MLANGO 2

FADHILA YA RAMADHANI NA KUFUNGA

Hapa tunaeleza baadhi ya utukufu na fadhila za mwezi wa Ramadhani.  Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani hivi:-

ÔóåúÑõ ÑóãóÖóÇäó ÇáøóÐöíó ÃõäÒöáó Ýöíåö ÇáúÞõÑúÂäõ.

 'Mwezi huo (mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao hii Qur'ani ndipo imeteremshwa.

åõÏðì áøöáäøóÇÓö æóÈóíøöäóÇÊò ãøöäó ÇáúåõÏóì æóÇáúÝõÑúÞóÇäö

"Imeteremshwa Qur'ani katika mwezi huo ili iwe uongozi kwa watu na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi wa baina ya haki na ubatili". Qur'ani ni kipimo baina ya haki na ubatili, na ni mizani ya kuangalia uzuri na ubaya. Kwa sababu kila kitendo na amali, Ukiweka mbele ya Qurani, ikiwa inawafikiana na Qur'ani basi hiyo ni haki na nzuri, na ikiwa haiafikiani basi ni batili na mbaya.

Mtume (S.A.W.) alisema katika hotuba yake aliyohutubia kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Ijumaa ya mwisho wa Shabani (na iliyopokewa kwa Imaam Ali bin Musa Ar-Ridha (A.S.) aliyoipokea kwa baba zake watukufu (A.S.) kutoka kwa Amirul-Mumineen) hivi:

"Ay-yuhan-nass In-nahu qad aq-bala ilay-kum shah-rul-laah bil-bara-kati war-rah-mati wal-magh-firah. Shah-run huwa in-dal-ILaah af-dha-lush-shu-huur wa ay-yaa-muhu af-dha-lul, ay-yaam; wa layaa leehi af-dha-lul layaa-Iee wa saa-aatu-hu a£-dha-lus-saa-aat; wa ama-Iukum fee-hi maq-buul; wa du-a-akum feehi mus-ta-jaab. Fas-alul-lLaa-ha rab-bakum bi-niy-yaa-tin saa-diqa, wa qu-luu-bin, taa-hira an yuwaf-fiqa-kum lisiyaa-mihi wa ti-laa-wati ki-taa-bih, fain-nash-sha-qiy-ya man hur-rima ghuf-raa-nal-laahi fi haa-dha-ash-sha-iil-adheem".

"Enyi watu, hakika mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu (Ramadhani) umekukabilini (umewadia) kwa Baraka, Rehema, na maghfira: Mwezi ambao kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko miezi yote; mchana wake ni bora kuliko mchana wote; na usiku wake ni bora kuliko usiku wote; Na saa zake (mchana na usiku) ni saa bora kabisa; na amali mtaoifanya inakubaliwa, na Dua mtazo omba zitakubaliwa. Basi mwombeni Mala wenu kwa nia ya ukweli (halisi), na nyoyo safi akuafikini mfunge mwezi huu, na kusoma Qur'ani. Kwani hakika "Shaqiy" mkosefu ni yule ambaye atakosa kughufiriwa na Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu. Bila shaka mtu atakayekosa kughufiriwa na Mwenyezi Mungu katika mwezi huu ndiye "Shaqee" mpotevu na dhalili".

Unapoingia mwezi mtukufu wa Ramadhani watu hujifunga kwa Ibada. utii, kufanya mema, na kila jambo la kheri kwa kiasi cha uwezo wao.

FADHILA YA KUFUNGA:

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani tukufu: Yaa ayyuhal-ladhina aa-manu kutiba alay-kamus-siya-amu kamaa kutiba alal-ladhina min qab-likum; La'allakum tat-taquon; Ay-yaa-raam maa-duu-daat". (2:183-4)

(Enyi mlio amini mumefaradhishiwa kufunga kama waliyyo faradhishiwa wale walio kutangulieni, ili muweze fanya subira. siku chache tu kwa kufunga huko". Zile siku chache ndio mwezi huu wa Ramadhani ambao umefaradhishwa kufunga. Husemwa kwamba hekima ya kuainishwa mwezi huu wa Ramadhani minghairi (pasipo) ya miezi mingine ni kuwa Mwenyezi Mungu ameeneza uongozi wake katika mwezi huu, juu ya viumbe wake wote kwa jumla, na juu ya Waislamu kwa halisi alipoteremsha Qur'ani, kama tulivyo eleza mbele.

Katika hadithi iliyopokewa kwa Amirul Muminiin Ali (a.s) inasemwa, '"Mtu wa kwanza ulimwenguni aliyefaradhiwa kufunga saumu ni baba yetu Adam (A). Maana yake si kwa nyie Waislamu ndio mmefaradhishiwa kufunga tu, bali mtu wa kwanza, na umma wote waliopita walifaradhishiwa kufunga, lakini tunatafautiana kwa wakati na namna ya kufunga.

Katika mwisho wa aya 183, (áóÚóáøóßõãú ÊóÊøóÞõæäó), yaani mjizuie (mwepukane) na uovu na Maasi, kwani inavunja nguvu ya matamanio ambayo ni sababu na njia kubwa ya maasi kama ilivyo katika hadithi (MAN LAM YAS-TATI-IL-BAAH FAL-YA-SUM), maana yake, asiyejiweza kujizuia na mambo ya matamanio basi afunge kwani saumu hupigana na mambo ya matamanio. "TAQWA" hasa inatoka moyoni na ni hali halisi ya roho iliyochanganyika na hadhari na hofu kumcha Mungu.

Umuhimu na fadhili za saumu hazina mfano wala makisio. Mwenyezi Mungu katika "Hadithul Qudsi" (hadithi takatifu) anasema AS-SAWMU LEE WA ANA AJZEE ALAYHI, (Saumu  hasa ni yangu na mimi ndiyo nitakaye toa jazaa na thawabu yake). Maana yake thawabu ya kufunga jinsi nyingi na adhimu, hata Malaika hawezi kukadiria au kujua kiasi cha thawabu yake. Basi Ibada kwa jiasi ilikuwa adhimu hata tukipata kidogo takalifu, tusifikiri kitu bali tuteketeze inavyotakikana ili tustahiki kuipata jaza hiyo.

Sababu na maana ya kufunga saumu ina .thawabu adhimu kama hiyo yawezekana kuwa ni hii. Mwenye kusali anaposali anaweza kuonekana na watu wengine; kuhiji na kupigana jihadi (vita vya dini) huwa mbele na pamoja na watu hutendeka na wengine pia wakaweza kuona; kutoa khums na zaka au sadaka kwa vyovyote kama hawakujua watu, yule mustahiki maskini unayempa hiyo zaka atajua! Hivyo hivyo tukichukua Ibada zote lazima mtu au watu watajua; na katika Ibada hizo zote inaweza kuwa mtu kumwingia Riya (kujipendekeza) kuonesha watu. Lakini kufunga saumu ni Ibada ile ambayo haitakiwi jambo lolote kudhihirisha, bali inatosha kufanya nia tu ua kujizuia na baadhi ya mambo. Kwa hiyo mpaka mtu aliyefunga asidhihirishe kuwa amefunga, mtu mwingine hawezi kujua kama fulani amefunga. Vile vile ni shida sana kwa mfunga saumu kumwingia Riya (kutaka kujipendekeza). Kwa yote hayo ndipo Mwenyezi Mungu kuita Ibada hii ya kufunga hasa yake, na kumjazi mwenye kufunga Yeye Mwenyewe.

Wapo baadhi ya watu miongoni mwetu, siku akifunga utamwona amenuna utafikiri kwa kufanya Ibada hiyo amewafanyia hisani wengine! Isitoshe haya, utaona kaghadhibika na watu wa nyumbani na watumishi, amejaa na uchungu! Hajijui maskini, kwa kufanya hivyo ile shabaha halisi kuwa ni Ibada ya siri inapotea; na watu wote wa mtaa wanajua kuwa fulani amefunga, kwa sababu leo anahamaki na kila mtu! Hakika tukitaka tufunge saumu kikweli kweli, basi lazima tuepukane. na tabia mbaya kama hiyo, tuwe wapole na wenye huruma zaidi juu ya watu wa nyumbani na watumishi tunapofunga.

Zimepokewa hadithi nyingi kutokana na Mtume (S.A.W.) na Ahlubayti wake pamoja na Maimamu kumi na mbili (S.A.) juu ya Saumu, na kuhimiza kufunga, maeleazo juu ya hekima za saumu, siri na adabu za mfungaji, na thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu. Hata mtu akiyaona maelezo au kuyasikia hayo atashangaa kwa kuona wingi wake.

Hapa tutaeleza zile haditbi zinazohimiza kudumisha na kushikilia kufunga, tulizozipata katika kitabu mashuhuri kinachoitwa, WASA-ILU-SH-SHlA.

Imepokewa hadithi kwa Imaam As-Saadiq (wa sita (a.s) isemayo kwamba, Mwenye kufunga (Saumu) anakuwa katika ibada, hata kama amelala (anapata thawabu ya ibada) lakini ikiwa hakumsema mtu.

Vile vile imepokewa hadithi kwamba Imaam As-Saadiq (A) amesema: "Mwenye kuificha saumu (asihubiri mtu kama amefunga), Mwenyezi Mungu anawahubiri Malaiki

hivi, 'Kiumbe wangu ametaka alindwe na adhabu yangu, basi mlindeni'". Mwenyezi Mungu amewaweka Malaika wakiamrishwa kumwombea mtu yeyote hapana budi ila dua hiyo hukubaliwa.

                      

Kumcha Mungu: Amali Bora Kabisa

Amali gani bora kabisa kutenda katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani?

Kila mmoja hujibu kwa mujibu wa maarifa yake na kiasi cha fikra na elimu zake. Lakini ni bora mno tutazame na tuyafahamu maneno ya hotuba aliyoitoa Mtume (S.A.W.) katika Ijumaa ya mwisho wa Shabani kuwapa waislamu maelezo, fadhila, utukufu na ufanyaji bora wa amali katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Anasema Ameerul-Mu-mineen Ali (a.s): Baada ya kumaliza Mtume (S.A.W.) hotuba hiyo, "nikasimama na nikamwuliza, 'Ya Rasuu-lallaah, Amali gani bora kabisa katika mwezi huu mtukufu?' Akajibu, 'Uchaji wa Mwenyezi Mungu kwa kila kilichoharamishwa na kukatazwa'".

Hakika uchaji ijapokuwa ni neno fupi na dogo, lakini maana na muradi wake ni kubwa mno na vigumu kwa vitendo. Kwa hivyo kusali suna, kufanya Ibada, kusoma Qur'ani, kulisha, kuvisha na mambo mengi yote ya kheri hayawezi kuwa sawa kabisa na Uchaji wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yote hayo ni sehemu moja ya uchaji nayo ni suna, lakini kujitenga na madhambi na alichoharamisha Mwenyezi Mungu ni jambo la wajibu, si mwezi wa Ramadhani tu bali maisha yake mtu yote, Mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwa kila alichoharamisha na kukataza, tutasema kwa yakini amefanya amali bora kuliko yote katika mwezi huu. Na hapana shaka akizifanya baada ya amali zote zingine suna zilizotajwa kuwa bora, basi mtu huyo kapata bahati nzuri sana. Tunaomba kwa Mwenyezi Mungu , kwa wasila ya Mtume wake (S.A.W.) na Ahlu Bait zake (A.S.), kwa baraka ya mwezi huu mtukufu awape Waislamu wote uwezo wa kufikiria kumcha Mwenyezi Mungu, (Na kwa sadaka ya hao wote, mumi mtungaji pia asinisahau). Amini.