SHIA  NA  SAHABA

Majibu Na Maelezo

Abdilahi Nassir

UTANGULIZI

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.

Hiki ni kitabu cha tatu katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khututul Aridhwa kilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Misingi Mikubwa lliyojengewa Dini ya Ushia.

Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu sahaba wa Mtume Muhammad s.a.w.w.; na kila tulilolijibu na kulieleza, kama desturi yetu, tumelitolea ushahidi wa vitabu vya Kisunni vyenyewe.

Hata hivyo, ni jambo la kufurahisha kujua kwamba, baada ya majibu yetu haya kutoka, baadhi ya mashekhe wa Kisunni walitukosoa kwa kusema kwamba mzozo huu tulionao si baina ya Sunni na Shia, bali ni baina ya Wahabi na Shia. Na hilo ni kweli. Maana, mbali ya kuwa huyo Sheikh M. al-Khatib mwenyewe alikuwa Wahabi, unapotazama wote wale waliojitokeza dhidi ya Shia katika mzozo huu unawakuta ni Wahabi vile vile — ima kwa imani au kwa kulipwa. Pamoja na hayo, katika majibu yetu haya, tumelazimika kuonekana tunajibizana na Sunni kwa sababu tu Sunni wenyewe wamemwachia Sheikh M. al-Khatib kutumia jina lao bila ya kujibari naye. Lau mashekhe wa Kisunni wangalijitokeza na kuwafahamisha Sunni wenzao hitilafu kubwa iliyoko baina yao na Wahabi, bila shaka ndugu zetu wa Kisunni wangalielewa ule uadui mkubwa dhidi ya Bwana Mtume s.a.w.w. na Uislamu kwa jumla, ambao Wahabi wanajaribu kuuficha kwa kujitokeza kama watetezi wa Usunni. Hilo inshallah ni nia yetu kulifanya, baada ya kumaliza mfululizo huu, pamoja na kuonyesha ushirikiano uliokuwako, na ambao ungaliko hadi leo, baina yao na ukoloni wa Kiingereza dhidi ya masilahi ya Uislamu!

Mara tu baada ya kutoa majibu yetu haya, mmoja kati ya 'wanafunzi' wa Sheikh M. al-Khatib alijitolea, katika darasa zake, kujaribu kutujibu. Kama ameweza kufanya hivyo au la si juu yangu kusema. Ni juu ya wale wanaohudhuria darasa zake na/ au wale waliowahi kuzisikia kanda zake. Lililo juu yangu ni kusema kuwa, ilipotoka tafsiri ya kitabu cha Sheikh M. al-Khatib, mimi sikujibu kwa darasa, japokuwa ninazo. Nimeijibu kwa maandishi vile vile. Kwa hivyo, ili wasomaji wetu wafaidike kwa majibizano haya, tunangojea majibu ya maandishi [1](sio ya mdomo).

Vile vile mmoja kati ya ndugu zetu alijitolea kuandaa majadiliano juu ya suala hili. Hivyo aliniandikia barua ambazo kwa kuwa, baada ya kutoka, zimeelezwa visivyo katika baadhi ya vyombo vya habari, na hata madarasani, nimechukua fursa ya kuzichapisha humu (uk. 45-49) ili wasomaji wetu wajue ukweli wa mambo ulivyo. Kwa sasa hivi, hadi kitabu hiki kilipokwenda mitamboni, tumefikia hapo. Inshallah chochote kitakachotokea baada ya hapo tutakitoa katika vitabu vyetu vijavyo. Na  kuwafikiwa ni  kwa  Mwenyezi  Mungu.

ABDILAHI NASSIR

 Mombasa, Kenya

 Jumadath Thaniya, 1410 Januari, 1990

SAHABA Nl NANI

Moja katika mambo makubwa ambayo kwayo Shia hushambuliwa na kukufurishwa ni lile linalohusu sahaba. Watu huambiwa kuwa wao ati hawawakubali sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w.; ati huwatukana na kuwalaani, na kadhalika! Na huambiwa hivyo kwa lugha kali ya uchochezi na kutia hamasa kwa kiasi ambacho huvuruga akili zao hata wakawa hawasikii tena la mwadhini wala la mteka maji msikitini.

Katika kitabu hiki nimejaribu kujibu yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib, katika kitabu chake, amewatuhumu Shia kwayo kuhusu sahaba, isipokuwa mambo mawili matatu yanayowahusu Khalifa Abubakar na Khalifa Umar b. al-Khattab. Hayo nitayajibu na kuyaeleza katika kitabu chetu kingine kiitwacho Shia na Maimamu, inshallah.

Bila shaka wengi sana wa watu wanaosoma vitabu vyetu hivi, na wale wanaoshughulishwa na maswala haya ya Usunni na Ushia, ni watu wa kawaida; si mashekhe wala si wasomi. Kwa hivyo karibu mara zote maoni yao hutegemea uamuzi wa yule shekhe au msomi wanayemjua wao na kumwamini kuliko wao wenyewe, kwa akili walizopawa na Mola wao, kuzizingatia hoja zinazotolewa na pande zote mbili.

Kutokana na msimamo huu basi, Sunni hukubali lolote linaloamuliwa na shekhe wa Kisunni; na Shia, hali kadhalika, hukubali lolote linaloamuliwa na shekhe wa Kishia — bila ya kujali uzito wa hoja zilizotolewa na wapinzani wao. Na hivyo si Kiislamu! Kiislamu ni kutafakari, kuzingatia, na kuzitia katika mizani hoja tunazopawa, kabla ya kuamua. Qur'ani Tukufu inatuuliza: jee, hamwoni? (Sura 28:72) Hamtii akilini? (Sura 2:44) Hamtafakari? (Sura 6:50).

Kwa kuwa mara nyingi mashekhe wetu hutuzukia na uamuzi wao tu kuhusu mambo mbalimbali ya dini, bila ya kutweleza vipi wamefikia uamuzi huo, na wakatutazamia sisi kuupokea uamuzi wao huo kama kwamba ni wa Mwenyezi Mungu au Mtume Wake s.a.w.w., ndiyo tukawa na vurugu hili tulilonalo! lli tuepukane nalo, kwa hivyo, ni lazima watu wa kawaida wawaambie mashekhe

wao wasizungumze na nyoyo zao bali wazungumze na akili zao. Kwa maneno mengine, mashekhe wasizungumze na wafuasi wao kwa lugha ya kuwachochea na kuwatia hamasa, bali wazungumze nao kwa lugha ya kuwaelimisha; wawaeleze vipi, na kwa hoja gani, wamefikia uamuzi walioufikia. Bila ya hivyo mizozo haitokoma.

lli uelewe kwa nini Sunni na Shia wana misimamo tofauti kuhusu sahaba, kama tulivyoeleza katika kitabu hiki, na ili uweze kujiamulia mwenyewe ni msimamo upi kati ya misimamo hiyo unaokuvutia zaidi, ni muhimu sana tuelewe mitazamo ya madhehebu mbili hizi kuhusu suala hili. Yaani Sunni na Shia anapotaja neno sahaba huwa anamaanisha nini?

Sahaba kwa Sunni

Kwa mujibu wa taarifa ya Imam Ibn Hajar al-Asqalani, iliyomo uk. 10 wa Juzuu ya Kwanza ya kitabu chake kiitwacho al-lsaba, 'sahaba ni yule aliyemkuta Mtume s.a.w.w., akawa amemwamini, na akafa katika Uislamu.' Akaendelea kufafanua kwa kusema: 'Hivyo, kwa waliomkuta (Mtume s.a.w.w.), aingia yule aliyekaa naye muda mrefu au mfupi; (aingia) na yule aliyepokea kwake au hakupokea; (aingia) na yule aliyepigana jihadi pamoja naye au hakupigana; na yule aliyemwona kwa macho japo iwe hakukaa naye, na (hata) yule ambaye hakumwona kwa kizuizi kama (cha) upofu.'

Kisha akasema (katika uk. 13 wa juzuu hiyo hiyo): 'Hakukubaki yeyote katika mwaka wa IO H, Makka wala Taif, ila alisilimu na kuhudhuria Hijja ya Kuagana[2] pamoja na Mtume ...(na) kwamba hakubaki yeyote katika Aws na Khazraj[3], mwisho wa enzi ya Mtume s.a.w.w., ila aliingia katika Uislamu ... wala Mtume s.a.w.w. hakufa kukiwa na yeyote miongoni mwao anayedhihirisha ukafiri.'

Tena Imam Ibn Hajar huyo huyo, katika uk. 5 wa Juzuu ya Saba ya Fathul Bari, amesema kwamba imepokewa kwa Ali b. al-Madini[4] kuwa amesema: 'Yeyote aliyefuatana na Mtume s.a.w.w., au aliyemwona japo ni kwa saa moja mchana, ni miongoni mwa sahaba wa Mtume s.a.w.w.'

Na Imam Nawawi naye, katika uk. 14 wa Juzuu ya Kwanza ya Tahdhibul Asmaa Wal Lugh-ghaat, amesema: 'Kuhusu sahaba kuna madhehebu mbili: lililo muhimu kati yayo — nayo ni madhehebu ya Bukhari na wanazuoni wengine wote wa Hadith, na jamaa katika wanazuoni wa fiqhi na wasiokuwa wao — ni kwamba kila Mwislamu aliyemwona Mtume s.a.w.w. japo ni kwa saa moja, na hata kama hakukaa naye na kuingiliana naye, (ni sahaba).'

Juu ya yote hayo, tunaposoma uk. 4 wa Juzuu ya Saba ya Fathul Bari na uk. 12 wa Juzuu ya Kwanza ya al-lsaba, tunamwona Imam Ibn Hajar al-Asqalani akisema: '...Lau mtu aliritadi, halafu akarejea katika Uislamu, lakini akawa hakumwona (Mtume s.a.w.w.) mara ya pili baada ya kurejea kwake (Uislamuni); lililo sahihi ni kwamba (mtu) huyo huhesabiwa ni sahaba kwa vile ambavyo wanazuoni wa Hadith wamemuhesabu hivyo Ash'ath b. Qays na mfano wake, kati ya waliofikwa na hilo, na kuzitoa Hadith zao katika vitabu vyao vya Hadith ...'

Hata wale waliomwona Bwana Mtume s.a.w.w. utotoni au uchangani (!), na wakawa bado wamo utotoni au uchangani wakati alipofariki dunia, kwa mujibu wa uk. 3 - 4 wa Juzuu ya Saba ya Fathul Bari, ni sahaba! Hii ndiyo sababu mtu kama Muhammad b. Abubakar, mtoto wa Khalifa wa Kwanza, aliyezaliwa miezi mitatu na siku chache kabla ya kufariki Bwana Mtume s.a.yv.w., akahesabiwa kuwa ni sahaba! Na ndiyo sababu pia Imam Hasan

a.s. aliyezaliwa mwaka wa 3H, na Imam Husein a.s. aliyezaliwa mwaka wa 4H, waliokuwa na umri wa miaka 7 na 6 wakati alipofariki Bwana Mtume s.a.w.w., wakahesabiwa kuwa ni sahaba.

Kutokana na taarifa tulizozitaja hapo juu, za wanazuoni wakubwa wakubwa wa Hadith, tunaelewa kwa hivyo — kwa muhtasari — kwamba sahaba kwa Sunni ni:

(i) yeyote yule aliyemwona Bwana Mtume s.a.w.w. na akafa hali yu Mwislamu;

(ii) wala si lazima awe amekaa naye sana, bali hata kama amemwona kwa saa moja tu inatosha;

(iii) na wala si lazima awe ni mtu mzima, bali hata kama alimwona utotoni au uchangani, na hata kama alikuwa bado yu utotoni au uchangani wakati Bwana Mtume s.a.w.w. alipofariki dunia; na

(iv) hata kama mtu huyo aliritadi, kisha akarejea Uislamuni, lakini asiwahi kumwona tena Bwana Mtume s.a.w.w. baada ya kurejea kwake huko!

Hivyo ndivyo anavyoeleweka 'sahaba' kisunni; na ni watu wanaoeleweka hivyo ndio tunao ambiwa tuamini kuwa wote ni waadilifu (taz. uk. 13 humu) na haifai kuwatuhumu kwa ubaya (taz. uk. 30).

Sahaba kwa Shia

Kwa upande wa Shia, neno sahaba halina maana ya kistilahi kama lilivyo kwa Sunni. Kwa hivyo wao hulitumia neno hili kama linavyotumika kilugha.

Kwa mujibu wa lugha ya_Kiarabu (taz. Lisanul Arab na Mufradat ar-Raghib chini ya neno 'sahaba'), neno sahaba ni wingi wa neno sahib. Na neno sahib maana yake ni 'mwenye kuingiliana na kushikamana na (mwingine).' Wala neno hilo 'hatumiliwi isipokuwa yule ambaye mshikamano wake • (na mwenziwe) ni mwingi.' Na ili kuwa sahib wa mtu yahitajia 'kukaa naye kwa muda mrefu.' Pia kwa kuwa suhba (usahibu) huwa ni baina ya wawili, neno hili — katika sentensi—siku zote huunganishwa na jina moja au jingine; na hivyo ndivyo lilivyotumiwa katika Our'ani Tukufu: k.m. sahibayis sijn (Sura 12:39) na as'habu Musa (Sura 26:61); na katika zama za Bwana Mtume s.a.w.w. pia: k.m. sahiburasulillahi au as'haburasuli llahi.

Kwa hivyo kwa Shia 'sahaba wa Mtume s.a.w.w.' ni yule anayetimiza yaliyotajwa katika taarifa ya neno hilo hapo juu.

Daraja yao

Baada ya kuona jinsi taarifa ya neno sahaba inavyotofautiana, baina ya Sunni na Shia, tumebakiwa na swali moja; nalo ni: jee, wote ni waadilifu? Wote wamehifadhiwa na kufanya makosa?

Majibu ya Sunni hapo ni: Ndiyo; sahaba wote ni waadilifu, na wote wamehifadhiwa na kufanya makosa. Hivyo ndivyo anavyotwambia She'kh M. al-Khatib katika kitabu chake.

Lakini Shia wasema: La; sio hivyo. Na wana hoja zao ambazo, japo kwa muhtasari, tumezidondoa katika uk. 13-20 wa kitabu hiki, na ambazo tafadhali zitazame na uzizingatie. Juu ya hoja hizo, kuna na nyingine mbili:

(i)  imani hiyo inapingana na misingi

inayoelezwa katika Qur'ani Tukufu kuhusu wale waliokuwa karibu zaidi na Mitume wa Mwenyezi Mungu kwa jumla kuliko sahaba zao, na Mtume Muhammad s.a.w.w. hasa kuliko sahaba zake; na

 (ii) inapingana na maumbile ya Binadamu yalivyo.

Inavyopingana na Qur'ani Tukufu

Tunapozingatia kwa makini taarifa ya Kisunni, tunaona kwamba kitu cha

pekee kililchofanya sahaba wapawe daraja waliyopawa ya utakatifu, na kuhifadhiwa na kufanya makosa, ni kule kuwa karibu na Mtume s.a.w.w. na kuweza kumwona-japo ni kwa mbali! Hakuna jingine.

Kama ni hivyo basi, hilo halitoshi. Maana tunapoisoma Qir'ani Tukufu tunaona watu waliokuwa karibu zaidi na Mtume Muhammad s.a.w.w. kuliko walivyokuwa sahaba zake kwake, na hata wale wa Mitume wengine, na bado Mwenyezi Mungu hakuwapa daraja ambayo sahaba wamepawa na kina Sheikh M. al-Khatib! Bali tunaona jinsi wanavyo onywa na kukemewa! Kwa mfano:

(i) tunapofungua Sura 11:45-46, tunasoma: 'Nuhu akamlingana Mola wake. Akasema: Mola wangu! Hakika mtoto wangu ni katika watu wangu; na hakika ahadi Yako ni kweli, na Wewe ni Mbora wa wenye kuhukumu.  (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Nuhu! Hakika huyo si katika watu wako. Yeye ni (mwenye) mwendo usiokuwa mwema. Basi usiniombe usilokuwa na ujuzi nalo. Mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga.'

Jee, kama mkuruba tu na Mtume wa Mwenyezi Mungu ndio unaompa mtu utakatifu, yuko aliye karibu zaidi kuliko mtoto wa kumzaa mwenyewe? Mbona hapo Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume Wake, Nuhu a.s., kwamba huyo mtoto wake si miongoni mwa watu wake? Kama mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu aweza kuambiwa kuwa ha miongoni mwa watu wake, kwa sababu tu amemwasi babake, vipi tunawapa utakatifu sahaba (hata kama maasia yao yamethubutu) kwa sababu tu walimwona Bwana Mtume s.a.w.w.? Jee, aliyetokana na damu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na aliyemwona tu, yupi yuko karibu naye zaidi?

Pengine wanafunzi wa Sheikh M. al-Khatib watatwambia kuwa mtoto wa Nabii Nuhu a.s. alikuwa kafiri. Kwa hivyo si sawa kumlinganisha na sahaba waliokufa wakiwa Waislamu. Sawa! Jee, Mwana Fatima, binti ya Mtume Muhammad s.a.w.w.? Hakuwa Mwislamu? Hakumwona Bwana Mtume s.a.w.w.? Hakufa katika Uislamu? Kama alikuwa na yote hayo, juu ya kuwa alikuwa kipenzi cha babake, kwa nini babake s.a.w.w. akamwambia (kama tuelezwavyo katika Hadith mashuhuri): 'Niombe unachotaka katika mali yangu. Lakini, kwa Mwenyezi Mungu, mimi sitokufaa kitu'? Au kwa nini Bwana Mtume s.a.w.w. kusema: 'Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Lau Fatima binti Muhammad angaliiba, ningalimkata mkono wake'? Jee, hayo yote si kuonyesha kwamba kuwa karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu peke yake hakutoshi, kama hakukuandamana na amali njema? Kama Mwana Fatima a.s.

hakupawa utakatifu, naye ni huyo kwa babake s.a.w.w.[5], bali anaambiwa nagalwaga kwamba kitakachomfaa kwa Mola wake ni amali yake, na kwamba akiasi ataadhibiwa, vipi na kwa kipimo gani tunawapa utakatifu huo sahaba kwa sababu tu walimwona Bwana Mtume s.a.w.w.? Na hata kama maovu ya baadhi yao yamethubutu?

(ii) tunapofungua Sura 66:10-11, tunasoma: 'Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wale waliokufuru -mke wa Nuhu na mke wa Luti. Walikuwa chini ya waja Wetu wawili wema miongoni mwa waja Wetu; lakini (wanawake hao) wakawafanyia hiana hao (waume zao), na wao (hao waume) hawakuweza kuwafaa chochote kwa Mwenyezi Mungu. Pakasemwa: Uingieni Moto pamoja na wenye kuuingia. Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano (mwingine) wa wale walioamini-mke wa Firauni; pale aliposema: Mola wangu! Nijengee Kwako nyumba katika Pepo, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake (viovu), na uniokoe na watu madhalimu.'

Haya! Hao hapo wake wawili wa Mitume wa Mwenyezi Mungu-Nabii Nuhu a.s. na Nabii Luti a.s. Kwa sababu hawakuwa na mwendo mzuri, mkuruba wao na Mitume hao haukuwafaa kitu, bali watatiwa Motoni! Sasa ikiwa ni hivyo kwa wake wa Mitume, kwa nini tuambiwe haiwi hivyo kwa rafiki (sahaba) zao?

Kwa nini tuambiwe tusiwatuhumu sahaba kwa ubaya hata kama wamefanya ubaya? Angalia kwenye aya hizo jinsi Mwenyezi Mungu alivyomhukumu kwa wema mke wa mtu mwovu mno (Firauni), akawahukumu kwa uovu wake wa watu wema mno (Mitume)! Yote hayo ni kutuonyesha kwamba kuwa karibu na mtu mwema hakufai kitu kama wewe mwenyewe si mwema, kama ambavyo kuwa karibu na mtu mwovu hakudhuru kitu kama wewe mwenyewe si mwovu. Na hivyo ndivyo inavyotakikana tuwapime sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w. Wale waliothubutu kuwa ni wema, tuwape haki yao. Na wale waliothubutu kuwa ni waovu, tuwape stahili yao. Hivyo ndivyo Kishia, na ndivyo ki-Qur'ani, kama tunavyoona. Maana kama mkuruba peke yake haukuwafaa watoto na wake za Mitume wa Mwenyezi Mungu, walio karibu zaidi nao, vipi utawafaa sahaba zao kwa sababu tu waliwaona?

Pengine na hapo wanafunzi wa Sheikh M. al-Khatib watatwambia tena kuwa wake wa hao Mitume wawili, waliotajwa hapo juu, walikuwa ni makafiri.

Vipi tunawalinganisha na masahaba? Sawa! Jee wake wa Mtume Muhammad s.a.w.w.; hawakuwa Waislamu? Hawakuwa ma mama wa waumini? Mbona Mwenyezi Mungu amewawekea sharti ya ucha-Mungu (Sura 33:32) ndipo wapate daraja yao, kwa kuwaambia: 'Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama yeyote kati ya wanawake, kama mtamcha Mwenyezi Mungu...' Hili ni kutuonyesha kwamba kama hawatakuwa na mwendo mwema (hawatamcha Mola wao), basi ile kuwa ni wake wa Mtume tu hakutawafaa kitu. Bali ikizidi, kama watafanya machafu yoyote, inatakikana adhabu yao iwe maradafu-kama inavyoelezwa kwenye Sura 33:30. Na hivyo ndivyo inavyotakikana tuwe kwa masahaba.

Badala ya kuambiwa tusiyataje maovu yaliyofanywa na masahaba, na tusiwatuhumu kwayo yanapothubutu kwetu, inataka tuwalaumu na kuwahukumu vikali- kama wanavyofanya Shia. Maana kama wao-waliokaa na Bwana Mtume s.a.w.w. na kupokea kwake maadili yote-hawatatwekea ruwaza njema, nani mwingine atatufanyia hilo? Na jee, kama hatutawatuhumu kwa yale maovu waliyoyatenda, watu wengine si watayachukulia kuwa ni mema kwa sababu tu yamefanywa na sahaba wa Mtume s.a.w.w.-hasa kwa hivi ambavyo, Kisunni, mwendo wa baadhi ya sahaba[6] wa Bwana Mtume s.a.w.w. huhesabiwa kuwa ni sunna?!

Kutokana na aya mbili tatu tulizozitaja hapo juu, nataraji nimeweza kuthibitisha kwamba ule mtazamo wa kuwa sahaba wote ni waadilifu, baada ya kuambiwa kwamba sahaba ni yule aliyemwona Mtume s.a.w.w-japo kwa mbali-na akafa ni Mwislamu, ni mtazamo unaopingana na Qur'ani Tukufu na mafunzo ya Bwana Mtume s.a.w.w. Kwa hivyo Shia hawaukubali. Sasa tutazame jinsi mtazamo huo unavyopingana na ukweli wa maisha yao wenyewe hao masahaba.

Inavyopingana na maumbile ya Binadamu

Kwa malezi tuliyolelewa sisi katika Usunni, kila tunapotajiwa sahaba husahau, au huwa hatutaki kukumbuka, kuwa tumetajiwa binadamu. Kwa namna moja au nyingine, hudhania kwamba tunazungumza ya viumbe vya aina ya kipekee! Na hapo ndipo penye shina la tatizo letu kuhusu watu hawa. Kama tungalikuwa tunatambua kwamba wao ni binadamu-si majinni wala si malaika-bila shaka leo pasingalikuwa na hitilafu hii iliyoko baina ya Sunni na Shia kuhusu viumbe hivi.

Lakini ukweli ni kwamba sahaba wote ni binadamu; na kama binadamu wote walivyo-tangu hapo kale hadi leo-kuna wema na wawi. Wale walioinukia na wema, kama wale walioinukia na uovu, lazima wabakiwe na tabia yao hiyo kwa muda; haiwezi kuondoka yote vuu pwaa, hata kama watajaribu kubadilika. Maana, kimaumbile, hakuna binadamu ambaye tabia yake hubadilika yote mara tu anapoingia katika dini fulani. Ni lazima achukue muda katika dini hiyo, na azitabiki sheria zake na misingi ya imani zake, ndipo tutakapokuwa na kipimo sahihi cha ubora wake.

Pengine tutalielewa vizuri jambo hili tunapochukua mifano ya watu wawili: mmoja kafiri (Abu Jahl), na mmoja sahaba (Abu Sufyan).

Wote watu wawili hawa walikuwa ni mabwanyenye wa Kikureshi waliokiwanyonya wanyonge wao, na kuwatesa. Wote wawili, kwa hali na mali, walikuwa ni maadui wakubwa wa Bwana Mtume s.a.w.w. Kwa bahati mbaya Abu Jahl aliuawa katika Vita vya Badr (mwaka 2H) akiwa upande wa makafiri, hali Abu Sufyan (kwa bahati nzuri) aliwahi kusilimu kabla ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia-ingawa kusilimu kwenyewe kulikuwa ni katika mwisho mwisho wa maisha ya Bwana Mtume s.a.w.w., baada ya kutekwa Makka, na ni kwa kukosa budi. Hivyo Abu Jahl akafa tukiwa hatujui wema wake hata mmoja, isipokuwa uovu na aibu; na Abu Sufyan naye akafa tukiwa hatujui (wala haturuhusiwi kukumbuka) uovu wake hata mmoja, isipokuwa wema na sifa! Kwa nini? Kwa sababu Abu Jahl alisadifu kufa akiwa kafiri, na Abu Sufyan akasadifu kufa akiwa sahaba. Hilo tu!

Lau Abu Jahl angalinusurika katika Vita vya Badr, kisha akabaki hai mpaka siku ya kutekwa Makka, na akasilimu, bila shaka angalikuwa ni miongoni mwa sahaba au viongozi wao-hata kama hangaliwahi kupigana vita vyovyote kuutetea Uislamu!

Lakini  jee  usahaba,  kwa  namna  hii  unavyoarifishwa  na  Sunni  (kama tulivyoona  katika  uk.4 huko  nyuma),  huweza  kumgeuza  mwovu  akawa mwema kwa haraka hivyo? Hasha! Na ushahidi ni wake yeye, yuyo huyo, Abu Sufyan!

Tunaposoma al-Fitnatul Kubra ya Twaha Husein (uk. 19 wa Juzuu ya Pili) tunaona, anapozungumzia suala la uchaguzi wa Khalifa baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia, anasema: 'Na pale palikuwako mtu mwingine miongoni mwa makureshi aliyetaka kumbai Ali baada ya Mtume kufariki-sio kwa kumpenda wala kumridhia, wala si kwa kuitambua daraja yake

maalum (aliyokuwa nayo) kwa Mtume, bali kwa ajili ya kuunga ujamaa wa  ukoo wa Abdi Manafi. Mtu huyo ni Abu Sufyan, kiongozi wa makureshi katika vita vyao na Mtume, na upinzani wao dhidi ya Uislamu, na ambaye

hakusilimu isipokuwa kwa kukosa  budi alipoyaona majeshi ya Waislamu yameizunguka Makka. Hapo Abbas akaenda naye kwa Mtume, akasilimu kwa kukosa budi, sio kwa hiari. Yeye hakusita kutambua kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu kwa sababu hakuona ubaya wa kulitambua hilo.

Lakini alipotakikana ashahidie kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, alisema: Ama kwa hili, nina kitu katika nafsi yangu. Na lau kama si  Abbas  kumhimiza  na  kumtisha  kuuwawa,  asingaliikubali shahada  hii aliyokuwa na kitu nayo ndani ya nafsi yake.'

Tunapokuja kwa Abbas Mahmud al-Aqqad naye, katika uk. 26 - 27 wa kitabu chake kiitwacho Abus Shuhadaa: al-Husayn Bin Ali, anatwambia: 'Abu Sufyan na mwanawe, Muawiya, walisilimu ilipotekwa Makka. Na kusilimu kwa nyumba yake (Abu Sufyan) ndiko kulikokuwa kusilimu kugumu mno kulikojulikana, baada ya Makka kutekwa.'

Na kabla ya hapo amesema: 'Kisha Makka ikatekwa. Abu Sufyan akasimama analitazama jeshi la Waislamu na huku anamwambia Abbas b. Abdilmuttalib: Wallahi, ewe Abul Fadhl, ufalme wa mtoto wa ndugu yako umekuwa mkubwa leo. Na Abbas alipomwambia: Huo ni Utume, (Abu Sufyan) alimjibu: Ndio! Sasa?

'Abu Sufyan akaendelea kwa muda, baada ya kusilimu kwake, anachukulia ushindi wa Uislamu ni ushindi dhidi yake. Mara moja akamtazama Mtume alipokuwa msikitini, mtazamo wa mtu aliyedangana na kushangaa, huku akisema na nafsi yake: Natamani ningalijua! Amenishinda kwa kitu gani? Mtume a.s. akaelewa maana ya mtazamo huo. Akamwendea mpaka akamwekea mkono wake baina ya mabega yake, akamwambia: Billahi nimekushinda, ewe Abu Sufyan.'

Huyo ndiye Abu Sufyan. Hivyo ndivyo alivyosilimu. Na hivyo ndivyo alivyokuwa, baada ya kusilimu na kuwa sahaba. Jee mtu kama huyo, pamoja na vihendo vyote hivyo, bado tutamhesabu ni mwadilifu kwa sababu tu

alisilimu na kumwona Bwana Mtume s.a.w.w.?

Sunni wasema: Ndio! Shia wasema: La! Jee wewe, ndugu msomaji, unaonaje?

Sasa tuendelee na madai mingine ya Sheikh M. al-Khatib.

SAHABA KWA SUNNI

1. Katika uk. 30 wa kitabu chake, Sheikh M. al-Khatib amesema hivi kuhusu sahaba: Ahlil sunnah wanaafikiana juu ya kuwahishimu na kuwaombea radhi za Mungu...

Majibu: Hata Shia ni vivyo hivyo; na ushahidi wa hilo ni ile dua waliyonayo wao ya kuwaombea Mwenyezi Mungu sahaba wa Mitume wote kwa jumla, na wale wa Mtume Muhammad s.a.w.w. hasa, ambayo tafsiri yake ya Kiswahili ni kamaifuatavyo:

"Ewe Mola! Wabariki wafuasi wa Mitume yote na wale wenye kuwasadikisha katika mambo ya ghaibu-miongoni mwa wakaazi wa dunia hii- wakati wapinzani wao wanapowapinga kwa kuwakadhibisha hali wao wana hamu ya (kuwaona) Mitume kwa imani ya kweli, katika kila wakati na zama ambapo ulituma Mtume na ukawasimamishia watu wake dalili-kuanzia kwa Adam mpaka kwa Muhammad s.a.w.w.-ya maimamu wa uongofu na viongozi wa wacha-Mungu, amani iwe juu yao wote. Tafadhali wakumbuke (wote) hao kwa maghfira na radhi zitokazo Kwako.

Ewe Mola! Wabariki na sahaba wa Muhammad hasa, ambao waliandamana naye kwa wema, na ambao walipigana kishujaa katika kumnusuru, wakamsaidia na kufanya haraka katika kuunga mkono ujumbe wake na kuuitikia mwito wake, waliomwitikia mara tu alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake, wakajitenga na wake (zao) na watoto (wao) katika kulidhihirisha neno lake, wakapigana na baba (zao) na watoto (wao) katika kuthibitisha utume wake, na wakanusurika kwaye.

Wabariki na wale waliozama katika kumpenda yeye, waliokitarajia biashara isiyoweza kuharibika ya mapenzi (yao) kwake.

Wabariki na wale ambao jamaa zao waliwahama pale waliposhikamana na makubadhi yake, na (wale ambao) akraba (zao) waliwakimbia pale walipokaa chini ya kivuli cha akraba zake.

Basi usisahau, ewe Mola, yale waliyoyaacha kwa ajili Yako katika Njia Yako. Wape radhi Zako kwa kuwakusanya viumbe Vyako katika (dini) Yako, na kwa kuwa walinganaji Wako pamoja na Mtume Wako, (waliolingania watu) Kwako. Uwalipe kwa kuyahama majumba ya watu wao kwa ajili Yako, na kwa kutoka kwenye maisha ya ufanisi na kuingia katika yale ya dhiki, na kwa mateso mengi yaliyowapata katika kuitukuza dini Yako.

Ewe Mola! Uwafikishie bora ya malipo Yako wale waliowaandama wao kwa wema, ambao walikisema: Mola wetu, tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani-walioamua kufuata njia yao iliyo wazi na kuelekea mwelekeo wao, wakafuata nyayo zao; ambao shaka haikuwatoa katika dini yao wala haikuwababaisha katika kuzifuata njia zao na kuongoka kwa uongozi wao. huku wakiwasaidia na kuwatia nguvu; waliofuata dini yao na kuongoka kwa kiongozi wao, wakawafikiana nao bila ya kuwatuhumu katika yale waliyowafikishia.

Ewe Mola! Warehemu na waandamizi wa masahaba, kutoka siku yetu hii mpaka Siku ya Malipo. (Uwarehemu) na wake zao, vizazi vyao, na wale waliokutii Wewe miongoni mwao, kwa rehema ambazo kwazo utawakinga na kukuasi Wewe, utawakunjulia bustani za Pepo Yako, utawakinga Kwazo na vitimbi vya Shetani na kuwasaidia katika mema waliyokuombea msaada, utawakinga na vituko vya usiku na mchana isipokuwa kituko kiletacho kheri, uwapelekee kwazo kuwa na imani ya kutarajia mema Kwako, kuwa na tamaa ya yaliyoko

Kwako, na kuacha kutuhumu yale yaliyomo mikononi mwa waja Wako ili uwarejeze katika kujipendekeza Kwako na kukuogopa, (na ili) uwafanye waupe mgongo ufanisi wa dunia hii na kuwapendekezea kuiendea mbio Akhera na kujitayarisha kwa yaliyoko baada ya mauti, (ili) uwafanyie jepesi kila zito litakalowazunguka siku ya roho kutoka miilini mwao, uwaafu na makatazo yote yale ambayo huletwa na mitihani, (uwaafu) na mateso ya Moto na kubaki humo milele, na (ili) uwapeleke kwenye amani ya makaazi ya wacha Mungu."

Jee, Sunni wanayo dua kama hiyo? Kama wanayo, tutafurahi kuijua. Kama hawana, basi vipi Sheikh M. al-Khatib ataweza kujigamba kuwa wao peke yao ndio wanaowaheshimu sahaba na kuwaombea radhi za Mwenyezi Mungu? Jee, baada ya kuisoma dua hiyo na kuielewa, bado unaweza kufikiri kwamba Sunni peke yao ndio wanaowaheshimu sahaba na kuwaombea radhi za Mwenyezi Mungu?

Kama wataka kukiona Kiarabu cha dua hiyo, tafadhali tazama uk. 52-50 humu; na kama wataka kuzijua dua nyingine ambazo Shia huziomba, pata kitabu kiitwacho Sahifa Sajjadiyya.

Sahaba wote ni waadilifu?

2. Akaendelea kusema (katika huo huo uk. 30) kwamba ni imani ya Sunni kuwa:

...wao (yaani sahaba) ni waadilifu wote...

Majibu: Hapo ndipo penye hitilafu baina ya Sunni na Shia; maana Shia hawaamini hivyo.   Waaminivyo wao ni kwamba baadhi tu ya sahaba ndio waadilifu, na baadhi nyingine si waadilifu; na kwa hilo wana ushahidi wa mambo yaliyofanywa na sahaba hao ambayo kwayo,  kwa mtu yeyote atumiaye akili yake, hawawezi kubaki kuwa waadilifu. Na hapa chini tunataja mifano michachetu kuthibitisha hilo:

(i) Qudama b. Madh'un: Huyu ni miongoni mwa Waislamu wa mwanzo mwanzo. Alihama hijra mbili, akawahi hata kupigana katika Vita vya Badr. Lakini pamoja na yote hayo aliwahi kushikwa amelewa, zama za Ukhalifa wa Umar b. al-Khattab, akapigwa haddi! Jee, sahaba huyu bado ni mwadilifu? (Taz. al-lsaba, Juzuu ya Tatu, uk. 219-221; na al-lsti'ab, iliyo chini ya al-lsaba, Juzuu ya Tatu, uk. 247-251)

(ii) Abdulrahman (al-Awswat) b. Umar b. al-Khattab: Huyu, kama jina lake lionyeshavyo, alikuwa ni mtoto wa Khalifa wa Pili, na alikuwa ni sahaba vile vile. Yeye naye alikamatwa amelewa, na babake akampiga haddi! Hata inasemekana kwamba alikufa kwa kipigo hicho. (Taz. uk. 405-406 wa Juzuu ya Pili ya al-lsaba; na uk. 395-396 wa Juzuu ya Pili ya al-lsti'ab, iliyo chini ya al-Isaba) Jee, na huyo naye atakuwa ni mwadilifu? Kwa kipimo gani?

(iii) Abu Mihjan: Huyu ni sahaba mwingine aliyekuwa akinywa pombe sana na kuzini; hata imeeelezwa kwamba Khalifa Umar b, al-Khattab aliwahi kumpiga viboko mara saba au nane kwa hilo! Akawahi hata kumfunga! (Taz. al-lsaba, Juzuu ya Nne, uk. 173-175; na uk. 181-187 wa Juzuu ya Nne ya al-lsti'ab iliyo chini ya hiyo al-lsaba.) Jee, sahaba kama huyo vipi huendelea kuwa mwadilifu?

(iv) Nu'aiman b. Amr. Huyu ni sahaba ambaye amepigana jihadi vita vyote. Lakini pamoja na hivyo, alikuwa mlevi! Mara nne Mtume Muhammad' s.a.w.w. alimkamata sahaba huyo amelewa! Kati ya hizo, mara tatu alimpiga haddi! Mara ya nne, ndipo Umar b. al-Khattab alipotaka akatwe kichwa chake, lakini Bwana Mtume s.a.w.w. hakumkubalia. (Taz. chini ya jina la Marwan b. Qais al-Aslami katika uk. 384 wa Juzuu ya Tatu ya al-lsaba; na pia juzuu hiyo hiyo, uk. 540-541, chini ya jina la huyo Nu'aiman. Vile vile taz. Usudul Ghaba, Juzuu ya Nne, uk. 199 - 200, na Juzuu ya Tano, uk. 36 - 37.) Haya! Jee?

(v) Samura b. Jundub: Huyu ni mmoja ya wale watu watatu walio ambiwa na Bwana Mtume s.a.w.w. kwamba, wa mwisho wao kufa, ataingia Motoni. Yeye alikiuza pombel (Taz. chini ya Hadith Na. 61 katika uk. 82-84 wa Mujallada wa Kwanza wa Silsilatul Ahadithidh Dhaifa Wal Mawdhu'a ya Muhammad Nasiruddin al-Albani.) Bado huyo ni mwadilifu?

(vi) al-Walid b. Uqba: Huyu ndiye  yule  ambaye Mwenyezi Mungu amemwita fasiq katika Sura 32:18 na Sura 49:6. Isitoshe; na ndiye yeye, pale alipokuwa Gavana wa Kufa zama za Ukhalifa wa Uthman b. Affan, aliyeswalisha watu swala ya asubudhi rakaa nne, na huku amelewa! Kisha akatapika kibulani, akatoa salamu na kuwauliza walioswali naye: Jee, niwaongezee? Kwa hivyo akapigwa haddi na kuondolewa kwenye Ugavana!

Kuhusu Sura 49:6, amesema Ibn Abdilbar kwamba hakuna hitilafu baina ya wanazuoni kuwa aya hiyo iliteremshwa kwa ajili yake (al-Walid b. Uqba). Hayo utayapata katika uk. 601 wa Juzuu ya Tatu ya al-lsaba. Na katika ukurasa huo huo, wa kitabu hicho hicho, amesema Ibn Hajar al-Asqalani: 'Kisa cha yeye kuswalisha watu asubuhi rakaa nne, ni mashuhuri; na kisa cha kuuzuliwa kwake baada ya kuthubutu kwamba amekunywa pombe, ni mashuhuri vile vile, na kimetolewa katika Sahih Mbili (yaani Bukhari na Musliml. Na Uthman alimwuzulu Kufa baada ya kumpiga viboko, akamtawalisha Said b. al-As (mahali pakeh' Jee? Huyo naye pia ni mwadilifu?

Hiyo basi ni mifano michache tu ya baadhi ya masahaba wa Mtume Muhammad s.a.w.w. na maasia yao! Na vyote visa vyao hivyo tumevitoa katika vitabu vya Kisunni; hapana kitabu hata kimoja cha Kishia hapo! Sahaba kama hao ndio ambao Shia hukataa kuwa ni waadilifu; na ni sahaba kama hao ndio ambao Sunni hushikilia kuwa ni waadilifu kwa sababu kwao, kama alivyosema Sheikh M. al-Khatib, sahaba wote ni waadilifu! Sasa mambo yakiwa ni hivyo, upi kati ya misimamo miwili hiyo ndio wa sawa? Wa kuwa sahaba wote ni waadilifu; au wa kuwa sio wote ni waadilifu? Jiamulie mwenyewe, ewe ndugu yangu.

Hapa napenda ijulikane kwamba kuna visa vingine k.w.k., vinavyowahusu masahaba wakubwa wakubwa, ambavyo nimeviacha kwa makusudi. Na sababu ya kutovitaja ni kwamba ninaamini kuwa wengi sana wa wasomaji wa maandishi haya hawajawa tayari kupokea visa hivyo! Hata hivyo, kama nitalazimishwa, sitakuwa na budi isipokuwa kuvieleza: japokuwa shingo upande.

Utabiri wa Mtume s.a.w.w. kuhusu sahaba

Na sio kwamba sahaba walifanya maasia tu, kama tulivyokwisha kuona hapo juu, bali Bwana Mtume mwenyewe (s.a.w.w.) alikwisha kutabiri, kabla ya kutawafu kwake, kwamba baadhi ya sahaba zake watazua mambo katika dini hii na kuibadilisha. Na yote hayo yamo katika vitabu vinavyotegemewa sana na Sunni! Hapa chini tunakutajia machache tu (sio yote) yaliyomo katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim:

(i) Imepokewa kwa Anas kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Watu miongoni mwa sahaba zangu watanijia kwenye Hodhi[7]. Nitakapowaona, na watakapokuwa waletwa kwangu, watazuiwa ili wasinifikie. Hapo nitasema: Sahaba zangu, sahaba zangu! Nami nitaambiwa: Wewe hujui walizua nini baada yako.

Hadith hiyo utaiona katika Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina s.a.w.w. Waswifatuhu.' Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 5706 kwenye uk. 1239 wa Juzuu ya Nne.

Hali kadhalika, Hadith yenye maneno karibu kama hayo yaweza kuonekana katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'. Na kwa Kiingereza, ni Na. 584 kwenye uk. 381 wa Juzuu ya Nane.

(ii) Imepokewa kwa Abu Hazim kwamba amemsikia Sahl (b. Sa'd) akisema kwamba amemsikia Mtume s.a.w.w. akisema: Mimi nitawatangulia nyinyi kwenye Hodhi. Atakayekuja, atakunywa. Na atakayekunywa, hatasikia kiu abadan. Na watanijia watu ninaowajua, na wao wananijua. Kisha pataingiwa kati baina yangu na wao.

Abu Hazim asema: Nu'man b. Abi Ayyash akanisikia nikiitoa Hadith hii. Akasema: Hivyo ndivyo ulivyomsikia Sahl akisema? Nikasema: Ndio. Naye akasema: Na mimi nashuhudia kwamba nimemsikia Abu Said al-Khudri akisema vivyo hivyo, lakini yeye alizidisha kwamba (Mtume s.a.w.w.) atasema: Hao ni (watu) wangu. Naye ataambiwa: Wewe hujui walifanya nini baada yako. Hapo nitasema: Ole wake! Ole wake, mwenye kuibadilisha (dini yake) baada yangu.

Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabul Fitan', Mlango wa Kwanza. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 174 iliyoko uk. 144 wa Juzuu ya Tisa. Na katika Sahih Muslim utaipata katika 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina s.a.w.w. Waswifatuhu.' Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 5682 iliyoko uk. 1236 wa Juzuu ya Nne.

(iii) Imepokewa kwa Abdullah kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Nitawatangulia kwenye Hodhi; na watu miongoni mwenu watainuliwa (niwaone). Kisha watazuiwa (kunifikia). Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! Ni sahaba zangu (hao). Nitaambiwa: Wewe hujui walizua nini baada yako.

Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 578 iliyoko uk. 378 - 379 wa Juzuu ya Nane.

(iv) Amesema Abduliah kwamba Mtume s.a.w.w. amesema:  Mimi nitawa tangulia kwenye Hodhi (ambapo) watu miongoni mwenu watainuliwa

(niwaone).  Nitakapotaka kuwafikia, wataondelewa (nisiwafikie)! Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! Ni sahaba zangu (hao). Naye atasema: Wewe hujui walizua nini baada yako.

Hiyo ni Hadith ya pili katika 'Kitabul Fitan' ya Sahih Bukhari. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 173 iliyoko uk. 144 wa Juzuu ya Tisa.

(v) Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Umma wangu utanijia kwenye Hodhi; nami nitafukuza watu (siku hiyo) kama mtu anavyofukuza ngamia wa watu (asichanganyike) na ngamia wake. (Waliokimsikiliza) wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, utatujua? Akajibu: Ndio, mtakuwa na alama ambayo mtu mwingine yeyote asiyekuwa nyinyi, atakuwa hana. Mtanijia na paku jeupe juu ya mapaji yenu ya uso, na alama nyeupe juu ya miguu yenu kwa ajili ya athari za udhu. Lakini kundi kati yenu litazuiwa kunifikia. Nami nitasema: Ewe Mola wangu! Hao ni sahaba zangu. Malaika atanijibu kwa kusema: Jee wajua walizua nini baada yako?

Hiyo ni Hadith ya 'Kitabut Twahara', Mlango wa 'lstihbabu Itwalatil Ghurrati Wat Tahjili Fil Wudhui' katika Sahih Muslim. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.480 iliyoko uk. 156-157 wa Juzuu ya Kwanza.

(vi) Imepokewa kwa Abdullah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Mimi nitawatangulia kwenye Hodhi; na nitawatetea watu lakini nitashindwa. Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! Sahaba zangu, sahaba zangu. Na patasemwa: Wewe hujui walizua nini baada yako. Hiyo ni Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 5690 iliyoko uk. 1238 wa Juzuu ya Nne.

Mpaka hapa tumeona Hadith sita (nyingine tumeziacha!) zinazotufahamisha kwamba kesho Akhera, wakati Bwana Mtume s.a.w.w. atakapokuwa kwenye Hodhi, baadhi ya sahaba zake watazuiwa kumfikia yeye; na atakapokumbusha kwamba hao ni sahaba zake, ataambiwa kwamba yeye hajui sahaba hao walizua nini baada yake! Hivyo ni kusema kwamba kuna baadhi ya sahaba amoao, baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia, walizua mambo kinyume cha dini yake; ndiyo sababu wasiruhusiwe kumfikia hata baada ya yeye mwenyewe kukumbusha kwamba hao walikuwa sahaba zake! Jee, sahaba wa aina hiyo bado wangali waadilifu? Jee, aliye mwadilifu hutengwa na Bwana Mtume s.a.w.w.? Huambiwa 'ole wake', kama ilivyo kwenye Hadith Na. (ii) hapo juu?! Neno ole! huambiwa mtu mwema au mwovu?

Kutokana na Hadith hizo basi, ni wazi kwamba sio sahaba wote ni waadilifu. Na vivyo hivyo ndivyo inavyoeleweka kutokana na aya k.w.k. za Qur.'ani Tukufu.

Hata Qur'ani Tukufu yasema vivyo. lli  tusije  tukakifanya kirefu sana kitabu hiki, hapa chini  tunataja  aya chache tu zinazoonyesha kwamba si sahaba wote waliokuwa waadilifu:

(i) Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema (Sura 9:43): 'Mwenyezi Mungu amekusamehe. Kwa nini umewapa ruhusa? (Ungengoja) mpaka wale wanaosema kweli wakupambanukie, na uwajue waongo.'

Jee, kutokana na aya hiyo[8], si wazi kwamba miongoni mwa sahaba kulikuwa na wakweli na waongo? Ikiwa wakweli ni waadilifu, jee na hao waongo pia huwa waadilifu kwa sababu tu ni sahaba?

(ii) Amesema tena (Sura 8:15-16): 'Enyi mlioamini! Mnapokutana vitani na wale waliokufuru, basi msiwageuzie migongo. Yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo-isipokuwa kama amegeuka ili kushambulia, au amegeuka ili kuungana na sehemu nyingine (ya jeshi lake)-basi huyo atastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake ni Jahannam. Napo ni marejeleo mabaya'.

Hizo ni aya mbili zilizowaonya sahaba wasikimbie vitani. Maana yeyote miongoni mwao atakayefanya hivyo, isipokuwa kwa nyudhuru mbili zilizotajwa hapo, bila shaka atastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mugu, na makaazi yake ni Jahannam!

Sasa hapa maswali yetu ni haya. Jee, katika historia ya Uislamu, hawakupatikana sahaba waliokimbia vitani? Bila shaka walipatikana. Kama ni hivyo, si wazi basi kwamba sahaba hao walistahiki ghadhabu za Mwenyezi Mungu, na makaazi yao ni Jahannam  kama inavyoelezwa katika aya hizo? Jee, mtu anayeghadhibikiwa na Mwenyezi Mungu na kutiwa Jahannam, bado ni mwadilifu?

 (iii) Akasema tena (Sura 9:56): 'Na wanaapa kwa (jina la) Mwenyezi Mungu kwamba wao ni miongoni mwenu, wala wao si miongoni mwenu. Bali wao ni watu wanaoogopa.'

Wazi kabisa hapo kwamba kulikuwa na watu, waliokuwa pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w., waliokidhihirisha Uislamu na kuficha kinyume chake! Jee watu aina hiyo huwaje wote waadilifu? Bila shaka hao ni wanafiki, kama tuelezwavyo katika aya ifuatayo:

(iv) Amesema Mwenyezi Mungu s.w.t. (sura 9:101): 'Na miongoni mwa mabedui wanaokaa pambizoni mwenu, mna wanafiki; na katika wenyeji wa Madina (pia). Wamebobea katika unafiki. Wewe huwajui; (lakini) Sisi tunawajua...'

Hapa Mwenyezi Mungu anatweleza wazi wazi kwamba miongoni mwa wale waliokuwa pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. (ambao ndio hao 'sahaba') walikuwamo  waumini  na  wanafiki. Na  kwamba  hao wanafiki,  yeye Bwana Mtume s.a.w.w. hakiwajua!  Aliyekiwajua ni Yeye Mwenyewe s.w.t. Kwa hivyo, baadhi yao waliendelea kuwamo miongoni mwa sahaba mpaka Bwana Mtume s.a.w.w. akafariki dunia.

Hilo, kwa mfano, li dhahiri mno kutokana na kisa kimoja tu; kisa cha Vita vya Uhud. Imam at-Tabari (katika uk. 504 wa Juzuu ya Pili ya Taarikh yake) na Ibn Hisham (katika uk. 17 wa Juzuu ya Tatu ya as-Siratun Nabawiyya) wamesema kwamba wakati Bwana Mtume s.a.w.w. alipotoka Madina na jeshi lake kwenda Uhud, alitoka na sahaba elfu moja. Lakini Abdullah b. Ubayy b. Salul alimkimbia Bwana Mtume s.a.w.w., akarejea Madina na watu mia tatu[9]. Watu mia tatu hao ni kina nani? Hakuna mahali tulipotajiwa majina yao isipokuwa hilo moja tu la kiongozi wao! Kwa hivyo tuna hakika gani kwamba wanafiki hawamo miongoni mwa hao sahaba tunaoambiwa na Sheikh M. al-Khatib kwamba wote ni waadilifu?

KutoKana na ushahidi mchache tulioutoa hapo juu kutoka katika Qur'ani na Hadith na historia, itadhihiri kuwa si sahaba wote waliokuwa waadilifu, wala si sahaba wote waliokuwa si waadilifu. Kunabaadhi yao waliofikia kilele cha ucha Mungu.  Kuna na baadhi waliokuwa wakweli, lakini hawakuwa waadilifu. Kuna na baadhi nyingine ambao hali zao hazikijulikana; na wengine wakijulikana hasa kwamba walikuwa na mambo ya kimatata matata! Na hiyo ndiyo imani ya Kishia. Maana kushikilia tu kuwa sahaba wote ni waadilifu ni kuwatoa katika ubinadamu!

Pia ikumbukwe  kwamba  hapa  hatukugusia wale walioritadi[10] baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia. Ya hao tumeyaeleza uk.36 humu.

Maafa ya imani hii

Mbali na kwamba ni kinyume na Qur'ani Tukufu, Hadith za bwana Mtume s.a.w.w., na hata matukio ya kihistoria, imani hiyo ya kwamba sahaba wote ni waadilifu imeiletea dini yetu ya Kiislamu maafa mawili makubwa:

Kwanza, imeugawanya umma wetu; si katika mambo ya akida tu, bali hata yale ya ibada na ya maingiliano (mu'amalaat)[11].

Kwa kuwa sahaba wamekuwa na kauli tofauti tofauti juu ya mambo hayo, na wakati mwingine kauli zinazo gongana hasa; na kwa kuwa inatakikana iaminiwe kwamba wote ni waadilifu, tumelazimika kuyakubali yote yanayotokana na wao bila ya kupinga! Bali bila ya hata kutumia akili zetu! Hivyo tunajikuta wengine tunaamini kwamba Mwenyezi Mungu haonekani-[12] wengine aonekana[13]! Wengine tunaamini Mwenyezi Mungu yuko juu ya Arshi Yake iliyoko mbinguni huko[14]; kwa wengine Mwenyezi Mungu hayuko mahali maalum[15]. Wengine tunaposwali tunafunga mikono[16]; wengine hatufungi[17], na kadhalika[18].  Na kila kundi linaamini kuwa loo peke yake ndilo lililomo katika haki!

Pili. imesababisha dini yetu kutukanwa na kudharauliwa kwa sababu ya vituko vituko na maajabu ajabu yaliyomo katika vitabu vyetu vya Hadith, kama tulivyoona (kwa mfano) katika uk. 16-32 wa kitabu chetu, Shia na Hadith.

Kwa kuwa Hadith kama hizo zimesimuliwa na masahaba; na kwa kuwa tunalazimishwa  kuamini  kwamba sahaba wote ni waadilifu,  huwa haturuhusiwi, bali hatuthubutu kamwe, kuwa hata na shaka na Hadith kama hizo- tusije tukatoka Uislamuni!  Matokeo yake ni nini? Ni kuziamini na kuzitetea, potelea mbali tuwe vichekesho!

Hatari kubwa!

Pengine, katika kumalizia nukta hii, ingekuwa vyema kama ningedokezea hatari kubwa inayoweza hata kutikisa moja ya misingi mikubwa ya Uislamu, kama watu wataendelea na 'imani ya kwamba sahaba wote ni waadilifu. Maana imani hii ndiyo iliyozalisha ile imani ya kwamba 'kila kilichomo katika Bukhari ni sahihi', kama tulivyoona katika uk. 17 wa kitabu chetu , Shia na Qur'ani.

Kama tutaamini hivyo (na hivyo ndivyo inavyotakiwa Sunni wote waamini) itabidi tuamini kwamba kitabu hicho hakina kosa! Kwa hivyo itabidi, tutake tusitake, tuamini kuwa ki sawa na Qur'ani Tukufu! Maana ni imani ya Waislamu kwamba kitabu, kilicho sahihi chote, ni Qur'ani peke yake. Sasa, kama tutaiongeza na Bukhari, haitakuwa tumeiwekea Qur'ani mwenzake? Jee, hivyo ni sawa? Twataraji tutaelezwa.

Jee, ni mambo ya ijtihadi?

3. Akaendelea kusema (katika huo huo uk. 30) kwamba Sunni huzingatia:

tafauti zote zilizozuka kati mwao (yaani sahaba) kuwa ni mambo ya ijitihadi[19] ambayo walifanya kwa ikhlaswi...

Majibu: Shia hawazingatii hivyo! Wao huzingatia jambo kuwa ni ijtihadi pale tu linapokuwa halipingani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya

Mtume Wake s.a.w.w. Linapopingana na mojawapo ya vitu viwili hivyo, au vyote viwili,  basi jambo  kama  hilo  'kwa  Shia)  huwa  ni  kosa moja  kwa. Moja-hata liwe limefanywa na nani! Na hivyo ndivyo msimamo wa Qur'ani Tukufu ulivyo[20].

Maana kama tutazingatia kila lililofanywa na sahaba, katika tofauti zao, kuwa ni ijtihadi-hata kama linapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.-na tuogope kusema ni kosa, bila shaka tutakuwa tumefanya sahaba ndio wanaoitawala Qur'ani na Sunna, badala ya Qur'ani na Sunna kuwatawala wao! Jee, hivyo ni Kiislamu[21]? Jee, wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wataweza kututhibitishia, kwa Qur'ani na Sunna, kwamba (i) sahaba wamepawa uwezo wa kufanya ijtihadi kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na/au Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.; na (ii) kwamba Waislamu hawaruhusiwi kukosoa masahaba iwapo imewadhihirikia kwamba ijtihadi zao hizo ni kinyume na hicho Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake s.a.w.w.? Kama wataweza, wanakaribishwa!

Hata hivyo, tunapopekua pekua vitabu (sio vya Kishia!) tunaona misimamo iliyo kinyume na madai ya Sheikh M. al-Khatib.  Tunaona kwa mfano, baadhi ya mambo yaliyofanywa na baadhi ya sahaba, katika tafauti zao, yaliyokataliwa kuwa ni ijtihadi iliyofanywa kwa ikhlaswi! Mengine haya-kufanywa kamwe na sahaba, lakini kwa kuwa yamefanywa na wanaopendwa na Sheikh M. al-Khatib na wenziwe, tunakatazwa kuyakosoa kwa kisingizio cha 'ijitihadi' na 'ikhlaSwi'. Kwa maneno mingine, wasio sahaba wamepawa 'usahaba wa heshima'!

Misimamo yenyewe ni kama ifuatayo:

(i) tunaposoma al-Faslu Fil Milali Wan Nihal (uk. 161 wa Juzuu ya Nne) tunamwona Imam !bn Hazm anasema kwamba yule aliyemwua Ammar b. Yasir, yaani Abdul Ghadiya[22], alifanya hivyo kwa ijtihadi ingawa alikosea! Kwa hivyo atapata ujira[23] mmoja! Kisha akaongeza kusema: 'Lakini huyo si kama wale waliomwua Uthman (r.a.). Maana wao hawana nafasi ya ijtihadi katika kumwua!'

Na vivyo hivyo ndivyo alivyosema Ibn Hajar al-Haytami katika uk. 215 wa as-Swawaiqul Muhriqah!

Sasa, kama yule aliyemwua Ammar alikuwa sahaba; na kama wale waliomwua Uthman b. Affan nao vile vile walikuwa sahaba, kwa nini tukaambiwa kwamba yule aliyemwua Ammar[24] tu ndiye aliyefanya hivyo kwa ijtihadi na ikhlaswi (kwa hivyo atapata malipo!), lakini sio wale waliomwua Uthman b. Affan?! Hilo dai la Sheikh M.al-Khatib hapo juu limekuwaje? Au kuna sahaba na sahaba; wengine wana ruhusa ya kufanya ijtihadi, na wengine hawana? Tungependa tujulishwe.

Hilo ni la sahaba. Sasa tuangalie ya wasio sahaba!

(ii) tunapotazama uk. 484 wa Juzuu ya Kumi ya al-Muhalla, tunamwona tena Ibn Hazm akitwambia kwamba yule aliyemwua Imam Ali a.s., yaani Abdulrahman b. Muljam, alifanya hivyo kwa ijtihadi!

Subhanallah! Vipi itakuwa hivyo hali Ibn Muljam hakuwa sahaba kamwe[25]? Au kwa kuwa aliyeuawa ni Imam Ali a.s., ambaye Shia wanamtambua kuwa ndiye Imam wao wa kwanza, ndio mwuaji huyo akapawa usahaba wa heshima[26]?

Ikumbukwe; Imam Ali a.s. aliuawa kwa upanga akiwamo ndani ya swala, kibulani!

(ii)tukija kwenye uk. 9 wa Juzuu ya Kumi na Tatu ya Taarikh Ibn Kathir, twamwona Abdul  Khair as-Shafi'i[27] akisema kuwa Yazid alikuwa 'imamu mujtahid'! Lakini ujue kwamba Yazid mwenyewe hakuwa sahaba! Yeye alizaliwa baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia; na kama vitabu vya historia vinavyoeleza, alikuwa mlevi, hasharati, mcheza na mbwa, na sifa nyingine mbaya mbaya! Yeye ndiye aliyetuma watu kumwua Imam Husein a.s.[28] baada ya babake, Muawiya b. Abi Sufyan, kumtawalisha[29] juu ya Waislamu kimabavu!

• Hiyo basi ni mifano miwili ya wasio sahaba tunaoambiwa kwamba walifanya waliyofanya kwa ijtihadi na ikhlaswi. Mbali ya wale waliompiga vita Imam Ali a.s. wakasababisha Waislamu wengi  kufa[30]! Kuna na wale waliomlaani imamu huyo juu ya mimbari[31] na kuwaua waliokataa kumlaani!  Sikwamba walio mwua Imam Hasan a.s., mjukuu wa Bwana Mtume s.a.w.w., wakasherehekea kifo chake na kuzuia[32] asizikwe karibu na babu yake! Jee waliomwua Hujr b. Adiy[33]? Waliomwua Malik b. Nuwaira[34]? Waliomwua Muhammad b. Abubakar[35], mtoto wa Khalifa wa Kwanza? na wengi wengineo! Jee, wote hao walifanya hivyo kama Sheikh M. al-Khatib atakavyo tuamini, kwa ikhlaswi? Kama walioua, waliua kwa ikhlaswi, nini hukumu ya waliouliwa? Nani hapo amemdhulumu mwenzake? Au wote wawili-walioua na waliouliwa- wamedhulumiwa? Amua mwenyewe, ewe ndugu Mwislamu.

Kwa hivyo anaposema Sheikh M. al-Khatib kwamba Sunni huzingatia tofauti zote zilizozuka kati ya masahaba kuwa 'ni mambo ya ijtihadi' ambayo waliyafanya 'kwa ikhlaswi', amekusudia mambo kama hayo tuliyoyataja hapo juu. Kwa maneno mingine, shekhe hapo anatwambia kwamba Sunni wanaamini kuwa hao walioua wenzao watapata malipo mawili, kama wamewaua kwa haki! Na kama walikosea, basi watapata malipo mamoja! Kwa nini? Kwa sababu walifanya hivyo 'kwa ijtihadi na ikhlaswi'!

Ewe ndugu Mwislamu! Kama wewe ni Sunni, jee unakubaliana na Sheikh M. al-Khatib hapo? Au unakubaliana na msimamo wa Shia kwamba lazima

kesi za watu hao ziamuliwe kufuatana na Qur'ani na Sunna ya Bwana

Mtume s.a.w.w.[36]?

Haifai kujenga mashingo[37]

4. Akaendelea kusema:

...na hali walizozifanyia ijtihadi zimekwisha wala haifai kwetu kujenga mashingo juu

ya tafauti hizo, yakawa yatadumu kwa vizazi vyenye kuendelea. Majibu: Ni kweli; hali ambazo sahaba walifanyia ijtihadi zao zimekwisha. Lakini athari yake ingaliko hadi leo, na itaendelea kuwako maadam baadhi ya Waislamu wanazifumbia macho ijtihadi hizo na kukataa kuzikabili kiume, na kuzitolea hukumu za Kiislamu kama ilivyoamrishwa katika Sura 4:59.

Maadam baadhi ya Waislamu wanakataa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake s.a.w.w. kwa sababu tu uamuzi huo unakubaliwa na wapinzani wao, basi bila shaka chuki itaendelea kati yao hadi kwa vizazi vinavyofuatia. Isipokuwa, labda, hao wapinzani wao nao wakubali kuutupilia mbali huo uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Bwana Mtume s.a.w.w.!  Na hilo ni muhali. Maana kama watakubali kufanya hivyo, kwa kweli kutabaki Uislamu?

Hebu tutazame mifano miwili mitatu tu ya sunna sahihi za Bwana Mtume s.a.w.w. ambazo wasio Shia wanashauriwa kuziacha kwa sababu tu Shia wanazifuata!!

(i) Katika kueleza 'kushabihiana na rawafidh[38], Ibn Taymiya amesema hivi

katika uk. 142  wa  Juzuu ya Pili  ya  kitabu  chake  kiitwacho  Minhajus  Sunnah:

'Kutoka hapa ndiyo wanazuoni wa fiqhi wakafikia kuacha baadhi ya sunna zinapokuwa ni alama yao.  Maana, ingawa kuziacha (sunna) hizo si wajibu, lakini zinapodhihirishwa, huwa ni kushabihiana nao. Hivyo huwa hatambuliwi Sunni ni yupi na Rafidhi ni yupi. Na maslaha ya kupambanua baina yao, kwa ajili ya kujitenga nao na kuwa tofauti nao, ni makubwa kuliko maslaha va sunna hiil'

Haya! Huyo ni Ibn Taymiya ambaye, kwa wote wale wanaopinga bid'a, na kwa wale wasiomjua, ni Shaikhul Islam na Muhyis Sunna (Mfufuzi wa Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.)! Ikiwa yeye, na wote wale wanaomfuata, wamekuwa tayari kugombana[39] na watu ili sunna za Mtume s.a.w.w. zisiongezwe, vipi hapo wako tayari kuziacha kwa sababu tu Shia wanazifuata? Ndicho Kiislamu, au ndicho Wi-ansaarus sunnah? Ndiyo tuseme Waislamu wanapoona jambo jema linatendwa na wapinzani wao, waliache ili tu wawe tofauti nao?

Hasha! Mwenyezi Mungu ametukataza kuishiriki chuki kiasi hicho kwa kutwambia (Sura 5:8): 'Wala chuki dhidi ya watu (fulani) isiwapelekee kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. (Kufanya) hivyo ni karibu zaidi na ucha Mungu.'

(ii) Sheikh Muhammad b. Abdulrahman  Dimishqi  amesema  katika kitabu chake kiitwacho Rahmatul Ummah Fikhtilafil Aimmah kilichochapwa pambizoni mwa al-Mizan ya as-Sha'rani (uk. 99-100 wa Juzuu ya Kwanza):

'Sunna ya kaburi ni tastwih[40]. Hilo ndilo bora katika kauli yenye nguvu katika madhehebu ya  Shafi. Na  Abu  Hanifa na  Malik na  Ahmad wamesema:  Tasfwih[41] ni bora, maana tastwih imekuwa ni alama ya Shia!

Ghazali naye, na Mawardi, wamesema: Kufanyia tastwih makaburi ndilo lililowekwa na sheria. Lakini, ilipokuwa Rafidha wamelifanya ni alama yao, tumeliacha na kufanya tasnim!

Na mwandishi wa al-Hidaya ya Hanafi amesema: Lililowekwa na sheria ni kuvaa pete mkono wa kulia. Lakini, ilipokuwa Rafidha wameshikilia hivyo, tunaivaa mkono wa kushoto[42]!

Ewe ndugu Mwislamu! Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi baadhi ya mashekhe walivyo tayari kuwaelekeza wafuasi wao (wa Kisunni) waache baadhi ya sunna za Bwana Mtume s.a.w.w. kwa sababu tu zinafuatwa na Shia. Ikiwa kwenye mambo madogo madogo tu, kama hayo ya makaburi na pete, wako tayari kwenda kinyume na Bwana Mtume s.a.w.w. watashindwa kufanya hivyo katika mambo yanayohusiana na utawala, na manufaa ya kidunia?Au yanayohusiana na uhai wao?

Hapo ndipo penye mushkeli. Chuki baina ya Waislamu haitaondoka kwa kukubaliana kwamba tuyanyamaze yale yaliyotendwa na sahaba; maana kufanya hivyo ni sawa na kukiri kwamba dhalimu na mdhulumiwa ni sawa. Chuki itaondoka, na hivyo itakoma kuendelea mpaka kwa vizazi vijavyo, pale tu Waislamu watakapokubaliana (i) kwamba hakuna sahaba wa Kisunni wala wa Kishia; sahaba wote ni wa Bwana Mtume s.a.w.w.; (ii) wote ni binadamu, wanaopata na kukosa; (iii) kila mmoja katika wao ni lazima ahukumiwe na Qur'ani na Sunna; (iv) yule ambaye matendo yake yamewafikiana na Qur'ani na Sunna, huyo amesibu, na atahukumiwa hivyo; (v) yule ambaye matendo yake yamekwenda kinyume na Qur'ani na Sunna, huyo amekosea, na atahukumiwa hivyo. Wakikubaliana hivyo, ushindi hautakuwa ni wa upande mmoja dhidi ya mwingine ila utakuwa ni wa Haki; na Haki ni Mwenyewe Mola s.w.t. Na hayo ndiyo ambayo wanazuoni wa madhehebu mbali mbali walikutana kuyajadili kwa lengo la kutafutia njia za kuleta umoja na uelewano baina yao-jambo ambalo Sheikh M. al-Khatib, kwa bahati mbaya, alilitungia kitabu chake hiki tunachokijibu, kulipinga!

Sahaba hawana makosa?

5. Akaendelea tena kusema (katika huo huo uk. 30):

Kamwe wao ndio ambao Mwenyezi Mungu amesema kuhusu wao maneno Dora ambayo hakuyasema kwa watu wowote. Amewasifu mahali kwingi na akawakanushia makosa khaswa.

Majibu: Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu amesema maneno bora na kuwasifu sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w. Lakini haya ni kwa wale waliostahiki sifa hizo kati yao. Ama wale waliostahili kulaumiwa na kukaripiwa, kwa sababu ya vitendo vyao viovu, Mwenyezi Mungu hakuwaacha. Amewafichua[43]!

Kuhusu Mwenyezi Mungu kuwakanushia makosa; hilo hatukumbuki limesemwa wapi katika Qur'ani Tukufu. kwa hivyo tutafurahi kama wale waliomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib watatukumbusha, ndipo tuweze kutoa majibu yetu.

Hata hivyo, dai hilo si rahisi kukubalika tunapokumbuka ile mifano ya makosa mbalimbali yaliyofanywa na masahaba, na ambayo tumetangulia kuitaja katika kitabu hiki[44]. Mbali ile Hadith ya Bwana Mtume s.a.w.w., ambayo wanazuoni wengi wa Kisunni huitolea ushahidi, isemayo: 'Hakika mimi ni binadamu; hupata ha hukosea!'

Kwa hivyo, ikiwa Bwana Mtume s.a.w.w. aweza kufanya makosa, vipi sahaba wake watakanushiwa hilo?

Juu ya hayo, unapotazama uk. 32 wa kitabu chake (mstari wa 8-9 kutoka juu), utamwona shekhe wetu huyo anavyoona vigumu kuamini kuwa maimamu 'wamehifadhiwa na kukosa'. Ikiwa ni hivyo kwa maimamu, vipi anataka sisi tuamini basi kuwa sahaba wamekanushiwa makosa?

Sahaba wasituhumiwe?

6. Akamalizia maneno yake kuhusu msimamo wa Sunni:

Basi haifai kwa yoyote kuwatuhumu baada ya sifa hizo. Wala halina maslaha hilo kwa yoyote.

Majibu: Kama tulivyosema, sahaba walikuwa ni binadamu; na kama binadamu wote walivyo, hawakuwa daraja moja. Wako waliokuwa bora kuliko wengine[45].  Kuna na waliokuwa wacha Mungu na pia waliokuwa walevi na wazinifu[46].  Jee, ni haki basi kuwachanganya wote hao asijulikane yupi ni yupi?

Kwa mfano, inajulikana kwamba miongoni mwa sahaba wako waliomsingizia[47] Mw. Aisha, mke wa Bwana Mtume s.a.w.w. mambo machafu! Wako waliotoka msikitini, wakamwacha Mtume s.a.w.w. anahutubu juu ya mimbari siku ya Ijumaa, kukimbilia biashara[48] na pumbao! Wako hata waliomtuhumu[49] Bwana Mtume s.a.w.w. katika kugawa sadaka! Jee, wote hao, na wengine wengi kama hao, tuwapokee sawa na wale waliokaa na Bwana Mtume s.a.w.w.kwa wema, tangu mwanzo hadi mwisho? Jee, huo utakuwa ni uadilifu? Bila shaka la!

Hapo basi ndipo penye hitilafu baina ya Sunni na Shia. Sunni waona, kama anavyopendekeza Sheikh M. al-Khatib hapo juu, kwamba sahaba wasituhumiwe kwa uovu-hata kama wameufanya! Shia waona la! Aliyefanya uovu, na ikathubutu kuwa ni uovu, sio kosa kumtuhumu. Maana kwa kutofanya hivyo, tutakuwa tumemwachia nafasi sahaba huyo aonekane ni mwema hali si mwema! Na madhara yake msimamo huo-wa kumfanya mwema asiye mwema-uwazi mno; hauhitajii hata kuelezwa.

Hata hivyo kuna upande mwingine wa suala hili, unaofanywa na Sunni, na ambao Sheikh M. Khatib yaonekana hakupenda kuutaja.  Nao ni huu:

Sheikh ametwambia hapo juu kwamba 'haifai kwa yeyote kuwatuhumu' sahaba. Lakini hakutukataza lililo kubwa zaidi; la kumpa cheo, sio aliyemtuhumu sahaba wa kawaida tu, bali aliyemtukana na kumlaani bora ya sahaba wote!

Tunaposoma vitabu vya Kisunni tunaona watu waliokimtukana na kumlaani Imam Ali[50] a.s. zinapokewa Hadith zao, pamoja na wao wenyewe kuitwa thiqah (wenye kutegemeka au waaminifu)! Jee? Kama Sunni, sio kwamba hawawalaumu tu watu kama hao ambao imethubutu (katika vitabu vyao wenyewe!) kwamba walikimlaani Imam Ali a.s. (ambaye kwao ni mmoja kati ya 'Makhalifa Wanne Walioongoka'), bali wanawapa daraja hiyo ya u-thiqah, vipi Sheikh M. al-Khatib anazuia watu wasiwatuhumu wale waliothubutu kuwa ni waovu? Lipi lililo ovu zaidi hapo? Kutuhumu sahaba, au kumlaani? Kama kina Sheikh M. al-Khatib wako tayari kuwalaumu wale wanaotuhumu sahaba wa kawaida tu, kwa nini waogopa kuwalaumu wale waliokimlaani Imam Ali a.s. ambaye fadhila zake tushaziona uk. 37 humu? Jee hiyo ni insafi?

Kwa faida ya wasomaji wetu, na wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. a.l-Khatib, hapa chini tunatoa mifano miwili mitatu tu ya watu aina hiyo:

(i) Hariz b. Uthman: Huyu, alipokuwa akisali msikitini, alikuwa hatoki mpaka amlaani Ali, Amirul Mu'minina, laana sabini kila siku!

Amesema Ismail b. Ayyash: Niliandamana na Hariz kutoka Misr mpaka Makka, akawa anamtukana Ali na kumlaani. Akaniambia: Haya (maneno) yanayosimuliwa na watu kwamba Mtume s.a.w.w. amemwambia Ali: 'Wewe kwangu u daraja ya Harun kwa Musa[51]' ni kweli. Lakini aliyeyasikia amekosea! Nikamwuliza: (Sawa) ni vipi? Akasema: Ni 'Wewe kwangu u mahali pa Qarun[52] kwa Musa'! Nikamwuliza: Umemsikia nani? Akasema: Nimemsikia al-Walid b. Abdilmalik akisema hivyo juu ya mimbari! (taz. uk. 115 wa Juzuu ya Nne ya Taarikh Ibn Asakir, na uk. 268 wa Juzuu ya Nane ya Taarikhul Khatib.)

Haya! Kisha mtu kama huyo Hadith zake zapatikana katika Sahih Bukhari, Sunan AbiDawud, Sunan Tirmidhi, na vinginevyo!

(ii) Khalid al-Qasr: Alikuwa 'nasibiy[53], mwenye chuki, dhalimu mkubwa'. Hivyo ndivyo alivyoelezwa na Imam Dhahabi[54]

Na katika uk. 20-21 wa Juzuu ya Kumi ya Taarikh Ibn Kathir imeelezwa kwamba alikuwa mtu mwovu aliyekimtukana Ali b. Abi Twalib.  Mamake alikuwa Mkristo, naye (huyo Khalid) alikituhumiwa katika dini yake. Alimjengea mamake kanisa katika nyumba yake!'

 Mtu kama huyo ameitwa thiqah na Ibn Hibban!

(iii) ls’haq b. Suwaid al-Adawi al-Basri: Alikuwa akimshambulia Ali vikali sana. Naalikisema:  Simpendi Ali[55]!

Mtu kama huyo ameitwa thiqah na Imam Ahmad, Ibn Mu'in, na Nasai; na Hadith zake zimo katika Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Abi Dawud, na Sunan Nasai! (taz. uk. 236 wa Juzuu ya Kwanza ya Tahdhihut Tahdhib ya Ibn Hajar al-Asqalani.)

Jee, wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wanaweza, kwa upande wao, kutweleza maslaha ya kuacha kuwatuhumu watu kama hao ambao, bila shaka, misimamo yao ni kinyume na Qur'ani na Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.?

SAHABA KWA SHIA

1. Amesema Sheikh M. al-Khatib, katika uk. 30 wa kitabu chake hicho, kwamba:

Mashia wanaona kwamba maswahaba walikufuru baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.) wasiokuwa watu kidogo katika wao hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili.

Majibu: Waliosema kwamba sahaba walikufuru baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kuondoka sio Shia. Aliyesema hivyo ni mwenyewe Mtume Muhammad s.a.w.w., kama ilivyoelezwa katika Sahih Bukhari, Sahih Muslim na Musnad Ahmad:

1. Imepokewa kwa Ibn Abbas kwamba: Mtume s.a.w.w. alisimama kati yetu akasema: Hakika nyinyi mtakusanywa (kesho Akhera) miguu chini, uchi na mkiwa mazunga[56]... na kwamba watu katika umma wangu wataletwa wachukuliwe kushoto (yaani Motoni). Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! (Hao ni) sahaba wangu. Na Mwenyezi Mungu atasema: Hakika wewe hujui walizua nini baada yako. Nami nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabii Isa a.s.): Nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa miongoni mwao. Lakini uliponifisha, Wewe ndiwe uliyekuwa'Mlinzi juu yao; na Wewe ni Shahidi juu ya kila kitu. Kama utawaadhibu, wao ni waja Wako; na kama utawasamehe, basi Wewe ndiwe Mwenye nguvu, Mwenye hekima. (Sura 5:117-118) Hapo patasemwa: Hakika wao hawakuacha kurejea nyuma kwa visigino vyao[57].

Hadith hiyo utaipata katika 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hashr' katika Sahih Bukhari, na vile vile katika 'Kitabul Jannati Waswifati Na'imiha Wa Ahliha', Mlango wa 'Fanaud Dunya Wabayanul Hashri Yawmal Qiyamah' katika Sahih Muslim.

Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 533 iliyoko uk. 349 wa Juzuu ya Nane y; Sahih Bukhari; na Hadith Na. 6847 iliyoko uk. 1487 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

2.  Imepokewa kwa Asmaa bint Abubakar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu   s.a.w.w. amesema:  Nitakuwa kwenye Hodhi ili niwaone wale
watakaonijia kati yenu. Lakini baadhi ya watu watazuiwa kunifikia. Hapo nitasema:  Ewe Mola wangu! (Hao ni) wafuasi wangu na ni katika umma
wangu. Patasemwa: Jee, watambua walifanya nini baada yako? Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hawakufanya wema na walirejea (nyuma) kwa visigino
vyao...

Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'; na katika Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina (s.a.w.w.) Waswifatuhu'.

Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 592 iliyoko uk. 385-386 wa Juzuu ya Nane ya Sahih Bukhari; na Hadith Na. 5684 iliyoko uk. 1236-1237 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

3. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema:  Kundi la sahaba wangu litanijia Siku ya Kiyama, lakini watafukuzwa kwenye Hodhi.  Hapo nitasema: Ewe Mola wangu!  (Hao ni) sahaba wangu. Naye atasema: Wewe hujui walizua nini baada yako. Wao walirejea nyuma kwa visigino vyao.

Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari,  'Kitabur Riqaq',  Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza ni  Hadith  Na. 6585 iliyoko uk. 382 wa Juzuu ya Nane.

4. Imepokewa kwa Ummu Salama kwamba Mtume s.a.w.w.
amesema:  Miongoni mwa sahaba wangu kuna ambaye sitamwona wala hataniona baada ya mimi kufa abadan...

Hadith hiyo utaiona katika uk. 298 wa Juzuu ya Sita ya Musnad Ahmad.

Tunapozitazama Hadith hizo tulizozitaja hapo juu, ambazo sio zote, tunaona kwamba kesho Akhera Bwana Mtume s.a.w.w. atakuwako kwenye Hodhi. Sahaba wake watataka kumwendea; lakini baadhi yao watazuiwa kumfikia! Bwana Mtume s.a.w.w. atawatapia na kusema kwamba hao ni sahaba wake; lakini ataambiwa kwamba, ingawa ni hivyo, yeye hajui sahaba hao walifanya nini baada ya yeye kufariki dunia! Wao waliritadi; walitoka katika dini ya Kiislamu! Hapo Bwana Mtume s.a.w.w. atajibari (atajitenga) nao kwa kusema, kama atakavyosema Nabii Isa a.s. atakapojibari na Wakristo  walio mwabudu hapa duniani, maneno yaliyomo katika Sura 5:117-118. Na hao bila shaka ndio hao aliosema kwamba yeye hatawaona, wala wao hawatamwona abadan.

Kwa hivyo, kutokana na Hadith hizo, ni wazi kwamba kuna baadhi ya watu, kati ya sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w., walioritadi baada yayeye kufariki dunia. Na hayo yamesemwa na mwenyewe Mtume Muhammad s.a.w.w.; sio Shia. Lakini swali hapa ni: jee, walioritadi ni wengi au kidogo?

Sahaba wengi waliritadi

Tunaposoma  Hadith  ifuatayo, tunamwona  Bwana  Mtume s.a.w.w. anatwambia kwamba watakao ritadi na kutiwa Motoni ni wengi! Wachache tu ndio watakaosalimika nao:

5. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Nilipokuwa nimelala, mara kundi (la wafuasi wangu likaletwa). Nilipowajua, alitoka mtu (malaika) akakaa baina yangu na yao. Akasema: Njooni. Nikasema: Wapi? Akasema: Motoni, Wallahi! Nikasema: Kwani wamefanya nini? Akasema: Wao walirejea nyuma kwa visigino vyao baada yako. Kisha mara kundi jingine (likaletwa). Nilipowajua, alitoka mtu (malaika) akakaa baina yangu na yao. Akasema: Njooni. Nikasema: Wapi? Akasema: Motoni! Nikasema: Kwani wamefanya nini? Akasema: Wao walirejea nyuma kwa visigino vyao baada yako. Basi sikumwona yeyote, miongoni mwao, aliyesalimika isipokuwa (wachache) mfano wa ngamia wasio na mchungaji.

Hivyo ndivyo alivyosema Bwana Mtume s.a.w.w. kama ilivyo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'.

Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 587 iliyoko uk. 383-384 wa Juzuu ya Nane.

Tunapotazama maelezo ya Hadith hiyo, kama yalivyo katika uk. 475 wa Juzuu ya Kumi na Moja ya Fathul Bari, tunamwona Imam Ibn Hajar al-

Asqalani anasema kwamba makusudio ya ngamia wasio na mchungaji ni 'wachache. Maana ngamia wakosao mchungaji ni kidogo ukiwalinganisha na wengineo.' Kwa hivyo, kutokana na Hadith hiyo, ni wazi kwamba watakao salimika na Moto, kati ya sahaba, ni wachache mfano wa ngamia waliokosa mchungaji. Na aliyesema hivyo ni Bwana Mtume s.a.w.w.; sio Shia!

Lakini jee, uchache wenyewe ni kwamba hawapati hata idadi ya vidole vya mikono miwili?

Neno kwa neno au majazi?

Sheikh M- al-Khatib, katika kueleza imani ya Shia, amesema (uk. 30) kwamba Shia wanaamini kwamba sahaba waliokufuru baada ya kuondoka Bwana Mtume s.a.w.w. ni 'kidogo... hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili.'

Majibu: Kama Sheikh M. al-Khatib hapo ametumia maneno: hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili kimajazi[58], majibu yetu ni: Ndio. Maana itakuwa ni sawa na kusema, kama alivyosema Bwana Mtume s.a.w.w., kwamba 'walikufuru wengi isipokuwa kidogo'.

Lakini kama ameyatumia maneneo hayo ki-neno kwa neno, basi majibu yetu ni: La! Shia hawasemi wala hawaamini hivyo. Maana, kwa kuyatumia maneno hayo hivyo, itakuwa ni sawa na kusema kwamba Shia wanaamini kwamba sahaba wote walikufuru isipokuwa 'chini ya watu kumi'! Na hivyo sivyo... kwa sababu moja nzima, mbali nyinginezo. Nayo ni hii:

Jinsi Shia watakavyokuwa tayari kuwakufurisha sahaba, ni muhali kwamba watakuwa tayari kuwakufurisha hata wale, miongoni mwao, waliopigana upande wa Imam Ali a.s. katika vita vyake dhidi ya Muawiya. Na hao, bila shaka, hawakuwa kumi. Walikuwa ni mamia, kama si maelfu. Kwa hivyo Shia hawawezi kusema, wala hawasemi, kwamba sahaba ambao hawakukufuru 'hawapati kumi'.

Daraja ya Imam Ali

2. Akaendelea kusema shekhe wetu (uk. 31) kwamba Shia: wanamweka Aliy kwenye daraja makhususi kabisa...

Majibu: Hilo ni kweli. Daraja ambayo Shia humpa Imam Ali a.s. hawampi yeyote kati ya sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w.; na hilo ni kwa sababu hivyo ndivyo alivyotukuzwa na mwenyewe Bwana Mtume s.a.w.w.- kama Hadith ifuatayo inavyosema:

Umar b. Maimun amesema: Nilikuwa nimekaa kwa Ibn Abbas. Mara akajiwa na viongozi tisa; wakamwambia: Ewe Ibn Abbas! Ama inuka utufuate, au waambie hawa waondoke watwache peke yetu. Ibn Abbas akasema: Nitainuka niwafuate. Hapo alikuwa angali mzima; hajawa kipofu. Wakazungumza, lakini hatujui walizungumza nini. Mara akarejea huku anakukuta nguo zake na kusema: Ole wao! Wanamtaja kwa ubaya mtu mwenye fadhila kumi ambazo hakuna yeyote mwingine mwenye nazo. Wanamtaja kwa ubaya mtu ambaye Mtume s.a.w.w. amesema:

(i) Bila shaka (kesho) nitamtuma mtu ambaye Mwenyezi Mungu hatamhizi[59] abadan; ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda yeye. Wakaitamani (fadhila) hiyo wenye kuitamani! (Mtume s.a.w.w.) akasema: Yuko wapi Ali? Mara akaja huku macho yanamwuma, haoni. (Mtume s.a.w.w.) akayapulizia macho yake. Kisha akaitingisha beremu[60] mara tatu; akampa. Ali akarejea[61] na Swafia bint Huyay.

Ibn Abbasakasema:

(ii) Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alimtuma mtu fulani[62] kuwasomea (makafiri wa Makka) Sura at-Tawba. Nyuma yake akamtuma Ali, akaichukua kwake (huyo fulani). (Mtume s.a.w.w.) akasema: Hakuna wa kwenda nayo (sura hii) isipokuwa mtu anayetokana na mimi, na mimi nikatokana na yeye.

Ibn Abbas akaendelea kusema:

(iii) Mtume s.a.w.w. aliwaambia binami zake: Yupi kati yenu yu tayari kuwa rafiki yangu hapa duniani na Akhera? Ali, ambaye alikuwapo hapo, aliinuka akasema: Mimi nitakuwa rafiki yako hapa duniani na Akhera. Wale wengine hawakujibu kitu. (Mtume s.a.w.w.) akasema: Wewe ndiye rafiki yangu hapa duniani na Akhera.

Ibn Abbas akasema tena:

(iv) Ali ndiye mtu wa kwanza, baada ya Khadija[63], kumwamini (Mtume Muhammad s.a.w.w.) Na vile vile:

(v) Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alichukua kishali chake, akamfunika Ali, Fatima, Hasan na Husein.  Kisha akasoma: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume), na kuwatakasa kikamilifu. (Sura 33:33) Akasematena Ibn Abbas: (vi) Ali aliiuza nafsi yake kwa kulala kitandani (mwa Mtume s.a.w.w.) na kujifunika guo lake huku washirikina (wa Makka) wakimvurumizia mawe.

(vii) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka (Madina), pamoja na watu wengine, kwenda kwenye Vita vya Tabuk. Ali akamwambia: Nikufuate? (Mtume) s.a.w.w. akasema: La! Ali akalia. Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akamwambia: Jee, huridhiki wewe kuwa daraja yako kwangu ni kama ya Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakuna mtume baada yangu? Hakika haiwezekani mimi kuondoka nisikwache wewe Khalifa wangu.

(viii) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia (Ali a.s.): Wewe ndiye mtawalia (mambo ya) kila mu'mini mwanamume na mu'mini mwanamke baada yangu.

(ix) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliifunga milango yote ya Msikiti (wake) isipokuwa mlango wa Ali. Ikawa huingia msikitini humo hali ana janaba. Hiyo ilikuwa ndiyo njia yake; hakuwa na njia nyingine isiyokuwa hiyo.

(x) Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alisema: Yeyote ambaye mimi nimemtawalia mambo yake,  basi na Ali  (pia)  ndiye mwenye kumtawalia mambo yake.

Imam al-Hakim, baada ya kuitoa hiyo Hadith ya mwisho, amesema: Hii ni Hadith ambayo sanad yake ni sahihi japokuwa (Bukhari na Muslim) hawakuitoa[64]. Na Imam Dhahabi naye ameitoa katika kitabu chake, Talkhis, nakusema: Nisahihi.

Hadith hiyo, ambamo ndani yake Ibn Abbas amezidondoa hizo fadhila kumi za Imam Ali a.s. ambazo hakuna sahaba yeyote mwingine mwenye nazo, unaweza kuiona katika vitabu vifuatavyo vya Kisunni: uk. 502 wa Juzuu ya Pili ya al-lsaba ya Ibn Hajar al-Asqalani, chini ya jina ia Ali b. Abi Twalib; uk. 330-331 wa Juzuu ya Kwanza ya Musnad Ahmad; uk. 122-123 wa Juzuu ya Tisa ya Majma'uz Zawaid; uk. 132 wa Juzuu ya Tatu ya al-Mustadrak ya Imam Hakim; uk. 183 wa Juzuu ya Kwanza ya Tarikh Dimashq ya Ibn Asakir as-Shafi'i, chini ya jina la Ali b. Abi Twalib; na vitabu vinginevyo k.w.k. ambavyo tumeviacha kwa kuogopa kukirefusha kitabu hiki.

Kutokana na fadhila zilizotajwa katika Hadith hiyo, na nyingine nyingi za kipekee ambazo inshallah tutazitolea kitabu chake maalum, nataraji itaeleweka kwa nini Shia wamemweka Imam Ali a.s. 'kwenye daraja makhususi kabisa'.  Kusema kweli, hilo lataka lifanywe na Waislamu wote; sio Shia peke yao.

Imam Ali a.s. ni wasii

3. Shekhe wetu akaendelea kusema (uk. 31):
Wengine wanamwona kuwa ni wasii 

  Majibu: Ni kweli; Shia wanaamini kwamba, kabla ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia,  tayari  alikuwa ameshamchagua Imam Ali a.s.

kuwa wasii wake.  Na hilo li wazi kutokana na Hadith zifuatazo zilizomo katika vitabu vya Kisunni: (i) Mwenyezi Mungu s.w.t. alipoteremsha Sura 26:214 isemayo:  Waonye jamaa zako walio karibu (nawe),  Bwana Mtume s.a.w.w. aliwaalika jamaa zake nyumbani kwa ami yake, Abu Twalib. Jumla walikuwa kiasi cha watu arobaini hivi ambao,  miongoni mwao, walikuwamo Abu Twalib,  Hamza,

Abbas na Abu Lahab.  Mwisho wa karamu hiyo, Bwana Mtume s.a.w.w. aliwahutubia waliokuwapo kwa maneno haya:

Enyi wana wa Abdulmuttalib! Hakika mimi simjui kijana kati ya Waarabu aliyewaletea watu wake jambo bora kuliko lile nililowaletea mimi nyinyi. Hakika nimewaletea nyinyi kheri ya dunia hii na Akhera; na Mwenyezi Mungu ameniamrisha niwalinganie nyinyi kwenye (kheri) hiyo. Basi yupi kati yenu aliye tayari kunisaidia mimi katika jambo hili ili awe ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu miongoni mwenu? Wote waliokuwapo hawakujibu kitu isipokuwa Ali, ambaye alikuwa ndiye mdogo wao wote. Yeye alisimama akasema:

Mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nitakuwa waziri wako katika jambo hilo. Hapo Bwana Mtume s.a.w.w. akaweka mkono wake shingoni mwa Ali a.s.,

akasema:

Hakika  huyu  ndiye  ndugu  yangu, wasii wangu  na  khalifa  wangu miongoni mwenu. Basi msikilizeni na mumtii.

Waliokuwapo wakainuka kuondoka, huku wakicheka na kumwambia Abu Twalib: Amekwamrisha umsikilize mwanao na kumtii!

Hadith hiyo, katika vitabu vya historia, utaipata katika uk. 319-321 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh at-Tabari; uk. 62-63 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh Ibnil Athir; uk.

311 wa Juzuu ya Kwanza ya Siratul Halabiyya; na pia uk. 85 wa Juzuu ya Kwanza ya Tarikh Dimashg ya Ibn Asakir.

Katika vitabu vya Hadith, utaipata katika uk. 131-133 wa Juzuu ya Kumi na Tatu ya Kanzul Ummal; na Muntakhab Kanzul Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 41-42 wa Juzuu yaTano ya Musnad Ahmad.

(ii) Imepokewa kwa Abu Ayub al-Ansari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alimwambia binti yake, Fatima: Jee hukujua kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka aliwatazama watu wa ardhi (hii), akamteua babako kati yao, akamfanya Mtume? Kisha akatazama mara ya pili, akamteua mume wako, akaniteremshia wahyi mimi, nikamwoza (wewe) na nikamfanya wasii (wangu)?

Hadith hiyo utaipata katika Muntakhab Kanzul Ummal iliyoko pembezoni mwa uk. 31 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad; na pia katika uk. 256 wa Juzuu ya Nane ya Majma'uz Zawaid.

Na katika uk.168 wa juu ya Tisa ya Majmauz’uzawaidi, katika Hadithi iliyopokelewa kwa Ali b. Al-Hilali, mna maneno haya.. na wasii wangu ndiye bora wa mawasii, na anayependeza mno kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mume  wako...’

(iii) Imepokewa kwa Abu Said al-Khudri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Wasii wangu, na mweka siri zangu, na bora ya nitakao waacha baada yangu, mtekelezaji ahadi zangu na mlipaji deni zangu ni Ali b. Abi Twalib.

Hadithi hii utaiona katika Muntakhab kanzil-ummal iliyoko pambizoni mwa uk.32 wa juu ya Tano ya Musnad Ahmad.

 (iv) Imepokewa kwa Anas b. Malik kwamba Mtume (s.a.w.w.) alitawadha, akaswali rakaa mbili na akamwambia: Mtu wa kwanza atakaye kwingilia mlango huu ni kiongozi wa wacha Mungu, bwana wa Waislamu, mlinzi wa dini, na mwisho wa mawasii... Mara akaingia Ali a.s., na Mtume s.a.w.w. akasimama na kumkumbatia kwa furaha huku akimpangusa jasho lililokuwako kwenye paji lake la uso, na kumwambia: Wewe utanilipia deni zangu, utawasikilizisha[65] (watu) sauti yangu, na utawabainishia (la sawa) watakapo hitalifiana baada yangu.

Hadith hii utaiona katika uk. 63 wa Juzuu ya Kwanza ya Hulyatul Aw/iyaa; na uk. 486 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir

(v) Imepokewa kwa Buraida kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Kila Mtume ana wasii na mrithi; na Ali ndiye wasii wangu na mrithi wangu.

Hadith hii utaipata katika uk. 5 wa Juzuu ya Tatu ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir; na uk. 178 wa Juzuu ya Pili ya ar-Riyadhun Nadhira.

Hizo basi ni Hadith tano za Bwana Mtume s.a.w.w., tulizozitoa katika vitabu vya Kisunni, zionyeshazo kwamba Imam Ali a.s. alikuwa wasii wa Bwana Mtume s.a.w.w. Mbali zile zilizomo katika vitabu vya Kishia. Ndiyo ikawa Shia huamini hivyo.

Ali a.s. hakuwa Mtume

4. Akasema tena shekhe wetu (uk. 31): ...wengine wanamwona kuwa ni mtume...

Majibu: Hilo si kweli. Maana kuamini hivyo, kwa Shia Ithnaashari, ni ukafiri. Kwa hivyo hakuna Shia Ithnaashari hata mmoja anayeamini hivyo. Kama wale waliokiswahilisha kitabu cha Sheikh M. al-Khatib wataweza kututajia kitabu kimoja tu (juzuu na ukurasa) cha Shia kisemacho hivyo, tutafurahi.

Ali a.s. si Mungu

5. Akasema tena (hapo hapo uk.31):
...na wengine wanamwona kuwa ni Mungu!

Majibu: Astaghafirullah! Uwongo! Wamesema wapi hivyo? Twaomba vile vile tutajiwe kitabu chao (juzuu na ukurasa) ambamo mmeandikwa maneno hayo ya kikafiri.

Imam Ali a.s. na waliomkhalifu

6. Shekhe akamaliza maneno yake kwa kusema (uk. 31):

Baada  ya hivyo  wana wahukumu  Waislamu kwa kulingana  na  msimamo  wao kukhusu Aliy. Yeyote aliye chaguliwa kuwa Khalifa kabla ya Aliy, basi mtu huyo ni dhalimu au ni kafiri. Na yoyote aliyemkhalifu Aliy kwa rai (fikra) basi mtu huyo ni dhalimu au ni kafiri au ni fasiki; na ni vivyo hivyo mwenye kuwakhalifu watoto wake.

Majibu: Kama tulivyokwisha kuona humu, ni imani ya Shia kwamba  kabla ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia alikwisha kuusia Ali a.s. awe'

Imam baada yake. Kwa bahati mbaya, na kwa sababu ambazo hapa si mahali pake kuzieleza, hilo halikuwa! Pamoja na hivyo Shia hawamwiti kafiri mtu anayekataa kuamini hivyo. Husema tu kwamba mtu huyo si Shia. Maana imani hiyo, kwao, si katika misingi  ya Uislamu; ni katika misingi  ya kimadhehebu. Tazama,  kwa  mfano,  maelezo ya jambo hilo ya  Sheikh Muhammad Jawad Mughniya katika uk. 158-159 wa Hawlal Wahdatil Islamiyya.

Pia unapotazama uk. 126-127 wa Aslus Shia Wa Usuuluhaa utamwona Sheikh Muhammad al-Husayn Kashiful Ghitaa akisema kwamba linalomfanya mtu kuwa Mwislamu ni kuamini tawhidi, utume na Siku ya Malipo. Hapo utaona kwamba hakutaja Uimamu wa Ali a.s.

Hali kadhalika, akija kwenye uk. 23-24 wa al-Fusulul Muhimmah Fii Ta'lifil Ummah, utaona jinsi al-lmam Abdulhusayn Sharafuddin alivyozipanga Hadith, kutoka katika vitabu vya Kishia, zionyeshazo kwamba yeyote anayepiga shahada, akasimamisha swala, akatoa zaka, akahiji Makka na kufunga Ramadhan basi huyo ni Mwislamu ambaye, mbali na kwamba ni haramu kumwua, inaruhusiwa kuoana na kurithiana naye. Sasa basi, ikiwa mambo ni hivyo, vipi itawezekana Shia kuwa na msimamo huo wanaosingiziwa na Sheikh M. al-Khatib? Bila shaka, hata kama kutakuwako wenye mawazo kama hayo, hatuwezi kusema kwamba huo ndio Ushia. Tutasema tu kuwa hayo ni mawazo ya baadhi ya Shia yaliyo kinyume na mafunzo ya Ushia; kama vile ambavyo hatuwezi kuulaumu Usunni kwa mambo yanayotendwa na Sunni kinyume cha mafunzo yake.

Mwisho

Kutokana na majibu na maelezo yetu yaliyomo humu, tumeona kwamba:

(i) kuna hitilafu baina ya Sunni na Shia kuhusu taarifa ya sahaba. Kwa kuwa Qur'ani Tukufu wala Sunna za Bwana Mtume s.a.w.w. hazikutwachia taarifa maalum, hatwezi kumwita kafiri yeyote kati yao asiyekubali taarifa ya mwenziwe;

(ii) kinyume na inavyoaminiwa na Sunni, si kweli kwamba sahaba wote ni waadilifu. Maana kama tutaamini hivyo, itatubidi (Mungu apishe mbali) tuikadhibishe Qur'ani Tukufu, Sunna za Bwana Mtume s.a.w.w., na hata historia yenyewe-kwa vile ambavyo vyote hivyo vimerekodi makosa, bali maasia hasa, yaliyofanywa na baadhi ya sahaba;

(iii) hata hivyo, hilo halina maana kwamba sahaba wote si waadilifu. Hasha!  Ni imani ya Shia kwamba wako sahaba waadilifu ambao wamesifiwaa hivyo na Mwenyezi Mungu s.w.t., na Mtume Muhammad s.a.w.w. pia;

(iv) si imani ya Kishia kwamba Imam Ali a.s. alikuwa Mtume wala kwamba ni Mungu. Imani yao ni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja asiye na mshirika, na kwamba Muhammad s.a.w.w. ni Mtume wa mwisho.  Pia ni imani ya Kishia kwamba yeyote asiyeamini hivyo ni kafiri. Hata hivyo, kwa kuwa Sheikh M. al-Khatib aliyaandika madai hayo bila ya kuyatolea ushahidi wa vitabu vya Kishia, tumewaomba wasaidizi wake watufanyie hivyo watakapo tujibu ili nasi tuje na majibu yetu kwa ukamilifu.

(v) Shia, kwa ushahidi uliomo katika vitabu vyao vya Hadith (na hata ule uliomo katika baadhi ya vitabu vya Kisunni), wanaamini kwamba Imam Ali a.s. alikuwa wasii wa Bwana Mtume s.a.w.w. Hata hivyo, hawaamini kwamba yeyote aliye au anayemkhalifu si Mwislamu. Wao husema tu kuwa si Shia; na

(vi) sio kweli kwamba Shia wanawachukia sahaba. Maana kama ni hivyo, wasingalikuwa wanawaombea Mwenyezi Mungu kwa ile dua tuliyoichapisha humu.

Kwa hivyo, kama mambo ni kama hayo, kwa nini Sunni wazuiwe kukurubiana na kuelewana na ndugu zao, Shia? Kwa nini Wahabi wametuzukia na njama hii sasa ambapo twaona jinsi watesi wasio Waislamu wanavyozidi kutafuta njia za kusuluhiana? Tafadhali, ewe ndugu msomaji, yape maswali mawili hayo uzito yanayoustahiki.

Inshallah, katika kitabu kijacho, tutatazama msimamo wa Shia juu ya taqiya.

KIJALIZO

Barua Na. 1

6th November, 1989 Assalaam Alaykum,

RE: MAJADILIANO

Mzozo wa Ushia na Usuni umekuwa mkubwa na athari yake kwa wasiokuwa Waslam itakuwa mbaya. Na nimefikiria mimi kutukuwa khatwa ya kusuluhisha mzozo huu.

Tangu zamani fikra ya wengi katika sisi ni kuwa ITIKADI ya Shia haifungamani na mafunzo ya Qur'ani. Nasi tukiamini hiyo ni dini mbali; sasa kwa kuwa wewe, kwa jitihadi yako, umetatukiwa kuwa ITIKADI ya Shia yalingana na nassi ya Our'an, nimeona ni bora kuwakutanisha maulamaa wa pande zote mbili, uweze kuwafahamisha uvumbuzi wako. Katika moja ya cassette zako umesema kuwa uko tayari kulifanya hilo. Na mimi niko tayari kuitisha mkutano huo.

Nakuhakikishia mkutano huo utakuwa ni wa maulamaa wa pande zote mbili peke yao na makusudio ni kuwathibitishia masunni kwa nassi za Qur-an pekee maoni yako juu ya Ushia.

Nakuhakikishia hakutakuwa na vitendo vyovyote vya kuleta uharibifu katika hafla hiyo.

Ikiwa u tayari kwa hilo tafadhali niarifu niweze kuipanga mipango ya mkutano huo.

Akhuk,

MUNIR M. K. MAZRUI

c.c. IMKL:

Maimamu wote wa Msikiti (Mombasa)

Barua iSia.2

  17.11.198©

Assalaamu Alaykum,

Yah: MAJADILIANO

Nakushukuru kwa barua yako ya 6.11.89 ambayo nasikitika sikuweza kuijibu

kabla ya leo kwa sababu ya kuchelewa kuipata. Barua yenyewe ilifika Bilal Muslim Mission ya Mombasa baada ya kuwa nishaondoka kuja huku Nairobi ambako nimeletewa hivi juzi.

Hata hivyo, kabla sijaijibu barua yako kwa urefu, nitashukuru kama utanipatia orodha na anwani za watu uliowapelekea nakala za barua yako hiyo ili nami

niweze kuwapelekea nakala za majibu yangu.

Tafadhali niachie orodha hiyo kwa sahibu yangu, Bashir M. Chandoo (dukani kwake), ambaye kwa nakala hii namjulisha kuipokea na kuniwekea mpaka

Nitakapo kuja huko wiki ijayo inshallah.

Wassalaam Alaykum.

Nduguyo, ABDILAHI NASSIR

n.k. Bw. Bashir M. Chandoo S.L.P.84202 MOMBASA

Barua Na. 3

30th November, 1989

Assalaam Alaykum,

MAJADILIANO

 Ahsanta kwa barua yako ya tarehe 17th November, 1989 ambayo nimeipata leo tarehe 30th November, 1989.

Nakala za barua hiyo nimewapelekeya maimamu wote misikiti ya Mombasa na masheikh wafuatao.

Shariff Abdallah Mohamed
,, Ahmed Badawy

,,   Abdulrahman Ahmed Khitami

Sheikh Nassor M. Nahdy Nassor Bin Khamis

Sheikh Ali M. Sheikh Islam Khiyar Ali Abdalla Khamis HammadMoh'd Kassim.

Anwani za wote hawa sina. Barua zilikwenda kwa mkono. Sina shaka kuwa Sheikh Bashir M. Chandoo aweza kufanya kazi hiyo maadam wote hao ni wakazi wa Mombasa.

Akhuk, MUNIR M. K. MAZRUI

c.c. Sheikh Bashir M. Chandoo

BaruaNa4 17th December, 1989

Assalaamu alaykum, Yah:

  MAJADILIAO

Ahsanta sana kwa barua yako ya 30.11.1989 niliyoipata 2.12.1989. Hata hivyo nasikitika, kwa sababu ya shughuli na safari nyingi, sikuweza kukujibu kabla ya leo. Na hata hii jawabu ya leo sitadiriki kuitia sahihi kwa kuwa naondoka kwenda ng'ambo; kwa hivyo nimemwachia mwanangu aitie sahihi kwa niaba yangu.

Katika barua yako ya 6.11.1989 ulieleza wasiwasi wako juu ya athari mbaya kwa Uislamu inayoweza kutokana na fitna iliyosababishwa na kampeni ya watu fulani kuwakufurisha Shia Ithnaashari. Fitna hii, kwa kweli, imetuhuzunisha sote; na nakubaliana nawe kwamba lazima hatua zichukuliwe kulisuluhisha tatizo hili, na'kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu. Jambo ambalo siwafikiani nawe ni lile dai lako kwamba 'tangu zamani fikra ya wengi katika sisi ni kuwa itikadi ya Shia haifungama'ni na mafunzo ya Qur'ani. Nasi tukiamini hiyo ni dini mbali...' Hilo ndilo silikubali; maana ukweli wa mambo ulivyo ni kinyume cha hivyo!

Kwa miaka mingi sana huku kwetu Afrika Mashariki, mbali sehemu nyingine za ulimwengu wetu, Shia Ithnaashari wamekuwa wakiishi pamoja na ndugu zao, Sunni, bila ya chuki. Pamoja na tofauti za kimadhehebu zilizoko, wamekuwa wakishirikiana kama ndugu Waislamu. Viongozi na mashekhe wakubwa wakubwa wa Kisunni walikihudhuria na kuhutubia hafla za Shia, na Shia nao walikialikwa na wakihudhuria hafla za Sunni. Sunni walikiwatia mashaurini ndugu zao Shia, na Shia wakishiriki katika mashauri yote yanayowahusu Waislamu kwa jumla nchini, kama vile sharia za mirathi, ndoa na talaka n.k. Vile vile, katika halmashauri zote muhimu za mambo ya Kiislamu, k.m. Kamati ya Utangazaji Vipindi vya Kiislamu, iliyokuwa chini ya Kadhi Mkuu, na Kamati ya Kutunga Silabasi (man-haj) ya masomo ya dini shuleni, utawakuta Shia wakishirikiana na ndugu zao Sunni. Ukija upande wa vyama vya Kiislamu, utakuta vyama mbalimbali vilivyobuniwa, na vyengine mpaka leo, vyasimamiwa na Sunni pamoja na ndugu zao Shia. Mbali walio owana.

Mpaka hivi majuzi tu palipozuka watu wanaofuata siasa za madola fulani yanayopingana na misimamo ya Kiislamu ya Jamhuri ya Iran, ndipo tulipobwagiwa shindo la 'ukafiri' wa Shia, kwa sababu tu viongozi na wengi wa raja wa Iran ni Shia Ithnaashari. Watu hao wamejaribu kutumia fikra ya kimakosa, waliyonayo baadhi ya Sunni na wenye ilimu chache, kuwa itikadi ya Shia Ithnaashari hailingani na misingi ya Uislamu, ili kuwachochea wawakufurishe hao ndugu zao, wapate na kuitenga Iran. llihali watu hao hao, mpaka hivi juzi na jana, ndio waliokuwa wakiwakufurisha Sunni kwa ajili ya baadhi ya itikadi za madhehebu yao walizozifanya ni shirk na kufr wakawagawanya makundi makundi, kila moja likilikufurisha lenziwe! Tulipoona athari mbaya itakayoufikia Uislamu na Umoja wa Waislamu kutokana na fitna hiyo, tulifanya wajibu wetu wa kuwakanya wale wenye kuieneza. Hilo li wazi ukizisikiliza /ukitizama kanda za darasa zangu za miaka ya nyuma. llipokuwa hawakukanyika, bali wakazidi kueneza bughdha baina ya Waislamu, ilitubidi tuwaeleze wale wasiojua hakika ya Ushia na hitilafu baina yao na madhehebu ya Kisunni ili wasiweze kutekwa na fitna hiyo. Ndio hivi majuzi nikaweka darasa mahususi na kuanza kuandika vitabu ili kuonyesha kuwa itikadi za Shia Ithnaashari zimetegemezwa Qur'ani na Sunna, na kuwa hakuna hitilafu kubwa hivyo baina yao na Sunni hata iwazuie kukurubiana na kuelewana. Kama nitafaulu kulithibitisha hilo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa maslaha ya Waislamu wote, inshallah. Namshukuru Mwenyezi Mungu kuona kwamba wenzangu sasa waiona hatari ya jambo hili kutosuluhishwa. Kwa hivyo nakubaliana na wewe kuwa iko haja ya kuwaleta 'ulamaa wa pande zote mbili kulijad'li hilo ili kuepusha sui-tafahum baina ya makundi mawili haya ya Waislamu. Kwa upande wangu mimi nitayari kufanya kila niwezalo kuufaulisha mkutano huo. Lakini kwanza nahitaji maelezo zaidi juu ya mambo haya yafuatayo kabla ya kukupa kauli yangu ya mwisho:

1) Jee, mkutano ni wa ulamaa wa pande zote mbili, au ni baina yangu mimi tu na ulamaa wa Kisunni?

2) Ikiwa ni wa ulamaa wa pande zote mbili, ni ulamaa walio humu humu
nchini tu ama kuna mipango ya kuwaalika walio nje ya nchi pia?

3) Ni nini hasa madhumuni ya mazungumzo yenyewe? Ni:

a) kueleza msimamo wangu juu ya Ushia tu, au

b)   ni kujadiliana juu ya msimamo wangu na/ au itikadi za Shia Ithnaashari? Au

c) ni kuangalia jinsi ya kuleta uelewano na mkuruba baina ya Shia na Sunni?

4) Ni jambo gani katika msimamo wangu kuhusu Shia Ithnaashari na/au itikadi za Shia Ithnaashari zenye mushkili, na mushkili wenyewe ni nini?

5) Kanuni zitakazo fuatwa katika mazungumzo /majadiliano;

6)  Watakaoshiriki, na idadi yao.
Mwenyezi Mungu Ajaalie taufiki.
Nduguyo,
ABDILAHINASSIR

n.k.

Maimamu wa Misikiti (Mombasa).

Mashekhe uliowataja katika barua yako ya 30.11.89

DUA YA KUWAOMBEA MASAHABA KWA MASHIA

[ÇáÏÚÇÁ ÇáÑÇÈÚ]

[æ ßÇä ãä ÏÚÇÆå (Úáíå ÇáÓáÇã) Ýí ÇáÕáÇÉ Úáì ÃÊÈÇÚ ÇáÑøÓõáö æ ãÕÏøÞíåã]

Çóááøóåõãøó æóÃóÊúÈóÇÚõ ÇáÑøõÓõáö æóãõÕóÏøöÞõæåõãú ãöäú Ãóåúáö ÇáÇóÑúÖö ÈöÇáúÛóíúÈö ÚöäúÏó ãõÚóÇÑóÖóÉö ÇáúãõÚóÜÇäöÏíäó áóåõãú ÈöÇáÊøóßúÐöíÈö æóÇáÇÔúÊöíóÇÞö Åáóì ÇáúãõÑúÓóáöíäó ÈöÍóÞÇÆöÞö ÇáÇíúãóÇäö. Ýöí ßõáøö ÏóåúÑ æóÒóãóÇä ÃóÑúÓóáúÊó Ýöíúåö ÑóÓõæáÇð¡ æóÃóÞóãúÊó áÇåúáöåö ÏóáöíáÇð¡ ãöäú áóÏõäú ÂÏóãó Åáóì ãõÍóãøóÏ Õóáøóì Çááå Úóáóíúåö æóÂáöÜåö ãöäú ÃóÆöãøóÉö ÇáúåõÜÏóì¡ æóÞóÇÏóÉö ÃóåúÜáö ÇáÊøõÞóì Úóáóì ÌóãöíÚöåöãõ ÇáÓøóáÇóãõ¡ ÝóÇÐúßõÑúåõãú ãöäúßó ÈöãóÛúÝöÑóÉ æóÑöÖúæóÇä. Çóááøóåõãøó æóÃóÕúÍóÇÈõ ãõÍóãøóÏ ÎóÇÕøóÉð ÇáøóÜÐöíäó ÃóÍúÓóäõæÇ ÇáÕøóÍóÇÈóÉó¡ æóÇáøóÐöíäó ÃóÈúáóæúÇ ÇáúÈóáÇóÁó ÇáúÍóÓóäó Ýöí äóÕúÑöåö¡ æóßóÇäóÝõæåõ æóÃóÓúÑóÚõæÇ Åáóì æöÝóÇÏóÊöåö æóÓóÇÈóÞõæÇ Åáóì ÏóÚúæóÊöåö

æÇÓúÊóÌóÇÈõæÇ áóåõ ÍóíúËõ ÃóÓúãóÚóåõãú ÍÌøóÉó ÑöÓóÇáÇóÊöåö¡ æóÝóÇÑóÞõæÇ ÇáÇÒúæóÇÌó æóÇáÇæúáÇÏó Ýöí ÅÙúåóÇÑö ßóáöãóÊöåö¡ æóÞóÇÊóáõæÇ ÇáÇÈÇÁó æó ÇáÇÈäÇÁó Ýöí ÊóËúÈöíÊö äÈõæøóÊöåö¡ æóÇäúÊóÕóÑõæÇ Èåö æóãóäú ßóÇäõæÇ ãõäúØóæöíäó Úóáóì ãóÍÈøóÊöåö íóÑúÌõæäó ÊöÌóÇÑóÉð áóäú ÊóÈõæÑó Ýöí ãóæóÏøóÊöåö¡ æóÇáøÐíäó åóÌóÑóÊúåõãõ ÇáÚóÔóÇÆöÑõ ÅÐú ÊóÚóáøóÞõæÇ ÈöÚõÑúæóÊöåö¡ æóÇäúÊóÝóÊú ãöäúåõãõ ÇáúÞóÑóÇÈÇÊõ ÅÐú ÓóßóäõæÇ Ýöí Ùáøö ÞóÑóÇÈóÊöåö¡ ÝóáÇó ÊóäúÓó áóåõãõ Çáøåõãøó ãóÇ ÊóÑóßõæÇ áóßó æóÝöíßó¡ æóÃóÑúÖöåöãú ãöäú ÑöÖúæóÇäößó æóÈöãóÇ ÍóÇÔõæÇ ÇáúÎóáúÞó Úóáóíúßó¡ æóßóÇäõæÇ ãóÚó ÑóÓõæáößó ÏõÚóÇÉð áóßó Åáóíúßó¡ æóÇÔßõÑúåõãú Úóáóì åóÌúÑöåöãú Ýöíúßó ÏöíóÇÑó Þóæúãöåöãú¡ æóÎõÑõæÌöåöãú ãöäú ÓóÚóÉö ÇáúãóÚóÇÔö Åáóì ÖöíúÞöåö¡ æóãóäú ßóËøóÑúÊó Ýöí ÅÚúÒóÇÒö ÏöíúäöÜßó ãöäú ãóÙúáõæãöåöãú. Ãáøåõãøó æóÃæúÕöáú Åáóì ÇáÊøóÇÈöÚöíäó áóåõãú ÈöÅÍúÓóÇä ÇáøóÐöíäó íóÞõæáõæäó: ÑóÈøóäóÇ ÇÛúÝöÑú áóäóÇ æóáÇÎúæóÇäöäóÇ ÇáøóÐöíúäó ÓóÈóÞõæäóÇ ÈöÇáÇöíãóÇäö ÎóíúÑó ÌóÒóÇÆößó¡ ÇáøóÐöíäó ÞóÕóÏõæÇ ÓóãúÊóåõãú¡ æóÊóÍóÑøóæúÇ æöÌúåóÊóåõãú¡ æóãóÖóæúÇ Úóáì

ÔÇßöáóÊöåöãú¡ áóãú íóËúäöåöãú ÑóíúÈñ Ýöí ÈóÕöíúÑóÊöåöãú¡ æóáóãú íóÎúÊóáöÌúåõãú Ôóßøñ Ýöí ÞóÝúæö ÂËóÇÑöåöãú æóÇáÇöÆúÊöãóÇãö ÈöåöÏóÇíóÉö ãóäóÇÑöåöãú¡ ãõßóÇäöÝöíäó æóãõæóÇÒöÑöíúäó áóåõãú¡ íóÏöíúäõæäó ÈöÏöíúäöåöãú¡ æóíóåúÊóÏõæäó ÈöåóÏúíöåöãú¡ íóÊøóÝöÞõæäó Úóáóíúåöãú¡ æóáÇó íóÊøóåöãõæäóåõãú ÝöíãóÇ ÃÏøóæúÇ Åáóíúåöãú. Ãáøóáåõãøó æóÕóáøö Úóáóì ÇáÊøÇÈöÚöíúäó ãöäú íóæúãöäóÇ åóÐÇ Åáì íóæúã ÇáÏøöíäö¡ æóÚóáóì ÃÒúæóÇÌöåöãú¡ æóÚóáóì ÐõÑøöíøóÇÊöåöãú¡ æóÚóáóì ãóäú ÃóØóÇÚóßó ãöäúåõãú ÕóáÇúÉð ÊóÚúÕöãõåõãú ÈöåóÇãöäú ãóÚúÕöíóÊößó¡ æóÊóÝúÓóÍõ áóåõãú Ýöí ÑöíóÇÖö ÌóäøóÊößó¡ æóÊóãúäóÚõåõãú ÈöåóÇ ãöäú ßóíúÏö ÇáÔóíúØóÇäö¡ æóÊõÚöíäõåõãú ÈöåóÇ Úóáóì ãóÇ ÇÓúÊóÚóÇäõæßó Úóáóíúåö ãöäú ÈöÑøò¡ æóÊóÞöíåöãú ØóæóÇÑöÞó Çááøóíúáö æóÇáäøóåóÇÑö ÅáÇø ØóÇÑöÞÇð íóØúÑõÞõ ÈöÎóíúÑ¡ æóÊóÈúÚóËõåõãú ÈöåóÇ Úóáóì ÇÚúÊöÞóÇÏö ÍõÓúäö ÇáÑøóÌóÜÇÁö áóßó¡ æóÇáØøóãóÚö ÝöíãóÇ ÚöäúÏóßó¡ æóÊóÑúßö ÇáäøõåóãóÉö ÝöíãóÇ ÊóÍúæíåö ÃíúÏöí ÇáúÚöÈóÇÏö áöÊóÑõÏøóåõãú Åáóì ÇáÑøóÛúÈóÉö Åáóíúßó æóÇáÑøóåúÈóÉö ãöäúßó¡ æóÊõÒóåøöÏõåõãú Ýöí ÓóÚóÉö ÇáÚóÇÌöáö æóÊõÍóÈøöÈõ Åáóíúåöãõ ÇáúÚóãóáó áöáÇÌöáö¡ æóÇáÇÓúÊöÚúÏóÇÏó áöãóÇ ÈóÚúÏó ÇáúãóæúÊö æóÊõåóæøöäó Úóáóíúåöãú ßõáøó ßóÑúÈ íóÍõáøõ Èöåöãú íóæúãó ÎõÜÑõæÌö ÇáÇäúÝõÓö ãöäú ÃóÈúÏóÇäöåóÇ¡ æóÊõÚóÇÝöíóåõãú ãöãøóÇ ÊóÞóÚõ Èöåö ÇáúÝöÊúäóÉõ ãöäú ãóÍúÐõæÑóÇÊöåóÇ¡ æóßóÈøóÉö ÇáäøóÇÑö æóØõæáö ÇáúÎõáõæÏö ÝöíåóÇ¡ æóÊõÕóíøöÑóåõãú Åáóì Ãóãúä ãöäú ãóÞöíáö ÇáúãõÊøóÞöíäó.


[1] - Wakati kitabu hiki ki mitamboni, tumepata nakala ya Udanganyifu wa Kishia Kukhusu Qur'ani. Maelezo zaidi katika kitabu chetu kijacho inshallah.

[2] - Hii ni hijja aliyohiji Bwana Mtume s.a.w.w. kabla ya kufariki dunia.

2. [3] - Haya ni makabila makubwa ya Madina yaliyomkaribisha Bwana Mtume s.a.w.w. na wafuasi wake huko.

[4]- Ni mmoja miongoni mwa maimamu wa Hadith za Mtume s.a.w.w.  Alikuwa shekhe wa Imam Bukhari na wengineo kati ya wanazuoni wakubwa wakubwa wa Hadith. Alifariki mwaka 234H.

[5] - Bwana Mtume s.a.w.w. amesema: Fatima ni kipande changu cha nyama. Yeyote anae mkasirisha yeye, amenikasirisha mimi. (Bukharil.

[6] - Taz. uk. 74 wa Juzuu ya Nne ya a/-Muwafaqat ya Shatibi.

[7] - Makusudio ya  Hodhi hapa  ni  ule  Mto  Kawthar uliotajwa katika Sura  108:1

[8] - Taz. para ya pili na ya mwisho ya maelezo ya Sheikh Abdullah Saleh al-farsy ya aya  hiyo, yaliyoko uk. 257 wa Tafsir yake, uone anavyosema.

[9] - Pia taz. uk. 229 wa Muhammad Rasulullah ya Muhammad Ridhaa.

[10] - Kuritadi ni kutoka katika dini (Uislamu).

[11]- Inshallah ni nia yetu, tutakapopata wasaa, kuandika kitabu cha kueleza jinsi madhehebu  yalivyozuka na kuenea, na jinsi mengine yalivyokufa.

[12] - k.v. Shia na Ibadhi.

[13] - k.v. Sunni na Wahabi. Wao waaamini ataonekana kesho Akhera.

[14] - Hao ni Wahabi.

[15] - Hiyo ni imani ya Shia, Sunni na Ibadhi.

[16] - k.v. Hanafi, Shafi na Hanbali.

[17] - k.v. Shia. Maliki na Ibadhi.

[18] - Mmoja katika masultani wa Kiislamu alrtaka kuchagua baina ya madhehebu ya Shafi na ya Hanafi. Mwanachuoni mmoja akampendekezea ya Shafi kwa kusali rakaa mbili Kishafi-kwa nguzo, sharuti na sunna zake zote. Kisha akasali rakaa mbili nyingine vile inavyoweza kujuzu Kihanafi: 'Alivaa ngozi ya mbwa iliyodibighiwa (iliyotiwa rangi); akaichafua roboo yake kwa najisi. Akatawadha kwa nabidhi (aina ya pombe).  Na ilikuwa katikati ya kaskazi, jangwani. Nzi na mbu wakamkusanyikia

Udhu (wake) ulikuwa kinyumenyume. Kisha akaelekea kibla. Akafunga swala bila ya nia. Akapiga takbiri kwa Kifursi. Kisha akasoma aya kwa Kifursi. Kisha 'akadona' midono miwili kama ile ya jogoo bila ya kusita, na bila ya kurukuu. Mwishowe akasoma tahiyatu na kujamba pasi na (kutoa) salamu' Kisha akasema: Ewe Sultan! Hii ndio swala ya Abu Hanifa. Sultan akamwambia: Kama hii sio swala yake, nitakuua. Maana yeyote mwenye dini hawezi kuiruhusu swala kama hii.

Hanafi wakakataa kuwa hiyo ni swala ya Abu Hanifa. Yule mwanachuoni (jina lake ni al-Qaffal) akaagiza viletwe vitabu vya makundi mawili hayo. Sultan naye akamwamrisha mwandishi mmoja wa Kikristo avisome. Naye akayasoma yote madhehebu mawili. Ikaonekana kwamba swala katika madhehebu ya Abu Hanifa ni kama alivyoeleza al-Qaffal. Sultan akayaacha madhehebu ya Abu Hanifa, akafwata ya Shafi! (taz. uk. 174-175 wa Taarikhul Fiqhil Islamiy ya Dkt. Umar Suleiman al-Ashqar)

[19] - Ijtihadi ni 'kitendo cha kutumia rai katika kutoa hukumu ya kisheriapamoja na kutoitia  maanani nassi iliyopo kinyume chake'

[20] - Amesema Mwenyezi Mungu: Naapa kwa Mola wako; hawawi ni wenye kuamini mpaka wakufanye wewe (Muhammad) hakimu katika yale wanayozozana. Kisha  wasione  uzito nyoyoni mwao juu ya uliyo yahukumu, na wasalimu amri kikamilifu (Sura4:65)

Akasema tena: Haimfalii mu'mini mwanamume wala mu'mini mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapoamua jambo. kuwa na hiari katika jambo lao (hilo). Na mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi hakika amepotea upotevu ulio wazi. (Sura 3336)

[21] - Ajabu hapa ni kwamba miongoni mwa wanaoona uzito kuwakosoa sahaba, hata wanapokuwa wanapingana na Qur'ani na Sunna, ni Wahabi-kama Sheikh M. al Khatib- japokuwa wako tayari kuwakufurisha wengine, na hata kuwafanya washirikina. wanapofanya kama hivyo!

[22] - Jina lake kamili ni Yisar b. Sabu'i al-Juhani. Yeye ni miongoni mwa waliomsikia Mtume s.a.w.w. akisema: Hakika damu zenu na mali zenu niharamu...'Hivyo sahaba walikistaajabu sana kuwa mtu kama huyo, baada ya kusikia maneno kama hayo kwa Bwana  Mtume s.a.w.w.,alijitolea kumwua Ammar b. Yasir! (taz. uk. 150 wa Juzuu ya
Nne ya al-lsaba)

[23] - Ujira maana yake ni 'malipo'.

[24] - Ukumbuke Ammar huyu ni yule ambaye Sura 39:9, 6:52, 16:106, 6:122, na 28:61

ziliteremshwa kwa ajili yake pekee au pamoja na wenziwe wengine. Mbali zile Hadith za Bwana Mtume s.a.w.w. zisemazo kuwa Ammar amejaa imani-tangu utosini hadi kwenye kidole gumba, na kwamba imani imechanganyika na nyama yake na damu yake, na kwamba ni haramu Moto kula au kuigusa damu yake, na kadhalika (taz. uk. 22 - 28 wa Juzuu ya Tisa ya al-Ghadir).

[25] - Taz. uk. 67-68 wa Maisha ya al-lmam Aly ya Sheikh Muhammad Kasim Mazrui uone jinsi huyo Ibn Muljam alivyohadawa na mwanamke, kwa kusalitika naye, hata akajitolea kumwua 'Mpenzi wa Mwenyezi Mungu'!

19. [26] - Linganisha heshima hiyo anayopawa aliyemwua  Imam Ali a.s., na hukumu
zifuatazo zilizotolewa kwa wanaomtukana tu Abubakar na Umar ndipo utakapoelewa
chuki inavyofanya kazi:

Katika uk. 23 wa Juzuu ya Pili ya Mis'bahudDhwalaam amesema al-Jurdani kwamba wanazuoni wengi wanasema kwamba anayemtukana Abubakar na Umar huwa kafiri.

Ibn Kathir naye anasema (uk. 324 wa Juzuu ya Kumi ya Taarikh yake) kwamba Isa b. Ja'far b. Muhammad aliuawa kwa amri ya al-Mutawakkil al'Allah kwa kumtukana

Abubakar, Umar, Aisha na Hafsa!

Na katika uk. 575 wa as-Swarimul Maslul ya Ibn Taymiya imeandikwa kwamba Kadhi Abu Ya'la aliulizwa kuhusu mwenye kumtukana Abubukar. Akasema: Kafiri. Akaulizwa: Asaliwe? Akajibu: La! Akaulizwa afanyweje naye asema 'Laa ilaaha illallah?' Akajibu: Msimguse kwa mikono yenu. Msukumeni kwa ubao mpaka mumtumbukize shimoni mwake!

Ukumbuke, ewe ndugu Mwislamu, kwamba Abubakar mwenyewe alipotukanwa mbele za Bwana Mtume s.a.w.w., Bwana Mtume s.a.w.w. hakutoa hukumu hiyo iliyotolewa na mashekhe hao, bali alitabasama tu! (taz. uk. 436 wa Juzuu ya Pili ya Musnad Ahmadl. Bali yeye mwenyewe Abubakar alipotukanwa na mtu, na Abu Barzatal Aslami akataka kumwua mtu huyo, alimkaripia na kumwambia: Hilo (la kuuawa mtu kwa kutukana mtu) si la yeyote baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w.! (taz. uk. 109-111 wa Juzuu ya Saba ya Sunanun Nasai)

Basi vipi mashekhe hao wanatutolea hukumu zao kinyume na ile ya Bwana Mtume s.a.w.w., na hata ya Abubakar mwenyewe? Au kwa nini wanamwacha aliyemwua Imam Ali a.s. katika hukumu zao? Jiulize.

[27] - Huyu  alikuwa  ni mufassir, na  alikisomesha katika Chuo  cha Nidhamiya, Baghdad. Alifariki mwaka 590H.

[28] - Katika kueleza jinsi Imam Husein a.s. alivyouawa. Sheikh Abdullah Saleh Farsy, katika uk. 37 - 38 wa Maisha Ya Sayyidnal Huseyn amesema hivi: 'Alipowajibu kwa yakini kuwa hakubali kwenda kuuawa na Ubeydillah na kudhalilishwa. wanaume na wanawake na watoto waliwazunguka darmadar wasiwe na njia ya kupenya na kukimbia. Wakakosa maji na chakula tangu hapo mwezi nane Mfunguo Nne, 61 mpaka mwezi kumi 61H; hapo wakaingia kuwapiga baada ya kuwa hawajifai kwa njaa na kiu. Wakapigana kwa ushujaa mkubwa kabisa usiokuwa na mfano. Wakaua zaidi ya idadi ya hao kuwaua wao ... Na Sayyidnal Husein anawalinda wanawake na waliotaka kuwashambulia au kuwafanya mambo mabaya. Kisha wakamzingira kila upande  kwa kumpiga  kwa  mishare,  mikuki  na  panga  mpaka  akaanguka  chini wakamkata kichwa. Na kawli mashuhuri kuwa aliyemkata kichwa ni Shimr bin Dhiljawshan-baba yake alikuwa sahaba.' Sheikh Farsy akamalizia:  Pesa na kutaka ukubwa kunafanya kazi.'

[29] - Taz. uk. 18 - 29 wa Maisha Ya Sayyidnal Huseyn uone jinsi Sheikh Abdullah Saleh Farsy alivyoeleza kwa tafsili vile Muawiya b. Abi Sufyan alivyombandika mwanawe, Yazid, kimabavu juu ya Waislamu.

[30] - K.m. inakisiwa kwamba wale waliokufa katika Vita vya Siffin peke yake ni baina ya 70 000 na 110 000, wakiwamo miongoni mwao sahaba 25 walio wahi kupigana katika Vita vya Badr pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. (taz. uk. 404 -405 wa Juzuu ya Pili ya Murujudh Dhahab).

[31] - Wa kwanza ni Muawiya b. Abi Sufyan. Yeye ndiye aliyeanzisha jambo hilo. Alikimlaani Imam Ali a.s. katika hotuba yake ya kila Ijumaa juu ya mimbari. Na ili watu  waweze kuisikia laana hiyo siku za Idd, mtu huyo aliibadilisha sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.  Badala ya hotuba kuwa baada ya swala, akaiweka kabla ya
swala! Wengine ni kama vile Busr b. Artwaat. Mughira b. Shu'ba, Marwar b. al-Hakam. Ziyad b. Sumayya,na wengi wengineo.

Desturi hii ya kumlaani Imam Ali a.s. iliendelea kwa miaka -mingi sana-tangu pale alipouawa mwaka 40H mpaka Umar b. Abdulaziz aliposhika Ukhalifa mwaka 99H. Yeye ndiye aliyeipiga marfuku desturi hiyo; akaiondoa hiyo laana, na badala yake akaiweka Sura 16:90 ambayo husomwa hadi hii leo katika hotuba zote za misikiti ya Sunni.

[32] - Aliyezuia hivyo ni Marwan  b. al-Hakam ambaye wakati huo alikuwa ameshauzuliwa. Alifanya hivyo ili kumfurahisha Muawiya! (taz.uk.13-14 wa Juzuu ya Kumi na Moja ya al-Ghadir ya Sheikh Abdulhusein Ahmad al-Amini).

[33] - Hujr alikuwa ni sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w. aliyesifiki kwa wema mtupu. Yaye, pamoja na sahaba wengine kumi na moja. Walikataa kumlaani Imam Alia.s.walipoamrishwa kufanya hivyo na Muawiya na vibaraka wake. Sita kati yao wakauawa; mmoja,  aliyekiKwa Abdulrahman b. Hasan  al-'Anziy,  aliuliwa kwa kuzikwa mzima mzimal

[34] - Malik  b. Nuwaira  aliuawa  na Khalid b.  al-Walid ambaye,  siku hiyohiyo aliyomwua alimwoa mjane wake aliyekuwa mzuri sana! Jee, tusemeje na hao ni sahaba?

[35] - Huyu ni mtoto wa Khaiifa Abubakar. Kwa sababu alikuwa upande wa Imam Ali a.s., aliuawa kinyama.  Sheikh Muhammad Kasim Mazrui anatwambia, katika uk. 66 wa Maisha Ya al-lmam Aly: 'Baada ya kumtesa, walimkata kata viungo kimoja kimoja mpaka akakata roho! Na yote hayo yu kimya, hapigi kelele wala halalaiki mpaka akafa kishujaa!  Baada ya ukatili huo. wakamtia   katika kiribacha punda, wakamchoma motol'

[36] - Kwa kufanya hivyo-yaani kuwahukumu sahaba kwa mujibu wa Our'ani na sunnah, na kutangaza hukumu hizo-ndipo inaposemwa kuwa Shia wanatukana sahaba!

[37] - Mashingo maana yake ni 'chuki".

[38] - Hili  ni jina ambalo  wale  wapinzani  wao,  hupenda  kuwaitia  Shia. Lakini  Shia wenyewe hawalikubali jina hilo kwa sababu linaipotoa historia.

[39] - Ni jambo linalo julikana kwamba kuna watu wanaowaita wengine makafiri au mushrikina kwa sababu tu wanatawasali, au wanasoma maulidi, talkini au hitima. au wanaweka nadhiri makaburini, na kadhalika. Watu hao huwakufurisha wengine hivyo kwa kuwa ati wamefanya jambo ambalo halikufanywa na Bwana Mtume s.a.w.w. Na katika kufanya hivyo,huwa wanamfuata huyo Ibn Taymiya tuliyemtaja hapo juu! Sasa lipi kubwa hapo? Kufanya ambaio halikufanywa na Mtume s.a.w.w., ingawaje hakulikataza, au kuliondoa lililofanywa na yeye?

[40] - Tastwih ni kuutandaza mchanga  wa kaburi, baada ya kulifunika, likawa tambarare.

[41] - Tasnim ni kuukusanya mchanga wa kaburi baada ya kulifunika, likawa na nundu kama ya ngamia.

[42] - Tazama mambo hayo! Yakifika hapo, tusemeje?

[43] - Tazama, kwa mfano, Sura ya at-Tawba na at-Munafiqun katika Qur'ani Tukofu, utayaona hayo.

[44] - Taz. uk. 14-20 humu. Pia kwa wale wanaojua Kiarabu, nawatazame uk. 82 (chini ya Hadith Na. 60) na uk. 83 - 84 (chini ya Hadith Na. 61) wa Juzuu ya Kwanza ya SilsilatulAhadithidh Dha'ifa WalMawdhu'a •  sheikh muhammad Nasiruddin al-Albany ambaye ni mpinga bid'a mkubwa!

[45] - Mwenyezi Mungu anasema: ... Hawawisawa miongoni mwenu wale waliotoa kabla ya kushinda na wakaendelea kupigana. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao wametoa baadaye na wakapigana ...' (Sura 57:10)

[46] - Tazuk. 14.15 humu.

[47] - Taz.Sura 24:11-20.

[48] - Taz. Sura 62:11 na maelezo yake katika Tafsir ya Sheikh AbduilahSalehal-Farsy.

[49] - Taz.Sura9:58-59.

[50] - Imam Ali huyo, kama inavyoelezwa katika vitabu k.w.k., ndiye mwanamume wa kwanza kusilimu.  Ndiye wa kwanza kusali pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. Ndiye yule ambaye Bwana Mtume s.a.w.w. alimteua kuwa wasii na khalifa wake baada yake, na sifa nyingi nyingine ambazo zinahitaji kitabu kizima lau tutazikusanya zote! Pia taz. uk. 37-42 humu.

[51] - Hii ni Hadith ambayo imepokewa katika vitabu vingi vya Hadith vya Kisunni k.v. Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan  Tirmidhi,  Sunan Ibn Majah,  Musnad Ahmad, Mustadrak, Majmauz Zawaid, na vinginevyo.

[52] - Huyu alikuwa binami yake Nabii Musa a.s., lakini alikuwa akimpinga. Vipi atalinganishwa na Imam Ali a.s. ambaye, ingawa vile vile alikuwa binami yake Bwana Mtume s.a.w.w., lakini alikuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono na kumtetea? Tazama chuki inavyofanya kazi!

[53] - Nasibiy ni yule mwenye chuki na uadui na Imam Ali a.s. na wafuasi wake.

[54] - Tai. uk. 633 wa Juzuu ya Kwanza ya Mizanul l'tidal.

[55] - Ikiwa yeye asama hivyo, na Bwana Mtume s.a.w.w. asema kuwa asiyempenda Ali ni mnafiki (taz. Sahih Muslim), vipi mtu huyo atakuwa thigah? Jamani!

[56] - Zunga ni mtu ambaye hakutahiriwa.

[57] - Yaani, hao walirejea ukafirini

[58] - Kutumia neno 'kimajazi' ni kuliyumia kwa maana isiyokuwa yake kikawaida.

[59] - Hatamhizi maana yake 'hatamwaibisha' au hatamtweza.

[60] - Buremu maana yake 'bendera'.

[61] - Yaani, kutoka kwenye Vita vya Khaibar.

[62] - Mtu wenyewe alikuwa ni Khalifa Abubakar as-Siddiq.

[63] - Mw. Khadija r.a. ndiye mke wa kwanza wa Bwana Mtume s.a.w.w., na ndiye wa kwanza kumwamini. Kabla ye yeye kufariki, Bwana Mtume s.a.w.w.hakuoa mke yeyote mwingine.

[64] - Hivyo ieleweke kwamba si lazima Hadtth iwemo katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim ndiyo iwe sahihi. Kuna Hadrth k.w.k. zilizo sahihi, hata kwa kufuatana na masharti ya yeye Bukhari na Muslim, ambazo hawakuzitia katika vitabu vyao!

[65] - Yaani, utawafikishia ujumbe wangu.