akiuona mtu mmoja mwadilifu hata akiapa kiapo pia. Lakini ikiwa kwa jambo lolote inakuletea yakini na uthibitisho rohoni mwako kwa kuandama mwezi basi juu yako wewe tu, ni wajibu kuifuata, si mwenzio.

Ikiwa imethibiti mwezi katika mji mmoja, kwa watu wa mji wa pili haina faida, isipokuwa mji huo uwe karibu na mji wako, au wenye 'ufuq (MATLAI) moja. Ufuq (Matlai) moja ni miji ile ambayo ipo karibu na mji uliomo wewe. (Aga Khui haafikiani hapa).