MLANGO 6

NAMNA  ZA  SAUMU (KUFUNGA)

Saumu ipo namna nne: Kwanza, Wajib (fardhi). Pili, Haramu. Tatu, Makruuhu (yenye karaha). Nne. Mustahab (sunna).

Saumu zilizo faradhi (Wajib)

(1)Saumu ya mwezi wa Ramadhani.

(2)SaumuyaNadhiri,AhadinaYamini,ambazofungahizohufaradhikakwakuwekanadhiri,auahadiaukuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu.

(3)Saumu ya kadha (malipo ya mwezi wa Ramadhani kwa wale wasiofunga).

(4)Saumu ya kaffara:

(5)Samu ya kufunga badala ya mtu aliyekufa kwa kulipiwa.

(6)Saumu badala ya kuchinja nyama katika Hija ikiwa mtu hana uwezo wa kununua mnyama wa kuchinja, afunge siku kumi (Tatu huko Maka na saba akirejea nyumbani).

(7)Saumu ya siku ya tatu katika siku za Itikafu.

(8)Saumu kwa mtoto mwanamme wa kwanza badala ya wazee wake ambao walikufa kabla ya kuzilipa saumu zao.

              Saumu za haramu (Zilizokatazwa kufunga)

(1)Saumu ya sikukuu mbili (a) Idi ya Ramadhani Idul-Fitri  siku ya kwanza ya shawwal (mfungo mosi): na (b) Idul-Adh-Ha (Sikukuu kubwa, mwezi kumi mfungo tatu (Dhil-Haj-ja) sikukuu ya kuchinja).

(2)Kufunga kwa watoto saumu za sunna bila ya radhi ya wazee; vile vile mke kufunga sunna bila ya radhi ya mumewe ikiwa kwa kufunga mke hatekelezi haki ya mume.

(3)Saumu ya siku ya shaka baada ya kwisha siku 29 ya shabani. Kwa sababu ya mvua na mawingu, mwezi tisa

na ishirini, mwezi haukuonekana na hukupata hakika ya kuandama kwa mwezi, siku hiyo ya pili ni siku ya shaka

ilivyokuwa simwisho wa Shabani wala simwanzo wa Ramadhani. Basi haijuzu kufunga kwa nia ya Ramadhani bali

unaweza kwa nia ya sunna tu.

(4)Saumu Ay-Yaa-Mut-Tash-reeq: Siku tatu baada ya sikukuu kubwa (ya kuchinja) nazo ni tarehe kumi na moja,

kumi na mbili, na kumi na tatu, mfungo tatu (Dhil-Hajji) kwa wale walioko Mina katika Maka wanapohiji.

(5)Saumul Wisaal: Kufunga kwa mfululizo bila kufuturu usiku hadi alfajiri au siku ya pili magharibi. Lakini ikiwa hukutumia zivunjazo saumu si kwa nia ya kufunga, bali basi tu, haidhuru saumu yako.

(6)Saumus-Samt: Kwamba anuwie katika saumu kukaa kimya kabisa mchana kutwa, au baadhi ya nyakati, ni

haramu. Lakini ikiwa hakunuwia hivyo na ikatokeya sudfa siku hiyo kutwa hakuongea, basi haidhuru neno, kwani hakunuia hayo.

Saumu zilizo Makruhu (ya karaha)

Maana ya makuruhu hapa (na katika Ibada yote) ina thawabu kidogo sana; na bora zaidi kuiwacha. Nazo ni hizi:

(1) Saumu siku ya Ashura: (mwezi kumi Muharram, mfungo nne). Imepokewa kwa baadhi ya wanavyuoni kwamba Banu Umayyah walikuwa wakiifurahia siku hiyo na wakiifunga kuonesha furaha yao kwa kumwua Imaam Husain, A.S. (Bwana wa Vijana wa Peponi) siku kama hiyo. Zimepokewa hadithi nyingi zilizosemwa na Ahlul-Bait (A.S.) kulaumu kufunga siku mbili (mwezi tisa na kumi) ya Muhar-ram na hasa siku ya Ashura. Hadithi nyingi wamemzulia Mtume (S.A.W.) kuonesha fadhila ya kufunga siku mbili na hasa Ashura hadithi za uzushi tu. Naam, ukiwacha kula na kunywa bila nia ya kufunga, kwa kuihuzunikia masaibu yaliyompata Sayyidinal Husain (A) na Ahl-Bait wa Mtume (S.A.W.) siku hiyo, na kuikumbuka njaa na kiu chao, baada ya sala ya Alasiri ukifungua kinywa kwa maji tu, bila shaka ni kama unampa Mtume (S.A.W.) mkono wa rambi rambi.

(3, 2) Kufunga siku ya Arafa (mwezi tisa Dhil-Haj, mfungo tatu) ikiwa siku hiyo inatiliwa shaka kwamba ni Idi (mwezi kumi); na kwa yule anayeogopa kudhoofika kwa kufunga siku hiyo na akachelea kuzisoma Dua na kufanya Amali ambazo ni bora kuliko kufunga.

(4) Kufunga saumu mgeni (aliyeshuka kwa mtu) bila ya idhini ya mwenye kukaribisha.

Saumu   za Sunna

(1)Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni suna, imepokewa hadithi kwamba kufunga huko ni sawa na kufunga maisha; na inaondoa joto la kifua. Na njia bora ni kufinga hivi; afunge  Alhamisi ya kwanza na  ya mwisho wa  kila mwezi, na jumaa tano ya mwanzo katika kumi ya pili ya mwezi. Na  mwenye  kuacha kufunga siku  hizo, basi ni sunna  azilipe, na  akiwa hajimudu  kwa uzee,  basi inafaa afidie kwa kila siku Mud moja (kibaba kimoja) cha ngano au pesa.

(2)Saumu ya Ay-yaamul Beedh: Kufunga kila mwezi 13, 14, na 15.

(3)Kufunga kila Alhamisi na Ijuma pamoja, au Ijumaa tu.

(4)Saumu ya miezi ya Rajab na Shabaan (mfungo kumi na kumi na moja) siku zote, au baadhi ya siku, ijapokuwa siku moja katika kila miezi miwili hizo. Zimepokewa hadithi ya Imaam Musa bin Jaffer (A.S.) amesema hivi:

"Rijab ni mwezi adhimu mtukufu, Mwenyezi Mungu huzidisha katika mwezi huu bakhshishi, na hufuta madhambi. Basi mwenye kufunga siku moja katika Rajab moto wa Jahannam huwa mbali naye mwendo wa mwaka mmoja, na mwenye kufunga siku tatu ataingia Jannah (Peponi).

Na katika hadithi nyingine, Al-lmaam As-Saadiq (A) amesema: "Mwenye Kufunga siku kumi na tano katika Rajab,

Mwenyezi Mungu humpa atakayo, na akizidisha kufunga atamzidishia"

Na katika hadithi nyingine, Imaam huyo amesema: "Mwenye kufunga siku moja katika Shabaani basi ataingia Jannah."

Na katika hadithi nyingine, Imaam huyo amesema: "Mtume (S.A.W.) alikuwa hafungi mwezi kamili katika miezi ya mwaka ila mwezi wa Shabaani na akiunganisha na mwezi wa Ramadhani".

(5)Saumu ya Mab-Ath:  Mwezi ishirini na saba ya Rajabu (mfungo kumi), ambao hapa kwetu ni maarufu sana,

kuwa ni siku ya Miraji, lakini hakika ni siku ambapo Mtume )S.A.W.) alibashiriwa aanze kudhihirisha Utume wake. Na

inayumkinika usiku wake kenda Miraji, ijapokuwa Mtume )S.A.W.) alikwenda Miraji mara nyingi. Imepokewa hadithi

inayotokana na Al-Imaam As-Saadiq (A) kwamba alisema:

"Usiwache mfungo wa mwezi ishirini na saba ya Rajabu, kwani ni siku ambayo aliteremshiwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W.) utume wa kuwafikishia umma, na thawabu ya mfungo huo, ni kama kufunga miezi sitini"

(6)Kufunga siku ya mwezi wa 15 wa shabaan siku ambayo amezaliwa Imaam wetu wa kumi na mbili, Al-Imaan

Muhammad Mahdi (A), mwaka"256 ya Hijra katika mji wa Samarra (Iraq).

(7)Kufunga siku ya nne mpaka mwezi tisa Shawwal )mfungo mosi).

(8)Kufunga siku ya Dah-wul-Ardh: siku ya kuenewa ardhi (Dunia) kutoka chini ya Al-Kaaba. Nayo ni siku mwezi ishirini na tano ya Dhil-Qaada, mfungo pili. Imepkewa hadithi kwa Al-Imaam AR-RIDHA (A) Imaam wa nane, amesema kwamba mwenye kufunga siku hiyo anapata thawabu sawa na kufunga miezi sitini.

(9)Kufunga mwezi ishirini na tisa wa mfungo pili (dhilqaada).

 (10)     Kufunga siku ya kwanza ya mwezi mfungo tatu Dhil-Haj au kila siku katika siku tisa za mwanzo. Imepokewa hadithi ya Imaam Musa bin Jafar (A.S.), imaam wa saba, amesema hivi: "Mwenye kufunga siku tisa katika kumi ya mwanzo wa mfungo tatu anapata thawabu ya kufunga maisha.

(11)      Kufunga siku ya Arafa (mwezi tisa mfungo tatu) kwa yule ambaye kwa kufunga hatadhoofika kwa kufanya

amali na dua.

 (12) Kufunga siku ya Ghadeer nayo ni siku ambayo Mtume (S.A.W.) alimteua Sayyidna Ali (A) kuwa ni Wasii na wazir wake wa haki kwa amri ya Mwenyezi Mungu alipoteremsha aya ifuatayo njiani akirudi kutoka Hija ya mwisho   kwenye   mahala   paitwao  íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáÑøóÓõæáõ ÈóáøöÛú ãóÇ ÃõäÒöáó Åöáóíúßó ãöä ÑøóÈøößó æóÅöä áøóãú ÊóÝúÚóáú ÝóãóÇ ÈóáøóÛúÊó ÑöÓóÇáóÊóåõ " (5:7)

"Ewe Mtume! Fikisha ulioteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wetu". Baadaye akakamata mkono wa Sayyidna Ali (A) na akasema, "MAN KUNTU MAW-LAA-HU FA'HADHA ALIY-YUN MAW-LAAHU". "Mwenye (kunikubali kuwa mimi ni bwana wake, basi huyu Ali pia ni bwana wake", na akasema maneno haya juu yake, "AL-LAA-HUM-MA, WAA-LI MAN, WAA-LAA-HU, WA AA-DI MAN, AA-DA-HU, WAN-SUR, MAN NASA-RAHU, WAKH-DHUL MAN KHADHA-LAH", (Ee Mola wangu, mpende mwenye kumpenda Ali, mfanyie uadui na mwenye kumfanyia Ali uadui, msaidie mwenye kumsaidia Ali mchukie mwenye kumchukia Ali). Nayo ni siku ya mwezi wa kumi na nane (18) wa Dhil-Haj-ja (mfungo tatu). Imepokewa hadithi, kutokana na Al-Imam As-Sadiq (A), kwamba amesema; "Kufunga siku ya Ghadeer ni malipo ya fidia ya miaka sitini".

(13) Kufonga siku ya "Mubaahala" (mwezi ishirini na nne wa Dhil-Haj mfungo tatu). Nao ni siku ya kuamrishwa Mtume (S.A.W.) na Mwenyezi Mungu kwenda kuapizana Yeye  na Ahlu-Bayti wake mbele ya Makasisi wa Makristo wa Naj-raani na kama inavyoeleza aya(3:61) hivi:

"Watao kuhoji (sasa) katika haya baada ya kukufikilia elimu hii (na kuwafikilia wao), waambie, "Njoni tuwaite watoto wetu na watoto wenu na wanawake wa kwetu na wanawake wa kwenu na sisi na nyinyi; kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Myenyezi Mungu iwashukie Waongo"

(15), (14)  na (16) Kufunga siku ya awali ya Maharram, ya tatu na ya saba (mfungo nne).

(17) Kufunga siku aliyozaliwa Mtume Muhammad )S.A.W.) nao ni mwezi kumi na saba (17) Rabeeul-Awwal (mfungo ita).

(18) Kufunga siku ya nusu (15) ya Jumaadal-Ula (mfungo nane).

(19) Saumu ya Nairuuz (mwezi 21au 22 March).