KITABU  CHA  SAUMU

S.MUHAMMAD MAHDI AL-MUUSAW

Mateuzi Kutoka Dibaji ya Chapa ya Kwanza

BISMIL LAA HIR RAHMAA NIR-RAHEEM

Kwa jinsi kitabu hiki kina maelezo na mafundisho ya maana juu ya kufunga na maamrisho yake, hata inambidi kila Mwislamu na asiye Mwislamu kuwa na kitabu hiki, na kukisoma, na hasa wale wanaotaka kujua Uislam.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa taufiki ya kukitunga kitabu hiki ili wapate faida watu, na namwomba Mola kwa utukufu wa Muhammad na Ahlu Baiti wake (s.a.) na kwa baraka ya siku ya leo tukufu ya kuzaliwa Imaam wetu Ameerul-Mumineen Ali (A.S.) mwezi kumi na tatu ya Rajab 1387 Al-Hijra, anikubalie kwa takabali njema na aniwekee akiba yangu siku ya Qiyama. Na naomba kwa Mola atupe taufiki mimi na Waislamu wote kuyafuata yaliyomo humu.

Vile vile napenda kumshukuru sana Maulana Sayed Saeed Akhtar Rizvi kwa kuchukua taabu ya kuipanga kwa uzuri milango na maelezo ya kitabu hiki.

Al-Ahqar Muhammad Mahdi Muuiawy

13th Rajab, 1387 

DAR ES SALAAM

I8th October, 1967

  Dibaji ya Chapa ya Pili

Chapa ya kwanza ya kitabu hiki kilitolewa mwisho wa 1971. Kwa jinsi kilivyopendwa hata katika muda ya miaka 24 nakala zote zikauzikana, lakini bado watu wanavitaka.

Kwa hiyo Bilal Muslim Mission inakichapisha kwa mara ya pili. Safari hii maelezo na Masail yote yamesahihishwa kwa mujibu wa Fatwa za Mujtahid wetu AyatuHah Agha e Sayyid Abul Qasim Al Khoui Dama-Dhilluhul Aali.

DAR ES SALAAM